Simulizi: Macho ya ajabu

Simulizi: Macho ya ajabu

bioto

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
1,261
Reaction score
2,099
Riwaya:MACHO YA AJABU
Na:Humph de throne
WhatsApp:0629314605

Sehemu ya kwanza
Yapata karne kadhaa zimepita toka kipindi ambacho himaya kubwa ya mfalme Sangu akiwa kama mtawala mwenye nguvu Katika makabila mbalimbali yaliyokuwa yanaizunguka himaya yake, kabla ya kuwa na ngome hii isiyoingilika kirahisi kulikuwa na vita kubwa isiyoelezeka kati ya makabila haya yanayopatikana ukanda huo.

Mfalme Sangu alipoona hali ni tete ndipo aliamua kuwaita waganga wake wote ili afahamu wataisaidiaje himaya yao kwa kutumia nguvu hizo walizo nazo, walijitokeza waganga wengi wenye uwezo tofauti tofauti.

Mfalme Sangu alikuwa ni mtu mwenye akili sana alichokifanya ni kuwaambia kuwa "nataka wote muungane mjadili ni jinsi gani mtaikomboa himaya hii kwa njia yoyote ile mtakayoona inafaa"

Hilo lilikuwa agizo la mfalme kwahiyo haikuwa rahisi mtu awaye yote kupinga hivyo jopo hilo lilikaa chini na kuanza kutafakari, wa kwanza alinyoosha mkono kuashiria ana wazo, mwenyekiti wa kikao alimruhusu aongee "Mimi nafikiri ngome yote hii izindikwe haswaa ili iwe vigumu kwa maadui kuingia"

Mwenyekiti "asante kwa hoja naomba wanao kubaliana nae wanyooshe mikono" walijitokeza wengi kasoro mtu mmoja tu ambaye alionekana hajaafikiana nae

Mwenyekiti "Nashukuru kwa kumuunga mkono lakini bwana Mpao hapo nadhani unajambo lingine tofauti na wazo la mwenzio unaweza kutudokeza tafadhali?"

"Aaaaa! Ni kweli Mwenyekiti Mimi sipingi kwani ni wazo zuri tu ila mapendekezo yangu ningeomba tutengeneze kitu ambacho kinaweza kututabiria matukio yajayo nadhani hii inaweza kutusaidia kutambua udhaifu wa maadui zetu"

Mwenyekiti "ndugu zangu nafikiri mmemsikia bwana Mpao sasa ni wangapi wanakubaliana nae?"

Wote walinyoosha mikono kuashiria wamekubaliana lakini swali likawa ni kitu gani kitengenezwe, kimya kilitawala kwa dakika kadhaa ndipo mikono miwili iliibuka Mwenyekiti akamruhusu wa kwanza kisha atamalizia wa mwisho

"Ahsante ndugu Mwenyekiti kwa kunipa nafasi hii mimi napendelea tutengeneze hirizi ambayo mfalme ataifunga mkononi"

Mwenyekiti "wanaomuunga mkono tafadhali"

Wachache walinyoosha mikono ndipo alipomruhusu Mzee Mandevu nae atoe hoja yake "Kwa upande wangu mwenyekiti natazamia tuunde macho ya ajabu hii itakuwa hivi macho hayo yatakuwa hayaonekani kwa mtu wa kawaida na mvaaji wa macho hayo atakuwa kawaida kama awali hiyo itamsaidia kutambua tukio baya litakalotokea mda wowote ule"

Mwenyekiti "wangapi wanaungana na hoja ya mzee Mandevu"

Wote walikubali kwa kunyoosha mikono,Mwenyekiti akamkabidhi uongozi Mzee Mandevu katika hilo zoezi ambalo lilitakiwa kuanza kesho yake baada ya maandalizi.

Asubuhi na mapema shughuli ilianza chini ya mzee Mandevu na ilipofika jioni zana yao ilikuwa imekamilika ilikuwa na mng'ao kama wa dhahabu iliyo katika mtindo unaofanana na macho. Alikabidhiwa mfalme,alipoishika na kuanza kuikagua ghafla ikamrukia machoni mwanga mkali ukatokea eneo lote hilo ikawa kama maajabu mfalme alitetemeka kwa woga na hali ilipotulia alikuwa kama awali japo alijihisi tofauti na mwenye nguvu zaidi kuliko awali.

Mfalme akiwa amelala aliota maadui wanakuja kuivamia himaya yake alionyeshwa njia zote watakazopitia alipostuka kutoka usingizini alienda moja kwa moja kwa mkuu wa majeshi akamuelezea ambaye aliagiza vikosi vingi sana kuelekea sehemu alizoonyeshwa na mfalme katika ramani yao hivyo ndivyo himaya yake ilivyozidi kupanuka.

Baada ya kuja wakoloni mfalme Sangu aliuawa macho yale ya ajabu yalifichwa na wazee wenye busara katika mapango yenye michoro ya kale ili yasijekufikia katika mikono ya watu wabaya.

********Karne ya leo********
Tulikuwa katika safari ya kishule kutazama michoroya mapangoni tukijifunza kutokana na somo la historia linavyoelezea Mimi Humph na wanafunzi wenzangu katika kutembea tembea humo tukielezewa mambo mbalimbali Mimi niliona pembeni yangu kuna kama kapango kadogo halafu kuna giza lakini kulikuwa na kitu kinawaka waka.

Kwakuwa nilikuwa mbovu wa macho,miwani yangu ikiwa imeshika vyema katika paji la uso nikapuuzia, moyo uligoma kabisa kulipotezea hilo suala nikaamua kwenda,haikuniwia vigumu kuondoka katika kikundi chetu kwasababu nilikuwa wa mwishoni, nilisogea mpaka pale panapong'aa kama dhahabu nilipotaka kushika ili nijue ni kitu gani nilistukia kimenirukia machoni nikapiga kelele za kuomba msaada mwanga mkali ukasambaa kila kona katika hiyo sehemu ukitokea machoni mwangu,popo wengi waliruka wakanifanya
nizidi kupiga kelele kwa uoga....
 
Sehemu ya pili

...........ilipoishia........
nikapiga kelele za kuomba msaada mwanga mkali ukasambaa kila kona katika hiyo sehemu ukitokea machoni mwangu,popo wengi waliruka wakanifanya nizidi kupiga kelele kwa uoga....

.......Endelea...........
Ule mwanga mkali uliotoka machoni mwangu na kupotea ndiyo ulisababisha wale popo wakimbie, wanafunzi walikimbilia niliko pamoja na mwalimu wa zamu, walifanya juhudi za kuninyanyua ila miwani yangu ilikuwa imevunjwa na wanafunzi wenzangu kwa kukanyagwa kutokana na giza lililokuwepo katika pango lile dogo

Nilitolewa mpaka nje ambapo mwalimu mwenye dhamana ya kutusimamia aliomba wanafunzi wakusanyike na walipofanya hivyo alitoa onyo Kali kwa yeyote yule atakaye kiuka taratibu zilizowekwa katika ziara hiyo kama nilivyofanya Mimi ataadhibiwa vikali japo Mimi nilisamehewa kwa kuwa sikuwa mkorofi shuleni pia nilijulikana kama mzembe shule nzima tena na nusu upofu juu

Siku hiyo usiku nilikuwa naota ndoto za ajabu ajabu mojawapo ikiwa hii "nilikuwa nimesimama na mzee mwenye ndevu nyingi akawa ananionesha vita Kali kati ya wazungu na waafrika ambapo Mfalme mmoja aliuwawa kwa kukatwa kichwa huku macho yake yakitoa mwanga mkali ukiambatana na vumbi katikati yake alikuwa huyo mzee mwenye ndevu nyingi"

Nilistuka mwili ukiwa umelowa jasho huku nikitweta uoga ukanitawala usingizi nao ukanipaa kabisa,nilienda kuoga baada ya hapo sikutaka tena kulala nilichukua daftari nikawa napitia pitia masomo mbalimbali, niliona utofauti nilionao kwa muda mfupi kwani hakuna siku niliyowahi kusoma bila miwani lakini siku hii nilisoma mpaka kulipokucha bila kutumia miwani yangu ya macho

Kulipo pambazuka vyema safari ilianza ya kurudi nyumbani kwani siku hiyo ndiyo ilitakiwa turejee nyumbani kila mwanafunzi kutoka katika ziara hiyo ya siku chache, ndani ya basi wanafunzi walikuwa wanaimba nyimbo mbalimbali kwa furaha lakini haikuwa hivyo kwangu nilikuwa na uchovu wa kutolala na mawazo mengi juu ya kile kilichonitokea nikihisi nimepata miujiza iliyoponya magonjwa
niliyonayo japo ile ndoto ilinitia wasi wasi mkubwa.

Nilipokelewa kwa bashasha mno na wazazi wangu ndipo furaha ilinirejea mara mbili kwani sikuwa natumia miwani tena,nilipofika nyumbani niliwaomba wazazi wangu nipumzike kwanza na baada ya hapo nitawasimulia jinsi safari ilivyokuwa ya neema upande wangu.

Baada ya masaa kadhaa familia nzima tulikuwa sebuleni tukizungumza mawili matatu hasa kuhusu ziara iliyofanyika. Niliwaelezea kiundani lakini nilipofika katika suala la nimewezaje kupona macho nilieleza kwa kuficha sana na ninakumbuka niliwaambia kuwa niliamka siku hiyo ya kumaliza ziara nikiwa tofauti na siku zote yaani mwenye siha njema na niliweza kusoma Vila miwani.

Haikuwa rahisi kuwa shawishi lakini ilibidi tu wakubaliane nami kile ninachokisema maana hakuna aliyeshuhudia wala kuwepo eneo la tukio. Usiku uliingia haraka sana hivyo kila mmoja aliingia chumbani kwake kulala

Nikiwa usingizini niliota ndoto nyingine hii haikuwa ya kutisha,alionekana Madam Remijo akitufundisha darasani Mara John akaanza kuzomea mwanafunzi aliyeuliza swali kwa kuwa John alikuwa mwanafunzi mtukutu aliejulikana shule nzima,Madam Remijo alikasirishwa na kitendo cha John hivyo alimuadhibu vikali na kumtoa John nje ya darasa tunalosomea.

Madam Remijo alipomaliza kufundisha alitoka darasani akielekea upande ambao kuna ngazi ili ashuke nazo mpaka ofisini kwake, John alikuwa amesimama karibia na zile ngazi akimtazama madam Remijo kwa chuki mno,madam aliliona hilo lakini alichukulia kawaida.

Madam Remijo alipokuwa katika harakati za kumvuka John ghafla alijikwaa katika mguu mkakamavu uliotegeshwa vizuri na John,kutokana na mwendo aliokuwa nao katika zile ngazi kwa kubiringita(kugeuka geuka) mpaka katika sakafu kichwa kikiwa kinavuja damu nyingi.

Nilistuka usingizini ilikuwa tayari ni asubuhi hivyo nilijiandaa mapema na kuelekea shuleni,njiani nilikuwa na mawazo mno kuhusu ndoto ya madam Remijo,mpaka nilipowasili shuleni mawazo yalikuwa yale yale nikiwa naamini ni moja kati ya zile ndoto mbaya zinazoniandama.

Marafiki zangu walinishangaa siku hiyo kutokana na kutovaa miwani ya macho na nilikuwa natazama na kusoma vizuri kama wao,walinipongeza kwa kupona ugonjwa huo unaosumbua wengi na hasahasa huwa hawaponi mpaka kufa hiyo ikiwa kama itilafu ya
moja kwa moja mwilini.

Ilifika kipindi cha madam Remijo akawa anafundisha vile vile nilivyoota,jambo ambalo liliniacha hoi ni pale ambapo John alimzomea mwanafunzi aliyeuliza swali sehemu ambayo hajaelewa,madam Remijo alimuadhibu vikali kama ilivyonitokea katika ndoto
nikazidi kustaajabu

Sijawahi kuota ndoto ikatokea kweli hii ilikuwa ni mara ya kwanza nikahisi nimeanza kuwa mtabiri au ni bahati tu ya siku hiyo kuota tukio la kweli kama lile,John alipoadhibiwa alitolewa nje na madam Remijo Kisha akaendelea kutufundisha.

Nilivyoona kuwa yote yanayotokea ni ya kweli japo sikuwa na uhakika sana kwasababu nilijihisi naota au ni mchezo fulani wa kuigiza kwani kila kitu Mimi nilikuwa nimekishuhudia ndotoni. Moyo ulikuwa unanituma nitoke darasani lakini nilikuwa napingana nao,nilianza kuhisi kuna mtu ananihimiza nitoke darasani na mda huo huo Madam Remijo aliruhusu maswali.

Nikajua kuwa madam Remijo anaelekea kumaliza kipindi hivyo niliinuka haraka kama moyo ulivyotaka na kwenda kuomba ruhusa lakini ilikuwa vigumu kupewa kwasababu madam Remijo huwa haruhusu mwanafunzi yeyote kutoka wakati wa kipindi chake na kama uko nje hauruhusiwi kuingia darasani mpaka amalize kipindi.

Nilichofikiria kwa haraka ilikuwa ni kushika zipu yangu na kuinama ili kuonesha haja ndogo inakaribia kutoka hapo madam Remijo aliniruhusu haraka ili nisi aibike mbele ya darasa,wanafunzi waliangua kicheko kutokana na mbio nilizotoka nazo darasani.

Sikufika maliwatoni kama nilivyopanga,nilitembea kufuata korido huku nikitazama huku na kule mpaka nilipohakikisha nimemuona John aliyekuwa ameegemea ukuta kama anafikiria jambo Fulani.

Nilisogea kama hatua kumi nikiwa nimebakiwa na hatua kama sita kumfikia John nilipotazama pembeni niliona ubao wa matangazo ukutani,kwa kuwa sikuwa na mazoea na john kutokana na ukorofi wake nikaamua kusimama hapo ili nisubiri kuona kile kitakachotokea.

Madam Remijo alikuwa anakuja kufuata korido akiwa na vitabu mkononi na Mimi nikaona hiyo ni nafasi ya pekee nitakayotumia kumuokoa madam Remijo japo sikujua nitaanzaje kufanya hivyo.

Nikaamua kumfuata madam Remijo nakuomba vitabu vyake nimsaidie kubeba kama ilivyo desturi ya kusaidia wakubwa wanapokuwa na mizigo japo kwa vizazi vya sasa si rahisi kufanya hivyo isipokuwa wanapokuwa shuleni ambapo hufanya hivyo kutimiza sheria.

Tulianza kutembea kuelekea sehemu yenye ngazi zinazoshuka karibia na ofisi ya madam Remijo,Yeye akiwa upande aliopo John,baada ya kitambo kifupi tulikuwa tumemfikia John pale alipo Mimi nikiwa napiga hesabu ya kile kitakachotokea ili niweze kusaidia kwani John alionekana yupo kishari zaidi ya vile alivyofikiria madam Remijo walipotazamana kwa macho yanayotangaza chuki.

kabla hata sijapata njia ya kumuokoa nilitaharuki kumuona madam Remijo amejikwaa na kuruka juu kutokana na mwendo mkubwa kiasi aliokuwa nao huku kichwa kikiwa kimetangulia kuanguka,Mimi nilikuwa tayari nimeachwa na madam Remijo kama mita tatu kutoka pale alipo....
 
Sehemu ya tatu
..........ilipoishia..........
kabla hata sijapata njia ya kumuokoa nilitaharuki
kumuona madam Remijo amejikwaa na kuruka juu
kutokana na mwendo mkubwa kiasi aliokuwa nao
huku kichwa kikiwa kimetangulia kuanguka,Mimi
nilikuwa tayari nimeachwa na madam Remijo kama
mita tatu kutoka pale alipo....
.........Songa Nayo........
Kwa kasi ya ajabu niliruka bila kutarajia na kumdaka
madam Remijo kwa mkono mmoja huku mkono
mwingine ukiwa umeshikilia vyema vitabu vyake..
Nilistaajabu sana kujiona mwepesi kiasi kile,mda
huo madam Remijo alikuwa ametumbua macho
asiamini kile kinachotokea mbele yake akiwa
amenusurika kifo japo hakuonekana kushangaa
alivyonusurika ajali hiyo.
Alionekana wazi kushangazwa na uwezo
niliouonesha hasa ukizingatia nilikuwa bwege sana
shuleni.
****************************
John aliogopa sana baada ya kuona nimemsaidia
madam Remijo aliamua kukimbia kuelekea
darasani,ndipo na mimi nikang'amua kuwa
nimemshika madam Remijo sehemu mbaya
Madam alikuwa ananitazama kwa mshangao mkuu
huku nikiwa nausikia moyo wake unavyokwenda
mbio mbio
Nilimbwaga chini nakuanza kujiuliza nimewezaje
kumdaka msichana mwenye umbo la kinyamwezi
namna ile akiwa amebeba uchumi wa mabilioni
kadhaa chini ya kiuno chake tena kwa kasi kubwa
namna ile kabla hajapata madhara
Niliushangaa sana mwili wangu ulivyo ukilinganisha
na nguvu nilizotumia havikurandana kabisa,Madam
aliinuka kwa kujizoa zoa huku wasi wasi ukishamiri
wazi wazi usoni mwake eti kimbau mbau kama
kama mimi kumdaka juu juu namna ile tena kwa
mkono mmoja huku mwingine ukiwa umeshika
vitabu bila kupepesuka wala kutetereka ajabuuu!!!!
Niliweka vitabu chini nakuanza kuelekea darasani
nikiwa na aibu tele lakini kabla sijafika mbali
nilimsikia madam ananisemesha
"We Humph unaenda wapi sasa?"
"da..ra..sa..ni" nilijibu kwa kubabaika nikiwa
naangalia chini
"Kha! k'o unataka kuniacha?" duh! nusura nicheke
kumbe madam ni muoga vile
"Samahani kwa hilo,kwani umeumia ili nikupatie
msaada" niliongea kwa msisitizo nikijua wazi kuwa
amedata nilivyonshika maeneo kama wacheza
dance aina ya tango
Niliamua kumfuata ili nimuinue,nikajua nikimuinua
basi atakuwa na uhakika kuhusu nguvu
nilizonazo,nikaanza kuzuga baada ya kumshika
mkono nakuanza kuuvuta lakini hakuwa na dalili
yoyote ya kuinuka pale sakafuni
Nilihema kwa nguvu nikamuachia mkono na bahati
nzuri katika korido lile hakupita mwanafunzi wala
mwalimu.Ghafla mlio wa kengere ya pumziko
iligonga hivyo wanafunzi walihitajika wakapate
chochote mda huo kulingana na hali zao kiuchumi.
Madam aliinuka haraka pale sakafuni na mimi
nikachukua vitabu nikapeleka ofisini,nilipokuwa
natoka nikakutana na madam ana kwa ana ila
aliwahi kuinama na kabla hajainua paji lake la uso
nilimpita kasi nikielekea kantini nikiwa tayari
nimekamilisha msemo ule wa"tenda wema nenda
zako".
******************************
Katika jengo moja refu kulikuwa na mtu mmoja
nadhifu mno anaangalia dirishani katika ofisi yake
hiyo ya kisasa,aliinua mkonga wa simu na kupitisha
namba kadhaa kisha akasikiliza kwa utulivu wa hali
ya juu
"Mwambie Lamson afike mara moja ofisini kwangu"
"Sawa bosi"ilijibu sauti ya kike isiyokuwa na mvuto
kwa bosi huyu
Baada ya muda alifika kijana mmoja aliejazia
vilivyo"naam bosi nimeitikia wito wako"
"Nimekuita hapa ili nikupe kazi si unakumbuka ile
historia ya yale macho ya ajabu?"
"ndiyo,vipi yamepatikana au?"
"nimepata mahali yalipo katika mji mmoja mdogo
lakini sijafahamu ni nani aliyenayo"
"Sawa nitafuatilia nani mhusika"
********************
Muda wa kwenda nyumbani ulifika siku hiyo
nilikuwa wa mwisho kuondoka kwa kuhofia madam
anaweza kuniita akiniona,nilikuwa mwanafunzi pekee
katika barabara hii ya lami.
Nilitembea taratibu kutokana na njaa ilivyokuwa
inanisokota kadri muda unavyokwenda
Nilikuwa pembeni ya barabara ya lami hasa
ukizingatia kuwa watembea kwa miguu huwa
tunasehemu maalumu ya kupita vivyo hivyo magari
na baiskeli
Nilijikaza kiume ili walau nifike nyumbani lakini
wakati nawaza na kuwazua hayo ghafla zile hisia za
maono zikanijia,mtoto mmoja hivi mdogo mdogo
alikuwa na puto zilizofungwa kamba ,ile kamba
ilikuwa imeshikiliwa vyema na mtoto yule
Akiwa anacheza cheza na kuzifurahia zile Puto
hakutazama mbele anakoenda ndipo alipojikwaa
katika kingo za barabara na kuanguka zile puto zote
zikapeperuka na kuelekea katikati ya Barabara
ambayo magari yake ni Yale yaendayo kasi
Mtoto yule aliinuka na kuzikimbilia puto zake mama
yake hakugundua kama mwanae anaenda
barabarani,alizifikia puto na kuzinyanyua,alipogeuka
ili arudi alipotoka loooh! Alikuwa amechelewa gari
ilimgonga,kishindo kikubwa kikasikika kutoka chini
ya magurudumu ya gari ile aina ya fuso huku
mpasuko wa kitu ukishamiri eneo hilo
Akina mama na watu wenye mioyo miepesi
walipiga mayowe na wengine wakipoteza fahamu
kutokana na presha.Nilistuka baada ya kupigwa
kikumbo na mzee wa makamo na kuanza
kunikaripia eti niwe mwangalifu ninapotembea
Barabara niliyoiona ni hii hii ninayopita muda
huu,nilianza kutembea haraka ili ikiwezekana
nimuokoe yule mtoto nikiwa nimeshasahau njaa
zangu nilizonazo,kutokana na uwingi wa watu
ilikuwa vigumu kuwahi eneo la tukio
Kwa mbali niliona puto zikiwa zinaelea nikazidi
kusonga mbele huku moyoni nikihisi sauti inanisihi
nifanye haraka
*****************
Lamson alikuwa tayari amefika katika sehemu
ambayo kifaa chake kilikuwa kinamuelekeza (radar
au redioloketa)na kilionyesha kuwa amekaribia
kuyafikia yale macho ya ajabu,aliongeza umakini
zaidi sambamba na kupunguza mwendo wake
**************
Nilipokuwa nakaribia sehemu aliyopo yule mtoto
nikaziona zile puto zikihama toka sehemu ya
watembea kwa miguu mpaka barabarani
Moyo ukaanza kwenda mpito mpito(kasi),kwa kuwa
sikutaka kufahamika kuwa nimetoa msaada
niliamua kuvua shati nikabaki na flana iliyoubana
vyema mwili wangu,muda huo nilijibanza pembeni
ya ngazi za kuelekea nyumba yenye mgahawa huku
nikiwa upesi upesi kabla yule mtoto hajagongwa na
gari
Nilijifunga leso nusu uso kisha nikaweka begi langu
mgongoni,nilipogeuka kutazama barabarani yule
mtoto alikuwa ameshika zile puto na kunyanyuka
nazo.Nilitoka mbio kuelekea barabarani,nikiwa
katika mwendo huo niligongana na mtu ambaye
alikuwa kama kisiki kwani hakutikisika hata chembe
Sikumjali nikaendelea kukimbia kuelekea
barabarani,kitendo cha kutokeza tu niliona gari ile ile
niliyoiona ikisababisha ajali ikiwa sentimita chache
kutoka pale alipo yule mtoto,nikaongeza kasi zaidi
na miguu yangu ikatii japo akili na moyo viliniambia
tayari nimechelewa........
 
Sehemu ya nne
.......... Ilipoishia..............
Sikumjali nikaendelea kukimbia kuelekea
barabarani,kitendo cha kutokeza tu niliona gari ile ile
niliyoiona ikisababisha ajali ikiwa sentimita chache
kutoka pale alipo yule mtoto,nikaongeza kasi zaidi
na miguu yangu ikatii japo akili na moyo viliniambia
tayari nimechelewa.........

........... Shuka nayo..........
Nikaanza kukata tamaa ya kumfikia lakini kuna sauti
fulani nilihisi inanihimiza niongeze kasi na kweli
nikatuliza mawazo yangu kabisa na akili yote
ikahamia kwa yule mtoto
Kitendo cha kutilia mkazo kwa yule mtoto nilistukia
nimepotea na kumfikia yule mtoto kama kunguru
anavyoshuka kunyakua kifaranga, nilipotoa unyayo
wangu kuna kitu kama upepo kilinipuliza lakini
sikigeuka maana nilitambua kuwa ilikuwa ile gari.
Akina mama hawakubaki nyuma katika tukio kama
lile walikuwa wakipiga ukunga na yowe za
masikitiko lakini kilichowashangaza zaidi ni yule
mtoto kuonekana upande wa pili wa barabara akiwa
salama salimini na puto zake japo alikuwa
ameduwaa kama aliyekuwa anapingana na akili yake
kuhusu jambo fulani kiukweli alifanana na mdoli
kwa mda ule ama sanamu la barabarani.
*****************
Kifaa cha Lamson (redio loketa) ilikuwa inatoa mlio
mkali kuonyesha kuwa amefikia eneo sahihi lakini
ghafla alichomoka kijana mdogo(Humph) katika
sehemu isiyojulikana kwa Lamson ndipo
walipopigana vikumbo hiku radar ya Lamson ikizidi
kuongeza mlio na kuonyesha kuwa kitu
anachotafuta ndiye huyo kijana aliye mpita kwa
kasi.
Alianza kumfuata kwa nyuma lakini aliishia
kumpoteza katika mazingira yasiyo eleweka. Pia
alishuhudia yale maajabu ya mtoto kuokoka ajali
bila kumuona aliyemuokoa.
Aliamua kutoweka eneo hilo mapema asiamini
kama yule kijana mdogo vile kapotea katika upeo
wa macho yake kirahisi namna ile.
"Lamson nieleze vizuri kijana wangu mbona
unababaika namna hiyo eeeeh!?" Aliuliza mzee yule
wa makamo aliyekuwa bado amesimama dirishani
kama ilivyokuwa awali alipomuagiza Lamson
"Kiukweli Profesa radar yangu iloitambua sehemu
ambayo kuna windo letu lakini ile ajali mmmh!"
Alipofika hapo akainamisha kichwa kama mtu
anaelazimisha kukumbuka kitu
"Lakini nini Lamson?, yaani badala ya kufanya kazi
niliyokuagiza unaenda kutazama ajali eeeh?" Profesa
aling'aka sasa hasira ikiwa imedhihirika wazi wazi
"Sivyo bosi wangu ulivyoelewa" alijaribu kujitetea
Lamson
"Sasa labda unataka kusema nini wewe,nimefanya
utafiti kwa muda wa miaka thelathini sasa mpaka
kufikia hapa lakini wewe unazembea kukamilisha
hiki kidogo"
"Nimekuelewa mkuu lakini nahisi hayo macho yapo
kwa huyo kijana, kwani alipokatisha tu radar yangu
ilitoa mlio mkali mno"
"Unasemaaa?, hebu atafutwe mara moja huyo alafu
pitia kwa katibu mwambie akupatie chek/hundi ya
kiasi utakachoona kinafaa kuifanya hiyo kazi
ipasavyo"
"Sawa Profesa" Lamson aliinuka na kuondoka eneo
hilo
*******The rise of sorceress******
******Kuibuka kwa mchawi wa kike**
Asubuhi na mapema niliwahi shuleni kama ilivyoada
ili kutii sheria zilizowekwa na kutekeleza. John
alionekana mnyonge sana tofauti na siku zote
nikamaizi kuwa ameingiwa na uoga wa kufukuzwa
shule kutokana na kitendo alichomfanyia madam
Remijo.
Ilipohitimu muda wa kurejea nyumbani kabla
hatujatawanyika nilihisi hali ya hewa imebadilika
kiasi Fulani,baada ya kuangaza sana katika mistari
ya wanafunzi nikafanikiwa kumuona binti mmoja
mrefu Na mrembo wa wastani
Alikuwa amesimama pembeni ya john huku
akiniangalia akiwa na tabasamu pana lililochanua
vyema usoni pake,safarii alirudisha macho kwa
John akamgusa kichwani kisha akaanza kuondoka
kwa mwendo wamadaha
Sikuelewa anaamanisha nini lakini punde baada ya
kupotelea katika mistari ya wanafunzi John aligeuka
na kunitazama akiwa ametabasamu vilivyo na
kuruhusu meno kadhaa yachungulie akanikocheza
Mmmh!!! Nilishangaa John yule mnyonge ameanza
kutabasamu,huenda amepatwa na tatizo la
akili.Safari ilianza ya kuelekea nyumbani John
alikuwa nyuma yangu kwa kila hatua niliyopiga.
Baada ya kufika njia inayoelekea nyumbani kwetu
nilikatisha na kwa bahati mbaya nilikuwa peke
yangu,nilitamani nipate Yale maono ili nijue john
amekusudia nini lakini La! Haikuwa vile nilivyotaka
Nilijua Leo napigwa kipigo cha mbwa mwizi kama
sitafanya lolote,nikaanza kukimbia kidogo kidogo
mwisho nikatimua mbio kabisa ili kumkwepa huyu
mbogo aliyejeruhiwa kwa risasi na visasi vya
kumkosa madam Remijo
Nilikimbia mno pumzi nayo ikawa si rafiki
tena,nikafika mahali nikajipumzisha chini ya mti ili
walau nivute pumzi loooooh!! Sikujua kama
nimejipalia makaa ya moto
John alikuja kwa mbele kama mzimu bila Mimi
kumuona aliponikaribia akakohoa kidogo,nilistuka
mno lakini John hakucheka hata chembe na
machoni alikuwa mweusi tiiiii
Nikiwa katika hali hiyo nilinyanyuliwa na mikono
iliyokomaa Barabara na bila kuulizwa nilianza
kupokea kipigo cha haja,makonde yaliyoshiba kama
ya mcheza masumbwi Michael Tyson amvayo
yalinichakaza vibaya mno
Na kama ingekuwa kwa binadamu wa kawaida basi
angekuwa tayari ameaga mashindano haya mapema
sana nasema hivi kwasababu ngumi zile nzito nzito
zilizomtoka John hazikuweza kuniharibu wala
kunitoa hata chembe ya damu mpaka nikajiuliza
Mimi ni kiumbe wa aina gani japo maumivu
niliyokuwa nayapata hayakuwa na kifani
Sikuweza kupata zile nguvu za ajabu upesi hali
iliyochangia kupigika haswaa mpaka nikakumbuka
ule msemo unaosema "siku ya kufa nyani" na
sikuweza kujitetea mpaka pale niliposikia sauti za
watu wakiimba Paranda yaani nyimbo za kuelekea
mazishini na hiyo nd'o ikawa ponepone yangu Siku
hiyo.John aliniachia na kupotea eneo hili kwa kasi
ya ajabu ambayo sikuwahi kuiona kwa binadamu
yeyote hapo kabla
Nilijikongoja japo kwa shida sana na sikuweza
kupukuta vumbi katika sare zangu,nilikatisha
kichakani na kuelekea nyumbani ili kuwakwepa
waliokuwa wanaenda kuzika
Njiani nilikuwa najiuliza maswali kwanini John
anishambulie vile na iweje nishindwe kuzitumia zile
nguvu nilizonazo na je ni nani atakuwa msaada
wangu katika kuyatatua haya.
Nilifika nyumbani na bahati ilikuwa upande wangu
kwani nyumbani kulikuwa kweupe na ukimya
ulitawala ikiamanisha hakuna mtu yeyote
Niliingia bafuni na kufua sare zangu nikiwa namlaani
John kwa kipigo alichonipatia nikijiapiza kuwa
lazima alipe kwa gharama yoyote ile kutokana na
vita aliyoianzisha na kusahau kama Mimi ndiye
mnunuzi wa vita ile toka awali
Nilisafisha mwili pia nikapata chakula nilichoachiwa
baada ya hapo nikaelekea chumbani kwangu
kupumzika nikiwa tayari nimemeza dawa za
maumivu.........
 
Sehemu ya tano
........ilipoishia.......
Niliingia bafuni na kufua sare zangu nikiwa namlaani
John kwa kipigo alichonipatia nikijiapiza kuwa
lazima alipe kwa gharama yoyote ile kutokana na
vita aliyoianzisha na kusahau kama Mimi ndiye
mnunuzi wa vita ile toka awali
Nilisafisha mwili pia nikapata chakula nilichoachiwa
baada ya hapo nikaelekea chumbani kwangu
kupumzika nikiwa tayari nimemeza dawa za
maumivu.........
.............Endelea..........
nilistuka baada ya kuitwa na Sifa,nikaelekea katika
chumba ambacho Mara nyingi huwa tunakitumia
kwaajili ya kula chakula familia nzima.
nilirudi chumbani kwangu kulala,nilipopitiwa na
usingizi ndoto ya kwanza ilikuwa ya mzee Mandevu
akiwa ameketi pembeni yangu,alinishika katika paji
la uso kwa muda kisha akatikisa kichwa kama mtu
alielewa jambo flani.
"Humph kitu kilichofanya ushindwe kutumia nguvu
zako ni kutokana na kutokuwa na imani nazo pia
moyo wako haujakubaliana na hali halisi ya jinsi
ulivyo". Alieleza mzee Mandevu
"Mzee hata Mimi sielewi kwanini nguvu hivi
zinanigomea alafu kwanini hazikwenda kwa mtu
mwingine ila Mimi?"
"Yote hayo ni kwasababu umechaguliwa na
inakubidi uzilinde nguvu hizo ikiwa ni kama zawadi
ya pekee kwako na kwa watu wanaoteseka kwa
kukandamizwa na kuonewa na binadau
wenzao,ukumbuke kuwa bila wao huwezi na bila
wewe hawawezi kufanya kitu kuleta ukombozi"
"Sasa nifanye nini ili kuendana na nguvu hizo na
kuzitawala pale ninapotaka kuzitumia"
"Kwanza inatakiwa ukubali kuwa wewe ndiye
uliechaguliwa kurithi hizi nguvu,pili ule kiapo kuwa
hutozitumia vibaya wala hutozitumia kwa manufaa
yako ila jamii inayokuzunguka na kuwa tayari
kuyatoa Maisha yako kwaajili ya mtu mwingine ni
hayo tu" aliongea mzee Mandevu kwa msisitizo
Haikuwa rahisi kukubaliana nae lakini
nilipokumbuka kichapo alichonipa John niliona
haina haja ya kukataa kwani naweza kupoteza
Maisha kwa ujinga wangu mwenyewe
"Nimekubali kwa moyo wangu wote na nitasimamia
ahadi yako na kamwe sitokuangusha"
Papo hapo bila kuchelewa mzee Mandevu
alisimama na kuinua mikono juu na kupokea taji
ambalo sikujua amelitoa wapi kwa wakati
huo,nikavalishwa taji hilo la kifalme huku nikiwa
tayari nimeshuka kitandani na kupiga magoti,mwili
ulianza kusisimka nikahisi nguvu za ajabu zikinijaa
na kuongezeka maradufu zaidi ya zile za mwanzo
ndipo nikainuliwa na mzee Mandevu "sasa u mmiliki
halali wa nguvu hizi" alisisitiza akiwa na tabasamu
pana usoni mwake
"Ahsante lakini nina swali mzee wangu,Yule
msichana niliyemuona Leo ni nani?" niliuliza nikiwa
na shauku ya kutaka kumfahamu yule binti mrembo
niliyemuona shuleni
"Yule alikuwa ni malkia mwenye nguvu nyingi za
giza na amebahatika kuishi karne nyingi duniani
vilevile alikuwa ni mpinzani wetu namba moja sasa
muda wake wa kuishi umeisha kwani amebakiza
mwaka mmoja tu ili apotee kabisa duniani lakini
nguvu ulizonazo endapo atazipata basi ataishi karne
nyingine nyingi"
"Mmmh!!! sasa nitamshindaje hapo mbona ni kama
mambo yatakuwa magumu?" niliuliza nikiwa na wasi
wasi mwingi
"Jiamini Humph na uhakikishe hazipati hizo nguvu
sawa mimi niko nawe bega kwa bega wakati wote
ukihitaji msaada wangu usisite niite". Alimaliza
kuongea na kupotea huku maneno yake yakabaki
yakijirudia kama mwangwi
Niliamua kusogea kwenye kioo maana nilipojishika
kichwani sikuona dalili ya kitu chochote,nilipo
jitazama sikuamini kuuona mwili wangu
umeongezeka kama mtu ambaye huwa anafanya
mazoezi kila kukicha na kichwani sasa daaah!
nilikuwa na taji la kifalme moja matata kwani
lilikuwa limenakshiwa kwa maandishi flani ya
kung'aa ambayo sikuyaelewa yana maana gani.
Sikulala kutokana na furaha niliyonayo nilichoamua
kufanya ni kupiga goti na kuanza kuomba kwa dhati
nipate mwanga wa kuzitumia nguvu nilizopewa,baad
a ya nusu saa niliinuka nikiwa na jibu moja tu "tuliza
hisia zako mawazo YAKO na akili YAKO kwa ujumla"
hilo jibu ndilo lilinijia moja kwa moja kichwani
kwangu
Kwakuwa nilifahamu wazi kuwa John ataniwinda
shuleni basi nilianza mazoezi ya kutumia nguvu hizi
ninapozihitaji,Japo nilikuwa nimekubali kuwa Mimi
ndiye niliyechaguliwa kuzitumia nguvu hizo
nilichukua masaa mengi kuzitawala nguvu hizi
Nilijaribu saa la kwanza,la pili,la tatu nikafanikiwa
Mara moja niliporudia nikashindwa tena,mda ulizidi
kusonga hatimaye sauti ile inayopenda kusema na
Mimi ikanambia "Tuliza akili unaweza kuliko hata
unavyofikiri"
Nilitiii sauti ile kisha nikajaribu tena huku
nimefumba macho,nikaanza kuhisi utofauti
nilipofungua macho mwanga ukaenea chumba
kizima,nikasogea dirishani ila kabla sijafunua pazia
niliweza kuona mpaka nje tena kwa umbali mrefu
mno
****************************
Kama ilivyo desturi nilikuwa darasani John alikuwa
mbele yangu lakini alikuwa akigeuka Mara kwa
Mara kunitazama akiwa anatabasamu mno na Mimi
sikuonyesha udhaifu kama mtoto wa kiume
nikaamua kurudisha tabasamu licha ya kwamba
moyoni nilikuwa na uchungu wa kipigo alichnipiga
bila huruma.
******************************
Profesa hakuwa nyuma katika mipango yake
alitafuta kamera za barabarani na kuziingilia(hac
king) kisha akaanza kutazama matukio
yaliyorekodiwa na hapo ndipo alipomuona kijana
mdogo Humph akiwa amejibanza kwenye ngazi
mpaka anapojifunga kitambaa usoni na kutoa
msaada
Profesa alitoa tabasamu la ushindi lakini swali
likawa anampataje maana hafahamu anaishi wapi ila
kwa kuwa profesa alikuwa na hisa kubwa ya akili
(IQ) aligundua muhuli wa shule katika shati la
Humph akausogeza mpaka akapata picha kamili ya
muhuli ule.
Simu ya Lamson ilitoa mlio hafifu kumjulisha kuwa
kuna dharura,akaiendea lifti ya jengo hilo na
kupandishwa ghorofa za juu kama kawaida ya
Profesa alikuwa anatazama dirishani akitafakari
mambo kadha wa kadha.
"Ndio mkuu nimeitikia wito" alisema Lamson kwa
ukakamavu wa hali ya juu
"Nimepata mahali(location) lilipo windo letu fika
St.Machele na maelezo mengine yapo katika
bahasha hiyo,hakikisha anafika Leo." Profesa
alimsisitiza Lamson
 
Sehemu ya sita
........ilipoishia.......
Simu ya Lamson ilitoa mlio hafifu kumjulisha kuwa
kuna dharura,akaiendea lifti ya jengo hilo na
kupandishwa ghorofa za juu kama kawaida ya
Profesa alikuwa anatazama dirishani akitafakari
mambo kadha wa kadha.
"Ndio mkuu nimeitikia wito" alisema Lamson kwa
ukakamavu wa hali ya juu
"Nimepata mahali(location) lilipo windo letu fika
St.Machele na maelezo mengine yapo katika
bahasha hiyo,hakikisha anafika Leo." Profesa
alimsisitiza Lamson
...........Tiririka nayo........
*******************************
Upande wa shuleni baada ya kutoka pumziko
tulikuwa tunaelekea chooni kujisaidia John akawa
ananifuata kwa nyuma,nilifurahi mno kumuona
ndege mjanja kanasa kwenye tundu bovu namna
hii.Nilichoamua kufanya ni kumpeleka sehemu nzuri
ili tupambane vyema,nilifika mpaka katika uwanja
wa mpira wa kikapu(basketball) ambao ulikuwa
umejificha kidogo pale shuleni
Haikuchukua muda hasimu wangu akawa amewasili
akiwa na tabasamu tele "Humph hii ni nafasi yako
ya mwisho kutii amri au kufa,nipatie hizo nguvu
ulizonazo nami nitakuacha hai"
kitu ambacho John hakukitambua ni kuwa tayari
nina uwezo mkubwa wa kuzitawala nguvu zile
isitoshe tayari nimesha kabidhiwa kama mmiliki
halali
"Sio kirahisi rahisi hivyo bwana mdogo,kamwambie
huyo mama yako nimegoma tena ikibidi njoo nae"
Niliamua kumjibu John mbaya mbovu tena kwa
kujiamini
"Sintokuacha hai siku ya Leo mwanaharamu wewe
tena utanisamehe kwa hilo" Alibwata John kwa
hasira
Kabla sijamwambia neno la nyongeza nilistukia
amechomoka kama risasi kwenye gobole tena
safari hii alizidi kuwa mweusi machoni machoni
hata kiini chake hakikuonekana,alianza kumimina
makonde yasiyo na idadi tena yenye uzito wa hali ya
juu kiasi kwamba nilikuwa nikiyakwepa basi upepo
wake unanisukuma kidogo
ilikuwa ni mtanange kiukweli yani si wa kitoto
ambao nilijitahidi mno kukabiliana nao ila ulihitaji
ujuzi wa ziada ambao kiuungwana sikuwa nao
kabisa
Nilipoona nimezidiwa na masumbwi ya John baada
ya kuyatoka machache niliamua kumfanyia hila kwa
haraka nikaanza kukimbia pale uwanjani,John akajua
ninamkimbia ikabidi aanze kunikimbiza
Niliongeza kasi na John nae hakuwa nyuma kwani
tulienda sambamba,nikafanya kile nilichokusudia
nkkaongeza kasi Mara mbili ya ile ya mwanzo kwa
kuwa nilikuwa na nguvu hizi za ajabu,John akabaki
nyuma kabisa lakini hakukata tamaa akawa
ameongeza kasi ya kukimbia ili anikamate
Nilivyoona John ameongeza kasi basi nikasimama
ghafla kitendo kilichompagawisha John ambaye bila
kutarajia alipitiliza kidogo pale niliposimama,si
kumpa nafasi ya kusimama nikambatiza teke Kali la
mgongoni na kabla hajadondoka kwa kasi ya hali ya
juu nikamuongeza ngumi nzito ya kisogo iliyompata
sawia na kumbamiza chini na kutoa mlio mkali wa
maumivu kisha kimya kikatawala.
Nikashusha pumzi kwa nguvu nikijua kazi
imekwisha,haikupita hata dakika John akaanza
kujizoa zoa ili ainuke loooooh!!! nikahisi labda John
amekuwa kama mazombi yaani kipigo chote kile
bado ni mzima,Kijasho kikaanza kunishuka taratibu
huku mapigo ya moyo yakianza kuongezeka
taratibu.
John alipoinuka nikawa nimeshapata wazo,John
aliponigeukia tuu nikachomoka kwa kasi
mno,tukakutana uso kwa uso,jicho kwa jicho
kumbuka kuwa John alikuwa na macho meusi tiiii
sasa tulipokutanisha macho mwanga wangu wote
ukaishia machoni mwake taratibu akaanza kulegea
mpaka akaànguka kabisa.
Nikiwa katika kushangaa shangaa kuna kitu kama
sindano kilipenya shingoni mwangu,nikajaribu
kuchomoa nikafanikiwa lakini giza likawa limeanza
kuchukua nafasi machoni mwisho nikaanguka na
sikutambua kilichoendelea eneo hilo.
**********Ilivyokuwa***********
Wakati John na Humph wakiwa katika mpambano
mkali Lamson alikuwa ameshafika na timu yake
mkononi alikuwa amekamata radar yake
inayomuongoza lilipo windo lake
Aliushuhudia ule mpambano ulivyomkali
hakuthubutu kusogea eneo lile maana alijua wai
kuwa hawezi kudumu hata kwa dakika mbili na watu
hao yaani John na Humph, alichoamua ni kusubiri
mshindi Kwakuwa aliamini kuwa kazi yake
imerahisishwa kwa kiasi Fulan.
Alimpa kazi kijana wake mmoja arekodi tukio zima
linavyokwenda,Lamson alichukua bunduki yake
maalumu ya kudungulia maarufu kama sniper kisha
akaweka kisindano kimoja chenye dawa ya usingizi
na kulenga eneo la tukio na aliyafanya yote hayo
maana alifahamu vyema uwezo wake katika
kudungua(shabaha).
Bahati ilikuwa upande wake kwani Humph
alipomzimisha John basi Lamson akafanya yake
bila kukosea,Lengo lake likawa limetimia.
Akaagiza vijana kuubba mwili wa Humph na
kuondoka nao eneo hilo bila mwanafunzi yeyote
kutambua.
*******-**--*-******--*--**
Profesa alikuwa ameandaa maabara maalumu
kwaajili ya kumfanyia humph uchunguzi
anaoufahamu yeye binafsi una lengo gani,jambo
ambalo Profesa hakulijua ni kwamba nguvu za Yale
macho ya ajabu hazikuwa za kisasa bali za kienyeji
zaidi
Profesa hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo
alimlaza Humph katika kitanda mojawapo na
kuruhusu mwili huo uingizwe katika chumba kidogo
kwaajili ya uchunguzi
Baada ya dakika kadhaa uchunguzi ulikamilika,Pro
fesa aliangalia majibu kwa umakini wa hali ya juu
Kisha akachukua sampuli ya damu kiasi ya Humph
na kuelekea nayo katika maabara.
Baada ya kuchunguza kwa muda mrefu hakuambulia
chochote hivyo akaona bora amuingize Humph
katika chumba alichokuwa amekiandaa maalumu
kwaajili ya majaribio,Lengo kuu alikuwa anahitaji
kutambua ni namna gai ataweza kutengeneza nguvu
kama zileza macho ya ajabu.
Alimuweka Humph katika chumba chennye taa
zenye mionzi mikali katika kila kona ya chumba
hicho,akaruhuu mlango kufunga kisha akachukua
iPad yake na kuanza kuminya minya
Haikuchukua muda zile taa zenye mionzi zikawaka
lakini hazikuwa na madhara yoyote latika mwili wa
Humph jambo lililomfanya Profesa aongeze
mwanga zaidi na zaidi mpaka kompyuta zake
zikaanza kumpa onyo na ving'ora vya hatari ilikuwa
vikipokeza kumpa taarifa kuwa anachokifanya
kitaleta athari mda si mrefu.
Hakujali hilo zaidi ya kuendelea kuongeza volti
mpaka cheche zikaanza kutoka katika mitambo
yake na hatimaye mlipuko mkubwa ukatokea eneo
hilo...
 
Sehemu ya saba
........ilipoishia.......
Hakujali hilo zaidi ya kuendelea kuongeza volti
mpaka cheche zikaanza kutoka katika mitambo
yake na hatimaye mlipuko mkubwa ukatokea eneo
hilo...
...........Endelea...........
Mlipuko huo ulimtupa mbali sana Profesa ambaye
mpaka mpaka kikosi cha zima moto na watoa
huduma ya kwanza wanafika eneo hilo Profesa
alikuwa hatamaniki katika macho ya kiumbe yeyote
ambaye angefanikiwa kimtazama kwa mda huo.
***************************
Humph alistuka akiwa katika chumba ambacho
kilikuwa na mhudumu (nesi)mmoja alievalia nguo
nyeupe tupu. Kwa mawazo ya haraka haraka alifikiri
huenda amefika mbinguni kutokana na madhari ya
chumba na nesi huyo alivyovalia.
Baada ya kukutanisha macho na nesi huyoo nesi
alitabasamu na kuanza kumsogelea Humph
"Pole sana kijana kwa matatizo yaliyokupata tena
afadhali umeamka"
"Samahani dada ni matatizo gani unayozungumzia
na hapa niko wapi?"
"Ooooh!! kweli samahani kwa kutoku kueleza,hapa
ni hospitali,hispitali ya Dr.Alex Jr nadhani
unaifahamu pia uliletwa hapa kutokana na ajali ya
moto uliosababishwa na mlipuko"
Humph alitikisa kichwa kuashiria amekubaliana na
maneno ya nesi huyo.
Wazazi wa Humph walifika na kukuta mtoto wao
akiwa salama salimini licha ya kuwa na majeraha
madogo madogo mwilini.Waliruhusiwa kuondoka na
mgonjwa kwani Huduma zilizobaki angepatiwa
nyumbani
*****************************
Ilipita wiki moja kutokana na ushauri wa daktari
kwamba ilipaswa mgonjwa apate muda mzuri wa
kupumzika.Ndipo nilianza kwenda shule maana afya
yangu ilikuwa imeanza kuimarika kama ilivyokuwa
hapo awali.
Kila mwanafuni niliekutana nae alikuwa ananipa pole
kutokana na lile tukio la mlipuko na kutoweka
kwangu kwa muda mrefu.Nilifanikiwa kumuona
John ambaye kwa sasa alikuwa tofauti mno na yule
wa mwanzo niliemzoea huyu alikuwa mpole
balaaaaa!!
Kwa kipindi chote hiki niliishi kwa amani shuleni
japo sikujiaminisha kuwa maadui wangu wameisha
kwahiyo nilikuwa tayari kwa lolote na muda
wowote.
Siku moja asubuhi nikiwa nasafisha madirisha ya
darasani kwetu ndipo nikamuona Madam Remijo
akiwa amesimama katika korido ndefu linaloelekea
darasani kwetu
Alipoona nimemtazama tu akaniita kwa ishara
nimfuate nami bila ubishi nikamfuata maana
waswahili wanasema kubali wito kataa neno
Nilimfuata mpaka katika gari lake,akaniomba niingie
ndani kisha tukaondoka eneo hili la shule.
Barabarani kila mtu alikuwa kimya muda wote
akiwaza ya kwake yanayomsibu mpaka pale
tulipoifikia nyumba moja ya kawaida na yenye wigo
mpana.
Tuliingia ndani ambako kilikuwa na samani za
gharama mno tofauti na matarajio yangu kwani
nyumba haikuwa ya hadhi kubwa sana kulinganisha
na samani hizo.
Madam akaelekea katika vyumba vingine na
aliporudi alikuwa na glasi mbili za juisi mkononi
"Karibu sana hapa nd'o nyumbani kwangu"
"Nashukuru kupafahamu"
"Hapa ninaishi peke yangu kwahiyo kuwa huru kwa
chochote sawa"
"Mmmmh" niliguna
"Achana na hayo,nimekuleta hapa kutokana na
matatizo mbalimbali yanayokukabili pia ilikuwa
nahitaji nikushauri mambo mawili matatu kama
mdogo wangu ama mwanafunzi wangu"
"Mambo yapi hayo Madam"
"Nafikiri ni matukio kadhaa sasa yamejitokeza
katika kipindi hiki cha karibuni sasa nina imani
wewe ndiye mtu ambaye unawakomboa wahanga
hao." Madam akashusha pumzi na kunitazama
kuashiria niongee kitu hapo
"Aaaaah!!! hapana madam utakuwa umekosea
kubashiri." nilizungumza kwa utulivu kabisa nikiwa
najaribu kuikwepa kesi hii
"acha upuuzi wewe sijakuleta hapa kukuuliza ila
nimekuleta hapa ili nikupe onyo alafu uchukue
tahadhari juu ya haya uyatendayo maana mpaka
sasa utakuwa unawindwa na vyombo vya dola kwa
kujifanya shujaa kuliko wao pili utakuwa
umejitengenezea maadui maana unawaharibia
mipango yao upo halo?". Looooh! nilichoka kwa
maneno yale ambayo kiukweli yalinifungua akili na
kutambua kuwa kweli mtu mzima dawa.
"Sasa hakikisha unajiandaa na hatari zinazokuja
mbele yako na uwalinde uwapendao la sivyo
utapoteza kila kitu"
sikuwa na swali zaidi ya kubaki mdomo wazi kwani
yote aliyoyasema madam yalikuwa sahihi kabisa na
yenye upeo wa mbali sana.
******************************
Kama kawaida yangu usiku nd'o ulikuwa wa
majanga kwangu kuliko mchana,nikiwa nimelala
nilianza kuota ndoto ambayo ilikuwa kama maono
kwangu. Mdogo wangu wa pekee Sifa alikuwa
amekamatwa na mnyama mmoja hivi mfano wa
simba ila yeye alikuwa na meno marefu yaliyotokeza
kwa nje na pembe kama za faru.
Macho yake yalikuwa yanawaka waka mithili ya
moto mkali uliochochewa vilivyo.Alionekana yupo
kwenye pango liliokuwa linafanana na mapango ya
zamani mno ambayo yalitumiwa kama makazi ya
kuishi enzi za mababu zetu
Pia ilikuwa limezungushiwa miale ya moto
iliyotumika kama taa za eneo hilo huku mdogo
wangu akiwa amelala chini hajielewi.
Nilistuka kutoka usingizini ikiwa bado ni usiku
katikati nikaelekea chumbani kwa Sifa,mlango was
chumba chake ulikuwa wazi jambo ambalo halikuwa
kawaida yake. Mapigo ya moyo yalianza kunienda
mbio nilipochungulia ndani na kushuhudia vitu
vikiwa vimetupwa ovyo ovyo ni kama kulikuwa na
ugomvi eneo hilo.
Nklibaki nimeduwaa nikiwa siamini kile kilichotokea
mda mfupi uliopita maana hakuna aliestukia kama
mle ndani kuna mtu ametekwa na cha ajabu zaidi
hatukuweza kuisikia sauti ya mtu kuingia mle ndani
wala kelele zozote za Sifa wakati wa kukamatwa
Nilichanganyikiwa lakini kwasababu jamaa
wamegusa pabaya namimi nitawafanyia timbwili la
hatarii. Nikafunga macho kwa muda nikaanza
kuvuta hisia kisha nikayafungua ghafla macho
yakawaka na kutoa mwanga mkali mno kutokana na
hasira inayowaka mwilini mwangu........
 
Sehemu ya nane
........ilipoishia.......
Nilichanganyikiwa lakini kwasababu jamaa
wamegusa pabaya namimi nitawafanyia timbwili la
hatarii. Nikafunga macho kwa muda nikaanza
kuvuta hisia kisha nikayafungua ghafla macho
yakawaka na kutoa mwanga mkali mno kutokana na
hasira inayowaka mwilini mwangu........
.........Teremka na moto mnene......
Ramani nzima ya pangoni nilikuwa naiona machoni
mwangu kutokana na hasira niliyokuwa nayo nilitoka
nje taratibu kisha nikachomoka kama risasi
nikiifuata ile njia niliyokuwa naiona kwenye ramani
ya macho yangu
Nilikimbia kwa umbali mrefu mno na hatimaye
nikafika ndani ya lile pango nikakutana na maudhui
yale yale niliyoyaona ndotoni,ndipo nilikutana na
adui yangu ambaye alionekana wazi aliufahamu ujio
wangu mahali pale hivyo alikuwa amejiandaa
vilivyo.
Alianza kuwaka macho na Mimi nikawa na kazi ya
kumtazama akazidisha mwanga wa macho yake na
Mimi nikazidisha mwanga wa macho yangu ikawa
kama mashindano ya nani nwenye mwanga mkali
japo tulitofautiana yeye alikuwa anatoa mwanga
wenye miale kama ya moto Mimi nikatoa mwanga
Mweupe kama dhahabu
Mnyama yule aliunguruma kwa hasira Mimi sikuwa
na papara nilisimama tu nikiwa namtazama mda
huo Sifa alikuwa amelala pembeni hajitambui.
Nikakunja ngumi na hofu ikiwa imenitanda
vilivyo,Mnyama yule alifungua kinywa chake moto
ukatoka kwa kasi kuja kwangu
Niliteleza chini moto ukapita juu na kabla sijakaa
sawa moto mwingine ulinifuata chini nikajirusha juu
lakini kutokana na kasi ya moto ule suruali ilishika
moto miguuni nilipotua chini ukazima kwa haraka
kabla haujasambaa japo nilihisi maumivu ya
kuungua kwa mbali
Nilipouzima moto ule yule mnyama alitulia macho
yakiwa yamebadilika na kuwa ya kawaida lakini
hayakuchukua muda yakawa ya rangi ile ya miale ya
moto kama awali
Alianza kutema vitu kama goroli mfululizo kazi
yangu ikawa kukwepa ambapo niliyumba
kulia,kushoto,chini na kuruka juu huku vile vidude
vikitoa mlipuko wa moto vinapodondoka au
kugonga ukuta wa pango.
Sikuwahi kujifunza kuruka sarakasi ila siku hiyo
ilikuwa maajabu kwani niliweza kuruka shufwa kwa
wepesi mno nikirudi nyuma mpaka katika ukuta wa
pango ambapo niliruka na kunasa juu kama popo
yaani kiukweli nilikuwa naaujuzi zaidi ya maninja.
Yule mnyama alitulia tena,kwa haraka akili yangu
ilicheza haraka kabla macho yake hayajabadilika
nikaanza kukimbia kwa kasi nikimfuata sehemu
alipo,nilipomkaribia macho yake alikuwa yamesha
badilika,kengele ya hatari ikagonga kichwani
mwangu.
Alipojaribu kufungua mdomo ateme moto nilikuwa
tayari nimeshamfikia nikauziba mdomo wake kwa
kutumia nguvu zote,ule moto ukalipuka na kunitupa
mbali Yule mnyama akawa amesambaratika.
Niliinuka kwa kujikakamua mpaka pale alipo Sifa
nikamnyanyua na kumbeba mgongoni japo nilikuwa
na maumivu makali mwilini.
Kutokana na mtikisiko uliotokea katika lile pango
udongo ulianza kuporomoka jambo ambalo lilikuwa
hatari kwa Maisha yetu,sikuwa radhi kufa kizembe
namna ile,nikajikaza kiume na kuanza kukimbia kwa
kujivuta mpaka nikafanikiwa kutoka nje ya lile
pango nakuliacha likididimia ardhini.
Tulifika nyumbani alfajiri hii ni kutokana na umbali
mrefu kutoka pangoni mpaka nyumbani,Sikuwa na
haja ya kulala tena,nikaanza kupanga vitu
vilivyokuwa vimevurugwa mle chumbani kisha
nikaingia kuoga na baada ya hapo nikajiandaa
kwenda shule huku nikimuacha Sifa akiwa
anakoroma kutokana na usingizi mzito aliokuwa nao
japo haikujulikana aliwekewa nini mpaka akawa vile.
******************************
Asubuhi na mapema nilikuwa shuleni nikifanya usafi
katika vioo vya madirisha ya darasani kwetu ndipo
nikamuona madam Remijo akiwa amesimama
katika korido,alipogundua namtazama aliinita kwa
ishara nimfuate nami bila ubishi nikafanya kama
anavyotaka
Nilimfuata mpaka katika gari yake ambapo
aliniomba niingie kisha tukaondoka eneo hilo.
*****************************
Barabarani kila mtu alikuwa kimya muda wote
akiwaza ya kwake yanayomsibu mpaka pale
tulipoifikia nyumba moja ya kawaida sana na yenye
wigo mpana.
Tuliingia ndani kisha madam akashuka nami
nikamfuata kwa nyuma hadi sebuleni ambako
kulikuwa na samani za gharama tofauti na kazi
anayofanya kwani Mara nyingi waalimu wanaongoza
kwa kuwa na Maisha ya taabu hii yote ni kutokana
na mishahara midogo
Madam aliingia katika chumba kimoja na alipotoka
alirudi na glasi mbili za juisi na kunipatia moja.
"Karibu hapa ndipo nyumbani kwangu"
"Ahsante na ninashukuru kupafahamu"
"Bila kupoteza lengo nimekuleta hapa kwasababu
moja tu ni kuhusu matukio kadhaa yanayotokea
hapa mjini nadhani unayafahamu"
"Hapana sifahamu"
"usiwe na wasi wasi hapa ninaishi peke yangu hivyo
kuwa huru, nazungumzia ajali ile iliyotokea shuleni
siku ile na ajali iliyotokea barabarani siku kadhaa za
nyuma."
"Sawa nalifahamu hilo suala endelea"
"Sasa nafahamu kuwa wewe ndiye Yule kijana
ambaye anazungumziwa sana na watu pamoja na
vyombo vya habari pia nafahamu kuwa wewe ndiye
huyo kijana maana uliniokoa siku ile nilipopatwa na
ile ajali" akakaa kimya kidogo akiruhusu mate yapite
kooni kisha akanitazama vizuri usoni ikiwa
hakutambua kuwa ameniacha njia panda maana
sikuelewa anataka kuzungumzia kitu gani
 
Sehemu ya tisa
........ilipoishia.......
"Sasa nafahamu kuwa wewe ndiye Yule kijana
ambaye anazungumziwa sana na watu pamoja na
vyombo vya habari pia nafahamu kuwa wewe ndiye
huyo kijana maana uliniokoa siku ile nilipopatwa na
ile ajali" akakaa kimya kidogo akiruhusu mate yapite
kooni kisha akanitazama vizuri usoni ikiwa
hakutambua kuwa ameniacha njia panda maana
sikuelewa anataka kuzungumzia kitu gani
.........Shuka nayo...........
"kitu cha kwanza naomba nikupe tahadhari juu ya
uokoaji wako kwani ni lazima uwe unawindwa na
watu wasio penda unachokifanya pili lazima
upelelezi ufanyike ili wamjue mtu anayejifanya
shujaa kuliko vyombo vya dola,tatu kuna watu
lazima tu watahitaji kukupata wewe au kutambua
chanzo cha nguvu zako na ukumbuke si kila
amaeluchekea basi ana mapenzi mema na
wewe,upo hapo?"
duuuuh!! ukisikia mwanaume kuchoka Mimi kweli
nilichoka maana hata matukio ya nyuma yote ya
kufuatwa fuatwa ni kwasababu ya hizi nguvu
nilizonazo na niliamini kuwa mtu mzima dawa
kutokana na maneno yake kunigusa na kunifungua
akili
"kwahiyo hakikisha unajiandaa na hatari zinazokuja
mbele yako ama la! acha hiyo kazi itahatarisha
Maisha yako japo uamuzi ni wako" Aliongezea
madam Remijo
Sikuwa na la kumjibu zaidi ya kutafakari maneno
yake kwa kina
******************************
Lisa alikuwa ni binti mmoja mrembo sana katika
shule yetu yaani ukisema ushindanishe kuanzia wale
wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha
sita,alikuwa anashika nafasi ya kwanza,si waalimu
si wanafunzi walimsifu kwa uzuri wake
kutokana na Sifa hizo haikuwa rahisi kwa
mwanaume yeyote yule kujitumbukiza bila
mahesabu kwani wengi wao walishatupwa nje yaani
aliwakatalia kata kata kuanzisha mahusiano binafsi
nasema ni msimamo ambao wadada wengi sana
huwa wanafeli hicho kitu na kujikuta wakichezewa
kama mpira wa kona
Sikuwahi kumsemesha darasani sababu ilikuwa ni
hadhi yake aliyonayo,sasa siku hii ilikuwa ya
ngekewa kwangu,nisikie vizuri hapa mda wa kutoka
shuleni ulifika kama kawaida yangu nilikuwa peke
yangu tena wa mwishoni mwishoni njaa ilikuwa
imenizibua mno wale wenzetu wanaita ubao basi
nikiwa nimefika karibu na getini zile hisia za maono
zikapita chwaaapu unaweza kuziita ndoto za
mchana
Niliona bango moja kubwa likiwa linafanyiwa
marekebisho na mafundi katika jengo moja refu
mno liliopo jirani na shule yetu likianguka na kwa
bahati mbaya kuna msichana alikuwa akikatisha
eneo hilo hilo likamponda vibaya mno
ikanibidi nisimame kwanza na kulifikiria hilo tukio
naanzaje kukabiliana nalo ila kilichonistua zaidi ni
yule msichana asiye na hatia anavyoenda
kuangamia
kutokana na uwingi wa wanafunzi nilishindwa kuona
mbele ikanibidi nikimbilie getini na kusimama juu
ya nguzo moja iliyomiminwa kwa zege pembeni
kabisa ya geti,nilipotupa macho mbele nikijaribu
kutazama uelekeo wa jengo nililoliona,sikuamini
kwa haraka baada ya kumuona lisa peke yake akiwa
anakaribia kuvuka barabara kuelekea lilipo lile
ghorofa
Nilitazama kushoto na kulia sikumuona mtu yeyote
anaenitazama kwani wengi wao walikuwa wanawahi
usafiri na wengine walikuwa wamezama katika soga
za hapa na pale hata mlinzi nae hakushughulika na
Mimi
ndipo nilipoamua kufanya yangu,kwa tahadhari ya
hali.ya juu nilishuka katika nguzo ile na
kuchuchumaa pembeni yake ili isiwe rahisi kwa mtu
wa upande wa pili kunitazama,nikaondoa shati langu
la shule upesi nikabaki na tisheti ile ya kazi nadhani
wengi wenu mnaitambua ni ile tisheti inayoubana
mwili wangu kiasi,bila kuchelewa kwa kasi ile ile
nikatoa kofia niliyoiandaa maalumu kwaajili ya kazi
hii alimaarufu kama kapelo,kisha nikachukua
kitambaa cheusi nilichokiteua baada ya kukabidhiwa
rasmi nguvu hizi za macho yangu ya ajabu
nikajifunga vuzuri tayari kwa kumkomboa Lisa
Niliinuka kwa kasi kubwa bila kusahau begi langu
ambalo tayari lilikuwa mgongoni na kufuata uelekeo
ule alioenda lisa,nilipotaka kuvuka barabara gari
zikawa zinazidi kupita alafu Lisa alikuwa amebakiza
hatua chache kulifikia lile jengo,sikuwa na njia
nyingine ya kufanya ikabidi nijitose barabarani na
kukatisha kitendo kilichowakera sana madereva
walionikwepa na kunitupia matusi mazito mazito
huwezi amini ndugu msomaji nikikuambia kuwa
kuwa kuna njemba zimebarikiwa kwa matusi kama
huyoo uliemsikia yaani ni kasheshe sijui
hawatambui kuwa wanajishusha hadhi.
Nilikimbia mno ila kiufupi nilikuwa nimechelewa
mno kumfuata mrembo yule,nikaanza kumwita sasa
ili labda nimwambie anisubiri japo moyoni nilijua
hawezi kwasababu yeye ni matawi ya juu iweje
anisubiri mimi matawi ya chini nd'o mjifunze hapo
wadada unaweza kuitwa si kwa kutongozwa bali
kusaidiwa na mengine kedekede.
Na kweli nilivyowaza ndivyo ilivyotokea kwani
hakujihangaisha hata kugeuka nyuma looh!! kweli
siku yako ya kufa huwezi kuijua, nilikadhana lakini
wapi cha kustaajabisha zaidi na kuniacha hoi ni pale
aliposimama pale pale usawa wa lile bango kisha
akageuka na kutazama ni nani anayemuita,aliangaza
angaza kila sehemu huku na kule kwa muda na
macho yalipotua kule sauti inapotokea akabaki
ameduwaa ni kama mtu anaetafakari kitu Fulani
nadhani hapo msomaji utakuwa umenielewa na
kama sivyo naamanisha kuwa hata kama ingekuwa
ni wewe umeitwa unageuka unamuona anaekuita
anakuja kwa kukimbia na kupenya kwa watu alafu
mbaya zaidi haonekani sura ila sauti pekee huku
watu wakimshangaa wakidhani huenda anacheza
kamchezo fulani au amerukwa na akili
Tuachane na hilo Lisa alibaki na mshangao usio
elezeka na hapo ndipo nilipopataka lengo ikiwa ni
kumsimamisha asisonge mbele japo mtihani huo
nilikuwa nimeshafeli kwasababu alisimama eneo la
tukio
Nilijitahidi kusogea kadri niwezavyo ili mradi niokoe
roho ya mwanadada huyu mrembo,kila hatua
niliyopiga moyo uliongeza kudunda kwa kasi ikiwa
ni kama ishara ya kuwa tukio baya linakaribia
kutokea lakini kwa ubishi wangu sikutaka
kushindwa kirahisi namna ile
Chozi lilianza kunidondoka hata kabla sijafika kwa
Lisa sikujua ni kwasababu gani lakini yote kwa yote
niliamini ni wasi wasi wa kushindwa kumuokoa Lisa
katika kizaa zaa kile.
Ukisikia mwanaume mawazo yanapishana ni hapa
kwani ile taswira ya kifo cha Lisa ilinijia kichwani na
bila kutarajia lile bango kule juu likaachia na Mimi
bila kujizuia nilistukia nimepiga makelele
"hapanaaaaaaaaaaaaaa" zikiambatana na mwanga
mkali mno uliowafanya watu kuziba macho yao japo
ni mchana.....
 
Sehemu ya kumi
........ilipoishia.......
Ukisikia mwanaume mawazo yanapishana ni hapa
kwani ile taswira ya kifo cha Lisa ilinijia kichwani na
bila kutarajia lile bango kule juu likaachia na Mimi
bila kujizuia nilistukia nimepiga makelele
"hapanaaaaaaaaaaaaaa" zikiambatana na mwanga
mkali mno uliowafanya watu kuziba macho yao japo
ni mchana.....
............Endelea..........
Lisa hakutambua kinachoendelea lakini kutokana na
kelele za watu aliinua uso juu ndipo akashuhudia
bango lile linavyokuja kwa kasi akawa ametumbua
macho kwa uoga wa ajabu uliomuingia
Bila kutarajia zile kelele zangu zilizoambatana na
mwanga mkali ambao ulilifanya bango lile kupungua
kasi na kubadilika rangi,ghafla kuna sauti ile
inayopenda kuzungumza nami ikaniambia nifunge
macho kisha nifungue maana bado nilikuwa mbali
mno ili kumfikia Lisa
Nikaifuata ile sauti na kufumba macho ukapita
kama upepo hivi nilipofumbua nilikuwa tayari
nimemfikia Lisa bila kuzubaa nikamshika Lisa na
kufumba macho tena kisha nikafungua,ajabu kweli
tulikuwa tayari tuko mbali kidogo na lile bango
lililotua chini kwa kishindo kikubwa na kutawanyika
vipande vipande
Lisa alikuwa amenikumbatia kwa woga mno huku
akitetemeka na kichwa amekilaza kifuani kwangu
mpaka mapigo yake ya moyo nikawa nayasikia
yanavyopiga kwa hasira,akawa analia kwa kwikwi
ndipo nikamtoa taratibu katika mwili wangu
Watu na wanafunzi walikuwa wakitushangaa na
wengine wakitusindikiza kwa makelele na wengine
wakipiga makofi. Kuna baadhi walithubutu kusema
"Shujaa" wengine"jeshi la mtu mmoja"
Lisa aliponyanyua macho kunitazama usoni alistuka
na kunisukuma kando,kutokana na uoga aliokuwa
nao alizidi kutetemeka kuliko awali.Nikagundua
kuwa ameyaona macho yangu yanavyotoa nwanga
mweupe
Nilivyoona bado ananiogopa nikafunga macho na
kutoweka eneo lile baada ya kuona amegeuka
kuwaangalia watu wanaoshangilia.
****************------******************
Lisa alibaki ameduwaa akijiuliza maswali kichwani
mwake"inakuaje mtu awe anawaka machoni? tena
mwanga mweupe ni kama hana mboni au ni jini? na
kama ni jini kwanini awe amevaa viatu wakati
hadithi za majini zinazosimuliwa huwa wanasema
huwa hawana miguu ya kawaida.
alafu mbona amevaa mkufu wenye msalaba laaah!!
ila kama kweli ni jini nimekwisha Mimi litanifuata
kila mahali.
Akiwa amezama katika dimbwi la mawazo
waandishi wa habari walikuwa wameshafika eneo
hilo na kuanza kumpiga picha na wengine wakiwa
wanamhoji maswali lukuki
"ilikuwaje mpaka ukaokoka katika hatari kubwa
namna hii?"
"unamzungumziaje huyo kijana aliyekuokoa"
"He unadhani kijana aliyekuokoa ni shujaa katika mji
huu kama wengine wanavyosema?"
"Je huyo mtu anaesemekana amekuokoa
unamfahamu au mna uhusiano wowote ule?"
"kwanini yule kijana amekuokoa wewe tu na si mtu
mwingine maaana ajali zinazotokea ni nyingi mno"
"hivi unatambua kuwa wewe ni miongoni mwa watui
wenye bahati duniani?"
Kana unavyofahamu waandishi wa habari wakiwa
kazini huwa ni wasumbufu mno ilimradi wapate kitu
cha kuandika katika tukio hilo.
Lisa aligutuka baada ya maswali kumfikia akatafuta
upenyo na kwa bahati nzuri aliweza kupata nafasi ya
kukimbia na waandishi hawakuwa nyuma
walimfuata,kuna taxi moja ilikuwa imepaki kando ya
barabara Lisa akaingia humo na kumuamuru dereva
kuliondoa haraka eneo hilo nae bila ubishi akatii
kwani lengo lake ilikuwa kupata pesa.
*******-***--*****--***--**
Humph alipofungua macho alikuwa tayari amefika
karibu na uzio wa nyumbani kwao,akatoa kofia na
kitambaa usoni kisha akaelekea ndani
kitendo cha kuingia sebuleni akakuta baba yake
anataza taarifa ya habari zilizofika punde kimombo
tunaita(breaking news) zikiwa zinaelezea tukio la
ajali ya kushangaza ambapo msichana mmoja
aliponea chupuchupu baada ya bango moja
lililokuwa katka matengenezo kudondoka kutoka juu
lakini msichana huyo aliokolewa na kijana mdogo
kimiujiza na haijulikani kijana huyo alitokea wapi
wala alikoelekea mpaka muda huu.
Inasemekana kijana huyo ni Mara ya pili kutenda
msaada,pia kijana huyo ni mfano wa kuigwa
miongoni mwa vijana wengine bila kujali umri elimu
na hali ya Maisha ya mhanga huyoo.
Humph aliachia tabasamu pana baada ya kuzisikia
Sifa zinazotolewa na waandishi wa habari,ndipo
mzee Kasai akamgeukia Humph
"umesikia wenzio wanavyosifiwa,tena inasemekana
ni kijana mdogo rika lako kabisa"
"Ndiyo baba nikesikia lakini hiyo ni nafasi yake tu
na uwezo alionao ambao kwa hao wengine
hawajajaaliwa"
Mzee Kasai hakuelewa kama nimetumia fumbo
ambalo alihitaji akili ya ziada kulifumbua
"kweli kabisa mwanangu lakini wewe kama mtoto
wa kiume yakupasa ujifunze matendo mema kama
hayo ya kusaidia watu katika shida mbalimbali
ambazo unaweza kuzitatua ili na Mimi siku moja
nijivunie kuwa na kijana shupavu kama huyoo"
"Sawa baba nitajitahidi na Mimi niwe mfano bora
katika jamii"
"Eeeh! mwanangu kazana bwana kwani hata wazazi
wa huyu kijana wanajivunia sana kuwa na mtoto
shujaa katika familia yao".....
 
Sehemu ya kumi na moja
.....Ilipoishia.........
"Eeeh! mwanangu kazana bwana kwani hata wazazi
wa huyu kijana wanajivunia sana kuwa na mtoto
shujaa katika familia yao".....
.........Shuka nayo........
Humph aliondoka sebuleni pale ila kichwani alikuwa
akijisemea usilolijua litakusumbua lakini naamini
ipo siku utaufahamu ukweli japo sifahamu matatizo
nitakayokumbana nayo mbeleni.Aliingia chumbani
mwake na kuelekea moja kwa moja katika kioo
kikubwa cha chumbani kwake akawa anajitazama
jinsi alivyobadilika maumbile yake tofauti na hapo
awali hapa alikuwa akionekana ni mwanaume wa
shoka
Lakini alishangaa sana eneo la shingoni mwake na
kugundua kuwa kuna kitu kimepungua,ilikuwa ni
mkufu wake haupo katika shingo yake na alipovuta
kumbukumbu alikumbuka kuwa aliuvaa alipokuwa
anaenda shuleni na alihisi wazi kuwa atakuwa
ameuangusha eneo lile la tukio.
****************************
Asubuhi na mapema Lisa aliwahi kwenda shuleni
tofauti na hapo awali kama alivyozoeleka na siku hii
alikuwa nafuraha mno,mkononi alikuwa ameahikilia
mkufu wenye msalaba ambao aliamini kabisa kuwa
mmiliki ni yule aliyemuokoa na huenda atakuwa
anamfahamu yeye vilivyo nd'o maana alimuokoa
tena kitu kilichompa asilimia nyingi ni kwasababu
mtu yule alikuwa anamwita jina lake.
Alipokuwa anaingia darasani alikuwa ameushikilia
ule mkufu ila akaona itakuwa sio vyema wenzake
wakauona na kuanza kumhoji kama ilivyo kawaida
ya wadada huwa hawapendi kitu kipite hivi hivi,
hivyo akauweka mfukoni na kuendelea kukatisha
kwenye vinjia vilivyopo katika safu zile za madawati
ya kukalia.
Ilikuwa ni muda wa masomo.Humph alikuwa
anachora picha yake akiwa amevaa kofia na
amejifunga kitambaa huku amemkumbatia
lisa.Akiwa ametuliza mawazo katika karatasi Lisa
alifika na kuketi jirani yake huku akiitazama ile
karatasi na mchoro wake. Lahaulaaa!! akakumbuka
tukio lililotokea siku iliyopita na picha inayochorwa
akagundua vinafanana kabisa.
Moyo ukamlipuka kwa mshangao ikifuatiwa na sauti
iliyomponyoka "tobaaaaaaaaaa!!!!"
Ndipo Humph alipostuka pamoja na wanafunzi wote
wakageuka kumuangalia,Lisa aliyekuwa ametoa
macho kisha wakaanza kumcheka bila kujua
yaliyomsibu moyoni mwake.
Humph aliifunika ile picha mapema baada ya
kubaini kuwa mtahiniwa amemfumania bila chenga
"Samahani Humph unajua hiyo picha uliyoichora ni
ya siku ile ya tukio sasa sijui..." Alishindwa
kumalizia baada ya kuanza kuweweseka na hofu
kumjaa akiyakumbuka yale macho aliyoyaona
"ni sawa na usijali kuhusu hilo kwani nilivutiwa tu na
jinsi mlivyokuwa mmeendana nd'o maana nimefikia
hatua ya kuchora"
"Mmh!! unataka kuniambia kuwa......" akashindwa
kumalizia
"Mnafaa kuwa pamoja"
Alimalizia Humph kwa kuwa aliamini nafasi za
dhahabu kama hizi hutokea Mara moja moja sana
hivyo akaamua kuirusha karata yake
Lisa akicheka"Mmmh! inaonekana unamfahamu
vilivyo...." kabla hajaongeza neno mwalimu aliingia
ndipo Lisa akainuka na picha aliyochora Humph bila
kuomba huku akitabasamu na kumkonyeza Humph
aliebaki ameganda kama amepigwa shoti ya
umeme
"We Humph hebu simama bwana inamaana
haujamuona mwalimu au?" Ilikuwa ni sauti ya Jeko
iliyomzindua Humph baada ya kuhamishia mawazo
kwa Lisa
***************************************
Ilipohitimu saa moja usiku Humph alitoka nyumbani
kwa madai kuwa anaenda kwa rafiki yake Jeko
akaazime daftari kwaajili ya kuandika nukuu huku
kichwani akiwa na lengo la kwenda eneo la tukio
kutafuta mkufu wake
Kwa kuwa haikuwa mbali sana ilimchukua robo saa
kuwasili eneo hilo,Alitafuata kila mahali alikohisi
labda atakuwa ameangusha mkufu huo lakini
hakufanikiwa kuupata.
Wakati huo huo Lisa alikuwa akiitazama picha
aliyoichora Humph na katika hali ya kushangaza
alikuwa akitabasamu peke yake kila mara
anapoitazama picha ile na mwisho akaona bora
atoke eneo hilo la nyumbani kwao na kuelekea
sehemu tukio lilipotokea ili walau amuone kijana
huyo.
Humph aliendelea kuzunguka zunguka maeneo hayo
na kwa bahatk mbaya alipokuwa anaangalia chini
kama atauona mkufu wake akapigana kikumbo na
mtu aliyopo mbele yake.
Kwa haraka alimdaka mtu yule asianguke lakini
punde tu alipomtazama usoni na ktanguliza
samahani za dhati kutoka moyoni mwake
alishangaa kuona ni Lisa mwanafunzi mwenzake.
"Haaa!! Lisa vipi usiku huu unafanya nini huku?"
"Mmh!! kwani ajabu natembea tu kuangalia mji"
"weee! huogopi??"
"nimeshazoea maana mara nyingi huwa napenda
kuona taa zinavyoupendezesha mji wakati wa usiku.
Kwani we umefuata nini?"
"Hata Mimi nilikuwa matembezini tu kama wewe."
Yaani kiukweli wote tulikutana ni waongo watupu na
kila mtu akabaki na siri yake kilichomleta mahali
hapo bila kujua kwamba tunatafutana.
"Basi twende huku nikuonyeshe kitu" Alisema Lisa
ambaye tayari alikuwa ameanza kujenga mazoea na
Mimi.
Waliongozana mpaka katika daraja dogo ambalo
chini yake kulikuwa na maji yanapita yaani mto
mdogo hivi huku wakichombeza stori mbili tatu
"Hivi Humph unamfahamu yule kijana aliyeniokoa
yaani yule uliemchora?"
"Ndio yaani hapana ila nimetokea tu kumpenda
ghafla ndio maana nikamchora"
"Mbona kama hauna uhakika usinifiche bhana"
"kweli simfahamu japo niliwahi kuonana nae na
aliniambia kuwa Mimi ni rafiki mzur tu kwako"
nilikuwa najichanganya maneno
"Mmh!! kumbe ni binadamu mi nilidhani Jini"
"Hahahaahaha!! amna Mimi binadamu mbona"
"ukimuona tena mwambie asante kwa kuniokoa"
"Usihofu nimeshasikia kwahiyo usiwe na hofu"
Nilivyoona nazidi kujikoroga kwa Lisa na
kujiuma.uma ikabidi niage na kurudi nyumbani japo
kilichonipeleka kule nilikikosa lakini nilikuwa na
furaha kuona nimeanza kuuteka moyo wa Lisa bila
kujua hatari ninayoitengeneza....
 
Sehemu ya kumi na mbili
........Ilipoishia...........
Nilivyoona nazidi kujikoroga kwa Lisa na
kujiuma.uma ikabidi niage na kurudi nyumbani japo
kilichonipeleka kule nilikikosa lakini nilikuwa na
furaha kuona nimeanza kuuteka moyo wa Lisa bila
kujua hatari ninayoitengeneza....
...........Teremka nayo........
**********The rise of the dark ghost*******
**********Kuibuka kwa Mzuka wa kiza****
Mwandishi mmoja wa habari katika gazeti la
maarufu la CHANZO ambaye alikuwa machachari
sana mjini kwa kufuatilia visa na habari
zilizoshindikana,nwandishi huyo alijulikana kama
Edison Mwamba.
Kutokana na tamaa na hali ya kupenda kufuatilia
vitu Edison alijibebesha jukumu zito mno la
kumfuatilia Humph na kumtangaza hadharani huku
akiwa na imani ya kuwa taarifa hizo zitampa
umaarufu maradufu mjini hapo na huenda akapewa
tuzo alizokuwa akiziwania kwa muda mrefu bila
mafanikio yoyote yale.
Alianza moja kwa moja kumfuatilia Lisa ambaye
aliokolewa na Humph akijua wazi kuwa lazima
muokoaji atakuwa mtu wa karibu wa binti huyo na
kama sivyo atakuwa hayuko mbali nae.
Kwanza kabisa alianza kufuatilia marafiki wa Lisa
wenye ukaribu nae hasa wakiume ambapo
hakuambulia chochote kile kwani Lisa hakuwahi
kujenga mazoea na wanaume isipokuwa Humph
pekee ambae nae hawakuzoeana sana.
Siku zilizidi kukatika hatimaye Edison akaanza
kupoteza matumaini ya kumpata mlengwa kwa
kuwa alipoteza muda mwingi mno,fedha na akili
nyingi bila mafanikio
Akiwa katika gari amejipumzisha kutokana na wingi
wa mawazo katika dirisha la gari yake alipita binti
mmoja ambaye ni Lisa akiwa na Humph waliokuwa
wakipiga soga za hapa na pale sasa kutokana na
kicheko alichokuwa akicheka lisa,Edison alistuka
toka usingizini na kukeleka mno na kicheko kile
alipotazama katika kioo cha pembeni ya gari (site
mirror) aliweza kumtambua binti yule kuwa ni Lisa
na kijana asiyemfahamu ambaye ni Humph.
Alihisi kitu maana haikuwa rahisi binti yule
kutembea na mwanaume hivyo akatoka na vifaa
vyake kuanza kuwafuatilia nyendo zao huku akipiga
picha.
Humph aliagana na Lisa wakiwa wametoka
matembezini kama marafiki waliozoeana kwa muda
mfupi tu,kila mtu akapita njia yake.
Edison alipoona hivyo akaamua kumfuata Humph ili
ikiwezekana ambananishe au ajue mahali anapoishi
na kuanza kumfuatilia haraka iwezekanavyo
Akiwa katika hayo mawazo ghafla alitokea
mwanamke mmoja mrembo mno aliezihamisha
hisia za Edison bila kutaka hakuwa mwingine ila
Sorcerers (Sor) ambaye hakujua ametokea wapi
kwani awali hakuwepo mbele bila kujielewa Edison
alijikuta akitabasamu tu na Sor akamkonyeza kisha
akamfuata mpaka pale alipo.
Edison akiwa katika hali ya sintofahamu aliguswa
bega na Sor na kumnong'oneza kisha
akaondoka.Edison alipogeuka hakuona chochote
zaidi ya mwili wake kusisimka na mwisho joto kali
likaanza kupanda mwilini mpaka akaanza kufuka
moshi huku akipiga kelele ambazo hazikuendana na
sauti za binadamu wa kawaida
Edison alianguka chini na kuanza kugalagala chini
mwili wake ulizidi kukakamaa na kuwa mweusi na
kupukutika kama vumbi lililotawanywa,Vifaa vyake
vikabaki ardhini.
******************************
Nikiwa njiani kuelekea nyumbani nilianza kuhisi
kuna kitu hakiposawa,Nilijaribu kutuliza akili lakini
sikuweza kubaini chochote. nikiwa nafikiria ni kipi
kilichotokea ghafla ile hali ya maono ikanipitia
kama sinema vile nikaona kiumbe kimoja
hakieleweki maana kilikuwa cheusi mno kisha ile
hali ikaisha.
Lakini sikuelewa wala sikupata jibu sahihi hivyo
nilizidi kutokomea mitaani,kabla sijafika mbali
moyo ulilipuka kwa nguvu mno nikastukia natamka
neno "Lisa" bila kutaka.
Hapo nikatambua kuwa Lisa yupo katika hatari
nasikuwa tayari kumuona akiumia kwa lolote
nikabadili njia na kuufuata uelekeo ilipo nyumba
yakina Lisa kwani nilipafahamu vyema.
Nikiwa nimefika njia inayoelekea kwa kina Lisa kuna
wingu Fulani Leusi lilinipita kwa kasi.Kwasababu
lilipita chini kwa chini nikadhani kuwa ni moshi
mzito ulionifanya nishangae kwa muda nikiwa
najiuliza ni moshi gani unaoweza kukatisha kwa
kasi kubwa namna ile lakini sikuwa na wakunijibu
Nilikaza mwendo na hatimaye nikaamua kuanza
kukimbia ili nimuwahi Lisa kabla hajafika nyumbani
kwao,palikuwa na umbali kiasi kutoka pale nilipo
mpaka kwa akina Lisa
Nilijitahidi mno na milipofikia jirani na nyumba ya
kina Lisa nilishangaa kumuona mtu mweusi mno
kama giza totoro japo alikuwa na macho meupe
peeeeeee!! yaliyomtambulisha yeye kama ni
binadamu
Alivyoniona tu alinikazia macho na kumshika Lisa
ambaye hakumuona mtu huyo hapo awali ila
alivyoshikwa tu aligeuka lakini kitu alichokutana
nacho kilimfanya azirai hapo hapo.
kutokana na kigiza kilikuwa tayari kimeanza kuingia
Edison alipotelea kusikojulikana na Lisa akimuacha
Humph akiwa amesimama asijue kipi cha kufanya
mpaka muda huo.
 
Sehemu ya kumi na tatu
..........Ilipoishia........
kutokana na kigiza kilikuwa tayari kimeanza kuingia
Edison alipotelea kusikojulikana na Lisa akimuacha
Humph akiwa amesimama asijue kipi cha kufanya
mpaka muda huo.
..........Shuka nayo.......
Edison baada ya kumpata Lisa alienda moja kwa
moja mpaka katika jengo moja lililochakaa
ikiamaanisha Kuwa halijatumika kwa muda mrefu
mno.Akaingia mpaka sehemu zilizopo chini ya ardhi
ya jengo hilo na kumfunga Lisa katika kiti kama
mateka ili ampate Humph kwa kuwa aliamini huo
ndiyo utakuwa udhaifu mkubwa wa Humph
ikumbukwe kuwa yote hayo anayoyafanya Edi si
kwa mapenzi yake bali kutokana na nguvu za Sor
ambazo ziko mwilini mwake
****The rise of iceman********
****Kuibuka kwa barafu ume*****
Lamson alikuwa bado anaomboleza kifo cha
Profesa kwa kujilaumu kwa kosa la kutomlinda bosi
wake mpaka amepatwa na mauti na hajamuingizia
kiasi cha kutosha kuanzisha miradi yake binafsi ya
kumuingizia kipato japo Lamson alisahau kama
kiasi alichopata alikitumia vilivyo kuponda raha bila
kuacha akiba yoyote.
Daima hakujua kama kuna Leo na kesho,Akiwa
katika majuto mazito na viapo vya kumuangamiza
adui yake popote alipo mara aliguswa begani kwa
kupigwa pigwa kusikoumiza katika hali ya
kumbembeleza atulie
Hakugeuka zaidi ya kuanza kuangua kilio lakini kilio
kile hakikudumu hasa pale alipomtazama
anaemliwaza hakuwa mwingine bali msichana
mrembo wa karne na karne maarufu kama Sor
ambaye hakujulikana ni wapi haswa alipotokea
mpaka kufikia eneo hilo.
"Lamson,inaonesha kifo cha Profesa kimekugusa
sana ukiwa kama mtu wake wa karibu" Aliuliza Sor
au sorceress
"Kwani we ni nani na umenitambuaje kama ni mtu
wa karibu kwa Profesa" Aliuliza Lamson kwa sauti
ya uchovu na kukata tamaa
"Haina haja ya kufahamu kwani mimi ni msaada wa
pekee uliobakia kwako endapo tu utakubaliana na
Mimi" Sor alimueleza Lamson
"Sijakuelewa unamaanisha nini?" aliuliza Lamson
"Unahitaji kazi sio?" aliuliza Sor badala ya kujibu
"Ndiyo nahitaji kazi" alijibu Lamson
"Pia unahitaji kulipa kisasi eeeeh?" aliongeza Sor
"Haswaaa ndiyo lengo langu kubwa" alijibu Lamson
"Basi nitakupatia vyote kwani huyo adui yako nami
simuhitaji katika dunia hii" Sor alieleza kwa
machungu akiaamanisha kile akisemacho
"Kama ni hivyo kwanini tusiungane?" Lamson
alimuomba Sor
"Nitakuwa kama bosi wako na nitakulipa mshahara
Mara tano ya ule aliokuwa akikulipa Profesa ila
kwanza inatakiwa nikuongeze nguvu za ziada kwani
adui yako anauwezo mkubwa mno"
"Nguvu zipi tena" aliuliza Lamson
"Nifuate nikuonyeshe" alitoa ufafanuzi Sor
Bila kupinga Lamson alisogea kwa Sor na
kuwekewa mikono kichwani huku akinena maneno
yasiyoeleweka kwa dakika kadhaa zilizomfanya
Lamson aanze kutetemeka na kubadilika viini vya
macho yake kutoka weusi mpaka ubluu Fulani wa
ajabu na nywele zikiwa na rangi nyeupe peeeeee!!!!
Kwa mbwembwe Lamson aliishika simu yake ya
rununu mparuzo ama smartphone na kujiangalia
kiukweli alipendeza mno na ile rangi ya nywele
lakini katika hali isiyotegemewa simu yake ilianza
kupitisha mipasuko ikionesha imeganda mno kwa
muda huo huo na alipoiachia na kugusa ardhi
ilisambaratika kabisa ikiwa katika vipande vya
barafu.
***********The death of the dark ghost****
******Kifo cha mzuka wa kiza*******
Lisa alizinduka akiwa katika chumba chenye giza
kali mno akiwa anajaribu kujiinua alishindwa,ndipo
alipogundua kuwa amefungwa katika kiti kile
mikono na miguu
Akiwa katika hali hiyo ya sintofahamu alisikia sauti
ikimsemesha "Tulia mpuuzi wewe umsubiri huyoo
mmeo ajilete mwenyewe na akishindwa kutimiza
masharti nitakayomwambia kifo ni halali yenu"
Lisa akazidi kupatwa na hofu na jambo lingine
lililomuweka njia panda ni kwamba yeye hajaolewa
sasa huyo Mme wake nd'o yupi tena anaekuja
kumtoa mahali hapo
Wakiwa katika kimya cha muda mfupi zilisikika
kelele za sakafu iliyokuwa ikisurubiwa na viatu vya
mkanyagaji ambaye hakujali maumivu ya sakafu
hiyo
Sauti ilianza kusikika ikiita "Lisa,Lisa ,Lisa " "uko
wapi Lisa" "Lisa,Lisa,Lisa,itika basi"
Lisa alitamani afungue mdomo ama apige kelele
lakini karatasi ya plastiki yenye gundi(plaster)
ilimzuia kufanya hivyo akabaki akisubiri mtu huyo
ambaye kwa muda huo ndiye alikuwa tegemezi la
Lisa.
Alikuwa ni Humph ambaye alifika katika hilo jengo
kumuokoa Lisa bila kujua ni mtego amewekewa. Ni
hatari kiukweli kwa sisi wanaume hata kama
msichana hajaomba msaada au kitu chochote
tunatoa tu kisa eti nikimuona moyo wangu
unakwenda mbio.
Humph alipofika chumba kile kikawa na mwanga
ambao ulitokea machoni mwake.Lisa alianza
kuhema kwa pupa lakini Humph alimtuliza kwa
ishara kuwa asifanye chochote kisha akamsogelea
ili amfungue kamba lakini Lisa alikuwa akitikisa
kichwa kuashiria asisogee eneo alilopo.
Wakati yote hayo yanaendelea Edison alikuwa
amejibanza juu akishuhudia kile anachokifanya
Humph na ikumbukwe kuwa Edison alikuwa katika
mfumo wa giza.
Humph akiwa ameanza kufungua kamba ghafla
akaangukiwa na Edison,Humph akasimama tena na
kabla hajakaa vizuri akapigwa kikumbo alipoinuka
na kutazama kote hakuona mtu.
Akiwa katika kushangaa shangaa alistukia makonde
yanapita kwa kasi kama upepo,vibao,makucha
mfululizo kila sehemu ya mwili,kila alipojitahidi
aliambulia maumivu tu. Alivyoona hali ni tete kipigo
kimezidi kama.mtoto mdogo tena mbele ya
msichana anaempenda.
Akiwa anasimama kwa shida aliamua kupaza sauti
"unataka nini eeeh!! kama unanitaka Mimi muache
huyu msichana hana kosa wala hatia yoyote kwako"
"na kama wewe ni mwanaume kweli kwanini
unavizia wewe na kujificha hebu jitokeze tupambane
kiumee njoo acha uoga au wewe ni dada ndiyo
maana unajificha"
Loooh!!! maneno yale yalimtia hasira mno Edison
ambaye alijitokeza akiwa anatamani amvunje vunje
au amtafune kabisa Humph.
Humph aligwaya baada ya kumshuhudia Edison bila
chenga ambaye alionekana ni kitu Kama giza au
moshi mweusi ila lina macho ya binadamu
kabisa,kwa hofu alianza kutetemeka na kuhisi
miguu inakosa nguvu.
Kabla Humph hajafanya lolote Edison alikurupuka na
kuanza mashambulizi ambayo ilikuwa afadhali na
mwanzo.
Safari hii.Humph alihisi kifo kipo jirani yake.........
 
Sehemu ya kumi na nne
......Ilipoishia.........
Kabla Humph hajafanya lolote Edison alikurupuka na
kuanza mashambulizi ambayo ilikuwa afadhali na
mwanzo.
Safari hii.Humph alihisi kifo kipo jirani yake.........
..........Tiririka Nayo...........
Kwa akili za haraka haraka na maarifa aliyonayo
Humph aliona asije kufa buree bila kujitetea. Ule
msemo wa "Lila na fila havitangamani" ulikuwa na
maana kubwa sana uliofanya avumbue kuwa "Giza
na nuru haviendani" sasa kwakuwa kule ni chini ya
ardhi afanyaje?,Uamuzi wa haraka akaona bora
ajitose kubomoa ukuta kwa juu lakini kulingana na
uzito wa ukuta hesabu zake zikagonga mwamba.
Akakumbuka kuwa ni vioo pekee vinavyoweza
kuakisi mwanga na kuufikisha kule chini. Alifunga
macho kwa haraka na kupotea eneo hilo aliporudi
ndani ya dakika chache alikuwa na vioo wakati huo
huo Edison alibaki na mshangao baada ya Humph
kutoweka na pia alifurahi kuona asilimia 90% ya vita
ile ameshinda.
Humph alianza kazi ya kupanga vioo kwa
kutegeshea sehemu ambayo jua linamulika humo
ndani na kwa wepesi wa ajabu aliweza kuvipanga
vizuri kushuka chini ambako ndipo yupo Edison na
Lisa.
Edison hakutambua hili wala lile alizidi kuhangaika
kumtafuta Humph bila mafanaikio yoyote. Ule
mwanga wa vioo ulizidi kufuata mtiririko ambao
Humph aliutengeneza na mwisho alishuka mpaka
katika kile chumba
Edison alitahamaki kumuona Humph amesimama
mbele yake. Humph hakuongea lolote zaidi ya
kutazamana na Edi
"Bwana mdogo umekuja kusalimisha Mali yetu au
bado unahitaji kipigo?" aliuliza Edison
"Sijaleta chochote zaidi ya hikiiii..."
Alijibu Humph huku kwa kasi ya ajabu akitegesha
kile kioo kilichobakia na kusababisha mwanga
mkali wa jua umulike katika chumba kile.
Edison alikodoa macho ya mshangao na papo hapo
akaanza kupiga yowe la uchungu likiambatana na
kelele za ovyo ovyo zisizo na mpangilio
zilizosababisha kioo kile kipasuke.
Muda wote huo Humph alikuwa amewahi na
kumkumbatia Lisa na kufunga macho wakati kioo
kinapasuka. Alimuachia Lisa na kumfungua kamba
alizofungwa lakini kabla hawajaondoka sehemu hiyo
walisikia sauti ya mtu akikoroma.
Alikuwa ni Edison amerudi katika umbile lake la
kawaida akiwa na kijibukta kilichopasuka pasuka.
Edison na Lisa walitolewa nje ya jengo hilo ili
wapate msaada mwingine kwani Humph hakuhitaji
malipo ya wema wake kwao.
Humph akiwa amelowa damu na nguo zake
kuraruka pamoja na vumbi kumtapakaa aliamua
kuondoka eneo hilo bila kuaga.Wakati anaondoka
Lisa alimuita na kuzungumza mane no machache
kwa hisia kali mno
"Samahani kaka umekuwa mtu mwema sana
kwangu na msaada mkubwa katika maisha yangu
kila mara kiukweli sina cha kukulipa zaidi ya
kusema asante. Japo ningependa hata kuiona sura
yako kaka yangu naomba uniruhusu"
Mwanaume alikuwa amempa mgongo Lisa na
alitamani sana kugeuka maana hakuwa na kitambaa
usoni wala kofia na katika purukushani zote Lisa
hakuweza kung'amua kuwa yule ni Humph maana
nguo alizokuwa amezivaa ndiyo zile zile alizokuja
nazo kumkomboa,Kweli matatizo husaulisha kila
jambo hata yale ya msingi
Kwakuwa Humph hakutaka kutambulika kabisa kwa
Lisa na ijapokuwa alikuwa akimpenda mno lakini
kamwe hakuthubutu kujitambulisha na kufikia hatua
ya kumuamini msichana huyo asilimia nyingi namna
hiyo.
Alichofanya ni kupotea maeneo hayo maana milio
ya gari za askari ilikuwa imetawala kwa wingi
ikionesha wanaelekea eneo hilo.
******The fall of iceman ********
******Kuanguka kwa barafu ume********
Lamson alikuwa katika nguvu mpya zilizomfanya
awe katili kupita kiasi ukilinganisha na ujasusi
aliokuwa nao ndiyo kabisaaaa.Kwakuwa alikuwa
akimfahamu Humph vizuri na alitambua wazi kuwa
ndiye adui yake namba moja tena mpenda kuokoa
watu,akabuni njia rahisi ya kumkamata.
Aliamua kuelekea katikati ya jiji kubwa la Reycity na
kusimama katikati ya barabara kubwa yenye magari
yaendayo kwa kasi. Kitu cha kwanza alianza
kuyafumua magari kwa kutumia barafu alizonazo
ilikuwa ni patashika maana magari yalikuwa
yakirushwa mno mengine yalikosa uelekeo na
kufanya mrundikano wa magari,
watu walikosa kwa kupita wakabaki wakipiga
mayowe kutaka msaada.Polisi na waandishi wa
habari walifiika mara moja na kuanza kuchukua lile
tukio na kulirusha moja kwa moja yaani laivu(live)
Polisi walianza kutoa kauli za vitisho kwa Lamson
lakini Lamson hakuwa na hata chembe ya
kujisalimisha
"Sisi ni polisi jisalimishe kabla hatujakuvuruga hapo
ulipo narudia tena sisi ni polisi jisalimishe mikononi
mwetu kabla hatujatumia nguvu,nitahesabu mpaka
moja kutoka tano usipojisalimisha tutatumia nguvu"
Lamson hakujishughulisha nao ndiyo kwanza
alipanda juu ya Gari moja kubwa huku akiwatazama
polisi kwa ghadhabu ya hali ya juu.
"Sisi.ni maafisa wa polisi tunaomba raia mkae
mbali na sehemu hii ili kuepusha madhara
yanayoenda kutokea narudia tena raia wema
naombeni mkae mbali na eneo hili" Ilisikika sauti ya
askari ikitokea katika kipaza sauti
Raia walitii maneno ya polisi wakaanza kwenda
mbali na eneo lile ila wengi wao walitafuta sehemu
nzuri ambayo wanaweza kuwaona vizuri polisi
wanavyopambana na mhalifu huyo ambaye ni
Lamson.
Bado Lamson hakutaka kujisalimisha na moyoni
alikuwa akijisemea"sitaki kuwadhuru lakini
mkianzisha tu nawatia jamba jamba ambayo kamwe
hamjawahi kutana nayo"
Polisi hawakuchoka walisubiri Lamson ajisalimishe
lakini hakufanya hivyo hapo ndipo na Mimi niliamini
kumbe na polisi wakati mwingine huwa ni waoga
wanakuchimba mkwara hapo waone kama
utatetereka.
Kiongozi wa msafara wa Polisi alionekana ni mtu
mwenye msimamo mkali mno kama Al-shabab lile
kundi la kigaidi. alianza kwa kuhesabu
Tano......nne........tatu........mbili.........mo..
Kabla hajamalizia Lamson alishusha kombora moja
la barafu lilioinua gari ya mbele kabisa ya polisi na
kuirusha nyuma yao. Sauti ya kiongozi ilisikika
ikisema "Ooooooooooh!!" tunashambuliwa jificheni
Muda huu Lamson alikuwa anainua gari kubwa
aliyokuwa amesimama juu yake.....
 
Sehemu ya kumi na tano
.......Ilipoishia.........
Kabla hajamalizia Lamson alishusha kombora moja
la barafu lilioinua gari ya mbele kabisa ya polisi na
kuirusha nyuma yao. Sauti ya kiongozi ilisikika
ikisema "Ooooooooooh!!" tunashambuliwa jificheni
Muda huu Lamson alikuwa anainua gari kubwa
aliyokuwa amesimama juu yake.....
.........Endelea..........
Polisi walianza kukimbia ovyo wakiwa
wamechanganyikiwa huku waandishi wa habari
wakiwa wanasifia jinsi Lamson alivyo na nguvu
nyingi za kuweza kunyanyua gari la namna ile.
Lamson aliirusha ile gari kwa nguvu iliyoenda kutua
moja kwa moja kwenye gari za polisi na
kusababisha mlipuko mkubwa. Kabla polisi
hawajajiandaa kufanya mashambulizi Lamson
aliwastukiza na mvua ya makombora ya barafu
iliyowachanganya askari mpaka kufikia hatua ya
kuanza kukimbia.
Wakati yote hayo yanaendelea Humph alikuwa
chhmbani mwake anajisomea ghafla Mzee Kasai
ambaye ni baba yake anaingia chumbani humo na
kuomba Humph aache kusoma amfuate sebuleni.
Humph anabaki na mshangao baada ya kuona tukio
linaloendelea katika jiji la Reycity, Hofu ya watu
kuuawa kikatili inatanda moyoni mwake na kuamua
kumuaga baba yake kuwa anaenda kulala maana
tukio aliloliona linatisha mno.
Alivyofika tu chumbani alikuwa amefura kwa hasira
juu ya kitendo wanachofanyiwa askari kule mjini bila
kujua anafanyiwa hila na Lamson
Alichukua viatu vyepesi alivyoviweka maalumu
kwaajili ya kazi,kofia pamoja na kitambaa akavaa
vizuri na kupotea chumbani humo akiwa ameacha
mito kitandani iliyopangwa kama mtu amelala.
*****************************
Lamson aliendelea na vurugu za hapa na pale ila
hakuthubutu kuwaumiza watu kwani alikuwa na
lengo kubwa mno na la muhimu kuliko hawa raia
wasio na hatia.
Lamson alinyanyua gari na kulirusha sehemu walipo
watu lakini kabla halijatua chini lilirudishwa kwa kasi
kubwa na Humph japo halikumpata Lamson
Humph alinyanyua kipaza sauti na kuanza kuongea
"ndugu wananchi kaeni mbali tulishughulikie hili
tatizo" aliongea kwa sauti nzito tofauti na mwili
alionao
Lamson hakusubiri maneno mengi alianza
kuporomosha makombora ya barafu yaliyokuwa
yanakwenda kasi mno na yalitoka mfululizo lakini
kwa kuendana na kasi ile ile ya makombora
alifanikiwa kuyatoka baadhi jambo lililosababisha
watu waaanze kushangilia
Haikuwa furaha kwa Lamson alizidi kuchukia kile
kitendo cha raia kumshangilia Humph. Alianzisha
varangati lingine la aina yake akiwa na kusudio
moja tuu "kuua"
Humph alikosa umakini kwasababu ya shangwe zile
ghafla Lamson akaanza kutuma makombora safari
hii alikuwa anakuja mbio. kufumba na kufumbua
alikuwa amemfikia Humph na kumtupia ngumi moja
matata iliyomfanya aruke na kujibamiza vibaya
katika magari ya raia.
Humph alikuwa hoi bini taaban kutokana na ngumi
aliyokutana nayo ilivyokuwa nzito kupita maelezo.
Alijaribu kujinyanyua lakini ilishindikana. watu
walivyoona vile walitulia kimya hali iliyomfanya
Lamson aanze kucheka cheko la dharau huku
anamfuata Humph alipo.
Alipomfikia alimnyanyua na kumtazama vizuri usoni
kisha akaongeza kicheko kikubwa, ikumbukwe kuwa
Lamson alikuwa na nguvu zenye asili ya barafu na
tayari alikuwa amemshikilia Humph kooni
Ndani ya dakika chache Humph alianza kutetemeka
kutokana na ubaridi mkali kupenya mwilini mwake
mpaka ule mwanga wa machoni ukaanza kutoweka
Katika hali ya kustaajabisha na kushangaza Lamson
alipigwa na kitu kizito mgongoni mpaka akayumba
alipogeuka alikutana na msichana ambaye hakuwa
mgeni kwa Humph huyu alikuwa ni Lisa ambaye
alikuwa ameshaokolewa Mara mbili na Humph.
Lamson kwa hasira alimrusha Humph ambaye safari
hii alijipigiza vibaya mno kuliko mwanzo kisha
Lamson akamgeukia Lisa na kuanza kumsogelea
lakini kabla hajafika raia walianza kumrushia
maneno yenye kuudhi
Lamson aligeuka nyuma kuwaangalia raia na hilo
lilikuwa kosa kubwa sana kwani askari mmoja
alimfuata Lisa na.kuanza kukimbia naye kutoka
eneo hilo.
Lamson aliponaki peke yake eneo lile zilianza
kusikika helikopta zikisogea eneo hilo. Lamson
aliamua kurusha makombora machache ya barafu
yaliyowapotezea umakini polisi wale kisha
akatokomea kusiko julikana akiwa ameacha hasara
ya mamilioni
Humph alikuwa hoi kutokana na kipigo alichopewa
na lamson,Alijitahidi kuinuka ila akashindwa muda
huo watu wa kikosi cha huduma ya kwanza
walikuwa tayari wamefika eneo hilo wakamfuata ili
wamuinue lakini akakataa kuhofia kuwa wanaweza
kumuona sura yake.
Kwa bahati nzuri Lisa alikuwa jirani na kile kikosi
cha msaada wa kwanza hivyo Humph alimuita na
kumuomba amsaidie kunyanyuka lakini kutokana na
hali aliyokuwa nayo Lisa alimuomba nesi mmoja
waongozane katika ambulance ili ampe msaada
Humph.
*********************
Asubuhi Lamson alikuwa katika jengo moja ambalo
linamilikiwa na kituo cha habari kinachorusha
matangazo ndani ya jiji la Reycity.Wafanyakazi
walikuwa wakikimbia ovyo lakini aliomba
wasikimbie ila wampe kipaza sauti
Baada ya kupewa alitoka nje na kumkata mtoto
mdogo kisha akapanda nae juu ya ghorofa moja
ndefu kwa bahati nzuri kile kipaza sauti kilikuwa
kimeunganishwa moja kwa moja katika lile jengo la
kurushia matangazo hivyo haikumuwia vigumu
kusikika pia kamera zilikuwa zinamchukua moja
kwa moja na kumrusha katika runninga zilizofungwa
maeneo hayo ya jiji.
"Naomba polisi yeyote asijihusishe na hili
ninachohitaji ni huyu mwanaharamu aje hapa
tumalizane,huu mchezo ni wa Mimi na yeye tu,
ndani ya dakika kumi namtaka hapa"
Humph alikuwa bado yuko nyumbani kwao
anaugulia maumivu lakini punde tu baada ya
kuisikia ile taarifa alianza kijiandaa japo maumivu
aliyokuwa nayo alihisi huenda ataenda kufia huko
huko japo alijipa moyo kuwa ni heri afe akiwa
anajaribu kuokoa Maisha ya yule mtoto mdogo....
Lamson alikuwa tayari amebakiwa na dakika moja
kati ya kumi alizotoa na hakuona dalili yoyote ya
Humph kujitokeza akaamua sasa ni muda wa fujo
mtindo mmoja mpaka pale atakapojitoleza.
Alitupa kipaza sauti chini kisha akamshika yule
mtoto mkono na kusogea naye mpaka katika ncha
ya ukuta akiwa na kusudio la kumning'iniza yule
mtoto. Watu walikuwa wanalia kwa uchungu hasa
wale wenye mioyo miepesi na wengine wenye
mioyo migumu walikuwa wanapiga kelele tu ilimradi
Lamson aghairi zoezi lake.
Lamson alistukia sauti ikitokea nyuma yake "Hey!!
mwache huyo mtoto aende tupambane kiume"
Lamson alitabasamu tu kisha akamsukumia yule
mtoto pembeni na ikumbukwe endapo Lamson
akimshika mtu kwa muda mrefu basi lazima ugande
au baridi kali isambae mwilini mwako na hivyo
ndivyo ilivyokuwa kwa yule mtoto.
Humph bila kutegemea alijikuta katika wakati
mgumu baada ya kuzungukwa na barafu zilizotolewa
na.Lamson kwa kasi kubwa. Kisha Lamson aliruka
na ngumi za mwendokasi wa 4G ilikuwa ni hatari
mno kwani Humph alikutana nazo sawa sawia.
Ilikuwa kama kutoneshwa vidonda kwani Humph
aliona dunia nzima ameibeba kichwani .......
 
Sehemu ya kumi na sita
.......... Ilipoishia...........
Ilikuwa kama kutoneshwa vidonda kwani Humph
aliona dunia nzima ameibeba kichwani .......
..............Endelea........
Kutokana na maumivu ya mwanzo ambayo yalikuwa
bado hayajatulia.
Humph alijinyanyua kwa kujizoa zoa safari hii
alijaribu kutuliza akili yake kwani kutumia nguvu
nyingi bila maarifa ni sawa na bure.Kwa kasi na
wepesi wa ajabu Lamson alistukia anapokea
mateke dabo ama ukipenda ziite double kick
mpaka akapepesuka lakini hakukubali akajiweka
sawa kumkabili Humph
Lamson alitabasamu na kuinama chini kwa haraka
looh!! kumbe alikuwa na lengo la kujifyetua bila
kujua kuwa tayari Humph alishamsoma nia yake.
Lamson alifyetuka kwa makonde yenye hadhi hapa
nazungumzia makonde si Yale ya Mike Tyson la
hasha!! haya yalikuwa hayaelezeki hata Humph
alikiri kuwa Lamson angekuwa mnyama basi
angefananishwa na faru au mbogo kwa jinsi
alivyokuwa amechafukwa.
Humph alikuwa anezidiwa lakini kadri muda
ulivyozidi kwenda alianza kumudu mchezo ule na
mwisho akaanza kutumia mtindo ule alioutumia
Lamson akiwa ameubadilisha katika namna ambayo
anaijua yeye na kumfanya Lamson ashindwe
mpambano ule.
Baada ya Lamson kuona hana mbinu mpya
akamrukia mtoto ili awe kama ngao ya kumuokoa
eneo hilo na hakuhitaji maongezi alichofanya ni
kumrusha yule mtoto kutoka juu ya ghorofa.
Humph alichoka akili asiamini ujanja alioutumia
adui yake na kumzidi maarifa,kitendo kile
kilimchukiza mno kwani Lamson alitumia ujanja
ujanja sasa hasira zile zilipelekea akunje ngumi
ambayo kiukweli ilikuwa si ya karne hii kwani
ilipompata Lamson alitoa yowe kali sambamba na
kutupwa juu na kabla hajashuka alisindikizwa na
mateke mengi mno yaliyomtoa juu ya ghorofa
kuelekea chini.
Kwa kuwa ghorofa ilikuwa ndefu mno Humph
alishuka kwa kuteleza kama wale wachezaji katika
milima ya barafu.safari hii kasi yake aliidhibiti kweli
kweli sijui ni kwasababu alikuwa na hasira maana
alishuka kama kimbunga
Kabla mtoto hajafika chini Humph alikuwa
amemfikia na kuikamata nguo yake kwa kitendo
cha haraka akafumba macho na kupotea kisha
akatokea chini akiwa mtoto mkononi kiukweli watu
hawakuamini wengi wao walikuwa wamefumba
macho wasione kifo kinachoenda kumkuta mtoto
yule
Kishindo kikubwa kilisikika pembeni kikifuatiwa na
ardhi kudidimia sehemu fulani bila Shaka alikuwa ni
Lamson ambaye alianguka vibaya na kupoteza
maisha pale pale .
Wazazi wa mtoto walimfuata na kumkumbatia
wakitokwa na machozi ya furaha wasijue ni zawadi
gani au pongezi anayostahili Humph.
Waandishi wa habari walijaribu kwenda kumhoji
Humph lakini polisi waliwazuia. Ikumbukwe kuwa
Lamson alikuwa na nguvu zenye asili ya barafu
zilizomfanya yule mtoto azidi kuwa wabaridi mno
hali iliyomfanya apoteze fahamu hapo hapo
Humph aliliona hilo na kumkimbilia mtoto yule na
kumtoa katika mikono ya wazazi wake mpaka katika
ambulensi.
Baada ya Humph kutoa maelezo ya kina kwa watoa
Huduma ya kwanza alianza kuondoka japo watu na
waandishi wa habari walizidi kupiga picha na
wengine wakishangilia.
Askari mmoja hakupendezwa na yale aliyoyafanya
Humph taratibu alitoa bastola yake na kuifunga
kiwambo cha kuzuia sauti kisha akalenga sehemu
aliyopo Humph.
Humph alihisi hali Fulani ya utofauti na kwa kuwa
hakupenda umaarufu alipotea Mara moja na kutokea
juu kabisa ya ghorofa lile ambalo hapo awali
alikuwa akipambana na Lamson akaanza kupunga
mikono kwa wananchi ambao walizidisha shangwe
kisha akajiachia kama tai anapotaka kunyakua
vifaranga,watu wakazidi kupiga may owe na
shangwe za hofu alipofika katikati ya ghorofa
akafumba macho na ghafla akapotea katika hali
isiyoeleweka akiwa amewaacha waandishi wa
habari polisi na wananchi katika mazingira ya
kushangaaa.
Yule polisi alibaki ameduwaa na kusahau lengo
alilokuwa nalo huku akiamini kuwa yule si binadamu
wa kawaida.
******The hidden treasure ********
*****Hazina Iliyofichwa********
Kabla Humph hajafika kwao Sor alikuwa tayari
ameshawasili katika viunga vya nyumba yao kwani
tayari alishashuhudia mpambano mzima kati ya
Humph na Lamson hivyo alikuwa tayari amebuni njia
nyingine mahsusi kumkabili Humph.
Alitafuta sehemu nzuri ambayo itakuwa kama kitovu
cha nyumba hiyo akiwa amekusudia kufanya jambo
fulani la hatarii.
Alipofanikiwa alianza rasmi harakati zake kwanza
kabisa alitia alama eneo lile kwa kutumia maneno
machache yaliyofanya eneo lile lianze kufuka moshi
mzito ambao moja kwa moja haukufika juu zaidi
ulipotea kimya kimya.
Sor alisogea mpaka mlangoni ambapo alibisha hodi
aliposikia sauti ya mtu kuitikia akarudi nyuma kisha
akanena maneno kadhaa yaliyosabababisha ukungu
mwingi kutanda eneo lile.
Punde tu mfunguaji alipofungua mlango ambaye ni
Sifa alistukizwa na ukungu ule ambao ulisongamana
kuingia ndani kwa kasi ni kama ulikuwa ukisubiri
mtu afungue nao uingie.
Ule ukungu haukuwa wa kheri,Sifa alipouvuta tu
katika pua zake alizirai pale pale na ndivyo
ilivyokuwa kwa familia nzima,wote walizirai
kutokana na ukungu huo.
Sor alitoa tabasamu la ushindi kwani hii ilikuwa
nusu ya kutimiza dhamira yake.Waswahili
wanasema kumfahamu adui ni nusu ya ushindi na
hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa binti mrembo wa karne
na karne yaani Sor.
Sor baada ya kumaliza hatua ya kwanza alirudi na
kusimama pale alipoacha moshi mzito unafuka
kisha kwa kutumia mikono yake akaanza kuchora
pentagoni.
Hakutumia muda mrefu alimaliza mchoro huo
wenye maana maalumu sana kwake kisha akaingia
katikati ya pentagoni lile,ngoja nikwambie kidogo
ndugu msomaji Mara nyingi Pentagon huwa ni
mchoro ambao unafanana na nyota ila unaduara
Fulani kwa nje
Sor alizungumza maneno machache na kuiinua
mikono yake ambapo ilipoinuliwa tu moto uliwakaka
katika pentagoni lile. Sor hakushangaa kwani hata
macho yake yalianza kutoa mwanga unaofanana na
miale ya moto ule.
Alianza kunena maneno ambayo yalisikika
akisema"Je me léve la pire Maladie Sur cette
Famille pour le prixdu Trésor et personne ne pouvail
guérir sans qu'il" tafsiri yake ni "Nainua ugonjwa
mbaya katika familia hii kwa malipo ya hazina na
hakuna atakaye we za kuwaponya pasipo hazina
hiyo"
Baada ya kimaliza kuyasema hayo moto ule
ulizimika na Sor akarudi katika hali yake ya kawaida
kisha akatoweka eneo hilo.
 
Sehemu ya kumi na saba
.........Ilipoishia.........
Baada ya kimaliza kuyasema hayo moto ule
ulizimika na Sor akarudi katika hali yake ya kawaida
kisha akatoweka eneo hilo.
........Tiririka nayo...........
Nilikuwa nimetoka katika varangati lile na
Lamson.majeraha yalikuwa yameenea mwilini
ukijumlisha na maumivu mwili mzima sikuwa hata
na hamu ya kuzungumza na mtu yeyote yule
nyumbani endapo angeniuliza swali
Nilipofika katika wigo wa nyumbani kuna picha
Fulani ya watu waliolala hawajielewi ilipita ghafla
usoni kwangu sasa nikaanza kuhisia ni wapi wale
watu walipo ikabidi nisimame ili nivute taswira ya
tukio lile na kweli niliweza kutambua kuwa ni
familia yetu.Kwa haraka nilipata nguvu za kukimbia
na kuingia ndani
Hali niliyoikuta mle ilinishangaza kwani sikujua
wamepatwa na nini haswa,nilikaa chini kutokana na
kuishiwa nguvu na kuanza kulia kama mtoto mdogo
maana kila ambaye nilimpata na kujaribu
kumtikisa hakuonesha ushirikiano wowote
**********★★★★★★★★★★
Lisa alifika mpaka shuleni kama kawaida na
Kwakuwa alikuwa ameanza kujenga ukaribu na
Humph alitulia darasani akimsubiri lakini muda
ulizidi kwenda hatimaye muda wa masomo ukaisha
ikafika muda wa kupumzika lakini bado Humph
hakutokea katika maeneo ya shule.
Baada ya kuona hivyo alianza kuhisi kitu kutokana
na matukio ya hapo awali yaliyowahi kutokea hasa
ya Yule kijana aliyekuwa akimuokoa,alipojumlisha
matukio yote na lile la mpambano uliotokea Jana
yake alianza kufikiria kuwa Humph anaweza kuwa
huyo kijana ambaye huwa anaokoa watu.
Aliona kuliko kukurupuka bora aanze na moja
kumfuatilia Humph kiukaribu zaidi.kitu cha kwanza
kabisa Lisa alichukua ule mkufu na kuuvaa shingoni
ili iwe rahisi kumpata mhusika.
*************************
Humph alikesha usiku kucha akiwa amelia mpaka
amechoka,akiwa katika majonzi hayo upepo ulivuma
kwa kasi mno ikiwa ni kwa ghafla hali iliyopelekea
Humph aache anayoyafanya na kuangalia upande
ambao upepo umetokea.
Alikuwa ni mzee Mandevu ambaye alisindikizwa na
upepo ule nae alionekana yu katika majonzi
makubwa hasa kutokana na tatizo lililomkumba
Humph.
Humph alianza kulia upya ikawa ni kazi ya mzee
Mandevu kumbembeleza atulie,Haikuchukua muda
Humph alinyamaza kimya,
Ndipo ulimi ukampata tena mzee Mandevu
aliyeanza kuzungumza kwa sauti ya chini iliyosikika
na wao wawili tu.
"Hii kazi yote ameifanya malkia Sor kama kigezo
cha kutaka wewe ulegeze msimamo wako" akatulia
kidogo kisha akaendelea
"Bado nafasi ipo ya kuweza kumdhibiti na pia kuna
uwezekano wa kuiponya familia yako ndani ya siku
tatu kuanzia Jana"
Humph alistuka baada ya kusikia kuwa inawezekana
familia yake ikapona kutoka katika ule ugonjwa wa
ajabu ambao ulifanana na ule unaoitwa coma
(kupooza)
"Nambie kwanza jinsi ya kuiokoa familia yangu
Tafadhali" Aliongea Humph kwa msisitizo
"Sawa,kitu cha kwanza inatakiwa uende katika
mapango ya Mlima Lai ambayo hayajulikani na mtu
yeyote wakawaida zaidi ya jamii yetu" kisha
akamuangalia Humph lakini haikuwa angalia ya
kawaida ilionekana wazi kuna kitu alikuwa akifikiria
"Humph hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo ila ni ya
hatari mno sijui...." alishindwa kumalizia
"Sijui nini mzee Mandevu mbona sikuelewi"
aliongeza Humph
"Laaaah! ngoja tu nikwambie ni hivi sidhani kama
utarudi ukiwa hai kiufupi naogopa kukupoteza"
alitoa hisia zake mzee mandevu juu ya kinachoenda
kutokea
"Kwanini useme hivyo,sikia hii ni familia yangu na
nina uchungu nao na ukiangalia kwa undani Mimi
ndiye mwanzilishi wa matatizo yao kwahiyo sina
jinsi nitafanya lolote kwaajili yao" aliongea Humph
akiwa na uchungu mkubwa
"Sawa nimekuelewa kijana katika lile pango kuna
milango miwili unapoingia na miwili unapotoka nje
sasa unapoingia ingia mlango wa kulia ambao una
shimo kubwa lisiloeleweka ukubwa wake rasmi na
humo ndimo hazina inapatikana katikati kabisa mwa
shimo hilo pia ukumbuke endapo utaingia mlango
wa kushoto huko kuna buibui ambao wanasumu kali
na endapo wakikuuma hauwezi kumaliza sekunde
kadhaa kifo ni halali yako,buibui hao ni wakubwa na
hawajawahi kupatikana sehemu nyingine ni wa karne
na karne humo ndani" swali mpaka hapo
"Sina swali mzee ila labda kama nikipotea njia
nitatokaje?"
"oooooh!! kweli sasa wakati wakutoka utakutana na
milango miwili vile vile pita kushoto maana kulia
kuna bui bui wengi mno na kama ukipotea angalia
hiyo hazina yako utakayoipata itakuonesha sehemu
ya kwenda japo sina hakika kama unaweza
kuwatoroka buibui" aliongea mzee Mandevu
"Sawa mzee mimi naona niende sasa maana muda
si rafiki"
"Bahati njema kijana wangu kumbuka kufanya hayo
kwaajili ya familia yako hivyo kuwa mwangalifu na
nikukumbushe kuwa ukiwa ndani ya pango huwezi
kupotea kimiujiza kutokana na nguvu zilizopo mle
ndani"
************************
Nilikuwa tayari nimefika katika pango nililoelekezwa
na mzee Mandevu moja kwa moja niliifuata njia ya
kuingia ndani na kuanza kuzamia ndani
zaidi,kutokana na Giza kuwa kali nilitumia mwanga
wa macho yangu katika safari hii isiyo na
matumaini
Niliifikia milango ile miwili nikafuata mlango wa
kulia kama maelekezo yalivyokuwa. Nilitembea
umbali mrefu kidogo nikaanza kuona mwanga wa
zambarau na kadri nilivyozidi kwenda ndiyo mwanga
ulivyozidi kuongezeka na mwisho nikafika katika
shimo lile ambalo sikujua urefu wake maana chini
kulikuwa ni giza tu na upana haukueleweka japo
niliona mwisho wake ambapo ukiruka unaenda
kuishia katika kuta za shimo lile.
Nilifikiria ni njia gani itakayonisaidia kupita pale
nichukue ile hazina sikupata jibu nikachukua kibegi
kidogo nilichokuja nacho nikasogea pembeni na
kuuegemea ukuta
Nikatoa chakula kiasi nilichobeba kisha nikaanza
kula taratibu huku nikiwa nawaza na kuwazua jinsi
ya kuikwapua ile hazina. Nilipomaliza kula
nikasogea tena karibia na lile shimo nikapima ule
umbali uliopo kati ya sehemu nilipo na usawa wa
ile hazina alikuwa na jinsi zaidi ya kuruka tu.
Nilirudi nyuma na kujipanga nikaanza kuhesabu
kuanzia moja..mbili..tatu nikachomoka mbio na
kuruka mpaka katika ukuta ule na kama
nilivyotegemea niliteleza kwenye ukuta kwenda chini
hofu ikiwa imeniandama vilivyo.
Je Humph atatoka salama?
 
Sehemu ya kumi na nane
.........Ilipoishia.........
Nilirudi nyuma na kujipanga nikaanza kuhesabu
kuanzia moja..mbili..tatu nikachomoka mbio na
kuruka mpaka katika ukuta ule na kama
nilivyotegemea niliteleza kwenye ukuta kwenda chini
hofu ikiwa imeniandama vilivyo.
.........Endelea...........
Niliteremka kwa kasi mno kufuata ukuta mpaka
nilihisi maumivu ya michubuko kuanzia tumboni
mpaka kifuani. Niliifikia ile sehemu ambayo kuna
hazina kwa kuwa nilikuwa nashuka kwa mwendo wa
hatari nilitegeshea mkono na nilipofikia tu ile hazina
nikaikwapua kwa nguvu maana ilionekana imeshika
maeneo fulani.
Nilipoikwapua tu ghafla kuna kitu kama giza
kikapita unaweza kusema nilifumba macho na
kufumbua. Nilikuwa sehemu nyingine tofauti na ile
niliyopita mwanzo,bado kulikuwa na giza totoro
Nikabofya saa yangu ya mkononi ambayo iliwaka
nikatazama muda ulikuwa ni saa 7 za usiku hii
ikiamanisha nimebakiza masaa kadhaa niwe
nimemaliza siku tatu. Kwa mara ya kwanza toka
nipate yale matatizo nilitabasamu nikiwa nina imani
kuwa nimeushinda mtihani niliokuwa nao.
Nilitazama hazina ile nikabaki nimeduwaa baada ya
kuona ni jiwe fulani la mviringo linatoa mwanga
wenye rangi ya zambarau,Sikujali sana nikaliweka
katika begi langu na kulirudisha tena mgongoni
Kwa mwendo wa haraka nilianza kufuata ile njia kwa
msaada wa macho yangu yaliyokuwa yanatoa
mwanga,ilinichukua kama nusu saa nikakutana na
milango miwili tena kila mmoja ukiwa na giza nene
Nilipokuwa hapo sikuangalia ni mlango upi naingia
kulingana na sheria nilizoambiwa,Mimi niliingia tu
kutokana na haraka haraka zangu za kuwaisha
hazina ile ili familia yangu ikapate matibabu.
Nilitembea kwa kwa kitambo kifupi nilipofika
maeneo fulani nilianza kuhisi kama miungurumo ya
chini chini ikitokea mbele ninakoenda sikuitilia
shaka nikajua huenda nimesikia vibaya. Nilizidi
kusonga mbele mpaka maeneo fulani ambako
miungurumo iliongezeka nilipotazama pembeni
nikaona kuna mlango nikarudisha macho mbele njia
imenyooka
Kabla sijajiuliza swali nikasikia vishindo vinakuja
upande wangu nilipotazama kule nilikouona mlango
asalaleeee!! moyo ulipiga kwa nguvu paaaah!!
sikuamini kama ni kweli ninachokiona mbele yangu
Lilikuwa bui bui moja kubwa lenye manyoya kila
sehemu ya mwili wake na niliporudisha tena macho
kwenye njia ninayokwenda ndiyo balaaa!! ile njia
ilikuwa pana kwahiyo buibui wawili walikuwa
wanakuja kwa madaha upande wangu huku udenda
wa hamu ya nyama ukiwatoka
**********************
Mzee Mandevu alistuka ghafla akasimama sebuleni
pale kisha akashika kichwa kwa muda na kushusha
mikono sijui kama alipatwa na nini lakini
hakuchukua muda akatamka neno "Humph"
Alianza kuzunguka katika sebule lile mara kushoto
tena kutoka kushoto mpaka kulia kama
amechanganyikiwa vile
Baada ya muda alianza kuongea na mtu japo
hakuonekana ni nani aliyekuwa akiongea
naye."Uniruhusu nimsaidie huyu kijana kwani
akipotea yeye tutakuwa tumepoteza mtu muhimu
ambaye tumemsubiri kwa miaka mingi mno"
"Hapana,kijana bado hajashindwa hebu vuta subira
kwanza utafahamu ni kwanini tunasema yeye ni wa
kipekee"
Mzee Mandevu alone kana hajaridhishwa wazi na
kauli ile lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kutii.
**************************
Mwalimu Remijo hakuweza kukaa kwa amani baada
ya kuingia darasani na kumkosa Humph katika
kipindi chake hakika alijua kuwa ni lazima Humph
atakuwa matatizoni
muda wote ofisini alionekana mwenye mawazo
mno,alijiuliza maswali kadhaa afanye nini lakini
hakuna alichovuna kwa kuwa sheria za kazi
haziruhusu mwalimu kutoka kama sio muda wa
kutoka kazini pia ilikuwa hairuhusiwi kutoroka
kazini.
Akiwa na mawazo hayo wazo moja likampitia
akakumbuka kuwa mwalimu mkuu huwa hapendi
wanafunzi wazembe hasa wanaokosa kiholela Mara
nyingi hupewa adhabu kali au kusimamishwa
kwenda shule.
Aliinuka kutoka ofisini mwake na kuelekea kwa
mwalimu Odey ambaye alikuwa ni nwalimu wa
darasa analosomea Humph.
"Samahani madam Ode kuna kijana mmoja
aliombewa ruhusa na mzazi wake na kwa bahati
mbaya anasoma katika darasa lako"
"Anaitwa nani?" aliuliza madam Ode
"Humph, Humph Isack" akahitimisha
"sawa nashukuru kwa taarifa" akaongeza madam
Ode
madam Remijo alishusha pumzi nyingi kuona
ameutua mzigo huo na moja kwa moja akaendelea
na kazi baada ya kupunguza kiasi Fulani cha
wasiwasi.
**************-***----**********
Nilikuwa nakimbia katika lile pango kurudi nyuma
lakini sikufika pale nilipotokea ndipo nilizidi
kuchanganyikiwa na nilijua wazi kuwa nimepotea na
nilipoikumbuka ile kauli ya mzee Mandevu
aliyosema hakuna mtu aliyewahi kutoka akiwa hai
loooh!! ilizidi kunikata maini na kuniongezea uoga
juu ya wadudu wale.
Kila nilipoenda walinifuata kwa bahati nzuri nilipata
kaupenyo fulani nikaweza kujifinya buibui wale
wakanipita kisha kimya kikatanda,Nilikaa pale kwa
muda nilivyoona kimya nikawasha saa yangu
niangalie muda
ule mwanga ulivyowaka nikatazama saa ile nainua
macho nikakutana na kichwa cha fuvu
tunaangaliana,nilipiga ukunga yalaaaaaaaa!!!!
nakufaaaa!!
Ile sauti ikasambaa katika lile pango ikawa
inajirudia rudia.Niliinuka na kuanza kukimbia tena
nikiwa sijui wapi naelekea lakini ghafla mbele
lilikuja buibui moja kubwa kuliko yale ya mwanzo
nilipogeuka nyuma nikakutana na buibui wale
wengine wanakuja kwahiyo nikawa nimewekwa Kati
Nilianza kuona mwili unatetemeka wenyewe na
nguvu zinaniishia akili ikiwa haifanyi kazi kabisa
lakini kwa wakati huo kuna sauti ile inayopenda
kusema na Mimi ilinisemesha"kumbuka familia
yako ipo katika matatizo mazito na muda umebaki
mchache mno"
Niliposikia vile nilipata ujasiri na nguvu mpya ya
kupambana wakati huo lile buibui la mbele
limekaribia kunifikia yale ya nyuma yalikuwa bado.
Nikarudi hatua kadhaa nyuma alafu kwa kasi ya
risasi nikajichomoa kama namfuata yule buibui
kisha nikabadili uelekeo na kukanyaga ukutani kwa
kukimbia na kuruka juu mpaka nikamfikia yule
buibui juu ya mgongo wake nikang'ang'ania
manyoya aliyokuwa nayo.
Buibui wale wengine walianza kupiga kelele na huyu
niliyempanda hakutaka kukubali kiurahisi vile nikae
juu yake alianza kukigonga ukutani kwa nguvu zote
lakini hakufanikiwa kunishusha maana nilishikilia
mno.
Buibui wengine walivyoona vile wakaanza
kumshambulia mwenzao ambaye naye hakukaa
kimya alijibu mashambulizi na walipompisha tu
alianza kukimbia akielekea nisipokujua huku na
wenzake wakiwa wamemuungia kwa nyuma....
 
Sehemu ya kumi na tisa
..........ilipoishia.........
Buibui wengine walivyoona vile wakaanza
kumshambulia mwenzao ambaye naye hakukaa
kimya alijibu mashambulizi na walipompisha tu
alianza kukimbia akielekea nisipokujua huku na
wenzake wakiwa wamemuungia kwa nyuma....
.............shuka nayo...........
Nilikuwa na hofu kwasababu yale manyoya yalikuwa
yanateleza hivyo niliogopa kuanguka kisha niliwe na
buibui wale kama kitoweo.
Tulifika sehemu moja ambayo haikuwa na njia yule
buibui akasimama na kuanza kujigongesha ukutani
ilimradi tu nianguke lakini niling'ang'ania mno ili
kuokoa Maisha yangu.
wale buibui wengine walipofika waliniona naning'inia
kwa juu na Kwakuwa yule buibui alikuwa mkubwa
kiasi hawakuweza kunitoa na matokeo yake
wakaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe.Walipig
ana mno hatimaye katika ile vita nilijikuta
nikichomoka maana mikono ilikuwa inateleza
nikaangukia katika upenyo mmoja ambao hapo
awali sikuuona
Niliinuka nikafungua begi na kuangalia ile hazina
nikakuta ipo salama.saa yangu ya mkononi ilikuwa
inaonesha kuwa ni saa tatu za usiku,hapo nikaanza
kupatwa na wasiwasi kuwa huenda nikachelewa
masaa mawili yaliyobaki,niliikumbuka ile kauli ya
mzee Mandevu kuwa nikipotea niangalie ile hazina
ina ramani
Nilipoichunguza mara ya kwanza niliambulia
mwanga tu uliokuwa unatoka kwenye hazina
ile,Nikaamua kutumia nguvu za macho niliyonayo
nikaona ramani inayoonesha nilipo na kutokana na
somo la ramani kuwa vizuri kichwani kwangu
nilianza kufuata njia ambayo ilinichukua takribani
saa nzima kufika eneo lenye milango miwili ya
kutokea.
Nikukumbushe tu kidogo kuwa baada ya kurushiwa
katika upenyo ule na yule buibui wao walibaki
wanapigana bila kujua kuwa nimefanikiwa
kuwatoroka. Sikufanya ajizi kwani nilihitaji sana
kuisaidia familia yangu nikapita mlango wenye
matumaini na kutokea sehemu yenye mwanga hafifu
wa mbalamwezi unaotokea nje nikafuata uelekeo ule
mpaka nje kabisa nikiwa hoi bin taaban.
Niliendelea kutoka maeneo yale ya pango maana
sikuwa na uwezo wa kupotea katika yale maeneo.
Ghafla nilianza kuzisikia sauti kali za miluzi bila
kuuliza nikagundua ni popo lakini kwa sauti zile
zilivyokubwa ilionekana wazi kuwa wale si popo wa
kawaida hata kidogo.
Nilianza kujivuta vuta nikimbie,kila nilipogeuka
nyuma niliona vivuli vinakuja kwa kasi upande
wangu,nilijitahidi mno kukimbia na nilipoona hali
inakuwa tete
nikachukua hazina ile na kuiweka ndani ya begi
kisha nikalirudisha mgongoni na kuanza kukimbia
tena kwa kujikongoja.
nilipokimbia hatua kadhaa nikatazama nyuma
loooh!! nilifanya kosa kwani nilipogeuka tu
nikapokea Kofi lililonirusha umbali wa kama hatua
tano hivi,maumivu niliyoyasikia ni kasheshe lakini
bado nilikuwa mbishi nikaanza kunyanyuka
kumbe wakati na nyanyuka wale popo walikuwa
wananilia dolia,nikafanikiwa kusimama kabisa
ghafla nikaisikia sauti ya popo nyuma yangu
inayonifanya nigeuke kwa kasi,cha ajabu zaidi
nakuta hakuna kitu basi nikageuka tena nyuma kwa
hofu kuu nikapokelewa na Kofi lingine nzito
lililonirusha mbali zaidi
Ndipo niliamua kulala hivyo hivyo nikiwa naangalia
juu pia nikilaani kitendo cha mzee Mandevu
kutoniambia kuwa kuna popo hatari namna
ile.Nikiwa pale chini naikumbuka familia yangu
kuwa inauhitaji sana msaada wangu
Hasira zinanivaa na kusema liwalo na liwe
nitapambana kufa na kupona,Nilipoangalia juu moyo
ulilipuka mno kwani wale popo walikuwa
wanalizunguka anga huku wakipiga makelele alafu
walikuwa wakubwa kama mbuni
Sikurudi nyuma nikainuka kwa kujitahidi kisha
nikapiga hatua moja ile hatua ya pili sijaimaliza
nikakwapuliwa kama kifaranga juu kwa juu na
kutupwa chini na kudondoka vibaya. Wale popo
wakaanza kupiga kelele zilizokuwa zinaniumiza
masikio mpaka nikafikia hatua ya kuyaziba
Begi nililokuwa nalo lilidondokea mbele yangu
kutokana na zile.sauti kuwa kali nilibaki na gaa gaa
chini mpaka pale zile sauti zilipokoma.Nikaanza
kutambaa kulifuata begi lenye hazina.
*************************
Mzee Mandevu alisubiri sana mpaka akachoka
lakini Humph hakutokea maeneo hayo,akiangalia
hali ya wagonjwa wale wala haikuwa na matumaini
badala yake walikuwa wanakoroma tu. Alia za
kujisemea peke yake "Humph fanya kitu kijana
nakutegemea tafadhali sana usife eeeh! sawa kijana
wangu Fanya kitu kwaajili ya hii familia"
Japo mzee huyu alikuwa jasiri mno lakini ajabu ya
mwaka ni kwamba katika macho yake kulitengeneza
maji maji Fulani ambayo yaliashiria kuwa mda
mfupi ujao itashuka mvua kubwa ya machozi.
Macho ya mzee Mandevu yalitua ukutani ambako
kulikuwa na saa moja kubwa ya ukutani iliyosomeka
kuwa ni saa tano na dakika mbili usiku.
Mzee Mandevu alikodoa macho asiamini kile
anachokiona katika saa ile akatamani kusema kitu
lakini mdomo ukamsaliti na kuwa mzito huku
ukibaki unacheza cheza tu kusema kwamba
umeshikwa na hasira kali.
*****KWA HUMPH*******
Nilizidi kutambaa mpaka katika begi langu
nikafanikiwa kulishika nikalivuta na kulikumbatia
kisha nikawa naiangalia anga. Bahati niliyokuwa
nayo ni sauti ile ambayo huwa inanipa matumaini
na safari hii haikuwa mbali na mimi
Iliniambia "chukua hiyo hazina uioneshe juu kwa hao
popo kufuata uelekeo wa mbalamwezi hakikisha
mwanga wake unagonga hapo katika hazina hiyo"
Kwa haraka nikafungua begi na kutoa hazina
ambayo moja kwa moja niliangalia uelekeo wa
mbalamwezi na kuinyoosha juu,mwanga wa
mbalamwezi ulipogonga kwenye hazina ule mwanga
wa zambarau ukasambaa eneo lote wale popo
walianza kulia wakiashilia maumivu makali
yanayowapata. wakatoweka kwa fujo eneo lile
Nikainuka taratibu na kuanza kuondoka eneo
lile,nilipotazama saa yangu ilikuwa saa tano na nusu
hali iliyofanya nikose raha kwasababu ikifika saa
sita basi hakutakuwa na uwezekano wa familia
yangu kupona.
Nilitembea mpaka pale nilipotoka katika ule msitu
kwa haraka nikajaribu kupotea na nikafanikiwa.
**********************
Ilikuwa saa tano na dakika arobaini usiku mzee
Mandevu akiwa amesimama sebuleni anatazama
mshale wa saa hiyo ya ukutani ghafla akasikia
kishindo nje akawahi kwenda kufungua mlango
Kishindo kile kilikuwa ni cha Humph ambaye
alipokelewa na mzee Mandevu akiwa hoi mno.
Wakasogea mpaka katika kiti na kumkalisha Humph
Mzee Mandevu alitengeneza Pentagon kwa ushapu
wa ajabu pale pale sebuleni kisha akaingia katikati
na ile hazin,aliposimama tu na moto ukawaka
pande zote na ndipo alipoanza kutamka maneno
haya kwa kurudia rudia japo mwanzo hayakuwa
yakisikika wazi.
"Je libère cette maladie sur cette famille pour le
prix de ce trésor. Veuillez l’accepter" ikiwa na
maana kwamba
"Naachia magonjwa yote yanayoikumba familia hii
kwa sadaka ya hazina hii.Tafadhali ipokeeni"
Alinyoosha mikono juu baada ya kumaliza maneno
hayo huku akiwa ameishika vyema hazina
hiyo.Tahamaki ni kwamba saa sita ilikuwa tayari
imefika hivyo moto ukazima wenyewe na hazina
ikapoteza nuru yake na kuwa jiwe la kawaida
Mzee Mandevu alipiga magoti kwa uchungu na
kushusha pumzi ndefu..
 
Sehemu ya ishirini
........Ilipoishia..........
Alinyoosha mikono juu baada ya kumaliza maneno
hayo huku akiwa ameishika vyema hazina
hiyo.Tahamaki ni kwamba saa sita ilikuwa tayari
imefika hivyo moto ukazima wenyewe na hazina
ikapoteza nuru yake na kuwa jiwe la kawaida
Mzee Mandevu alipiga magoti kwa uchungu na
kushusha pumzi ndefu..
..........endelea.............
Hakufanya vile kwa ridhaa yake bali ni kutokana na
muda kumtupa mkono,alifadhaika mno kwa kitendo
kile kilichotokea ambacho ukweli ulibaki kuwa
walifanya kazi isiyo na faida licha ya taabu zote
walizopitia
Humph nae aligundua kuwa tayari amechelewa
kufikisha hazina hiyo.Alianza kulia maana alipoteza
watu muhimu mno katika Maisha yake,si hivyo tu
bali kupoteza ndugu katika hali ya utata namna hiyo
si jambo jema hata kidogo ukizingatia uwezo wa
kuwaokoa ulikuwa ndani ya uwezo wake.
wote waliomboleza haswaaa mpaka ikafikia mahali
kila mtu akakaa peke yake akitafakari nini afanye
japo Humph alikuwa kila sekunde anamlaani Sor
kwa kitendo alichomfanyia.
Wakiwa katika hali hiyo ghafla kikohozi kikavu
kilianza kusikika kikitokea sakafuni na chafya
mfululizo,walipotazama kwa pamoja walishangaa
kuona Sifa ameamka na muda huo huo na wengine
nao wakaanza kukohoa huku wakijitahidi kuinuka
sakafuni hapo.
Vilio vilikata na furaha ikaanza kuchanua upya baada
ya kuona familia imerejea tena katika ubora wake
.Mzee Mandevu akamgeukia Humph "leta maji ya
kunywa Fanya haraka" na Humph bila kuuliza akatii
Baada ya kupewa maji kila mtu na kunywa ndipo
fahamu zikawarejea,wakainuliwa rasmi na kuketi
kisha mazungumzo mafupi yakafuatia
"Poleni sana ndugu zangu kwa matatizo
yaliyowakumba" mzee Mandevu aliongea huku
akiwatazama kwa zamu
"Niseme asante Kwakuwa umetoa pole lakini
sijafahamu haswaa hiyo pole inahusu nini Mzee"
aliongea mzee Kasai akiwa ameyatumbua macho
yake kwa mzee Mandevu
"Hii pole ni kwasababu mlipatwa na ajali
iliyosababishwa na gesi chafu ambayo ilipulizwa
katika nyumba yenu na haijulikani ni nani aliyefanya
hivyo na kwa lengo lipi" aliongopea mzee Mandevu
"oooh! kwahiyo...? au...? aaah...? sawa sawa
nashukuru kwa msaada wako" Alishindwa kuongea
mzee Kasai yote ni kwasababu ya kushindwa
kuelewa ni nani hasa aliyefanya hivyo na hata
akijaribu kuvuta kumbukumbu ya maadui alionao
hakupata jibu maana yeye ni mtu mwema sikuzote
na hata kama wangekuwa na nia mbaya kwanini
hawajabeba kitu chochote kile hilo ndilo
lililomsumbua kichwani mwake
Humph alikuwa akitabasamu tu na kustaajabishwa
na akili za mzee Mandevu katika kubadilisha ukweli
wa mambo kuwa vile anavyotaka.
Hatimaye mzee Mandevu aliaga na kuondoka akidai
kuwa alikuwa mpita njia tu ili asitiliwe shaka huku
akiwa amejizolea shukrani nyingi ambazo kama
wangefungashia basi angeondoka na pipa nzima la
shukrani.
**************************
Lisa hakuwa na subira hata kidogo kwani alihisi
kabisa kuwa endapo atafanya mchezo basi yule
mwokozi wake atanyakuliwa na msichana mwingine
kabla yake,alikuwa na shauku mno ya kumfahamu ili
amwambie yanayomsibu kila siku amfikiriapo mtu
huyo.
Alipanga kuwa ifikapo asubuhi awahi shuleni kisha
akutane na Humph na ajaribu kumshawishi
amuonyeshe huyo mtu ambaye anautesa moyo wake
kwa asilimia kubwa.
Hakuchi hakuchi hatimaye kulikucha Lisa akiwa na
hamu ya kufika shuleni na hivyo ndivyo ilivyokuwa
kwani alifika mapema kuliko kawaida yake,akiwa
ameegemea ukuta huku ameushika mkufu na
kujiongelea kama chizi Humph nae alikuwa anapita
maeneo hayo akiwa anachechemea kwa mbali na
alama Fulani ya kibao ikiwa imejichora shavuni
pake.
Alivutiwa na mtindo aliokuwa amekaa Lisa ambao
ulimpa hamasa ya kumsogelea pale alipo,alipomfik
ia alishindwa kuelewa maneno ambayo yalikuwa
yanatamkwa na Lisa na kingine.kilichomuacha hoi
ni pale ambapo Lisa hakugundua uwepo wake eneo
lile.
Humph alipiga hesabu akaamua kumstua kwa
kupiga kelele"arrrrrrrrrrrrrr" zilizomfanya Lisa
akurupuke na kurukia pembeni huku ameshikilia
kifua chake na kuhema kwa fujo mno.
Humph bila kujali alikuwa amekauka kwa kicheko
mpaka machozi yakawa yanatiririka aiseeeee!
duniani kuna watu huwa wanacheka ni kama
midomo yao inatumia mashine na mbavu zao zina
jenereta.
Lisa alichukia mno kwa kitendo hicho akazira na
kuondoka eneo hilo akiwa tayari amesahau ni kitu
gani kilimpeleka pale katika ukuta ule. Humph
alikuwa ameshalikoroga hivyo inambidi atumie njia
mbadala kumrudisha hemani ndege yule mwenye
uzuri wa kila rangi ambaye ni Lisa.
*******------**********
yapata mida ya saa tisa alasiri Lisa akiwa njiani
anarejea kwao baada ya masomo,kwa muonekano
tu alidhihirisha kuwa hayuko sawa na ndivyo
ilivyokuwa kwani alikuwa amezama mno katika
dimbwi la mawazo juu ya kumpata mkombozi wake
ambaye mpaka wakati huo hakufahamu kuwa ni
Humph.
Humph anamkimbilia Lisa kisha wanaongozana
kurudi nyumbani,wakiwa wanatembea Humph
anaamua kuvunja ukimya
"Hey! um! aaaaah!! najua kama..."
"umenikwaza lakini haina haja ya kuniomba
msamaha" alidakia Lisa kwa sauti inayoamanisha
"Hapana nimetenda kosa tena kosa kubwa
linalostahili msamaha tafadhali nimekosa na
ninahitaji msamaha wako" Humph alikuwa akijieleza
kwa upole
"Isingekuwa nimempenda yule mwanaume ambaye
alinikomboa hakika huyu nae alikuwa ananifaa
kabisa" alijiongelea Lisa moyoni
"Usijali Humph wewe ni rafiki mwema kwangu hivyo
sina budi kukusamehe uwe na amani" Lisa aliamua
kumaliza kabisa tatizo hilo
Walitembea njia nzima wakiwa wametawaliwa na
ukimya wa aina yake ambao ulivunjika pindi Lisa
alipokumbuka kuwa alihitaji msaada wa Humph
kumfahamu yule aliyemuokoa mara kadhaaa
"Humph kuna kitu nahitaji unisaidie" aliongea Lisa
huku akimgeukia Humph
"Nakusikiliza Lisa" Humph alijibu kwa unyenyekevu
"Sijui kama utanielewa lakini nd'o hivyo ninavyotaka"
Lisa alizidi kuongea huku akiwa hajiamini
"Sema tu nipo kwaajili yako kama rafiki yako"
alisema Humph
"Humph Mimi namtaka Yule rafiki yako ambaye
aloniokoa kuna kitu natamani nimwambie tukiwa
wawili hivyo nahitaji msaada wako unikutanishe
nae" Lisa alijitetea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom