Simulizi: Kitanda cha sokwe mtu

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
16,420
30,776
0


Ni simulizi la ukweli linalo husu maisha ya kijana Lugwisha , kutoka kitongoji cha Goweko, wilayani Uyui mkoani Tabora.


Kijana Lugwisha, baada ya kumaliza shule ya msingi mnamo mwaka 1994 huko kijijini kwao, alifunga safari hadi jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya kutafuta maisha.


Miaka kumi baadae , kijana Lugwisha akawa amepata mafanikio makubwa yaliyo badilisha maisha yake.



Mafanikio katika maisha ya Lugwisha yanasababisha kuinuka kwa maadui ambao hawapendezwi na kufanikiwa kwake.


Maadui hawa wanapanga njama mbalimbali za kupambana dhidi ya mafanikio ya Lugwisha.


Kati ya maadui wa Lugwisha, ni maadui wawili tu ndio wanaonekana kuwa na nia thabiti nay a dhati katika mapambano dhidi ya Lugwisha.


Maadui hao ni Beka Msangi pamoja na Bundala.


Beka Msangi alikuwa mmiliki wa bar iliyo kuwa jirani na bar iliyo milikiwa na Lugwisha.


Bar hii ya Lugwisha ilikuwa ni moja kati ya makumi ya vitega uchumi vyake vilivyo muingizia fedha nyingi.


Bar ya Lugwisha ilikuwa maarufu sana jijini Dar Es Salaam na ilikuwa ikifurika wateja kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.


Bar hii ya Lugwisha ilikuwa katika eneo lenye bar nyingi. Uwepo wa bar ya Lugwisha katika eneo hilo uliua biashara ya karibu bar zote zilizo kuwepo katika eneo ikiwemo bar ya Beka Msangi.


Beka Msangi hakutaka kukubaliana na hali hiyo na hivyo kufikia uamuzi wa kusafiri hadi katika kijiji cha Mchukwi wilayani Rufiji mkoani Pwani, kwa ajili ya kumroga Lugwisha.


Baada ya kupiga ramli, wachawi wa Rufiji wanaona njia pekee ya kupambana na Lugwisha ni kumuhamisha kichawi yeye na bar yake kwa kutumia uchawi wa kizigua, ujulikanao kama “Sunkwa”.


Lengo la skadi hili la kichawi lilikuwa kumfanya Lugwisha, yeye mwenyewe kwa hiari yake afunge bar yake katika eneo hilo na kuhamia katika eneo jingine na wala asipate kabisa wazo la kurudi tena kufanya biashara katika eneo hilo, hali ambayo ingemfanya Beka Msangi aweze kufanya biashara yake ya Bar bila ya kupata upinzani wowote mkubwa.


Ama kwa upande wa Bundala, huyu ni mdogo wa damu wa Lugwisha. Lugwisha na Bundala wamezaliwa kwa baba mmoja lakini mama tofauti.



Baada ya kujaribu kuomba misaada ya mara kwa mara kwa Lugwisha bila mafanikio yoyote, Bundala , mama yake ( ambae ni mama wa kambo wa Lugwisha ) pamoja na dada yake aitwae Kalunde ambae alikuwa Mwalimu wa shule moja ya msingi huko mkoani Kigoma, walijiridhisha pasi na shaka yoyote kwamba, Lugwisha anawadharua sana kwa sababu Mwenyezi Mungu amemjalia fedha na mali na kwamba, anawabagua wao kwa sababu ni watoto wa mama wa kambo.


Hivyo basi Bundala, Kalunde pamoja na mama yao alieitwa Bi. Mkamiti wakaamua kusafiri hadi wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa ajili ya kwenda kumroga Lugwisha ili afilisike kabisa, awe kama wao au awe chini yao.


------------------------------------------------------------------



JE BEKA MSANGI ATAFANIKIWA KUMUHAMISHA LUGWISHA KWA KUTUMIA UCHAWI ? JE BUNDALA, KALUNDE NA BI MKAMITI WATAFANIKIWA KUMFILISI LUGWISHA KWA KUTUMIA UCHAWI KUTOKA KIGOMA ?


Jiandae kusoma kitabu “ KITANDA CHA SOKWE MTU “ upate kujua ukweli kuhusu kisa hiki cha ukweli. Kitabu hicho kitatoka hivi karibuni na utakipata kwa gharama ya SHILINGI ELFU KUMI TU ZA KITANZANIA .


Katika kitabu hicho utapata kufahamu mambo mbalimbali kama vile ;


A. Jinsi wachawi wanavyo tengeneza uchawi wa kumuhamisha na kumfukuza mtu kwa kutumia uchawi, kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na kumfanya mtu huyu asirudi tena katika eneo hilo hadi anaingia kaburini, pamoja na jinsi ya kujiepusha dhidi ya uchawi huo.



B. Utapata kufahamu jinsi wachawi wanavyo tengeneza uchawi wa kumfilisi mtu fedha na mali zake zote kwa kutumia uchawi pamoja na jinsi ya kujikinga dhidi ya uchawi wa namna hiyo hali kadhalika jinsi ya kumzindua mtu aliye tupiwa uchawi wa aina hiyo.


Vile vile katika kitabu hiki utapata kujua matumizi ya kichawi na kiganga kuhusu vitu na mambo mbali mbali kama vile :

1. Miti ya kwenye kitanda cha sokwe mtu


2. Mizizi iliyo kutwa kaburini wakati kaburi linachimbwa


3. Majani yaliyo peperushwa na kimbunga kikali ambayo yamedakwa bila kufika chini ya ardhi


4. Dawa chafu ya kiarabu ambayo inafanana na lami : Dawa hii ya kiarabu ni miongoni mwa madawa machafu kabisa yatumikayo kwa ajili ya mambo ya shari za aina mbalimbali. Utafahamu pia jinsi ya kujikinga na heri za dawa hiyo.


5. Mzizi ya mti uitwao Mbono Kaburi


6. Mizizi ya mti uitwao Mtopetope


7. Mizizi ya mti uitwao Mshindwi


8. Marashi ya waridi


8. Sindano


9. Nyembe zilizo katwa na kwanini huwa zinakatwa


10. Makaburi ya zamani yaliyo kwisha kusahaulika


11. Jogoo mweusi au jogoo mwekundu aliye wekwa porini kwa muda wa siku saba.


12. Chungu cheusi kilicho kesha kaburini kwa muda wa siku saba


13. Kaniki nyeusi pamoja na kamba za kaniki nyeusi


14. Ngorani yangu : Utapata kujua neno la lugha ya kiha “ NGORANI” lina maanisha kitu gani katika ulimwengu wa waganga na wachawi na linatumikaje, wakati gani, kwa sababu, gani, namna gani nakadhalika.


15. Mwiko uliotumika kupika kwenye msiba mkubwa


16. Mzizi wa mti ulio katisha njia : Kwa ufupi tu hiki ni kizimba kikubwa sana chenye matumizi mengi sana katika ulimwengu wa kiganga. Ni kizima kinacho tumika kufungua vifungo vingi sana vya kichawi. Kila mtu anapaswa kufahamu kuhusu kizimba hiki.


17. Maji ya mchele yaliyo kesha


18. Maji ya zamzam


19. Mizizi ya mti wa mkurungu


20. Jogoo aliye wika alfajiri mara moja tu na kuchinjwa hapo hapo, huku damu yake ikiwekwa kwenye chungu cheusi


21. Mizizi ya mti uitwao Mkubashengelo


22. Mizizi ya mti uitwao Mzungupori


23. Maseko : Hii ni dawa ipatikanayo kwa kuchanganya dawa saba za porini ambazo, kati ya dawa hizo ni pamoja na magamba ya mti wa ukwaju pori, pamoja na mafuta ya mnyama fulani afugwae


24. Mkuki mdogo wa asili


25. Sarafu ya fedha


26. Asali mbichi ya nyuki wadogo


27. Panya mdogo aitwae Msuswe


28. Mafuta ya simba


29. Mafuta ya nyuki wa Nimba : Nimba ni mnyama wa porini ambae anafanana na nyumbu. Mnyama huyu huwa anatembea na mzinga wa nyuki kichwani kwake. Yupo katika kundi la wanyama washirikina. Hapatikani wala kuonekana kwa urahisi na huwa anapotea kimiujiza.


30. Nywele za saluni


31. Punda, kondoo, au mbwa aliye pita duniani bila kuonekana


PAMOJA NA MAMBO MENGINE MENGI.


KITABU HIKI KITAFUNGUA UFAHAMU WAKO KUHUSU MAMBO MENGI KATIKA ULIMWENGU USIO ONEKANA.


SABABU YA KUTOA KITABU : Wafuatiliaji wa makala zangu wamekuwa wakilalamika, ninachelewa sana kutoa matoleo yanayo fuata ya makala mbalimbali zilizo andikwa au kusimuliwa nami. Hii imekuwa ikisababishwa na kutingwa na shughuli nyingi na hivyo kukosa muda wa kutosha wa kuandika makala. Watakao pata bahati ya kusoma kitabu hiki, watapata fursa ya kukisoma kuanzia mwanzo hadi mwisho wake.



WEKA ODA YAKO MAPEMA : Weka oda yako mapema . Utaratibu wa kuweka oda ni kama ifuatavyo : ANDIKA UJUMBE MFUPI WA MANENO KUPITIA SIMU YANGU YA MKONONI


0744 000 473 UKISEMA “ KITANDA CHA SOKWE MTU”. Nami nitahifadhi namba zako, na kitabu kitakapo toka jikoni basi utakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupata nakala yako.


Au unaweza kuandika ujumbe mfupi wa maneno ukiambatanisha na namba zako simu kupitia barua pepe yengu :mungwakabili@gmail.com.



Kwa maelezo zaidi kuhusu kitabu hiki na mambo mengine kuhusu ulimwengu usio onekana. Nitembelea : www.mungwakabili.blogspot.com


source : mpekuzi blog
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom