SEHEMU YA 28
Huo ndiyo ulikuwa udhaifu wake mkubwa, alipenda sana wanawake japokuwa moyo wake ulikuwa umezama na kuoza kwa Nandy. Kila alipokuwa akiongea na msichana huyo ndivyo alivyozidi kuchanganyikiwa naye.
Mwisho wa siku wakaanza kupiga stori za kawaida na kuzoeana huku Amina akimwambia Dickson kwamba katika maisha yake alikuwa amekutana na mwanaume kimwili mara moja tu, tena maumivu aliyoyasikia siku hiyo, hakutaka kurudia tena.
“Huwa inauma kwa siku moja tu, baada ya pale, mambo yanakuwa mukide,” alisema Dickson kwani alijua kuwa aliyekuwa akiongea naye alikuwa msichana wa uswahilini hivyo naye akaanza kuingiza mikato ya kiswahili.
“Basi sawa.”
“Nimefurahi sana. Hebu nitumie picha zako!”
“Upo WhatsApp bebi?”
“Nipo!”
“Sawa nakutumia!”
Kwa kipindi cha dakika chache tu tayari alikuwa amemsahau Nandy, msichana mpya akamuingia moyoni mwake na hakutaka kusikia la mtu yeyote yule.
Akaingia WhatsApp huku tayari akiwa amesave namba ile kama Cute Ammy.
Baada ya dakika chache, picha zaidi ya kumi na tano zikaingia kwenye simu yake, alipozipakua na kuziangalia, Dickson bado nusu azimie kwa mshtuko.
Hakuamini kama angekutana na mwanamke aliyekuwa na kalio kama lile alilokuwa akiliona, alichanganyikiwa, aliliangalia mara mbilimbili, lilikuwa kama pembe la ng’ombe, hata lilipokuwa likifunikwa khanga bado lilionekana tu.
Macho yakamtoka, ashki ya kufanya mapenzi na Amina ikamkamata kwa kiwango cha juu kabisa. Wakati akiwa amepigwa butwaa, akatumiwa video ilioyomuonyesha msichana huyo akikatika kitandani huku akiwa amevaa taiti na cheni kiunoni.
“Mamaaaaaaaaa..” alijikuta akisema kwa sauti, akainuka kabisa kitandani ili aone vizuri kwani alihisi kama anapitwa.
Udenda ukamtoka, alikuwa kama fisi aliyeona mzoga. Hakutaka kuchelewa, hapohapo akampigia simu.
“Amina. Naomba nikuone!” alisema Dickson huku akionekana kuchachawa.
“Jomoniiiiiii!”
“Please naomba nikuone! Siwezi kuvumilia, nitakulaje kwa macho na wakati nina mikono!”
“Utaweza?”
“Nijaribu!”
“Basi sawa. Kwa sasa nipo Dodoma, nitakuja kesho, nitapanda basi la asubuhi, nahisi saa kumi nitakuwa huko,” alisema msichana huyo, hakuwa Dodoma, alikuwa chumbani kwake huko Manzese.