Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Abdallahking

JF-Expert Member
Mar 19, 2018
3,983
10,804
Simulizi: Kurudi Kwa Moza
Mwandishi: ATUGANILE MWAKALILE
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES

SEHEMU YA 1



Moza alikuwa msichana mrembo ila aliishi maisha ya shida na kumfanya ajaribu kufanya kazi za ndani, na kwa bahati akapata kazi kwenye nyumba ya mama mmoja tajiri, aliyejulikana kwa jina la Rose ila huyu mama mara nyingi alikuwa hadumu na wafanyakazi wa ndani mara nyingi huwa anawafukuza na watu walijua hivyo hakuna aliyejua ukweli kuhusu wafanyakazi wa Rose kwani gafla utakuta wamepotea na ameleta mfanyakazi mpya kwahiyo wengi walihisi huwa anawafukuza.
Siku ya kwanza kumleta Moza nyumbani kwake alimpa onyo kabisa,
"Mambo ya nyumba hii uyaache kama yalivyo, wewe fanya kazi zako tu basi. Usiingilie mambo yasiyokuhusu"
"Sawa mama nimekuelewa, unadhani naweza kuingilia yasiyonihusu? Siwezi kufanya huo ujinga "
"Yani usithubutu kuingilia utaishia kubaya"
"Mbona unanitishia mama?"
"Sikutishii ila nakwambia hali halisi, umbea kwangu sitaki kabisa kama huwezi kazi unaweza umbea useme kabisa uondoke"
"Hapana mama simaanishi kuwa naweza umbea, kwanza binafsi umbea siupendi kabisa kwahiyo hata usijali kuhusu mimi"
Basi huyu mama alimuonyesha kazi zote za ile nyumba na vyumba vyote vya kusafisha, kwakweli nyumba ilikuwa ni kubwa sana lakini alimuonyesha yote, ila kulikuwa na chumba flani kilikuwa na chumba kwa ndani kile chumba kilikuwa kama choo cha ndani ya chumba na vigumu kujua kama kuna chumba ndani ya chumba, yule mama alimwambia Moza
"Hiki chumba ukishasafisha unakifunga halafu funguo unaweka juu ya mlango"
"Na hiko choo je nitakuwa nakishafishaje maana naona kufuli au hakisafishwagi?"
"Wee binti mbona umeanza kunitisha, umekionaje hiko?"
"Nilijikuta nimeangalia tu nyuma ya hilo kabati, nisamehe lakini. Kwani hakisafishwi au?"
"Hiko kilitengenezwa kwa lengo la kuwa choo ila kishazibwa na hakitumiki, nyuma yake kushabomolewa ila hapa mwanzo mlango ulibakia na kufuli, huwa hapafunguliwi maana hakuna choo wala nini na ukitoka ni nje kabisa ndiomana nimeweka kabati kama kuziba. Na wewe uache kuchunguza chunguza, kazi yako kwenye chumba hiki ni kusafisha tu nikikwambia ili kusiwe na vumbi basi ingawa halali mtu lakini panatakiwa kusafishwa."
Wakatoka nje na kumuonyesha sehemu zingine za kusafisha kisha alipomaliza ndipo Moza alianza kazi rasmi kwenye nyumba hiyo.
Moza alianza kumfahamu mtoto mmoja mmoja wa yule mama na hatimaye akamfahamu mume wa yule mama aliyejulikana kwa jina la Mr.Patrick, ila kitu kilichomshangaza Moza ni kuwa huyu baba hakuwa na sauti yoyote kwa mkewe yani chochote kitakachosemwa na mkewe kwake ni sawa, Moza alishangaa sana na kujiuliza,
"Ina maana huyu baba hawezi kuhoji? Au ndio mambo ya mjini ya mume kulelewa na mke wake, hata kama ndio akubali kila kitu. Ila nishaambiwa nisifanye umbea kwenye nyumba hii, ngoja niendelee na kazi zangu mie "
Moza aliendelea na kazi zake ila alijikuta akizoeana sana na mtoto wa kwanza wa yule mama, mtoto huyo alikuwa ni mdada mkubwa na alijulikana kwa jina la Sara, huyu msichana alimpenda Moza sababu Moza alikuwa anamsikiliza mambo yake,
"Unajua kwanini nakufagilia? "
"Sijui, hebu niambie kwanini"
"Sababu wewe unapenda kunisikiliza ninachosema "
"Unajua kila mtu anapenda kusikilizwa, lakini kwanini wewe hupendagi kumsikiliza baba yako?"
"Achana na yule baba bhana utaniudhi, kwanza hana hadhi ya kuwa na mtoto kama mimi. Yule ni bwege la mama tu"
Sara akaondoka zake ila Moza alibaki na maswali mengi sana kuwa kwanini yule Sara aseme vile, inamaana si mtoto wa yule baba? Na watoto wengine je, mbona wote hawamuheshimu yule baba? Moza aliwaza sana lakini badae alijiambia.
"Mambo ya umbea nilishaonywa kwenye nyumba hii"
Muda kidogo akiwa anafanya usafi wa kusafisha dirisha aliwasikia watoto wawili wa kiume wa yule mama Wakiongea, yule mama alikuwa na jumla ya watoto wanne, wa kwanza wakike aliyejulikana kwa jina la Sara, wa pili ni wakiume ambao walikuwa ni mapacha walijulikana kama Kulwa na Doto, wa mwisho alikuwa wakike ila alikuwa sio mkubwa sana na alijulikana kwa jina la Ana. Sasa watoto ambao Moza alitegesha sikio lake kuwasikiliza ni hao mapacha na hata hawakujua kama kuna mtu anawasikiliza, Moza alitulia tu akiwasikiliza:
"Yani mimi nikitaka kuoa nitamwomba sana Mungu nisije pata mke kama mama yetu"
Mwenzie akasikika akacheka kisha akasema,
"Kumbe inakuuma eeehh anavyofanyiwa huyu baba? "
"Yani inaniuma kinoma, sema tu ndio hivyo sio baba yetu hatuna cha kufanya ila inaniuma sana yani sana"
"Lakini moyoni unafurahia maisha ambayo mama anatupa, hivi ushawahi kujiuliza ungekuwa wapi maana baba yetu alishatukataa toka kitambo."
"Mi nadhani alichofanyiwa mama na baba yetu labda ndio kimemfanya awe hivi alivyo, ila nashukuru Mungu tunakula vizuri, tunaishi maisha mazuri tunayoyataka. Ila anayoyafanya mama yetu duh!"
"Mama alishasema tusiwaze sana na anachokifanya, tuwe makini na maisha yetu tu."
"Hata kama, hivi unakumbuka juzi aliku.......... "
Moza gafla alishtuliwa na Ana, na kumfanya ashtuke sana na aache kusikiliza umbea,
"Dada twende ukanitandikie kitanda"
Moza aliondoka na Ana huku akijiuliza maswali mengi sana juu ya yule baba mwenye Nyumba.
Moza alifika chumbani kwa Ana na kumtandikia kisha akamuuliza,
"Hivi mtoto mkubwa kama wewe unashindwaje kujitandikia kitanda"
"Wenzako kama wewe walikuwa na maswali ya kudadisi sana kwangu, kazi ikawashinda na mama akawatokomeza. Wewe umekuja kufanya kazi au kuuliza maswali?"
Ikabidi Moza amuombe msamaha mtoto Ana kisha kuondoka zake kwenda kuendelea na kazi zake huku akijiuliza maswali mengi sana.
Usiku wake Moza alishangaa yule mama akimuita kwa ukali sana,
"Wee Moza wewe"
Moza alishangaa kuitwa kwa ukali vile na kwenda kwa haraka sana, alivyofika pale tu cha kwanza alipigwa kofi hadi chini, akamtazama yule mama aliyeonekana na hasira sana, kisha yule mama akamuuliza Moza,
"Maswali gani ya kijinga hayo unamuuliza mwanangu?"
Moza alikuwa kimya alishindwa kujibu maana hakujua ubaya wa swali lake kwa yule mtoto ukizingatia anaonekana ni binti tayari wa karibia miaka kumi na mbili.
 
SEHEMU YA 2


Usiku wake Moza alishangaa yule mama akimuita kwa ukali sana,
"Wee Moza wewe"
Moza alishangaa kuitwa kwa ukali vile na kwenda kwa haraka sana, alivyofika pale tu cha kwanza alipigwa kofi hadi chini, akamtazama yule mama aliyeonekana na hasira sana, kisha yule mama akamuuliza Moza,
"Maswali gani ya kijinga hayo unamuuliza mwanangu?"
Moza alikuwa kimya alishindwa kujibu maana hakujua ubaya wa swali lake kwa yule mtoto ukizingatia anaonekana ni binti tayari wa karibia miaka kumi na mbili.
Moza alibaki akishangaa tu, mara kibao kingine akapigwa, kasha Yule mama akamwambia,
“Si nilishasema mambo ya udadisi kwenye nyumba yangu sitaki, huyu mtoto asipoweza kutandika kitanda wewe inakuhusu nini? Inamaana wewe ndio unajua kulea sana au, mambo ya mtoto wangu hayakuhusu. Kama hajui kufanya kazi yoyote mwache tu kama alivyo, nimekuajili wewe sio uje kukaa tu na kuuliza uliza maswali ya kijinga. Sitaki, na ninakwambia sitaki kabisa huo upuuzi na nisisikie tena”
Ikabidi Moza amwombe msamaha mama huyu,
“Nisamehe mama, kwakweli haitajirudia tena. Naomba nisamehe. Nisamehe sana”
“Mimi sio wa kuniomba msamaha, nenda kamuombe msamaha Ana huko”
“Lakini Ana nilishamuomba msamaha”
“Mpaka kaniambia mimi inamaana hajakusamehe, nenda kamuombe msamaha tena mpaka akusamehe ndio uje hapa. Na asipokusamehe jiandae kurudi kijijini kwenu”
Moza akaondoka taratibu mpaka chumbani kwa Ana akaingia na kumuamsha kasha kuanza kumuomba msamaha, Ana akamuangalia Moza akamsonya kasha akamwambia,
“Hivi unaingiaje chumbani kwangu bila ya hodi, hujui kugonga hodi au? Halafu unaniombaje msamaha huku umesimama kama mlingoti? Toka nje huko, ugonge mlango nikuruhusu kuingia kasha uje na magoti ndio uniombe msamaha”
Moza akatoka nje na kugonga mlango, aliporuhusiwa na Ana alipiga magoti, akaingia chumbani kwa Ana na magoti kisha akamuomba msamaha, Ana alicheka kasha akamwambia,
“Nimekusmehe ila siku nyingine usirudie tena. Nilijua na wewe ni kiburi kama waliopita. Haya ondoka zako”
“Asante Ana”
Moza alitoka huku macho chini, alienda kumalizia kazi zake kasha akaenda kulala.
 
SEHEMU YA 3


Alipokuwa chumbani aliwaza sana, na kujisemea
“Jamani umasikini huu loh, yani mimi kweli wa kudhalilishwa na yule mtoto mdogo jamani? Yule si sawa na mtoto wa dadangu jamani, yani kanidhalilisha nimpigie magoti nimuombe msamaha, yote haya ni sababu ya umasikini tu. Ningekuwa na uwezo au kwetu kungekuwa na uwezo yasingenipata yote haya, ila wadada wengi wa kazi tunateseka sababu ya umasikini.”
Alijifikiria sana, ila aliamua kulala ili kesho awahi kuanza usafi na shughuli zingine.
Akiwa kwenye usingizi mzito wakati panakaribia na kukucha akajikuta yupo kwenye ndoto nzito sana, alijiona yupo mahali halafu kuna wadada kama watano wapo pande ya pili wakimuomba msaada, akawa anasikia kelele,
“Moza tusaidie, Moza tusaidie tafadhari,Moza ni wewe tu unaeweza kutusaidia”
Wakati anataka kwenda kuwasaidia akashtuka kutoka usingizini, alikaa akitafakari kuwa ni ndoto ya aina gani ile. Lakini alipoangalia saa aliona karibu panakucha, alitoka chumbani na kwenda kuanza shughuli za usafi, alishangaa kumkuta baba mwenye nyumba yani Mr.Patrick akiwa sebleni muda ule amesinzia, hakutaka kuhoji kwani taratibu za nyumba ile bado hakuzijua vizuri kwahiyo alianza tu kufanya kazi zake hadi muda wanaamka wengine na kujiandaa kutoka huku wengine wakisubiria chai mezani ikabidi awaandalie.
Siku hiyo Ana alichelewa kuamka, ila kwavile hakujua taratibu za nyumba ile alijua ndio kawaida, mama mwenye nyumba aliamka na kumfata Moza jikoni,
“Umeshamuamsha mtoto aende shule?”
“Mtoto yupi mama? Kwanza shikamoo”
“Nitolee uwendawazimu wako mie, inamaana humuoni Ana kuwa ni mtoto! Kwahiyo hujamuamsha hadi muda huu unategemea nini? Mwanangu haendi shule, au ulijua hasomi kama watoto wa kijijini kwenu? Haya nenda kamuamshe na utaenda nae shule, wewe ndio utamtetea kuchelewa kwake”
Moza hakubisha ila alienda hadi chumbani kwa Ana, ila alipofika mlangoni akasita kuingia maana jana yake huyo Ana alimfokea kwa kitendo cha kuingia bila ya hodi. Ikabidi aanze kugonga hodi, aligonga na kugonga na kugonga ila hakuitikiwa akawa anajishauri tu kuwa afanyaje, wakati anajishauri, Sara alipita pale na kumkuta anagonga,
“Weee huyo mtoto analalaga kama pono, yani hapo utagonga hadi vidole viote sugu. Ingia tu umuamshe”
Moza akamwambia Sara,
“Lakini jana alinikataza kuingia chumbani kwake bila ya hodi”
“kitoto kina amri sana hicho sijui kwanini, ila ingia tu. La sivyo atazidi kuchelewa shuleni”
Ikabidi Moza aingie huku akiwa na hofu ya kufokewa na Ana. Akaanza kumuamsha kwa utaratibu,
“Ana, amka uende shule mtoto mzuri”
Ana alimka, kasha akatabasamu baada ya kuamka, na kumwambia Moza
“Kaniwekee maji ya kuoga nioge halafu niandalie na sare kabisa”
Moza alimuandalia huku akimsikiliza kuwa ni nguo gani amuandalie kasha Ana akaenda kuoga na kuvaa, baada ya kumaliza ilitakiwa Moza ndio ampeleke Ana shuleni, akatoka sebleni na kumkuta mama na baba,
“Mama, ndio nataka kumpeleka Ana shuleni”
“Si umpeleke, unataka mimi nifanyeje?”
“Nampelekaje mama?”
“Hivi si uzembe wako, gari ya shule imemuacha? Mpeleke sasa utajua wewe utampelekaje”
Moza akajifikiria akakosa jibu, mjini kwenyewe hajawahi kuishi kivile sasa ni njia gani atampeleka huyo mtoto shuleni ikiwa hata shule ilipo hajui, wakati anawaza hayo akamsikia Yule baba mwenye nyumba akisema,
“Naomba niwapeleke mke wangu, nipe ruhusa yako.”
“Si mafuta yako hayana kazi”
“Ila mke wangu, huyu mdada bado ni mgeni”
“Bhana wee wapeleke ila ndio ajifunze sio kesho tena amuache mtoto alale mpaka muda huu. Na hakikisha unaenda kumtetea mtoto kwa walimu. Tumeelewana Moza?”
“Ndio mama”
Kisha, Moza, Ana na Mr.Patrick wakatoka na kuelekea kwenye gari la Mr.Patrick halafu safari ya shule ikaanza.
Walipofika shuleni, Moza alishuka na Ana hadi kwa walimu wake, ambapo mwalimu mmoja akasikika akisema
“Ana umechelewa na leo ila kama kawaida yako umeletwa na mtetezi. Haya dada tunashukuru kwa kumleta Ana, nenda tu. aAna nenda darasani”
Moza alimshukuru pale kasha akarudi kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza, huyu baba alimuuliza Ana,
“Hivi kitu gani kilifanya uje kufanya kazi pale kwetu?”
“Nilikuwa natafuta kazi tu ndio nikapata pale”
“Unajua kama ukiingia pale hutoki?”
“Sitoki kivipi?”
“Yani huwezi kurudi kwenu”
“Kivipi baba mbona sijakuelewa?”
“Ile nyumba nilijenga mwenyewe kwa mikono yangu, kwa hela zangu ila hata mimi kutoka siwezi. Nafahamu vingi ila sina ufahamu wa kutoka”
Moza akajikuta akivutiwa sana na mazungumzo haya, huku akimuuliza Yule baba kwa makini,
“Hebu nieleweshe vizuri baba, nasikia wafanyakazi waliotangulia mama aliwafukuza sasa sijui walifukuzwa kwa nini?”
“Hawajafukuzwa ila walipo hata mimi sijui na mke wangu hajanipa nafasi ya kujua. Nimechagua leo kukusindikiza ili nikwambie haya. Nakuona huna hatia, ila umeingia sehemu sio yenyewe. Mimi ni baba mwenye akili zangu timamu kabisa lakini zipo kama hazipo. Nina mtoto ambaye ni damu yangu kabisa, naamini ni damu yangu ila mke wangu huyu ananiaminisha kuwa Yule mtoto si damu yangu”
“Yuko wapi huyo mtoto? Je ni mmoja kati ya waliopo nyumbani?”
“Hapana si mmoja wao, yupo kwa mamake anaitwa. Yani Yule mtoto ni damu yangu kabisa ila mke wangu hataki kumuona wala hataki niwasaidie. Ujana umeniponza mimi, mwanangu anapata shida huko alipo ila kumsaidia siwezi. Kwa wale waliopo nyumbani, siamini hata mmoja kuwa ni mwanangu, wale watatu nilimkuta nao mke wangu ila huyu Ana amezaa akiwa na mimi. Ila siamini kama ni mwanangu kwani kuna mwanaume alishaletwa nyumbani, na mke wangu alikuwa anamuita baba Ana halafu Ana nae alikuwa anamuita huyo mwanaume baba”
“Baba, yani sielewi kabisa. Na kwanini umeniambia yote haya?”
“Nimejisikia tu kukwambia, kisha kuwa makini sana. Ila mke wangu sijue kama nimekwambia, usithubutu kuongea chochote na kumuonyesha kama kuna jambo nimekwambia. Mimi siendi sehemu nyingine mpaka aniruhusu yeye. Ningepata mtu wa kunisaidia, kunitoa kwenye hiki kifungo ningefurahi sana”
“Pole sana baba”
“Tafadhali usiseme, nakuomba usiseme. Utapotea”
Gari ikaingia ndani, kisha kimya kilitanda na wakashuka garini, moza alipoingia ndani alimkuta Yule mama akijiandaa kuondoka ila kabla hajatoka alimwambia,
“Haya mume wangu umesharudi naomba ukalale hadi nitakapokuja”
Yule baba hakupinga, alienda moja kwa moja chumbani kisha Yule mama akamuangalia moza na kusema,
“Kama nilivyokwambia, kuwa makini. Mambo ya umbea kwenye nyumba yangu sitaki”
Yule mama akatoka zake, na Moza akaenda kwenye shughuli zake zingine.
 
SEHEMU YA 4


Akiwa jikoni, walikuja wale mapacha na kumuaga pia,
“Sie tunatoka, sasa ukipika vyakula kama vya kijijini kwenu utakula mwenyewe”
Wakaondoka zao, na muda kidogo akaja Sara nae na kusema,
“Leo nina hamu na maini rosti na chapati na juisi. Tafadhali nitengenezee hivyo, nikirudi nitakula maana nataka kutoka”
“kwahiyo ndio niandae chakula hicho leo?”
“Sijui wengine wanapenda nini, kwani mama hajakwambia anachotaka leo?”
“Hajasema”
“Basi mkaangie samaki, mwekeena viungo. Mama anapendaga samaki sana”
“Na chakula gani sasa?”
“Utamuwekea na hizo chapatti, anapenda pia. Ila Ana anapenda wali, yani fanya ufanyavyo ila wali usikose. Halafu baba anapenda ugali, ila baba usimjali sana maana atakachosema mama atakula tu. Mimi ndio natoka hivyo, tuitaonana badae”
Sara akaondoka zake, yani moza kabaki tu anajiuliza,
“Humu ndani kama hotelini, yani kila mtu anaagizaa chakula anachotaka yeye yani nitakonda humu. Ila umaskini huu loh, ndio umesababisha yote haya. Ila wale mapacha hawajasema ni chakula gani, natumaini nao watakula maini rosti na chapati.”
Moza alianza kuandaa mapishi yake huku akijikuta anamfikiria sana Yule baba, yani maisha ya Yule baba yalimsikitisha sana, hakuwa na kauli yoyote kwa mkewe na alimsikiliza mkewe kwa chochote alichomwambia.
Wakati anaendelea na mapishi, roho yake ikamtuma aende kwenye kile chumba ambacho kinaonekana kina choo ndani kilchofungwa,
“Mmh mama akinikuta kwenye kile chumba, nitamwambia nilikuwa nafanya usafi. Ngoja niende”
Alipomaliza tu kuandaa chakula, moja kwa moja akaenda kwenye kile chumba na kuchukua ufunguo juu ya mlango kisha akafungua na kuingia ndani. Ila mawazo yake yalikuwa ni kwenye mlango wenye kufuri basi huku akijiuliza kama ule mlango unatoka nje mbona kwa nje hauoni? Akajisogeza moja kwa moja huku akihisi kuwa huenda akishika kufuli unaweza kufunguka, basi Moza akasogelea na kushika lile kufuli gafla alipigwa na shoti ya ajabu na kutupwa kabisa.
Hapo akazimia, na lilipita lisaa limoja akazinduka akiwa amechoka sana, akajaribu kuinuka akaweza, kisha akatoka na kufunga mlango halafu funguo akazirudishia pale pale juu. Akaelekea sebleni sasa, Mara akakutana na mama mwenye nyumba nae anaingia sebleni kutoka nje akiwa na hasira sana.

 
SEHEMU YA 5



Hapo akazimia, na lilipita lisaa limoja akazinduka akiwa amechoka sana, akajaribu kuinuka akaweza, kisha akatoka na kufunga mlango halafu funguo akazirudishia pale pale juu. Akaelekea sebleni sasa, Mara akakutana na mama mwenye nyumba nae anaingia sebleni kutoka nje akiwa na hasira sana. Alikuwa anahema juu juu, akamsogelea Moza na kumuuliza kwa ukali
“Umefanya nini?”
“Sijafanya chochote mama”
Rose alimuacha Moza pale sebleni na kuelekea mitaa ya chumbani ambapo moja kwa moja alielekea kwenye kile chumba, Moza alienda jikoni huku uoga ukiwa umemshika na kuomba kuwa huyu mama asijue kama aliingia mule chumbani. Ingawa moza alikuwa kamaliza kupika ila alikaa tu jikoni akiwaza, muda kidogo Rose alirudi sebleni na kumuita Moza kwa ukali, kitendo ambacho kilimuogopesha Moza na kuhisi kuwa pengine Rose amegundua. Alienda sebleni kwa uoga kiasi, kisha huyu mama akamuuliza,
“Baba aliamka toka ameenda kulala?”
“Hapana mama, toka muda ule sijamuona tena sebleni?”
“Sikia Moza, naomba vitu vya nyumba hii uviache kama vilivyo”
“Ila sijafanya kitu mama”
“Nilikuwa mbali sana, ila kuna kitu kimefanyika ndani nimepata taarifa ndiomana nikaja haraka sana. Ila kwavile umesema hujafanya kitu, basi. Hata hivyo hicho kitu ambacho nilikuwa nakihisi kuwa umekifanya basi muda huu ningekukuta na hali mbaya sana. Tafadhali Moza, vitu vya nyumba hii viache kama vilivyo. Unaweza ukanishangaa kuwa mbona narudia rudia msemo wangu, nina maana kabisa, viache kama vilivyo”
“Sawa mama nimekuelewa”
“Na sitoki tena saivi,ngoja nikapumzike tu. Nipikie ugali na samaki, nitakula nikiamka”
Moza alienda jikoni kuandaa huo ugali huku akiwaza kuwa amepona ila aliwaza ameponapona vipi bila kubambwa ingawa alizimia kwa karibu lisaa lizima, pia akawaza kuwa huyu mama kapata vipi taarifa huko alipokuwa kwamba ule mlango ulishikwa? Hapo kidogo akapatwa na uoga, akawa tu anajisemea mwenyewe
“Mimi Moza mimi jamani nitulie tu, kwetu nakupenda pia. Nitakuwa sirudi mmmh”
Alipomaliza alienda chumbani mara moja.
 
SEHEMU YA 6



Alipoingia chumbani alijiweka kitandani, mara usingizi ukampitia. Akaanza kuona kama anaingia tena kwenye kile chumba, kisha anafungua mlango wa kile choo ila mule aliwakuta wadada watano wakiwa wamechoka sana, ni wadada walewale ambao walikuwa wakimuomba msaada kwenye ndoto ya jana yake. Kwahiyo ndoto hii ilikuwa kama muendelezo wa ile ndoto ya usiku ila ndoto hii ilikuja kivingine. Wakati anawashangaa wale wadada, halafu akawa kama anataka kuwahoji, mara gafla akasikia sauti ikiita…
“Moza, Mozaa…”
Akashtuka kutoka usingizini na aliposikiliza vizuri ilikuwa ni sauti ya Ana, ikabidi atoke haraka kwani alitambua itakuwa Ana amerudi shuleni. Moza alivyofika sebleni akamkuta Ana amekaa na amevimba kwa hasira, ilibidi Moza aanze kwa kumuomba msamaha
“Nisamehe Ana, nilipitiwa na usingizi kidogo”
“Umekuja kulala au kufanya kazi, yani mimi nakuita muda wote huitiki, haya piga magoti”
Moza hakubisha alipiga magoti, kisha Ana akamwambia,
“Nivue viatu”
Moza alimvua Ana viatu, kisha akanza kumsikiliza ujumbe mwingine
“Begi langu la madaftari nimeliacha pale getini kwa mlinzi kalichukue unipelekee chumbani.”
Moza alienda kwa mlinzi kuchukua begi, Yule mlinzi akamwambia Moza
“Usisubiri siku nyingine akukumbushe, yani akirudi tu uje uchukue begi lake. Yeye hawezi kubeba eti ni zito”
Moza aliondoka na lile begi hadi chumbani kwa Ana akagonga na kuruhusiwa kuingia, kisha akaenda kuliweka lile begi. Ana akamwambia Moza,
“Nipikie tambi na mayai, nataka kula hivyo leo”
Moza aliitikia kisha akaenda jikoni kuandaa huku akiwaza moyoni,
“Hivi mimi ni mfanyakazi wa ndani au ni mfanyakazi wa hotelini? Mmmh hii nyumba unaweza kujikuta siku nzima unapika tu”
Aliwaza Moza huku akifikiria kutoweza kufikisha hata miezi miwili humo ndani,
“Kazi za humu ni za kitumwa sana, yani mwezi huu ukiisha tu nipate mshahara wangu nirudi kwetu nikaangalie ustaarabu mwingine”
Alipika na alipomaliza, alitoka nje na moja kwa moja alienda getini kwa mlinzi, kisha akamuuliza
“Kaka samahani, hivi wewe una muda gani toka uanze kulinda hapa?”
Huyu mlinzi akacheka kwanza, kisha akamwambia
“Ni kitambo sana, kabla huyo Ana hajazaliwa. Mimi nipo hapa, yani huyo Ana anakuwa namuona”
“Kheee kumbe! Mbona nasikia wafanyakazi wa hapa hawakai yani wanafukuzwaga”
“Ni wa huko ndani sio mimi, ni sababu hawawezi kufatilia sheria za huyu mama. Mfanyakazi ambaye alikaa hapa kwa muda mrefu ni mmoja tu, ambaye anaitwa Ashura. Yeye peke yake ndio alikaa hapa kwa muda mrefu na aliondoka mwenyewe ila ni mtu mwenye siri nzito sana”
“Yuko wapi huyo Ashura?”
“Dada, tambua kwamba unaongea na mwanaume. Nimekaa kwa muda mrefu kwenye nyumba hii sababu mimi ni mwanaume. Mambo ya umbea sifanyi. Naomba kaendelee na kazi zako”
Moza aligeuka nyuma akamuona mama mwenye nyumba amesimama, ikabidi Moza aende upesi kumsikiliza,
“Kule getini unatafuta nini?”
“Nilikuwa namuuliza mlinzi masoko yalipo kwa hapa”
“Yule mwanaume na mambo ya masoko ni wapi na wapi? Moza, chunga sana nakuangalia ujue nakuangalia sana, huo mwenendo wako sijui kama tutawezana. Haya kaniwekee chakula mie”
Moza aliingia ndani, kisha Yule mama alienda kwa mlinzi, inaonyesha alienda kumuuliza pia kilichompeleka Moza pale getini.
 
SEHEMU YA 7


Moza alipomaliza kuandaa, Yule mama aliingia na kukaa mezani, kisha akamwambia Moza
“Una bahati sana, Yule mlinzi kaniambia ni kweli ulikuwa unamuuliza kuhusu masoko. Vinginevyo ungenitambua. Haya kaniitie kipenzi changu Ana nije kula nae”
Moza aliondoka kwenda kumuita Ana huku akijiuliza, Yule mlinzi kama amepanga nae vile, imekuwaje nae amesema kama yeye kuwa alikuwa anaulizia masoko, yani kama alikuwa kwenye akili ya Moza.
Kma kawaida aligonga kwa Ana na kumuita ambapo aliitikia wito na kwenda sebleni, kisha akamwambia Moza amletee chakula chake, ambapo Moza akafanya hivyo. Rose alipoona mwanae ameletewa kile chakula akasema,
“Oooh kipenzi changu leo umetaka tambi na mayai”
“Ndio mama, kuna sehemu nimeona picha nikatamani”
Kisha Rose akamuita Moza na kumuuliza,
“Wengine umewaandalia chakula gani?”
“Dada Sara amesema nimuandalie chapati na rosti ya maini, wale mapacha wamesema niwaandalie chakula chochote kizuri. Kwahiyo nao nimewaandalia chapati na rosti ya maini. Ila kuhusu baba nilimuuliza Dada Sara akasema anapendeleaga ugali kwahiyo nae nimemuandalia ugali”
“Wewe Moza wewe, hizo habari sijui za dada Sara sijui mapacha sitaki kuzisikia, sijui baba sitaki kusikia. Hao wote wanakula chakula ninachosema mimi. Mwenye amri humu ndani ni mimi tu, na Ana. Kwahiyo chakula ukiambiwa ukiandae na Ana, fanya upesi au mimi nikikwambia uharakishe ila usiniletee hayo madudu mengine.”
“Lakini si watoto wako pia?”
“Wewe, wewe, weeee msichana wewe usitafute maneno yani naona unachokonoa chokonoa mambo. Kwani wakiwa watoto wangu ndio nini sasa? Wawe na amri kwani nyumba yao hii? Tena sitaki kusikia. Mwenye amri humu ndani ni mimi na Ana tu nimemaliza”
Moza aliitikia na kwenda zake jikoni huku akijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu, na haswa ni kuhusu baba mwenye nyumba, masikini toka alipoambiwa akalale hajapewa amri ya kuamka hadi muda ule.
Moza akiwa kule jikoni, Yule mama alimuita kutoa vyombo kisha akamwambia,
“Siku nyingine sio mpaka nikuite kutoa vyombo, unatakiwa kujiongeza mwenyewe.”
“Sawa mama”
Moza alitoa vile vyombo ila alihisi kama Ana na mama yake wana maongezi ya ishara ambayo yeye hakuyaelewa moja kwa moja, na muda kidogo Ana na mama yake wakatoka yani wakaondoka kabisa hapo nyumbani ila muda huu hata hawakumuaga wala hawakumwambia kama wanatoka, kwahiyo Moza alibaki akishangaa tu mwenendo wa watu kwenye nyumba ile ila akajisemea kuwa atazoea tu.
Muda si muda akarudi Sara na alionekana kuwa amechoka sana, Moza alimkaribisha na kumpa pole
“Pole na mizunguko dada Sara”
“Asante, yani ni mizunguko haswaa. Vipi mama karudi?”
“Ndio alirudi ila ameondoka tena”
“Kheeee alirudi duh! Aliniambia kuwa leo atachelewa sana kurudi kumbe alisharudi mmmh huyu mama nae. Kwahiyo kaenda wapi sasa?”
“Sijui ila kaondoka na Ana”
“Yani mama na Ana mmh! Ngoja nikaoge mie uniandalie chakula changu”
Sara aliondoka zake ila Moza alitamani amdadisi na Sara pia ili aujue undani wa familia ile.
 
SEHEMU YA 8


Kwenye mida ya saa tatu usiku, wale mapacha nao walirudi na cha kwanza kabisa waliulizia chakula ambapo Moza aliwaandalia, pacha mmoja akaulizia kuhusu mama yao na Moza aliwapa taarifa kama aliyompa Sara, kisha Yule pacha akamuuliza kuhusu baba yao, mwenzie akamkatisha
“Sasa unamuulizia wa nini huyo?”
“Ni binadamu mwenzetu Kulwa, eti baba yuko wapi?”
“Kalala”
“Kalala saa hizi?”
“Hapana, ni tangu asubuhi mama alipomwambia akalale hajaamka tena”
“Duh”
Yule pacha akainuka pale mezani, Moza alitulia tu akiangalia picha inavyoendelea, baada ya muda Yule Dotto akarudi na Mr.Patrick na kumkaribisha mezani pia, ambapo Yule mzee alikula kama anakimbizwa, baada ya hapo Yule pacha akaongozana na Yule baba na kumrudisha tena chumbani kisha yeye akarudi sebleni. Yule Kulwa nae alikuwa ameshamaliza kula, akamwambia mwenzie
“Mama akigundua hili sijui utamwelezaje?”
“Vyovyote vile, Yule ni mwanaume mwenzetu, najua hata wewe hupendi kufanyiwa vile ila sababu unamuogopa mama”
Wakaondoka na kuelekea chumbani, Moza alitoa vyombo haraka haraka ili aende dirishani akawasikilize pia, na kweli alipoenda dirishani aliwakuta bado wana mada za Yule baba,
“Nimekuuliza Kulwa, unapenda anavyofanyiwa Yule baba?”
“Sipendi, lakini sina cha kufanya”
“Cha kufanya kipo ila hatujakifikiria”
“Kipi hicho?”
“Nahisi tutakigundua pindi huyu baba akifa”
“Hivi unadhani mama atamuachia huyu baba afe? Anamtesa tu, hajafikia hali ya ukatili kiasi hicho”
“Ila kwa nini mama yetu yupo hivi? Yani nawazaga hata sipati jibu”
“Hata mimi mwenyewe sijui halafu sasa yani mimi na wewe ni kwavile tu ni watoto wake ila mama hatupendi pia, labda baba yetu alimfanya vibaya mama. Yeye kipenzi chake anaanza Ana halafu anafatia Sara, yani mama sisi hatupendi kabisa”
“Ila kuna kitu nahisi kuhusu mama”
“Kipi hicho?”
Sauti ya Sara ikasikika akimuita Moza, naye Moza aliamua kwenda kimya kimya kwani alijua akiitika tu atawashtua wale mapacha.
Alivyofika kwa Sara,
“Inamaana mama bado hajarudi?”
“Hajarudi ndio”
“Nilitaka nimpe taarifa”
“Taarifa gani?”
“Leo nimekutana na Ashura, humjui wewe yani Yule mdada mama anamtafutaga sana. Ngoja nikuonyeshe picha yake nimepiga nae leo”
Sara akatoa simu yake na kumuonyesha Moza picha ya Ashura, ila Moza alishtuka kidogo sema alijigelesha ili Sara asigundue mshtuko wake.
Kisha Sara akamwambia Moza,
”Yani huyu Ashura alikuwa mzuri sana, halafu hata hakufanania na kazi za ndani. Alikuwa mpole na mkimya. Ni yeye tu aliweza kuishi kwa muda mrefu kwenye nyumba hii akifanya kazi za ndani ila baada yeye kuondoka hakuna tena msichana aliyeweza kuishi kwa muda mrefu hapa. Mmmh halafu sijui hata ni kwanini nakuambia yote haya, nenda kaendelee na shughuli zako Moza”
Moza alitoka pale na kwenda jikoni kusafisha vyombo huku akifikiria kuhusu Ashura,
“Mbona namjua Yule, alikuwa akifanya kazi za ndani duh! Si nimefanya kazi kwao Yule! Hapa lazima kuna kitu”
Moza alimaliza shughuli zote, kwenye saa sita kasoro ndipo Rose na mwanae Ana walirejea na kama kawaida Moza alipewa amri ya kwenda kutandika kitanda cha Ana.
Wakati anatandika kitanda cha Ana akasikia kama sauti inamwambia afunue godoro, wakati anataka kufunua mara Ana akaingia ndani na kumuuliza kwa ukali,
“Unafanya nini?”
Moza alipatwa na bumbuwazi tu, alishikwa na kigugumizi asiweze kujibu, mara Ana akamsogelea na kumzabua kofi.
 
SEHEMU YA 9


Kulipokucha akafanya shughuli zake kama kawaida ikiwa ni pamoja na kumuamsha Ana aende shuleni, leo Rose alionekana nyumbani kwake na kuwafanya wanae waage tu kuondoka bila kutoa oda ya chakula wanachotaka wapikiwe, hapo ndio moza akaelewa kuwa walifanya vile jana sababu walijua kuwa mama yao hayupo. Ila leo ilikuwa siku ya tofauti kidogo kwani hadi mr.Patrick aliruhusiwa kutoka,
“Nenda tu kwenye shughuili zako, zunguka tani yako leo. Utarudi nyumbani pindi tu nikikupigia simu kuwa urudi”
“Je usiponipigia nisirudi? Na je naweza kwenda kwa ndugu zangu?”
“Ole wako Patrick, usitake nibadili mawazo.Kwanza nenda ofisini kwetu, wamekumisi sana maana ni kitambo sana hawajakuona”
Mr.Patrick akaondoka zake na hakupenda kuongea sana.
Baada ya muda mfupi alikuja mgeni, mgeni huyu alikuwa ni Ashura ila alijifanya kamavile hamfahamu Moza yani utadhani ni mara yake ya kwanza kumuona, kitendo ambacho Moza kilimpa shauku kubwa ya kutaka kujua kuna nini katikati.
Rose na Ashura walikaa katika maongezi ila Moza alienda kukaa sehemu ambayo angewasikiliza, maana maongezi yao walifanyia sebule nyingine ambayo mara nyingi wale mapacha walifanya kama chumba chao cha kusomea vitabu.
Moza alikuwa makini kabisa kusikiliza maongezi ya Rose na Ashura.
“Sikia nikwambie Ashura, mi nilishakwambia sitaki Patrick ajue ukweli kuhusu Yule mtoto Salome lakini kwanini ameanza kuulizia?”
“Anamuulizia hadi jina?”
“Hapana, jina la mtoto halijui”
“Lakini mimi dada ukweli kabisa sijamwambia wala sijawahi kukaa na shemeji Patrick kumueleza chochote kile kuhusu mtoto wake. Nadhani ni watu waliomuona Salome kuwa kafanana sana na shemeji ndio wamemwambia”
“Mmh hivi kafanana nae sana eeh!”
“Yani dada uongo dhambi kwakweli ila kadri Yule mtoto anavyozidi kukua ndio shemeji mtupu”
“Mmh tuachane na hayo kwanza. Unajua wewe ndio unajua kila kitu kuhusu Yule mtoto. Wengine wote hawajui Ashura, mimi nimekupeleka kwenye ile familia kwa makusudi ili siri isitoke sitaki habari za Yule mtoto zisikike. Tena natamani ningekuwa na uwezo ningekimaliza kabisa”
“Mmh dada usifikie huko jamani”
“Sasa unadhani tutafanyaje? Nataka kuizima kabisa hii ishu maana hata ndugu wa Patrick wakijua wataleta varangati. Unafikiri mchezo, hata kumfanya huyu Ana ahisi ni mtoto wake”
“Kwakweli cha kufanya sijui”
“Halafu kwanini nakutafuta sikupati mpaka ukutane na wakina Sara”
“Hapana dada, unajua wakina Sara walianza kuhisi kitu ndiomana nikajiweka mbali kabisa ili wasifikirie chochote”
“Achana na wale watoto bhana, unajua Ashura nakutegemea sana. Huniangushagi wewe”
“Ila dada kuna jambo nataka nikwambie”
“Jambo lipi”
“Ni kuhusu huyu mdada wa kazi uliyemuweka sasa hivi”
“Eeh hebu nieleze”
“Yani huyu aliwahi kufanya kazi kwa Neema, kule ninakoishi mimi na watoto wa Neema akiwepo na Salome anawajua vilivyo”
“Mmmh inamaana anajua kila kitu?”
“Hamjui baba wa Salome ila nina mashaka nae sana, ngoja nimuone kama ananikumbuka vizuri”
Moza akasikia harufu kama mboga inaungua ikabidi akimbilie jikoni, na kweli alikuta mboga inaungua, hapo sasa wakati anahangaika iliafiche soo la kuunguza mboga akasikia Rose akiita kwa nguvu huku akitembea,
“Moza, weeee Moza wewe”
Moza aliitikia na kwenda,
“Ulikuwa unafanya nini hadi umeunguza mboga”
“Nisamehe mama”
Rose akacheka kisha akamwambia Moza,
“Dawa yako inachemka”
Halafu akatoka na Ashura wakaondoka. Hapo Moza alikuwa na maswali mengi sana, kuwa Ashura na Rose wako vipi vipi, na kwanini Ashura alikuwa akiishi kule ambako Moza alikuwa akifanya kazi mwanzoni na mbona anaishi nao kama ndugu kivipi?
“Mmmh kumbe Yule Salome ndio mtoto wa mzee Ptrick. Ila sasa naanza kupata picha, Yule Salome kweli amefanana na huyu mzee. Masikini mzee Patrick jamani, masikini na dada Neema nae jamani anaishi na nyoka ndani bila kujua dah”
Kisha Moza akarudi tena jikoni, ni kweli alikuwa ameunguza mboga sababu ya kufatilia umbea. Akaanza kufanya jitihada za kuiweka sawa, akaibadilisha kwenye sufuria linguine, muda kidogo Rose alirudi na kumuita sebleni, Moza alienda
“Hivi nilikwambiaje kuhusu habari za humu ndani?”
“Nisizifatilie”
“Haya, niambie sasa Ashura unamjua?”
Hili swali lilikuwa la mtego sana kwa Moza, akajikuta akiwa kimya tu kwani hakujipanga na hakutegemea kuulizwa swali la namna ile, Rose akamuuliza tena kwa kumshtua
“nijibu basi, unamfahamu vipi Ashura?”
Moza akatetemeka na kujibu,
“Simfahamu”
Rose akacheka kisha akamwambia
“Vizuri sana. Humfahamu eeh!”
“Ndio simfahamu”
“Na kipi kimekufanya uunguze mboga?”
“Nisamehe mama”
“Hivi unadhani msamaha wangu ndio unatoka kirahisi rahisi hivyo?”
“Nisamehe mama”
“Nadhani wewe hunijui vizuri, ila nataka unijue ili safari ijayo ujiheshimu. Msamaha wangu utaupata leo saa nane usiku”
Moza akashtuka na kuuliza kwa hamaki,
“Saa nane usiku!”
“Ndio saa nane usiku, mbona unashtuka? Huo si muda tu kama muda mwingine. Mbona kuunguza mboga hukufikiria kuiambia mboga ikusamehe isiungue? Leo saa nane usiku utaona msamaha wangu utakavyoupata. Haya kaendelee na kazi zako, na unikaangie ndizi. Hiyo mboga ya kuungua iweke pembeni halafu saa nane usiku nitakwambia inafanywa nini ila sitaki uwape wanangu mboga ya kuungua”
Moza aliondoka na kuendelea na shughuli zake huku akiulaumua umbea wake kwani ndio uliomponza hadi akaunguza mboga, na ndio uliomponza hadi anapewa msamaha saa nane usiku.
 
SEHEMU YA 10



Siku hiyo Ana nae aliwahi kurudi ila alionekana kuwa amechoka sana kwani alivyofika tu sebleni akalala. Ikabidi kama kawaida aende getini kuchukua begi la Ana kwa mlinzi. Alipoenda kuchukua, mlinzi alimuuliza,
“Na leo Ana anaonekana kuchoka sana, ameenda wapi saa hizi?”
“Amelala sebleni kwenye kochi”
“Sikia sasa, cha kukusaidia. Peleka begi lake, kisha urudi kumbeba na kumpeleka chumbani kwake akalale.”
Moza akamshukuru na akafanya vile, akambeba Ana na kwenda kumlaza ambapo kitandani akaamua amvue viatu kisha amwache amelala halafu yeye akatoka.
Kufika sebleni wale mapacha nao walikuwa wamerudi na walimwambia Moza awaandalie chakula ila muda huo huo mama yao nae alienda pale sebleni, akamzuia Moza kuandaa chakula kisha akatoa pesa na kuwapa watoto wake,
“Nendeni mkanunue na mkale mnachotaka”
Wale mapacha walifurahi sana na kutoka zao, Moza alimuuliza Yule mama
“Mbona umezuia nisiwaandalie chakula?”
“Moza, unataka nikutukane au? Hivi mboga yako iliyoungua hiyo uwaandalie wanangu wakiumwa matumbo je!”
Moza akawaza kuwa tatizo ni mboga kuungua au kuna lingine.
Sara nae aliporudi ikawa vilevile, mama yake alimpa pesa akatafute chakula, kwakweli Moza aliwaza sana siku ya leo kuwa tatizo bado ni kuunguza mboga au kuna linguine, muda huu akaamua kumuuliza tena huyu mama,
“Mama, tatizo ni kuunguza mboga au kuna linguine?”
“Lingine lipi?”
“Sijui”
“Lakini unataka kujua?”
“Ndio, ningependa kujua”
“Wewe si mbea, utajua tu”
Huyu mama aliinuka na kwenda chumbani, kwakweli Moza aliogopa ukizingatia ni kweli mboga iliungua sababu ya kufanya umbea. Moza alikuwa na mawazo sana, kitu kilichomfanya atoke na aende kwa mlinzi ili kujaribu kumdadisi kama kawaida yake,
“Kaka samahani, naomba unisaidie”
“Nini tena? Umefanya vituko vingine ndani?”
“Nimeunguza mboga bahati mbaya kaka, ila mama kawapa watoto wake wote hela wakale nje sababu nimeunguza mboga”
“Sasa wewe umekuuma nini kuwapa watoto wake hela wakale?”
“Kumbuka nimepika ila amewapa watoto wake hela wakale, kwahiyo kile chakula kitamwagwa?”
“Unajua katika wafanyakazi vimeo bosi aliowahi kuwaleta, basi wewe ni kimeo namba moja. Kwa kifupi, hii nyumba haiunguzwagi mboga, yani kama umeunguza mboga leo ujipange”
Moza alizidi kupatwa na uoga, mara akaitwa na mama mwenye nyumba alikuwa mlangoni, Moza akaenda kisha Yule mama akamuuliza
“Na leo ulikuwa unaulizia masoko?”
“Hapana”
“Ila ulikuwa unaulizia nini?”
Moza akawa kimya tu, na kumfanya Yule mama aongee tena
“Wewe Moza wewe yani nitakachokufanya leo hutakaa kusubiria umbea tena, akili itakukaa sawa. Nitakukomesha”
“Ila mama nimekuomba msamaha”
“Unadhani huo msamaha wako ndio umenunua mboga? Huo msamaha wako ndio hela? Nakwambia nitakukomesha”
“Mama nina ombi”
“Eeeh ombi gani?”
“Naomba kurudi kwetu”
Rose akacheka sana, na kumuangalia Moza kisha akamwambia
“Yani wewe hata mwezi huna kwenye nyumba hii unataka kurudi kwenu, tena baada ya kufanya makosa. Hivi unafikiri kuondoka hapa ni rahisi kiasi hicho? Mboga yangu uliyounguza una hela ya kunilipa? Nijibu sasa”
Kabla hajajibu alimsikia Ana akimuita kwa nguvu sana,
“Mozaaa”
Rose alimuangalia Moza na kumsonya kisha akamwambia
“Nenda huko, malkia anakuita”
Moza alienda huku akitetemeka maana aliitwa kwa nguvu sana.
Alipoingia chumbani kwa Ana alizabuliwa kofi kwanza, kisha Ana akamwambia kwa ukali
“Nani amekutuma univue viatu”
Kabla Moza hajajibu alishtukia akizabuliwa kofi lingine lililompeleka hadi chini, yani la sasa hivi alipigwa na mtu mzima kabisa sio kofi la kitoto kama la Ana.
 
SEHEMU YA 11



Moza alienda huku akitetemeka maana aliitwa kwa nguvu sana.
Alipoingia chumbani kwa Ana alizabuliwa kofi kwanza, kisha Ana akamwambia kwa ukali
“Nani amekutuma univue viatu”
Kabla Moza hajajibu alishtukia akizabuliwa kofi lingine lililompeleka hadi chini, yani la sasa hivi alipigwa na mtu mzima kabisa sio kofi la kitoto kama la Ana.
Moza aliugulia pale chini na kusikia sauti ya Rose sasa,
“Unamvuaje mwanangu viatu bila ruhusa yake?”
Rose akamwongezea Moza teke, kisha akamwambia atoke mule chumbani.
Moza alitoka na kwenda bafuni ambako alijikuta akilia sana huku akijiuliza,
“Kwani kosa langu ni nini jamani? Hivi kumvua mtu viatu ni vibaya?”
Akaitwa tena na mama mwenye nyumba, kwahiyo Moza akajifuta machozi yote na kwenda,
“Unafanya nini?”
“Sifanyi kitu mama”
“Unanificha eeh! Hujui kama nyumbani kwangu huruhusiwi kulia bafuni?”
“Nisamehe mama”
“Yani wewe ni hodari sana wa kuomba msamaha, sasa nataka ukae hapa sebleni hadi hiyo saa nane usiku ifike ikukutie hapa hapa. Umenielewa?”
“Ndio mama”
Moza alikaa pale sebleni huku akiwa na mawazo sana, kwakweli leo hakuwa na raha kabisa alijiona yupo ufungwani. Muda kidogo, Rose na mwanae Ana wakatoka, Moza akaelewa tu kuwa nao wanaenda kula. Alikaa pale sebleni amenyong’onyea kama kamwagiwa maji.

Kwenye mida ya saa tatu usiku wale mapacha walirudi na walimkuta Moza pale sebleni, walimsalimia tena na kutaka kuelekea chumbani ila mmoja akamuuliza moza
“Mbona unaonekana umenyong’onyea sana”
Moza akajibu bila hata kufikiria mara mbili,
“Nimeunguza mboga kwa bahati mbaya”
“Yani kuunguza mboga ndio unyong’onyee hivyo!”
“Mama kaniambia nikae hapa hadi atakaporudi kunipa adhabu”
Yule pacha mwingine akacheka na kusema,
“Yani mama yetu bhana, ana vijimambo vya ajabu ajabu. Sasa mtu kuunguza mboga ndio mpaka adhabu!”
Wakaondoka zao na kumuacha Moza pale sebleni, muda kidogo Sara nae alirudi na alimuuliza Moza swali lile lile aliloulizwa na wale mapacha nae akamjibu kama vile vile ila Sara alionyesha mshtuko kidogo,
“Mungu wangu, umeunguza mboga? Nyumba hii haiunguzwagi mboga”
“Ni bahati mbaya Sara”
“Pole sana”
“Asante”
“Unatia huruma sana”
Sara akawa anaelekea chumbani ila akaonekana anakumbuka kitu, kisha akamfata Moza na kumuuliza,
“Kwahiyo mama ndio kakwambia ukae hapo sebleni hadi atakaporudi?”
“Ndio kaniambia hivyo”
“Kakwambia adhabu yako anakupa saa ngapi?’
“Kasema saa nane usiku”
“Pole sana, nina uhakika mama na Ana watarudi hiyo saa nane muda wa adhabu ila kwa kukuokoa wewe na hiyo adhabu nenda chumbani kwako muda huu kalale yani hiyo saa nane ikukute umelala”
“Mmmh mama si atasema nimekiuka amri zake?”
“Moza, nimekusaidi tu ila usinitaje. Wewe nenda kalale, akikuuliza mwambie usingizi ulikushika kwa uoga. Mwambie kuwa wewe ukiogopa kitu unapatwa na usingizi”
Moza aliamua kumsikiliza Sara na kwenda chumbani kwake kulala ingawa ilimchukua muda sana kupatwa na usingizi.
 
SEHEMU YA 12


Moza alikuwa amelala lakini usingizi wake ulikuwa umejawa uoga wa hali ya juu huku akihisi kwamba hiyo saa nane atakuja kuamshwa na kufanyiwa hiyo adhabu ila alishangaa hiyo saa nane ilionekana kupita kwani alisikia kwa mbali majogoo yakiwika na kuhisi kuwa huenda ikiwa saa tisa na nusu au saa kumi alfajiri.
Usingizi ukampitia sasa, akajiona kwenye ndoto yupo kwenye kile chumba na wale wadada watano wakimshukuru sana kwa kuunguza mboga, mmoja akamwambia Moza
“Ila wewe una bahati sana, kwani wenzako unafikiri makosa yetu nini kuwa huku. Ni kuunguza mboga tu”
“Kuunguza mboga!”
“Ndio, tuliunguza mboga tukaletwa huku. Ila wewe una bahati sana. Yani unafanya makosa makubwa zaidi yetu ila bado upo. Sikia Moza kile chumba unacholalia kuna kitabu change kidogo sana, kapekue utakiona. Kina habari za bibi yangu atakupa mbinu za kutusaidia”
“Mbona huku unaongeaga wewe peke yako?”
“Wenzangu wote vinywa vyao vimefungwa, hwawawezi kuongea chochote. Kuhusu mimi ukisoma kile kidaftari change utaelewa. Kipo kwenye droo, kuna taiti nyeusi katikati kuna kitabu changu”
“Ila bado sijaelewa, yani kuunguza mboga ni furaha yenu ili mimi niletwe humu?”
“Furaha yetu ukiunguza mboga tunakuwa huru sana, ila siku ukifikia kuunguza na kuwa kama mkaa……”
Moza akashtuliwa na kelele za kuitwa, ambapo akashtuka kutoka kwenye ile ndoto, aliyekuwa anamuita ni Sara ambaye aliingia ndani na kumgusa Moza, kisha akamwambia
“Kheee bado umelala tu! Amka bhana utuandalie chai unajua muda umeenda sana”
Kisha Sara akatoka mule chumbani, Moza alikurupuka na kufungua dirisha ambapo aliona jua kali limeshawaka yani pameshakucha kabisa, alipotazama saa ilikuwa ni saa mbili asubuhi,
“Mungu wangu, yani nimelala hadi saa hizi! Sijamuamsha Ana aende shule, sijafanya usafi bado. Mungu wangu”
Alijitoa matongotongo kwa kidole kisha akatoka nje, ila sebule ilikuwa kimya sana ambapo alikuwepo Sara tu akichezea simu yake,
“Nisamehe madam Sara, nilipitiwa na usingizi”
“Nimekuelewa, niandalie chai tu halafu nikaangie na mayai”
“Wengine wameenda wapi?”
“Wote wameshaondoka”
“Ana nae?”
“Hebu acha kunichekesha na wewe, Ana awepo anafanya nini muda huu? Kashaenda shule”
Moza akaenda jikoni na kuanza kumtaarishia Sara kifungua kinywa ila kichwa chake hakikuwa sawa kabisa, alijikuta akijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu.
 
SEHEMU YA 13



Alipomaliza alimuandalia Sara mezani na kumkaribisha, ila aliona karatasi mezani na hela, akalifunua lile kafratasi limeandikwa ‘KANUNUE SAMAKI’ Sara aliposogea pale mezani akamuuliza,
“Eti huu ujumbe kaacha mama”
“Itakuwa ni yeye tu”
Moza akamuacha Sara pale anakunywa chai kisha yeye akaenda kujiandaa ili akanunue hao samaki.
Alikuwa akijiandaa huku akijiuliza maswali mengi sana ila bado hakupata majibu ya maswali yake yote, hakuna jibu alilolipata. Akawa amezubaa tu, ila akasikia sauti ya Sara ikimuaga
“Tafadhali Sara naomba unisubiri ili unionyeshe tu mabucha ya samaki”
“Fanya upesi, nina haraka zangu”
Moza akafanya haraka akatoka na Sara, ila walipokuwa njiani Moza alimuuliza Sara
“Kwani wewe unafanya kazi au unasoma?”
“Kwanini umeniuliza hivyo?”
“Kila siku unatoka”
“Mimi nafanya kazi ila nasimamia miradi ya mama”
“Na wale mapacha je!”
“Nao wanasimamia miradi ya mama sehemu nyingine, na leo wametoka na mama”
“Na baba je!”
“Sasa nimeelewa kwanini mama anataka kukuadhibu wewe”
“Kwanini?”
“Hivi hujioni kuwa ni mbea sana, yani unajifanya kama FBI.”
“FBI ndio nini?”
“Sitaki maswali bhana, mabucha ya samaki yale pale. Kwaheri”
Sara aliondoka na kumuacha Moza akielekea kwenye yale mabucha, ila moza tabia ya kuuliza maswali alikuwa nayo kwenye damu yani hata akijifanya siulizi tena anajikuta tu ameshauliza.
 
SEHEMU YA 14


Moza alienda kwenye bucha la samaki kununua samaki, wakati anaondoka akashikwa bega kutazama alikuwa ni Salome ambapo alimkumbatia kwa upendo,
“Kheee Salome umekuwa, umekuwa sana”
“Ndio dada, shikamoo”
“Marahaba, upo darasa la ngapi saivi?”
“Nipo kidato cha tatu”
“Kheee hongera sana. Mama hajambo!”
“Hajambo”
“Nimewakumbuka sana, na wale wadogo zako mapacha”
“Nao hawajambo”
“Twende ukapafahamu ninapofanyakazi siku hizi”
“Mmh dada, nitachelewa. Unajua tumehama pale tulipokuwa tunakaa”
“Hakuna shida, huchelewi wewe twende ukapaone basi”
Moza akaongozana na Salome hadi kwenye ile nyumba aliyokuwa anafanya kazi, na kumkaribisha Salome ndani. Kwakweli mlinzi alishikwa na bumbuwazi alipomuona Salome ila hakuweza kuuliza zaidi.
Waliingia ndani, kwakweli Salome alishangaa ukubwa wa nyumba ile,
“Kumbe ndiomana ulitukimbia dada, kumbe matajiri walishakuiba”
“Hapana sio hivyo mdogo wangu, kipindi kile nilirudi kweli kijijini kwetu. Bibi yangu alikuwa anaumwa sana na nimemuuguza kipindi chote hiki ila mwisho wa siku alikufa. Nilikaa kijijini nikaona sina ishu nikarudi mjini, nilikuja pale mlipokuwa mnakaa nikaambiwa mmehama ila ndio nikapata kazi hii, yani hata sina siku nyingi hapa”
“Pole dada”
“Asante, ila umlete na mama yako hapa aje kuniona na apafahamu”
Salome akamuaga Moza, na wakati anamsindikiza Mr.patrick nae akawa anaingia akawakuta ndio wanatoka wakamsalimia pale na kuondoka ila moyo wa Mr.Patrick ulihisi kitu, alijikuta akitamani sana kujua kuhusu huyo mtoto kwahiyo alikuwa anangoja Moza aingie ndani amuulize.
 
SEHEMU YA 15


Mlinzi nae, Moza alivyoagana tu na Salome kisha kurudi ndani akamuuliza,
“Yule mtoto ni nani?”
“Anaitwa salome Yule”
“Mbona kafanana sana na mzee Patrick!”
“Si ulisema wewe ni mtoto wa kiume, umbea hupendi. Kwaheri”
Moza alienda ndani na kumuacha mlinzi ameduwaa tu, ila alipoingia sebleni tu alibambana na swali kutoka kwa mzee Patrick,
“Yule mtoto ni nani?”
“Anaitwa Salome Yule”
“Ni mtoto wa nani na anaishi wapi?”
“Nilikuwa nafanya kazi kwao kabla ya hapa”
“Mbona swali na jibu haviendani? Nimekuuliza ni mtoto wa nani na anaishi wapi?”
Mara mlango ulifunguliwa na aliingia Rose, ambaye alionekana kumungalia kwa hasira sana mume wake, kisha akamuuliza bila hata ya salamu
“Kwanini jana hujarudi?”
“Sasa ningerudi vipi mke wangu na umeniambia mpaka unipigie simu”
“Sasa leo nimekupigia simu?”
“Nimehisi labda umejisahau mke wangu ndiomana leo nimeamua kurudi. Jana mbu wamening’ata sana usiku pale ofisini”
Rose akacheka sana, kisha akamuangalia Moza na kukunja sura, halafu akamwambia
“Na wewe unasikiliza nini? Yanakuhusu haya? Hivi kwanini wewe ni mbea mbea, hebu kwenda kwenye kazi zako huko”
Moza aliondoka pale sebleni na kuelekea jikoni, ila ingawa alikuwa jikoni ila masikio yote yalikuwa sbleni akisikiliza tu kinachozungumzw na Rose pamoja na Patrick.
Aliwasikia vilivyo mazungumzo yao kwani hayakuwa ya kunong’ona yani yalikuwa ya sauti kabisa,
“Sikia nikwambie Patrick, humu ndani kuna kidudumtu naa hicho kidududumtu lazima nikikomeshe”
“Ni nani huyo?”
“Si huyu mfanyakazi, yani ni mbea sijapata kuona. Ndio amefanya nisahau kukupigia simu jana, ni mbea ameshindikana, unaelewa maana ya umbea mume wangu. Huyu msichana ni mbea na lazima nimkomeshe”
“Sasa unataka kumfanya nini?”
“Utaona leo usiku yani akilala tu ninae”
“Mmmh mke wangu yani akilala ndio unamkomesha? Kwanini usimsamehe?”
“Nimsamehe! Thubutuuu, jana kaunguza mboga yangu sababu ya umbea wake. Yani leo akilala tu namkomesha”
“Sasa mbona unaongea kwa sauti, huoni kama anakusikia?”
“Hanisikii bhana, na leo nitamkomesha”
“Halafu kama maajabu hivi, kwanini unanieleza yote hayo leo?”
“Sababu nakupenda mume wangu, kila kitu ninachotaka kufanya lazima nikueleze”
“Mmmh!”
“Usigune mume wangu, yani huyu msichana leo akilala tu ninae. Anadhani nimesahau, twende chumbani mume wangu nikakukande kande kwa uchovu”
“Kila siku ingekuwa hivi sijui ningenenepaje”
“Unene mimi siupendi, twende bhana achana na mawazo hasi”
Rose na mume wake walielekea chumbani huku Moza akiwa amejawa na uoga na kujilaumu kuyasikiliza yale mazungumzo, yani anawaza kuwa bora asingesikia chochote.
“Mmmh mimi Moza leo silali yani silali kabisa”
Alikuwa na uoga wa hali ya juu.
 
SEHEMU YA 16



Ana alirudi, na leo ni tofauti na siku zingine kwani begi lake alilibeba mwenyewe na kwenda kuliweka chumbani kwake, hakumuongelesha Moza kabisa. Ila muda kidogo alienda chumbani kwa mama yake, ambapo Moza kama kawaida akanyata ili akasikilize kitu ambacho Ana aliongea na dada yake.
“Yani mama, huyu dada nikimuona nahisi kichefuchefu balaa kwa kitendo chake cha jana”
“Hata usijali mwanangu yani huyu akilala tu leo ninae, nimepanga kumkomesha”
“Mmh mama akilala? Sio akiwa macho?”
“Akilala mwanangu, yani leo akilala tu ninae. Nitamkomesha leo”
Kimya kikatawala na kumfanya Moza arudi jikoni huku amenyong’onyea maana leo aliona amepangiwa mapango kabambe. Huku akijisemea
“Ila umbea wangu umesaidia maana mipango yote aliyonipangia huyu mama nimeijua”
Kulwa, Dotto na Sara walirudi kwa kuongozana, mama yao alitoka sebleni na kumtaka Moza aandae chakula.
Moza aliandaa kisha Yule mama aliita watoto wake wote na mume wake, yani leo familia nzima ilikuwa mezani wakila kasoro Moza aliambiwa akale jikoni.
Wakati wanakula pacha mmoja akamwambia mama yake,
“Mama ingekuwa hivi kila siku basi familia yetu ingekuwa ni kati ya familia znye furaha sana”
“Hata hivyo tunafuraha, kwani hakuna mwenye furaha hapa? Mimi nafurahi sana kuwaona watoto wangu na mume wangu tukiwa pamoja tunakula”
Sara akadakia na kusema,
“Ila mama mmh leo sio bure, haijawahi kutokea kama hivi kwakweli. Sio bure kabisa mama”
“Sasa sio bure ndio nini?”
“Nahisi kuna kitu unataka kufanya”
“Cha kufanya kipo ndio, kuna mjinga mmoja lazima nimkomeshe leo”
“Nani huyo mama?”
“Nyie kuleni tu wanangu, hata hamuhusiki”
Moza bado tumbo joto hata hamu ya chakula hakuwa nayo kwani alijua hata akisinzia siku hiyo basi lazima atakomeshwa na huyu mama, na kinachomuumiza kichwa zaidi ni kuwa hajui atakomeshwaje komeshwaje.
Moza akachemsha maji na kutia kahawa sababu alishawahi kusikia kuwa maji ya kahawa yanakata usingizi, alikunywa vikombe vinne ila bado alikuwa akihofia kuwa akisinzia itakuwaje.

Muda wa kulala ulipofika, kila mtu alienda chumbani kwake hata Moza pia alienda chumbani kwake ila alikuwa na mawazo sana na alikuwa akiwaza ni jinsi gani anaweza kukaa macho kwa usiku wote hadi asubuhi, Ilipofika saa sita usiku akapata wazo la kwenda kukaa sebleni maana aliamini kama angekaa sebleni basi asingepata usingizi na mfano ungemnyemelea basi angeenda kunywa kahawa tena.
Wakati anataka kutoka akasikia sauti,
“Moza lala”
Akashtuka sana na kugeuka ili aone sauti inatokea wapi, ila hakumuona mtu yoyote akataka akafungue malango tena, kasikia
“Moza lala”
Safari hii ile sauti ilimwambia kwa ukali kidogo.
 
SEHEMU YA 17





Wakati anataka kutoka akasikia sauti,
“Moza lala”
Akashtuka sana na kugeuka ili aone sauti inatokea wapi, ila hakumuona mtu yoyote akataka akafungue malango tena, kasikia
“Moza lala”
Safari hii ile sauti ilimwambia kwa ukali kidogo. Moza alizidi kupatwa na uoga hadi akawaza kutoroka kwenye ile nyumba ila atatorokaje usiku huo na kuna mlinzi getini, yani akawa na mawazo mbali mbali mpaka akajihisi kuchanganyikiwa. Ila bado alikuwa na wazo la kwenda sebleni kukaa lakini sauti ile ilizidi kumwambia moza alale, alipoona ile sauti inazidi maana ilianza kuongea kama mwangwi,
“Moza lala, Moza lala, Moza lala”
Uoga ulimjaa Moza hadi akataka kutoka kwa nguvu ila alipofungua mlango ulikuwa mgumu na ile sauti ilizidi kumsihi alale, Moza alitetemeka zaidi akataka kupiga kelele ili afunguliwe mlango ila moyo mwingine ukamwambia ukipiga kelele ndio utamshtua mwenye nyumba kuja kukuadhibu, akaamua kwenda kukaa kitandani huku akiombea asilale ila sauti ya kumsihi kulala ilizidi na kumtia hofu zaidi. Alipotaka kuinuka tena muda huu alishtukia akipigwa kibao kilichomuangusha hadi chini halafu taa ya chumbani ilizimwa yani hapo ndio uoga zaidi ukamshika na kujikuta akishindwa kuinuka pale chini ila cha kumshangaza wakati anaogopa sana, usingizi ukampata pale pale.

Wakati amelala akajiona yupo mahali chini ya mti halafu kaja Yule dada anayeongeaga kati ya wale wadada watano, akaanza kuongea nae ila leo Moza hakuweza kujibu wala kuuliza swali.
“Moza, ni mbishi sana wewe ndiomana nimekufanyia hivi. Yani hujui kutofautisha kati ya mtego na kitu cha kweli. Yule mama angetaka ulale ili akufanyie mambo mabaya unafikiri angeongea kwa sauti kubwa vile? Kaongea kwa sauti kubwa sababu amejua wewe ni mbea na utasikiliza tu kwahiyo alikuwekea mtego, na usingelala ndio angejua kama ni mbea kweli maana kwanini unasikiliza maongezi yao? Halafu kwa sheria za huyu mama amfanyiagi kitu mbaya mtu akiwa amelala, ndiomana hata jana hakukufanya lolote sababu ulilala ila ungekuwa macho ungepatwa na makubwa. Usifikirie siku zote nitaweza kukusaidia, nimeweza leo sababu ile juzi uliunguza mboga kwahiyo nimepata nguvu. Jifunze kuelewa mitego Moza, tutakupoteza na wewe. Usifikirie ni rahisi hivyo kutoroka kwenye hii nyumba. Kitabu nilichokwambia kipekue kesho uanze kukisoma ndio kitakusaidia sana kwenye mambo yote ya kufanya. Halafu unatakiwa kuwa makini sana kwenye kila kitu unachofanya, yani fikiria kabla ya kutenda jambo lolote. Kwasasa lala tu”
Huyu mdada aliondoka, ila ni usingizi mzito sana ulimshika Moza wakati huo.
Kuja kushtuka ilikuwa ni kumeshakucha, akaamka pale chini na kujishangaa shangaa kuwa imekuwaje mpaka akalala hapo chini, akaanza kukumbuka matukio na kukumbuka kuwa mara ya mwisho alinaswa kibao na kuanguka hapo chini kisha kukawa na giza kubwa lililompa uoga na kupitiwa na usingizi kwa uoga, pia akakumbuka alivyoota. Akainuka pale chini haraka haraka baada ya kukumbuka kuwa alitakiwa kuadhibiwa, akatoka sebleni ila nyumba ilikuwa kimya kabisa yani ilionyesha hapakuwa na mtu yeyote mule ndani.
Akasogea mezani ambapo alikuta ujumbe, ‘UPIKE WALI, MAHARAGE NA SAMAKI’ akaelewa kuwa ujumbe huo umeachwa na mama mwenye nyumba, hivyo akahisi kuwa huenda nyumba nzima wameondoka na hivyo kwenda kuoga na kuanza kufanya kazi za hapa na pale mule ndani hadi alipoanza kupika kile chakula alichoagizwa.
Alipomaliza kupika alikiandaa kabisa mezani ila alikuta ujumbe mwingine ‘TENGENEZA NA JUISI YA MATUNDA YAPO KWENYE FRIJI’ akaangalia kulia na kushoto, mbele na nyuma na kujiuliza,
“Mbona ujumbe huu sikuukuta mwanzoni? Humu ndani si nimebaki mwenyewe? Au sikuangalia vizuri!”
Akajiuliza bila ya jibu kama kawaida kisha akaanza kuiandaa hiyo juisi na kuiweka kwenye friji, ila aliporudi mezani alikuta ujumbe mwingine ‘CHEMSHA MAJI YA KUOGA YA ANA UMUWEKEE KWENYE CHUPA’ hapo uoga ukamshika na kuanza kuhisi tofauti, kisha akajiuliza,
“Mbona huyo Ana hajawahi kusema nimchemshie maji ya kuoga? Huu ujumbe ananiwekea nani? Siwezi kwakweli, naogopa. Inamaana sikuuona pia?”
Alikuwa na mashaka sana ila akaenda kuchemsha hayo maji na kuyaweka kwenye chupa, alipomaliza alirudi tena mezani na kukuta ujumbe mwingine ‘DEKI TENA NYUMBA’
Aliogopa sana sasa hivi na kuamua kukimbilia nje hadi kwa mlinzi huku akihema juu juu, Yule mlinzi alimuuliza,
“Humo ndani sielewi”
“Huelewi nini?”
“Nimebaki peke yangu ila nakutana na ujumbe mezani, kila nikifanya nakuta ujumbe mwingine. Naogopa kwakweli”
Yule mlinzi alianza kucheka sana kisha akamuuliza,
“Kwahiyo wewe unahisi ni nini?”
“Nahisi labda ni jinni”
“Usinichekeshe wewe, hivi jini unalijua wewe? Ushawahi kuona jini?”
“Sijawahi”
“Sasa unaogopa nini?”
“Naona mambo ya ajabu, ukizingatia ndani nipo mwenyewe”
“Upo mwenyewe wapi wewe, fanya tu ujinga wako uone. Mama yupo ndani leo hajatoka”
Moza akapumua kidogo na kujiona kama mjinga, kwani alihisi mitego ya Yule mama iliendelea kwahiyo ikabidi ajipange na majibu kama mwenye nyumba akimuuliza.
 
SEHEMU YA 18


Moza alirudi ndani sasa na kuanza kudeki, na alipomaliza Rose alitoka ndani na kwenda sebleni ila Moza hakuonyesha kushtushwa sababu ameshaambiwa na mlinzi kuwa Rose yupo ndani, huyu mama alimuangalia Moza na kumuuliza
“Mbona hujashtuka?”
“Nishtuke nini sasa mama?”
“Ushtuke kuniona”
“Sijashtuka sababu nilijua tu kuwa upo ndani”
“Umejuaje”
“Nilipoona ujumbe mara ya kwanza, na nilipoona mara ya pili nikajua tu kuwa upo ndani”
Rose akacheka kisha akamwambia Moza,
“Unajifanya mjanja eeh wakati ushafanya umbea kwanza, nilitaka leo kukufundisha kazi za kufanya maana ni uhakika hujui kazi za kufanya ndiomana unapata na muda wa kufanya umbea. Laiti kama ungekuwa na kazi za kufanya basi umbea usingefanya. Haya nenda kamwagilizie maua maji, na nikitoka nikute yamelowana haswaaa”
Moza alitoka nje na kwenda kufunga mpira na kuanza kumwagilia maua, wakati anamwagilia kuna sauti ikamtuma kupekua ua moja wapo, akahisi kama kuchimba mzizi wa lile ua. Ikabidi amwagilie kwanza ili pakilowana achimbe mzizi huo aone ni nini na kwanini hisia zake zinamtuma afanye hivyo.
Palivyolowana, akaitwa na Rose kwani Ana alikuwa tayari amesharudi. Moza alivyofika pale, akashangaa kumuona Ana akiwa amebeba mwenyewe begi lake halafu Yule mama alimwambia kwa ukali,
“Hivi Moza huoni mtoto anahangaika na begi, si umpokee”
Moza akataka kumpokea lile begi Ana, ila Ana akawa mkali sana na kumkatalia kisha akamwambia mama yake
“Hili lidada limbea sana, lisije likafungua begi langu bure. Siwezi kumruhusu tena abebe begi langu”
Ana akaondoka zake, Rose akamuangalia Moza na kumfokea pale,
“Unaona sasa faida ya umbea wako, hadi mwanangu hakutaki yani wewe sijui kama mwezi huu utamaliza humu ndani. Umbea wako utakuwa umekuponza, haya kaendelee na umwagiliaji huko, sasa ole wako nisikie unafanya umbea hadi kwenye maua yangu”
Moza akataka kutoka, wale mapacha nao walirudi na walikuwa wakilalamika njaa sana,
“Ila chakula nimeshaandaa mezani”
“Hivi wewe Moza si nishakwambia kaendelee na umwagiliaji, mtu gani wewe hujielewi. Kwani hawa wakilalamika njaa ni wanakulalamikia wewe? Wewe ndio unaetafuta chakula humu ndani au? Hebu nenda zako huko”
Moza akondoka kwa aibu maana hakutegemea kama muda huu huyu mama angesema hivi.
 
SEHEMU YA 19

Alienda tena kwenye ile bustani ya maua na kuendelea kumwagilia,ila bado mawazo yake yalimtuma kwenye lile ua ili afukue mzizi ajue kuna nini ila akakumbuka ile sauti ya mwenye nyumba kuwa ole wako nisikie unafanya umbea kwenye maua yangu,ile kauli ikawa inamrudia ila akajisemea.
“Kwani mimi natafuta umbea au nataka kuangalia mizizi ya lile ua? Kwani kuangalia mizizi ni umbea nao? Hapana bhana si umbea, nataka tu kuridhisha roho yangu maana inanituma niangalie mizizi ya ua lile, mbona haujanionyesha ua lingine zaidi ya lile! Huu si umbea bhana”
Yani alikuwa anajihoji mwenyewe na kujijibu mwenyewe basi aliacha kumwagilia na kwenda kufukua, alipokuwa anafukua hakuona mizizi kama alivyodhani ila alichokiona alistaajabu sana kwani alikuta mfuko na kitu kimefungwa kama mpira akataka kukifungua ila akajua akifungua hapo atabambwa kwahiyo akakificha kwenye nguo zake ili akakifungue ndani akiingia chumbani kwake kulala.
Tangu amkificha kile kimfuko nguvu ya kumwagilia ilimuisha kabisa na akajisikia hamu ya kuangalia kuna nini ila akajikaza kuwa ataenda kuangalia ndani. Roho yake ikamtuma kuwa akipeleke chumbani kwake kabisa, basi akaacha tena kumwagilia na kuanza kutembea ili apelike ule mfuko ndani ila kadri alivyokuwa anatembea nguvu zilikuwa zinamuisha, yani mpaka anaingia chumbani kwake alianguka kabisa ndipo alipotoa ule mfuko haraka haraka, ila alipoutoa tu na kuutupia pembeni nguvu zake zilirejea tena na kumfanya awe na mashaka zaidi kuhusu ule mfuko,
“Kilichomo humu kwenye mfuko si kimpira kama ninavyodhani ila nadhani kuna kitu kingine haiwezekani nguvu ziniishe kiasi hiki, lazima niangalie kuwa ni nini”
Ila muda huo akaitwa na Sara na kumfanya ainuke na kwenda alipo Sara ambapo alienda moja kwa moja chumbani kwa Sara, alifikiwa na swali,
“Jana ulikuja na nani hapa nyumbani?”
“Jana?”
“Ndio jana, usijipumbaze”
“Aaah nilikuja na mtoto mmoja hivi anaitwa Salome”
“Ni nani huyo mtoto?”
“Kwani wewe kakwambia nani kama nilikuja nae?”
“Moza, unafikiri umbea unauweza peke yako tu? Usitake kujua kaniambia nani, ila nijibu huyo mtoto ni nani na anamahusiano gani na familia yetu?”
“Ila kwanini umeniuliza hivyo Sara?”
“Moza, usiniulize maswali ila nijibu nilichokuuliza”
“Kwakweli sijui nikujibu vipi hilo swali lako, ila Yule mtoto ni wa bosi wangu wa zamani yani mwanzoni nilikuwa nafanya kazi kwao. Nimekutana nae buchani sasa nikamlete ili apafahamu ninapoishi kwasasa”
“Mama anajua kama uliwahi kufanya kazi kwa mama wa huyo mtoto?”
“Hajui, kwani kuna uhusiano gani kati yenu na huyo mtoto?”
“Sitaki maswali Moza, ila hili swala lazima mama nimfikishie maana umemleta mtu bila ruhusa ya mama. Vipi baba alimuona?”
“Alimuona ndio wakati namsindikiza”
“Yani wewe Moza wewe unatafuta mabalaa ambayo huwezi kuyatatua. Sikia nikwambie ujue kama ulikuwa hujui, Yule mtoto aliwahi kusingiziwa baba kuwa mtoto wake yani ilitokea mtafaruku mkubwa sana hapa nyumbani. Kipindi hicho hadi mama akaanza kutafuta mtoto kwa haja zote ndio baada ya miaka kadhaa akampata Ana. Sasa mama ana hasira sana na familia ya Yule mtoto halafu wewe unaenda kumchukua na kumleta nyumbani”
“Lakini mimi nilikuwa siyajui yote hayo, na kama ndio hivyo mbona Salome hakuonyesha kama anapafahamu hapa?”
“Sikia Moza, kwanza Yule haitwi Salome nadhani hilo jina wamempa ukubwani. Alikuwa anaitwa Maria, mamake anapajua hapa vilivyo na hawezi kusogelea hapa. Yule mtoto hapajui hapa, usijaribu tena kumleta Yule mtoto kwenye nyumba hii”
“Lakini ningependa unieleweshe zaidi, mbona kafanana sana na baba”
“Moza Moza, naenda kukusemea kwa mama maana naona unazidi kuchokonoa mambo”
“Tafadhali, naomba unisamehe”
“Unamuogopa eeh”
“Ndio namuogopa”
“haya, kaendelee na shughuli zako”
Moza alitoka mule chumbani kwa Sara na kwenda jikoni kuosha vyombo ambavyo tayari walikuwa wamelia chakula, hapo akawaza tena kuhusu Salome kuwa Yule baba inasemekana kasingiziwa lakini inaonyesha wazi Salome ni mtoto wa Patrick, ila kwanini Patrick mwenyewe anauwalakini kuhusu mtoto wake huyo na kwanini Salome alibadilishwa jina kama ni kweli alibadilishwa jina, alitamani kujua kwa undani zaidi ambapo alijua wa kumjibu mwingine ni mama yake Salome ambaye ni Neema.
Alitamani apate muda wa kwenda kuzungumza na Neema ili ajue kwa undani zaidi,
“Lakini umbea huu loh hata kuacha sitamani, najikuta tu natamani kujua sijui nifanyeje masikini Moza mimi”
Kumbe maneno hayo aliongea kwa sauti ya kusikika, akasikia sauti ikimwambia, ilikuwa ni sauti ya Rose,
“Haya ni nini unachotamani kujua?”
Moza akashtuka na kumjibu kwa uoga uoga,
“Hakuna kitu mama”
“Usinichekeshe Moza, wakati nimekusikia kila kitu. Niambie unachotamani kukijua ili nikusaidie ukijue”
“Hakuna kitu mama”
“Hakuna kitu eeeh!”
“Ndio mama hakuna kitu”
“Mimi nakiona kipo”
Rose alimshika mkono Moza na kuanza kumkokota, kwakweli Moza alishikwa na uoga kwani moja kwa moja Rose alimpeleka Moza kwenye kile chumba chenye chumba kidogo ndani kisha akamwambia,
“Unataka kujua kilichopo mule eeeh!”
Moza alikuwa kimya tu,
“Najua unajiuliza kuwa ukubali au ukatae, huku moyo wako mwingine ukitamani kujua siri iliyomo kwenye chumba kile. Haya chukua funguo hapo juu”
Rose alimwambia Moza kwa kumkaripia ambapo Moza alichukua funguo huku akitetemeka,
“Haya fungua sasa”
Moza alianza kufungua huku akitetemeka kwani alihisi kama hapelekwi nay eye kwenye chumba hiko basi ataona vitu vya ajabu, ila leo tofauti na siku ile aliyotaka kuchungulia kwani alipigwa na shoti ila leo hakupigwa na cheche yoyote. Na alipofungua tu alijiona yupo nje,
“Umeona sasa, huu ni mlango wa kutoka nje. Sasa wewe ulikuwa unafikiria ni nini?”
“Hapana mama, sijafikiria chochote”
“Haya tuzunguke tukaingie ndani”
Wakazunguka na kuingia ndani tena, kisha Rose akamuuliza moza,
“Sasa una amani eeh”
Moza aliitikia kwa kichwa tu kuwa ameridhika, Rose alicheka na kumuacha moza anaenda jikoni ambapo alienda kumalizia vile vyombo vyake ila alikuwa na mawazo mengi sana.
 
SEHEMU YA 20




Moza aliingia chumbani kwake ila bado alikuwa na maswali mengi sana, kwanza kabisa alijiuliza kuhusu chumba alichopelekwa ambacho mlango wa ndani ulimtoa nje,
“Mmmh huyu mama hajanifanyia mtego kweli, mbona kama chumba sio kile? Nahisi kanifanyia mchezo Yule mama lakini kwanini anifanyie mchezo wakati mimi si chochote wala lolote kwenye hii familia”
Wazo lingine likamjia ni kuhusu Ana maana siku hizi Ana hakutaka kitu chochote afanyiwe na Moza jambo ambalo lilimchanganya pia. Wakati anawaza hayo, mlango wake uligongwa alipoenda kufungua alimkuta mama mwenye nyumba ambaye alimwambia
“Dawa yako inachemka”
Huyu mama akaondoka, Moza akatoka na kwenda jikoni huku akiangalia hiyo dawa aliyoambiwa inachemka iko wapi maana hakubandika dawa yoyote kwahiyo ule usemi wa dawa yako inachemka kwa muda huo hakuelewa alijua ni dawa kweli.
Moza alivyoona hakuna dawa inayochemka alirudi tena chumbani,muda huu akili ikamtuma achunguze ule mfuko alioutoa kwenye maua. Akuchukua ule mfuko na kuanza kuuchunguza kwa kuufunua ambapo kweli alikuta kama mpira wa makaratasi umefungwa fungwa. Moza akaanza kufungua ila kadri alivyofungua ndivyo nguvu zilivyomuisha, hadi mwishoni akaanguka kabisa na kuwa kimya hapo hapo.


Moza alivyoona hakuna dawa inayochemka alirudi tena chumbani,muda huu akili ikamtuma achunguze ule mfuko alioutoa kwenye maua. Akachukua ule mfuko na kuanza kuuchunguza kwa kuufunua ambapo kweli alikuta kama mpira wa makaratasi umefungwa fungwa. Moza akaanza kufungua ila kadri alivyofungua ndivyo nguvu zilivyomuisha, hadi mwishoni akaanguka kabisa na kuwa kimya hapo hapo.
Kimya kilitanda sana chumbani kwa Moza hadi kesho yake asubuhi kila mtu aliamka kwenye ile nyumba na kufanya shughuli zao za hapa na pale kasoro Moza, ila Rose alijua Moza amepitiwa kama kawaida yake ila aliona kengele ya hatari ikilia kwenye kichwa chake lakini alipuuzia na kuondoka kama kawaida yake kisha akaacha ujumbe mezani ila bado nyumba ilitawaliwa na ukimya.
Rose ile asubuhi alimpeleka mwanae shuleni kisha na kupanga kupitia kwenye shughuli zake,
“Hivi kwanini siku hizi Ana hutaki kabisa kupelekwa shule na Moza?”
“Mama, kiukweli ni kuwa Yule dada simpendi kabisa yani simpendi mfukuze bhana mama”
“Namtafutia kosa la kumfukuza ila sikutaka kumfukuza kwanza mpaka nitakapomfunza adabu, unajua Yule msichana amezidi sana”
“kwahiyo mama umepanga tufanyaje nae? Maana unamchekea tu Yule, jitu linachunguza kila kitu mara kutandika kitanda hadi atake kufunua godoro langu, mara anivue viatu bila ruhusa yangu. Na siku ile aliyonivua viatu kanimaliza nguvu kabisa mama”
“Sawa mwanangu naelewa, ila ukitoka shule nisubirie hapo hapo shuleni twende mahali kwanza, tukitoka hapo twende nyumbani na Yule Moza atakoma. Yani Yule simfukuzi ila atajitegesha mwenyewe”
Rose alimfikisha mwanae shule na kumuacha hapo, kisha yeye akaenda kwenye shughuli zake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom