Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Yaani nimejikuta nataka kutoa chozi as if ni mhusika mwenyewe. If it's a true story I can't imagine how the situation became after receiving a letter from mtu mbaya manager wake.
Unexpected environments Ni mbya mno na huku umeshaanza kuvimba fensi kubwa gari ghafula unarudi naseri Ila always in life expect unexpected
 
Madamu anamponza tolu anajikutwa amefukuzwa kazin kwa kuonekana maeneo tofaut tofaut na madam
Tolu ana 10m je atafanya biashara au ataendelea kutafuta kazi
Vip ester kwa sasa anaonekana maisha yake si haba vip atamsaidiaje tolu? Madam je
Hii kitu ni yamoto vibaya mno[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Nahisi mtu wa pili mbaya kwa tolu ni yule muhindi dereva madam
 
Tupo wanawake bwana😇😇
 
SEHEMU INAYOFUATA...........

Niliingia ndani nikatulia huku nikikaa na kujiinamia,

mume wangu vipi naona kama haupo sawa vipi Kuna shida gani?Mimi ni mkeo kama Kuna jambo usinifiche. aliongea mke wangu akiwa kashika kiuno akisubiri majibu.

Kusema ukweli sikupanga kumwambia mke wangu niliona ni mapema mno, nilimwangalia vile alivyojifunga mavitenge huku nikiangalia miguu ilivyochafuka kwaajili ya maji na vumbi za pale nje huku nikijivunia kuwa na wife material, nilimuwaza mke wangu jinsi alivyokuwa ananishauri vitu vingi halafu nikawa nampuuzia nilimuhurumia sana.

Hivi kwani mume wangu upoje dakika 5 nzima nimesimama nasubiri majibu chaajabu unanipandisha na kunishusha, sawa ukijisikia utaniambia, lakini nikwambie tu kuwa fundi aliyemalizia ujenzi hapa anasema hela yake vipi, Ina maana umesahau. Niko nje Mimi Nina kazi chungu mzima. alisema mke wangu Huku akitoka nje.

Niliwaza kitu nikaona nimpigie madam au nikaushe tu lakini hata hivyo haitasaidia kukaa kimya lazima nitampigia. Ina maana kuanzia kesho Tena naanza kutembea na handbag kutafuta kazi jamani watu waliniombea, nikaenda Hadi kwa mganga lakini wapi kweli kisicho riziki hakiliki asilani,.

Niliikumbuka ofisi ile jinsi nilivyokuwa naongea na wakubwa huku nikizunguka kwenye kiti, wakiniona msomi na mtu wa maana huku baadhi nikikataa rushwa zao, na pesa nyingi lengo niwe muaminifu kwenye kampuni ambayo Leo imeamua kunifukuza kazi bila kosa lolote, hivi wanadhani kuongea na madamu nilikuwa namtongoza , aisee MUNGU naomba unisaidie bado Nina maisha magumu na watoto ni wadogo hawa nilijikuta naongea peke yangu.

Wewe baba Jack nakujua vizuri, wewe una tatizo, Tena una tatizo haswaaa kuendelea kunificha ni kuzidisha matatizo Sasa Mimi sitaki mtu aje achukue maamuzi magumu nisiyoyajua, naenda kwa mjumbe nikamwambie kuwa una shida na hutaki kuniambia. aliongea mke wangu akitaka kuondoka.

Nikamshika mkono. Tulia mke wangu, matatizo yangu siyo Kila mtu ajue usiwe na haraka, nitakwambia tu wewe ndiyo mke wangu, nikiwa mdogo kila kitu nilikuwa nawaambia wazazi, lakini nilikua na wazazi wakaridhika kuwa Nina uwezo wa kujitegemea, hata nilipowaambia kuwa nataka kuoa hawakusita Wala kuguna walitambua kuwa Nina uwezo wa kuishi na mwanamke.
Hivyo wakatoa baraka zao.

Walibariki utengano wetu Kati ya Mimi na wao wakijua fika naenda kutengeneza familia Kati ya Mimi na mke wangu, unajua Kuna Siri zangu nyingi unazijua na wazazi hawazijui? Niliuliza

Akaitikia kwa kutingisha kichwa.

Hivyo hakuna kuwapigia wazazi Wala kumwambia jirani
Haya ni mambo madogo yametokea hivyo tutasolve wenyewe hakuna shida, nenda kaendelee na kazi zako nitakwambia tu usijali mke wangu.

Mmmhh, sawa baba, aliitikia kinyonge.

Nilichukua simu nimpigie MADAM, sikutaka kuvunga tena kwanza kama kazi nishatimuliwa sina cha kupoteza.

Simu ilipokelewa..

Hello tolu niambie, naona huna lingine zaidi ya kuniambia umeachishwa kazi. ni madam aliongea bila hata salamu.

Ni kweli madam, nasikitika kwa yaliyotokea, nilisoma barua eti inaonesha kwanini Mimi na wewe tulikuwa tukikutana kwani Kuna kosa kukutana na wewe. Niliuliza

Tolu naamini barua umeisoma vizuri kabisa, na unajua maamuzi yametoka wapi, najua suala linakuumiza kwakuwa hujawahi kunitongoza kama wambea walivyokuripoti kwa boss, lakini yote kwa yote kauli imetoka kwa mtu aliyeko juu zaidi Tena huwezi amini hata Mimi Niko kwenye wakati mgumu, hivyo kwa kufupisha stori Sina Cha kukusaidia, wewe una elimu nzuri tu huwezi kukosa kazi si lazima ufanye kazi na sisi,

Na nikuombe kitu baba ni marufuku kunipigia simu kuanzia Leo usije kuniweka kwenye matatizo zaidi watu wakazidi kuamini, kwamba nilikuwa na mahusiano na wewe tena shukuru MUNGU wamekuona ni kifaranga tu
Akakata simu.

Mapigo ya moyo yalienda mrama maana sikutegemea mawazo yale, nikaona Haina shida ngoja nimtafute Rose mpenzi wangu. Nikatoka nje nikawa nje ya ile fence yangu mpya nikawa nazungusha macho huku nikiwa sielewi naangalia Nini.Simu ikiwa sikioni.lakini licha ya kupiga Mara kadhaa simu haikupokelewa, nikakata tamaa,

Imani yangu kwa Rose haikuwa kwenye mapenzi, bali nilitaka nimweleze ukweli kuhusu mie kufukuzwa kazi , hasa kwakuwa anajua halafu anaonekana yupo karibu na watu wazito wazito maana tukiwa kwenye maongezi yetu huwa nagundua anajua mambo mengi.

Nikiwa kwenye lindi la mawazo simu iliita mpigaji ni Rose, nilitoka nje fasta fasta huku nikienda mbali zaidi ili niwe huru kuzungumza.

Nikapokea...

Nambie mpenzi wangu,

Salama na niko poa sana tu, samahani simu ilikuwa mbali sikuisikia, nambie . aliongea kwa sauti ya uchangamfu

Sina cha kukwambia zaidi ya kusema Sina kazi mpenzi wangu, niliongea kwa huzuni.

Pole sana my najua jinsi gani unaumia, ila usijali ni mambo ya kupita tu hayo utapata kazi baby usijali, lakini na wewe kwanini utembee na mke wa boss wako, ujue utakuja kufa, yaani mtu mzito kama yule utembee na mke wake, kweli? wewe sikuwezi baba. Aliweka kituo

Nikajikuta nashindwa kumjibu maana aliongea kitu ambacho sijawahi kufanya maishani.

Tena mpenzi wangu nikwambie Kuna taarifa nilipata si nzuri kwamba walipanga wakupoteze sema wakagundua kuwa hakuna uhakika wa asilimia nyingi kuwa umetembea naye wakapanga tu waku black list,pole sana Dani wangu.
aliongea akionesha hajashtuka maana tayari alikuwa anajua mambo mengi.

Baby naapa viapo vyote, sijawahi kumtamkia yule madam jambo linalohusu mapenzi ila nilikuwa karibu naye kwa mambo mengine tu, halafu mpenzi wangu, kwanini mlinificha baadhi ya mambo kumbe mlikuwa mnajua mnanichora tu. niliongea kwa uchungu.

Yaliyotokea yametokea unatakiwa umshukuru MUNGU kwa Kila jambo Kisha utainuka Tena, sema Nini naomba uniache nitafute kesho Kuna jambo tutazungumza usijali sana. usijali. alimalizia Rose.

Sikuona Cha maana alichokitamka Rose nikakata simu nikarudi ndani. Pamoja na yote sikutaka mke wangu ajue lile suala nilipanga kumuongopea kivingine ili mradi tu hata akiniona nyumbani ajue ni harakati za kawaida tu.

Nilimuita mke wangu, akaja haraka maana muda wote alikuwa na shauku ya kujua jambo,

Mke wangu, usione nimekuja kwa unyonge hapa ni kwamba kule ofisini kwetu kumetokea matatizo hivyo wafanyakazi wote tumesimamishwa ili kupisha wamalize matatizo yao,

Mume wangu hayo matatizo hayakuhusu na wewe kweli maana nishachoka kusikia Mara oooh Kuna vitu vimeibiwa, Mara nini. Alihoji mke wangu

Hapana, ni matatizo ya matajiri wenyewe yaani huenda Wana matatizo na serikali hivyo , tumesimamishwa Hadi pale mambo yatakapokuwa sawa. nilimdanganya akaamini.

Afadhali baba maana nikajua yale yaleeee, safari hii tungerudi mkoani tukalime maana kama mji unakuwa umekushinda. aliongea mke wangu Huku akionekana kashusha Presha
Nilifurahi kumuona akiwa vile maana sikupenda hali nayopitia ajue, namjua angekuwa kwenye wakati mgumu kuliko Mimi.

Wanaume tumeumbwa mateso, kama kazi Sina kukaa ñdani kuanza kufikiria mengine Wala haisaidii nikawaza kesho asubuhi naenda maeneo ya mjini. naenda kubahatisha mambo huko huku kubwa zaidi nikilenga kutafuta kijieneo Cha biashara.

Simu yangu iliita,ilikuwa mida ya saa kumi kuangalia jina ni yule Binti ambaye nilikuwa naye ofisi moja, yaani mdogo wake Rose, nikaipokea simu

Niambie mdogo wangu, vipi kwema. niliongea kwa sauti ya uchangamfu ili asijue situation nayopitia.

Mr Daniel, kweli umeondoka umeniacha, lakini sikia tumeongea na baadhi ya wanasheria wa kampuni wanasema bado una nafasi ya kujitetea, kwanza hakuna mahali uliposaini kwamba unaacha kazi kwahiyo bado una nafasi Mr tafadhali usiwe na hasira kaka yangu Kaa ukijua kuwa bosi hanuniwi wewe mpigie simu mwambie ukweli naamini atakuelewa, kupitia simu ya yule Binti nilipata kuongea na wafanyakazi wenzangu wapatao wanne nikajua kuwa walikuwa kikundi .

Nilichowajibu ni kwamba kosa langu ni kubwa zaidi Kuna mtu akikufukuza waweza omba msamaha, lakini kwa kosa langu ni kama nitakuwa naamsha hasira zao tu.

Wote walinielewa huku wakionesha masikitiko makubwa, kama ilikuwa ni kweli MUNGU awabariki kama ilikuwa masikitiko ya kinafiki Mimi sijui, nilikata simu huku nikijitahidi kusahau ile kampuni na habari zake ,
Ndugu msomaji

Kujikumbusha ofisi na kazi yako yenye mshahara mzuri , maumivu yake hayaelezeki

Mume wangu, kesho ndiyo ile siku ya msaada niliyombiwa na akina ESTA , Sasa hapa najiuliza sijui niende au nisiende. ni mke wangu alivunja ukimya Mara baada ya kupata dinner.

Wewe nenda mke wangu, tena jambo lako liweke kwenye ratiba zako kabisa. niliongea kwa msisitizo.

Kesho asubuhi na mapema nilikuwa maeneo ya mjini nikiwa na washikaji fulani tukishauriana jambo, wakinipa madili ya biashara ya mbao, namna wanavyofuata mzigo huko kusini na kuja kuchana hapa mjini, Kila nikifikiria ile biashara na mlolongo niliopewa naiona ngumu.
Lakini nilipiga moyo konde, nilirudi jioni sana huku nikishauriana na mke wangu mambo fulani, huku kukiwa na mafurushi ya zawadi walizopewa huko ikiwemo cherehani mpya.

Unaona Sasa mke wangu ulitaka usite kwenda huoni Kuna mashine hii , yaani hii ukivurugwa unapiga bei unapata hela ya kukusogeza siku mbili tatu.niliongea kiutani

Wewe nani auze hata kama sijui kushona vizuri, nakwambia hii itanishawishi nitahakikisha nakuwa bonge la Designer. sema nini mume wangu Mimi nakuona umenyongea kana kwamba wewe ndiye boss wa kampuni, changamka basi. aliongea mke wangu.

Kesho asubuhi niliamka nikawa nafanya kazi pale home, Mara nikusanye mchanga niweke hapa, Mara nihamishe tofali ili kuji keep busy nisiwe na mawazo.Sms hewa iliingia kwenye simu, niliangalia inatoka kwa Rose. Ikabidi niangalie hali ya usalama nikaona ni shwari nikampigia.

Naomba uje nyumbani kwetu, baba anakuhitaji, ni vyema ukabeba na Documents zako na vyeti vyako, aliongea haraka haraka na kukata simu. Kwao ilikuwa mbali kidogo lakini nilihakikisha nafika ili nijue Kuna shida gani.

Nilimuaga mke wangu Huku nikishikilia mkoba wangu vyema nikatafuta usafiri wenye kunifikisha nyumbani kwa akina Rose.

Karibu mgeni, nilikaribishwa na Rose ambapo alikuwa kwenye vazi la kiislamu hata sijui aliwaza nini kuvaa vile, nikaingia ndani huku nikimtambua haraka mama yake Rose kwani walifanana sana .

Nilimwakia yule mama ambaye niligundua ni mkarimu sana tu,

Mama huyu anaitwa Daniel, nilikwambia Mimi ukanibishia , waliangaliana wakacheka, nikashindwa kujua kwani mama mtu alimbishia Nini mwanaye,.

Karibu sana baba, hapa ndiyo nyumbani kwaakina Rose , na huyu Rose tunaye hapa maana kuolewa hataki eti hakuna wanaume. aliongea huku akimtazama Rose wakacheka huku wakigongana mikono. Nilichogundua ni kwamba Rose na mama yake wanaishi kwa masihara sana, kama mbele za wageni ndiyo vile je wakiwa wenyewe?

Baadaye alikuja pale sebuleni mzee fulani ambaye alikuwa akitembea upande ikionesha mguu mmoja ni mfupi sijui ni ajali sijui alizaliwa vile sikuuliza,.

Habari yako Daniel, alinisalimia yule mzee huku nikishangaa kanijuaje au kwakuwa aliambiwa nitakuja?

(Akicheka)najua unashangaa nimekujuaje, ila ni kwamba Mimi nakujua, nakujua kivipi, Kuna barabara fulani ilijengwa chini ya kiwango yaani geji ya kifusi ikiwa nyembamba, basi tulilalamika kwa kwa wakala wa barabara za vijijini wakatwambia , siku mkiwaona muwaambie ukweli kwakuwa bado mlikuwa mnaendelea na kazi.

Sasa basi Kuna korongo katika njia za shamba ilibidi wamwage kwanza mawe Kisha waweke kifusi, lakini wale maoperator walikataa huku HR akituporomoshea matusi, tukagundua harufu ya rushwa na upigaji kwa mkandarasi yaani boss wako, Sasa kwanini nakukumbuka,
Ni kwamba wewe ulikuja siku ya pili tukiwa tumekata tamaa tulivyokueleza namna inavyotakiwa pawe ulituelewa , Kisha ukaagiza tipper zianze kumwaga mawe, hakika ulinifurahisha sana, maana pale kifusi bila mawe ilikuwa kazi bure maana kipindi cha masika maji yanaondoka na kifusi chote. aliweka kituo

Sasa mzee wangu wewe unaishi mjini kwanini ulikuwa unaipigania ile barabara? Niliuliza maana nakumbuka ile rough road inaingia vijijini huko ndani ndani.

Ni kweli mwanangu una haki ya kuuliza ila ni kwamba Mimi huko nafuga na nalima hivyo kahela kangu ka kustaafu niliweka huko. aliongea tukacheka.

Sasa mwanangu nimekuita kwasababu moja, leo nilimsikia Binti yangu akiongea na simu huku akitaja jina lako,Mimi nikajua labda watu wake tu Sasa baada ya kusikia neno kufukuzwa kazi, ikabidi nimuulize ni nani huyo?

Ndipo akanifahamisha nikawaambia kama ni huyo kijana Mimi namfahamu aliwahi kufanya kazi kampuni ya (akiitaja ile ya kwanza)
Lakini Rose akanibishia kuwa si wewe ikabidi nitaje wajihi wako.

Nikawaambia ni mrefu na anapenda kufuga nywele, hapo hawakubisha japo huyu mama yako ndiyo kwanza anakuona. aliweka kituo baba yake Rose ni mzee muongeaji sana.

Nilichokuitia ni suala la wewe kufukuzwa kazi, nimeamua kukutoa hofu.....

Nilikwambiaje Rose, (akimuuliza Binti yake)

Uliniambia kama ni yule kijana Mimi nitampeleka shirika la(jina kapuni) alijibu Rose huku nikishangaa ile familia ilivyo na utani hadi raha .

Basi kijana kazi umepata we kajiandae tu muda wowote nakupeleka Mimi mwenyewe, huwezi kufukuzwa kwa kosa kama lile ambalo haliingii akilini , nikashangaa Hadi kosa lishakulikana,huku nikimuona Rose kama hajapenda uongeaji wa baba yake .

alisema yule mzee ambaye anaonekana ni wale wazee wa mjini, mjanja mjanja hivi.

Hakika nilifurahi sana kwani ni shirika la kiserikali lililosheheni wanasiasa, na vigogo wengi tu, nikaona kama naota, nilimshukuru sana yule mzee kwa uungwana wake huku nikiwa nishapanua wigo wa kujuana na watu.

Alamski.

Itaendelea.................
 
Nice Sana [emoji1666] kiongozi
 
Katika swala la uaminifu kazini kuna jambo kubwa la kujifunza hapo
 
Mlango mmoja umefunga,mwingine unakaribia kufunguka,duuu!!
 
Kwa hii episode umetutendea haki.
Hapa hata ukikaa wiki mbili bila muendelezo ni sawa tu Tolu.
Tumeridhika sana.
 
Katika swala la uaminifu kazini kuna jambo kubwa la kujifunza hapo
Kwakifupi ni kwamba sio kila ofisi unatakiwa kuwa mwaminifu kwao...Inategemeana sana na ofisi hiyo husika.

Mwaka 2015-16 nilikua mwaminifu sana kwenye kampuni moja hiv Hapa jijini ila baada ya kugundua wananitumia tu kama toilet paper nikaanza kupiga deal... kwanza waliniondoa kazin af baadae sijui ikawaje wakataka nirudi ..aisee nilipiga deal kama kichaa..uaminifu kwangu ilikua ni msamiati ... nikijua waz hawa jamaa watanitema tena tu just a matter of time.....na kwel 2020 nikaondoka (kama nilivyo comment huko juu).

Ila this time niliondoka nikiwa nimejenga nyumba kuubwa safi ya kisasa kwa pesa za michongo ambazo ningejifanya Yesu ingekula kwangu....

Hii stori ina vipengele vinanihusu sana..Hakika hapa kuna mengi ya kujifunza
 
Jamani Kuna michepuko una faida mno mjue yaani mno. Ila sio Hawa hàwaeleweki hawajasoma,mpaka vocha ya buku wanaomba. Kutana na mtu ambaye anakuomba milioni kwenda juu jamani.
Mapovu ruksa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…