Simulizi: Lisa

SIMULIZI.....LISA
KIRASA......36-40

SURA YA 36

Nusu saa baadaye, wote wawili walifika katika moja ya maduka makubwa ya kifahari ya Oyster Bay. Lisa hakuacha kunung'unika tangu dakika ile alipoingia dukani. “Kwa nini umenileta hapa? Nguo zao ni ghali. Alvin ni mtu wa kawaida na mchumi sana kwenye hela. Pamoja na pesa zote alizonazo yeye anaendesha Harrier tu. Ndiyo, avavaa vizuri na anapendeza lakini nguo zake hutengenezewa na wabunifu wake binafsi, hakika amenituma kwa hili kama mtego tu. Atanifokea sana kwa kumnunulia nguo za gharama kama hizi”

"Lakini mfanyabiashara aliyefanikiwa kama yeye anapaswa kuvaa kitu cha gharama zaidi. Wewe unatakiwa umbadilishe. Angalia, vipi kuhusu mtindo huu?" Pamela alimkokota hadi kwenye duka la kifahari la nguo za kiume na kumuelekezea suti moja kali.

Lisa aliitazama kwa haraka. "Suti ni nzuri, lakini umbo lake haliendani na la Alvin."

"Sawa, basi mchukulie ile pale, ni nyembamba kama yeye, itamfaa sana au vipi," Pamela alishauri lakini Lisa alikuwa bado na wasiwasi. Hata hakuwa na uhakika alitaka kumnunulia nini Alvin.

"Twende zetu. Ni ghali sana hapa.” Kwa aibu, Lisa alianza kumkokota rafiki yake kuelekea mlangoni.

Muuzaji akawasogelea na ghafla wakasimama kumsikiliza. "Suti hii ni mtindo mpya kabisa, imetengenezwa na mbunifu maarufu Sheria Ngowi. Kuna suti mbili tu kama hizi katika nchi nzima.”

"Hah, unaweza kuokoa muda na nguvu yako. Watu hohehahe kama yeye hawataweza kumudu.” Maneno ya dhihaka yalivuma hewani. Kisha, Janet Kileo na Cindy Tambwe wakaingia machoni mwao.

“Miss Kileo, Bibi Tambwe…” Macho ya muuzaji yaling’aa huku mara moja akikimbia kwenda kuwasalimia.

Janet alimtupia jicho la pembeni Lisa huku akijigamba. “Kwa hiyo umejipatia bwana mpya? Lakini yeye ni mtu mdogo tu hana lolote. Mtu wako ni mwanasheria uchwara tu. Hata angekuwa na mafanikio kiasi gani katika kazi yake, bado anategemea matajiri tu kama sisi ili kupata pesa.”

Pamela alicheka kwa hasira. “Mwanasheria? Je! unajua kuwa mpenzi wake…”
Kabla Pamela hajamaliza usemi wake, Lisa alimshika mkono wake na kutikisa kichwa. Ndoa yake na Alvin ilikuwa siri. Alijiuliza ni mwanaume gani Janet alikuwa amekosea na kudhani kuwa mi mpenzi wake.

Tabasamu la furaha likaangaza usoni mwa Cindy. Alikumbuka jinsi alivyokuwa akiambatana sana na Lisa hapo zamani kwa sababu familia yao ilikuwa bora zaidi. "Lisa, labda unapaswa kununua mahali pengine. Nijuavyo mimi kuna pesa chache tu kwenye kadi yako sasa.”

“Cindy, usivuke mipaka.” Pamela alikasirika. Kabla hawajakosana urafiki, Pamela alikuwa amemueleza Cindy juu ya hali ngumu ya Lisa, bila kutarajia Cindy angewageuka na kuwasaliti bila wasiwasi.

Kama ilivyotarajiwa, muuzaji alionyesha kutokuwa na subira aliposikia kwamba kina Lisa walikuwa hawana pesa za kutosha. “Tafadhali muondoke ikiwa hamna uwezo wa kumudu hili. Tuna upungufu wa wafanyakazi na hatuwezi kuhudumia kila mtu.”

"Nani kasema hatuwezi kumdu?" Pamela akatoa kadi yake ya benki.

Janet alidhihaki, “Cindy, ni bora ulivyoamua kuachana nao. Marafiki kama hawa watakuchoresha tu.”

Cindy naye akazidisha machungu ya Lisa. "Kwa kweli, lazima apige vizinga kwa marafiki ili anunue nguo."

Lisa , ambaye kwa kawaida alikuwa mvumilivu sana, hakuweza tena kuvumilia dhihaka hizo.
“Hakuna shida hivi ni vitu vidogo sana kwangu nikitaka nanunua tu pesa ipo.” Lisa aliwarusha roho. “Hili ni toleo la pekee, hakuna hata mmoja wenu anayeweza kugusa hapa.” Alichomoa kadi ya benki aliyopewa na Alvin na kumkabidhi muuzaji. “Si ulisema una seti mbili tu za hii suti? Nazitaka zote. Sitaruhusu mtu mwingine yeyote kuvaa nguo zinazofanana na za mpenzi wangu.”

Hii ilimshangaza muuzaji, lakini ni nani angekataa pesa? "Kwa seti zote mbili zitafikia jumla ya shilingi milioni tano."

Lisa alihisi miguu yake ikiishiwa nguvu. Hakuwa na hakika kama Alvin angemvumilia kwa kumnunulia nguo za gharama ya shilingi milioni tano. Lakini, vipi ikiwa ingezidi kikomo cha kadi? Alijiuliza huku akihisi angeibeba vipi aibu yake mbele ya wale wambea waliokuwa wakimkodolea macho. Alipoibia sura za Janet na Cindy waliokuwa wakingoja kwa hamu aaibike ili wamcheke, alijilazimisha kutoa kadi. 'Naomba tu iwe na pesa za kutosha,' alijiwazia mara kwa mara.

"Lakini, ni lazima nikukumbushe kwamba hatukubali kurudishiwa bidhaa za toleo maalum, ukinunua umenunua," muuzaji alimpa angalizo mapema.
Lisa alihisi ubongo wake ukiganda, lakini akajisemea kimoyomoyo, ‘potelea mbali’.’

Cindy aliziba mdomo kwa mshangao wa madaha. "Lisa, natumai haukuwa umepanga kurudisha nguo baadaye."

Lisa alicheka kana kwamba alikuwa anasikia utani wa kuchekesha. "Sitafanya kitu cha kimasikini kama hicho. Pia, acha kuniita Lisa . Kusikia ukisema unaita jina langu masikio yangu yanauma.” Aligeuka kumwangalia muuzaji. “Fanya haraka uniandalie. Sitaki kuendelea kuwasikia mbwa vichaa wakinibwekea.”

“Wewe…” Donge la hasira lilitawala usoni mwa Cindy lakini hakuwa na cha kufanya.

Janet alimshika mgongo Cindy na kumwambia kwa kujishaua. “Achana naye. Ngoja tuangalie duka la gharama zaidi. Kiukweli, nadhani nguo za hapa bado ni nafuu sana. Labda sweety wangu hatazipenda.”
“Kweli.” Cindy alielewa maana yake mara moja. Aliridhika hasa alipowazia sura ya Lisa yenye aibu baadaye wakati kadi itapokataliwa.

Lisa akawakazia macho na kuwafanyia kiburi kana kwamba yeye ndiye tajiri mkubwa duniani. Kadi ilikubaliwa bila shida yoyote. Muuzaji alimkabidhi begi la shopping. "Hizi hapa ni nguo na risiti, Bibiye." Lisa alihisi kuguswa ghafla wakati huu. Hakutarajia Alvin angempa kadi ya benki yenye zaidi ya shilingi milioni moja.

“Inatosha. Twende!” Janet ambaye alisubiri pembeni kumuona Lisa akidhalilishwa, aliunganisha mikono yake na Cindy na kuondoka huku akiwa amefadhaika moyoni.

Pamela alimpiga Lisa kwa kiwiko. "Sio mbaya. Alvin ni mkarimu sana, ila basi tu."

Lisa hakuweza kuachia tabasamu licha ya kujilazimisha. Alihisi mzigo mzito ukimlemea kifuani. Miguu yake iligeuka kuwa mrenda alipokuwa akitoka nje ya duka na nguo za thamani ya shilingi milioni tano.

“Hapana, lazima atafikiri ninamfanyia ubadhirifu makusudi. Hivi unamjua Alvin wewe, hapa amefanya kunitega tena apate sababu ya kunisema baadaye.” Lisa alihofia

“Acha kujiogopesha. Alvin ana thamani ya mamia ya mamilioni ya pesa. Kiasi hiki kwake ni cha kununulia karanga tu.” Pamela alimtuliza.

“Huelewi. Yeye ni mchumi. Akiwa na utajiri wote huo mfukoni mwake, anaishi katika nyumba ya vyumba vitatu tu, anaendesha gari la milioni 30, na anatumia tishu za bure tu zinazotolewa na kituo cha mafuta. Simu anatumia ya kichina, Saa kwenye mkono wake pia ni chapa ndogo isiyo na umaarufu. Hata sabuni anazoogea na losheni anazopaka ni bei ya kawaida tu. Nyumbani kwake hataki kuajiri hata mtumishi mmoja. Unafikiri ataacha kunisema kwa kumnunulia nguo za milioni tano, tena kwa pesa yake?”

"Vema, yeye ... Yeye ni mzuri sana na pesa zake, basi." Pamela hakujua matajiri wengine ambao waliishi kichumi kama yeye. "Naweza kukukopesha hiyo pesa, kama atakuzingua utamrudishia."

“Sawa. Nitaona jinsi atakavyojibu kwanza. kama atanisema vibaya nitamrudishia milioni tano yake. Wewe nitakulipa pole pole.” Lisa aliafiki.

Lisa alipoteza hamu ya kuendelea kununua baada ya hapo. Hakutaka kukutana tena na wasichana wale wawili wasio na maana.

Lisa alikula chakula cha usiku na Pamela hadi saa nne usiku. Kisha, alielekea nyumbani huku akiwa na hofu. Kwa kuogopa kwamba angemsumbua Alvin aliyekuwa ndani ya nyumba, hakuthubutu kuwasha taa.

SURA YA37

"Umerudi mapema sana!" Alvin alitokea ghafla kwenye mlango wa chumba cha kulala, na kulikuwa na makali ya uhakika katika sauti yake.

Lisa alipata mshtuko na kujiona mwenye hatia sana. Alijiuliza ikiwa alitumia muda mrefu kumngojea arudi nyumbani ili kuuliza ni pesa ngapi alizotumia.

"Linapokuja suala la shopping, wanawake huwa wanasahau wakati." Alvin akawasha taa pale sebuleni, kisha akamtazama Lisa kwa sekunde mbili. Akamsogelea na kunyoosha mkono wake.

"Unataka nini?" Lisa hakusogea hata kidogo. Hata hivyo, baada ya kidole chake cha shahada kugusa midomo yake, hali alianza kupata hisia ngeni kwenye mwili wake. Lisa alitazama ncha ya kidole kile cha Alvin kwa butwaa. Ukucha wake ulionekana nadhifu na mzuri, lakini alikuwa akijaribu kufanya nini? Akiwa amechanganyikiwa, alimng'ata kidole kwa upole kwa kutumia meno yake.

Mwili wa Alvin uliganda. Alihisi kana kwamba mguso wa shoti ya umeme ulikuwa ukisafiri katika mwili wake mara moja. Alimkazia macho kwa macho meusi ambayo yalionyesha kutokuamini. "Unafanya nini?"

'Hivi si ndivyo unavyotaka? Lisa aliachia kidole chake na kusema kwa sauti ya chini, "Uligusa midomo yangu na kuingiza kidole chako baada ya hapo, sasa mimi ningefanyaje ..?"

"Lisa, una akili chafu sana." Alimpotezea kabisa. "Nilitaka tu kukuonyesha mabaki ya chakula kwa kidole changu kwa sababu haukufuta mdomo wako vizuri baada ya chakula."

Lisa aliaibika sana hivi kwamba akainamisha chini uso wake. Alitamani hata kuchimba shimo na kujifukia humo. Hata hivyo, kilichofanyika kilifanyika. Hakuwa na la kufanya ila kusema kwa kusita, “Huwezi kunilaumu kwa hili. Una kidole kizuri sana. Nilishindwa kuzuia hisia zangu nilipokiona.”

Alvin alitoa kidole chake kilichokuwa kinawaka kwa msisimko. Alicheka alipotamka maneno hayo yasiyo na aibu huku uso uso ukiwa mkavu kama kauzu. “Umeshika nini?”

Lisa alitetemeka, kisha akanong'ona, "Suti yako. Samahani, nilikununulia suti zenye thamani ya shilingi milioni tano kwa bahati mbaya.”

Alvin alikunja uso kwani hakuwahi kuvaa suti ya bei nafuu namna hiyo. Suti zake ziligharimu bei kama ya gari.

Moyo wa Lisa ulimshtuka alipomuoa Alvin yupo kimya. "Ni nzuri na za kipekee pia -"

"Kwanini zote mbili zinafanana?" Alvin alimkatisha maneno yake.

“Huu?” Lisa alipigwa na butwaa. “Kwa sababu… Ni toleo maalumu. Kuna suti mbili tu za aina hii katika nchi nzima. Sikutaka kuona mtu mwingine akivaa suti sawa na wewe maana itakuwa ni fedheha. Machoni mwangu, wewe ni mtu wa kipekee sana, mzuri, na mtanashati. Nadhani rangi hii inafaa zaidi kwako. Huwa nakuona umevaa suti kama hizi na hata sijachoka nazo. Tafadhali nisamehe kwa kuwa mbinafsi kidogo.”

Alipomaliza kuongea, alitazama sura yake kwa siri. Aligundua kuwa Alvin alikuwa akimtazama na kukunja midomo yake.

"Kazi nzuri. Nimependa ustadi wako wa kuchagua rangi” Alvin akanyoosha mkono wake na kuyabana mashavu ya Lisa. "Utakapostaafu kuwa mbunifu wa majengo katika siku zijazo, unaweza kuwa katibu wangu. Utakuwa ukinipangia nguo za kuvaa kila siku.”

“Umezipenda?” Lisa aliuliza huku akiyakodoa macho yake.

“Kwa nini nisizipende?”

“Nilikuwa na wasiwasi kwamba utalalamika ni za gharama kubwa kwa sababu… niligundua kuwa nguo unazovaa kwa kawaida hazionekani kuwa za gharama…” Lisa alilazimisha tabasamu kwa aibu kwa kuogopa kuwa maneno yake yangeumiza jeuri ya Alvin. “Hehee. Kwa kweli, hakuna ubaya wowote. Ninaelewa kuwa wewe ni mtulivu na mtu usiyependa kujionyesha, na hilo ndilo linalonivutia sana kwako.”

Alvin alipigwa na butwaa. Hapo ndipo akagundua kuwa nguo alizokuwa akivaa kawaida zilionekana za bei rahisi kwa Lisa. Alimshangaa sana Lisa kwa jinsi alivyomchukulia juu juu. hakujua kuwa nguo zote alizokuwa anavaa Alvin Kimaro zilikuwa ni 'customized brand', ama nguo zilizotengenezwa mahususi kwa wateja maalunu. Nguo zake zote zilikuwa za kipekee za hazikufanana na wengine. Si zile za kuchagua chagua tu kwenye maduka.

“Ni sawa. Utaelewa baadaye.” Alvin akagusa kichwa chake kwa huruma, kisha akaingia chumbani.

Siku iliyofuata, Alvin alivaa suti ya kahawia aliyonunuliwa na Lisa. Alipotoka nje ya chumba kile, Lisa alimtazama na kupigwa na butwaa kwa muda. Ingawa alimuona akiwa amevalia kila aina ya suti, hisia za ajabu zilimjaa kichwani kwa sababu tu hiyo ndiyo suti aliyomnunulia. Alihisi mchanganyiko wa furaha na kuchanganyikiwa. Ilionekana kana kwamba alikuwa mume wake halisi wakati huo. Alvin akampiga jicho. Alipogundua kuwa alikuwa akimtazama kwa butwaa, kwa namna fulani alikuwa katika hali ya uchangamfu.

Alipokuwa akitoka nje ya nyumba hiyo, kuna jambo lilimjia kichwani. “Sikuona umenunua nguo yoyote jana usiku, kwanini” Alimuuliza

"Hapana, nilikuwa na kazi ya kukununulia wewe nguo." Alipokumbuka furaha ya kumnunulia mpenzi wake nguo tabasamu lilisambaa usoni mwake.

"Nadhani ulikuwa na shida ya kwenda kula chakula cha jioni na si kununua nguo, ungesema ukweli tu." Alvin alimdhihaki, akimuonyesha waziwazi.

"Ah, kwa nini unanifikiria hivi?" Ili kuficha aibu yake, Lisa alisema kwa sauti nzito ya kutaniana, ”nilikosa tu nguo zinazonifaa, nitaenda siku nyingine.”

Alvin alihisi koo lake linamuuma. Alifungua vifungo viwili kwenye shingo ya shati lake na kusema, “Kama una muda, nenda ukanunue nguo leo kwa kutumia kadi yangu. Nguo hizo zitakuwa malipo kwa kunipikia na kumhudumia Charlie kama mhudumu wangu.” Alielekea ofisini kwake mara baada ya kumaliza kuongea.

Hans alipoingia tu kwenye kampuni ya mawakili, alipigwa na butwaa kuona suti ya Alvin. Kwa haraka akasema, “Bw. Kimaro, sijawahi kukuona ukivaa suti za aina hii…”

“Lisa aliinunua madukani jana.” Alvin aliongea huku akifungua faili la kesi.

Sam, ambaye alikuwa amefika tu mlangoni, alisikia maneno hayo. "Wow, unavaa suti zinazouzwa madukani siku?” Sam aliuliza huku akitazama suti ya Alvin kwa shauku na kuichunguza. "Ni toleo maalum la Sheria Ngowi…. Nimezoea kukuona ukivaa nguo zilizotengenezwa mahususi kwa ajili yako pekee, tena na wabunifu wa nje ya nchi, au ni kwa sababu Lisa alikununulia hii…?”

Kwa hali ya huzuni, Alvin alimtupia jicho la kijeuri. “Mwanamume mzima unakuja kuchunguza nimevaa nini leo, huna kazi za kufanya, eeh?”

“Sikuja kwa ajili hiyo.” Sam alisema.

Alvin alimtupia faili usoni mwake, na maneno “toka ofisini kwangu” yakachomoka mdomoni mwake.

"Sawa sawa. Usiwe na wazimu. Niko hapa kukuambia kitu.” Sam akamwambia. “Babu yangu atasherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 80 kesho usiku. Amesikia kwamba upo Dar hivyo ameniomba nikwambie kuhudhuria sherehe hiyo.” Sam alichukua kadi ya mwaliko na kuiweka juu ya meza.

Alvin aliitazama kadi hiyo na kukumbuka kitu. Lisa pia alimwalika kwenye sherehe ya kuzaliwa ya miaka 80 ya bibi yake.

"Pia ni bora ukaja na mpenzi wako," Sam alikumbusha. “Kama unavyojua, dada yangu amekuwa akipendezwa nawe kwa miaka mingi. Pia, babu yangu amekuwa akitaka sana kukuoza dada yangu. Hataacha kukusumbua kwa hilo”

Alvin alijipapasa paji la uso huku akiwaza ni nani aende naye kama mpenzi wake.
Lisa?

SURA YA38

Siku mbili zile Lisa alikuwa busy sana na kazi huku pia akilifikiria ushauri aliopewa na Pamela wa kuweka mambo sawa na Alvin. Siku hiyo jioni akiwa anawaza hayo, Alvin alimpigia simu. “Uko wapi?”

"Ofisini."

“Nitumie anwani yako. Nitakuchukua hapo chini ndani ya dakika 20. Nataka unisindikize kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa.”

Hapa ndipo Lisa alipoona fursa. Macho ya Lisa yaling'aa, lakini baadaye alijawa na kinyongo. “Tufanye dili, kama utakubali kunipa kampani kwenye sherehe ya kuzaliwa ya bibi yangu, na mimi nitakubali kukupa kampani leo.”

“Kama hutaki niitatafuta mtu mwingine.” Alvin hakumbembeleza.

Alvin alipotaka kukata simu, Lisa alitupilia mbali kiburi chake na kukubali haraka. “Njoo unichukue. Katika uwanja wa mapenzi, yule anayependa sana ndiye anayepoteza. Nimejikuta nikipoteza kabisa moyo wangu kwako. Alvin una nini?” Lisa alichombeza kijanja. Alichukua chupa ya thermos na kuendelea kunywa kahawa yake. Hata yeye alivutiwa na ustadi wake wa kumtania Alvin kimapenzi.

Sekunde chache baadaye, sauti ya Alvin ilisikika upande wa pili. "Simu yangu imeunganishwa kwenye gari kupitia Bluetooth, na Sam ameketi kando yangu anakusikia ukiongea upuuzi wako.”

Lisa alitema kahawa mdomoni mwake ikamwagikia kwenye skrini ya kompyuta bila kujijua. Sauti ya Sam baadaye ilisikika, “Si vibaya shemeji. Sikuwahi kufikiri kama na wewe unajua maneno matamu ya mapenzi kiasi hiki. Haishangazi Alvin--"

"Nakuja kukuchukua." Alvin alimwambia Lisa na simu ilikatwa moja kwa moja kabla Sam hajamalizia usemi wake.

Lisa alilala juu ya meza, akiona aibu hadi kufa. Alinyanyuka baadaye kidogo na kupakia vitu vyake na kushuka chini. Wakati huo alipokea simu kutoka kwa Pamela.

“Mambo yalikuwaje? Ulifanikiwa kufanya chochote na mume wako jana usiku?”

“Hapana,” Lisa alimjibu haraka, “lakini aliniomba nimsindikize kwenye hafla ya siku ya kuzaliwa usiku wa leo. Nadhani hii ndiyo nafasi. Lakini nina wasiwasi kama atakunywa pombe. Anapotoka kwa shughuli za kijamii usiku, sijawahi kumuona akinywa pombe!” Lisa alihema huku akijua kuwa Alvin alikuwa ni mtu mwenye kujitambua.

"Hafla ya kuzaliwa?" Pamela alipigwa na butwaa kwa muda. “Ni siku ya kuzaliwa ya babu ya Sam ya miaka 80? Mimi pia nitakuwepo.”

“Nafikiri hivyo. Alvin hana rafiki mwingine zaidi ya Sam.” Lisa alisema.

“Hiyo itakuwa poa sana, tutakutana. Nitawapanga watu kunywa na Alvin na kujaribu kumlewesha. Hilo lisipofanikiwa, nitaleta dawa…” Pamela alimhakikishia. “Hakika Alvin atakutaka mwenyewe bila kupenda.”

Lisa akashusha pumzi ndefu. Hakuwa na uhakika kama alikuwa amejipanga kiakili kwa hilo licha ya Pamela kuwa ameanza kumsaidia kuandaa kila kitu kwa haraka. Alisubiri kwa hamu kando ya barabara. Lakini Alvin alipofika Lisa alionekana kuzama kwenye mawazo mazito kiasi kwamba hakusikia mlio wa honi.

Beep! Beep!

Alvin alimkazia macho Lisa aliyekuwa kazama kwenye mawazo fulani yaliyomfanya atabasamu kwa aibu. Alikuwa amejifunika uso huku kasimama kando ya barabara. Alishindwa kabisa kumwelewa. Hakuwa na uhakika ni nini kilikuwa akilini mwake pia. Je, alikuwa kiziwi?

Sam alikodoa macho na kutabasamu. "Alvin, kwa njia fulani ninahisi kuwa mke wako anafikiria juu ya kitu kichafu, na labda uko kwenye mawazo yake ..."

"Yeye si wewe, sawa?" Alvin alimtazama kwa ukali, ingawa alikuwa na mashaka pia juu ya hilo.

“Kusema kweli, kadiri ninavyomwangalia Shemeji, ndivyo namuona kuwa mzuri. Kwa kweli, nashangaa uliwezaje kumpata kabla yangu hali wewe ni mgeni na mimi ninaishi naye kitongoji kimoja.. "

Kabla Sam hajamalizia sentensi yake, sauti kali ikamkatisha. Alvin alimwonya bila huruma, “usijaribu kuwa na mawazo machafu juu yake. Yeye si mtu ambaye unaweza kumpata kirahisirahisi tu.” Baada ya hapo, alifungua mlango na kutoka nje ya gari. Alitembea moja kwa moja kuelekea kwa Lisa.

Lisa alipomwona Alvin ghafla alishtuka kutoka kwenye mawazo kiasi kwamba alipiga hatua mbili nyuma na kutaka kudondoka kutokana na viatu vyake virefu. Alvin alipomuona Lisa anakaribia kuanguka, alinyoosha mkono wake kumshika kiuno na kumweka kwenye mikono yake ili aweze kujiweka sawa.

Ikiwa hii ingetokea siku nyingine yoyote, Lisa angekuwa na wasiwasi kidogo. Hata hivyo, alikuwa akimuwaza Alvin ambaye hana nguo muda mfupi uliopita. Sasa kwa vile ncha ya pua yake ilikuwa karibu na kifua chake, mwili wake ulibadilika ghafla na kutetemeka kama amepigwa shoti ya umeme.

“Ninatisha kiasi hicho, hata unataka kuanguka baada ya kuniona?” Alvin alinua kichwa chake na kumuuliza.

"Hapana, umenishtua tu." Haraka alirudi nyuma na kujiweka sawa.

"Ingia kwenye gari." Alvin alifungua mlango na kukaa kwenye kiti cha dereva.

Lisa aligundua kuwa kuna mtu alikuwa kwenye siti ya mbele, kwa hivyo bila kupenda akaenda kwenye siti ya nyuma. Kwa aibu, hakuweza kukabiliana na Sam.

“Habari, Shemeji. Ulikuwa unafikiria nini sasa hivi, mbona hukusikia honi?” Sam alionyesha tabasamu baya. "Kutokana na mwonekano wako, naweza kukisia kuwa ulikuwa ukimfikiria Alvin."

"Ndio, nilikuwa nikimfikiria," Lisa alisema bila kujali kwa sauti ya upole. Kisha, akatazama chini haraka.

Baada ya kuachia 'wow', Sam alijifunika kifua chake na kusema kwa huzuni, “Sikupaswa kuuliza swali hilo. Kuona haw lovey- dovey nyote wawili mlivyo, ninahisi kushikwa na wivu. Hata hivyo, Alvin hana utu wa kupendeza, na ana hasira mbaya. Pia ana tabia nyingi chafu. Unapenda nini hasa kutoka kwake?” Sam aliuliza kwa utani.

Moyoni mwake, Lisa alimpa Sam mia kwa mia kwani alikuwa sahihi kabisa. Hata hivyo, alimsifia tu Alvin ili kumlinda kihisia, “Kwa kuwa sasa ninampenda, naona udhaifu wake wote kuwa ni sifa zake nzuri. Kinyume chake, wanaume wapole na waelewa hunifanya nihisi kutokuwa salama. Napenda sifa zake tu. Akinizingua na mimi namzingua basi, yanaisha!” Maneno ya Lisa yalimvimbisha kichwa haswaa Alvin, Akamgeuzia macho Sam na kumwangalia kwa kejeli.

Sam alihisi kana kwamba alikuwa amedhihakiwa na Lisa. "Sikupaswa kusema chochote kumbe?" Alvin alimpuuza tu.

Lisa akasema, “Hapana, hapana. Wewe ni mcheshi, Sam Harrison. Uwepo wako unanifanya nihisi nimetulia zaidi.”

“Unamaanisha kwamba huna utulivu unapokuwa pamoja nami?” Alvin aligeuka ghafla.

Lisa alisafisha haraka hali ya hewa. “Hivi mtu aliyependa huwa ana utulivu kweli? Unapokuwa na mtu unayempenda, unahisi kana kwamba moyo wako unadunda kwa nguvu kila wakati na unashindwa kabisa kuutuliza." Alvin aligonga usukani kwa kidole bila kusema chochote. Pamoja na taaluma yake ya uanasheria, alikuwa amekutana na mjuzi wa kubumba na kuchezea maneno kama yeye.

Akiwa ameketi kando ya Alvin, Sam alishikwa na wivu. Hakuwahi kukutana na msichana yeyote ambaye aliendelea kukiri mapenzi yake kupitia hotuba yake.

Lisa akabaki kimya akicheza na simu yake katika siti ya nyuma. Ghafla, Pamela alimtumia video mbili. Pamela alikuwa na kawaida ya kumtumia video za vichekesho. Lisa alifikiria vivyo hivyo wakati huo, kwa hivyo alibofya video hizo mara moja. Kabla hajajua niki kitajiri, sauti kali ilijaza sehemu sehemu yote ya ndani ya gari. Tukio la ajabu likaonekana kwenye kioo cha simu yake baadaye. Lisa aliingiwa na kiwewe cha ajabu na kuizima simu mara moja.

Hata hivyo, gari lilikuwa tayari limesimama. Wanaume hao wawili walimtazama kwa namna ya ajabu. Mara moja, alitamani kukimbia kwa kuruka nje ya dirisha.

“Aha… Acha nieleze. Nilikuwa nikisoma kitabu na mara kirusi kikaingia...” Lisa alibabaika.

Sam aligusa pua yake kwa sura ya aibu. “Sawa shemeji. Ni kawaida tu, hata mimi hutazama hizo vdeo kwa siri nyumbani. Sikujua kwamba na wewe huwa utazama mpaka kwenye gari.”

Lisa alikosa la kusema.

Uso wa Alvin ulijawa na hali ya huzuni. "Ninakuonya, usitazame tena mambo machafu kama hayo hata kama ni kwa siri"

SURA YA39

Alvin alipandwa na hasira kila alipofikiria kuwa Lisa alikuwa akimwangalia mwanamume mwingine akiwa uchi kwenye video. Hakuwa na haya kama nini!

Sam alimtetea Lisa, "ili kuiweka kwa njia nyingine, inaweza kuchukuliwa kama nyenzo ya kujifunza wakati mwingine. Labda shemeji anajifunza kwa ajili yako."

Lisa aliitikia kwa kichwa chinichini, akikubaliana na kauli ya Sam. Lakini Alvin alizungumza kwa sauti ya huzuni, “hakuna haja ya hilo. Hatahitajika kufanya hivyo na mimi. Hata kama hilo likitokea, mimii ndiye nitapanga tufanyeje, si yeye.”

Kauli ya Alvin ilikuwa tofauti kabisa na vile alivyoamini Lisa. Sasa alifahamu kwamba Alvin hakuvutiwa naye hata kidogo, aliinamisha kichwa chini kwa kukata tamaa. Sam akamtazama kwa huruma. Kisha akahema kwa masikitiko baada ya kuona jinsi Alvin alivyokuwa mkatili wa hisia zake na hana mapenzi naye.

Baada ya nusu saa, gari lilisimama. Lisa aliinua kichwa chake na kugundua kuwa walikuwa wamefika ‘Miracle studio’, saluni ambayo ilitoa huduma ya urembo na mitindo mbalimbali. Ingawa hakuwahi kufika hapo awali, alisikia kwamba ‘Miracle Studio’ ilikuwa saluni ya kike inayojulikana zaidi kwenye huduma ya urembo na mitindo huko Masaki.

Alvin akageuka na kusema, “Nenda wakakuhudumie kwanza, mimi kuna jambo naenda kufanya. Nitakuchukua baada ya muda mfupi.”
Lisa alipigwa na butwaa. "Alvlisa, labda hujui utaratibu wa saluni hii kuwa haikubali mtu yeyote hata kama wewe ni tajiri kiasi gani hadi uwe umeweka appointment mwezi mmoja kabla.”

“Alvinani?” Sam akaangua kicheko. Muda mfupi baada ya kuanza kucheka, macho makali yakaelekezwa kwake. Uso wa Sam uliganda kidogo, kisha akasema haraka, “Hatuhitaji kuweka nafasi. Nenda tu juu. Nimemjulisha mhusika mkuu kuhusu hilo.”

“Oh.” Lisa alipumua kwa siri kwa kuridhika. Kwa hakika, familia ya Harrison ilikuwa familia yenye nguvu sana, hawakuweza kupingwa kwa lolote. Mara tu alipopanda ghorofani, meneja wa saluni alimkaribisha na kumfanyia huduma binafsi ya urembo na mavazi yeye binafsi.

Saa moja baadaye, Alvin alikuwa amerudi, lakini Lisa hakuwa amemaliza kuhudumiwa. Alvin alikaa kwenye kochi na kumsubiri kwa muda. Upesi mlango wa chumba cha watu mashuhuri ulifunguliwa na Lisa akatoka nje akiwa tofauti na alivyoingia. Alivalia vazi refu lililopambwa kwa almasi mwili mzima. Sio tu kwamba vazi hilo lilikuwa la kung'aa, lakini pia lilifafanua sura ya umbo lake la kuvutia na kupendeza kikamilifu. Nywele zake, ambazo zilionekana kuwa nyeusi kama mwani, zilijipinda kwa mawimbi na kuanguka juu ya mabega yake. Alionekana mrembo na mwenye kuvutia kuliko siku zote.

Macho ya Alvin yalimtoka kwa hisia inayowaka. Kwa muda mrefu alikuwa amejua uzuri wake. Tofauti na wanawake wengine wengi siku hizi, hakuwa amepitia upasuaji wa plastiki ama kuongeza makabrasha mengine mwilini ili kuwa na uzuri kama huo. Hakutarajia kuwa angeonekana kuvutia sana hata akiwa amejipodoa kidogo tu.

"Alvlisa, ninaonekana mzuri?" Mara tu Lisa alipoona macho yake, midomo yake iliangaza tabasamu la furaha. Alitembea kuelekea kwake, akitumaini kwamba angeelekeza macho yake kwake.
Alvin alikaa kimya huku akikazia macho yake kifuani mwake. Lisa aliona haya baada ya kuona hivyo. Alihisi macho ya Alvin kama yanamchoma kifua. "Hey, unatazama nini?"

Alvin aliongea kwa mkazo, kinyume na matarajio ya Lisa. "Nenda ukabadilishe."

“Kwanini, kwani kuna shida gani?” Lisa alichanganyikiwa.

"Nguo hii inakufichua sana, siipendi.” Aligeuka na kushuka chini mara baada ya hapo.

Kwa hasira, Lisa alihisi bomu la atomiki likilipuka kichwani mwake. Kutokana na mtazamo wake mapema, ilikuwa imempa hisia kwamba alikuwa amevutiwa naye, lakini alivyobadilika kwa kauli yake akashindwa kumwelewa kabisa.

Msimamizi wa duka kando yake alisema kwa tabasamu, "Bi Jones, Bw. Kimaro anakujali sana." Lisa alitoa macho na kumtazama meneja wa duka. Macho yake yalionyesha hali ya kutokuamini. “Kwa kawaida, mwanamume anapomjali sana mwanamke, anakuwa na wivu naye. Asingetaka mwanamke wake avae mavazi ya kuvutia wanaume wengine, na ni yeye pekee anayeruhusiwa kukuona hivyo.”

Kwa tabasamu meneja wa saluni aliongeza, “Baada ya kufanya kazi hapa kwa miaka mingi, nimekutana na wanaume wengi lakini wachache wa aina ya Kimaro. Mimi ni mjuzi mzuri wa tabia za wanaume.”

Aliposikia maneno yake, Lisa alijawa na moto wa matumaini. Je, Alvin hakutaka watu wengine wamwone akiwa amevaa nguo za kufichua umbo lake? Hiyo liliwezekana.

Lisa alibadilisha na kuvaa nguo ndefu nyeupe ambayo haimkumbana sana. Ilimpendeza lakini haikuyafichua maumbile yake. Baada ya hapo akashuka chini na bila kutarajia, alimuona Alvin akivuta sigara. Alvin alivuta sigara mara chache sana. Siku hiyo labda ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona akifanya hivyo hadharani. Hata hivyo, alionekana kuvutia tu alipovuta sigara. Kwa kuwa alikuwa akimpenda Alvin, chochote atakachofanya hakika kingeonekana kuwa kizuri tu kwake.

"Alvlisa, nguo hii ni sawa?" Lisa alimwendea na kumvuta mkono.
Alvin alimtupia jicho la kuridhika. Wakati huu, alikuwa amevaa kizamani, kistara na kujisikia kifahari. Lakini bado Alvin alikuwa na uhakika kuwa Lisa angevutia macho ya watu usiku huo. Ghafla, alijuta kuchagua kumtoa nje. Alipaswa kumficha.

“Twende zetu.” Alvin aliiweka sigara kwenye sinia ya majivu na kuongoza kutoka nje.

Akiwa ameshika gauni lake, Lisa alitembea taratibu kiasi. Wakati Alvin alipogeuza kichwa chake, uso wake ulikuwa umekunjamana. Akamsogelea na kumuinua kiunoni moja kwa moja. Kwa ushirikiano, Lisa aliweka mikono yake shingoni mwake, kisha akatazama kidevu chake kizuri. Alichukuliwa na mshangao wa sura yake ya kuvutia.

Lisa akamuuliza kwa upole, “Hukuniruhusu nivae lile gauni kwa sababu ulihisi linaufichua sana mwili wangu? Je, ni kwa sababu unanipenda au?” Pamoja na hayo, kulikuwa na hali ya ukimya.

Baada ya kushuka chini, Alvin alimweka Lisa moja kwa moja kwenye siti ya nyuma ya gari lake. Kwa sauti ya kejeli, alisema, "Kitaalam, wewe ni mke wangu, hata hivyo. Sitaki uvae kwa njia isiyofaa na kujidhalilisha.” Uso wa Lisa ulimtoka. Hakujisikia kuzungumza naye katika safari yao yote.

Gari liliingia ndani ya nyumba ya familia ya Harrison iliyojaa wageni. Msururu wa magari ya kifahari ulionekana kwenye eneo la maegesho nje ya jumba hilo la kifahari. Lisa alikasirika kidogo kwani hakuyaona magari ya akina Masawe na Mushi. Ethan angetokea pale, bila shaka angeshangaa kumuona akiwa amemshika mkono mjomba wake.

Waliingia ndani huku mikono ya Lisa ikiwa imeizunguka mikono ya Alvin. Alvin aligeuza kichwa chake na kumpa ukumbusho, “Usiku wa leo, unaweza kujidai hadharani kwamba wewe ni mpenzi wangu.”

Macho ya Lisa yalimtoka. Dakika iliyofuata, hata hivyo, Alvin akabadilika tena. “Usiwe na furaha kupita kiasi. Hii ni kwa sababu sitaki tu Mzee Harrison anitambulishe kwa msichana mwingine.”

Katika usemi huo, Lisa alijihisi kutumiwa kama ngao tu, na uwepo wake ukakosa maana ghafla! Lisa alikosa la kusema. “Sawa. Niko tayari kukulinda kutokana na kila aina ya majanga na kukusaidia bila kujali!”

Kabla hajamaliza maneno yake, msichana mmoja aliyevalia gauni la rangi ya shampeni alitembea kuelekea kwa Alvin kwa umaridadi. "Alvin, ni muda mrefu umepita tangu tulipokutana mara ya mwisho."

Lisa alishindwa kuendelea na kitendo chake. Msichana huyo alikuwa binti mdogo wa familia ya Harrison, Angela Harrison, ambaye pia alikuwa dada mdogo wa Sam. Lisa alikuwa amemwona mara moja kwa mbali alipohudhuria hafla furani ya chakula cha jioni kipindi cha nyuma. Kutokana na usemi wake uliojaa sauti nyororo, Lisa alifikiri kwamba Angela angeweza kuwa mshindani wake.

“Alvin, vipi mbona mkeo hujaja naye leo? Ni muda mrefu umepita tangu nilipomwona mara ya mwisho. Nimem’miss sana.”

"Hajambo," Alvin alijibu kwa unyonge.

Angela kisha akapiga kelele. “Alvin, mbona umekuwa Dar kwa muda mrefu, lakini hukuja kuniona. Bado unakumbuka kuwa uliahidi kutazama jinsi ninavyoimba na kucheza violin? Hujatimiza ahadi.” Kwa hayo alimkazia macho Alvin kwa husuda.

Lisa alishikwa na wivu. Alikuwa amesimama pale pale, lakini Angela alionekana kumchukulia kama hamuoni vile. Lisa akajikoholesha na kusema. “Alvlisa, unaweza kumtambulisha kwangu? Yeye ni…?” Lisa alimshika mkono Alvin huku akionyesha sura ya kimahaba.

SURA YA 40

Alvin alitabasamu alipoona jinsi Lisa alivyopata wivu haraka. “Dada yake Sam.”

“Yeye ni nani? Kwa nini yupo karibu yako” Sura ya uchungu ikapita usoni mwa Angela.

Akikunja midomo yake myekundu, Lisa alisema, “Halo, Bi. Harrison. Mimi ni mpenzi wake. Huenda hujaniona hapo awali, lakini ulipaswa kusikia kuhusu jina langu. Mimi ni Lisa Jones, msichana mrembo zaidi niliyetokea kuuteka moyo wa Alvin.” Mdomo wa Alvin ulimsisimka kwa maneno yake ya aibu.

Angela alitoa macho huku akiwa haamini jinsi msichana huyo alivyokosa aibu. Kisha akadhihaki, “Hehe. Samahani, sijasikia kuhusu wewe kuwa msichana mrembo zaidi. Hata hivyo, nimesikia kuhusu tabia ya kipumbavu ya Lisa kutoka kwa familia ya Jones Masawe hivi majuzi. Ulipoteza urithi wako kwa dada yako, ambaye alitoka mashambani, akapewa haki ya urithi wa familia ya Masawe, na baadaye ukafukuzwa kutoka kwa familia hiyo. Siamini kuwa Alvin angetaka kuwa na mtu kama wewe usiye na future yoyote...”

Lisa alihisi kana kwamba kuna kitu kimepenya moyoni mwake. Alikosa la kusema.

“Angie.” Macho ya Alvin yalimwelekea Angela. “Jiangalie. Lisa ni mpenzi wangu kweli.”

“Inawezekanaje?” Angela aligeuka rangi. "Hata halingani na hadhi yako nzuri."

Lisa hakuridhika, akajibu mapigo ya Angela, “kwanini nisiendane naye? Mimi ni beatuful na yeye ni handsome. Tunaposimama pamoja, tunaendana vizuri kwa sura. Mtoto wetu wa baadaye bila shaka ataonekana kuvutia.”

Mdomo wa Angela ukasisimka kwa hasira. Alisema kwa kejeli, “Unajidanganya. Utapunguza IQ ya kizazi cha Alvin."

Kuwatazama wanawake hao wawili wakirumbana kulimfanya Alvin apate maumivu ya kichwa. Kisha akapiga paji la uso wake na kusema. “Sawa, Angie. Nitapeleka salamu zangu kwa babu yako sasa. Tutaonana baadaye.” Alipomaliza kuongea, alipiga hatua kuelekea kwenye jengo kuu akiwa na Lisa bila kumsubiri Angela ajibu.

Lisa akafunga mdomo wake, hakusema neno lolote katika safari hiyo. Kwa vile alikuwa akila vizuri na kulala vizuri kwa siku za karibuni, mashavu yake yalikuwa yamenenepa tena. Alionekana mrembo sana.

Alvin alinyoosha mikono yake ili kuyabana mashavu ya Lisa huku akimwambia. “Angie bado ni mtoto, na amekuwa akidekezwa tangu akiwa mdogo. Usijishushe kwa madhaifu yake.”

Lisa akacheka. "Usijali, sitajishusha kufikia kiwango cha Angie. Kwa kuwa upo naye karibu sana, kwanini hukufikiria kumfanya ajifanye mpenzi wako? Baada ya yote, unalibebisha hadi jina lake, unamwita Angie. Mimi ni mtu wa kukaa tu kama picha, mtu ambaye hata jina langu linakukera.”

Alvin akajibu, “…Kwa hiyo ni kwa sababu nilimuita Angie na sikuiti Lisa?”

"Bila shaka hapana. Je, mimi ni mtoto mdogo kuweza kuona hisia za mtu?" Lisa alidlazimisha tabasamu.

Alvin alijihisi mnyonge ghafla. "Angela alikuwa akicheza na Sam na mimi nyuma ya nyumba tulipokuwa wadogo. Ninamchukulia kama dada mdogo."

Hapo hapo wakafika kwenye jengo kuu. Akiwa amevalia suti yake safi, Mzee Harrison alimpungia mkono Alvin kwa nguvu. “Alvin, yaani leo ndo unakuja kuniona ingawa umekuwa Dar es Salaam kwa muda mrefu sasa. Kwanini kunisusa hivi? Unanidharau kwa sababu mimi ni mzee?” Aliongea huku akikenua tabasamu la kizee, Mzee Harrison.

“Hapana kabisa. Unaonekana mdogo kuliko hapo awali, Mzee Harrison.” Alvin alimkabidhi mzee yule zawadi yake ya siku ya kuzaliwa.

Mzee Harrison alielekeza macho yake kwa Lisa na Alvin akamtambulisha. “Huyu ni mpenzi wangu.”

“Ah, hatimaye umepata mwenzi. Hiyo inasikitisha. Hapo awali nilipanga kukupatia mtu. Kuna wanawake wengi wa ajabu hapa." Mzee Harrison alimkabidhi zawadi Lisa . “Hii hapa ni zawadi kwa ajili yako tunapokutana kwa mara ya kwanza, mke wa mjukuu wangu. Alvin ameteseka sana katika maisha yake. Tafadhali mtunze.”

Lisa alifurahishwa. Hakuwa na uhakika kama aikubali au laa. Isingeonekana vizuri kama angeikataa.

"Ikubali tu kwani ni ishara ya upendo ya Mzee Harrison kwako." Alvin alitikisa kichwa.

Lisa alipopokea zawadi hiyo, Alvin akampigapiga mgongoni. "Nisubiri kwenye ukumbi wa wageni." Pengine alikuwa amekwisha maliza kucheza kipande chake, hivyo akamwona hana umuhimu tena kuwa karibu yake. Lisa akajiondokea zake.

Aliposhuka tu aligongana tena na Angela. "Ulikuwa unanisubiri hapa kwa makusudi, Bi.Harrison?"

Bila kustaajabisha, tabasamu lilitanda usoni mwa Angela. Angela alinyanyua kidevu chake kwa maneno ya jeuri. “Afadhali ukae mbali na Alvin. Yeye si mtu unayeweza kumudu kuwa naye.”

“Itakuwaje kama sitakaa naye mbali, eeh?” Lisa aliuliza kwa shauku ya kutaka kujua. “Unampenda sawa, lakini yeye anakuchukulia tu kama dada mdogo.”

Angela alibaki akihema. "Kwa hiyo? Kwa familia ya kifahari kama Kimaro, wanajali kuhusu ndoa iliyolingana vizuri katika suala la hadhi ya kijamii. Kusema ukweli hata humjui vizuri Alvin. Wanafamilia yake hawatakukubali kwa sababu hulingani naye. Kwa sasa, anaburudika tu na wewe. Familia yake itakutimulia mbali na hautakanyaga hata msingi tu wa geti.” Alidhihaki kwa kejeli na baadaye akaondoka kwa njia ya kiburi.Lisa alikasirishwa kwa namna fulani na maneno yake lakini hakufikiria kabisa. Hata hivyo cheti cha ndoa kingekuwa tegemeo lake kubwa kwa wakati wote.

Baada ya Lisa kuondoka kwenye jengo kuu, punde alikutana na Pamela. “Angalia, hii ndiyo pombe niliyotayarisha. Nitatafuta mtu wa kumlewesha Alvin baadaye. Ikiwa hajalewa, lazima uchukue mbinu yoyote kwa kumfanya ale hii kitu. Kumbuka, hii itaanza kutumika saa mbili baada ya kuila." Pamela aliweka vitu vile mikononi mwa Lisa.

Lisa alijisikia vibaya sana. "Je, hii itasababisha madhara yoyote?"

“Mbona bado una wasiwasi nami kwa jinsi ninavyokupambania? Haina shida na haitaathiri afya yake.”

"Ikiwa atashtukia, hakika ataniua." Lisa aliogopa.

“Labda awe hanithi lakini kama ni rijali hatatoboa! Ikiwa ningekuwa mwanamume nikaamka na kumwona mwanamke mrembo kama wewe akiwa amelala kando yangu asubuhi na mapema, bila shaka ningehisi raha. Alvin pia ni mtu wa kawaida.” Pamela alimtoa wasiwasi.

Lisa alivutiwa na maneno yake. Muda mfupi baadaye, Alvin alirudi.
Alvin alipofika tu mlangoni, kuna mtu wa ajabu alienda kumsumbua. "Bw. Kimaro, sifa yako inakutangulia. Kwa kweli, kwa muda mrefu nilitaka kukufahamu. Ngoja nikupe toast.”

“Kunywa tu mwenyewe. Sihitaji kinywaji.” Baada ya kukutana na watu kama yeye mara nyingi sana tangu ujana, Alvin hakutaka kuwa karibu nao.

Kisha Alvin aligongana na watu wachache kama hao ambao alibaki kuwa jeuri kwao. Pamela alipumua, akitazama tukio hilo kwa siri. “Jamani, mumeo ni mtu wa kipekee ambaye haonyeshi heshima kwa wengine hata kidogo. Bado hajanywa hata glasi moja hadi sasa, ana kiburi. Watu wasiomjua wangedhani kwamba anatoka katika familia yenye nguvu zaidi nchini.”

“Ngoja nimfuate.” Lisa alimwambia Pamela huku akijongea kwa Alvin.

Muda si muda Alvin akamtazama Lisa ambaye alimsogelea kimya kimya. Lisa alifikiri kwamba Alvin angekuwa busy kujichanganya na wengine na kuzungumza mambo ya biashara kama watu wengine walivyofanya. Hata hivyo, walikuwa wakihudhuria sherehe ya kuzaliwa iliyojaa watu wa tabaka la juu ambapo ilikuwa ni kawaida kwa watu kupanua mitandao yao. Lakini Alvin alijitenga nao na kumpeleka Lisa nyuma ya ukumbi ambapo waliketi na kunywa.

“Si unatoka kwenda kujumuika? Ninaona matajiri wachache kutoka sekta ya fedha.” Alijaribu kumshawishi atoke nje. Aliingiwa na hofu kwani asingeweza kufanya lolote ikiwa angeendelea kubaki naye.

"Sipendezwi." Alvin alipiga kinywaji chake kama hataki hivi.

Lisa akapepesa macho. “Unataka nikumiminie mvinyo kidogo? Kuna mvinyo hapa wa kiitaliano unaonekana kuwa na ladha nzuri."

"Ikiwa unataka kuinywa, endelea. Lakini utafute kabisa pa kwenda endapo utailewa na kufanya vituko.” Alvin alijibu na kumpa tahadhari.

Baada ya kukaa kimya, mara Lisa alisimama tena. “Ngoja nikuletee chakula, sawa? Hujapata chochote usiku wa leo.”

"Hakuna haja." Hakupendezwa na chakula kingine chochote zaidi ya chakula alichopika Lisa.

"Hapana. Chakula ni nishati kwa wanadamu. Lazima ule kitu hata kama hujisikii, jilazimishe kiasi.” Kwa hayo, Lisa alitoka kwenda kuchukua matunda na vyakula vingine.

Kwa siri, Lisa alitia kile kitu alichopewa na Pamela kwenye chakula. Aliporudi, aliweka chakula mbele ya Alvin. Kisha, akaweka kipande cha nyama ya mbuzi iliyochomwa karibu na mdomo wake. Kwa kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya kitendo hicho kiovu, alihisi kukosa amani. Mikono yake ilitetemeka hasa pale macho makavu ya Alvin yalipomkazia usoni. Aliapa kwamba angekata tamaa ikiwa Alvin angekataa kula.

TUKUTANE KURASA 41-45

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI......LISA
KURASA.....41-45

SURA YA 41

Muda mfupi baadaye, Alvin aliinamisha kichwa chake na kula kipande cha nyama alichokuwa ameshika Lisa.

"Endelea kunilisha." Alvin alinogewa. Lisa alikosa la kusema. Hata hivyo, aliendelea kumlisha chakula chote kwenye sahani huku akihisi woga na hatia. Alvin aliinuka mara baada ya kumaliza kula. “Twende nyumbani.”

Lisa alishtuka. "Tunaenda nyumbani saa hii?" Haikuwa imefika hata saa mbili bado. Ikiwa wangeondoka mara tu baada ya kula, bila shaka Lisa angekuwa mtu wa kwanza kushukiwa baadaye.

“Wewe usiondoke. Unaweza kukaa hapa usiku kucha.” Alvin aliweka msimamo. Alvin aliona ni kupoteza muda kujichanganya na watu wengine, hakuwa pale kwa ajili ya kujionyesha. Alijitokeza tu pale kwa ajili ya heshima yake kwa Mzee Harrison. Kwa kuzingatia kwamba alikuwa akisisitiza kuondoka, Lisa hakuwa na jinsi zaidi ya kuondoka pamoja naye.

Baada ya kuingia kwenye gari, alimkabidhi zawadi ambayo alipokea kutoka kwa Mzee Harrison.

"Ishike," Alvin alisema kwa upole.

“Lakini ni ghali. Sidhani kama ni lazima nichukue…”

“Hii ni ghali kwako tu." Alvin alitabasamu kwa dharau hafifu. Inavyoonekana, alikuwa akidhihakiwa kama maskini. Lisa alitazama chini akaingiwa na hofu akijua kwamba kuna dhoruba ingetokea muda si mrefu.

Walipofika nyumbani, alimtazama kwa siri Alvin kwa nyuma huku akiwa na woga na wasiwasi, akijisemea kimoyomoyo. 'Samahani, Alvin. Hakika nitakutendea vyema siku zijazo. Nitii tu usiku wa leo.’

Baada ya kuingia ndani, Alvin alienda kuoga. Kisha akaelekea kwenye chumba chake cha maktaba ili ili kufanya mkutano kwa njia ya video. Katikati ya mkutano huo, ghafla alihisi mwili wake unawaka moto. Hakujisikia vizuri hata baada ya kuvua koti lake.

“Uko sawa, bosi? Uso wako umekunjamana.” Msaidizi wake upande wa pili wa video aliuliza kwa mshangao.

“Sijisikii vizuri. Tuendelee kesho. Mfuatilie kwa uangalifu Jack Kimaro huko.” Alvin alizima kompyuta yake na kurudi moja kwa moja bafuni kwa ajili ya kujimwagia maji baridi. Haijalishi alijimwagia maji kiasi gani, bado alihisi joto likpanda kwa kasi. Alijua kwamba kuna jambo lilikuwa baya kwake. Hakula wala kunywa sana usiku ule, lakini kwanini… Subiri! Alikuwa amekula chakula alichochukua Lisa. Kwa wazo hili, uso wake ulionyesha hasira kali. Alithubutuje!

Mlango wa bafuni ulipigwa teke kwa kishindo. Jambo hilo lilimshtua sana Lisa aliyekuwa akitandika kitanda chake. Alimwona Alvin akimfuata, matone ya maji yamefunika mwili wake. Uso wake ulijaa ukali. “Dawa yake ilianza kumchukua ama?” Lisa alijiwazia.

“Kuna nini… Una shida gani?” Lisa alikurupuka huku akirudi nyuma kwa hofu. Ghafla, aliogopa.

"Uliweka nini kwenye chakula ulichonilisha kwenye sherehe?" Alvin alimshika mkono na kumburuta kutoka sakafuni. Macho ya Lisa yalimtoka. Hakutarajia kwamba angefahamu mapema namna ile.

“Mimi… sijui unasema nini.”

"Bado unakataa, huh?" Alvin akaibana shingo yake, macho yake yakidhihirisha chuki. "Nani mwingine angepata nafasi ya kufanya huu ujinga kama si wewe?"

Lisa alikuwa karibu kukosa hewa. Hakuwahi kufikiria kwamba majibu ya Alvin yangegeuka kuwa ya kutisha sana. Aliogopa sana. “Ilikuwa… mimi ndiye niliyefanya… Samahani!” hatimaye Lisa alikiri.

Shingo ya Lisa iliuma sana hivi kwamba machozi yalitiririka usoni mwake. Alihisi kwamba alikuwa amekutana ana kwa ana na Ziraili! Alijuta sana!

“Mwovu kiasi gani wewe! Nilikuamini sana!” Hasira zikamlipuka Alvin kifuani. Kwa nini afanye jambo kama hilo? Alichochukia zaidi maishani mwake ni kudanganywa! Alimchukia, lakini taratibu alianza kuhisi anapoteza fahamu. Baada ya kutoka nje ya udhibiti, akamtupa Lisa kitandani. Nguo za Lisa zilichanika kwa sababu ya vurumai hiyo. Aliamka na kukimbilia bafuni kuoga tena.

Kelele ya mshindo wa mlango ikasikika. Mshindo huo ulimfanya Lisa ahisi kama umepiga moyoni mwake. Lisa alitetemeka kwa woga huku akijizuia kulia. Alipojiuliza ni nini kingeendelea baada ya hapo alikosa nguvu kabisa. Alikuwa amekosea! Alikuwa amekosea sana. Hakupaswa kushawishiwa kutumia mbinu ya aina hiyo! Lisa aliacha macho yake yatoe machozi, akijihisi mwenye hatia sana.

Maji katika bafu yalimwagika kwa dakika 45. Akiwa na wasiwasi kuwa kuna jambo limemtokea Alvin, Lisa alijipa moyo na kuusogelea mlango wa bafu na kuugonga. "Uko salama? Samahani. Je! unanihitaji—”

"Nyamaza. Afadhali nife kuliko kumgusa mwanamke kama wewe.” Mlango wa bafuni ulifunguliwa kwa nguvu. Akiwa amelowa kichwani hadi miguuni, Alvin alimtazama Lisa kwa macho mekundu yaliyoiva hasira. Lisa aliduwaa kwa mshangao.

"Uliweka kiasi gani kwenye chakula?" Alvin alikuwa katika hali mbaya lakini alijikaza tu na kujifanya mgumu. Hakutaka kabisa kujishusha na kukubali msaada wa Lisa. Kwa hasira, alimvuta bafuni na kumlowesha kwa maji ya baridi.

Kabla hata maji ya baridi hayajamwagika kichwani mwake, Lisa alianza kutetemeka. Ni pale tu Alvin alipogundua kuwa anashindwa kupumua ndani ya maji ndipo alipomwachia. Alilaani kwa sauti nzito na kuupiga mlango kwa nguvu. Kisha, akavaa nguo zake na kukimbia nje haraka. Lisa alitoka bafuni kwa aibu. Alitaka kumfuata, lakini alikuwa amechelewa.

Saa sita usiku Sam alikimbia hospitali na kumkuta Alvin akipokea dawa kwa njia ya dripu kitandani. Wakati huo, alipigwa na butwaa, asijue amcheke au amhurumie Alvin kwa jinsi alivyokuwa akihangaika kumtuliza askari wake aliyeng’ang’ana kusimama wima muda wote. Sam alijikuta akimuonea wivu Alvin, alitamani tukio hilo lingemkuta yeye, asingelaza damu. Uso wa alvin ulikuwa bado haujatulia kwa wakati huo.

“Kwa nini umekuja kutesekea hospitalini? Ulipaswa kumtii Lisa mara moja na kumaliza matatizo yako nyumbani. Suala hilo lingetatuliwa chumbani kwako.” Sam alimwambia Alvin huku akizuia kicheko chake.

“Sema hivyo tena uone nitakachokufanyia.” Alvin aliyakodoa macho yake yenye uchungu. Alikasirika sana hata akakaribia kumpiga chupa ya dawa kichwani.

Hans alikunja uso. “Zingatia maneno yako, Bwana Harrison. Bwana Kimaro hapendi kabisa wanawake wanaotumia mbinu za aina hii.”

Sam alipigwa na butwaa. Ilimjia kumbukumbu kwamba Alvin alishawahi kumsimulia kisa cha mama yake kutumia dawa za nguvu za kiume kumlazimisha baba yake kulala naye kimapenzi na mimba iliyotokana na kitendo hicho ndiyo iliyomzaa Alvin.

Alvin alikua hana mapenzi ya baba yake. Alvin aliamini kuwa alikuja duniani kwa kupitia mbinu hizo chafu za mama yake. Kwa hiyo, alichukizwa na matumizi ya mbinu hiyo, ambayo ilitosha kuelezea kwa nini alichukizwa sana na kitendo cha Lisa.

"Ikiwa hutaki kumuona tena, mwambiee aondoke," Sam alipendekeza baada ya kushusha pumzi.

Alvin alicheka. “Hata nikimfukuza anaweza asiondoke. Kwanza hana hata pa kwendai."

“Kwa nini usihamie kwingine? Nitakusaidia kutafuta sehemu nzuri huko Mbezi Beach.” Sam alipendekeza.

“Hapo ndipo mahali pangu. Kwanini niondoke?” Aliuliza kwa dharau Alvin.

Ghafla Sam aliinua macho yake na kuuliza kwa shauku, "umekaa naye kwa muda mrefu sasa, lakini kwanini huna hisia zozote kwake?"

"Hisia?" Alvin alidhihaki. “Vipi kuhusu hisia zako kwa mfanyakazi wa nyumbani anayepika chakula cha familia yako? Labda ningevumilia uwepo wake kama asingenifanyia hivi, lakini sasa… sitamsamehe.”

Sam akatoa macho. “Vipi kuhusu kumlipizia kisasi? Mfungie chumbani umlishe na yeye hivyo vitu halafu mwache apate maumivu kama unayopitia wewe.”

Alvin alijibu kwa ukali, "sitaki tena kusikia mawazo yako yakijinga, Sam.”

SURA YA 42

Saa kumi alfajiri, Alvin alimaliza dozi yake ya dawa za dripu. Alirudi nyumbani tu baada ya ‘joto’ mwilini mwake kupungua. Mara baada ya kuingia ndani ya nyumba yake, alimuona Lisa akiwa amelala fofofo kwenye kochi lililokuwa pale sebuleni. Hapo awali, alidai kwamba aliogopa kutokana na ndoto mbaya ikiwa alikuwa peke yake chumbani. Hata hivyo, alionekana kulala vizuri wakati huo. Alvin alihisi yote yalikuwa ni sehemu ya mbinu zake chafu.

Ni nini kilimpa haki ya kumfanya apate maumivu makali na kupokea sindano ya dripu hospitalini na yeye akiwa amelala kwa raha ndani ya nyumba? Kwa hasira kali, alichukua maji kutoka kwenye meza na kummwagia moja kwa moja usoni. "Amka."

Lisa alishituka kwa mshtuko, akamkuta Alvin akiwa amekaa upande wa pili wa kochi. Alihisi kama amekutana na shetani. Huku akitetemeka, Lisa aliuliza, “Ulirudi saa ngapi? Kwahiyo… Mambo vipi sasa?”

"Kwa sababu yako, nilikuwa na dripu ya sodium chloride IV usiku kucha hospitalini." Alvin alipomtazama Lisa, tukio la yeye kuteseka hospitalini usiku mzima lilimpitia tena mawazoni. Ilimfanya ahisi kudhalilishwa sana. “Lisa, ninachojutia zaidi maishani mwangu ni kukuoa. Sikupaswa kukuokoa ulipokuwa umefungwa kwenye jumba la kizamani hapo awali.”

Lisa alipandwa na hasira, lakini hakuwa na haki ya kukasirika. Kama ni yeye ndiye angekuwa amentendewa kama Alvin, bila shaka asingefurahi pia, hivyo akaona jambo la maana ni kumwangukia kwa msamaha. “Samahani… samahani sana… sitafanya tena wakati mwingine.”

"Wakati mwingine?" Alvin alibana kidevu chake kwa nguvu. “Unafikiri bado kuna wakati mwingine? Ninachukia kukutazama tu. Ulitaka kunilazimisha nilale na wewe kwa kutumia hila chafu. Huna aibu? Wewe ni mchafu kama makahaba wa barabarani!” Alvin aliongea kwa hasira kana kwamba ametiwa sumu.

Macho ya Lisa yalififia mara moja kwa kujawa na machozi, hakuweza kujizuia tena kulia. Lisa alifikiri kwamba alikuwa mjinga sana. Alikuwa amefanya nini?

“Kulia ndo nini? Sitakuhurumia eti kwa sababu tu unalia.” Alvin alikerwa na kilio chake. “Sikiliza nikwambie, sitaki kula chochote utakachotengeneza tena. Usionekane mbele yangu. Pia, usiingie kwenye chumba changu cha kulala. Uwepo wako hapa ni kero tu kwangu." Alvin alielekea chumbani kwake mara baada ya kumaliza kuongea kwa hasira kali.

Akiwa amelala chini, Lisa alikuwa ameshuka moyo na amechoka kabisa. Kwake, Alvin alikuwa ukuta usioweza kuvunjika. Sio tu kwamba alishindwa kudhoofisha ukuta huo, lakini pia Alvin alimchukia kabisa sasa. Hah. Sawa. Liwe liwalo. Asilazimishe kitu chochote ambacho si chake. Hakika ilikuwa ni kosa lake. Hakupaswa kumfanyia jambo la aina hiyo.

Yote aliyokuwa amefanya mpaka wakati huo ilikuwa ni kumkosea tu Alvin, jambo ambalo lilimfanya ajione kuwa hana maana kabisa kwake. Aliburuta blanketi lake na kurudi chumbani huku miguu ikitetemeka. Wakati huo, alikuwa na kizunguzungu, mwili na roho vyote vilikuwa vimekosa raha. Alijilaza kitandani kupumzika. Muda si muda alipitiwa na usingizi na kulala.

Kisha, aliamshwa na simu kutoka kwa Pamela. “Kwa hiyo mambo yalikuwaje? Uliifanikiwa?"

"Nini kimetokea?" Kwa tabasamu la uchungu, Lisa alimweleza tukio hilo Pamela ambaye alizidiwa na hisia ya hatia.

“Samahani Lisa, nimekuponza. Labda sikufikiria mambo vizuri…”

Lisa alimpoza rafiki yake aliyekuwa akijihisi hatia. “Kwa vile hanipendi, sikupaswa kumlazimisha. Zaidi ya hayo, nilikutana naye kwa sababu za zangu binafsi. Pamela, unadhani sikupaswa kuolewa na Alvin kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa Ethan?”

Pamela alipumua. “Tayari yameshatokea. Nini kingine unaweza kufanya wakati tayari umefunga naye ndoa? Utakata tamaa na kudai talaka?"

Lisa alibaki kimya kwa muda. “Haki. Ninapaswa kuomba talaka. Nahisi kama sina amani kuendelea kuishi naye.” Lisa aliongea kwa uchungu na kukata simu.

Mlango wa chumba cha kulala ukiwa umebaki wazi, aliona tayari Alvin ameshatoka. Akashusha pumzi. Baada ya tukio hilo, alionekana kubadilika na kuwa mtu tofauti kabisa, jambo ambalo lilimfanya awe na wasiwasi mwingi.

Alipika chakula cha kawaida. Baada ya kumaliza kula alipokea simu kutoka kwa Joseph Ruta, bosi wake. "Lisa , umemaliza kutoa mchoro wa nyumba ya Bw. Mushi?"

“Nimemaliza."

“Sawa. Peleka mchoro kenye ofisi za Golden Corporation utakutana na Kelvin Mushi anakusubiria. Amekuwa akihimiza kwa hilo.”

“Sawa.” Lisa hakuthubutu kuchelewa. Alijiandaa haraka na kuelekea Golden Corporation.

Ofisi hiyo ilikuwa katika ukanda wa kibiashara katikati ya jiji, eneo lililozungukwa na majengo marefu. Lisa alijitambulisha vizuri kwa dada wa mapokezi aliyemkuta kwenye ofisi za Golden Corporation. Dada huyo wa mapokezi alimruhusu kupanda juu mara moja. Alipokuwa akingojea lifti, mtu mmoja alitoka kwenye lifti nyingine. Kwa kumbukumbu zake, alionekana kama mama yake Ethan, Sonya Mushi. Sonya alishindwa kumtambua Lisa. Alielekea tu kwa haraka kwenye mlango mkuu akiwa na mkoba wake.

Wakati huo huo, lifti ilifika na mlio wa ‘ding!’ Lisa aliingia kwenye lifti huku mashaka yakizidi kuibuka kichwani mwake. Alikuwa amegongana na Ethan maeneo ya Mbezi Beach alipokuwa akitoka kuonana na Kelvin Mushi kwenye jumba lake, na pale tena alikutana na Sonya akiwa anaenda kuonana na Kelvin pia. Ni bahati tu au kuna kitu ndani yake, je wawili wale walikuwa na uhusiano na Kelvin?

Lisa alianza kuunganisha nukta. Jina la ukoo la Kelvin lilikuwa ni Mushi. Je, anaweza kuwa jamaa wa Sonya?” Lisa alijiuliza. Lakini, Lisa alikuwa hajawahi kusikia kutoka kwa Ethan kabla ya hii kwamba alikuwa na uhusiano na mtu mwenye nguvu kama Kelvin. Ghafla, kichwa kilimuuma kwa kuwaza mambo magumu aliyoshindwa kuyajua.

Lifti ilifika ghorofa namba ishirini na nane, Lisa alitoka kwenye lifti na baadaye akaingia katika ofisi ya bosi. Ilitokea kwamba Kelvin Mushi alikuwa akimsikiliza mgeni, kwa hivyo Lisa alingoja kando kwa muda. Ni baada tu ya mgeni kuondoka ndipo aliwasilisha mchoro na ufafanuzi wake kwa Kelvin.

“Kwa kweli, nilimpigia simu Joseph kukuulizia bila nia yoyote ya kukuhimiza. Sikutarajia kuwa tayari ulikuwa umemaliza. Kwa kweli, wewe ni mzuri sana." Kelvin alichukua mchoro kutoka kwake. Alipopeleka macho yake kwa Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. “Bi Jones, huonekani kuwa mchangamfu sana. Je, umekosa usingizi kwa kukesha ukiandaa mchoro huu?”

Lisa alipigwa na butwaa. Katika siku mbili zilizopita, alikuwa amechoka kimwili na kiakili. Hakika, alionekana mnyonge. Kabla hajaondoka nyumbani alikuwa amejipodoa kidogo usoni. Hakutarajia kwamba Kelvin angeona sura yake ya uchovu. "Ndiyo. Nilikosa usingizi hivi karibuni.” Alijibu tu ili kumridhisha.

Kelvin alifikiri kwamba alikuwa akisumbuliwa na kukosa usingizi pengine kwa sababu Ethan na Lina walikuwa wakienda kuchumbiana. Hakuweza kujizuia kumuonea huruma sana.

Muda mfupi baadaye, jambo lingine likapita akilini mwake. Alikuwa amesahau kushika kadi ya mwaliko ambayo dada yake alimletea muda si mrefu!
Hata hivyo, alikuwa ameshachelewa. Lisa aliishaiona kadi hiyo yenye maneno 'Sherehe ya uchumba ya Ethan Lowe na Lina Jones'. Alikazia macho na kutoa tabasamu hafifu. "Bw. Mushi, unajuana na familia ya Mushi na Masawe?"

Kelvin aliweka kadi ya mwaliko pembeni, kisha akatoa kikohozi kidogo. "Hao ni jamaa zangu wa mbali tu." Alikuwa na wasiwasi kwamba huenda Lisa angegundua kuwa yeye ndiye mjomba wa Ethan, jambo ambalo lisingemfurahisha kabisa.

Zaidi ya yote, Lisa alikuwa binti kijana. Angeweza kukata tamaa katika kubuni jumba lake kwa sababu hiyo. Kwa kumhurumia, Kelvin alitaka sana kumsaidia.

“Oh.” Jibu lake lilikuwa sawa na vile Lisa alitarajia. "Naomba nikueleze mchoro kwa undani, Bw. Mushi."

Kelvin aliitikia kwa kichwa. Kwa kuzingatia kwamba hakuwa mtaalamu wa mambo ya ubunifu wa majengo, alikuwa na uelewa mdogo kabisa wa mchoro wa kina. Hapo awali, Lisa alisimama mbele ya meza ya ofisi huku akielezea mchoro huo. Lakini, haikuwa rahisi kwani mchoro ulikuwa umepinduliwa kutoka kwa pembe yake. Kelvin alielekeza upande wake wa kulia. “Njoo usimame hapa.”

Baada ya kupata ruhusa yake, Lisa alipita kwenye dawati na kufika upande wake wa kulia. Aliinama, kisha akanyoosha kidole kuelekeza eneo fulani. "Niliogopa kuwa hakutakuwa na nafasi ya kutosha kuweka rafu za vitabu, kwa hivyo nilipanga safu moja zaidi hapa ..."

Kelvin alitazama vidole vyake virefu na vyembamba vilivyofanana na ncha za machipukizi ya mianzi. Alikuwa amesimama karibu naye. Ingawa bega lake lilikuwa umbali fulani kutoka kwake, aliweza kunusa harufu ya kiuvutia ya kiasili iliyotoka kwenye nywele zake.

Baada ya kufanya kazi na watu mbalimbali kwa miaka mingi, Kelvin alikuwa na uzoefu na harufu ya manukato kutoka kwa wanawake mbalimbali. Ilikuwa nadra kupata wanawake kama Lisa ambao walidumisha harufu ya asili, na aina hii ya harufu ilimfanya asisimke.

Kelvin alimtazama kwa kuibia binti huyo ambaye alikuwa na nywele nadhifu nyeusi. Licha ya kuwa alivaa nguo za kawaida, suruali isiyobana na tisheti pana, alionekana mrembo na mwenye kuvutia.

"Bw. Mushi, umeridhika na mpango kama huo?" Sauti ya Lisa ilimrudisha akilini ghafla.

"Ndio, inaonekana nzuri." Kelvin aliona aibu kidogo kwani alishindwa kabisa kukumbuka alichokisema muda huo. Kisha, Lisa alitumia dakika 20 zilizofuata kuelezea mchoro kwa undani, akidhani kwamba Kelvin angeomba mchoro huo urekebishwe kwa njia fulani. Baada ya yote, mbunifu yoyote hawezi kutimiza mahitaji ya mteja kwa 100%.

Kelvin alisema kwa uthabiti, “Nimeridhika sana. Hakuna kitu kinachohitaji kurekebishwa. Anza kazi kesho kulingana na mpango huu."

“Haraka hivi?” Lisa alishangaa.

"Naamini katika uwezo wako. Natamani ukarabati ufanyike haraka ili niweze kuingia ndani haraka iwezekanavyo. Hivi sasa, ninaishi na kundi la watu ambao kila wakati wananihimiza kuoa. Sipendi,” Kelvin aliongea kwa sauti ya utani.

“Bado hujaoa, Bw. Mushi?” Lisa alishangaa.

Kelvin aliinua uso wake. “Kwanini? Ninaonekana kama nimeoa?”

"Kwa kuzingatia umri wako na mafanikio katika kazi yako, nilifikiri utakuwa umeoa."

“Sivyo.” Alisisitiza maneno hayo waziwazi.

Lisa hakutaka kuendelea kujadili zaidi suala hilo, akarudi kwenye kazi iliyompeleka pale. "Nikirudi, nitajadili suala hili na timu ya ukarabati na kuwaomba waanze kazi ya ukarabati kesho." Lisa alimpa mkono kabla hajageuka na kuondoka.

Muda mfupi baada ya Lisa kuondoka, Ethan akampigia Kelvin simu.

“Mjomba Kelvin, ulikubali kweli kupendekeza jumba la rafiki yako lililoko Kigamboni likarabatiwe na Kibo Group?

“Yote ni kwa sababu ya mama yako ambaye alikuja ofisi kwangu kunisumbua asubuhi na mapema. Ulisema hutanisumbua, mjinga wewe. Kwa hivyo ukamtuma mama yako afanye hivyo, huh?" Kelvin alisema kwa mzaha, “Hii itakuwa mara ya mwisho. Usiniombe nikusaidie tena masuala ya familia ya akina Masawe.”

“Mjomba Kelvin, kwani una matatizo na familia ya akina Masawe? Kwa kweli—”

“Naliweka hili wazi. Ndoa yako na familia ya Masawe inahusiana na familia ya Lowe, sio mimi.” Kelvin alikata simu mara baada ya kumaliza kuongea. Kila alipomuona Lisa alizidi kuchukizwa na familia ya akina Masawe ambayo ilikuwa ikimtendea bila huruma.

SURA YA 43

Saa kumi jioni baada ya kutoka kazini, Lisa alienda pharmacy kuchukua dawa ya homa kisha akaelekea nyumbani. Ulipofika wakati wa chakula cha jioni, Alvin alikuwa bado hajarudi. Alimtembeza Charlie kuzunguka uani mara tu baada ya kumaliza kula chakula chake cha jioni.

Charlie alikuwa amechoka kutembea, hivyo alilala kwenye uzio akitazama kundi la vijana wakicheza mpira wa kikapu jirani. Mwanamke ambaye pia alikuwa akitembea na paka wake alikuja kumtazama Charlie. Alitabasamu na kusema, "Pengine paka wako atazaa baada ya mwezi mmoja."

Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. Kwa tabasamu, alisema, “Bibi, nadhani umekosea. Paka wangu ni mnene tu.”

“Sidhani hivyo. Niligongana na mumeo mapema na hata kumuuliza juu yake. Mumeo alikiri kwamba paka ni mjamzito.”

"Mume wangu?" Lisa akashangaa. Je, bibi huyo alikuwa anamaanisha Alvin? Hakika, Alvin alikuwa akitembea na paka mara moja moja. Hata hivyo, Charlie hakuwa na mimba.

"Bibi, nina hakika umemchanganya mtu mwingine na Alvin." Lisa alimkosoa.

“Hilo haliwezekani. Naweza kuwa sioni mbali, lakini mwonekano wa mumeo ni wa aina yake. Hakuna mtu mwingine jirani anayefanana naye. Zaidi ya hayo, paka wangu anamfahamu paka wako kwani wamecheza pamoja mara kadhaa.”

Mwanamke huyo alipokuwa akiongea, paka wake alimsogelea Charlie. Charlie mara moja akainama kumsalimia paka huyo. Walionekana kuwa karibu kana kwamba walikuwa marafiki wa zamani. Lisa alikata tamaa kabisa. Je, Charlie alikuwa na mimba? Subiri, Charlie alikuwa paka wa kike au wa kiume? Daima alikuwa akidhani kwamba Charlie alikuwa paka wa kiume. Ilikuwa ni kwa sababu Charlie kila mara alikuwa akimsumbua Lisa, na zaidi ya hayo, jina lake lilisikika kuwa la kiume.

"Inaonekana, unaona vibaya, binti. Kutokana kwa tumbo lake kubwa, unaweza kuona wazi kuwa ni mjamzito. Je, mumeo hakukupa taarifa kuhusu hilo?”

“Asante kwa kunikumbusha. Ni mara yangu ya kwanza kufuga paka.”

Baada ya Lisa kumuaga bibi huyo kwa aibu, alichukua teksi haraka hadi hospitali ya mifugo. Baada ya daktari wa mifugo kumfanyia paka uchunguzi wa ultrasound, alishikilia miwani yake na kusema, “Paka wako atazaa hivi karibuni."

Msururu wa maswali uliangaza akilini mwa Lisa. Kutoka kuwa mjamzito, hadi kujifungua hivi karibuni, na yeye hakuwa na habari yoyote! Kwanini Alvin alimficha jambo hilo? Lisa alijiona ni mjinga kwa kiasi fulani.

“Bado kuna siku kumi zaidi kabla ya tarehe zake kukamilika.” Daktari akaongeza, "Mwangalie kwa uangalifu kwa siku hizi. Hata hivyo, manyoya yake yanaonekana laini na ya kung'aa, kwa hivyo nadhani kwa kawaida ana lishe bora na inayofaa kabisa. Anapaswa kujifungua kwa njia ya kawaida.”

"Naweza kujua kama paka hutapika wakati wa ujauzito?" Lisa aliuliza.

"Paka wengine hufanya hivyo. Wanaweza kupoteza hamu ya kula katika tarehe za mwanzo za ujauzito."

Baada ya maelezo ya mtaalamu, Lisa alitoka nje ya hospitali kama hana akili. Wakati huo, alikuwa na mawazo ya kudanganywa na Alvin. Kulingana na ratiba, Alvin alipaswa kujua kuhusu ujauzito wa Charlie wakati wa kuchunguzwa hospitalini alipotapika ile siku. Pia, Charlie alitapika si kwa sababu Lisa alimlisha chakula kisichofaa bali kwa sababu tu alikuwa mjamzito. Kwa hivyo, kwanini hata amekuwa akimlaumu kuhusu jambo hilo wakati wote huu? Kulikuwa na maana gani kwa yeye kumdanganya Lisa kuwa alimlisha chakula kibaya ili tu amhudumie Charlie?

Hata hakuwa amefanya kosa lolote. Hata hivyo, Alvin alikuwa amembebesha lawama za bure ambazo zilimfanya ajisikie mwenye hatia sana kila alipomwona Charlie. Alikuwa amedanganywa. Hilo ndilo wazo pekee lililompata. Laiti isingekuwa Alvin ambaye alimuokoa mara mbili kabla ya hapo, angemkimbilia kumpiga makofi mawili.

Lisa alipofika nyumbani, Alvin alikuwa bado hajarudi. Baada ya kunywa dawa, Lisa alijilaza kidogo akapitiwa na usingizi. Asubuhi, alisikia mlango wa chumba cha Alvin ukifunguliwa huku akipiga mswaki bafuni. Kuona hivyo, alijifuta mdomo na kutoka nje mara moja.

"Unafanya nini?" Alvin akauliza kwa hasira. Ikiwa Lisa alikuwa akipanga kumuomba msamaha, ni bora angeacha tu.

"Ulikuwa unajua suala la ujauzito wa Charlie, sivyo?" Lisa alimkazia macho baada ya kumuuliza.

“Ana mimba?” Alvin akatazama pembeni kwa jeuri akijifanya hajui lolote.

“Acha kujifanya! Ulimwambia jirani yako kuwa Charlie ana mimba. Nilipoenda kwa daktari wa mifugo kuuliza kuhusu hilo, niliambiwa kwamba atajifungua hivi karibuni. Alitapika kwa sababu tu ni mjamzito na si kwa sababu ya chakula nilichompa.” Lisa alizidi kukereka wakati akiongea. Kisha akapandisha sauti kwa hasira. “Alvin, unafikiri ni jambo la kufurahisha kunidanganya kwa kunichukulia kama mpumbavu?”

Alvin alionesha hali ya kusikitika kidogo na kuongea kwa aibu kidogo. “Lisa , afadhali uelewe jambo hili wazi. Wewe ndiye uliyetaka kuhamia kwangu, na nilitimiza tu matakwa yako kwa kukupa nafasi ya kunifurahisha.”

“Kwa hiyo napaswa kukushukuru kwa kunidanganya?” Lisa alizidi kuchemka kwa hasira.

“Ulikuwa hauna pa kuishi, nikakuhifadhi. Zaidi ya hayo, nilikuokoa mara mbili baadaye. Kama nisingekuwa mimi, unafikiri bado ungeweza kuwa hapa na kuzungumza nami kijeuri?” Alvin alikunja uso kwani Lisa alionekana kusahau hali yake. Wakati hakuwa na pesa na mahali pa kukaa wakati huo, alikuwa amemkaribisha kwa fadhili. Lakini Lisa, kwa kweli hakumuheshimu! Alithubutu vipi kumkosoa wakati huo? Nani alimpa haki ya kufanya hivyo?

Lisa alikasirika na alishindwa cha kusema. Kwa kweli, Alvin alikuwa mkombozi wake, lakini je, ilimaanisha kwamba angeweza kumtendea anavyotaka? Sawa. Lisa ndiye aliyekuwa amemwendea kwa nia mbaya kwanza. Alistahili kudanganywa. Kwa sura iliyofifia, hakusema neno lingine.

Alipogundua hilo, Alvin alijiamini zaidi. "Lisa , unapaswa kutafakari juu ya mtazamo wako. Ikiwa si Charlie ambaye ni mjamzito na anahitaji matunzo ya mtu wa kumhudumia nisingemvumilia mtu kama wewe kukaa hapa.”

Lisa aliondoka kwa hasira. Alihisi kizunguzungu na wazimu sana hivi kwamba alitaka kupigana naye. Laiti angejua mapema kama safari ya kuwa Aunty wa Ethan ingekuwa ngumu vile, hakika asingemkaribia Alvin!

SURA YA 44

Saa mbili na nusu asubuhi, Lisa aliendesha gari hadi Mbezi beach. Alielekea kwenye jumba la kifahari la Kelvin ili kusimamia maendeleo ya ukarabati. Alikaa kwenye saiti siku nzima. Kelvin alifika alasiri ili kutoa zawadi kama ishara ya kushukuru kwa juhudi za wafanyakazi.

Lisa alizidiwa na bahasha nene iliyowekwa mikononi mwake. "Bw. Mushi, zawadi hii labda ni zaidi ya ninavyostahili."

“Ni ishara ndogo tu ya shukrani." Kelvin alimsihi Lisa huku akimkazia macho usoni kwa udadisi. “Unaonekana vibaya. Unaumwa?"

"Labda ni homa ya kawaida tu." Lisa alijibu kinyonge.

"Pumzika kwa siku kadhaa uisikilizie hali yako. Naamini ukarabati utaendelea kwa muda uliopangwa. Mimi si bosi mbaya.” Sauti yake ilikuwa tulivu na ya kubembeleza.

Lisa aliitikia kwa kichwa. Mtu wa nje alikuwa na huruma naye zaidi ya Alvin ambaye aliishi naye pamoja. Alvin hakuwa amemuuliza anajisikiaje hata kidogo. Pengine alimchukia sana sasa, kwa nini ajisumbue? Mwanamke hawezi kuishi kwa furaha na mtu asiyemjali.

"Asante, Bw. Mushi." Aliitikia tena na kuanza kuondoka zake.

Lisa likuwa amepiga hatua kadhaa tu kabla ya kuhisi kizunguzungu kichwani. Kwa bahati nzuri, Kelvin alimwona haraka na kusogea mbele kumshika asianguke. Joto lililotoka kwenye mwili wake lilimshangaza. “Una homa kali. Ngoja nikupeleke hospitali.”

“Niko sawa nitaenda tu mwenyewe…” Lisa aliona haya.

"Bi mdogo, acha kujaribu kuwa mgumu. Unanifanyia kazi sasa na nitahitaji kuwajibika endapo lolote baya litatokea,” Kelvin alimwambia huku akimbeba hadi kwenye gari.

Lisa alishindwa kupambana na udhaifu ulioenea mwilini mwake na kujikuta akipoteza fahamu muda si mrefu baada ya kuingia ndani ya gari. Kufikia wakati alirejewa na fahamu, aligundua kuwa alikuwa amelazwa katika kitanda cha hospitali na bomba la dripu limewekwa mkononi mwake. Kelvin alikuwa akimenya tunda kwenye kiti karibu na kitanda. "Ulikuwa na homa yenye joto kali ya 102 ° F. Nilikaribia kukulipa fidia ya majeruhi kazini.”

“Samahani kwa kukusumbua.” Lisa alijiinua na kuomba msamaha kwa dhati. “Kuumwa kwangu hakuhusiani na kazi. Nilishikwa na homa jana na nikafikiri ningejisikia vizuri baada ya kumeza vidonge. Sikutarajia hali ingekuwa mbaya zaidi. Hakika ilikuwa ni uzembe wangu. Sikupaswa kufanya kazi leo.”

“Ni sawa, ugonjwa huwa unatokea tu.” Kelvin alibaki mpole tangu mwanzo bila kuonekana kukasirika.

Lisa akazidi kujihis hatia. "Samahani kwa kuanza ukarabati wa jumba lako kwa mkosi."

Tabasamu lilitanda usoni mwa Kelvin baada ya kusikia Lisa akiomba msamaha bila kukoma. "Acha kusema hivyo. Mtu yeyote anaweza kupata homa wakati wowote.”

Lisa alikengeushwa kwa muda mfupi. Hakuweza kujizuia kuwaza jinsi uhusiano wake na Alvin ungekua ikiwa Alvin angekuwa na utu kama Kelvin. “Bw. Mushi asante kwa siku ya leo. Sio lazima ubaki hapa. Naweza kumpigia rafiki yangu simu.”

"Nichukulie kama rafiki yako na utaacha kuhisi kama unanisumbua." Kelvin alimtoa wasiwasi huku anampa tunda lililokatwa.

“Bw. Mushi, kweli ukarimu wako umepitiliza. Siwezi…” Lisa alishtuka chini ya macho yake.

Lisingekuwa jambo la kawaida kwake kufanya urafiki na Kelvin iikiwa bado alikuwa yule mwanadada tajiri kama hapo awali. Lakini, alikuwa tu mbunifu asiyejulikana sasa. Je, inawezekana kwamba alipendezwa naye?

“Kila mtu anapaswa kutendewa sawa. Mimi ni kama binadamu mwingine yeyote anayehitaji marafiki.” Kelvin alimuonea huruma sana yule binti.
•••
Akiwa nyumbani kwake mtaa wa Buzwagi, Alvin alikuwa akipitia chaneli za TV akiwa amechukuliwa na mawazo ya mbali sana. Hakuna hata chaneli moja kati ya hizo 200+ iliyomvutia macho. Akaitupa rimoti kando huku akihisi kuchanganyikiwa. Ilikuwa yapata saa moja usiku muda huo na Lisa bado hajarejea nyumbani.

Ilikuwa imepita saa moja tangu Alvin arudi nyumbani kutoka kazini na hapakuwa na dalili zozote za kuwepo Lisa. Hakumjali hata Charlie tena. Ilionekana kweli alikuwa amefikia kikomo cha uvumilivu.

"Njoo, Charlie. Twende tukanunue matunda.” Alvin akambeba paka mikononi mwake. Charlie alicharuka mara kadhaa akigoma kubebwa. Paka yule mjamzito alikataa kutoka, lakini Alvin alilazimisha kutoka pamoja naye.

Kulikuwa na maduka kadhaa yaliyokuwa kando ya barabara kuu ya mtaa huo. Alvin aliingia kwenye duka la matunda. Alitazama na kukagua matunda kwa muda lakini hakuwa na uhakika wa kununua. Mawazo makuu kichwani mwake yalikuwa juu ya Lisa! Kwa nini Lisa hakuwa nyumbani bado?

Muuza duka la matunda akiwa amesimama kando ya mlango alikuwa akimtazama kwa siri kijana huyo mzuri wa kipekee. Nini kilikuwa kikiendelea juu yake? Alikuwa akizunguka duka mara nyingi zaidi kuliko alivyoweza kuhesabu lakini hakuwa amenunua chochote. Pia alimuona akiendelea kutupa macho kuelekea barabarani. Je, inawezekana kwamba alipendezwa naye lakini alikuwa na haya kumuanza? Sura ya aibu ilitanda usoni mwake. Hatimaye, akapata ujasiri wa kumkaribia.

Bila kutarajia, Alvin akamkwepa muuza duka yule huku akipiga hatua kubwa kuelekea mlangoni. Akatoka nje akiwa na ameghairi kununua chochote. Akiwa amefika kwenye barabara inayoelekea nyumbani kwake, hapo ndipo alipogundua gari la BMW likiwa limeegeshwa kando ya barabara ile upande wa pili. Mwanadada mrembo alitoka kwenye gari.

Wow, Alvin alishuhudia mwanamume mwingine alishuka kwenye gari na kuajribu kumshika mpenzi wake. Alikuwa amesalitiwa licha ya kubarikiwa na sura nzuri kuliko yeye. Iliuma sana sana!

Upande wa pili wa barabara. Lisa alimshukuru Kelvin kwa dhati tena. Alipogeuka tu, alimuona Alvin akimsogelea kwa hatua kubwa huku akiwa amemkumbatia Charlie. Mwangaza hafifu wa mbalamwezi kutoka juu ulimulika uso wake wenye huzuni. Alikosa la kusema!

Ilikuwa ni mara ya pili tu kwake kurudi nyumbani usiku namna ile akiwa amesindikizwa na wanaume tofauti. Kwanini siku zote alikutana na Alvin? Na mara zote mbili alikuwa na mwanaume mwingine aliyempa lifti kumleta nyumbani? Alijua kwa vyovyote vile Alvin angemdhalilisha milele kwa tukio hilo. Kwa hiyo, alijitetea kabla Alvin hajapata nafasi, “Sijisikii vizuri sana leo. Kama kuna chochote unataka kuniuliza, tafadhali subiri kesho ili uniulize chochote.”

“Sidhani hivyo. Nahisi lazima utakuwa umechoka kwa kutumia siku nzima na jamaa yako. Vizuri? Ulipewa lifti ya kurudi nyumbani kwa Range Rover mara ya mwisho na sasa imebadilika kuwa BMW, huh? Si mbaya, Lisa. Unapanda matawi siku hizi. Jambo la muhimu ni kwamba, wanajua wewe ni aina ya mwanamke wa hali ya chini ambaye unaweza kufanya lolote ili tu kuingia kwenye kitanda cha mwanamume!”

Alikuwa ametoka tu hospitalini na hajaingia hata ndani. Kichwa chake kilikuwa kimeanza kujisikia vizuri lakini homa yake ilianza kumpanda tena baada ya kusikia matusi ya Alvin.
Hili lilimchosha sana kiakili. Alvin aliongea mara chache sana siku za nyuma lakini mbona amekuwa muongeaji ghafla?

"Sitaki kubishana na wewe." Ilikuwa inachosha kurumbana kila walipokutana. Lisa aliinamisha kichwa chake na kuanza kuondoka.

Tabia yake ya kumpotezea ilimkasirisha zaidi Alvin. Akamshika mkono kwa nguvu. "Unamaanisha nini? Kwa hiyo huniongeleshi sasa kwa kuwa umepata mtu tajiri zaidi? Umetoka siku nzima na haujarudi nyumbani hadi usiku wa manane. Je, ni makosa kwangu kukuuliza kuhusu hilo?”

SURA YA 45

Kwa namna alivyomshika alikua akimuumiza, lakini hakuwa na nguvu ya kuutoa mkono wake. Alichohisi ni kukata tamaa na uchovu. Aliinua macho yake kukutana na macho makali ya Alvin. “Inakuathirije nikichelewa kurudi nyumbani? Ninakaa kwako, lakini nimekuwa nikikupikia na kukusafishia. Isitoshe, ulinidanganya kuhusu mimi kumpa Charlie chakula kilichomdhuru tumbo wakati kumbe paka wako ana mimba. Paka anaendelea vizuri zaidi kuliko hapo awali. Si lazima niwajibike kwa ujauzito wake. Mimi si niliyempa mimba.”

“Unathubutu vipi kunijibu hivi?” Alvin akamtupia macho ya jeuri na magumu. Uso wake ulikuwa umetanda hasira. Mwanamke huyo alikuwa amefanya jambo baya lakini alikuwa akibishana kana kwamba alikuwa katika haki. “Usisahau kuwa wewe ni…”

“Ninajua kuwa mimi ni mke wako kisheria, lakini je, umewahi kunitendea kama mke?” Lisa alicheka. "Kwa maoni yako, mimi si kitu zaidi ya mwanamke asiye na aibu, duni kuliko mtu yeyote unayemjua."

“Ikiwa ndivyo ilivyo, kwa nini ulitaka kuolewa na mimi? Alvin alikasirishwa na tabia yake ya kupindukia. “Ni vyema ukajua hilo…”

"Hiyo ni sawa. Sikujua hili hapo awali na niliendelea kufikiria ningeweza kupata nafasi. Niache tu kuanzia sasa! Tuko kwenye ndoa ya mkataba tu hata hivyo, na ni mimi ndiye niliyekulazimisha.”

"Angalau unakumbuka kuwa ulilazimisha kuingia kwenye hii ndoa." Sauti ya Alvin ilikuwa kali. “Sitaki kuwa na uhusiano wowote na wewe. Sitaki kuchafuliwa na ugonjwa mchafu utakaoleta nyumbani baada ya kuupata kutoka mahali pengine.”

Lisa alihisi damu ikikimbilia juu ya kichwa chake. Mwili wake ulikuwa ukitetemeka kwa hasira.
Alikuwa amepanga kukaa hadi Charlie ajifungue kwa kuwa paka huyo alikuwa amempenda kwa dhati. Lakini, aligundua kuwa asingeweza kukaa pale kwa dakika nyingine tena.

Lisa akafungulia tabasamu la kejeli. "Hakika, ili nisichafue nyumba ya Bw. Kimaro kwa uwepo wangu mchafu, nitahama wakati huu."

"Je, hii ni moja ya hila zako?" Tabasamu la kujilazimisha lilienea usoni mwa Alvin. Hakuamini angefanya hivyo. Alikuwa ametumia bidii nyingi kujaribu kulala naye, hata hivyo.

Bila kumjali, aliondoa mkono wake kutoka kwake na kukimbilia chumbani. Alichukua begi lake na kuanza kufungasha vitu vyake kwa kasi ya radi. Hakuwa na vitu vingi kwa hiyo haikuchukua muda.

Alvin alimtazama kando ya mlango. Akiwa amechanganyikiwa, alifungua vifungo vya juu vya shati lake. Mwanamke huyu alikuwa mzuri sana katika uigizaji. Hakutafakari makosa yake mwenyewe hadi sasa. Je, asingemkaripia hata kama angekuja nyumbani kwa gari la mwanamume mwingine?

Lisa alimaliza kupakia mizigo yake na kuiweka mezani ile kadi ya benki aliyompa hapo awali. "Sikutumia senti ya ziada mbali na gharama za kila siku."

Hakufurahishwa na sauti ya hiyo. “Nimefurahi kusema hivyo. Si mimi niliyekulipia gharama za chakula cha kila siku na ziara zile za hospitali?” Alisema kwa tabasamu la kejeli.

"Hakika, nitapata malipo ya kamisheni kutoka kazini kesho na nitakulipa." Baada ya kumjibu hayo, Lisa hakuweza kujizuia kukaa hapo kwa sekunde nyingine tena. Alichukua begi lake na kuelekea mlangoni. Kabla ya kuondoka, alimuona Charlie akimtazama kwa huzuni. Machozi yalimtoka. Alishuka chini ili kumpigapiga paka kichwani.
'Samahani, siwezi kukutunza tena. Jitunze.'

"Charlie, rudi hapa!" Alvin alihisi kukasirishwa na tukio lililokuwa mbele yake. Uso wake ulikuwa umeharibika kwa mikunjo ya hasira. Alifikiri mwanamke huyo alikuwa anajifanya tu. “Lisa usijutie uamuzi wako. Ukitoka kwenye mlango huu, sitakuruhusu urudi hata ukipiga magoti kuomba.”

“Usijali kwa sababu sitafanya hivyo!” Lisa aliinuka na kupiga hatua bila kuangalia nyuma.

Kelele za kitu kikivunjika vipande vipande zilisikika nyuma yake wakati akifunga mlango. Hata hivyo, haikujalisha tena.

Hatimaye Lisa aliondoka. Dakika 40 baadaye, alionekana nyumbani kwa Pamela. Akiwa kazidiwa na usingizi wa kufa mtu, Pamela alipiga miayo ya usingizi kwa mgeni ambaye hakumtarajia. “Mmegombana tena? Unapanga kukaa hapa kwa siku ngapi wakati huu?" Pamela alimpokea kwa maswali.

“Ni mbaya zaidi wakati huu, sitarudi huko tena.” Lisa alibadilisha slippers za nyumbani kabla ya kuingia.

"Unatania. Ulimtaka mwenyewe akuoe na sasa umebadilisha mawazo yako?"

Lisa alilazimisha tabasamu la uchungu. "Sio kila mpango utakupatia faida. Nitaufikiria kama uwekezaji ulioshindwa."

"Una uhakika?"

"Ndio." Lisa alijilaza kwenye kochi. Bado alionekana kutokuwa sawa. "Nimechoka. Kweli, nimechoka sana."

Pamela alikunja uso. "Una homa?"

"Ndio." Lisa alipambana na machozi yaliyokuwa yakimtoka. “Kila mtu aliliona hilo isipokuwa Alvin. Natamani pia kujaliwa na kutunzwa. Hata kama yeye ni mjomba wa Ethan, siwezi kupata heshima ya Lina ikiwa Alvin hatanipenda na kuniheshimu.”

Pamela alimtazama kwa makini na akagundua kuwa kweli amekata tamaa. Walikuwa marafiki bora kwa miaka mingi. “Hamna shida. Ninaheshimu uamuzi wako. Kwanini usikae hapa na mimi? Hata hivyo ninaishi peke yangu.”

”Sio wazo bora. Wewe na Patrick je…?” Kwa aibu, Pamela alimkodolea macho rafiki yake. “Achana naye, anaishi kwao na huwa tunaonana kwa miadi.

"Lakini mmekuwa pamoja kwa mwaka mmojana bado hamtaki kuoana."

Lisa alipepesa macho na kujibu baada ya muda. "Amekuwa na shughuli nyingi hivi karibuni tangu achukue uongozi wa kampuni ya familia yao. Tunaonana mara moja au mbili tu kwa wiki, kwa hivyo unaweza kuwa na uhakika. Nilipendekeza utafute mahali hapo awali kwa sababu Ethan alikuwa anakuja kukutafuta hapa. Lakini sasa ameacha.”

Tabasamu usoni mwa Lisa likabadilika na kuwa dhihaka kwa kutajwa kwa mtu huyo. "Nadhani anachoweza kufikiria kwa sasa ni Lina."

“Basi, ni mtu mjinga sana. Sherehe ya uchumba wake inafanyika katika siku chache. Una uhakika unataka kuhudhuria hafla hiyo?" Pamela alimtazama kwa wasiwasi.

"Ndio, lakini nitaenda kwa sababu ya sherehe ya bibi yangu kwenye siku yake ya kuzaliwa."

"Naogopa akina Masawe watajaribu kukuhadaa tena. Nasikitka sitaweza kukusindikiza kwa sababu nina mtihani chuoni siku hiyo. Lakini Patrick anahudhuria tukio hilo pia. Nitahakikisha yupo kukusaidia.”

Lisa alihisi utulivu usio wa kawaida. Hata ingekuweje, mpango wa kumtumia Alvin kama njia ya kulipiza kisasi ulikuwa umekwama! Alikuwa amepata amani na hilo hatimaye. Alikuwa karibu kupoteza maisha hapo awali na heshima yake ilikuwa imekanyagwa. Hakuna kitu ambacho kingeweza kumtisha tena.
Pamoja na hayo, ilimbidi atafute njia ya kumlipa Alvin haraka.

TUKUTANE KURASA 46-50

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.....LISA
KURASA.....46-50
SURA YA 46

Siku iliyofuata, bosi wake, Joseph Ruta, alirudi kutoka katika safari yake ya kikazi nje ya nchi. Lisa alimfuata ofisini akiwa na ombi maalum. “Je, inawezekana kuomba malipo ya awali ya mshahara wa mwezi huu? Ninadaiwa pesa na watu…” alisema kwa sauti ya chini, kwa aibu.

“Hakuna jambo kubwa. Unadaiwa kiasi gani? Niambie kiasi hicho na nitakutumia pesa mara moja.” Joseph alimwambia Lisa. “ Bw. Mushi anaendelea kupongeza uwezo wako. Ninaweza pia kukulipa mapema juu ya mradi wa Mbezi Beach." Akatoa simu yake. "Je, Shilingi milioni ishirini zinatosha?"

Hilo lilimshangaza sana Lisa. "Hapana, hapana, milioni tano zinatosha."
Bado alikuwa na bahasha nzito aliyopokea kutoka kwa mzee Harrison, pamoja na ile aliyopewa na Kelvin jana yake mchana. Alipanga kumlipa Alvin ziada kidogo endapo angetaka kupiga hesabu.

“Usionekane umezidiwa sana. Mradi wa Mbezi Beach wa Bw. Mushi unagharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano. Kamisheni yako juu ya hili ni zaidi ya milioni hamsini kwa haraka haraka." Joseph alihamisha milioni ishirini kwenye akaunti ya Lisa mara moja. “Endelea kufanya kazi hiyo nzuri,” Joseph alisema ili kumtia moyo.

Lisa aliguswa sana. Aliamua kwamba aangeendelea kuzingatia kazi yake kwa moyo wake wote na kuachana na mawazo ya Alvin.


•••
Tangu Lisa aondoke nyumbani kwa Alvin, Alvin alikuwa amebadilika sana. Hakuwa na raha na alikuwa mkali muda wote. Sam alikuwa akimwonea huruma na wasiwasi sana kwani hata kula hakula vizuri.

"Lisa bado hajarudi?" Sam alimuuliza.

"Sitaki kusikia jina la huyo mwanamke likitajwa masikioni mwangu." Alvin alijibu kwa dharau. Ilikuwa ni mida ya chakula na mara tu aliposikia jina la Lisa likitajwa tumbo lake lilianza kunung'unika ghafla.

Sam alikuna ncha ya pua yake. "Najua umezoea chakula chake, lakini huwezi kujiua kwa njaa kwa kuwa ameondoka."

"Sivyo," Alvin alijibu, akionekana kukasirika. "Hatimaye naweza kujiweka sawa sasa kwa kuwa ameondoka."

Jasho lilitokeza kwenye paji la uso la Sam. Hakuwa amegundua upande huu wa rafiki yake hapo awali. Ghafla alimshangaa Lisa kwa kuweza kuishi na mwanaume huyo kwa muda mrefu. Angekuwa ni yeye angepandwa wazimu baada ya siku chache.

“Kesho ni sherehe ya uchumba ya Lina na Ethan. Lisa labda atakuwa huko pia. Familia ya Masawe ilinitumia mwaliko pia. Je! niende na… nimshawishi?”

Alvin alimgeuzia macho Sam na kumuuliza. "Nilidhani ni sherehe ya kuzaliwa kwa Bibi Masawe wa miaka 80?"

"Sijawahi kusikia hivyo." Sam akatikisa kichwa.

Uso wa Alvin ulionekana mzito. Ilionekana kuwa familia ya Masawe haikupanga kusherehekea siku ya kuzaliwa ya bibi kizee huyo hata kidogo, sasa Lisa alipanga kwenda huko kufanya nini? Mwanamke mjinga huyo. Je, hakuogopa kuonewa tena na watu hao? Alvin alijiwazia hayo na punde akaona bora aachane nayo.

"Hakuna maana kufanya hivyo. Huu ni ujanja wake mwingine tu. Ngoja uone. Nina hakika atakuja na kuniomba msamaha kabla ya uchumba.” Alvin alimhakikishia Sam.

Baada ya sekunde chache, alipokea ujumbe mfupi kwenye WhatsApp kutoka kwa Lisa .
"Angalia, inakuja." Akabonyeza ujumbe huo kuona Lisa amefanya uhamisho mara tatu na kuweka shilingi milioni sita kwenye akaunti yake. Uso wa Alvin uliganda.

Sam alisogea mbele kidogo ili kuibia. Akiwa amechanganyikiwa, alisema, “Anatumia pesa nyingi kukuvuta tena.”

"Ndio." Uchangamfu wa Alvin ulirejea kidogo. “Ni lazima itakuwa moja ya mbinu zake nyingine.”

Status ilionyesha bado Lisa anaandika. Alisubiri kuona angesema nini. Sekunde 20 baadaye, Alvin alipokea ujumbe mwingine wa maandishi. [Milioni sita zinajumuisha gharama za hospitali hapo awali. Nina hakika ni zaidi ya inavyotakiwa lakini ninahisi fadhili leo.]

Tabasamu la fumbo lilienea kwenye uso wa Alvin. “Naam, vizuri. Mwanamke huyu ana ujasiri wa simba.” Alijiwazia Alvin.

Sam, ambaye alikuwa ameibia mtazamo wa ujumbe huo, alisema. “Hii lazima iwe mbinu ya kuvutia umakini wako. Sio tu kwamba anajaribu kukuhonga pesa bali angalia jina lake la mtumiaji-Alvlisa,."

Alvin alijisikia vizuri zaidi aliposikia hivyo na akafunua tabasamu la kejeli. "Kwa hiyo? Haijalishi tena. Hata kama atapiga magoti mbele yangu na kuomba kwa usiku tatu…” Hata hivyo, kabla hajamaliza sentensi hiyo, Lisa alibadilisha jina lake la mtumiaji la WhatsApp na kuwa 'Mwanzo Mpya'. Alibadilisha hata status yake kuwa: [Nataka tu kujali mambo yangu kuanzia sasa na kuendelea.]

Macho mazito na meusi ya Alvin yalichuruzika kwa jazba. Aliiweka simu yake pembeni, na punde si punde, uso wake ukabadirika. "Usimtaje mtu huyu mbele yangu tena." Kisha, akaondoka kwa hasira. Sam alishindwa kabisa kusema chochote.
•••
Lisa aliingiwa na wasiwasi baada ya kutuma ujumbe huo wa kejeli. Hata hivyo, pamoja na kumsaidia, Alvin alikuwa amemdhalilisha sana kwa siku za karibuni na alihisi anahitaji kujisimamia yeye mwenyewe.
Hata hivyo, baada ya kutopata jibu lolote kutoka kwa Alvin, alihisi kana kwamba mzigo huo mzito umeondolewa kifuani mwake. Hatimaye, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na deni kwa mwenzake tena.

Simu yake ilitetemeka ghafla. Kulikuwa na maandishi mapya ya WhatsApp. Alinyanyua simu akidhani ni Alvin, kumbe ujumbe ulitoka kwa Kelvin. [Ni vizuri kuwa na mwanzo mpya. Mwanamke anahitaji kujitendea vizuri zaidi. Ikiwa huna furaha na maisha, sio kwa sababu hautoshi. Baadhi ya watu au mambo fulani hayafai kuthaminiwa.]

Lisa alihisi kizunguzungu moyoni mwake. Alihisi matumaini zaidi kuhusu wakati ujao aliposoma ujumbe huo wenye kutia moyo. Hata hivyo, aliona ni ajabu sana kwani ilionekana kana kwamba Kelvin alijua alikuwa ameachwa.

Mbali na hilo, alikuwa amebadilisha status yake sekunde chache tu zilizopita. Je, Kelvin alikuwa akimfuatilia zaidi kwenye mitandao yake ya kijamii? Baada ya kufikiria hili kwa ufupi, alijibu: [Asante kwa kitia-moyo]

Hata kama Kelvin alikuwa amependezwa naye kweli, Lisa hakuwa na mpango tena wa kuwa na mpenzi. Mahusiano yake yote ya awali yalikuwa yamemuumiza sana. Isitoshe, hakuwa hata na talaka bado.

SURA YA 47

Zilkuwa zimebaki siku chache tu kufikia siku ya kuzaliwa kwa bibi yake Lisa, Bibi Masawe. Siku hiyo pia ndiyo ingekuwa sherehe ya uchumba kati ya Lina Jones na Ethan Lowe. Sherehe zote mbili zilifanyika kwa pamoja katika hoteli ya nyota saba ya ‘Heavens On Earth Resort.’ Ni matajiri tu ndiyo wangeweza kufanya sherehe katika hoteli hiyo.

Siku ya sherehe hiyo, familia ya Masawe na familia ya Lowe walikuwa wametumia kiasi kikubwa sana cha pesa kukodisha ‘The Paradise Hall’, ukumbi wa kifahari zaidi wa sherehe unaopatikana katika hoteli hiyo.

Lisa alikuwa amesimama kwenye mlango wa ukumbi huo akiwa na kadi ya mwaliko mikononi mwake. Hakuweza kujizuia kuachia machozi ya huzuni machoni mwake. Wakati fulani huko nyuma kabla Lina hajarudi, Jones Masawe aliahidi kupanga harusi yake na Ethan katika hoteli hiyo hiyo na kwenye ukumbi huo huo. Kweli, sherehe ya uchumba ilikuwa ikifanyika na Ethan bado alikuwa bwana harusi. Lakini, aliyebadilika ni chumba wa kike, baala ya Lisa, alikuwa ni dada yake, Lina!

Lisa aliingia kwenye ukumbi wa sherehe, akiwa amevalia nguo ile nyeupe aliyovaa kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Mzee Harrison mara ya mwisho. Kundi la waandishi wa habari lilikuwa likingoja mlangoni kwa ajili ya kuripoti matukio ya sherehe hiyo ya familia hizo mbili maarufu. Waandishi walimvizia Lisa na kumrushia maswali mfululizo.

“Bi Lisa, si ulidai familia ya akina Masawe ilikufungia na kukutesa? Kwa nini bado uko hapa kuhudhuria sherehe ya uchumba ya Lina na Ethan?”

'Je, ni kwa sababu akina Masawe hawakukutendea vibaya hata kidogo? Je! kila kitu kilikuwa ni uzushi wa mawazo yako mwenyewe?"

Lisa hakuwa mjinga. Alijua mara moja kwamba waandishi walikuwa wamepangwa na familia ya Masawe. Bila shaka walikuwa wamehongwa na kuelekezwa cha kusema. Alitarajia jambo hili litokee, hivyo akaitikia kwa utulivu. "Leo ni siku ya kuzaliwa ya bibi yangu, anatimiza miaka 80. Nipo hapa kusherehekea pamoja naye.”

“Kweli? Hatukusikia chochote kuhusu hilo. Tunajua tu kuwa sherehe ya leo ni ya uchumba kati ya familia ya Masawe na familia ya Lowe.”

“Lisa, mavazi uliyovaa ni ya kuvutia. Ikiwa sijakosea, ni mavazi ya toleo la kipekee kutoka kwa mkusanyiko wa msimu wa joto wa brand ya kifahari. Si ulisema akina Masawe walikutendea vibaya sana, sasa umewezaje kumudu vazi la gharama kiasi hiki?”

Tabasamu la kejeli lilienea usoni mwa Lina kabla hajauliza. "Sawa, familia ya Masawe imekulipa kiasi gani ili kuniaibisha leo?"

“Haya siyo majibu mazuri. Wewe ni tofauti sana na Lina ingawa nyote wawili mnatoka katika familia moja.”

“Hakika! Lina hata alituletea juisi na soda mapema. Umelelewa na wanandoa wa Masawe tangu kuzaliwa lakini adabu yako haiendani na familia hiyo.” Waandishi walizidi kumshambulia Lisa.

Lisa alikodoa macho. Kijana mtanashati aliyevalia suti ya kijivu alikuja kumuokoa. Vitisho vikali vilionekana katika sauti yake. "Leo ni siku muhimu kwa familia ya Masawe na Lowe. Wageni wengi wa heshima watajitokeza kwenye tukio hili, akiwemo Cindy Tambwe. Hata hivyo kundi hili la mapaparazi limemvizia msichana dhaifu ili kumwaibisha. Je, yeye ni msanii au mtu maarufu mtandaoni? Kwa kuwa mnapenda sana kumhoji, kwa nini msimhoji kwa mazuri?”

Waandishi wa habari walitawanyika polepole, na kicheko cha kicheko kikatoka kwenye midomo ya Lisa .

"Asante sana, Bw. Patrick Jackson. Umekuwa tofauti baada ya kuchukua nafasi ya ukurugenzi katika kampuni yenu. Si ajabu rafiki yangu Pamela anaanguka kichwa chini kwa ajili yako.” Lisa alimpa sifa za shukrani mtu huyo, mpenzi wa Pamela, Patrick Jackson aliyemwokoa kutoka kwa mapaparazi.

"Acha wewe. Pamela amekuwa akinipigia simu tangu jana usiku ili kuhakikisha nakulinda kwa lolote. Twende,” alisema huku akitabasamu.

Lisa alikuwa karibu kuitikia kwa kichwa wakati mwanamke mrembo aliyevalia mavazi ya manjano angavu alisonga mbele ya mwanamume huyo kwa miguu yenye viatu vya visigino virefu ili kumshika mkono. “Patrick unatembea haraka sana na siwezi kukupata. Karibu nianguke sasa hivi.”

Lisa alimtazama mwanamke huyo. "Huyu ni Linda Sheba kutoka kwa familia ya Sheba. Pia amealikwa kwenye sherehe ya uchumba usiku huu,” Patrick alimtambulisha Linda kwa Lisa.

"Loo," Lisa akadakia, akielekeza macho yake kwa mwanamke huyo na kumpa mkono wa salamu. Alicheka na kuongea ki-nusu-utani. “Nilishtuka sana kumuona akijibebisha kwako. Nilidhani ndiye mpinzani wa Pamela."

Patrick akashtuka akamtazama Linda aliyekuwa kamuegemea kichwa chake kwenye bega lake, akamtoa taratibu na kumwambia Linda kwa uchungu, “Linny, nilikuambia hivyo mara nyingi hatuwezi kuishi kama tulipokuwa wadogo tena. Watu wengine wanaweza kutufikiria vingine.”

“Nimezoea. Isitoshe, baada ya kuja hapa, kwa kawaida ninakuona kama mwenza wangu kwa usiku huu.” Linda alitoa ulimi kwa kucheza kabla ya kumwambia Lisa , “Haya, mimi ni rafiki wa Pamela pia na huwa tunabarizi kila wakati. Nitasikitika ikiwa utaathiri uhusiano wao kwa kumpelekea maneno yasiyo sahihi.”

"Ni sawa, Lisa hajasema chochote kibaya." Patrick akampigapiga Linda kichwani. “Twendeni tukaketi.”

Wote watatu walianza kutembea kuelekea kwenye ukumbi wa sherehe kwa pamoja. Lisa alimtazama kwa haraka Linda kwa pembe ya macho yake. Kwa sababu fulani, alimtilia mashaka yule binti. Msichana huyo hakika alikuwa na nia ya siri.

Tangu Lina alipomwibia Ethan, Lisa alihisi kana kwamba alikuwa amesitawisha uwezo wa pekee ambao ungeweza kuchanganua kwa usahihi utu wa mwanamke. Isitoshe, mwanaume anawezaje kuwa na urafiki wa karibu hivyo na mwanamke mwingine mbali na mpenzi wake? Hii bila shaka haikuwa ishara nzuri.

Wakati huohuo, Jones Masawe na mkewe walimwona Lisa kwa mbali na kumpa ishara kwa tabasamu. Lisa hakutaka kuona sura zao bali alitembea kuelekea kwao hata hivyo kwa sababu ya bibi yake.

Bila kutarajia, ghafla Mama Masawe alimkumbatia karibu na kuzungumza kwa upendo. “Bw. Chande, huyu ni binti yangu mwingine kipenzi, Lisa. Yeye sio jasiri tu, bali pia mkarimu na mwadilifu. Si muda mrefu uliopita, hata alishirikiana na polisi kama wakala wa siri ili kuangusha kikundi kinachotengeneza video haramu. Dada yake ataolewa hivi karibuni lakini yeye bado hajapata mchumba. Je, huna mtoto wa kiume mdogo…”

Msururu wa hisia ulipita usoni mwa huyo mzee Chande. Kwa kiasi fulani video iliyomwonyesha Lisa akiwa karibu kubakwa na Zakayo kabla hajaokolewa na Alvin ilikuwa imesambaa kwa watu wengi na kuathiri sana sifa yake. Hakuna familia ambayo ingethubutu kumchukua tena.

"Oh, sawa, anaonekana kama msichana mzuri. Nasikitika mwanangu mdogo tayari yuko kwenye uhusiano. Huyo, si Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari? Imekuwa muda mrefu…ngoja nionane naye mara moja.” Mzee Chande alitoa udhuru na kuondoka haraka.

Jones Masawe alisema kwa kukata tamaa, “Usijali, Lisa . Nitakutafutia mume mwema leo.” Lisa alichukia sana kwa maigizo aliyoyaona yakifanywa na wazazi wake. Tayari alikuwa amekata tamaa kwa wanandoa hawa.

“Mnaweza kuacha kujifanya sasa. Ninyi ndio mliopanga waandishi wa habari mlango kwa ajili yangu, na sasa, maneno yanawatoka kana kwamba sisi ni familia yenye furaha. Hakuna haja ya kuendelea kuigiza. Niko hapa tu leo kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Bibi. Sipendezwi na kitu kingine chochote.”

Mama Masawe alipunguza hasira yake na kusema taratibuo, “Lisa mwanangu, ni nini kilikupata hata ukakosa moyo kiasi hicho? Haijalishi ni nini, tumekulea tangu kuzaliwa kwako na tulitumia muda mwingi na bidii kukuelimisha. Ni jambo moja kwamba hutambui makosa yako lakini hata unatudharirisha hadharani? Je, dhamiri yako imekuacha? Mbali na matatizo yako na Lina, je kuna kitu kingine tulichokukosea? Tulikupeleka katika nyumba ya zamani pia kwa faida yako mwenyewe!”

“Umesema kweli, sina sababu ya kuwachukia. Nyinyi wawili mlinileta katika ulimwengu huu, lakini hiyo haimaanishi kuwa nanyi mnaweza kuchukua uhai wangu pia!” Lisa alicheka kwa hasira.

Jones alipiga kelele, “Tangu lini tukataka kuchukua uhai wako? Kulikuwa na kila kitu kwenye ile nyumba ya Moshi, kila kitu cha msingi kilikuwepo. Na ile nyumba haijawahi kukatika maji wala umeme, sasa nilishangaa kusikia kuwa nilikuwa nimekukataza kula au kupata maji.”

Jambo hilo lilimshangaza sana Lisa. Ina maana bibi kizee alikuwa ni mpango wa nani? "Lakini yule bibi mzee… " Kabla hata hajauliza swali lake, sauti kali ilimkatisha ghafla.

SURA YA 48

“Lisa , umeikuja kweli!" Sauti ya Lina ya mshangao ikajaa chumbani.
Kabla Lisa hajajibu, Lina alimshika kwa mkono wake wa kushoto na kuunganisha na mkono wake wa kulia na wa mama yao. “Vipi mkuu! Hatimaye familia yetu imekamilika.”

Lisa aliinua mkono wake aliokuwa ameushika Lisa na kusema kwa ukali, “Tafadhali sogeza mkono wako mbali. Sitaki mazoea na wewe!”

“Lisa , unamaanisha nini?” Sura ya aibu ilisambaa kwenye uso mzuri wa Lina. Haraka haraka akamshika Ethan mkono na kumsihi kwa upole. “Ethan, zungumza na Lisa . Tumealika wageni wengi leo na ni muhimu familia yetu iwe na amani kati yetu.”

Ethan alifikiri Lisa alimaanisha kuzua matatizo tena hivyo akamwangalia kwa makini. Lakini, katika sekunde iliyofuata alishtushwa kabisa na mvuto wa Lisa.
Lisa alikuwa amevaa nguo ndefu nyeupe. Nywele zake nzuri zilikuwa katika hali ya kawaida lakini maridadi. Alionekana kuvutia sana.

Lina alionekana mrembo pia, lakini ilikuwa hasa kwa sababu ya mapambo na mapodozi yake. Hakuweza kulinganishwa na uzuri wa asili wa Lisa hata kwa tabaka nene za mapambo. Ikiwa sio kwa kila kitu kilichotokea huko nyuma, Lisa angekuwa mtu ambaye alikuwa akimchumbia siku hiyo.

Uchungu mwingi ulimkumba Lina baada ya kumuona Ethan akimtazama Lisa kwa butwaa. Alisema tu kwa lengo la kumshtua Ethan. "Lisa unaonekana mrembo leo. Natumai ulitumia masaa mengi kujiandaa kwa usiku wa leo. Tazama, kila mtu hawezi kuacha kukutazama.” Aibu ilitanda kwenye uso mzuri wa Ethan huku akirudisha macho yake mara moja.

Mama Masawe alichukizwa na hali hiyo. "Lisa , nimekualika hapa leo ili kutoa baraka zako, sio kuwa kivutio cha sherehe. Leo ni siku kuu kwa dada yako.”

Bila kukawia, Lisa alijibu kwa huzuni, “Samahani kwa hilo lakini halikuwa kosa langu kupendeza, ilinichukua dakika kumi tu kujiandaa. Yote inakuja kwa sababu ya uzuri wangu wa asili. Sipaswi kulaumiwa kwa kuzaliwa mrembo kuliko yeye. Hata hivyo si mimi niliyemzaa.”

“Wewe…” Mama Masawe hakupata neno la kumfaa Lisa kutokana na maneno yake ya kejeli.

Lisa aligeuka kumwangalia Lina kabla ya kucheka tena. “Una wivu wa siri kwamba mimi ni mrembo kuliko wewe, sivyo? Sema moja kwa moja badala ya kujaribu kutupa vidokezo vya hila kushoto na kulia wakati wote.”

“Lisa sivyo namaanisha. Ninakupongeza kwa dhati." Machozi ya huzuni yalikuwa yakibubujika taratibu machoni mwa Lina.

Ethan hakuweza tena kuvumilia. “Lisa umetosha? Wewe pekee ndiye uliyekuwa mkali kwa Lina tangu mwanzo.”

"Hapo sasa, kuna mtu anajitokeza kukulinda, raha iliyoje?" Lisa aliongea kwa tabasamu la kejeli. Ethan alitoa macho kwa hasira.

Hatimaye Johes Masawe alizungumza, “Sawa, bado tuna wageni wanaingia. Lisa nenda kwenye chumba cha faragha ukamwangalie bibi yako. Utarudi tena sherehe itakapoanza."

“Nitaondoka baada ya kumuona bibi, sina shida na sherehe hii.” Lisa alijibu kwa jeuri kama kawaida.

“Itabidi umlishe chakula baadaye.” Jones akamkatisha kwa kukosa subira, “Bibi yako alipooza baada ya kuanguka muda mfupi uliopita. Hawezi hata kujilisha mwenyewe sasa hivi.”

Habari hizi ziliulipua moyo wa Lisa kama bomu. Hakuamini alichokisikia. Ilikuwa imepita mwezi mmoja tu tangu amtembelee bibi yake mara ya mwisho na alikuwa mzima. Hili lingewezaje kutokea? “Mbona unaniambia vitu vya ajabu?!” Lisa aliuliza kwa mshangao.

“Nenda, hutufai hapa. Hakuna kingine unaweza kufanya mbali na kutukasirisha tu”

Lisa aliondoka kwa haraka kuelekea chumba cha faragha. Bibi kizee mwenye mvi alikuwa ameketi kwenye kiti cha magurudumu, akitazama dirishani bila mwelekeo. Mwanamke mwingine karibu naye alikuwa akimnywesha maji.

Machozi yalitiririka mashavuni mwake. "Samahani bibi, nimekuja kukuona sasa hivi." Hakuwa amemtembelea kwa siku chache zilizopita ili kuepusha kumfanya bibi yake kuwa na wasiwasi.

Mbali na babu yake ambaye alikuwa ameaga dunia, bibi yake ndiye pekee aliyesalia katika familia ya akina Masawe ambaye alimtendea mema tangu akiwa mdogo. Tangu alipokuwa msichana mdogo, Jones Masawe na mkewe walikuwa wakimkalipia bila hata sababu. Bibi yake ndiye pekee aliyempenda kwa dhati bila masharti. Hata hivyo, alipoondoka kutafuta elimu zaidi nje ya nchi, bibi yake huyo alirudi Moshi.

"Bibi Masawe kwa kiasi fulani ni kiziwi sasa, kwa hivyo hasikii vizuri," mwanamke aliyekuwa akimhudumia alisema.

“Na wewe ni…” Lisa hakumtambua mwanamke huyu. Shangazi Manka ndiye alikuwa daima mlezi wa bibi yake.

"Familia ya Masawe waliniajiri kumtunza Bibi Masawe. Unaweza kuniita Shangazi Helen.” Alijitambulisha yule mwanamke.

“Lakini vipi kuhusu Shangazi Manka?”

"Inavyoonekana, aliona shida kumtunza Bibi Masawe baada ya kupooza na akajiuzulu." Alijibu Helen

Jambo hilo lilimshangaza Lisa. Manka alikuwa amemtunza bibi yake kwa zaidi ya miaka 30 na wote wawili walikuwa wamejenga uhusiano mzuri. Bibi Masawe alimhitaji zaidi kwa kipindi hicho, kwa hiyo ilionekana kuwa haiwezekani kwamba angeondoka wakati huo. Labda Manka alikuwa akizeeka naye na kazi hiyo ilikuwa imemchosha. Alisikitika sana kufikiria hali ya bibi yake. Alipiga magoti mbele ya yule mzee na kuushika mkono wake. “Bibi, mimi ni Lisa, niko hapa kukuona.”

Bibi Masawe alimtazama kwa mshangao kabla ya kufunua tabasamu alilolifahamu. “Ni wewe, Sheryl. Umekuwa nje siku nzima tena? Haraka ubadilishwe nguo safi. Baba yako anatupeleka out kwa chakula cha jioni.”

Lisa alipigwa na butwaa kwa muda mfupi baada ya kusikia hivyo. Sheryl alikuwa shangazi yake, lakini alikuwa ameaga dunia zaidi ya miaka 20 iliyopita.

“Bibi, umem’miss tena Shangazi Sheryl?” Bibi Masawe hakuonekana kumuelewa na kuanza kunung'unika bila mpangilio. Lisa aliketi karibu na bibi kizee huyo akihisi kukata tamaa.

Karibu saa 12 jioni, Jones alitokea tena chumbani. "Mlete bibi yako nje kwa chakula."

"Naweza tu kumlisha humuhumu ndani kutokana na hali yake." Alihisi kuudhika kumtazama baba yake usoni.

"Sijakupa chaguo. Lazima utoke naye huko nje sasa hivi ili kula chakula cha amani na familia yetu. Vinginevyo, sitakuruhusu kuonana na bibi yako tena,” Jones aliagiza.

Lisa hakujua Jones alikuwa na maana gani. Alikuwa amesema maneno 'familia yetu'. Ilionekana kwamba alikuwa ameamua kumtenga kabisa na familia.

“Sawa, nitamleta.”

SURA YA 49

Lisa alimsukuma Bibi Masawe, aliyekuwa kwenye kiti cha magurudumu kutoka nje ya chumba hicho na kuelekea kwenye ukumbi wa sherehe. Waliekezwa kuketi kwenye meza moja na wanandoa waliokuwa wakichumbiana, Lina na Ethan.

Baada ya kuketi, alimuona Kelvin Mushi akiwa ameketi kwenye meza kuu nyingine iliyotengwa kwa ajili ya jamaa wa karibu. Sura ya kuchanganyikiwa ilienea usoni mwa Lisa. Hapo mwanzo Kelvin alimwambia kuwa ni ndugu wa mbali kwa familia hizi zote mbili lakini kwanini alikuwa amekaa pamoja na Jones Masawe na Bibi Masawe?

Kingine kilichomshangaza Lisa ni kuhusu Alvin. Kwanini hakuhudhuria sherehe hiyo ingawa alikuwa mjomba wa Ethan? Kinyume chake, Janet Kileo na Cindy Tambwe, ambao walikuwa ni marafiki wa kudandia tu wa Lina, walijitokeza. Lisa alicheka kwa ndani. Hakika Lina alikuwa amejitolea kujenga uhusiano wa kinafiki na watu ambao hakuwapenda.

Sherehe ya uchumba ilianza saa kumi na mbili na nusu jioni. Emcee wa shughuli alipanda jukwaani kumshukuru kila mtu kwa uwepo wake. Hatimaye, Ethan na Lina walialikwa kwenye jukwaa. Lina aliyekuwa amevalia nguo nyekundu alisimama karibu na Ethan aliyekuwa amevalia suti nyeusi. Wawili hao walionekana wakamilifu pamoja.

Wageni walianza kutoa maoni juu ya wanandoa. "Nilisikia kwamba binti wa kwanza wa Masawe, Lina amekulia kijijini ilhali yeye ni mrembo na mwenye utulivu. Si ajabu kwamba Ethan amemwangukia.”

“Kulikuwa na uvumi mwaka jana kwamba Ethan angechumbiana na Lisa. Hakika ningemchagua Lina pia kama ningekuwa katika viatu vyake. Utu mzuri hushinda zaidi ya yote."

“Uko sawa.”

Kelele hizo zilipita masikioni mwa Lisa kama dhoruba za upepo, lakini aliamua kuzipuuza na badala yake akazingatia kumlisha bibi yake. Kilichomuumiza zaidi Lisa ni baada ya Cindy, ambaye alikuwa ni rafiki yake wa zamani, kupanda jukwaani kukabidhi pete za uchumba.

Cindy alisema kwa mzaha kwenye kipaza sauti, “Kwa kweli, nimemjua Ethan kwa takriban miaka saba au minane sasa na ni kama kaka mkubwa kwangu. Wasichana wengi walikuwa wakimfuata nyuma katika shule ya sekondari lakini hakuna hata mmoja wao aliyemvutia macho. Nilifikiri hakuna mtu angewahi, hadi alipokutana na Lina na kumkubali mara ya kwanza.” Akamtupia macho Lisa . “Lisa , utaungana nami na kuwapa salamu zako, sivyo?”

Lisa aliweza kuhisi kejeli katika kila neno lake. Cindy asingeweza kujuana na Ethan kama Lisa asingalikuwa rafiki yake. Rafiki yake wa zamani sasa alikuwa akimpongeza mpenzi wake wa zamani kwa ndoa yenye furaha. Je, hii inaweza kuwa kejeli kiasi gani?

“Oh, hakika.” Lisa aliinua glasi yake taratibu huku tabasamu la ajabu likienea usoni mwake. "Nimegundua hakuna mtu anayeweza kukosa aibu kuliko ninyi watatu." Lisa alikohoa kidogo kama anayejiweka sawa kwa jambo furani kisha akasema. “Naomba kwanza tushuhudie hadithi ya mapenzi ya hawa wachumba. Tafadhali elekezeni macho yenu kwenye skrini, " Lisa alisema.

DJ aliweka wimbo mzuri wa kimahaba. Lakini, onyesho la picha kwenye screen lilikuwa linaonyesha picha za Lisa na Ethan. Baadhi ya picha zilichukuliwa walipokuwa watoto wadogo. Chache kati ya picha hizo zilimwonyesha Ethan alipokuwa amesafiri maili nyingi kuvuka anga na bahari ili kumtembelea Lisa alipokuwa akisoma nje ya nchi. Walionekana wenye furaha sana kwenye picha.

Ni wazi kwamba wageni waalikwa katika ukumbi wa sherehe walishtuka.
Familia za Lowe na Masawe hazikufurahishwa. Jones alipiga meza na kuinuka haraka. “Upuuzi gani huu? Zima mara moja.”

Mara moja skrini ilifungwa, lakini sekunde chache za kuonekana picha zile zilitosha kusababisha ghasia kati ya wageni.

“Nini kinaendelea? Je, Lisa na Ethan walikuwa pamoja hapo awali?”

“Nani alifanya hivi? Inaweza kuwa Lisa?"

"Pengine. Nilifikiri alikuwa anafanya mambo ya ajabu tangu alipoingia ndani.”

Lisa alikunja uso kidogo kama alikuwa na machale kwamba kitu mbaya ilikuwa karibu kutokea. Lisa hakuhusika na chochote juu ya jambo hilo lakini ni wazi, mtu fulani alikuwa akijaribu kumseti. Mtu pekee ambaye angeweza kufanya haya yote labda alikuwa Lina! Mwanamke huyo kweli alitoa sadaka sherehe yake ya uchumba kwa sababu ya kumdhalilisha Lisa? Ukatili ulioje!

"Ni nani aliyefanya hivi?!" Mama Masawe alipiga kelele kwa hasira.

Fundi mitambo akasonga mbele haraka. “Mama Masawe, samahani sana. Tuligundua kuwa memory card imebadilishwa.

"Nani amefanya kitu kibaya kama hiki?!" Sonya, mama yake Ethan naye alipiga kelele.

Cindy alijibu mara moja, "Shangazi Sonya, ni dhahiri kwamba kuna mtu anajaribu kuharibu sherehe."

"Hiyo ni sawa. Lazima tujue ni nani yuko nyuma ya hili!” Sonya alisisitiza.

Wakati huo huo, Aunty Helen, ambaye alikuwa akimtunza Bibi Masawe, alisimama kwa woga na kugugumia, “Nilimwona Lisa akiingia kwa siri mapema kwenye chumba cha mitambo.”

Lisa alishtuka ghafla akaelewa kitu. Alikaa kimya, lakini Jones tayari alikuwa akimtazama kwa hasira. “Hivi ulikuwa unafanya nini?”

Lina alionekana akiwa amepauka kama karatasi. "Lisa , sikuzuii kunidharirisha nyumbani lakini unawezaje kunidharirisha hivi hadharani?"

Mama Masawe alikubaliana na Lina, "Umevuka mipaka wakati huu. Huwezi kudhibiti hisia za mtu. Ethan amekuwa akikuchukulia kama dada yake mdogo tangu utoto.”

Mara moja, Sonya akasogea mbele kueleza hali hiyo. "Tafadhali msiichukulie hii vibaya wageni waalikwa. Ethan na Lisa walikua pamoja tangu wadogo na amekuwa akimpenda kama dada mdogo. Lakini, mapenzi ni makubaliano ya wawili, huwezi kubadili hisia za mwenzako kama hakutaki. Si hivyo, Ethan?”

Ethan bila fahamu alimgeukia Lisa. “Samahani Lisa, nilikosea kukukosesha nia yangu. Kweli nilikuwaga nakuona wewe kama dada mdogo. Tulichonacho si mapenzi ya kimahaba.”

Baada ya kusema hivyo, aliona Lisa akichezea pembe za midomo yake na kutabasamu. Kulikuwa na utulivu na kejeli machoni pake. Alihisi moyo wake ukirukaruka. Hakuwahi kuwa na aibu hivi hapo awali.

Kwa hasira, Jones Masawe alimnyooshea kidole Lisa na kusema kwa sauti kubwa, “Muombe radhi dada yako mara moja la sivyo sitakutambua kuwa wewe ni binti yangu!”

Lisa alitabasamu na kupiga makofi taratibu huku akinyanyuka kuelekea jukwaani. Alinyakua kipaza sauti kutoka kwenye mikono ya MC na kusema. “Ni onyesho la ajabu kama nini! Kwa kweli siwezi kujua ni nani aliyepanga hii. Alikuwa Mzee Masawe? Mama Masawe? Au labda binti kipenzi wa familia ya Masawe, Lina…”

"Unaongea ujinga gani?" Jones alikimbilia mbele kunyakua kipaza sauti lakini Lisa akaruka haraka hadi kwenye meza ambayo Kelvin alikuwa ameketi.

Lisa alisema kwa sauti kwenye maiki. “Mzee Masawe, mbona unaogopa ninachotaka kusema? Ulinilazimisha kuhudhuria sherehe hii kwa kutumia kisingizio kwamba ni siku ya kuzaliwa Bibi yangu ya miaka 80, ili tu kudhibitisha kwa jamii kwamba familia ya Masawe inanijali! Ili tu uweze kukomboa sifa ya kampuni ya Kibo Group!”

Watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza. Lisa akaendelea. Niliitika wito kwa heshima ya bibi na kujitokeza, lakini inaonekana kama umesahau kuwa kuna kumbukumbu ya kuzaliwa mama yako. Mama yako amerukwa na akili na kupooza, hata hivyo hukumtaja hata sekunde moja katika sherehe nzima. Wewe ni mtoto wake wa aina gani?”

Uso wa Jones Masawe ulikuwa umetapakaa kwa hasira na aibu. “Ninazungumzia suala la wewe kuharibu sherehe ya uchumba, kwa hivyo acha kujaribu kugeuza mawazo. Nitataja siku ya kuzaliwa ya bibi yako baada ya hili."

“Hakika, turudi kwenye sherehe ya uchumba basi. Kulingana na maneno ya mlezi wa bibi aliyeajiriwa hivi karibuni, unamtuhumu binti yako mwenyewe bila kusita! Je, umeangalia picha za usalama? Nimekaa chumba cha faragha na Bibi tangu nilipokanyaga mahali hapa na sikutoka hadi mapokezi yalipoanza. Ninaamini hoteli ya kifahari ya nyota saba kama hii itakuwa na kamera nyingi za usalama zilizowekwa." Lisa alisema kwa kujiamini. "Ikiwa picha za usalama zitaonyesha kuwa nimekuwa ndani ya chumba cha mitambo, licha ya kuomba msamaha, nitaomba radi ishuke na kunipasua vipandevipande"

"Labda ulimwagiza mtu mwingine kuifanya." Cindy aliropoka.

“Lakini Shangazi Helen alidai kuniona mimi mwenyewe nikiingia kwenye chumba cha mitambo. Je, hilo si jambo linalopingana?” Lisa alimsuta.

Wageni walikuwa wakipata ufahamu bora na picha kamili sasa. Kelvin alikunja midomo yake kwa tabasamu hafifu kabla ya kupendekeza kwa upole, “Ikiwa ni hivyo, hebu tukague picha za usalama. Hata hivyo haitachukua muda mrefu.”

Sura ya hofu ilitanda usoni mwa Helen.

SURA YA50

Akiachwa bila njia mbadala, Lina alisema, “Pengine hii yote ni kutokuelewana. Angalau tuendelee na chakula kabla ya kuangalia picha. Nina hakika kila mtu ana njaa sasa. Zaidi ya hayo, hatupaswi kukosa wakati huo mzuri—”

“Hatuwezi kuacha mambo hewani,” Lisa alijibu kwa dhihaka, “Je, kuna yeyote kati yenu aliyezingatia hisia zangu uliponituhumu kwa hilo?”

"Inatosha! Tumependekeza tukague picha baadaye. Unataka nini tena?” Ethan alifoka kwa sauti ya chini huku akimtazama Lisa aliyesimama juu ya meza. “Unataka wazee wakuombe msamaha mmoja baada ya mwingine?”

"Nyamaza!" Lisa alifoka kwa sauti. "Majuto yangu makubwa ni kuangukia kwenye ulaghai wako! Ulisema unanichukulia kama dada mdogo. Ukweli ni kwamba, sisi wawili tumekuwa kwenye uhusiano tangu shule ya sekondari hadi miezi miwili iliyopita. Unafikiri sina uthibitisho kwa sababu nimekaa kimya? Mungu anajua ni rekodi ngapi za sauti ambazo umenitumia kwenye WhatsApp kwa miaka mingi.”

Kisha, alicheza rekodi za sauti kwenye maikrofoni. Sauti nyororo ya kubembeleza Ethan ilijaza chumba mara moja.

“Sawa, mpenzi Lisa usiwe na wazimu tena. Nitakununulia keki nikirudi nyumbani usiku wa leo sawa?

“Lisa , nimekumiss. Je, wewe hujanimiss?”

Aliendelea kucheza rekodi kadhaa za sauti baada ya hapo. Wageni wote walipigwa na butwaa. Wote walikuwa wamezungumza na mtu huyo hapo awali, kwa hiyo waliitambua sauti yake.

Tabaka nene za vipodozi juu ya Lina hazikuweza kufunika weupe wa uso wake wakati huo. Ethan naye sasa aliona aibu kabisa. Hakuwahi kuwa na hasira kama hiyo hapo awali katika maisha yake. Akasonga mbele kwa nia ya kumshika Lisa aliyekuwa amesimama juu ya meza. Wakati huo huo, mkono uliruka kutoka nje hewani ili kumzuia.

Alikuwa ni Kelvin Mushi, mjomba wake, akamtazama Ethan kwa ukali. “Tayari umewakatisha tamaa wengine. Usipoteze neema ya mwisho uliyo nayo kama mwanaume.” Lisa alitabasamu. Hakufikiri Kelvin angeangukia upande wake.

“Ethan Lowe, mwanzoni sikutaka kukuweka wazi. Tulikuwa marafiki wa kucheza utotoni, hata hivyo. Na unaweza kuwa kaka yangu mkubwa hata tusipokuwa pamoja. Hata hivyo, unatia aibu sana! Ni jambo moja kwamba ulinitupa lakini kwa nini unitupe kisha uanzishe uhusiano wako mpya na dada yangu? Wewe ni mwanaume wa aina gani?”

Lisa aliachiwa jukwaa sasa na yeye akaendlea kulitumia vyema.

“Isitoshe, ni kweli mlikutana na Lina kwa sababu ya mapenzi? Ni kwa sababu yeye ndiye mrithi wa familia ya Masawe. Uliniacha mimi uliposikia kuwa Lina ndiye mrithi wa familia ya Masawe.” Kisha akageuka na kumtazama Cindy. "Mwimbaji mkubwa Cindy Tambwe! Wakati mmoja tulikuwa marafiki bora. Je, ungemjua Ethan kama si mimi?”

“Wewe…” Cindy alikuwa akitetemeka kwa sauti sasa.

"Acha wewe. Tulikuwa marafiki wa karibu kwa miaka sita yote ya sekondari na tumepiga picha nyingi pamoja. Usinilazimishe kuthibitisha.”

Lisa alipeperusha macho yake kwa utulivu mbele ya wageni kabla ya kuwaangazia wanandoa wa Masawe. "Hakuna haja ya kuangalia picha za usalama kwa sababu familia ya Masawe haitaruhusu ifanyike hata hivyo. Sitaki kukaa kwenye sherehe hii kwa dakika moja zaidi. Kusema kweli, ninachukizwa na nyinyi wanafiki wote.” Kisha, akatupa kipaza sauti kando, akaruka kutoka kwenye meza, na kuanza kutoka nje ya ukumbi wa sherehe huku akitazamwa na kila mtu. Familia za Masawe na Lowe zilionekana kuwa na aibu sana.

Ethan alikuwa na aibu zaidi kuliko wote. Mwishowe, Zakaria Lowe, baba yake Ethan, alijitokeza na kuwatangazia wageni, “Na tuanze sherehe wakati wale vijana wanabadilisha na kupumzika ghorofani. Nadhani wamechoka pia.” Alimtupia jicho la onyo Ethan baada ya kusema hivyo kisha akatoka jukwaani na kuelekea nyuma ya jukwaa.
•••
Wasiwasi ulimtawala Lisa huku akisubiri lifti ifike. Ilibidi aondoke haraka iwezekanavyo. Alikuwa amefanya hayo yote kwa ujasiri tu kwa sababu walikuwa chini ya macho ya umma. Alikuwa mbwa mwitu pekee sasa kwenye pori la simba. Wangeweza kuja kushughulika naye bila msaada. Hata hivyo, lifti hiyo ilichukua muda mrefu kwani ilipitia zaidi ya ghorofa 30 tofauti.

"Lisa, simama hapo hapo!" Sauti ya hasira ya Ethan ilisikika nyuma yake. Alimtazama na kuona uso wake mzuri umepambwa kwa hasira kali. Hakuwahi kuona hasira hii kwake hapo awali. Hakukuwa na shaka kwamba angeweza kumshambulia.

Wakati akifikira kujinasua na hatari hiyo katika akili yake, umbo refu lilipita mbele yake kama ngao. Alikuwa ni Kelvin. “Ethan, unafanya nini?”

“Mjomba, mimi ndiye ninapaswa nikuulize swali. Hili ni suala la faragha kati yangu na Lisa, wewe haalikuhusu."

“Mjomba?” Lisa alihisi kana kwamba amepigwa na radi. Alisema nini? Je, Ethan alimuita Kelvin mjomba wake? Akili yake sasa ilikuwa imechanganyikiwa. Ikiwa Kelvin alikuwa mjomba wa Ethan, basi Alvin alikuwa nani? Oh hapana!

Kelvin alikunja uso huku akimuonya, “Simama hapohapo na ugeuke. Ni sherehe ya uchumba wako usiku wa leo. Rudi juu haraka.”

"Yeye ndiye kaharibu sherehe ya uchumba wangu." Macho ya Ethan yalijaa miale ya moto. "Sifa niliyotumia miaka mingi kuijenga iliharibiwa leo. Hukuona jinsi baba alivyonitazama kwa hasira mapema?”

“Ni yeye ndiye aliyeharibu uchumba? Unategemea Lisa angekaa kimya pamoja na nyinyi nyote kuungana kumshambulia?” Mwonekano wa kukatishwa tamaa ulitawadha usoni mwa Kelvin. “Ethan, uko sahihi kufanya kazi kwa bidii kuelekea kurithi kampuni ya Lowe Enterprises, lakini huwezi kuvuka mipaka. Yote yaliyokupata leo ni kwa sababu tu ulivuka mstari dhidi ya Lisa!” Maneno yake yalimgusa Lisa. Hakutarajia mwanaume huyu kumuelewa vizuri hivi.

Akiwa ameshtuka, Ethan alisema kwa kusitasita, “Mjomba, umemsaidia Lisa mara kadhaa leo. Kwanini? Je! ni kwa sababu wewe ni…”

Kelvin akamkatisha haraka Ethan utadhani alijua alichotaka kusema. “Nimepata fursa za kumfahamu, na kutokana na kile nilichokiona, yeye ni msichana wa tofauti sana. Ikiwa yuko tayari kunipa nafasi, anaweza hata kuwa shangazi yako mdogo siku moja.”

Lisa alikuwa karibu kupoteza akili! Ethan aliposikia hivyo alishtuka. Nani angeweza kukubali mpenzi wake wa zamani kuwa shangazi yake? Isitoshe, Ethan hakuweza kuyavumilia maumivu ya moyo kwa kumfikiria Lisa akiwa na mwanamume mwingine.

“Mjomba, nadhani umepatwa na wazimu. Baadhi ya watu si kama wanavyoonekana juu-juu—”

“Nimekuwa na uzoefu wa kitaaluma kuliko wewe na pia nina umri mkubwa zaidi yako kwa miaka michache, kwa hivyo unaweza kuacha kuniambia la kufanya," Kelvin alimkatisha Ethan kwa upole. "Zaidi ya hayo, wewe ni mwanamume wa aina gani hata ukamkashifu mpenzi wako wa zamani ambaye kimsingi ulipaswa kuwa unamvika pete ya uchumba leo?"

Uso wa Ethan ulikuwa haufai kwa aibu, akajitahidi na kumwambia mjomba wake. “Nasema hivyo kwa manufaa yako. Babu na Bibi hawatamkubali kamwe katika familia.”

“Ni kwa manufaa yangu au yako? Nina hakika unajua jibu kuliko mtu mwingine yeyote.” Kelvin alimwambia.

“Ding.” Wakati huu, mlango wa lifti ulifunguka. Kelvin alimuongoza Lisa ndani ya lifti, akaufunga uso wa hasira wa Ethan upande wa pili wa milango ya lifti. Akiwa ndani ya lifti, Lisa alitawaliwa na hisia zilizomzidi uwezo.

Kelvin akamtazama. Akifikiri kwamba lazima angekuwa na hofu, alimpigapiga begani huku akitabasamu. “Lisa umetisha! Ulithubutu vipi kuruka juu ya meza na kuongea maneno yale mbele ya kila mtu?” Kusema kweli, Kelvin alishindwa kuuzuia mshangao wake. Pengine hiyo ilikuwa ni sherehe ya kukumbukwa zaidi aliyowahi kuhudhuria. Hata hivyo, alionekana kuvutia zaidi aliposimama juu ya meza.

“Bw. Mushi… wewe ni mjomba wa Ethan?” Lisa aliuliza jambo lililokuwa likimchanganya sana!

>LISA INAENDELEA KWENYE KITABU CHA PILI>>

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
KARIBU KATIKA KTABU CHA PILI CHA SIMULIZI YA LISA

SIMULIZI......LISA
KURASA.....51-55
Sura ya 51

“Ndiyo,” Kelvin alikiri. "Nimefahamu kuwa wewe ni binti wa pili wa Mzee Jones Masawe muda si mrefu uliopita. Ninaufahamu uhusiano kati yako na Ethan. Alikuwa akizungumza nami juu yako wakati wote huko nyuma. Yaani nilijua ni Ethan ndiye aliyesaliti uhusiano wenu. Samahani sana kwa hilo. Bila shaka, baada ya kufanya kazi nawe katika mradi wa nyumba yangu, nilitambua kwamba wewe ni binti mwenye kipawa anayestahili kuthaminiwa.”

"Kwa nini ulinidanganya kuwa ni jamaa yake wa mbali?" Lisa aliuliza tena.

“Najua unamchukia, kwa hiyo sikutaka uwe na kinyongo kwagu,” alieleza ukweli. "Pongezi zangu kwako ni za kweli!"

Lisa akavuta pumzi kwa nguvu. “Samahani kwa kuuliza hivi, lakini je, Ethan ana mjomba mwingine wa upande wa mama yake mbali na wewe?”

Swali hilo lilimshangaza, lakini alitikisa kichwa huku akitabasamu. "Hapana."

Alipofikiria kuhusu Alvin Kimaro kuwa mjomba wa Ethan, Lisa alipoteza kabisa maneno. Alihisi kama angeweza kuzimia muda wowote. Kwa hiyo alikuwa kaingia chaka? Pamela alikuwa wapi? Aliahidi asingempa mwanamke huyo kifo cha haraka! Badala yake, angechukua muda kumchuna ngozi taratibu akiwa hai. Pamela alikuwa amemwambia kwa kujiamini kabisa kwamba amepata mtu sahihi. Hivi ndivyo alivyomsukuma Lisa kwenye shimo la giza.

“Um… Uko sawa?” Kelvin aliona hali isiyo ya kawaida usoni mwake. Alionekana kana kwamba alikuwa karibu kuzimia.

“Sijambo. Labda nilikuwa nimechoka kwa vita yangu mapema. Nahitaji kupumzika vizuri na kujituliza.” Lisa alitoka kwenye lifti akihisi dunia yake inasambaratika.

"Ngoja nikupeleke nyumbani." Kelvin alitoka kwa wasiwasi.

"Hapana, naweza kuendesha gari." Alitikisa mikono yake hewani kumkatalia

'Sawa basi. Lakini tafadhali kuwa makini. Nitumie SMS ukifika nyumbani.” Akamsindikiza mpaka kwenye gari.

Lisa alimpigia Pamela mara moja wakati gari lake likitoka nje ya hoteli hiyo. “Uko wapi?”

"Nimemaliza mtihani wangu na nilikuwa karibu kutafuta mahali pa chakula cha jioni haraka. Nina mtihani mwingine saa mbili usiku. Nilimpigia simu Patrick mapema akanisimulia kuhusu matendo yako ya ajabu—”

“Nitakuja kwako sasa hivi. Kuna kitu nahitaji kukuambia. Sawa, labda unafaa kuvaa mavazi ya kivita na kofia ya chuma kwa sababu ninaweza kuutoa uhai wako muda wowote.” alisema kwa sauti ya kutisha, lakini ya utani.

Hii ilimshangaza Pamela. “Nimekufanya nini tena mtoto wa mwenzio?”

“Hujanikasirisha bali umenisukuma kaburini kabisa!” Lisa ambaye alishindwa kujizuia alianza kupiga kelele. “Alvin si mjomba wa Ethan kabisa! We ni mtu mbaya sana!"

“Hapana…usinitanie bwana!” Pamela hakujua la kusema zaidi.

“Nilikutana na mjomba halisi wa Ethan leo, ni Kelvin Mushi. Nilipewa mradi wa kubuni jumba lake la kifahari huko Mbezi Beach siku chache zilizopita.” Lisa alijisikia kulia wakati huo. “Ni nini kilikufanya ufanye kosa hili?” Pamela aliamua kunyamaza na kukata simu huku mshtuko ukipita ndani yake. Hakuweza kuelewa ni kwa nini iwe hivyo, kwani alikuwa amesikia kutoka kwa kaka yake mwenyewe.

Nusu saa baadaye, Lisa alijitokeza mbele ya Pamela kwa kasi kama ya radi. Pamela akasimama na kujipinda kama mcheza karate au judo, akamwambia kwa utani. “Hii hapa kanuni. Unaweza kunipiga lakini si usoni mwangu.”

Lisa akatabasamu kichovu. "Kwa aibu hii natamani kujichimbia shimo nijifukie, lakini lazima nijifukie na wewe sababu ndiye uliyeniponza. Alvin si mjomba wa Ethan, nilikuwa najidanganya kabisa!"

Pamela alitabasamu kwa huzuni. “Niikuwa nasoma kujiandaa na mtihani lakini ilibidi niache kwanza na kutafakari makosa yangu kwa dakika 30 zilizopita. Nimewaza tena eneo lile kaka aliponielekezea mtu ambaye alitakiwa kuwa mjomba wa Ethan. Kulikuwa na wanaume wawili wakitembea pamoja wakati huo. Hakika Alvin alikuwa mmoja wao. Alikuwa na tabia ya jeuri na majivuno kama mwanamfalme…”

"Na kwa hivyo ulidhani kuwa ni mjomba wa Ethan?" Lisa alikatiza kwa kicheko cha kejeli.

Pamela aliinamisha kichwa chake chini, akiuma kucha bila kujua. "Naam, ni kawaida kwamba ningefanya kosa hilo. Mtu aliyesimama karibu na Alvin hakuwa chochote kwa kulinganisha naye ... "

"Mtu huyo alionekana kama huyu?" Lisa alionyesha picha ya Kelvin kutoka kwa simu yake, ambayo alikuwa ameipiga kwa bahati mbaya siku ambayo walianza mchakato wa ukarabati.

"Lo, sikuwa makini wakati huo." Pamela alikunja uso huku akitoa macho kutazama kwa makini. "Inaonekana kama yeye. Ndiyo, alikuwa yeye. Kwa hiyo ni mjomba wa Ethan?”

Lisa aliweka mkono kifuani ili kupunguza maumivu. “Kukuamini kwangu kumeniponza, niliitoa ndoa yangu kwa sababu yako ya kusema vitu bila uhakika. Hivi unajua jinsi nilivyoteseka katika miezi miwili iliyopita? Kila siku, niko kwenye hatihati ya kupoteza akili yangu kutokana na matusi ya mtu huyo mwenye dharau, sembuse kulazimika kufua nguo, kupasha joto kitanda chake, kutunza paka, na kuwa mlinzi wake wa nyumbani bila malipo! Kila nilipojisikia kukata tamaa, nilijiambia ni sawa kwa sababu hii itanisaidia kupata nafasi yangu ya kuwa shangazi wa Ethan. Inatokea kwamba nimekuwa nikicheza kimapenzi na mtu ambaye si sahihi!”

Pamela, ambaye alijawa na hatia, aliweka macho yake chini. Machozi yalimtoka Lisa huku akilazimisha tabasamu. "Kwa bahati nzuri kwa bibi pako salama vinginevyo ungenioza kwa kaka yako"

"Samahani, ni kweli," Pamela alisema kwa unyonge, "Itakuwaje, nikuunganishe na kaka yangu?"

Lisa alishtuliwa na maneno ya mwanamke huyu. "Kwanza uliharibu maisha yangu, na sasa unataka kumvuta kaka yako kwenye vurugu hii? Sahau, labda ilikuwa nistahili yangu. Ulinionyesha mtu huyo tu bila nia yoyote ya ubaya. Ni mimi niliyekuwa na ndoto za mchana kulipiza kisasi kwa kuwa shangazi wa Ethan. Labda Mungu aliamua kuniadhibu kutokana na mawazo yangu mabaya. Pengine ndivyo hivyo.”

“Acha kusema hivyo. Sawa, hukusema siku chache zilizopita kwamba mmiliki wa huo mjengo wa Mbezi Beach anavutiwa nawe? Kama ni hivyo bado unayo nafasi ya kuchukua hatua na kuwa shangazi wa Ethan, kwa sabau tayari amevutiwa na wewe. Rafiki yangu bado nafasi unayo, ni wakati wako wa kuangaza." Pamela alimpiga bega rafiki yake kwa kumtia moyo.

"Najisikia kulia kadiri unavyosema hivyo." Lisa alitazama angani na kuhema kwa muda mrefu. "Kelvin ni mzuri zaidi kuliko Alvin kwa tabia, ni mpole, anajali na anaonekana ana upendo. Ikiwa angekuwa ni yeye niliyempata mwanzoni, huenda tayari tungekuwa tunaishi pamoja kwa furaha kufikia sasa.”

"Usijali, bado kuna nafasi kati yenu." Pamela alizidi kumtia moyo.

“Nafasi gani? Nimeolewa kisheria, unakumbuka? Kwa kuzingatia malezi ya familia ya Mushi, hakika hawatakubali bikira ambaye aliwahi kuolewa hapo awali. Labda ninapaswa kuzingatia kutafuta pesa zaidi. Sithubutu kuota kuhusu mapenzi tena.” Lisa alionekana kukata tamaa.

"Lakini wewe… Labda unapaswa kuomba talaka kwa Alvin," Pamela alimkumbusha kwa tahadhari.

Lisa alishtuka baada ya kusikia hivyo. Kweli, ilikuwa ni wakati wa kutatua hilo. "Je, akikataa kutoa talaka?"

“Haiwezekani. Pengine atapiga makofi kwa furaha kwa kuweza kukuondoa kwenye maisha yake.”

Lisa alitabasamu kwa uchungu uliochanganyikana na furaha.

Sura ya 52

Ndani ya hoteli kubwa ya Heaven On Earth, familia za Masawe na Mushi zilikusanyika baada ya sherehe ya uchumba kumalizika. Uso mzuri wa Ethan ulikuwa umepauka mithili ya msukule alipotazama kipande cha video kwenye simu yake. Ilikuwa ni kutokana na matarajio yake kwamba ndani ya saa chache, video ya Lisa akiharibu sherehe hiyo ingekuwa imesambaa mtandaoni. Ilikuwa imepokea maoni zaidi ya milioni tano kwa muda mfupi.

“Pumbavu wewe, tazama jinsi ulivyonidhalilisha!” Zakaria Lowe, baba yake alimpiga kofi usoni kabla ya kunyanyuka na kuondoka kwa hasira.

“Nitazungumza naye," Sonya mama yake Ethan, alisema kabla ya kuamka na kumfuata mumewe aliyekuwa anaondoka.

Ethan, aliyeachwa nyuma, alikunja ngumi kwa hasira kana kwamba anataka kupigana na hewa. Macho yake yalikuwa mekundu kwa hasira.

“Ethan…” Lina alimbembeleza mchumba wake kwa upole lakini Ethan akautupa mkono wake kwa nguvu.

"Je, ni wewe uliyebadilisha picha leo?" Ethan likuwa amewauliza wasimamizi wa hoteli hiyo lakini meneja wa jukumbi huo alisema picha za usalama za mchana ule zikuwa zimefutwa. Kando na hilo, Helen alikuwa mlezi mpya aliyeajiriwa na familia ya Masawe. Alikuwa na sababu nzuri za kutilia shaka maneno yake. Kwa upande wake, alimdharau zaidi mtu aliyebadilisha picha hizo kuliko kumlaumu Lisa.

“Unanitilia shaka?” Lina alitetemeka kana kwamba amezidiwa na uchungu moyoni. "Ni sherehe ya uchumba wetu leo, nilifanya kazi kwa bidii kuhakikisha siku hii itaenda vizuri na kikamilifu. Isitoshe, ningefaidika na nini kufichua picha hizo? Kila mtu aliyehudhuria sherehe hii leo ananilaumu!”

"Haiwezi kuwa Lina." Mama Masawe akasonga mbele kumtetea binti yake. “Ethan, unawezaje kumshuku? Unaamini kweli maneno yaliyotoka kinywani mwa Lisa ? Nadhani yeye ndiye mtu nyuma ya haya yote. Nimemjua shangazi Helen kwa miaka mingi. Yeye si mtu wa aina hiyo anayesema uwongo.”

“Mama, acha.” Lina akatikisa kichwa kwa unyonge. “Hata kama sikufanya, haya yote yalianza kwa sababu yangu, kwa hiyo lazima nibebe lawama zote. Ethan, unaweza kurudi kwa Lisa ikiwa hujisikii vizuri kuwa na mimi. Sikustahili tena, na sitaki kukuletea fedheha zaidi.”

“Usiseme hivyo. Nakuamini. Nililemewa na hiasira tu.” Ethan alibadilisha mtazamo wake haraka sana.

Baba yake alikatishwa naye tamaa kabisa siku hiyo. Ikiwa angempoteza Lina pia, mrithi wa baadaye wa familia ya Masawe, basi ingekuwa changamoto zaidi kwa Ethan kuchukua kampuni ya Lowe Enterprises.

Mama Masawe akasema. “Sio kosa lako. Lisa anapaswa kulaumiwa kwa ustadi wake wa kuigiza. Ni jambo moja ambalo hatukulitilia maanani. Baada ya juhudi tulizotumia kumlea miaka hii yote, ameharibu sifa ya Kibo Group ambayo tumejitahidi sana kuijenga. Ni mtu mbaya kama nini!”

Lina alilazimisha tabasamu la uchungu. “Tukimwacha hivihivi tu bila shaka ataendelea kutudhalilisha kwa kashfa zake. Ni lazima tumfunze adabu!”

“Sitaruhusu aendelee kutuharibia sifa yetu. Najua amechukua mradi wa ukarabati wa jumba la mjomba wangu huko Mbezi Beach. Ninaweza kupata njia ya kumwadhibu.” Nia ya hatari ikamjaa machoni Ethan. Alikuwa akihisi hatia kidogo kwa Lisa hapo awali lakini hisia hizo zilibadilishwa kabisa na kuwa chuki kali kwa wakati huo.

Jones alikunja uso wake. Midomo yake iliachana kidogo lakini hakuna neno lililotoka mwishoni.

Dakika 20 baadaye. Shangazi Helen alipiga hatua kwa tahadhari kuelekea kwa Lina. Alionekana akiwa hajatulia kabisa. “Bi. Lina, Mzee Masawe na mkewe watanishuku kwa kile kilichotokea kwenye sherehe leo? Mimi sina hatia. Ni wewe uliyenitaka nitoe mashtaka ya uwongo.”

“Ni sawa. Tayari nimeshalimaliza hilo.” Lina alichukua kitita cha noti kutoka kwenye mkoba wake na kumpa mwanamke huyo. “Hii ni fidia yako. Weka midomo yako vizuri. Sitaki mtu yeyote ajue kuhusu kilichotokea leo.”

Macho ya shangazi Helen yaling'aa. Haraka alipokea zawadi ile na kutikisa kichwa kushukuru mara nyingi sana. "Nimefurahi kuwa katika huduma yako."

“Jambo moja zaidi…” Lina alitoa tabasamu lisilo la kirafiki. “Lazima umwangalie sana bibi yangu. Sitaki kuona hali yake ikiimarika hata kidogo.”

Hii ilimshtua Helen. Alishindwa kumtafakari huku akimtazama mwanadada huyo. Ni ukatili ulioje? Hata hivyo, alitikisa kichwa bila kusita baada ya kufikiria kitita cha pesa alichotoka kupokea punde. "Hakuna shida. Sawa, nitahakikisha ninafanya kama unavyotaka. Hata hivyo hongera kwa kupata mume!”

"Sio ndoa bado." Uso wa Lina ulijidhihirisha waziwazi. asingekuwa mjinga vya kutosha kuolewa na Ethan ikiwa angepoteza haki ya kuchukua Kampuni ya Lowe.

Sura ya 53

Ndani ya ofisi za wanasheria ya ‘Jennings Solicitors, Sam Harrison, ambaye alikuwa amerudi kutoka kwa mapumziko yake ya chakula cha mchana, aliingia ofisini akiwa na raha kama zote. Alipopita kwenye ofisi ya Alvin, alimwona sekretari wake akikaribia kuingia na kikombe cha kahawa. "Wakili Kimaro alichukua mapumziko yake ya chakula cha mchana?" Aliuliza Sam.

"Hapana, amekuwa akishughulika na kesi mpya mfululizo," sekretari wake alinong'ona. "Wakili Kimaro anashughulikia kesi kwa bidii tangu majuzi. Je, anakabiliwa na matatizo yoyote ya kifedha? Kwa kawaida alikuwa akipokea kesi mbili tu kwa mwezi, lakini sasa anashughulikia kesi nne kwa wakati mmoja. Ana shughuli nyingi sana hivi kwamba anafanya kazi ya ziada katika kila mapumziko ya chakula cha mchana.”

“Ulishawahi kuna bahari inakaukiwa maji?” Sam alidhihaki. Alvin asingeweza kukabiliwa na matatizo ya kifedha. Yeye angeweza kukosa pesa lakini si Alvin, kamwe katika miaka milioni. Utajiri aliokuwa nao ungeweza kudumu kwa muda wa maisha yake yote. “Sawa, nipatie hiyo kahawa niingie nayo.” Sam aliichukua kahawa kutoka kwa sekretari na kuingia ofisini.

“Iache hapo,” Alvin alisema bila kuinua kichwa chake.

Sam akahema. "Ah, jana ilikuwa ni sherehe ya uchumba kati ya familia ya Masawe na Lowe. Rafiki yangu mmoja aliyehudhuria tukio hilo aliniambia picha za mapenzi za Lisa na Ethan zilionyeshwa kwenye skrini kubwa. Kila mtu pale alimshutumu Lisa kwa kupanga mambo yote. Msichana maskini alionewa bure.”

Picha zake za mapenzi na Ethan? Je, yeye Alvin aliwahi kupiga picha yoyote pamoja naye? Hakuna hata moja zaidi ya passport walizopiga siku ya ndoa yao bomani. Alijiwazia Alvin wa watu maskini! Alvin akanyanyua macho yake kwa kiburi. “Ni lazima nikuambie mara ngapi? Acha kutaja jina lake mbele yangu. Sijali hata kama angekufa.”

Sam alikosa la kusema. Angeweza kumkatisha mapema ikiwa hakukusudia kusikia zaidi. "Hakika, ikiwa ndivyo unavyotaka. Ngoja nitazame kipande hiki ambacho rafiki yangu alinirushia.” Sam alicheza clip ya video na kumuona Lisa akiruka juu ya meza.

Uso wa Alvin ulikunjamana. Alikuwa anakaribia kumtoa Sam ofisini kwake lakini akaduwaa kwa kusikia sauti ya Lisa kutoka kwenye kipande hicho cha video. Je, ni kweli aliwahi kuwa mpenzi wa Ethan? Hiyo haikuwa ishu kubwa, lakini ni kwanini bado alikuwa akihifadhi rekodi za sauti zilizotumwa na Ethan kutoka hapo awali?
Je, hakujali hisia za mume wake hata kidogo?
Je, alikuwa amesahau kuhusu hali yake ya ndoa?
Je, huyo Ethan mjinga angewezaje kumfananisha naye?
Je, alikuwa amefikia umbali gani na Ethan wakati wa uhusiano wao? Kukumbatiana? Kubusiana? Au ni zaidi ya hapo?

Sam hakuona mabadiliko yaliyojitokeza kwenye uso wa rafiki yake. Alivutiwa sana na jinsi mambo yalivyokuwa kwenye ile video. "Hey, angalia jinsi alivyoitawala sherehe utadhani msanii wa mashairi anaghani mbele ya hadhira, Inapendeza sana! Kumbe Lisa ni mbabe hivi?” Mara tu baada ya kusema hivyo, alihisi Alvin anakosa amani. Hatimaye, Sam alikohoa ili kugeuza upepo wa mazungumzo. "Lakini kwa kweli ni fedheha kubwa kwa familia ya Masawe wakati huu. Nina hakika Lisa asingefanya jambo hili kama hawakumkorofisha.”

Alvin alicheka. Sam akaendlea kusema. " Kwa kuzingatia historia ya awali ya familia ya Masawe, labda hawataruhusu hili lipite burebure tu. Mara ya mwisho kidogo wamuue kwa kumfungia ndani ya jumba la ukoo. Unafikiri hataweza kuwa hatarini tena baada ya hili? Au tumtafutie mtu wa kumlinda?”

Alvin akarudisha macho yake kwenye laptop na kuendelea kusoma nyaraka zake. "Sipo tayari kwa hilo mpaka aje mwenyewe kuomba msaada wangu."

Wakati huo huo simu yake ya mkononi iliita. Aliifikia na kugundua Lisa alikuwa anapiga. Baada ya kuona simu hii aliyokuwa akiisubiri kwa muda mrefu, hasira ya moyo wake ilitawanyika ghafla. "Atakuwa ameshalikoroga tena huko. Nina hakika kuwa ananipigia simu ili nimsaidie kwa sababu amejiingiza matatizoni tena," Alvin alisema kwa sauti ya kawaida, lakini kila neno likiwa na harufu ya dhihaka.

Sam alitaka sana kumkumbusha Alvin jinsi alivyopigwa kibuti mara ya mwisho. Hata hivyo, hakuthubutu kusema hivyo baada ya kugundua furaha iliyotanda usoni mwa Alvin.

"Sipokei." Alvin alizidiwa na kiburi chake ghafla. Aliitupa simu kwenye dawati bila kujali lakini akaendelea kuiangalia ikiita bila kujijua. Iliendelea kuita kwa dakika nzima zaidi na aliiokota tena ilipokaribia kukatwa. "Labda anaweza kuwa anamkimbia muuaji aliyetumwa na familia ya Masawe. Ikiwa atauawa kwa sababu sikujibu simu yake, hapo itakuwa shida kubwa.”

Sam alitoa macho kwa mshangao. Alitamani sana kupiga picha ya Alvin na kuituma kwenye kundi lao la Whatsapp.

“Acha kunitazama. Toka nje.” Alvin alimtimua rafiki yake kwa hasira. Bila kusita, Sam alitoka nje ya ofisi ile. Kabla mlango haujafungwa nyuma yake, alimsikia Alvin akiitikia simu hiyo kwa sauti ya chini. “Niko busy. Una sekunde kumi." Sam likaribia kujikwaa baada ya kusikia hivyo.

Upande wa pili wa simu, Lisa alikasirika sana kusikia sauti ya Alvin. Hapo awali, angekuwa na wasiwasi kuwa anamsumbua, lakini haikuwa wakati huo. “Mimi pia nina shughuli nyingi. Ninapiga simu ili tupange muda tusaini talaka katika ofisi ya usajili.”

Kulikuwa na ukimya wa kutisha upande wa pili wa simu. Sekunde kadhaa baadaye, Alvin aliegemea kiti cha ngozi na kucheka sana. “Naona umenogewa sana na huu mchezo wa vuta n’kuvute. Lisa, nakuonya usizidishe.” Hakuwa na la kusema zaidi.

“Nipo serious. Nataka talaka haraka iwezekanavyo.” Lisa alisisitiza.

“Hutajutia hii baadaye?” Uso wa Alvin sasa ulikuwa umetanda wasiwasi. Hakuamini maneno aliyokuwa akiyasema. Mwanamke huyu alikuwa amejitolea kuuteka moyo wake. Angewezaje kukata tamaa namna ile?

“Hapana. Utakuwa huru lini?" Lisa hakuonyesha utani.

"Sawa, nina muda sasa hivi." Alikuwa tayari kucheza mchezo wowote alioupanga akilini.

Hilo lilimshangaza Lisa. Alvin alikuwa amesema kwamba alikuwa busy, na ni kweli aliifahamu ratiba yake ngumu ya kazi. Ilikuwaje akubali kutenga mudanje ya ratiba yake ngumu ili kwenda kuandikisha talaka? Ina maana na yeye alikuwa amechoka naye na alitamani kuachana naye kweli?

“Nitaelekea huko sasa hivi. Tuonane kwenye ofisi ya msajili nusu saa baadaye.” Kulikuwa na ladha ya furaha katika sauti ya Lisa. Alikata simu mara moja baada ya hapo.

Sura ya 54

Alvin alichanganyikiwa ghafla. Lisa alisikika mwenye furaha sana aliposema anelekea kwenye ofisi ya usajili kudai talaka yake. Je, alifurahi kwa sababu hatimaye angeweza kupata talaka? Au alifurahi kwa sababu angeweza kuonana naye tena? Usiku uliopita, alikuwa ameondoka kwa hasira sana. Lazima alijutia uamuzi wake kwa kufikiria mara ya pili lakini alikuwa na aibu sana kukiri makosa yake.
Labda alikuwa akitengeneza kisingizio cha kukutana naye ili amwombe msamaha. Ikiwa ndivyo, azungumze naye kwa upole watakapokutana baadaye? Alvin alikuwa akijiwazia hayo. Baada ya yote, hakula na chakula kizuri tangu Lisa alipohama. Ikiwa angemwomba msamaha bila shaka angemsamehe ili aendelee kunufaika na mlo mnono aliokuwa akimuandalia.

Alvin alinunua kipande cha keki ya siagi kabla ya kuelekea kukutana na Lisa. Alipofika kwenye ofisi ya usajili, Alvin aligundua kwamba Lisa alikuwa ameshafika hapo kitambo sana. Alikuwa amevaa nguo ndefu nyeupe aliyomnunulia mara ya mwisho wakati wanakwenda kwenye sherehe za kuzaliwa babu yake Sam. Nuru ya alasiri iliyomwangukia ilimulika kikamilifu ngozi yake nzuri. Midomo yake minene iliyovutia na kukolezwa rangi za lipstick ilipanuka na kutabasamu kidogo.

Alikuwa amevaa na kupendeza vile kwa ajili tu ya kwenda ofisi ya usajili. Je! kweli alitaka talaka au alikuwa akijaribu kumrusha roho? Alvin alizidi kujiuliza kwa wasiwasi. Akamsogelea kwa hatua kubwa, huku akiwa ameshika boksi la keki mkononi. Macho yake yalimtoka alipomuona.

“Twende zetu.” Alvin alimjaribu kuona u-serious wake, kisha, akageuka na kuelekea katika ofisi ya usajili. Alikosa maneno baada ya kumuona Lisa akimfuata bila wasiwasi. Hilo silo alilotarajia. Alitarajia kumuona Lisa akimsimamisha na kumwomba msamaha badala yake.

“Simama hapo.” Alvin akakunja uso. Mwanamke huyu alikuwa hana akili kweli. Hakuona kipande cha keki alichokuwa ameshika? Ni dhahiri alikuwa amechukua hatua ya ziada ili kumfurahisha. "Kuna nini?" Alimtazama akiwa amechanganyikiwa.

"Nini unadhani; unafikiria nini?" Lisa alionyesha tabasamu la fumbo.

"Lisa, nimekupa nafasi nyingine tena." Sura ya kuchanganyikiwa ilijionyesha usoni mwa Alvin. Hakujua alikuwa anazungumza nini.

“Si tulikubaliana kwamba tunakuja kusaini talaka? Haya, tuyamalize. Bado nahitaji kurejea kazini baadaye.” Lisa alisisitiza.

Alvin aliuchunguza uso wake kwa makini na kugundua hakukuwa na chembe ya utani kwenye macho yake. Moyo wake ulizama mara moja. Je, alikuwa serious? Alitaka talaka kweli? Kwa nini? Hasira ilimjia juu yake kama mawimbi ya bahari alipofikia ufahamu huu. "Ni lini nilikubali kukupa talaka?"

Lisa alionekana kushtuka. "Si tumeongea katika simu mapema-"

"Nilisema maneno kamili kwamba nitakuja kutia sahihi hati za talaka?" Akamshika kidevu na kuachia tabasamu la uongo na kweli. “Lisa , unadhani mimi ni nani? Je, unafikiri unaweza kuanzisha na kumaliza ndoa na mimi wakati wowote unapotaka? Nilikuomba uachane nami wakati huo lakini uliendelea kunisumbua ili nikuoe. Nakumbuka nilikuambia kuwa ndoa yetu ina mkataba wa miaka mitatu. Usipokuwa na tabia nzuri, sitakuacha uende hata baada ya miaka kumi.”

Lisa alianza kuhisi kidevu kinamuuma. Akiwa amekasirika, alijibu, “Hata hunipendi na inaonekana unakerwa na uwepo wangu! Kwa nini unazuia talaka yangu?"

“Huelewi?” Alvin alikazia macho huku akiongea kwa vitisho, “Umenitia hasira. Wewe ndiye mwanamke wa kwanza kuthubutu kunipinga. Unafikiri nitakuacha uende kwa urahisi hivyo?”

Lisa alijisikia kulia, lakini machozi hayakutoka. Je, kulikuwa na vidonge duniani ambavyo vingeweza kuponya majuto? "Nifanye nini ili kubadilisha mawazo yako?"

“Unataka talaka? Hakika.” Alvin alikenua kidogo na kumwaga tabasamu. "Uwe mpishi wangu kwa miaka mitatu na nitakubali ombi lako."

Lisa likunja uso huku tabasamu la kejeli likienea usoni mwake. “Sheria inasema kwamba wanandoa wanaweza kupeana talaka baada ya kuishi tofauti kwa miaka miwili. Kwa vile hutaki kunitaliki leo, naweza kuendelea kusubiri. Miaka miwili itapita kwa kufumba na kufumbua. Nina muda wote ulimwenguni." Kisha, akaondoa mkono wake kutoka mkononi mwa Alvin na akageuka kuondoka.

Alvin alitabasamu kwa jeuri badala ya kujaribu kumzuia Lisa asiondoke. "Neno moja kutoka kwangu, hakuna wakili yoyote hapa duniani atakayethubutu kuchukua kesi ya talaka yetu. Ebu jaribu kama huniamini, lakini wakati huo ukifika, itabidi ukae nami kwa miaka 30 badala ya mitatu.”

Lisa akageuka kumkazia macho. Kusema kweli, Lisa hakujua alikuwa anashughulika na nani. Hakuweza kusema kuwa alikuwa mwanaume wa kawaida kwani Sam Harrison alionekana kuwa rafiki yake mkubwa. Hakuweza kusema kwamba alitoka katika familia ya kitajiri kwani hakuendesha gari la kifahari wala kuishi katika jumba la kifahari.

"Hata ukininyima talaka sitarudi kwako. Afadhali niishi peke yangu milele kuliko kukaa na mwanaume kama wewe.” Sauti ya Lisa ilikuwa ya dharau pia. Aligeuka na kuondoka. Baada ya yote, hakuwa na chochote zaidi cha kupoteza sasa.

Alipomuona akiondoka bila hata kuangalia nyuma, Alvin aliitupa keki chini kwa hasira. “Talaka? Endelea kuota!”

Sura ya 55

Saa moja ya asubuhi siku iliyofuata ilimkuta Lisa alikuwa bado amelala kivivu. Alijisikia kama mtu mpya tangu kuhama kwa Alvin kwani hakulazimika tena kujihimu alfajiri na kumwandalia kifungua kinywa kila siku.

Simu yake iliita kwa kishindo. Sauti ya fundi wa ujenzi iliyojaa wasiwasi ilisikika kutoka kwenye simu mara tu alipoitikia simu. “Lisa , kuna jambo baya limetokea. Nimefika tu kwenye saiti ya ujenzi na kukuta bomba limeachwa wazi usiku kucha. Sehemu yote ya ndani ya nyumba imejaa maji."

Lisa aliruka kutoka kitandani mara moja. “Usijali. nitakuwepo hapo muda si mrefu.”

Muda si muda, alifika kwenye eneo la ujenzi. Maji yalikuwa yakitiririka kutoka ndani ya jumba lile hadi ngazi za nje. Mabomba mapya ya maji na umeme yalijaa maji kabisa. Akiwa amechanganyikiwa, Lisa alishindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kimetokea. Fundi Maiko alikuwa akitetemeka baada ya kumuona.

"Tufanye nini, Injinia Lisa? Bw. Mushi hakika atachunguza hili na siwezi kumudu kulipa uharibifu. Nina hakika nilifunga mabomba yote kabla sijaondoka jana usiku.” Fundi Maiko alilalamika kwa huruma.

Lisa alijaribu kumtuliza mwanaume huyo. "Nakuamini."

Kwa wazi, hiyo haikuwa bahati mbaya. Ufungaji wa mabomba ya maji na umeme ulitarajiwa kukamilika katika muda wa siku mbili. Pesa zilizopotea hazikuwa nyingi, lakini aliogopa ikiwa kuta zingezama na ikiwa maji yangepita kwenye msingi, basi mradi ungechelewa. Muhimu zaidi, hii ingeharibu sifa yake na ya kampuni yake.

Kampuni ya Ruta Building Design ilikuwa ndiyo kwanza imeanzisha tawi huko Dar es Salaam hivi karibuni. Tukio kama hilo lingeweza kugharimu sifa ya kampuni. Lisa, ambaye alikuwa meneja mkuu wa mradi, kwa kawaida angekuwa mbuzi wa kafara. Labda hata watu wa karibu wasingethuhubutu kumwajiri tena katika siku zijazo. Hakika aliamini kulikuwa na njama nyuma ya mpango huo.

Alikuwa anawaza hayo tu wakati gari la kifahari lilipopita kwenye lango. Kisha Kelvin, Sonya, na Mzee Mushi, baba yake Kelvin wakatoka kwenye gari mmoja baada ya mwingine.

“Baba, hii ni nyumba mpya ya Kelvin . Ni mara yako ya kwanza kufika hapa, kwa hiyo chukua muda wako kutazama huku na kule,” Sonya, mama yake na Ethan, alisema huku akimsaidia mzee huyo kutoka kwenye gari.

“Baba nilishasema ndiyo kwanza tumefunga mabomba ya maji na umeme tu. Bado hakuna kitu cha kuvutia,” Kelvin , ambaye alitoka kwenye kiti cha dereva, alisema bila kusikilizwa.

Ninaweza kukaa hapa siku chache zijazo, kwa hiyo, ninaruhusiwa kutembelea wakati wowote ninapotaka.” Mzee Mushi alielekeza ghafla fimbo yake mbele. "Halo, mbona maji yametapakaa kisa sehemu kama baharini?"

Sonya naye alitoa ukelele wa mshangao. "Inaonekana kama nyumba imefurika maji."

Kelvin aliliona hilo pia. Akamgeukia Lisa kwa sura ya ukali. "Kwa nini kuna maji kila mahali?"

Fundi Maiko aligugumia, “Sisi… Hatujui. Bomba liliachwa likimwaga maji tangu jana usiku…”

Sonya aliziba mdomo huku akihema. “Unamaanisha nini kusema hujui? Ninyi nyote mmepewa jukumu kamili la mchakato wa ukarabati lakini sasa mnajaribu kuelekeza wapi lawama? Ee Mungu, bado unaweza kuokoa nyumba hii? Natumai maji hayakupitia kuta.”

Mzee Mushi alikanyaga fimbo chini. “Umeajiri kampuni gani isiyo na ubora? Fanya haraka uwaite polisi.”

Rangi zote zilimtoka fundi Maiko usoni, na alionekana kana kwamba alikuwa karibu kupiga magoti chini. Lisa alisogea mbele kumshikilia mara moja.

“Hakika, tutoe taarifa polisi. Lazima waje wahakikishe kuwa anayehusika na huu upuuzi lazima alipe ghara zote.” Sonya akatikisa kichwa, akionekana kukasirika.

“Lisa, unajaribu kukwepa lawama? Meneja wa mradi anapaswa kubeba matokeo ya makosa yake. Nyinyi mna funguo za jumba hili na pia ni nyie tu mnaojua nenosiri, sivyo?” Kelvin alimbana Lisa.

“Kelvin, naelewa ulimkabidhi mradi kwa sababu unampenda. Lakini bado anahitaji kubeba majukumu yanayohitajika.” Sonya alidakia.

"Nini? Unampenda?!” Mzee Mushi nusura aanguke chini. “Yeye ni mpenzi wa zamani wa Ethan. Huogopi kudhihakiwa kwa kuwa na ex wa mpwa wako?”

Sonya akampigapiga baba yake mgongoni kumtuliza haraka. “Tulia baba. Lisa ni binti mdogo na mrembo. Ni kawaida kwamba wanaume watamkubali.”

Mzee Mushi akawaka kwa hasira. "Hawezi kuwa mchumba wa Kelvin kwa sababu tu yeye ni binti mdogo na mrembo." Mzee Mushi alimnyooshea kidole Lisa na kupiga kelele, “Binti kivipi umekosa aibu? Si ajabu Ethan kukuacha. Mwanamke kama wewe hastahili mtu yeyote kutoka kwa familia yetu.”

“Baba!” Uso wa Kelvin ulikuwa umetanda hali ya kuchanganyikiwa. “Lisa na mimi hatujawahi kuzungumzia mambo ya mapenzi. Yeye ni mhandisi tu wa nyumba yangu. Tafadhali usimwaibishe.”

“Nadhani amekupofusha hata huoni ukweli. Tazama amefanya nini kwenye jumba lako?” Mzee Mushi alifoka kwa hasira, “Kama unataka kusamehe kuhusu jambo hili, basi nakuambia sasa hivi kwamba haiwezekani! Sonya, piga simu polisi sasa hivi. Ni lazima alipe gharama zote.”

Lisa ghafla akatoa simu yake. Tabasamu la kujiamini lilienea usoni mwake. “Hakika. Niliweka kamera ya usalama kwenye jumba hili kabla ya hili kutokea. Ukweli utadhihirika mara tu polisi watakapofika na kuangalia."

Sura ya mshangao ikaangaza usoni mwa Sonya. Kelvin alionekana kufurahi. Alitamani kuwa upande wa Lisa lakini hakujua jinsi ya kufanya hivyo mbele ya mzee huyo. "Sawa, nitahakikisha polisi wanachunguza hili kwa kina."

"Hakuna haja ya kuwasumbua polisi. Tayari nimeitazama kwenye simu yangu.” Lisa alimwonyesha picha. "Baada ya fundi Maiko kuondoka jana usiku, msaidizi wako binafsi alikuja. Ni yeye aliyefungua mabomba.”

Macho ya Kelvin yalichomoka kama mshale alipokuwa akitazama picha hiyo. Sekunde chache baadaye, aligeuka taratibu kumtazama Sonya.

Mzee Mushi alikunja uso kabla ya kusema, “Kelvin kuna tatizo gani na msaidizi wako?”

Kabla Kelvin hajajibu, Lisa alisema huku akitabasamu. "Hiyo ni sawa. Kwa nini msaidizi wake afanye hivi ili kuniharibia? Labda alifanya hivyo chini ya agizo la mtu mwingine.”

Sonya alitetemeka. Hakujua tena la kusema. Kelvin hakuwa mpumbavu. Jana yake usiku, Sonya alikuwa amerejea ghafla kwenye makazi ya Mzee Mushi. Kisha kwa namna fulani, Mzee Mushi akapendekeza ghafla kwenda kwenye jumba lake la kifahari ili kuona maendeleo ya ukarabati.

“Bi Jones, hili jambo limesababishwa na upande wangu na halina uhusiano wowote na wewe, hivyo unaweza kurudi kwanza. Mara tu jumba hili litakapokaguliwa upya, nitawasiliana nawe ikiwa tutaamua kuendelea na ukarabati,” Kelvin alieleza kwa sauti ya uchangamfu.

“Hakika. Ninakuamini, Bw. Mushi. Wakati huo huo, pia nina masikitiko makubwa kwako kwa hasara hii.” Lisa aliitikia kwa kichwa na kuondoka na fundi Maiko.

Katika jumba hilo, Mzee Mushi alikuwa bado amechanganyikiwa hadi Kelvin alipoenda na kumwambia, “baba, nitakupeleka nyumbani.” Walipoingia kwenye gari, Kelvin aligeuka na kumwambia Sonya, “dada, mwambie Ethan aje ofisini kwangu.”

Sonya alipigwa na butwaa. Je, mdogo wake alikuwa na akili kiasi gani? Tayari alijkuwa amejua kila kitu kuhusu njama zao…

TUKUTANE KURASA 56-60

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI......LISA
KURASA......56-60

Sura ya 56

Nusu saa baadaye, katika ofisi ya Kelvin Mushi, mkurugenzi mkuu wa Golden Corporation, Ethan aligonga mlango kwa wasiwasi. Hakuwahi kufikiria kuwa Lisa angeweka CCTV katika jumba lake la kifahari ambalo lilikuwa chini ya ukarabati. Sasa alikuwa na wasiwasi sana baada ya kuitwa na mjomba wake baada ya njama zake kubainika.

“Mjomba…” Mara tu Ethan alipomwita, Kelvin aligeuka na kumpiga kofi kali usoni. Masikio ya Ethan yakashikwa ganzi kwa maumivu. Jana yake baada ya sherehe ya uchumba baba yake alimpiga shavu moja, na siku hiyo tena mjomba wake akampiga kwenye shavu la pili.

“Kwa nini?” Ethan hakuamini. Kelvin alimthamini zaidi. Haidhuru Ethan alifanya nini, Kelvin alikuwa tayari kumsaidia, kumsamehe, na kumlinda. Alishangaa siku hiyo kwanini alimtwanga kofi bila huruma.

"Nini unadhani; unafikiria nini?" Kelvin alishika kola yake, akionekana kukata tamaa kabisa. "Ulitumia nyumba yangu kama njia ya kumkomesha yule msichana. Je! unaniheshimu hata kidogo?"

Ethan alikuwa hajaelewa, na macho yake yakawa mekundu. “Unafanya hivi kwa sababu ya Lisa Masawe? Umenipiga kwa sababu yake?”

"Funga mdomo wako." Kelvin alikasirika. “Hata sasa, hujutii ulichofanya. Sasa, ushirikiano wote uliopendekezwa kati ya kampuni yangu na kampuni ya baba yako ya Lowe Enterprises mwaka ujao utasitishwa. Pia nitaondoa uwekezaji wangu kutoka kwa baadhi ya miradi iliyotangulia. Uko peke yako sasa.”

"Hapana!" Ethan aliingiwa na hofu mara moja. “Mjomba Kelvin, huwezi kufanya hivyo. Miaka yote hii, familia yetu imeendelea kwa sababu ya usaidizi wa familia ya Mushi ndiyo sababu baba yangu hathubutu kumdharau mama yangu. Hiyo ndiyo sababu pekee iliyonifanya niwe mrithi wa Lowe Enterprises. Ukiondoa uwekezaji wako, mtoto wa nje wa baba bila shaka atachukua nafasi yangu.”

"Ikiwa ulijua hayo, basi kwa nini uliamua kufanya ujinga?" Kelvin alisema kwa upole, “Ikiwa unaweza kumhonga msaidizi wangu binafsi leo, si utaweza kuwanunua wasimamizi wakuu na wakurugenzi wa kampuni yangu kesho?”

“Mjomba Kelvin, sitafanya hivyo. Nisingethubutu. Nilitaka tu kumfundisha Lisa somo,” Ethan alisema kwa uchungu.

Ingekuwa sawa kama asingeongea vile, lakini kwa vile alikuwa amekiri bayana, Kelvin hakuweza kujizuia kuokota faili lililokuwa kwenye meza na kumtupia Ethan. "Unataka kuharibu sifa yake kwa sababu tu alifunua rangi zako halisi jana? Unataka kumweka jela bila kosa?”

“Siyo hivyo,” Ethan alikanusha kwa uso uliopauka.

“Kama sivyo, baada ya kufanya hujuma kwenye jumba langu kwanini umemfanya mama yako amlete babu yako kwenye jumba kwa makusudi? Si kwa sababu ulitaka kutumia ushawishi wake kama shinikizo? Hujuma na njama zako zote za hila zinakuondolea uaminifu. Ondoka, sitaki kukuona tena. Usije kwenye kampuni yangu siku zijazo.” Kelvin alitoa wito kwa usalama kumtoa Ethan nje.

Kwa mara ya kwanza maishani mwake, Ethan alitupwa nje ya Golden Corporation. Alikuwa amepaniki.

Muda si muda, Ethan alipigiwa simu na baba yake kwa hasira. “Mwanangu hufai, umefanya ujinga gani? Hata mjomba wako aliudhika na Golden Corporation imetoa pesa zake zote kwenye kampuni yetu. Rudi hapa mara moja.”
•••
Kesho yake asubuhi, Lisa alipokea simu kutoka kwa Kelvin . “Una muda wa kula chakula cha mchana pamoja na mimi? Nataka kuongea na wewe kuhusu mradi wetu."

“Hakika.”Lisa aliafiki.

Nitakuchukua kwenye gari langu,” Kelvin alisema kwa sauti nyororo, “naogopa hutajua njia ya kwenda mgahawani.” Lisa hakukataa kufuata maombi ya Kelvin.

Saa sita mchana, gari la Kelvin lilitokea. Lisa aliingia, na Kelvin akamkabidhi kopo la chocolate. "Samahani, ulikosewa jana."

Lisa aliongea kwa upole wakati akipokea kopo la chocolate. "Nimezoea sasa Bwana Mushi. Nimechomwa sana visu na ndugu zangu kwa hiyo sioni ajabu kwa mtu baki kunifanyia hivyo."

“Wewe ni mwerevu sana.” Macho ya Kelvin yalikuwa yamejaa uchungu, lakini kulikuwa na shukrani ya dhati katika sauti yake. “Ethan amenivunja moyo sana. Hakuwa hivi hapo awali.”

Lisa alikata tamaa na kufadhaika pia. Alikubaliana na mawazo ya Kelvin.

"Nimesitisha ushirikiano wote kati ya Golden Corporation na Lowe Enterprises." Kelvin almwambia Lisa wakati anawasha gari.

"Hilo lazima liwe pigo kubwa kwa Ethan." Lisa akahema. Nafasi ya mrithi wa Lowe Enterprises ambayo Ethan alitamani haikuwa dhabiti tena.

Lisa akawa na hamu kidogo ya kujua. Ikiwa Ethan asingekuwa tena mrithi wa Lowe Enterprises, Lina bado angebaki naye? Ingependeza ikiwa Lina angemtupa na kupanda tawi lingine ili Ethan akome kabisa!

“Mbona kama hujafurahishwa?” Kelvin alimuuliza Lisa huku akimwangalia usoni.

"Nimefurahi sana, lakini shangazi Sonya atakuja kwako kumuombea msamaha."

Kelvin alimtazama huku akitabasamu. “Haina maana kuomba msamaha. Lilikuwa kosa lake kwa kuwa mkatili sana kwako.” Macho ya Kelvin yalikuwa yanavutia, Lisa alishtuka, hakuthubutu kumwangalia.

"Um... Acha nikuandalie chakula ili kukushukuru kwa kutokuwa na upendeleo." Lisa alisema huku akitabasamu.

“Hapana, kama ningekuwa sina upendeleo, ningekabidhi kesi hiyo kwa polisi. Acha nichukulie kama msamaha kwako.

"Hapana, wewe ni familia, hata hivyo. Tayari umelishughulikia zaidi ya matarajio yangu.” Lisa hakuweza kubishana naye tena.

Nusu saa baadaye, gari lilifika kwenye mgahawa maarufu wa hali ya juu huko Masaki. Lisa alipigwa na butwaa. Ilikuwa ni utata kidogo kwa mwanamume na mwanamke kuja kwenye mgahawa kama huo kwa chakula, ulikuwa ni mgahawa maalum kwa ajili ya wapendanao, na kulikuwa na menyu special kwa ajili ya wapenzi.

“Twende zetu.” Kelvin alimfungulia mlango wa abiria. Lisa hakuwa na jinsi zaidi ya kumfuata.

Kwa hakika Kelvin alikuwa ameshaweka oda, na mhudumu akawapeleka wawili hao kwenye meza iliyokuwa kwenye bustani ya nje yenye upepo mwanana na mazingira ya kifahari sana. Bustani hiyo ilikuwa ikitazamana na barabara kwa hivyo hata wapita njia wangeweza kuona kwa uwazi watu waliokaa kwenye meza za bustani hiyo. Maua ya waridi yaliyonunuliwa kutoka nje ya nchi yalipambwa juu yao.

“Maua ya waridi. Yanamaanisha 'Ninapenda tabasamu lako angavu'." Kelvin alichukua maua na kumkabidhi Lisa kwa macho ya upole. "Lisa , inaweza kuwa ujasiri sana kwangu kusema hivi, lakini lazima nikuambie kwamba nina hisia na wewe. Umeteseka sana siku hizi za hivi karibuni, lakini ninatumai kwa dhati kwamba katika siku zijazo, ninaweza kukukinga na upepo na mvua.”

Lisa alishangaa kabisa. Hakutarajia Kelvin angekiri kwake wakati huo. Ahhhhhhhh! Mbingu zilikuwa zikimfanyia hila? Mjomba halisi wa Ethan alimpenda, lakini alikuwa ameolewa na mtu asiyefaa! Alikuwa amejawa na makovu. Angekuwaje katika hali ya kuendelea na uhusiano mwingine? “Mimi… Pm pole, Bw. Mushi. Mimi… ninakufikiria tu kama rafiki.”

"Nimefurahi kusikia hivyo." Kelvin alikata tamaa kidogo, lakini aliendelea kutabasamu. "Ni sawa. Sikukiri kwako kwa sababu nilitaka unikubalie. Nataka tu uelewe hisia zangu ili niweze kutulia moyoni.”

Lisa alihisi kichwa kinamuuma. “Lakini sina nia ya kuiingiza kwenye uhusiano kwa sasa. Nataka kuzingatia kazi kwanza."

“Naweza kukusubiri. Sawa, ngoja tukae na uagize kwanza.” Kelvin kwa uungwana akamtolea kiti. Lisa alikuwa hoi, alijitahidi tu kujituliza na kuagiza chakula.

Sura ya 57

Katika makutano ya barabara kando ya mgahawa huo, gari moja la kifahari lilikuwa likingojea taa ya kijani iruhusu kuendelea na safari yake. Aliyeendesha gari hilo alikuwa Sam Harrison na aliyeketi kwenye kiti cha abiria alikuwa Alvin Kimaro, ambaye macho yake meusi yaliganda ghafla alipotupa jicho lake nje. Macho makali mithili ya kipanga ya Alvin yalikuwa yameshaona kitu kwenye bustani ya mgahawa ule.

“Geuka kushoto na uingie kwenye ule mgahawa. Tutakula kwenye mgahawa huo chakula cha mchana.” Alvin alimuamuru Sam

“Alvin, hilo halitawezekana. Tuna miadi na Bw. Jackson kuzungumzia kesi yake.” Sam alifuata macho ya Alvin na kutazama. Alielewa mara moja kwa nini hali ya joto kwenye gari ilishuka ghafla. Alvin alikuwa na wivu.

"Ahirisha huo mkutano," macho ya Alvin yalikuwa yanatisha kwa ukali alivyoamuru. Sam angeweza tu kufanya kama alivyoagizwa na kusimamisha gari baada ya kuingia mgahawani.

Wawili hao walipotokea kwenye mlango wa mgahawa huo, mhudumu wa mapokezi aliduwaa kwa muda. Ilikuwa ni kawaida kuona vijana watanashati wakikutana pamoja kula kwenye mgahawa huo lakini walikuwa na wapenzi wao, lakini kwa siku hiyo alishangaa vijana watanashati wakiwa single, kwa sababu mgahawa huo ulikuwa kwa ajili ya wapendanao, na kila mtu aliyeingia humo alikuwa na mpenzi wake. Alihisi labda vijana hao walikuwa katika mahusiano ya jinsia moja.

Mhudumu wa mapokezi alionekana kushangaa lakini akauliza kwa upole, “Je, mngependa tuwaandalie meza ya wanandoa?”

Sam alijikwaa kwa mshangao, lakini akavumilia kuropoka tusi baya alilokusudia kumtukana mhudumu yule.

"Hakuna haja." Alvin alimpuuza mhudumu huyo na kutembea moja kwa moja kuelekea alipokuwa amekaa Lisa na Kelvin. Kadiri alivyokuwa anamsogelea ndivyo alivyokuwa akiona wazi kuwa mtu aliyekuwa anakula naye ni mwanaume. Hakuwahi hata kufanya hivyo na Alvin hapo awali. Alikuwa akicheka kwa furaha sana pia.

Sam alishtuka. “Huyu si Kelvin Mushi kutoka Golden Corporation? Walitaka kukuomba ushughulikie kesi yao hapo awali.”

Ujeuri usoni mwa Alvin ukazidi kuongezeka. “Haishangazi Lisa alikuwa akipiga kelele kutaka talaka. Tayari alikuwa ameweka macho yake kwenye shabaha nyingine.”

Alvin akatazama Lisa alivyokuwa amevaa, mavazi mazuri yaliyoibua umbo lake maridadi, yakionyesha mikunjo yake yote na kuacha sehemu kadhaa hadharani kwa faida ya mtazamaji. Pia aliseti mwonekano mpya wa nywele zilizopendeza, na kuufanya uso wake uonekane maridadi zaidi na wa kuvutia.

Lisa alikuwa anazungumza na Kelvin kuhusu mambo fulani ya nje ya nchi wakati ghafla alihisi hewa yenye baridi kali ikimzunguka. Kisha, mkono mwembamba, mweupe, ukabanwa nyuma ya kiti tupu cha kulia kando yake. Kuangalia mkono, alifuata njia hadi akaona saa ya chapa isiyojulikana kwenye kifundo cha mkono huo. Ingawa ilikuwa ya bei rahisi na ya kawaida, kwa kuwa kifundo cha mkono cha mtu huyo kilikuwa kizuri sana, ilifanya saa hiyo ionekane kama saa yenye chapa maarufu. Alikumbuka kwamba ni Alvin Kimaro pekee ndiye aliyevaa saa kama hiyo.

Wazo hilo lilipojitokeza, Alvin alikokota kiti na kuketi. Akiwa amevalia suti ya khaki yenye shati jeupe na tai, uwepo wake ulitawala eneo hilo kwa mwonekano wake mzuri. Mwonekano adhimu uliotoka kwenye mwili wake ulizidi mbali ule wa kifahari wa Kelvin, na kumfanya aonekane hafifu na mwepesi kwa kulinganishwa naye. Lisa alionekana kuelewa jinsi Pamela alivyowachanganya mmoja kwa mwingine sasa. Hakika, wakati watu hawa wawili walipokuwa pamoja, wengi wangemzingatia Alvin kwa mtazamo, kuliko Kelvin. Mwonekano wake mzuri haukuweza kuchosha macho, lakini hasira yake sasa, ilikuwa ya kuchukiza! Hata hivyo, kwa nini alikuwa pale? Lisa alipata hamu ya kuchukua begi lake na kukimbia.

"Bw. Kimaro! Bw. Harrison!” Kelvin alisimama kwa mshangao na kupeana mikono na wawili hao. Hata hivyo, aliponyoosha kumpa mkono Alvin, Alvin alimtazama tu kwa uvivu na macho makali.

Zilipita sekunde kadhaa Kelvin akaanza kuona aibu. Alipoona Alvin kaupuuza mkono wake, Kelvin alirudisha mkono wake na kutingisha kichwa. "Samahani, naona hauko katika hali nzuri leo."

Kelvin aliwahi kuzungumza na Alvin Kimaro mara kadhaa hapo awali, haswa alipopanga kumwomba Alvin kusimamia kesi ya kibiashara kwa ajili yake. Awali mazungumzo yalikwenda vizuri, lakini baadaye kampuni ya mawakili ilisema kwamba alikuwa na shughuli nyingi. Kusema kweli, alikuwa anahisi kutoridhika kidogo na Alvin Kimaro.

Lakini, Alvin alikuwa mtu mashuhuri katika ulimwengu wa sheria. Kwa kuwa alikuwa na sifa nzuri, ilimbidi Kelvin amuonyeshe heshima fulani. Labda kungeweza kuwa na fursa za kufanya kazi pamoja katika siku zijazo. Hivyo, alitabasamu tu na kuwakaribisha.

Vidole vyembamba vya Alvin vilichomoa waridi kutoka kwenye shada lililokuwa juu ya meza na kuichezea. "Je, wanawake wote wanapenda uchafu wa namna hii?"

Uso wa kifahari wa Kelvin uliganda. Kwani, alikuwa ametoka tu kumpa Lisa maua hayo kwa heshima, lakini baadaye kidogo yaliitwa 'uchafu' na mwanaume mwingine. Alvin hakuwa akizingatia utu wake hata kidogo.

"Inaweza kuwa uchafu kwako, Bw. Kimaro, lakini kwa mwanamke, maua huwa na thamani." Kelvin alimkosoa.

“Si ajabu.” Macho ya Alvin yalimtoka. "Labda ni kwa sababu sifahamu hilo ndiyo maana mke wangu anatoka na mwanamume mwingine zaidi yangu."

Lisa ambaye alikuwa akinywa juisi kwa woga, alijikuta akipaliwa ghafla. Kelvin harakaharaka akamkabidhi tishu akaipokea huku akiinamisha kichwa chini. "Asante."

Alvin aliweka tabasamu la uwongo na kuinamisha kichwa chake kwake. "Bibiye, unafanya kazi gani?"

Lisa alinyamaza akiuma meno kwa aibu na kushusha hasira tumboni mwake, kisha akajifanya kutabasamu kwa furaha. “Bwana, nadhani umemkosea sana mkeo heshima. Uliwahi kushuhudia mkeo akimbusu mwanaume mwingine kwa macho yako mwenyewe, au ulimwona akipanda kwenye kitanda cha mwanaume mwingine? Ikiwa haukufanya hivyo, basi ni bora kuchunga maneno yako. Usipende kuropoka vitu ambavyo huna ushahidi navyo. Utajitia aibu tu. Sisi wanawake huwa tunaumia sana tukisikia mwenzetu akidhalilishwa!”

Wakati huo, sifa nzuri za Alvin zilikuwa gizani sana licha ya mwanga mkali. Hali kati ya Lisa na yeye mara moja ikawa ya wasiwasi.

Kelvin alikohoa polepole na kusema haraka, “Bw. Kimaro, Nitaomba msamaha kwa niaba ya Lisa.”

Msamaha? Jinsi gani walivyokuwa karibu. Mwanamke wake alikuwa akimfanya mwanaume mwingine amuombee msamaha kwa niaba yake? Alvin alibwabwaja kicheko. Ni Sam pekee aliyemfahamu vyema ndiye alijua ni hasira kiasi gani zilichanganyikana na kicheko kile kidogo. Ilikuwa ni mtangulizi wa dhoruba!

Sam aliburuta kiti kilichokuwa tupu kwa haraka na kumuuliza Lisa kwa sauti nyepesi, “Lisa ,una uhusiano gani na Bw. Mushi? Je, nyinyi wawili…”

“Bw. Harrison, unamfahamu Lisa ?” Kelvin alishangaa kidogo.

“Bila shaka. Nimekutana naye mara kadhaa kwenye hafla za biashara au chakula cha jioni.” Sam alieleza. Baada ya kutulia, kwa haraka akamkonyeza Lisa na kumwambia afikirie namna ya kujieleza.

Lisa hakutaka kutuhumiwa kukosa uaminifu akiwa kwenye ndoa hivyo alijieleza, “Kampuni yetu inafanyia kazi mradi unaohusisha nyumba ya kifahari ya Bw. Mushi, lakini hivi karibuni kumekuwa na matatizo hivyo tunayajadili kwa sasa.”

Alvin alicheka moyoni mwake. Je, kulikuwa na haja ya kucheka na kutaniana pamoja wakati wa kujadili biashara? Je, kulikuwa na haja ya kuja kwenye mgahawa wa wapendanao ili kujadili biashara?

Sam alitabasamu tu na kusema, “Ni majaliwa kwamba tumeweza kukutana leo. Kwanini tusile pamoja?”

Sura ya 58

Kelvin akaguna, “Sawa.” Asingeweza kukataa mbele ya mafahari wale wawili wa jiji.
Lisa naye akabaki kuguna tu. Je, anaweza kukataa? Ilikuwa ngumu sana kuukabili uso wa kishetani wa Alvin.

“Hapana, hamuonekani kufurahia sana wazo hilo. Labda tunawasumbua?" Alvin akawatazama akiwauliza kwa sauti yake ya kina na ya sumaku.

“Hapana, tafadhali tuketi pamoja.” Kisha Kelvin akamwomba mhudumu alete menyu.

Kukiwa na watu wanne mezani, nafasi ilikua finyu huku shada la maua likiwa juu ya meza. Lisa alinyoosha mkono kuweka waridi kando yake, lakini Alvin alikuwa mwepesi kuliko yeye, akawahi kuchukua na kukabidhi shada la maua kwa mhudumu.“Ondoa hii. Nina aleji na vitu hivi.”

Lisa alishangaa kama alimsikia vibaya. Hakuwahi kumuona akipata athari za aleji hapo awali aliponunua maua ya kupamba nyumbani kwake. Lazima alikuwa anafanya hivyo makusudi.

"Sikujua kuwa una aleji na maua, Bw. Kimaro." Kelvin hakuweza kujizuia kucheka.

"Ndio, nina aleji ya maua, ni maua ya waridi pekee lakini." Alvin alifungua menyu kwa utulivu na kuagiza chakula kwa raha zake.

Baada ya kila mtu kuagiza, Kelvin alibadilisha mada. "Kwa kweli, nimekuwa na hamu ya kujua kwanini Bw. Kimaro alikataa kesi yangu mara ya mwisho."

Sam aliogopa kwamba Alvin angezungumza kwa ukali sana na kumuudhi kabisa Kelvin, kwa hivyo akasema haraka, "Alipata shughuli nyingi sana ghafla."
Lisa alikunywa juisi yake kimyakimya huku akiwasikiliza akiwa ameinamisha kichwa chini. Hakuwahi kujua taaluma ya Alvin ni nini, lakini sasa alijua. Ilibainika kuwa alikuwa wakili ama mwanasheria, na ilionekana kuwa alikuwa mahiri sana. Alitaka sana kuchukua sahani ya chuma na kujipiga nayo hadi kufa.

Alikuwa ameona kwenye mtandao kwamba wanasheria walikuwa mojawapo ya taaluma kumi zinzosumbua sana kwenye mahusiano ambazo mtu hashauriwi kuolewa nazo. Ikiwa umeolewa na wakili, hutaweza kuondoka hata na chupi yako kama suluhu wakati wa talaka. Hata ukishtakiana na wakili, atakutoboa tu kwa mianya ya kisheria. Haishangazi alithubutu kusema kwamba maadamu hakubaliani na talaka yao, asingeweza kumtaliki hata baada ya miaka 30.

Damn it, ni shetani gani amemchokoza?! Ngoja, huyo shetani alikuwa akifanya nini? Kwa kweli alikuwa akiupapasa mguu wake chini ya meza. Lisa uso wake ukafura, na yeye akampiga teke nyuma yake.

Lakini, sekunde iliyofuata, Alvin alimtazama na kumuuliza kwa sauti. “Bi. Jones, kwa nini umenipiga teke?” Watu wengine wote kwenye meza walimkazia macho.

Sam alipepesa macho kwa kucheza. "Bibie, ingawa Bw. Kimaro ni mzuri na anavutia, usisahau kwamba ulikuja hapa kwa miadi na Bw. Mushi."

Lisa alimtazama kwa hasira. "Meza ni ndogo, kwa hivyo niligongana naye kwa bahati mbaya. Nyinyi ndio mmevamia na kubana nafasi kwenye meza yetu.”

"Kwa hiyo unatulaumu kwa kukatiza miadi yako?" Alvin alisema kwa sauti ya chini.

“Hapana, sipendi watu wenye mzaha namna hiyo. Baada ya yote… Bw. Kimaro si type yangu.” Lisa alishtuka na kuinamisha uso wake.

Tabasamu usoni mwa Kelvin likachanua kabisa. “Bw. Harrison alikuwa anatania tu. Najua hukufanya makusudi.”

"Naam, ninaenda msalani." Lisa hakutaka kubaki. Aliinuka na kuondoka kwenye kiti chake.

Muda si muda, Alvin naye akasimama. "Nitaenda kupiga simu."

Katika choo cha wanawake, Lisa kwa makusudi alijificha ndani kwa muda kabla ya kutoka nje. Alimwona mtu mrefu amesimama karibu na mlango akivuta sigara wakati anatoka. Kichwa chake mara moja kilihisi kulipuka. Alvin alibana sigara kati ya vidole vyake na kuvuta kwa nguvu. Moshi ulitanda huku akiutoa mdomoni. Aliweka kitako cha sigara kwenye pipa la takataka kando yake na kumwendea kwa hatua ndefu.

“Njoo.” Akamkokota hadi upande wa pili wa mgahawa.

Lisa alivutwa hadi nyuma ya korido la ukumbi wa makabati ya mvinyo. Mwangaza mle ndani ulikuwa hafifu, na uso wa Alvin ulionyesha hali ya hatari huku akimtazama kwa hasira.

"Unafanya nini hapa?" Lisa alikisukuma kifua chake lakini hakuweza kumshtua.

"Ulichukua maneno kutoka kinywani mwangu, mimi ndiye nilipaswa nikuulize hivyo." Alvin akamshika mkono, uso wake ukiwa na giza. “Una wakati mzuri na Kelvin Mushi? Umesahau kuwa umeolewa? Si ajabu unataka talaka. Tayari umepata shabaha yako inayofuata, sivyo?”

"Alvin Kimaro, angalia maneno yako." Lisa alitetemeka kwa hasira kufuatia maneno hayo. “Hakuna kinachoendelea kati ya Kelvin na mimi— “

“Je, angekutumia maua ikiwa hakuna chochote kinachoendelea kati yenu? Je, angekuleta kwenye mgahawa wa wapendanao? Je, unaweza kumpa tabasamu kwa furaha hivyo?!” Hasira za Alvin zilizidi kuongea. Alimshika usoni na kumlazimisha kumtazama.

Lisa alikasirika na kuchukia. “Nitamlaumu vipi kwa kunipenda wakati ninavutia na ni mrembo? Sio kosa langu kuzaliwa mzuri sana.”

Alvin alicheka kwa hasira na alikuwa anakaribia kuongea lakini Lisa alimkatisha. “Najua unanidharau. Sina thamani na sina haya machoni pako, lakini hiyo haimaanishi kwamba nilichukua hatua ya kumshawishi mtu mwingine anipende. Nakudai talaka kwa sababu ninahisi kwamba siwezi kuendelea na wewe tena. Haina uhusiano wowote na mtu mwingine yeyote.”

“Huwezi kuendelea nami?” Alvin alicheka kwa uchungu.

“Ndio hivyo, si unanidharau kwa sababu mimi hupanda kwenye vitanda vya wanaume? Umesahau jinsi ulivyonidhalilisha siku ile? Ulisema kwamba mimi ni wa bei nafuu, mchafu, na kunitazama tu kunakuchukiza. Alvin, mimi ni mwanadamu, sio mtakatifu. Nitajisikia vibaya pia.” Kadiri alivyozidi kusema ndivyo alivyozidi kuwa na hasira na huzuni zaidi. Hata alitoa hisia zote alizokuwa amezivumilia siku zote. “Nimechoshwa na mtu kama wewe. Wewe ni fedhuli, una dharau, mbinafsi, na unajua kupokea tu bila kutoa. Ni kama ulinioa ili niwe yaya wako wa wakati wote. Hata siheshimiwi! Hapana, labda sistahili hata nafasi ya yaya machoni pako. Lazima nilikuwa nimerukwa na akili hata kutaka kukaa na wewe."

“Nyamaza,” Alvin alionya kwa huzuni.

“Sitanyamaza....Mmh…” Macho ya Lisa yalimtoka wakati Alvin alipombana ghafla. Aliinamisha kichwa chake kuziba mdomo wake, akimkandamiza kwenye kabati la mvinyo. Alimsukuma kwa nguvu lakini hakuweza kuyumba hata kidogo.

Alvin awali alitaka tu kumlazimisha busu la mdomo mara moja. Labda alikuwa amepaka kitu kwenye midomo yake kwa sababu ilikuwa tamu sana na laini kama jeli, na kumfanya ashindwe kuacha na kutaka kuonja zaidi.

Lisa alitaka kupinga, lakini harufu hafifu ya tumbaku iliyochanganyikana na harufu ya kipekee ya mwili wake ilimfanya apate kizunguzungu. Hakuweza kutumia nguvu yoyote.
Baada ya muda usiojulikana, ghafla simu yake iliita. Mara akarudi kwenye fahamu zake na kummwondoa Alvin. Safari hii, Alvin alimruhusu amsukume.

Lisa aliugeuza mwili wake uliokuwa ukiungua kutoka kwake na kujibu simu, "Halo..."

Alipozungumza, aligundua kuwa sauti yake ilikuwa ya kupendeza sana. Mungu, imekuwaje hivi? Kwa bahati nzuri, Kelvin hakuona. “Lisa , umekuwa chooni kwa muda wa nusu saa. Mbona bado hujarudi?”

Nusu saa? Lisa alishtuka. Je! alikuwa akimbusu Alvin kwa muda huo? Hakuwa ameona kabisa. “Oh, mimi… nina maumivu ya tumbo. Karibu namaliza.”

Sura ya 59

Lisa alikata simu haraka. Alipokutana tena na macho ya Alvin, alihisi kweli tumbo la kuhara limemshika ghafla kwa hofu.

Alvin pia aliliona hili na alikuwa na furaha isiyoelezeka kwa muda mchache. Midomo yake ilijikunja kwa dharau. “Unaumwa na tumbo?”

Lisa alimkazia macho huku akizidi kuona aibu. “Huna haki ya kujua kuhusu hilo. Wewe si mume wangu tena, nakushauri unitaliki haraka.”

“Unathubutu kunitishia?” Alvin akamshika tena na kuongea kwa sauti yake ya jeuri. "Lisa Masawe, wewe bado ni mke wangu. Ikiwa utathubutu kunisaliti, nitakufanya ulipe kwa gharama kubwa."

Lisa hakuogopa hata kidogo. “Najua wewe ni mwanasheria na kuna njia mia za kunifanya nipoteze sifa, lakini haina maana dhidi yangu. Sifa yangu iliharibiwa zamani sana, na sheria haisemi kwamba kudanganya katika ndoa ni kinyume cha sheria, sivyo? Hakuna mali tuliyochuma pamoja baada ya ndoa, kwa hivyo hakuna cha kubishana. Sina pesa na sina sifa. Unaweza kunifanya nini?” Lisa aliinua macho yake kwa ushindi. Alvin hakujua kama alitaka kucheka au kukasirika.

“Nani kasema hauvunji sheria? Wakati wa ndoa, mke alikiuka wosia wa mume, akajaribu kumlazimisha mwenzi mwingine kufanya naye ngono kwa njia zisizo za haki, na alitumia dawa za kulevya ili kuhatarisha afya ya mume wake. Je, utaniamini nikisema hivyo kwa uwezo wangu, naweza kukupa kifungo cha miaka mitano jela?” Alvin aliegemea sikio lake na kumuonya neno kwa neno kwa sauti ya sumaku lakini ya hatari.

Lisa aliganda. Je! hiyo ilikuwa kweli? Ama alikuwa anatania?

“Tsk, inaonekana kweli hujui sheria. Unaondoka na mimi sasa hivi. Nikikukuta unapata chakula tena na Kelvin Mushi tena, nitakutumia barua ya wakili moja kwa moja kwenye kampuni yako.” Alvin alitabasamu kwa jeuri na kumshika mkono Lisa na kumtoa nje ya mgahawa huo.

Alvin alikaa kwenye gari la Sam, lakini Sam aliyekuwa na funguo za gari alikuwa bado anakula bustanini. Alipositasita kumwita msaidizi wake Hans ili awachukue, Lisa alitupa mkono wake na kukimbilia kwenye kituo cha daladala kilichokuwa mbele yake.

“Simama hapo hapo.” Alvin alimfukuza bila kujua. Alvin akamfuata na kuingia hadi kwenye daladala. Alipokaa tu kwenye kiti, konda akadai chake. "Hapo!!?"

Alvin akajisachi, hakuwa hata na sarafu ya mia mfukoni. Alikuwa na mamilioni ya pesa lakini yote yalikuwa ndani ya kadi ya benki, afanye nini sasa? "Sina pesa."

“Unasemaje?” Konda akawaka.

Uso wa Alvin ukawa giza. "Kuna mtu atakulipa huko nyuma…"

“Oya! unazingua ujue..” Konda alimkoromea. "kama huna nauli, basi shuka. Unaonekana kama kama wakishua hivi, au ndiyo nyie mliovamia madaladala baada ya mafuta kupanda bei? Oyaa suka tuache hapo mbele.."

Alvin alikuwa hajawahi kudhalilishwa hivyo hapo awali. Akamkazia macho Lisa aliyekuwa amekaa nyuma. "Njoo hapa unilipie." Lisa alichungulia dirishani, akijifanya hamjui.

Kundi la watu waliokuwa ndani ya basi hilo walimkodolea macho Alvin. Mwonekano na uvaaji wake ulimfanya kuwa mzuri zaidi kuliko wale mastaa wa kiume kwenye majarida ya mitindo, lakini kwanini hakuwa na pesa, alikuwa Marioo?

Msichana mmoja aliyeketi mbele alisema kwa haya, “Handsome boy, nina pesa. Naweza kukusaidia?"

"Mimi pia, konda shika hii... Ninaweza kulipia nauli yako ya daladala kwa mwaka mzima ukitaka.” Msichana mwingine alijikaza kusema.

Alvin hakushtuka lakini ghafla alimtazama Lisa kwa mahaba kabla ya kusema kwa sauti, “Mpenzi, usikasirike. Najua nilikosea na sikupaswa kuwa na wivu sana. Unaweza kunisaidia tu kulipa nauli ya daladala?”

Mara moja, zaidi ya jozi kumi za macho zilimwangukia Lisa. Macho ya wasichana wale waliokuwa wakijipendekeza yalijaa wivu na husuda.

Lisa akamjibu kikauzu “Mimi sio mpenzi wako. Usiongee ujinga. Sikujui hata kidogo.”

“Mpenzi, unaweza kunipigia kelele nyumbani. Kwa nini tugombane nje?” Alvin akiwa hoi akaachia tabasamu la uchungu na kutoa simu mfukoni. "Jamani, hiki ni cheti chetu cha ndoa nimehifadhi nakala yake kwenye simu, huyu ni mke wangu kabisa na pesa ya kulipa anayo yeye sema anataka kunidhalilisha tu." Alikionyesha ili kila mtu aione.

Mzee mmoja akasema, “Kweli ni mke wako. Bibie, unaenda mbali sana. Karibu tudanganywe na wewe." Konda naye alikasirika. “Fanya haraka ulipe nauli ya mumeo. Daladala si mahali pa kufanyia maugomvi yenu.”

Wasichana wengine walinung’unika, “Una mume mzuri sana lakini humtaki. Baadhi ya watu wasingejua bahati ikiwa ingewapiga makofi usoni.”

Lisa akaguna na kujisemea, “mh! wangejua!!”

Katikati ya shutuma hizo, Lisa ilimbidi ajilazimishe kumlipia Alvin. Alvin alizungusha mkono wake kwenye kiuno chake chembamba na kumpulizia sikioni huku akisema kwa sauti ya sumaku, “Asante mpenzi.”

Pumzi yake ilimwagika kwenye ncha ya sikio mbele ya watu wote, na kumfanya awe mpole kwa aibu.Aliweza tu kumtazama bila nguvu na kutumia macho yake kumwambia, 'funga domo lako' Alvin alibaki bila kutikisika na kutulia ndani ya gari.

Lisa alimpuuza na akainamisha kichwa chake kumtumia Kelvin ujumbe: [Bw. Mushi, samahani. Shangazi yangu Flo alikuja ghafla, kwa hivyo sina budi kurudi nyumbani mara moja.]

Alvin alitazama huku na huko hali yake ikawa mbaya. Sio tu kwamba alikuwa amebadilisha jina lake la WhatsApp, lakini hata alikuwa akituma ujumbe kwa Kelvin mbele yake. Hakumjali hata kidogo.

“Ulikuwa na Aunt Flo lini? Bado unawasiliana na familia ya Masawe?"

Lisa alipigwa na butwaa, kisha akamcheka Alvin kwa ushamba wake. Hakumwambia kitu lakini, shangazi Flo ni jina la kificho la hedhi.

Alvin, ambaye siku zote alikuwa akijiona kuwa ni mtu mwenye ujuzi wa kila aina ya mambo, alikohoa kwa utulivu. "Wewe ni mzuri sana katika kusema uwongo, sivyo?"

"Sitaki kusikia hivyo kutoka kwako." Lisa alirudi nyuma. “Kwa nini unanifuata hata hivyo? Miye naenda kazini."

"Nina njaa. sijala.” Alvin alimtazama kwa macho ya kudeka.

"Hiyo sio kazi yangu. Kwani mimi ni chakula, si umekiacha chakula kule mgahawani? Sitajali hata kama ukifa kwa njaa.” Lisa naye akamjibu kijeuri.

Hali ya ujeuri na isiyo na huruma ya mwanamke huyo ilimfanya Alvin kuudhika. Kwa kweli hakuwaelewa wanawake. Hisia zao zilibadilika badilika kwa ghafla.

"Usiponilisha, nitakufuata kwenye kampuni."

Lisa alitaka kupasuka kwa kicheko. “Nikulishe? Ndugu, wewe ni mbwa au paka?” Lakini, kusema ukweli, yeye pia alikuwa hajala na alikuwa akihisi njaa kidogo.
Kuchungulia dirishani, nuru fulani ilimulika machoni mwake alipopata wazo. “Haiwezekani nikupikie, kwa hiyo tutakula mgahawani. Ninachagua. Ikiwa hupendi, basi utabaki na njaa yako."

Alvin akamtazama na kushindwa kumkatalia. Kwa sababu fulani, alitaka kukaa naye kwa muda mrefu kidogo. “Sawa.”

Dakika kumi baadaye, watu hao wawili walisimama kwenye mlango wa mgahawa wa kihindi. Alvin alisita na kumkazia macho. Alikuwa akifanya hivi makusudi. Alijua kwamba tumbo lake lilikuwa na shida na hakupenda vyakula vya pilipili na viungo vikali, lakini Lisa alijifanya hajui na kuingia moja kwa moja kwenye mgahawa.

Sura ya 60

Baada ya kuingia, aliagiza chakula chenye viungo mbalimbali, kama unavyojua tena vyakula vya kihindi. Alijua Alvin alikuwa na aleji na pilipili na alitaka kumkomesha tu. Lisa alikuwa wa kwanza kuagiza bila kujali hata Alvin angekula nini. Alvin alichukia sana na hata mhudumu alipomuuliza oda yake alibaki kimya tu kama bubu. Chakula kilipofika, Lisa alichukua kipande cha nyama na kukiweka mdomoni baada ya kukizungusha kwenye bakuli la viungo kwa muda. Ilikuwa tamu sana, yenye harufu nzuri sana!

Alvin alinyamza kadri inavyowezekana. Lisa alikuwa amezingatia kabisa chakula chake na hakumtazama hata kidogo. Ingekuwa kama zamani, bila shaka angeagiza kile anachopenda na kisha akaanza kumkaribisha Alvin kwa shauku kabla ya kula. Sasa, hakufikiria tena juu yake. Ni kana kwamba hakumwona kabisa.

Ghafla alihisi kujaa kifuani mwake na akaamuru kwa sauti ya jeuri, "Niagizie chakula."

“Huna mdomo? Ikiwa unataka kula, basi fanya mwenyewe." Lisa hakuinua hata kichwa chake. Mashetani yake yalipanda, lakini hakuwa na chaguo ila kuchukua kipande cha nyama kutoka kwenye sahani ya Lisa.

Baada ya kutia mdomoni, uso wake mzuri ulibadilika na kuwa wa ajabu kutokana na uvile viungo na akatema ile nyama pamoja na maneno, "Uliagiza nyama ya aina gani?"

“Kwani nimekulazimisha kula chakula nilichoagiza mimi? Si uagize cha kwako?” Lisa alichukizwa.

Alvin akatabasamu kwa ujeuri. "Unajaribu sana kunichukia."

Lisa alikunja uso na kumwangalia. “Nimekuwa nikipenda kula chakula cha pilipili nyingu, lakini ili kukuhudumia, sikuweka pilipili kwenye chakula nilichokuwa nakupikia nyumbani. Sasa, nitakula tu kile ninachopenda kula. Sitajitolea tena kwa mtu yeyote, unaelewa?"

Alvin alihisi mgongano. Alipenda kula chakula cha pilipili? Kwa hiyo alicha kula pilipili kwa ajili yake?. Hata hivyo, mtazamo wake ulimfanya akose furaha sana, na maneno yake yalikuwa ya kijeuri kama zamani. "Unapaswa kujua kwamba sikuwahi kukuambia kujitolea kwangu. Ulifanya mwenyewe."

Lisa alielewa na wala hakumlaumu. Ikiwa angelazimika kumlaumu mtu, basi angejilaumu yeye mwenyewe kwa kuwa mjinga na kujidanganya kuwa Alvin ni mjomba wa Ethan. Aliinamisha kichwa na kuendelea kula.

Baada ya chakula, aliuliza bili kutoka kwa mhudumu. Alipotajiwa gharama, Lisa alisema, "Nitalipa nusu na yeye atalipia nusu nyingine."

Mhudumu na Alvin wote walishangaa. Muda kidogo, Alvin aliweka kijiko chake chini bila furaha. “Iweke chini. Siwaruhusu wanawake kunilipia chakula.”

"Samahani sana, lakini wewe ni mwanasheria, kwa hivyo sitaki kuingia kwenye mzozo wa pesa." Lisa alilipa nusu ya bili na kuchukua begi lake kabla ya kuondoka kwa furaha. Haikuwa rahisi kwake kupata pesa, lakini hakutaka atumie tena pesa ya Alvin.

Alvin alisugua kichwa chake huku maumivu ya kichwa yakiongezeka. Alilipa sehemu yake kwa kadi yake na kumfuata Lisa kwa haraka. Hata hivyo, maumivu makali ghafla yaligonga tumbo lake, na kufanya uso wake mzuri kukunjamana. ilimbidi tu kukaa chini kwanza na kupumzika.

Dakika chache baadaye, Sam alimpigia simu akilalamika kwa hasira. "Alvin, unanifanyia vibaya bwana. Wewe ndiye uliyeng’ang’ania kuja kwenye mgahawa huu, lakini ukaniacha hapa na Kelvin Mushi na wewe ukamteka Shemeji. Umenitia aibu sana. Kama nisingekufichia siri na kumweleza mambo fulani, Kelvin angeshuku kwamba umesepa naye.”

“Wacha ashuku hivyo…aaaasshh” Alvin alikuwa anagugumia maumivu ya tumbo, na Sam akawa ameelewa vinginevyo… “Mshkaji, usiniambie Shemeji na wewe mnaa… Je, mwishowe amefaulu kukunasa? Basi, ngoja nikuache kwanza."

Tumbo la Alvin lilimsisimka kwa hasira huku akimjibu. "Nyamaza! Nilikula pilipili kwenye mgahawa wa kihindi na ninaumwa na tumbo sasa.”

Sam aliona aibu. "Kwa nini ulikula pilipili hata hivyo?" Alvin alikasirika.

“Njoo unichukue. Nunua dawa ya tumbo njiani.” Alvin alimuagiza.

Zaidi ya dakika kumi baadaye, Sam alimuona Alvin akiwa ameinama kwenye nguzo ya umeme iliyokuwa kando ya barabara. Alikimbia na kumpa dawa ya tumbo pamoja na chupa ya maji. Alisema kwa huruma, “Ndugu, tumbo lako ni dhaifu. Kwa nini ulienda kula chakula chenye pilipili? Nani alikupa ujasiri? Celine Dion?"

"Alitaka kula, kwa hivyo sikuwa na chaguo." Alvin aliishusha ile dawa ya tumbo kabla ya kuinamisha kichwa chake ili anywe maji na dawa.

Aliposema kwamba 'hakuwa na chaguo', maneno yalikuwa yamejaa udhaifu na kutokuwa na msimamo. Sam alikosa la kusema. "Kwa hiyo, yuko wapi sasa? Alikutelekeza hapa baada ya kula?"

"Nyamaza." Alvin alimkazia macho. Alifungua mlango wa gari na kufumba macho baada ya kuingia ndani. Alikuwa anaumwa sana hata kuongea hakutaka.

Sam alitazama mwonekano wake ulionyong’onyea na kumpiga picha kwa siri na kutuma kwenye WhatsApp ya Lisa. [Shemeji, Alvin aliumiza tumbo ili akusindikize kula chakula. Ninampeleka hospitali sasa. Lisa, usimkasirikie. Hasemi kwa sauti kubwa, lakini anajali kuhusu wewe.]

“Umepiga picha gani sasa hivi?” Alvin alifumbua macho ghafla na kumpokonya Sam simu. Alisoma alichoandika Sam na kuhisi amepoteza heshima na sifa. “Ninamjali? Nadhani kichwa chako hakina skrubu chache."

“Huu ni mpango wangu wa kumfanya arudi akupikie. Ni mbinu ya kutumia jeraha kushinda dhidi ya adui.” Sam akahema. Ilikuwa ngumu sana kwa Alvin kukubali kwamba alimpenda.
Alvin hakuongea tena. Hata hivyo aliendelea kuutazama ujumbe huo kwenye simu.

Punde simu ikaingia ujumbe. Lisa aliambatanisha ujumbe na nambari hospitalini na kujibu: [Hii ndiyo hospitali bora zaidi ya kutibu matatizo ya tumbo. Mpeleke huko. Ni yeye ndiye alitaka kunifuata kwenye mgahawa wa kihindi. Sio jambo langu….]

Sam aliisugua shingo yake kimya kimya na kunyoosha mkono wake kuelekea kwa Alvin. “Unaweza kunirudishia simu yangu? Nimeinunua si muda mrefu uliopita…”

Kabla hajamalizia, tayari Alvin alikuwa ameivunja vibaya simu hiyo na kuitupa nje ya dirisha. Sam aliuma mdomo kwa hasira ya kimyakimya, lakini alipomtazama Alvin ambaye alionekana kuwa karibu kulipuka, hakuthubutu kumfanya kitu. Sio tu kwamba Alvin alikuwa anaumwa na tumbo sasa, lakini pia moyo wake ulijawa na dalili za maumivu. Hakuelewa ni kwa jinsi gani moyo wa mwanamke unaweza kubadilika haraka hivyo. Lisa alikuwa amempenda hadi kufa siku chaache zilizopita, lakini sasa alikuwa amebadilika kabisa.
•••
Siku chache zilizofuata, Ethan na Sonya walienda tena kuonana na Kelvin Mushi kwenye ofisi za Golden Corporation. Hata hivyo, Kelvin alikataa kukutana nao na hata hakupokea simu. Ethan hakuwa na chaguo ila kwenda kwenye jumba la kifahari huko Mbezi Beach kumtafuta. Lakini, Kelvin alikuwa kwenye safari ya biashara na Lisa aliwajibika kwa kila kitu kwenye saiti ya ujenzi.

"Lisa , unaweza kunisaidia kuwasiliana na mjomba wangu?" Ethan akaenda hadi kwa Lisa. Katika siku chache tu, umbo lake la kupendeza ilibadilika na kuwa baya.

Lisa alimtosa bila huruma. “Kwanini nikusaidie? Sina ukoo na Kelvin mimi, yeye ni mjomba wako.”

Hapo zamani, Ethan Lowe alizingatiwa kuwa mmoja wa vijana bora zaidi huko Masaki, lakini sasa, alizidi kuwa mbaya na kuzoofika zaidi.

“Usiseme hivyo. Umesahau kuwa tulikua pamoja?" Ethan alisema kwa uchungu, “Ikiwa sitarejesha ushirikiano na Golden Corporation, bodi ya wakurugenzi itaniondoa kwenye nafasi ya mkurugenzi mkuu na nitapoteza haki zangu za urithi…”

“Hilo si jambo langu. Wewe si mchumba wangu hata hivyo. Nenda ukamtafute Lina akusaidie badala yake.” Lisa aliongea huku akila kipande cha andazi. Alikuwa hajala tangu kifungua kinywa na alikuwa na njaa sana.

"Mjomba wangu hampendi Lina." Ethan akamshika mkono. “Lisa , najua unanichukia, lakini sikuwa na jinsi. Nilimchumbia Lina ili niweze kurithi biashara ya familia. Isitoshe, bado sijamuoa. Moyo wangu unajazwa na wewe kila wakati. Je, umesahau hisia tulizokuwa nazo sisi kwa sisi tulipokuwa bado wadogo?”

Lisa alichukizwa sana kiasi cha kupoteza hamu yake ya kula.

TUKUTANE KURASA 61-65

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI......LISA
KURASA.....61-65

Sura ya 61

“Vipi hukuweza kutambua kabla hayajakukuta jinsi ulivyo huna aibu? Umesahau jinsi ulivyonipiga kwenye mlango wa Idara ya ujenzi? Au ulivyonisukuma kwenye tope kwa sababu ya Lina Masawe? Au jinsi ulivyomlipa mtu kufungulia maji kwenye nyumba ili kuniharibia siku chache zilizopita? Ikiwa sikujua kuhusu hilo mapema, sio tu ningehitaji kulipa fidia, lakini kampuni yangu pia ingepoteza sifa.” Lisa alieleza kwa hisia. “Ethan Lowe, ubaya wako unanifanya nipoe, na kutajwa tu kwa uhusiano wetu wa zamani hufanya moyo wangu kuchacha. Lakini wewe? Siyo tu kwamba huna majuto na huna nia ya kuomba msamaha, lakini pia huna haya hata kusimama mbele yangu.”

Uso wa Ethan uliwaka k kutokana na kukaripiwa kwake, lakini hakuweza kusema lolote kutokana na aibu yake. Kwa kweli, alikuwa amekasirika sana siku hiyo na alijutia kitendo chake. Hata hivyo, kiburi chake kilimfanya ashindwe kuinamisha kichwa chake.

Lisa alimtazama huku na kule, kisha akahema ghafla. "Sahau. Usiseme mimi ni mkatili sana. Kwani, je, tatizo si kuhusu Golden Corporation kuondoa uwekezaji wao? Ukirudisha pesa si tatizo litakuwa limeisha? Nilikuwa Kibo Group kwa muda na ingawa sijafahamu masuala mengine, najua kuwa baba yangu bado ana mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 200. Utakuwa mkwe wake wa baadaye, hivyo lazima awe tayari kusaidia.”

Ethan alipigwa na butwaa. "Familia ya Masawe bado ina pesa nyingi hivyo?"

“Pia aliwekeza kwa siri katika makampuni kadhaa, hivyo mapato yake ni mazuri sana.” Lisa alimpa kipande cha ushauri na kuondoka. Alipotoka, alimtazama tena Ethan aliyekuwa amesimama huku akiwa na mawazo, na midomo yake ikiwa imejikunja. Hakuwa amedanganya, lakini hakuwa na hakika kama familia ya Masawe ingekuwa tayari kumsaidia katika wakati huu mgumu.

Ethan haraka aliendesha gari hadi kwenye makazi ya familia ya Masawe. Hata hivyo, safari yake ilikuwa bure. Swali la haraka kwa mfanyakazi wa ndani lilifichua kwamba familia hiyo ya watu watatu ilikuwa imetoka tu kusafiri nje ya nchi siku ya jana yake kwa ajili ya mapumziko.

Ethan alikunja ngumi kwa hasira na kushusha pumzi ndefu kabla ya kumpigia simu Lina, lakini haikuweza kutoka. Siku iliyofuata Lina alimpigia tena. “Samahani, Ethan. Nilikuwa kwenye ndege jana."

"Kwanini hukuniambia kuwa unaenda nje ya nchi?" Ethan alilalamika.

Lina alionekana kumkosea Ethan. “Wazazi wangu wamekuwa katika hali mbaya kwa sababu ya Lisa, hivyo tuliamua kwenda nje ya nchi kutuliza akili na kuacha mambo yatulie. Sikuwa na muda wa kukuambia kwa sababu ulikuwa uamuzi wa dakika za mwisho.”

Ethan alisisitiza shida yake. “Lina, kuna matatizo katika miradi kadhaa niliyowekeza na kuna uhaba wa fedha. Unaweza kumshawishi baba yako kuingiza mtaji?"

“Samahani, Ethan, lakini siwezi kukusaidia. Kibo Group ina matatizo ya pesa kwa sasa pia," Lina alisema, "baba yangu hatakubali."

“Lina, huwezi kufikiria njia? Mimi ni mchumba wako.” Ethan akazidi kubembeleza. “Au hunipendi?”

"Samahani, lakini mimi si msimamizi wa pesa za familia ya Masawe. Mtandao hapa si mzuri, kwa hivyo nitakata simu sasa. Tuongee nikirudi, sawa?” Kisha, simu ikakatwa. Moyo wa Ethan ulikuwa umepoa hadi kwenye mfupa. Huyo ndiye mwanamke aliyedai kumpenda, lakini hakuwa tayari kuomba msaada kwa ajili yake.

Punde,alipokea simu kutoa ofisini kwake, Lowe Enterprises, akakimbia kwenda huko kwa ajili ya mkutano wa wanahisa. Maswali ya wanahisa yalikuwa ni mengi na magumu!

“Ethan, umekuwa ukienda Golden Corporation siku chache zilizopita, lakini je, umeshatatua tatizo? Kwa nini bado wana nia ya kufuta ushirikiano?”

“Mwanzoni, ni nyinyi mlioapa kwamba mpango huu unawezekana. Je, unajua kampuni imewekeza kiasi gani cha fedha?”

"Unaweza kufanya hivi au la?" Akikabiliwa na shutuma za wanahisa, Ethan aligeuka rangi.

Wakati huo, mtoto wa nje wa babake, Percy Lowe, alisimama na kusema, “Acheni kumshinikiza kaka yangu. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Ingawa Golden Corporation imeghairi ushirikiano na sisi, nimezungumza na bosi wa Helios na yuko tayari kushirikiana nasi. Ataingiza mtaji wake mara baada ya kukaa kikao na bodi ya wakurugenzi kujadili mkataba.”

"Helios pia ni biashara kubwa. Percy Lowe ana uwezo kweli kweli." Wanahisa wakaanza kuteta kwa sauti

"Ndio, bora zaidi kuliko mtu kaka yake ambaye anachojua pekee ni jinsi ya kuchumbia wanawake tu.”

Ethan alimkodolea macho mtu aliyezungumza. “Thubutu kusema hivyo tena!”

Mtu huyo alikuwa meneja mwanamke wa kampuni hiyo. Alisimama na kusema, “Nimekosea? Ni nani ambaye hajui kuwa mkurugenzi mkuu Ethan Lowe alimwacha mpenzi wake wa miaka mingi na kumchumbia dada yake ili kuwa mrithi? Si hivyo tu, hata alipita juu ya wengine ili tu aweze kuhesabiwa haki kama mrithi. Ni aibu iliyoje kwa Lowe Enterprises!”

“Hiyo ni sawa. Mwenyekiti Lowe, huyu mwanao anahitaji kufundishwa ipasavyo. Fadhila zake hazifai nafasi yake,” mwanahisa mwingine alimwambia Zacharia Lowe.

Zacharia alifedheheshwa kabisa na aliweza kusema tu kwa upole, “Ethan, acha Percy asimamie nafasi yako kama mkurugenzi mkuu kwa muda. Sio lazima ushiriki katika miradi ijayo ya kampuni.”

Ethan hakuamini. “Baba…”

“Umenivunja moyo sana.” Zacharia aliondoka mara baada ya kutoa maagizo.

Baada ya mkutano, Percy alimwendea Ethan na kutabasamu kwa furaha. “Usijali, Kaka. Nitasimamia kampuni vizuri, kwa hivyo unaweza kujiunga na idara ya usafirishaji bila wasiwasi." Percy alitoka nje ya chumba cha mikutano na kusikia sauti ya kitu kikivunjwa ndani ya chumba hicho. Wala hakujali. Mtu anayesimamia Lowe Enterprises alikuwa amebadilika.

Habari zilienea mitandaoni na mitaani mara moja. Habari za jambo hilo zilipomfikia Lina, ambaye alikuwa mbali na nyumbani, alikasirika sana hivi kwamba akakaribia kuvunja kikombe chake cha chai kilichokuwa mononi mwake. Hata hivyo, alijizuia na kurukia mikononi mwa mama yake badala yake. “Mama nifanye nini sasa? Ethan si mrithi wa Lowe Enterprises tena. Hana hata nafasi ya ukurugenzi kwa sasa.”

Mama yake alimpapasa Lina mgongoni, moyo ukimuuma. Binti yake alikuwa na bahati mbaya sana. Hii inawezaje kutokea mara tu baada ya kuchumbiwa? “Yote ni makosa ya Lisa.” Lawama zikamshukia Lisa tena. “Nitashughulika naye mapema au baadaye.”

Jones aliwatazama wawili wale, mama na binti. “Lazima tubadilishe mchumba wa Lina. Ni wanaume bora tu ndio wanaostahili binti yangu."

"Lakini kila mtu anajua kwamba Ethan ni mchumba wangu sasa," Lina alisema, kwa uchungu. "Ikiwa nitakatisha uhusiano wangu naye sasa, jamii itazungumza nini juu yangu?"

Jones alitabasamu kwa maana. "Ikiwa atarudi kwa Lisa kinyemela, basi hakuna mtu anayeweza kukulaumu."

Alipomaliza kuongea akavuta picha kadhaa kwenye simu yake. Zilikuwa ni picha za Ethan na Lisa. Walikuwa wamechukuliwa kwenye mlango wa Mlima wa Kilimanjaro ambapo Ethan alionekana akiwa amemkumbatia Lisa.

Macho ya Lina yakaangaza. “Baba umepiga lini hiyo picha? Unashangaza.”

"Picha ni za siku kidogo na walipiga wao wenyewe. Nilipojua kwamba Galden Corporation iliondoa ufekezaji wake kwenye kampuni ya Lowe Enterprises, kwa kweli ilibidi nianze kufikiria jambo la kukuokoa mwanagu kutoka kwenye uchumba wa Ethan, hakufai tena." Jones alisema kwa upole.

Sura ya 62

Lisa alijua juu ya jambo hilo la Ethan kuvuliwa ukurugenzi wa kampuni kutoka kwa Pamela wakati aliporudi jioni.

"Safi sana! Huyo fisadi hatimaye amepata anachostahili." Pamela alimkumbatia Lisa kwa furaha. "Asante, mjomba mpendwa."

Lisa akashtuka. “Usimtaje Alvin. Utaniumiza kichwa.”

“Hehehe. Simaanishi Alvin, namaanisha Kelvin” Pamela alibadilisha mada kwa aibu. “Unafikiri Lina ataendelea kuwa na Ethan?”

"Si rahisi, lakini nadhani hivi karibuni atavunja uhusiano wake na Ethan." Lisa alijibu akionekana kusisimka kutokana na taarifa hiyo.

Pamela alipepesa macho kwa umbea. "Hapana. Ina maana hampendi Ethan bila kuwa na cheo kenye kampuni yao?”

Lisa alitabasamu kwa unyonge. "Watu wasio waaminifu kama yeye huweka masilahi yao kwanza. Isitoshe, wazazi wangu pia ni watafutaji wa fursa tu za maslahi, kwa hiyo watamwacha Ethan hivi karibuni kwa kuwa amepoteza cheo chake kama mrithi.”

“Hii inahitaji kusherehekea. Twende kwenye baa tukafurahie usiku wa leo.” Pamela akauvuta mkono wa Lisa. Lisa alikubali kwa urahisi tu. Muda mrefu ulikuwa umepita tangu atoke nje kwenda kuenjoy. Hata hivyo akiwa anatoka nje ghafla alipokea simu kutoka kwa Alvin. Alitazama skrini ya simu na kuikata.

Punde Alvin alituma video. Charlie alikuwa akihangaika huku na kule na kuachia milio ya maumivu. Lisa alifadhaika sana hivi kwamba alimpigia simu mara moja.

"Charlie anakaribia kujifungua?" Lisa aliuliza kwa wasiwasi.
"Kwa hivyo uko tayari kunipigia simu sasa kwa sababu ya Charlie si ndiyo?" Sauti ya Alvin ilikuwa kali sana.

“Nimekuuliza swali!” Lisa alikereka ghafla. Alikuwa na wasiwasi na Charlie kwani kwani alimtunza muda mrefu kidogo, hivyo alimjali kiasi chake.

"Anapata shida kujifungua." Alvin alipunguza jeuri yake na kujibu kinyonge.

"Basi mpeleke kwa daktari wa mifugo!" Lisa alipiga kelele kwa hasira. Angewezaje kuvumilia kuruhusu paka mzuri kama huyo kuteseka?

“Sasa ana uchungu, ni mkali sana kwa hiyo siwezi kumsogelea. Afadhali uje. Charlie anakumiss na anahitaji faraja yako kwa wakati huu. Bila shaka, lolote likitokea, bado unaweza kumuona kwa mara ya mwisho.”

Lisa alimrukia. “Usiongee upuuzi, nakuja sasa hivi.”

"Harakisha. Ninahofia hatashikilia muda mrefu zaidi.” Alvin alikata simu baada ya kuongea. Alikuwa hafai kwa hasira. Alipokuwa na maumivu ya tumbo hapo awali, Lisa alimtupia tu nambari ya mawasiliano ya hospitali lakini aliposikia kuhusu Charlie alionekana kuguswa. Alikuwa na wasiwasi zaidi juu ya paka kuliko yeye.

“Lalalala, mdogo wangu kipenzi Lisa, nimeshamaliza kujipodoa basi twende.” Pamela alikuwa amebadilika na kuvaa nguo ya mtoko na akatoka kwa kujishebedua. “Ninaonekana mrembo?”

“Pamela, samahani sana lakini, Charlie anajifungua sasa hivi lazima niende. Hatupaswi kutoka usiku wa leo.” Lisa alimtupia maneno machache na kutoka nje ya mlango kwa haraka.

Pamela akamshangaa tu "...Je, umekuwa mkunga wa paka?" Hata hivyo kilichomjibu ni sauti ya mlango kufungwa.

Pamela alichukia sana. Ilikuwa imemchukua muda mrefu kabla ya hatimaye ya kupata vazi hilo, lakini Lisa alimwacha kwa sababu ya paka?

Lisa alikimbia kwa kasi hadi kwa Alvin, mtaa wa Buzwagi. Alipofika mlangoni, aligundua kuwa nenosiri lilikuwa halijabadilishwa. Taa za chumbani zilikuwa zikiwaka. Alvin alikuwa amechuchumaa mbele ya chumba alichokuwamo Charlie, akitazama ndani kwa utulivu. Alikuwa kama baba mzee anayesubiri binti yake mpendwa ajifungue.

"Vipi? Amejifungua?" Lisa alikuwa na wasiwasi.

“Ndiyo.”Alvin alimtazama kwa sura tata. Tangu alipohama, alikuwa ameanza kuvaa ujana zaidi. Usiku wa huo, alivaa kitopu cha mikono ya kwapani pamoja na kimini cha magotini chini kilichombana kiasi. Chini zaidi kulikuwa na soksi nyeusi na buti fupi ambazo zilizunguka vizuri kwenye miguu yake myembamba, zikionekana kuvutia sana.

Lisa hakuwa katika hali ya kuona macho yake. Alikimbilia kwenye chumba cha paka na kumuona Charlie akiwa amelala kwenye blanketi kwa unyonge. Karibu naye kulikuwa na paka watatu wadogo sana. Paka walikuwa wamefunga macho yao na bado walikuwa na unyevunyevu. Ni wazi walikuwa wametoka tu tumboni mwa mama yao. Moyo wake ulikaribia kuyeyuka. "Wanapendeza sana."

Alvin akaingia ndani. “Ni wazuri?”

“Jinsi walivyoa cute?” Lisa aliongea kwa upole. Alionekana kuwapenda. Manyoya yao yote yalikuwa yametandikwa na walionekana kama panya wenye vipara.

“Unawapenda?” Alvin akamtazama.

“Bila shaka. Ni nani ambaye hatapenda paka wadogo kama hawa?" Lisa aliwapiga picha kwa kamera ya simu yake. Aliwapiga wale paka picha kadhaa kisha akampigapiga Charlie mgongoni kwa kumpongeza. “Charlie, umefanya kazi kubwa. Wewe ni jasiri sana. Wewe ni bora kuliko wote."Charlie aliinama kwa nguvu, akiwa amechoka kabisa.

"Ana njaa," Alvin alisema kwa jeuri.

Lisa aliwaza hivyo pia. Kuzaa ilikuwa kazi ngumu. “Nitamtengenezea kitu kitamu.”

Taa na jiko ziliwaka na Lisa akavaa aproni aliyokuwa akivaa hapo awali. Alvin alisimama nyuma yake na kumwangalia Lisa akichagua viungo vya chakula cha paka. Jambo hilo likimpendeza macho na kumkumbusha mapishi ya Lisa. Hakika, tumbo lake lilisikika likianza kudai kodi yake ghafla. "Nina njaa pia.”

Lisa alijifanya hamsikii, Alvin akamwendea na kumpulizia sikioni. “Nimesema nina njaa. Umenisikia?” Macho yake yalitetemeka, na karibu adondoshe mwiko.

Kuangalia nyuma katika uso wake handsome, alitoa tabasamu kidogo. "Bw Kimaro, nakumbuka kukusikia ukisema kwamba mimi ni mchafu kama wanawake wanaosimama kujiuza kando ya barabara na kwamba hutaki kula chakula changu tena kwa sababu kitaharibu hamu yako.”

Uso mzuri wa Alvin ukakakamaa kwa muda. Alikuwa amesema hivyo? Hata kama alikuwa naamesema ilikuwa ni sababu ya hasira tu. Kulikuwa na haja gani ya yeye kukumbuka jambo hilo tena?

“Nilikuwa… Huwezi kujua ninapozungumza kwa hasira?” Akainua uso mkali. “Ni mwanamume gani anayeweza kubaki mtulivu na asikasirike anapoumizwa kwa njia zisizofaa? Unamaanisha kwamba sina haki ya kukasirika tena kwa sababu mimi ni mwanaume?"

Lisa aliishiwa nguvu. Sawa. Alikuwa mwanasheria. Alikuwa bora katika kukanusha maneno.

“Pika.” Alvin aligonga meza ya jikoni alipokaa kimya.

“Sawa, nitapika.” Kwa jibu hilo, Alvin alifunua tabasamu.

Ingawa hakuwa pale kwa muda, friji ilikuwa imejaa viungo. Kwa kweli, vyote viilikuwa viungo vya gharama kubwa na vya ‘premium’. Alipika nyama ya mchuzi na sambusa za paka kwa ajili ya Charlie. Ilipofika zamu ya Alvin, bila mpangilio akapiga nyama ya ng’ombe, akajaza viungo vingi sana pamoja na kijiko kikubwa cha pilipili halafu akamsongea na ugali mgumu wa kisukuma.

"Nimepika tu kwa haraka haraka." Alvin alitembea na kuganda alipoona sahani ya ugali na bakuli la nyama lililojaa mchuzi. Kisha, akatazama kwenye mlo wa Charlie. Ilikuwa ni tofauti kati ya mbingu na dunia.

“Meow.” Charlie alikuwa hajala chakula cha Lisa kwa muda mrefu na kwa furaha akaingia kwenye mchuzi wa nyama na kuanza kuramba. Kilikuwa kitamu sana.

Alvin alicheka. "Kwa hiyo paka amekuwa wa muhimu kuliko mimi, sivyo??"

“Nadhani uliniita hapa kwa ajili ya paka, au umesha sahau?.” Lisa alicheza na paka. “Hata hivyo niliishi kwenye hii nyumba kama mhudumu wa Charlie. Laima awe muhimu kwangu.”

"Unanijibu jeuri?" Alvin alimtazama na ghafla akatabasamu.

“Kwani nimekosea nini?” Lisa alipomaliza kusema sura ya Alvin ilibadilika huku akimtazama moja kwa moja kwenye macho yake meusi. "Kwani chakula nilichokupikia hakijakufurahisha?"

“Unanipikia chakula gani hiki, mchuzi kama maji ya bahari?” Alvin aliongea kwa hasira na kukata tamaa. Alichomeka kidole kwenye ugali kikagoma hata kupenya. “Ugali gani huu kama mgumu kama jiwe?”

Lisa alihisi hitaji la kumweka wazi kabisa. "Ninakubali kwamba hapo awali nilikufuata bila aibu na hata nikatumia njia zisizofaa kukupata. Huenda nilikuwa nimepagawa wakati huo. Sikulaumu kwa majina uliyoniita kwani ulichosema kilikuwa sahihi. Uhusiano kama huu una maana tu ikiwa pande zote mbili zinapatana. Isitoshe, uliniokoa mara mbili hapo awali, sawa! Lakini na mimi nimekuwa yaya wako kwa muda mrefu sana, kwa hivyo wacha tuseme mimi na wewe basi. Hakuna anayemdai mwingine chochote.”

Sura ya 63

Alvin alisimama na kutabasamu kijeuri. "Ulinisumbua sana hapo awali. Mambo yote uliyofanya na mambo yote uliyosema, unayafuta kwa maneno rahisi tu ya 'Labda nilikuwa nimepagawa'?Hapo zamani, ni nani aliyesema kwamba alifurahi sana kwa sababu ya kukutana na mpenzi wake? Ni nani ambaye aliapa kwamba atakuwa mwema kwangu peke yangu na kufanya yote aliyoahidi? Ni nani aliyesema kwamba dosari zangu zote ni sifa machoni pake na kwamba alipenda sauti yangu?" Alvin alimkumbusha Lisa aliyeonekana kusahau.

“Aa…” Lisa alipigwa na butwaa, “Ni kweli lakini nilikosa sapoti yako. Kwa hiyo kwa sababu nilisema hivyo ndiyo unanichukulia mjinga na zezeta?”

Alvin alimtazama kwa ukali kwa muda kabla ya kucheka kwa hasira. “Wacha kujifanya mjanja wewe. Wewe ndiye ulikuwa ukinichukulia mimi kama zezeta. Unajifanya bingwa wa kuahidi mambo makubwa lakini huna uwezo wa kuyatekeleza.”

Lisa alimwangalia kwa tahadhari Alvin aliyekuwa kakasirika sana kiasi kwamba angeweza kumkwida muda wowote. Alirudi nyuma kwa hofu. "Basi sawa. Kwa hiyo nikiyatekeleza hayo uliyoniahidi, utaendelea kunipenda?"

"Endelea kuota." Alvin mara moja alilipuuka kama simbamarara ambaye mkia wake ulikanyagwa. Sauti yake ilienda juu zaidi. “Kwa mapenzi gani na wewe?” Bado alikuwa na sura ile ya kibabe ambayo ilimfanya Lisa akose raha.

“Unafikiri wewe ni nani?” Lisa naye uzalendo ukamshinda akatema maneno ya kejeli. “Wewe umesoma na mimi nimesoma. Wewe ni mwanasheria, na mimi ni mbunifu mkubwa wa majengo. Unapata pesa na na mimi napata pesa. Naweza kuishi bila kukutegemea sawa?"

Alvin alimpandisha juu na chini. Akili yake ilionekana kukazia kwenye swali la 'Unafikiri wewe ni nani?' Je, mwanamke huyu hakujua yeye ni nani? Kweli hakujua. Na yeye hakutaka kabisa ajue.

Lisa aliendelea kusema kwa dharau, “Kama usingelikuwa rafiki wa Sam Harrison bila shaka hakuna ambaye angekuwa anakufahamu hapa mjini.”

Alvin alihisi tumbo linamuuma kwa hasira. Lisa alipomwona amenyamaza alifikiria kuwa alikuwa amemtia heshima yake. “Kama hutaki kula chakula basi kitupe mbali. Kwa vyovyote vile, sitakupikia tena. Ngoja niliweke wazi hili, nilikupikia hapo awali kwa sababu nilikuwa nakaa kwako. Kwa kuwa sasa sikai kwako, sina jukumu la kukupikia tena.” Lisa alimtazama usoni huku akiongea na hakuthubutu kubaki tena. Alisimama na kuchukua mkoba wake ili aondoke.

Macho ya Alvin yalimtoka kwa nguvu, na sauti yake ilijaa chuki. "Lisa Jones, kati ya wanawake wote ambao nimekuwa nao hapo awali, wewe ndiye uliyenisumbua zaidi. Ulinipenda kweli?”

Mapigo ya moyo ya Lisa yalidunda kwa kasi huku akimkazia macho, ghafla akajiona mwenye hatia. Kweli hakuwa na mapenzi naye ila alimfuata tu kwa sabau ya Ethan. Je, angewezaje kusema ukweli kwamba alikuwa amemfuata tu kwa sababu alidhani ni mjomba wa Ethan Lowe? Sasa kwa kuwa alijua si mjomba wa Ethan, kwa kweli asingeweza kuendelea kumpotezea muda. Bila shaka angeweza kufa ikiwa angemwambia ukweli.

"Jibu swali langu." Alvin alimshika mkono wake kwa nguvu na kumweka pembeni ya meza ya chakula.

"Bila shaka, nilikupenda." Lisa alituliza akili yake na kujaribu kujizuia asionekane anadanganya. “Wewe… wewe ni mzuri sana, kwa hivyo nilivutiwa nawe nilipokuona…”

"Kwa nini umeacha kunipenda?" Alvin aliinamisha kichwa chini.
Harufu nzuri ya mwanamke huyo ilimkumbusha kuhusu busu katika mgahawa hapo awali, na kumfanya atamani kumbusu tena.

Kichwa cha Lisa kilisisimka huku akisema bila mpangilio, “Kwa sababu… Kwa sababu baada ya kukaa na wewe niligundua kuwa hunipendi. Kila nikiwa na wewe nakosa amani kabisa, nahisi ninampenda mtu asiyenipenda hata kidogo, kila mara unanikasirikia tu!”

Midomo myembamba ya Alvin iliyokuwa karibu kumpiga busu ilitulia ghafla. Macho yake yalififia taratibu huku hasira zikipanda kifuani mwake. “Kwa kuwa unanipenda, hupaswi pia kupenda hasira yangu? Je, hisia zako ni duni na za juujuu tu? Ulikuwa unacheza na mimi?"

Miguu ya Lisa ilikuwa ikitetemeka kwa hofu. Alitaka kulia. Nini kilimpeleka kwa Alvin usiku huo? "Nilikosea, nisamehe! Tafadhali niruhusu niende.”

Moyo wa Alvin ulishikwa na maumivu yasiyoeleweka. “Ondoka nje.” Hakuweza kudhibiti hasira yake na kumsukuma chini. “Sitaki nikuone tena.”

Nguvu za Alvin zilikuwa nyingi sana, na Lisa aliishia kupiga goti sakafuni alipoanguka.
Alijilazimisha kusimama, na kuongea pia akiwa na hasira. “Kama si Charlie, unafikiri ningekuja hapa? Wewe una hasira na mihemko, nani anaweza kukuvumilia?” Kisha, kwa haraka akakimbia kuelekea nje. Wakati huo, aliapa hatorudi tena!

Ndani ya nyumba, hasira ndani ya kifua cha Alvin zilikuwa zikifukuta kama ‘pressure cooker’ Alishika chakula alichopika Lisa kwa lengo la kukimwaga, lakini akakumbuka kwamba hakuwa amepata chakula kizuri kwa siku kadhaa. Aliweka hotpot la chakula chini na kuvunja kikombe badala yake.

Moyo wa Alvin ulikuwa mtupu na uliokosa raha. Kwanini alikasirika kwa sababu ya mwanamke yule? Alisema kwamba hawezi kumvumilia. Je, alikuwa amesahau maneno yote matamu aliyosema hapo awali? Alibadilika haraka sana kana kwamba alikuwa anaigiza. Sawa. Hakutaka arudi tena. Hakufikira kumsamehe tena hata kama angerudi kwake na kumsihi.
Alikula chakula kile kwa chuki. Nyama ile ilikuwa na viungo vya ajabu sana, na pilipili nyingi kiasi kwamba tumbo lake lilianza kumuuma tena. Hata hivyo maumivu aliyoyapata tumboni hayakuweza kulinganishwa na maumivu ya moyo wake.

Sura ya 64

Lisa aliporudi nyumbani kwa Pamela, Pamela alimtania na kusema, “Hey, umerudi? Nilidhani ungelala huko usiku kucha.”

“Unawaza nini? Nilienda huko tu kwa sababu nilikuwa na wasiwasi kuhusu Charlie.” Kwa kumfikiria Charlie, moyo wa Lisa ulimuuma alipowakumbuka watoto wake watatu waliopendeza.

Pamela akasogea na kukaa karibu yake. "Haufikirii tena kuhusu paka wa kwenye suruali ya Alvin?"

“Unajaribu kusema nini?” Lisa alikunja uso.

Pamela aakacheka na kusema. “Mlikuwa mkiishi pamoja kila siku na hata alikuokoa mara kadhaa. Lazima kamoyo kako kawe kanampendampenda?"

Lisa aliganda, akihisi mgongano kidogo. “Mwanzoni nilimwendea kwa makusudi, lakini niliguswa kidogo alipotuokoa mgahawani dhidi ya kina Janet, aliponiokoa nilipokuwa nikionewa na Zakayo. Kisha, aliniokoa tena nilipokuwa nimefungwa kwenye jumba letu la ukoo. Kwa kweli nilitaka sana kutumia maisha yangu yote pamoja naye, lakini tabia zake zimenichosha na kunifanya nirudiwe fahamu. Yeye siyo mhuni, siyo malaya, wala siyo mlevi, lakini ana ghubu!”

Lisa alitabasamu kwa uchungu. "Mimi ni mwanamke, napenda kutunzwa na kuthaminiwa, lakini kwa Alvin, yote niliyopitia ni kejeli, dharau, na hakuna heshima. Ni kana kwamba kila kitu ninachofanya sio sawa. Ni kana kwamba mimi ni mtu anayechukiza zaidi kwake kuliko nzi. Sina hata uhuru. Nimechoka, na baada ya kujua kwamba yeye si mjomba wa Ethan, ndiyo kabisaa nikachoka. Sina hamu kabisa sasa hivi.”

“Lisa …” Pamela alimpiga bega kwa faraja.

“Ni bora kuwa na wewe.” Lisa alimshika mkono Pamela. “Tunaweza kula pamoja, kupika pamoja, kwenda shopping pamoja, na kupumzika pamoja. Kwa bahati mbaya, bado una Patrick. Ingekuwa vizuri kama ungeweza kukaa na mimi tu.”

"Lakini Patrick pia ana shughuli nyingini sana, kwa hivyo nitakuwa na wewe kwa muda huu." Pamela alimtoa wasiwasi.

Lisa ghafla akamkumkuka Linda Sheba ambaye hapo awali alikuwa na Patrick kwenye sherehe ya uchumba ya Lina na Ethan. "Nilikutana na Linda Sheba kwenye sherehe ya uchumba wa Lina. Ana uhusiano gani na Patrick?”

“Babake Patrick na babake Linda ni marafiki. Baada ya kustaafu kutoka utumishi wa kijeshi, walianzisha biashara pamoja. Patrick na Linda waliishi eneo moja na kukua pamoja. Anamchukulia tu Linda kama dada yake.” Pamela alieleza kwa ufasaha.

“Kwa namna fulani, ninahisi kwamba Linda hamchukulii Patrick kama kaka yake.” Lisa alimtupia jicho la tahadhari Pamela.

Pamela alikaa kimya kwa muda, kisha akasema. “Na wewe unafikiri hivyo pia? Mimi nilikuwa na shaka pia, lakini sina ushahidi.”

"Mchunguze vizuri tu." Lisa alimkumbusha Pamela.

“Sawa.” Pamela aliitikia kinyonge.

Sura ya 65

Wiki moja baadaye, Lina na wazazi wake walirudi Tanzania baada ya likizo. Muda mfupi baada ya kuingia kwenye jumba lao la kifahari, Ethan alimpigia Lina simu nyingine ya whatsapp. Lina alipotazama taarifa ya simu inayoingia, macho yake yalimtoka kwa hasira. Lakini, aliishia kupokea simu. Kwa tabasamu, aliuliza, “Kuna nini, Ethan?”

Ethan alisikiliza kwa upole wakati sauti ya upole ya Lina iliposikika, lakini, swali lake lilimwacha katika hali ya huzuni. "Ina maana siwezi kukupigia simu mpaka kuwe na kitu?"

"Unafikiria nini? Bila shaka, unaweza.” Lina alimjibu kwa upole.“Lakini bado niko ng’ambo. Na nina ratiba ngumu.”

Ethan alikuwa mahali fulani karibu na lango la jumba lao ambapo alikuwa amemwona Lina na wazazi wake wakiingia. “Kweli?” Ethan alihisi hasira ikiwaka kifuani mwake. “Lakini nilikuona ukiingia nyumbani sasa hivi. Niko nje ya mlango wa nyumba yenu. Kwa nini unanidanganya?” Lina alitazama nje ya dirisha.

Ethan aliendelea kusitasita. "Au, ni kwa sababu mimi si mkurugenzi wa Lowe Enterprises tena kwa hiyo unajaribu kukataa uhusiano na mimi?"

“Sawa. Kwa kuwa unafahamu hilo, sitazungusha maneno.” Kwa sauti kavu Lina aliongeza, “Ethan, ngoja nikuweke wazi, kwa kuwa umeshindwa kuwa mrithi wa Lowe Enterprises, hadhi yako hata hailingani na yangu. Mimi ndiye mrithi wa Kibo Group na nitakuwa na thamani ya mabilioni ya pesa. Kwa kuwa hali ndivyo ilivyo, kuna pengo kubwa kati yetu. Tutengane tu bila kuwa na kinyongo.”

Japo alikuwa anategemea kitu kama hicho kutokea, Ethan hakuamini kumsikia Lina akimpasulia ukweli wake waziwazi. "Lina, sikujua kama ulikuwa ukilenga maslahi yako binafsi katika uhusiano wetu. Uliniambia hapo awali kuwa umenipenda. Uliniambia kuwa uko tayari kujitolea kwa ajili yangu. Kumbe ulikuwa ukinidanganya?”

"Kwa kweli, hayo yote yalikuwa kweli kwa sababu ya hadhi yako wakati huo. Kwa sababu sasa umeshapoteza hadhi yako, acha kunisumbua. Tafuta mwanamke wa type yako!" Lina alikata simu mara baada ya kumaliza kuongea.

Ethan alikaa ndani ya gari kama mzimu uliopotea. Baada ya muda kidogo, alijifunika paji la uso wake na kuanza kulia kwa uchungu. Ni aibu gani iliyomkuta! Katika uhusiano huo, alikuwa akifikiria kila wakati kuwa yeye ndiye alikuwa dereva. Hakujua kuwa alikuwa ameingia kwenye mtego wa Lina.

Alijidanganya kwamba Lina alikuwa kapagawa naye kiasi kwamba angekuwa tayari kufanya chochote kwa ajili yake. Kwa ajili ya Lina, Ethan alikuwa amemuumiza hata Lisa. Alimpiga, akamtukana, akamkosoa, na karibu kumwangamiza. Alijigonga kichwa kwa nguvu akishangaa kwanini alikuwa mjinga kiasi hicho.

Ni Lisa ambaye alikua naye tangu akiwa mdogo Ikiwa Lisa angekuwa katika viatu vya Lina, asingeweza kukata tamaa juu yake. Ethan alikumbuka wakati alipojua kwamba baba yake alikuwa na mtoto wa nje ya ndoa, alihisi kuwa maisha yake yamejaa giza wakati huo. Lisa ndiye aliyekaa pembeni yake na kuendelea kumtia moyo wa kupambana. Aliweza hata kujifunza kupika kwa ajili yake. Kwa nini alikuwa amesahau kuhusu mambo haya yote? Haishangazi mjomba wake alifikiria kuwa kuna kitu kibaya kwake. Haikuwa ajabu Lisa kumfikiria kuwa ni kipofu. Hakika macho na moyo wake vilikuwa vipofu.

Chini ya dakika kumi baadaye, Ethan alipokea simu ya ghafla kutoka kwa mama yake. “Kuna nini Ethan? Lina alitangaza hadharani kwenye Facebook kwamba ameghairi harusi yake na wewe kwa sababu bado una hisia na Lisa ."

Ethan alipigwa na butwaa kwani hakutarajia Lina angefanya haraka hivyo. Mara moja alibofya maelezo mafupi ya page ya Facebook ya Lina na kukutana na post ndefu iliyokuwa na likes na maoni ya kutosha. Alikuwa ameandika hivi: [Msichana asiye na hatia, ambaye alifikiri kwamba alikuwa amekutana na mwenzi wake wa maisha, na kugundua kwamba alimfuata kwa sababu tu ya nafasi yake kama mrithi wa familia.
[Hivi majuzi, wengi wamekuwa wakinikosoa kwa kuingilia mapenzi kati ya mdogo wangu na mpenzi wake. Kwa kweli, sikujua.
[Alisema ananipenda, nami niliamini. Kwa hivyo, nilikubaliana naye kwa gharama yoyote. Nisingejali hata kungekuwa na zogo wakati wa harusi yetu.

[Hata hivyo, niligundua tu kwamba bado ana hisia kwa mtu mwingine. Alijifanya kunichumbia kabla ya hili na alinichukulia tu kama hatua ya kupata wadhifa wake katika kampuni ya Lowe. ili baadaye aje anitupe.]

Kufuatia ujumbe huo, Lina alichapisha picha ya Lisa na Ethan. Kwa upande wa picha hiyo, ilimuonyesha Ethan kuwa na mazungumzo mazito na Lisa huku akimshika mkono na nyingine akiwa amemkumbatia. Aligundua kuwa picha hzo walipiga wao wenyewe wakati huo akiwa na Lisa. Kwa kweli, familia ya Masawe ilikuwa imepanga kumpaka matope Ethan mapema, jambo ambalo lilimwezesha Lina kupata sababu ya kuachana naye.

Ilikuwa ni kwa sababu Kibo Group, Janet, Cindy, na watu wengine walikuwa wame’share chapisho hilo jambo ambalo lilisababisha post hiyo kuongoza katika kutafutwa mitandaoni. Watu wengi walimkosoa Ethan kwa kuwa msaliti, wakimwita mhuni.

Sonya kwa wasiwasi alimuuliza mwanaye, "Una uhusiano na Lisa tena? Umerukwa na akili?”

“Hapana, Mama.” Maneno ya Ethan yalikuwa yamekaa kooni mwake. “Huoni jinsi Lina anavyonirushia matope akijaribu kujiweka mbali nami?”

Sonya alishangaa. Alionekana kufahamu kila kitu mara moja. "Sikutarajia kwamba angekuwa mhusika wa hii kitu. Nilikuwa nikibweka juu ya mti usiofaa. Sasa uko katika kiwango cha chini zaidi maishani mwako, na hapo anajaribu kuharibu sifa yako.”

“Hasa. Sikutarajia hivyo pia. Labda hii ni stahiki yangu." Ethan aliumia sana moyoni.

TUKUTANE KURASA YA 66-70

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.......LISA
KURASA......66-70


Sura ya 66

Ndani ya kampuni ya Ruta Building Design & Construction. Lisa alipojikuta kwenye kashfa ya kuvuruga uchumba wa dada yake kwa kujiingiza tena kwenye mapenzi na Ethan, alitamani kuirusha simu yake. “Lina anathubutu vipi kughushi suala hilo?!”

Lina ndiye aliyempokonya Ethan. Aliishia kumtupa na sasa alikuwa akiwashutumu Lisa na Ethan kwa kumsaliti tena. Zaidi ya hayo, Cindy alizidisha moto wa jambo hilo kwa kutumia nafasi yake kama msanii mashuhuri, jambo ambalo lilifanya watu wengi kumkosoa Lisa.

“Taarifa nyingi mtandaoni ni za uwongo. Usijisumbue kuhusu hilo.” Joseph Ruta, ambaye alikuwa ameona suala hilo likimtatiza Lisa, alimfariji. "Nenda nyumbani mapema ukapumzike ikiwa hujisikii vizuri."

“Sawa.” Hakika, Lisa hakutaka kuwafanya wenzake wamtazame kwa sura ya ajabu. Baada ya kutikisa kichwa, alipakia vitu vyake na kuelekea nyumbani. Nani alijua, aliposhuka tu kwenye lifti umati wa waandishi wa habari za udaku ulikuwa ukimsubiri nje na kumzingira kwa makamera na vinasa sauti. Mvua ya maswali ikaanza kumwagika kwa Lisa.

"Bi Jones, umerudiana na Ethan?"

"Kurudiana pamoja? Kwa kweli, nyinyi hamjawahi kutengana. Nyinyi mlijifanya kuwa mmetengana ili Ethan amlaghai Lina!”

“Tetesi zinasema kwamba una wivu sana na dada yako uliyempoteza kwa muda mrefu. Ni kweli?"

"Kulingana na jamaa wa familia ya Masawe, ulikuwa ukiwaambia wazazi wako kwamba Lina na wewe msingeweza kuishi pamoja, sivyo?"

“Hiyo ni mbaya sana kwako. Ni dada yako wa tumbo moja ambaye ameteseka sana tangu mdogo.”

“Je, unamnyanyasa kwa sababu tu ametoka kijijini? Kuna ubaya gani kutoka kijijini? Unadharau watu wa vijijini, huh?"

Lisa alizungukwa na umati wa waandishi wa habari wakiwa na vinasa sauti mikononi mwao. Alitaka kueleza, lakini hakuna mtu angeweza kuwa na imani juu yake. Waliendelea kumsukuma japokuwa alikuwa amevaa viatu virefu. Mwishowe, alianguka chini. Hakuna hata mmoja wa waandishi aliyemsaidia. Walikuwa wanashughulika tu kumchukua picha za hovyo.

“Mnafanya nini? Pisha njiani!" Ethan, aliyefika pale kwa wakati ufaao, aliona hali hiyo. Hapo hapo akawasukuma waandishi na kumsaidia Lisa kuinuka. “Uko sawa Lisa?”

Badala ya kufarijika, Lisa alihisi kuzama baada ya kumuona Ethan. Hakika, waandishi wa habari walikua na shauku.

“Ni Ethan! Almefikaje hapa mara moja?” Waandishi walipiga kelele.

"Hakika nyinyi wawili mna uhusiano wa kimapenzi."

“Inachukiza kama nini!”

Ethan alipandwa na hasira huku matusi yakizidi kutupwa kwa Lisa na yeye. Alijikuta akiongea kwa hasira. "Zingatia maneno yenu. Yote hayana uhusiano wowote naye. Mimi ndiye niliyekosea. Niliyemuumiza ni Lisa, si Lina.”

"Pah, bila shaka, unamlinda Lisa kwa sababu unampenda." Waandishi waliendelea kupiga kelele.

“Lina ana huzuni kama nini!”

“Hasa. Kwa kweli Lina hana bahati kuwa na dada kama huyo!”

Lisa alimkasirikia Ethan ambaye alikuwa akisababisha matatizo zaidi katika wakati huo muhimu. Lisa na Ethan walishindwa kuondoka, na mbaya zaidi, umati ulikuwa ukiwazuia njia kwa fujo zaidi.

Baada ya zogo kuzidi sana, walinzi wa eneo hilo waliwatawanya waandishi hao kwa haraka. Kwa bahati nzuri Kelvin alikuwa amefika hapo kwa lengo la kwenda kuonana na mkurugenzi wa kampuni ya Ruta Buildind Design & Construction, kuzungumzia maendeleo ya ujenzi wa jumba lake la Mbezi Beach. Alilazimisha kupita kwenye mapengo, nakumkuta Lisa akiwa aanagalagala chini huku mapaparazi wakiwa wanamchua picha. Kisha akawaambia waandishi wa habari kwa ukali.

“Nyie mnamuhoji au mnamtuhumu? Kwanini mnamnyanyasa hivi? Hayo ndiyo maadili ya uandishi wa habari?”

Waandishi wa habari walipoona mamlaka iliyomzunguka Kelvin na mavazi yake ya gharama kubwa, hawakuwa na ujasiri wa kutosha kuendelea na mashambulizi hayo ya nguvu. Lakini, hawakuridhika. "Tunataka tu kuweka uhusiano wao wazi."

"Hawana uhusiano wowote na kila mmoja." Kelvin alimvuta Lisa kwa nguvu na kumwinua kuelekea kwake. “Ni mpenzi wangu. Mkizidi kumsababishia matatizo tena, bila shaka nitafwashitaki nyote kwa kuzusha taarifa zisizo na ukweli.”

Ethan alishtuka. Lisa naye alishtuka. Ikiwa Alvin angejua kuhusu hilo, angedhania kuwa amesaliti ndoa yao. Lisa akiwa amezama kwenye fikra hizo, Kelvin alifikiri kwamba alikuwa ameumia. Akaweka mkono wake mabegani mwake, kisha akamwingiza ndani ya gari.

Ethan akawafuata mara moja. Baada ya kuingia ndani ya gari, aliuliza kwa wasiwasi, "Mjomba Kelvin, ninyi kweli mna uhusiano?"

“Kwa kweli, nilitumia kama kisingizio cha kukanusha uhusiano wake na wewe sasa hivi. Ila anaweza kuwa mpenzi wangu maadamu yuko tayari.” Kelvin alimtazama Lisa akiwa hoi. “Samahani Lisa. Uko tayari?"

Lisa alikosa la kusema. Sasa kwa kuwa alikuwa ameolewa, angewezaje kusema ndiyo? Hata hivyo, ilikuwa ni juhudi ya Kelvin yenye nia njema. Aliitikia kwa kichwa na kujibu kiutata. "Naelewa."

Ethan alishusha pumzi kwa kufahamu kuwa huo ni uongo. "Lisa, mimi…"

“Usiongeze neno zaidi, unanichukiza.” Lisa alipomuona Ethan hasira zilimpanda. “Ethan, unajaribu kunisukuma kwenye matatizo? Unajua kwamba kila mtu anapinga uhusiano wetu, na bado unakuja kunivutavuta mbele ya waandishi wa habari, kama si kuchochea moto ni nini? Nimeshakuachia dada yangu, huridhiki. Unataka utumiliki wote au? Sikuelewi!”

“Mimi… sikuwa na maana ya kufanya hivyo.” Ethan hakujua hata amweleweshe vipi Lisa. Akili yake ilikuwa imejaa mambo chanya ya Lisa na mambo hasi ya Lina wakati huo.

“Nilikuwa sijui chochote, nimekuja hapa kwa sababu tu nataka kukuomba msamaha. Nilipokuona umezingirwa sasa hivi, niliogopa kwamba ungejeruhiwa, kwa hiyo sikuweza kujizuia kukusaidia. Samahani Lisa. Samahani sana. Ilikuwa ni upumbavu sana kwangu kudanganywa na Lina. Sasa hatimaye najua kwamba wewe ndiye uliyenitendea vyema zaidi.”

Hasira ya Lisa ilipungua. Wakati huo huo, bado aliona maneno ya Ethan kuwa ya kipuuzi. “Ujinga gani kusema hivyo? Lina ni mwerevu, mwenye bidii, mpole, na mkarimu, ilhali mimi ni mwovu na mkatili.”

Sura ya 67

Baada ya kusikia maneno hayo ya kejeli, Ethan alifedheheka sana hivi kwamba uso wake mzuri ulijawa simanzi. “Lisa , nisamehe kwa kukuumiza wakati ule. Samahani sana. Nitakujibu polepole kwa maisha yangu yote. Je, uko tayari kurudi kwangu? Ninaahidi kwamba sitarudia makosa yangu tena. Nilikuwa mjinga sana wakati huo. Ulisema kweli kwamba mimi bado ni kijana na ninaweza kufanya kazi kwa bidii peke yangu. Kila kitu kitakuwa sawa mradi tu utakuwa karibu nami." Kisha kusema hayo, alimtazama kwa shauku.

Uso wa Kelvin ukajawa giza. Hakujua kuwa mpwa wake ni mtu asiye na haya. Kilichomtia wasiwasi sana Kelvin ni kwamba Lisa angeguswa na maneno ya Ethan. Baada ya yote, Lisa na Ethan walikuwa na hisia kwa kila mmoja. “Fikiria kwa busara Lisa. Ethan amekusaliti mara moja, na inaweza kutokea mara ya pili…”

“Mjomba Kelvin!” Ethan alifoka, “Najua unampenda Lisa, lakini huwezi kulazimisha uhusiano. Baada ya yote, mimi ndiye ananipenda sana.”

Mabishano yao yalisababisha kichwa cha Lisa kumuuma. Ilimlazimu akatishe mabishano yao kwa sauti kubwa. “Sawa Ethan. Funga mdomo wako! Umeniumiza vya kutosha. Unathubutuje kusema nakupenda?! Huna aibu? Ninachukizwa sana kwa kukutazama tu. Ikiwa muda ungeweza kurudi nyuma, ningetamani nisingekufahamu.” Hakutaka kuhusika tena katika mabishano yao, Lisa alifungua mlango na kutoka nje ya gari moja kwa moja.

“Usiondoke!” Ethan alimshika haraka. “Nipe nafasi nyingine. sitakata tamaa.”

“Kaa mbali nami. Namaanisha kaa mbali." Lisa alimkaripia na kumzuia kumshika.

Kelvin aliingilia kati, “Acha nikupeleke nyumbani. Ethan ndiye anayepaswa kuondoka. Kuna mtu anajaribu kuchochea matukio haya kwa siri. Nitafuatilia.”

"Hakuna haja. Nitatafuta njia ya kukabiliana nayo.” Lisa alitoka mikononi mwa Ethan na kuondoka bila kugeuka nyuma.
Alihisi kuwa angelipuka kwa hasira ikiwa angekaa tena na Ethan. Zaidi ya hayo, hakutaka kuwa na deni la Kelvin.
•••
Upande mwingine, Sam alipokuwa akiitazama video ya Kelvin iliyorushwa mtandaoni akitangaza hadharani kwamba Lisa ni mpenzi wake, alishangaa hadi mwisho wa akili yake. “Alikuwa na uhusiano na Lisa tena.?”

Hali ingekuweje kwa Alvin baada ya kuona hii? Sam aliawaza. Kama kwa kuondoka kwa Lisa tu kulimfanya Alvin aende mahakamani akiwa na uso wa hasira kana kwamba anaenda kwenye uwanja wa vita, ingekuweje baada ya kujua Lisa ana mpenzi mwingine?

Kwa kuongezea, mazingira ya kampuni yake ya mawakili yalikuwa tuli kama maji ya mtungi. Kila mtu alikuwa na hofu. Ikiwa Alvin angejua kuhusu habari hiyo, Lisa angekuwa kwenye maji yenye kina kirefu ambapo angeweza kuzama. Alisubiri aone nini kitajiri.

Ilibidi Sam awasiliane na Hans mara moja ili kumzuia asimpe taarifa Alvin kuhusu tukio hilo. Hakuweza kumfikia Hans baada ya kufanya majaribio kadhaa ya kumpigia simu. Kabla hata hajafikiria nini afanye baada ya hapo, Alvin akiingia kwa hasira kama mbogo mjeruhiwa. Hali ya ofisi ikabadilika ghafla.

“Alvin…” Sama alimuita kwa tahadhari.

“Kama unapanga kunijulisha kuhusu tukio la Kelvin huna haja ya kuniambia.” Alvin aligeuka na kuzungukazunguka mle ofisini kama kichaa. Sam alimtazama Hans ambaye alikuwa amesimama wima.

Hans kisha akasema, “Mimi ndiye niliyemwonyesha. Mwanamke huyu amemsaliti Bosi Kimaro hadharani.”

Sam alishindwa cha kusema.Kwa mawazo yake, iIlibidi Lisa ajiandae sasa. Akakohoa kidogo. "Kuhusu tukio hili, lazima kuwe na sababu ..."

"Kwa nini kila wakati unasimama kwa ajili yake?" Alvin aligeuka ghafla, macho yake yakionyesha hasira kali iliyotokota moyoni mwake. "Ni kwa sababu unampenda?"

Sam karibu kuuma ulimi wake. Maneno yalimkaba kooni.
“Inawezekanaje? Ninajua wazi kuwa sitakiwi kumpokonya mke wa rafiki yangu.

"Hivi karibuni, Lisa hatakuwa mke wangu tena." Hali ya uhasama iliujaza uso mzuri wa Alvin. "Nitampatia talaka yake haraka iwezekanavyo."

Sam alishangaa. "Lakini haujasuluhisha suala la nyumba ya Bibi kimaro … siamini kama umesahau juu ya lengo lililokufanya uone."

'Nitatafuta njia ya kusuluhisha baadaye." Alvin aliinamisha kichwa chini. Alichukua sigara na kuivuta. "Hakuna wanawake wenye heshima huku Bongo. Wengi wao ni wapumbavu. Huna haja ya kuniambia mambo kuhusu yeye tena.”

Alvin aliyaona mahusiano kuwa kama maigizo tu. Dakika moja, mtu anaweza kuwa na upendo, na dakika nyingine mtu anaweza kubadilisha mawazo yake kwa urahisi. Mtu anaweza hata kumdanganya mwenzi wake. Kwa mawazo ya Lisa, Alvin alihisi hamu ya kumnyonga.

Wazo la kuwa huenda Lisa ana uhusiano na Kelvin lilipomjia, alihisi hisia kali za uchungu kifuani mwake. Mwanamke huyo alikuwa mchafu! Sam alijisikia vibaya, akamuuliza ni nini kilikuwa kibaya kwa wanawake wa Bongo. "Una uhakika?"

“Ndiyo. Nisaidie kutafuta nyumba nyingine mara moja. Sitaki kuishi tena mahali ambapo mwanamke huyu ameishi hapo awali. Ni kama namuona anazungukazunguka ndani kila wakati. Ikizingatiwa kuwa Charlie amejifungua watoto watatu, sehemu hiyo ni ndogo sana kwake pia. Nahitaji bustani kubwa zaidi." Alvin alimwambia Sam.

“Sawa.” Moyoni Sam alitatizwa na ujinga wa Lisa . Alvin alikuwa mtu wa nguvu na wanawake wengi wakimgombea. Alishindwaje kujua jinsi ya kuchukua nafasi ya kumweka karibu naye? Ujinga mkubwa!.

Baada ya kugeuka, Alvin alitazama nje ya dirisha. Sam hakuwa na uhakika ni nini kilikuwa kichwani mwake. Hans aliona sigara katika mikono ya Alvin ambayo ilikuwa karibu kuchoma vidole vyake bila habari. Hata hivyo, Alvin hakuonekana kutambua hilo. Hans alimuonea huruma, alihisi kuwa jambo hilo lilikuwa limemtatiza sana Alvin.

Sura ya 68

Siku mbili zilizofuata, Lisa alibaki tu nyumbani. Suala linalohusiana na Ethan na yeye lilikuwa limeenea mtandaoni. Maoni yote yalikuwa yakimkosoa zaidi yeye. Kila mara Pamela aliposoma maoni hayo, yalimkebehi na kumkejeli Lisa.

“Unataka nimtafute kaka yangu ili ashughulikie suala hili?” Pamela alimuuliza Lisa.

"Hakuna haja. Nahitaji mashabiki wengi zaidi wa Facebook,” Lisa alijibu kwa utulivu huku akitikisa kichwa.

Pamela alikosa la kusema. "Hawa wanaokuchukia wako hapa kukukosoa."

"Haters wanaweza kugeuka kuwa fans wangu pia." Lisa alilishughulikia jambo hilo kwa njia nyepesi na kutoa tabasamu la kudharau.

Siku ya nne, alikuwa amepata zaidi ya followers milioni nane.
Alipost video kamili ya Ethan akimvuta pamoja na ujumbe uliosomeka hivi: [Baada ya kushambuliwa kwa siku kadhaa, siwezi kuvumilia tena. Anathubutuje kunirushia matope kwa kutegemea tu picha za zamani? Lina ulimwacha Ethan yote kwa sababu alishindwa kuwa mrithi wa Lowe Enterprises. Ungeweza kusema sababu yako waziwazi badala ya kumlaumu mtu mwingine.
[Lina, wewe pia ni aibu kwa watu wanaoishi vijijini. Tofauti na wewe, wale wa vijijini ni wasafi na wenye moyo mwema.
Unalingana na Ethan vizuri sana kwani nyote wawili ni wasaliti na wanafiki. Yeye alinisaliliti mimi na wewe umemsaliti yeye. Afadhali nyote wawili mrudiane ili kunusuru nyuso zenu.]

Zogo likazuka tena mtandaoni muda mfupi baada ya video kusambazaa. Wale ambao hapo awali walimkosoa vikali Lisa walikuwa wamelipwa kufanya hivyo. Baadaye, watu zaidi waligundua ukweli kupitia video hiyo.

Ukweli ulipodhihirika, wale walioitazama video hiyo, kila mmoja wao alianza kumshambulia Lina kwenye page yake.

[Alikuwa Ethan ambaye alimkumbaia Lisa kwa hiari yake mwenyewe, na baadaye Lisa aliitoa mikono yake. Lazima ulijua juu yake mapema. Wewe ni mbaya kiasi gani kumsukumia lawama mdogo wako!]

[Tazama! Lisa alisema kwamba unaendana na Ethan vizuri. Ninyi nyote afadhali mrudiane.]

[Hiyo ni aibu sana kwenu. Malaika gani b*tch na mnafiki. Wewe ndiye mtu wa kuudhi zaidi. Nenda ukajiue!]

Mtu fulani ali-coment malezi bora ya Lisa na pia mafanikio yake mengi ya ng'ambo. Watu zaidi walianza kuwa makini na Lisa. Kwa kweli, sehemu kubwa ya maoni pia ilijazwa na pongezi kwa Lisa.

[Halo, wewe ni mzuri. Hakika wewe ni role model wangu. Ninakuheshimu sana!]

[Halo! Unaonekana mrembo kwenye wasifu wako wa Facebook. Pia, huna tabia ya kujionyesha kama wanawake wengine matajiri. Mimi ni shabiki wako.]

[Halo, unapatikana? Unaweza kunisaidia ku-design nyumba yangu?]


[Halo, unapatikana? Unaweza kunisaidia ku-design ukumbi wa burudani?]

Ndani ya siku chache tu, watu wengi walikuwa wamemtafuta Lisa mtandaoni ili kudesign nyumba zao. Hata hivyo, Lisa hakukubali maombi yao moja kwa moja bali aliweka tu anwani ya kampuni yake. Kutokana na kuvuma kwa Lisa, Kampuni ya Ruta Building Design & Construction ilijikuta ikigeuka kuwa jina kubwa kwenye mitandao na hivyo kuvutia mkondo wa wateja wengi.

Joseph Ruta alivutiwa sana na namna Lisa alivyoipa umaarufu kampuni yake kupitia mitandao. Harakaharaka akampa bonus Lisa na kumuongezea mshahara. “Kwa sababu yako, kampuni yetu imepokea miradi michache mikubwa yenye thamani ya zaidi ya mabilioni ya pesa. Ulitumia akili nzuri sana kugeuza mambo. Imekufanya kuwa mbunifu maarufu sasa. Inashangaza sana! Kwa sasa wewe ndiye mbunifu majengo maarufu zaidi nchini.”

“Sawa, asante kwa kunikaribisha wakati huo,” Lisa alisema huku akitabasamu.
•••
Wakati huohuo, nyumbani kwa familia ya Masawe, Lina alikuwa akipandwa na hasira. Siku za karibuni, amekuwa akipokea zaidi ya maelfu ya messages za faragha zenye shutuma zinazoelekezwa kwake. Hata akaunti rasmi za mitandao ya kampuni ya Kibo Group ilijazwa na shutuma kali. Lina alianza kuepukwa na wale wanawake matajiri waliokuwa karibu naye. Ikiwa hali hiyo ingeendelea, hakuna mwanamume tajiri ambaye angechagua kumuoa.

Mama Masawe alikuwa kwenye mfadhaiko. Alifikiri kwamba haingefaa kumwambia bintiye, hivyo akamlenga Mzee Masawe. "Binti yetu yuko katika matatizo makubwa kwa sababu ya wazo lako baya."


"Nani alijua kutakuwa na kamera za uchunguzi katika jumba la Kelvin linalofanyiwa ukarabati?" Jones alipandwa na hasira pia. Kutokana na mambo yalipokuwa yamefikia, hakuwa na uvumilivu hata kidogo kwa Lisa. Alichotaka kufanya kwa wakati huo ni kumuua.

Mara tu Jones alipomaliza kuzungumza, James aliingia ndani haraka. “Shangazi, mjomba Jones, kuna jambo baya limetokea. Hoteli ya Lublin inawaka moto."

Mabadiliko makubwa yalionekana katika uso wa Jones baada ya kusikia maneno hayo. Hoteli ya Lublin ilikuwa hoteli ya nyota tano, mali ya familia maarufu ya Zongo ambayo ujenzi wake ulisimamiwa na kampuni ya Kibo Group ambapo kazi za ujenzi zilikuwa zikiendelea. Kufikia wakati huo, zaidi ya shilingi bilioni 5 zilikuwa zimewekezwa katika hoteli hiyo.

“Ni nini kinaendelea? Hali ikoje sasa? Je, moto umezimwa?" Jones Masawe aliuliza maswali dabodabo.

”Moto umezimwa. Hata hivyo, ghorofa tatu zimeharibiwa kabisa na moto huo. Familia ya Zongo tayari inafahamu tukio hilo,” James alibainisha kwa wasiwasi mkubwa. Hatimaye, aliangusha kilio na kupiga magoti chini mara moja. "Mjomba Jones, familia ya Zongo hakika itateua timu kuchunguza suala hilo. Nadhani… nyaya feki za umeme ndizo zilizosababisha moto huo.”

"Ulisema nini?" Jones alimuelekezea macho yake huku akitetemeka. "Ulipata wapi nyaya?"

“Ni Bw. Mayanja ndiye aliyenipendekeza. Alinipa punguzo la milioni chache wakati huo. Unakumbuka kwamba nilikupa ile Volkswagen yenye thamani ya zaidi ya milioni arobaini? Pesa hizo ndio…”

Kabla hajamaliza kueleza upuuzi wake, Jones aliinua mkono wake na kumpiga James kibao usoni kwa nguvu. “Umekuwa ukipata pesa nyingi katika miaka ya hivi karibuni, sivyo? Kwa nini ufikirie kuchukua rushwa kupitia ununuzi wa nyaya? Umeharibiwa na tamaa ya pesa, huh?"

"Nisamehe, mjomba Jones." James aliendelea kuvuta shati lake kwa nguvu. "Nilifanya hivi kwa nia ya kumfurahisha Shangazi na wewe."

“Nawezaje kukusamehe, unifurahishe mimi nilikuambia nina uhaba wa pesa? Familia ya Zongo ni familia ya pili yenye nguvu zaidi hapa Masaki baada ya familia ya Harrison. Mara tu suala hilo litakapobainika, matokeo yatakuwa mabaya." Jones alitikisa kichwa chake kwa masikitiko.

Lina akahema kwa nguvu kisha akasema. “Mbona James ulikuwa mzembe sana? Nakumbuka kwamba ni Lisa ambaye alikuwa meneja mradi wa ujenzi hapo awali kabla yako. Kwa nini hakukuzuia kabisa?”

Akiwa amepatwa na mawazo, Mama Masawe akasema haraka, “Nilikuwa nikitafakari jinsi ya kumpa somo Lisa. Sasa hii ni fursa. Tunaweza kuelekeza lawama kwake. Hatutaweza kuishi kwa amani hadi apelekwe jela. Suala hili likishawekwa hadharani, kila mtu atajua kuwa yeye ndiye aliyehusika na rushwa.

Sura ya 69

Jones alipigwa na butwaa kwa muda. Wakati huo, alishawishiwa na wazo hilo. Aliona kuwa ni suluhisho linalowezekana kwa vile hakujua jinsi ya kujisafisha kutokana na suala hilo. “Sawa basi. Moto uliozuka katika hoteli hiyo hauna uhusiano wowote na wewe. Lisa ndiye aliyekuwa akisimamia ujenzi wa hoteli hiyo hapo awali, na tukio hilo lilitokea kutokana na yeye kuchukua rushwa.”

Lina bado alikuwa na wasiwasi. “Baba, nasikia kwamba Kelvin Mushi amekuwa akimtetea sana Lisa siku hizi. Anaweza kumsaidia.”

"Usijali, familia ya Zongo sio kama familia nyingine yoyote. Wakishaamua kumpa mtu somo, hakuna atakayeweza kuwazuia kufanya hivyo.” Jones alidhihaki.
•••
Katika ofisi za kampuni ya Ruta Building Design & Constructions, Joseph Ruta aliwapanga kuwapeleka wafanyakazi wake kwa chakula cha machana baada ya kikao cha kusherehekea mafanikio ya kampuni. Wakati tu Lisa alipokuwa akipakia vitu vyake kuelekea mgahawani pamoja na wafanyakazi wenzake, maafisa wachache wa polisi waliingia ndani. “Lisa Masawe ni nani?”

Wenzake walitazamana kwa nyuso za wasiwasi. Lisa alihisi kuzama, kisha akasimama na kusema, “Ni mimi…” Mara tu alipojibu, mikono yake yote miwili ilifungwa pingu.

“Sisi ni polisi kutoka Kituo ch Polisi Oyster Bay. uko chini ya ulinzi.” Polisi waliomkamata walijitambulisha huku wakionyesha kadi zao.

“Nimefanya kosa gan?” Lisa aliuliza kwa mshtuko.

Polisi walisema bila kujali, “Moto umezuka katika Hoteli ya Lublin asubuhi ya leo, ambao umesababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni kumi na Kibo Group inadai kuwa wewe ndiye uliyesimamia ujenzi wa hoteli wakati huo. Inabidi uende kituo cha polisi kuchunguzwa."

Lisa alihisi kama kichwa kimemlipuka. “Haina uhusiano wowote na mimi. Ni zaidi ya miezi miwili tangu niachane na huo mradi. Pengine wanajaribu kunifanya kuwa mbuzi wao wa kafara!”

“Samahani, lakini Kibo Group wameleta mashitaka yakiambatana na ushahidi kuhusu upokeaji wako wa rushwa katika matumizi ya nyaya feki. Acha kukataa.” Polisi walimkamata mara moja na kutoka nje. Wakati huo huo, waandishi wengi walikuwa tayari wanasubiri chini.

"Yeye ni mbunifu majengo wa aina gani maarufu? Anatumia nyaya feki ambazo zinaweza kusababisha moto.”

“Mungu wangu! Nimelipia tu Ruta Building Design & Construction kwa gharama ya ukarabati. Nitaighairi na kuomba kurejeshewa fedha.”

"Mimi pia. Nani anajua, nyumba yangu inaweza hata kuteketea kwa moto?"

Kwa muda mfupi tu, wateja wote ambao hapo awali walikuwa wamefanya mkataba na Ruta Building Design & Construction walisitisha mikataba yao na kuomba kurejeshewa pesa. Baadhi ya wateja walikuwa na wasiwasi kuhusu kazi ya ukarabati iliyokuwa ikiendelea na kuja kuiwajibisha kampuni. Sifa ya kuvutia ya Ruta Building Design & Construction hapo awali iliharibiwa kabisa mara moja.

Katika kituo cha polisi, Lisa alihisi kizunguzungu huku mwanga mkali ukimulika kwenye chumba cha mahojiano. Hata hivyo, aliendelea kuongea kwa hasira, “Nimesema kwamba hii haina uhusiano wowote na mimi. Nilikuwa meneja mradi wa hoteli wakati huo, lakini nilinyang’anywa ghafla na James ndiye aliyepewa kuwa msimamizi wa ujenzi. Yeye ndiye anayesimamia nyenzo na vifaa."

“Imetosha, acha kubisha. Bwana Mayanja, ambaye uliiba naye pesa, alisema kuwa umekuwa ukiwasiliana naye. Ulipata zaidi ya milioni sitini kutokana na wizi huo, kisha ukalipa milioni kumi kwa mkuu wako ili asifichue jambo hilo. Miezi miwili iliyopita, hatimaye James alifichua hili kwa Bw. Jones Masawe kwani asingeweza tena kuvumilia tabia yako. Kwa hayo, Bw. Jones Masawe aliamua kukufuta kazi. Una akili kiasi gani kujaribu kukanusha ushahidi wa wazi namna hii?” Polisi sasa ikageuka kuwa mahakama.

Afisa mwingine wa polisi wa kike aliongeza, “Wewe pia unatoka katika familia tajiri, lakini kwa nini unakuwa na tamaa sana ya pesa ukiwa na umri mdogo, au una honga wanaume?”

Lisa alihisi kupigwa na kitu kizito kichwani . “Huu si ukweli. Mimi ndiye niliyemripoti James, lakini kwa namna fulani…”

“Inatosha. Acha kueleza. Hata baba yako amekubali kwamba ni kazi yako. Wewe ni binti yake wa kumzaa, wakati James ni mpwa wake tu.Atawezaje kukusingizia wewe ili kumtetea mpwa wake? Ingekuwa kinyume chake labda ningeamini.” polisi walikatiza hotuba yake.

"Hiyo haiwezekani." Lisa akatikisa kichwa huku akionekana kuchanganyikiwa. Kisha akasimama kwa fadhaa. “Mimi ni binti yake wa kuzaa, lakini kwa nini ananituhumu kwa ushuhuda wa uongo? Je, mimi si muhimu kama mpwa wa mke wake?”

“Acha kuigiza kichaa. Mtoe hapa na umfungie lockup.” Polisi aliagiza.

“Nataka kupiga simu. Nataka kupata wakili wa kuniwekea dhamana,” Lisa alifoka.

“Samahani. Ikizingatiwa kuwa kesi yako ni kali sana, hairuhusiwi kukutana au kuwasiliana na mtu mwingine yeyote kabla ya kesi kufungwa." Polisi walikataa katakata kumpa dhamana Lisa na kumfungia kwa mara nyingine tena.

Chumba kidogo kilijaa watu saba hadi wanane. Kila mmoja wao alipewa kigodoro kidogo sana kwa ajili ya kulalia. Mara tu alipoketi, mwanamke mmoja mrefu alimsogelea na kumwagilia ndoo ya maji kitandani mwake.

"Unafanya nini?" Lisa alifoka. Kundi la wanawake wenye sura mbaya walimvamia mara moja.

"Unathubutuje kunipigia kelele?!" Mwanamke mrefu alikunja mikono yake, kisha akasema kwa ukali, "Unajua, nilimuua mwanamke ambaye alinifokea ndiyo maana niko hapa?"

“Samahani… Unaweza kumwaga upendavyo.” Lisa hakuwa mjinga. Alijua kabisa kuwa haikuwa rahisi kukabiliana na kundi la watu waliofungiwa humo ndani, hivyo alijitahidi kuwavumilia.

Hata hivyo, hawakuwa na mpango wa kumwacha hivyohivyo tu. “Oh, lazima nikufundishe kazi. Ninawachukia zaidi wanawake warembo kama wewe kwa sababu waliwahai kuniibia mume wangu.” Mwanamke huyo alimkimbilia na baadaye akampiga teke.

Kadiri Lisa alivyokuwa akitaka kupiga kelele za kuomba msaada, mtu huyo alimziba mdomo. Muda mfupi baadaye, alihisi kizunguzungu baada ya kupigwa sana. Akiwa ameduwaa, alionekana kusikia mtu akisema, “Endelea kumpiga, muue kabisa. Hakuna mtu atakayetulaumu kwa kumuua.”

"Anastahili kwa vile alimkosea mtu ambaye hakupaswa kukosewa."

Alikuwa amemkosea nani wakati huu? Lina? Jones? Nani angeweza kumwokoa wakati huu? Uhusiano wake na Alvin ulikuwa umekwisha, ambapo Pamela. Pamela hakuwa na uwezo wa kukabiliana na familia ya Zongo pia. Labda Kelvin ndiye angekuwa tegemeo lake kubwa! Lakini alizuiliwa na polisi kuwasiliana na mtu yoyote hadi kesi yake itakapofikishwa mahakamani, angewezaje kuwasiliana na Kelvin?

Sura ya 70

Mara tu Pamela alipopata habari kwamba polisi walikuwa wamemkamata Lisa, aliharakisha hadi kituo cha polisi. Alipofika tu mlangoni, akagongana na Ethan aliyekuwa akitoka na wakili.

“Kwanini upo hapa?” Pamela alianza kuhema kwa hasira baada ya kumwona yule fisadi.

Ethan akamwambia. “Nilikuwa hapa kumwekea dhamana Lisa lakini nimekataliwa. Nimejaribu kuwaambia polisi kwamba Lisa aliondoka Kibo Gruop kwa sababu James alipewa kazi ya kusimamia mradi huo. Kwa maana hii, angewezaje kupokea rushwa? Lakini polisi wamepata ushahidi kutoka Kibo Group Ushahidi wote unamwangukia Lisa. Ni wazi kwamba Kibo Group wanajaribu kumtupa Lisa kwenye hii kashfa.” Ethan alionyesha hali ya huzuni huku akikunja ngumi kwa hasira.

“Oh hapana!” Pamela alihisi hali ya kutokuamini. "Lisa ni binti yake wa kumzaa, na anatarajia kumfunga jela?"

Ethan pia alishikwa na hatia na kusema. “Bila shaka, Lina atakuwa ameingilia jambo hilo pia.”

Wakati huo, Ethan alijutia sana maamuzi yake. Kama asingedanganywa na Lina kabla ya hilo, angeweza kuwa na Lisa. Kwa njia hiyo, Lisa asingeishia katika hali hii.

“Nitapiga simu kwa kaka yangu sasa hivi. Nitamwomba atafute wakili bora zaidi huko nje.” Pamela aliongea kwa hasira.

“Usijisumbue kupiga simu. Nimemleta wakili hapa sasa hivi, na hakuna alichoweza kufanya.” Ethan akamkatisha tamaa Pamela. "Jambo hili linahusiana na familia ya Zongo, kwa hivyo hakuna mtu anayeweza kufanya chochote juu yake."

Moyo wa Pamela ulishuka. Hakika, familia ya Zongo ilikuwa moja ya familia chache sana zenye nguvu huko Masaki. Lisa alikuwa ameiudhi familia ya Zongo. "Kwa hivyo tunaweza kufanya nini ili kumsaidia?"

"Nimemjulisha mjomba wangu aje hapa." Mtazamo wa huzuni na kukata tamaa ulipita usoni mwa Ethan. Ingawa kwa wakati huo Kelvin alikuwa mpinzani wake wa mapenzi dhidi ya Lisa, hakuwa na jinsi zaidi ya kumuomba msaada ili kumuokoa Lisa. “Mjomba wangu ana mtandao mpana. Anaweza kuwa na njia ya kutokea."

"Sawa." Pamela alikuwa amesikia kutoka kwa Lisa kwamba Kelvin alikuwa akivutiwa naye. Kwa hakika, Ethan alilazimika kumtegemea mjomba wake katika nyakati muhimu kama hizi.

Pamela alipokuwa akimwangalia Ethan, macho yake yalizidi kujawa na karaha. Hakuweza kujizuia kumdhihaki. “Baada ya kuachwa na mchumba wako, hatimaye unajua Lisa ni muhimu kwako. Huoni aibu, Lisa tena, huh?”

"Hapo zamani, ilikuwa kosa langu. nilikuwa kipofu.” Ethan alijitetea.

Pamela alikoroma. "Mazingira ya lockup ni mabaya sana. Tangu Lisa alipofungiwa katika jumba la ukoo wao huko kijijini, aliathiriwa sana na tukio hilo. Tunapaswa kumtoa nje usiku wa leo.”

Ethan alipigwa na butwaa. "Ni nini kilitokea kwenye jumba hilo? Nasikia hakupewa chakula na maji, ni kweli?”

“Kwani hukusikia wala kusoma mtandaoni? Alinyanyaswa vibaya sana huko, na karibu apoteze maisha yake.” Pamela alimkazia macho Ethan kana kwamba ni mlemavu wa akili. "Alifungiwa huko kwa siku tatu na madirisha na milango yote ilifungwa. Hakuweza kuona hata mwanga wa jua kwa siku tatu. Nguo alizoingia nazo akiwa amevaa ndiyo hizohzio, hakuwa na blanketi wala shuka. Hakukuwa na umeme wala maji. Hakuweza hata kuwasiliana na mtu yeyote nje na alikuwa karibu kufa katika nyumba hiyo. Kwa bahati nzuri… Kwa bahati nzuri, tulifanikiwa kumuokoa. Alipofika hospitalini, alikuwa karibu kufa.”

Mwili wa Ethan ulitetemeka kwa nguvu. Alikuwa ametembelea nyumba ya familia ya Masawe kuuliza kuhusu hilo, lakini sivyo alivyoambiwa. Sasa alipokumbuka sura za Jones, mkewe na Lina, alishtuka! Hakuweza kufikiria jinsi walivyokuwa wabaya kuwa na nia ya kumuua binti yao wa kumzaa. Walikuwa wanatisha sana!

Haikuwa ajabu Lisa kumchukia Ethan. Ethan alikuwa mjinga sana na hakuweza kuona tukio hilo. Wakati huo, Lisa bila shaka alikuwa amekata tamaa kabisa.

Punde, Kelvin alifika akiwa anakimbia. “Mjomba Kelvin, lazima umwokoe Lisa,” Ethan alimsihi huku macho yakiwa yamevimba. “Hana hatia. Nina deni lake kupita kiasi."

“Iwapo nitamwokoa au la, haina uhusiano wowote na wewe. Yeye ni mpenzi wangu, na bila shaka nitaenda kumwokoa.” Kelvin alipokuwa akiongea, alielekea ghorofani kwa huzuni pamoja na wakili. Nusu saa baadaye, alirudi chini na sura ya huzuni. “Dhamana imeshindikana.”

"Kwanini? Hata wewe umeshindwa?" Pamela alianza kuogopa. Akiwa amepigwa na butwaa, aliuliza, “Je, ninaweza kuomba msaada wa familia ya Harrison?” Pamela alikuwa na namba ya Sam, lakini Lisa na Alvin kwa wakati huo walikuwa na mahusiano mabaya. Haikujulikana kama Sam angekuwa tayari kumpa mkono wakewa msaada.

“Haitasaidia. Nilisikia kwamba familia ya Zongo ina hasira sana wakati huu. Kuingilia kati kwa familia ya Harrison katika suala hilo kutamaanisha kuwa wanaenda kinyume na familia ya Zongo, kwa hivyo Sam hawezi kuthubutu.” Kichwa cha Kelvin kilimuuma. Alikuwa amefikiria njia zote zinazowezekana akiwa njiani kuelekea pale polisi.

“Kwa hiyo hakuna ninachoweza kufanya zaidi ya kumtazama Lisa akiendelea kufungwa hadi hukumu itakapotolewa?” Pamela alikua hana raha. "Hii sio tu ataishia kuwa gerezani kwa miaka kadhaa. Huenda ikaharibu maisha yake.”

“Kweli, Mjomba Kelvin. Tafadhali jaribu kutafuta njia ya kutokea.” Kwa uso uliopauka, Ethan aligeuza macho yake ya kubembeleza kwa Kelvin.

Kelvin alikunja macho kana kwamba vilele viwili vya milima vilibanwa pamoja. “Kuna mtu mwingine ambaye anaweza kusaidia, lakini ni vigumu sana kumshawishi. Yeye ni wakili maarufu wa kimataifa ambaye hajawahi kushindwa. Hajapoteza kesi yoyote hadi sasa, wala hajashindwa kumtoa mtu yeyote jela.”

“Yeye ni nani?” Pamela na Ethan waliuliza kwa wakati mmoja.

"Kimaro. Alvin Kimaro!" Kelvin alitamka kisha akasema, “Kabla ya hili, alikuwa akiishi peke yake kwa miaka mingi huko Kenya. Ghafla alikuja Dar muda mfupi uliopita, lakini ni vigumu sana kumfanya amsaidie Lisa. Hapo awali, nilimwomba anisimamie kesi yangu ya biashara kwa malipo ya shilingi milioni 300, lakini alikataa. Bila shaka, amekataa ofa nyingi, ikiwa ni pamoja na zile za wafanyabiashara na za wanakisiasa. Machoni pake, pesa na madaraka si kitu.”

TUKUTANE KURASA 71-75

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.......LISA
KURASA.......71-75

Sura ya 71

Pamela alikosa la kusema. Alvin Kimaro alikuwa rafiki mkubwa wa Sam anayetoka kwenye familia ya Harrison, familia tajiri na yenye nguvu ambayo pia ilikuwa na urafiki wa karibu na familia tajiri ya Clark Zongo. Kwa hiyo kama Alvin Kimaro angeingia kumsaidia Lisa, basi angekuwa anamweka matatani Sam Harrison. hapo kulikuwa na utata mkubwa. Sam angekubali Alvin achukue kesi hiyo?

“Usijali. Nitamsihi,” Kelvin alisema.

“Uh…” Pamela alitoa kikohozi chepesi. "Ikiwa unamaanisha Alvin Kimaro, hakuna haja ya wewe kumsihi wakati huu. Kwa kuwa alishawahi kukataa kesi yako, anaweza akakataa tena! Nilifahamiana naye hivi karibuni, nitamtafuta nijaribu kumshawishi.”

Wasiwasi wa Pamela ulikuwa kwamba, iwapo Kelvin angeenda kumsihi Alvin, hali hiyo ingesababisha mgogoro wa kimapenzi. Haiwezekani mpinzani wa mapenzi amuombe mume rasmi wa mpenzi wake amwokoe mke wake ambaye alitaka kuachana naye kwa sababu yake. Sio tu kwamba Alvin angekataa kumuokoa Lisa, lakini pia angeweza kumfanya aishie jela milele. Katika hali hiyo, Kelvin alitakiwa aachane kabisa na Alvin.

"Unamjua Alvin Kimaro?" Kelvin alimtazama Pamela kwa sura tofauti.

Ethan naye alishangaa. “Nimesikia kuhusu Bw. Kimaro, ni mtu wa kujisikia sana. Sikutarajia kwamba ungekuwa unamjua mtu kama yeye, Pamela.”

Pamela alisema kwa aibu, "Sijui mengi juu yake, lakini nina rafiki anayefahamiana naye."

"Rafiki yako ni mzuri." Kelvin alisifu. "Tutasubiri habari njema kutoka kwako."

Pamela alishindwa tu kusema, ila alikuwa akimaanisha rafiki yake ni Lisa.
Mara baada ya kuachana, Pamela akampigia Sam simu. “Bw Harrison, nina uhakika umesikia kuwa Lisa amekamatwa na polisi. Inavyoonekana, ushahidi unaopatikana wote ni dhidi yake. Ninge… ningependa kumwomba Bw. Kimaro amwekee dhamana.”

Sam akahema. “Siku hizi, Alvin hataki kabisa kusikia jina la Lisa. Hakika hatamsaidia. Zaidi ya hayo, amefanya uamuzi wa kuachana naye siku chache zilizopita.”

Pamela alikuwa mwisho wa akili yake. “Yuko wapi sasa? Unaweza kunipa nafasi ya kuzungumza naye ana kwa ana?”

"Kwa bahati mbaya, kuna kesi anasimamia nje ya nchi. Alisafiri kwa ndege hadi Nairobi kwa kazi jana na atarudi kesho kutwa.

Pamela alizidiwa na mfadhaiko ndani ya moyo wake. Ilikuwa ni vigumu kumwokoa Lisa usiku huo. “Unaweza kuniambia hoteli anayoishi huko Nairobi? Nitaenda huko kukutana naye.”

Kwa upande mwingine, Sam alikaa kimya kwa muda. Hatimaye alimwambia Pamela anwani. Mafanikio ya dhamana ya Lisa sasa hatimaye yalimtegemea Pamela.

Usiku huo, Pamela alifunga safari ya haraka sana kuelekea Nairobi na moja kwa moja akaitafuta hotel ya ‘Villa Rosa Kempinski’ aliyofikia Alvin. Baada ya kufika hotelini, aligonga mlango wa chumba hicho.

Alikuwa ni kijana mwembamba aliyefungua mlango. Baadaye alihisi hewa ya joto ikitoka kwenye chumba hicho. Mwanamume huyo alivalia shati jeupe na vifungo kadhaa vya shati chini ya shingo vilikuwa vimelegezwa, ikionyesha sehemu ndogo ya kifua chake cha kuvutia.

Alipotazama kifua cha mwanaume huyo, Pamela alipigwa na butwaa. Mwanaume huyo alikuwa akipapasa kidevu chake, macho yake ya kuroga yakionyesha tabasamu la kuvutia.

“Tsk, nyie jamaa kuna mtu aliagiza mwanamke aje. Anaonekana chombo, ingawa…” kijana yule aliongea akiwa kamkodolea macho ya udadisi Pamela.

Uso wa Pamela ulionyesha kuchanganyikiwa. Alihisi huenda alikuwa mahali si penyewe. Hata hivyo, alisikia sauti za watu wakicheza karata ndani ya chumba hicho. Kisha akauliza, “Namtafuta Alvin. Yupo hapa?”

Akiwa ameduwaa, mtu huyo aligeuza kichwa na kutazama chumbani, “Kuna mtu anakutafuta, Alvin.” Kisha kusema hayo akamgeukia tena Pamela na kumuuliza, “ajabu sana, hatimaye leo namuona mwanamke wa Alvin, umemfahamu vipi Alvin?"

"Mimi ni rafiki wa mke wake." Pamela aliusukuma mkono wake uliokuwa ukiuzuia mlango na kuingia chumbani humo huku akihema.

Kulikuwa na wanaume watatu sebuleni, na wote walikuwa na mwonekano wa kuvutia. Mmoja wa wanaume aliyekuwa na sigara inayoning’inia kutoka mdomoni mwake alisema, “Rodney, nimekuomba tu ufungue mlango. Sikukuambia umruhusu aingie!”

"Huwezi kunilaumu." Rodney Shangwe aliketi kwenye kiti tupu. Alichukua sigara na kuiwasha, kisha akamtazama Pamela kwa shauku.

Alvin, akiwa amekaa kwenye kiti cha heshima, alimtazama Pamela kwa kawaida huku akiwa ameshikilia kadi zake. Alitupa kadi kwenye meza na kusema, “mtoe nje.”

“Subiri kidogo.” Pamela alikimbia kuelekea kwa Alvin bila kufikiri mara mbili. “Lisa kafanyiwa njama mbaya na wazazi wake na sasa yuko katika kituo cha polisi. Wewe ndiye mtu pekee ambaye unaweza kumwokoa sasa. Polisi walisema kwamba kesi hiyo itafungwa baada ya siku tatu, na atahukumiwa kufikia wakati huo.”

"Sio jambo langu," Alvin alitamka maneno haya matatu bila kujali.

"Lakini yeye ni mke wako." Pamela alifanya kama kumkumbusha.

Alvin alikunja midomo yake ghafla. “Umekosea. Yeye ni rafiki wa kike wa Kelvin, na maisha yake hayana uhusiano wowote na mimi. Potea haraka!” Kutajwa kwa jina la Lisa kuliharibu hisia zake.

“Inatosha. Alvin anataka upotee. Fanya haraka uondoke sasa hivi.” Rodney, ambaye alimruhusu aingie, akamkokota kuelekea mlangoni.

Akijua kuwa hii ndiyo nafasi pekee, Pamela alishika kizingiti cha mlango, akijaribu awezavyo asiachie. "Hapana. Lisa hajawahi kuingia kwenye uhusiano na Kelvin. Kelvin aliyasema hayo kwa makusudi mbele ya waandishi wa habari juzi, lakini hayana ukweli. Alikuwa anajikosha tu. Wewe ndiye anayekupenda Lisa. Wewe ndiye mtu pekee ambaye una nafasi moyoni mwake. Tangu alipokutana nawe, ameanguka kichwa chini kwa ajili yako. Ingawa amekuwa akiishi nami siku hizi, anachofikiria ni wewe tu. Amekuwa akilia kila siku.”

Sura ya 72

Macho ya Alvin hatimaye yakamtoka. Alizitupa zile karata na kisha akainama nyuma na kumwamuru Rodney, “achana naye.” Kisha akamwambia Pamela aendelee na aliichokuwa anakisema.

Macho ya Pamela yaling'aa alipoona mwanga wa matumaini. Kwa haraka akaongeza, “Lisa aliniambia kwamba tangu umwokoe kutoka kwenye lile tukio la Zakayo Tarimo, alianza kukupenda sana. Anataka tu kuwa mwanamke wako. Lakini, haijalishi alifanya nini, haukumjali kamwe. Anahisi kuchoka na huzuni, kwa hivyo alichagua kukuacha.”

Pamela akaendelea kuitumia vizuri nafasi aliyopewa. “Alisema inamuuma sana kwa sababu huonyeshi kumpenda. Humuuma zaidi unapomtendea kwa dharau. Juzi alipanga kutoka nami wakati paka wako alipojifungua watoto wake usiku. Mara tu alipojua juu yake, aliniacha na kuja nyumbani kwako badala yake. Alisema kuwa Charlie ni muhimu sana kwako, kwa hivyo ikiwa kitu chochote kitampata Charlie, utavunjika moyo.”

Midomo migumu ya Alvin ililainika na kuachia tabasamu. “Kweli? Lakini sivyo alivyofanya alipokuja siku hiyo.”

"Bila shaka, asingeweza kueleza hisia zake moja kwa moja." Mwonekano wa huzuni ukapita usoni mwa Pamela. "Anataka kukupikia milele na sio kwa muda tu. Anataka kuwa mke wako na sio mhudumu wako. Kweli huelewi wanawake tulivyo.” Pamela alipunga mkono kwa hisia huku machozi yakimlenga lenga.

Alvin alipigwa na butwaa, mapigo ya moyo yakimuenda mbio sana. Je, haya yalikuwa ni mawazo ya mwanamke huyo kweli? Alvin alijiuliza.

Pamela aliendelea kuongeza hadithi. "Bw. Kimaro, unadhani Kelvin anamvutia Lisa kama wewe? Je, Kelvin amewahi kumuokoa Lisa? Fikiri juu yake. Je, Lisa angewezaje kumwangukia Kelvin na si wewe? Je, yeye ni kipofu?”

Alvin alizidi kusisimka na ngonjera za Pamela. Pamela naye akazidi kumimina mashairi masikiono mwake, akizidi kumjaza upepo na kumvimbisha kichwa.

"Alisema kwamba ingawa humpendi na nyote wawili hamuwezi kuendelea kuwa pamoja, hakuna kinachoweza kumzuia kuzidi kukupenda."

Mara moja, chumba cha faragha chenye kelele kikawa kimya sana hivi kwamba mtu angeweza kusikia pini ikidondoka. Alvin aliondoa wasiwasi kwenye uso wake alipogonga kadi kwenye meza kwa vidole vyake. Ilikuwa vigumu kutambua hali ya uso wake, ni yeye tu ndiye angetambua hisia zilizokuwa zikimemshika ndani yake. Inaweza kuwa kweli kwamba Lisa alikuwa akimpenda. Walisema kadiri mtu anavyopenda zaidi ndivyo anavyoteseka zaidi. Hata hivyo, alikasirishwa sana na mwanamke huyo kujihusisha na wanaume wengine.

Baada ya kile kilichoonekana kama kimya cha milele, hatimaye Alvin alifungua kinywa chake kuzungumza. “Nitafikiria juu yake. Unaweza kuondoka sasa hivi.”

"Unahitaji kufikiria hadi lini? Lisa amefungwa kwa saa nane sasa.” Pamela alisisitiza.

“Kwa hiyo saa nane ni muda mrefu sana kwa sababu yeye ni wa thamani?” Alvin alichukua kadi zake tena. "Ikiwa utaendelea kukaa hapa, anaweza kufungwa hadi atakapofikisha umri wa miaka 80."

Macho ya Pamela yaling'aa alipogundua mwanga wa matumaini katika maneno yake. Kwa hayo, alitoka nje ya chumba.

Mara mlango ulipofungwa, Chester Choka alichanganya kadi mikononi mwake kwa mbinu ya ajabu na akauliza kwa mshangao, “Kweli utamwokoa?”

Alvin alichukua kikombe chake na kunywa kahawa bila kusema neno.

Rodney hakuweza kujizuia kusema, “Vema, mwanamke huyo anaonekana mjanja. Sidhani kama alichosema ni cha kweli.”

"Unadhani sentensi gani ni ya uwongo?" Alvin alikodoa macho yake ambayo yalidhihirisha kero.

Akiwa amepoa mpaka kwenye mfupa, Rodney alikosa la kusema.

"Umechukizwa, huh?" Chester aliuliza huku akicheka.

“Unawaza kupita kiasi.” Alvin kwa utulivu alikunywa kahawa na kusema. "Kwa kweli, yeye ni mke wangu, na kuhusika kwake katika suala hili kutaniletea aibu."

"Kweli, bado unaweza kutumia siku mbili zaidi hapa Nairobi kabla ya kurudi kumuokoa. Sio suala la maisha na kifo hata hivyo. Ni muda mrefu umepita tangu tukutane pamoja.” Rodney alikaa kwenye kiti kilichokuwa tupu. "Changa karata, Chester."

“Sawa.” Chester alimtazama Alvin bila huruma.

Takriban nusu saa baadaye, Alvin alizitupa zile kadi na kupiga miayo. "Nimechoka. Nitaishia hapa.”

"Si ulitukuahidi kucheza hadi usiku wa manane?" Rodney alipigwa na butwaa.

"Nilikumbuka tu kwamba sijashughulikia kesi ya dharura huko Dar. Tukutane tena wakati mwingine.” Alvin akijibu kizembe.

Rodney aliachama mdomo kwa mshangao, akionyesha kutokuamini. “Ndugu, tuliacha kazi zetu na tukaja kukutana nawe hapa kwa sababu ni wewe ndiye ulitupigia simu. Sasa unapanga kuondoka wakati hatujamaliza hata siku moja? Unatuchukuliaje?”

"Anasema kwamba ana jambo la dharura la kushughulikia. Naelewa." Chester alisimama na kumpiga Rodney begani huku akitabasamu. Alimwambia Alvin, "Salamu zetu kwa mkeo. Mwambie tutamtembelea huko Bongo tukiwa na nafasi."

“Hah. Hebu tuone." Alvin alisimama na kuondoka moja kwa moja.

Rodney aliyapapasa macho yake akidhani alikuwa anaota. "Ni kweli Alvin anarudi bongo sababu ya mwanamke?"

"Hebu fikiria, hivi Alvin ametushinda katika raundi yoyote tangu mwanamke huyo aondoke?" Chester aliuliza. Wazo hilo lilimgusa Rodney. Kwa kawaida, ilikuwa karibu haiwezekani kumshinda Alvin kwenye mchezo huo kwa kuzingatia akili yake. Lakini, alionekana kutokuwa na umakini mara baada ya Pamela kuondoka.

Kwenye lango kuu la kuingilia hotelini, Pamela alikuwa akitafakari kama angojee hapo hadi kupambazuke. Haikupita hata nusu saa alipokaa, ghafla alimuona Alvin akitoka kwenye lifti. Nyuma yake alikuwa msaidizi wake Hans ambaye alikuwa akiburuta begi.

"Bw. Kimaro, una uhakika na hili?” Hans alimuuliza. Pamela pia hakuamini kinachoendelea. Alikuwa na mawazo kwamba angengoja angalau hadi kupambazuke.

“Afadhali nirudi Dar kwani nimeishiwa na bahati." Alvin alijibu baada ya kuingia ndani ya gari.

Pamela alikuwa karibu kupiga kelele kwa furaha. Aligundua kuwa Alvin alikuwa akijifanya tu ila alimpenda sana Lisa, vinginevyo asingeacha mambo yake na kurejea Dar ess Salaam usiku namna ile.

Sura ya 73

Baada ya kufika Dar, Alvin alielekea moja kwa moja kwenye kituo cha polisi. Kwa mshangao mkubwa, utaratibu wa kumwekea dhamana na kumtoa Lisa nje ulifanywa kwa chini ya dakika 20 tu. Wakati huo, Pamela aliona polisi wa kike akimtoa Lisa nje.

Ndani ya masaa kumi tu, Lisa alikuwa amelowa kabisa. Alijikongoja nje akiwa na nywele chafu. Uso wake mzuri ulikuwa umevimba na kuwa na makovu mabaya. Mikwaruzo mingi ya kucha ilionekana kwenye ngozi yake.

Alvin alisimama upande mmoja, macho yake meusi yakiwasilisha hisia kubwa ya uhasama. Kwa nini mwanamke huyu mpumbavu ashindwe kujilinda kila mara? Siku zote angeishia kujeruhiwa vibaya wakati yeye hayupo.

"Mungu wangu. Nini kimekupata? wamekuadhibu kinyume cha sheria?" Pamela alipiga kelele na mara moja akamshika. Lisa alikuwa dhaifu sana kuliko vile alivyofikiria.

Jozi ya mikono mikubwa ilinyooshwa na baadaye kumbeba Lisa kwa mlalo. Lisa alijitahidi kufumbua macho yake yaliyovimba. Akiwa anautazama uso mzuri wa Alvin chini ya taa hafifu, Lisa hakuogopa hata kidogo. Kwa kweli, alihisi hali ya faraja isiyoelezeka kumwona mkombozi wake kwa mara nyingine tena. Kwanini ni Alvin tu ndiye aliyekuja kumuokoa kila mara alipoangukia matatizoni? Kwa kweli alizidi kujihisi kuwa na deni kubwa kwake. Hata hivyo, alikuwa amechoka na kuhisi maumivu makali wakati huo. Alichotaka kufanya ni kumuegemea kimya kimya.

Lisa alijikunja mikononi mwa Alvin kama paka. Alvin alimtazama Lisa aliyeonekana dhaifu kutokana na majeraha yaliyotapakaa mwili wake mzima. Kuna mtu alimtesa mke wake na kumuumiza hivyo.

“Nani alimfanya hivi?” Macho ya kusikitisha ya Alvin yalielekezwa kwa afisa polisi wa kike.

Afisa Seda alitoa mshtuko wa woga. "Ilikuwa ni kazi ya wafungwa. Haina uhusiano wowote na sisi.”

Alvin aliposikia hivyo alicheka. “Inaonekana nyie hamjui sheria za kazi yenu. Yeye ni mshukiwa ambaye anachunguzwa tu hapa, hajathibitishwa kuwa na hatia, kwa hivyo yeye si mfungwa. Nyinyi kama poilisi mlipaswa kutunza usalama wake katika kipindi hiki, lakini ni wazi, hamkufanya hivyo. Afadhali mnipe maelezo ya kuridhisha. Vinginevyo, kama wakili wake, nitawashtaki ninyi nyote mnaosimamia mahali hapa.”

Afisa yule wa kike aliogopa sana. Alikuwa amesikia kwamba kijana huyo alikuwa wakili wa kimataifa ambaye alikuwa na ujasiri wa kutosha kumshtaki mtu yeyote.

“Usi… Usijali. Nitamjulisha mkuu wangu kuhusu hilo. Wale watakaobainika walimpiga Miss Jones wataadhibiwa vikali." Alijitetea afande Seda.

"Lazima nione matokeo ya adhabu." Mara Alvin alipomaliza kuongea, aligeuka na kuondoka huku akiwa amembeba Lisa wake. Baada ya hapo wakaingia kwenye gari.

Baada ya kumbeba hadi kwenye kiti cha nyuma cha gari, Alvin alinyoosha mikono yake ili kulitoa shati la Lisa lililokuwa limelowa maji. Lisa alimzuia huku macho yake yakionyesha aibu.

“Acha kuhangaika na unyamaze. Ngoja niangalie.” Alvin alitumia mkono mmoja kukandamiza mkono wake na mkono mwingine kufungua shati lake kwa nguvu. Ngozi yake ya awali ilijaa michubuko wakati huo, ambayo ilimfanya ahisi maumivu makali.

Alvin kwa namna fulani alihisi huruma fulani, na uso wake ulionekana kuwa na huzuni sana. Lisa hakuweza kuwa na wasiwasi juu yake. Aliona aibu tu kuhusu michubuko yake isiyopendeza wakati huo.

“Umemaliza kutafuta?” Alijitahidi kuongea kwa aibu. Alipojaribu kusogea kidogo, alisikia maumivu makali sana hivi kwamba uso wake ulibadilika rangi.

"Afadhali utulie." Alvin moja kwa moja akazitupa upande mmoja nguo zake zilizokuwa zimelowa maji. Kwa haraka akavua fulana yake kisha akamvalisha. Mara tu alipogusa majeraha mwilini mwake, alishtuka kwa maumivu.

"Inaumiza" Lisa alilalamika. Alvin kisha akaongeza, "Kumbuka maumivu haya na ujifunze somo lako." Akamwonya ili asimuache hivyohivyo tena. Aliona umuhimu wa kumfanya aelewe kwamba angekuwa salama zaidi tu atakapokaa kando yake.

Lisa alikenua meno yake kwa utiifu na kubaki tuli huku akivumilia maumivu. Alvin aliridhika kabisa kwamba Lisa alikuwa akisikiliza ushauri wake. Alifungua mlango wa gari na kutoka nje, akamwambia Pamela, "Keti naye nyuma ya gari na umwangalie. Mimi nitaendesha.”

Gari lilisafiri kwenye barabara ya jiji yenye shughuli nyingi saa za asubuhi. Lisa alimtazama Pamela kwa mshangao na akapata nguvu ya kunong'ona, "Kwa nini alikuja kuniokoa?"

Pamela akatoa macho yake kwa huruma. "Lisa, unajua kuwa umeiudhi familia ya Zongo wakati huu kwa hivyo hakuna mtu mwingine anayeweza kukuokoa? Hata Kelvin na Ethan hawakuweza kupata jeuri yoyote ya kukutoa lockup, kwa hiyo sikuwa na budi ila kumwomba Alvin msaada.”

"Ina maana Sam alikataa?" Lisa alishangaa.

"Sam hatajiweka kinyume na familia ya Zongo kwa sababu yako, sawa. Je! unajua kuwa umeolewa na mume mwenye nguvu? Alvin ni mwanasheria mwenye nguvu zaidi hapa mjini. Yeye ndiye mwanasheria wa familia nyingi tajiri na watu mashuhuri hutumia pesa nyingi kumfanya akubali kusimama na kesi zao bila mafanikio. Lakini wewe hajawahi kuacha kukusaidia.”


Siku chache zilizopita, hata hivyo, Lisa alikuwa ametamba mbele yake kwamba alikuwa mwanasheria tu ambaye mapato yake yalikuwa sawa na yake. Hakujua nguvu yake na umuhimu wake mpaka yalipomkuta makubwa, aliona aibu sana. Aliwezaje kuthubutu kutoa maneno ya aibu kama hayo?

"Lakini kwa nini alikubali kuniokoa?" Lisa alirejewa na fahamu zake. Kwa kuzingatia tabia yake ya kawaida, bila shaka asingekuja kwa kuwa alikuwa amemkosea sana.

Akijisikia hatia, Pamela alitoa kikohozi kidogo. "Hakuwa na mpango wa kukuokoa mwanzoni. Mimi ndiye niliyemwambia jinsi ulivyokuwa unampenda sana. Pia nilimwambia kwamba ulimwacha kwa sababu tu unampenda sana na kwamba huwezi kustahimili dharau zake…”
Pamela baadaye alirudia kile alichosema hapo awali.

Je, hii ingemaanisha kwamba Alvin alimwona Lisa kama mwanamke anayemlilia kila siku?

“Usinilaumu.” Pamela aliendelea. “Nilifanya haya yote kwa ajili ya kukuokoa. Ikiwa ungechelewa kuokolewa wakati wowote baadaye, ungeweza kuteswa hadi kufa huko jela.”

Akiwa amemegemea kwa huruma, Pamela alimnong’oneza sikioni, “ingawa umedhaminiwa, haimaanishi kuwa familia ya Zongo haitafungua kesi dhidi yako. Ikiwa unataka kutoka kwenye ndoano, una Alvin pekee wa kumtegemea."

Lisa alikuwa karibu kuzimia baada ya kusikia hivyo. Mwisho wa siku, bado alihitaji kujipendekeza kwa Alvin?

Pamela aliendelea kusema, "Vema, hakuna mtu yeyote isipokuwa Alvin ambaye ataweza kukusaidia. Bila yeye, utahukumiwa zaidi ya miaka kumi au utatozwa faini ya mamia ya mabilioni ya shilingi. Mbaya zaidi sifa yako yote kama mbunifu majengo maarufu itaharibiwa na kufutika kabisa kwenye uso wa dunia.

Roho ya Lisa ilishuka. Alikunja ngumi kwa hasira. Kwa kweli, hakustahili kuteseka kwa kutukanwa. Aliona haja ya kuthibitisha kwamba hakuwa na hatia katika hilo.

Gari lilifika hospitalini. Daktari alimpeleka Lisa chumbani ili kumfanyia uchunguzi wa kimatibabu. Alvin na Pamela walikuwa wamesubiri kwa muda mrefu kwenye mlango wa chumba cha dharura. Baadaye matokeo ya uchunguzi yalitolewa. Taarifa ilikuwa mkononi mwa Alvin. Majeraha ya Lisa yalikuwa mabaya zaidi kuliko vile alivyofikiria. Aliyempa majeraha hayo alikuwa mkatili sana. Vidonda vyake vilionekana kuwa vidogo, lakini mifupa na viungo vyake vya ndani vilijeruhiwa kwa kiasi fulani.

"Bw. Kimaro, mbali na majeraha haya, sehemu za ndani za mwili za Miss Jones zimejeruhiwa vibaya pia. Asipoanza kupata tiba mapema, anaweza kupata shida ya uzazi baadaye.”

Alvin alipigwa na butwaa kwa muda. Baadaye, alielewa hali yake.
Lisa alikuwa amepata mateso makali mara mbili. Mwanaume yeyote wa kawaida hawezi kustahimili hilo, sembuse mwanamke yule kijana?

"Lazima umuuguze arudi kwenye afya yake." Alvin alikunja uso. Kama mwanamke wake, angewezaje kuwa tasa? Angelazimika…Subiri. Alikuwa anawaza nini? Japo mwanamke huyo alimpenda sana, hakuwa amefikiria kuhusu kupata naye watoto.

Sura ya 74

Baada ya daktari kuondoka, Hans alimpa haraka Alvin habari alizokusanya. “Bw. Kimaro, moto ulizuka katika hoteli ya Lublin kwa sababu James, msimamizi wa ujenzi ambaye ni mpwa wa mke wa Jones Masawe alitumia nyaya feki za umeme. Wale walioko Kibo Group wanafahamu ukweli, lakini James amewahonga. Kwa hiyo, kila mtu anafumbia macho tu. Ili kumlinda James baada ya tukio hilo, familia ya Masawe ilimfanya Lisa kuwa mbuzi wa kafara.”

Alvin hakuamini. "Kwao, mpwa ni muhimu zaidi kuliko binti wa damu, huh?"

“Labda… Hawampendi binti huyu sana. Zaidi ya hayo, James ni mzuri katika kujipendekeza kwa watu. Amepata mengi sana miaka hii yote na kutoa zawadi nyingi za thamani kwa Masawe na mke wake.” Hans alinyamaza kwa muda na kuendelea, "Baada ya kujua kwamba Lisa ameachiliwa, familia ya Zongo ilitafuta wakili ambaye angefungua kesi dhidi yake."

“Sawa, nimeelewa.” Alvin alichukua nyaraka na kuelekea katika wodi ya watu mashuhuri.

Mara tu Pamela alipomwona Alvin akiingia wodini, aliinuka na kusema,“nitaenda kumnunulia Lisa chakula nje.”

“Hakuna haja,” Alvin alijibu kwa upole, “Chakula kinachouzwa huko si safi. Nimeagiza chakula kutoka hoteli ya Serena, ambacho kitaletwa hapa muda si mrefu.”

Pamela alikosa la kusema. Lo! Lisa angeweza kula chakula kutoka hoteli ya nyota saba licha ya kulazwa kwenye hospitali ya hali ya juu. Jinsi alivyobarikiwa! Pamela akakisogelea kitanda na kumkonyeza Lisa . Baada ya hapo, alikimbia kutokanje mara moja.

Lisa alijionea aibu kwani hakutarajia Alvin angemtendea mema kiasi kile. “Kwa kweli, sijisikii kula chochote." Lisa aliongea kwa sauti ya chini huku akiwa na wasiwasi na woga.

“Chochote?” Alvin alitoa kicheko kirefu, lakini macho yake yalikuwa yamepoa. "Je, hukusoma cheti cha matibabu kilichotolewa na daktari?" Lisa alikuwa ameduwaa. Alikuwa hajakisoma.

“Mjinga wewe.” Kwa kujieleza kwa huzuni, Alvin aliendelea, “hujui jinsi mwili wako uliolaaniwa ulivyo dhaifu? Daktari alisema hutazaa milele usipojitunza.”

Maneno yale yalimshtua sana Lisa. Hakika, hakuwa akiutunza mwili wake kwa sababu tu alikuwa kijana. Sasa baada ya kusikia taarifa hizo, alikumbuka kwamba alikuwa na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida na vya mfululizo siku za karibuni.

“Ngoja nikuonye kuwa sitataka kujumuika na mwanamke asiyeweza kuzalisha mayai,” Alvin alimkumbusha ili afahamu. Ikiwa bado alitaka kuwa naye, ilimbidi ajiuguze ili apate afya.

Mdomo wa Lisa ukasisimka kwa hasira. Alikanusha kwa dharau, “Bila shaka, siwezi kuzalisha mayai. Mimi si kuku.”

“Unathubutu vipi kujibu utumbo?” Alvin akasogea mbele huku akikodoa macho. Lisa aliogopa sana hivi kwamba alijikunja kwenye blanketi lake. Alipogusa majeraha yake mwenyewe kwa bahati mbaya, alitetemeka kwa maumivu.

"Njoo utie saini hii." Alvin alitupa hati kwenye blanketi lake.

Mara tu Lisa alipoona maneno 'Makubaliano ya Ndoa na Uchumba' yameandikwa kwenye waraka huo, alipigwa na butwaa. Aliifungua hati hiyo bila kupenda ili kuitazama. Kimsingi, ilielezwa kwamba angeishi naye na kuchukua jukumu la kupika, kusafisha, kumtunza paka na yeye, na ...Alilazimika kufika nyumbani si zaidi ya saa tatu usiku kila siku. Pia hakuruhusiwa kufuatana na mtu yeyote wa jinsia tofauti peke yake.

“Huu ulikuwa upuuzi gani?” Lisa alijikuta akiduwaa kwa mawazo.

Alvin akatoa kikohozi kirefu huku akikunja ngumi. “Usifikirie kupita kiasi. Kwa taarifa ya mwisho, itategemea utendaji wako. Vinginevyo, usiwahi kufikiria juu ya kupanda kitanda changu. Pia, usitumie mbinu zozote za siri tena kwani zinanichukiza sana. Unaelewa?"

Hapana. Hakuelewa kabisa. Lisa alikuwa amepoteza akili yake kabisa.

Alvin akanyanyua kidevu chake kwa jeuri. “Saini makubaliano haya, nami nitakusimamia kesi yako kuhusu hoteli hiyo. Pia nitahakikisha mhalifu anapata adhabu anayostahili.”

“Unamaanisha James?”

“Ndiyo.” Alvin akakaa kitandani huku akiinyoosha miguu yake mirefu yenye kuvutia. “Familia ya Zongo imeamua kukushtaki. Kesi hiyo huenda ikapelekwa mahakamani wiki ijayo. Kwa sasa, hakuna mtu yoyote aliye na ujasiri wa kushughulikia kesi yako, isipokuwa mimi. Nina wazo baya ni nani familia ya Zongo itamwajiri kama wakili wao. Ana kipaji, na anaweza kukufanya ukabiliwe na kifungo cha zaidi ya miaka 20.” Lisa alitetemeka.

Alvin kisha akakunja midomo yake myembamba. " Ni wazi kwamba kuna mtu anayejaribu kukuingiza kwenye matatizo makubwa.”

“Je, kundi hilo la wafungwa lilihongwa ili kunidhuru kimakusudi jana?” Lisa aliinua kichwa chake na kuuliza ghafla.

“Hiyo ni kweli. James Komba ndiye anayehusika na hilo.” Alvin akamtupia Lisa jicho la haraka. "Ni mtu aliyekufa tu ndiye atakayetunza siri. Unaelewa?"

Lisa alianza kutetemeka huku moyo wake ukichomwa na miali ya hasira. James hakika alikuwa amepoteza kabisa utu. “Um… Je, inawezekana kubadili masharti?” Lisa aliuliza kwa kuhema baada ya kupata utulivu. Kwa kweli hakutaka kuwa mhudumu wake tena. Mbali na hilo, hakukuwa na tarehe ya kumalizika kwa mkataba huo. Ingekuwa mateso ya maisha yake yote.

“Hakika.” Tabasamu likatanda usoni mwa Alvin. “Kulingana na bei ya kawaida, huduma yangu ya kisheria inagharimu angalau shilingi milioni 500 kwa kila kesi. Kesi yako mahususi ni ngumu na nina hatari ya kukasirisha familia yenye nguvu zaidi ya Zongo. Naam, nitakupa punguzo la 20%. Hiyo itakuwa shilingi milioni 400.”

"Shilingi milioni 400?" Macho yakamtoka. "Unataka nikavunje benki?"

"Kwa kweli unapaswa kushukuru zaidi hata kupata ofa hiii. Unajua ni watu wangapi huko nje wanaonipa zaidi ya milioni 400 kushughulikia kesi yao na bado nawakatalia?” Akainuka na kusimama. “Ni chaguo lako. Lakini wakati wangu ni wa thamani.” Akaanza kutembea kuelekea mlangoni ili kumpima. Ilimkatisha tamaa sana kuona Lisa hakumwita. Alvin akaondoka zake kwa hasira.

Pamela alirudi dakika 20 baadaye. Alimpa ushauri wake Lisa baada ya kuuliza juu ya kile kilichotokea. “Nafikiri pengine anavutiwa nawe pia. Kwanini tena aweke masharti haya ya kimapenzi na kukukataza kutoka na wanaume wengine? Hakika ana wivu.”

Lisa alihisi moyo wake ukirukaruka. “Sidhani hivyo. Pengine anapanga kuniweka karibu ili niwe mtu wa kukaa bure na kwa kweli sitaki hilo tena. Kuishi naye mara ya mwisho haikuwa rahisi kwa afya yangu ya akili.”

“Sawa. Lakini naamini ndiye mtu pekee anayeweza kukusaidia kwa sasa.”

Muda huo huo simu ya Lisa ikaita. Kelvin alikuwa akimpigia simu. Akapokea simu. Alitaka kuja kumtembelea hospitalini lakini Lisa alikataa. Ethan pia alipiga baada ya hapo. Lisa alikataa kujibu. Matukio yaliendelea kufuatana. Muda mfupi baadaye, alipokea barua ya kisheria iliyotumwa kwake na familia ya Clark Zongo. Kesi ilipangwa kwa wiki iliyofuata.

Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, Lisa alizunguka jiji zima la Dar kutafuta usaidizi wa kisheria lakini hakuna wakili aliyethubutu kusikiliza kesi yake.

"Bi Jones, kusema ukweli, mtu yeyote anayekubali kesi yako anatangaza vita waziwazi na Bw. Clark Zongo."

“Bi Masawe, hakuna kitakachobadilika hata ukinisihi. Sitaweza kushinda kesi hii hata nikichukua changamoto.”

Hayo ndiyo majibu aliyokutana nayo kutoka kwa baadhi ya mawakili.
Kesi ilikuwa inakaribia. Lisa alikuwa na wasiwasi na mawazo sana kwamba hakuweza kulala vizuri usiku.

Sura ya 75

Hatimaye, akiwa hana njia nyingine, alimpigia simu Alvin. Ni msaidizi wake ambaye alipokea simu. “Lisa, Bw. Kimaro hayuko huru kwa sasa. Naweza kukusaidia?"

"Bw Kimaro alisema angeshughulikia kesi yangu mara ya mwisho na ninataka kumwambia kwamba nitasaini mkataba…” Lisa alifunguka moja kwa moja.

Hans alijibu kwa tabasamu, "Samahani, lakini umechelewa. Bi Jones, muda wa Bw. Kimaro ni wa thamani sana. Fursa zingine hazisubiri milele.” Hans alikata simu baada ya hapo. Aligeuka nyuma na kumuona Alvin, ambaye alikuwa anasikiliza sekunde chache zilizopita, akinywa kahawa yake bila kujali. Hans alitabasamu kidogo kabla ya kusema kwa upole, “Bosi, nimefanya kama ulivyoagiza. Nina uhakika Bi Jones atakuja kukuomba hivi karibuni.”

Alvin alikubali kwa kutikisa kichwa haraka. Alijisikia raha kidogo aliposikia hivyo. “Maandalizi ya kesi hii yanaendeleaje?”

"Kila kitu kiko tayari." Hans alijibu. Alvin alikuwa amekusanya taarifa za kesi ya Lisa mahakamani kwa siri lakini bado alikuwa akijifanya kutojali. ‘Bosi, hujui kuwa tabia yako hii itakukosesha mke?' Hans alitamani kumwambia hivyo lakini hakuthubutu hata kidogo.

Kwa upande mwingine, Lisa ambaye alikuwa amekatiwa simu alikuwa hajui la kufanya, alisongwa na majuto na kukumbuka mashariti ya Alvin. “Hakika kuwa mhudumu wa Alvin ilikuwa bora kuliko kufia gerezani.” Hatimaye Lisa alikiri mbele ya Pamela.

“Sawa, vaa hii haraka na uende kuomba msaada wake.” Pamela alimkabidhi rafiki yake mavazi meupe ya maua mapya.

Lisa alilitazama vizuri lile gauni na kugundua lilikuwa na shingo ya chini chini ambayo ineyaweka wazi matiti yake kwa sehemu kubwa. “Unanifanya nivae hivi ili kujitongozesha kwa Alvin? Anachukia hili. Nitakuwa nimejitakwa mwenyewe matusi yake ya chuki.”

“Kwa kuzingatia masharti aliyoweka mezani, ni dhahiri kwamba anavutiwa nawe kwa njia hiyo. Jaribu hata hivyo. Nyakati za kukata tamaa hazihitaji hatua za kukata tamaa." Pamela alimshauri. Hakuweza kufahamu jinsi Alvin alivyombadilisha rafiki yake kipenzi na kuwa mtu wa kumhofia. “Hii ndiyo anwani ya eneo lake la kazi. Nimeipata kutoka kwa Sam."

Lisa akavuta pumzi ndefu huku akiitazama ile anwani. Hatima yake ilikuwa mikononi mwake, na hakuweza kuitupa nafasi hiyo. Kabla ya hapo, alitayarisha chakula alichopenda Alvin, akakipakia kwenye bakuli la hotpot, kisha akaendesha gari kuelekea Jennings Solicitors, kampuni ya mawakili ya Alvin na Sam. Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kufika pale ofisini kwa Alvin. Aliingia ndani ya jengo hilo na kuelezea nia yake kwa dada wa mapokezi.

Dada wa mapokezi alipiga simu kabla ya kurudi kwa Lisa na taarifa. "Bw. Kimaro yuko kwenye mkutano na wateja. Tafadhali subiri."

Nusu saa ikapita huku akingoja. Alvin, ambaye alikuwa akicheza drafti na Sam ofisini kwa juu, aliendelea kutazama saa kila baada ya dakika tano. Sam hakuweza kuvumilia tena. "Mruhusu aingie tu."

"Hapana, ninamfundisha somo." Alvin alijibu kikauzu na kuendelea kusukuma kete.

Lisa alingoja kwa takribani saa moja kabla ya yule mhudumu wa mapokezi kumuongoza kwenda juu. Ofisi binafsi ya Alvin ilichukua sakafu nzima. Alipoingia ndani, alimuona akiwa amekaa kwenye kiti kilichotengenezwa kwa ngozi halisi kilichokuwa kando ya meza, akifanya kazi kwa bidii. Alikuwa amevaa shati la bluu giza siku hiyo. Jozi ya miwani yenye fremu za dhahabu ilikaa kwenye daraja la pua yake. Tai iliyowekwa vizuri kwenye shingo yake ilikuwa imeniga shingo yake kwa kupendeza. Kichwa chake kilikuwa kimeinamishwa chini huku akiandika kwenye laptop. Kutoka upande wa Lisa, alionekana maridadi na mwenye fahari.

Lisa hakuthubutu kupiga hatua mbele. Hata alikuwa akipumua kwa upole na kwa uangalifu bila kujitambua.
Alvin aligonga keyboard kwa hasira akiandika kwenye laptop. Alipokaa kwenye kiti, Alvin alimwangalia kumwambia bila subira. “Utakaa hapo hadi lini? Muda wangu ni wa thamani. Niache kama huna la kufanya hapa."

“Niliona kwamba ulikuwa unafanya kazi na sikutaka kukusumbua.” Sura ya aibu ilitanda usoni mwa Lisa baada ya kusikia maneno ya hasira ya Alvin. Lakini, aligundua kuwa hii yote ilikuwa makosa yake mwenyewe.

"Kweli, umenisumbua kazini." Alvin alivusha mikono yake mbele ya kifua chake, akijifanya kana kwamba alikuwa amekasirika na kukosa subira kwa kusumbuliwa.

Hans, ambaye alikuwa akitazama hii pembeni, bila shaka alishtuka. Alitaka kusema hivi, 'bosi, umekuwa ukingoja siku kadhaa kwa hili. Acha kuigiza! Au utakuwa na wasiwasi tena akiondoka.' Lakini alikwempesha mada ili kupunguza hali ya wasiwasi, Hans alitabasamu. "Bi Lisa, hiyo ni zawadi kwa Bw. Kimaro ambayo umeishikilia?"

"Ndio, ni kweli. Nilimtengenezea chakula cha mchana.” Haraka akatoa hotpot la chakula kutoka kwenye begi lake.

Alvin alianza kuchezea kalamu yake juu ya meza. Macho yake yaling'aa kwa kejeli. "Lakini nakumbuka kumsikia mtu fulani akisema hatajaribu kunipikia tena, kwa hiyo halazimiki kuniandalia chakula."

Lisa aliuma meno kwa shambulio hilo la ghafla. "Alvlisa, sikujua vizuri hapo zamani…”

“Uliniita nani?” Alisema, akigonga kalamu kwenye meza. Maneno yake yalizidisha vitisho. Hilo lilimshangaza. “Alvinani?” Akatabasamu tena kwa kejeli, huku akionekana kutofurahishwa.

Lisa alishindwa la kusema. Hakika ilikuwa vigumu kuelewa kilichokuwa kikiendelea akilini mwa mtu huyu.
Hans alihisi kumwonea huruma Lisa aliyekuwa anajikanyagakanyaga tu kujibu. Majibizano yao yalimfanya awe na wasiwasi. "Bi Lisa, amekuita jinsi alivyokuwa akikuita zamani. Alvlisa!”

Hata hivyo, jambo hilo lilimkasirisha Alvin na kumtupia jicho la kutisha msaidizi wake. “Huna kazi ya kufanya? Toka nje.”

“Samahani.” Hans aliinamisha kichwa chake kabla ya kutoka nje ya chumba hicho.

"Hajafanya kosa lolote." Lisa alimtetea msaidizi huyo mwenye moyo mkunjufu.

Alvin akacharuka kwa hasira na kumkazia macho. “Unathubutuje kumtetea mwanaume mwingine mbele yangu?”

Lisa akatulia tuli na kuvuta pumzi kabla hajasema kwa upole. “Ni karibu saa sita mchana. Una njaa. Chakula kimepoa kidogo. Je, niwashe moto nikupashie?" Sauti yake ilikuwa laini na tamu. Alikuwa na tabia ya kujinyenyekeza kwake tena kama hapo awali.

Alvin alifurahishwa na sauti hiyo. Hivi ndivyo alivyotaka Lisa awe badala ya ujeuri ambao alikuwa akimwonyeshea hivi karibuni. Hata hivyo, hakukubali kwa maneno machache tu ya Lisa, alitaka kubembelezwa zaidi.."Sipendezwi tena na upishi wako."

"Samahani, Alvlisa, kwa kweli sitaki kabisa kwenda gerezani. Tazama, mimi ni mke wako kisheria. Je! ni nini kitatokea ikiwa habari itaenea kwamba hauchukui kesi ya mke wako mwenyewe? Wanaweza kufikiria kuwa unamuogopa wakili wa familia ya Zongo.”

"Sio mbaya. Naona unanijaribu njia hii isiyo ya moja kwa moja ya kisaikolojia kutaka kunishawishi.” Alvin alimwambia.

"Ni sawa ikiwa hutaki, lakini natumai utakubali chakula hiki cha mchana nilichokuandalia. Huenda kikawa chakula cha mwisho kwangu kupata nafasi ya kukupikia kabla sijaenda jela. Hii ni shukurani yangu kwako kwa kuniokoa mara ya mwisho.”

Macho ya Lisa yaling'aa kwa uaminifu. Maneno hayo yalitoka ndani ya moyo wake safari hii. Ingawa maneno yake makali yalikuwa yamemuumiza kabla, bado alimshukuru. Angalau, siku zote alikuwa akitokea wakati muhimu kabisa kwa ajili yake pindi alipokuwa hana ulinzi kabisa.

“Unapaswa kunishukuru kweli. Unafikiri Kelvin au Ethan wangeweza kukusaidia?” Alvin alidhihaki. “Sawa, nitakupa nafasi ya mwisho. Ingia huko ili upashe moto chakula.”

“Hakika.” Macho ya Lisa yalitiririka kwa uzuri huku akiingia kwenye chumba cha kunawia.

Kulikuwa na microwave. Alipasha moto chakula ndani ya dakika tatu, akakiweka mbele ya mwanaume huyo. Ilikuwa ni nyama ya nguruwe aliyoipenda sana. ilikuwa imechomwa vizuri pamoja na ndizi za kuchoma pia. Alvin aliitazama na papo hapo akahisi tumbo lake likiunguruma. Tangu alipoondoka, hakuwa amefurahia chakula kizuri kilichopikwa nyumbani. Baada ya dakika chache, alikula sahani nzima, hakuacha chochote kwenye hotpot alilobeba Lisa.

TUKUTANE KURASA 76-80

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI......LISA
KURASA.....76-80

Sura ya 76

Lisa alishtuka kwa mshangao wa pembeni. Huyo ndiye mtu aliyesema kuwa havutiwi tena na upishi wake!

"Unashangaa nini?" Alvin alimwona Lisa akimtazama na ishara ya aibu ikaangaza kwenye uso wake mzuri.

“Hapana, um… nimefurahi kukuona ukifurahia chakula changu tena,” Lisa alisema kwa utani nusu-nusu. Kisha, alimwona Alvin akiokota hati zilizokuwa ubavuni kana kwamba yuko tayari kuanza kazi tena.

Lisa akavua taratibu kijikoti alichokuwa ametupia kwa juu kwa kisingizio cha joto na matiti yake makubwa kiasi ambayo yalisimama bila nguvu ya sidiria yalionekana yakipanda na kushuka kufuatisha mapigo ya moyo wake. Sehemu kubwa ya juu ya kifua chake ilikuwa wazi hivyo kuzidi kumvutia Alvin.

“Umekuja kunitega tena eeh?” Alisikika kikejeli Alvin, lakini alifurahishwa kwa siri. Kama ilivyotarajiwa, bado alikuwa akivutiwa naye kimapenzi.

Kwa aibu, Lisa alitamani apotee hewani wakati huohuo lakini bado alijitetea kwa ukaidi, “Hapana, aaah…. Ah, kuna joto sana humu ndani."

"Ikiwa ni hivyo, kwa nini usiondoe ... kila kitu?" Alvin alisema kwa utani huku akiinua macho. Uso mzuri wa Lisa uliganda kwa sekunde moja. Kisha, akalivaa lile koti tena kimya kimya.

"Njoo hapa." Allvin alitoa ishara kwa mkono. Lisa alitembea kuelekea kwake huku tabasamu la kulazimishwa likiwa limetanda usoni mwake. Alvin alimshika kifundo cha mkono na kumvuta ndani ili aanguke akiwa amekaa kwenye mapaja yake. Kila kitu kilitokea haraka sana. Alipozikwa kwenye harufu mpya aliyoitoa, mwili wake wote ulisisimka kana kwamba alipigwa na radi. Uso wake ukabadilika ndani ya sekunde chache.

Lisa alijihisi kupoteza fahamu. Ingawa alikuwa na mawasiliano ya karibu na Alvin hapo awali, hii ilikuwa mara yake ya kwanza kukaa kwenye mapaja yake. Tukio hili lilikuwa kama wanandoa wachanga waliopendana sana. Alvin alifurahi baada ya kuona uso wa Lisa ukiwa umelegea kabisa. Jambo hilo lilimfanya Lisa azidi kuona aibu.

“Saini!” Alvin akaitoa ile hati ya mkataba kutoka kwenye droo. “Kaa upande wangu kuanzia sasa. Nitakulinda!”

Baada ya kupata utulivu, Lisa alichukua kalamu na kutia sahihi chini ya hati hiyo.

"Binti mzuri!" Alvin alimshika kidevu chake na kumgeuza ili asipate la kufanya zaidi ya kuutazama uso wake mzuri. Walikuwa wamesogeleana karibu sana kiasi kwamba kila mmoja aliweza kusikia pumzi ya mwenzake.

"Mimi ... ni wakati wa mimi kwenda." Lisa hakuweza kuvumilia tena.

"Unafikiria kuondoka?" Alvin akamsogeza karibu moja kwa moja. “Ni matumizi mabaya ya mavazi uliyovaa ikiwa nitakuacha uende sasa hivi." Macho ya Alvin yalifumba taratibu huku akiweka mkono wake wa kulia nyuma ya shingo ya Lisa na kumsogeza mbele ili kumpa busu la mdomo. Hizo ndizo hisia ambazo Alvin alikuwa akizikumbuka baada ya busu lao kwenye mgahawa mara ya mwisho.

Alijiuliza Lisa alikuwa amepaka nini kwenye midomo yake maana ilikuwa ina ladha tamu isiyo ya kawaida. Lisa naye alikuwa amechanganyikiwa. Alvin alikuwa akimdharau, sasa kwa nini aliendelea kumbusu? Maneno na matendo yake yalipingana. Lakini, Lisa hakuthubutu kudhani kwamba Alvin alikuwa akimpenda kimapenzi. Labda alikuwa akitosheleza tu matamanio yake kama mwanamume.

Hapo mwanzoni, Lisa aliweza kuwa mgumu kidogo, lakini katika muda mfupi tu baadaye, alijipoteza mwenyewe katika busu lile zito. Hasa kutokana na harufu safi iliyotoka kwenye mwili wa Alvin. Lisa aliuzungusha mkono wake shingoni mwa Alvin bila fahamu.

"Lisa, ni muda mrefu…" Mlango wa ofisi ulisukumwa ghafla na Sam akaingia ndani kwa hatua kubwa. Macho yake yalimtoka kwa kile alichokiona mbele yake.

Lisa alitetemeka na kwa kuchanganyikiwa akamsukuma Alvin. Uso wake ulikuwa umepagawa kwa aibu huku akisimama kutoka mapajani mwake. Uso wa Alvin ulikuwa na rangi isiyo ya kawaida ya waridi. Licha ya hayo, macho yake wakati huo yaliwaka kwa hasira kama simba aliyekasirika.

“Um… Pole. sikuona chochote.” Kwa mshtuko, Sam mara moja akatoka chumbani na kufunga mlango nyuma yake. Sam hakuwa na wazo lolote tofauti wakati anaingia. Ilikuwa ni kwa sababu aliogopa kwamba Alvin angekwaruzana tena na Lisa kutokana na tabia yake mbaya, hivyo aliingia kwa nia nzuri tu. Nani angetaraji kama angekuwakuta katika hali ile… Ha! Naam, bila shaka hakuwa ametarajia kitu kama hicho.

Ndani ya ofisi, Lisa alishusha macho yake chini na kuzungusha nywele zake kwa kuchanganyikiwa. Alikuwa na aibu kabisa. Alvin alikasirika kwa kuingiliwa lakini alifurahi kumuona msichana huyo mrembo akionyesha aibu.

"Njoo hapa." Akampa ishara tena kama hapo awali. Lakini, Lisa hakuthubutu kusonga mbele wakati huu.

“Usifanye hivyo. Mimi ni mhudumu tu…” Alijitete Lisa

“Mhudumu?” Alvin alicheka. Alisimama na kumwendea Lisa. Vidole vyake viligonga midomo yake myekundu taratibu. Uso wake ulikuwa umeduwaa kwa kuchanganyikiwa. Akatoa macho.

Lisa alikumbuka kuwa Alvin alikuwa mgumu sana, lakini kwa nini alikuwa kalainika hivi punde? Tayari alikuwa ametoa viashiria vingi sana vya kumtaka.

"Kumbuka, wewe ni mwanamke wangu kuanzia leo," Alvin alisema bila subira.

Lisa alizidi kushangaa. Hiyo haikuwa akili ya kawaida ya Alvin. “Lakini hufikirii kuwa sikustahili wewe. Unalalamika kwamba mimi ni mwanamke wa kiwango cha chini na mchafu.”

"Nyamaza." Alvin alikasirika. “Kwa kuzingatia kwamba una deni langu la milioni 400, nitafanya chochote ninachotaka kwako.”

Lisa hakuwa na la kusema. Alidhani Alvin alifanya vile kwa sababu alipmenda, lakini tamko lake lilitosha kumdhihirishia kuwa yeye alikuwa ni bidhaa tu kwake kutokana na hilo deni, alijikuta akimaliza raha ghafla. Lisa alijiona hana thamani tena. Baada ya yote, alikua mwanamke mdogo mwenye ndoto pana. Ilikuwa ngumu sana kwake kukubali haya kuwa maisha yake kwa wakati huo.

"Ninapaswa kuondoka sasa." Lisa alisisitiza kwa kukata tamaa na kuanza kuondoka baada ya kukusanya vyombo vyake..

“Simama hapo hapo.” Alvin alitupa rundo la funguo na kadi ya benki kwenye meza. “Nimehamia Mtaa wa Haile Sellasie. Hizi ndizo funguo za lango kuu la nyumba. Na hiyo ndiyo kadi ya benki uliyotumia hapo awali kwa matumizi ya nyumbani.”

Jambo hilo lilimshangaza Lisa . "Mbona umehama ghafla?"

"Charlie ana watoto watatu sasa na mahali pa zamani hapana nafasi ya kutosha. Wanahitaji bustani ya kuota jua.” Alvin alijibu kwa upole.

Hakuwa na la kusema. Alitamani bora angekuwa paka tu kwa alvin kuliko kuwa mke wake maana paka alikuwa na thamani kuliko yeye. Paka hakuweza kumhudumia bwana wake na alifurahia fursa ya kukaa katika ya nyumba ya kifahari!

Sura ya 77

Baada ya kuondoka ofisini kwa Alvin, Lisa alirudi kwa Pamela ili kubeba vitu vyake. Walikula chakula cha mchana pamoja kabla ya kuondoka hatimaye. Pamela alimpatia boksi dogo mkononi mwake huku akitabasamu vibaya. "Kumbuka kujilinda usipate mimba.”

Lisa alikitupa kitu hicho kana kwamba ni kipande cha mkaa wa moto. "Acha ujinga sasa."

"Sawa, nilifikiria kuitumia mwenyewe. Patrick alikuja kulala hapa siku moja. Nilidhani kitu kingetokea wakati huo lakini alilazimika kuondoka ghafla." Pamela alimwambia. "Sio lazima uitumie, lakini usinilaumu kuwa sikukutahadharisha utakapopata ujauzito."

Baada ya kutafakari maneno ya Pamela, Lisa alilichukua boksi lile na kuliweka ndani ya mizigo yake. Labda Alvin alitaka kufanya naye hivyo? Bora tahadhari.

Muda mfupi baadaye, Lisa aliwasili kwenye Jumba jipya la kifahari la Alvin, mtaa wa Haile Sellasie Oysterbay. Alikuwa amehamia katika jumba la kasri la ghorofa mbili. Bustani ilikuwa kubwa na nafasi nyingi za mazoezi na mapumziko. Baada ya kugundua kuwasili kwa Lisa, Charlie alimkimbilia mara moja akifuatiwa na paka wadogo watatu. Lisa alimchukua paka mmoja mwenye manyoya meupe safi na ya kupendeza!

“Bi Kimaro? Mimi ni Shangazi Linda, mfanyakazi wa nyumbani.” Mwanamke mwenye umri wa kati ya miaka 50 alijitokeza na kujitambulisha.

Sura ya mshangao ikaangaza usoni mwa Lisa lakini punde si punde ikabadilishwa na tabasamu. Jumba la ukubwa ule bila shaka lilihitaji mtunzaji. Ikiwa angeshughulikia peke yake kila kitu humo ndani, basi hakika angekuwa mwanamke mzee aliyefifia chini ya miaka mitatu.

"Ngoja nikuonyeshe chumba chako." Shangazi Linda akamuongoza hadi kwenye chumba kimojawapo. “Hiki ndicho chumba chako cha kulala.”

“Oh, sawa. Asante.” Lisa alipatwa na mshangao. Chumba hicho cha kulala kilikuwa kikubwa kama chumba cha kulala mwanamfamle, bila kusahau kwamba kilikuwa safi na nadhifu kiasi kwamba hata shuka tu zilikuwa za gharaka kubwa. Ilikuwa ya kifahari zaidi kuliko mahali pa mwanzo.

Aunty Linda aliendelea kumwambia. “Taulo na miswaki tayari viko humo ndani. Nijulishe ikiwa unahitaji kitu kingine chochote."

Baada ya mwanamke huyo kuondoka, Lisa alianza kupanga vitu vyake. Alitoa vipodozi na kuviweka juu ya meza ya kujipodolea. Aliona mashine ya kukaushia nywele ndani ya droo pia. Kwa siri alimshukuru Aunty Linda kwa mawazo yake. Alimalizia kwa kupanga nguo zake kwenye kabati. Kwa vile ilikuwa jioni hata hivyo, alibadilisha na kuvaa nguo nyepesi akajilaza kitandani.

Godoro lilikuwa la kustarehesha sana, bila kusahau shuka laini na nyororo. Mbali na hilo, kesi yake ilikuwa ikimsumbua akili kiasi kwamba hakuweza kulala vizuri usiku kwa siku za karibuni. Hatimaye, hakuwa na wasiwasi tena. Baada ya dakika chache, akili yake ilimtoka na akapitiwa na usingizi mzito.

Gari la Alvin liliingia ndani ya jumba lake la kifahari mwendo wa saa kumi na moja jioni. Shangazi Linda alishangaa kumuona akirudi nyumbani mapema. Ijapokuwa Alvin alikuwa kahamia pale muda si mrefu uliopita, alikuwa akitoka mapema asubuhi na kuchelewa kurudi jioni kila siku. Zaidi ya hayo, kila mara alikuwa na milo yake mitatu mahali pengine. Ilikuwa ni kana kwamba nyumba hiyo ilikuwa tu mahali pake pa kulala.

“Bw Kimaro, sikuwa na wazo kwamba utarudi kwa wakati huu. Sikuandaa chakula cha jioni.”

"Ni sawa, sio lazima." Alijua alikuwa nyumbani mapema kuliko kawaida. Naam, alikuwa amejishughulisha sana na kazi baada ya Lisa kuondoka ofisini. Labda aliacha kazi mapema kwa sababu asingeweza kuacha kufikiria chakula ambacho Lisa angemwandalia. Hata hivyo, zilikuwa zimepita takribani dakika tatu tangu aingie ndani ya nyumba hiyo lakini Lisa alikuwa bado hajajitokeza kumkaribisha.

"Yuko wapi? Nje?” Alvin akatazama huku na kule huku akiwa amekunja uso.

Shangazi Linda alionekana kushtuka kidogo. “Hajashuka tangu aingie chumbani kwako. Nadhani lazima atakuwa amelala."

Alvin akainua macho kwa udadisi. Katika chumba chake tena? Naam, alikuwa mwanamke shupavu kiasi gani kulala chumbani mwake mara tu alipofika. Je, kweli alikuwa na papara kiasi hicho cha kumvuta kitandani?

Hii haikukubalika kamwe kwake. Ingawa alikuwa ameamua kuwa mwanamke wake, hakuwa amekubali watumie chumba kimoja bado. Kwa kuchukizwa, Alvin akaelekea chumbani kwake. Mlango uliachwa wazi hivyo akaingia bila kusita. Wakati akiipita mizigo yake iliyoachwa wazi sakafuni, kitu kilichofichwa kwenye lundo la nguo kilimvutia machoni.

Alvin alikiliinua kitu hicho. Alikiangalia na kupata wazo kwamba Lisa alionekana kujiandaa kikamilifu. Baada ya kukiweka kile kitu, alitembea hadi kitandani ili kumwangalia Lisa aliyelala juu yake. Nywele zake ndefu nyeusi zilikuwa zimetapakaa kwenye mto wake. Mashavu yake madogo yalikuwa na rangi ya kupendeza kutokana na usingizi mnono wa mchana.

Chumba kilikuwa na joto sana, hivyo Lisa hakuwa amejifunika chochote. Nguo nyepesi za kulalia alizovaa zilionyesha kila kitu cha ndani. Alikuwa amejiachia akijua ni chumbani kwake. Mguu wake mmoja ulikuwa umetanda juu ya kitanda, ukining'inia hewani. ‘Vibe’ katika chumba cha kulala hakika ilikuwa ya kupendeza zaidi kwa uwepo wa mwanamke huyo.

Hasira moyoni mwa Alvin ilitoweka mara moja, nafasi yake ikachukuliwa na nia ya fumbo iliyotoka ndani kabisa ya macho yake.

Lisa alikuwa katika usingizi mzito. Ghafla, alihisi kama kitu kilikuwa kikisonga midomo yake. Haikuumiza, lakini hakika ilikuwa ya kusisimua. Alijaribu kukisukuma kitu hicho lakini hakufaulu. Akiwa hana mbadala, alifumbua macho kwa unyonge. Kitu cha kwanza kilichomwingia machoni mwake ni kope nene za Alvin. Macho yake yalishushwa kidogo kana kwamba alikuwa akijishughulisha na kitu kitamu. Alvin akafumbua macho yake muda mfupi baadaye, yakakutana na ya Lisa.

Kwa nini Alvin alikuwa hapo? Lisa alitetemeka bila kujijua kabla ya kumsukuma kwa nguvu. Msukumo huo ambao haukutarajiwa ulikaribia kumfanya adondoke kitandani.

Baada ya kusimama vizuri tena, Alvin alinguruma kwa sauti nzito. "Lisa Masawe, unabeep kifo?"

"Ni kosa lako kupanda kitandani kwangu ghafla." Lisa aling’aka kwa hasira.

Alvin naye alikuwa na hasira badala ya kupigiwa kelele. “Kitanda chako?” Alicheka kwa hasira. “Angalia ujasiri huo. Kwa hiyo kitanda changu kimekuwa chako ghafla?”

Akiwa amekasirika, Lisa aliunguruma. “Najua hii ni nyumba yako, kwa hivyo unamiliki vitanda vyote. Lakini kwa kuwa nimekubali kuhamia, unapaswa kuniruhusu nafasi yangu binafsi pia. Ni utovu wa adabu sana kuingia chumbani kwangu bila hata kubisha hodi.”

Alvin alimtazama juu chini huku midomo yake ikilegea kwa tabasamu la kejeli. “Unalala kitandani kwangu, chumbani kwangu, na bado una shavu la kulalamika kwamba sikupi nafasi ya kibinafsi? Umeondoka kwa muda mfupi tu lakini kujiamini kwako kumeongezeka.”

Lisa alishtuka baada ya kusikia hivyo na hatimaye akaja kufahamu. "Subiri, unasema hiki ni chumba chako cha kulala?"

"Acha kujifanya." Alvin alisogea mbele na umbo lake refu, na ghafla akajitupa na kuanguka chali kwenye kitanda. Aliweka viganja vyote viwili pande zote za masikio yake. Tabasamu likatanda usoni mwake huku akimtazama. "Hakika una mipango mizuri. Kuishi nyumba moja hakukuridhishi vya kutosha? Kwa hivyo unataka kulala kitanda kimoja pia, huh?"

Lisa alipigwa na butwaa kwenye ukimya. Je, alilala chumbani kwake mchana mzima tangu afike? “Hapana, sikuwa na habari. Shangazi Linda ndiye aliyeniongoza hapa.”

“Sawa, sawa, na sasa unamlaumu Aunty Linda.” Alvin alimshika Lisa kwa kidevu kabla ya kugeuza macho yake kuelekea chini. “ Tizama na nguo ulizoamua kunivalia chumbani kwangu, mbinu zako za kunitega ni za kibunifu sana wakati huu.”

Lisa hakuwa na la kusema. Hiyo haikuwa nia yake hata kidogo. Alikuwa amevaa tu nguo za mapumziko alizonunua kutoka mitaani kwa bei nafuu.

“Najua unatamani sana kuwa nami, lakini angalia wakati. Usiku bado haujaingia.” Akamshika viganja vyake huku akizidi kumsogelea taratibu.

Moyo wa Lisa ulikuwa ukidunda kwa nguvu ndani ya kifu chake. “Naapa kwa Mungu kwamba niliingia hapa tu kwa sababu Aunty Linda alinionyesha na kuniambia ni chumba changu.”

"Bado unajaribu kubishana, huh?" Alvin alitania, kabla ya kuchomoa kitu mfukoni taratibu. "Niambie haukutayarisha hii kwa makusudi?"

Mashavu ya Lisa yakaumuka kwa mshangao na kuvimba kama mimba ya panya huku akitazama lile kasha dogo mkononi mwa Alvin ambalo Pamela alikuwa amempa kabla ya kuondoka. Sasa kwa kweli hakuwa na nafasi ya kujitetea kutokuwa na hatia kwake.

“Napenda mwanamke mwaminifu. Ni sawa kujifanyisha mara moja baada ya nyingine lakini kujidai kupita kiasi hakika ni kukera.” Alvin aliinamisha kichwa chake tayari kuweka busu kwenye midomo yake ya kupendeza.

Akiwa amechanganyikiwa, Lisa alimsukuma kifuani kwa nguvu zake zote. “Hebu tuelekee chini kwanza chakula cha jioni kwanza. Umefanya vyema kuniamsha kwani ningelala mpaka kesho.”

Alvin aliganda ghafla baada ya kusikia maneno yake. Tumbo lake liliguna alipofikiria juu ya chakula ambacho alikuwa akienda kuandaa. “Sawa, tutaendelea na kesi yetu usiku wa leo.”

Alisimama na kumrushia boksi lile la kondomu huku akiachia tabasamu la kejeli. "Ondoa hii, mjinga wewe."

Sura ya 78

Baada ya kuteremka, Lisa alijitosa hadi jikoni. Shangazi Linda alipomkaribia ili kumsaidia kuchagua viungo, Lisa hakuweza kujizuia kuuliza, “Aunt Linda, kwa nini umenipeleka chumba cha kulala cha Alvin mchana huu?”

Mwanamke mtu mzima alishikwa na butwaa. “Si ninyi wawili mmeoana? Niliona cheti cha ndoa yenu nikiwa nafanya usafi chumbani kwake hapo awali.”

Maneno ya Aunty Linda yakamkaba kooni Lisa . "Kwa kweli, sisi ni ..."

“Mpo kwenye marumbano?” Aunty Linda akamkatiza, “Nimewahi kushuhudia haya pia. Ulihama muda si mrefu uliopita? Fikiria kuchukua hatua nyuma kwa kuwa hatimaye umerejea nyumbani. Wanandoa hawapaswi kulala katika vyumba tofauti au uhusiano utapoteza shauku yake.”

Aunty Linda aliendelea. "Nyumba sio nyumba bila mmiliki wake wa kike. Nyumba ilikuwa kimya sana nilipoajiriwa siku chache zilizopita. Bw.Kimaro angeondoka mapema na kurudi nyumbani usiku sana. Angalia, mambo yamebadilika tangu kurudi kwako. Hii ni mara ya kwanza kwake kufika nyumbani mapema hivi. Haraka, jitahidi upate mtoto. Nitakuwa mlezi wa mtoto kwa furaha.” Lisa akiwa hoi, alinyamaza huku Aunty Linda akizidi kukazia mada.

Usiku huo, Lisa alimuandalia Alvin chakula cha nyota tano. Furaha yake iliongezeka mara moja baada ya kuona aina zake zote za vyakula alizozipenda zimeenea kwenye meza. Mwanamke huyu bado alikumbuka vipendeleo vyake. Baada ya Alvin kula sahani tatu za chakula, Charlie alimwendea akiwa na paka watoto watatu.

“Wana majina?” Lisa aliuliza huku akiokota mmoja kati yao.

"Bado." Alimtazama Lisa kisha akamtazama tena paka kabla ya kusema ghafla, “Lakini nimekuja kufanya uamuzi sasa, kwa sababu kuna jike moja na madume wawili, wanaitwa Lisa, Jones na Masawe.”

Lisa hakuwa na la kusema. “Kwa nini?”

“Imenijia tu akilini. Ni majina rahisi tu au sivyo?,” Alvin alisema. Kisha, akaelekea kwenye maktaba yake.

Shangazi Linda akasogea huku akitabasamu. "Wanandoa wachanga wa kupendeza."

Lisa hakuthubutu kuongea tena na Aunty Linda baada ya mazungumzo ya awali. Mara moja, alipanda juu haraka na kuhamisha vitu vyake kwenye chumba cha wageni.

Saa sita usiku Lisa aligundua kuwa Alvin alikuwa bado hajaondoka kwenye chumba chake cha maktaba alikokuwa akifanya kazi zake. Labda alitingwa na tafiti za kesi yake mahakamani. Ilikuwa ni changamoto kweli kweli. Kwa huruma, akamtengenezea bakuli la uji wa ulezi. Alibisha hodi kwenye mlango wa maktaba.

“Ingia ndani.” Aliingia na uji baada ya kupata ruhusa ya mwanaume huyo.

Kama hapo awali, alikuwa akisoma hati na miwani yake. Nuru ya mwanga chumbani mle iliangazia kwa upole umbo lake lenye sifa nzuri. “Nilikuwa na wasiwasi kwamba unaweza kuwa na njaa.” Alitembea kumwendea akiwa na bakuli la uji wa ulezi.

"Ninaweza kuwa na njaa baada ya kula sahani tatu za chakula wakati wa chakula cha jioni?" Alvin aliinua macho. “Au unadhanimimi mroho sana wa kulakula hovyo?”

Lisa alikuwa amesahau kabisa hilo. "Jaribu hata hivyo." Aliweka bakuli kwenye meza. Kisha, akamvuta karibu na kukaa kwenye mapaja yake. Mapigo ya moyo wa Alvin yakaanza kudunda kuliko kawaida. Ilionekana ajabu kwamba ni Lisa ndiye aliyeanza kumchokoza muda huo.

"Unaniletea chakula kwa makusudi kumbe una shidazako zingine?" Alvin akamnong'oneza sikioni.

Lisa alikosa la kusema. “Nilitaka tu kukushukuru.”

“Unadhani nitaamini hivyo?” Macho yake yalidhihirisha wazi kuwa haikuwa hivyo. Pamela alikuwa ameweka picha kichwani mwake kwamba Lisa alikuwa akimpenda sana na hakujiweza kwake.

“Unafanya uchunguzi wa kesi yangu?” Lisa alibadilisha mada ya mazungumzo kwa makusudi.

Haikuwa hivyo, kwa asili. Kesi rahisi kama hiyo haikustahili wakati wake wa baada ya kazi. Alikuwa akikagua tu ripoti za faida za kampuni alizowekeza, ingawa kwa sababu fulani, aliitikia kwa kichwa.

Kwa ujanja alivuta nyaraka zilizohusiana na kesi yake na kusema kana kwamba amechanganyikiwa sana, “Kesi yako ni ngumu sana. Jones Masawe alifuta ushahidi mwingi ili kumlinda James.”

Lisa alisisimka baada ya kusikia hivyo. "Bado kuna matumaini ya kushinda?"

“Kushindwa? Sijawahi kushuhudia hilo,” Alisema kwa dharau, lakini kila neno lilikuwa na kiburi.

Kwa kweli Lisa hakujua la kusema zaidi. Lakini, alikiri kwamba wanaume huwa wa kuvuta wakati wakiwa wamejawa na ujasiri, haswa mwanaume kama Alvin ambaye sura yake tayari ilikuwa nzuri. Aliona aibu kidogo kumuona Alvin akimtazama kwa karibu bila kupepesa macho. Je, alikuwa anaweza kuwa na kiasi fulani cha kujizuia? Alikuwa bado anafanya kazi.

Alvin ghafla alikumbuka jinsi Lisa alivyokuwa na busu tamu na kumwinua mikononi mwake mara moja. “Twende chumbani.” Sura ya kuchanganyikiwa ikaangaza katika uso wake.

"Subiri, si unafanya kazi?" Lisa alimwambia huku kimoyo cha hofu kikimdunda na sauti yake ikitetemeka kwa hofu pia. Alikuwa ameliamsha dude yeye mwenyewe!

"Nilidhani ulitaka niache kazi?"

Lisa akamtupia jicho la pembeni. “Ni lini nilisema hivyo?”

"Ulisema kwa sauti kubwa na wazi kwa macho yako." Alvin alimtazama kwa unyonge kabla ya kuelekea chumbani, akiwa bado amembeba mikononi mwake.

Alijisikia kulia wakati huu. Je, hakumwelewa au kulikuwa na kitu? Alvin alipoanza kuvua nguo zake mbele yake, alianza kutambua kitakachofuata…

Mara moja Lisa akaketi kitandani. "Hapana, niko kwenye siku zangu."

Macho yake yalimtoka kwa hasira. Ulikuwa ni wakati ambao Alvin alikuwa kapandisha mizuka hatari kiasi kwamba alitamani kwenda nje ili kutimiza matakwa yake. Ni balaa gani.

Kwa upande mwingine, Lisa alishusha pumzi kwa siri. Kwa bahati nzuri, hedhi yake ilianza wakati alipokuwa anaoga mapema. Kusema kweli hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Alvin kuhisi msukumo mkali wa kushiriki mapenzi tangu amuoe Lisa.

"Sawa, nitarudi chumbani kwangu." Lisa alisema kinyonge.

Ndita kati ya nyuso za Alvin zilizidi kuanika hasira zake za moyoni. “Si unalala chumbani kwangu?”

“Sitaki kukusumbua.” Hakika hakutaka kulala chumba kimoja naye.

“Ni sawa, lala tu hapa. Sitaki tena uje kunigongea mlangoni utakapoanza kuweweseka kwa ndoto zako za jela.” Akamrudisha kitandani. “Nipatie nguo mpya za kubadilisha. Ninaenda kuoga.”

Lisa hakuwa na la kusema. Akawajibika pia kumwandalia nguo Alvin kama mke wake halisi. Alimletea nguo na akaingia nazo bafuni. Wakati wa kuoga, Alvin alifikia hitimisho kwamba ilikuwa vizuri kuwa na mwanamke nyumbani.

Baada ya kuoga, Alvin aligundua kuwa Lisa tayari alikuwa amelala ndani ya blanketi, lakini, alikuwa amejikunyata mwisho wa kitanda. Akaingia kitandani na kumsogeza karibu yake.

"Nini jamani?” Lisa alihisi kero.

"Sogea katikati. Sitaki kusikia ukianguka kitandani usiku,”

Kwa mujibu wa rekodi, hii ilikuwa ni mara ya pili kwa wawili hao kulala katika kitanda kimoja. Wote wawili walikuwa wamechoka sana mara ya kwanza na walilala moja kwa moja, lakini wakati huu, ilikuwa tofauti.

Alvin alikuwa amemkumbatia Lisa kwa nyuma. Alihisi kwa mara ya kwanza kwamba harufu ya mwanamke huyo ilikuwa imejaa kitandani kabisa. Isitoshe, mwili wake ulikuwa laini sana hivi kwamba ulikuwa mzuri zaidi kuliko mto. Hakutaka kujiachia.

Kwa upande mwingine, Lisa alikuwa akipitia hisia tofauti na Alvin kabisa. Hakuweza kujisikia raha hata kidogo. Maumivu ya tumbo ya hapa na pale yalimfanya awe macho. Angeweza tu kujaribu kuzunguka kwa upole mikononi mwake ili kupata nafasi nzuri zaidi.

"Unafanya nini?" Kuhangaika kwa Lisa kulimmnyima Alvin usingizi.

"Nina maumivu ya hedhi. Je, ninakupotezea usingizi? Ni bora nilale tu kwenye chumba cha wageni.” Aliinuka na kutaka kuondoka.

Alvin alimzuia mara moja na kuweka mkono wake mkubwa wenye joto juu ya tumbo lake.

“Unaumwa hapa?"

“Ndiyo.” Akaanza kumpapasa eneo lile kwa upole. Sauti yake ilisikika haswa katika usiku wa utulivu.

"Unajisikia vizuri sasa?"Mkono wake mkubwa ulifanya maajabu kama tishu ya joto. Lisa alijisikia vizuri na maumivu yake yalipungua kwa dakika chache.

Kitu cha ajabu pia kilionekana moyoni mwake. Ingawa Lisa alikuwa na uhusiano na Ethan hapo awali na Ethan alimtendea vizuri, wawili hao hawakuwa wamewahi kulala kitanda kimoja—bila kusahau kuchua tumbo lake. Kwa kweli hakutarajia Alvin, mwenye hulka ya kibabe angefanya kitu kama hicho. Isitoshe, alikuwa mvumilivu sana. Mwishowe, yeye ndiye alikuwa na aibu.

"Sawa, haina maumivu tena “ Lisa aliitika kwa aibu.

“Nyamaza na ulale sasa.” Alvin aliamuru bila kuuzuia mkono wake.

Lisa hakuthubutu kuongea zaidi. Muda si muda, kwa sababu maumivu yalikuwa yamepungua, alilala usingizi mzito.

Sura ya 79

Asubuhi iliyofuata saa kumi na mbili asubuhi, Lisa alishtuka kutoka usingizini alipokuwa na kushuka kitandani kwenda kuandaa kifungua kinywa.

"Unaenda wapi?" Alvin aliuliza.

“Endelea kulala. Nitaandaa kifungua kinywa…” Lisa akamwambia kwa upole.

"Sio lazima ufanye hivyo kwa kuwa haujisikii vizuri." Kwa mara nyingine tena, akamvuta mikononi mwake. Aliweka kiganja chake juu ya tumbo lake tena.

"Haina maumivu tena." Lisa alijaribu kumzuia.

“Oh.” Akafumba macho tena. Wakaendela kulala kuufaidi usingizi wa asubuhi pamoja.

Siku ya kesi ilikuwa imefika hatimaye! Siku ya kesi, Lisa, Alvin, na msaidizi wake, Hans walifika mahakamani pamoja. Walipofika mahakamani hapo, ghafla simu ya Alvin iliita wakati wanashuka kwenye gari. Ilikuwa ni simu kutoka kwa Mzee Mayanja.

"Hans, mpeleke Lisa kwenye chumba cha mahakama. Nahitaji kupokea simu hii.” Alitembea pembeni baada ya kusema hivyo.

Lisa na Hans waliingia kwenye lifti. Kundi la watu lilikuwa limesimama nje ya lifti dakika moja walipotoka—pamoja na wanandoa wa Masawe, kulikuwa na Lina, James, Clark Zongo pamoja na wakili wake.

Clark alimwendea Lisa , akionekana kuwa na hasira. "Lisa Masawe, furahia dakika zako chache za mwisho ukiwa huru. Maisha yako ya uraiani yatafikia mwisho kesi hii itakapofungwa.”

Lisa hakuwa na mashaka. Baada ya yote, Clark pia alikuwa mwathirika wa ajali hiyo ya moto. "Bw. Zongo, amini usiamini, sina uhusiano wowote na tukio hili."

"Hauhusiki kivipi?" Clark aliuliza kwa hasira. “Ni wewe uliyekuwa ukinisumbua nikupatie mradi huu na kuahidi utaniundia hoteli ya kipekee zaidi. Kila kitu kinasambaratika sasa. Sijali ni kiasi gani umefaidika na mradi huu au ni nani mwingine uliyemhonga, lakini lazima uwajibike kwa tukio hilo.”

Mzee Jones Masawe alishusha pumzi kabla ya kwenda mbele. “Bw Zongo, ni kosa langu kwamba sikumfundisha binti yangu vyema. Kwa kweli sikupaswa kumpa mradi mkubwa kama huo. Usijali, Kibo Group itachukua jukumu kamili kwa uharibifu uliokugharimu wakati huu. Nitakufidia na kuahidi kutumia vifaa vya ubora wa juu zaidi wakati huu.”

“Natumai utatimiza ahadi yako. Nitaajiri timu ya wataalamu ili kukagua maendeleo katika hatua ya baadaye. Ikiwa kuna kitu kitaenda vibaya tena, basi itakuwa wewe ambaye utapelekwa gerezani, Bw Masawe." Zongo hakuweza kuhangaika kushughulika na akina Masawe tena. Aliondoka na wakili wake baada ya kusema hivyo.

Uso wa Masawe ulibadilika baada ya Zongo kuondoka. "Lisa, umenivunja moyo sana."

"Baba, ni wakati wa kusitisha mchezo mchafu unaoucheza." Lisa nusura apasuke kwa hasira wakati anaongea maneno hayo. "Ni wazi kuwa James ndiye mtu aliyesababisha hujuma hii. Sio lazima kunipenda lakini mimi ni binti yako wa kuzaliwa. Je, mimi si chochote kwako kuliko mpwa wako ambaye hana uhusiano wa damu na wewe?”Hisia ngumu ikaangaza machoni pake.

Mama Masawe aliingilia kati mara moja. “Unaongea upuuzi gani? James hana hatia. Sio tu kwamba unaharibu sifa ya kampuni ya Kibo Group lakini pia unajaribu kumpaka matope binamu yako sasa? Unawezaje kuwa hivyo. Ukatili ulioje?”

"Mama, mimi ni binti yako!" Lisa alipiga kelele kwa jazba. "Unajua kuwa James aliwahonga wafungwa ndani ili kuniua?"

"Haya, achana na ujinga huo." James alifoka, “Kusingizia uongo ni kosa. Una ushahidi wowote?"

“Nyamaza kama huna uthibitisho wowote.” Mama Masawe alimkazia macho Lisa . "Ni nini kingine unaleta kwa familia mbali na matatizo? Unastahili hali uliyonayo leo. Chukua muda kujitafakari ukiwa gerezani!”

Lisa aliduwaa kama mtu aliyepigwa na kitu kizito kichwani. Siku zote watu walisema kwamba hata simba hawezi kula watoto wake, lakini alihisi kwamba Mama Masawe na Mzee Msawe walikuwa wakali kuliko simba, tayari kabisa kumla mtoto wao.

"Nyinyi wawili adhabu yenu inakuja!" Lisa alifoka kwa hasira, “Ni jambo moja kwamba mlinitendea kwa ubaya na dharau siku za nyuma lakini hamkupaswa kuendelea kufuatilia maisha yangu ili kuyaharibu. Ninaahidi nitachukua muda wangu kuiharibu Kibo Group!”

Lina alicheka kwa kejeli. “Unafikiri una muda mwingi uliobaki? Wakili wa Zongo alisema kuwa utapewa kifungo cha angalau miaka 20. Dada yangu mpendwa, jitunze ukiwa gerezani. Nitakutembelea nikipata muda.”

"Nyinyi nyote mnaonekana kuwa na hakika kwamba nitafungwa." Lisa alidhihaki kuona nyuso hizo ambazo hazikuweza kusubiri kumtupa gerezani.

James naye akaibuka kwa jeuri, “Ni vizuri kuwa na matumaini, lakini labda kuna kitu huelewi. Zongo amemwajiri Harry Stewart, wakili bora katika Dar es Salaam yote, wakati wewe…” Alimtupia jicho la haraka Hans kabla ya kutoa dhihaka za kejeli. “Ha, huyu ni nani? Je, umeajiri mwanafunzi aliyehitimu kutoka shule ya sheria hivi karibuni kuwa wakili wako?” Akasogea kumshika kifua Hans. “Haya, mwenzangu, unajua unapingana na nani? The Zongos! Usipite kwenye mlango huo na kuharibu maisha yako ya baadaye. Ushauri wangu kwako ni kwamba uondoke haraka iwezekanavyo.”

Hans aliinua macho kwa mshangao. Hakika, alikuwa na uso mdogo, kwa hivyo wengine waliweza kumdhania kama mhitimu wa hivi majuzi.

Lina alipendekeza kwa fadhili, “Hakuna mtu anayethubutu kuchukua kesi ya Lisa. Pengine hujui mengi kwani bado wewe ni mgeni kwa jumuiya ya wafanyabiashara. Lakini tunasema haya kwa faida yako mwenyewe.”

“Kwa nani?” Sauti yenye kishindo ilisikika ghafla. Lisa alijua sauti hiyo ni ya nani bila ya kumtazama mwenyewe. Ghafla, alitamani sana kuona sura zao watakapokabiliwa mahakamani baadaye. Lina, Jones, na wengine wakahamishia macho yao kwenye chanzo cha sauti hiyo.

Sekunde chache kabla, milango ya lifti ilifunguliwa na ndani yake akatoka kijana mrefu. Suti ya kijivu nyepesi ya kijana huyo ilisisitiza kikamilifu muundo wake wenye nguvu na mrefu. Uso wake mzuri lakini wenye kutisha haukuonyesha hisia zozote. Macho yake tulivu na makini yalipotazama nyuso za walio mbele yake, wale wengine hawakuweza kujizuia kutetemeka kidogo.

Alikuwa ni yeye! Lina alimtambua mtu huyo ndani ya sekunde chache. Alikuwa mtu ambaye alijitokeza katika mgahawa Grapefruit na Sam mara ya mwisho. Huyu ndiye aliyekuwa amewaagiza wahudumu wa mgahawa huo wamtoe yeye na marafiki zake kwa kuwadhalilisha pale mgahawani. Janet alikuwa amemfuatilia baada ya hapo na kugundua kuwa alikuwa wakili tu. Je, alikuwa wakili aliyechukua kesi ya Lisa?

"Sikujua kuwa uko karibu na watu hawa." Macho makali ya Alvin yalimgeukia Hans huku akiongea kwa upole.

Hans alielezea kwa tabasamu la heshima, "Walidhani kwamba mimi ni wakili wa Bi Lisa na walidhani kwamba mimi ni mhitimu mpya."

"Uso wako… Hakika, unaonekana kinda sana," Alvin alitoa maoni baada ya kuangalia haraka. Hans alitabasamu na kunyata taratibu.

James alielewa kinachoendelea sasa. Hata hivyo, kwa kuwa alizoea kuungwa mkono na Masawe wakati huu wote, alikuwa amechukua mtazamo wa kiburi. Hakumfikiria sana Alvin. “Oh, nimeelewa sasa. Wewe ni wakili wa Lisa ? Sigh, mtu mzuri kama wewe haipaswi kuwa na kazi kama wakili. Tafuta tu ‘li-sugar mamy’ moja hapa mjini likulee na nina uhakika unaweza kuishi maisha bora kuliko haya."James aliropoka kwa msauti wake uliosheheni dharau za kutosha.

Dokezo la mshangao likaangaza machoni pa Hans. Naam, mtu wa mwisho ambaye alithubutu kuzungumza na Alvin kwa sauti hiyo alikuwa kaburini kwa muda mrefu.

Sura ya 80

Lisa pia alimtupia jicho Alvin kwa woga, na kuona tu kwamba alibaki bila kujali kana kwamba hakuwa ametukanwa tu.

"Kipande cha takataka hakistahili kuongea nami." Alvin akarudisha macho yake makali na kumgeukia Lisa. “Twende!” Alvin akaongoza kuelekea chumba cha mahakama. Haraka Lisa akafuata nyuma yake.

“Aunt, nitakuwa sawa?” James alitetemeka alipokaribia kuingia kwenye chumba cha mahakama. Yeye na familia ya Masawe ilibidi wawepo mahakamani kama mashahidi.

Mama Masawe alimtazama kwa upole. “Usijali, Mjomba wako Masawe amesafisha ushahidi wote uliobaki. Uko hapa tu leo kama shahidi.

“Utakuwa sawa. Lisa hana pesa, hana ushawishi wala marafiki wakueleweka. Angewezaje kuajiri wakili mwenye uwezo zaidi kuliko Bw. Stewart?” Jones Masawe alisema kabla ya kuwaongoza wengine kwenye chumba cha mahakama.

Sura ya matumaini ikaangaza usoni mwa James. "Lakini Lisa anaonekana hana wasiwasi kabisa, kwani huyu kijana aliye naye ni nani, mbona ni mgeni machoni pangu na anaonekana kujiamini sana?" Jones Masawe alitoa mkoromo wa dharau.

Lina alikunja uso na kujibu. “Nimewahi kumuona huyu jamaa. Yeye ni rafiki mzuri wa Sam Harrison. Ni yeye aliyeamuru mimi, Janet, na Cindy tutupwe nje ya mgahawa mara ya mwisho. James, labda unapaswa kutazama mdomo wako.”

"Nini? Yeye ni rafiki wa Sam Harrison?!" James alishikwa na mshangao kabisa lakini punde akapata utulivu. "Ni sawa, Zongo hakika atamwadhibu kwa kuchukua kesi ya Lisa. Nina uhakika Sam Harrison hatomuunga mkono kwa kumhofia Zongo.”

Milango ya lifti ikafunguka tena. Wakati huu, Kelvin na Ethan walitoka humo kwa wakati mmoja. Ethan aliuma meno yake kwa hasira mara ya pili alipomuona yule Lina. “Lina, wewe b'*stard. Lazima nilikuwa kipofu hata nilikuamini!”

"Angalia mdomo wako!" Mzee Jones Masawe alikemea, “Wewe ndiye uliyetaka kumdhulumu binti yangu. Ni aibu. Jiangalie vizuri sasa. Humstahili hata kidogo.”

Ethan alicheka ghafla huku akigeuka kumtazama Masawe. “Ulikuwa unaona fahari na kunichukulia kama mwanao kwa sababu tu nilikuwa mrithi wa Lowe Enterprises. Sasa nimepoteza urithi sina thamani tena kwako, Lina hakika ni binti yako wa kuzaliwa. Nyinyi watatu mnafanana kabisa.”

Lina alichukia vibaya sana kwa maneno ya dharau kutoka kwa Ethan. “Niliyatambua mawazo yako tangu mapema. Ulinichumbia tu kwa sababu mimi ndiye mrithi wa Kibo Group.”

“Wewe…” Uso wa Ethan ulikuwa umetanda hasira tupu. Alikuwa karibu kutema maneno makali wakati Kelvin alipomkumbusha, “Hiki ni chumba cha mahakama. Si mahali pa kubishana.” Hakuwa na jinsi zaidi ya kunyamaza.

Hata hivyo, ndani ya chumba cha mahakama, hali ilikuwa ya wasiwasi upande wa mlalamikaji.Clark Zongo alikuwa amevaa sura ya huzuni. Pembeni yake, wakili wake Bw. Stewart, alikuwa akinywaa maji huku akionekana kushangaa.

Kwa upande mwingine, Lisa alikuwa akipiga soga kwa furaha na Pamela. Mwisho hakuweza kuacha kucheka. Wakili aliyekuwa kando yake hata alikuwa akicheza michezo ya kuchangamsha akili kwenye simu yake.

“Nitajua nini kinaendelea." Wasiwasi ulimwingia Masawe kwa mbali alipokuwa akimkaribia Zongo. “Bw. Zongo, nini tatizo la wakili Stewart? Haonekani sawa kwangu.”

Clark alijibu kwa sauti ya kukata tamaa, "Binti yako ni kichwa kweli!"

Jambo hili lilimshangaza sana Masawe. Bw. Stewart alieleza huku akihema, “Lisa ameajiri wakili msomi ambaye hajawahi kushindwa kesi hapa Tanzania kama wakili wake. Ni changamoto kubwa kwangu kushinda kesi hii.”

"Ni hadithi gani unayotuletea?!" Jones Masawe alishangaa. “Ndivyo ulivyoahidi? Ulituambia hakika utashinda."

Muonekano wa uso wa Stewart ulidhihirisha kukerwa kwake na ujinga wa mtu huyo. "Sikujua kama mtu ninayepambana naye ni huyu! Wewe ni bosi wa kampuni kubwa ya biashara. Hujasikia kuhusu wakili msomi wa kimataifa Alvin Kimaro? Hajawahi kushindwa kesi yoyote ingawa bado ni mdogo. Yeye ni wa ajabu. Hakuna anayeweza kumshinda. Lazima niwe mkweli tu.”

Jambo hilo lilimfanya Jones Masawe anyamaze kimya. Haishangazi Lisa hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo. Ni lini alifahamiana na mtu kama huyo? "Bw. Stewart, una uhakika gani atashinda?" Masawe aliuliza kwa kuhema.

Wakili alikunja uso huku tabasamu la ajabu likienea usoni mwake. “Bw. Masawe, wewe ni mtu wa ajabu. Lisa ni binti yako, baada ya yote. Unapaswa kufurahi ikiwa atashinda."

Masawe alikosa cha kusema. Lengo lake lilikuwa Lisa aende gerezani na hiyo ilikuwa ni fursa muhimu kwake. Masawe akarudi kwenye kiti chake kwa huzuni sana baada ya kusikia hivyo.

Wakati huo huo, mahakama ilikuwa tayari kuanza kusikiliza kesi hiyo. Lisa alianza kuhisi woga. Alimtazama kwa haraka Alvin aliyekuwa amekaa karibu yake, na kumuona tu akiiweka simu yake ya mkononi ndani ya droo ya meza, huku akiwa ameweka uso wake sawa. Alijiendesha bila kujali kana kwamba hayupo mahakamani bali anafanya shopping au anatalii.

Hakimu kiongozi aligonga nyundo kutangaza kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo. Wakili wa Clark Zongo alisimama kuwasilisha ushahidi na taarifa husika. Kisha akatangaza uhalifu wa Lisa. Jopo la mahakimu waliitikia kwa kichwa huku wakisikiliza. Kosa hili liliungwa mkono wazi na ushahidi wa uhakika.

Hakimu kiongozi akageuka kumkabili Alvin. "Mapingamizi kutoka kwa mshtakiwa?"

Alvin aliinuka hadi urefu wake kamili, macho yake yakionekana kutulia. “Mteja wangu hakuwa na uhusiano wowote na tukio hili tangu mwanzo kwa hiyo hana hatia. Kila kitu kilikuwa jukumu la meneja wa mradi James Komba peke yake.”

Mahakama nzima iliingia kwenye vurugu baada ya kusikia hivyo. James akasimama huku akifadhaika. "Hiyo ni bullsh*t!"

Hakimu msimamizi alionya, “Chunga lugha yako.” Sekunde fupi baadaye, hakimu alizungumza tena, "Wakili wa utetezi, una ushahidi wowote?"

Alvin akatoa lundo la ushahidi. "Hii ni historia ya mazungumzo kati ya James Komba na mtu wa kati, Terry Mayanja. Inaonyesha kuwa Mayanja ndiye aliyeweka nyaya feki za umeme zenye ubora duni na kuziuza nyaya halisi na faida iliyopatikana aligawana na James Komba. James Komba alipata milioni sitini kutokana na mkataba huu ambapo Terry Mayanja alipata milioni kumi. Pia kuna picha za James Komba na Terry Myanja wakitembelea kilabu ya starehe pamoja.”

Baada ya rekodi za mazungumzo na picha kuwasilishwa kwa hakimu msimamizi, James alianza kuhisi wasiwasi. Alijitokeza tu kama shahidi, bila kutarajia kesi kumgeukia. “Sikufanya hivyo. Hii ni kashfa.”

"Ikiwa hufikiri kuwa ushahidi huu unatosha, basi tafadhali, niruhusu nimwite Terry Mayanja kama shahidi," Alvin alisema kwa utulivu.

Punde Terry aliletwa kwenye chumba cha mahakama. Alvin alimkazia macho mtu huyo kana kwamba anataka kumtoboa na macho yake. “Ni nani aliyeshirikiana nawe kubadilisha nyaya orijino za umeme na kuweka feki?”

Terry alifunganisha macho yake na James na kumwelekezea James. “Ni yeye.”

Akiwa amechanganyikiwa, James akapaza sauti, “Unasema uongo. Hukupokea rushwa kutoka kwa Lisa?"

Terry alijibu kwa upole, “Si yeye bali ni wewe uliyenihonga. Baada ya moto kuangusha hoteli, ulihamisha shilingi milioni kumi kwa mwanangu ambaye anasoma nje ya nchi na ukaniamuru nipeleke lawama kwa Lisa Masawe.” Rangi zote zilimtoka James usoni. Mama Masawe alianza kuonekana kuwa na wasiwasi pia.

Zongo alikasirishwa. “Kwa hiyo ni wewe uliyebadilisha nyaya za umeme! Kwanini unajaribu kunihadaa kwa kuelekeza lawama kwa Lisa Masawe?”

TUKUTANE KURASA 81-85

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.....LISA
KURASA....81-85

Sura ya 81

Tabasamu la fumbo likaangaza usoni mwa Alvin. "Bw. Zongo, familia ya Masawe hata inamtoa binti yao wenyewe kama mbuzi wa kafara. Hawajaribu kukudanganya, wanajaribu tu kumwangamiza Lisa na kumwokoa mpwa wao.”

Maneno ya Alvin yalizua vurugu kwenye chumba cha mahakama. Kila mtu akawa anaongea lake.

“Unafikiri Jones Masawe anajua kuhusu hili?”

“Asijue wakati yeye ndiye mkurugenzi wa Kibo Group?”

“Ee Mungu, nafikiri James Komba ni mwanawe wa haramu? Kwa nini atoe dhabihu binti yake ili kumlinda mpwa wake?”

"Nilisikia uvumi hapo awali kwamba familia ya Masawe haimpendi binti huyu. Inageuka kuwa kweli. Ni waovu.”

Familia ya Masawe iliaibishwa kabisa mahakamani hapo. Jones Masawe alisema bila subira, “Wakili Kimaro, tafadhali chagua maneno yako kwa uangalifu. Mke wangu na mimi hatukujua kuhusu hili. Hatukujua kuwa Terry alihongwa.”

Alvin aliitikia kwa kichwa taratibu kabla hajatoa risiti. "Labda ninyi wawili hamna habari, lakini si muda mrefu uliopita, Bw. Masawe alipokea gari jipya aina ya VolksWagen lenye thamani ya shiingi milioni arobaini kutoka kwa James Komba."

Maneno yakazuka tena ndani ya chumba cha mahakama. "Wow, kwa hivyo alifumbia macho kwa sababu alipokea hongo kutoka kwa mpwa wake."

“Bila shaka. Kwa nini msimamizi wa ujenzi awe na kiburi kiasi hicho? Ni dhahiri alipata uungwaji mkono kutoka kwa bosi mkuu wa Kibo Group.”

"Sifa ya kampuni ya Kibo Group imeharibika. Aibu kwa kuwa moja ya kampuni zinazotambulika za ujenzi na usanifu nchini.”

"Hatupaswi kamwe kushirikiana nao siku zijazo."

"Kibo Group inapaswa kufilisika hivi karibuni. Kampuni chafu iliyoje."

Baada ya dakika chache, sio tu waliokuwa katika chumba cha mahakama walikuwa kwenye mjadala mkali kuhusu kesi hii ya mahakama, bali ulimwengu wa mtandaoni pia.

Baada ya yote, mwenendo wa kesi hiyo uilikuwa ukionyeshwa moja kwa moja kwenye mtandao. Idadi ya watu waliotazama iliongezeka sana kila dakika. Masawe alifikiri angezimia. Hakika hakutarajia wakili huyu kuwa amefahamu kuhusu gari la VolksWagen. Mshenzi!

Lina, ambaye alihisi mambo yanazidi kwenda kombo, alisimama haraka na kutoa maelezo. "Inakaribia siku ya kuzaliwa ya baba yangu hivi karibuni. James alimpa zawadi mapema tu. Je, hii inaweza kuwa ni tuhuma? Wakili Kimaro, bila ushahidi madhubuti, yote uliyosema hivi punde ni mashtaka matupu."

"Mashtaka matupu?" Alvin alijibu kwa kucheka, lakini macho yake yalidhihirisha dhamira kubwa. "Sijaituhumu familia yako hata kidogo. Nimemaanisha kuwa James alinunua hilo gari kwa pesa za hujuma."

Watu wakaanza kunong’ona tena; “Hiyo ni sawa. Wakili hakusema lolote lakini familia hii wanajishtukia.”

"Nina hakika kuwa ni dhamiri zao zinawasuta."

Lina aliganda papo hapo. Jasho likaanza kutomka kwenye uso wake taratibu. Wakili huyu alikuwa mkali sana. Aliweza kuharibu upande wao kwa maneno machache tu.

“Sawa, sasa rudi kwenye mada kuu.” Hakimu alimkumbusha Alvin.

Umakini ulirudi kwenye uso wa Alvin ndani ya sekunde chache. "Mheshimiwa, sio tu kwamba James Komba alibadilisha kwa siri nyaya orijino za umeme za Hoteli ya Lublin na kuweka zile feki, lakini pia alitumia nyenzo za maji zisizo na kiwango kwa ujenzi. Kwa kawaida, mbinu kama hizo zimetumika katika miradi mingine ya ujenzi aliyoisimamia kando na ushirikiano huu na familia ya Zongo. Amefanya vivyo hivyo katika majengo ya kifahari, majumba ya makumbusho na kumbi mbalimbali, kutaja machache tu.”

“Unadanganya. Sijafanya jambo kama hilo!” James alifoka huku akitikisa kichwa kwa nguvu. Hakuweza kujua ni namna gani Alvin aliweza kufahamu kila kitu.

Alvin akaendelea. "Baadhi ya wamiliki walitoa maoni hasi baada ya ukarabati, wakitaja matukio ya uvujaji wa maji, matatizo ya umeme na kesi zingine kama hizo. Waheshimiwa, hizi ni rekodi za video za wamiliki wenyewe.” Alvin aliwasilisha kumbukumbu nyingine kwa hakimu.

"Zaidi ya hayo, kuna ushahidi pia wa yeye kutelekeza miradi ya ujenzi aliyoshiriki kabla ya hii. Matukio machache yalikuwa yametokea wakati vigae vilianguka kutoka kwenye mapaa na kuwajeruhi watu kwenye eneo la tukio. Hata hivyo, kwa sababu ya kukingiwa kifua kwake wahusika waliojeruhiwa walinyamazishwa kwa kiasi kidogo cha fedha.”

Wakati skrini ya TV ilipoonyesha video za malalamiko zilizorekodiwa na wamiliki, James karibu aanguke chini. Watu hawa wote walikuwa wameshirikiana naye hapo awali. Alikuwa amefunika kwa uangalifu ajali hizo baada ya hapo, akifikiri kwamba angeweza kuficha zile kashfa kabatini milele. James aliingiwa na woga na kukata tamaa kabisa. Hakuwahi kuhisi majuto haya maishani mwake.

Akageuka na kumwangalia Lisa kana kwamba ndiye tegemeo lake la mwisho la maisha. "Tafadhali naomba unisamehe. Nilifanya makosa. Sikupaswa kukukwaza. Mimi ni binamu yako na sisi ni kama kaka na dada. Sisi ni familia,” James aliomba badala ya kupiga kelele kwa jeuri kama hapo awali.

Lisa alihisi kuchukizwa hata kumtazama. "Je, uliniona kama binamu yako wakati unanifanyia haya? Mbali na hilo, umfanyialo mwenzako ndilo litalokurudia. Ni wakati wa kupata malipo unayostahili kwa makosa yako yote ya hapo awali."

Kisha, Lisa akamgeukia Clark Zongo. “Bw. Zongo, ninawajibika kwa kile kilichotokea kwenye hoteli. Sikupaswa kuiamini Kibo Group na sikupaswa kukufanya usaini nao mkataba. Kwa kweli, sababu ya mimi kufukuzwa kutoka kwenye mradi huo ni kwamba niligundua James alikuwa akipata faida isiyo halali kutokana na mradi huo. Nilipeleka malalamiko hata kwa mkurugenzi wa Kibo Group lakini alifumbia macho na kuziba masikio yake hata akaamua kunifukuza.” Lisa alimtupia jicho la kejeli Masawe, ambaye sasa alikuwa amepauka kama msukule.

Kwa hasira, Clark Zongo alipiga meza na kuinuka kwa hasira. “Jones Masawe, unathubutuje kunidanganya?! Hili halitaishia hapa.”

Mzee Masawe alikuwa karibu kufa kwa presha kutokana na hasira. Hakutarajia kuwaudhi hata familia ya Zongo mwishowe. Lakini, kipaumbele hivi sasa kilikuwa ni kujiepusha na tuhuma hiyo.

“Bw. Zongo, naapa kwamba kwa kweli sikujua kilichokuwa kikiendelea. Lisa na James siku zote walikuwa hawana maelewano kati yao. Nilidhani alikuwa akizusha tu makosa kutoka kwa migogoro ya kibinafsi.” Akamtazama James kwa chuki. “Hiyo ni sawa?”

"Ndio, nilifanya haya yote kwa kumzunguka mjomba wangu." James akauma meno na kuinamisha kichwa chini. Familia ya Masawe ingeweza tu kumtoa kwenye tuhuma hiyo ikiwa wangebaki na nguvu na bila kuyumbayumba.

Alvin alirudisha macho yake na kumgeukia hakimu. "Huu sio mwisho wa uhalifu wa James Komba. Si muda mrefu uliopita, Lisa Masawe alikamatwa na polisi na kutupwa jela kwa sababu ya mashtaka yake. Katika kipindi hiki, James alikodi wafungwa waliokuwa katika gereza moja ili kumuua. Huu ndio ushahidi.”

James alimtazama Alvin na kushindwa kuacha kutetemeka. Ilikuwa kana kwamba alikuwa akimtazama shetani mwenyewe! Alijua kwamba huo ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake!

Kisha, Alvin akasema, “Mheshimiwa, mshtakiwa anahitimisha utetezi wake.”

Mwishowe, hakimu kiongozi alimhukumu James kifungo cha maisha kwa makosa ya kukusudia yaliyogharimu maisha ya watu wengi.

Sura ya 82

Baada ya kesi kuisha, James alianguka ghafla na kuketi chini akiwa dhaifu kama mtu asiye na uhai. Maafisa wa polisi waliingia kumtoa nje ya chumba cha mahakama. Lina na wazazi wake walichukua fursa hiyo kutoka nje ya chumba cha mahakama kabla ya mtu yeyote kuona.

Pamela alikimbia mbele kwa furaha kumkumbatia Lisa . “Hii ni habari njema! Na Bw. Kimaro, wewe ni mzuri! Nilidhani unaweza kupata kifungo cha miaka 20 kwa ajili ya James lakini akapata kifungo cha maisha ambacho hakiwezi kubadilishwa. Hiyo ni ajabu. Wewe ni malaika wangu kabisa.”

“Nakubali. Wewe ni mzuri sana." Lisa aliitikia kwa kichwa.

Kesi hiyo iliisha haraka kuliko alivyotarajia lakini matokeo yake hakika yalikuwa ya kuridhisha. Mbali na hilo, Alvin alikuwa amelenga kumshambulia James kwa muda wote. Ingawa familia ya Masawe ilifanikiwa kutoroka wakati huo, aliamini kuwa hii iliashiria mwisho wa kampuni ya Kibo Group. Hakuna mtu ambaye angethubutu kushirikiana nao tena.

“Umefurahi?” Alvin aliinua macho yake nzuri na kumkazia Lisa. Watu walimsifu kila mara baada ya kushinda kesi lakini kwa sababu fulani alitaka kusikia maoni yake juu yake.

Lisa aliinua macho yake na kukutana na macho ya Alvin. Macho ya Alvin yaliufanya moyo wa Lisa udunde bila mpangilio.

Wakati huo huo, Kelvin aliwasogelea kwa adabu. Nyuma yake alikuwapo Ethan.

"Lisa, pongezi." Baada ya kumtazama kwa upole kwa sekunde kadhaa, akamgeukia Alvin. "Bwana. Kimaro, ninashukuru sana kwa kumpigania Lisa .”

Uso wa Alvin ukabadilika ghafla, Macho yake yenye hasira yalitangaza hali ya hatari. Mwanamume mwingine alikuwa akimshukuru kwa kumsaidia mke wake? Alvin alihisi kupoteza utulivu wote. Pamela na Lisa walihisi kwamba kuna jambo baya lilikuwa karibu kutokea.

Hata hivyo, Ethan alikuwa na wasiwasi kwamba Kelvin angeweza kupata kibali cha Lisa. Hapo hapo, akasogea mbele kuikamata mikono ya Alvin. "Bw Kimaro, asante sana kwa siku ya leo. Ningependa kutoa shukrani zangu kwa niaba ya Lisa. Je, una muda baadaye kwa ajili ya chakula labda?"

"Hahaha…haaa.." Kicheko kilisikika kutoka ndani ya koo la Alvin. Macho yake yalidhihirisha hali ya kiburi.

Lisa alihisi kutetemeka baada ya kusikia hivyo. Haraka akasonga mbele kuisukuma mikono ya Ethan. “Unapaswa kuzingatia heshima yako. Sina uhusiano wowote na wewe tena.”

“Lisa, najua bado una hasira lakini ni sawa. Naweza kusubiri hadi siku utakaponisamehe.” Ethan alisema kwa majuto. “Kesi ya leo ilinionyesha jinsi nilivyokuwa mjinga zamani. Sikufikiri kwamba James alikuwa mtu wa namna hiyo. Alikuwa anakusema vibaya sana mbele yangu!”

“Hakuna haja ya kulilia maziwa yaliyomwagika. Hakuna mtu atakungojea milele. Baadhi ya fursa hazitajirudia mara mbili. Lisa amechoka sana siku za hivi karibuni, hivyo hupaswi kuendelea kumkumbusha mambo ya zamani yasiyofurahisha,” Kelvin alimkatisha Ethan kabla ya kugeuka na kumwangalia Lisa kwa macho ya matarajio. "Je, tusherehekee pamoja usiku wa leo? Jiunge nasi, Mheshimiwa Kimaro. Kwa kweli, nina maswali mengi ya kisheria ambayo ningependa kupata ushauri wako.”

Alvin akarekebisha tai yake shingoni. Wanaume hawa wote waliomtongoza Lisa walikuwa wakijaribu kumwonyeshea mbele yake.

Hakuna aliyemfahamu Alvin zaidi ya Lisa. Alijua bila shaka kwamba huo ulikuwa utulivu kabla ya dhoruba, kwa hiyo alipunga mikono yake haraka bila kutarajia. “Hapana… ni sawa. Ninashukuru kwa wema wako lakini mimi na Bw. Kimaro tutakuwa na mapumziko ya faragha usiku wa leo.”

Pamela aliruka haraka ili kumuokoa rafiki yake. "Bw. Kimaro amemsaidia sana leo, kwa hivyo anahitaji kumhudumia kwa chakula na mambo mengine.”

“Ndio, natakiwa kumhudumia mume wangu. Tutaonana Mungu akipenda.” Lisa alisema huku akimkokota Alvin kuelekea mlangoni. Vinginevyo, alikuwa na wasiwasi kwamba angerudi mahakamani tena kama shahidi namba moja wa kesi ya mauaji.

Kelvin na Ethan walikunja nyuso kwa mshangao baada ya kumuona Lisa akimkokota Alvin kutoka kwao. Hasa Kelvin ambaye tayari alikuwa na mabadilishano machache na Alvin. Kwa kadiri alivyojua, Alvin alikuwa na kiburi na mkorofi, lakini Lisa aliweza kumvuta kwa mkono? Ghafla akakumbuka jinsi wawili hao walivyotoweka kwenye mgahawa juzi juzi. Ilimjia wakati huo kwamba lazima wawe na uhusiano usio wa kawaida.

Ethan pia alichukizwa na tukio hilo. Alimhoji Pamela ambaye bado alikuwa pale mahakamani. "Inaonekana kama Lisa ni rafiki kabisa na Bw. Kimaro. Inawezekana kwamba anampenda?” Kabla swali hilo halijajibiwa akamtwanga jingine. “Sawa, ulisema kwamba kuna rafiki yako anamjua Bw. Kimaro. Ulikuwa ukimmanisha Lisa? Kama tena haitoshi akamwongeza jingine. "Nilisikia kwamba ni changamoto kubwa kumuajiri Bw. Kimaro kama wakili. Lisa alipata wapi ushawishi, achilia mbali pesa za kumuajiri wakili Kimaro?"

Pamela alikerwa na kuulizwa mlolongo wa maswali mengi hivyo. "Haikuhusu. Ondoka kwangu, mchafu wewe."

“Wewe…” Uso wa Ethan ulikunjamana.

“Kama si kwa sababu ulikuwa umejaribu kila uwezalo kujaribu kumwokoa Lisa kutoka gerezani mara ya mwisho, ningekuwa tayari nimetupa mkoba huu usoni mwako.” Pamela alitoa mkoromo wa dharau kabla ya kuondoka.

Ndani ya gari, Hans alikuwa nyuma ya usukani. Watu wawili walikuwa wamekaa kimya kwenye siti za nyuma. Alvin alikuwa busy na simu yake, lakini, hasira yake kali iliyojionyesha kwenye mtazamo wa sura yake ilipunguza utulivu ndani ya gari kwa digrii kadhaa.

Lisa alikuwa akigeuka mara kwa mara na kumwangalia. Alijua hakufurahishwa na maneno ya Kelvin alikuwa na uhakika ilikuwa kwa sababu ya wivu. Labda alishuku kwamba alimhisia vibaya tena. Kwani kila mara mwanamume mwingine alipompa usafiri wa kumpeleka nyumbani, kwa mawazo yake alifikiri kwamba alikuwa akimtongoza. Alielewa mawazo haya. Wanaume kwa ujumla huwa na tabia ya ubinafsi wanapomiliki mwanamke.

Mwanamume anataka mwanamke wake awe wa kwake tu, hata kama hakumpenda kiasi hicho. Sauti ya wasiwasi ikatoka kwenye midomo yake, na kwa uangalifu akavuta kona ya mkono wake. “Sikuwa na wazo kwamba wangejitokeza. Hakuna kinachoendelea kati yangu na wao.”

“Hakuna kitu?” Alimdhihaki na kumtupia jicho la kejeli. “Hivi kwa nini wanaendelea kukufuatafuata kila wanapokuona? Mmoja ni mchumba wako wa zamani wakati mwingine ni mpenzi wako. Wawili hao wakawa wanakuja kunishukuru katika hali hiyo. Kwanini wasimfuate hata Pamela, Lisa, wewe ni mrembo kuliko wanawake wote, sivyo? Maneno yake yalimfanya Lisa atetemeke na ghafla asijue la kusema.

"Nijibu." Alvin alikasirika zaidi alipokabiliwa na ukimya wake.

Kwa sauti ya kutetemeka, Lisa alijibu, “Lakini si kosa langu kama mtu atavutiwa na mimi! Kwani mimi niliwafuata na kuwaambia wanifuate?”

Hans, ambaye alikuwa akiendesha gari kwenye kiti cha mbele, alisali kimya-kimya kwa ajili ya Lisa. Kama ilivyotarajiwa hasira kali liliangaza usoni mwa Alvin. Alimtazama Lisa kwa jicho kali huku akivuta tai yake shingoni. Lisa aliogopa sana. Alvin alimkaba shingo huku akihema kwa hasira.

"Unafanya nini? Unajaribu kuniniga. Nitaruka nje ya gari sasa hivi.”

Kwa mshtuko, Alvin aliitazama ile tai iliyokuwa mkononi mwake na kutabasamu baada ya kujua ni nini kilikuwa akilini mwake.

"Ruka nje ya gari ukitaka." Alvin alinyoosha tai yake shingoni kwa makusudi huku akimuelekeza Hans, “Hans ongeza mwendo. Ikiwa ataruka nje sasa hivi afe hapohapo.” Lisa alibaki kimya akiwa kajikunyata kwenye kona ya gari.

"Sogea hapa." Alvin alimpa ishara ya kumsogelea.

“Maadamu hutanikaba.”Lisa alisema kwa wasiwasi.

“Nimesema nataka kukukaba? Wewe ndiye unayefikiria mawazo haya machafu.” Kwa papara alimshika karibu na kumweka kwenye mapaja yake.

Sura ya 83

Kulikuwa na mtu mwingine ndani ya gari, hivyo Lisa asingependa kufanya kile alichohisi Alvin alitaka kufanya. Ili kupotezea, alianzisha mada nyingine. “Ungependa kula nini usiku wa leo? Nitafanya chochote utakachoomba kukushukuru kwa msaada wako leo."

“Siku zote ni chakula na wewe.” Akamtupia jicho la dhihaka kabla ya kucheka kwa kejeli. "Unajua nini kingine zaidi ya kunipikia?"

Lisa alikosa la kujibu. Alijua mada ya chakula ingemwamisha Alvin haraka kwenye yale mawazo lakini ilionekana tofauti.

“Kwa nini Kelvin na Ethan walikuwa hapa leo?” Alvin alimrudisha kulekule.

"Sijui." Lisa alijibu kifupi tu huku akimwangalia kwa macho yake ya mviringo.

"Naona umeshaanza kupuuza mashariti ya mkataba wetu tayari," alionya. “Inaonekana hukubaliani nami si ndiyo?”

"Bila shaka nakubaliana na wewe." Lisa alijaribu mara moja kumvimbisha kichwa Alvin. “Kelvin na Ethan hawako kwenye kiwango chako. Jinsi ulivyoshinda kesi ya leo mahakamani imemshangaza kila mtu. Umemchimbua James nje ndani kuliko nilivyoweza kutegemea. Wewe ni shujaa wangu kabisa!”

Alvin alitabasamu huku akionyesha dole gumba na kuonekana kana kwamba alikuwa amevutiwa kabisa na maneno yake. Licha ya hayo, Lisa alikuwa akisema ukweli. Hapo awali, alifikiri ingekuwa changamoto kushinda kesi hii. Haikuwa kazi rahisi kumshinda mtu msaliti kama James. Lakini, ilionekana kuwa Alvin aliishughulikia kwa urahisi.

Alvin kwa uvivu aliweka mkono mmoja kwenye sehemu ya kichwa huku akichezea nywele ndefu za rangi nyeusi za Lisa kwa mkono wake mwingine. “Unajua ni nguvu kiasi gani niliyowekeza katika kesi hii? Kila taarifa na ushahidi haikupatikana kwa urahisi.”

"Najua, na ninashukuru sana." Lisa alisikitika zaidi aliposikia hivyo.

Ghafla, Alvin alishika paji la uso wake, akionekana kuishiwa nguvu na kusema kwa uvivu. "Nimechoka."

"Ngoja nikufanyie masaji." Haraka Lisa akaketi wima na kuanza kusugua taratibu kichwa chake. Alvin alifunga macho yake na kufurahia kimya kimya wakati akifanyiwa masaji hiyo.

Hans, ambaye alikuwa ameketi mbele, alitingisha tu kichwa chake na kutabasamu kwa unyonge. Alishtushwa na hali ya Alvin ambaye alionekana ghafla kukosa aibu. Hans ndiye alifanya kazi kubwa kwenye kesi ya Lisa lakini ujiko wote akajimiminia Alvin peke yake. Alichokifanya Alvin ni kutoa maagizo tu. Hans ndiye aliyekimbia huku na huko bila kuchoka kutafuta taarifa.

Gari lilisimama taratibu mbele ya jumba la kifahari la Alvin. Mikono ya Lisa ilikuwa inamuuma kidogo kutokana na masaji hayo marefu. Alvin alifumbua macho taratibu na kutoka nje ya gari. “Naenda kuogelea. Unapaswa kuanza kuandaa chakula cha jioni, na utengeneze chakula kizuri zaidi kuliko kawaida. Kesi yako imenipa tabu sana."

Lisa alitikisa kichwa. Angefanya hivyo hata bila kuambiwa. Ili kutoa shukrani zake, alijishughulisha jikoni kuandaa vyakula vyote avipendavyo Alvin.

Kwa wakati huo, alikuwa akipika huku akiangalia mitandao yake ya kijamii. Naam, wafuatiliaji wa mtandaoni walikuwa wakikosoa kampuni ya Kibo Group. Ingawa Masawe alikwepa hukumu ya mahakama wakati huo, watu hawakuamini kuwa bosi huyo mkuu wa kampuni hakuwa na hatia. Kulikuwa na maoni pia mtandaoni ya kuisusia kampuni ya Kibo. Kibo Group ilianza kushuka rasmi!

Wale ambao awali hawakumwelewa kwa kupokea rushwa wote walibadili mawazo na kuanza kumuonea huruma baada ya kujua kuwa amerubuniwa. Alikuwa na wafuasi milioni nane lakini sasa idadi ilikuwa imeongezeka na kufikia zaidi ya milioni kumi. Alikuwa maarufu zaidi kuliko baadhi ya wasanii mashuhuri.

Baada ya chakula cha jioni kuwa tayari, Shangazi Linda hakuweza kujizuia kustaajabia mlo huo wenye sura ya kupendeza. “Sikujua wewe ni mpishi mzuri kiasi hicho. Si ajabu Bw. Kimaro hayuko tayari kula kile ninachoandaa mimi.”

Hili lilikuwa jambo la kushangaza kwa Lisa. Alijua Alvin alikuwa tu anasitasita kukiri lakini bila shaka alikuwa ameshazoea upishi wake. “Anti Linda, naweza kukuonyesha jinsi ya kuzitengeneza wakati mwingine. Kwa njia hii unaweza kumpikia Bw. Kimaro hata nisipokuwepo.”

“Kweli, lakini kwanini usiwepo? Ninyi wawili mmefunga ndoa sasa, na mnapaswa kukaa pamoja maisha yenu yote.” Shangazi Linda alitabasamu huku akipanga vyombo mezani. Ni wazi kwamba hakuwa amefikiria mara mbili kuhusu maneno hayo. Lisa alikosa la kusema. Alihitaji kujitahidi zaidi kupata pesa sasa kesi ilipofungwa. Hakuweza kujiruhusu kuwa mfungwa wa Alvin milele.

Aunty Linda alikuwa na shughuli nyingi wakati huo, hivyo Lisa alipanda juu ili kuchukua seti ya nguo za kupumzikia za Alvin kabla ya kuelekea kwenye bwawa la kuogelea.

Lisa aliyekuwa amesimama kando ya bwawa alionekana kupigwa na butwaa na ustadi wa Alvin katika kuogelea. Ustadi wake wa kuogelea ulikuwa mzuri kama waogeleaji wa kitaalamu. Alvin alitoka majini kama mzamiaji. Nywele zake fupi nyeusi zilitiririsha maji kwenye ukingo wa paji la uso wake. Matone ya maji yalitiririka kwenye nywele zake, usoni mwake, juu ya daraja lake refu la pua, mdomoni, shingoni, kifuani, tumboni…

Kwa aibu, Lisa akamtazama na kumwambia. “Chakula cha jioni kiko tayari. Nimekuletea seti ya nguo zakubadilisha.” Aliziweka pembeni na kugeuka kuondoka.

Alvin aliweka viganja vyote viwili kwenye ukingo wa bwawa na kujiinua kutoka kwenye maji kwa namna ya haraka. Alikuwa amevaa bukta tu ya kuogelea na si kitu kingine. Mapaja yake yalikuwa yameshikana na kitambaa cha bukta, na matone ya maji yalisisitiza kila mstari na ukingo kwenye ngozi ya mwili wake mzuri. Alionekana safi kama sanamu ya Daudi.

“Nikaushe,” Alvin aliamuru huku akijifuta maji usoni kwa kisogo cha mkono wake.

Lisa alishikwa na butwaa. “Um… Si wazo zuri. Unapaswa kufanya mwenyewe."

"Nimechoka." Sura ya uchovu iliuva uso wake.”kesi yako ilikuwa ngumu, imenichosha sana.”

Lisa hakuwa na la kusema. ‘Una uhakika? Bado ulikuwa na nguvu sekunde moja iliyopita ndani ya maji.' Lisa alinong’ona mwenyewe.

"Harakisha. Ninasikia njaa,” Alvin alihimiza. "Kuna nini? Nimekushindia kesi mahakamani lakini huwezi hata kunifanyia jambo hili dogo? Fanya hivyo sasa hivi.”

Lisa alisogea mbele na kutandaza taulo. Alijaribu kukausha nywele zake kwanza lakini Alvin alikuwa mrefu zaidi yake, hivyo ilimbidi asimame kwa vidole vyake. Hakuona kwamba sehemu ya juu ya mwili wake ilikuwa karibu kuangukia kifuani mwake.

Harufu ya kupendeza ya Alvin ilijaza hewa karibu naye. Hakuzingatia sana hilo. Badala yake, aliendelea kukausha sehemu ya mbele ya mwili wake na kuzunguka nyuma ya kichwa chake. Wakati Lisa alipozunguka mbele tena na macho yao kukutana, uso wake ukawa na aibu kutokana na kumtazama na akainamisha macho yake harakaharaka.

Alvin akamshika Lisa kiunoni ghafla. "Umemaliza?"

Lisa alichanganyikiwa kidogo na hakuweza kujibu. Aliweza tu kutikisa kichwa bila fahamu. Mara baada ya hapo, Alvin alimyanyua juujuu.

"Unafanya nini?" Lisa hakupenda lakini hakuwa na namna. Alimkumbatia shingoni kwa woga.

"Lisa Masawe, ninakubali kwamba ujuzi wako wa kunishawishi unazidi kuwa bora na bora." Sauti ya Alvin ilisikika akiwa amembeba hadi chumbani juu.

Mwanamke huyo alikuwa akipandwa kichaa. 'Nimekushawishi na nini? Wewe ndio umenibeba juujuu. Nashangaa imekuaje wakati zamani ulikuwa ukisema mimi sikufai!”

Lisa alipotupwa kitandani, alitetemeka.

Sura ya 84

Ingawa tayari alitarajia siku hilo lingetokea siku yoyote baada ya kusaini mkataba siku hiyo, bado alikuwa na hofu kubwa. Baada ya yote, yale mabusu ya awali yalikuwa yameacha kiwewe kikubwa juu yake. Alvin alibana ncha ya pua yake ndogo, akimtania.

“Subiri.” Lisa alikisukuma kifua chake kwa ghafla na kuonyesha hali ya maumivu. “Alvin, hatuwezi kufanya hivi. sikustahili wewe.”

"Kwanini?" Alvin alitulia na kuuliza kwa shauku.

“Ni kwa sababu namekufahamu vizuri kwa sasa. Hadhi yangu haifikii ile ya kwako. Wewe ni mwanasheria mkubwa na mashuhuri wakati mimi ni mbunifu mdogo tu. Kuna ulimwengu mzima wa tofauti kati yetu. Kulala na wewe ni sawa na kukushusha kutoka kwenye fahari yako. Hiyo ni kufuru. Ni tusi.” Lisa alijitetea.

"Kwanini uliniwekea mpaka dawa kwenye chakula ili tu nilale na wewe kama unafikiri hivyo?" Alvin aliinua uso wake.

'Hiyo ni kwa sababu tu nilifikiri wewe ni mjomba wa Ethan.' Lisa alitaka kusema hivyo lakini hakuthubutu, akaishia kusema kwa unyonge tu, “Ni kwa sababu sikuwa najua lolote wakati huo. Nilifikiri kwamba kuushinda mwili wako kungenipatia moyo wako, lakini nikagundua kwamba nilikosea.”

"Ulikosea?" Alvin alikipapasa kidevu chake tena na tena huku akiachia tabasamu zito. “Usijali, nilichukia tu kwa sababu ulitumia njama kutaka kulala na mimi, lakini hayo yamepita, sasa nimekupa nafasi kwa moyo wangu mweupe.”

Macho ya Lisa yalimtoka. Kila kitundu kwenye mwili wake kilionekana kuvuja jasho. Alipoona midomo ya Alvin inazidi kusogea, aliishiwa nguvu. Alipokaribia kufumba macho Alvin alisimama ghafla. “Wewe nisubiri hapa. Naenda kuoga."

Alvin alikumbuka kuwa alikuwa ametoka tu kwenye bwawa la kuogelea na hakuwa msafi. Ingekuwa shida ikiwa mwili wake ungeambukizwa na vijidudu. Alisimama na kuelekea bafuni kwa umaridadi, huku Lisa akiwa amejilaza kitandani akipingana na hisia zake zinazokinzana kwa muda mrefu. Ingawa tayari alikuwa amejiambia mara kuwa jasiri, hatimaye wakati wa kutokea kwake ulipofika, ghafla aliogopa. Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, bado aligeuza mkia na kukimbia.

Alvin alipotoka kuoga, chumba cha kulala kilikuwa tupu na hakuna mtu aliyebaki kitandani.

Shangazi Linda aliuliza kwa mshangao, “Ni karibu wakati wa chakula cha usiku. Kwa nini bibi alikimbia?"

Hapo ndipo Alvin alipogundua kuwa mapambano ya Lisa mapema ni kwa sababu hakuwa tayari. Hapo mwanzo alidhani amempa fursa ya kumlidhisha tamaa yake ya muda mrefu, lakini alikataa!

Alvin alikasirika sana mara moja akampigia simu. “Lisa Masawe, rudisha mat*ko yako hapa sasa hivi! Unahitaji nikukumbushe yaliyomo kwenye mkataba? Unafikiri ninaendesha shirika la hisani na nitafanya kazi bila malipo kwa sababu tu unaogopa kunikaribia? Au unafikiri ujuzi wako wa kupika una thamani ya shilingi milioni mia kadhaa? Alivin aliwaka kwa hasira. “Mbali na hilo, si mara yako ya kwanza. Mbona bado unajifanya unaogopa mbele yangu?”

Kila alichokisema Alvin kilikuwa kama kiboko moyoni mwa Lisa huku akisikiliza upande wa pili wa simu. “Umejuaje kuwa si mara yangu ya kwanza?”

“Ethan na wewe mlianza mahusiano mkiwa shule ya sekondari. Inawezaje kuwa mara yako ya kwanza?" Alvin hakuamini hata kidogo kwamba vijana wa siku hizi wanaweza kudumisha uhusiano safi.

"Sijawahi kufanya naye hata kidogo." Lisa alijisikia vibaya sana. 'Bado nina usichana wangu. Kuniamini au kutoniamini ni juu yako.”

Alvin alipigwa na butwaa, moyo wake ukiwa umechanganyikiwa kidogo. “Nitakupa dakika kumi. Rudi hapa sasa au jiandae kwa madhara.”

Upande wa pili wa simu, Lisa alisimama kando ya bwawa la kuogelea kwa muda kabla ya kurudi ndani ya jumba hilo. Baada ya yote, alikuwa na deni kwake. Hakutaka kuwa mtu asiye na shukrani. Alvin alikuwa kasimama mlangoni akimsubiri.

“Samahani, sikukusudia. Niliogopa tu…” Lisa kwa utii alienda upande wake na kuomba msamaha. “Kama bado unataka, nitafuatana na wewe kurudi chumbani.”

Alvin akauma mdomo kwa hasira. “Mbona sikukuona unaogopa ulipokuwa ukinitega hapo awali?”

"Wakati huo ... Huenda ikawa kwa sababu upendo hutokea bila kujua, kwa hivyo nilikufuata bila habari!" Lisa alidanganya, akitaka kulia lakini hakuweza kutoa machozi. "Baada ya kukataliwa, nilianza kukuogopa."

Alvin akaguna, “Sawa. Sitakugusa kwa sasa. Ingia ndani ule.” Akageuka na kurudi sebuleni huku akiwa na uso mpole. Lisa alipigwa na butwaa, huku akiwa haamini kwamba alimruhusu aende vile vile.
•••
Katika ofisi ya Kampuni ya ujenzi ya Kibo Group, mwenyekiti, Jones Masawe, alikuwa akisikiliza ripoti ya meneja mkuu.

“Tayari kuna wabunifu watano wakuu na ujenzi wa daraja la kwanza ambao wamewasilisha barua zao za kuacha kazi mara moja. Kampuni tanzu na kampuni mama wanataka kuondoa miradi yote ambayo waliagiza. Kwa sasa, mtandao mzima unasusia Kibo Group. Kila mtu anasema kwamba Kibo Group inakula rushwa na hakuna aliye tayari kushirikiana nasi tena. Thamani yetu kwenye soko la hisa imeshuka leo na ninatarajia itaendelea kushuka."

Hatimaye, meneja mkuu alimpa mwenyekiti Masawe barua ya kuacha kazi. "Bw. Masawe, nataka pia kuacha kazi.”

Macho ya Jones Masawe yalimtoka huku hali ya moyo wake ikikaribia kuwa mbaya. “Paka usiye na shukrani! Kibo Group bado haijaisha!

Meneja mkuu alisema, “Kampuni inajengwa na sifa nzuri. Sifa ya Kibo Group haikuwa nzuri kwa miezi miwili iliyopita. Nikiweza kuwa mkweli, haya yote yalitokea kwa sababu ya mambo ya familia yako. Nakushauri uiuze Kibo Group. Hivi sasa, kampuni hii itaweza tu kuishi kwa kubadilisha umiliki.” Meneja mkuu aliondoka baada ya kumwachia ushauri.

Masawe alikasirika sana hadi akavunja kila kitu ofisini kabla ya kurudi nyumbani kwake. Alipoingia tu ndani ya nyumba, alimpiga Mama Masawe kofi zito. “Ni kosa lako kwa kumdekeza na kumlinda James wakati wote. Sasa, Kibo Group imeharibika!”

Mama Masawe alipigwa na butwaa, lakini pia alichukua mto na kumpiga mumewe usoni kwa dharau. “Kosa langu? Sijawahi kukuona ukikataa kila James alipokupa faida. Ukiniuliza, yote ni makosa yako. Ikiwa asingekuwa Lisa, familia yetu ingekuwa sawa. Hatungeishia hivi!” Mama Masawe alitokwa na machozi.

“Baba, mama, acheni kupigana!” Lina alikimbia kuwaamua wazazi wake. “Baba, umesahau? Sasa si wakati wa kukata tamaa. Bado tuna Mawenzi Investments mikononi mwetu. Ni mojawapo ya makampuni 100 ya juu nchini. Ni kubwa zaidi kuliko Kibo Group!”

"Lakini hiyo ni ... ya...." Masawe alisitasiita.

"Baba, ikiwa utachanga vyema karata zako, inaweza kuwa mikononi mwako!" Lina alisema kwa sauti ya chini.

“Lina yuko sahihi,” Mama Masawe alisema kwa ukali, “ Mara tu Kibo Group itakapoanguka rasmi, familia yetu haitakuwa na mahali pa kusimama tena hapa Dar es Salaam!”

Masawe alijitahidi kufikiri kwa muda kabla ya macho yake kuangaza kwa makini “Uko sahihi!”

Sura ya 85

Ndani ya jumba la kifahari la Alvin, Lisa alikuwa na ndoto. Katika ndoto, alionekana kuwa amerudi Moshi. Alipokuwa mtoto, babu na bibi yake walikuwepo na walimpenda sana, hivyo mara nyingi alikaa Moshi.Hata hivyo, baada ya babu yake kufariki, bibi yake alisema, “Lisa, Bibi amechoka na anataka kwenda kuandamana na babu yako.”

“Usi…” Alilia na kuketi kwa nguvu, akihema kwa hofu.

“Ni nini?” Sauti nzito na kali ya Alvin ilisikika masikioni mwake kabla ya kumbusu.

“Niliota kwamba bibi yangu amekufa." Lisa alikwepa busu lake na kunung'unika.

Alvin akanyamaza na kuona bado macho yake yamelowa. Alinyoosha mkono kumsugua kichwa na kumkandamiza uso wake kifuani. “Ni ndoto tu, usihuzunike."

“Hmm.” Ilikuwa ni mara ya kwanza kuwa karibu sana kwa kila mmoja wao. Ilikuwa ni kana kwamba walikuwa wanandoa wanaopendana muda mrefu sana. Lisa alimsukuma mbali na kumkwepa kijanja. “Kumekucha. Nitaenda kuandaa kifungua kinywa."

Walikuwa wamekula chakula cha jioni jana yake usiku, lakini Lisa alipotaja tu chakula, Alvin alihisi njaa sana. Baada ya kula kifungua kinywa, Lisa alikuwa tayari kwenda kazini.

Alvin alikumbusha ghafla, "Hauruhusiwi kusimamia mradi wa jumba la kifahari la Kelvin, sitaki ukutane naye tena."

Lisa alikunja uso. "Je, unaweza kuzuia mashariti yako kwenye kazi yangu?"

"Lisa Masawe wewe sasa ni mwanamke wangu. Biashara yako yote ni biashara yangu." Alvin akasimama, mwili wake mrefu ukimuunga mkono kwenye ukingo wa meza ya chakula. “Nilichokuonya jana hakikuwa mzaha.”

"Ninaweza kukubaliana nawe katika maisha ya kibinafsi, lakini sio kazini." Lisa alimkataa.

"Vipi, hunisikii tena baada ya kushinda kesi?" Hali ya furaha ikapotea machoni mwa Alvin.

Lisa alikosa la kusema na kukasirika kidogo, lakini alijua haina maana kubishana na mtu kama Alvin. Akashusha pumzi ndefu, akainamisha uso wake na kuvuta mkono wake. “Huwezi kuniamini zaidi? Mwanaume pekee niliye naye ni wewe, na mtu ninayempenda pia ni wewe. Uliniokoa mara nyingi kana kwamba wewe ni malaika anayeshuka kutoka mbinguni kwa ajili yangu. Ningewezaje kuwa na mtu mwingine moyoni mwangu?" Baada ya kusema hivyo, alimpigapiga mgongoniili kumfariji. Alikuwa ameingia katika taaluma isiyo sahihi. Alipaswa kuwa mwigizaji.

"Unanipenda?" Alvin aliinua kidevu chake na kumtazama.

"Ndio ... nakupenda." Midomo ya Lisa ilitetemeka. Aliogopa kwamba atajidhihirisha.

Moyo wa Alvin ulionekana kulipuka kama fataki kwa maneno hayo, lakini uso wake ulibaki na kiburi.

Maongezi yao magumu yakaishia hivyo hivyo, Lisa akahema kwa furaha. Ilionekana kwamba bado alipaswa kujifanya kuwa katika upendo sana katika siku zijazo.

Saa tatu kamili asubuhi, baada ya kufika ofisini, moja kwa moja Lisa alikwenda kumtafuta mkurugenzi, Joseph Ruta. Alipata safari ya ghafla tangu alipokamatwa na polisi hapo awali na hakuwa amefika kwenye kampuni hiyo tangu wakati huo.

Kwanza, aliogopa kuwa maneno ya wenzake yangefanya mambo kuwa magumu kwa Joseph, na hakutaka sifa ya Ruta Buildind Design & Construction iharibiwe tena.
Ingawa kesi yake ilikwisha, bado alihisi hatia kumwelekea Joseph, bosi wake.

“Joseph samahani sana. Ndiyo kwanza nimeanza kazi kwenye kampuni yako na bado ninakuletea matatizo wewe na kampuni.” Lisa alisikitika sana.

"Ni sawa, nimekuwa nikiamini sana kwa tabia yako." Joseph alitabasamu na kummiminia kikombe cha kahawa. "Mbali na hilo, tunaweza kufikiria hii kuwa baraka iliyojificha. Hatimaye nilipoingia Dar es Salaam, Kibo Group daima amekuwa mshindani wangu mkubwa, lakini sasa, Masawe anapanga kuuza Kibo Group.

Lisa aliganda kwa sekunde kadhaa. Ingawa alijua kuwa Kibo Group ilikuwa imekumbana na kikwazo kikubwa wakati huo, kwa haiba ya Masawe, hakuwa mtu ambaye angekata tamaa kirahisi hivyo. Ikiwa angeuza Kibo Group, familia ya Masawe ingepoteza msimamo wao ndani ya jiji la Dar. Je, wangeweza kukubali hilo?

“Hutakiwi kushangaa sana. Kashfa ya James Komba ilikuwa kubwa sana na Kibo Group ina sifa mbaya sana sasa. Hakuna atakayethubutu kushirikiana nao kwa miaka miwili ijayo angalau. Wengi wa wafanyikazi wa usimamizi wa juu na wabunifu pia wameondoka. Jones Masawe hataweza kufikia lolote bila usaidizi.” Joseph alimweleza. “Hakuna atakayekuwa mjinga kiasi cha kuingiza mtaji ndani ya Kibo Group. Labda itaweza kuinuka tena mara tu upepo utakapopungua, lakini kama hawataiuza kwa sasa hasara kubwa inaweza kuishia kufilisi familia ya Masawe.”

Lisa alielewa. Masawe alitaka kuuza Kibo Group kwa wakati huu ili apate faida na pia kukomesha hasara zake kwa wakati. Kisha, angeweza kuchukua pesa na kuzitumia katika uwekezaji mwingine.

"Unastahili sifa kubwa zaidi kwa hili Lisa." Joseph aliinua kikombe chake cha kahawa na kumpa toast.

Lisa alikunywa kahawa yake na kusema, “Joseph, tafadhali niandalie kazi zaidi. Nimemaliza kesi na ninadaiwa deni kubwa la ada za kisheria."
"Hiyo ni kweli. Gharama ya kuajiri jina la wakili huyo mkubwa lazima iwe ghali.” Joseph alisema kabla ya kutoa hati kwenye droo na kuikabidhi kwa Lisa. “Unaijua kampuni ya Mawenzi Investments? Iko katikati ya jiji na kwa sasa iko katika ujenzi. Niliuliza huku na kule na kukuta kuna vyumba vinne na nyumba saba za makazi ambazo zinatakiwa kufanyiwa ukarabati. Ukiweza kunyakua hii tenda, nitakupa kamisheni ya milioni ishirini. Gharama za muundo zitahesabiwa tofauti.”

Macho ya Lisa yaliangaza huku akisema kwa msisimko, “Nitajitahidi, Joseph.”

"Meneja wa Mawenzi Investments na mimi tumefanya kazi kadhaa hapo awali, kwa hivyo unaweza kwenda kwake moja kwa moja." Joseph alimpa kadi ya biashara.

Lisa alipigwa na butwaa kidogo akaduwaa hadi kukosa la kusema. "Joseph, vipi ikiwa wabunifu wengine katika kampuni watajua kuhusu hii na kufikiri kuwa unanipendelea?”

“Nimekupa tu nambari ya simu. Kufanikiwa au kutofanikiwa ni juu yako." Joseph alimkonyeza. “Hapo hakuna upendeleo wowote.”

Lisa alishikilia wazo hilo. Ilimbidi achukue mradi huo na ahakikishe hamwangushi bosi wake. Baada ya kurudi ofisini kwake, alikuwa karibu kuangalia habari za Mawenzi wakati Ethan alimpigia simu ghafla. Hakutaka kuwa na maongezi naye na alikataa kupokea simu yake. Ethan alipiga simu mara kadhaa zaidi, na kumkasirisha Lisa, hivyo akaiweka namba yake kwenye orodha iya blacklist.

Alasiri, Lisa alikuwa ametoka tu kwenye lifti wakati umbo la Ethan lilipotokea na kumzuia njia.

“Unajua jinsi unavyoudhi? Unataka nikuambie mara ngapi kuwa sitaki unifuatefuate?” Lisa alikasirika kama apasuke vile.

"Lisa, bibi yako amekufa!" Ethan ghafla akamshika mkono. "Ina maana hujui chochote kuhusu hilo?"

Mwili wa Lisa ulitetemeka. Aligeuka taratibu huku macho yake yakiwa yamejaa hali ya kutoamini. “Unadanganya!”

“Nitakudanganya vipi kwenye jambo zito kama hilo? Nilikupigia simu leo kwa sababu nilitaka kukufariji, lakini inaonekana kama familia ya Masawe haikukuambia chochote.” Ethan alikuwa amemaliza kuongea Lisa alipoachana naye na kukimbilia gari lake. Hata hivyo, mikono yake ilikuwa ikitetemeka sana hivi kwamba hakuweza kuufungua mlango.

“Acha nikupeleke, hutaweza kuendesha gari.” Ethan alichukua funguo za gari lake na kufungua mlango. Alimsaidia kuingia ndani na kumfunga mkanda kabla ya kwenda kwa kasi hadi kwenye nyumba aliyohifadhiwa Bibi Masawe.

TUKUTANE KURASA 86-90

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.....LISA
KURASA....86-90

Sura ya 86

Picha ya Bibi Masawe ilipoonekana machoni pake, ukweli ambao hakutaka kuamini hatimaye ulitiwa nguvu. Machozi yalidondoka mashavuni mwake kwa matone makubwa. Hakuwahi kufikiria kuwa sherehe ya uchumba wa Ethan na Lina ingekuwa mara ya mwisho kuonana na bibi yake.

“Nani amekuruhusu kuingia hapa?” Akiwa amevalia nguo nyeusi, Jones Masawe alimtazama kwa jicho lililojaa hasira na kumkokota hadi mlangoni. "Ondoa wazimu wako hapa!"

“Kwanini unanifukuza? Mimi ni mjukuu wake!” Lisa alisimama na kuhangaika mithili ya mnyama wa porini aliyenasa kwenye mtego. “Mbona hukuniambia kuwa Bibi amefariki? Ulininyima hata haki yangu ya kuonana naye kwa mara ya mwisho! Wewe mzee umechanganyikiwa siyo siri!”

"Unathubutuje kunikaripia?!" Masawe aliinua mkono wake ili kumpiga kofi usoni, lakini Ethan alikimbia kumzuia, akisema kwa hasira, " Lisa amekukosea nini, kuna lolote baya alilosema? Bibi Masawe alimpenda Lisa tangu alipokuwa mtoto. Usipomruhusu Lisa amuage kwa mara ya mwisho, huogopi kwamba roho ya Bibi haitapumzika kwa amani?”

Maneno 'kupumzika kwa amani' yalifanya macho ya a Masawe yapungue sana. Lisa hakuliona hilo na akauliza tu kwa uwazi, “Kwanini Bibi alikufa ghafla? Ingawa alikuwa amepooza mara ya mwisho nilipomwona bado aliweza kula vizuri. Hakupaswa kuondoka ghafla hivyo.”

Midomo myembamba ya Masawe ilitetemeka. Kwa kushangaza, ilionekana kana kwamba alikuwa amesahau jinsi ya kuongea. Pembeni, Lina alipumua kwa huzuni na kusema, “Bibi alipoteza hamu ya kula baada ya hapo na hali yake ya akili ilikuwa mbaya. Kwa kuongezea, tukio la James na wewe lilisababisha hali mbaya ya kampuni, kwa hivyo mama na baba wamekuwa wakijaribu kurekebisha hali hiyo na mara kwa mara walikosa nafasi ya kuwa karibu na Bibi. Nani angefikiria kwamba bibi angetutoka ghafla.”
Lina alitokwa na machozi alipokuwa akisema, “Baba, usijutie moyo sana.”

Masawe alikumbushwa na maneno ya Lina na kuzunguka zunguka kumkabili Lisa. “Haya yote ni makosa yako! Ikiwa usingeivuruga Kibo Group, nisingesumbuka na mambo mengi na bibi yako asingekufa.”

Ethan alishindwa kumsikiliza tena. "Mjomba, unawezaje kusukuma lawama kwa Lisa hata wakati huu? Ni dhahiri kwamba ni kwa sababu hukumwadhibu James vizuri. Alifanya mambo hayo yote kwa sababu ulimchekea. Sasa unavuna ulichopanda.”

“Ethan, najua hutufikirii mema tena kwa sababu tulibatilisha ndoa yetu, lakini huwezi kumkashifu baba yangu hivi,” Lina alishutumu kwa macho makali.

Huenda Ethan aliweza kustahimili hilo siku za nyuma, lakini baada ya kuona rangi halisi za Lina, alihisi chuki zaidi kila alipomuona. “Lina Masawe nimefurahi sana kwamba sikuishia kuoa mbweha mwenye sura mbili kama wewe, vinginevyo ningejuta maisha yangu yote!” Ethan alikaza sura na kusema kwa hasira.

“Je, mnaweza kuacha kupigana kuhusu mambo yenu ya kibinafsi kwenye msiba wa Bibi?!” Lisa akawakatisha kwa ukali kisha akaliendea jeneza.

Ilionekana kana kwamba asingeweza kufanya chochote kwa bibi yake sasa isipokuwa kupiga magoti na kulia. Alijisikia uchungu sana. Bibi na Babu yake wote walikuwa watu wenye uwezo huko Moshi wakati Lisa alipokuwa mdogo. Bila wao, kusingekuwa na familia ya Masawe leo.

Hata hivyo, walipokufa, walikuwa wameondoka haraka na kimya kimya. Hapakuwa na hata wageni wengi hapo waliofika kuomboleza.

Ethan alimfuata Lisa na kumfariji kwa huzuni, “usilie sana. Twende nikupeleke ufukweni ukaangalie mandhari? Huenda ukapata faraja kidogo”

Ethan akatoka na Lisa kwenda baharini ili kumliwadha na kupoteza mawazo. Alikumbuka kuwa zamani walikuwa wakitoka kwa safari fupi na alizikumbuka ghafla siku hizo.
•••
Jua likazama na usiku ukaingia. Alvin aliendesha gari na kurudi nyumbani na kukuta ni Aunty Linda peke yake alikuwa anapika nyumbani. “Lisa yuko wapi?”

“Bado hajarudi.” Shangazi Linda alikuwa amemaliza kuongea ndipo alipoona sura ya Alvin ikibadilika ghafla.

Alvin alitazama saa yake iliyokuwa ikionyesha saa mbili za usiku. Lisa hakuwa nyumbani bado. Japo ilikuwa mapema wasiwasi ulimwingia. Je, alikuwa amekwama kwenye trafiki? Alimpigia simu haraka, lakini hakuna aliyejibu.

“Damn it!” Mwishowe Alvin alitukana kwa kiingereza. Alikuwa kamtendea wema kidogo tu lakini yeye alikuwa tayari kavuka mipaka yake. Ingawa mkataba ulisema kwamba angeweza kurudi nyumbani kabla ya saa tatu usiku, alikuwa akivuka mipaka kwa kutojibu simu zake.

"Bw Kimaro, unapaswa kula chakula cha jioni kwanza." Shangazi Linda alimtengea chakula.

Alvin alivitazama tu na kuuliza, “umepika wewe?”

"Ndiyo, Bi. Kimaro aliniambia nijifunze kutoka kwake." Shangazi Linda akacheka. “Alisema asipokuja siku moja, angalau nitaweza kukupikia. Nilijaribu kuionja na ni sawa na—”

Aunty Linda alikuwa bado hajamaliza kuongea pale Alvin alipofagia vyombo mpaka chini. Ilionekana kutoka kwa macho yake kwamba alikuwa na hasira. ‘Inaonekana kwamba mwanamke bado anafikiria kuniacha.’ Alvin alijiwazia. Mwanamke huyo aliyelaaniwa. Alikuwa anacheza na akili yake. Ina maana alimwendea kimakusudi ili tu aweze kushughulikia kesi yake bila malipo?

Shangazi Linda akaruka kwa hofu. Tangu Lisa arudi, Aunty Linda alihisi kwamba Alvin amekuwa na hasira zaidi na zaidi. "Bi. Kimaro alimaanisha kwamba anaweza kufanya kazi ya ziada. Hakusema kwamba anaondoka.”

Alvin akanyamaza, hasira iliyokuwa machoni mwake ikapungua taratibu. Aliamua kutulia kwa muda huo. Ilikuwa bado haujafika muda wa kikomo kulingana na mktaba. Aligeuka na kupanda juu ghorofani.

Shangazi Linda alimwita, “Bw. Kimaro, chakula chako cha jioni…”

"Sili."

Baada ya kupanda ghorofani, ingawa alikuwa anapitia nyaraka za kesi fulani, tumbo lake lilikuwa na njaa zaidi. Alikuwa akiangalia muda kila baada ya dakika mbili. Hata ilipofika saa nne usiku, Lisa alikuwa bado hajarudi. Akili yake ikiwa imejazwa na taswira za mambo mabaya kumhusu, alitoa simu na kupiga kwa Hans. "Fuatilia Lisa yuko wapi."

Hans alikosa la kusema. Alipanga kupendekeza tu kwamba Alvin aweke mtu maalum wa kumfuatilia Lisa wakati ujao.

Dakika kumi baadaye, Hans aliona picha za CCTV za maegesho katika jengo Ruta Buildind Design & Construction na akanyamaza. Skrini ilionyesha wazi Lisa akiingia kwenye gari la Ethan. Hans alitaka kuchunguza zaidi, lakini Alvin aliendelea kumhimiza kwenye simu, ili aweze kumpa picha Alvin.
Baada ya kumtumia picha, alijaribu tena kumpigia simu Alvin lakini hakuweza kumpata. Hapo ndipo alipohisi kilichokuwa kimetokea, na hakusubiri hadi aambiwe.

Hans alishusha pumzi na kuelekea madukani kwenda kununua simu mpya na kumpelekea Alvin. Alipoingia kwenye chumba cha maktaba baada ya kugonga mlango, aliona simu ya mkononi ikiwa imevunjwa vipande viwili chini. Alvin alikuwa amejikalia kwa mawazo huku uso wake ukiwa na hali ya hasira ya kutisha.

Kusikia hatua za Hans zikiingia, Alvin aliuliza kwa sauti ya ukali, "Je, mimi si mzuri sana kwake?"

"Bosi, labda kuna zaidi ya hii kuliko inavyoonekana. Nitaendelea kuchunguza. Labda nijue walienda wapi…” Hans alimweleza tarataibu bosi wake.

“Lazima ujue kama walienda hotelini!” Alvin aliinuka hasira ikizidi kumtawala usoni.
Hans Alikuwa msaidizi wa Alvin kwa muda mrefu na mara chache alimuona akiwa na hasira kiasi kile. Labda hata Alvin mwenyewe hakutambua ni kiasi gani Lisa aliathiri hisia zake.

"Au basi tu, hakuna haja ya kujua, achana naye." Alvin alikunja ngumi, sauti yake ikiwa kubwa na kali. "Nataka kuona ni muda gani atakaa nje."

Sura ya 87

Katika chumba cha maombolezo. Lisa alipiga magoti usiku mzima akimlilia bibi yake. Jones Masawe, Mama Masawe, na Lina walirudi usiku wa manane wakiwa wamelewa. Ukiacha wana ukoo wachache waliokuwa wakiomboleza nao, ni Ethan na Lisa pekee ndio walikuwa wamebaki ndani ya jumba hilo kubwa.

"Rudi nyumbani." Lisa alijua kwamba Ethan alikuwa anakaa kwa sababu yake, lakini hakutaka kuwa na shukrani.

“Siondoki. Bibi Masawe alikuwa mzuri sana kwangu zamani. Kumuomboleza kwa mara ya mwisho ni jambo ninalopaswa kufanya.” Ethan alisisitiza na kukaa pembeni yake.

Lisa alitabasamu kwa hasira za ndanindani. Hata Ethan alijua kumuomboleza vema Bibi yake, lakini vipi kuhusu Masawe? Masawe alikuwa mtoto wa Bibi yake kweli? Bibi yake pia alikuwa akimtendea Mama Masawe kama binti yake mwenyewe. Ukatili wa wanandoa hao ulibadilisha sana mtazamo wake.

Katikati ya usiku, ukumbi ulikuwa wa baridi na wa kutisha.Lisa alikazia kukesha na hata hakuona kwamba Ethan alikuwa ameweka nguo mabegani mwake.

Kulipopambazuka, taratibu za mazishi ziliendelea na hatimaye Mida ya mchana, ndugu jamaa na marafiki wa ukoo wa Masawe na wengine walikuja kumpeleka bibi Masawe mazikoni. Alizikwa kwenye makaburi ya Kinondoni.

Macho ya Lisa yalikuwa mekundu kwa machozi. Hata alipotoka kwenye mazishi, bado alikuwa amezama katika huzuni na kuchanganyikiwa. Hatimaye, mtu wa mwisho katika familia ambaye alimpenda kikweli alitoweka. Kwa kweli alikuwa peke yake katika ulimwengu huu.

Baada ya kumaliza kumpumzisha bibi yake, Lisa aliamua kuelekea ofisi kwenda kuchukua gari lake na mizigo yake aliyoacha ofisini.

"Lakini wewe…" Etha alitaka kumzuia apumzike walau siku mbili hivi kabla yakuanza tena kazi.

“Hakuna haja. Mambo mengi sana yametokea mwaka huu kwa hiyo nimekuwa na nguvu za kutosha,” Lisa alimkatisha kwa nguvu sana.

Ethan alihisi kana kwamba moyo wake ulikuwa ukichomwa kisu. Alikuwa katika mazingira magumu sana, lakini sasa, ilibidi akabiliane na haya yote peke yake. Ni kwa sababu alikuwa ameshindwa kutimiza wajibu wake.

Ethan alimpeleka Lina hadi kwenye jengo la ofisi ya kampuni ya Ruta. Baada ya Lisa kushuka kwenye gari Ethan hakuweza kujizuia kumsogelea na kumvuta. "Lisa, iwe unaniamini au la, nitakuwa pamoja nawe siku zote."

Lisa alikunja uso na alikuwa karibu kuuondoa mkono wake mara sauti ya mlango ukibamizwa ghafla ikasikika. Kisha, akasikia sauti ya kutisha kama simba masikioni mwake ikimwamuru. "Njoo hapa."

Lisa alishtuka na kugeuka kutazama. Alvin alikuwa amesimama mita moja, akiwa amevalia suruali nyeusi na koti jeusi. Alikuwa amevimba kwelikweli kama puto lililotayari kupasuka muda wowote. Hisia mbaya ilimjia moyoni mwake huku akiurudisha mkono wake kwa haraka.

Lakini, machoni pa Alvin, ilionekana zaidi kama alikuwa akijaribu kuficha kitu. Uchungu ulioje! Alikaa nje usiku mzima bila taarifa huku Alvin akienda kumfuatilia ofisi na kumsubiri tangu saa moja asubuhi. Hadi mida hiyo ya saa nane! Mwishowe, alichokiona ni mwanaume mwingine akimpeleka kwenye kampuni na yeye akiwa amevaa nguo zake. Na aliposhuka kwenye gari, Ethan hata akamshika mkono kana kwamba ni wanandoa waliopendana ambao hawakuweza kuvumilia kutengana.

Mara Alvin alipofikiria jinsi ambavyo Lisa alikuwa kwenye kitanda cha Ethan usiku mzima, moto usioelezeka uliwaka kwa nguvu moyoni mwake. Moto uliwaka kana kwamba unataka kumyeyusha kama donge la mafuta kikaangoni.

"Bw Kimaro…” Ethan alishtuka kidogo, hakuelewa kwa nini Alvin alikuwa hapo mchana ule.

Alvin alimpuuza Ethan na kukomaa na Lisa. “Lisa Masawe wewe ni kiziwi? Umesikia nilichosema?” Alvin alionya vikali kwa mara nyingine tena.
Lisa haraka akamsogelea. Kwa nguvu alimkumbatia mikononi mwake na kumvua nguo na kuzitupa chini.

Lisa pia alipigwa na butwaa. Hapo ndipo alipogundua sweta ya Ethan ilikuwa mabegani mwake. Kweli, lazima Alvin angechanganyikiwa kwa kuona vile, lakini Lisa alikuwa amechoka sana kiasi kwamba hakuwa katika hali ya kueleza chochote.

"Bw Kimaro, unafanya nini?" Macho ya Ethan yalimtoka. Taratibu aliweza kuhisi ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kati ya Alvin na Lisa. Hata hivyo, hakuelewa mambo mengine. Alichokuwa anajua ni kwamba, Alvin alikuwa amemsaidia Lisa tu kwa kesi yake mahakamani.

“Unafikiri ninafanya nini?” Alvin alikibana kidevu cha Lisa kwa nguvu na kumbusu midomo yake bila kujizuia. "Yeye ni mwanamke wangu, kwa hivyo kaa mbali naye. Vinginevyo, utachochea mambo kati yangu na familia yako.”

Ethan alishtuka kabisa. "Hiyo haiwezekani! Yeye hakupendi hata kidogo. Lisa, nini kinaendelea?”


“Bado hujaelewa tu?” Alvin alipoona Ethan anazidi kuwatumbulia macho ya mshangao, alizidi kumpiga busu la mdomo Lisa hadi mate yalipomkauka mdomoni.

“Kumsaidia kusimamia kesi yake haimaanishikuwa yeye ni mpenzi wako!” Ethan aling’aka kwa sauti kubwa ya hasira.

"Hakuna kitu cha bure ulimwenguni. Kwa kuwa alitaka nichukue kesi yake, anahitaji kulipa ikiwa hataki kwenda jela.” Alvin aliongea bila aibu.

Ethan alichukizwa na maneno yake na kupiga hatua mbili nyuma. Alitikisa kichwa huku uso wake ukiwa umebadilika rangi kana kwamba hawezi kuukubali ukweli huo. “Haiwezekani. Haiwezekani.” Ethan hakuamini kabisa, msichana mzuri ambaye alikuwa amemtunza tangu utotoni angewezaje kuwa mali ya mtu mwingine sana.

"Huna la kufanya hata kama huamini." Alvin alizidi kuumiza kichwa Ethan.

Ethan hakuvumilia tena kusikiliza dharau za Alvin na kumrukia mara moja. Kwa haraka Alvin alimvuta Lisa nyuma yake na kukwepa shambulizi hilo kabla ya kulipiza kisasi haraka, akampiga Ethan chini.
Hata hivyo, hasira moyoni mwake haikutulia. Alipokaribia kuinua mguu wake Lisa alimkimbilia na kumkumbatia kwa woga. "Acheni kupigana."

Alvin alinyamaza kwa chini kwa sababu yake, lakini Ethan alichukua nafasi hiyo kuruka na kumpiga Alvin usoni haraka. Mdomo wa alvin ulipasuka mara moja na kumshtua Lisa. Alvin alimkamata Ethan na kumtupa chini na kuanza kumpiga bila huruma mpaka akashindwa kusimama tena. Lisa alipigwa na butwaa. Hakujua kamwe Alvin alikuwa na ujuzi wa upigana kiasi hicho.

Baada ya kipigo hicho, Alvin alimnyanyua Lisa na kumtupa kwenye gari. Kisha akamkimbiza kama upepo kuelekea nyumbani.

Baada ya kufika kwenye jumba lao la kifahari, Alvin alimkokota Lisa kutoka kwenye gari moja kwa moja hadi chumbani na kumwambia kwa macho ya ukali, “unathubutu vipi kuungana na mwanaume mwingine kunishambulia?”

“Si…sikufanya.” Lisa alijaribu kuinuka, lakini magoti yake hayakuweza kupata nguvu baada ya kupiga magoti kwa muda mrefu sana jana yake usiku. “Ni kwa sababu…”

“Nyamaza, wewe mwanamke mwongo!” Alvin akamfokea, “Unadhani nitakuamini tena? Ulisema unanipenda, lakini ni kwa sababu tu ulitaka nichukue kesi yako mahakamani. Sasa kwa kuwa imekamilika, unataka kunitosa mara moja. Ulisema kwamba humpendi Ethan tena, lakini umethubutu kwenda naye hotelini.”

Ikiwa haya yangetokea zamani, Lisa angebishana naye, lakini alikuwa amechoshwa na huzuni ya msiba siku hiyo. Hakuwa hata na nguvu ya kubishana. “Umeniona nikienda naye hotelini?”

“Kama hukuenda hotelini, kwa nini hukurudi jana usiku? Kwanini ulikuwa umevaa sweta lake? Angalia tu mwonekano wako. Ni wazi kuwa hukulala kabisa jana usiku.” Alvin alimtazama kwa macho yaliyojaa karaha.

Lisa alihisi hasira kabisa. Jana yake usiku mzima alikuwa akimkeshea marehemu bibi yake, hakuwa na nguvu ya kumweleza hayo bado lakini mawazo yake yalikuwa machafu sana. Kana kwamba amerukwa na akili, Lisa alivua nguo zake zote na kuzitupa chini. “Niangalie vizuri. Angalia vizuri na uone ikiwa utapata dalili yoyote ya kulala na mwanamume kutoka kwangu. Angalia uone kama nilishawahi kufanya huo uchafu unaoufikiria kichwani mwako!"

Kadiri alivyokuwa akiongea ndivyo alivyokuwa akifadhaika na kufadhaika zaidi. Ghafla, alionekana kudondoka kabisa huku machozi yakimdondoka kwa matone makubwa machoni mwake. Alvin alikuwa mwisho wa akili yake akimwangalia akilia. Alichukua nguo zake kwa kuchanganyikiwa na kuziweka juu ya mwili wake.

"Sawa, hata kama hukufanya chochote na Ethan, ukweli ni kwamba ulikaa nje na mwanaume mwingine usiku kucha na haujarudi nyumbani Hii inathibitisha kuwa haujali mkataba wetu hata kidogo. Lisa Jones, nitakufundisha bei ya kuvunja mkataba.”

"Utafanya nini?" Lisa alimkazia macho kwa hasira.

"Kuanzia sasa, unahitaji kukaa hapa na huwezi kwenda kazini tena, usije ukanifanya kuwa mjinga." Alvin alikoroma kwa ukali kabla ya kuufunga mlango kwa nguvu na kuondoka. Lisa hakujaribu kugonga mlango. Alikuwa amechoka sana.

Bibi yake ambaye ndiye ndugu yake pekee aliyekuwa amebaki akimpenda alikuwa amekufa, na Alvin naye ndiyo huyo hakuwa hakimwamini hata kidogo! Alijisikia kama vile anapoteza kabisa matumaini ya kuishi. Hiyo ilikuwa sawa. Angalau angekufa tu. Hakukuwa na kitu cha kuogopa. Hakuhitaji tena kufikiria jinsi ya kumlipa Alvin.

Sura ya 88

Alvin alifikiri kwamba Lisa angefanya fujo, au kukubali makosa yake na kuomba msamaha, lakini alikuwa kimya sana.

Saa kumi jioni, Aunty Linda alimpelekea chakula lakini alirudi tena baada ya muda akitikisa kichwa. “Bw. Kimaro Bi. Kimaro anakataa kula. Hali yake inaonekana kuwa mbaya kidogo."

"Ikiwa hataki kula, basi mwache afe njaa." Alvin alilitupia gazeti lake kando na kujibu kijeuri.

“Bw. Kimaro, umeuliza ni wapi hasa Bi. Kimaro alienda jana usiku? Labda kuna kutokuelewana.” Shangazi Linda alishindwa kuvumilia. Vijana daima hugombana kwa sababu hakuna anayetaka kumsikiliza mwenzake. Wala hawakuwa tayari kukubali kushindwa na kusujudu, hata hivyo wao hawakutaka kujieleza pia. Waliendelea kukorofishana japo ilionekana wazi Alvin alikuwa anamjali sana mke wake.

"Kuna kutokuelewana gani?" Alvin aliuliza, lakini moyo wake uliguswa. Alikuwa akimshutumu tu Lisa bila kumpa nafasi ya kujieleza. Alipapasa macho yake kwa kuchanganyikiwa na kusita kwa muda kabla ya kumpigia simu Hans. "Nenda ujue walichofanya baada ya hapo." 'Kama walienda hotelini… Heh, Lisa Jones, maisha yako yatakwisha.”

Hans alikosa la kusema. Alvin alikuwa amemwambia aachane na habari hiyo, lakini ghafla tena alitaka kujua! Alvin alimchosha sana kijana wa watu.

Saa moja za jioni, Hans alimwendea Alvin akiwa na habari ya kusikitisha. “Bw. Kimaro, umemwelewa vibaya sana Bi Lisa. Ingawa alikuwa na Ethan Lowe jana usiku, walikuwa pamoja katika chumba cha maombolezo. Bibi yake amekufa na leo ilikuwa ni siku ya mazishi. Ethan na marehemu Bibi Masawe walikuwa wanafahamiana, kwa hiyo alienda kutoa heshima zake.”

Alvin alipigwa na butwaa. Alisimama ghafla na kutamani kumpiga Hans teke bila sababu lakini akajizuia. “Kwanini hukuniambia hivyo jana usiku?” Alvin alikataa kabisa kubeba lawama. Alipokumbuka alichokifanya kwa Lisa mapema siku hiyo, moyo wake ulimsuta.

"Wewe ndiye ulinizuia baada ya kufuatilia nusu tu." Hans naye alijitetea.

“Lazima Lisa anahisi kufedheheshwa sana, haswa bibi yake alipokufa na ndipo moyo wake ulipofadhaika sana. Haishangazi Aunty Linda alisema hali yake ilikuwa mbaya.” Alvin alijawa na simanzi ghafla.

Alvin alipata hisia kwamba huenda Lisa angechukua maamuzi mabaya. Harakaharaka akapanda juu na kufungua mlango, akasogea mpaka kitandani. Huko, alimwona Lisa amelala na macho yake yamefunga. Uso wake ulikuwa umepauka kama karatasi na hakuonekana kuwa anapumua.

Moyo wake uliingiwa na woga usioelezeka huku akinyoosha mkono kuweka kidole chake chini ya pua yake. Lisa alifumbua macho kwa unyonge. Alipomuona Alvin, aliongea kwa sauti yake ilijyoaa uchovu na huzuni. “Haitoshi kunifungia chumbani, Unataka kunipa adhabu gani nyingine? Sema tu.”

Moyo wa Alvin uliokuwa umeshikwa kwa nguvu ulilegea ghafla. Ilikuwa kana kwamba hatimaye angeweza kupumua kwa uhuru. Lakini alipomtazama Lisa aliona aibu kidogo. Alitaka kuomba msamaha, lakini kiburi chake hakikumruhusu. "Bibi yako alikufa lini?"

“Juzi” Lisa alijibu kinyonge.

“Kwa nini hukuniambia? Nilikupigia simu usiku kucha lakini hukupokea. Nilidhani kuna kitu kimetokea kwako…” Alvin aliuliza akiwa ameungana na huzuni ya Lisa.

“Hukuogopa kwamba kuna kitu kilinipata. Ulikuwa na mawazo kwamba nitakuwa sehemu mbaya nikikusaliti.” Lisa alimchana Alvin. “Hivi, umewahi kumpoteza mtu wa familia yako mpendwa zaidi hapo awali? Unapozama katika huzuni, ungekuwa na nguvu ya kujibu simu?!”

Moyo wa Alvin ukajawa maumivu. Alielewa hisia hiyo, hasa pale alipompoteza mpenzi wake, Sarah Langa.

“Isitoshe, hukuniuliza na hukuniamini. Tangu mwanzo, ulinituhumu kwamba mimi na Ethan Lowe tulikuwa tumeenda hotelini kulala pamoja.” Maneno ya Lisa yalizidi kumchoma Alvin. “Wakati mimi nimekesha usiku kucha nikilia, wewe unasema kwamba nimechoka kwa sababu nilikuwa nafanya mambo mengine. Ulinishushia hadhi mbele ya Ethan kana kwamba… Kana kwamba mimi ni mwanamke ninayejiuza.” Machozi yake hatimaye yalitiririka bila kujizuia.

Alvin alishindwa cha kusema, lakini alishindwa kuyazuia mawazo yake. “Kwanini unajali sana hisia za Ethan? Ina maana bado unamjali moyoni mwako?”

“Nimjali mtu niliyeachana naye wanini?” Lisa aliapa, “Nilisalitiwa na kutupwa naye hapo awali. Tayari ameshanipotezea heshima yangu, na wewe bado unaendelea kunididimiza zaidi. Umenifanya nionekane kama bidhaa. Maadamu mtu akiwa na pesa na nguvu, basi anaweza kunipata na kulala nami. Je, nina heshima yoyote iliyobaki?"

Alvin alimtazama kwa muda mrefu kabla ya kuyaminya maneno yale kooni. “Unanikemea?”

“Hapana, siwezi kukukemea!” Lisa alitabasamu kwa kujidharau. Akapigapiga kifua. “Umeniokoa, kwa hiyo nina deni kwako. Hata ukinipiga kofi lazima nifurahi na kupiga magoti kama mbwa. Sipaswi kukupinga. Nilikosea!"

Alvin aliduwaa kabisa na kushindwa kujibu. Japokuwa alikuwa mwanasheria mahiri, mwenye uwezo mubwa wa kupinga hoja mahakamani, hakujua la kusema tena.

“Unataka nipike sasa? nitakwenda.” Lisa alijikaza ili kuinuka.

“Acha!” Alvin alimlazimisha chini tena. "Lala tu, usihangaike.”

“Sawa, nilisahau. Bado umenifungia,” Lisa alisema kwa dhihaka.

“Lisa Jones, umemaliza? Ninakubali nilikosea. Nilikuhukumu vibaya. Ilikuwa kosa langu, sawa?" Alvin aliinamisha kichwa.

Lisa alikosa la kumwambia, na macho yake yalikuwa matupu. “Si lazima uombe msamaha hata kidogo. Wewe ni bwana wangu, kwa hiyo chochote unachofanya ni sawa.”

Alvin alikuwa anaumwa na kichwa sasa. Kwa kweli hakupenda vmaneno yake yaliyojaa kashfa za chinichini.

"Kwa vyovyote vile, unapaswa kupumzika tu kwa sasa. Huruhusiwi kwenda popote.” Alvin alishuka kwenda jikoni na kurudi na chakula. "Kula chochote."

Alvin alifikiri kwamba Lisa angegoma, lakini Lisa alikaa tu na kula bila kusita, kama vile roboti inayotii maneno ya bwana wake. Kwa kweli Alvin hakujua la kufanya. Alikuwa na uzoefu mdogo sana wa kubembeleza wanawake. Tayari alikuwa ameomba msamaha. Kwake yeye ilikuwa imetosha.
•••
Katika maktaba yake usiku, Alvin alianza kwa kupiga simu ya video na marafiki zake kadhaa. Chester Choka alikuwa amevaa pajama na ameshikilia glasi ya mvinyo. Alitabasamu kwa umaridadi na kusema, “Ni mshangao ulioje. Uko huru vya kutosha kutufikiria leo.”

Rodney Shangwe pia alicheka. "Ndio, huwa haujisumbui kuwasiliana nasi ikiwa hatutawasiliana nawe kwanza, leo utakuwa na tatizo gani?"

Sam Harrison alicheka pia. "Nadhani utakuwa umemchukiza mwanamke wako na hujui la kufanya."

Alvin alimtazama Sam bila furaha. Alijua kwamba Hans asiye na siri lazima alimwambia.

“Ukiniuliza, wakati huu nitasema kwa kweli ni kosa lako,'”Sam alisema, "Nilisikia kwamba Bibi Masawe amekuwa akimtendea vyema Lisa siku zote. Familia ya Jones sasa haimjali kabisa Lisa, kwa hivyo unaweza kusema kwamba Bibi Masawe ndiye alikuwa familia yake pekee.”

Alvin alikasirika kimya kimya na kuwasha sigara. Kila mtu alimtazama kwa macho magumu. Marafiki wa karibu tu kama wao waliujua uso wa Alvin anapokuwa na jambo linalomtatiza..

“Nini hasa kilitokea?” Chester aliuliza huku akicheka. “Wacha tuwape mawazo. Nina uzoefu katika kushughulika na wanawake."

Sam alisema, "Kwa kifupi, Lisa alikwenda kwenye mazishi ya bibi yake lakini alituhumiwa kwa kumsaliti Alvin na akafedheheshwa sana."

Rodney aliguswa. "Hiyo sio tu kuongeza moto kwa jeraha?"

Chester alinyonya midomo yake. "Hiyo ni ... kidogo sana."

Alvin akawakazia macho. "Nisaidie kufikiria njia. Mwanamke anapompoteza mtu wake muhimu zaidi katika familia, unawezaje kumfariji vipi?”

Chester aliinua uso wake. “Nunua vito, umtumie pete, maua, au ukodishe kisiwa ili kumfurahisha?”

Rodney alisema, “Mpe pesa, nadhani. Mama yangu huwa na furaha kila anapopokea pesa.”

Sam akaingia, “Mtoe nje kula aiskrimu. Dada yangu anapenda kula aiskrimu kila anapokuwa katika hali mbaya.”

Alvin akasugua kichwa chake. "Mwanafamilia yake amekufa, tunawezaje kutoka katika hali ya kimapenzi?"

"Hiyo ni kweli." Chester alidakia. “Kwa kweli sina uzoefu katika eneo hili. Hakuna hata mmoja wa familia ya rafiki zangu wa kike aliyefariki tukiwa wapenzi. Ikiwa hakuna kitu kingine kitakachosaidia, basi tayarisha sadaka za mazishi kwa bibi yake ili aweze kuishi kwa furaha katika maisha ya baadaye.”

Alvin aliganda, bila hata kutambua wakati sigara iliyokuwa mkononi mwake ilidondosha majivu kwenye mguu wake wa suruali.

Sam na Rodney walishtuka. “Mkuu, usiniambie umependezwa na wazo lake?!”

“Ni wazo zuri.” Alvin akakata simu ya video na kumpigia Hans. "Nunua sadaka za mazishi, gharama kubwa zaidi ni bora zaidi, nguo, viatu, kila kitu. Nunua nyingi iwezekanavyo.”

Hans alipigwa na butwaa. Hii ilikuwa mara ya kwanza kuamriwa kufanya kitu kama hicho.

“Unataka kiasi gani?”

“Haijalishi. Hata ukijaza Lori."

Hans akaguna.

Sura ya 89

Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Lisa aliamka kwa wakati kama kawaida. Alvin alikuwa ameamka zamani sana. Baada ya kumuona akinyanyuka alimuuliza. "Unafanya nini?"

"Naenda ktengeneza kifungua kinywa."

Alvin alikunja uso. Bibi yake alikuwa amekufa, lakini bado alikuwa na hamu ya kutengeneza kifungua kinywa? “Usiende, acha tu Aunty Linda afanye hivyo asubuhi hii.” Akamshika mkono.

"Hapana, ni jukumu langu kukuandalia kifungua kinywa." Lisa kwa utii alitenda kama mtumishi.

Alvin alikaa kitako huku akiwa amechanganyikiwa. “Sisi hatuli. Jiandae kuna sehemu tunaenda.”

Lisa alikunja uso. Ikiwa hakuwa akimfungia, basi angetaka kwenda kazini. Lakini, alikuwa na sauti ya mwisho. "Sawa.'

Baada ya kuoga na kuvaa, Alvin alimpakia kwenye gari lake. Lisa hakujua wanaelekea wapi na wala hakuuliza. Hakutaka kuwasiliana naye hata kidogo. Ni mpaka walipofika makaburini ndipo alipotambua kuwa ni sehemu aliyozikwa bibi yake.

“Kwa nini umenileta hapa?” Lisa aliuliza kwa mshangao.

"Kutoa heshima." Alvin alifungua mlango na kushuka, lakini Lisa alikaa kimya ndani.

“Tayari nimeshamaliza kutoa heshima yangu na huna haja ya kwenda kwani haikuhusu wewe.” Lisa hakutaka hisia zake zichanganyike tena.”

Alvin alikasirika na akasema kwa upole, “Ethan anaweza kutoa heshima yake, lakini mimi, siwezi? Unamaanisha nini kusema hivyo? Unahitaji nikukumbushe kwamba mimi bado ni mume wako wa ndoa?”

“Hunichukulii mimi kama mke,” Lisa alinung’unika kwa sauti ndogo na kupiga kelele. "Wewe ndio ulisema hautakutana na familia yangu."

"Sikusema sitamheshimu mtu wa familia ambaye amefariki." Alvin alimtoa nje ya gari.

Mara baada ya hayo, gari ndogo ya mizigo aina ya kirikuu ilisimama kando ya makaburi na Hans akaruka kutoka ndani yake. “Bw. Kimaro, nimetayarisha sadaka nyingi za mazishi hapa.”

Lisa alilitazama gari hilo na kugundua kuwa lilikuwa limejaa vitu vingi vya thamani. Alipigwa na butwaa. "Hii ni nini…"

Hans alikuwa na wasiwasi kwamba Alvin angesema kitu kibaya na mara moja akaeleza, “Bosi aliniambia niandae vitu hivi kwa ajili ya kumtolea sadaka Bibi Masawe. Ingawa hayupo nasi tena na hakuna anachoweza kufanya kuhusu hilo, anatumaini kwamba anaweza kuishi maisha ya starehe katika ulimwengu wa baadaye.”

Alvin akaguna na kujisemea kimoyomoyo, ‘ni lini alisema kitu kama hicho? Wow, yule kijana mdogo Hans hakika alijua jinsi ya kupamba maneno yake.’

Lisa alimtazama Alvin kwa macho ya mshangao na kuonyesha kutoelewa.

“Ndiyo.” Alvin aliitikia kwa upole. "Hii ni shukrani yangu kwa bibi yako."

Mtazamo wa Lisa ulikuwa wa kushangaza. Hakutarajia Alvin angefanya vile. "Lakini ... una uhakika unaweza kuiteketeza hapa? Je, mlinzi wa makaburi atakubali kuchoma vitu vyote hivyo hapa?”

"Kwa nini isiwe hivyo? Pesa inaweza kurekebisha kila kitu.” Hakika, kila kitu kilishughulikiwa kwa muda mfupi. Aliajiri watu kadhaa kubeba vitu na kuviweka sehemu ya wazi kisha vikachomwa. Kulikuwa na vitanda, magodoro, masofa, na vitu vingine vingi vya kifahari. Moto uliwaka kwa muda mrefu na Lisa aliutazama bila kusogea.

Alvin alimwendea na kumnong'oneza, "Usijali, bibi yako ataishi vizuri sana katika maisha ya baadaye."

“Ndiyo.” Lisa alishindwa kujizuia. Hali ya huzuni ambayo alikuwa nayo kwa siku chache zilizopita ilionekana kuboreka sana. Bibi yake alikuwa akimkumbuka babu yake kila wakati, kwa hivyo hii ilikuwa nzuri. Labda angeweza kuwa na furaha na babu na shangazi yake.

Baada ya kuchoma sadaka, Alvin ghafla alisimama mbele ya jiwe la kaburi la Bibi Masawe na kupiga magoti kwa huzuni. Midomo yake ikasogea kidogo kana kwamba alikuwa akisema kitu.

Lisa alishangaa kidogo. Ingawa bibi yake alikuwa mzee, hakutarajia kama Alvin angefanya jambo kama hili kwa mtazamo wake wa hali ya juu na wa nguvu. Hisia ya mshangao ilimwangazia moyoni mwake. "Ulimwambia nini bibi yangu?"

Alvin akamtazama. “Nilisema, mradi utakaa karibu yangu kwa utii, nitakulinda ili apumzike kwa amani.

Lisa alishindwa kujizuia. "Inatosha kama unaweza kuniamini zaidi.”

Lisa alimwonyesha Alvin kaburi la shangazi yake ambaye naye alizikiwa humo., Alvin aliona picha juu yake na ghafla akatulia. “Huyu mwanamke…Anafanana sana na wewe," Alvin alisema wakati akiiangalia kwa makini picha ya kaburi.

"Ndio, bibi yangu pia alisema kwamba mimi na shangazi yangu tunafanana sana." Lisa alishtuka.

Alvin alitafakari kabla ya kusema, “kwa kweli, sidhani kama unafanana na mama yako. Jones Masawe na mkewe pia hawaonekani kukutendea vyema. Wewe si binti wa huyu shangazi kweli?”

Lisa alipigwa na butwaa lakini akatikisa kichwa mara moja. "Hiyo haiwezekani. Shangazi yangu hakuwahi kuolewa na alifariki akiwa na umri mdogo. Angewezaje kupata binti? Sahau. Kuna wazazi waovu kila mahali."

Alvin akanyamaza kimya. Baada ya wawili hao kutoka makaburini, Lisa alitazama juu kwa wasiwasi na kusema, “Nataka kwenda kazini leo.”

Alvin alikunja uso na kumwambia. “Chunga masharti ya mkataba wetu. Unahitaji tu kukaa mbali na Ethan Lowe na Kelvin Mushi na wale wote kutoka jinsia tofauti. Pia, lazima ujibu simu zangu hata iweje, na urudi nyumbani kwa wakati."

"Sawa." Lisa aliitikia kwa utii. Ilimlazimu tu kuwa hivyo. Ni kwa kupata pesa zaidi haraka ndipo angeweza kuwa na ujasiri wa kumwacha kabisa.

Baada ya kurudi kwenye kampuni, aliwasiliana na meneja wa Mawenzi Investments. Baada ya kufanya miadi na meneja, alikwenda kwenye ofisi za kampuni hiyo mchana.

Ghorofa ya kwanza ya kampuni hiyo ilikuwa ni kituo cha mauzo. Ilijaa watu wanaoingia na kutoka. Alisimama ghorofa ya chini ili kusoma mipangilio ya ghorofa za juu, bila kuona kwamba kuna mtu alikuwa amesimama kwenye ghorofa ya pili akimwangalia kwa chini. Mtu huyo hakuwa mwingine ila ni Lina Jones Masawe, ambaye alikuwa ametokea tu na kuwa meneja mkuu wa mradi mpya wa ukuzaji mali wa Mawezi Investiments.

"Yeye ni nani na kwa nini yuko hapa?" Lina aligeuka kumwangalia naibu wake, Bruno Malisa, ambaye alikuwa na shughuli nyingi za kumtembeza kwenye mazngira ya kampuni.

“Yeye? Yeye ni mbunifu kutoka Ruta Buildind Design & Construction. Alikuja kumuona meneja wa idara ya mipango, labda kwa ajili ya usanifu wa mambo ya ndani wa nyumba zetu mpya.”

Lina alifikiri kwamba angekuwa mrithi wa kampuni ya Kibo Group kama si kwa figisufigisu za Lisa. Sasa kwa kuwa Kibo Group iliuzwa, alimchukia Lisa hadi mifupa yake.

"Je, hakuna kampuni zingine hapa Dar? Kwa nini ni lazima iwe Ruta Buildind Design & Construction?"
"Umaarufu wa Ruta kwa sasa unapanda kwa kasi sana baada ya kuanguka kwa Kibo, lakini bado makubaliano hayajawekwa sawa. Yupo hapa tu kuzungumzia jambo hilo.” Bruno alijbu.

Macho ya Lina yalimtoka na ghafla akatabasamu. Kwa vile alikuwa meneja wa kitengo cha ukuzaji mali kilichosimamia mradi huo sasa, angeweza kushughulika na Lisa vyovyote vile alivyotaka. Akamnyooshea kidole Bruno. “Si ulisema ulitaka kuchukua kandarasi ya madirisha na milango ya mradi huo? Unaweza. Ukimfundisha mtu huyu somo, nitakupa.”

Macho ya Bruno yakaangaza kwa mshangao. "Unamaanisha somo la aina gani?"

“Hilo ni juu yako. Haijalishi kama ataishi au atakufa.” Macho ya Lina yalikuwa na nia mbaya. "Ajali mara nyingi hutokea kwenye maeneo ya ujenzi, kwa hivyo huwezi kulaumiwa kwa masuala haya madogo. Kuwa mwangalifu tu.”

Bruno alipumua kwa hofu. Mwanamke huyo alikuwa mkatili kweli. Lakini alikuwa binti wa mwenye hisa mkuu wa kampuni hiyo, Jones Masawe, ilibidi tu ajipendekeze kwake. “Usijali, nitashuka na kulipanga mara moja.” Bruno alimhakikishia Lina.

Baada ya Kibo Group kuanguka, mara moja Jones Masawe aligeuka na kubadilika kuwa mwenye hisa mkuu wa Mawenzi Investments.
Sasa, kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba Jones Masawe angechukua nafasi ya mwenyekiti wa Mawenzi Investments, kwa hivyo ilimbidi Bruno ajipendekeze kwa Lina.

Sura ya 90

Lisa alingoja chini kwa nusu saa kabla ya mtu kumchukua na kumpeleka kwa ofisi ya meneja Mkuu —Bwana Lazaro Changala. Bwana Changala akammiminia kikombe cha kahawa. Walipokaa na kujiandaa kuanza maongezi yao, ghafla simu yake ikaita. Aliomba udhuru na kusema, “Bi. Jones, jambo la dharura lilikuja katika Idara ya Uhandisi. Tafadhali subiri kidogo.”

Lisa hakuweza kufanya chochote zaidi ya kutikisa kichwa. Baada ya kusubiri tena kwa zaidi ya dakika 20, ilikuwa karibu kumi na moja na nusuza jioni. Alianza kuwa na wasiwasi kwa siri. Ilionekana kuwa angerudi tena nyumbani kwa kuchelewa siku hiyo.

Kusudi Alvin asije akamtilia shaka tena, akachukua hatua ya kumpigia simu. “Naweza kuchelewa kurudi leo. Bado nasubiri mteja.”

Alvin aliridhika kabisa kwamba Lisa alichukua hatua ya kuripoti ratiba yake, lakini alichukizwa sana na mwanamke wake kusubiri mtu mwingine. “Uko wapi?”

"Katika kampuni ya Mawenzi Investments."

Alvin alitazama nje. Ilionekana hakuwa mbali na Mawenzi. “Sawa.”
Lisa aligundua kuwa hakukusudia kuuliza chochote zaidi na akakata simu baada ya maneno machache.

Muda si muda, mwanaume mmoja aliyevalia suti nyeusi akaingia. “Habari, wewe ni Bi Jones? Bw Changalka ametingwa na shughuli kwa sasa, ngoja nikupeleke saiti ukaangalie zile nyumba. Hii ni kadi ya jina langu."

Lisa alitazama kadi ya biashara. Jina lake lilikuwa Hector. "Tunawezaje kuingia ndani ya nyumba kabla hatujazungumza mipango ya makubaliano?" Lisa aliona ajabu.

"Moja yao tayari imeezekwa na haina ukuta wa nje, kwa hivyo tunaweza kuingia na kuangalia." Hector alicheka. "Kampuni inatilia maanani sana nyumba hizi. Kampuni za kubuni zinazokuja kawaida hufanya vipimo vyao kwenye saiti.”

Moyo wa Lisa uliguswa kidogo. "Je, kuna makampuni mengine ya kubuni yaliyokuja?"

"Ndio, kuna kampuni nyingine ambayo meneja wetu anaijua." Hector alijibu.

Wawili hao walizungumza huku wakitoka nje. Lisa alijaribu kupata habari zaidi kuhusu kampuni pinzani kutoka kwa Hector na walikuwa wamefika saiti bila kujua.

“Bi. Jones, unaweza kuingia kupitia hapa." Hector alimwelekeza na yeye akajificha chini ya paa.

Lisa naye alikuwa anakaribia kuingia pia mara sauti ya ukali ya mwanaume ilisikika kwa nyuma yake "Ondoka hapooo!"

Kabla hajajibu, aliona kivuli cha mtu kikimkimbilia na kumvuta pembeni. Kisha…Kama ajali hivi.. Vigae saba au nane vya kauri vilianguka mahali alipokuwa amesimama mtu huyo, vikivunjika na kusambaa ardhini.

Lisa alilindwa salama chini ya kifua cha mtu huyo. Mazingira yalipotulia, alitoka mikononi mwake akiwa na uso uliopauka. “Uko sawa?” Alikuwa ni Alvin!

“Mjinga wewe! Nani alikuambia uingie kwenye eneo la ujenzi bila hata vifaavya usalama?" Alvin haraka akamnyanyua kwa mkono mmoja na kumpeleka sehemu salama.

"Mimi... nipo hapa kupima vyumba." Miguu ya Lisa ilikuwa inatetemeka. Alijiuliza sana ikiwa huu ulikuwa mwaka mbaya kwake. Kwa nini alikumbana na hatari popote alipoenda?

"Basi kwa nini hukuvaa kofia ya usalama?" Alvin alimfokea. “Kama nisingekuwa karibu, kichwa chako kingekuwa chapati sasa hivi!”

"Samahani, nilisahau." Lisa ghafla aliona uchafu kwenye mkono wake wa kulia. Alikumbuka kwamba alikuwa ametumia mkono wake wa kulia alipokuwa akimkinga na vigae mapema. "Wewe, mkono wako umeumia?"

Alitaka kutazama, lakini alikurupuka kwa nguvu alipomgusa bega. “Usiniguse.”

Lisa alijua mara moja kuwa halikuwa jeraha jepesi. "Nitaita ambulensi mara moja."

Alikuwa ametoka tu kukata simu wakati Hector alitoka ndani ya jengo kwa wasiwasi. “Bi. Jones, uko sawa? Samahani, sikujua hili lingetokea.”

“Kwa hiyo wewe ndiye uliyemleta hapa? Nitafuatilia hadi mwisho wa hili." Alvin akamshika mkono Lisa na kutoka nje ya eneo la ujenzi.

Hata hivyo, kadri alivyokuwa akitembea kwa kasi ndivyo uso wake ulivyobadilika na ndivyo Lisa alivyokuwa na wasiwasi. “Acha kutembea. Tusubiri gari la wagonjwa lifike.”

"Usijali, ni jeraha dogo tu." Uso wa Alvin ulikuwa mtulivu kama dimbwi la maji yaliyotuama.

Lisa alikuwa amepoteza kabisa utulivu. “Basi nionyeshe.”

“Wewe ni daktari? Je! unajua jinsi ya kukagua majeraha?"

Lisa alinyamazishwa na maneno yake, lakini aliingiwa na hofu kabisa baada ya kuona madoa ya damu yakitoka mgongoni mwake. "Mgongo wako unavuja damu."

"Nyamaza." Lisa alinyamaza kweli. Aliita tena gari la wagonjwa kwa wasiwasi.
Kwa bahati nzuri, gari la wagonjwa lilifika baada ya dakika chache.

Baada ya kuingia, mhudumu wa afya alizikata nguo za Alvin mara moja. Wakati eneo kubwa la michubuko ya damu na majeraha yakifunuliwa mgongoni mwake, Lisa alipigwa na butwaa. Hakuthubutu kufikiria ikiwa yeye ndiye angepata majeraha hayo. Bila shaka angezimia kutokana na maumivu, lakini Alvin alikuwa hajasema neno tangu alipojeruhiwa. Hata akamshika na kuondoka naye. Ghafla hakujua jinsi ya kumuelezea mtu huyu. Wakati mwingine, alimchukia kwamba alimdhalilisha kila wakati, lakini alimwokoa mara kwa mara kutoka kwenye hatari zilizomwandama mara kwa mara. Wakati huo, hata alijeruhiwa ili kumwokoa yeye!

Alikuwa na hakika kwamba kama asingetokea siku hiyo, hakika angekuwa amekufa sasa.

“Binti, usilie. Majeraha ya mgongoni ni majeraha ya juu juu tu,” mhudumu wa afya alimwambia.

Lisa hakujitambua. Alikuwa analia? Hakuwa ameona kabisa. Alipojifuta uso kwa mkono, machozi yalimtoka kweli.

Alvin akamtazama. Hisia hafifu ya kutokuwa na uwezo ikajaa moyoni mwake, pamoja na ladha ya utamu. Hakika alimpenda kupita kiasi. Alijua kulia tu alipomuona anaumia.

"Lakini anaweza kuwa na mshipa uliochanika kwenye bega lake, kwa hivyo lazima afanyiwe upasuaji mara moja," mhudumu wa afya aliendelea kueleza.

Lisa alikosa la kusema. Hisia za maumivu alliyopata Alvin zilimfanya ajisikie kana kwamba anakaribia kufa. Maumivu ya kupasuka mshipa yalikuwa nje ya mawazo yake.

Muuguzi aliuliza, “Una uhusiano gani naye? Tutahitaji mwanafamilia kutia sahihi hati za upasuaji huo baadaye.”

Lisa alipigwa na butwaa. Pia hakujua uhusiano wake na Alvin ulikuwaje kwa wakati huo, lakini Alvin alimtangulia kusema, "Yeye ni mke wangu."

“Vizuri, atatakiwa kusaini karatasi baadaye.” nesi alisema.

Katika gari la wagonjwa, Lisa alimtazama Alvin akiwa kwenye machela. Alimtazama moja kwa moja, macho yake yalikuwa yamezama na giza. Uso wake ukasinyaa bila kuelezeka na moyo wake pia ulienda mbio. Mkewe…?!! Ilikuwa ni mara ya kwanza kumuita hivyo nje. Alipata hisia isiyoelezeka na ya ajabu! Hata hivyo... leseni yao ya ndoa ilikuwa halali.

Baada ya kufika hospitali, muuguzi alimsukuma Alvin kwenye chumba cha dharura ili apimwe MRI. Pia alimruhusu Lisa asaini karatasi hizo baada ya utambuzi kuthibitishwa. Alishikilia vitu vyake na kusubiri nje. Sam na Hans walifika pia hospitalini muda si mrefu. Baada ya upasuaji wa Alvin kukamilika, wawili hao walisaidia kupanga akae katika wodi ya watu mashuhuri.

Sam alilalamika kwa uchungu, “Alvin, kwa kuwa sasa umelazwa hospitalini, kampuni yetu ya mawakili inabidi kuchelewesha kesi kadhaa kubwa. Hasara zetu huenda zikaongeza hadi zaidi ya bilioni moja.”

"Atalipa huyu!" Alvin alimkazia macho Lisa. "Ni kwa sababu nilikuwa najaribu kumuokoa."

TUKUTANE KURASA 91-95

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI......LISA
KURASA.....91-95

Sura ya 91

Lisa aliishia kuguna tu. Alitaka kulia. Bilioni moja? Hakuwa na uwezo wa kumlipa hiyo pesa.

Sam naye aliligundua hilo na kumpa sura ya huruma. “Lisa, hutaweza kamwe kuepuka makucha ya Alvin kwa maisha yako yote.”

Lisa alikohoa na kusema. “Nilikosea."

Sam aliongeza kwa upole. “Hata hivyo, Mawenzi Investiments wanathubutu vipi kukuumiza bila kutoa maelezo?! Hakika nitavuruga mradi wao wa uendelezaji mali.”

"Nilisikia kwamba Mawenzi Investiments imegeuka kutoka kuwa biashara ndogo na kuwa moja ya biashara 100 bora Tanzania ndani ya muongo mmoja tu. Imekuwa ikifanya vyema kwa miaka hii yote kwa sababu kuna nguvu ya ajabu inayoiunga mkono," Hans ghafla alisema.

Kauli hiyo ilimshtua Sam. Alvin alifungua mdomo wake na kuongea “Ndio. Yuko sawa. Nenda kachunguze kama kilichotokea leo ni mpango wa makusudi au makosa ya kibinadamu, Hans."

Lisa alipigwa na butwaa kwa muda. "Labda ilikuwa ajali kwani sikumkosea mtu yeyote hapo Mawenzi Investiments. Kando na familia ya akina Jones Masawe, Janet, na Cindy, sidhani kama nina tatizo na mtu yeyote hapa Dar!”

"Shemeji, umewaudhi watu wengi, huh?" Sam aliongea kwa kejeli kidogo.

Alvin alimtazama na kusema kwa jeuri, “Haijalishi. Mradi tu uko chini ya mbawa zangu, nitakulinda hata kama ungemkosea kila mtu hapa Tanzania.”

Hans na Sam walikosa la kusema. Wakiwa kama mabachela, waliona kwamba uwepo wao haukuwa wa lazima.

"Hans, afadhali tuondoke.” Sam alikohoa huku akikunja ngumi mdomoni. “Kwa kuwa Alvin aliumia wakati akimwokoa Lisa, Lisa atalazimika kumhudumia Alvin. Niko sawa, Lisa"

"Ndio ndio. Hamna shida.” Lisa aliitikia kwa haraka.

Hans na Sam walipoondoka tu ndipo Lisa alipogundua kwamba haikuwa rahisi kwa mwanamke kama yeye kumwangalia Alvin. Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba alikuwa amekubali mbele yao, hangeweza kuvunja ahadi yake. Kwa bahati nzuri, ilikuwa wodi maalum yenye vifaa kamili ambapo angeweza hata kupika. Ilikuwa kama ghorofa kubwa.

"Una njaa? naenda kukununua…”
"lam. Nataka nyama ya nguruwe iliyochomwa.” Akiwa amelala kitandani kwa unyonge, Alvin alimtupia jicho.

Lisa alishindwa cha kusema. “Umesahau ushauri wa daktari kuwa huwezi kula chakula chenye mafuta? Vinginevyo, hutapona vizuri.”

“Haijalishi. Hakuna kitu kibaya sana na mwili wangu. Sijambo.”

"Hapana. Sitakupikia. Nitasimamia menyu yako wakati ukiwa hospitalini." Lisa alionyesha sura ya msimamo. Alvin aliinua uso wake lakini hakuwa na hasira.

“Lala tu upumzike hapa. Nitaenda kutafuta mboga.” Baada ya kumkumbusha Alvin, Lisa alishuka haraka haraka kwani aliogopa kumuacha peke yake kwa muda mrefu. Alirudi baada ya kununua nyama na mboga kwa haraka.

Alvin aliitazama mboga iliyokuwa mikononi mwake kwa sura isiyoelezeka. “Unapanga kunipikia chakula cha kawaida na viungo hivi?”

“Nimebaki sina jinsi. Hivi ndivyo viungo pekee vilivyouzwa nje ya hospitali, na wewe ndiye ulitaka nikupikie.” Kisha Lisa akasema kwa uchungu, “Usijali, hakika nitatayarisha chakula kitamu.”

Alipoelekea jikoni kuanza kupika, Hans alikuja tena.

“Umekuja kwa wakati ufaao. Nenda ukalete viungo vizuri vya chakula hapa,” Alvin alisema, “Jaza viungo kwenye friji.”

“Sawa.” Ndani kabisa, Hans aliendelea kunung'unika. 'Utakaa hapa kwa siku chache tu. Pia hutabaki hapa kabisa.' Lakini hakusema hivyo na badala yake akasema kilichompeleka. "Aah bosi, nilirudi baada ya kumaliza kuchunguza tukio la ajali yenu kule Mawenzi Investiments. Tofali lilianguka kwa sababu mfanyakazi alishindwa kulishikilia vizuri alipojaribu kuliweka kwenye ukuta wa nje.”


Alvin alikunja paji la uso wake kwa hasira. “Hakuna chochote cha kutilia shaka kuhusu hilo. Vipi kuhusu yule mtu aliyemuongoza Lisa pale? Alionekana kuwa salama wakati huo.”

"Alidai kwamba alikuwa na jukumu la kumwongoza Miss Jones kuchukua vipimo. Wakiwa njiani, wawili hao walikuwa wamezama sana katika mazungumzo kiasi kwamba alisahau kumpa Miss Jones kofia ya chuma ya usalama.”

"Hata hivyo, anahitaji kubebeshwa lawama za ajali hii," Alvin alisema kwa upole, "Tuma barua ya mwanasheria wa Mawenzi Investiments. Ikiwa fidia ambayo Mawenzi Investiments itatoa si ya kuridhisha, sitawaacha salama.”
“Sawa.”

Wakati huo, Lisa alileta chakula kwenye meza. Alipogundua uwepo wa Hans, alipigwa na butwaa. "Samahani, nimeandaa chakula cha watu wawili tu."

'Ni sawa. Tayari nimekula. Hata hivyo, nitaondoka baada ya muda mfupi.” Macho ya Hans yalizama kwenye chakula kilichokuwa mezani, jambo lililomshtua. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona Bw. Kimaro akiwa na mlo wa kawaida hospitalini. Kwa kweli, milo ya Alvin ilijumuisha zaidi ya aina kumi za vyakula. Kilichomshtua zaidi Hans ni kwamba Alvin hakuongea chochote kuhusu hilo.

Baada ya Lisa kuweka vyakula vyote, aliutupia macho mkono wa Alvin wa kushoto ambao bado angeweza kuutumia. “Unataka nikulishe? Au bado unaweza kula peke yako?"

“Upuuzi gani unaongea. Nitakulaje kwa mkono wangu wa kushoto tu?” Ndita usoni kwa Alvin zilikunjamana.

Mdomo wa Hans ulitetemeka. “Tafadhali, Bw. Kimaro. Mkono wako wa kushoto una nguvu zaidi kuliko mkono wako wa kulia. Na ndiyo unaotumia mara kwa mara”

“Ondoka sasa hivi.” Alvin alimtimua Hans bila huruma.

"Ndiyo ndiyo, bosi, natoka sasa hivi.” Hans alikimbia.

“Mbona unakuwa mkali sana kwa Hans? Nadhani yeye ni mzuri sana." Lisa hakuweza kujizuia kumuonea huruma Hans.

“Yeye ni mzuri?” Macho ya Alvin yalimtoka kwa huzuni. "Je, yeye ni mzuri kuliko mimi?"

Lisa alikuwa ameduwaa kwa muda. Ghafla, macho yake yakawa ya kushangaza. "Inaonekana ... una wivu."

“Mwenye wivu?” Uso wa kuvutia wa Alvin ulianguka kwa sekunde. Sentensi hiyo ilionekana kama mzaha kwake. “Naweza hata kupata wivu kwa sababu yako? Hivi ndivyo ambavyo huwa unajidanganya? Najaribu kukukumbusha tu, wewe usiye na shukrani. Usisahau ni nani ambaye amekuokoa mara nyingi."

"Ni wewe. Nakumbuka ni wewe. Haraka basi uanze kula. Usife njaa, la sivyo nitakosa mtu wa kunikoa siku nyingine.” Kwa vile Lisa hakutaka tena kusikiliza mihadhara yake, alimshawishi haraka kula huku akimlisha.

Hizi zilikuwa aina za vyakula vya kawaida ambavyo Alvin hakupenda kula wakati huo. Hata hivyo, mara tu Lisa alipomlisha chakula hicho, alikiona kitamu sana hivi kwamba akaomba zaidi.
Baada ya kula, Alvin alifumbua macho kwa uvivu. “Niinue. Nataka kwenda chooni.”
Lisa alijaribu kumuinua. Kwa mawazo ya mgongo wake uliojeruhiwa, alisita kabla ya kuweka mkono wake kiunoni mwake. Kiuno chake kilikuwa chembamba sana. Aliweza hata kuhisi misuli yake kupitia gauni jembamba la hospitali. Alvin akaketi. Vidonda na mshono kwenye bega lake vilimuuma sana hivi kwamba alitokwa na jasho baridi mara moja. Uso wake ulikuwa umepauka sana.

Kwa mshtuko, Lisa akasema mara moja, “Usishuke. Nitakuletea beseni.”
Mara moja akapata beseni mpya kutoka kwenye kabati kando yake. Alvin alivuta mdomo kwa kuhisi maumivu. Muda mfupi baadaye, alinong'ona, "Ninahitaji msaada wako."

Lisa alikosa la kusema. "Je! huna mkono mwingine?" Aliuliza kinyonge.

“Huoni jinsi maumivu yanavyokuwa yanavyoongezeka nikijisogeza?” Alvin alijaribu kusogeza mkono wake, na akasaga meno yake kwa ghafla. "Harakisha. Vinginevyo, nitajikojolea.”

Sura ya 92

Akiwa amejawa na aibu, Lisa alisogea mbele na kuingiza mkono wake ndani ya shuka aliliokuwa kajitanda Alvin. Hatimaye Alvin alishindwa kukojoa kwani Lisa alihangaika tu akiogopa kushika nanihii yake!

“Utachukua muda gani?” Alvin alimtazama kwa haya.

Akiwa amedhamiria moyoni, Lisa akataka kuishika na kuitoa nje….Muda huo huo daktari akaingia. "Bwana. Kimaro, ngoja niangalie…” Kwa kuona hali hiyo, daktari aliona haya huku akiwa amesimama palepale akiwa ameganda. “Samahani. Samahani. Nilikuja kwa wakati mbaya? Ninaondoka sasa hivi… Sasa hivi…”

Lisa alitoka haraka kwa Alvin. Alikuwa katika butwaa. Daktari aliwaelewa vibaya?
“Hapana, Dokta. Nilikuwa tu - "

"Usijali, na sikuona chochote. Nitakuja tena baada ya muda mfupi. Mnaweza kuendelea.” Akiwa na uso wenye haya, daktari alikwepa macho yake. Kisha mara moja akatembea hadi mlangoni.
Alipoufikia mlangoni, hakuweza kujizuia kugeuka. “Najua nyinyi wawili bado ni vijana, lakini afadhali muwe waangalifu. Kwani, ametoka tu kufanyiwa upasuaji.”

“Sikuwa…” Kabla Lisa hajamaliza sentensi yake, daktari aliondoka kwa haraka.
Lisa alibaki hoi. Jinsi alivyotamani kuruka kutoka kwenye jengo hilo na kukatisha maisha yake kwa aibu. Kwa hasira, akamtazama yule mchochezi Alvin pale kitandani. "Yote ni kazi yako."

“Imekuwa mimi ndiyo sababu siyo?” Alvin aliongea huku akivumilia maumivu. “Pengine. Sikupaswa kukuokoa wakati huo. Labda ungekuwa umelala kwenye chumba cha kuhifadhia maiti chenye barafu kufikia sasa. Basi nisingehitaji kuomba msaada wakati wa kutumia choo…”

“Inatosha. Acha mada zako za kijinga!” Lisa alifadhaika. "Sitakulaumu kwa kuwa wewe ni mkombokozi wangu."

“Vizuri.” Alvin alifumbua macho. "Unaweza kunisaidia sasa."

Lisa akashusha pumzi. Aligeuka huku akionyesha mkanganyiko kwenye uso wake mdogo mzuri. “Je, nimuombe Hans aje? Sitaweza kufanya hivyo. Tangu nilipoona mwili wako mzuri, siwezi kuacha kufikiria juu yake. Naogopa nita…”

“Midomo myembamba ya Alvin ilipinda na kuwa tabasamu la kuvutia. Akamwambia kwa tabasamu la utani. "Hata hivyo, ni nusu ya juu tu ya mwili wangu ndiyo imejeruhiwa."

Lisa alikaribia kuuma ulimi wake. Wakati huo, alifunga mlango na kukaa macho.
Ingawa aliuona mwili wake mara moja siku za nyuma, ilikuwa ni mtazamo wa haraka tu. Hakuwahi kuona kama alivyokuwa anafanya wakati huo. Alikuwa na umbo zuri sana, lililofanana na sanamu ya David, aliyejengeka vizuri.
Hah. Wakati ule hakupendezwa naye hata kidogo, na ilionekana kuwa alikuwa akijaribu kumnyanyasa kila alipoutazama mwili wake. Sasa ilikuwa ni nafasi yake kwa macho yake. Hmmph.

Alvin aliona sura yake. Alijua kwamba kwa muda mrefu macho ya Lisa yalikuwa yamelala juu ya mwili wake. "Harakisha. Utaendelea kujivuta hadi lini?" Alvin alimharakisha.

Kwa aibu, Lisa alifumba macho. Haraka akamalizia kumtolea ‘chululu’ yake na Alvin akakojoa.
Baada ya hapo alimuogesha kwa kumfuta na kitambaa palepale kwa sababu hakuweza kwena bafuni. Baada ya kuoga alijilaza nae kwa pembeni kwenye kitanda huku taa zikiwa zimezimwa.

Alvin hakumruhusu kulala naye. Mwanamke huyo alikuwa hajui kutumia nafasi ya kitanda na alikuwa akibiringita hovyo kitandani. Sasa kwa kuwa alikuwa amejeruhiwa, hakuweza kumudu kulala naye vinginevyo angetoneshwa majeraha yake yote.

Lisa hakuthubutu kulala fofofo. Katikati ya usiku, alimsikia mtu huyo akijirusharusha na kugeuka. Aliinuka na kuuliza kwa wasiwasi, "Je, unajisikia vibaya?" Alvin alifumbua macho.

Mwale wa mbalamwezi uliangaza kwenye mabega ya Lisa kupitia dirishani. Usiku huo, hakufanikiwa kurudi nyumbani kuchukua nguo zake, hivyo alikuwa amevaa tu nguo nyepesi ya ndani. Huku nywele zake ndefu na laini zikianguka juu ya mabega yake, alionekana mrembo na mzuri mithili ya video-vixen.

Maumivu bado yalikuwa yanavumilika kwake. Hata hivyo, kitu kingine kilitoka kinywani mwake. "Ndio, naumia."

“Nfanye nini?” Lisa alishikwa na hatia. “Ngoja nimpigie simu daktari.”

“Kuna umuhimu gani wa kumwita daktari? Hawezi kusaidia kupunguza maumivu yangu pia." Alvin alifumba macho, na macho yake yalionyesha kuchanganyikiwa. Akaachia mguno kwa unyonge. Alijifanya kana kwamba anajitahidi sana kuvumilia maumivu hayo. Usemi huo, pamoja na uso wake wa kuvutia, ulimfanya Lisa aushike mkono wake bila kujua. “Je, kuna chochote ninachoweza kukufanyia?”

“Utanisaidia?” Akafungua macho yake meusi.

“Ndiyo.” Lisa aliitikia kwa umakini.

“Uh…” Alvin alikunja uso kana kwamba anafikiria. Kisha, akasema, “Kwa nini usinipe busu ili niyasahau maumivu?”

Lisa alikodoa macho huku akijiuliza ni suluhisho gani hilo. Kama isingekuwa hali yake dhaifu, angetilia shaka sana kama hiyo ndiyo ilikuwa nia yake.

"Ikiwa hauko tayari kufanya, ni sawa basi." Alvin aligeuza uso wake pembeni na kuendelea kuugulia.

“Hapana, hapana. niko tayari kufanya hivyo.” Baada ya yote, alikuwa mwokozi wake.
Lisa alijipa ujasiri wa kumsogelea. Aliinamisha kichwa chake na kumbusu midomo yake myembamba.

Pengine ilikuwa ni kwa sababu alikuwa ametumia muda mwingi kupata sindano za dripu kwamba ladha hafifu ya dawa iliendelea kutawala kwenye midomo yake. Lakini ladha hiyo ilififia baada ya kumpiga busu lingine. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumbusu kwa hiari yake mwenyewe, na uso wake wote uliwaka furaha. Kwa bahati nzuri, taa hazikuwa zimewashwa.

Mwili wa Alvin ukawa mgumu, mapigo ya moyo yakaanza kwenda mbio.
Kabla hajapata fahamu zake, Lisa akarudi nyuma. Aliuliza kwa sauti nyororo iliyofanana na mlio wa mbu, “Umeridhika?”

"Ndiyo, nimefurahia sana na maumivu yalikuwa yanatoweka, lakini yamenza kurudi tena wakati ulipoacha," Alvin alijibu kwa sauti dhaifu ya kudeka.

“Lakini ninaogopa kwamba utakuwa na maumivu nikikubusu kwa muda mrefu,” Lisa alisema kwa unyonge.

"Njoo hapa." Alvin alitikisa kichwa kuashiria nafasi tupu upande wake wa kushoto.
Lisa alisita kwa muda kabla hajalala pale. Kisha, akambusu midomo yake tena.
Hapo awali, alionekana akimbusu kwa aibu. Baadaye, aibu zilianza kumwisha bila yeye kutambua. Huku akiwa ameduwaa, alimzungushia mikono yake kiunoni.

Hakujua ni muda gani walikuwa wamezama kwenye busu. Hatimaye Lisa taratibu alianza kuhisi uchovu. Alimuegemea Alvin na kulala baadae. Alvin akarudi nyuma, kisha akamtazama kwa jicho la giza. Baada ya hapo, alimbusu kwa upole kwenye paji la uso kabla ya kufumba macho na kulala. Maumivu aliyokuwa akiyasikia yalipungua baada ya huduma hiyo.

Kesho yake asubuhi, Lisa aliamka kabla ya Alvin. Bado alikuwa amelala wakati huo. Akiwa anatazama sura yake ya kupendeza kwenye uso wake mzuri kando ya mto, alikumbuka kila kitu kilichotokea usiku wa jana yake. Wazo hilo lilimfanya ajisikie haya. Lakini hakuonekana kuchukia.

Alishtushwa na mawazo yake hayo wakati mlango ulipogongwana sauti ikasikika. "Daktari anakuja kwa raundi."

Lisa alijitupia upande wa kanga aliyokuwa amenunua kwa haraka na kukimbilia kwa daktari. Ni Dokta Kane yuleyule aliyekuja usiku na kuwakuta kwenye pozi la utata, na kulikuwa na wahudumu wachache waliokuwa wakimfuata nyuma muda huo. Wote walipigwa na butwaa walipomwona Lisa. Macho yao yalikuwa yakimtazama kwa namna ya ajabu.

Uso wa Lisa ulishtuka. Alidhani kwamba wanafunzi wa mafunzo walikuwa wamegundua kutoka kwa Dk. Kane kuhusu kile alichokiona jana usiku.
Kwa bahati nzuri, Alvin alikuwa tayari ameamka wakati huo. Dokta Kane mara moja akamfanyia uchunguzi. Dakika kumi baada ya kufanyiwa uchunguzi, Dk. Kane alikuwa tayari kuondoka.

Alikunja ngumi na kukohoa kidogo. "Ingawa unapata ahueni ya haraka, bado lazima ujitunze."
Lisa alikosa la kusema. Alihuzunika sana hivi kwamba hakutaka kusema lolote lingine.
Ni baada tu ya kwenda kunawa uso ndipo aliona midomo yake ikiwa imevimba kwenye kioo. Alishtuka sana hata akakaribia kuangukia kwenye sinki la choo.
Hatimaye Lisa alitambua kwanini kila mtu alikuwa amemtazama kwa namna ya ajabu muda ule.

Sura ya 93

Muda mfupi baadaye, alitoka mle bafuni akiwa amechoka. “Yote ni makosa yako. Tazama jinsi midomo yangu ilivyovimba baada ya kunibusu. Nitaishi vipi hapa wodini?”

Baada ya kumwangalia, Alvin aliridhika moyoni na alichokifanya. Kwa uso uliopauka, alilalama kwa unyonge. “Samahani. Hiyo ilikuwa kwa sababu ya kunogewa sana kwangu. Mwili wangu uliuma sana jana usiku, na ilikuwa ni kosa langu. Usiku wa leo, nitajaribu kuvumilia maumivu na sitakusumbua.”

Kwa kuzingatia jinsi mwanaume huyo mzuri alivyokuwa dhaifu, Lisa hakuweza kujizuia kumkosoa wakati huo.

Hans na Sam walipofika saa tatu asubuhi, walishtuka kumuona Lisa akiwa amevaa barakoa. "Lisa, mbona umevaa barakoa?"

“Hospitali kuna watu wengi, kwa hiyo nadhani ni salama kuvaa barakoa, ukizingatia na hii hali ya korona” Lisa alijibu kwa sura ya ukali. "Nilisikia watu wengi wameambukizwa na homa hivi karibuni."

“Oh. Nipe na mimi barakoa basi, Shemeji. Nataka kuivaa ili kuepuka kuambukizwa pia.” Sam mara moja akataka kuvaa barakoa pia.

Alvin aliyekuwa amejilaza kitandani alikosa la kusema.
….
Ndani ya ofisi ya Mawenzi Investments, Jones Masawe alipopokea barua ya wakili, alimwomba Lina aje na baadaye akampa kipande cha mawazo yake.

“Umefanya nini? Nilihangaika sana kupata mradi mpya wa ukuzaji mali kutoka kwao ili tupate pesa lakini mlisababisha fujo mbaya muda mfupi baada ya kuchaguliwa. Nagombea nafasi ya mwenyekiti mwisho wa mwaka. Je, huwezi kuharibu mipango yangu?”

“Samahani, Baba. Kumwona Lisa kulifanya damu yangu ichemke, na nilitaka kumfundisha somo.” Akiwa na huzuni, Lina alipiga kelele. "Lakini sikutarajia kwamba Alvin angefanya hivyo kwa wakati ili kumuokoa."

“Alvin tena!” Masawe aliuma meno. “Lisa alimfahamuje mtu wa aina hii?”

"Lazima alilala naye." Lina akahema. "Nimemchunguza Alvin na kugundua kuwa hata wale ambao wako tayari kutumia mamia ya mamilioni ya pesa wanaweza kukosa kumwajiri, sembuse Lisa ambaye hana uwezo?"

Masawe aliposikia hivyo alionyesha sura ya kuchukia. "Anajidharirisha sana huyu binti."

“Baba, Alvin anaendelea kuharibu mipango yetu na sasa anaomba hata malipo ya fidia ya juu kutoka kwetu. Hebu tumfundishe somo.” Lina alisaga meno yake. “Hata hivyo, yeye ni mwanasheria tu. Zaidi ya hayo, yeye pia ni mgeni.”

"Usifanye haraka." Jones Masawe alimkazia macho. "Alvin ni wa kushangaza sana."

Lina alijibu kwa kutoridhika, “Ajabu, ili iweje? Kama mwanasheria, lazima atakuwa amewaudhi watu wengi kwa miaka mingi. Haitashangaza kama kuna watu wanataka kulipiza kisasi kwake…”

Jones alishawishika na wazo hilo. Baada ya muda, alipiga picha ngumu kwa binti yake.

“Nendeni mkachunguze kesi zote alizoshughulikia awali. Na je, umesuluhisha suala hilo na mradi wa usimamizi wa mali?"

“Usijali. Nimemhonga muuzaji na mfanyakazi pesa. Kilichotokea kwenye saiti ya ujenzi ilikuwa ajali tu, lakini fidia…”

“Lipa tu. Tunapaswa kulipa. Hatupaswi kumuacha Alvin afanye jambo kubwa juu yake.” Masawe aliongeza kwa kutoridhika, “Unapaswa kuacha kuendelea kurumbana juu ya suala hilo na Lisa. Kwa kuwa sasa umeachana na Ethan, unapaswa kuangalia familia nyingine tajiri na zinazojulikana.”

“Sawa.” Lina alitazama kwa aibu, kisha akasema, “Hivi majuzi, nimekuwa nikichangamana na Janet Kileo usiku, na kaka yake, Stephen Kileo, huja kila mara. Anaonekana kunipenda.”

Macho ya Jones Masawe yakaangaza. Stephen Kileo alikuwa mrithi wa familia tajiri ya Kileo, ambaye alikuwa kijana mzuri sana. Hata Ethan alikuwa hawezi kufananishwa naye.
Kwa kuongezea, familia ya Kileo ilikuwa imepanda juu zaidi ya miaka michache iliyopita. Ingekuwa nzuri ikiwa familia ya Jones Masawe ingeweza kuunganishwa nao kwa ndoa.

“Sawa. Wewe bado ni bikira katika familia yetu. Ni lazima uuteke moyo wa Steve.” Jones aliangua kicheko.

Siku iliyofuata, katika wodi ya watu mashuhuri kule hospitalini, naibu meneja mkuu wa Mawenzi Investiments alifika ana kwa ana akiwa na hundi mbili.
“Samahani sana, Bw. Kimaro. Lilikuwa kosa la mfanyakazi wetu. Hapa kuna fidia ya Bi Jones na wewe.

Lisa alipepesa macho baada ya kuona hundi yenye thamani ya shilingi milioni 30 mkononi mwake. Kisha akaitazama ile hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100 aliyokuwa nayo Alvin.
Damn, kuna pengo gani kubwa katika matibabu kati yao wote wawili. Ingawa hakuumia, alipatwa na kiwewe kikali na karibu kupoteza maisha yake. Alikuwa amekata tamaa kabisa.
Kilichozidi kumhuzunisha ni kwamba Alvin aliitupa tu hundi kwenye meza ya kitanda. “Sawa. Mnaweza kuondoka sasa hivi.”

"Bw. Kimaro, una nia ya kubadilishana kadi za biashara na mimi?" Naibu meneja mkuu alijaribu kuchukua fursa hiyo kufahamiana na wakili huyo mkubwa.

"Nimechoka, unaweza kwenda tu." Alvin alifumba macho bila subira.

Naibu meneja mkuu, ambaye aliheshimiwa sana kazini kwake alihisi uchungu. Mara akatoka nje akiwa na uso uliosinyaa.

Lisa alimfuata alipokuwa ametoka mlangoni. "Samahani. Majeraha ya Bw. Kimaro yamekuwa yakimuumiza sana siku hizi chache. Naomba kujua kuhusu mradi wa usanifu wa nyumba…”
“Mimi sihusiki na jukumu hilo. Unaweza kuwasiliana na mtu katika idara husika.” Naibu meneja mkuu aliondoka mara baada ya kumaliza kuzungumza. Hakuweza kujisumbua kuwasiliana na mbunifu yule masikini.

Lisa alikuwa mnyonge. Laiti isingekuwa kwa lengo la kupata pesa zaidi, asingeenda hatua ya ziada kwake. Aliporudi wodini, macho ya Alvin yakafumbuliwa na ndita zake usoni zilikuwa zimekunjamana. “Umerukwa na akili? Kwa nini bado unafikiria kuchukua mradi huo chini ya Mawenzi Investiments?"

'Ikiwa nitachukua mradi huo, nitapokea kamisheni yenye thamani ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Mawenzi Investiments. Ninaweza kupata angalau milioni 20 kutokana na ukarabati huo baadaye.”

Lisa alitazama hundi yake na kusema kwa huzuni, "Milioni 20 zinaweza kuonekana kuwa si kitu kwako, lakini ni kitu ambacho mtu wa kawaida hawezi kutengeneza maishani mwake."

"Je, umefungwa kwa pesa?" Alvin aliuliza kwa ujeuri. Kwa mshangao alimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka mezani. "Unaweza kuitumia."

Miguu ya Lisa karibu ikageuka kuwa laini kama mrenda. Ilikuwa imepita muda tangu alipoona pesa nyingi namna hiyo. Lakini hakuweza kuichukua. Akatikisa kichwa. “Ni pesa zako. Siwezi kuchukua.”

“Lisa.” Macho ya Alvin yalitiwa giza. Alionekana kukasirika. "Wewe ni mwanamke wangu, na ninakuruhusu kutumia pesa zangu."

"Nataka kupata pesa kwa uwezo wangu. Sitaki kuwa mwanamke ninayemtegemea mpenzi wangu.” Lisa aliendelea kushikamana na kanuni alizojiwekea. "Ikiwa ningetaka kupata pesa kupitia njia rahisi, ningeweza kupata mtu tajiri zaidi kuliko wewe kwa uzuri wangu, lakini mimi sio mtu wa aina hii. Ninaweza kuzeeka na uzuri ukapotea. Uwezo wa kweli pekee ndiyo utabaki.”

Baada ya kumaliza kuongea, aliguswa na maneno yake mwenyewe.
Bila shaka, Alvin angemwona kuwa mwanamke mwenye busara na heshima kubwa ambaye hakuchochewa na faida za kibinafsi. Mwanamke wa aina hii alitokea mara chache sana. Hakika ilikuwa ni nadra kumpata mwanamke yeyote mwenye tabia kama hiyo.

Lisa alinyanyua kichwa, ndipo alipogundua kuwa macho ya Alvin ya kejeli yalikuwa yakimtazama. "Unaweza kupata mwanaume tajiri kuliko mimi? Umeshiba sana. Ni nini kinakufanya ujiamini hivyo?” Maneno yake yalionekana kama kofi usoni kwa Lisa, jambo ambalo lilimfanya awe na hasira sana. Ilibidi akubali kwamba labda alikuwa mwanasheria mwenye uwezo zaidi linapokuja suala la kupata pesa. Baada ya kusema hivyo, daima kutakuwa na mtu bora zaidi yake huko nje. Kelvin alikuwa na uwezekano wa kuwa na makali juu yake katika suala hilo.
"Bw.Kimaro, usiwe na hila."

Alvin alikoroma. "Ni heshima kubwa kwako kukutana nami."

“Ndio, nina bahati kukutana nawe. Wewe ni nyota yangu ya bahati, mwokozi wangu.” Lisa hakutaka kubishana na mgonjwa.

Sura ya 94

Alipomaliza tu kuzungumza, Kelvin alimtumia ujumbe wa WhatsApp. [Nilisikia kutoka kwa Joseph kwamba kuna kitu kilikutokea ulipokuwa ukifanya kazi. Uko salama? Je, ninaweza kuja kukutembelea? Nina wasiwasi sana.]

Lisa alihema sana. Hakika, Kelvin alimtendea vyema kabisa. Ila cha kusikitisha, tayari hakukuwa na haja ya kulipiza kisasi kwa Ethan. Hivyo hakukuwa na haja ya yeye kuolewa na mjomba wa Ethan pia.

Akajibu, [Asante kwa wasiwasi wako. Niko sawa. Maendeleo ya ukarabati wa jumba lako hayataathiriwa.]

Kelvin: [Mradi wa jumba langu sio wa dharura. Kilicho muhimu zaidi ni kwamba uko salama.]

“Unachat na nani?” Alvin aliuliza kwa hasira.

“Pamela.” Lisa mara moja akaweka simu yake chini. Aliposema uwongo, hakuona haya, wala moyo wake haukuenda mbio.
“Nilifikiri ulikuwa unazungumza na Kelvin, Ethan, na kundi hilo la watu. Afadhali usiniruhusu kujua kuwa unawasiliana nao kupitia Whatsapp,” Alvin alionya.

"... Unawaza kupita kiasi."

Lisa alipata mshtuko, akishangaa kuona Alvin alikuwa na macho kama ya X-ray.
“Aha, njoo hapa. Majeraha yangu yanaanza kuuma tena.” Alvin alimtazama kwa hasira.
Lisa alikosa la kusema. Je, Alvin alikuwa anataka kumbusu tena.
***
Alvin aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya wiki moja. Lisa alikuwa akimuhudumia Alvin muda wote huo.

Joseph Ruta, bosi wake kazini, hakumlaumu. Baada ya yote, alikuwa karibu kupoteza maisha yake kwa sababu ya kazi. Aliuliza kwa upole, “Je, bado unapanga kuchukua mradi chini ya Mawenzi Investiments? Vinginevyo, nitateua mtu mwingine wa kuifanya."

“Ningependa kujaribu tena. Ikiwa nitashindwa, unaweza kuamuru mtu mwingine kuifanya."
Lisa hakuweza kuvumilia kuachia kamisheni hiyo nzito.
Wakati akiwa anafikiria namna ya kulishughulikia jambo hilo, ghafla bwana Frank akampigia simu. “Bi Jones, samahani kwa kilichotokea mapema. Nimejaribu kuwauliza wasimamizi kuhusu hilo katika siku chache zilizopita na wameomba radhi kuhusu hilo. Kwa hivyo, wameamua kupitisha mradi kuhusu muundo wa nyumba kwa Ruta Buildind Design & Construction.

Lisa alikuwa alihisi kana kwamba amesikia vibaya. Bila kujali, alihisi kwamba hatimaye angeweza kuona mwanga mwishoni mwa handaki.
"Lakini hatujazungumza juu yake ..." Lisa alisema.

"Ruta Buildind Design & Construction iko kila wakati. Kweli, ninahitaji uje na mpango wa kina wa muundo na ni wa haraka sana. Uongozi wa juu ungependa kuliangalia kesho yake.”
Lisa alichanganyikiwa. Mradi huo wa Mawenzi Investiments ulihitaji miundo kumi tofauti ya nyumba, ambayo alihitaji kuwasilisha kesho yake. Angewezaje kufanikisha? Baada ya kusitasita kwa muda, alitikisa kichwa kwa njia ya moja kwa moja. "Sawa, lakini tunahitaji kusaini mkataba kwanza."

"Njoo ofisini mchana na tutasaini basi."

Mchana wa siku hiyo, Lisa alielekea kwenye kituo cha mauzo tena. Alipaswa kusaini mkataba na Mawenzi Investiments bila kusubiri kwa muda mrefu. Aliporudi nyumbani usiku, aliandaa chakula cha jioni kwa ajili ya Alvin. Baada ya kumsaidia kuoga, alisema kwa wasiwasi, “Ninahitaji kutengeneza michoro ya kazi yangu usiku kwenye maktaba yako baadaye. Nenda kalale mapema uniache.”

Alvin alikunja uso. Ijapokuwa alifahamu umuhimu wa dhamira ya msichana huyo ya kujitutumua, lakini hakuipenda. Hata hivyo, alikuwa kimya kuhusu hilo. Hata hivyo, alipoendelea kukesha na asilale tena siku iliyofuata, alipandwa na hasira. “Lisa, una wazimu? Hukulala vizuri wakati ulilazimika kunihudumia hospitalini kabla ya hii. Sasa kwa kuwa uko nyumbani, hutalala tena. Unapanga kufa kwa mshtuko wa moyo?"

“Kazi itakamilika baada ya usiku wa leo, usiwaze.” Lisa alikunywa kahawa. Ndani kabisa, aliguswa kidogo na huruma ya Alvin.

Alvin alimuamuru kwa uthabiti, “Sijali. Rudi chumbani kwako na ulale sasa. Sio jambo kubwa ikiwa utakufa kwa kwa presha ya moyo. Jambo kuu ni kwamba hakuna mtu atakayenipikia. Ninakataa kutumia juhudi zangu kuchukua kesi yako bure."

Lisa alisikitika baadaya kugundua wasiwasi wake kwake ulikuwa ni udanganyifu tu.
Lisa aliuma mdomo wake kisha akasema kwa uchungu, “Usijali. Kwa kuwa nimekuahidi kukupikia, nitahakikisha sitakufa.”

“Je, huelewi? Ninautawala mwili na maisha yako. Huna nguvu tena juu ya maisha yako."
Bila kusita zaidi, Alvin akautumia ule mkono ambao haukujeruhiwa kumbeba kutoka kwenye kiti.
“Alvin…”
“Ikiwa unapanga kupinga, ni bora ufunge mdomo wako,” Alvin alimwonya kwa kukunja uso.

"Hapana. Nilitaka kukwambia uniweke chini. Naweza kurudi chumbani kwangu mwenyewe. Majeraha yako yatakuwa mabaya zaidi ikiwa utatumia mkono wako mwingine kunibeba hivi,” Lisa alijibu. Alipumua na kujisalimisha kwa hatima yake. Alvin aliridhika na jinsi Lisa alivyokuwa mtiifu na kumuelewa. Baada ya kumuacha, akaenda naye chumbani kwa ushirikiano.

Awali alipanga kuendelea na kazi yake baada ya Alvin kusinzia. Hata hivyo, mara tu alipokuwa kitandani, alizidiwa na usingizi sana hivi kwamba alilala fofofo.
Alfajiri na mapema, Alvin akiwa anatoka bafuni baada ya kupiga mswaki, alimuona mwanamke huyo akiwa amelala kama gogo kitandani. Alikuwa amepitiwa na usingizi mzito kiasi kwamba hata mate ya pembeni ya mdomo yalidondoka kwenye mto.

Alvin akampiga picha kwa siri. Angemuonyesha picha hiyo baadaye na kumfanya aaibike.
Aliweka picha kwa kuridhika. Baada ya hapo, aligeuka na kuelekea sebuleni karibu na chumba cha kulala. Kwa mkono mmoja tu, alifanikiwa kupekua neno la siri kwenye kompyuta ya Lisa ya mkononi kwa muda mfupi. Alibofya programu ya kubunia mchoro na kuona michoro kadhaa migumu ndani yake.

Akakodoa macho. Alitakiwa kuwasilisha michoro mingi ndani ya siku moja na nusu. Mawenzi Investiments alikuwa anajaribu kumpa wakati mgumu kwa makusudi?

Lisa alipoamka saa tatu asubuhi, alitazama muda na kupigwa na butwaa kabisa. Alikuwa tayari kachelewa sana. Mara moja akainuka na kukimbilia maktaba. Akawasha laptop yake kuendelea na michoro yake.Mara tu alipobofya kwenye programu, alipigwa na butwaa. Hapo awali, bado alikuwa na nyumba nne zaidi za kubuni rasimu. Jambo la kushangaza ni kwamba michoro yote ilikuwa imemalizika.

Michoro yake ilikuwa imekamilika?

Zaidi ya hayo, michoro ilifanyika vizuri sana. Dhana hizo zilikuwa za ajabu, na zililinganishwa na zake. Nini kimetokea? Je, alilala jana usiku? Au aliamka na kumalizia akiwa usingizini?
Je, alizimaliza lakini akapoteza kumbukumbu? Alijaribu awezavyo kukumbuka, lakini alikuwa na hakika kwamba hakumaliza michoro hiyo. Nani alimfanyia? Alishuka chini huku akionekana kupigwa na butwaa.

Katika chumba cha chakula, Alvin alikuwa amevaa nguo za kawaida za kijivu na akizungumza kwenye simu ambayo aliishika kwa mkono wake wa kushoto.

“Ndio. Agiza safari ya ndege ya mchana. Naenda Mbeya…”

Hadi simu inakatika, tayari Lisa alikuwa amekaa kwenye kiti kilichokuwa pembeni yake. sura ya mshangao kupita uso wake. "Bado unaendelea na safari ya kikazi katika hali hii?"
“Ndio kuna dharura imejitokeza." Kulikuwa na suala la mradi huko Mbeya ambao aliwekeza, kwa hivyo alipanga kwenda huko kutazama. “Nitakuwa huko kwa siku mbili. Afadhali uwe na tabia njema ndani ya nyumba ... "

“Najua, najua. Hakika sitakutana na Kelvin wala Ethan,” Lisa aliendelea na hotuba yake huku akiwa hana la kufanya.

“Unaweza kusema kitu tofauti? Nimechoshwa na maneno yako.” Kwa kuona aibu, Alvin alimkazia macho. Mwanamke huyo alizidi kupata ujasiri. Anathubutu vipi kumdhihaki.


Lisa aliuliza kwa udadisi, “Macho yako yana damu. Jana usiku hukulala vizuri? Ilikuwa ni kwa sababu….” Ghafla akabanwa na kikohozi.

Alvin alikasirika sana. Je, alikuwa akishuku kuwa aliamka alfajiri kumalizia michoro yake jana usiku? Hakutaka agundue kwamba alimfanyia hivyo.

Kwa usemi wa kupotezea, alisema haraka, "usielewe vibaya ...Samahani, nilipaliwa na mate. Najua labda ni kwa sababu majeraha yako yalikuwa yanauma jana usiku na hukuweza kulala tena. Ilikuwa ni kosa langu kwamba nililala kama gogo. Mbona hukuniamsha?” Lisa alijisikia hatia sana.

Sura ya 95

Uso wa Alvin uliganda bila kuonekana akizungumza kwa muda.

"Ulisema nini?" Lisa aliuliza.

Alvin alikoroma kwa namna ya kutania. "Nilitaka kukuuliza kwa nini hukupaliwa hadi kufa."

Lisa alishindwa cha kuongea huku akijiuliza kwanini mwanaume huyo aliongea kinyama namna ile. Kilichomtia shauku zaidi ni kile kilichotokea jana yake usiku. Kwa kuwa nyumba ilikuwa yake, alikuwa na uhakika wa kujua. “Jana usiku… Je, unajua ni nani aliingia kwenye chumba cha maktaba na kutumia kompyuta yangu? Kuna mtu alinimalizia michoro yangu.”

“Oh. Nilipata rafiki wa kukukamilishia jana usiku ili usife kwa mshtuko wa moyo. Vinginevyo, ningehitaji kutafuta mpishi mpya.” Alvin aliikunywa glasi ya maziwa aliyokuwa ameshika.

Lisa alipigwa na butwaa kabisa. Alikumbuka kwamba ilikuwa karibu saa sita usiku alipoenda kulala jana yake usiku. Hivi kweli aliweza kumpigia simu mtu wa kumsaidia usiku wote huo?
Ingawa siku zote alisema kwamba ni kwa sababu alitaka aendelee kumpikia chakula, je, ni kweli kwa kweli kwamba alimtendea hivyo kwasababu yeye ni mpishi tu?
Isitoshe, hata alijeruhiwa alipomwokoa kwenye eneo la ujenzi mara ya mwisho. Kichwa chake kilikaribia kupigwa na tofali, na karibu kupoteza maisha yake.
Moyo wake ulianza kudunda. Muda huo, alikasirishwa na maneno yake makali, lakini hisia tayari zilikuwa zimefutwa kwa muda mfupi.

Pengine alikuwa mtu ambaye alikuwa mgumu kwa nje lakini kwa ndani alikuwa laini.
Baada ya muda fulani, alisema, “Asante. Rafiki yako ni mzuri sana. Anafanya kazi wapi? Nikipokea kamisheni hiyo, nitagawana naye nusu yake.”

Sauti yake ya kiume iliyotoa dokezo la kejeli ilisikika, “Sahau kuhusu hilo. Yeye hajali kuhusu pesa.”

Lisa hakujali. "Sawa, nitampikia chakula kitamu kama ishara ya shukrani yangu basi ..."

“Huna sifa,” Alvin alikatiza sentensi yake huku akiwa amekunja uso. "Unaweza kunilaza tu ikiwa unataka."

“Sawa.” Lisa alijibu na kukaa kimya, hakuwa na la kusema zaidi.

Alvin alikodoa macho yake na kukunja midomo yake kwa utulivu. "Ngoja nikuonyeshe kitu." Alvin akabonyeza kufungua picha ya simu iliyokuwa kando yake na kumuonyesha. Lisa aliitazama. Papo hapo, mcho yake yakamtoka kana kwamba yanataka kufyatuka. Kweli alimpiga picha akiwa amezama usingizini? Ni mzaha ulioje!

Hakuweza kujisogeza kuitazama ile picha, akanyoosha mkono wake kwa lengo la kumpokonya simu. Alvin aliikwepesha simu yake mara moja kabla hajaipokonya. Lisa akakosa balance na baadaye akaanguka mikononi mwake. Kwa bahati mbaya, mkono wake wa kushoto ulitua kwenye sehemu isiyo ya kawaida ya mguu wake. Lisa alimsikia Alvin huku akihema kwa mshtuko. Kwa aibu kabisa, aligeuka na kutaka kukimbia lakini hakuweza. Mkono wa kulia wa Alvin ulikuwa umefungwa kiunoni mwake. Sauti ya kupumua kwake ilidumu masikioni mwake kimahaba. Sauti yake ya kiume ilikuwa ya kupendeza kama sauti iliyotolewa na zeze.

“Unajaribu kunitega asubuhi na mapema hii?”

“Umenielewa vibaya tu…” Kwa kuona haya, Lisa alipata shida kuinua kichwa chake. Macho yao yalipokutana, macho yake yalikuwa meusi kama sumaku. Hakuweza kuangalia pembeni.

Alvin alimtazama Lisa mikononi mwake ambaye uso wake wa aibu ulikuwa kama ua linalochipuka. Alihisi hamu ya kumbusu.
Kwa kweli alifanya hivyo.Alvin alikuwa akitumia kisingizio cha kupunguza maumivu kama njia ya kumpiga denda Lisa kila siku. Mara nyingi alimbusu usiku kama njia ya kumzuia kuhisi maumivu.

Kitendo hicho kilikuwa kimezoeleka kwa Lisa. Hata mwili wake ulionekana kuzoeana na busu hilo. Lakini alihisi moyo wake ukimwenda wazimu zaidi kuliko hapo awali. Busu lla muda huo ilikuja na ladha ya utamu pia.
Huko nyuma, mara nyingi alikasirishwa na jinsi Alvin alivyozungumza kwa ukali. Hata hivyo, alikuwa amemsaidia sana. Busu lilikatishwa kwa muungurumo wa tumbo lake.

Baada ya kuishiwa nguvu, Lisa kwa aibu alielekea jikoni kupata chakula. Alvin alitoa tabasamu alipokuwa akimtazama kwa nyuma.

Baada ya kifungua kinywa, Lisa aliwasiliana na Bwana Frank kumjulisha kuwa alikuwa amemaliza kuandaa michoro. Bwana Frank alijibu kwamba alikuwa ametoka kazini wakati wa mchana na akamwomba wakutane kwenye hoteli ya SleepWay alikokwenda kupata lunch. Kiongozi wake alikuwepo pia, ili waweze kujadili miundo hiyo pamoja. Lisa alikuwa akihudhuria aina hiyo ya mialiko mara nyingi wakati akikutana na wateja wake. Ingawa hakutaka kwenda, hatimaye alikubali kufanya hivyo.

Saa nane mchana, Lisa aligonga mlango wa chumba cha faragha kwenye hoteli hiyo ya nyota tano kabla ya kuusukuma. Chumba kilikuwa cha kifahari na kikubwa, kilicho na mapambo ya Magharibi.

Aliyemshangaza Lisa ni Lina. Alikuwa amevaa koti la manyoya na kuketi katikati ya kochi. Bwana Frank alisimama kando ya Lina na kummiminia mvinyo kwa uangalifu. Hapo hapo, Lisa alihisi kuwa kuna jambo haliko sawa. Aligeuka, akijaribu kuondoka. Hata hivyo, wanaume wawili wazito waliingia ndani na kumshika moja kwa moja. Michoro aliyokuwa ameshikilia ilianguka chini.

"Bwana. Frank, umekuwa ukinidanganya muda wote huu.” Lisa alionekana kufahamu kila kitu kwa wakati huo. Aliwatazama kwa hasira. “Nimeelewa sasa. Tukio la eneo la ujenzi lilikuwa ni mipango yenu nyote wawili, sivyo?
Bwana Frank alimtazama Lina kwa woga. Aligundua tu juu ya tukio hilo baadaye. Yeye alikuwa mwajiriwa tu, na kupata nafasi yake ya juu ndani ya kampuni ya Mawenzi Investiments alipata shida kubwa. Kwa hivyo, hakutaka kumuudhi Lina kwa ajili ya Lisa na kampuni ya yake, ambayo inaweza kutishia maisha yake ya baadaye.

“Una hisia za haraka, lakini kwa bahati mbaya…” Lina alimwendea kwa uzuri huku akiwa ameshikilia glasi ya mvinyo. Hakuwa tena maridadi na mwenye kujidai kama zamani. Badala yake, alikuwa amekuwa mtu wa hali ya juu na mwovu.

Lisa alijua kwamba hii ndiyo asili ya kweli ya Lina. Hata hivyo, Kibo Group ilikuwa imeuzwa, na sifa ya familia ya Jones Masawe ilikuwa imeharibiwa. Familia ya Masawe haikuzingatiwa kuwa familia tajiri tena. Kwa nini Lina bado alionekana ameridhika?

"Unashangaa kwa nini Bwana Frank angenisikiliza?" Lina alikibana kidevu cha Lisa huku akitabasamu. "Je, ulikuwa na hisia kwamba kesi hiyo ingeharibu hadhi ya familia ya Masawe? Kweli, umekosea. Ninaweza kufikia mambo makubwa zaidi bila Kibo Group.
"Unamaanisha nini?" Lisa alichanganyikiwa kabisa.

Bw. Frank alisema kwa uungwana, “Bi. Lina sasa ndiye meneja mkuu mpya wa majengo kwenye kampuni Mawenzi Investiments. Jones Masawe ndiye mwenyehisa nyingi zaidi katika Mawenzi Investiments, na pengine atakuwa mwenyekiti mpya wa bodi mwishoni mwa mwaka. Mawenzi Investiments inaweza kuwa ya Miss Lina katika siku zijazo."

“Hili haliwezekani. Lisa alishtuka sana. “Sijawahi kusikia kutoka kwa Baba na Mama kwamba tuna hisa nyingi sana Mawenzi Investiments.”

“Kwa nini baba na mama wakuambie hayo? Hata hawakupendi. Wewe ni mgeni tu.” Lina alimwambia, na kwa sauti nzito, Lina aliongeza kwa kejeli, “Hujawahi kushuku sababu ya kwanini Baba na Mama hawakupendi? Hata wanatamani kukuua?”
Macho ya Lisa yalimtoka. Aliinua kichwa chake na kumkazia macho Lina.

Kwa hali ya huruma, Lina alibofya ulimi wake. “Ni kwa sababu wewe si binti wa kuzaa wa Baba na Mama. Nilipochukuliwa kimakosa wakati huo, Baba alitambua kwamba Mama alikuwa ameshuka moyo. Kwa kuhofia kuwa angekufa kwa presha, akakuchukua wewe kutoka katika kituo cha watoto yatima. Kimsingi, wewe ni mtu ambaye wazazi wako wa kibiolojia walikutupa wakati wa kuzaliwa! Usingefanikiwa kile ulichonacho leo bila familia ya Jones Masawe. Lakini sio shukrani kwako kuwa na nia ya kulipiza kisasi kwetu. Ulisababisha hata James kuishia jela. Siku zote Baba na Mama husema kwamba kama wangelijua hili mapema, wasingethubutu kukuchukua wakati huo!”

TUKUTANE KURASA 96-100

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.......LISA
KURASA.....96-100

Sura ya 96

Maneno hayo yalionekana kama bomu lililosikika kando ya masikio ya Lisa.
Hata hivyo, Lisa alijikuta ametulia bila kutarajia.

Ukweli hatimaye ulimpata. Haikuwa ajabu Mama Masawe alimtendea kwa ukali zaidi na kwa ukatili tangu alipokuwa mdogo. Siku zote Lisa alidhani kwamba Mama Masawe alikuwa mama asiye na urafiki, lakini Lina aliporudi, aliona upande mwingine wa Mama Masawe. Kwa muda mrefu alikuwa ameshuku kuwa yeye ni yatima asiye na wazazi, lakini alikataa kuamini.
Ukweli uligeuka kuwa mbaya kuliko vile alivyofikiria. Familia yake ilimchukia sana na ikawa na wazo la kumtupa.

"Unajua kuwa nimekuchukia kila wakati?"Lina aligonga uso wake mdogo mzuri. "Niliteseka sana wakati wa kutekwa nyara, lakini vipi kuhusu wewe? Ulichukua nafasi yangu na kuishi kwa anasa. Hata wanaume wazuri kama Ethan walikufuata …”

"Lakini sasa, nimeachwa bila chochote, na sitaweza kunyakua tena vitu vyako." Lisa aligundua kuwa Lina hakuwa mnafiki tu bali pia alikuwa na mawazo potofu.

"Lakini umenidhalilisha tena na tena. Nilipoteza mchumba wangu, na zaidi ya hayo, Kibo Group imeuzwa. Unafikiri nitakuacha utoke kwenye ndoano?" Lina alidhihaki. Akatoa chupa ya dawa. "Unadhani Alvin bado atakusaidia hata baada ya kuangalia unaharibiwa na mwanaume mwingine? Unafikiri Kelvin na Ethan bado watakufuata?”

“Wewe ni mtu wa ajabu, Lina. Utapata malipo yako kwa hili.” Lisa alianza kumfokea Lina kwa maneno makali na kuhangaika kwa nguvu.Hata hivyo, wanaume wawili waliokuwa nyuma yake walimkamata kwa nguvu sana hivi kwamba hakuweza kusogea hata kidogo.

"Malipo?" Lina aliuliza bila kujali, "Mimi ni meneja wa Mawenzi Investiments na binti wa kwanza wa Jones Msawe. Nani anathubutu kunichokoza? Hata kama ni Alvin, nitamlipa kidogo kidogo."

Alipomaliza tu kuongea, akawakonyeza watu waliokuwa nyuma yake. Wakati huo, Lisa alihisi mdomo wake kufunguliwa kwa nguvu. Kimiminika kidogo baadaye kilimwagwa kinywani mwake.
Alikabwa vibaya sana hadi uso wake ukawa mwekundu. Alihisi kutapika, lakini alishindwa kufanya hivyo.

Lina alichukua michoro mmoja baada ya mwingine kutoka chini. Baada ya kuitazama, alicheka kwa dharau na kusema. "Miundo hii ni mizuri. Asante. Nitaikubali."

Lisa hakuridhika, alianza kumfokea. "Wewe ni mtu wa kudharauliwa. Nini kingine unaweza kufanya mbali na kunyakua vitu vya mtu mwingine?"

“Ndio. Nafurahia kunyakua vitu. Unaweza kufanya nini kuhusu hilo?”
Lina aliwakonyeza wale wanaume wawili na kuwaambia. “Kuwa na wakati mzuri naye. Ninyi watu lazima mumridhishe, sawa?" Kwa hayo, Lina akaondoka na bwana Frank.

Baada ya kuutazama mlango uliokuwa ukifungwa, Lisa alihisi mwili wake unawaka ghafla.

Hapo awali, alimnywesha Alvin dawa kama hiyo. Lakini, hakuweza kuelewa kabisa maumivu yake wakati huo. Sasa, aliyaelewa kabisa.

Wanaume hao walimwendea huku wakisugua mikono yao. Wanaume hao walikuwa ni mabaunsa waliokuwa wakitumika kama walinzi wa baadhi ya matajiri. Walisikia jina la Lisa na hata walikutana naye hapo awali. Ingawa walikuwa walinzi tu, hawakuweza kumtamani Lisa, mwanamke mrembo zaidi kutoka katika familia tajiri maarufu. Hawakutarajia kwamba wangepewa nafasi hiyo, walichanganyikiwa sana!

“Usinikaribie.” Lisa alijikongoja kurudi nyuma kwa hofu. Akatoa simu yake kumpigia Alvin. Hata hivyo, alipoitoa, jamaa mmoja aliwahi kumpokonya simu na kuitupa kando.

“Huoni kinachoendelea? Hakuna mtu atakayeweza kukuokoa.” Mmoja wa watu hao alijitupa mikononi mwake kwanza.

***
Kelvin Mushi alikuwa anaenda kuhudhuria shughuli ya kijamii pamoja na msaidizi wake ndani ya hoteli hiyohiyo. Akiwa kwenye ngazi, alitokea kumwona Lina na mwanamume wa makamo wakitoka kwenye chumba cha faragha na kuelekea kwenye lifti. Mzee yule wa makamo akabonyeza kitufe cha lifti kwa Lina kwa ustaarabu. Hata alimruhusu aingie kwenye lifti kwanza, akifanya kama mtumishi.

Msaidizi wa Kelvin aliuliza kwa udadisi, “Huyu si Bwana Frank Gumbo, meneja wa idara ya mipango ya Mawenzi Investiments? Inashangaza kumuona akiwa mnyenyekevu sana kwa mwanamke huyo.”

Kelvin alikodoa macho. Aliweza kumtambua Lina mara baada ya kumwona tu Kwa kuzingatia kwamba kampuni ya Kibo Group ilikuwa umeanguka kutoka kwenye ulimwengu wa biashara, kwa nini mtu kutoka Mawenzi Investiments amtendee kwa adabu hivyo?

Ikamwingia akilini kuwa Joseph alimwambia kwamba Lisa alikuwa anashughulika na mtu kutoka Mawenzi Investiments hivi karibuni. Inavyoonekana, alikuwa akijaribu kuchukua mradi kuhusu tenda ya kutengeneza muundo wa nyumba za kampuni hiyo. Akiwaza hayo, alihisi kuna kitu kibaya kilikuwa kinaendelea.

Lina alikuwa mtu mbaya sana. Labda angemlenga Lisa, haswa baada ya Kibo Broup kuanguka kutoka katika miliki yao. Bila kusita sana, Kelvin alielekea kwenye chumba cha faragha ambacho Lina alitoka. Akageuza kitasa cha mlango, na kugundua kuwa chumba kilikuwa kimefungwa. Akiwa amesimama karibu na mlango, alisikia kelele za mwanamke.
Alikuwa ni Lisa.
Alinyanyua kiti kwenye korido na kuufungua mlango kwa nguvu.
Dakika alipoingia ndani, aliona wanaume wawili wakimkandamiza Lisa chini kila upande. Shati lake lilikuwa limechanwa vipande vipande. Akiwa amekunja uso, aliendelea kuhangaika kwa nguvu.

"Wewe ni nani?" Maneno ya walinzi wawili yalibadilika. Kelvin alikimbia kuelekea kwao na kuwapiga chini. Baada ya kugundua kuwa mambo hayakuwa sawa, wanaume hao walichukua nafasi hiyo kukimbia.

Kelvin hakuwa na wakati wa kuwakamata. Hapo hapo akamkimbilia Lisa na kumbeba.
Huku harufu ya kiume ikimtoka, Lisa alijitupa mikononi mwake bila kujizuia.
Msaidizi wa Kelvin aliingia chumbani na kuliona tukio hilo. Kwa aibu, mara moja akafunga mlango na kuondoka.

Kelvin alikuwa na wasiwasi. Ingawa alijua kwamba Lisa alikuwa amekula kitu kisichopendeza, hakutaka kujinufaisha naye wakati huo. Akamsukuma kwa nguvu na kumwambia. “Amka Lisa. Ngoja nikupeleke hospitali, sawa?”

"Hapana." Meno ya Lisa yaligongana. "Najisikia vibaya sana." Mwili wake ulitoa harufu ya kipekee, yenye kupendeza.
Papo hapo, matukio mengi kutoka walipokutana mara ya kwanza yalijitokeza katika akili ya Kelvin. Kwa muda mrefu alikuwa amempenda Lisa. Hata hivyo, siku zote alikuwa amejiweka mbali naye, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kumkaribia. Alikuwa tayari kuwa naye milele ikiwezekana. Hiyo ilikuwa nafasi. Alikiri kwamba nia yake ya binafsi ilikuwa imeshinda tabia yake ya kiungwana wakati huo.

“Lisa niruhusu nikuoe. Nitawajibika kwa matendo yangu.” Kelvin alipomaliza tu kuongea alimbeba mpaka kwenye kochi na kumbusu midomo yake.

Lisa alimkumbatia kwa nguvu. Wakati huo, simu iliyokuwa sakafuni iliita ghafla.

Kusikia mlio wa simu, sauti ya Alvin ilipita kichwani mwa Lisa. Akiwa amepigwa na wazo hilo, akajaribu kupata fahamu na kumsukuma Kelvin. Kisha akajigonga na kwenye kifundo cha mkono, akatoa damu.

“Lisa…” Kelvin aliumia moyoni.

"Hapana. Hatuwezi kufanya hivi.” Lisa akatingisha kichwa kwa huzuni. “Tafadhali nipeleke bafuni.”

“Samahani.” Kelvin hakutarajia kwamba angepata fahamu zake tena. Alifadhaika, lakini hatimaye aliheshimu uamuzi wake na kumpeleka bafuni. Baada ya kuwekwa kwenye beseni la kuogea, mara Lisa akafungua bomba. Alijimwagilia maji baridi, na kujisikia nafuu kidogo.

Simu iliyoachwa chumbani iliita tena. Aliamini kuwa ni Alvin ndiye aliyekuwa akimpigia simu. Ikiwa hangepokea simu, bila shaka angeshuku kwamba alikuwa amemsaliti tena.
"Bwana. Mushi, naomba unipitishie simu yangu,” Lisa alisema huku midomo ikimtetemeka.
“Sawa.”

Sura ya 97

Kelvin alipotoka bafuni na kuchukua simu kutoka kwenye zulia, taarifa ilionyesha simu iliyokuwa ikiingia ilitoka kwa Alvin. “Alvin? Kwa nini amempigia simu Lisa?” Wakati huo mawazo na mashaka mengi yalipita kichwani mwa Kelvin. Hatimaye akainyanyua ile simu na kumpasia Lisa huku akiizuia dhiki yake.

Lisa akabonyeza kitufe cha kujibu na kuiweka simu sikioni. Sauti ya Alvin iliyobeba chembe ya kero ilisikika mara moja. “Nimekupigia simu mara tatu, Lisa. Ikiwa hukujibu simu yangu wakati huu, nilikuwa tayari kupiga simu polisi.”

Akiwa amelowa maji, Lisa aliyabana mapaja yake kwa nguvu ili kujisitiri. "HHuko umefika mbali sana."

"Ninajua vizuri jinsi ulivyo hatarini," Alvin alisema kwa mshtuko, "Unaweza kunaswa kwa urahisi mara tu unapoacha tahadhari yako."
Machozi yakaanza kumtoka Lisa. Hakika, alikuwa amenaswa katika mtego na alikuwa karibu kuharibiwa, lakini hakutaka kumjulisha hili. Kwanza, ni kwa sababu hakutaka aharakishe kurudi kutoka Mbeya. Sababu nyingine ni kwamba hakutaka ahusishwe na Mawenzi Investiments. Bila kujali uzuri wake, Mawenzi Investiments ilikuwa miongoni mwa makampuni ya juu ya Kitanzania. Hakuweza kumudu kuichokoza kampuni.

“Mimi… Pm sawa. Nilikuwa tu naongea na Pamela. Simu yangu ilikuwa kwenye mkoba wangu… kwa hivyo sikuisikia.”

"Nini kilichotokea kwa sauti yako, Lisa?" Alvin aliuliza kwa kukereka, “Kwa sauti yako ya kishindo, nitafikiri kwamba unajaribu kunitongoza.”

Lisa ambaye jasho lilikuwa likimtoka, alijaribu kuzuia hisia zake na kusema kwa sauti ya utulivu, "Inawezekanaje? Nitakata simu sasa. Nataka kununua nguo.”

"Afadhali urudi nyumbani mapema."

"Ndio ndio." Lisa alikata simu na kuitupa pembeni simu yake kwa haraka. Baada ya hapo, mara akainuka kutoka kwenye maji.

Huku akicheka, alisema, “Bw. Mushi, tafadhali unaweza kwenda nje kwanza?"

“Hakika. Nijulishe ikiwa unahitaji chochote." Kelvin aliitazama simu pale sakafuni kwa hisia tofauti kabla hajageuka na kutoka nje. Akili yake ilijawa na mazungumzo kati ya Lisa na Alvin hapo awali. Kwanini Lisa alichagua kumdanganya Alvin? Uhusiano wao ulikuwaje? Kelvin aliwasha sigara na kukaa nje hadi asubuhi iliyofuata.

Saa moja asubuhi, Lisa alitoka bafuni huku akitetemeka. Alivaa shati ambalo msaidizi wa Kelvin alinunua jana yake usiku.

"Ngoja nikupeleke hospitali," Kelvin alisema kwa wasiwasi.

“Hapana, ni sawa. Nataka kwenda nyumbani nikapumzike.” Lisa alihisi uchovu na usingizi wakati huo.

“Nitakurudisha nyumbani basi,” Kelvin alisema kwa kubembeleza, “Usikatae ombi langu. Huwezi kuendesha gari katika hali hii.”

Baada ya kusita kwa muda, Lisa aliitikia kwa kichwa. Akiwa njiani kuelekea nyumbani, Kelvin alimtazama kwa wasiwasi. "Kuhusu jana usiku ..."

"Jones Masawe sasa ndiye mwanahisa mkubwa zaidi katika Mawenzi Investiments, na atagombea nafasi ya mwenyekiti mwezi ujao. Nadhani kuna uwezekano mkubwa atashinda. Ikiwa ndivyo, ninahofia Lina atafanya ujinga mwingine wa kinidhamu katika Mawenzi Investiments.” Lisa alifunua yote.

Kelvin alipigwa na butwaa kwa kiasi fulani. "Tangu lini familia ya Jones ikawa na uhusiano na Mawenzi Investiments?”.

'Mimi pia sijui." Lisa alikunja uso, akiona kilikuwa kitu cha kushangaza. " mimi ni binti wa kufikia tu. Haishangazi kwamba hawakuniambia kuhusu mambo fulani.”

Kelvin alimwonea huruma. “Unataka nikuchunguze historia yako…”

“Hakuna haja ya hilo kwani sipendi kujua. Kwa vile wamenitupa, ina maana kwamba sihitajiki. Hakuna maana katika kuchunguza historia hiyo yenye uchungu.” Lisa akatikisa kichwa na kusema kwa kutoridhika, “Nahisi maisha hayana usawa. Kwa nini watu kama familia ya Jones wanaweza kubadilisha mambo na kupata mafanikio makubwa kwa urahisi hivyo? Kwa hilo, wanaendelea kufanya mambo maovu.” Mbele ya biashara kubwa kama Mawenzi Investiments, alijua wazi kuwa hakuwa na uwezo wa kuwapinga.

Kelvin alisita kwa muda, kisha akasema kwa ghafla, “Ninaweza kukusaidia ikiwa unakubali—”

"Hakuna haja," Lisa alikatiza sentensi yake.

“Lisa kila nilichosema jana usiku ni kweli. Nataka kukuoa,” Kelvin aliongeza kwa dhati, ‘Ninamchukulia adui yako kama adui yangu.”

Lisa akatikisa kichwa mara moja. Aliolewa na Alvin kwa ajili ya kulipiza kisasi, na akajuta. Hakutaka kurudia kosa. Akiwa ameshika usukani, Kelvin alisema kwa unyonge, “Kama ni Alvin angekuwa amekuambia hivi badala yake, je, ungekubali?”

Sura ya mshangao ikaangaza machoni mwa Lisa. Aliinua kichwa chake na kugundua mawazo ya Kelvin mara moja. Pengine Kelvin alikuwa amesikia jinsi alivyojibu simu ya Alvin mapema.

Kwa akili yake ya haraka, Kelvin alikuwa kishagundua kitui. "Nyinyi wawili mmefahamiana tangu zamani, sivyo? Nilipaswa kujua hili mapema. Alvin ni mtu mwenye kiburi ambaye asingeweza kukubali tu kuchukua kesi yako kirahisirahisi. Huna pesa wala mamlaka, kwa nini akusaidie kwa urahisi hivyo?”

Lisa aliuma mdomo bila kuongea chochote. Kwa kuwa Kelvin alikuwa ameshtukia, hakuona haja ya kueleza zaidi bila kujali alikuwa anamuonaje. Baada ya yote, uhusiano wake na Alvin haukuwa umeendelea hadi hatua ya mwisho. Hata hivyo, alipotia saini mkataba hapo awali, alikuwa amejizatiti kuuza mwili wake.

Ukimya wake ulichukuliwa kama jibu la ndiyo na Kelvin. Moyo wa Kelvin ulimuuma, akalazimisha tabasamu. "Ninajilaumu tu kwa kutokuwa na uwezo wa kukuokoa."
"Hapana. Niko sawa kwa sasa.” Kusema ukweli, Lisa angependelea Alvin kuliko Kelvin. Labda ni kwa sababu alikuwa ameolewa na Alvin.

“Unampenda?” Kelvin alimkazia macho ghafla. Lisa alikuwa ameduwaa kwa muda. Alikwepa macho yake kwa mshangao. Kelvin alisema kwa upole, “Lisa, natumai mnaishi kwa furaha. Hata unapokuwa na mtu mwingine, maisha yako yanapaswa kujazwa na mwanga wa jua na baraka. Wakati huo huo, nyote wawili mnapaswa kuwa na uhuru sawa. Mmoja hapaswi kunaswa na mwingine. Ukitaka kuondoka kwake siku zijazo, hakika nitakusaidia.”

"Asante." Lisa alionekana kuguswa. Kelvin hakumdhihaki au kumdharau, na pia alikuwa mvumilivu sana kwake. Ikiwa angekutana naye mapema bila kutokuelewana, labda angempenda mtu huyu mpole na mzuri.

“Kama unanithamini sana, acha kuniita Bwana Mushi basi. Nina umri wa miaka michache tu zaidi yako. Niite tu 'Kelvin'. Ikiwa Alvin atakuonea siku zijazo, unaweza kuniomba msaada wakati wowote.” Kwa kukonyeza macho, Kelvin aliendelea kusema kwa mzaha, “Usikatae ofa yangu, la sivyo nitahisi kufedheheshwa.”

Lisa hakuwa na la kufanya zaidi ya kutikisa kichwa. Kwa tabasamu alisema, “Sawa, Kelvin.”
Alifurahi kwamba mambo yalikuwa hivi. Bado angehitaji kukutana na Kelvin mara kwa mara kuhusu mradi wa ukarabati. Kwa kuwa mambo yalikuwa hivi, uhusiano wao haungekuwa mbaya sana.

Dakika 40 baadaye, Lisa alishuka kwenye gari mbele ya Jumba la Alvin. Kisha akaingia ndani.
Shangazi Linda alikuwa ametoka kwenda kuchukua mboga. Lisa alijikunja chini ya blanketi ili apate usingizi mzuri.

Saa sita mchana, Aunty Linda alimwamsha ili kula chakula cha mchana. “Ulipokosa kurudi jana usiku mzima, Bw. Kimaro alikuwa na wasiwasi kuhusu wewe. Aliendelea kunipigia simu usiku wa manane. Kwa kuzingatia kwamba tayari wewe ni mtu mzima katika miaka yako ya 20, hakuwa na wasiwasi sana juu yako.” Kwa tabasamu, Aunty Linda aliongeza, “Wanasema mwanamume anayeoa mwanamke asiyefaa atatumika kama mama na mhudumu. Mwanamke akiolewa na mwanaume sahihi, atabembelezwa kama mtoto na mwanamume. Hakika, Bw. Alvin anakutukuza kama mtoto na kukuchukulia kama kipenzi chake.”

Sura ya 98

Hapo awali Lisa alihisi kusinzia kidogo. Hata hivyo, baada ya kusikia maneno ya Aunty Linda, alishikwa na butwaa. Hakuweza kujizuia kuamini kwamba alikuwa kipenzi cha Alvin. Kujua kwamba mtu fulani alikuwa na wasiwasi juu yake kulimfanya ahisi joto kidogo.

Shangazi Linda alikumbusha, “Wakati ujao, afadhali umjulishe Bw. Kimaro ikiwa hutarudi. Wanaume huwa na mawazo kupita kiasi.”
“Sawa.” Lisa aliitikia kwa hisia tofauti. Ikizingatiwa kwamba alikuwa karibu kuingia kwenye mtego wa Lina jana yake, alihitaji kukaa macho kila wakati. Asingekuwa na bahati kila wakati kwa kuwa na mtu wa kumuokoa. Ilimsikitisha sana alipokumbuka kwamba alipoteza michoro yake ambayo Alvin alikuwa amemsaidia kuimalizia kuichora usiku wa manane. Mtu huyo alikuwa na kipaji hakika.

“Aunty Linda, umemuona mtu akitoka kwenye chumba cha maktaba jana asubuhi? Je, mtu huyo alikuwa mwanamume au mwanamke? Alionekana ana umri gani?” Lisa alidhani kwamba mtu mwenye kipaji aliyemaliza michoro yake alikuwa amekesha usiku wa manane na kuondoka tu asubuhi.

Shangazi Linda aliona ajabu. "Hakuna mtu aliyekuja jana. Nilipoamka saa kumi na mbili asubuhi, nilimwona Bw. Kimaro akitoka nje ya chumba chako.”

“Ina maana hukusikia sauti ya gari ikiingia au kutoka ndani ya geti?”

“Hapana kabisa. Kwa kuzingatia uzee wangu, mimi huwa na usingizi duni. Ningekuwa wa kwanza kusikia kama kuna mtu amekuja." Shangazi Linda akatikisa kichwa moja kwa moja.

Lisa alipigwa na butwaa kabisa. Ikiwa hakuna mtu aliyekuja usiku wa manane jana yake, mtu aliyefanya michoro hiyo alipaswa kuwa Alvin. Baada ya kusema hivyo, alishangaa Alvin angewezaje kujua jinsi ya kubuni? Ujuzi wake wa kubuni ulikuwa mzuri sana!
Zaidi ya hayo, wakati huo aliweza tu kutumia mkono wake wa kushoto. Mkono wake wa kulia ulikuwa majeruhi, hivyo hakuweza kula vizuri na hata alihitaji kumlisha. Naam, bila shaka, alikuwa amedanganywa!. Hakujua kuwa mwanamume huyu… alikuwa hodari katika kuigiza!

“Kuna nini madam?” Shangazi Linda alishangaa kumuona Lisa akiwa amekunja uso dakika moja na kucheka dakika iliyofuata. Aunty Linda akabaki anamshangaa tu, kuweza kujua ni nini kilikuwa kikiendelea akilini mwa mwanadada huyo.

Baada ya chakula, Lisa alirudi chumbani kwake akajitupa kitandani na kulala. Hakujua ni muda gani alikuwa amelala, hatimaye alifumbua macho kwa kuduwaa. Ghafla, aliona umbo refu limekaa pembeni yake.
Mwanamume huyo alikuwa amevalia nguo nyeusi ya juu, ambayo ilielezea umbo lake kamili. Alimtazama kwa uso wake mzuri na macho ya kina, meusi ya kupendeza.
Akiwa amechanganyikiwa, Lisa alipepesa macho yake mazuri. Alihisi kama ndoto. Alikuwa anaota kuhusu Alvin? Alipoona ujinga wake, mwanamume huyo alinyoosha mkono wake na kubana pua yake.

"Inauma." Lisa mara moja akaketi na kuachia mwayo. Ncha ya pua yake nzuri, yenye kupendeza, ikawa nyekundu, huku macho yake yakiogelea kwa machozi yaliyofanana na umande wa asubuhi unaometameta.

Macho ya Alvin yalitfifia kidogo. “Ulienda wapi jana usiku?”

“Si ulitakiwa kurudi kesho tu?” Lisa alikuwa ameduwaa.

“Nataka kujua ulikoenda jana usiku,” Alvin alirudia kwa sauti ya chini. “Lisa, vipi? Nimeondoka kwa usiku mmoja tu na tayari ulikuwa umelala mahali pengine.”

Akitazama msururu wa hisia zilizosonga kwenye uso mzuri wa mwanamume huyo kama dhoruba, Lisa alirudi nyuma kwa woga."Unafikiria nini tena juu yangu?"

Mwili wa Alvin ulisisimka kabla ya kujibu kwa hasira, “Kama isingekuwa mimi kukuokoa tena hapo awali, unafikiri bado ungeweza kulala hapa kitandani muda huu? Na sasa hivi unaniuliza eti nafikiria nini juu yako!”

Lisa aliinamisha kichwa chake na kujibu. "Nilienda shopping na Pamela jana usiku. Baada ya hapo, tulikula chakula cha jioni na kwenda kwenye muziki kidogo. Kwa kuwa tulikuwa tumechoka, tulilala hotelini na tukarudi nyumbani asubuhi baada ya kuamka.”

"Una uhakika hausemi uwongo?" Alikaza macho yake hatari.

"Sikufanya chochote kibaya." Alimwangalia kwa hurma. “Nilikuwa na mfadhaiko tu wa akili kutokana na mawazo. Tazama, nina umri wa miaka 24 tu lakini tangu umenioa ni matatizo tu yameniandama. Sijatoka kujichangamsha hata chakula cha jioni. Mimi huja nyumbani mara baada ya kazi kila jioni ili kuandaa chakula chako cha jioni. Nitazeeka mapema bwana! Bora siku moja moja natoka kuchangamsha akili.”

Alvin aliibuka kwa uso wenye hasira. "Je, unalalamika kwamba maisha yako hayana raha?"

“Hapana, hata kidogo,” alijibu mara moja, “Lakini ni muhimu kuwa na wakati wa burudani. Kwa nini usijaribu kumuuliza Sam?”

"Kwani ni lazima nimuulize Sam? Unafikiri anakufahamu vizuri?” Akamtupia jicho kali.

“Sio hivyo. Ninahisi tu kwamba yeye ndiye aina ya wanaume wanaopenda starehe.” Alitikisa kichwa kwa ukali kama kifaranga anayezama kwenye maji. "Lakini wewe ni mume unayejali kazi muda wote. Angalia mtindo wako wa kuishi, kazini-nyumbani, nyumbani-kazini. Wewe ndiye kielelezo kamili cha mwanamume mkamilifu, ukiweka na kipengele cha kunitoa out mara moja moja utakuwa umenimaliza kabisaa!”

“Hivi ndivyo unavyofikiri kweli?” Akainama mbele taratibu. Uso wake wa kupendeza ulikaribia macho yake. Aliweza kuhisi moyo wake ukidunda chini ya macho yake makali.

Kwa kutikisa kichwa, Lisa akajibu kwa uthibitisho, "Sijawahi kusema chochote cha uwongo."

"Kumbuka, hii haipaswi kutokea tena." Alivin alimuonya Lisa huku akibana mashavu yake.

“Kwa nini umerudi nyumbani ghafla? Si ulitakiwa kurudi kesho?” Lisa aliuliza ili kumpotezea.

“ Nimerudi nyumbani kwa sababu kazi ilikamilika mapema kuliko ilivyotarajiwa,” alijibu huku akigeuza uso wake.

Lisa akauliza kwa utani. "Ulikuwa na wasiwasi juu yangu?".

"Endelea kuota.” Alvin alijibu harakaharaka.

Lisa angeamini hivyo siku za nyuma lakini alikuja kugundua kuwa Alvin alikuwa na tabia ya kusema kinyume na mawazo yake. Alihamisha mada na kumuuliza swali jingine. "Ni wewe uliyenisaidia kumalizia michoro?"

Lisa alikuwa akichezea kifua cha Alvin. Alihisi mwili wake unasisimka. Midomo ya Alvin ilitetemeka kidogo. Tayari alijua jibu. “Asante kwa kunisaidia, najua unanipenda sana ila basi tu.”

"Lisa, usisahau wewe ni nani." Akamkazia macho kwa uso ulionyooka.

Lisa akajibu kwa tabasamu kubwa usoni. "Nakumbuka jukumu langu katika uhusiano huu. Kwa kawaida, mtu tajiri angempa mpenzi wake pesa na asijihusishe na maisha yake ya kibinafsi. Lakini, sio tu kuwa unafuatilia nilipo 24/7, lakini pia unahatarisha kila kitu ili kuniokoa ninapokuwa hatarini. Isitoshe, unanipa mkono kwa siri kazini wakati mambo yananizidi kidogo. Mbali na hilo, mkono wako wa kushoto unafanya kazi vizuri kabisa. Lakini bado unataka nikulishe.

“Sasa nisipokufuatilia nikuache ufe huko nje nani atanipikia hapa? Umesahau mkataba wetu? Hiyo inaonyesha una hatia.”

Lisa alimtazama machoni kwa umakini. "Alvlisa, ni ngumu kukukubali kama mimi? Nakupenda pia. Ni sawa kama hunipendi. Sitakuuliza tena. Naondoka kwenda bafuni.” Kisha, akatoka kitandani na kuvaa slippers zake.

"Lisa Jones, niambie, wewe ni mtoto mdogo uliyetumwa na Mungu kunitesa?" Akionekana kukasirika kidogo, akamvutia mikononi mwake. "Huna nguvu zozote bora zaidi ya ustadi wako wa kupika, sembuse unaonekana kuwa kivutio cha kila aina ya shida. Nina bahati mbaya sana.”

Sekunde chache baadaye, Lisa aliinamisha kichwa chake ili kubusu mdomo wake.

Sasa kwa kuwa wote wawili walijua hisia za kila mmoja, hakuhisi tena haja ya kuwa mwangalifu karibu naye. Alvin, ambaye alikerwa sana na busu hilo, nusura ashindwe kujizuia. “Haya, nenda, niache nipumzike. Nimechoka."

“Sawa.”

Sura ya 99

Siku iliyofuata, baada ya kifungua kinywa, Alvin alikuwa akijitayarisha kwa ajili ya kazi.
Ghafla, Lisa akamshika mkono. “Sijisikii kuendesha gari leo. Unaweza kunipa usafiri?”
Alivin akakunja uso. Mahali alipokuwa akielekea siku hiyo palikuwa kinyume kabisa na sehemu yake ya kazi. Mbali na hilo, alikuwa na mkutano ukimngoja kazini asubuhi ya siku hiyo.
Kwa kweli Lisa alitaka tu kujidekeza kwa Alvin.

"Lakini unayo gari."

"Nataka kutumia muda zaidi na wewe kwenye gari." Alimkonyeza kwa kutania.

Alivin akamtupia jicho kana kwamba anahisi kuudhika. “Twende zetu.”
Furaha ilijaa moyoni mwake.

Mkono wa Alvin ulijeruhiwa, kwa hivyo Hans alikuwa akimwendesha. Foleni ya magari asubuhi hiyo ilikuwa ya kutisha. Haikumsumbua Hans sana, ingawa. Alionekana mtulivu kumfananisha na Alvin ambaye alikuwa ametawaliwa na sura ya wasiwasi.
Alimsugua Lisa taratibu katikati ya paji la uso, akihisi kujuta kidogo kwa kukubali kumpeleka kazini kwake. Angemkodishia teksi au uber ikiwa angejua.

“Usiwe na papara.” Lisa aliweka kiganja chake cha kushoto nyuma ya shingo yake. "Foleni ndefu inamaanisha tunaweza kutumia wakati mwingi pamoja."

Alvin alikodoa macho na kuitazama saa yake. Lisa aliweza kuona tafakari yake machoni pake, akakisogeza taratibu kichwa chake na midomo yao ikakutana pamoja. Ghafla, mfadhaiko wa moyo wake ukatoweka. Uso wa Alvin uliokuwa umekunjamana hatimaye ukalainika na kulegea. Alikoroma na kutazama pembeni, lakini mdomo wake ulijikunja juu kwa unyonge. “Kwa kweli sijui nikufanyie nini.” Kiburi kilionekana katika sauti yake.

Vidole vya Hans vilitetemeka kwenye usukani. Hakuwa na wazo kwamba Alvin aliyezoea kumwona mgumu na asiyejali kabisa kuhusu mapenzi angefanya vile kwenye uhusiano wake na Lisa. Ilionekana pia kuwa uhusiano kati ya wawili hawa ulikuwa umeboreka sana.
Alijihisi kama mtu wa pembeni asiyehitajika katika hali ileakatamani safari iishe haraka.
***
Saa tatu kasorobo asubuhi gari likafunga breki mbele ya ofisi za Ruta Buildind Design & Construction Company.

Lisa alikuwa anataka kufungua mlango ghafla Alvin alihoji, “Si ulisema jana usiku ulienda kufanya manunuzi? Mbona hujavaa nguo mpya ulizonunua?”

Alitengeneza kisingizio papo hapo. "Hakuna kitu kilichonivutia macho yangu. Zile nguo ninazopenda zilikuwa za bei sana.”

"Hmm, unanishawishi kijanja kwamba nikununulie nguo zaidi?" Aliinua macho yake, akimtania.
Lisa alipiga kelele za furaha ndani kwa ndani, wakati akimjibu. “Sikuwa…”

“Sawa, nitakupeleka shopping baada ya kazi,” Alvin akakatiza. Hakuwa na nafasi nyingine ya kusema kwani gari liliondoka kwa kasi baada ya yeye kushuka. Lisa akaelekea ofisini.

Alipokaribia mlango wa kuingilia, Ethan alitokea mbele yake, akionekana kuchoka na kulegea. Shinikizo kutoka kwa familia ya Lowe na mapenzi yake ya kibinafsi yalikuwa magumu sana kwake. Sambamba na makapi yaliyokuwa kwenye midomo yake, alionekana pia amekata tamaa na mwenye huzuni.

Kuonekana kwake kulimshangaza Lisa. Karibu hakumtambua mtu huyo. “Mbona upo hapa tena?” Hakutarajia kumuona tena Ethan baada ya Alvin kumshambulia bila huruma siku ile anatoka kwenye msiba wa bibi yake. Alidhani asingethubutu kumtafuta tena baada ya hapo.
Akiwa ameinamisha kichwa chini, Ethan akachukuaa kadi ya benki mkononi mwake. "Kuna milioni mia tano humu. Mpe Alvin. Fikiria kama malipo yake ya uwakili anayokudai na uachane naye kabisabaada ya hili.”

Lisa alishtuka kweli!

Ethan aliendelea, “Nimeuliza kote na nina uhakika shilingi milioni 500 ni zaidi ya anazokudai. Lisa sitaki kukuona ukijishusha kwa kiwango hicho. Nilikukatisha tamaa siku za nyuma kwa kushindwa kukulinda lakini nitafanya vyema kuanzia leo.”

Alikuwa akihangaika kurudisha uhusiano wake na Lisa. Ingawa alijua kunaweza kuwa na uwezekano kwamba Lisa hakuwa bikra tena, alijua sio kosa lake. Baada ya yote, yeye mwenyewe alikuwa na lawama.

Sura ya kutatanisha ilimulika usoni mwa Lisa aliporudisha kadi. "Sitakukubali."

Lisa…” Aijibu bila subira, “Je, unataka kukaa karibu na Alvin milele? Hata wewe humpendi. Zaidi ya hayo, fikiria jinsi alivyokutazama siku ile. Hata hakuheshimu. Mwanamume huyo anakufikiria wewe kama bidhaa tu ambayo anaweza kununua tu kwa pesa ama huduma yake.”

"Si kweli kwamba simpendi." Alikunja uso. "Alikuwa na hasira siku hiyo." Lisa alimchana Ethan.

"Kwa nini unamtetea?" Mshtuko huo ulionekana katika sauti ya Ethan, lakini pia alisikika mwenye huzuni kwa wakati mmoja. “Bado unanikasirikia? Hii sio njia ya kulipiza kisasi. Kuwa msichana mzuri na uachane na Alvin sasa hivi. Kata uhusiano naye na turudi tulipokuwa hapo awali. Ninaweza kuanza kupanga harusi yetu mara moja.”

“Ethan, ni upuuzi gani huo? Umerukwa na akili?!" Sonya, mama yake Ethan,alitokezea ghafla na kunyakua kadi kutoka mkononi kwa mkono wa Lisa. Kisha, akampiga Ethan usoni kwa nguvu.

"Sisi wawili tumeanguka katika hali mbaya na bado unampa milioni 500, una wazimu? Pesa hii ni mtaji wako ili usimame tena!”

“Mama…” Uso wake ulikuwa umepauka kama karatasi. “Sitaki kuishi na majuto tena. Lisa ndiye mtu pekee ninayepaswa kumthamini.”

"Lakini hawezi kusaidia kwa sasa kwa kuwa hana uwezo na maskini," Sonya alisema katikati ya kilio, "baba yako hayupo nyumbani, kanitelekeza na kutekwa na mwanamke mwingine huko. Bila kusahau kuwa wewe hauna tena sifa ya kurithi kampuni. Ninawezaje kuridhika? Ikiwa kweli utamuoa mwanamke huyu, huo utakuwa mwisho wa maisha yako ya baadaye!”

Ethan alikunja ngumi huku sura yake ikiganda kwa maumivu. "Sitaki kuwa na mtu ambaye simpendi ili tu kupigania kampuni ya Lowe."
“Inatosha. Hukuwa unampenda Lina hapo awali lakini bado ulitaka kumuoa mwishowe, sivyo?” Sonya aliropoka bila kujizuia. “Ukithubutu kuwa na Lisa tena, nitajiua leo kwa kukimbilia kwenye mlango huu!”

“Tafadhali usinilazimishe…”

Mama na mwanawe waliokuwa wakizozana karibu na mlango wa kampuni hiyo waliwavutia wapita njia. Akiwa amechanganyikiwa, Lisa alisema, “Ethan, msikilize mama yako. Kwa kuzingatia utu wako, hakika utajuta katika siku zijazo ikiwa utarudiana nami.”

“Lisa, usimsikilize mama yangu—”

“Sikupendi tena,” Lisa alimkatisha kwa sauti ya dhati. “Fikiria jambo hilo. Kwa nini bado nikupende baada ya kuumizwa na wewe mara nyingi? Alvin ni wa kushangaza na hata aliokoa maisha yangu mara kadhaa. Usidanganywe na sura yake isiyojali. Kwa kweli yeye ni mpole na mwenye mawazo makubwa kuliko wewe ingawa haonyeshi waziwazi. Ninampenda sana sasa hivi.” Alihisi uzito mkubwa ukiinuliwa kutoka kifuani mwake baada ya kusema hivyo. Hakutarajia ni kiasi gani Alvin alikuwa ameathiri maisha yake.

Ethan alimkazia macho. Mwanamke huyo alikuwa akimsumbua ili amuoe tangu wakiwa wadogo. Hakufikiria hata siku moja kusikia maneno kama haya kutoka kwake. Hakuweza
kukubali hili!

“Hapana, unajidanganya tu!” Akasogea mbele kumshika kifundo cha mkono lakini akamkwepa kwa kipesi cha haraka.

“Naomba uache kunisumbua tena. Ninaishi na Alvin kwa sasa. Matendo yako yanaweza kusababisha kutokuelewana.” Kisha akaondoka bila kuangalia nyuma.

Ethan alipiga kelele kwa hasira na kupiga teke ukutani.

“Twende nyumbani. Babu yako amepanga umuoe msichana mdogo wa familia ya Urassa!” Sonya alisema.

Sura ya 100

Saa tatu na dakika ishirini asubuhi ile hatimaye Alvin aliingia kwenye chumba cha mikutano cha kampuni ya mawakili Jennings Solicitors. Mkutano wa asubuhi ulikuwa ukiendelea kwa utaratibu.

Sam Harrison bosi wa kampuni hiyo, alinung'unika, "Bw. Kimaro, umechelewa sana leo.”
Alvin alitembea kuelekea kwenye kiti cha ngozi na kusema kwa sauti ndogo. “Usijali," Aliinua kichwa chake kuweka umakini. Wakati huo huo, simu yake ilitetema.
Aliichukua simu yake na kuona ujumbe wa WhatsApp kutoka kwa Lisa. [Umefika?]

Mdomo wake ulipanuka kwa tabasamu. [Ndio.]

Kila mtu katika chumba cha mkutano aliachia mshangao baada ya kuona tabasamu usoni mwa Alvin.

“Nini?!” Walijiuliza ni nani aliyekuwa akituma meseji na Alvin ambaye kwa kawaida hakuwa na na muda wa kuchati. Kuona tabasamu usoni mwake lilikuwa jambo la kushangaza.

Sam haswa, alikuwa na udadisi wake. Alipunga mkono wake hewani na kuahirisha kikao “Sawa basi, ndiyo hivyo kwa leo. Endelea kufanya kazi kwa bidii wiki ijayo."

Mawakili wengine walikosa la kusema. Alikuwa anazungumzia kuboresha utendaji kazi muda si mrefu uliopita, lakini akashindwa kuchukua hatua ya kumkanya Alvin kwa kuchelewa. Ni bosi gani asiyewajibika! Kwa kuwa mkutano ulikuwa umekwisha, wengine walitoka nje ya chumba polepole.

Alvin aliinuka kwa uvivu, na Sam alimuuliza ndani ya sekunde chache. “Unamtumia nani meseji? Kuna nini kwenye tabasamu hilo la kuchekesha? Inaweza kuwa Lisa?" Sam alitania. "Inaonekana kuna kitu kimetokea kati yenu."

Alvin akamtupia jicho la pembeni. Hakuwa na wakati mzuri kama ule mara ya nyingi, kwa hivyo hakuruhusu kuharibu furaha ile. "Ndio, alikiri kwangu jana."

"Si yeye anakiri kwako kila siku?" Sam alikuwa na wivu sana juu ya hilo. Angependa rafiki wa kike kama huyo pia.

Tabasamu zito usoni mwa Alvin liliendelea kuboreka. "Hmm, anaendelea kunisumbua kuwa naye na hataacha hadi nikubali. Kwa kweli sijui nifanye nini naye.”

Macho ya Sam karibu yatoke nje ya kichwa chake. 'Hey, rafiki yangu! Hongera sana! Unapaswa kunishukuru kwa kukualika hapa Dar au usingekutana na Lisa vinginevyo.”

"Kukushukuru?" Mwonekano wa sura ya Alvin ukabadilika kidogo. "Ni kwa sababu yako haswa kwamba ninasumbuliwa na mwanamke huyo kila wakati. Na siwezi hata kumuondoa kwa sasa.”
Sam alishindwa cha kusema. “Sawa, huwa unafanya nini baada ya kazi?” Alvin alihoji bila tahadhari. "Lisa alisema maisha yake sasa yanakosa furaha. Anataka niwe namtoa out kuchangamka kidogo."

“Kwa hakika, yeye bado ni binti na yuko katika ujana wake. Inachosha sana kurudi nyumbani na kupika chakula cha jioni baada ya kazi kila jioni. Nichukue, kwa mfano. Kila siku baada ya kazi, huwa naenda kwenye baa kupata moja baridi moja moto, kwenda kucheza muziki kidogo, kuogelea, kuvua samaki kwenye jahazi langu, au kufurahia mlo wa usiku na marafiki. Ni maisha ya kuvutia.”
Alvin aliposikia hivyo alikunja uso. Sam alivuta uso kabla ya kusema tena. "Je, tumtoe ‘out’ shemeji usiku wa leo? nitafanya mipango yote.”


“Si usiku wa leo. Lakini tuifanye siku nyingine.” Alvin alisita kidogo kabla ya kukubaliana.
Saa kumi na moja za jioni Lisa alishuka kwenye gari jeupe la ‘uber’ na kuingia kwenye gari la Alvin. Alvin alikuwa akisoma nyaraka za kazi ndani na wala hakupoteza muda wake kumwangalia Lisa alipokuwa akiingia.
“Alvlisa mbona huniangalii? Je, hukun’miss?” Alimsogelea na kumkumbatia mkono.
"Napitia mafaili ya kesi." Akamtupia jicho la haraka. Lisa alivua koti lake alipoingia ndani ya gari, huku akifunua shati iliyombana sana alilokuwa amevaa ndani ambayo ilikazia umbo lake la kupinda. Macho ya Alvin yalikuwa na utata. Alikuwa amechanganyikiwa sana wakati huo na hakuendelea kufanya kazi.
“Oh, samahani kwa kukusumbua. Endelea basi.” Lisa alimwambia na kumwona akikaa sawa ghafla. Angewezaje kuendelea na kazi baada ya kile alichofanya?
Aliziweka pembeni zile nyaraka na kumnyanyua Lisa hadi mapajani mwake. Lakini, alikuwa mwanamke mrefu wa futi tano na kidogo, kwa hivyo kichwa chake kiligonga paa la gari mara moja. Gari lilikuwa fupi sana. Alikaza macho yake na kusema, "Ni wakati wa kununua gari mpya sasa."
Hans aliuliza karibu mara moja, "Bosi, ni aina gani ya gari unafikiria?"
"Lolote lililo na kiti cha nyuma kirefu na cha starehe. Fanya hivyo kesho."
Lisa hakujua afanye nini katika mazungumzo haya. Hakuweza kufahamu maisha ya matajiri wakubwa. Mwanaume mara moja aliamua kubadilisha gari lake kwa sababu la sasa lilikuwa na usumbufu alipomkumbatia mpenzi wake kwenye siti ya nyuma. Alikuwa akianguka kwa undani zaidi kwake.
“Unataka kula nini usiku huu?” Aliuliza.
'Kuna baridi hivi kwa sasa. Ninataka kula hotpot, na ninajua mahali pazuri pa kuzipata." Aliongeza baada ya kuona hasira iliyojitokeza usoni mwake, "Tunaweza kujaribu kuagiza hotpot ya wapendanao."

Baada ya kufika kwenye mkahawa wa hotpot, Lisa alimwalika Hans lakini Alvin alikataa mara moja. "Anaweza kula mahali pengine." Hatimaye alikuwa na wakati wa kuenjoy na mke wake, kwa hiyo bila shaka asingeruhusu mtu mwingine kukatiza.
Hans alitikisa kichwa haraka. "Ni sawa. Sipendi hotpot hata hivyo. Nitapata kitu kingine katika mgahawa wa karibu. Furahieni chakula chenu." Mara moja, akatoka nje ya mgahawa. Lisa akamtupia jicho la huruma.
Alvin akaketi kwanza. Alifikiria kuketi mkabala naye lakini haraka akasema kwa kuchukizwa, “Njoo ukae karibu nami."
Baada ya kumaliza kula, Lisa alitoka mezani na kuelekea msalani. Alipokuwa karibu kuondoka, ghafla alisikia wanawake wawili wakizungumza karibu na sinki.
"Je, uliona kule mgahawani, yule mwanamume aliyeketi kwenye meza 26 ni mzuri sana."
“Haya, anavutia kuliko hata wasanii wa muziki na filamu. Hata nilipimga picha chache kwa siri.”
"Lakini mpenzi wake sio wa kuvutia."
“Kweli. inavoonekana mwanamume hampendi. Aliendelea kumlisha mwanaume huyo lakini alionekana kutomkubali sana.” Mwanamkemwingine alidakia.
"Tulia, hakika mtu yeyote angefanya chochote kumfurahisha mtu huyo handsome." Mwingine akamjibu.
Lisa nusura alipuke kwa hasira. Kwa uangalifu, alipaka lipstick juu ya midomo yake nzuri. Kisha akasisitiza midomo yake pamoja. Mara moja, alichukua chumba cha kuosha na uzuri wake usio na shaka.
Kwa aibu, wanawake hao wawili waligeuka na kukusudia kuondoka.
Alishika mikono yao mara moja na kuelekeza nyuso zao kwenye kioo. “Jiangalieni vizuri. Wewe umejidunga ma botox kiasi kwamba misuli ya uso wako inaonekana imekaza kupita kiasi. Kwa mtazamo mmoja, unaweza kuona kwamba huyu mwenzako ana vichungi vilivyoingizwa kwenye pua yake. Lakini hata baada ya kupitia hiyo bado hamuonekani warembo kama mimi. Hata hivyo hamna ubavu wa kukosoa sura yangu.”
'Inatosha. Zilikuwa ni porojo tu zisozo na maana. Kila mtu ana viwango tofauti vya uzuri. Hakuna haja ya wewe kuja kwetu na mashambulizi yako binafsi. Tunaweza kutumia uhuru wa kujieleza.” Mmoja wa wanawake hao alipigwa na maji kwa sababu ya matusi.
“Na mimi pia. Ni wazi nyinyi wawili mna wivu kwa sababu hamna mpenzi mzuri kama wangu. Uhusiano wetu unaweza usiwe bora. Lakini nyinyi inawauma nini?"
Alinawa mikono yake na kuikausha kwa kitambaa. Kisha, alitoa mkoromo wa dharau kabla ya kuondoka kwenye chumba cha kuosha.
Baada ya kulipa bili, Alvin alingoja kando ya mlango kwa muda kabla ya Lisa kutokea tena. Lakini, hakuonekana mwenye furaha kama alivyoondoka. Ni kana kwamba kuna mtu alikuwa amemkosea.
Lakini Lisa hakusema chochote. Alvin hakujua ni nini kilikuwa kikiendelea.
Baada ya kuingia ndani ya gari, alibaki akiikazia macho simu yake bila kuongea neno lolote. Paji la uso wake liliinamishwa muda wote. Kwa kweli, kuwa katika uhusiano ilikuwa shida.
Alvin akatoa simu yake na kutuma meseji kwenye kikundi cha whatsapp alilokuwa kajiunga na marafiki zake wa karibu. [Inamaanisha nini mwanamke anapokataa ghafla kuongea?]
Sam: [Hakika yuko kwenye siku zake.]
Rodney: [Wanawake wanaudhi. Wana vichochezi na sababu nyingi za kukasirika.]
Chester: [Hakuna wasiwasi, mpeleke tu shopping na ulipe kila kitu.] Alvin alitumbukia katika mawazo mazito.
Wazo la Chester lilimpendeza Alvin.

LISA INAENDELEA KWENYE KITABU CHA 03

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.......... LISA
KURASA......101-105

Sura ya 101

Lisa hakuwa na wasiwasi juu ya shopping baada ya kufika kwenye maduka. Alichagua nguo chache bila mpangilio na kuzitazama kwa haraka kabla ya kuzirudisha kwenye rafu.
Alvin akamgeukia muuzaji na kumwambia, “Nitanunua nguo yoyote atakayogusa."
Hilo lilimshangaza Lisa. “Unamaanisha nini?”
"Tutanunua chochote kinachokuvutia." Alvin hakumpa nafasi ya majadiliano. "Mwanamke wangu anaweza kununua chochote anachotaka. Nina zaidi ya pesa za kutosha."
Muuzaji alisema kwa wivu, “Lo, mpenzi wako anakujali vizuri sana! Sijawahi kuona mwanamume yeyote mkarimu namna hii akiwa na mpenzi wake.”
Lisa alishtuka sana na kumwangalia Alvin aliyesimama mbele yake. Ghafla, aliweza kusikia moyo wake ukipiga kwa nguvu. Hata alihisi hatia kwa kumkasirikia muda mfupi uliopita.
Alvin hakuwa mtu wa kujali zaidi kuhusu pesa, lakini kwenye mapenzi alikuwa haeleweki. Lisa hakumwelewa kabisa msimamo wake, alimpenda kweli au alikuwa anamzingua tu? Kwa mtu wa nje angeweza kudhani kuwa upendo wake ulikuwa wa kujilazimisha na mapenzi yao yalikuwa ya upande mmoja. Lakini, wao tu ndio waliojua ukweli juu ya uhusiano wao. Haikuhitaji mtu mwingine yeyote kuthibitisha jinsi walivyotendeana.
“Ni sawa, basi nitachagua chache tu.” Lisa alitikisa kichwa. Hatimaye, aliendelea kujaribu mavazi kadhaa. Kila nguo ilionekana nzuri kwenye mwili wake kwa ujumla. Mwishowe, Alvin alilipa kila kitu ambacho alijaribu. Lisa aligundua tu baada ya malipo kupita.
Lisa alimshika mkono Alvin kwa furaha, wakatoka huku akijisikia vibaya kidogo kwa sababu nguo za hapo zilikuwa za bei ghali. "Sikuhitaji nguo nyingi kiasi hiki, Alvilisa."
'Ni sawa. Ilimradi unazipenda,” Alijibu Alvin. “Mi sijali kuhusu gharama.”
"Asante." Lisa alihisi kuguswa, alisimama kwa vidole vyake ili kumfikia Alvin sikioni na kumpa busu la shukrani. Sura ya aibu ilimwangazia usoni mwake.
Macho ya Alvin yaliingiwa giza na ubongo wake kuhisi kama umepigwa shoti kwa sekunde kadhaa baada ya busu la Lisa kupenya sikioni mwake. Kwa kweli, Chester alikuwa sahihi. Kumpeleka shopping mwanamke aliyekununia bila sababu kunasawazisha kila kitu.
•••

Siku iliyofuata. Lisa alivaa nguo zake mpya kabla ya kwenda kuangalia maendeleo ya ukarabati wa jumba la Kelvin Mushi huko Mbezi Beach. Mafundi walikuwa wakiendelea na kazi ya ujenzi. Alizunguka eneo hilo na kujadili maendeleo na fundi mkuu.
Kelvin aliingia kutoka nje na kuelekeza macho yake kwenye nguo zake mpya. "Nguo ni nzuri sana mrembo. Ni shopping ya hivi karibuni?" Kelvin alimuuliza kwa mshangao.
"Ndio." Lisa alitabasamu kwa furaha baada ya kufikiria kuwa ni zawadi kutoka kwa Alvin. Furaha iliyofurika moyoni mwake na kuonekana machoni mwake ilimshangaza Kelvin ambaye alijikuta akiingiwa na kiroho cha wivu.
Maongezi yao yalikatishwa ghafla baada ya Lisa kupokea simu kutoka kwa nambari isiyojulikana.
“Halo, wewe ni Lisa Jones?” Sauti kutoka kwenye simu iliuliza na kuendelea kueleza. “Mwanamke anayeitwa Manka amezimia katika nyumba yake ya kupanga. Nimejaribu kutafuta majina ya ndugu zake kwenye simu yake lakini nimekuta namba iliyoseviwa ni yako tu…”
“Manka… Shangazi Manka?” Lisa alimkatisha mara moja, “Tafadhali piga simu ambulance ili kumpeleka hospitali ya karibu. Usijali kuhusu nauli nitakuja sasa hivi.”
Baada ya kukata simu, alitoka kuelekea mlangoni na Kelvin alimfuata. “Nitakusindikiza.”
Lisa aligawanya midomo yake ili kuzungumza lakini alikatishwa na Kelvin, “Usitake kunizuia. Kuna kila aina ya usumbufu hospitalini na kuwa na mtu wa kukusaidia ni bora kuliko kuwa peke yako. Kama mtu ninayekuthamini sana siwezi kusimama kando na kukuacha uhangaike peke yako. Isitoshe, huu si wakati wa kubishana, twende tuwahi kwa mgonjwa.” Lisa akiwa amezidiwa na wasiwasi, hakuweza kuwa mgumu zaidi.
Baada ya kufika hospitalini, muuguzi mmoja alikuwa akipiga kelele karibu na mlango wa chumba cha dharura. "Ndugu yoyote wa Bi Manka? Jitokezeni tadhadhari na mwende kwenye mapokezi ili kulipa bili haraka iwezekanavyo."
"Niko hapa." Lisa alijitokeza na kukimbia kwa daktari. “Dokta anaendeleaje?”
"Ana hitilafu kubwa katika ubongo. Upasuaji lazima ufanyike mara moja. Nenda ukafanye malipo sasa hivi na muandae mtu wa kutia saini fomu za upasuaji." Daktari alisukuma ankara ya malipo mikononi mwake.
Lisa alikimbia chini kushughulikia malipo. Upasuaji ulikuwa tayari umeanza wakati aliporudi kwenye ghorofa ya juu.
"Ninafahamiana na madaktari kadhaa katika hospitali hii, kwa hivyo nilimeshashughulikia kila kitu na wanaendelea na upasuaji," Kelvin alieleza.
“Asante, Kelvin.” Lisa aliguswa.
Upasuaji huo hatimaye ulikamilika saa tatu baadaye. Aunty Manka alitolewa nje ya chumba cha dharura. Lisa karibu hakuweza kumtambua mwanamke huyo dhaifu. Aunty Manka alikuwa akionekana mwenye afya njema na mwenye nguvu wakati bado akiwa mlezi wa bibi yake Lisa, lakini alionekana kuwa mtu tofauti kabisa muda huo. Mbali na kichwa chake kilichojaa mvi, mashavu yake yaliyozama pia yalimfanya aonekane mzee sana. ‘Ni nini kilikuwa kimetokea kwake?’ Lisa alijiuliza.
Ilikuwa ni saa kumi na moja jioni wakati Aunty Manka alipofumbua macho na kumuona Lisa. Machozi yalitiririka mashavuni mwake mara tu alipomuona. "Bi Jones, sikufikiria kama ningekuona tena."
"Huna haja ya kuniita hivyo tena." Lisa alilazimisha tabasamu la uchungu. “Mimi si mtoto wa Jones.”
"Hapana, utakuwa Bi Jones daima."Aunty Manka aliongea kwa sauti dhaifu.
“Aunty Manka, ni sawa, tayari ninajua ukweli kwamba nilichukuliwa na familia ya akina Jones. Nina hakika unajua hilo pia baada ya kuwa mlezi wa bibi yangu kwa miaka mingi iliyopita.”
“Nani kasema hivyo?” Aunty Manka alijibu huku akiwa amekasirika. "Bila shaka wewe ni sehemu ya familia ya Jones!"
Jambo hilo lilimshangaza Lisa. “Nilisikia kutoka kwa Lina. Mbali na hilo, sidhani kama wanandoa wa Jones wangefanya mambo hayo kwa binti yao wa kuzaa wenyewe.”
“Haya yote lazima yamekuwa magumu sana kwako. Familia ya Jones imekosa utu kabisa." Aunty Manka alikohoa mara kadhaa kwa hasira. "Sio tu kwamba walinifukuza nyumbani kwao, lakini hata walikuambia kwamba wewe si mtoto wao. Ina maana wamesahau ahadi walizotoa kwa babu yako na bibi yako??"

"Anti Manka, ulifukuzwa nyumbani?" Lisa alishtushwa na habari hii. "Lakini nilichosikia kutoka kwao ni kwamba uliondoka kwa sababu haukuwa tayari kumtunza Bibi baada ya kupooza."
“Bibi Masawe amenisaidia sana na alinitunza maisha yangu yote. Nisingeweza kumtupa alipokuwa akinihitaji sana.” Aunty Manka alijibu. Macho yake yaling'aa kwa machozi. “Bibi mdogo Lisa, kwa kweli wewe si binti wa Jones Masawe. Mama yako mzazi ni Sheryl Masawe, yule mwanamke unayeamini kuwa ni shangazi yako. Alikuwa na mimba yako kabla ya ndoa. Babu na Bibi yako waliogopa kupoteza heshima yao, bila kusahau kwamba hii ingeweza kufanya iwe vigumu kwa mama yako kuolewa tena. Ndiyo maana walikukabidhi kwa Jones Masawe ambaye ni mjomba wako.”
Lisa alihisi ulimwengu wake ukipinduka chini-juu. Kamwe asingetarajia kuwa Sheryl alikuwa mama yake. Ilikuwa na maana sasa kwamba babu na bibi yake walimchukua kutembelea kaburi la Sheryl kila tarehe ya kumbukumbu ya kifo chake. Haishangazi pia alifanana naye sana! Hata Alvin alishawahi kumwambia hivyo siku walipokwenda kumtolea sadaka bibi yake kaburini.
"Baada ya kukuzaa, mama yako alifunga safari ya kikazi kwenda Kigoma na kwa bahati mbaya akatoweka kwenye ajali ya kimbunga," Aunty Manka alisema katikati ya kwikwi. “Kilikuwa kimbunga cha ajabu na cha kutisha na zaidi ya watu kumi walikufa. Kufikia wakati walipoupata mwili wake, ulikuwa umeharibika sana, hata hawakuweza kumtambua.”
Lisa alihisi kukosa hewa kana kwamba hewa yote ilikuwa ikitolewa kwenye mapafu yake. Kelvin, ambaye alikuwa akisikiliza kando, alimpigapiga begani kwa upole.
Aunty Manka aliendelea, “Mama yako alikuwa mwanamke aliyefanikiwa ingawa alikuwa mdogo. Mawenzi Investiments, ambayo ni kati ya biashara 100 zilizofanikiwa zaidi Tanzania, ilianzishwa na yeye peke yake.
"Mama yangu ndiye mwanzilishi wa Mawenzi Investiments?" Sura ya mshangao iliwaka usoni mwa Lisa. Mwanga wa upeo ulipita akilini mwake." Sasa aliweza kutambua ni kwanini Jones alifanikiwa kuwa mwenyehisa mkuu wa Mawenzi Investiments."
"Nini? Jones ndiye mmiliki mkuu wa hisa?" Aunty Manka alicheka. “Inawezekana bibi yako ana…”
"Bibi alifariki siku chache zilizopita." Lisa alimkatisha ghafla. Aunty Manka alitoa macho kwa mshtuko. Dakika chache baadaye, hatimaye machozi mengi yalimtoka kwenye kona za macho yake.
Aunty Manka alijikaza na kusema kwa unyonge, “Bibi yako asingekufa ghafla. Hakika kuna mengi nyuma ya kifo chake! Lisa, kuna kitu unahitaji kujua. Baada ya mama yako kufariki, babu na bibi yako walikuwa wakisimamia Mawenzi Investiments kwa siri. Ili kuhakikisha Jones atakutunza, aliweka wosia. Wewe na Jones kila mmoja angepewa 30% ya hisa za kampuni hiyo mara tu utakapokuwa mkubwa na baada ya bibi kufa.”
Lisa alianguka kwenye kiti alipopokea habari hiyo ya kutisha kama bomu.
“Baada ya Kibo Group kushuka, kuna uwezekano kwamba Jones Masawe alipanga njama ya kumuua bibi yangu ili kurithi hisa zote za Mawenzi Investiments? Hapana, hilo haliwezekani. Yeye ni mama yake, baada ya yote.” Lisa alishindwa kuamini.
Kelvin alishusha pumzi na kusema. “Jones amezoea kuwa katika nafasi ya madaraka maisha yake yote. Huenda hujui hili lakini watu wanaweza kufanya lolote ili kudumisha maisha yaliyojaa utajiri na ushawishi. Tangu mwanzo wa wakati, kumekuwa na rekodi za ndugu wa damu kushambuliana, kurogana na kuuana wakipigania kuwa warithi wa familia tajiri. Isitoshe, bibi yako alikuwa amepooza kabla ya hii. Pengine alimwona kuwa mzigo.

Sura ya 102

Aunty Manka aliitikia kwa kichwa. “Pia, sikuwahi hata siku moja kuamini kuwa kupooza kwa bibi yako ilikuwa ajali. Siku moja Lina alikuja nyumbani na mara bibi yako akaanguka kutoka ghorofa ya pili muda mfupi baada ya kupanda. Tangu siku hiyo nikafukuzwa na baadaye nikasikia kuwa bibi yako amepooza."
Lisa aliinua macho yake kutoka chini huku mshtuko ukipita ndani yake. Mtu kama Lina angewezaje kuwa mshenzi kiasi hicho kumdhuru bibi yake mwenyewe?
"Nina hakika kwamba lazima amegundua kuhusu uhusiano wako na Mawenzi Investiments na kwamba wewe si binti wa kuzaliwa wa Jones" Aunty Manka alikisia.
"Shangazi Manka, ulipaswa kuniambia kuhusu hili mapema." Lisa alijisikia hatia sana.
“Nilitaka sana lakini nilishindwa kwa sababu familia ya Jones ilikuwa ikinitafuta ili kunidhuru. Sikutaka kukuingiza katika matatizo makubwa. Nadhani Jones hakuridhika bila kujua asilimia 30 ya hisa zimeenda wapi, au labda alitaka kuniua ili nipeleke siri hii kaburini. Ndiyo maana nimekuwa nikiishi kwa kujitenga na kujificha, bila kuthubutu kuonyesha uso wangu hadharani. Na hata namba za simu nilibadilisha.” Aunty Manka alimshika Lisa mikononi na kumwambia, "mtafute mmoja wa wanahisa huko Mawenzi Investiments anayeitwa Chris Maganga. Mama yako aliokoa maisha yake hapo awali. Anazo nyaraka zinazohitajika za kampuni ya Mawenzi."
“Sawa.” Lisa alikubali kwa huzuni, hatimaye akauliza kwa msisitizo, “Shangazi Manka, unajua baba yangu halisi ni nani?”
Mwanamke yule mzee akatikisa kichwa, akihema. "Sina hakika, lakini nadhani anaishi huko Nairobi."
Mwanga wa matumaini ukaangaza machoni mwa Lisa. Ilionekana kuwa angeweza kupata nafasi ya kukutana na baba yake mzazi siku moja. Hata hivyo, kwa nini alimtelekeza yeye na mama yake? Labda alikuwa ameanzisha familia nyingine kwa muda mrefu.
Wanawake wote wawili katika wadi ya hospitali walinyamaza kimya. Bila kujali, Kelvin alipendekeza, “Kwa ajili ya usalama wa Aunty Manka, ni bora tukimhamishia hospitali nyingine ili akina Jones wasimpate. Namfahamu mkurugenzi mkuu wa hospitali binafsi ambaye anaweza kutusaidia.”
“Uko sahihi. Aunty Manka hawezi kubaki hapa,” Lisa alikubali.
Baada ya hapo, walitumia saa iliyofuata kuwasilisha makaratasi yaliyohitajika kwa ajili ya uhamisho huo. Hata hivyo, alipokuwa akiandaa taratibu pale mapokezi, Lisa alishindwa kumuona Angela Harrison, yule dada mdogo wa Sam Harrison aliyekuwa anampenda sana Alvin, ambaye kwa bahati mbaya alikuwepo kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi wa kawaida mama yake. Alichukua picha ya Lisa akiingia kwenye lifti na Kelvin.
Angela alimtumia Alvin picha hiyo bila kusita. [ Alvin, huyu si mpenzi wako? Ina maana mmeachana? Nilimwona akiwa na mwanaume mwingine.] Angela alifurahi baada ya kutuma ujumbe huo. Kwa muda mrefu alikuwa amekasirishwa na Lisa na alikuwa akitafuta nafasi ya kumgombanisha na Alvin. Sasa, hatimaye alipata nafasi ya kumchongea.
Alvin ambaye alikuwa anatoka kazini ghafla alisikia simu yake ikitetemeka. Uso wake ulianguka mara ya pili alipobonyeza ujumbe huo. Picha hiyo ilidhihirisha wazi Lisa na Kelvin wakiwa pamoja hospitalini. Akampigia simu mara moja. “Uko wapi?”
“Um… Hospitalini,” alikiri baada ya kusitasita kwa muda mfupi.
Uso wa Alvin ulilegea kidogo. Angalau hakusema uwongo juu ya hili. “Upo pamoja na nani?”
Lisa alimtupia jicho la haraka Kelvin ambaye alikuwa akiongea na daktari aliyehusika kabla ya kwenda pembeni. "Nipo na daktari. Mlezi ambaye alikuwa akimtunza bibi yangu ametoka tu kufanyiwa upasuaji. Yeye hana ndugu au jamaa wa karibu wa kumwangalia. Labda nitachelewa kufika nyumbani baadaye kidogo leo."
Alvin alijua Lisa alikuwa anadanganya. Alijua alikuwa na Kelvin. Nia ya hatari ikaangaza machoni pake. Alvin alijisikia vibaya kwa kuona Lisa akiwa na shida angependelea kutafuta msaada kutoka kwa Kelvin badala yake. Uhusiano wake na mwanaume huyo ulikuwa wa karibu kiasi gani, kweli?
"Umekasirika?" Lisa aliuliza kwa tahadhari baada ya ukimya wa muda mrefu kutoka kwa Alvin. "Muuguzi wa zamu anaweza kuja saa tatu usiku, kwa hivyo itabidi nisubiri hadi wakati huo."

"Sawa!" Alvin alijibu kinyonge kabla ya kukata simu ghafla. Kisha, alijaribu kutuliza hasira yake iliyokuwa ikimpanda kwa kukisugua kichwa chake taratibu.
Alvin alijikumbusha kuwa asiwe na huzuni sana. Alihisi huenda labda Lisa hakuwa na mpango naye ndiyo maana mara nyingi alikuwa akitaka kuwa karibu na Kelvin.
Simu ilikatika ghafla. Lisa alibaki akiitazama simu ile kwa sekunde kadhaa mpaka Kelvin alipomshtua. "Alikuwa Mheshimiwa Kimaro? Anakuja kumuona Aunty Manka? Basi labda niende ili kuzuia ugomvi usio wa lazima.”
"Hapana, hakusema kama anakuja au la." Ghafla, hisia ya ajabu ikatokea moyoni mwake. Hiyo ilikuwa ni hisia yake tu. Alvin alikuwa hajasema lolote kuhusu kwenda ama kutokwenda kumuona Aunty Manka.
Kelvin alionekana kushtuka lakini punde akaonyesha tabasamu. “Naam, ni kawaida. Yeye si familia hata hivyo.” Alichana na mada hiyo na kumwambia, “nilizungumza na daktari mapema kwa hiyo usiwe na wasiwasi sana.”
“Asante.” Lisa alikuwa na shukrani za dhati kwa Kelvin. Asingefanikiwa sana siku hiyo bila msaada wake. Kwa kweli, alifikiria kumwomba Alvin msaada hapo awali lakini alipokumbuka tabia yake ya dharau na kutojali, alikuwa na hakika kwamba wasingeishia pazuri. Pia alikumbuka kwenye makubaliano ya ndoa yao alishawahi kumwambia kwamba hataonana na ndugu zake.
"Ni sawa. Naam, naweza kuondoka sasa. Nina miadi ya chakula cha jioni kazini jioni hii." Kelvin alielewa umuhimu wa kutovuka mipaka.
“Sawa.” Lisa akamsogeza mpaka mlangoni.
Alvin hakumpigia simu usiku mzima. Hatimaye Lisa aliendesha gari hadi nyumbani baada ya muuguzi kujitokeza. Ukiachana na Charlie na watoto wake watatu waliokuwa wakicheza huku na kule, alikuwepo Aunty Linda pekee aliyekuwa akitazama TV sebuleni.
"Mheshimiwa Kimaro yuko wapi?" Swali hilo lilimshangaza sana Aunty Linda.
“Si alikuaga? Bw. Kimaro alinipigia simu mapema jioni hii akisema anaenda kwa safari ya kikazi hadi Nairobi. Hatarudi kwa siku chache.”
Lisa alipigwa na butwaa na kukaa kimya. Kwa kweli hakuwa na habari kuhusu hilo. Lisa aliingiwa na simanzi sana. Akiwa mpenzi wake, Alvin hakuuliza kuhusu hali ya Aunty Manka wala hakumjulisha kuhusu kwenda safari zake za kikazi. Nini kilikuwa kikiendelea naye?
Baada ya kuelekea ghorofani, alimpigia simu Alvin. Kelele ya mandhari iliyosikika nyuma ilikuwa kubwa kwenye simu. Aliweza kujua mara moja kwamba alikuwa mahali fulani pa starehe kama baa au klabu.
“Uko wapi? Si umeenda kwa safari ya kikazi?” Lisa alimuuliza kwa mshangao.
"Ndio." Sauti yake ilionyesha kutojali.
Lisa hakufurahishwa na jibu hilo. “Mbona hukuniambia?”
“Kwani ni lazima nikuage kila ninaposafiri?” Sauti yake kujeuri na ya dharau ilimkatisha tamaa.
"Sawa, sitauliza tena siku nyingine." Lisa alikata simu, akajilaza kitandani na kuanza kulia.
Hata hivyo, Lisa alifurahishwa sana na taarifa alizopata kutoka kwa Aunty Manka siku hiyo, kwamba mtu alyeamini kuwa ni shangazi yake kumbe ndiye alikuwa mama yake, na yeye ndiye mrithi wa Mawenzi Investments. Alitamani kumwambia habari hizo Alvin lakini hakumpa hata nafasi hiyo.

Sura ya 103

Siku mbili zilizofuata, Lisa alitumia juhudi nyingi kupata anwani ya nyumbani ya Chris Maganga. Lakini, mtu huyo aliishi Mwanza muda mwingi. Hakuwa na chaguo ila kuchukua ndege ya mapema kuelekea huko.
Baada ya kufika kwenye jumba lake, mlinzi alifungua mlango na kuuliza, “Shida?”
Lisa akajitambulisha moja kwa moja.“Tafadhali mwambie Bw. Maganga kwamba mimi ni binti ya rafiki yake wa zamani, Sheryl Masawe.”
Mlinzi alimpandisha juu na chini kwa mashaka kabla ya kupiga simu. Alipopata jibu, mlinzi huyo alimkaribisha Lisa ndani kwa upole, “Bw. Maganga anakungoja ndani.” Akaingia mara moja.
Alitarajia kuona kuwa Chris Maganga angekuwa mzee katika miaka yake ya mapema ya 70, kwa hivyo alishangaa kumwona mwanamume wa makamo ameketi kwenye kochi. Mtu huyu alionekana mdogo kuliko miaka 40. Ingawa kulikuwa na mikunjo kwenye pembe za macho yake, alionekana kuwa bado kijana kabisa. Lazima alikuwa mzuri sana alipokuwa mdogo.
“Wewe ni… Mjomba Chris?” Lisa aliuliza kwa wasiwasi.
Alama ya mshangao ilimtoka Maganga machoni mwake alipokuwa akimchunguza binti huyo. “Miaka 20 imepita kwa kufumba na kufumbua. Mtoto mdogo wa kike kutoka wakati huo umekua sana. Unafanana na mama yako kweli.”
Lisa alikuwa na hamu ya kutaka kujua. "Nilisikia mama yangu aliokoa maisha yako hapo awali, kivipi?"
"Hiyo ni sawa. Usidanganywe na unachokiona sasa. Wakati fulani nilikuwa kijana mdogo mwenye madeni makubwa. Kwa bahati nzuri, nilikutana na mama yako, akaniajiri na kuanza kumfanyia kazi. Ndivyo nilivyofika hapa nilipo leo.” Chris Maganga aliachia tabasamu hafifu huku akikumbuka yaliyopita.
Lisa alipepesa macho taratibu. Machale yake yalimwambia kwamba huenda mwanamume huyo aliwahi kupendezwa na mama yake kimapenzi kwa namna alivyoongea kwa hisia kila alipomtaja mama yake.
"Kwa bahati mbaya ... alikufa angali bado mwanamke mdogo sana," Maganga alisema kwa majuto. “Ndiyo. Sielewi kwanini mama yako aliamua ghafla kuelekea Kigoma. Wengine walisema ni bahati mbaya lakini sikuweza kamwe kuondoa hisia kwamba kuna mtu alikuwa nyuma ya hili. Asingesombwa na kimbunga kama si kwa hili…” Huzuni ilikuwa imeandikwa usoni mwa Chris.
Lisa aliona habari hiyo kuwa ngumu kumeza. "Unamaanisha kuwa mama yangu aliuawa?"
"Ndio, babu na bibi yako hawakujua lakini nilikuwa nikimfanyia kazi wakati huo." Maganga alifumba macho ghafla. “Nilichunguza baadaye. Mtu aliyesababisha kifo chake anaweza kuwa yuko Nairobi.” Chris alisema na kunyanyuka mara moja kuelekea chumbani. Lisa alitikisa kichwa kwa unyonge.
"Hizi ndizo hati ambazo babu yako alinikabidhi ili nizihifadhi." Chris alishusha pumzi huku akimkabidhi Lisa faili alilorejea nalo kutoka chumbani. “Kwa bahati nzuri, babu yako alikuwa na mpango mbadala dhidi ya Jones ingawa nina uhakika hakutaka siku hii itokee. Lakini Jones hakuwa na uhusiano wowote na mafanikio ya Mawenzi Investiments leo. Alitengewa asilimia 30 tu ya hisa kwa sababu ya kukulea, na bado hajashukuru.”
'Hiyo ni sawa. Kama wasingenifukuza mimi, angeweza kupata hisa zote baada ya Bibi kufa, lakini hakutaka kusubiri. Badala yake alimuua bila huruma.” Alizungusha vidole vyake kwenye faili. "Kwa hati hizi, anaweza kusahau kuhusu kuwa mwenyekiti wa Mawenzi Investiments mwezi ujao."
"Usijali, nitakusaidia kupata nafasi hiyo." Chris akatabasamu.
“Asante Mjomba Chris.” Lisa alihisi kuguswa. “Umekuwa ukifanya kazi kwa ajili ya mama yangu kwa muda mrefu. Ulishawahi kumuona baba yangu?" Aliuliza kwa kusitasita.
Uso wa Maganga ulianguka kabla ya kujibu baada ya muda mrefu, “Nimewahi. Lakini usifadhaike sana. Hajui uwepo wako."
Ghafla, Lisa alihisi faraja. “Sawa. Ili mradi tu nimefahamu ukweli kuhusu wazazi wangu.”
“Kwa kweli mchango wake ndiyo uliofanya Mawenzi Investiments kufanikiwa leo. Lakini ... tayari ana familia." Chris alimtazama kwa huzuni.
Lisa alielewa. "Nilitarajia tu. Miaka 20 ni mingi sana. Hakuna mtu ambaye angengojea milele."
Chris akamuonya. "Kuwa makini na Jones, amekuwa akijaribu kupata upendeleo kwa wanahisa na wafanyikazi wa ngazi za juu wa kampuni. Lazima uchukue hatua kwa tahadhari."
"Ndio. Hakika nitarudisha kilicho changu.” Lisa alimhakikishia.

Alasiri hiyo, Lisa alikataa mwaliko wa Maganga wa kukaa muda mrefu na akapanda ndege ya kurudi Dar. Aliwasha simu yake baada ya kushuka kwenye ndege lakini bado hakukuwa na habari yoyote kutoka kwa Alvin. Hisia ya uchungu ilionekana moyoni mwake. Alijiuliza nini kilikuwa kimeharibika tena kati yao.
Baada ya kuwaza mara mbili, aliamua kumtumia ujumbe. [Uko wapi?] Bado hakusikia majibu kutoka kwake baada ya muda mrefu. Aliamua kuachana na Alvin na kumtafuta shoga yake Pamela ili kumpasha habari.
"Hongera, bosi wa baadaye wa Mawenzi Investiments! Ah, utakuwa na thamani ya mamia ya mabilioni ya shilingi hivi karibuni. Ninapaswa kukaa karibu nawe na kamwe usinisahau.” Pamela alicheka vibaya. “Unafikiri Cindy atajisikiaje mara tu atakapojua?”
"Hakuna maana kufikiria juu ya watu wanaoyumbishwa na upepo." Lisa akatikisa kichwa. “Angekuwa pamoja nami ningemdhamini hata kwenda kufanya shooting Afrika Kusini au Ulaya.”
"Lakini nilisikia kwamba ... amepata bwana tajiri," Pamela alinong'ona, "mtu mashuhuri huko Nairobi. Umaarufu wake umekuwa ukiongezeka hivi karibuni."
Wakati huo huo, Sam alimtumia Lisa ujumbe kwenye WhatsApp. [Lisa, umepata chakula cha jioni? Kama bado unaweza kuja Millionaires' Pub kwa muziki? Alvin yuko hapa pia. Unaweza kuja na rafiki yako.]
Moyo wa Lisa uliruka kwa kumfikiria Alvin. Alimuonyesha Pamela ujumbe huo. "Vipi, twende?"
“Twende.” Pamela alikonyeza macho. “Ulikuwa unaniambia tu kwamba Alvin hajazungumza na wewe kwa siku kadhaa. Nini tatizo?”
Lisa akakunja uso kabla ya kusema tena kwa kufadhaika, “Lazima kuna jambo linamsumbua. Alikuwa vizuri tu siku chache zilizopita lakini sasa…Ananiona kama toy! Hajafika nyumbani kwa siku chache sasa, sijui….”
"Ah, nasikia harufu ya wivu kutoka kwako!" Pamela alitania.
“Mimi sina wivu. Sipendi tu anavyonichukulia, yaani anapenda niwe nambembeleza na kumyenyekea kila dakika.” Lisa alikataa kukubali. “Haya, ni bora kwa kuwa mali zangu zitarudi, hatimaye nitapata uhuru wangu tena.”
Kabla hawajaondoka, Lisa alimkumbusha kitu Pamela. "Sawa, uliendesha gari kuja hapa lakini nina uhakika kuwa utakunywa pombe baadaye huko Club, nakushauri ungemwambia Patrick akuijie baadaye.”
‘Wazo zuri, ngoja nimpigie simu.” Pamela aliafiki.
Patrick ambaye ni mpenzi wa Pamela alipopigiwa simu alijibu kinyonge sana, “bado kuna vimeo vichache ninayohitaji kuvikamilisha ofisini jioni hii, nitakutumia pesa ya usafiri utachukua taxi.”
Katika dakika chache, Pamela alipokea shilingi laki mbili kwenye akaunti yake ya m-pesa. Hakuweza kumlaumu au kumkasirikia tena mpenzi wake, kwani alionyesha kumjali hata hivyo.

Sura ya 104

Millionaires' Pub ni Club ya starehe iliyopo Masaki ambayo hutoa huduma kwa matajiri wenye hadhi ya umilionea pekee. Huwezi kuingia kama humo kama weye ni hohehahe ama hadhi yako ni chini. Si ajabu kukuta bia ambayo inauzwa elfu na mia tano mitaani pale ikauzwa elfu hamsini au zaidi. Usishangae kuuziwa sahani ya chipsi kwa elfu hamsini, na vitu kama hivyo.
Saa mbili usiku, Lisa na Pamela ndo kwanza walikuwa wanaingia pale Millionaires' Pub walipoona mwanamume na mwanamke wakitembea kuelekea kwao kutoka upande wa pili. Mwanamke aliyevalia vizuri alionekana mrembo wa kuvutia sana. Mwanaume naye alikuwa ametokelezea kiroho safi. Kwa kweli walikuwa wamevunja kabati siku hiyo. Papo hapo, Pamela alihisi kufadhaika kabisa. Mwanamume aliyekuwa ametoka kumwambia muda si mrefu kwamba alikuwa amebanwa sana na kazi ofisini alikuwa amesimama mbele yake akiwa na mwanamke mwingine.
Lisa alikunja uso. Alimvuta rafiki yake hadi kwa wawili hao na kusema kwa tabasamu la kubandika, “Bw. Patrick, ni sadfa iliyoje! Nilidhani ulimwambia Pamela unafanya kazi za ziada ofisini? Ulisema ulikuwa na shughuli nyingi na usingeweza kuja kumchukua baadaye, mbona sasa upo hapa tena na mtu mwingine?" Kauli yake ya moja kwa moja ilimfanya Patrick aone haya.
"Ilibidi nifanye kazi ya ziada lakini Linda alniipiga simu kusema kuna mtu alikuwa akimsumbua, kwa hivyo nilifika hapa mara moja kumsaidia."
Linda akaongeza haraka, “Hiyo ni kweli. Pamela, nina hakika umewahi kusikia kuhusu Master Cook. Yeye ni mkorofi kama nini."
Pamela alitingisha tu kichwa chake.
Lisa alisema, akitabasamu. “We binti, nakuonea wivu sana kwa kuwa na kaka anayekujali. Sio tu kwamba anahudhuria kila sherehe na wewe kama mwenza wako wa kiume bali pia anakimbia haraka mara moja kukuokoa unapokuwa na matatizo. Lakini huenda usiweze kupata mchumba ikiwa utaendelea na tabia hii. Wanaume wengine wanaweza wakafikri kuwa nyinyi wawili ni wapenzi.”
Bila kutarajia, sura iliyochanganyikiwa ilitanda kwenye uso wa Linda. “Lisa, unajaribu kusema nini? Kwa nini huamini kwamba sisi hatuna uhusiano mbaya? Umefikiria jinsi maneno yako yanavyoweza kumuathiri Pamela?"
Patrick pia alikunja uso baada ya maneno hayo ya Lisa. Linda akageuka kumtazama kwa hatia. “Patrick, samahani. Unapaswa kwenda kwa Pamela. Nitatoka mahali hapo haraka nikihisi hatari yoyote.”
Kwa hasira, Patrick akamtupia jicho Lisa. "Bi Jones, kama kuna mambo ambayo huelewi, nakushauri usiwe unachonga mdomo wako."
Lisa akafuatia na kusema. "Nilikuwa tu nampa ushauri wa kirafiki ..."
“Tunajua tunachofanya bila kuhitaji ushauri wako,” alikatishwa kwa maneno yaliyonyooka.
“Kweli? Nadhani hujui unachofanya.” Pamela alihisi hasira ikizidi kumpitia rafiki yake alipotukanwa. "Unakimbia mara moja kila wakati Linda anapokuhitaji. Lakini vipi kuhusu mimi? Nilienda hospitalini peke yangu nilipougua na nilichukua teksi kunipeleka nyumbani baada ya kurudi kwa safari ya ndege usiku wa manane. Siku hizi hata hutoki kula chakula pamoja nami tena…”
“Tafadhali usimsikilize rafiki yako. Moyo wa Patrick upo kwako tu.” Linda alisema kwa haraka.
"Funga mdomo wako." Pamela alimfokea mwanamke huyo, “Kama mnapendana kwanini msiweke wazi tu nikawaachia uhuru wenu?”
“Pamela, sikuwa…” Machozi yalitiririka mashavuni mwa Linda.
Patrick hakuweza kuvumilia zaidi na mara moja akapiga hatua mbele ya Linda. “Pamela Masanja, una tatizo gani? Linda hajafanya lolote la kukukera. Kwanini ukubali kushawishiwa kwa urahisi na rafiki yako? Jifunze kufikiri kwa kujitegemea,” alifoka.
"Uko sawa, mimi ni mjinga, na ndiyo sababu nilikukubali." Kisha kusema hayo, Pamela akamshika Lisa kwa mkono na kuondoka hadi ghorofa ya pili.
Nyuma yake, Linda alimhimiza mwanaume huyo. “Patrick, mfuate haraka ukambembeleze. Amekasirika.”
"Aah! Achana naye bana. Kwa nini unamjali? Hukusikia alichosema sasa hivi?”
“Nilisikia kila kitu. Lakini….”
"Achana naye..."
Pamela alisikia sauti zao zikitokomea kwa mbali nyuma yake. Machozi ya hasira yalianza kuteremka kwenye mashavu ya Pamela alipokuwa akipanda ngazi. Kwa bahati nzuri, Lisa alikuwepo kumshikilia.

"Samahani, sikupaswa kusema hivyo." Lisa alimfariji.
“Siku zote nilitaka kusema hivyo, sema wewe umenisaidia tu." Pamela alifuta machozi kwa nyuma ya mikono yake. "Uligundua kuwa kuna kitu kibaya baada ya kuona mwingiliano wao mara mbili. Lakini mara ambazo nimemwona Linda akiwa na Patrick zinakaribia kulingana na zile nilizotoka na Patrick.”
Jambo hilo lilimshtua Lisa. Alikuwa akisoma nje ya nchi kwa miaka michache iliyopita, kwa hivyo hakufahamu sana juu ya maisha ya mapenzi ya rafiki yake. Tabasamu la uchungu lilienea kwenye uso wa Pamela.
“Mara saba kati ya mara kumi tulizotoka na Patrick, alikuwa na Linda, hata kwenye ukumbi wa sinema. Mara nyingine tatu tulipokaa peke yetu, angeondoka baada ya muda mfupi kwa sababu alipigiwa simu na Linda.”
“Mbona hukuniambia?” Lisa alijisikia vibaya lakini pia alikasirika kwa wakati mmoja. “Basi, sikupaswa kuwa mpole. Ningewapaka zaidi ya hapo.”
“Sikutaka kukuona wewe na Patrick mkipigana,” Pamela alisema kwa huzuni, “Ninampenda sana na nilijaribu kwa muda mrefu kumfanya awe pamoja nami. Pia niliiambia hadi familia yangu kwamba nitampeleka nyumbani Krismasi hii. Ndiye mtu ninayetaka kuolewa naye.”
Lisa alisema kwa hasira, “Ikiwa siku zote anachukua upande wa Linda, inawezekana kwamba mtatalikiana hata mkifunga ndoa.” Hii ilimshangaza Pamela. Alionekana kuchanganyikiwa kabla ya kutikisa kichwa polepole. “Usifikirie sana kwa sasa. Zimisha hisia zako na pombe. Nitakupeleka nyumbani baadaye.” Lisa alimshika mikono na wakatembea kuelekea ukumbi binafsi aliokodisha Sam kwa ajili ya ‘bata’ hilo usiku ule.
Mlango ulisukumwa na mbele yao wakaonekana watu kumi au zaidi waliokuwa wameketi ndani ya ukumbi huo wa kupendeza. Kati ya umati mkubwa, alimjua tu Sam Harrison, Clark Zongo, na mtu aliyeketi kwenye kona ya mbali… Alvi Kimaro. Kiyoyozi kilikuwa kimewashwa. Alvin alikuwa amevaa shati jeupe na ameshika glasi ya mvinyo katika mkono wake wa kushoto. Ilikuwa ngumu kutomtambua mtu huyo aliyeonekana kama mfalme miongoni mwao.
Pia alikuwa katikati ya tahadhari, alikuwa makini zaidi hata katika chumba kilichojaa watu. Hata hivyo, Alvin hakumtazama Lisa tangu alipotokea. Macho yake hayakutilia maanani kabisa ujio wake. Jambo hili lilimtia aibu Lisa. Ghafla, alijutia uamuzi wake wa kwenda pale.
"Halo, warembo Lisa na Pamela!" Sam aliwasalimia kwa shauku. "Nendeni mkakae na Alvin." Baada ya kusitasita kidogo, alimnong’oneza Lisa sikioni, “Alvin hayupo hapa kimawazo. Nenda ukaongee naye.”
Lisa pia aliingiwa na kiburi, kwanini yeye awe wa kwanza kumfuata Alvin? Kwa kweli alishindwa kutembea kumfuata wakati Alvin alikuwa akijifanya hamjui kabisa. Kwa hivyo, Lisa alibaki kama kaota mizizi kwenye miguu.
Kwa bahati mbaya au nzuri, Clark Zongo alimpa ishara na kusema, “Lisa, njoo uketi hapa.”
Watu wengi walimgeukia waliposikia hivyo. Pamoja na hayo, bado Alvin alikuwa busy tu akiongea na mtu aliyekaa karibu yake. Uso wake uligeukia upande mwingine na kumpuuza kabisa Lisa kana kwamba hakuwa na uhusiano wowote naye. Kwa hasira, Lisa alimkokota Pamela kuelekea kwa Clark. "Bwana Zongo..."
"Lisa, njoo tafadhari nina deni kwako. Nimekuwa nikikusudia kukuomba msamaha siku nyingi lakini sikupata nafasi ya kuonana na wewe,” Clark Zongo alisema kwa dhati. "Sikuelewa mara ya mwisho na karibu nikutupe gerezani. Ingawa ulishinda katika kesi ya mahakama, angalau nilipata kujua ni nani hasa aliyekuwa akijaribu kunichezea.”
"Bwana Clark, bila samahani, bila shaka mahakama iliwawajibisha wale wote waliohusika kwa kile kilichotokea."
"Sawa, acha yaliyopita yawe yamepita basi." Wawili hao walipeana toast kabla ya kuanza kujadili mradi wa hoteli ya Lublin.
Kwa pembeni kabisa, Alvin, ambaye aliwaona wakipiga soga na kucheka kwa furaha, alihisi hasira ikipanda ndani yake. Joto la hewa karibu naye lilionekana kuwa limeshuka sana.

Sura ya 105

Wakili aliyekuwa akizungumza na Alvin alihisi tofauti ya ghafla katika mazungumzo ya Alvin na akanyamaza haraka. Alichukua glasi yake ya mvinyo na kwenda kujiunga na mchezo wa pool pembeni.
Sam alimfuata Alvin. Aliketi karibu na rafiki yake na kumwambia taratibu. “Kaka nimeshamkaribisha Lisa hapa kwa wema. Utaacha lini tabia yako ya kumkaushia?"
“Una uhakika hukumwalika hapa kwa ajili ya Clark Zongo?” Alvin alidhihaki kwa kejeli.
“Noo.” Sam hakuwa na uhakika wa kusema. "Kweli, wewe ndiye ambaye hukuonyesha kupendezwa alipojitokeza."
Tabasamu la kujilazimisha likaangaza usoni mwa Alvin. "Hah, achana naye. We endelea na mishe zako tu.”
Wakati huo huo, watu wengine wachache waliingia ukumbini. Alikuwa ni Stephen Kileo pamoja na dada yake, Janet Kileo wakiwa wameambatana na Lina Jones. Sam alishindwa cha kusema. Hakuwa amewaalika watu wale na hakujua walijuaje kwamba ameandaa ‘bata’ kwa ajili ya marafiki zake. Ilionekana kama vile alipanga kualika maadui wakubwa katika chumba kimoja. Alikuwa na utabiri kwamba kitu kibaya kingetokea.
Stephen Kileo alikagua chumba kwa macho makali kabla ya kuelekea kwa Sam. “Bw. Harrison, nilikuwa tu nikitembea na marafiki zangu kwenye ukumbi mwingine. Master Cook akaniambia kwamba wewe pia uko hapa, kwa hiyo nilikuja kukusalimu. Na huyu… lazima awe wakili anayeheshimika, Bw. Kimaro. Nimesikia mengi juu yako na nimefurahi hatimaye kukuona ana kwa ana.”
Alvin hakutetereka, aliendelea kubaki na sura ya dharau na kutojali usoni mwake. Lakini, Sam hakuweza kufanya vivyo hivyo. Ilibidi amjali Janet na kaka yake. Stephen ndiye aliyekuwa kaka mkubwa na mrithi mpya wa biashara za familia ya Kileo, kwa hiyo ilimbidi aonyeshe heshima. Mbali na hilo, familia ya Kileo ilikuwa ikipata nguvu na ushawishi mkubwa wakati huo.
"Hongera, Bw. Kileo, kwa kuchukua biashara ya familia." Sam alimtupia jicho la haraka Lina huku akiweka tabasamu usoni mwake. "Lakini kwa nini uko na mwanamke wa familia ya kutisha ya Jones? Kwani hakuna samaki tena baharini mpaka unaamua kwenda kuvua kwenye vidimbwi?"
Stephen alicheka kwa sauti kubwa kabla ya kumshika Lina karibu na kumbatio lake na kupiga kelele, “Sikilizeni kila mtu, wacha nimtambulishe mpenzi wangu, anayejulikana pia kama binti Jones Masawe—mwenye hisa mkuu wa Mawenzi Investiments.”
Kila mtu aliingia kwenye mjadala mkali. Wote Sam na Alvin walishtushwa na habari hiyo."Hapana, tangu lini Jones Masawe akawa mwenye hisa mkuu wa Mawenzi Investiments?"
“Unadiriki kutudanganya?” Alvin aliuliza.
“Stephen, tuachane nayo,” Lina alisema kwa haya.
“Kwanini? Sio uongo kusema wewe ndiye mwanamke kijana tajiri kwa sasa, kutokana na hadhi yako mpya.” Stephen akambusu Lina shavuni. "Hata sijui niliwezaje kupata hazina kubwa kama wewe!"
"Acha bwana." Lina alishusha macho yake chini huku akionekana kuwa na aibu.
Janet alimtupia jicho Lisa aliyekuwa kando kabla ya kusema kwa sauti, “Ndugu yangu hapa hapakufai. Ukijilinganisha na wengine wewe humu una nini? Humu tunaingia watoto wa matajiri tu kama vile warithi wa Mawenzi Investiments, pesa ni za kusaini tu muda wowote. Na wewe mpaka usubiri kuajiriwa au kupewa vijihela na bwana wako utaweza wapi mambo haya?”
Chumba kikawa na fujo. "Wow, kwa hiyo Lina ndiye atakuwa mrithi wa Mawenzi siku zijazo?"
"Halo, Bi Jones, nilikuwa na mpango wa kukutana na watendaji wa Mawenzi Investiments hapo awali. Tunaweza kupata nafasi ya kuonana na kuongea jambo?” Jamaa mmoja akaona fursa papo hapo.
Lina aligeuza uso wake wenye tabasamu na kusema. “Bila shaka. Msipojali, nyote mnakaribishwa kujumuika nasi katika ukumbi niliokodi upande wa pili.”
“Twendeni.” Stephen alisema kwa bashasha. “Sam Harrison, mnakaribishwa pia.”
Baada ya dakika chache, ni Lisa, Pamela, Alvin, Clark, na Sam pekee ndio walioachwa kwenye ukumbi wa faragha uliokuwa umechangamka sana hapo awali.
“Nakufahamu wewe Stephen Kileo. Unafanya hivi kwa malengo yako, siyo bure, sawa?” Sam alimuuliza Stephen kwa sauti ya chini kabla hajaondoka.

"Nadhani unanijua vizuri. Watu wenye fedha hufuata pesa zilipo." Stephen alimjibu kwa kejeli. "Labda hivi karibuni pia mtalazimika kuniabudu kama kijana tajiri zaidi Masaki nzima, tehtehteheee…”
"Utakuwa unaota kama bado unafikiria kupata mafanikio kwa njia za kijima kama hizo." Sam alimnyooshea kidole Lina na kucheka kwa kejeli. “Mwanamke gani huyu unayejivunia? Alikuwa mchumba wa mtu mwingine mwezi uliopita tu, leo unatutambia kwa mbwembwe utadhani umepata bikira?"
Hasira kali ilujaza uso wa Lina ndani ya sekunde chache. “Sam, chunga kauli zako. La sivyo, mara baba yangu atakapokuwa mwenyekiti wa Mawenzi mwezi ujao, ninaweza kuiangusha familia ya Harrison mapema kabisa.”
Lisa aliyekuwa akisikiliza pembeni alicheka kejeli. “Usijiaibishe sana. Itakuwa aibu kubwa kama hilo halitatokea.”
"Hiyo ni sawa." Pamela alicheka kwa furaha. "Familia ya Jones ina sifa mbaya. Ni bora kutolichafua jina zuri la Mawenzi Investiments pia.”
"Nimekubali," Sam aliingia pia, akicheka.
"Chekeni mnavyotaka, ongeeni yote mnayotaka, ila nitawaona nyote mkifyata mikia yenu baada ya mwezi mmoja tu." Kwa uso ulionyooka, Lina alimshika Stephen kwa kifundo cha mkono na kuondoka kwenye ukumbi ule wa matajiri.
Janet aliyeachwa nyuma, alijisogeza karibu na Alvin huku akitabasamu kwa upole. "Bwana Kimaro, kwanini usiende na sisi? nina machache ya kukuambia.”
Alvin alimtazama tu kwa kejeli. Janet hakujali kuonekana mtovu wa akili. Tangu alipomwona Alvin kwa mara ya kwanza kule kwenye mgahawa wa Grapefruit, kwa kweli alivutiwa naye sana. Hakuwahi kumwona mwanaume mwingine wa kifahari zaidi yake. Pamoja na uzuri wake, Janet aliona Alvin haendani naye kwa hadhi ya utajiri wa familia yake. Hata hivyo, baada ya kujua kwamba alikuwa wakili bora zaidi wa kimataifa, alifikiri kwamba wangeweza kulingana kikamilifu.
"Bwana Kimaro, labda hujui mengi kuhusu familia ya Kileo.” Janet aliendelea kujinadi huku akitabasamu. "Familia ya Kileo ina utajiri wa zaidi ya shilingi bilioni 50 za mali na kwa sasa tunawekeza katika biashara ya mavazi, usafiri, fedha, teknolojia na sekta nyinginezo. Hivi karibuni, tutashirikiana na Mawenzi Investiments, ambayo ni mojawapo ya makampuni 100 yaliyofanikiwa zaidi Tanzania. Siku zijazo kwa kweli naamini tutazipita familia zote tajiri hapa jijini.”
"Pfft." Kicheko kilimponyoka Sam mdomoni bila kupenda. Alitamani sana kumfokea yule binti asiye na haya ambaye alikuwa akijitongozesha kwa mtu tajiri zaidi kuliko familia yake.
Uso wa Alvin ulimsisimka huku akitamani sana kumsukuma yule binti. Harufu kali ya pombe iliyokuwa ikimtoka mdomoni ilikuwa inashambulia pua zake. Hata hivyo, baada ya kumwona Lisa akiwatazama pembeni, aliizuia ile jazba yake na kuibana midomo yake kimya kimya.
Akifikiri alikuwa amepata nafasi, Janet kwa ujasiri alilaza kichwa chake kwenye bega la Alvin na kumwambia kwa mahaba. "Ikiwa uko tayari kuwa mtu wangu, utakuwa na pesa nyingi kuliko utakayopata maisha yako yote kwa kufanya kazi kama wakili."
Macho ya Alvin yaliganda. Janet akajua hiyo ilikuwa ni ishara ya kueleweka, akazidi kumnong'oneza sikioni, "Lisa hakufai, yeye sio maskini tu bali pia mjinga. Mimi ni bora kuliko yeye.”
Mkono wake ukasogea taratibu kwenye kifua cha Alvin. Lisa hakuweza kutazama tena kwani hisia kali za hasira zilimpanda. Alichukua glasi ya mvinyo na kumkimbilia Janet kabla ya kumtupia usoni. Vipande kadhaa vya barafu hata vilitua kwenye kichwa chake.
"Ah, Lisa Jones! Umerukwa na akili!” Janet alipiga kelele kwa hasira na akasimama kwa nguvu. Mara moja akatoa leso ili kujifuta uso na mwili wake.
“Nadhani wewe ndiye uliyerukwa na akili. Ni dhahiri kwamba uko kwenye joto, kwa hivyo ninakusaidia kukupunguzia joto." Lisa akakaa mapajani mwa Alvin kabla ya kusema kwa ujeuri, “Ninakuonya kuwa kaa naye mbali, huyu ni mtu wangu. Nitakukata mkono ikiwa nitakuona ukimgusa tena.”
“Mtu wako?” Janet alicheka kana kwamba ameambiwa utani. “Ulikuwa umekaa mbali naye sana hapo awali, una uhakika kuhusu hili? Mapenzi ya upande mmoja huishia katika fedheha wakati mwingi.”

Lisa alikosa kujiamini kwa sababu muda wote Alvin alikuwa kimya. Hata hivyo, kejeli za Janet zilimfanya asiwe na chaguo zaidi ya kumlinda mtu wake. Wakati huohuo, sauti kali ya Alvin ilisikika nyuma yake. “Hebu tokeni nje.”

TUKUTANE KURASA 106-110

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI............LISA
KURASA.......106-110

Sura ya 106

Rangi zote zilitoka kwenye uso wa Lisa ndani ya sekunde chache, akidhani kwamba kauli hiyo ilimlenga yeye pia.
“Ninamaanisha wewe.” Alvin aliinuka taratibu, akaupanua mguu wake mrefu na kumpiga teke Janeth kwenye kochi.
Kila mtu alishtuka. Binti huyo alipiga kelele, "Alvin Kimaro, unafikiri wewe ni nani?! Unathubutuje kunipiga teke! Sitakucha kwa hili.”
“Oh, kweli? Ngoja nione basi.” Akiwa na sura ya kuchukizwa usoni mwake, alinyakua kitambaa kutoka mezani na kujifuta bega kwa uangalifu ambapo Janeth alikuwa ameegemeza kichwa chake muda mfupi kabla.
Hasira ndani ya moyo wa Lisa ilitoweka ghafla baada ya kuona vile. Angalau Alvin alifanya jambo sahihi. Vinginevyo, angeweza tu kumchukia milele.
“Alvin, utajuta kwa hili. Ngoja uone. Siku moja, utakuja kuniomba mwenyewe nilale na wewe.” Janet aliuma meno na kuondoka baada ya kudhalilishwa.
Sam alimkaripia yule binti, “pumbavu! Unadhani unastahili kulala na Alvin wewe? Takataka! Rundo la kinyesi wewe!”
Pamela na Clark walishindwa kuzuia vicheko vyao. Lisa na Alvin pekee ndio walibaki na nyuso zilizonyooka.
“Una hata jeuri ya kusema hivyo? Tazama umati mchafu ulioalika leo.” Alvin alimshushua rafikiye Sam kwa tabasamu la kejeli.
Sura ya aibu iliufunika uso wa Sam. "Sijawaalika mimi wehu hawa wamevamia tu. Bora wameenda, njooni tunywe na tuendelee na furaha. Ni wale wa kweli tu ndio waliobaki humu.” Aliongoza na kuchagua wimbo. Pamela alimfuata pia na kuchangua nyimbo kadhaa na kuziweka kwenye playlist.
Ukumbi mkubwa ukawa mtupu ghafla. Kwa bahati mbaya, Lisa alikuwa ameketi kati ya Alvin na Clark. Uso wake ulitiririka kwa aibu. Kweli, alikuwa amedai hadharani tena kwa kiburi kwamba Alvin alikuwa mtu wake muda si mrefu. Oh hapana…
"Sogea karibu." Alvin akapapasa nafasi iliyokuwa karibu naye huku akimtaka Lisa asogee. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kujisogeza karibu zaidi na Alvin hata wakagusana kabisa. Akamkumbatia mkono mmoja na kumshika kidevu kwa mwingine. "Ulitangaza mapema kwamba mimi ni mtu wako?" Alisema, akiinua macho yake kumtazama.
Lisa alihisi mashavu yake yakiwaka moto. Alipotazama moja kwa moja ndani ya kina cha macho yake yenye giza, hakuweza kujua ni nini kilikuwa akilini mwa Alvin, lakini alimtazama na kusema, “Hiyo ni kweli, wewe ni mtu wangu. Nirekebishe wakati wowote ikiwa unaona kuwa hii si sawa. Naahidi sitakusumbua tena.” Hisia ngumu ikaangaza machoni pake. Hakujua kama ahisi hasira au furaha.
Alvin alionyesha kuguswa na kufurahi ghafla. “Sawa, nimefurahi bado unakumbuka msimamo wako. Lakini kwa nini huwa unasahau niliyosema? Kwanini unafurahia kuzungumza na wanaume wengine?"
Lisa alishtuka, akakumbuka alikuwa anazungumza tu na Clark mara baada ya kuingia ukumbini mle. “Clark alikuwa akinishukuru mara baada ya kuniona. Nilitaka kuja kuketi karibu nawe lakini wewe… Kwanza hujafika nyumbani kwa siku chache zilizopita na bado uliendelea kunipuuza hata uliponiona nikiingia. Ulijifanya hunijui kabisa.” Sauti yake ilishuka kuelekea mwisho. Ilionekana kuwa alikuwa na aibu na alihisi kama alikuwa amekosewa.

“Una jeuri ya kusema hivyo? Nachukia sana wanawake wanaponidanganya,” Alvin alisema huku akikoroma. “ Mimi simaanishi Clark Zongo. Nilikuambia usikae karibu na Kelvin lakini hukunisikiliza. Unafikiri ninaweza kukuvumilia na kukusamehe kila mara?”
Hatimaye ikawa wazi kwake. "Unamaanisha tukio la hospitali siku chache zilizopita, ulijuaje?" Aliendelea kuwa na uso ulionyooka ingawa macho yake yalionyesha wazi kutofurahishwa. "Nilikuwa Mbezi Beach wakati huo nilipokea simu kuhusu Aunty Manka. kelvin alikuwepo kwa bahati kwenye saiti kuangalia maendeleo ya kazi. Alinisikia kwenye simu na kuniambia kuwa anamfahamu mtu kutoka hospitalini hivyo alitaka kunisaidia ndo nikaongozana naye. Ni hayo tu,”Lisa alieleza.

Alvin hakujisikia faraja aliposikia hivyo lakini alikata tamaa zaidi. “Hukuja kwangu mara moja ulipohitaji msaada. Badala yake, ulimgeukia mtu ambaye anavutiwa nawe. Lisa Jones, mimi ni nani kwako na Kelvin ni nani kwako?"
“Hapana, nilizungumza na Kelvin na anaelewa pia—”
“Usithubutu kuniambia kwamba anakuona tu kuwa rafiki sasa hivi.” Alitabasamu kwa kejeli. "Kwa hivyo utakuwa sawa na mimi kuwa na urafiki na wanawake ambao walijaribu kunishawishi hapo awali?"
Hilo lilimshangaza. Baada ya kujiweka katika viatu vyake, hatimaye aligundua kosa alilofanya.
"Samahani." Muda mrefu baadaye, aliinamisha kichwa chake. “Nitakupigia simu mara moja nikihitaji usaidizi siku nyingine na sitakubali msaada kutoka kwake tena. Hakika nakujali wewe tu.”
Alvin akamuachia na kuwasha sigara. Alipovuta pumzi na kuzitoa, moshi ukafuka kimya kimya.
Kwa bahati mbaya, aligundua wimbo wa mapenzi ambao Pamela alikuwa ameweka ulikuwa ukiisha. Wazo likamjia akilini. Alikimbilia kwenye mashine ya kucheza muziki na kuuweka wimbo huo kwenye playlist. Baada ya dakika chache, wimbo wa mapenzi uliokuwa ukitamba ulijaza chumba. Kila mtu alijua ni wimbo gani huu na mara akageuka na kumtazama Lisa kwa mshangao.
Mashavu yake yalimtoka kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kujaribu kitu kama hiki hadharani. Hata hivyo, alipoona mwonekano mzuri wa Alvin, alivuta pumzi ndefu kabla ya kuogea hadharani kwa aibu. "Ningependa nitoe dedication ya wimbo 'Tupendane' kutoka kwa Wananjenje, kwa mtu ninayempenda."
Alimtazama Alvin haraka baada ya kusema hivyo. Alvin aliinua macho yake kumtazama. Mwangaza mkali ulioning'inia kutoka kwenye dari ulimwangazia usoni mwake. Aliona mashavu hayo mekundu na macho yaliyokuwa yakimeta kama nyota zinazometa angani usiku. Alihisi kuna kitu kilikuwa kinaonekana moyoni mwake.
Sam alipiga mluzi na kuanza kupiga makofi. “Oh, jamani Lisa! Alvin, umesikia hivyo? Anakiri kukupenda.” Alvin aligeuza uso wake bila kutoa maoni. Alisimama na kumtazama moja kwa moja Lisa.
Lisa alinyanyua kipaza sauti na kukisogeza kwenye midomo yake taratibu.
"Mpenzi wangu, ninaombaa…nikueleze pendo, langu lililo moyoni, moyoni mwanguuu…,
"Mpenzi wangu, Mwenyezi Mungu, muumba ardhi na mbingu, ndiye shahidi wa pendo, mhh…moyoni mwanguuu…
"Mapenzi niiii…kuvumilianaaa…Nami mpenzi, nimekuvumiliaaaa…,
"Mapenzi niii ...Kuaminianaaa….Nami mpenzi nimekuaminiiii…."
Hakuwa amemsikia akiimba hapo awali. Sauti yake tamu na nyororo ilituliza moyo wake na kutoa burudani masikioni mwake. Kusikiliza muziki haikuwa tabia ya Alvin, sembuse muziki wa kiutu uzima kama huu, lakini, alihisi wimbo huo kuwa mzuri sana wakati huo.
Nyimbo iliisha. Ilikuwa huzuni sana kwamba iliisha haraka. Watu wote walianza kupiga makofi. Wote wawili Sam na Pamela walianza kupiga kelele. " Busu, busu, busu ..."
Akiwa na aibui, Lisa alimkodolea macho rafiki yake wa karibu akitamani kwenda kujiunga naye.
"Njoo hapa." Alvin akampungia mkono.
Lisa alitembea kuelekea kwake kwa aibu. Alvin alimweka kwenye mapaja yake, akamshika uso wake mdogo, na kufunga midomo yake kwa midomo yake.
Lisa, akiwa na aibu kufanya hivyo hadharani, alitamani apotee hewani papo hapo. Hata hivyo, alipofikiri kwamba hakuwa na hasira naye tena, alimbusu kwa upendo.
Bila kutarajia, Alvin alipoteza fahamu zake kabisa katika busu hilo. Moyowake uliachilia kabisa chuki za mvutano wote uliokuwa ukijengeka ndani yake katika siku chache zilizopita. Hata hivyo, wengine bado walikuwa wakiwatazama.
Lisa alijisikia kulia kwa aibu. Haraka alitazama huku na huko baada ya busu kuisha, akagundua kwamba wengine tayari walikuwa wameenda upande mmoja kucheza pool.
Sam alicheka na kumwambia. “Njoo ujiunge nasi kwa kuwa umemaliza kumbusu. Tayari tumemaliza mechi chache tangu wakati huo.” Alihisi mashavu yake yakimtoka kwa mara nyingine.
“Hapana,” Alvin alijibu kwa uvivu na kuuzika uso wake kwenye nywele zake ndefu. “Tunaelekea nyumbani.”
"Bado." Lisa alimzuia. "Pamela amekuwa akinywa pombe. Nahitaji kumsindikiza kwenda nyumbani.”
"Atachukua teksi."

Lisa alisita kwa muda mfupi kabla ya kukataa. "Hapana, aligombana na mpenzi wake na niliahidi kumrudisha nyumbani. Siwezi kumpuuza kwa sababu nimekuona wewe.”
Sura ya kukasirika ikaangaza tena usoni mwake. "Unamaanisha nini, mimi si muhimu kuliko rafiki yako?”
"Bila shaka wewe ni muhimu sana, lakini marafiki ni muhimu pia." Lisa aliweka wazo hilo moyoni na kujibu kwa sauti ya kupendeza, “Hey, acha kuwa na haraka kupita kiasi. Hatujawahi kutoka na kufurahi kama hivi, kaa kwanza. Kuna mengi zaidi nataka kukuambia.”
Alvin alilegea na kukaa. Bila kujizuia, Lisa alimweleza yote aliyoyasikia kutoka kwa Aunty Manka katika siku chache zilizopita.
Alvin alitabasamu kwa furaha huku akielewa picha kubwa sasa. "Inaonekana kujeruhiwa kwangu kwenye saiti ya ujenzi mara ya mwisho haikuwa ajali pia lakini mpango kutoka kwa familia ya Jones. Kweli, vizuri, wanathubutuje kunidanganya?"
Mtu wa mwisho aliyemsababishia madhara hakuwa tena katika ulimwengu huu. Wawili hao, baba na binti Jones walikuwa na hamu ya kuishia gerezani. Alvin akatoa simu yake kuitafuta namba ya Hans.
"Unafanya nini?" Lisa aliuliza.
"Nataka kumwambia Hans aandae hati ya mashtaka kwa ajili ya bwana na bibi Jones, nawashtaki kwa mauaji." Kiburi kilionekana katika sauti yake.
“Usifanye kwa kukurupuka. Familia ya Jones Masawe imeanza kupata ushawishi mkubwa kwa sasa na huwezi kumudu kuwashtaki, wanaweza wakakusumbua sana. Mbali na hilo, wanapanga kuunganisha nguvu na familia ya Kileo kupitia ndoa. Wataipiku hata familia yenye nguvu zaidi hapa Masaki kwa sasa, familia ya Harrison.”
Alvin akanyamaza. Eti hawezi kumudu kuwashtaki? Alvin alihisi kucheka.
"Usijali, nitalipiza kisasi." Lisa alimfariji kwa dhati. “Ninapanga kujiunga na Mawenzi Investiments kupigania nafasi ya Mwenyekiti wa bodi iliyo wazi. Nitahakikisha kwamba familia ya Jones inaangamizwa mwishowe na mimi binafsi nimtupe gerezani muuaji wa bibi yangu.”
Alvin alimwangalia Lisa na kumlinganisha na uzito wa maneno aliyotamka. Hakuweza kujua kama Lisa aliongea kwa dhati ama kwa kujiridhisha tu. Hakuongea lolote bali uso wake haukuonyesha imani kwa maneno ya Lisa.
Lisa alikohoa kidogo na kuendelea. "Niamini kwamba nina ushahidi wa 100%. Mawenzi Investiments ilianzishwa na mama yangu na lazima niirudishe. Hilo likitokea… ninaweza kukusaidia kifedha pia ikiwa unataka kustaafu kutoka kwenye kazi ya uanasheria.”
“Umh, sawa. Nitasubiri siku hiyo.” Tabasamu la fumbo lilimwangazia usoni mwake.
Hakika, ikiwa ndivyo alitaka, basi Alvin asingeingilia kati. Hakuweza kusubiri kuona ni kiasi gani alikuwa amekomaa katika miezi michache iliyopita. Baada ya yote, ilibidi akabiliane na familia yake siku moja kwa kuwa walikuwa wamefunga ndoa.
Lisa na Alvin walibarizi pamoja hadi saa tano usiku. Pamela hakuweza kuacha kuangalia simu yake kila baada ya dakika tano. Alikata tamaa kabisa kwamba Patrick alikuwa hajampigia simu tangu wakati huo. Alikunywa pombe nyingi zaidi kuliko kawaida kwa sababu ya hali yake mbaya kimawazo.
Lisa hakunywa sana pia kutokana na kelele za kina Lina waliovamia ghafla. Alvin akawapa lifti ya kwenda nyumbani wale wanawake wawili. Wakiwa njiani, Pamela ghafla alilia kwa sauti kubwa na kuanza kupiga kelele kuhusu mpenzi wake mchafu. Lisa aliingilia kati kumfariji.
Alvin alikuwa akipata maumivu ya kichwa kutokana na kelele za hao wanawake. Kwa hiyo, alikanyaga mwendo na kuongeza kasi ili kuharakisha safari ya kuelekea nyumbani kwa Pamela.
"Asante, ah, asante, mjomba." Pamela alifungua mlango na akatoka nje ya gari kwa uangalifu na miguu yake iliyokuwa imelegea kama mlenda. Hakusahau kumsujudia mwanaume huyo. "Tafadhali mtunze vizuri mpenzi wangu Lisa kila siku, usiwe kama huyu mbwa wa kiume Patrick..."

Sura ya 107

Wakati huo, Lisa alishtuka sana hadi akakosa hata amani. Haraka akasema, “Hiyo ni… Unaweza hata kutembea kweli? nitakupandisha juu.”
“Hapana, mimi si mlevi. Sitawahi kulewa.” Pamela alipunga mkono bila utulivu na kujikongoja hadi jirani. “Mjomba?” Pamela alizidi kumuita Alvin, ambaye aliinua tu macho yake kwa kushangaa.
Lisa alimwambia kumtoa shaka, "ni kwa sababu unafanana kidogo na mjomba wake, kwa hivyo anakuita 'Mjomba' kujifariji."
“Mwambie asiniite hivyo. Sina uhusiano naye.” Alvin akawasha gari, na Lisa akapumua. Kwa bahati nzuri, hakushuku chochote. Pamela alikuwa kimwita Alvin mjomba kwa maana ya mjomba wa Ethan.
Wakati wa kurudi nyumbani, pombe na usingizi vilimkamata Lisa kwa pamoja. Akalala kama pono. Baada ya muda usiojulikana, alihisi kuna mtu akimbeba kwa upole. Alifumbua macho kwa kuduwaa na kuona wazi uso mzuri. Akifikiri alikuwa anaota, aliinua midomo yake minono na kuizungusha mikono yake shingoni.
“Alvilisa, usikasirike, sawa? Nimekukumbuka sana siku hizi chache. Nimechoka. Mambo mengi yametokea hivi karibuni na ninataka mtu wa kuzungumza naye. Nina wewe tu sasa. Utakuwa karibu nami kila wakati, sawa?"
Kisha, alilia ghafla huku akimkumbatia. Machozi yake yalishuka shavuni mwake na kutiririka shingoni mwake. Alvin alipigwa na butwaa. Pengine alichanganyikiwa baada ya kuzinduka na kudhani bado hajarudi. Moyo wake ulijawa na dalili za maumivu. Lazima siku hizo chache alikuwa na msongo wa mawazo sana. Baada ya yote, bado alikuwa mwanamke. Mambo mengi sana yalimtokea lakini hakuwa karibu naye. "Ndio, nitakaa karibu nawe kila wakati," alinong'ona sikioni mwake.
Sauti ya upole ya Alvin ilimtuliza taratibu Lisa. Alifumba macho na kulala begani mwake. Alvin alimbeba juu juu na kumuweka kitandani taratibu. Kuangalia mashavu yake laini, akahema. Alikuwa amechoka kabisa wakati huo. Siku chache alizokuwa hayupo hakulala hata kidogo.
Wakati anakaribia kwenda kuoga, kuna mtu aligonga mlango polepole nje. Alifungua mlango na kumuona Hans akiwa amesimama nje, akamwambia kwa sauti ya chini, "Kuna kitu kimetokea."
Alvin alitoka nje ya mlango, na Hans akamkabidhi picha ya mtu fulani. "Nilipata habari kwamba Zigi Kabwe amefika Dar es Salaam kukutafuta. Naamini yuko hapa kulipiza kisasi cha dada yake tena.”
"Alijuaje kuwa niko Dar?" Mwanga wa tahadhari ulimulika machoni mwa Alvin.
"Ulikuja Dar na kushughulikia kesi kadhaa kubwa, haswa kesi ya Kibo Group ambayo ilivuma sana. Ingawa nimejaribu kuficha sana jina lako,8 lakini mitandao sasa imeenea mno…” Hans alikunja uso na kutafakari kabla ya kusema, “Mtu huyu amekuwa akikusumbua tangu miaka mitano iliyopita. Kwani huwezi ku…”
“Hakuna haja.” Alvin alikunja uso na kumkatisha.
Hans alikuwa na wasiwasi. "Ninajua unaweza kufikiria moyoni mwako jinsi anavykuchukia kwa sababu ya kesi ya dada yake, lakini yeye ni- ... Yeye ni hatari sana na ameapa kulipiza kisasi kwa mtu unayempenda. Lisa atakuwa hatarini.”
"Mletee mtu wa kumlinda." Alvin aliamuru.
Siku iliyofuata, Lisa aliamkaalibadilisha nguo zake za kulalia na kushuka chini. Aliona kwamba kulikuwa na mwanamke kijana mwenye nywele fupi na umbo thabiti.
“Habari, Bi Jones. Mimi ni mlinzi wako, Shani. Nitawajibika kwa usalama wako kuanzia sasa.” Lisa alipepesa macho na kumtazama Alvin aliyekuwa amekaa pembeni. “Umenitafutia mlinzi?”
“Mmh, familia ya akina Jones inapanda tena. Huna bahati, kwa hivyo nitakuwa na amani zaidi ikiwa kuna mtu kando yako." Alvin hakumwambia ukweli, asije akakasirika siku nzima. kuna jambo alikuwa akimficha Lisa.
"Alvlisa, wewe ni mzuri sana kwangu." Lisa alikumbuka mara ya mwisho alipoangukia kwenye mtego wa Lina. Baada ya kufikiria kidogo, hakukataa.
“Ni vizuri kwamba unajua. Macho ya Alvin yalikuwa ya upole, lakini yakawa makali tena alipomgeukia Shani. “Mlinde vyema. Ikiwa mtu yeyote ataweka mkono juu yake, utawajibika kabisa. Pia, nijulishe ikiwa mtu wa jinsia tofauti atamkaribia.”
Shani akaitikia kwa kichwa. “Imeeleweka.”
Kwa pembeni, Lisa alikosa la kusema. "Unanipeleleza tu kwa kisingizio cha ulinzi, sivyo?"

Alvin alibana mashavu yake. “Sitaki upate shida, bado nasubiri kwa hamu kustaafu kazi yangu baada ya wewe kuipata Mawenzi Investiments.” Sauti ya sumaku ilimfanya Lisa ashindwe kabisa kusema lolote.
Baada ya Alvin kwenda kazini, alimuuliza Shani huku akitabasamu, “Unamfahamu Alvilisa?”
Aliposikia jina la 'Alvilisa', Shani alitabasamu na kujibu kwa heshima, "Ndiyo."
Lisa alitazama huku na huku na kuuliza, “Basi lazima ujue kama amewahi kuwa na mpenzi zamani. Amekuwa nao wangapi na…"
“Bi. Jones, unaweza kumuuliza Bw. Kimaro kuhusu hili wewe mwenyewe.” Shani aliifuta mada hiyo kwa maneno machache. Lisa alikata tamaa ghafla. Mlinzi huyu alionekana kuwa na msimamo sana.
Baadaye siku hiyo, Lisa alijiuzulu kazi yake huko kwenye kampuni ya zamani na kufanya maandalizi yake kwa ajili ya kujiunga rasmi na Mawenzi Investiments.
Nako katika makazi ya Jones, Jones Masawe alikuwa katika hali nzuri baada ya kupokea simu kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya Mawezi Investments. "Mwenyekiti Amiri hatimaye alikubali kuniunga mkono. Nafasi ya mwenyekiti itakuwa yangu kesho.” Jones alimwambia mkewe.
"Mpenzi, pongezi." Mama Masawe alitabasamu kwa kiburi. Habari za hadhi ya Jones kuwa mwenye hisa mkuu wa Mawenzi Investiments zilikuwa zimeenea kila mahali, hivyo wanawake wale matajiri waliokuwa wakimdharau walikuwa wanakimbilia na kumtamani tena. "Unapochukua nafasi ya mwenyekiti na Lina na Stephen watakapooana, familia yetu ya Masawe itasimama kileleni mwa matajiri wa jiji hili."
"Hiyo ni sawa. Muda mrefu tulikuwa tukiongozwa na familia za Harrison na Zongo, lakini hivi karibuni, tutazipita na kuwa familia yenye nguvu zaidi hapa Masaki.” Jones alizidi kuibuka mshindi kadiri alivyozidi kuwaza juu yake na hakuweza kujizuia kuangua kicheko.
Lina naye akacheka. “Baba umeshampata Aunty Manka? Yeye ni bomu linalosubiri kulipuka. Atatuharibia usipoangalia"
“Ndiyo, yule mwanamke mzee anajua mambo mengi sana,” Mama Masawe alisema kwa haraka.
"Kwa hivyo hata kama anajua mambo? Mimi ndiye niliye madarakani sasa. Lisa ni msichana mdogo tu. Anaweza kunifanya nini?” Jones alidhihaki bila kuweka umuhimu wowote kwa watu hao hata kidogo. "Hata kama ana Alvin Kimaro nyuma yake, ninashuku kuwa Alvin hatabaki hai kwa muda mrefu."
"Baba, huyu Alvin hata asikutishe, habari zimeenea kuwa anatafutwa na mtu hatari anayeitwa Zigi Kabwe." Lina aliachia tabasamu la ajabu. “Tangu kifo cha dadake, anamchukia sana Alvin kiasi kwamba hatamuacha hadi amuue. Kusudi lake lote la kuishi ni kumuua Alvin Kimaro.”
"Hiyo ni habari nzuri sana." Jones alimpa tano za kumsifu. "Endelea kupeleleza habari zake, kama atamuua atakuwa ametusaidia sana." Lina hakuweza kuficha furaha yake. Baada ya kumiliki Mawenzi investiments, angekuwa sosholaiti nambari moja jijini Dar es Salaam. Hakutaka kuvumilia tena wengine kumdharau.

Sura ya 108

Siku iliyofuata saa tatu asubuhi, mkutano wa mwaka wa wanahisa wakuu ulifanyika. Jones Masawe alifuatana na Lina wakaingia ukimbini kwa hatua kubwa. Alipokelewa na watu wote waliosalimiana naye kwa kupeana naye mikono.
“Mwenyekiti Jones, hongera! Ninaamini nafasi ya mwenyekiti itakuwa yako mara mwenyekiti Amiri atakapoondoka madarakani.” Mwanahisa mmoja alimpokea Mzee Jones Masawe kwa bashasha.
"Unasema nini? Ndo kwanza nimejiunga na Mawenzi Investiments na bado sijaelewa kabisa mambo ya ndani yanavyofanyika,” Jones alijibaraguza kwa unyenyekevu huku akizuia nia yake isijulikane.
“Una nini cha kukuzuia? Hivyo ndivyo watendaji tunaowaajiri kwa mishahara mikubwa wanavyokufikiria” mtu mwingine alisema kwa kujipendekeza, “Maendeleo ya baadaye ya kampuni yanakutegemea Mwenyekiti Jones sasa.”
“Ndiyo, ndiyo, Mwenyekiti Jones. Hata mimi na familia ya Levy tutakuwa tunakutegemea wewe na Mawenzi Investiments,” Bwana Levy pia aliunga mkono.
"Hakuna shida, kama ndivyo mlivyoamua." Jones hakuweza tena kuzuia sura ya furaha usoni mwake na kucheka.
Mwenyekiti aliyekuwa anaachia ngazi, Amiri Gumbo, alikunywa chai ili kulainisha koo lake na kuuliza, "Kila mtu amefika?"
"Kila mtu amewasili, isipokuwa hakuna mwakilishi wa KIM International inayomiliki asilimia 2`5[ ya hisa, labda na BwanaChris Maganga. " Bwana Issa Kawe, katibu wa bodi, alisema, "Lakini kila mtu anajua kwamba KIM International kamwe haishiriki katika masuala ya kampuni na inasubiriaga tu gawio la faida, na Chris Maganga huwa hahudhurii mkutano wa wanahisa kwa sababu anaishia mbali. Kwa hiyo hatuna haja ya kusubiri"
"Kwa hali hiyo, acha kikao cha bodi kianze." Mwenyekiti Amiri aliidhinisha.
Mwenyekiti wa bodi na kiongozi wa mkutano, Mzee Amiri alisema, “Sasa nina umri wa miaka 70 na afya yangu si nzuri kama ilivyokuwa zamani. Nataka kuachia nafasi yangu nijali afya yangu, hivyo nafasi ya mwenyekiti lazima ijazwe na mtu mwenye uwezo. Kwa bahati ni kwamba mwaka huu, Bibi Mkubwa Masawe alifariki na 60% ya hisa zake zilipitishwa kwa mtoto wake, Jones Masawe. Katika siku zijazo, atakuwa mwenye hisa mkuu wa kampuni na atakuwa na mamlaka kamili ndani ya bodi. Kwa hiyo tunaweza kufikira kumwachia kiti hiki cha mwenyekiti kama hamtajali.”
Chumba cha wanahisa mara moja kilimtazama Jones Masawe kwa wivu. Uso wa Jones ukanyanyuka juu kwa sifa.
Bwana Levy, mmoja wa wanahisa, akatabasamu na kusema. "Mwenyekiti Jones yuko katika umri wake wa dhahabu na ni mkomavu na thabiti. Naamini ni bora achukue nafasi ya mwenyekiti.”
"Ndio, tunakubali." Ukumbi mzima ukaripuka kwa makofi.
“Acha awe Mwenyekiti Jones. Anafaa kwa nafasi hii." Maneno ya watu fulani yakasikika. Chumba kikubwa cha mikutano kilijaa kila aina za sauti za kuunga mkono.
Mwenyekiti Amiri Gumbo aliitikia kwa kichwa na kusema, “Kwa kuwa huu ni uchaguzi, bado tunapaswa kufuata utaratibu wa kawaida. Kila mtu anayemkubali Jones Masawe anyanyue mkono wake juu."
Wanahisa wa bodi waliinua mikono yao, na Mwenyekiti wa mkutano akahesabu. “Kura kumi kati ya wanahisa 15. Inaonekana kama nafasi yangu ni ya Bwana Jones sasa. Hapana, nikuite Mwenyekiti Masawe sasa hivi.”
Jones Masawe aliinuka na chemchemi ya majivuno katika hatua yake. "Asanteni kwa ushirikiano wenu. Kwa kuwa mmeniamini na kuniwezesha kuchukua wadhifa wa mwenyekiti, bila shaka nitaifikisha Mawenzi Investiments hadi kwenye orodha ya makampuni 10 bora Tanzania, au hata 100 bora Afrika. Nitamwezesha kila mtu kupata faida nzuri zaidi kila mwaka.”
"Tunaimani na wewe." Kila mtu aliinua mikono yake na kupiga makofi.
Mwenyekiti Masawe hakuweza kuacha kutabasamu. Mwili wake wote ulionekana kuelea kwenye ombwe la furaha. Alikuwa mwenyekiti wa Kibo Group kwa nusu ya maisha yake, lakini Kibo Group haikuwa chochote ikilinganishwa na hadhi ya Mawenzi Investiments. Katika siku za usoni, Dar yote ingekuwa chini ya miguu yake.
Na wale ambao hawakumpigia kura siku hiyo …! Akamgeukia Lina na kusema, “Niandikieni majina ya wale ambao hawakuniipiga kura.”

“Usijali, Baba. Nimeandika majina yote.” Lina alijibu kwa jeuri kama ya baba yake. “Baba naweza kuwa na nafasi ya meneja mkuu wa kampuni? Sihitaji tena kuwa meneja wa mradi wa ukuzaji mali, ni nafasi ndogo sana kwangu hiyo.”
“Kuwa na subira. Nitalizungumza kwenye kikao baadaye.” Baba yake hakumvunja moyo.
Lina alitetemeka kwa furaha. Katika siku zijazo angekuwa binti mdogo mwenye utajiri wa thamani ya makumi ya mabilioni ya shilingi. Mtandao mzima wa watu mashuhuri nchini ungekuwa kituo chake, achilia mbali Dar es Salaam. Kwa Lisa, angekuwa mchwa tu.
“Mwenyekiti Jones, kaa kiti changu. Mahali hapa ni mali yako sasa." Mwenyekiti mstaafu, mzee Amiri akainuka. "Mkutano unaofuata wa wanahisa utakuwa mikononi mwako."
"Mwenyekiti Amiri, wewe ni mwema sana." Mwenyekiti Jones alisema kwa furaha, na miguu yake mara moja ikasogea kuketi.
Ghafla, mlango wa chumba cha mkutano ulifunguliwa kwa kishindo, na mzee wa makamo aliyevalia suti nyeusi akaingia ndani akionekana mwenye nguvu na mamlaka. Nyuma yake, mwanamke kijana alimfuata. Suti yake ya kifalme ya bluu ilifunika ngozi yake nzuri, na nywele zake ndefu ziliwekwa juu ya mabega yake. Haiba yake ilisisitiza sifa zake za kupendeza. Uso wake mdogo haukuwa na hisia, lakini ulibeba tu hali ya tahadhari kwa mwonekano wake. Wakati huo, nyuso za Jones na Lina zilibadilika papo hapo.
Lina akapiga kelele kwa nguvu, “Lisa, unafanya nini hapa? Toka nje! Hii ni mali ya Mawenzi Investiments. Nani alikuruhusu kuingia humu? Ondoka sasa hivi!”
Sauti yake ilikuwa ya kiburi, lakini Lisa naye alikuwa ameshiba dharau huku Chris Maganga akiuliza, "Kwani nimepoteza haki yangu ya kuleta mtu kwenye mkutano wa wanahisa kwa sababu tu sijaja kwenye kampuni kwa miaka michache?"
Jones Masawe alihisi tu kwamba mtu huyo hakuwa mgeni machoni pake, lakini hakumtambua. Mwenyekiti aliyetoka madarakani Amiri alisimama na kusema, “Bwana Maganga, si unaishi Mwanza kwa sasa? Kwanini umekuja ghafla kwenye mkutano wa kampuni leo?”
Uso wa Lina ukapoa. mara moja akawa ametambua kwamba huyo ndiye mwenyehisa ambaye alionekana mara chache sana kwenye kampuni, Chris Maganga. Hata hivyo alikuwa na 10% tu ya hisa ukilinganisha na baba yake aliyekuwa na 60%. zaidi ya hayo, Jones Masawe alikuwa tayari ni mwenyekiti wa Mawenzi Investiments, hivyo Lina hakuwa hata na tone la wasiwasi moyoni mwake. Hakuonyesha heshima yoyote kwa Chris na alimdhihaki bila kujali, akisema, "Ni kweli, unaweza kuingia kwenye mkutano kama mwanahisa, lakini huwezi kutumia nafasi yako kuleta takataka." Alimtazama Lisa baada ya kuongea.
Lisa aliinua ndita zake na kucheka. “Unajizungumzia wewe mwenyeweee, au kuna takataka nyingine?”
"Lisa, bado unaota?" Lina alidhihaki, “Baba yangu sasa ni mwenyekiti wa Mawenzi Investiments. Ninaweza kuja hapa wakati wowote ninapotaka. Unafikiri wewe ni nani?”
“Hata sijapiga kura. Ilikuwaje akawa mwenyekiti mpya?" Chris akaburuta kiti na kuketi.

Sura ya 109

Mwenyekiti Jones alimdharau Chris. “Inaonekana kwamba Bwana Maganga hajaridhika nami, lakini tayari kuna watu kumi katika kampuni ambao walinipigia kura. Hata ukipiga kura haina maana.”
“Ndiyo.” Mwenyekiti mstaafu Amiri alijisikia vibaya. “Bwana Jones ndiye mwenyekiti mpya. Hakuna anayeweza kubadilisha hilo. Kura moja haitabadilisha matokeo.”
“Pia ndiye mwanahisa mkubwa ambaye anamiliki asilimia 60 ya hisa. Unawezaje kujilinganisha naye?” Baadhi ya watu walianza kudhihaki.
Mwonekano wa Mwenyekiti Masawe ulikuwa wa kiburi. "Bwana Maganga, ikiwa uko hapa kuleta shida, usinilaumu kwa kuagiza walinzi wakutoe nje."
"Nani alisema wewe ndiye mwenyehisa mkubwa?" Chris akatabasamu. "Una 30% ya tu ya hisa."
Jones alikunja uso. "Mama yangu alipofariki, nilipewa 60% ya hisa."
"Si zako." Chris akazitupa zile nyaraka zilizokuwa mkononi mwake mezani. “Bibi Mkubwa Masawe alitoa wosia kabla hajafa. Baada ya kufa, Lisa Jones atakuwa na 30% kati ya 60% ya hisa. Vipi, unapanga kuchukua kila kitu bila kusema chochote?"
Wakati kauli hii inatolewa, chumba kizima kilikuwa na ghasia. Nyuso za Jones na Lina zilibadilika sana. Mwenyekiti mstaafu Amiri alichukua nyaraka na uso wake ukageuka ghafla. 'Ni kweli. Muhuri na saini ya Bibi Masawe viko juu yake."
“Hilo haliwezekani…” Jones alipiga meza na kusimama.
"Ni nini kisichowezekana juu yake?" Lisa alienda kutazama umati wa watu. "Ninaamini kuwa wanahisa wote wanajua kuwa Mawenzi Investiments ilianzishwa na Sheryl Masawe zaidi ya miaka 20 iliyopita. Mimi ni binti wa Sheryl, na hii ni kampuni ya mama yangu. Babu na bibi yangu walimpa tu 30% ya hisa kwa sababu Jones Masawe alinilea, lakini hajatosheka na anataka kumiliki yote.”
“Funga mdomo wako!” Jones alijaribu kumpiga kofi, lakini kuna mtu alikuwa mwepesi kuliko yeye, Shani alimshika mkono na kumminya kwa nguvu, na kumfanya apige kelele kwa maumivu mara moja.
"Wewe ni nani? Niache mara moja, la sivyo!” Jones Masawe alijitetea kinyonge.
"Ukithubutu kumpiga mwajiri wangu tena, nitakuvunja mkono." Shani alionya kwa upole kabla ya kuachilia mkono wake. Jones alipiga hatua chache nyuma. Mkono wake ulikuwa umekufa ganzi kwa maumivu.
Lina alimuunga mkono baba yake na kusema kwa kutokuamini, “Lisa, unazungumzia nini? Kwa ajili ya utukufu na mali, ungeweza hata kumkana baba yako mzazi? Kila mtu anajua kwamba Sheryl Jones hajawahi kuolewa. Angewezaje kupata binti? Umekuwa wazimu?"
“Sivyo ulivyosema hapo awali?” Lisa alimuumbua “Uliniambia mwenyewe kuwa mimi si binti wa Jones Masawe bali ni mtoto wa kuokota kwenye vituo vya watoto yatima.”
Macho ya Lina yaliangaza kwa dhihaka. “Nilikuwa naongea upuuzi tu wakati ule. Wosia wa babu na Bibi unasema waziwazi.”
Mwenyekiti Amiri alitikisa kichwa tena kinyonge. "Ndio, imeandikwa kweli kwamba Lisa Jones ni binti wa Sheryl Masawe."
Jones Masawe alikunja ngumi kwa nguvu na kusema. “Hata kama ni kweli, hisa zote zimehamishiwa kwenye jina langu. Ni upuuzi kuendelea kuongea. Kikao hiki cha bodi hakiwezi kubadilisha ukweli kwamba mimi ni mwanahisa mkuu.”
“Nani alisema kwamba hisa zote zimehamishiwa kwa jina lako?” Lisa alitabasamu kijeuri. “Hujatazama? 30% ya hisa zimehamishwa kwa jina langu kwenye Idara ya Viwanda na Biashara.”
Uso wa Jones ukabadilika. Hakuweza kuvumilia tena na akachukua simu na kupiga moja kwa moja kwenye idara ya viwanda na biashara. Chini ya dakika moja tu baadaye alimgeukia Lisa kwa macho makali, hakutaka kingine zaidi ya kumchuna ngozi akiwa hai.
Lisa akaugeukia umati. “Imekuwa bahati sana. Bibi yangu alifariki ghafla baada ya kupooza ghafla pia. Taarifa za kifo chake niliambiwa na mtu baki, na ni kitambo kifupi tu baadaye nikagundua kuwa nina uhusiano na Mawenzi Investiments. Vinginevyo hisa zangu zote zingekuwa mali ya mjomba.”
Umati wote ukalipuka kwa minong’ono. “Mungu wangu, inaonekana kwamba kuna kitu cha ajabu juu ya kifo cha Bibi Masawe.”
"Hiyo ni kweli. Yule bibi alikuwa mwenye afya nzuri tu nilipomuona siku si nyingi...”
“Tsk, kweli hafai. Alikuwa ni mama yake mzazi!”
“Lazima tumwepuke mtu huyu. Anatisha!”
Mtazamo wa kila mtu kwa Jones ukabadilika.

Jones aligonga meza kwa hasira. “Lisa Jones, jaribu kuongea upuuzi tena uone!”
“Mjomba, sijakutusi. Kwanini unajihami sana? Kweli hauna hatia kwenye hili?” Lisa alipaza sauti kwa macho makali. “Lakini sikuamini kabisa kama ungemuua mama yako mzazi. Kama ulimuua, bibi yangu hata kuacha uishi kwa amani.”
Jones alikurupuka na kutokwa na jasho baridi. Haraka alibadilisha mada katika hali mbaya. “Unapanga kufanya nini hapa?”
"Bila shaka, ni kugombea dhidi yako kwa nafasi ya mwenyekiti." Lisa alimtazama kila mtu. "Sasa nina 30% ya hisa, sawa na Jones Masawe, kwa hivyo ninastahili kushiriki."
"Lazima una wazimu." Jones alionekana kama amesikia utani mkubwa. "Una miaka mingapi? Wewe ni msichana mdogo tu mjinga. Huna uzoefu na huna uwezo. Nani atakuwa na imani na wewe kukukabidhi kwa hiari kampuni kubwa kama hii?”
"Hiyo ni sawa." Bwana Levy akaitikia kwa kichwa. "Hatutaki kuingilia ugomvi wako na familia ya Jones, lakini kusimamia kampuni sio mzaha."
“Ndiyo, Mawenzi Investiments haikosi watu. Hata iweje, huyu binti mdogo hawezi kuwa mwenyekiti.” Baadhi ya wanahisa walikunja uso na kupinga. Jones Masawe aliridhika sana na akaketi tena na kunywa chai yake. Baada ya yote yaliyosemwa na kufanyika, ilionekana kuwa nafasi ya mwenyekiti bado ilikuwa ni yake.
"Kwanini siwezi kuwa mwenyekiti?" Lisa aliuliza bila kuhangaika, “Kama sote tunavyojua, Jones Masawe aliwahi kuwa mwenyekiti wa Kibo Group aliyorithi kutoka kwa babu, lakini chini ya uongozi wake, Kibo Group ilisusiwa na mtandao mzima wa wafanyabiashara na hata ikamlazimu kuiuza kwa hasara. Mtandao bado unazungumza juu yake sasa. Sifa yake imeharibika kabisa na hakuna anayemwamini. Aliongoza kampuni hiyo kupokea hongo, huku ufisadi na visasi vingine vikiwa vimeshamiri. Ikiwa ataiongoza Mawenzi Investiments, ulimwengu wa nje utatilia shaka ubora wa bidhaa na mali za Mawenzi Investiments.” Taarifa hii iliposemwa, wanahisa kadhaa walikubali kwa kutikisa kichwa. Uso wa Jones ulizidi kuwa mgumu huku akimkazia macho Lisa, hakutaka kitu zaidi ya kumla akiwa hai.
Lina alisema kwa hasira, “Bado una ujasiri wa kusema hivyo! Kwani sifa ya Kibo Group ingeharibika ikiwa si wewe? Yote ni makosa yako."

Sura ya 110

Lisa alicheka kwa madaha. “Ndiyo, mimi ndiye niliyeibua ufisadi wa mpwa wa mtu fulani. Aliingiwa na pupa ya tamaa ya pesa kuanza kuharibu miradi ya ujenzi kwa kutumia vifaa feki akishirikiana na wewe Lina. Huwezi hata kujenga nyumba lakini sasa unataka kuwa mbunifu. Nani atathubutu kukubali mradi uliobuniwa na wewe?"
"Ndio, hiyo haitafaa." Bwana Haruna, mmoja wa wanahisa alikuwa wa kwanza kupinga hadharani dhidi yake.
“Nataka kutafakari upya pia. Hatuwezi kuharibu sifa ya Mawenzi Investiments.” Mwanahisa mwingine akadakia.
Wanahisa walipoanza kurudi nyuma, Lisa alisema kwa sauti ya upole kwa kila mtu, “Ni kweli kwamba mimi ni mdogo, lakini nina mawazo wazi na makini. Ikiwa sijui chochote, naweza kuwauliza wazee wangu waliopo hapa kwa ushauri. Haikuwa rahisi kwa Mawenzi Investiments kufikia kiwango ilichopo. Haijalishi ni faida ngapi ambazo Jones ameahidi kwa kila mtu, lengo letu kuu ni kukuza faida ya kampuni ili tupate gawio bora zaidi.
“Ndiyo hivyo,” hatimaye Chris alizungumza. Sauti yake ilikuwa na mamlaka sana. "Wasifuwa bosi wa kampuni kubwa kama hii ni muhimu sana. Nitamuunga mkono kikamilifu Lisa ikiwa atakuwa mwenyekiti. Kila mtu anapaswa kujua kwamba niliwahi pia kumsaidia Sheryl. Ni shukrani kwa Sheryl kwamba Mawenzi Investiments ndivyo ilivyo leo.”
"Bado tunaamini katika uwezo wa Bwana Maganga." Bwana Haruna alikubali kwa kutikisa kichwa.
“Kwa hali hiyo, tupige kura tena. Una maoni gani, Mwenyekiti Amiri?" Chris Maganga alimtazama Mkwenyekiti Amiri na kumkumbusha, “Mwenyekiti Amiri, kama ningetaka kushindana na wewe katika nafasi ya mwenyekiti hapo awali, usingekaa kwa furaha hapa leo.”
"Nakubali." Mwenyekiti Amiri alikwepa kumtazama Chris Maganga na kutikisa kichwa. "Wacha tuanze kupiga kura upya."
Kila mtu aliinua mkono wake mmoja baada ya mwingine, na matokeo ya mwisho yalikuwa tisa kwa saba. Lisa ni tisa dhidi ya saba za Jones.
"Wacha tumpongeze Lisa Jones kama mwenyekiti mpya." Chris aliongoza kupiga makofi.
Jones Masawe alipiga meza, uso wake ukiwa na hasira. “Uchaguzi huu si mchezo. Unawezaje kurudia mchakato wa kupiga kura? Ni mimi niliyechaguliwa hapo awali. Unafikiri wewe ni nani?”
"Bwana Jones anaonekana kutoshawishika." Kulikuwa na kitu kingine kilichojificha chini ya tabasamu la Lisa. "Lazima uelewe kwamba kama si ukarimu wa mama yangu, usingekuwa na uhusiano wowote na kampuni hii. Unapaswa kuridhika na ulichonacho.”
“Wewe…!” Jones alimkazia macho. Hakuamini yule binti ambaye aliwahi kuwa adabu sana mbele yake sasa alithubutu kuwa mkaidi mbele yake.
“Ikiwa utaendelea kufanya fujo, ninaweza kuwaita walinzi wakutoe nje,” Lisa alionya bila huruma.
Jones alipandwa na hasira. Kulikuwa na wanahisa wengi hapo, lakini hakuna hata mmoja aliyemtetea.
"Bw. Jones, kaa chini." Mwenyekiti Amiri alihema kwa nguvu. "Tayari tumechelewesha hii kwa muda wa kutosha. Bado kuna mambo mengi tunapaswa kuyashughulikia katika mkutano huu."
"Ni sawa, lakini kabla ya hapo, ni wakati wa watu wa nje ambao hawana uhusiano wowote na mkutano kutoka nje." Lisa alimtazama Lina.
Lina alikuwa akifedheheshwa hadharani, na macho yake yakiwa mekundu, aliongea kana kwamba amedhulumiwa, “Lisa, najua hunipendi, lakini—”
“Nimesema kitu kibaya? Kwani wewe una sifa za kukaa hapa?” Lisa alidhihaki. “Bi. Jones hajui hata sheria za nidhamu za kampuni."
"Inatosha, nenda nje," Mwenyekiti Amiri alisema bila subira.
Lina alijawa kiburi, akatuna kama puto lililopulizwa, lakini hakuwa na ujanja zaidi ya kutoka nje. Mlango wa chumba cha mikutano ukafungwa tena, naye alikasirika sana hivi kwamba machozi yakamtoka.

Muda si muda, Stephen Kileo alimpigia simu. "Lina, hongera! Baba yako lazima awe mwenyekiti mpya wa Mawenzi sasa.” Sikio la Lina lilihisi uchungu kana kwamba alipigwa kofi kali. Stephen hakujua na akaendelea kusema, “Baba yako anapochukua ofisi, mradi wa Nairobi ambao tulijadili mara ya mwisho unaweza kuanzishwa mara moja. Kisha, familia za Kileo na Masawe zitashirikiana kuunda hotel ya nyota tano huko Nairobi. Hivi karibuni, iwe ni Nairobi au Dar es Salaam, itakuwa ulimwengu wetu. Hahahaa, nataka sana kuona nyuso zilizoshindwa za familia za Harrison na Clark sasa…! Hee..Lina, mbona huongei chochote?” Stephen, ambaye alikuwa akizungumza kwa muda, hatimaye alishtuka kwa kuona kimya chake.
"Ni Lisa ndiye ameshinda nafasi ya uenyekiti." Hatimaye Lina akaongea ukweli mchungu.
"Nini?" Stephen akapiga kelele. “Si ulisema una uhakika 90% baba yako atakuwa mwenyekiti? Wewe na baba yako mnafanya nini? Hamwezi hata kumshughulikia Lisa Jones?”
Uso wa Lina ulihisi joto aliposema bila raha, “tungejuaje kwamba angeungana na Chris Maganga? Sisi pia tulishikwa na bumbuwazi.”
“Kweli mambo ndiyo yamegeuka kuwa hivi? Hata nilijitapa nikisema kuwa mpenzi wangu ni binti wa mwenyekiti wa Mawenzi. Ni fedheha iliyoje sasa eeh....! sitaki kusikia hii tena." Stephen alilaani sana.
Sauti ya Lina ilikata. “Stephen, unamaanisha nini kusema hivyo? Sasa unanichukia kwa sababu baba yangu hakupata nafasi ya mwenyekiti?”
Stephen alirudi kwenye fahamu zake ghafla. Hata kama baba yake Lina hakuwa mwenyekiti wa Mawenzi Investiments, mwaka wa gawio ulikuwa unatosha kuwafanya wawe na pesa nyingi mno. Alicheka kwa haraka na kusema, “Bila shaka, usinifikirie vibaya. Nimekasirishwa tu na dhuluma uliyotendewa. Nakupenda wewe, sio utambulisho wako."
“Usijali. Hii ni ya muda tu. Lisa hatakaa katika nafasi ya mwenyekiti kwa muda mrefu,” Lina alisema kwa ukali.
“Uko sahihi. Si rahisi kufanikisha mambo makubwa ikiwa Lisa atakuwa mwenyekiti.” Stephen pia alitabasamu kwa huzuni. "Sitaacha juhudi yoyote kukusaidia."
"Asante." Lina akajibu na simu ikakatwa.
Mkutano uliisha saa sita mchana. Mmoja baada ya mwingine, wanahisa walipeana na mwenyekiti mpya mikono na kuondoka kwa heshima.
"Mwenyekiti Jones, nitakupeleka ofisini kwako." Msaidizi wa mwenyekiti, Tunu Omari, alimjia Lisa kwa hatua kubwa. Alikuwa na tabia njema na mwenye bidii.
“Sawa, nipeleke huko.”
Alikuwa ameanza kuondoka tu wakati Jones alipomzuia njia. Maneno yake yalikuwa ya huzuni na ya kutisha. "We paka malaya, lazima utajuta mwenyewe. Umeweza kuketi kwenye kiti hicho, lakini hiyo haimaanishi kuwa utaendelea kukaa muda mrefu—”
“Paah!” Lisa aliinua mkono wake na kumpiga kofi Jones Masawe bila huruma wala aibu.
Jones hakuwahi kutarajia kitu kama hicho. Alishikwa na machozi na hasira sawasawa. Hatimaye alipojibu, alitoa meno yake kwa hasira na kumkimbilia ili kumfundisha somo. Lakini, Shani alisimama mbele ya Lisa na kumpiga teke Jones, na kumfanya aruke mita kadhaa chini. Hakuweza kuinuka kwa muda mrefu kwa sababu ya maumivu.
“Wewe… Wewe msichana usiye na shukrani! Unathubutu vipi kumpiga mzee? Utapata laana ya Mungu.!" Jones alinguruma kwa hasira.
"Uliniita malaya, kwa hivyo kama mkuu wako, ni kawaida tu kukufundisha somo." Lisa akapuliza kiganja chake kilichokuwa kikiwaka kwa maumivu. “Zaidi ya hayo, kwani wewe na mkeo mmenipiga makofi mara ngapi? Sijafikia hata chembe ya makofi mliyokuwa mkinipiga bila hata kosa.”
“Kwa hiyo tulikuwa tunakuonea? Tulikuwa tunakulea. Tunakudai deni kubwa la shukrani kwa kukulea,” Jones Masawe alisema kwa huzuni.

TUKUTANE KURASA 111-115

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI......... LISA
KURASA....116-120


Sura ya 116

“Ni rahisi sana kupata tena mamlaka," Stephen Kileo alisema ghafla.
Wakishangazwa na maoni hayo, Jones na familia yake walimtazama kwa makini. “Stephen, tuambie haraka wazo lako. Sisi ni familia,” Lina akasema mara moja, “Mara tu Lisa atakapoanguka madarakani, tutaoana mara moja.”
Stephen alikodoa macho na kusema; "Willie Kimaro kutoka familia ya Kimaro anakuja Dar kwa ukaguzi wa miradi waliyowekeza hapa jijini. Kma tutaweza kumfurahisha, tunaweza kumtumia kuwamngusha Lisa.”
Macho yao yote yakang'aa. Willie Kimaro alitoka familia tajiri ya Kimaro. Yeye na Alvin Kimaro walikuwa watoto wa kaka na dada, yaani mtu na binamu yake. KIM International, ni kampuni ya familia ya Kimaro na ilikuwa ikimiliki asilimia 25 za hisa za Mawenzi Investments. Kwa maana hiyo ilikuwa na nguvu kubwa kwenye bodi ya wakurugenzi. Kama kweli KIM International ingeungana na Jones Masawe kumwangusha Lisa, basi angeondolewa kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti na mtendaji mkuu wa Kampuni ya Mawenzi.
Mgawanyo wa hisa katika Kampuni ya Mawenzi ulikuwa ni 30% kwa Lisa, 30% kwa Jones Masawe na 25% kwa KIM International, 10% Chris Maganga na 5% zilizobaki zilimikiwa na wanahisa wengine wadogowadogo. Kwa hiyo wanahisa wakubwa walikuwa wanne, Lisa, Jones Masawe, KIM Internatonal na Chris Maganga. kama wawili kati yao wangeungana basi ilikuwa rahisi kumwangusha mwingine, ndiyo njia aliyotaka kutumia Jones Masawe, kutafuta njia ya kuungana na KIM International kumwangusha Lisa.
Jones alitetemeka kwa fadhaa. "Familia ya Kimaro ndiyo inamiliki KIM International. Ingawa Willie si mzao wa moja kwa moja wa familia ya Kimaro, tutaweza kumtumia kuunganisha nguvu yetu mradi tu tufahamiane na familia ya Kimaro. Ikitokea hivyo, hatutasumbuliwa na Lisa tena.”
"Ni wazo zuri sana." Stephen aliitikia kwa kichwa. “Sifahamiani na Willie lakini najuana na msaidizi wake. Kwa kuwa msaidizi wa Willie nipo naye vizuri, nitajitahidi anisaidie kuwa karibu naye na kuwatambulisha nyinyi kwake. Ili kumteka kwa urahisi mnatakiwa kuandaa zawadi ya kumfurahisha. Willie anavutiwa na vito vya thamani, na pia wanawake warembo!"
“Asante Stephen. Ninajuta kutokutana na wewe mapema. Wewe ndiye ninayeweza kukutegemea kwa sasa.” Lina alimtazama kwa hisia za kuguswa.
"Ni jukumu langu kukusaidia. "Stephen alijaribu kuficha chukizo lake kwake.
••••
Ndani ya Mawenzi Investiments, saa kumi na mbili za jioni, Lisa alipozima taa na kutoka nje ya ofisi, mjukuu wa mmoja wa kwakurugenzi wa bodi ya Mawenzi, Amiri Gumbo alikuwa nje akimsubiria na alipomuona alimsalimia kwa shauku.
“Lisa, unatoka kazini. Ningependa kukukaribisha kwa chakula cha jioni kwenye hoteli maarufu ambayo hutoa chakula kizuri…”
Lisa alikuwa mwisho wa akili yake. Tangu alipoanza kupata tena mamlaka katika kampuni, wakurugenzi wa bodi wote walijaribu kujipendekeza kwake kwa kuwatambulisha watoto wao na wajukuu zao kama washirika wake watarajiwa.
"Nashukuru, lakini nilipanga kula chakula cha jioni nyumbani ... " Lisa alimtosa kwa upole.
“Ngoja basi nikupeleke nyumbani.” Kijana yule aliongea kwa shauku. “Mkoba wako unaonekana kuwa mzito. Acha nikusaidie kuubeba.”
Kabla hajaugusa, Shani alishika mkono wake. Macho ya mwanamke huyo yalimtoka kwa ukali, jambo lililomfanya kijana yule ashtuke. Alikuwa amesikia kwamba mlinzi wa Lisa alikuwa mkatili na hasa stadi wa kupiga watu makofi. “Ikiwa utafanya hivyo kwa mara nyingine, sitasita kukuvunja mkono,” Shani alimwonya kwa ukali.
Kijana yule alirudi nyuma kwa aibu. "Unajua mimi ni nani? Sawa, hata hivyo wewe ni mlinzi tu. Ulinzi ni kazi gani? Hata mbwa anaweza kulinda, kwa hiyo mimi siongei na mbwa, naongea na mwenye mbwa.” Kijana yule aliropoka tu kwa aibu ya kuadhibiwa na mwanamke.
Wakati huo lifti ilikuwa tayari imefika. Kiijana huyo alipoona Lisa anaondoka akamfuata akiwa na maneno ya kuvutia. “Lisa, umesikia kuhusu mkufu wa Malkia? Kuna stori kuwa miaka mingi iliyopita, mfalme alimpa malkia wake mpendwa mkufu. Mtu yeyote ambaye atavaa mkufu huo atafikia furaha katika uhusiano wake. Mkufu huo utauzwa kwa mnada hivi karibuni kule Mlimani City. Nitakununulia, sawa?"

"Hapana Asante. Sihitaji.” Lisa alijibu kifupi. Kijana yule alionekana kumganda kama jojo iliyong’ang’ania kwenye nguo ambayo ilikuwa vigumu kuiondoa.
Mara tu Lisa alipotoka nje ya jengo hilo, aliona mtu aliyemfahamu vizuri akiwa amesimama kwenye mraba. Alijawa na mchanganyiko wa mshangao na furaha. Taa za rangi mbalimbali ziliwaka polepole usiku. Alvin, ambaye alisimama kando ya geti kuu, alikuwa amevalia suti nyeusi na koti la rangi ya parachichi kana kwamba alikuwa ametoka kushiriki katika Wiki ya Mitindo ya Paris. Alionekana mtanashati sana, na sura yake ilikuwa ya kuvutia kweli. Hata hivyo, macho yake meusi yaliangaza kwa huzuni dakika moja alipomwona mtu aliyemfuata Lisa kwa nyuma.
"Alvlisa, kwa nini uko hapa?" Lisa hakugundua mawazo ya Alvin. Alimkimbilia na kuzungusha mikono yake kwenye kiuno chake kwa furaha.
Unyogovu ndani ya macho yake ulipungua polepole. Alimwangalia yule kijana kwa macho mabaya. "Inaonekana nilikuja kwa wakati mbaya, ona sasa nimevuruga miadi yako."
"Yeye ni nani, Lisa?" Yule kijana naye alikasirishwa na Alvin. Huku wote wawili wakiwa wamevalia kifahari, jinsi Alvin alivyokuwa na umbo bora na maridadi ilimfanya yule kijana aonekane mtu wa chini sana.
Alvin alikaa kimya. Aliinua uso wake huku akimwangalia Lisa, akiwaza ni namna gani atamtambulisha kwa mwanaume huyo.
“Ni mpenzi wangu,” Lisa alijibu moja kwa moja. "Ninajua nia ya babu yako, Mzee Amiri Gumbo, lakini tayari ninampenda mtu mwingine. Tafadhali pia mwambie babu yako kuwa nina shughuli nyingi hivyo asitume tena vijana wake kuja kunisumbua. Sina wakati wa kukaa kuongea na vijana wadogo kama nyinyi."
Hakutaka kukata tamaa, yule kijana mjukuu wa Mzee Amiri alisema, “Wewe ni mjanja. Afadhali ufikirie kwa busara. Ukiolewa na familia ya mkurugenzi katika kampuni, itatusaidia sote wawili. Kwa maoni yangu, mpenzi wako hana kitu kingine isipokuwa sura ya mauzo tu. Yeye si mpenzi mzuri kwako.”
Uso wa Alvin ukaingia giza huku mikono ya Shani ikianza kumuwasha na kuchezacheza kwa nguvu, akisubiri tu ruhusa ya bosi wake ili agawe kichapo. Shani alimtazama kijana yule kana kwamba ni mtu wa ajabu sana.
“Asante kwa ushauri wako, lakini ndiye ninayempenda. Nimeanguka katika kumpenda bila matumaini, na ndiye anayestahili upendo wangu. Tafadhali ondoka sasa hivi.” Lisa alimfukuza kwa namna ya kudharirisha sana.
"Kwa kweli hujui ni nini kinachokufaa." Kijana yule alimkodolea macho Lisa kabla hajaondoka kwa kukata tamaa.
Lisa akashusha pumzi. Aligeuza kichwa chake na kukutana na macho ya Alvin yaliyochangamka. Alishtuka kwa kufikiria maneno ambayo alikuwa ametoka kusema yangekuwa yamemuudhi. “Nilitaka tu asiendelee kunisumbua. Usielewe vibaya…”
“Kwani umekosea nini?” Alvin aligeuka ghafla. Akayakazia macho yake huku akitoa tabasamu la busara. “Ina maana unanipenda bila matumaini?”
“Tatizo lenu wanasheria kila kitu lazima mtafsiri.” Lisa akacheka.
“Hili lipo wazi wala halihitaji tafsiri, kwamba unanipenda tu lakini huna matumaini yoyote na mimi, sivyo?” Alvin alidadavua na kumchosha kabisa Lisa. Lisa akakosa la kusema.
Ukimya wake ukamfanya Alvin atabasamu. "Ingia kwenye gari."
Lisa alimwambia Shani aondoke na gari lake kisha yeye akaingia kwenye gari la Alvin. Gari ilisafiri hadi barabara kuu na ili kuondoa upweke, Lisa alijaribu kuanzisha mazungumzo mengine. "Umekula?"
Tumbo la Alvin lilinguruma hata kabla hajajibu. Baada ya kimya cha sekunde mbili, Lisa alicheka. "Ni saa kumi na mbili tu sasa hivi. Mbona tayari una njaa? Hukula chakula cha mchana?”
“Chakula cha ofisini hakikuwa na ladha nzuri,” Alvin alisema kwa hasira, “Ni muda mrefu umepita tangu unipikie. Unafikiri kwamba kuvunjika kwa mkataba ndiyo mwisho wa makubaliano? Kumbuka bado sisi ni wanandoa.”
"Nina mengi kwenye kichwa changu sasa hivi." Lisa alihisi kuchoka kabisa. “Nitatayarisha kifungua kinywa ili uende nacho ofisini kila asubuhi, sawa?”
"Unanichukulia kama mwanafunzi?" Alvin alimkazia macho. Sekunde chache baadaye, aliongeza, "Sawa basi, utakavyopenda mwenyewe." Lisa alikosa la kusema.

Ni mabadiliko ya haraka kama nini katika maisha ya Lisa ndiyo yaliyomnyima raha Alvin. Tangu aanze kufanya kazi huko Mawenzi Investiments, hakuwahi kumwandalia chakula kitamu kama zamani, Alvin ali’miss sana mapishi yake.
“Nisikilize. Tukifika nyumbani usiku huu, ninataka kula nyama ya choma ya nguruwe, saladi ya…”
Lisa alimshika mkono na kupiga kelele za furaha kabla hajamaliza sentensi yake. “Tulia…Acha! Wacha nikupeleke tukale vyakula vya uswahilini usiku wa leo. Ghafla natamani miguu ya kuku, shingo, vichwa, firigisi na vipapatio vya kuku vilivyokaangwa, mihogo ya kuangwa na kachumbari...”
“Una kichaa? Unawezaje kunilazimisha kula takataka za aina hii?" Alvin alishtuka na kukasirika sana hata ndita zake zilikuwa zimejikunja.
“Umekosea kusema hivyo. Watu wengi wanaishi kwa kula aina hii ya chakula, sawa? Weka vizuri kauli zako. Hata kama hupendi lakini mimi nina hamu ya firigisi za kuku zilizokaangwa. Kama mume wangu ni wajibu wako kunisikiliza, haya ndiyo makubaliano yetu mapya!”
Lisa aliendelea kukuna mikono yake. Wakati mkataba ulipovunjika na makubaliano mapya yalipoanza kutumika, msimamo wao katika uhusiano haukuwa kama zamani na ilimbidi Alvin amsikilize. Sasa, angeweza kufanya chochote alichotaka na kula chochote alichotamani na roho yake.
Alvin hakuwa na la kufanya zaidi ya kuendesha gari hadi Coco Beach na kuegesha kando ya barabara. Wawili hao waliingia kwenye vibanda vya wakaanga nyama za kuku pamoja.

Sura ya 117

Msongamano wa wateja wengi waliokuwa wakiingia na kuondoka pale Coco Beach pamoja na harufu ya nyama vilimyima kabisa amani Alvin. Alikosa raha hadi akakunja uso.
“Nenda ukachukue kiti. Chukua kiti hicho kiko wazi..." Lisa alimwambia Alvin aliyekuwa amesimama tu akishangaashangaa. Lisa alionekana kutokuwa mgeni sana kwenye mazingira kama hayo.
Lisa alinyoosha kidole kuwelekeza Alvin kwenye meza tupu ambayo ndo kwanza mteja alikuwa ametoka. Takataka za mabaki zilizokuwa mezani hazikuwa hata zimesafishwa.
"Sitakaa hapo mimi." Alvin alimpiga Lisa jicho kali. Lisa akamfuata na kumsisitiza. Maneno ya Lisa ya kubembeleza yalimfanya Alvin akose la kusema. Kwa hayo, akasogea pale na kuketi kwa kusitasita.
Dakika kumi baadaye, Lisa aliandaa mlo kamili wa familia, ambao ulijumuisha firigisi na kila sehemu ya kiungo cha kuku vikiwa vimekaangwa, mihogo ya kukaangwa, kachumbari na aiskrimu.
“Kula hii firigisi ya kuku, ni tamu.” Lisa alinyakua kipande na kumlisha kwa shauku. Alvin akakwepesha na kusukuma mkono wake pembeni.
"Ngoja nikuonyeshe kitu." Alvin akatoa simu yake na kusogeza hadi kwenye ukurasa unaoonyesha habari mbaya kuhusu nyama za kukaangwa hovyo mitaani. Kisha, akampitishia Lisa.
Baada ya kuangaza macho kwenye picha mbaya ya sahani ambayo ilikuwa na vipande vichache vya vipapatio na zaidi ya miguu kumi ya kuku, Lisa alijawa na karaha. "Alvin, huwezi kupata madhara kwa kula chakula hiki mara moja tu."
"Vitu vya aina hii vina kiasi kikubwa cha viambato vya sumu. Baada ya leo, huruhusiwi kula aina hii ya chakula tena. Wewe hata si mtoto.” Alvin alidhamiria.
Lisa hakuweza kuwa na wasiwasi juu yake. Aliinamisha kichwa chini na kupiga msosi kisawasawa. Baada ya kula vipande kadhaa, aligundua kuwa vingine vilikuwa na ladha mbaya, na badala yake akaviingiza kinywani mwa Alvin.
Huku mdomo wake ukiwa umejaa chakula ghafla, Alvin alimtupia jicho la hasira. Lisa alijifanya kuwa mwadilifu. “Si wapenzi wa kiume hutakiwa kula chochote ambacho wasichana wao huwalisha? Angalia wanandoa kando yetu. Ndivyo wanavyofanya pia.”
Wapenzi vijana walioketi kando yao walikuwa wanafunzi wa chuo kikuu. Baada ya msichana kukerwa kidogo na kipande cha nyama alichokuwa anatafuna mdomoni, alimpa mpenzi wake. “Haina ladha nzuri. Unaweza kula?”
Mpenzi wake naye akajibu, "Unafikiri naweza kusema hapana?"
Lisa naye alikoroma kwa wivu. “Kwanini hutaki kula firigisi niliyoiuma, unanionea kinyaa, huh? Kumbe hunipendi?” Alvin alishindwa cha kusema.
Lisa aliyekaa mkabala naye alikunja uso huku akimwangalia. “Jinsi ninavyowatamani. Ninapenda kuwa kwenye uhusiano kama huo."

"Nyamaza." Huku akifungua mdomo, Alvin alichukua kipande cha kuku kilichobaki mkononi mwake na kukiuma.
Kwa wakati huo, Alvin bado hakuweza kumwelewa Lisa hata kidogo. Alikuwa akimtii, lakini kwa nini kulikuwa na badiliko kubwa hivyo ndani yake sasa?
Baada ya hapo, walimaliza kula firigisi zote za kukaanga, na hata ice cream iliyobaki. Hawakutambua kuwa kuna mtu alikuwa amewapiga picha kwa siri na kuiweka kwenye group whatsapp la kikundi cha wanasheria wenzake na Alvin.
Sam alikuwa akipata nyama choma katika mgahawa mmoja wa kisasa alipoona picha hiyo. Karibu apaliwe na minofu ya nyama. Haraka alisevu picha hiyo na kuisambaza kwenye makundi mengine aliyokuwa na marafiki zake.
Chester: [Macho yangu yananidanganya? Alvin angewezaje kuingia Coco Beach?]
Rodney: [Damn! Sijawahi kuona Alvin akila firigisi za kukaangwa uswazi. Huyu ni Alvin kweli?]
Sam: [Nooooo. Hii ni kweli. Mwanasheria mwenzetu kutoka kampuni yetu alimpeleka binti yake huko Coco beach na kumwona Alvin akila vipande vya nyama ya kuku wa kukaangwa kwa furaha pamoja na Lisa.]
Chester: [Hiyo ni mbaya sana, si hadhi ya Alvin. Utakaporudi, nitakupokea kwa mlo wa hali ya juu wa Kijapani.]
Rodney: [Nakubali. Rudi haraka, Alvin. Nitamwomba mmoja wa wapishi wakuu Kenya akuhudumie.]
Sam: [Nathubutu kuweka dau la milioni tano kwamba Alvin hawezi kuhangaika kuhusu nyinyi. Nina hakika hatajali kula hata Losholi la kimasai ama kichuri cha kikurya mradi tu Lisa yuko karibu naye.]
Ni pale tu Alvin alipotoka kwenye eneo la ufukwe huo ndipo alipogundua fujo zilizokuwa zikiendelea kwenye group hilo la whatsapp. Alifadhaika sana na kujawa na hasira.
Baada ya kuingia kwenye gari, Lisa alimsogelea na kumbusu mdomoni. Macho yake meusi angavu yaliwasilisha hisia za furaha na mahaba. “Asante, Alvilisa. Nimefurahia sana chakula cha jioni ya leo."
Alvin hakuonekana kufurahia kabisa. "Kwa hiyo unajaribu kunifanya nisahau kuhusu jambo hili kwa njia hii, huh? Unajua kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kuingia Coco Beach usiku wa leo na kula chakula cha ajabu?”
Lisa alihisi kuwa Alvin alikuwa anajifanya tu kuchukia. Wakati mwingine, wanawake hutawala kwa urahisi tu. Mara baada ya kugundua kuwa Alvin alifurahia kitu alichomfanyia, alimwongezea dozi ili kumlainisha kabisa. Aliuma mdomo wake wa waridi, kisha, akaweka mikono yake shingoni mwake na ulimi uliojaa mate na akambusu tena.
Safari hii, Alvin alimshika kichwa na kumpiga busu refu. Alipoanza kuvuta pumzi za uchovu ndipo alipomwacha apumue.

Sura ya 118

Katika hoteli moja ya kifahari, Stephen Kileo na dada yake Janet walikuwa wakimfanyia mapokezi ya heshima mtu mmoja maarufu aliyeketi katikati ya kochi. Mtu huyo alikuwa ni Willie Kimaro ambaye alikuwa ametoka Nairobi. Willie na Alvin walikuwa mtu na binamu yake. Familia ya Kimaro ilikuwa familia ya kifahari sana na utajiri wa kutupwa. Ilimiliki makampuni mengi hapa Tanzania na Kenya, yakiwemo ya mawasiliano, Vyombo vya habari, usafirishaji na hata vituo vya mafuta ya magari. Pia walimiliki hisa kwenye makampuni mengine makubwa nchini ikiwemo Mawenzi Investiments. Ni vile tu Alvin hakuwa tayari kujionyesha kwa watu kama alitokea kwenye familia hiyo ndiyo maana watu wengi hawakumjua kiundani. Hata hivyo Kimaro ni jina la ukoo kwa familia nyingi za kichaga hivyo ilikuwa rahisi sana kwa Alvin kuficha uhusiano wake na familia yake.
“Bwana Kimaro, ngoja nikutambulishe kwa mpenzi wangu, Lina.” Stephen Kileo alikuwa ameambatana na Lina. "Baba yake, ambaye ni mwanahisa mkubwa katika kampuni ya Mawenzi Investiments, amekuletea zawadi usiku wa leo."
Usiku huo, Lina alivaa nguo ndefu ya rangi isiyokolea iliyokazia mikunjo ya mwili wake maridadi. Ingawa hakuwa mrembo kama Lisa, alikuwa amependeza sana. Familia ya Jones ilichukuliwa kuwa mojawapo ya familia za juu zilizo na ‘mbegu’ nzuri. Alikuwa amejipodoa ipasavyo usiku huo. Alipotabasamu kwa upole, hakika alionekana kama malaika aliyeshuka duniani kwa bahati mbaya.
Macho ya Willie Kimaro yaliangaza kwa hisia. Lina alikuwa na mawenge sana na wanaume matajiri. Ikiwa angeweza kumvutia kimapenzi mwanamume yule kutoka familia maarufu ya Kimaro, asingekuwa na muda na watu kama Stephen Kileo tena.
Lina alimfuata kwa tabasamu la kichokozi. “Willie, familia yangu ingependa kukupa zawadi hili. Mkufu wa dhahabu wenye kidani cha jiwe la thamani la Tanzanite kutoka Mererani, umenakshiwa na sonara maarufu hapa jijini, Enjipai Jewellery."
Alipomaliza tu kuongea, alifungua boksi. Macho ya Willie yakaangaza. “Woooh! Kidani hiki kina thamani ya mamilioni ya pesa, sivyo?”
“Sio muhimu sana, ilimradi tu unaipenda," Lina alijibu huku akijaribu kumfurahisha.
“Hahaah! Kwa kweli sikutegemea. Nakupenda sana wewe!” Willie alisugua kidani kwenye sehemu ya juu ya pua yake. Haikujulikana kama alimaanisha kuwa anampenda Lina au kidani.
Ghafla, kimya kikatanda kwenye chumba kile cha kifahari cha Hoteli maarufu. Macho ya kila mtu yalikuwa kwa Willie. Stephen alitabasamu kwa utulivu, na mara akanyanyuka yeye na Janet wakatoka nje. Kisha Lina alikaa na Willie kwa muda wote wa usiku. Aliimba na kuzungumza naye. Kwa vile alikuwa mzuri katika kukonga nyoyo za wanaume, mara alimfanya Willie acheke kimoyomoyo.
Baadaye Lina alielekea mapokezi mara moja. Dakika alipotoka nje ya kaunta, alimuona Stephen akisubiri nje.
“Asante kwa usiku wa leo, Stephen. Natumai Willie anaweza kuisaidia familia yangu kurejesha nafasi ya mwenyekiti wa Mawenzi Investiments.” Lina alitabasamu huku akizungusha mkono wake kiunoni kwa Stephen.
"Natumai atasaidia." Stephen alitabasamu bila huruma. “Kwa hiyo Willie na wewe—”
Lina akamkatisha mara moja, “Usinielewe vibaya. Unajua kuwa wewe bado ndiye ninayekupenda. Sasa hivi, Kimaro bado nina maongezi naye—”
“Ninaelewa. Sina wazo lolote baya kuhusu hilo.” Stephen alimpiga piga nyuma ya mkono wake. "Ni wakati tu familia yako itakaporejesha kiti chake cha uenyekiti wa kampuni ya Mawenzi ndipo familia zetu zote mbili zinaweza kufanya maendeleo zaidi na kufikia mambo bora zaidi."
"Ni vizuri umeelewa." Lina hakuwa akimfikiria kabisa Stephen moyoni mwake tena baada ya kuona Willie amekaa mkao wa kueleweka.
"Kilicho muhimu zaidi kwa sasa ni kumfurahisha Willie Kimaro." Stephen alipitisha vidole vyake kwenye nywele zake. “Nitakusubiri.”
“Asante.” Lina alijibu kisha akarudi na keti kando ya Willie tena. Wakati huo, Willie aliweka mkono wake kiunoni mwake na kuanza kumpapasa kama alivyotaka.
Saa tano usiku, Willie alikuwa amelewa. Stephen alimuomba Lina ampeleke chumbani akapumzike.

Sura ya 119

Baada ya Lina na Willie kuondoka, Janet alimwambia Stephen kwa mshtuko, “Umerukwa na akili, Lina si mpenzi wako? Kwa nini hukunitambulisha mimi kwa Willie? Bila shaka ningeifaidisha familia yetu ikiwa ningekuwa binti-mkwe wa familia ya Kimaro.”
“Willie hakuvutiwa nawe,” Stephen alijibu kwa dharau huku akiwasha sigara.
Janet alipandwa na hasira. "Unamaanisha nini? Machoni pako, mimi si mrembo kama Lina, huh? Kwanza mimi sikukulia kijijini kama yeye—”
“Ninafanya hivi kwa faida yako.” Stephen akamkatisha. “Willie ana tabia chafu ya kulala na wanawake hovyo, hajali hata kama ni mpenzi au mke wa mtu.”
Janet alipigwa na butwaa. Stephen aliongeza, “Wewe ni dada yangu wa damu. Ikiwa kuna njia rahisi ya mafanikio makubwa, bila shaka ningekupendelea wewe kwanza. Hata hivyo, Willie ni mhuni na malaya sana. Amewahi hata kuua mwanamke.”
"Una uhakika?" Janet akatetemeka.
“Ni kweli kabisa. Isingekuwa jamaa yetu ambaye anafanya kazi kama msaidizi wake, nisingelijua hilo.” Stephen alisimama taratibu na kusimama. “Vinginevyo, kwa nini unadhani nilimpa Lina nafasi kubwa namna hii? Yeye hana heshima pia.”
Stepehen alitulia kidogo kisha akaongeza tena, “Lakini usijali. Willie atashukuru kwamba nilimpa nafasi ya kuwa karibu na Lina. Katika hali hiyo, nitapata fursa ya kuwa rafiki wake wa karibu. Nitatumia nafasi hiyo kuinufaisha familia yetu kibiashara.” Mara Janet akaridhika.
Asubuhi iliyofuata Lina aliporejewa na fahamu, alishtuka baada ya kumuona mwanaume aliyekuwa pembeni yake ambaye alikuwa akimtumbulia macho. Huku kila kitu kilichotokea jana yake usiku kikimulika akilini mwake, alihisi kana kwamba alikuwa ameenda kuzimu kwa mara nyingine tena. Mtu huyo alikuwa anatisha, kwa kweli. Kifupi alikuwa mnyanyasaji. Wakati huo, Lina alikuwa ameumizwa vibaya sana kutokana na kuingiliwa kinyama kinyume na maumbile.
“Umeamka?” Willie alipogeuza kichwa chake na kumwangalia Lina, mtetemeko ulimtawala mwili mzima.
“Umenifanyaje hivi?” Lina aliuliza kinyonge huku akishika sehemu zake zilizokuwa zinawaka kwa maumivu.
“Kwanini? Hujaridhika na mimi?" Willie aliwasha sigara, macho yake yakimeta kwa chuki.
"Hapana." Lina alilazimisha tabasamu. Kwa kuwa alikuwa ameyataka mwenyewe kulala naye, alifikiri kwamba haikuwa na maana tena kujutia yaliyomkuta. Aliuma meno na kujifanya kuwa na haya. Aliongeza, "Ni furaha yangu kuweza kulala na wewe, Mpenzi Kimaro."
'Ni vizuri kwamba umefurahia. Kwa kweli wewe mtoto ni mtamu sana.” Willie alivuta sigara, akimwangalia Lina kwa udadisi. "Ilikuwa mara yako ya kwanza kufanya jana usiku?"
Lina alipigwa na butwaa. Alikumbuka kwamba alikuwa amefanyiwa upasuaji wa plastiki kurudisha bikra yake kimakusudi ili kumfurahisha Stephen endapo kama wangekutana kabla ya hapo. Hakutarajia kwamba angelala ghafla na Willie jana yake usiku. Inavyonekana, Willie hakuelewa jambo hilo.
“Ndiyo-Ndiyo.”
"Sikutarajia." Willie akamgusa kidevu chake. "Huogopi kwamba Stephen atachukia?"
"Kama nilivyosema, ni heshima yangu kuweza kulala na wewe kwa usiku kucha nikizingatia hadhi yako nzuri," Lina alijibu kwa kujiamini.
Aliposikia hivyo, Willie aliangua kicheko. “Inavutia. Nakupenda sana. Nitakuwa Dar kwa muda, na utanisindikiza katika muda wangu wote hapa.”
“Sawa.” Lina alilazimisha tabasamu. "Nashangaa ni mradi gani uliokuleta hapa Dar, bila shaka ni mkubwa sana!"
“Oh. Kando na kuhudhuria hafla ya Mawenzi, Kampuni ya teknolojia chini ya familia ya Kimaro ingependa kuwekeza katika sekta ya viwanda. Nimekuja kutazama fursa.”
Lina aliuliza kwa tahadhari, “Utawekeza kiasi gani?”
"Pengine mamia ya mabilioni ya shilingi. Hakuna kikomo kwa kiasi, ukomo utategemeana na fursa itakayopatikana.” Willie alijibu kwa kawaida.
Roho ya Lina ilimruka. Ikiwa Mawenzi Investments ingeweza kufanya kazi kwenye mradi huu, Jones na hadhi yake ingeinuliwa.
"Mpenzi Kimaro, nadhani ungetaka kufanya kazi na kampuni ya ndani kwenye mradi mkubwa kama huu..."
"Mawenzi Investments ana nia ya kushiriki katika hilo, huh?" Willie alitoa tabasamu la nguvu.

“Mpenzi, ningependa kushirikiana nawe kwa ajili ya mradi huu, lakini nimefukuzwa kutoka kwenye kazi yangu huko Mawenzi Investments. Baba yangu pia amenyang’anywa cheo cha uenyekiti wa Kampuni” Akiwa amekata tamaa, Lina alitoa tabasamu la uchungu. "Baba yangu na mimi wote tupo hatarini ..."
"Naweza kukutatulia chochote mradi tu ufanye wajibu wako vizuri katika kuniweka sawa." Tabasamu likaangaza usoni mwa Willie. "Wanawake wote wanaonizunguka hawajawahi kushindwa kupokea thawabu nzuri kutoka kwangu."
"Kwa hali hiyo, hakika nitakutendea vizuri." Kwa dhamira mbaya, alimbusu kwa hiari yake mwenyewe.
Muda mfupi baadaye, kilio cha Lina kilisikika kutoka chumbani kwa mara nyingine tena. Willie alimgeuza tena na kuanza kumshughulikia kinyama. Akiwa analia kwa uchungu, alijiwazia, 'Lisa, ninateseka sana sasa kwa ajili yako. Hakika nitakulipa na riba katika siku zijazo!”
•••
Mwaka ulikuwa unaelekea ukingoni. Maadhimisho ya kumbukumbu ya Mawenzi Investments yaliadhimishwa katika hoteli ya nyota saba.
Sio tu kwamba Mawenzi Investments alialika watu mashuhuri wachache kwa usiku huo, lakini idadi kubwa ya wafanyabiashara wenye nguvu pia walikuwa wamejitokeza.
Ilikuwa ni saa moja kamili jioni ambapo Lisa akiwa ni mwenyekiti aliyeteuliwa hivi karibuni, aliwasili katika hoteli hiyo. Lisa aliendesha polepole hadi hotelini kwa gari aina ya Range Rover.
Mlango wa gari ulipofunguliwa, alionekana akiwa amevalia gauni refu jeusi la mtindo wa zamani na akiwa ameshikilia mkoba wa zamani uliopambwa. Kwa kawaida si rahisi kuwa kivutio cha watu kwa mtu aliyevaa nguo nyeusi. Hata hivyo, Lisa alibaki mrembo na mzuri akiwa na uso wake mwanana na wa kuvutia na mdomo uliokolea lipstick nyekundu iliyofanana na waridi linalochanua.
Waandishi wa habari walianza kuchukua kamera zao ili kupiga picha zake. Kwa wadhifa wake na utambulisho wake, angeweza kuchukuliwa kuwa C.E.O mwanamke mwenye umri mdogo na mrembo zaidi jijini Dar es Salaam. Lisa akapiga pozi kwa ajili ya picha, lakini muda mfupi baadaye, kelele za ghafla zikasikika kando yake kutoka kwa waandishi wa habari.
“Fanya haraka utazame! Je, hili si toleo la pekee la Bugatti Veyron L'Or Blanc?"
“Nilisikia limetengenezwa kwa chuma cha titanium. Linagharimu zaidi ya Shilingi milioni mia saba!"
“Angalia namba ya usajili, ni private number. KIMARO! Inashangaza.”
“Kweli inashangaza. Ni nani huyo? Yuko hapa kuhudhuria sherehe ya ukumbusho wa Mawenzi Investments?”
“Tazama! Mlango unafunguliwa.”
Akiwa amezungukwa na sauti za watazamaji, mwanaume mmoja aliyevalia suti ya bluu iliyokolea alitoka kwenye kiti cha dereva. Sifa zake zilitamkwa, na tabasamu la kishetani lilionekana usoni mwake.
Kulikuwa na vifijo kutoka kwa waandishi wa habari katika umati huo.
"Yeye ni mzuri sana!"
“Namfahamu yeye ni nani. Yeye ni Willie kutoka familia ya Kimaro."
"Familia ya Kimaro? Familia yenye utajiri zaidi hapa Tanzania?”
“Ndiyo. Ni hiyo familia ya Kimaro! Wanakaaga Nairobi.”
"Mungu wangu. Mawenzi Investments wana uhusiano na familia ya Kimaro?”
Katikati ya majadiliano ya umma, mlango wa abiria ulifunguliwa. Akiwa amevalia gauni jekundu, Lina alitoka nje ya gari kwa kuvutia huku akiushika mkono wa Willie. Sauti ikazidi kuvuma tena kutoka kwa umati.
“Huyu ni nani?”
"Lina, binti ya Jones Masawe ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya Mawenzi Investments."
“Kwa hiyo yuko kwenye uhusiano na Willie. Anajaribu kugeuka kutoka kuwa mkulima hadi kuwa binti wa kifalme, huh?
"Kwa kuwa sasa ana uhusiano na familia ya Kimaro, familia ya Harrison na familia ya Zongo sasa watamheshimu Jones."
Maneno hayo yalimfanya Lina azidi kuridhika. Ilifaa kujipendekeza na Willie kama mtumwa kwa siku chache ili apate taji la utukufu na heshima siku za baadaye. Alipogeuza macho yake, alitokea kumwona Lisa aliyekuwa mbele yake akiwa anamshangaa bila ukomo.
Akiwa amekunja midomo ya waridi, Lina alimshika Willie mara moja na kuelekea kwa Lisa. "Halo, Lisa. Willie, huyu ni dada yangu, ambaye pia ni Mwenyekiti na CEO wa Mawenzi Investments.”

Sura ya 120

Baada ya kumwona Lisa mapema, Willie alimtazama kwa shauku. Hakujua kamwe kuwa Lisa aliyekuwa amemsikia mapema alikuwa mwanamke mwenye sura nzuri kama hiyo. Uzuri wake ulionekana kuwa wa aina yake miongoni mwa mamia ya wanawake aliokuwa amekutana nao.
"Halo, Bi Jones." Willie alinyoosha mkono wake kwa kumpa salamu. Lisa pia alishangaa kwamba Lina aliwezaje kupata ushirikiano na mtu kutoka kwa familia ya Kimaro. Lisa hakuwa na la kufanya zaidi ya kunyoosha mkono wake bila kupenda, akijua kuwa hawezi kukataa salamu yake bila sababu.
Nani alijua baada ya Willie kumshika mkono, alichora miduara kwenye kiganja chake kwa utani kwa kutumia kidole chake kidogo na kumchoma kichokozi Lisa. Mabadiliko kidogo yalionekana katika uso wa Lisa. Alijaribu kujinasua kutoka kwa mguso wake, lakini kwa makusudi Willie alimshika kwa nguvu na kumzuia.
"Bi Jones, unataka kunishika mkono wangu hadi lini?" Willie alitabasamu kwa ujanja.
Lina mara moja akainua mdomo wake na kusema, "Unafanya nini, Lisa?" Hapo hapo Lina akamvaa Lisa na kumwanzishia varangati, akidhani kwamba Lisa alijaribu kumchombeza Willie.
Waandishi wa habari waliosimama kwenye ukingo wa zulia jekundu walichukua picha za watatu hao mara moja. Pamoja na dada wawili kutoka kwa familia ya Jones wakipigana juu ya mtu maarufu wa familia ya Kimaro, lilikuwa tukio ambao lingetengeneza kipande cha habari nzuri.
“Kwanini hukumuuliza alichonifanyia pia?" Akiwa na tabia ya utulivu, Lisa hakuwa na jeuri wala kujidharau. “Hivi nyie mnafikiri kwamba mimi kama mtu anayesimamia Mawenzi ningemtongoza mpenzi wa binamu yangu bila aibu? Samahani, hata hivyo si mpenzi wako. Ninavyokumbuka, Stephen ndiye mpenzi wako, sivyo?”
Waandishi wa habari walianza kushangaa. “Kweli? Stephen ni mpenzi wa Lina kweli, lakini kwa nini alikuja na Willie leo?”
“Sasa kwa kuwa alikutana na Willie, inawezekana kwamba anajaribu kumtosa Stephen?”
“Hilo linawezekana. Hapo awali alikuwa mchumba wa Ethan, lakini Ethan alipokabiliwa na wakati mgumu, mara moja alimbwaga kwa kushutuma za usaliti.”
“Ni fedheha iliyoje! Willie anavutiwaje na mwanamke wa aina hii?"
Uso wa Lina ulikuwa mweupe kama karatasi wakati huo. Willie hakutambua kwamba Lina alihusishwa na habari nyingi mbaya. Aliishia kujiingiza kwenye matatizo.
Bila bughudha, Lisa alijiondoa kwa nguvu kutoka kwa Willie na kugeuza mkono wake kwa maumivu. "Ulinibana mkono wangu kwa nguvu sana hadi unauma, Bwana Kimaro."
Mkono wake, ambao hapo awali ulikuwa wa kawaida, ulikuwa mwekundu wakati huo. Waandishi wa habari waliposogea karibu, waliweza kuiona ngozi yake nyekundu vizuri. Macho ya Willie yakaangaza kwa dharau mara moja. Hawakutarajia mtu kutoka kwa familia ya Kimaro angekosa haya.
Siku zote Willie alikuwa mtu wa kupenda kunyenyekewa na wengine. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kudhalilishwa na mwanamke hadharani. Macho yake yalionyesha uhasama, lakini alitabasamu kwa unyonge.

"Samahani kwa kukuumiza bahati mbaya." Akamsogelea Lisa hadi karibu na kumnong’oneza, “Utanijua mimi ni nani, Lisa.”
Alipomaliza tu kuongea, aliingia moja kwa moja ndani ya hoteli hiyo. Na Lina alimfuata haraka. Lisa alipoutazama mgongo wa Willie, alihisi kana kwamba alikuwa amelengwa na nyoka mwenye sumu kali. Alikuwa na hasira ya kuzama.
Willie alipanda lifti uso wake ulikuwa na hali ya huzuni. Akiwa ameingiwa na mawazo ya wasiwasi, Lina alisema kwa utulivu, “mpenzi, natumai hautajali kuhusu hilo. Lisa anajidai na anajigamba kwa kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa kampuni na kufanya mambo yasiyo ya kiungwana.”
“Yeye ni nani wa kufanya hivyo? Yeye ni mwenyekiti tu wa kampuni, kufumba na kufumbua anaweza kukuta kiti hicho kina mtu mwingine.” Willie alikuwa akifuka kwa hasira.
"Kwa kweli, yeye si kitu ikilinganishwa na wewe. Labda ni kwa sababu ana mpenzi mwenye nguvu, na yeye ni mwaminifu sana kwake.” Baada ya kukaa siku chache na Willie, Lina alijua kuwa Willie alipenda sana kusifiwa.

Kwa hakika, macho ya Willie yalionyesha kupendezwa kwake dakika tu aliposikia hivyo. Alipenda sana wanawake ambao muda wote walikuwa wakimsifia, kumbembeleza na kumpetipeti. Zaidi ya hayo, ukizingatia jinsi Lisa alivyokuwa mkali muda si mrefu, alifanana na waridi lenye miiba na alionekana mrembo zaidi kuliko Lina.
Alipoona hali ya kuvutia machoni pake, Lina alitabasamu na kusema, “Ninaweza kumfanya alale nawe kama utapenda.” Lina alisema bila aibu. Kwa kuwa amekuwa akidhalilishwa na Willie kama mbwa kwa muda waliokuwa pamoja, alitaka Lisa pia aonje adha hiyo.
"Wewe ni mwanamke mbaya sana." Willie alimpiga jicho la mshangao.
"Furaha yako ndiyo muhimu kwangu. Hutaki kumfundisha somo?” Lina aliuliza kwa kupendeza.
Willie aliinua macho yake. Aliwasha sigara kisha akasema kwa uovu, “Wale walionidhalilisha wote waliishia katika hali mbaya sana. Lisa pia anastahili kujuta!”
•••
Sherehe kuu ya kumbukumbu ya kampuni ya Mawenzi ilianza rasmi. Lisa alipaswa kuwa kivutio cha tukio hilo, hata hivyo, wageni wote walimzunguka Willie, Jones, na Lina badala yake.
Kwa macho ya wengi, familia ya Kimaro ilionekana kuwa ya hadhi ya kipekee. Ingawa Willie hakuwa mzao wa moja kwa moja wa Kimaro, uwepo wake jijini Dar es Salaam ulikuwa na nguvu ya kutosha kupata heshima kutoka familia kubwa za kitajiri.
Chris Maganga akajongea kuelekea kwa Lisa na kumuuliza. "Jones Masawe aliwezaje kujenga uhusiano na Willie Kimaro?"
"Nadhani Lina alilala naye." Lisa alifanya dhana ya kuridhisha. Tayari aliweza kuona tabia mbaya ya Willie kupitia tukio fupi alilokutana nalo mlangoni wakati wanaingia.
Sura ya dharau iliosha usoni mwa Chris. “Babu na bibi zako walikuwa na sifa ya uungwana na uadilifu, hii tabia chafu yenye aibu ameitoa wapi dada yako?”
“Ni kwaida yake kujua ndani ya kila suruali ya mwaname aliyefanikiwa kuna mdudu gani.” Lisa kichwa kilimuuma. Hapo awali, alikuwa na uwezekano mkubwa wa kumvutia kila mtu, lakini mwonekano wa Willie ulimfunika kabisa. Willie alikuwa amevutia umakini wa wasanii, waalikwa, wakurugenzi wa kampuni na wasimamizi wakuu.
Kwa wakati huo, wakurugenzi wawili wa bodi ya kampuni ya Mawenzi, Amiri Gumbo na Mzee Levy walimwendea na kumwambia. "Lisa, ulipaswa kuwa wa kwanza kutoa hotuba kwenye jukwaa usiku wa leo. Lakini baada ya kujadiliana na wakurugenzi wengine, tuliamua kumwacha Bwana Kimaro aanze kwanza, akifuatiwa na Jones kisha—”
“Nyie watu ni wazima kweli?” Chris alipandwa na hasira. “Bwana Kimaro hata hajui kinachoendelea katika kampuni yetu, wao huja kuchukua faida tu. Unahitaji kujua kuwa usiku wa leo ni sherehe ya kumbukumbu ya Mawenzi Investments. Pia, kwa nini Jones anapanda jukwaani kabla ya mwenyekiti? Hii haina maana.”
Mkurugenzi Amiri alijibu kwa aibu, “Angalia Bwana Kimaro ni nani. Ukweli kwamba amejitokeza kwenye sherehe ya ukumbusho wa Mawenzi Investments unaonyesha kwamba anatufikiria sana. Zaidi ya hayo, yuko tayari kupanda jukwaani kutoa hotuba, ambayo ni heshima yetu kubwa. Bei ya hisa za kampuni yetu itaongezeka kesho. Kuhusu Jones, ni Bwana Kimaro ambaye alimwomba azungumze. Ana uhusiano wa karibu naye. Huwezi kunilaumu kwa hili.”
Uso wa Lisa ulibadilika kidogo. “Itakuwaje kama sikubaliani?”
"Hapana," Mkurugenzi Levy alijibu kwa njia ya moja kwa moja, "Sote tulifikia uamuzi huu kwa ajili ya kampuni. Lazima ukubaliane nao.”
Lisa alicheka. "Ikiwa Willie ataamua kumpendekeza Jones kuwa mwenyekiti, nyinyi pia mtakubaliana naye? Je! ni Sheryl au Kimaro ambaye alianzisha Mawenzi Investments?"
"Tunafanya hivi kwa ajili ya matarajio ya kampuni," Mkurugenzi Levy alisema kwa kukerwa, "Kwa kuzingatia hali ya familia ya Kimaro, utajiri wa familia yao una thamani ya mamia ya mabilioni ya shilingi.” Mkurugenzi Amiri alikubali kwa kichwa pia.
Saa mbili na nusu usiku, Willie alipanda jukwaani na kutoa hotuba, akifuatiwa na Jones Masawe…

TUKUTANE KURASA 121-125

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.......... LISA
KURASA..... 121-125

Sura ya 121

Saa tatu usiku, Lisa alikuwa kwenye chumba chake cha mapumziko baada ya kumaliza kutoa hotuba yake. Alisimama kwenye kioo akipaka lipstick yenye rangi ya hudhurungi kwenye midomo yake maridadi, huku akitafakari hotuba aliyotoka kuitoa punde.
Lina akaingia ghafla. Akiwa na tabasamu la ufidhuli, alisema, “Pengine hukutarajia kwamba hivi karibuni ungeweza kupoteza nafasi yako ya uenyekiti ambayo ndiyo umeipata hivi punde, sivyo?”
"Wewe bado hujabadilika kabisa Lina." Lisa aligeuza kichwa chake na kukutana na macho ya Lina. “Kwanza, ilikuwa Ethan, ikifuatiwa na Stephen na sasa Willie. Umelala na wanaume wangapi zaidi kabla ya hawa? Wewe ni zoazoa, cha wote, au chakula cha wageni?”
Kauli fupi kama hiyo iligusa ujasiri wa Lina ghafla na kusababisha damu yake kuchemka. “unanionea wivu, huh? Sasa ninakupa nafasi hii pia. Ni heshima kubwa sana kuweza kulala na Willie Kimaro sivyo? Nadhani utafurahia pia, yupo vizuri kwa bedi.”
Mara tu alipomaliza kuzungumza, Willie aliingia ndani ya chumba akiwa amevimba kama mbogo.
"Bwana Kimaro, nitakusaidia kulinda nje." Lina alifunga mlango wa chumba mara baada ya kusema hayo.
“Unataka kufanya nini?” Lisa alijaribu kukimbia, lakini Willie alimshika mkono. Kukiwa na mlango kati yao, alisikia sauti ya mlango ukiwa unafungwa.
Wimbi la wasiwasi lilimkumba Lisa. Shani hakuwemo chumbani wakati huo. Alimwambia abaki tu nje kwenye gari kwani hakutarajia tukio kama hilo kutokea wakati wa hafla ya ndani ya kampuni.
“Niache niende, Kimaro.” Lisa alimuuma Willie kwa nguvu.
Willie aliachia mkono wake kwa maumivu kisha akacheka. “Hakika wewe ni mjanja. Hiyo inavutia. Napenda wanawake wachangamfu kama wewe.”
“Una kichaa?” Lisa alishangaa, “familia ya Kimaro ni moja ya familia zenye heshima kubwa. Sikutegemea kama kuna mtu mwenye kuchukiza na mchafu kama wewe katika familia yenu, au wewe si mtoto halisi wa familia ya Kimaro?” Lisa alikosoa.
“Endelea kunikosoa. Kadiri unavyonikosoa, ndivyo nitakavyokuletea taabu zaidi.” Willie alidhihaki. “Wakurugenzi wa kampuni yako wote wananichukulia kama mheshimiwa. Jones Masawe ameniomba nimsaidie kupata nafasi ya mwenyekiti kesho. Ninaweza kusema kitu kwa urahisi na kukufanya upoteze nafasi yako mara moja. Unajua nina nguvu ya 25% ya hisa za kampuni. Kwa hivyo, nitafikiria upya ikiwa utanihudumia vizuri usiku wa leo.”
Akiwa na mawazo, Lisa alijifanya kuwa na hofu na kusema, “Hii ni kweli?”
“Bila shaka.” Willie alifoka, akijua kuwa Lisa tayari alikuwa anaingia kwenye anga zake.
"Lazima unisaidie, Bwana Kimaro," Lisa alidakia na kusema kwa huruma, "naweza kukufanyia chochote."
“Vizuri sana kwa kuwa umeelewa. Unajua kilicho bora kwako. Njoo hapa basi.” Willie alifungua mikono yake.
Lisa akajitupa mikononi mwake. Harufu ya kuburudisha ya mwili wake ilijaza pua yake. Kwake, umbo lake lilikuwa bora zaidi kuliko la Lina. Moyo wa Willie ulikuwa unawaka. Alipotaka kumkumbatia kwa nguvu, alipigwa na nguvu kubwa.
Willie akainama kwa uchungu. Lisa alikuwa amechukua kalamu ya chuma kutoka kwenye mkoba wake na kumchoma nayo Willie kwa nguvu kwenye mbavu. Kalamu hiyo ilikuwa na kichwa chembamba kilichopenya kwenye nyama kama risasi. Willie aliganda kwa maumivu na hakuweza kusogea hata kidogo.
Lisa alivua viatu vyake virefu na kumpiga usoni na mwilini kwa visigino vikali vya viatu vyake. Alimpiga hadi chini, na akaishia kuwa kama samaki aliyetolewa baharini na kuwekwa nchi kavu, asiweze kusogea hata kidogo. Baada ya kuona amefanikiwa kumdhibiti Willie yeye mwenyewe, Lisa hakuwa na haja hata ya kumpigia Shani.
Baada ya kumpiga Willie, Lisa alishtuka kuona uso wake umevimba. Alifikiria kwa muda na kugundua kuwa alihitaji kumfanyia zaidi ya hivyo, na akamvua nguo zake pia.
“Unataka kufanya nini?” Willie alilalama kwa uchungu. Siku zote ndiye aliyekuwa akiwavua nguo wanawake. Yeye kamwe hakuwahi kufikiri kuwa kuna siku nguo zake zingekuja kuvuliwa na mwanamke. Macho wake yalidhihirisha ukali. Alitamani kumpasuapasua Lisa lakini hata hivyo hakuwa na nguvu hata kidogo ya kupinga kwani alipigwa vibaya viatu vya mbavuni na usoni.

Baada ya kumvua nguo, Lisa alichukua simu yake na kumpiga picha zaidi ya kumi kutoka pembe tofauti. Alimtisha kwa njia ya dharau, “Ikiwa utathubutu kuniletea matatizo kuhusu kilichotokea leo, nitatupia picha zako hizi chafu mtandaoni. Hebu tuone kama familia ya Kimaro inajali utu wao.”
“Wewe…” Willie alikasirika. Katika kipindi cha miaka 25 ya maisha yake, hakuna hata mwanamke mmoja aliyekuwa na ujasiri wa kumfanyia hivyo. “Nakuonya! Nitakushughulikia, Lisa."
“Na mimi nitakushughulikia pia.” Lisa alimjibu kwa dharau. “Ni mara yangu ya kwanza kuona mwili mbaya kama huu. Unakera na kuchukiza kama nini!"
Lisa akampa kidole cha kati na kuziitupa nguo na simu ya Willie dirishani. Baada ya hapo, alimburuta hadi chooni na kumfungia humo. Kisha Lisa alitoroka kupitia dirishani ili kumfanya Lina asielewe chochote.
Willie alilala kwenye sakafu baridi ya choo kile akiwa uchi. Hata baada ya kutumia muda mrefu kuomba msaada kwa sauti dhaifu, hakuna mtu aliyekuja kumsaidia.
Ni baada ya nusu saa kupita ndipo alianza kupata nguvu. Alitetemeka huku akinyanyuka na kuufungua mlango kwa nguvu. Baada ya kusikia kelele, Lina alikimbia kwa uangalifu kuelekea kwenye chumba hicho na kufungua mlango.
Pindi alipouona tu uso wa Willie uliojeruhiwa, alipiga kelele kwa mshtuko. “Imekuwaje tena mpenzi…”
“Nyamaza, mpuuzi wewe!” Willie alimpiga Lina kibao cha usoni na kumpiga mateke machache dhaifu kwa hasira. “Nilikuwa nakuita sasa hivi. Ulikuwa kiziwi?”
“Usinipige, mimi sikusikia. Niliogopa kukusumbua, na nilikuwa nimesimama mbali sana… Ohoo-hoo!” Lina alipiga magoti na kumsihi. Mwanaume huyo alitisha sana alipokuwa na Lina, utadhani si yeye aliyekuwa kama panzi mbele ya Lisa muda mchache uliopita.
"Potea, wewe huna maana kabisa!" Willie alianza kutetemeka tena. Kwa hasira alifoka na kuapa, “Lisa, nikishindwa kukuua, nitakula mavi yangu!”

Sura ya 122

Alvin, ambaye alikuwa na mkutano wa video katika chumba chake cha maktaba, alisikia sauti ya gari kutoka chini. Wakati huo alikuwa anasikiliza mipango mbalimbali ya maendeleo ya miradi yake. "Mpango huu hauwezekani. Njoo na mwingine." Alipomaliza tu kuongea, alikatisha mkutano na kuelekea chini.

Akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa, Lisa akaingia mlangoni. Alisahau hata kubadili viatu vyake. Alvin alikodoa macho na kutazama gauni lake refu jeusi. Alionekana kuvurugwa tofauti na alivyoondoka.

Akiwa amekunja uso, Alvin alimtupia macho ya mshangao na udadisi Lisa. Alipoyaelekeza macho yake chini, ghafla aliona ufa kwenye pindo za gauni lake.

“Mbona nguo yako imetatuka?” Macho yake meusi yalikuwa yakimtazama kama mshale.

Alipojitazama tu chini ndipo alipogundua. Labda nguo hiyo ilikuwa imeshikana na kitu chenye ncha kali alipotambaa nje ya dirisha kutoka kwenye chumba kile cha hoteli. “Nilinasa sehemu kwa bahati mbaya.” Lisa aligeuza macho yake, hakutaka ajue kwamba alikuwa amemchokoza Willie Kimaro. Hata hivyo hakujua kabisa kama wana uhusiano wa aina yoyote. Kwa mawazo yake, Alvin alikuwa wakili tu, na asingekuwa na uwezo wa kuwa na uhusiano wowote na familia tajiri ya Kimaro. Alijua ni majina ya ukoo tu ndiyo yamefanana.

"Una tabia mbaya ya kunitazama kila wakati unaposema uwongo." Alvin alishika kiuno chake chembamba kwa nguvu, macho yake meusi yakionyesha hisia kali ya ukali. “Ulihudhuria sherehe ya ukumbusho usiku wa leo, sivyo? Nani alikuletea shida?”

“Hakuna aliyenifanya chochote. Haya, nani anaweza kunigusa wakati mimi ni mwenyekiti?” Lisa alimsukuma na kwenda juu. “Naenda kuoga."

"Usinifiche Lisa." Alvin akamvuta kuelekea kwake tena. “Angalia jinsi ulivyokosa amani kwa sasa. Afadhali unieleze ukweli kama unanichukulia kama mume wako.”

Lisa alipiga kelele, na macho yake yakawa mekundu licha ya yeye mwenyewe kupenda. “Nimemkosea mtu ambaye sikupaswa kumkosea katika ulimwengu mzima wa kibiashara. Alvlisa, kama… Ikiwa… mtu huyo ananilenga, usithubutu kufikiria kunisaidia. Afadhali unikane kabisa kuliko kunisaidia vinginevyo utapoteza kila kitu. Yeye si sawa na Clark Zongo…”

Alvin aliinua macho yake na kuuliza. “Unaamaanisha nani huyo anaweza kunitisha mimi?”

"Willie Kimaro, kutoka familia ya Kimaro." Lisa alisema huku akihema. “Biashara zao kubwakubwa zimetapakaa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki yote, pia wanamiliki asilimia 25 za hisa za Mawenzi.”

Alvin alishindwa cha kusema. Hilo lilimshangaza sana. Tangu lini Willie, yule bwana mdogo mpuuzi tu, akawa mtu ambaye kwa hakika anaogopwa kiasi kile na matajiri wa Dar es Salaam? Ina maana Lisa hakumchukulia yeye kama mtu mwenye nguvu? Anyway, halikuwa kosa lake kwa sababu alimficha utambulisho wake halisi.

“Umeshtuka sana?” Lisa alituliza baada ya kumuona Alvin akiwa kimya sana, hivyo mara moja akamfariji. “Lakini usijali. Kwa bahati nzuri, nilikuwa na kalamu ya chuma kwenye mkoba, alipojaribu kunivamia chumbani nilimchoma na kalamu kwenye mbavu akaanguka, nikampiga sana na visigino vya viatu. Kisha, nilimvua nguo zake na kumpiga picha…”

“Ulimvua nguo?” Macho ya Alvin yalionyesha hasira na huzuni, na kusababisha hali ya mazingira kuwa tata ghafla.

"Ah ... nilikuwa najaribu kumtisha tu akae mbali na mimi, nimemwambia akijaribu kunifuatilia wakati mwingine nitamdharirisha mtandaoni." Kwa kupoteza, Lisa alieleza, “Sikuwa na la kufanya. Unafikiri nitakuwa nimekosea sana?”

“Una akili?” Alvin alishusha pumzi ndefu huku akihofia kuwa angepatwa na wazimu. “Kwa hiyo umeona na nanihii yake?”

Akiwa chini ya macho ya hatari ya mwanaume huyo, Lisa alikuna kichwa na kukohoa kidogo. " Eeh..Aah..Hapana. Inachukiza. Yeye ni ngozi na mifupa tu, na umbile lake si zuri kama lako pia. Kinyume chake, wewe ni mrefu na umejengwa vizuri. Ninapokutazama, ninavutiwa na wewe. Kukutazama kwa mara ya pili kunanipaga wazimu kwe—”

“Nakupandisha wazimu?” Macho meusi ya Alvin yalimtoka huku akivaa tabasamu la sifa.

Lisa alijisikia mkanganyiko wa kimawazo. Akijihisi hana cha kusema, alimwambia, “Sasa si wakati wa kuzungumzia jambo hili…”

“Nipe simu yako.” Alvin alinyoosha mkono wake kuelekea kwake.
Mara moja akampitishia simu yake. Alvin alipozitazama zile picha alizidi kusononeka. Muda mfupi baadaye, alihamishia picha hizo kwake na kuziondoa zote kwenye simu ya Lisa.

“Haya, kwanini umezifuta…” Lisa alikosa raha.

"Kama mwanamke wangu, huoni aibu kuweka picha za mwanamume mwingine kwenye simu yako?" Akiwa anamwangalia kwa ukali, alionya, "tena umepiga picha ukiwa umezingatia kabisa sehemu zake za siri!" Lisa alikosa la kusema. Aliinamisha kichwa chini bila kutamka neno lolote.

“Nenda ghorofani ukalale. Usifikirie mambo kupita kiasi kwani tayari umempiga picha kama hizo. Familia ya Kimaro inajali sana hadhi yao, hawawezi kukuacha salama pindi utakapozisambaza picha hizi.” Alvin alisema kile ambacho hakumaanisha kumfariji.

“Kweli?” Lisa alikuwa na shaka juu yake. "Lakini sidhani kama Willie ni mtu anayejali hadhi ya familia yake. Anastahili kutendewa vibaya kama hivyo. Nilimpiga vibaya sana.”

“Hujui ni kiasi gani wanaume wanajali utu wao ikilinganishwa na wanawake. Wewe si mwanaume, kwa hivyo hutaelewa. Naamini hatakuwa na ujasiri wa kukutafuta. Umelishughulikia jambo hili vizuri sana,” Alvin aling’oa risasi na kuendelea kueleza kimafumbo.
Ni mara chache alimpongeza Lisa. Kwa hivyo Lisa alishtuka kidogo aliposikia pongezi zake. Labda Alvin alikuwa sahihi. Huenda alikuwa haelewi kabisa wanaume.

"Baada ya kusema hivyo, usivue nguo za mwanaume tena." Baada ya kutulia, Alvin alimuonya kwa huzuni, "Bila shaka, isipokuwa mimi tu." Lisa alishindwa cha kusema na kubaki anacheka tu.

“Nenda ukaoge. nitakusaidia kwa hilo.” Alvin hakujali macho yake ya kusema, akauweka mkono wake kiunoni na kumbeba juu juu moja kwa moja.

“Sitaki." Lisa alipiga kelele kwa aibu. Alikuwa ameweka wasiwasi na hofu nyuma yake.

Usiku, ilimchukua Alvin muda kutafuta usingizi wake bila mafanikio. Mwishowe aliamua kushuka chini, akaingia kwenye gari na kuondoka kwenye nyumba yake ya kifahari.
•••
Usiku wa manane, Willie alirudi hotelini baada ya kufungwa majeraha yake hospitalini. Kwa hasira kali, akatoa simu yake ili apige.

"Kwa ndoano au kwa hila, nyinyi watu lazima mumtie Lisa kuzimu. Sitaki kusikia anaendelea kuishi mbwa yule.”

Alipomaliza tu kuongea, mlango ukasikika ukigonwa kwa nguvu. “Ni nani huyo mwenye kelele anayebisha saa za usiku hivi? Una hamu ya kifo, huh?" Willie alikimbia kuelekea mlangoni ili kuufungua, lakini akafunikwa na gunia. Ghafla, mtu fulani alianza kumpiga.

Mtu huyo alikuwa mkatili na mkali. Aliendelea kuupiga teke mwili wa Willie kwa nguvu. Wakati gunia liliipofunuliwa. Mtu mrefu na mpana aliingia ndani. Mwanaume huyo alikuwa amevalia sweta nyeusi. Vipengele vyake vya kuvutia vilipoainishwa chini ya taa zenye giza kwenye chumba, Willie alihisi hofu na hali ya hatari iliyouzunguka mwili wake.

“Alvin… Hapana, ninamaanisha kaka Alvin. Kwa nini… Kwa nini uko hapa?” Willie angeweza kumtambua mara ya kwanza. Kwake, mtu huyo alifananishwa na shetani. Alikuwa mwanaume pekee katika familia nzima ya Kimaro ambaye Willie alikuwa anamuogopa.

"Umekuwa ukifanya kazi na Jack Kimaro hivi karibuni lakini hukujua nilipo?" Huku mikono yake ikiwa mfukoni, Alvin aliingia ndani kwa majivuno na kumkanyaga Willie kifuani.

Willie alitetemeka kwa hofu. “Kaka Alvin, sijui unasemaje. Ndiyo, ni Jack ambaye amekuwa akisimamia KIM International hivi karibuni, lakini… Lakini sote tunafahamu kuwa uwepo wako katika kampuni ni wa umuhimu mkubwa. Kwa kweli, wewe ndiye bosi wa KIM International.”
"Ujuzi wako wa kuongea maneno ya kuhadaa umeongezeka. Hivi ndivyo unavyofanya mbele ya Jack pia?" Alvin alimpiga teke Willie kidevu kwa madaha kwa kutumia ncha ya kiatu chake. “Bado ninakumbuka mambo yote ambayo baba yako alifanya. Alimsaidia Jack kushusha cheo changu.”
“Hapana, kaka Alvin. Sote tunakungoja.” Willie aliogopa sana kufanya kelele yoyote.
"Mnaningojea wapi wakati umekuja Dar es Salaama kimyakimya kukagua biashara na kufanya mipango ya kupanua uwekezaji?" Sura ya dharau iliosha usoni mwa Alvin. "Mnajaribu kubadilisha teknolojia za kimsingi za kampuni wakati mimi sipo karibu, huh?"

Sura ya 123

Huku akiendelea kumkaripia kwa hasira, Alvin alikanyaga kifua cha Willie. "Leo, umeonekana kuwa wa kushangaza sana huko kwenye sherehe za Mawenzi, huh? Kwa tabia zako chafu, unawezaje kuthubutu kuanzisha fujo huko hotelini? Huenda usijali kupoteza sifa yako, lakini familia ya Kimaro inajali sana hadhi yake. Unajichukulia kama bosi wa KIM international na kisha unatumia nafasi hiyo kufanya mambo ya hovyo ya kushusha hadhi ya kampuni?"

“Kaka Alvin, najua ni kosa langu. Sitafanya tena,” Willie aliendelea kumsihi kwa woga.

"Hapana. Nadhani wewe ni jasiri sana. Unathubutu hata kujaribu kupata kipande cha mapenzi ya mwanamke wangu.” Alvin alicheka kwa huzuni.

Willie alipigwa na butwaa. "Lina ni mwanamke wako?"

"Sitavutiwa na mwanamke mchafu wa aina hiyo." Alvin akainama taratibu na kuchuchumaa. Macho yake ghafla yakageuka kuwa makali sana.

Akiwa amepigwa na mawazo, Willie akauliza kwa mshangao, “Unamaanisha… Lisa…?”

“Ni vizuri kwamba unamkumbuka. Sipendi kudhani kwamba nilimuonea mtu asiye na hatia baada ya kumalizana na wewe.” Alvin akajiweka sawa.

Willie alifahamu mbinu ambayo Alvin angetumia. Akiwa amechoka, mara akatambaa kwa shida. Alipiga magoti sakafuni na kumsujudia Alvin. “Pole, kaka Alvin! Kwa kweli sikujua. Ni kosa langu. Nilikuwa kipofu. Tafadhali niruhusu niachane na…”

Alvin alimpiga teke kali hadi akajibamiza ukutani. Willie alitema damu iliyojaa mdomoni. "Kwa kuwa huwezi kudhibiti hiyo sehemu yako ndogo ya mwili, wacha tuiondoe kabisa..." Alvin akapiga hatua kuelekea kwake.

"Hapana." Willie alitetemeka kwenye buti zake. “Kaka Alvin, sitarudia tena. Ukiharibu, bibi yangu ataumia moyoni kwani ananipenda. Pia Babu atakasirika.”

"Sawa, niambie ninachoweza kufanya ili nifikirie kukusamehe." Alvin alimkanyaga kwa nguvu kwenye ‘jongoo’ lake.

Machozi yalitiririka usoni mwa Willie kutokana na maumivu. Akiwa ameshikilia sehemu ya chini ya suruali ya Alvin, aliomba na kusihi, “Hapana, hapana. Naweza kufanya vile unavyotaka. Nitapiga magoti na kuomba msamaha kwa Lisa kesho.”

“Sawa. Kumbuka ulichosema.” Alvin aligeuza kichwa chake na kumwambia mtumishi wake wa chini, “Kwa vile anafurahia kufanya wanawake vibaya, vua nguo zake na umpeleke kwenye kibaraza. Wacha apigwe na upepo baridi wa baharini usiku kucha, labda ataikumbuka siku ya leo kila atakapokuwa anafikiria kufanya ujinga.”

Mtetemeko ulishuka kwenye uti wa mgongo wa Willie. Kabla ya hapo, Lisa alikuwa amemvua nguo na kumwacha amelala kwenye sakafu ya choo kwa muda wa nusu saa, na kumfanya ashikwe na baridi. Mbaya zaidi alikuwa anaenda kupigwa na upepo wa baharini kwa usiku mzima. Ilikuwa ni saa sita usiku na dakika kadhaa. Wawili hao walikuwa wakatili kwelikweli.

“Kaka Alvin, nitaganda hadi kufa.” Willie alijitetea.

“Usijali. Kwa kuzingatia kuwa wewe ni binamu yangu, sitakuacha ufe. Ambulance ya hoteli hii iko kwenye standby hapo chini. Utaokolewa mara moja ukibaki na pumzi yako ya mwisho." Alvin akampiga bega huku akimkumbusha kwa sauti ya upole. Kwa hayo, aligeuka na kuondoka.

Willie alikuwa kwenye hatihati ya kuanguka. Aliapa kwamba hatamchokoza Lisa tena.
•••
Saa mbili kamili asubuhi, Lisa alipokuwa akiandaa kifungua kinywa jikoni, alipokea simu kutoka kwa Chris Maganga. "Lisa, wakurugenzi wanataka kufanya mkutano mkuu wa dharura leo asubuhi." Chris alieleza. “Wanadai kwamba ulimpiga Bwana Kimaro jana usiku, kwa hivyo wanaomba ufukuzwe kwenye nafasi yako ya mwenyekiti. Pia, ikiwa hautapiga magoti na kuomba msamaha kwa Bwana Kimaro, watakuondoa kwenye bodi ya wakurugenzi pia."

Lisa aliondoa apron yake mara moja. “Nakuja sasa hivi.” Alipokata simu, alielekea mlangoni kama upepo.

“Kifungua kinywa changu kiko wapi?” Akiwa amevalia nguo za kulalia nyeusi, Alvin alitokea akishuka chini kivivu huku akipiga miayo. Haijalishi alivaa nini, alikuwa akivutia tu kwa macho kutokana na umbile lake lenye nguvu.

"Kuna jambo la dharura limetokea ofisini. Shangazi Linda atakuja kukuandalia.” Lisa alibadilisha viatu vyake haraka na kukimbilia nje ya jumba hilo. Ndita za Alvin zilijikunja sana. Ilikuwa ni muda mrefu sana tangu apate kifungua kinywa kilichoandaliwa naye.

Saa mbili na nusu asubuhi Katika chumba cha mkutano, wakurugenzi wote walikuwa na nyuso za huzuni na zenye hasira. Kwa kutajwa kwa Lisa, walitamani kumla.

"Chris ndiye wa kulaumiwa kwa jambo hili. Kama asingemtetea Lisa na kuwa mwenyekiti, Mawenzi Investments isingeiudhi familia ya Kimaro."

“Amerukwa na akili? Alithubutu vipi kumpiga Willie? Kimaro ni familia mashuhuri, na kwa wazi hatuwezi kumudu kuwachokoza.”
"Nilisikia mtu ambaye alimuudhi Willie kabla ya huyu alikuwa bilionea kutoka Kenya. Familia yake ilifilisika kwa usikummoja tu.”

“Ndiyo. Willie anatisha."

Katikati ya majadiliano ya wakurugenzi, Jones Masawe alishusha pumzi ndefu. “Yote ni makosa yangu. Sikupaswa kumruhusu Lina kumleta Willie jana. Lakini nilisikia Willie alikuja hapa kwa ajili ya ukaguzi, na nilikuwa na matumaini kwamba Mawenzi Investments ingeweza kufanya kazi na KIM International.”

“Kweli. Ikiwa tungeweza kushirikiana na KIM International, ingeinufaisha sana Mawenzi Investments.

“Tulikosea. Tungemfanya Jones kuwa mwenyekiti.”

“Najutia uamuzi wangu pia. Sikupaswa kumpigia kura Lisa wakati huo.”

Akihisi mnyonge, Mkurugenzi Amiri alisema, “Sasa kwa vile mambo yamekuwa hivi, hatuna chaguo ila kumwondoa katika nafasi yake ya mwenyekiti kwa ajili ya matarajio ya Mawenzi Investments. Labda Jones ndiye pekee anayeweza kutusaidia kukabiliana na dhoruba wakati huu. Baada ya yote, binti yake ana uhusiano wa karibu na Willie.

Jones alipunga mkono kwa unyenyekevu. “Sina hakika kama naweza kusuluhisha hili. Baada ya kusema hivyo, Bwana Kimaro anampenda sana Lina. Ataenda naye popote aendako. Una maoni gani, Lina?"

Akivumilia maumivu kutoka kwenye majeraha yake ya sehemu za siri yaliyosababishwa na Willie jana yake, Lina alilazimisha tabasamu tamu. "Bwana Kimaro ananipenda sana. Hata aliniambia mambo mengi kuhusu mradi huo.”

Kila mtu alishangilia kwa furaha. Mkurugenzi Amiri alisema, "Ni mpango wetu sasa. Jones atakuwa mwenyekiti wetu mpya.”

Lisa aliusukuma mlango na kujipenyeza ndani. Macho ya wazi na makali yaliwakumba wakurugenzi wote. “Kwangu, ninyi nyote ni wakurugenzi wa Mawenzi Investments, ambao pia mnachukuliwa kuwa wazee wangu. Nilimpiga Willie jana usiku, ndiyo! Lakini kuna yeyote kati yenu aliyeniuliza kwa nini nilifanya hivyo?” Kila mtu alipigwa na butwaa.

Lisa aliongeza kwa hasira, “Jana usiku, Willie alinifungia kwenye chumba changu cha hoteli na karibu kunibaka. Lina alisimama nje ili kumsaidia kufuatilia hali ya nje. Kwa sababu ya njama yao chafu, mimi, kama mwenyekiti wa Mawenzi Investments, nilikuwa karibu kuharibiwa. Kwa nini? Kwa sababu Willie ni mjanja na hajali kabisa. Hakuwa tu anajaribu kunidhalilisha mimi bali pia Mawenzi Investments nzima.”

'Hilo ni jambo lisilo na akili kwa Willie," mkurugenzi alinong'ona.

“Vipi Lina anathubutu vipi kufanya vile?! Hiyo inatisha.”

“Sikufanya hivyo. Lina alisimama mara moja. “Wewe ndiye uliyetaka kumtongoza Bwana Kimaro, lakini hakuwa na hamu na wewe. Anaweza kupata mwanamke yeyote anayemtaka kwa urahisi. Kwa nini atake kujilazimisha kwako?”

Jones alisema kwa mzaha, “Hata waandishi walikupiga picha ukiwa umemshika Bwana Kimaro kwa mkono wake kwenye lango la hoteli jana usiku. Hata hivyo, Bwana Kimaro alidai kuwa ulimvua nguo.

"Ni aibu kama nini!"

"Ni aibu kubwa kuwa na mkurugenzi kama huyu Mawenzi Investments." Kila mtu alimtazama Lisa kwa dharau.

Mkurugenzi Amiri alikunja uso na kusema. “Acha kujitetea. Umeingia kwenye matatizo makubwa wakati huu. Tunataka tu kuilinda Mawenzi Investments. Kwa kuwa lilikuwa ni kosa lako, unapaswa kubeba jukumu. Kusema kweli, huwezi tena kukaa katika kampuni tena.”

Mdomo wa Lisa ulitetemeka kwa kejeli huku macho yake yakionyesha sura ya jeuri. "Kwa hivyo mnapanga kunifukuza kutoka kwenye bodi ya wakurugenzi?"

Jones alitabasamu kwa dharau. “Hilo ndilo jambo pekee tunaloweza kufanya. Afadhali ufungashe na kuondoka sasa hivi.”

Lisa alidondosha macho yake. Alikuwa amechanganyikiwa kabisa na kampuni hiyo. Wakati huo, mfanyakazi mmoja alikimbia ndani na kupiga kelele, "Willie yuko hapa! Sasa yuko chini, na anataka kukutana na Mwenyekiti Jones.”

Sura ya 124

"Nilijua Bwana Kimaro angefanya jambo kuhusu hilo." Jones Masawe alimwonyesha kidoleLisa na kumwambia, "Tazama, Bwana Kimaro yuko hapa sasa. Afadhali umalizane naye peke yako.”
"Usiende kinyume naye kamwe." Lina alijaribu kumpiga teke alipokuwa chini. "Ikiwa utamkosea tena Bwana Kimaro, hata mimi sitaweza kumtuliza kwa niaba yako."

"Hebu tumshike tu na kumpeleka chini." Pendekezo la Jones lilikubaliwa mara moja na wengi.

Maofisa usalama wanne hadi watano mara moja wakatembea kuelekea kwa Lisa. Akiwa amekunja uso, Shani akawazuia mbele ya Lisa. "Ikiwa nyinyi watu mtathubutu kumgusa, msinilaumu kwa kukosa adabu."

“Nyie mnangoja nini? Washikeni wawili hao sasa hivi." Jones Masawe bado alimchukia Shani kwa kumpiga teke siku nyingine. Sasa ikaja nafasi ya kulipiza kisasi kwake.

Lisa alipogundua kwamba wangepigana, alimzuia Shani. “Ni sawa. Hakuna haja ya kunishika. Nitaenda huko peke yangu." Mara tu alipomaliza kusema, alikuwa wa kwanza kutoka kwenye chumba cha mikutano.

Lina alipendekeza, “Twendeni tukaangalie pia. Ni afadhali kujionea kuliko kusimuliwa.”

“Kweli. Hata hivyo, inabidi tumzuie asimkasirishe Bwana Kimaro zaidi.”
Kila mtu alishuka pia. Wakaelekea kwenye chumba cha mapokezi pale chini. Akiwa amefungwa bandeji nene chini, Bwana Kimaro alikuwa amejikunyata huku akiwa ameshikilia kikombe cha kahawa ya moto. Kutoka kwa sura ya uso wake mzuri, ilionekana wazi kuwa alikuwa ameshikwa na homa na kuugua.

Lisa alipofikiria juu ya tukio la Willie akiwa amelala kwenye sakafu ya choo akiwa amevua nguo zake jana yake usiku, hakuwa na uhakika ni muda gani alikuwa amepatwa na homa hiyo. Pengine alishikwa na homa kwa sababu ya tukio hilo, ambalo lilimfanya akose raha kabisa. Kwa kweli alihisi kwamba mtu asiye na haya kama Willie huenda asisumbuliwe kuhusu picha hizo.

Lisa hakuwa na wasiwasi juu yake mwenyewe kwa vile hakuwa na ndugu pia. Hakukuwa na kitu kingine chochote alichokuwa na wasiwasi nacho, isipokuwa kwamba Alvin angeweza kuvutwa kwenye matatizo tena.

"Samahani sana, Bwana Kimaro." Jones Masawe alimsogelea na kisha akainamisha kichwa kwa kumwomba msamaha kwanza. “Natumai utakuwa mkarimu wa kutusamehe. Usitazame kiwango cha makosa yetu.”

“Hasa.” Mkurugenzi Amiri aliongeza mara moja, "Tumemfukuza Lisa kutoka kwenye nafasi ya mwenyekiti na kumfukuza kutoka bodi ya wakurugenzi."

Willie Kimaro alikuwa ameganda tu, na moyo wake ulikuwa ukitetemeka kwa nguvu. Aliinua kichwa chake huku macho yakiwa yametapakaa damu. "Kwa hiyo yeye si mwenyekiti tena?"

“Ndiyo.” Jones alisema kwa uungwana, “Ni kwa sababu alikudhalilisha. Hatukufikiri Lisa angekuwa na ujasiri wa kukufungia kwenye chumba na kukutongoza. Hiyo haikuwa aibu kwake.” Bila shaka, Jones alijua ukweli vizuri. Hata hivyo, ili kumpa Willie njia ya kutoka, alimshtaki Lisa huku akiamini kwamba Willie angemshukuru.

Alipokuwa akiwaza kabla hajaongea, Willie alimuangaza kwa hasira. Kabla Jones hajapata fahamu zake, Willie aliinua mguu wake na kumpiga teke kali. “Nani aliwaambia nyie kumfukuza Lisa kwenye nafasi hiyo? Nani alisema kuwa alinitongoza? Nyinyi mnajaribu kuniletea matatizo!” Willie alimpiga teke Jones Masawe kwenye mwili wake kwa nguvu. Alikuja kuchelewa sana kuokoa hali hiyo. Ikiwa Alvin angejua kuhusu hilo, labda angepoteza maisha yake kabisa.

Kila mtu alishtuka sana, na hata Lisa pia. Lina akapiga kelele. Alimkimbilia Willie kwa haraka na kumshika mkono. “Acha kumpiga teke, Bwana Kimaro. Huyu ni baba yangu—”

“Nyamaza, btch!” Willie alimpiga kofi usoni, na baadaye akaanguka chini. "Yote ni kazi yako. F*ck! Ninachojutia zaidi ni kukufahamu wewe malaya mkubwa!”

Kama si Lina, Willie asingemkasirisha Lisa, akifuatiwa na Alvin. Licha ya kupigwa na kjeruhiwa, alikabiliwa na upepo wa baridi wa usiku kucha kwenye kibaraza cha hoteli kwa muda wote wa jana yake usiku. Akiwa ameganda kwa baridi, karibu apate hamu ya kuruka kutoka kwenye jengo ili kumaliza mateso yake.

"Unafanya nini, Bwana Kimaro?" Lina alihisi kizunguzungu baada ya kupigwa kofi hadharani. Alipokuwa na Willie kwa siku chache zile, Willie alijifurahisha naye kila siku. Alimfanya na kumgeuza kwa jinsi alivyotaka. Akitaka kwa bibi, twende! Akitaka kwa mpalange twende! Akitaka mdomoni, haya! Alifanya hayo yote kwa nia moja tu ya kujisaidia yeye na Jones kubadilisha mambo katika kampuni.
Hata hivyo, kabla ya kumfanya Lisa ajifunze somo lake, badala yake yeye ndiye aliyepigwa.

Akiwa na huzuni, Lina alilia. “Bwana Kimaro, alikuwa Lisa. Yeye ndiye aliyekuumiza.”

“Najua. Sihitaji uniambie.” Macho ya Willie yakatulia kwa Lisa.

Moyo wa Lisa ulimshtua. Haraka akatoa simu yake na kuizungusha kama ukumbusho kwake. “Bwana Kimaro, wewe—”

“Bi Jones, kuhusu tukio la jana usiku, lilikuwa kosa langu.” Willie alimsogelea na kumuomba msamaha wa dhati. Umati ukakosa la kusema. Lisa naye alishindwa cha kusema. Alipigwa na butwaa kabisa. Kumbe kutumia picha zake zisizo na heshima kumtishia ilifanya kazi? Kweli Alvin alikuwa sahihi, familia ya Kimaro walikuwa wanajali zaidi kuhusu utu wao. Hawakuweza kumudu kuipoteza heshima yao.

Lina na Jones walipapasa macho yao kwa nguvu. Walitilia shaka sana ikiwa macho yao yalikuwa yanawadanganya. "Bwana Kimaro, nadhani umekosea." Lina akaongeza ujasiri wake tena na kuvuta upindo wa shati la Willie. "Umesahau jana usiku -"

“Funga mdomo wako!” Akihisi kukosa subira, Willie alimpiga Lina teke. “Nilikukera kwa bahati mbaya baada ya kulewa jana usiku, Bi Jones. Samahani kwa tabia ya ghafla na ya kimbelembele. Mimi ni fisadi ambaye sistahili kuwa binadamu. Bahati nzuri uliniamsha kwa kunipiga, au ningeharibu sifa ya familia ya Kimaro na kuwadhalilisha wazee wangu.”

Umati ulishangaa na kuhisi kuwa ulimwengu umegeuka kuwa ndoto. Lisa alipepesa macho na kumtazama Willie kwa makini. Je, ilikuwa ni kalamu ya chuma aliyomchoma mbavuni jana yake usiku ambayo ilikuwa imeharibu ubongo wake, au? Alikumbuka vizuri kwamba hakuwa amelewa jana yake usiku. Ingawa alikuwa na picha za kumtishia, hakuhitaji kuwa na tabia ya unyenyekevu hivyo.

Mkurugenzi Amiri alikuwa mwishoni mwa akili yake. “Lakini sisi…”

“Lakini nini? Nyinyi watu mnawezaje kuthubutu kumfukuza Lisa kwenye nafasi ya mwenyekiti na kumfukuza nje ya bodi ya wakurugenzi?!” Macho ya Willie yakawa magumu huku akiwatazama wakurugenzi. “hivi nyinyi wazee mnafikiri kwamba bado mna nguvu sana na hamwezi kufikiria kustaafu? Au mnafikiri kwamba bila nyinyi Mawenzi Investments itafilisika?"

Wakurugenzi walitetemeka na hawakuhisi kwamba walikuwa na umri wa kutosha kustaafu bado. Bado walipanga kufanya kazi kwa miaka kumi hadi 20 kwenye kampuni.

"Bwana Kimaro, tulikuwa bado hatujalipisha hilo," Mkurugenzi Amiri alisema mara moja kwa sauti ya kutetemeka, "Hakufukuzwa kazi yake. Yeye bado ni mwenyekiti, na hii haitabadilika kamwe.”

Mwili wa Jones ulitetemeka. Akiwa amezidiwa na hali ya kutokuamini, alinguruma kwa fadhaa. "Unasema nini, Amiri Gumbo? Nyinyi mlinichagua kama mwenyekiti asubuhi ya leo!”

Mkurugenzi Levy alimtazama kwa hasira. "Wewe na binti yako ndio mlidai kuwa Bibi Jones alimkosea Bwana Kimaro. Kumbe haikuwa hivyo. Hatuwezi kufanya lolote kwa sasa.”

“Hasa.” Wakurugenzi wakaanza kumgeuka.

"Kila mtu anajua kwamba una tamaa ya kuwa mwenyekiti, lakini haukupaswa kupeleka mambo mbali sana huku ukipuuza utu wako." mwingine akamshushua.

"Hata hivyo, Lisa ni sehemu ya familia ya Jones. Hukupaswa kumtendea ukatili hivyo.” Wanahisa walianza kumwambia Jones.

Jones na Lina walionekana wameanguka kutoka mbinguni hadi kuzimu. Kwa hasira, Jones alimfokea Lina, "Ni nini kinaendelea duniani?!"

"Sijui." Lina alikuwa ameduwaa, akishangaa kwa nini kila kitu kilikuwa kimebadilika kabisa usiku mmoja.

Lina ndiye aliyesema kwamba alikuwa amemweka Willie kwenye kiganja cha mkono wake. Yeye ndiye aliyesema kwamba Willie angewasaidia. Yeye ndiye aliyesema kwamba Willie alimchukia sana Lisa hivi kwamba asingeweza kungoja kumuua.

Kwa sura ya kusihi, macho yake yakatua kwa Willie. “Bwana Kimaro, Lisa alikuroga au? Si ulisema hivyo... unanipenda sana?”

Sura ya 125

"Ninakupenda?" Mwitikio wa Willie ulikuwa kana kwamba alisikia mzaha. “Uliingia kitandani kwangu licha ya kuwa una mpenzi. Unafikiri ningekuacha bure? Huna tofauti na makahaba wanaojiuza huko nje.” Kofi lilitua kwenye shavu lake, lakini safari hii, lilionekana kuwa limetua moyoni mwake pia. Lina karibu aanguke chini kabisa.
Kulikuwa na idadi kubwa ya watu karibu naye, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi na wanahisa wa Mawenzi Investments. Hali hiyo ilikuwa imezua tafrani miongoni mwao, wakamtazama kwa dharau.

“Sikutarajia angekuwa mtu wa aina hii. Kabla ya hili, alinipa hisia ya kuwa safi na mtukufu.” Mnong’ono ulisikika.

“Ndiyo. Wanaume wengi katika kampuni walimwona kama mungu wa kike.” Mwinginea naye akatoa yake.

“Bahati nzuri sikumtambulisha kwa mwanangu. Hakika hana aibu.”

Katikati ya fedheha ya mara kwa mara, uso wa Lina ulibadilika rangi. Alikuwa ameweka juhudi nyingi katika kujenga sifa ya kuvutia kabla ya hii, lakini yote iliharibiwa wakati huo.

Kama mwanaye, Jones Masawe alitetemeka kwa aibu. “Umeenda mbali sana, Bwana Kimaro. Lina anakupenda kweli. Alianguka kwa ajili yako mara ya kwanza.”

Bila kutarajia, Willie aliangua kicheko kana kwamba maneno ya Jones yalikuwa ya mzaha. “Anapenda nini kuhusu mimi? Kusema ukweli, baada ya kuwa na wanawake wengi, ninatambua kwamba yeye ndiye mwanamke mlegevu zaidi. Bwana Jones, ninafurahia jinsi unavyomchukulia binti yako kama kitu kwa ajili ya mali na mamlaka.”

Matamshi hayo yalibadilisha mtazamo wa umma kuhusu Lina na Jones kwa mara nyingine tena. Lisa, ambaye alikuwa akitazama tu tukio hilo, naye alishangaa. Hakushangaa kwamba Willie alikuwa mpotovu, kilichomshtua zaidi ni kwamba Lina aliweza kukubali.

Lisa alitoa kikohozi chepesi kisha akatabasamu na kumtazama Lina. “Dada siwezi kujizuia kukuona kwa mtazamo tofauti sasa. Je, wakati huo ulinipokonya Ethan kwa kutumia mbinu kama hiyo?” Swali hilo liliukumbusha mara moja umma wa watu kuhusu uhusiano wa awali wa Lina na Ethan.

Kila mtu alimtazama Lina kwa unyonge sana. Hata walijiweka mbali naye, wakiogopa kwamba angewachafua. Kutetemeka kulitawala mwili mzima wa Lina. Alitoa macho yake moja kwa moja, akijifanya kuzimia kwa hasira kali.

“Linal” Jones alimbeba upesi na kutoka ukumbini kwa aibu.

Willie alikunja uso. Kisha akageuza kichwa chake na kumtazama Lisa. "Alikuwa na mpenzi hapo awali?"

“Ndiyo. Hata wakachumbiana kwa sherehe kubwa. Hata hivyo, mara moja alimlenga mtu mwingine kwa sababu mpenzi wake wa zamani aliondolewa kwenye madaraka ya kampuni.” Lisa alimtupia jicho la ajabu. "Ulidhani kuwa wewe ndiye mwanaume wa kwanza kulala naye?" Willie alishindwa cha kusema. Hakika hilo ndilo alilolidhania lakini hakuweza kujihakikishia.

Akifikiria kwamba alimsaidia kushughulika na Jones na Lina, Lisa alimkumbusha hivi kwa fadhili, “Mambo fulani yanaweza kutengenezwa tu katika ulimwengu huu.”

“,..Bila shaka, najua hili, hehee! Asante kwa kunikumbusha.”
Kwa kujieleza kwa aibu, Willie alitabasamu bila kupenda. "Sasa naweza kustahili mshamaha wako, Bi Jones?"

Kwa kweli, Lisa hakuelewa ni nini kilikuwa kikiendelea kichwani mwake. Kabla hajamjibu alimuuliza, “Naweza kuwa na maneno machache nawe, Bwana Kimaro?”

“Hakika. Hakuna shida." Lisa alitoka ofisini huku Willie akimfuata. Miguu yake ilitetemeka baada ya kumtazama Shani aliyekuwa pembeni yake.

Shani alimtazama kwa tabasamu. “Uko sawa, Bwana Kimaro?”

“Mimi…Niko sawa. Kweli, wewe ni mtaalamu sana." Willie alihisi bomu la atomiki likilipuka kichwani mwake. Lisa alilindwa na Shani mahiri, ambaye alitoka ONA.

ONA lilikuwa kundi la siri zaidi la chini kwa chini chini ya familia ya Kimaro. Ilijumuisha maveterani kutoka jeshini na washiriki kutoka kwenye tasnia za sanaa ya mapigano ya kimwili. Kwa muda huo, ilisimamiwa na Alvin pekee. Lisa alimroga vipi Alvin hadi akawa naye? Shani alikuwa anashangaa kila siku, alimfahamu vizuri Alvin.

Jinsi Willie alivyomtazama Lisa sasa ilikuwa tofauti kabisa.

Lisa alisimama baada ya kufika umbali fulani. Shani kwa makusudi alienda mbali zaidi ili kuwapa nafasi wawili hao. Lisa alikaa kimya akimsubiri Willie amuulize kuhusu zile picha. Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hakusema neno. Alimtazama hata kwa mchanganyiko wa kupendeza, woga, na hofu.

Lisa alikosa la kusema kabisa. “Vema… Bwana Kimaro, unakumbana na madhara yoyote kutokana na kupigwa jana usiku?”

“Hapana kabisa. Badala yake nimekuwa mwenye busara.” Willie alitabasamu. “Bi Jones, ni heshima yangu kubwa kuweza kukutana nawe hapa Dar es Salaam. Tunaweza kuwa marafiki?"

“Lakini picha…”

Willie alipunga mkono wake. "Unaweza kuhifadhi picha ukipenda."
Lisa alijikuta midomo yake ikitetemeka. Kwa nini ahifadhi picha zake zisizo na heshima? “Usinilaumu kwa kukuvua nguo na hata kukufedhehesha jana usiku…”

Willie aliganda na kusema kwa kusitasita, “Ulikuwa unasema ukweli tu. Ningewezaje kukulaumu… Ah-choo!” Alijifuta pua kwa aibu huku komeo lake likishuka. "Bi Jones, nijulishe ikiwa unahitaji msaada wowote. Nitajitahidi kukusaidia.”

Baada ya kuwa kimya kwa muda, Lisa aliuliza, "Labda ulipiga picha za Lina akiwa amelala nawe, sivyo?"

Willie alipigwa na butwaa. Kwa jinsi alivyokuwa akimtazama Lisa ni kana kwamba ni rafiki yake wa karibu. "Sikutarajia ungenijua vizuri."

Lisa alijisikia vibaya. Kwa hakika alikutana na baadhi ya vitabu vya saikolojia na akajifunza kwamba wapotovu kama yeye kwa kawaida wangepiga picha za aina hiyo. “Hapana, mimi—”

"Naelewa. Nina idadi kubwa ya video zake. Unapanga kushughulika na Lina, sivyo? Ninaweza kukutumia video hizo sasa, lakini… Usiwahi kuzionyesha kwa mtu yeyote, hasa mpenzi wako.”

Ikiwa Alvin angegundua kuwa Lisa alitazama video hizo, bila shaka angemtoa utumbo Willie akiwa hai. Lisa alipigwa na butwaa. Wazo la ajabu likaangaza akilini mwake. “Sawa.” Aliitikia kwa kichwa.

Willie alimtumia video hizo mara moja. Alipopokea video hizo, Lisa alionekana kutojali kwa nje, lakini msukosuko wa mhemko ulikuwa tayari umeanza ndani yake. Kwa kweli, alikuwa ameomba tu video hizo kwa njia ya kawaida. Alidhani kwamba Willie asingeweza kuzituma kwake kwa kuzingatia tabia yake ya kishenzi jana yake usiku. Hata hivyo, alionekana kuwa tofauti kabisa leo. Alikuwa na hakika kwamba haikuwa tu kwa sababu ya picha zisizofaa alizotumia kumtishia, kulikuwa na sababu nyingine.

"Alvin, kwa nini uko hapa?" Ghafla, alitazama mahali fulani nyuma ya Willie wakati akiuliza.

Willie alitetemeka sana kwa hofu. Alivaa tabasamu la kubembeleza na kugeuka nyuma, na kugundua kwamba hakukuwa na mtu nyuma yake. Alipigwa na butwaa kwa muda. Hapo hapo akahamishia macho yake kwa Lisa ambaye alikuwa na sura ya ajabu machoni mwake.

“Bwana Kimaro, unamfahamu Alvin? Kwa nini ulionekana kuwa na wasiwasi na hofu nilipoita jina lake?” Wazo lisiloaminika likamwingia taratibu kichwani Lisa. "Majina yenu nyote wawili ni Kimaro. Je! inaweza kuwa hivyo…”

“Sijui unasema nini. Hata simfahamu Alvin.” Akiwa amechoshwa, Willie alitikisa mkono wake kwa haraka.

Lisa alicheka. "Kwa kuzingatia utu wako, wewe ndiye mtu ambaye utafanya chochote ili kufikia malengo yako. Wewe ni mkatili na unapenda kulipiza kisasi, kwa hivyo haishangazi kwamba hata picha zako nilizonazo hazikubabaishi. Kama huna mpango wa kuniambia, nitarudi na kumuuliza Alvin kisha…”

TUKUTANE KURASA 126-130

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI.........LISA
KURASA... 126-130

Sura ya 126

“Usifanye, usifanye.” Kwa kufikiria onyo la Alvin jana yake, Willie alimzuia Lisa mara moja. “Alikataa kuniruhusu nikuambie kuhusu hilo. Kwa kuzingatia kwamba nimeshiriki video zangu za faragha na wewe, tafadhali unaweza kujifanya kuwa hujui lolote, Bi Jones?”

Lisa alishangaa kusikia hivyo kutoka kwa Willie. Alvin alikuwa kweli mtoto wa familia tajiri ya Kimaro? Kwa kuwa Willie alikuwa akimheshimu na kumuogopa sana Alvin, inawezekana kwamba Alvin alikuwa na nguvu kubwa kuliko Willie? Inawezekana kuwa yeye ndiye mrithi wa familia ya Kmaro? Asingeweza kamwe kufikiria kuichokoza familia ya Kimaro. Familia ilikuwa ngumu sana kwa mtu wa kawaida kama yeye kufikiria.

“Sawa, nakuahidi, lakini naweza kujua Lina alikufahamu vipi?” Lisa aliuliza huku akijilazimisha kutulia.

"Ni Stephen ambaye alimtambulisha kwangu," Willie alidhihaki, "Msaidizi wangu anafahamiana na familia ya Kileo. Stephen alitaka kuanzisha uhusiano nami, kwa hiyo akamtuma mpenzi wake kwangu.”

Lisa alishangaa “Unafurahia kulala na rafiki wa kike wa rafiki yako?”

Willie alitoa kikohozi kidogo. “Kweli, mke si mtamu kama mchepuko. Inavutia zaidi kulala na mpenzi wa mtu mwingine.”

Lisa alikosa la kusema. Alikuwa na shauku kubwa ya kumuuliza ikiwa yeye ndiye pekee mwenye tabia mbovu katika familia nzima ya Kimaro au ikiwa kuna wengine wote walikuwa hivyo, ikiwemo Alvin, lakini hakufanya hivyo.

Baada ya kurudi ofisini, Lisa alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa. Hapo awali aliolewa na Alvin kwa kudhani kuwa alikuwa mjomba wa Ethan. Baadaye, aligundua kwamba alikosea na akafikiri kwamba Alvin alikuwa wakili tu. Nani alijua kuwa yeye alikuwa mtoto wa familia tajiri na maarufu zaidi nchini?

Naam, haikumshangaza. Badala yake, aliona kuwa ilikuwa na mantiki. Huenda Alvin alikuwa akimpima. Ikiwa angekutana na Alvin akajiweka wazi utambulisho wake, angehisi kwamba amempenda kwa ajili ya mali zake. Vilevile Alvin angempeleka kumtambulisha nyumbani kwao, familia yake labda isingemkubali.

Ghafla, alihisi kuchoka. Ili kujizuia kuwaza kupita kiasi, alibofya kipande kimojawapo cha video ambazo Willie alimtumia. Mwanzoni, alikuwa akijaribu tu kuangalia juujuu. Kinyume na matarajio yake, video hiyo iligeuka kuwa ya kufurahisha sana hivi kwamba Lisa ambaye alikuwa hajakomaa kama Lina aliguna.

Alipotambua kwamba alikuwa amezama katika video hiyo, Shani alimkumbusha hivi kwa uchungu, “Bi Jones, ulisema hutaitazama, sivyo? Zaidi ya hayo, Bwana Kimaro hatakuruhusu kutazama aina hii ya mambo.”

"Lo... Hatajua kama utatunza siri." Lisa alitoa tabasamu la aibu. Kwa kuwa Alvin asingemruhusu hata kutazama picha zisizofaa za Willie, bila shaka angemchuna akiwa hai iwapo angejua kuhusu jambo hili. Shani alishindwa cha kusema. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kulifumbia macho.

Lisa alipokuwa akiitazama video hiyo, wazo zuri lilimjia. Alimwita msaidizi wake haraka. “Nakumbuka mjukuu wa Amiri alisema kwamba kuna mnada unakuja?”

“Ndiyo, ni usiku wa leo. Mratibu wa manada amekualika pia kwenye tukio. Watu wengi matajiri wa hapa Dar na mikoa mingine watahudhuria.”

“Sawa. Hata mimi nitaenda.” Lisa alicheka. Leo itakuwa siku ya giza zaidi katika maisha ya Lina.
•••
Hotelini Baada ya kutoka kwenye ofisi za Mawenzi Investments, Willie alikuwa tayari kufungasha vitu vyake na kuondoka Dar. Kukaa katika jiji moja na Alvin kulitisha maisha yake. Alipousukuma tu mlango wa chumba, alimuona mtu mrefu akiwa ameketi kwenye kochi la ngozi, akifanana na mfalme. Miguu yake iligeuka kuwa milegevu kama mlenda, na midomo yake iliendelea kutetemeka. “Kaka Alvin, umekuja kwa wakati ufaao. Nilikuwa karibu kukuambia kuwa nilienda Mawenzi Investments na kusuluhisha suala hilo. Hakuna mtu atakayethubutu kumsababishia Lisa matatizo tena.”

“Najua. Umefanya vizuri sana.” Alvin alikaa pale bila wasiwasi huku hisia za heshima kubwa zikitoka kwenye uso wake mzuri. Willie alijawa na furaha moyoni kusikia hivyo. Kabla hajaongea, midomo myembamba ya Alvin ilianza kusonga. "Lakini ... hakushuku chochote?"

Mara tu Alvin alipomaliza kuongea, hali ya wasiwasi na hofu ilitawala mazingira. Moyo wa Willie ulionekana kuganda.

“Usinidanganye, Willie,” Alvin alionya kwa upole, “unakumbuka kilichotokea ulipokuwa na umri wa miaka 18 baada ya kunidanganya, sivyo?”

Willie akatetemeka. Mwaka aliofikisha miaka 18 ulikuwa mwaka wake wa giza kuwahi kutokea.

"Yeye ... alishuku." Huku akitetemeka kama jani linalopigwa na upepo, Willie aliogopa sana kumficha. "Sasa anajua kwamba unatoka katika familia ya Kimaro, lakini sikumwambia makusudi kuhusu hilo. Yeye ndiye aliyenitega, na nilifanya makosa. Zaidi ya hayo, majina yetu ya mwisho ... "

Alvin akasugua macho yake. Alijua mapema kwamba Willie, mpuuzi yule kijana, angeshindwa kufanya kulingana na maagizo yake na kuishia kumuumbua zaidi.

Willie alisema kwa kigugumizi, “Kaka Alvin, una wasiwasi kwamba atajikombakomba kwako na kukusumbua baada ya kukujua wewe ni nani? Kwa kweli, hii ni kawaida sana kwetu. Haijalishi tunaenda wapi, wanawake wengi humiminika kwetu. Hata hivyo, hadhi yake ni ya chini sana kuwa mpenzi wako.

"Nyamaza." Macho makali ya Alvin yalimkumba. "Ondoka Dar mara moja."

“Sawa, sawa. naondoka sasa hivi kaka.” Willie pia hakujisikia kubaki mahali hapo pabaya palipomchachia. Mara moja akafungasha vitu vyake na kuondoka kama anayefukuzwa.

Alvin aliinuka na kuelekea kwenye dirisha lililokuwa ndani ya chumba hicho. Akili yake sasa ilikuwa imevurugika kabisa Alikuwa mtu mwenye shaka. Alipokuwa akiishi katika neema ya utajiri wa familia ya Kimaro tangu alipokuwa mdogo, wanawake wengi walikuwa wamemtumia kwa kisingizio cha kumpenda kwa sababu ya utambulisho wake, jambo ambalo lilimjaza chuki. Kwa hiyo, hakuwahi kumwambia Lisa kuhusu utambulisho wake halisi, akitumaini kwamba angempenda yeye kama yeye na si kwa utajiri wake. Hata hivyo hakuna marefu yasiyo na ncha. Hatimaye Lisa alikuwa amejua kuhusu utambulisho wake. Angemwonaje?

Hans alimwambia kwa upole, “Usijali, Bwana Kimaro. Lisa alikupenda tangu alipokutana nawe kwa mara ya kwanza kwenye baa. Wewe ndiye anakupenda, na haihusiani na utambulisho wako.”

"Hiyo ni sawa." Alvin alijisikia raha. Kweli, kwa nini alikuwa anafikiria kupita kiasi? Alikuwa ameanguka kwa ajili yake bila matumaini, kama yeye mwenye alivyosema.
•••
Saa kumi na moja jioni, gari jeusi lililoonekana kuwa la gharama kwa mwonekano wake lilikuwa limeegeshwa nje ya mlango wa jengo la Mawenzi Investments. Muda mfupi baadaye, Lisa alishuka kwenye gari huku yule aliyekuwa kwenye kiti cha dereva akivua koti lake. Alionekana akiwa amevalia shati jeupe chini ya fulana, ambayo ilisisitiza umbo lake refu. Akiwa na sura nzuri ya kuvutia, alitoka kama mhusika kutoka kwenye kitabu cha hadithi za kubuni.

Ingawa alimuona kila siku, sura yake ya kuvutia haikukosa kumshangaza. Hakika asngechoshwa na sura ya mwanaume huyo.
Alipojua kuhusu utambulisho wake siku hiyo, alikuwa akipingana na mawazo yake kila mara. Hata hivyo, wakati huo, alikuwa na hakika kwamba asingeweza kuvumilia kumwacha mwanamume huyo.
Siku zote alikuwa mtu ambaye alikaa karibu naye katika nyakati ngumu zaidi. Siku hiyo, alimsaidia kukabiliana na dhoruba tena. Haijalishi jinsi gani safari yao ya mbele ingekuwa ngumu, alisisitiza kuwa pamoja naye.

“Mbona unanitazama?” Alvin alibana ncha ya pua yake, alikuwaakijshtukia.

Lisa aliitazama saa iliyokuwa kwenye mkono wake, jambo ambalo lilimkumbusha jinsi alivyokuwa akimshangaa kwa aina ya nguo zake. Ikamjia akilini kwamba huenda nguo hizo zilikuwa zikificha utambulisho wa Alvin kwa makusudi.

“Ninautazama uso wako mzuri. Pia, niko katika hali nzuri leo. Uliona jinsi Jones na Lina walivyofedheheka? Lina siku zote alijifanya kuwa safi na aliishi kwa unafiki wakati huo. Sasa, kila mtu anamdharau.”

“Ndiyo.” Baada ya kumsikia akipiga kelele, Alvin aliinua macho yake na kuuliza, "Kuna chochote unachotaka kuniuliza?"

Sura ya 127

Lisa alipigwa na butwaa. Alikuwa amepanga kumuuliza Alvin kuhusu utambulisho wake halisi. Hata hivyo, uhakika wa kwamba alimwomba Willie afiche utambulisho wake ulionyesha kwamba hakutaka kumfunulia. Katika hali hiyo, hakujisumbua kumuuliza.

"Hapana." Alvin taratibu akadondosha macho yake. Lisa alimtazama wakati huo na kusema, “Nitahudhuria mnada usiku wa leo, kwa hivyo sitakuwa nyumbani kwa chakula cha jioni. Unataka… kwenda pamoja nami?” Aliuliza kwa tahadhari ingawa alihisi kwamba Alvin asingekubali kwenda pamoja naye. Kwa kuzingatia tabia yake ya kiburi na dharau, asingependezwa na tukio la aina hiyo.

“Sawa.” Alvin akakubali.

“Huu?” Lisa aliduwaa, akifikiri kwamba alimsikia vibaya.

“Nimesema sawa. Mbona unashangaa?” Alvin alitazama sura yake iliyopigwa na tabasamu.

"Lakini hupendi kushiriki katika hafla zinazofanyika Dar se salaam, leo imekueje?"

"Ninakuja ili kuzuia wanaume wowote wasikucheze." Alvin alijibaraguza. Aliendesha gari kwa umakini huku macho yake yakiwa yametazama barabara iliyo mbele. Lisa aligeuza kichwa chake na kutazama wasifu wake kamili kwa muda. Hakuweza kujizuia kumpa busu la shavuni. Usukani uliokuwa mikononi mwake ulitetemeka, kisha akamwambia kwa utani, “Usinichezee kimapenzi ninapoendesha gari.”

Sentensi hiyo ilionekana kuwa ya kawaida. Lisa alicheka na kujibu, “Najua. Itasababisha ajali mbaya sana, si ndiyo?"

"Hapana." Akamtazama. "Itasababisha moyo wangu kuruka."

Mapigo ya moyo wa Lisa yakagongana na kifua. Hali isiyoeleweka ilionekana kujaa kwenye mishipa ya mwili wake mzima. Moyo ulimwenda mbio zaidi baada ya kumbusu. Wakati huo, alikuwa na hamu kubwa ya kumbusu kwa mapenzi. Hata hivyo, alitilia maanani zaidi usalama barabarani.

Saa moja na nusu usiku, Mnada ulikuwa karibu kuanza katika jumba la mikutano la Karimjee. Watu mashuhuri kutoka Dar es Salaam na mikoa jirani waliingia ukumbini mmoja baada ya mwingine. Kama mwenyekiti wa Mawenzi Investments, Lisa alionekana kuwa kivutio cha tukio hilo. Umati ulimsonga mara tu alipoingia ndani.

Ethan naye alikuwepo. Alivyoona jinsi Lisa anafuatwa sana na watu kwa mbali, Ethan alijawa na uchungu. Kamwe katika ndoto zake hakutarajia kuwa mpenzi wake ambaye awali alimwacha kwa ajili ya Lina angekuwa mwenyekiti mpya wa Mawenzi Investments ndani ya muda mfupi. Wakati huo watu wengi walimwona mpumbavu. Kwa kweli, Ethan alikuwa mpumbavu. Alimkosea kipumbavu sana Lisa na kwa hivyo akakosa nafasi ya kuwa naye. Akiwa na mwanamume bora kando yake sasa, aliona kwamba asingekuwa na nafasi yoyote kwake.

Mchumba wake mpya, Tracy Laizer, alikuwa ameketi kando yake na kuubana mkono wake. "Nilisikia kwamba yeye ni mpenzi wako wa zamani, ni kweli?"

'Yote ni ya zamani." Ethan alilazimisha tabasamu. Alijua kwamba angeweza tu kufanya kazi kwa bidii ili kuifurahisha familia ya Laizer kwa sasa.

“Ni vizuri kwamba unajua. Maadamu unanipenda sana, familia yangu itakutegemeza,” Tracy alisema kwa upole.

Upande mwingine, Lisa naye alimwona Ethan pia kwa sababu ya suti yake nyeupe iliyovutia. Mwanamke wa ajabu kutoka familia mashuhuri alisimama kando yake. Moyoni mwake, Lisa alihema huku akimfikiria mwanaume ambaye aliyemuona kuwa mkamilifu wakati ule. Kinyume na matarajio yake yote, mwanamume huyo aligeuka kuwa mtu ambaye angemsaliti kwa ajili ya mamlaka na umaarufu.

“Unamtazama Ethan?” Ghafla sauti ya Alvin ya kuonya ilisikika.

"Nilikuwa nikifikiria juu ya jambo fulani."

“Ulikuwa unafikiria nini?” Alvin alikasirika.

"Yajayo yanafurahisha. Onyesho nzuri inakuja. Utajua baada ya muda mfupi.” Lisa aliinua uso wake, macho yake angavu yaking'aa kwa ucheshi. Uso wa Alvin ukalegea taratibu.

Wanawake kadhaa ambao waliolewa na wafanyabiashara matajiri walimzunguka Lisa na kumpongeza.

“Mwenyekiti Jones, hili gauni umenunua wapi? Ni nzuri!"

"Mkufu uliovaa umetoka kwa Tiffany na ndio muundo mpya zaidi, sivyo?"

"Habari za jioni, the bosy lady?"

Ghafla Janet alishika glasi ya mvinyo mwekundu na kumsogelea Lisa kwa nia mbaya. “Ah, Mwenyekiti Jones, sikutarajia kwamba ungekuwa na jeuri ya kushiriki katika mnada. Subiri kidogo, sina uhakika kama bado nitakuita Mwenyekiti Jones sasa hivi.”

"Unamaanisha nini, Bi Kileo?" mmoja wa wanawake hao, Madam Clark, aliuliza huku akihema.

Janet akahema. “Pengine ninyi nyote hamfahamu kilichotokea. Nilisikia kwamba Mwenyekiti Jones alimpiga Willie Kimaro aliyetoka Nairobi wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya Mawenzi Investments jana usiku.”

"Nini? Unamaanisha huyo Willie kutoka familia ya Kimaro?"

"Ndio, ni yeye." Janet akaitikia kwa kichwa. “Rafiki yangu aliniambia kwamba Mwenyekiti Jones alisababisha uso wa Bwana Kimaro kuvimba, na Bwana Kimaro alikasirika sana. Sijui hata atafanya nini! Hiyo ilikuwa ni sawa na kujitakia matatizo makubwa sana kwako, Mwenyekiti Jones. Hivi mtu kama wewe unawezaje kuichokoza familia ya Kimaro? Natumai utakuwa uko salama na unaendelea vizuri nitakapokuona tena.”

Wanawake wote walishtuka na kurudi nyuma mmoja baada ya mwingine.

"Halo, mume wangu ananiita."

"Imekuwa muda tangu tulipokutana mara ya mwisho, Madam Ngololo."

Muda mfupi baadaye, kundi la wanawake lilitoa visingizio na kuondoka mahali hapo mara moja. Hawakuwa tayari kukaribiana na mtu aliyeiudhi familia ya Kimaro. Tukio hilo halikuwa la mzaha. Walijua kuwa kwa kuwa Lisa alikuwa ameichokoza familia ya Kimaro, alikuwa amejihukumu kifo. Ingekuwa haina maana kumsogelea.

Bila kujisumbua kuliweka wazi jambo hilo, Lisa alimkazia macho Janet kana kwamba ni mlemavu wa akili. Ikizingatiwa kuwa alikuwa na uhusiano wa kirafiki na Lina, kwa nini Lina hakumwambia ukweli?

"Lazima uwe na hofu, sawa? Pengine hukutarajia kwamba utapoteza nafasi ya mwenyekiti wakati ndio kwanza umeanza kuifurahia.” Janet alitabasamu kwa kuridhika kisha akageuka kumtazama Alvin. "Bwana. Kimaro, nakushauri ujiepushe naye ili usije ukaingizwa kwenye matatizo haya.”

Alvin alimwangalia tu bila kujali alichosema. Janet alifikiri kwamba maneno yake yalikuwa yameamsha kupendezwa kwake, hivyo mara moja akasema, “Msaidizi mkuu wa Willie ni jamaa yangu. Ukija na kuniomba msaada, hakika nitakuunganisha naye.”

Kwa namna fulani, Lisa alihisi kucheka. Hata Willie alimuogopa sana Alvin. Kwa wazi, msaidizi maskini asingekuwa na maana yoyote kwake.

“Alvlisa, mpuuze tu huyu kichaa. Hebu tutafute nafasi tukae.” Alisonga mbele huku akimshika mkono Alvin. Hakuwa hata na muda wa kupoteza kumwambia Janet ukweli.

Akiwatazama wanaondoka, Janet alicheka nyuma yao. Aliweza kuwa ameridhika kwa muda huo, lakini kile ambacho kingefuata kingemwacha akilia baadaye.

Mara baada ya kuketi, Alvin alimtazama mwanamke aliyekuwa kando yake kwa namna ya kinyonge. “Kwanini usingelifafanua sasa hivi hilo jambo lako? Au lina uhusiano wowote na madai yako kwamba yajayo yanafurahisha?”

"Unanielewa vizuri, Alvilisa." Lisa alitabasamu.

Alvin aligundua kuwa tangu Lisa awe mwenyekiti, alikuwa na ujuzi zaidi wa kucheza na wengine. Baada ya kusema hivyo, halikuwa jambo baya hata kidogo. Ilibidi awe mwovu na mkatili zaidi ili ahitimu kuwa mke wake katika siku za mbeleni.

Mnada ulianza muda mfupi baadaye. Kwa kweli, mnada wa usiku huo ulikuwa tukio la kuchangisha harambee fulani. Lisa aliinua kadi yake ya zabuni kwa picha mbili za uchoraji zenye thamani ya shilingi milioni kadhaa. Bidhaa ya mwisho ilikuwa 'Mkufu wa Malkia'.

Ulikuwa ni mkufu unaometa na kishaufu cha almasi ya rubi inayong'aa ukiwa umeketi juu ya satin nyeusi. Mkufu huo uliundwa kwa ustadi. Hata mnyororo huo ulipambwa kwa almasi ndogo, ambayo ilifanana na safu ya nyota.
Wanawake wote walishangaa kuuona ule mkufu, na pia ulikuwa umemvutia Lisa.

Alvin alimtazama Lisa kwa macho ya kina. Kwa wakati huo, mwendesha mnada alianzisha kwa shauku, "Sasa ni wakati wa kuvutia zaidi. Hapo awali, mfalme wa zamani wa nchi fulani alipata mbunifu mzuri zaidi wa kuunda mkufu, na ilimchukua miaka miwili kuukamilisha. Kito hiki kina karati 383.4 za almasi. Kuna uvumi kwamba ikiwa mtu atampa mwanamke wake mpendwa Mkufu huu wa Malkia, watakuwa pamoja milele. Huu ndio mkufu ambao kila mwanamke anauota. Zabuni ya kuanzia kwa bidhaa hii usiku wa leo ni shilingi bilioni 1.6.”

Bei hiyo ya ajabu ilizua taharuki ukumbini. Hata hivyo, upesi mtu fulani akapaza sauti na kusema, “bilioni 1.7.”

Kwa udadisi, Lisa alitazama upande ule, na kugundua kuwa alikuwa ni Ethan.

Sura ya 128

Kila mtu alianza kumzungumzia Ethan.

“Ni Ethan kutoka Lowe Corporation. Ni mkarimu kiasi gani kwake.”

"Nilisikia kwamba yuko kwenye uhusiano na yule mwanadada kutoka katika familia tajiri ya Laizer, yule tajiri wa Tanzanite."

“Naona. Familia ya Laizer ni maarufu sana huko Mererani. Bwana Laizer ameopoa mawe ya thamani ya bilioni sana juzijuzi tu, atakuwa na pesa sana.”

“Hasa. Lakini mwenyekiti wa sasa wa Mawenzi Investments, Lisa Jones, alikuwa ni mpenzi wake wa zamani.”

“Mpenzi wa Lisa wa sasa hana kitu, yeye ni wakili tu. Nadhani hawezi kumudu kumnunulia mpenzi wake mkufu huu wa gharama.”

Wakiwa wameingia kwenye tmajibizano ya kidaku, ghafla umati wa watu ukahamishia macho yao kwa Lisa. Lisa hakutarajia kwamba angehusika katika mazungumzo hayo. Haraka alimshika Alvin na kusema kwa sauti ya chini, “Usijisumbue kuhusu yale ambayo wengine wanasema. Maoni ni kama mapambo tu. Kimsingi, hayana faida yoyote isipokuwa kwa kuvutia pongezi kutoka kwa wengine. Ni kama vitu vya mitumba ambavyo havifai kuvitumia."

Alvin alimtazama Lisa kwa umakini. Kwa kweli aliona kuvutiwa kwake na Mkufu wa Malkia kupitia macho yake. Alifikiri kwamba angemwomba amnunulie, akizingatia kwamba alikuwa amejua kuhusu utambulisho wake kwamba alikuwa tajiri mkubwa kutoka familia maarufu ya Kimaro. Kinyume na matarajio yake yote, itikio lake lilikuja kama mshangao. Haishangazi kwamba walisema mwanamke atasaidia kuokoa pesa za mwanamume ikiwa kweli alikuwa akimpenda. Alikunja mdomo wake kuwa tabasamu la kupendeza, akainua kasia yake ya zabuni na kusema kwa sauti ya kiume na ya kiburi, "bilioni 2.5."

Akiwa ameduwaa, Lisa alihisi kana kwamba kichwa chake kilikuwa kinamlipuka. “Umerukwa na akili? Nilikuambia usiweke dau lolote.”

"Bilioni 2.6." Janet, ambaye alikuwa karibu, ghafla aliinua kasia yake ya zabuni.

Lisa alimshika mkono Alvin. “Acha kuinua kasia yako. Hakika hawezi kumudu. Anapandisha bei kwa makusudi kujionyesha tu ili akuvute na wewe umpandie kwa juu.”

Alvin hakuweza kuwa na wasiwasi juu yake. Alitumia mkono mwingine kuinua kasia yake. "Bilioni tatu." Ukumbi mzima ulikumbwa na ghasia baada ya Alvin kutaja bei hiyo iliyoonekana kufunga mnada.

Akiwa na shilingi bilioni 2.3 kuwa kikomo chake, Ethan alimkodolea macho Alvin kwa uchungu. Alvin alikuwa mkatili kiasi gani! Ethan alikunja ngumi kwa kutoridhishwa kwani si tu kwamba alishindwa kumpiku Alvin kumnyakua Lisa, bali pia alishindwa kumpiku kuunyakua ule mkufu.

Tracy aliyekuwa kando ya Ethan alipumua kwa husuda. “Sawa, inatosha. Mkufu wa thamani ya bilioni tatu si wa mchezo hata kidogo."

“Ndiyo.” Ethan alitazama chini, akivumilia maumivu yake ndani kabisa.

Tena, Janet aliinua mkono wake ili kupandilia dau. Alvin alitoa macho yake ya ajabu ghafla. “Unaweza kuinua mkono wako na kuropoka bei unayotaka, lakini sitakupandilia tena. Fikiri kwa makini ikiwa kuna pesa za kutosha mfukoni mwako kabla hujafanya hivyo.”

Mkono wa Janet ukaganda, akasita mara moja. Kwa kweli, alikuwa akijaribu tu kuongeza bei ili kumkomoa Alvin.

Stephen kwa haraka akaondoa kasia yake na kumwonya kwa hasira, “Usiwe mpuuzi. Ikiwa kweli utatumia mabilioni ya pesa za familia yetu kwenye mkufu tu, niamini, nitakupiga kofi hadi kufa."

Akiwa amekasirika, Janet alinyamaza kimyaa! Lakini, kwa kweli alikuwa na wivu wa ndani kwa ndani kwa wazo la utayari wa Alvin kutumia shilingi bilioni tatu kwenye mkufu kwa ajili ya Lisa. “Kaka, mbona Alvin ni tajiri kiasi kwamba anaweza kutumia mabilioni ya shilingi kirahisi rahisi tu? Inawezekana kwamba anatoka kwa familia ya Kimaro? Inawezekana kuwa ni ndugu yake na Willie Kimaro?”

"Nyamaza. Hiyo haiwezekani." Stephen hakukubaliana naye kabisa. “Sijawahi kusikia hivyo. Tofauti na yeye, tunahitaji kiasi kikubwa cha pesa kwa mtiririko wa biashara wa kampuni. Nadhani anatumia mapato yake ya uanasheria kununua mkufu. Labda anafikiria kuwa nafasi ya Lisa kama mwenyekiti wa Mawenzi Investments ni ya kudumu na kwamba thamani yake itakuwa ya mamia ya mabilioni ya shilingi. Kwa hivyo, anajaribu kugusa na kukamata moyo wake kwa kutumia bilioni hizi tatu. Kwa bahati mbaya, anashindwa kutambua kwamba Lisa atapoteza nafasi hiyo kwa muda mfupi tu.”

Hatimaye kulikucha kwa Janet, lakini alibaki na hasira. “Kaka, si alimkosea Willie jana? Kwa nini hajamfundisha somo?”

Stephen alipigwa na butwaa. Alipokumbuka kutoweza kumpata msaidizi wa Willie siku hiyo, ghafla alihisi kuzama. Punde si punde, alihisi kwamba alikuwa akiwaza kupita kiasi. "Nilisikia Bwana Kimaro aliumia sana jana usiku, kwa hivyo huenda labda hajapata nafuu."

“Kwa yote ambayo Lisa alimfanyia, hakika hatamwacha salama hadi ahakikishe kuwa amekufa." Janet alitoa tabasamu.

Sura ya 129

Hatimaye, Alvin alipata zabuni ya juu zaidi ya mkufu huo kwa bei ya shilingi bilioni tatu. Msimamizi wa mnada kwa tahadhari alimkabidhi Mkufu wa Malkia mbele ya macho ya kila mtu. Alvin akautoa ule mkufu mwekundu uliokuwa unameremeta kwa umaridadi. Alipoutoa nje, alimwambia Lisa ambaye alikuwa ameduwaa kwa sauti nzito, “Simama.”

Lisa alisimama huku akionekana kuchanganyikiwa. Umbo lake la kuvutia lilionekana katika macho yake angavu na safi.
Midomo maridadi na myembamba ya Alvin ilijikunja na kuachia tabasamu la kupendeza. Akainama kidogo na kuuweka ule mkufu shingoni mwake. Sauti yake ya kiume, tulivu ilisikika kwa mtetemo wa kupendeza. "Kuanzia leo na kuendelea, utakuwa malkia wangu."

“Wow!” Mwanamke mmoja kando yake alishtuka kwa mshangao.
Moyo wa Lisa ulikuwa unadunda. Ijapokuwa bei ya mkufu huo iliufanya moyo wake kumuuma sana kiasi cha kuvuja damu, tukio hilo lilikuwa limegeuza mnada kuwa harusi yao. Mwanaume huyo alikuwa ametimiza matakwa yake yote.

Kilichomshangaza zaidi Lisa ni tabia ya kimapenzi ya Alvin. Ule mkufu mwekundu wa almasi uliokuwa umeketi kwenye ngozi yake ya chokoleti ulikuwa unameremeta. Ulimfanya aonekane kama malkia wa heshima. “Asante. Nakupenda sana Alvilisa." Lisa alisimama kwa vidole vyake na kumbusu mdomoni hadharani. Ilikuwa ni denda zito haswa la karibia dakika nzima.

Baada ya busu, uso wake mzuri na wa kuvutia ulianza kuona haya kwa sababu aligundua kuwa watu wengi walikuwa wakimtazama. Macho ya Alvin yalimtoka kwa huzuni licha ya kuwa na furaha kubwa moyoni. Hakika, mwanamke wake alikuwa akivutia zaidi na zaidi. Alihisi hamu ya kuendelea kumbusu hadharani.

Ethan alitazama pembeni huku akionyesha huzuni. Ilionekana kana kwamba moyo wake ulikuwa umepasuliwa kwa uchungu. Hapo awali Lisa alipomwambia kuwa amemwangukia Alvin, hakuamini kabisa. Lakini hatimaye aliamini sasa. Hakika, mwanamke aliyekuwa akimchukulia kama mpenzi wake wa pekee sasa alikuwa amempenda mtu mwingine. Mtu huyo alikuwa bora zaidi na mzuri kuliko yeye. Akiwa amejawa na majuto, Ethan hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo hata kwa muda. Aligeuka na kuwa karibu kuondoka.

Lakini kabla hajaondoka, skrini kubwa ya video iliyokuwa jukwaani iliangaza ghafla. Kila mtu alifikiri kwamba ilikuwa ni shughuli ambayo mratibu wa mnada alikuwa ametayarisha. Hata hivyo, wote walishangazwa na tukio hilo la ajabu kabisa. Sauti tofauti kabisa zilisikika upesi kutoka kwenye spika.

“Huogopi kwamba Stephen atajua kuhusu hili? Eeh?.”

"Tayari anajua, na hatajali. Yeye ndiye aliyenitaka nilale na wewe leo.”

“Haah! Unasema kweli?. Kama ni kweli basi nashukuru kwa heshima yake ya kunipatia mwanamke wake."

Mazungumzo ya kushtua yalisikika katika ukumbi huo. Uso wa mwanamume ulikuwa umefichika, ilhali uso wa mwanamke ulionekana wazi kwa umma. Kwa kushangaza, alikuwa Lina, msichana kutoka kwa familia ya Jones Masawe, tajiri ambaye amekuwa akinyemelea kiti cha Lisa kwa gharama yoyote.

Stephen hata alikuwa ameambatana naye na kujionyesha hadharani wakati wa kuhudhuria hafla fulani na shughuli za kijamii siku za karibuni. Kwa hivyo, kila mtu tayari alijua kuwa Lina alikuwa mpenzi wa Stephen. Kilichoshtua kila mtu zaidi ni kwamba Stephen hakusalitiwa kuhusu jambo hili. Kweli alipanga mpenzi wake alale na mwanaume mwingine.

Ilitisha sana! Mnada wa usiku huo ulihudhuriwa na wanawake wengi matajiri. Walimtazama Stephen kwa dharau na karaha. Hali hiyo ilimfanya Stephen aingiwe na hofu ya upofu. Kamwe katika ndoto zake mbaya zaidi hakufikiria kwamba kuna mtu angethubutu kucheza video ya Willie na Lina wakiwa wamelala pamoja. Nani alifanya hivyo?! "Zima skrini! Zima sasa!” Alinguruma kwa hasira.

Lakini, hakuna mtu aliyemsikiliza. Kila mtu alikuwa akipiga porojo tu huku wakitazama tamthilia hiyo ikiendelea.

“Mtu wa aina hii anatisha kweli. Kwa kweli alimtuma mpenzi wake kwa mwanamume mwingine kwa ajili ya kutimiza lengo lake.”

"Kwa bahati nzuri, sikukubali wakati familia ya Kileo ilipotaka kuwa na uchumba na binti yangu."

“Ndiyo. Haendani kabisa na mambo anayoyafanya. Ni bora nikae mbali na familia ya Kileo siku zijazo.”

"Huenda pia anamtumaga Janet kulala na wanaume, si ndiyo tabia yake?"

“Hilo linawezekana. Hapo awali nilikuwa na hisia kwa Janet, lakini nitasahau tu juu yake. Sitaki kusalitiwa bure.”

Mbele ya shutuma za umma, Janet alikasirika sana hivi kwamba alipiga kelele, “Nani alifanya hivi? Haina uhusiano wowote na mimi!” Janet na Stephen, ambao mwanzoni walijisikia fahari, walikuwa na aibu sana wakati huo.

Ethan alipokuwa anajiandaa kuondoka, uso wake mzuri ulibadilika rangi. Alifikiri kwamba tayari alikuwa anajua rangi halisi za Lina. Hakujua kuwa alikuwa anachukiza zaidi kuliko vile alivyofikiria kuwa. Hakujua hata Lina kweli alikuwa na wanaume wangapi. Mara tu alipokumbuka kuwa alikuwa kwenye uhusiano naye hapo awali, alihisi hamu ya kutapika. Ethan alikuwa amezungukwa na wageni waliokuwa pembeni yake waliokuwa wakitazama tamthilia hiyo. Wakaanza kumsema waziwazi.

"Nilisikia kwamba Ethan alimtosa Lisa kwa ajili ya Lina wakati huo."

"Pengine alivutwa na matumizi ya Lina ya mbinu za hila. Sikutarajia Bwana Lowe kupendezwa na aina hii ya mwanamke.”

“Hasa. Lina ni mshenzi sana. Ninashangaa kama Bwana Lowe pia alikuwa akifanya uchafu wa aina hii na Lina wakati huo."

Akiwa mpenzi wake, Tracy hakuweza kustahimili maoni hayo, kwa hiyo aligeuka na kuondoka. Hakuweza kueleza maumivu yake kwa kutumia maneno, Ethan alimfuata haraka. Kabla hajaondoka, alimuona Lisa akimtazama kwa huruma na kejeli. Kwa wakati huo, alionekana kuelewa kila kitu. Pengine hii ndiyo ilikuwa adhabu na masaibu ya mwisho ambayo alimletea. Alikuwa amefaulu. Kuanzia wakati huu na kuendelea, angehisi kutapika kila alipomfikiria Lina.
Ni njia nzuri kabisa aliyotumia kuua ndege watatu kwa jiwe moja.
Lisa aliridhika kabisa na matokeo.

Tabia ya Lina isiyo na aibu iliwekwa wazi kwa watu wote wenye nguvu huko Masaki. Ilikuwa nzuri kwake kwa vile alifurahia ujasiri wa kutongoza wanaume. Hakuna mwanamume mmoja ambaye angekuwa na ujasiri wa kutosha kumuoa katika siku zijazo.

“Umemaliza kuitazama?” Akiwa amekunja sura yake sawasawa, Alvin alizungumza kwenye sikio la Lisa. Alifunika macho yake na kusema kwa sauti ya hasira nzito, "Hivi ndivyo ulivyomaanisha ulivyosema kuwa yajayo yanafurahisha? Nilikuonya jana usiku usiangalie miili ya wanaume wengine isipokuwa wangu tu.”

Hali ya huzuni ilimfunika Lisa na kumfanya ashtuke. Kisha akapigwa na wazo. “Sikuikagua. Shani ndiye aliyefanya hivyo."

“Unadhani nitakubali uongo wako? Unapima IQ yangu?" Alvin alicheka. Lisa alishindwa cha kusema. "Nitashughulika na wewe tukirudi nyumbani," Alvin alimuonya vikali.

Muda mfupi baadaye, mratibu wa mnada alizima skrini mara tu alipopata fahamu zake. Hata hivyo, karibu video nzima ilikuwa imechezwa. Ilikuwa imeharibu sifa za Lina na Stephen kabisa. Lisa akiwa ameridhika, akatembea hadi kwenye maegesho ya magari akiwa na Alvin.

“Simama hapo!” Sauti ya ukali ikasikika nyuma yao

Sura ya 130

Stephen na Janet Kileo waliwakimbilia wakiwa wamefura. Uso wa Stephen ulijawa na hasira kali. Hakutaka kitu zaidi ya kumnyonga Lisa akiwa hai. Alvin alimvuta Lisa nyuma yake, umbo lake refu na kubwa likitoa ulinzi wa nguvu kwa Lisa.

"Lisa Jones, wewe ndiye ulicheza ile video?" Stephen alifoka kwa hasira. “Sawa, umenikera mno. Ikiwa sitakuua, basi jina langu si Stephen Kileo.”

Janet naye alisema kwa msisimko, “Unajua umemkosea nani? Huyo ndiye Willie Kimaro! Hata kama umemficha uso, hatakuacha kwa kuwa umesambaza video zake kama hizi.”

Lisa aliinua macho yake na kutabasamu kwa dharau. “Umewahi kujiuliza hii video imetoka wapi na ni nani aliyenipa? Au ulifikiri ningethubutu kurekodi kitu kwenye chumba cha Willie Kimaro?”

Stephen na Janet wote walikua hoi kwa wakati mmoja. Muda mfupi baadaye, Stephen akatikisa kichwa. "Hiyo haiwezekani. Video hii huwezi kuwa ulipewa na Wiliie Kimaro. Ulimkosea jana usiku, kwa hiyo tayari anakuchukia. Umepata mtu wa kudukua simu ya Bwana Kimaro? Sawa, wewe ndiye uliyeanzisha hii. Nitampigia msaidizi wa Willie sasa hivi. Msaidizi wake ni rafiki yangu wa karibu sana.”

"Endelea kuota. Huenda hujui kuwa Willie Kimaro aliondoka Dar asubuhi ya leo.” Lisa alitabasamu kwa uso uliolegea. “Hivi mpenzi wako mzuri hakukuambia? Asubuhi ya leo, Willie alikuja Mawenzi Investments na kusema kwamba hatafuatilia suala la jana usiku tena. Willie pia alimdhalilisha sana Jones na binti yake. Sasa, kila mtu katika kampuni anajua Lina Jones alipanda kitanda cha mwanamume mwingine kutafuta kufadhiliwa. Wale wawili baba na binti yake hawana hadhi tena ya kuja kwenye kampuni."

“Usijaribu kunidanganya. Hakuna kitu kama hicho." Stephen hakumwamini hata kidogo. Alipiga moja kwa moja nambari ya msaidizi wa Willie Kimaro. Baada ya muda mrefu, simu iliunganishwa na sauti iliyolaaniwa kutoka upande wa pili, “Stephen Kileo, unawezaje kuthubutu kuwasiliana nami?! Umeniharibia! Hata nilipoteza kazi yangu.”

"Nini kimetokea?" Stephen aliuliza kwa sauti ya kuchanganyikiwa.

"Sijui. Vyovyote iwavyo, Lina Jones na wewe, nyinyi wawili ni mashetwain kabisa, mmemkasirisha sana Bwana Kimaro. Tayari amerejea Nairobi bila kupenda.” Simu ilikatwa kwa haraka.

Stephen aliganda kama sanamu ya mbao. Alimtazama Lisa ambaye alikuwa akitabasamu na ghafla akahisi damu yake ikishindwa kutembea kwenye mishipa. "Ulifanya nini kwa Bwana Kimaro?"

“Sina haja ya kujieleza kwa mtu kama wewe. Stephen Kileo, sikutaka kushughulika nawe, lakini ni kosa lako kumtambulisha Lina kwa Willie. Sasa, sifa yako imeharibika, na nadhani sio watu wengi watathubutu kuwasiliana na familia ya Kileo kwa ushirikiano katika siku zijazo. Unaweza kuendelea na ndoto ikiwa bado unataka kuoa mke kutoka katika familia yenye hadhi sawa na yako.” Lisa akamaliza hotuba yake na kuondoka zake kwa furaha huku akimshika mkono Alvin aliyekuwa kakasirika sana hadi kushindwa kuongea.

Janet aliyebaki nyuma alishika kichwa na kupiga kelele. "Stephen, haya mambo yametokeaje?" 'Yote ni kwa sababu ya ujinga wa Lina. Yule mjinga hata hajitambui kabisa.”

Stephen aliitoa hasira yake. "Sitamsamehe Lina kamwe. Naelekea nyumbani.”

Gari lilikuwa kimya, hewa ya wasiwasi ilitanda kila kona. Alvin akaminya midomo yake myembamba, umbo lake maridadi lkionekana kutulia kama sanamu. Lisa alimtazama kwa siri huku akijaribu kumwongelesha bila mafanikio.

“Bado una hasira? Kwa kweli nililazimika kukabiliana na Lina wakati huu. Nilitamani kutapika kila nilipoutazama mwili wa Willie Kimaro. Sasa, ninachotaka ni kwenda nyumbani na kuutazama mwili wako mzuri ili niweze kuosha macho yangu…”

“Sasa ndiyo unataka kunitazama?” Alvin ghafla alimkazia macho. Lisa akaguna na kukubali kwa kichwa.

"Sawa, nitakuruhusu uangalie usiku kucha." Alvin alikubali ghafla.
Lisa alipigwa na butwaa na kukosa la kusema. Alvin alikunja uso na kumuonya tena. "Ikiwa hii itatokea tena ..."

“Haitatokea tena,” Lisa aliapa, "Ikiwa itatokea, Mungu na aniadhibu nisiuone tena mwili mkamilifu wa Alvilisa maishani mwangu."

"Nyamaza." Alvin alicheka. “Hiyo video bado ipo kwenye simu yako? Nitafuta kila kitu kwenye simu yako tukifika nyumbani. Willie Kimaro ni mchafu sana kijana yule, sijui tabia hiyo kaitoa wapi!"

"Nakubali. Ingawa nimeona kidogo tu, sijisikii vizuri hata kidogo.” Lisa alijifanya kuchukizwa. "Alvilisa, najua huna tabia mbovu kama hii, si ndiyo?"

“Utaijua tu tabia yangu, ikiwa ni nzuri ama mabaya.” Alvin alijibu akicheka.

Baada ya kurudi nyumbani, Lisa alivua Mkufu wa Malkia wa almasi kwa uangalifu baada ya kukaa chini ya taa ya mezani na kuuangalia kwa upendo. “Ni mzuri sana. Hakuna dosari hata kidogo.”

"Nakumbuka ulisema haupendi vito vya mapambo." Alvin alitembea nyuma yake na kumtania, "Hata ulisema ni mtumba tu."
Lisa aliona haya na kusema kwa kigugumizi, “Mimi… nadhani ni ghali sana. Ni shilingi bilioni tatu. Itachukua muda gani kupata kiasi hicho cha pesa?"

"Ethan Lowe alikuwa tayari kutoa bilioni mbili kwa ajili ya mwanamke wake, kwa nini nijali kuhusu kiasi hiki?" Alvin alicheka kwa unyenyekevu. "Kwangu mimi, pesa haijalishi. Muhimu ni kwamba unaupenda."

Lisa akapepesa macho, mara akaelewa kuwa alikuwa akijaribu kushindana na Ethan. Hata hivyo, hiyo haikujalisha. Kadiri alivyokuwa akipambana na Ethan ndivyo ilivyokuwa ikionyesha kuwa anamjali.

“Alvilisa, Ethan kwa kweli hana uhusiano wowote nami. Mimi pia simpendi tena. Ninayempenda ni wewe." Aligeuka na kumkumbatia shingo na kumbusu usoni.

Moyo wake uliuma. Hapo awali, ingawa alipata pesa nyingi, hata hivyo ilionekana kama hazina faida yoyote. Sasa, ilionekana kana kwamba alikuwa amepata maana ya kupata pesa. Midomo yake myembamba ilijikunja huku akimpa sura isiyoeleweka. "Ni hayo tu?"
Lisa alionekana kujua alichokuwa akiongea na kuinamisha kichwa chini.

Alvin alicheka na kumnyanyua. "Si ulisema unataka kunitazama?"

“Hapana…” Uso wa Lisa ukageuka kwa woga. Alikuwa ni hodari wa kusema maneno makubwa, lakini ndani alikuwa ni mwoga kuyatekeleza.

"Kwa hiyo ulikuwa unanidanganya si ndiyo?" Alvin akakisugua kidevu chake taratibu. Sauti yake ilisikika kana kwamba ni sauti ya simba.

Mapigo ya moyo ya Lisa yalimuenda kasi, akazidi kuogopa. Alimsukuma kwa haraka. “Si ulisema hukula chakula cha kutosha wakati wa chakula cha jioni? Nitakwenda kukupikia.” Harakaharaka akamtoroka na kutoa tabasamu la hovyo chini ya macho ya Alvin.

Alvin alipotoka kuoga, Lisa alikuwa amepika chakula chenye harufu nzuri na kumtengea. Hakuwa amekula chakula cha jioni kilichopikwa na Lisa kwa muda mrefu na mara moja akakichukua ili kukionja. Kilikuwa ni chakula cha kawaida tu, lakini hakujua jinsi Lisa alivyokipika maana ladha ilikuwa ya kipekee sana kila wakati. Lisa alimsaidia kukausha nywele zake zilizolowa maji huku akimwangalia akila chakula kile kitamu.

“Upishi wangu bila shaka ni mtamu sana, lakini ulisema hukuupenda nilipokutengenezea mara ya kwanza. Wewe ni mnafiki sana, lakini wewe pia unajua kunipenda sana.”

Alvin aliona aibu. Ilikuwa ni kidogo sana kwa mwanamume kuelezewa kama mnafiki. Alimvuta kwenye mapaja yake na kuonyesha kutofurahishwa. “Unamwita nani mnafiki mkubwa? Hebu thubutu kusema tena?”

“Nakuzungumzia wewe. Bado unakataa kukiri… Mmh…”

Kabla Lisa hajamalizia, busu la kutawala la Alvin likaanguka kwenye midomo yake. Alimbusu bila kupumua, na hatimaye alipomwacha, alimwambia akiwa amemshika mabegani "Ukithubutu kusema tena nakuongeza zaidi ya hili..."

“Wewe ni mnafiki, kwani uongo…” Lisa alirudia tena huku akicheka. Inaonekana alikuwa amefanya kamchezo fulani ka makusudi.

Alvin akamkamata tena na kumpa busu. Wakati huu, alipigwa busu kali zaidi. Mikono yake mikubwa ilimkumbatia kwa nguvu kumzuia asikwepe. Lisa alikuwa na hasira na furaha kwa wakati mmoja. Alvin alikuwa jabari kupita kiasi na hakuruhusu mtu yeyote kuzungumza kwa utani juu yake.

Punde, Lisa alianza kulegea na kuzidiwa na hisia, Alvin alimbeba hadi kitandani. Alvin alikuwa amevaa bukta nyepesi tu alipotoka kuoga. Aliivua na kumtazama Lisa na kusema kwa sauti ya unyonge, “si ulisema unataka kunikodolea macho ili kuosha macho yako? Unaweza kuanza sasa.”

Uso wa Lisa uliwaka moto. Hakuwahi kufikiria kwamba Alvin angekumbuka jambo lile tena.

Umbo lake lilikuwa zuri sana. Hakuwa na misuli kupita kiasi bali mtanashati na mwenye nguvu. Zaidi ya hayo, alikuwa ametoka tu kuoga, hivyo harufu yake ya kiume na harufu ya gel ya kuogea ilimfanya apate hisia nzuri za utamu.

TUKUTANE KURASA 131-135

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
SIMULIZI..........LISA
KURASA.....131-135

Sur ya 131

Nywele za Alvin zilikuwa zimekaushwa tu na kuachwa zikiwa zimevurugika kwa fujo. Kwenye uso wake mzuri, kulikuwa na hisia zisizo na kikomo za kimapenzi zikitoka kwenye mwili wake wote.

Lisa alimtazama kwa shauku. Wakati huo, alitaka sana kumshukuru Pamela. Ni kosa alilofanya Pamela la kumchanganya Alvin na Kelvin, mjomba wake Ethan, ndilo lililompeleka Lisa kwake. Alikuwa amemsaidia mara kwa mara. Ni yeye pia aliyemfanya awe na ujasiri wa kuishi licha masaibu yote aliyokutana nayo.

Usiku huo, alimpatia Mkufu wa Malkia, kwa gharama ambayo ilimfanya kuwa mwanamke tajiri na aliyevutia kuliko wote Masaki nzima.

“Alvilisa…” Lisa alinyanyuka na kushika shingo yake. Uso wake wa ajabu uliangaza kwa aibu. "Tunaweza ... tujaribu?"

Alikuwa ameamua. Bila kujali kama familia ya Kimaro ingemkubali au la katika siku zijazo, alitaka kumpa Alvin kitu cha thamani zaidi alichostahili.

Alvin aliganda! Yeye alikuwa sugu kwa mambo hayo siku nyingi, na alikuwa hajaenda mbali zaidi pia. Mbona Lisa alikuwa ameamua ghafla…?! Au ni kwa sababu alijua utambulisho wake halisi?

“Kwa nini?” Macho yake mazito yalimtazama kana kwamba alitaka kuona kupitia kwake.

Lisa alikuwa amefunikwa na aibu na hakuona sura yake ya kushangaza. Alikuwa ameuzika uso wake mdogo katika kifua chake. “Kwa sababu nakupenda. Sijawahi kuwa na uhakika wa hisia zangu kama nilivyo sasa.” Lisa alijibu kwa aibu.

Alvin alisugua nywele zake laini na ndefu juu ya kichwa chake kwa udadisi. Hakuridhika na jibu lile. Kulikuwa na wanawake wengi sana waliomzunguka ambao walitaka sana kumrukia kwa sababu tu walijua utambulisho wake halisi, kwamba yeye ni mwanamume tajiri.

“Kwa nini? Je!… hutaki?” Lisa aliona haongei wala hafanyi chochote na akaona aibu. “Usinielewe vibaya, ni moyo tu ndiyo umenituma, sina nia ya kukujaribu na wala sikulazimishi. Kama hutaki basi tuache…” Alimsukuma na kukaribia kuinuka, lakini mwili wa Alvin haukumruhusu kunyanyuka.

"Ikiwa utanishinikiza kwa njia hiyo, basi nitakubali kwa kusita," Alvin alisema kwa sauti.

Lisa alimtazama kwa hasira. “Si lazima ufanye kwa kusitasita. Sikulazimishi na sijali hata hivyo…” Kabla hajamaliza, Alvin akambusu. Wakati huo, alielewa. Haijalishi alikuwa akifikiria nini, ni kweli alimtaka! Zaidi ya hayo, alikuwa amekiri kwake muda mrefu uliopita. Hakukuwa na haja ya kutilia shaka kwamba alimpenda.

Dakika chache baadaye, aliufunga mlango kwa nguvu na kwenda bafuni kuoga tena. Lisa alifoka kwa hasira ya kuachwa akiwa ‘ameiva’.

Dakika 20 baadaye, Alvin alitoka kuoga akiwa na sura tofauti. Hakumgusa tena Lisa wala kuwambia kitu chochote. Moyo wa Lisa uliumia alipofikiria juu yake.

‘Sitathubutu kumwambia katika siku zijazo.’ Alijiapiza kimoyomoyo kwa unyonge. Alikumbatia shingo yake na kuuzika uso wake kifuani mwake. Alikuwa na haya sana hivi kwamba hakuweza kuongea tenakwa muda mrefu.

"Potezea tu kwa leo. Utakuwa mwanamke wangu mapema au baadaye." Sauti ya Alvin alipomkumbatia ilikuwa ya kutetemesha sana.

Wawili hao walipolala, hawakujua kwamba habari kuhusu tukio la hisani usiku huo zilikuwa zimeenea mitandaoni. Kila mtu alijua kuhusu hilo. Wakati huo, katika makazi ya Jones Masawe, Jones kwa mara nyingine tena alipokea simu kutoka kwa wadaku.

“Bwana Jones, umeona sura duni ya binti yako? Hehe, nipe basi binti yako alale nami kwa usiku mmoja na nitafanya kazi nawe kwenye mradi."

"Nyamaza!" Mwili wa Jones ulitetemeka kwa hasira huku akilaani, “Weka kinywa chako ksafi unapoongea na mimi!”

“Hehe, ningewezaje kuwa msafi kuliko binti yako? Nani angethubutu kutaka takataka kama hiyo?"

"F*ck off! Usinipigie tena.” Jones aliivunja simu yake.

Alikuwa ameishi kwa miaka mingi na tayari alitumia nusu ya maisha yake, lakini hakuwahi kufedheheshwa kama ilivyokuwa siku hiyo. Hapo awali, alifikiria kwamba angeipata Mawenzi Investments kwa urahisi, lakini ilienda mbali zaidi na mikono yake. Si hivyo tu, hata alipoteza sifa na heshima yake ya mwisho. Alikasirika sana hivi kwamba alipoteza busara yake. Alichukua ufagio na kwenda juu ili kumpiga Lina.

“Wewe b*tch, yote ni makosa yako! Tangu uliporudi, tulipoteza Kibo Group na sifa yetu. Hata mimi pia nimefedheheshwa katika umri huu. Mjinga sana wewe!”

"Hapana!" Lina alipiga kelele mara kwa mara na kuendelea kujificha. "Baba, nilifanya hivyo kwa ajili ya familia ya Jones. Ni wewe ulinishauri nimfurahishe Bwana Kimaro.”

"Nilitaka umfurahishe kwa zawadi, sio kulala naye, paka wewe!" Jones alipiga kelele. Kadiri alivyokuwa akisema ndivyo hasira zilivyozidi kuongezeka na ndivyo mikono yake ilivyozidi kuwa matata.

“Una kichaa? Ni binti yetu!” Mama Masawe aliingia ndani na kumsukuma. Alipoona sura ya Lina iliyochubuka na kupigwa, alilia kwa huzuni.

“Afadhali nisiwe na binti kama yeye!” Jones alimnyooshea kidole na kumkaripia, “Ningejua kwamba haya yangetokea knisingekurudisha kabisa. Ikiwa sio wewe kurudi, ningekuwa na ugomvi na Lisa? Ikiwa hukunitia moyo, ningemuua mama yangu kwa mikono yangu mwenyewe? Isingekuwa wewe hata Lisa angeingia Mawenzi Investments angenisikiliza na kuniacha niwe mwenyekiti.”

Lina aligeuka rangi, na mwili wake ukatetemeka huku akijilaumu mwenyewe.

Mama Masawe hakuweza kumsikiliza tena. Alimkumbatia Lina kwa nguvu na kupiga kelele, “Inatosha! Ni wazi Lisa ndiye aliyetulazimisha kufikia hatua hii, lakini bado unamlaumu na kumpiga Lina. Unataka tu kumalizia hasira yako kwa kumuonea mtu mwingine."

“Bado una ujasiri wa kusema hivyo? Binti mzuri uliyemlea mwenyewe hana haya wala aibu. Ninachojutia zaidi ni kwamba nilikuoa na kumzaa!”

"Sawa, kwa kuwa unajuta, tutaondoka!" Mama Masawe alilia na kuushika mkono wa Lina kabla ya kutoka nje. Muda si muda, nyumba nzima ikawa tupu na ya kutisha.

Sura ya 132

Jones alitetemeka upepo wa baridi ulipovuma. Kwa mara ya kwanza, hisia ya majuto ilipanda moyoni mwake. Ilikuwa wazi kuwa alikuwa na familia nzuri. Ilivunjikaje kwa muda wa miezi mitatu tu?

Siku iliyofuata, Jones alipokea simu kwamba alikuwa amefukuzwa kutoka kwenye bodi ya wakurugenzi wa Mawenzi Investments. Alikimbilia kwenye kampuni hiyo kwa hasira, lakini mlinzi wa mlangoni hakumruhusu kabisa kuingia na kumfukuzia nje. Kwa kuwa hakuwa na mahali pengine pa kwenda, Jones aliishia kulewa kwenye baa na alirudi tu nyumbani usiku wa manane.

Usiku huo, kwa ulevi alisukuma mlango wa nyumba yake kwa unyonge na hakukuwa na taa ndani, na mwanga wa mbalamwezi wa baridi ulipenya kupitia madirishani. Kulikuwa na kiti cha magurudumu katikati ya sebule, na juu yake aliketi mwanamke mzee mwenye mgongo ulioinama na nywele zilizotawanyika. Sura hiyo ilionekana ya kutisha haswa. Jones aliogopa sana hivi kwamba miguu yake ilidhoofika. Aligeuka na kujaribu kukimbia. Hata hivyo, mlango ulifungwa nyuma yake, na sebule ikawa giza.

“Mama…” Jones alipiga magoti chini kwa woga, akitetemeka kama jani lililosukumwa na upepo.

“Mwanangu, mbona unaniogopa sana?” Kiti cha magurudumu kiliteleza mbele polepole, na sauti ya mwanamke mzee ikasikika.

Jones alirudi nyuma kwa hofu. “Mama, mama, usije. Tafadhali, si mimi niliyekudhuru. Kuna mtu mbaya."

“Si wewe uliyenidhuru?” Kicheko cha kutisha cha yule kikongwe kilisikika pale sebuleni. "Ulifanya hivyo kwa ajili ya hisa na pesa. Lakini kwa nini umenidhuru? Si nilikutunza tangu ujana? Ulimwengu wa kuzimu hautaki kunikubali kwa sababu mliniondoa kabla ya siku zangu, kwa hivyo imenibidi tu kurudi kukutafuta. Mwana…”

Kiti cha magurudumu kilikuwa kikikaribia zaidi na zaidi. Jones alipiga magoti chini na kuinama kwa nguvu, machozi na vilio vikimtoka. “Mama, nilikosea. Nilikosea. Nilianza kuhangaika, lakini sikutaka kukuumiza. Ilikuwa Mama Masawe. Mama Masawe ndiye alikusogezea mto. Nenda kwake badala yake.

“Kama hukukubali, angeniua?” Mwanamke mzee alicheka na kulia wakati huo huo.

“Mama, samahani.” Jones alibubujikwa na machozi, akijihisi mnyonge. “Nilitiwa moyo na wawili hao, mama na bintiye. Sikutaka kukukuua, samahani. Tafadhali niache uende…”

"Kwa kuwa unajua kuwa ulikosea, nitakuondoa sasa." Mkono wa mwanamke mzee ulimshika, lakini Jones aliogopa sana kusogea. Doa lenye unyevunyevu lilimtoka kwenye ‘gongo’ lake huku akijikojolea. Taa ziliwaka ghafla!

Maafisa kadhaa wa polisi walitoka jikoni, na mwanamke mzee kwenye kiti cha magurudumu akavua wigi lake kabla ya kusimama.
Jones alipigwa na butwaa na kutetemeka. “Shangazi Manka…”

"Bwana. Jones, kuna mtu aliripoti kwamba unashukiwa kumuua Madam Bibi Masawe. Na wewe mwenyewe umekiri hapa. Polisi sasa wanakukamata rasmi.” Afisa huyo akatoa pingu na kumfunga mikono.

“Hapana, hapana…” Jones alijitahidi sana kujificha. “Nilikunywa pombe kupita kiasi. Nilikuwa naongea ujinga tu.”

"Mjomba, nimerekodi kila neno ulilosema." Lisa alitoka na simu. Uso wake ulikuwa umejaa huzuni. “Ulikuwa mwana pekee wa kiume wa bibi. Alikuwa mzuri kwako na alikulea kwa uchungu, lakini mwishowe, ulipanga njama na wengine kumuua. Bado unakumbuka jinsi alivyokufa? Je, huoti ndoto mbaya? Je! dhamiri yako haikuumi?”

“Usiseme tena…” Jones alikuwa tayari amekunywa pombe nyingi. Sambamba na jinsi alivyokuwa amepatwa na woga, akili yake ilikuwa karibu kuzimia.

Lisa alisema kwa ujeuri, “Tayari nimekusanya ushahidi mwingi. Ikiwa hutaki kufa gerezani, bora utoe ukweli wako kwa uaminifu.
Vinginevyo, Mama Masawe bila shaka atajaribu kukwepa mashtaka mahakamani baadaye.”

Jones hakumwamini. “Umekusanya ushahidi gani?”

"Bibi alitibiwa hospitalini, na hospitali ina rekodi zake za matibabu. Daktari alisema kwamba ingawa bibi alikuwa amepooza wakati huo, haikuwezekana afe ghafla hivyo. Pia kuna Aunty Helen ambaye ulimwajiri badala ya Aunty Manka kumtunza Bibi. Yuko tayari kufika mahakamani sasa…”

Jones aligeuka rangi. Alijua kwamba alikuwa katika matatizo.

Kama asingetoa ushahidi muda huo, basi angeweza kuishia jela wakati Mama Masawe angesukuma shutuma hizo kwake. “Sawa, nitakiri. Ilikuwa Mama Masawe. Alichukua fursa wakati bibi yako alikuwa amelala na…” Labda ilikuwa dhamiri yake ya mwisho, lakini hatimaye Jones alianguka chini na kulia.

Lisa na Aunty Manka nao walilia. Hawakutarajia mwisho wa Madam Bibi Masawe kuwa mbaya kiasi hicho.

Aunty Manka aliuliza, “Swali la mwisho. Siku hiyo bibi madam Masawe alipoanguka kutoka kwenye ngazi, ni Lina ndiye aliyemsukuma?"

"Kwa kweli sijui kuhusu hilo." Jones Masawe alitikisa kichwa, lakini akifikiria juu ya utu wa Lina, alihisi kwamba labda alifanya hivyo. Hata hivyo, alikuwa na binti mmoja tu na hakutaka aende jela.

Mwishowe, Jones alichukuliwa na polisi kwa mahojiano. Lisa alitazama jumba la giza nyuma yake. Hapo awali palikuwa nyumbani kwake, lakini sasa palikuwa mahali ambapo hakutaka tena kukanyaga. Alichukua funguo na kuzitupa kwenye nyasi kabla ya kugeuka na kutoka nje ya mlango.

Gari lao la kifahari lilikuwa limeegeshwa mlangoni. Alvin alikuwa amesimama huku kaegemea gari. Kulikuwa na mvua kidogo usiku huo, na matone ya mvua yalitua kwenye kichwa na mabega yake. Lisa alimtazama kwa mahaba, macho yake mazito na safi yalipendeza kama mwanga wa nyota pekee angani.

Wakati huo, Lisa, ambaye hakuwa na nyumba, alionekana kuwa amepata nyumba. Aliruka mikononi mwake, na Alvin akafunua koti lake ili kumfunika ndani yake.

"Alvlisa, hatimaye nimelipiza kisasi." Lisa akasonga mikononi mwake. “Lakini sina furaha hata kidogo. Ninajuta kwamba sikukaa zaidi na Bibi hapo awali. La sivyo, asingekufa vibaya hivyo.”

Machozi ya Lisa yalilowanisha shati kifuani mwa Alvin. Alvin hakujua jinsi ya kuwafariji wengine. Alimsubiri amalize kulia na huku akimpigapiga tu kichwani. “Umefanya vizuri usiku wa leo. Hakukuwa na ushahidi wowote bado uliweza kumfanya Jones Masawe akiri yeye mwenyewe!"

“Nilicheza kamari, kupata ama kukosa. Nilicheza kamari juu ya ubinadamu wake. Nilicheza kamari kwenye kile kilichosalia kwenye hatia na dhamiri ya Jones. Nilicheza kamari kwamba angekuwa mbinafsi kiasi cha kumsingizia Mama Masawe.” Sauti ya Lisa iliendelea kusikika. "Nilikuwa tayari nadhani kwamba Jones asingefanya hivyo mwenyewe. Ili kupunguza adhabu yake, bila shaka angesema kwamba ni Lina au Mama Masawe waliofanya hivyo. Kwa kweli sikutarajia Mama Masawe angekuwa mkatili kiasi hicho.”

“Mama Masawe ana uhakika wa kwenda jela. Twende, usiku umeenda sana.” Alvin alifungua mlango wa gari.

Lisa ghafla akashika mkono wake. Macho yake makubwa meusi yalitazama ndani yake aliposema, “Alvlisa, nina wewe tu sasa. Utaniacha pia?”

“Sitafanya hivyo.” Alvin akainama na kumbusu kwenye paji la uso huku akiongea kwa upole.

Lisa alifumba macho. Kwa wakati huo, alifikiria kwamba asingemuacha kamwe maishani mwake. Ni baadaye tu ndipo alipogundua kwamba walikuwa bado wachanga sana kwenye mapenzi, na kulikuwa na mambo ambayo yangebadilika.
•••
Saa tisa usiku, Lina na Mama yake walikuwa wamelala fofofo kwenye chumba cha hoteli. Kengele ya mlango ililia ghafla.

"Ni nani huyo?" Mama Masawe alifungua mlango kwa hasira. Alifikiri kwamba ni Jones ndiye aliyewafuata kuwafanyia fujo.
Hata hivyo, mara mlango ulipofunguliwa, kundi la polisi liliingia na kumfunga pingu. “Mama Masawe, unashukiwa kumuua Mzee Madam Masawe. Upo chini ya ulinzi!”

"Nini?" Mama Masawe alipigwa na butwaa na kuruka kwa haraka. "Sikumuua mimi."

“Mumeo tayari ameshatoa maelezo kamili kituoni. Ni wewe uliyemkaba mama mkwe wako kwa mikono yako mwenyewe.” Macho ya polisi yalijaa dharau. Mwanamke huyo hata alimuua mama mkwe wake mwenyewe! Mtu wa aina hii hakuwa na maadili kabisa. Polisi hawakumpa nafasi ya kujitetea, wakamtoa nje.

“Mama, nini kinaendelea?” Lina alikurupuka kutoka kitandani na kukimbilia kumshika, lakini polisi hawakumruhusu kumgusa.

Sura ya 133

Mama Masawe akapaza sauti na kusema, “Baba yako ni mnyama! Kaenda kunichongea polisi kuwa nilimuua bibi yako. Lina, lazima ujilinde.”

Mama Masawe alichukuliwa upesi, na Lina akaanguka chini. Alikuwa ameteseka kijijini kwa zaidi ya miaka 20, na haikuwa rahisi kwake kuja mjini. Lakini, kabla hata mwaka haujaisha, familia yake ilisambaratika kabisa! Ikiwa kitu kingetokea kwa Jones Masawe na Mama Masawe, angekuwa na sifa gani za kuwa binti mkubwa wa familia ya Jones? Hapana, hapana. Hakutaka kurudi enzi hizo!

Alimpigia simu Stephen Kileo kwa haraka. “Stephen, nakuomba. Tafadhali nisaidie. Mama na baba yangu wamekamatwa na polisi. Maadamu utanisaidia, nakuahidi kuwa nitakuwa mkeo. Nitakupa nusu ya hisa za Mawenzi Investments.”

“Lina Jones, nimeelewa sasa. Bahati mbaya humwandama yule aliye pamoja nawe. Kwanza, ilikuwa Ethan Lowe, na sasa mama na baba yako wanaenda jela. Sifa yangu pia iliharibiwa kabisa na wewe. Potea na ukae mbali nami siku zijazo. Kukuona tu kunanifanya nitamani kutapika!” Stephen alikata simu moja kwa moja.

Lina alipigwa na butwaa kabisa. Hakuweza kuelewa. Haikuwa kitambo kirefu matajiri wote huko Masaki walikuwa wamemshikilia. Ilikuwa imechukua muda mfupi tu, na sasa, kila kitu kilikuwa kimebadilika. Kila kitu kilikuwa kosa la Lisa Jones! Aliamini ni Lisa aliyemharibia maisha na kumdumbukiza katika hali hiyo mbaya. Kwa nini Lisa alikuwa bado yupo hai?! Moyo wa Lina ulikuwa umejaa wazimu.

Wakati huo alikumbuka kitu kama mtu aliyeshukiwa na roho mtakatifu na kufunuliwa jambo. Alikumbuka alikuwa na picha za Lisa alizopigwa hotelini siku ambayo Lina alimtengenezea njama za kubakwa. Ni siku ile ambayo alilaghaiwa kwenda kuwasilisha michoro yake hotelini kwa ajili ya mradi wa Mawenzi aliokuwa akiupigania kuupata, ambapo kwa bahati nzuri aliokolewa na Kelvin. Alikumbuka picha hizo zilikuwa kwenye simu yake. Alipoziona, alishtuka kwanza kabla ya kusisimka mara moja.

Picha hizo zilikuwa za Lisa akiwa karibu sana na Kelvin Mushi utasema ni wapenzi. Alijua kutoka eneo ambalo picha zilipigwa kuwa ni wakati wa kumtia Lisa dawa ndani ya chumba cha hoteli.

Hapo awali, Lina alitaka wanaume fulani wambake Lisa, lakini Kelvin Mushi alikuwa amefika kwa wakati. Lakini Lina alifanikiwa kupata picha za video zilizomwonyesha Kelvin akiwa kamnyanyua Lisa mikononi mwake. Hakutarajia kamwe kwamba zingekuwa bado zimo kwenye simu yake.

“Haha, kwa picha hizi, Lisa atawezaje kukaa na Alvin?” Lina aliwaza kwa furaha. Sifa yake kama mwenyekiti wa Mawenzi Investments pia ingeathiriwa. Lina alitafuta haraka nambari ya mwandishi wa udaku!
•••
Saa tatu asubuhi Lisa alipoamka, alikuwa peke yake kitandani. Mvua ilikuwa imenyesha usiku kucha na alilala usingizi mnono sana. Sasa kwa kuwa alikwisha lipiza kisasi kwa kifo cha bibi yake na Bibi na Bwana Masawe wote walikuwa jela, alihisi utulivu na raha kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Pia ilikuwa ni nadra kwake kuamka akiwa amechelewa sana.

Alikaa na kuangalia muda lakini akagundua kuwa kuna missed call nyingi kwenye simu yake. Nyingine zilikuwa kutoka ofisini, nyingine kutoka kwa Kelvin, na hata kulikuwa na missed calls nyingi zaidi kutoka Pamela. Pamela alikuwa amempigia simu mara saba au nane.
Haraka alimpigia tena huku akicheka. “Mbona umenipigia simu mara nyingi sana asubuhi? Kuna kitu kilitokea?"
“Kuna kitu kilikutokea? Inamaana bado hujui?” Sauti ya wasiwasi ya Pamela ilisikika. "Nenda uangalie habari zinazovuma sasa."

Lisa alipigwa na butwaa alipoingia mtandaoni. Aliona video iliyokuwa inatrend ikiwa na jina lake na Kelvin na kubofya habari ile. Matokeo ya utafutaji yakasomeka, 'Mwenyekiti mrembo wa Mawenzi Investments afumwa kwenye pozi tata na mpenzi wake' ghafla yalitokea.

Lisa alihisi kuogopa. Alipobofya kwenye makala hiyo, alipigwa na butwaa kuona video ya Kelvin Mushi akiwa kambeba juujuu huku akiwa kamwinamia kama anambusu shingoni. Chumba kilikuwa na baridi, lakini ghafla alihisi joto sana!

“Unafanyiwa njama?” Pamela alisema kwa wasiwasi, "Kwa utu wako, haiwezekani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine zaidi ya Alvin. Ninakuamini, lakini wengine wanaweza wasikuamini.”

Pamela alikuwa hajamaliza kuongea wakati mlango wa chumba cha kulala ulifunguliwa kwa nguvu. Alvin aliingia kwa nguvu huku uso wake mzuri ukiwa umefunikwa na hasira kali. Machoni mwake kulikuwa na sura iliyoonyesha hakutaka kitu zaidi ya kumrarua vipande vipande. Lisa alikuwa hajamwona akiwa na hasira hivi kwa muda mrefu. Haraka akakata simu na kumueleza. “Umeona hizo picha? Usielewe vibaya—”

“Kwa hiyo unataka nikupongeze, sivyo?" Alvin aliikamata simu iliyokuwa mikononi mwake na kumrushia. Macho yake ya giza yalifunikwa na tamaa, karaha, na chuki. “Angalia wewe mwenyewe hizo picha za kuchukiza. Unadai kuwa humpendi Kelvin Mushi, lakini ulimkumbatia kwa nguvu na hata kumvua nguo. Lisa Jones, mbona huna haya?”

Simu yake iligonga kifua chake kwa nguvu. Ilimuuma, lakini sio kama moyo wake ulivyouma. Ni wanaume wangapi wangeweza kutulia ikiwa wangeona picha kama zile? Alikuwa kavurugwa kabisa na hizo picha zake.

“Hapana, nilifanyiwa njama, sema tu sikukuambia ukweli! Usiku huo, Lina Jones alinilazimisha kunywa dawa, na Kelvin Mushi alitokea kwa bahati nzuri akaniokoa. Hakuna kilichotokea kati yetu." Lisa alitikisa kichwa kwa masikitiko huku akieleza, “Nilijiloweka kwenye maji baridi usiku kucha.”

"Unanichukulia kama mjinga?" Kicheko cha kutisha cha kijeuri kilisikika kutoka kwenye koo la Alvin. “Uliponilisha kwa hila madawa kama hayo, hata mwanamume kama mimi nilishindwa kuvumilia. Ilinibidi niende hospitalini kuwekewa dripu ili nipate nafuu, lakini wewe unasema ulishinda kwa kujiloweka kwenye maji baridi tu?”

“Ninasema ukweli.” Lisa alilazimisha kujibu malalamiko yake na kujaribu kueleza, “Naweza kuapa—”

"Nyamaza! Lisa Jones, kwa kweli sitakuelewa!” Alvin ghafla akashika kidevu chake kwa nguvu. “Unajifanya kuwa msafi na mtulivu mbele yangu, ukisema kwamba unaogopa… Kumbe ni janja janja yako tu kuendelea kunifanya mjinga?! Ngoja nikuulize. Picha hizi zilipigwa lini? Nakumbuka… nilienda Nairobi kwa siku chache na Shangazi Linda akasema hukurudi usiku kucha…”

“Sikufanya hivyo! Hakuna kilichotokea kati yangu na Kelvin, simpendi…” Lisa akatikisa kichwa kwa nguvu.

"Kwa hivyo mawazo yangu yalikuwa sawa." Alvin hakumsikiliza hata kidogo. Macho yake yalijaa dhihaka na kejeli. “Nilikupigia simu usiku ule. Simu yako ilikuwa imezimwa usiku kucha. Hah, kumbe ulikuwa na Kelvin Mushi, sivyo?"

Kadri alivyozidi kuongea ndivyo hasira zilivyozidi kumpanda. Ilikuwa ni kama kuna jeraha kwenye moyo wake, na chumvi iliendelea kupakwa juu yake. Ilimuuma sana hata akashindwa kupumua.

Pamoja na mashaka na shutuma zake, moyo wa Lisa ukazidi kuwa mzito na mzito. Kulikuwa na uaminifu mdogo sana kati yao. Kwa kweli hakujua jinsi ya kumshawishi. “Kama… Kama huniamini, unaweza kuangalia mwenyewe,” Lisa alikunja ngumi na kusema bila kujielewa.

Alvin alicheka kana kwamba amesikia mzaha. Sauti yake ilijaa dharau alipozungumza, “Baada ya kutazama hizo picha, kukutazama tu kunanifanya nijisikie mchafu. Sitathubutu kushika mwili wako mchafu. Kumbe ndiyo maana jana machale yalishika nikaacha.”

Lisa alijeruhiwa sana moyoni mwake. Jana yake usiku, alijisikia kana kwamba alikuwa mwanamke mwenye furaha zaidi duniani, lakini mara tu kulipopambazuka, ilionekana kana kwamba dunia nzima ilikuwa imeporomoka. Picha hizo zilitoka wapi? Alikumbuka kwamba wakati wanaondoka, Kelvin alisema kwamba aliivunja kamera. Haraka akapiga namba ya Kelvin.

Simu ilipounganishwa, sauti ya Kelvin ya wasiwasi ilisikika. “Lisa, tayari nimeshaona kila kitu. Mimi sina neno ila nina wasiwasi na wewe. Alvin atakuelewa kweli? Naweza kumpigia simu ili nimweleweshe?”

Sura ya 134

Hapo awali, Lisa alihisi mashaka kidogo, lakini baada ya kusikia sauti ya Kelvin, alihisi kwamba alikuwa na mawazo potofu. Kelvin alikuwa muungwana sana. Asingeweza kamwe kueneza picha kama hizo.

“Amekasirika sasa. Ukimpigia simu utazidi kumkasirisha zaidi.” Lisa alitabasamu kwa uchungu. “Si ulisema siku ile uliharibu kamera? Kwa nini…”

"Niliiharibu. Hata niliiangalia wakati huo hakukuwana picha zozote." Sauti ya Kelvin ilionyesha jinsi alivyokuwa na huzuni. "Nadhani kamere zilikuwa zinahamisha picha wakati zikirekodi. Nilikuwa mzembe. Niligundua kuwa picha hizo mtandaoni zilisambazwa na ripota baada ya kupewa na Lina.”

Lisa alitabasamu kwa hasira. Alikuwa amemdharau Lina. Picha hizi zilikuwa za uchochezi sana.

“Samahani.” Kelvin aliomba msamaha tena. “Sijali kwa vile mimi ni mwanaume, lakini itaathiri sana sifa yako. Ikiwa kuna chochote ninachoweza kukufanyia, nijulishe tu na nitajaribu niwezavyo kukusaidia.”

"Asante. Nina simu kutoka ofisini ninayohitaji kuipokea. Tuongee baadaye.” Lisa haraka akakata simu kwa Kelvin na kupokea simu kutoka kwa msaidizi wake, Tunu.

“Mwenyekiti Jones, njoo ofisini haraka. Uvumi kuhusu kashfa yako unavuma na laini ya simu ya kampuni inashikiliwa na waandishi wa habari. Inabidi ushughulikie jambo hili haraka iwezekanavyo.”
“Sawa, nitakuja mara moja.” Lisa hakujali tena na kubadilisha nguo zake haraka kabla ya kushuka.

Alipotoka nje, aligundua kwamba Shani hakuwepo na hakumfuata tena ili kumlinda. Moyo wake ukaingia giza. Alvin ndiye alikuwa amepanga Shani amlinde. Sasa kwa kuwa alitaka kumuacha, alimfukuza Shani pia.

Baada ya kufikia kwenye kampuni hiyo, waandishi wengi walikuwa wamesimama mlangoni. Aliingia kutoka kwenye viwanja vya maegesho. Alipopanda ghorofani, watendaji kadhaa walikuwa tayari wakimsubiri ofisini.

"Mwenyekiti Jones, kuna wanamtandao wengi kwenye mtandao wanaokukaripia kwa kuwa... 'wazi' sana…” Paji la uso la Freddie Ngololo lilijawa na jasho baridi. Tayari alikuwa ametumia neno lenye ukakasi sana. “Kwa kifupi, hali si nzuri sana na sifa yako kama mwenyekiti wa kampuni naogopa kusema kwamba inaathiri sana.

Uso wa Lisa ambao tayari ulikuwa umekunjamana ulizidi kuwa mbaya. Mara nyingi alisoma magazeti ya udaku mtandaoni na alijua vyema uovu wa watumiaji wa mtandao dhidi ya wanawake katika kashfa kama hizi.

"Je, idara ya PR ina mawazo yoyote?" Lisa aliuliza huku akikuna kichwa.

Meneja Mkuu Ngololo alisema, “Idara ilifanya mkutano mapema asubuhi. Tunafikiri njia bora ni kutangaza rasmi kuwa wewe na Kelvin Mushi ni wapenzi ili kushusha joto. Kwa kweli, hata wafuatiliaji wa habari hii wanasema Kelvin Mushi na wewe mnaendana sana na mnalingana vyema katika hali ya kijamii. Hakika utapokea mwitikio chanya kutoka kwa watu mitandaoni na kashfa hii itageuka kuwa baraka kwako.”

"Ndiyo…Ndiyo!" Meneja wa idara ya PR alitabasamu haraka na kusema, “Wakati huo, tunaweza pia kuipandisha hadhi Mawenzi Investments, Kwa taswira yako kama mwenyekiti wa bodi, na taswira ya Kelvin Mushi kama mwenyekiti wa Golden Corporation, mnaweza kuwa mabalozi wazuri wa kampuni.” Watendaji walikubaliana na wazo hili.

Kadiri Lisa alivyozidi kusikiliza ndivyo alivyozidi kukosa la kusema. "Hapana, tayari nina mpenzi."

Meneja Mkuu Ngololo alianguka kwa aibu. “Sawa… Lakini ulipigwa picha ukiwa na Bwana Mushi. Ukikataa, itakuwa mbaya kwa picha yako, na kila mtu atakudharau kwa kuwa na maisha ya faragha yasiyo na uaminifu. Ikiwa suala hili halitashughulikiwa vyema, sura ya Mawenzi Investments itaathirika pakubwa.”

"Niliwekewa madawa ya kulevya wakati huo. Unaweza kueleza moja kwa moja kwenye tovuti rasmi.” Lisa alisimama na kuwatazama watendaji hao kwa macho makavu. "Hii ni kampuni ya mali isiyohamishika. Maadamu mali zetu zimejengwa kwa ubora mzuri, bado tunaweza kupata nyota zilizo na picha nzuri za kututangaza. Ikiwa kweli tumeathiriwa, basi haiwezi kusaidia. Siwezi kumuumiza mpenzi wangu kwa sababu ya kampuni, kama vile baadhi yenu hamtawaacha wake zenu kwa ajili ya faida. Kila mtu ana msingi wake."

Umati ukanyamaza. Baada ya nusu dakika ya kimya, Meneja Mkuu Ngololo alitikisa kichwa. "Tutafanya kama Mwenyekiti Jones anavyosema."

Baadaye, ukurasa wa Facebook wa Mawezni ulichapisha taarifa kwa umma.
[Picha zilipigwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Mwenyekiti Jones alifanyiwa njama na kulishwa madawa ya kulevya. Kwa bahati nzuri, Kelvin Mushi alionekana kwa wakati na kumuokoa Mwenyekiti Jones, lakini hakuna kilichotokea kati ya pande hizo mbili. Wawili hao bado ni marafiki wa karibu sasa. Tunatumai kila mtu ataelewa na ataacha kujadili suala hilo.]

Kisha, Kelvin binafsi ali’share chapisho hilo.

[Wakati huo, Mwenyekiti Jones alikuwa ameleweshwa dawa za kulevya, lakini aliokolewa haraka na kulowekwa kwenye bafu baridi. Ni mwanamke mwenye heshima sana. Natumai kuwa watu hawatamwelewa vibaya na kumtusi kwa sababu ya picha chache.]

Baada ya chapisho kupakiwa, athari ilikuwa nzuri ya kushangaza.
Watu wengi walimsifu Kelvin kwa kuwa mungwana na msikivu, na Lisa kwa kuwa hodari na jasiri. Baadhi ya watu hata waliwashauri na kuwaambia wawe wapenzi badala ya marafiki. Walisema walikuwa ni kapo zinazofaa zaidi katika ulimwengu wa biashara.
•••
Katika kampuni ya sheria, Jennings Sollicitors, Ofisi ilionekana kuwa na giza la ukiwa. Alvin alikuwa amekaa siku nzima kwenye simu yake. Asubuhi, kila mtu alimkemea Lisa, lakini upepo ulibadilika ghafla mchana. Kila mtu alipiga kelele kwa Lisa kuungana na Kelvin.

Aliibomoa simu yake pale pale kwa hasira. "Hivi watu kwenye mtandao siku hizi hawana kitu cha maana cha kufanya? Eti hawa wawili wanaendana vizuri? Hivi ni vipofu?”

Hans aliyekuwa amesimama pembeni aliitazama ile simu iliyosambaratika akiwa hoi. Angelazimika kununua simu mpya tena. Hakujua hata idadi ya simu ambazo Alvin alikuwa amevunja tangu awe na Lisa.

“Bwana Kimaro, watu kwenye mtandao wote ni wavivu sana. Usiwajali.” Hans alimpoza kimawazo.

Alvin alikodoa macho. Hakutaka, lakini alikuwa amesoma yale ambayo watu walisema kuhusu Kelvin Mushi kuwa na mapenzi makubwa kwa Lisa, na Lisa kuwa na hisia nzuri kwa Kelvin. Kulikuwa na watu wanaotunga hadithi ya mapenzi ya kipuuzi kuhusu kupendana kwao kwa siri.

Tumbo la Alvin liliwaka kwa hasira. Akaketi na kufungua laptop yake, vidole vyake vikiruka kwenye keyboard. Dakika chache baadaye, Hans aligundua kuwa habari ya Kelvin na Lisa ilikuwa imetoka kwenye habari zanazovuma mtandaoni! Ilishangaza! Bwana Kimaro kweli alikuwa amedukua akaunti ya facebook ya Mawenzi moja kwa moja.

“Alvin...” Mlango wa ofisi ulifunguliwa ghafla na Sam Harrison akaingia. Alipomwona Alvin ambaye alionekana kama mfalme wa pepo, alitetemeka. “Nilifanya uchunguzi. Usiku huo, Lina Jones aliingia na watu wachache na alionekana kwenye jumba hilo la hoteli. Wakati huo, pia alimwagiza meneja wa hoteli hiyo kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia katika chumba alichopanga.”

Alvin alikodoa macho. Ilionekana kana kwamba tukio hilo la Lisa lilikuwa ni njama. Hata hivyo, jinsi alivyokuwa amembusu Kelvin kimahaba bado ilimkasirisha.

"Umegundua ni wakati gani Lisa na Kelvin waliondoka?" Aliuliza kwa huzuni.

"Asubuhi," Sam alikohoa kwa upole na kusema kwa sauti ya chini, "Walitoka asubuhi baada ya kubadilisha nguo." Maneno hayo yaliposikika, Alvin aliivunja kompyuta moja kwa moja.

Mwanamume na mwanamke katika chumba pamoja, na mwanamke hata kulishwa madawa ya kulevya. Inawezekanaje kuamini kwamba hakuna kilichotokea kati yake na Kelvin?

Sam alimtazama kwa huruma. Kusema kweli, pia hakuamini kabisa kwamba Lisa hakuwa na hatia. “Sawa… Lisa pia ni mwathirika katika hili… Nilisikia kwamba Lina Jones aliingia na walinzi wawili wakati huo. Kama Kelvin Mushi asingetokea, matokeo yangekuwa mabaya zaidi.”

"Unamaanisha nini? Unasema ninapaswa kumshukuru Kelvin Mushi?” Macho jeuri ya Alvin yalimtoka. "Mwishowe, yeye ndiye mjinga. Anaendelea kuanguka kwa hila za familia ya Jones mara kwa mara. Baadaye, alijaribu hata kunihadaa na kuwa marafiki na Kelvin. Ananichukulia kama mjinga”

Sam alikuna ncha ya pua yake na kusema. “Hata hivyo, tayari nimekuchunguzia. Ni juu yako ikiwa unataka kuachana naye au kuendelea naye.”
Alvin hakuwa na mahali pa kutoa uchungu wake. Aliwasha sigara na kumwambia Sam. "Twende tukanywe vinywaji vichache na mimi leo usiku."

Sura ya 135

Usiku huo, Alvin alikunywa glasi baada ya glasi ya pombe. Sam hakuweza kumzuia. Uvumilivu wa pombe wa Alvin ulikuwa mkubwa, lakini alikunywa sana usiku huo na cha kushangaza alilewa kidogo.

"Nimemkumbuka Sarah ghafla." Alitazama usiku nje ya dirisha na kunong’ona, “Kati ya wanawake wote waliobahatika kuingia kwenye maisha yangu, ndiye pekee aliyekuwa na moyo wake wote kwangu. Hakukuwa na udanganyifu na hakukuwa na usaliti. Kwa nini alikufa?”

Sam alishika glasi yake, maumivu makali yakimtoka moyoni.
Kile ambacho wengine walikiona kwa Alvin kilikuwa ni Kilima cha juujuu kilichoonyesha ufahari wake, lakini Sam alijua kwamba Alvin alikua bila mapenzi ya wazazi wake. Ndani ya moyo wake alikuwa ni mtu asiyejiamini sana katka suala zima la mahusiano. Hata alipokuwa akisoma shule, waliomwendea walikuwa na ajenda za siri na kumfanya aingiwe na mashaka makubwa. Wakati huo, Alvin aliumia sana.

Kama rafiki yake, Sam ghafla alijuta kumwita Dar es Salaam. Hakutarajia kwamba moyo wa Alvin, ambao siku zote ulikuwa umeganda, ungehamaki ghafla. Sam aliongozana naye kunywa hadi Alvin akalewa sana. Ilikuwa ni mara ya pili Sam kumuona Alvin akiwa amelewa kiasi hicho.

Kwenye meza ya vinywaji, simu mpya ilitetemeka kila mara. Lisa alikuwa akimpigia simu Alvin mara kwa mara. Sam alichukua simu na kuitikia. Sauti ya Lisa ilisikika kutoka upande wa pili. “Uko wapi? Mbona umechelewa sana? Njoo nyumbani, tutayaongea tu yataisha sawa…"

"Alvin amelewa." Sam akamkatisha.

"Nakuja kumchukua mara moja," Lisa alisema kwa hofu.

"Hakuna haja. Hutaweza kumbeba hata hivyo. Nitamrudisha mimi mwenyewe.”

Baada ya simu kukatika, Lisa alisubiri mlangoni. Kulikuwa na mvua usiku huo tena, na matone ya mvua yalidondoka nje na kulowanisha kila kitu. Nusu saa baadaye, Sam aliegesha gari lake. Alipumua kwa huruma na upole baada ya kumuona Lisa akiwa amesimama kwenye upepo wa baridi.

Baada ya gari kuegeshwa, Lisa alifungua mlango wa siti ya nyuma. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona Alvin akiwa amelewa sana. Uso wake mzuri ulionyesha wazi kuwa alikuwa amelewa, na alionekana kupoteza fahamu pale kwenye siti ya nyuma. Yeye na Sam walimsaidiana kumwingiza Alvin hadi chumbani pamoja. Lisa alimtazama Sam huku akihisi mnyonge. “Bwana Harrison, asante. Mimi…”

“Ni sawa, Alvin aliniambia niachunguze jambo hili. Najua hukukusudia.” Sam alikuwa na maumivu ya kichwa. Pia hakujua la kusema. “Nitaondoka sasa hivi.”

Lisa aliona kuwa Sam alikuwa akimchukulia tofauti na hapo awali. Hakucheka na kutabasamu kama alivyomfanyia siku za nyuma. Alikua na huzuni kidogo kwa sababu yake. Alijua kwamba hakutaka kuzungumza naye sana, lakini hakuweza kujizuia kuuliza, “Bwana Harrison, unajua Alvin anachofikiria kuhusu hili?”

"Lisa, mwanaume yeyote angechukizwa na hilo," Sam alisema bila kuficha, "Ungemwambia Alvin juu ya hili mapema. Sasa kwa kuwa imejulikana bila wewe kusema, kusema kweli inatia uchungu sana.”

Uso wa Lisa ulipauka. “Hakuna kilichotokea kati yangu na Kelvin. Ni kweli."

“Ni bure kuniambia hivyo. Unahitaji Alvin akuamini.” Sam akatikisa kichwa na kuondoka.

Lisa alibaki ameduwaa kwa muda. Alielewa nini Sam alimaanisha. Alvin hakumuamini. Afanye nini? Alikuwa anampenda kweli sasa. Hakutaka kumuacha. Alimtazama sana yule mtu pale kitandani. Huenda ikawa ni kwa sababu alikuwa amekunywa pombe kupita kiasi na hakujisikia vizuri, hivyo tumbo lake pia likawa na usumbufu. Aliendelea kupapasa tumbo lake. Kiyoyozi cha kuongeza joto kiliwashwa mle chumbani na hakuwa amevua koti lake, kwa hiyo jasho likatoka upesi kwenye paji la uso wake. Lisa alichota beseni la maji ya baridi. Alivua koti lake, akafungua kola ya shati lake, na kuufuta uso wake mzuri kwa taulo.

“Sarah…” Mwanaume huyo alimshika mkono ghafla, na manung’uniko ya chinichini yakatoka kwenye midomo yake myembamba. Lisa aliganda kana kwamba ndoo ya maji baridi imemwagwa juu yake.

Sarah? Huyo alikuwa nani? Je, alikuwa mpenzi wake wa zamani?
Lisa aliuvuta mkono wake kutoka kwenye mshiko wake kwa nguvu. Mkono wa mtu huyo ulishika hewa, na akamwita tena, “Sara”.

Aligeuka na kukaa pembeni ya kitanda. Macho yake yalikuwa mekundu, na moyo wake ulikuwa umechomwa kana kwamba alikuwa akichomwa kisu. Inauma!

Asubuhi iliyofuata, Alvin aliamka na hangover. Kichwa chake kilimuuma, na tumbo lake lilihisi kukosa raha pia. Alitazama mazingira na kugundua kuwa alikuwa katika chumba chake cha kulala katika nyumba yake. Kwanini Sam alimrudisha pale? Kwa kweli hakutaka kukutana na Lisa kabisa. Hata hivyo, alikuwa amekunywa pombe kupita kiasi jana yake usiku na alikuwa akijisikia vibaya sana muda huo.

Alipotazama huku na kule, ghafla aliona kikombe cha maji ya uvuguvugu na vidonge viwili vya tumbo vimekaa kando ya kitanda cha kulalia. Macho yake meusi yalimtoka. Alihisi ni Aunty Linda ndiye aliyemwkea dawa hiyo. Alichukua dawa huku moyo wake ukiwa umechanganyikiwa. Alishuka tu baada ya kunawa na wakati tumbo lake lilihisi vizuri kidogo.

Shangazi Linda alipokuwa akifanya usafi alimuona Alvin akishuka. Alitabasamu. "Bi Kimaro anakuandalia kifungua kinywa sasa hivi."

Alvin akaenda kwenye meza ya chakula. Kulikuwa na nyama na nguruwe iliyochomwa, supu ya kuku wa kienyeji, maziwa fresh, maziwa, juisi ya limao...

Mlango wa kuteleza wa jikoni ukafunguliwa, na Lisa akatoka na chungu cha mtori. Alivaa gauni la rangi ya waridi na aproni iliyofungwa kiunoni mwake. Nywele zake zilikuwa zimefungwa kama mkia wa farasi, na kufunua uso wake mdogo na safi. Ilimfanya aonekane mpole na mtulivu.

"Ulikunywa sana jana usiku, kwa hivyo ni bora ukaanza kwa kula kitu chepesi asubuhi. Mtori ni rahisi kusagwa na hautakuwa mzigo kwenye tumbo lako.” Lisa alisema huku akivuta bakuli la mtori na kuliweka mbele yake.

Alvin aliutazama ule mtori kisha akamtazama Lisa. Taswira ya yeye kushika shingo ya Kelvin na kumbusu kwa nguvu ghafla ilionekana akilini mwake. Kamba ya uvumilivu moyoni mwake ilionekana kukatika kwa nguvu. Alinyanyuka na kuumwaga mtori moja kwa moja kwenye pipa la takataka. Kisha akamtazama kwa macho ya jeuri. "Vitu unavyopika ni vichafu."

Uso wa Lisa ulibadilika ghafla. Baada ya muda mrefu, alipepesa macho yake ambayo yalikuwa yakitoka kwa machozi. “Kwa kuwa unafikiri mimi ni mchafu, kwa nini nisiondoke?” Kwanza likuwa ameita jina la mwanamke mwingine alipolala, hata hivyo. Kwa kweli, labda hakumpenda sana.

Alvin aliganda alipomsikia hivyo. Macho yake yaliyokuwa na damu kwa mbali yalimtazama ghafla. “Unataka kuondoka? Unataka kwenda kwa Kelvin kukaa naye sasa? Kila mtu kwenye mtandao anawaambia nyinyi wawili mnafaa kuwa pamoja. Nyinyi ndio wanandoa wanaofaa zaidi katika ulimwengu wa biashara.”

"Hapana." Lisa hakuweza kulala usiku kucha kwani alijiona hana nguvu. “Naondoka kwa sababu hutaki kuniona.”

"Hata kama unanichukiza, unatakiwa kukaa katika nyumba hii," Alvin alifoka kwa hasira, "Maadamu nipo karibu, unaweza tu kuota kuwa na Kelvin. Acha nikuambie, Lisa Jones, kwa kuwa umenichokoza, usifikirie hata kuniacha nikiwa mzima!”
Kisha, akaondoka.

Lisa alitabasamu kwa uchungu. Hivi, alikuwa bado mzima? Tayari alikuwa amepoteza moyo wake kabisa.

TUKUTANE KURASA 136-140

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom