Simulizi: Naacha Uchawi

mastory

Member
Dec 5, 2018
18
45
SIMULIZI;NAACHA UCHAWI.
MTUNZI;RAJA SADY.
WHATSAPP;0756920739.
SMS;0621047841.

SEHEMU YA KWANZA ( 01 )

ANZA NAYO....

Napenda kuwasimulia kisa hichi ili nanyinyi wenye mipango ya kuwa wachawi muache kabisa na msifikirie hata kidogo kama utakuwa na faida yeyote kwenu.Maisha nilioyapitia ni magumu sana mpaka sasa naona ni vyema kumtumikia mungu wangu kwa sababu ndiye mkombozi wa maisha yangu.

Miaka mitano iliyopita.

Familia yetu ilikuwa inasifa mbaya sana na ilifanya Wanamtaa kutuchukia na kututenga sana.Kawaida ya kila kijana huwa anataka vitu viwili vikuu ikiwemo rafiki wa kweli pamoja na mpenzi kama ilivyozoeleka lakini kwa upande wangu nilikosa vitu hivyo kwani hata niliotarajia watakuwa wapenzi wangu,wote walikuwa wakinitenga na hata kunitupia macho makali na yadharau pindi tu wanionapo.

Hakika tangia nimeishi na wazazi wangu sikubahatika hata siku moja kuona Baba, au Mama anafanya jambo lolote la kishirikina kama Wanamtaa walivyokuwa wakidai.

Kutengwa na matusi juu ilikuwa kama vitu vilivyozoeleka kwa upande wetu na ilikuwa haishi siku hata moja Baba au Mama ajatukanwa na Mwanamtaa haidha katika pita pita zake au hata Mtukuja kuja hapo nyumbani na kuanza kukashifu.

Ilifika hatua nikaanza kupambana na kila mmoja aliediriki kumtukana Baba au Mama na hapo ndipo nilipokosea kwani yalivyofika majira ya usiku nyumba yetu ilitiwa moto huku mimi nikiwa ndani humo.Nilijitahidi kila niwezavyo ili nimuokoe Mama pamoja na Baba lakini ilishindikana kwani wao walikuwa chumbani na walikuwa wamefunga mlango wao kwa ndani.

Bila ya hija Mama pamoja na Baba walikufa kifo cha kikatili,kwa upande wangu nilinusurika katika kuokoa maisha yangu.

Taarifa mbaya zilisambaa kwa kusemwa na watu wengi yakwamba familia ya wachawi wote wamekufa kwa kuteketea na moto.Usiombe ukachukiwa na Mtaa mzima watakutesa hata kama huna kosa pia watafanya kila kashifu ili wakudhuru.

Baada ya kuwa nimesalimika katika kuungua na moto huo,bila ya kujali maisha yangu yakoje au nini nachotakiwa kufanya,nilielekea moja kwa moja hadi kwa Bibi yangu.Nilizoea kumuita Bibi japokuwa hakuwa Bibi halali kwangu sababu Baba na Mama wote walifiwa na wazazi wao hivyo walikuwa yatima.Na nilimuita Bibi huyo kama Bibi yangu ni kwa sababu kipindi ambacho Mama na Baba walivyokuwa wanapata shida waliweza kufika kwa Bibi huyo na kutatuliwa matatizo yao yote.

Nilivyofika kwa Bibi huyo,alinipokea kwa majonzi na masikitiko makubwa.Kiukweli niliumia sana kuwapoteza wazazi wangu wote wawili tena kwa pamoja, lakini nilikuwa sina jinsi ya kujiokoa katika hilo.

Nilianza kwa kudondosha machozi yaliyofanya Bibi huyo,aanze kunipa kisa kizima juu ya wazazi wangu na ni kwanini waitwe wachawi.

"Mwanangu Yonasi ni kweli wazazi wako walikuwa wachawi na tena uchawi waliununua kwangu ila mwanangu kilichofanya mpaka Mama yako pamoja na Baba yako wafe ni kwa sababu walitakiwa wakurithishe uchawi wao lakini wao walikataa hiyo ndio sababu.Lakini hata kama walikataa lakini bado uchawi tayari umesharithishwa kwako.Jitahidi usije ukawa kama wazazi wako.Mimi hapa nakutengezea dawa unachotakiwa kufanya ni kuoa ili upate mtoto utakayemrithisha uchawi huu na wewe usipofanya hivyo unaweza kufa kifo cha kikatili angalau hata ya wazazi wako."

Bibi alivyomaliza kuongea hivyo,machozi yalinilenga na kujikuta naanza kuwalaumu wazazi wangu kwani pasipo wao kununua uchawi wa huyo Bibi yasingetokea yote hayo mpaka kupelekea kifo chao.

Nilijitoa muanga na kuhaidi lazima nitizime kila kinachotakiwa na lazima niutumikie uchawi kwani nisipofuata masharti naweza kufa kifo cha kikatili.

Nililala hapo nje mpaka majira ya asubuhi.Asubuhi na mapema,Bibi aliniamsha na kunikalisha kitako.Kisha akaanza kuzungumza nami.

"Mwanangu kule ulipokuwa unaishi na wazazi wako kumechafuka sana na huwezi kurudi Mtaa ule,ila utakaa hapa kwangu mpaka pale utakapo pata makazi sahihi na leo usiku ndio usiku maalumu utakaoanza kula nyama za watu kwani tayari na wewe ni mchawi kwanzia sasa."

Bibi baada ya kumaliza kuzungumza aliondoka na kuniacha huku nikizidi kushangaa na kujiuliza maswali lukuki,kumbe hata Mama na Baba walikuwa wanakula nyama za watu na sikuweza kupata jibu sahihi.

Nilikaa kwa Bibi huyo mpaka yalivyofika majira ya usiku ndipo aliponiamsha huku akiwa uchi wa mnyama na kuniamuru niamke kisha nikafanya hivyo.

"Chukua hii dawa upake usone pia chukua na huu ungo huukalie."

Bibi huyo alizungumza vitu hivyo kisha akanikabidhi vitu hivyo na kuninong'oneza maneno nayotakiwa kuongea nami nikafanya kama alivyonena na kujikuta napotea eneo hilo.

Tulitokea katika uwanja mkubwa uwanja.Nilishuhudia vitu vya kutisha huku nikiwa natembea na Bibi huyo alioonekana kuwa na cheo mahali pale,ghafla......

Je,nini kitaendelea......

&SIMULIZI YA NAACHA UCHAWI NI SIMULIZI KALI NA BOMBA NA SIO YA KUKOSA.

%KAMA UKO TAYARI KWA KULIPIA SHILINGI ELFU MOJA MIATANO TU.NITAFUTE KUPITIA WHATSAPP NAMBA 0756920739 AU SMS NAMBA 0621047841 NIKUUNGE KATIKA GROUP LA SIMULIZI,UTAKALOPATA SIMULIZI MBALIMBALI ZA SAUTI IKIWEMO NA HII.

%LIKE YAKO NA MAONI YAKO NI MUHIMU KWANGU.Sent using Jamii Forums mobile app
 
%LIKE YAKO NA MAONI YAKO NI MUHIMU KWANGU.

1549985972861.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakurochi

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
2,227
2,000
Hii ni fiction wewe unataka kuifanya ionekane non fiction, ndio maana maelezo binafsi yako kiduchu husemi wewe ni wa ngapi umesoma vipi ulijuajev kwamba wazazi wachawi wadogo zako vipi yaani fasta ummenda kwenye main store
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom