SIMULIZI YA MAISHA: KWANINI MIMI? 10
MWANDISHI : MIKA AUTHOR
MSAMBAZAJI:
Simulizi za Gilbert
MAWASILIANO: +255621249611
Tulipoishia -
Kauli ya daktari ilimchanganya juma."mmmh hajamnyonyesha mtoto kivipi wakai asubuhi hii amaetoka kumnyonyesha? Halafu hii damu kupungua hivi maana yake nini? Au huyu mtoto ananyonya damu ?". Alijiuliza juma moyoni.
Endelea nayo.
" huyu mtoto atakuwa ananyonya damu sio bure" aliwaza juma.
" Naomba tafuta ndugu wa kumtolea damu mkeo" aliongea daktari.Juma alitoka nje kwenda kuwatafuta ndugu.Akiwa nje aliingiza mkono mfukoni hili achukue simu .Simu haikuwepo.Alipapasa mifuko yote hakukuta kitu.
" aaah! Sijui akili yangu iko wapi? Yaani natafuta kitu ambacho akipo.Simu niliporwa siku ile halafu saiz nimesahau najifanya kuitafuta." aliwaza juma moyoni.Alifikiria aanzie wapi hakupata mwanga.
Aliamua kwenda nyumbani kwa mama yake mzazi ili amuombe mdogo wake aende kumtolea damu.Kutokana na kutokuwa na hela ya nauli ilibidi atembee kwa miguu.Alitembea umbali mrefu sana hadi akafika.Alibisha hodi na kuingia ndani.
" afadhali umekuja mwenyewe.Yaani hapa nilikuwa napanga nije huko huko nyumbani kwako" aliongea mama juma.
" mbona ivyo mama? Kuna usalama kweli?"
" usalama haupo kabisa.Moyo wangu bado unaumia sana.Kuna muda uwa nawaza kama kweli wewe ni mwanangu au walinibadilishia"
" aaaah! Mama maneno gani ayo.Kwanini umasema ivyo lakini.Mbona kauli kali sana iyo.Mimi mwanao uliyenizaa wewe mwemyewe na kunilea maisha yangu yote leo unaniambia ivyo mama"
" kwanini nisikuambie?,kwani unayonifanyia wewe ni mazuri?""
" mmmh! Nimekufanyia nini mama.Mbona sioni ubaya niliokufanyia"
"Hivi una akili wewe mtoto? Uoni ubaya kivipi?,hivi uoni kama umetuletea mkosi kwenye familia yetu.Hivi mkeo yule mtoto aliyemzaa ni mtoto au ni kindondocha kile"
" mama tafadhli usimwite ivyo mwanangu.Kwanza nimeshampa jina.Kuanzia sasa acha kumuita majina ya ajabu.Jina lake ni ayubu.Nimeona nimpe jina la baba yangu ili kumuenzi baba."
" unasemaje wewe mwanaharamu? Umempa yule mtoto jina la baba yako.Naomba ushindwe katika ilo.Yaani ukome kabisa na ulegee.Jina la mume wangu kipenzi huwezi kumpa mshenzi yule.Sasa naomba unisikilize kwa umakini.Ukitaka mimi niendelee kuwa mama yako naomba yule mwanamke kamfukuze pamoja na mtoto wake."
" aaah sasa mama namfukuza aende wapi? Yule ni mke wangu ,na tulikubaliana tutasaidiana kwenye shida na raha.Namfukuza saizi aende wapi ? Na ukizingatia mkoa huu yeye hana ndugu"
" anaenda wapi ilo sisi halituhusu.Kitu ninachotaka mimi aondoke.Ametuletea gundu sana.Mtoto gani yule aliyezaa."
" kwani mama yeye kosa lake nini? Kwani yeye ndiye aliyepanga iwe vile? Ile si imetokea tu?"
" mmmmh! Imetokea tu wapi? Wala haijatokea tu.kilichasababisha mtoto azaliwe vile ni yeye kuchanganya mbegu.Alikuwa anakutana na wewe halafu anatoka tena kwenda kukutana na wanaume wengine.Matokeo yake ndo ayo"
" si kweli mama"
" eeeh wewe mtoto nimechoka kubishana na wewe.Ukikubali sawa ukikataa sawa ila kuanzia sasa wewe sio mtoto wangu na ninaomba utoke nyumbani kwangu."
" mama usinifanyie ivyo.kwanza mwanao nimekuja hapa nina shida.Mke wangu amelazwa hospital kaishiwa damu.Nilikuwa naomba huyu mdogo wangu akamtolee damu"
" mmmh utakuwa na wazimu wewe.Yaani mwanangu huyu aanze tu kwenda kumtolea damu yule mwendawazimu.Aisee ilo haliwezekani.Kwanza toka nyumbani kwangu" aliongea mama juma huku akimshika mwanae na kumtoa nje.
Juma alitolewa mkuku mkuku mpaka nje.Kinyonge na taratibu kichwa akiwa kakiinamisha chini aliondoka.Aliwatafuta marafiki zake wa msaidie .Akawapata wawili na yeye akawa watatu.Walienda hospital wakapimwa damu zao zikaonekana zipo sawa.Mke wa juma akawekewa damu.
.........
Turudi kwa mary yule mwanafunzi wa chuo
Mary tangu alivyokutana kimwili na baba tatu,alikuwa akimpigia simu baba tatu lakini simu yake haikupokelewa.Alipiga simu asubuhi mchana na jioni bila mafanikio yeyote.Moyoni alianza kuingiwa na wasiwasi.
" mmmh! Yule mbaba vipi? Mbona simuelewi?. Kwanini hapokei simu yangu.au hakufurahia mapenzi niliyomuonesha.mmmh! Hapana bana ,mapenzi alifurahia labda atakuwa na tatizo fulani" aliwaza mary.
Habari ya yeye kutembea na baba tatu alimwambia rafiki yake aitwae mage.Kwa jinsi mary alivyomsifia baba tatu kuhusu kutoa hela,mage na yeye aliingiwa na tamaa.Alimvizia rafiki yake akiwa amejiziuka akachukua simu yake na kuiba namba ya baba tatu.
Wakati mage anafanya ivyo mary alikuwa kwenye mawazo mazito.Alikuwa anawaza ni jinsi gani afanye hili aweze kukutana na baba tatu tena.Kitendo cha kutopokea simu yake kilimchanganya sana.Akiwa kwenye mawazo mazito rafiki yake mage alimshtua.
" mmmmh shoga,mbona ivyo? Utakufa na mawazo rafiki yangu.Tatizo nini?" aliuliza mage.
"Mwenzangu lile danga langu nililokuambia si alipokei simu yangu.Yaani toka jana namtafuta hewani simpati.Halafu naisi kama ameniblock .Maaana nikipigia simu inakata yenyewe bila kuita wala nini?" aliongea mary huku akionekana kama mwenye huzuni sana.
" mmmh shoga yangu wanaume ndivyo walivyo.We achana naye tu.Lamsingi mshukuru MUNGU amekununulia iyo laptop na pia kakupa hela nyingi za matumizi"
" mwenzangu kumshukuru namshukuru lakini mwenzio hela alizonipa sijafanyia chochote cha maana."
" aaah kwanini sasa?"
" si nilijua kila siku atakuwa ananipa.Sasa bahati mbaya ndio ivyo saizi hataki kabisa kupokea simu yangu."
" mmmmh! Halafu shoga nikuulize kitu?"
" uliza tu "
" mchumba wako alfani umemwambia laptop umepata wapi? ,maana tangu jana ananiulizia kweli .Na inaonekana kama hana amani kabisa."
"Nimemdanganya nimepewa na baba.Lakini tatizo ni kuwa siku ile naondoka na yule mzee na yeye aliniona,hivyo anahisi nimeongwa na yule mzee."
" duuuh! Kwahiyo kumbe anahisi tu ila hana uhakika"
" ndio.Anahisi tu ila hana uhakika kama nilitembea na yule mzee.Naomba ukikutana naye nisaidie kumwelewesha basi.Maana kiukweli nampenda sana.Huyu mzee mimi nataka kumchuna tu.ila mpenzi wangu wa kweli ni yeye" aliongea mary.
Mage ni rafiki mkubwa sana wa mary.Siri zote za mary, mage anazijua.ila pamoja na kuwa shoga yake mkubwa ,mage amekuwa akimuonea wivu mary.Mara nyingi alikuwa akitamani vitu alivyokuwa navyo mary.Mara nyingi amekuwa akimtega alfani ambaye ni mpenzi wa shoga yake.
Baada ya kupiga story na kuachana .Mage aliondoka akaenda kununua vocha na kumpigia baba tatu,kwani namba yake aliiba kwenye simu ya mary.Alimpigia na kujitambulisha kuwa yeye ni mwanachuo na alikuwa na shida naye.
Baba tatu baada ya kuisikia sauti ya mage kwenye simu alivutiwa na alijua kuwa hajawahi kukutana naye.Alimpa maelezo sehemu ya kuonana.Mage baada ya kuambiwa aende sehemu flan,alirudi hostel na kuoga mara tatu tatu.Alivaa nguo hii nakutoa,kila nguo aliyovaa aliiona haimpendezi.Mwishowe aliamua kuvaa ivyo ivyo.
Alichukua taksi kama alivyoelekezwa na kwenda kwenye hotel ambayo baba tatu alikuwa akimsubiri.Kama kawaida ya baba tatu akulaza damu,akifanya naye mapenzi kisha akampa hela ya matumizi na wakaagana na kuondoka .
..........
Turudi kwa mke wa juma.
Siku zilienda mke wa juma akaruhusiwa kutoka hospital.Yeye na mumewe wakaongozana mpaka nyumbani.Mawazo ya kutengwa na ndugu zake yalikuwa yanamsumbua juma.
" daaaah! Maisha bila kuelewana na mama nilikuwa siyataki kabisa.Sasa yametokea sijui itakuwaje" aliongea juma.
" kuna wakati mtu unakuwa hauna namna inabidi ukubaliane nayo ivyo ivyo.Wewe unazani utafanyaje.Kama ubaya ,hakuna ubaya wowote ambao sisi tumemtendea."
" mmmmh! Sawa lakini mke wangu.Kuna kauli ambayo mama aliiongea ambayo hadi saizi nikiifikiria nashindwa kuelewa.Sasa sifahamu kama ni kweli au la?"
" kauli ipi tena mume wangu?"
" mama amesema huyu mtoto kuzaliwa hivi imetokana na wewe kuchanganya damu"
" mmmmh! Kuchanganya damu kivipi tena?"
" Amesema inawezekana wakati upo mjamzito uliwahi kutembea na mwanaume mwingine ndiyo maana imekuwa hivi?.Kwa maelezo yake yeye anasema haiwezekani mwanamke akazaa mtoto wa ajabu kama hajafanya kitu chochote kibaya"
"Msema kweli ni mpenzi wa MUNGU mume wangu.Toka uliponioa sijawahi kushiriki mapenzi na mwanaume mwingine zaida yako.ilo naapa mbele ya MUNGU.Kama nasema uongo MUNGU anihukumu leo hiii hii"
" wewe mtaje taje tu MUNGU ovyo.Shauri yako mwenyewe.Kama umewahi kuchepuka ni bora ukawa muwazi ili tujue tunakusaidia vipi?"
" niliyochokuambia ni ukweli mtupu.Tangu uliponioa sijawahi kukutana na mwanaume mwingine kimwili.ila wakati tupo wachumba kabla hujanioa niliwahi kutembea na baba tatu.Na nilikuambia ukweli wote."
" ilo nakumbuka.Kuhusu baba tatu uliniambia.Si yule mzee aliyekurubuni kwa hela nyingi?"
" Ndiyo" alijibu mke wa juma kisha akaingia chumbani kumlaza mtoto.Muda ulikuwa umeenda.Baada ya kumlaza mtoto alienda kukaa barazani kupiga story na mume wake.Wakiwa wanapiga story ,gafla walisikia sauti ya paka ikilia kutoka chumbani.
" mmmmh! Mke wangu umemsikia paka uyo akilia ndani?"
" Ndio nimemsikia ila nashindwa kuelewa kaingia vipi chumbani?" aliongea mke wa juma kisha akasimama kuelekea chumbani.Kufika chumbani aliwasha taa.Alipoangalia sauti ilipokuwa inatoka alishika kichwa kwa mshangao." aaaah! Mwanangu" alitamka na kuacha mdomo ukiwa wazi kwa mshangao.
ITAENDELEA