Simulizi: Harakati za maisha

Jack Daniel

JF-Expert Member
Sep 23, 2021
2,149
10,390
Napenda sana kusoma vitabu, hali hii imenifanya nipende kuandika visa kadhaa ambavyo huwa ni vya kweli, Sina visa vya kutunga.simulizi zote zina ukweli kwa asilimia nyingi.lakini pia nitahadharishe , lugha zisizofaa huwa sipendi na kutukana siwezi, si kwamba siyajui matusi lakini huwa sioni faida yake.

Hii ni simulizi mpya ambayo inanihusu moja kwa moja, lengo likiwa ni moja tu burudani kwa wanajamvi,Code na vigezo vingine vimezingatiwa tiririka.........

SEHEMU YA KWANZA.

Kwa mara ya kwanza nilishiriki kampeni kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015,huku Mimi na washikaji zangu, tuliamua kujitosa kwenye zile kampeni baada ya mkubwa wetu wa kazi kutulazimisha tumuunge mkono kiongozi ambaye hakuna mtanzania yeyote aliwaza kuwa angekuwa Rais wa nchi, na kizuri zaidi hata yeye alikuwa anasema hakutegemea kuwa angeweza kuwa na cheo hicho cha juu.

Nikiwa karibu na nyumbani kwenye bar moja local nikiwa na konyagi ndogo na maji, simu yangu iliita nikaipokea,

Oyaa bob vipi uko wapi, aliongea yule jamaa yangu bila hata salamu.

Nipo home tu, vipi nambie bob, nilimjibu.

Oyaa jamaa naye kakatwa, huwezi amini amebaki (jina kapuni) pamoja na wanawake wawili, hebu niambie ni nani anaweza kushika kijiti? Jamaa yangu aliongea kwa mfumo wa swali Kisha akakata simu.

Nikapiga ili anipe data kamili akawa hapokei simu, licha ya kupiga mara kadhaa bado simu haikupokelewa,

Dah huyu mwafulani nilitegemea yeye ataweza kushika kijiti baada ya yule mwingine kukimbilia upande wa pili, kumbe naye kakatwa? nilijiuliza sana Kisha nikajikuta nacheka mwenyewe huku nikishindwa kuamini kama jamaa yetu kaingia top three.

Hata baada ya kuzama social network nilikuta kumechafuka , habari hiyohiyo, nikaamua kuachana na habari zile nikaendelea na nyagi zangu huku nikipokea simu kadhaa kwa watu mbalimbali zinazohusiana na ile habari mpya mjini.

Kesho nikiwa ofisini alikuja mkubwa wangu tukasalimiana , huku akionesha furaha ya moja kwa moja.

Dani eeh, nadhani umesikia ulichosikia , Sasa nakuomba wewe na wenzako mpo wengi inabidi tumsapoti mheshimiwa sawa . aliweka kituo.

Aaaaaaah Sasa boss Mimi na siasa wapi na wapi hapa nilipo hata sijui nipo chama gani cha siasa, halafu hata sijui naanzaje yaani, kifupi boss naona kama inaniwia vigumu , kama siasa ni kipaji basi nadhani kipaji hicho sina,. Niliongea huku nikijichekesha kwani nilikuwa naongea na mtu mkubwa sana kwangu.

Sikia Daniel Mimi nakujua mwanzo mwisho kuwa hujui kitu, kwani akina fulani wanajua nini? (aliwataja majina) lakini nishawaorodhesha!
Halafu najua Dani ni mtu wa kusahau wewe unajua fika Mimi nipoje na huyu mtu na pia hata wewe unamjua huyu mtu kwa kipindi kirefu sana aliongea huku akinikumbusha mambo mengi kiasi cha Mimi kutokuwa na pingamizi.

Sasa boss labda nikuulize, nitakuwa kwenye nafasi gani kwenye hii ishu maana nipo gizani. niliuliza

Ninachohitaji ni utayari wako tu, kuhusu cha kufanya utaelekezwa sawa. alinijibu Kisha akatoka.

Nilifikiria kwa muda Kisha nikaona moyo unapiga, niliwaza nitavyovaa mavazi ya ile rangi iwe kapelo , fulana na vingine nikajikuta sipendi kama nini ili sikuwa na namna.

Ikawa imebaki siku ya nani atapitishwa ili tuingie kwenye ule mpango, nakumbuka nikiwa home nilikuwa mubashara nikiangalia Television ya taifa kwa lazima kwani huko ndiko taarifa zote zilipatikana , nikawa active kwenye mitandao ya kijamii lengo nisiwe gizani , yaani nikiulizwa chochote iwe rahisi kujibu.
lakini nililazimika kujitengenezea TV ya chumbani maana nilishakuwa kero
Kwa familia lakini hata mke wangu alishtuka kidogo akauliza.

Mwenzetu si kawaida yako kufuatilia siasa zaidi ya taarifa ya habari ya kawaida, halafu watu sijui mkoje Kuna channel huwa unasema huipendi lakini nakuona kutwa huitoi vipi? aliuliza mke wangu.

Lakini sikumwambia chochote zaidi ya kusema nimeamua tu, labda ndiyo mwanzo wa kuijua siasa kwani hata hao wanasiasa hawakuanza tu.

My wife aliniamini na hakuwahi kuniuliza chochote tena, basi Mimi na washikaji zangu tulikutana maeneo fulani tukakaa na kujadili kiundani kuhusu kazi ya kutoa sapoti iliyopo mbele yetu, hakuna aliyekuwa anajua chochote tukajikuta tunacheeeeka, tukijua tushaingia cha kike mbaya zaidi nani angepinga maamuzi ya boss? Tukapiga maji yetu tukaagana.

Baada ya masiku kadhaa nilikuwa home nimetulia huku nikifuatilia kwa umakini yanayoendelea Dodoma,huku marafiki zangu wakiwadai wameenda kwenye tukio labda kwakuwa walikuwa na ile hamu lakini Mimi sikuipenda ile hali basi tu.
Mwamba akapita freshi huku nikistuka kumuona mgombea mwenza mwanamke kwa mara ya kwanza kwenye nchi yetu.

Baada ya lile zoezi niliingia mtaani kama kawaida nione sura watu wamelipokeaje, kumbuka upande wa pili Nako alisimama mgombea mwenye nguvu hivyo Mimi nikawa nashindwa kujua Nini kitajiri.

Baada ya siku tatu tuliitwa na boss wetu akatuambia kuwa zoezi ndiyo litaanza rasmi hivyo kwa kipindi chote cha kampeni tutakuwa kwenye msafara kila atakakokuwa mgombea na sisi tutakuwepo, jasho lilinitiririka sana tu , tena mno. huku nikishangaa wenzangu hawana wasiwasi kabisa ndiyo kwanza wanafurahia.

Mimi nadhani tumekubaliana na niwashukuru nyote kwa kuweza kukubali kushirikiana katika hili, japo nisiwafiche, namuona kama Daniel tunamlazimisha hivi, eeh eti Dani upo sawa? Kumbuka hata Dodoma hukuwepo, sijakulaumu kwakuwa kazi yenu ilikuwa bado ila kwasasa unatakiwa utuweke wazi kama utakuwa na sisi ama la! aliongea boss huku akinitazama bila kupepesa macho.

Hapana boss Mimi nipo na wewe na nitakuwa na wewe bega kwa bega tuliagana huku tukipewa baadhi ya taratibu tukaagana, lakini bado ule moyo sikuwa nao , ikabidi nimpigie simu baada ya kufika nyumbani.

Samahani boss kwani Kuna ulazima wowote wa kuvaa sare za chama? niliuliza swali ambalo ni kama niliropoka tu.

Alicheka sana Kisha akaniambia,
Sisi hatupo kwenye chama Dani sisi tupo kwenye kumsapoti mheshimiwa, kwani kuvaa hizo nguo ndiyo nini, unaweza kuvaa na ukawa moyo upo kwingine, na pia umesahau kama majukumu yetu yapo tofauti, halafu Dani sijui huwa upoje , hebu punguza pombe bwana, inawezekana Kila tunachojadili huwa hauko makini nacho. alikata simu huku nikigundua dizaini kama kachukia hivi.

Kesho asubuhi alinipigia simu na kuniambia kuwa, amekaa na kufikiria amegundua kuwa Mimi sipo pamoja na wao hivyo niendelee na majukumu ya kiofisi kama kawaida. licha ya kumbembeleza lakini ilishindikana, nikaamua kwenda ofisini kwake.

Ananiachaje kwenye huu mpango Sasa, haiwezekani.

Itaendelea.....................
 
Napenda sana kusoma vitabu, hali hii imenifanya nipende kuandika visa kadhaa ambavyo huwa ni vya kweli, Sina visa vya kutunga.simulizi zote zina ukweli kwa asilimia nyingi.lakini pia nitahadharishe , lugha zisizofaa huwa sipendi na kutukana siwezi, di kwamba siyajui matusi lakini huwa sioni faida yake.

Pamoja boss
 
SEHEMU YA PILI

Siku inayofuata nilikutana na boss wangu ambaye alikuwa na Harakati nyingi sana, nilisalimiana naye kisha akaniashiria niketi.

Unasemaje Dani, aliuliza.

Nimekuja tuongee masuala ya jana boss, nilishangaa kuona unanitoa kwenye mpango wetu, kwani Kuna nini boss. niliuliza

Akacheka sana,
Sikia Daniel, mimi sitaki tulazimishane kwenye mambo ya hiyari, siyo lazima.
Tangu mwanzo ulisema hutaki, yaani inaonesha huhitaji, halafuuuu Dani, gharama zote ni zetu , Kila kitu ni chetu shida ni nini? eeh acha moyo mgumu kiasi hicho Duniani tunapita.
aliweka kituo.

Hapana boss Mimi nipo pamoja na wewe kwenye Kila hatua, ni kweli Kuna kauoga kalinipata mwanzo lakini nishakuwa sawa, Nina Imani Kila kitu kitaenda sawa.nilijitetea.

Sawa nimekuelewa,Nina Imani hutaniangusha hakikisha tunakutana kwenye hotel xxxx kwani ndiko itafanyika semina fupi tuwape mikakati ya kazi.Alisisitiza.

Kwa kufupisha stori, ndani ya siku tano za mwanzo nilikuwa nyuma nyuma kwenye msafara wa mheshimiwa huku nikiwa sijui a b c
Zozote lakini hata boss wangu tukawa hatuonani kwani alikuwa Frontline, hata jamaa zangu wale licha ya kiherehere cha mwanzo waligundua ule muziki siyo.

Vipi Dani tunafanyaje, au tuvae sare tu ili tujue moja, maana huu ni wakati wa kujaribu bahati yetu, unaweza kukuta unapata shavu kubwa wazee tuache kujishusha. alishauri ndugu yangu mmoja ambaye alikuwa ndumilakuwili hivi.

Kujaribu bahati? Bahati gani halafu wewe ni scientist ujue, hapa tunaongelea vitu vinavyo prove sawa kiongozi,
acha mambo ya shavu sijui bahati hizo ni hekaya tu. alijibu jamaa yangu mwingine ambaye alishaanza kukata tamaa baada ya kuona hapati nafasi tofauti na matarajio.

Wakati huo tulikuwa Mkoa xxxx, tukiwa tunamngoja mheshimiwa ambaye tuliambiwa atafika saa Saba aongee na watu wa wilaya ile, kama kawaida yetu kiu zilitubana tukatafuta sehemu tupoze shida zetu, nakumbuka tulijisahau tukaja kusikia sauti ya mheshimiwa, kutega masikio vizuri kumbe alishafika muda , na alikuwa anawaaga wanakijiji wa pale. Tukaona tushazingua .

jamaa yangu akakaa kulia akawasha land cruiser akaichochea sana , tukafanikiwa kufika kwenye Kijiji ambapo kulikuwa na gari kadhaa za chama huku bendera zikiwa Kila mahali , akina mama nao walipendeza sana wakiimba nyimbo bila kuchoka,jamaa aliniacha kwenye gari nikiwa hoi nikawa nawaona watu kama wanazunguka, naiona kama gari inainuka mbele kumbe ni mizinga inafanya kazi. Huku nikiwaza , kwanza uchaguzi wa nini? Mbona huyu kashapita? nani mwingine anaweza shindana na chama tawala?Aargh kuchoshana tu yaani.

Jamaa yangu alirudi fasta kwenye gari, akaniambia boss anatuita,kichwa kilipata moto na pombe ziliisha nikaona boss akiniona hivi si balaa tena,paparazi nao hawakuwa mbali na maeneo yetu.kushuka naogopa usije pigwa picha mtu ukatia aibu ya mwaka.

Oyaa D eeh ,unajua tumezingua sana mwanangu! mshikaji wangu alivunja ukimya kabla sijajibu simu iliita
alikuwa ni boss wangu , nikaiweka sikioni.

Nyie ma**la mko wapi?
Kuanzia muda huu, washeni gari nendeni Dar es salaam, sihitaji neno lolote kutoka kwenu, Tena nilitakiwa niwanyang'anye na gari kabisa wajinga nyie . alitukana boss huku akionesha ni mwenye hasira sana.mmmh hapa ulevi ulituponza nidhamu ikawa ni ndogo.

Jamaa yangu akawasha gari akaingia kwenye kijizahanati fulani lengo tufiche gari,tukatoa mabango , bandua vitu vyote , toa stika zote za chama, jamaa akatia gia hao tunautafuta Mkoa unaofuata, mpaka saa tano kasoro usiku tulikuwa Dar, huku nikishindwa kwenda nyumbani nikaamua kwenda kulala kwenye lodge fulani katikati ya jiji, huku jamaa yangu yeye akienda kwake.

Asubuhi na mapema nikipokea sms toka kwa boss,

Hapo ofisini sitaki ukae, mwenzio nishampangia pa kwenda na wewe utaenda mkoani Lindi, maana yule aliyekuwa kule namrudisha aje huku ambako nyinyi mmeshindwa na mmenitia aibu wa***avu nyie.Kuna gari lipo utaoneshwa , chukua nenda kaifanye hiyo kazi.

Lindi tena, aarrrgh kwanza safi tu kampeni za Nini kuchoshana tu, nilifika home nikaaga vizuri kuwa naelekea kusini, nikarudi ofisini nikachukua gari nikaondoka, kwakuwa kulikuwa na foleni
Sikugundua matatizo ya gari haraka , baada ya kupita Kongowe njiapanda ya kwenda Tua Ngoma nikagundua gari haina nguvu mlio wa Cruiser siusikii kabisa. Lakini nikaiburuza hivyo hivyo. Nilitumia masaa mengi Hadi Lindi mjini, lakini kabla sijafanya chochote akasema , siyo Lindi mjini Tena Bali natakiwa kwenda wilaya nyingine ya Liwale kwani ndipo Kuna hiyo kazi ya kufanya nikaona huyu kweli kaamua kunikomesha ila Leo siendi nitaenda kesho asubuhi gari lenyewe bovu.

Kesho yake nikiwa Liwale huku nikishangaa mji gani upo kushoto vile halafu nilizunguka siioni lodge ya maana, na mwenyeji wangu akanipeleka gesti moja ambayo yeye alidai huwa wanafikia watu wazito kama alivyodai lakini sikuipenda nikakubali kishingo upande hasa baada ya kuhakikishiwa usalama na wa gari la watu, maana mmmmh unaweza kufungwa hivihivi.

Kituko kwenye kula , yaani vyakula vinafanana tu Kila sehemu,nikaenda kwenye restaurant moja ambapo wenyewe wanapaamini alhamdulillah angalau nilifarijika , nikala nikarudi nikawasha PC yangu, nikaset mambo fulani nikarudi kwa wenyewe huku mwenyeji wangu ambaye ni muongeaji huku akinionesha saloon fulani ya kiume.

Hii ndiyo Liwale bro, imebarikiwa vitu vingi sana, hata ukitaka mke huku utapata, ukitaka kulima zao la ufuta linakubali, pia zao la muda mrefu kama korosho, ni wewe tu Cha muhimu huduma.
Lakini bro Kuna saloon pia hiyo hapo.
Alikazana na saloon nikagundua ndevu zangu ni nyingi tena zimekaa vibaya sana hivyo ndicho anachokazania.

Kwa kifupi wenyeji ni wakarimu na wapole Ukiwa na heshima utaheshimiwa, nilikaa siku tatu bila kuwasha gari kwakuwa shughuli zilikuwa ni pale pale na hakukuwa na haja ya usafiri siku nawasha gari ilikataa kuwaka nikatumia ufundi wangu wote kitu iligoma. Nikatoa taarifa kwa wakubwa wangu , nikaambiwa Kuna fundi yupo Lindi mjini ambaye ni dereva pia atakuja kurekebisha, lakini fundi alikuja na kuniambia gari linahitaji service kubwa hivyo lazima spair ipatikane, nikaendelea na kazi huku nikiambiwa nikimaliza atatumwa dereva mwingine anifuate.

Baada ya kufanikiwa zoezi la kazi yangu, nikatoa taarifa nikaambiwa dereva atakaye nichukua yupo Lindi mjini ni yule fundi hivyo niwasiliane naye, kweli nikampigia simu tukakubaliana kuwa nipande basi na yeye nitamkuta Nangurukuru ananisubiri.

Nangurukuru ni Junction ambapo njia ya lami ni mpaka Mtwara , Mozambique unafika
pia Kuna Kilwa Masoko huko ilipo bahari ya Hindi, lakini linapozamia jua Kuna Rough road inayoenda Liwale kwa wasiotaka kuzunguka sijui Lindi mjini, sijui Nachingwea huko .

Nilienda booking nikapata tiketi ya Dar es salaam licha ya kuwa naishia Nangurukuru lengo nikiwa sitaki kusimama kwani kilomita mia mbili kwenye barabara ya vumbi tena mbovu, si mchezo. nikarudi nikakadhi gari upya nikalala tayari kwa safari.

Itaendelea.....................
 
SEHEMU YA TATU

Asubuhi na mapema kukiwa na baridi fulani kali kiasi nilioga , nikavaa nguo za kawaida kwani nilitahadharishwa na wenyeji kuhusu aina ya barabara ile wakinitaka nifike kwanza Nangurukuru ndipo naweza vaa nitakavyo. nilisogea stendi ya pale Liwale huku nikiiangalia aina ya siti nitakayokaa kwenye ile tiketi.

Watu walikuwa wengi huku magari mawili ya kwanza ya abiria yakiwa yanaondoka, sisi gari letu lilikuwa bado linapakia mizigo, sikutaka kuingia mapema kwani watu waliosongamana pale mlangoni walileta kero kiasi.
Baada ya watu kupungua pale mlangoni, niliingia nikipenyapenya katikati ya watu waliosimama, lakini nilikuta kwenye siti yangu amekaa mama mmoja aliyekuwa anaongea lafudhi ya kisukuma.

Samahani mama, nadhani hii sehemu nakaa Mimi angalia tiketi yangu, nikampa ajionee ili tuondoe utata.

Akasema hapana, ile ni sehemu yake, akanionesha tiketi yake, ikiwa imeandikwa sehemu ile ile, hivyo alikuwa sahihi, nililaumu sana kitendo cha watu kuuza siti mara mbili, nikaamua kuja huku mbele nikasimama Kisha nikampigia dereva wangu kuwa kama hajatoka Lindi mjini basi aje Liwale anichukue lakini simu haikupatikana.

Nikaamua moja kusimama huku gari likiondoka kwa mbwembwe, watu tumebanana kama tupo kwenye daladala za Gongo la mboto, tulitembea kwa muda fulani huku nikiwa sioni nje , yaani sijui tupo wapi Kuna muda gari inalala kama inaanguka huku mabonde nayo nikiyasikia vizuri . Baadaye gari lilisimama dereva akashuka, nusu saa nzima dereva haondoki gari linaunguruma tu, watu tukaanza kushuka mmoja mmoja huku tukamuona dereva kwenye uvungu wa gari akiwa na spana zake.

Nikaona kazi ipo, nikawauliza wenyeji kwani tupo wapi wakajibu tupo sehemu inayoitwa kaburi la mzungu, huku wakidai safari bado kabisa. nilitoka nikaenda kwenye mti fulani nikiwa peke yangu huku nikishangaa kundi kubwa la watu yaani wote Hawa tumetoka kwenye gari hii, kumbe hizi Marco polo Zina nguvu sana eeh. nilijisemea moyoni.

Nilimpigia dereva akapokea nikamweleza hali halisi akadai yeye iwe isiwe atanisubiri hivyo nisiwe na shaka. Lakini wakati nikiwa pale alikuja jamaa mmoja mwenye mwili uliokosa mazoezi huku akiwa hazingatii diet. akanisalimia kwa kunipa tano.

Loh kaka kumbe huku usafiri ni wa tabu hivi, hakika leo tumepatikana , yaani hiyo gari sijui hawakuikaguaaaa? Naona Springs zimecheza ndiyo wanahangaika kufunga hapo, tuombe MUNGU tuondoke salama dah. aliongea kwa masikitiko yule jamaa huku nikitambua kuwa naye ni mgeni kama mimi.

Yaani ndiyo hivyo huku usafiri shida,.......... Kabla sijamalizia sentensi yangu , alikuja mwanamke huku akimvuta jamaa mkono kwa nguvu.

Hivi Mume wangu unanitaka nini lakini, kwanini unaniharibia? mtaalamu ulimsikia vizuri sana, alitwambia msipeane mikono na mtu yeyote, hadi mtakapo fika na kuoga hii dawa , Sasa kwanini unakuwa hivyo? Mwanamke aling'aka huku akinitolea macho mimi kana kwamba ndiye niliyesababisha.
halafu na wewe mwenye midevu kwanini unapenda kusalimia salimia watu ovyo ovyo ili iweje. Kila mtu ana Harakati zake kwenye maisha,jitahidi kudili na mambo yako.mwanamke yule alianza kuniletea shombo.

Kwanza nilishangaa lakini nilishindwa nimfanyaje.

Mke wangu hebu kuwa na adabu basi, huyu jamaa nimemkuta Mimi na Mimi ndiye nimeanza kumsalimia hivyo makosa ni yangu , hebu achana na watu wengine mke wanguuu.
aliongea jamaa kwa kujikaza huku Kwa dakika kadhaa nilivyowaona ni dhahiri mwanamke alikuwa na sauti kuliko jamaa.

Haya ushaharibu tayari, inatakiwa turudi kwa mtaalamu , na Mimi duka langu sitafungua hadi tutakapo kamilisha vigezo na masharti yote, japo sharti moja umeshavunja , na turudi tu kwa mtaalamu Mimi siendi mjini tena . alilalamika yule mwanamke.

Lakini mke wangu mbona unakosa aibu vitu gani unaongea ? jamaa alimlaumu mkewe.

Mimi kuona vile nikatoka nikaenda kukaa kwenye mti mwingine nikiwaacha wanalumbana, huku nikiwaza mbali namna watu walivyo washirikina, au haya mambo yapo kweli, isije kuwa huwa nadharau tu kumbe waganga wanasaidia, maana hizi kazi za kutumwa hiziiiii, tutatumwa Hadi lini? Basi kama nimeandikiwa kutumwa, nipande hata cheo basi, si bado nitaendelea kuwa mtumishi. niliwaza sana huku majibu yakiwa mengi.

Watu walikaa vikundi vikundi wakipiga stori zinazofanana, wapo walizungumza namna ya uchomaji mkaa, wapi walizungumza kuhusu kilimo, wapo vijana waliongelea kuhusu uchimbaji wa madini sijui wapi huko. lakini baada ya Mimi kuona dereva na mafundi bado wapi uvunguni mwa gari nilirudi kwenye mti nilipokuwa mwanzo.

Nikaona yule jamaa na mkewe wanakuja nilipo, Hawa wanataka nini tena? Naamua kukaa peke yangu bado wananifuata fuata?
Wakizingua tena nawachana wasinione mnyonge, nilijisemea moyoni.

Dah aisee shemu noma sana yaani, gari sijui litapona saa ngapi,aliongea yule mwanamke huku jamaa akiwa mita kadhaa akiongea na simu.

Ila shemu naomba nisamehe bwana nimejikuta naropoka , nisamehe bure si unajua wanawake sisi. aliongea kwa sauti ya kubana huku nikibaini sauti nzuri lakini pia na yeye alikuwa Mashallah, sura nzuri na shepu ya kwenda. Wakati huo mumewe anaongea na simu na anazidi kwenda mbali zaidi.

Yaani wanawake bwana, wanakimbilia kwenye jinsia yao wakikosea, mwanzo walikuwa wanasema wakiwezeshwa wanaweza, si hawa?
Tena Sasa hivi wamebadilika wanadai , mwanamke anaweza bila kuwezeshwa. niliwaza sana.

Vipi shemu usinung'unike, naona nisamehe sana, alizidisha maneno.

Usijali shemu najua jamaa alikukwaza ikapelekea kuwa kwenye ile hali, nashukuru kama umetambua ulipoteleza, na MUNGU akubariki . Baadaye tukaitwa nikijua gari limepona.tukawa kwenye eneo la tukio.

Jamani tuwe wa kweli tumejitahidi kwa kadri ya uwezo wetu, lakini tumeshindwa hivyo Kuna gari linakuja kutufaulisha naomba tuwe wavumilivu kiasi ni bahati mbaya imetokea hakuna anayependa hii hali .Dereva aliweka kituo huku abiria wengi wakikata tamaa, Mimi nikarudi kwenye ule mti ili nimpigie dereva wangu anifuate lakini simu haikupokelewa.

Yule jamaa na mkewe walikuja tena,aisee kaka Kuna sehemu zingine sijui watu wanawezaje kuishi yaani tangu muda ule hakuna hata gari la mizigo kupita? jamaa aliongea huku akicheka sana. Lakini kumbe taarifa zilishafika Liwale mjini kuwa chombo kimeharibika hivyo pikipiki (bodaboda) zikaanza kuja ili kama Kuna wanaoahirisha safari basi warudi Liwale.

Wakati tukiwa pale chini ya mtu lilikuja gari lililopakia chupa za soda tupu , huku wakidai wanaenda Kilwa Masoko kwahiyo anayetaka kufika walau Nangurukuru ambako ndiko kwenye usafiri wa uhakika basi achangie elfu kumi, Mimi sikuuliza nilikuwa nishachomoa kumi yangu ipo mkononi huku baadhi wakidai hela ile ni nyingi sana na pia hawazi kuacha nauli zao walizolipa kwenye bus, umasikini mbaya sana.

Sisi watatu tulipanda kwenye ile Eicher, wanaume wawili tukiwa nyuma yule mwanamke akapanda kwa dereva.

Je, tutafika salama? usikose sehemu inayofuata.

Itaendelea.........................
 
Napenda sana kusoma vitabu, hali hii imenifanya nipende kuandika visa kadhaa ambavyo huwa ni vya kweli, Sina visa vya kutunga.simulizi zote zina ukweli kwa asilimia nyingi.lakini pia nitahadharishe , lugha zisizofaa huwa sipendi na kutukana siwezi, si kwamba siyajui matusi lakini huwa sioni faida yake.

Hii ni simulizi mpya ambayo inanihusu moja kwa moja, lengo likiwa ni moja tu burudani kwa wanajamvi,Code na vigezo vingine vimezingatiwa tiririka.........

SEHEMU YA KWANZA.

Kwa mara ya kwanza nilishiriki kampeni kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015,huku Mimi na washikaji zangu, tuliamua kujitosa kwenye zile kampeni baada ya mkubwa wetu wa kazi kutulazimisha tumuunge mkono kiongozi ambaye hakuna mtanzania yeyote aliwaza kuwa angekuwa Rais wa nchi, na kizuri zaidi hata yeye alikuwa anasema hakutegemea kuwa angeweza kuwa na cheo hicho cha juu.

Nikiwa karibu na nyumbani kwenye bar moja local nikiwa na konyagi ndogo na maji, simu yangu iliita nikaipokea,

Oyaa bob vipi uko wapi, aliongea yule jamaa yangu bila hata salamu.

Nipo home tu, vipi nambie bob, nilimjibu.

Oyaa jamaa naye kakatwa, huwezi amini amebaki (jina kapuni) pamoja na wanawake wawili, hebu niambie ni nani anaweza kushika kijiti? Jamaa yangu aliongea kwa mfumo wa swali Kisha akakata simu.

Nikapiga ili anipe data kamili akawa hapokei simu, licha ya kupiga mara kadhaa bado simu haikupokelewa,

Dah huyu mwafulani nilitegemea yeye ataweza kushika kijiti baada ya yule mwingine kukimbilia upande wa pili, kumbe naye kakatwa? nilijiuliza sana Kisha nikajikuta nacheka mwenyewe huku nikishindwa kuamini kama jamaa yetu kaingia top three.

Hata baada ya kuzama social network nilikuta kumechafuka , habari hiyohiyo, nikaamua kuachana na habari zile nikaendelea na nyagi zangu huku nikipokea simu kadhaa kwa watu mbalimbali zinazohusiana na ile habari mpya mjini.

Kesho nikiwa ofisini alikuja mkubwa wangu tukasalimiana , huku akionesha furaha ya moja kwa moja.

Dani eeh, nadhani umesikia ulichosikia , Sasa nakuomba wewe na wenzako mpo wengi inabidi tumsapoti mheshimiwa sawa . aliweka kituo.

Aaaaaaah Sasa boss Mimi na siasa wapi na wapi hapa nilipo hata sijui nipo chama gani cha siasa, halafu hata sijui naanzaje yaani, kifupi boss naona kama inaniwia vigumu , kama siasa ni kipaji basi nadhani kipaji hicho sina,. Niliongea huku nikijichekesha kwani nilikuwa naongea na mtu mkubwa sana kwangu.

Sikia Daniel Mimi nakujua mwanzo mwisho kuwa hujui kitu, kwani akina fulani wanajua nini? (aliwataja majina) lakini nishawaorodhesha!
Halafu najua Dani ni mtu wa kusahau wewe unajua fika Mimi nipoje na huyu mtu na pia hata wewe unamjua huyu mtu kwa kipindi kirefu sana aliongea huku akinikumbusha mambo mengi kiasi cha Mimi kutokuwa na pingamizi.

Sasa boss labda nikuulize, nitakuwa kwenye nafasi gani kwenye hii ishu maana nipo gizani. niliuliza

Ninachohitaji ni utayari wako tu, kuhusu cha kufanya utaelekezwa sawa. alinijibu Kisha akatoka.

Nilifikiria kwa muda Kisha nikaona moyo unapiga, niliwaza nitavyovaa mavazi ya ile rangi iwe kapelo , fulana na vingine nikajikuta sipendi kama nini ili sikuwa na namna.

Ikawa imebaki siku ya nani atapitishwa ili tuingie kwenye ule mpango, nakumbuka nikiwa home nilikuwa mubashara nikiangalia Television ya taifa kwa lazima kwani huko ndiko taarifa zote zilipatikana , nikawa active kwenye mitandao ya kijamii lengo nisiwe gizani , yaani nikiulizwa chochote iwe rahisi kujibu.
lakini nililazimika kujitengenezea TV ya chumbani maana nilishakuwa kero
Kwa familia lakini hata mke wangu alishtuka kidogo akauliza.

Mwenzetu si kawaida yako kufuatilia siasa zaidi ya taarifa ya habari ya kawaida, halafu watu sijui mkoje Kuna channel huwa unasema huipendi lakini nakuona kutwa huitoi vipi? aliuliza mke wangu.

Lakini sikumwambia chochote zaidi ya kusema nimeamua tu, labda ndiyo mwanzo wa kuijua siasa kwani hata hao wanasiasa hawakuanza tu.

My wife aliniamini na hakuwahi kuniuliza chochote tena, basi Mimi na washikaji zangu tulikutana maeneo fulani tukakaa na kujadili kiundani kuhusu kazi ya kutoa sapoti iliyopo mbele yetu, hakuna aliyekuwa anajua chochote tukajikuta tunacheeeeka, tukijua tushaingia cha kike mbaya zaidi nani angepinga maamuzi ya boss? Tukapiga maji yetu tukaagana.

Baada ya masiku kadhaa nilikuwa home nimetulia huku nikifuatilia kwa umakini yanayoendelea Dodoma,huku marafiki zangu wakiwadai wameenda kwenye tukio labda kwakuwa walikuwa na ile hamu lakini Mimi sikuipenda ile hali basi tu.
Mwamba akapita freshi huku nikistuka kumuona mgombea mwenza mwanamke kwa mara ya kwanza kwenye nchi yetu.

Baada ya lile zoezi niliingia mtaani kama kawaida nione sura watu wamelipokeaje, kumbuka upande wa pili Nako alisimama mgombea mwenye nguvu hivyo Mimi nikawa nashindwa kujua Nini kitajiri.

Baada ya siku tatu tuliitwa na boss wetu akatuambia kuwa zoezi ndiyo litaanza rasmi hivyo kwa kipindi chote cha kampeni tutakuwa kwenye msafara kila atakakokuwa mgombea na sisi tutakuwepo, jasho lilinitiririka sana tu , tena mno. huku nikishangaa wenzangu hawana wasiwasi kabisa ndiyo kwanza wanafurahia.

Mimi nadhani tumekubaliana na niwashukuru nyote kwa kuweza kukubali kushirikiana katika hili, japo nisiwafiche, namuona kama Daniel tunamlazimisha hivi, eeh eti Dani upo sawa? Kumbuka hata Dodoma hukuwepo, sijakulaumu kwakuwa kazi yenu ilikuwa bado ila kwasasa unatakiwa utuweke wazi kama utakuwa na sisi ama la! aliongea boss huku akinitazama bila kupepesa macho.

Hapana boss Mimi nipo na wewe na nitakuwa na wewe bega kwa bega tuliagana huku tukipewa baadhi ya taratibu tukaagana, lakini bado ule moyo sikuwa nao , ikabidi nimpigie simu baada ya kufika nyumbani.

Samahani boss kwani Kuna ulazima wowote wa kuvaa sare za chama? niliuliza swali ambalo ni kama niliropoka tu.

Alicheka sana Kisha akaniambia,
Sisi hatupo kwenye chama Dani sisi tupo kwenye kumsapoti mheshimiwa, kwani kuvaa hizo nguo ndiyo nini, unaweza kuvaa na ukawa moyo upo kwingine, na pia umesahau kama majukumu yetu yapo tofauti, halafu Dani sijui huwa upoje , hebu punguza pombe bwana, inawezekana Kila tunachojadili huwa hauko makini nacho. alikata simu huku nikigundua dizaini kama kachukia hivi.

Kesho asubuhi alinipigia simu na kuniambia kuwa, amekaa na kufikiria amegundua kuwa Mimi sipo pamoja na wao hivyo niendelee na majukumu ya kiofisi kama kawaida. licha ya kumbembeleza lakini ilishindikana, nikaamua kwenda ofisini kwake.

Ananiachaje kwenye huu mpango Sasa, haiwezekani.

Itaendelea.....................
Beb moneytalk mwamba huyu hapa
 
SEHEMU YA NNE

Gari ilianza kutembea huku mikito na mabonde vikifanya gari ikose utulivu, tukawa na kazi ya kuset makreti ya soda ambapo kwakweli ilikuwa ni kazi kubwa jumlisha na vumbi basi hakika ilikuwa ni siku ya aina yake. Dereva alionekana ni mzoefu wa njia ile kwani mwendo wake ulionesha.

Tukiwa kule nyuma jamaa alivunja ukimya kwa kuniuliza swali,

Vipi ndugu yangu inaongezeka na wewe siyo mwenyeji kama mimi, vipi una mishe au biashara gani kwa huku. aliuliza

Mimi nipo tu kaka si unajua tena harakati za maisha. nilimjibu kifupi.

Jamaa akatikisa kichwa kuonesha amekubaliana na mimi, kisha akanitupia swali lingine.

Sasa ushafanikisha mipango yako, maana naona kama unarudi nyumbani.

Hapana, sijafanikisha ila narudi kwasababu nimeitwa na mwajiri wangu. Nilimjibu

Jamaa alionesha ameshaanza kunidharau maana maswali mengine hata hayakufaa kuuliza, mavazi yangu, sandozi mbovu na mzula niliovaa pengine alishatabiri anavyojua yeye. Kumbe Mimi nilivaa vile kwakuwa nilishaambiwa ubovu wa barabara +vumbi nikaona nywele zitachafuka.

Ikabidi na Mimi nimtupie swali ,
Kwani kaka na wewe huku una mishe gani?

Sisi tulikuja kuangalia fursa ya biashara huku ,ila hatujaridhika nako ni kupo kushoto sana. alinijibu huku akiwa anapigapiga simu Kila mara lakini hakufanikiwa kwa hakukuwa na mtandao sehemu tulipo.

Nilimuangaliaaa Kisha nikatabasamu maana nilijua wanatoka kuroga lakini kwanini ameshasahau muda mfupi vile, wakati mkewe alinigombeza baada ya jamaa kunipa mkono. ila sikutaka mengi Sana.

Tuliendelea na safari huku nikiomba MUNGU nifike barabara kuu, angalau nitapata ahueni,tukafika Kijiji kimoja kinaitwa Njinjo, dereva akashuka akidai ana njaa anatafuta chochote kitu na Mimi nikashuka huku jamaa na mkewe wakadai hawali kwani hakuwa na Imani na vyakula vya pale, yaani watu wengine acha tu.

Nikazama kwenye kibanda cha mama ntilie nikakuta Kuna wali na mbaazi tena unauzwa elfu moja tu sahani, nikapiga nikanunua maji nikarudi kwenye gari ili tumsubiri dereva ambaye licha ya kuwa amekula lakini aliendelea kucheza Draft yaani hakuwa na haraka , nilitabasamu huku nikikumbuka vitu vingi sana

yule jamaa na mkewe walikuwa wanakula mikate ambayo walikuwa nayo kwenye mkoba wa mkewe, Kisha eti akanituma nikamnunulie maji, huku mkewe naye akinionesha dharau, sikujua moja kwa moja walinichukuliaje ila Kuna hasira ilikuwa lakini kwakuwa najua Dunia ilivyo nilienda dukani nikachukua maji nikawapa .

Hivi huyu dereva umemuona wapi shemu,aliuliza yule mwanamke.

Yupo kwenye vibanda vileee vyenye Solar panel, nilimjibu. Huku nikiwa na kitu moyoni lakini nilijitahidi nikajizuia yaani Mimi wa kutumwa maji? Jamani loh.

Nikiwa kwenye lindi la mawazo yule jamaa akanistua, oyaa kaka katustulie dereva , mbona anatuweka? Kama alijua ana mambo mengi kwanini alikubali kupakia watu hajui tuna haraka. aliongea huku akiwa na mkewe wameegamia gari huku wakiangalia vitu kwenye simu na kucheka Kila muda.

Duh yaani ananituma kwa mara nyingine, haaaaaa siwezi , nilijisemea Kisha nikaingia kwenye gari nikijifanya sijamsikia, nikatoa simu mfukoni lahaulaaaa missed calls zilikuwa nyingi akiwemo mke wangu, boss na dereva anayenisubiri Nangurukuru.

Nilianza na boss nikampigia akanipa pole tu Kisha akaendelea......yote haya umeyataka mwenyewe Dani ungekuwa huku wala yasingekukuta, umepishana na fursa kibao ambazo zingekutambulisha na kuzidi kukuweka mahali pazuri.ila jitahidi ufike nataka nikubadilishe maana hapa ofisini Kuna mambo yanayumba na dereva anakusubiri yeye ndiye kaniambia umekwama njiani.

Nilikata simu ya boss baada ya kuwa napigiwa kelele na vijana wa pale Njinjo, Oyaa mjomba shuka basi yaani jua lote hili upo juu ya gari? Una moyo mgumu sana, nilishuka kisha wale vijana wakawa wanapakia madumu yasiyo na kitu ila yalikuwa yananuka Diesel. Kisha wakapakia na vitu vingine kiasi cha kushindwa kujua tutakaa wapi.

Yule jamaa na mkewe waliniita , wakiwa wapo na yule dereva, oyaa bob kwani unaenda wapi unaonekana una haraka sana, lakini Nangurukuru siyo mbali si hapo tu Sasa hivi tunafika. aliongea yule dereva aliyeonekana anatumia majani mabaya huku suruali inaonesha hata huwa hafui.

Yule jamaa na mkewe wakawa wananionaje sijui, wakati huo begi lipo mgongoni. Nawaza nafikaje.

Sasa shemuu hilo begi si ushushe tu, utaliweka mgongoni Hadi saa ngapi hebu pumzika, kubali kuwa Leo ushapoteza hata kama ulikuwa unawahi mahali, aliongea yule mwanamke huku nikimuhurumia kimoyomoyo kwani jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza kinene.

Nilijichekesha kinafiki huku watu wengi wa pale wakiniona ni bonge la mshamba.

Sasa my tukifika highway jitahidi, kunikumbusha Nina vitu vya kununua njiani sawa, yule mwanamke alimwambia mumewe,

Sawa lakini tambua kuwa Mimi naenda kwanza Kilwa Masoko, umesahau mpango wetu, wewe Leo tangulia mpaka Dar Mimi nitakuja kesho, huyu jamaa si yupo? atakusaidia! Oyaa huyu shemeji yako nadhani umemsikia Sasa utamsaidia siyo Tena awe anatoa shingo dirishani wewe upo. si sawa. aliniamrisha jamaa, Sasa kwa kuwa Mimi mwenyewe ni mtukutu nilijifanya hamnazo nikamkubalia .

Na nauli yako nitalipa Mimi sawa jamaa yangu, alisema safari akijiamini zaidi Kisha akatoa kitambulisho na kunipatia nikaangalia nikagundua ni askari wa jeshi la polisi
Lakini nikajiuliza kwanini ni mjinga kiasi kile kwahiyo cheo chake kageuza fimbo ili aniongoze, halafu amepata mafunzo kweli huyu mbona ni mzembe anaruhusu ajulikane kirahisi. Yaani anatishia watu? Wakati yeye anacheza kwenye Volt 500 Mimi nipo kwenye Kilovolts 1000
yaani anilipie nauli ila moyoni nilifurahi yaani ananikabidhi mkewe nikasema nitamuonesha kwanini Kuna usiku na mchana kwenye hii Dunia.

Tulifika Nangurukuru freshi Kisha Nikaona gari ya taasisi yetu ikiwa karibu na mizani, sikutaka wale jamaa wajue kama Mimi ni nani kwani kwa dharau zao sikutaka kufanana nao. nikawaambia naenda kuoga kwanza , wakaanza kulaumu unaoga Nini badala ya kuwaza unafikaje mjini wewe unawaza kuoga. Wakawa wanasubiri basi toka Mtwara huku nikiwaza saa tisa hii watapata bus gani labda malori.

Itaendelea............
 
Like it
 
Sawa mkuu, tupo pamoja endelea kushusha vitu
IMG-20230619-WA0027.jpg
 
SEHEMU YA TANO

Nilimpigia simu dereva wangu kuwa nimeshafika na gari nimeliona ila anisubiri kwakuwa naingia kuoga kwanza, akajibu sawa.
Nilitafuta gesti moja local ya pale nikajiswafi nikabadilisha nguo kisha nikampigia dereva wangu kuwa anifuate nilipo.

Aisee pole sana kaka hii njia inasumbua sana , barabara ni mbovu pia hata magari yenyewe nadhani yanapakia kupita kiwango mizigo ni mingi mno kuliko hata abiria wenyewe, mbaya zaidi Haina magari ya kutosha nadhani umebahatika sana kupata usafiri,aliongea yule dereva huku akiwa kachangamka tu tofauti na nilivyowaza kuwa huenda alichoka kusubiri.

Ila samahani sana tena sana kaka
Ujue Mimi niliambiwa nikuletee tu gari Kisha nirudi Lindi mjini, ila Mimi nyumbani ni Hapo njianne Sasa hapa nikawa nafikiria ningefika tu nikawasalimie. aliongea huku akionesha yupo makini na Mimi.

Usijali lakini kwani familia yako ipo huku mbona unanichanganya? niliuliza kwani namfahamu fika hadi nyumbani kwake dar es salaam.

Hapana Mimi nimezaliwa huku , na wazazi wangu wapo huku na juzi nimepita tu nikiwa nampeleka Lindi boss (akimtaja jina) nilitamani niwasalimie lakini isingewezekana. Sasa nikaona leo ningefika tu. alifafanua

Hakuna shida, wazazi tena hata mimi mbona ningelala kabisa nipige stori na mshua, ila na wewe kumbe mbwembwe zote mjini tunakuonaga born town kumbe nyumbani kwenu porini hivi? nilimtania tukacheka.

Ila kaka, huko naona kampeni zimepamba moto sana, halafu nasikia na wewe ulikuwa sehemu ya kutoa sapoti kwa mheshimiwa, ilikuwaje ukaja huku tena. aliniuliza huku akijichekesha akijua labda nitachukia.

Bado nipo sehemu ya hiyo sapoti, hata hivyo ni mgawanyo wa majukumu tu si unajua lazima kazi zingine ziendelee. nilidanganya.
Kwani ukweli sikuwa sehemu ya kampeni kwani nilishazingua ila dereva hangenipinga kwani Mimi ni boss wake sema huwa tunaitana kaka kwa kuheshimiana tu.

Nilimuona anatabasamu huku akitekenya funguo za gari na akaanza kuja taratibu ilipo Roundabout. huku nikimwambia akifika lilipo geti la maliasili asimame, Kisha akaendelea

Kaka Mimi si mwanasiasa lakini mwaka huu umekuwa na ushindani wa aina yake, yaani ukifuatilia posts zilizoko mitandaoni na hata video mbalimbali, unaona kabisa unaweza ukawa ni mwisho wa hiki chama kikongwe maana ni balaa. aliongea dereva huku tukipita usawa ulipo mzani.

Weweee niulize mimi sisi ndiye tunaojua nini kinafanyika , unadhani ni rahisi hivyo? Haiwezekani na usidanganyike na habari za social network, huko unaweza Kuta mtu anaponda na kupinga jambo fulani kumbe lengo anataka tu kuchota watu. Laiti kura zingeangalia kwa kuwianisha mizani ya wanamtandao basi upande wa pili wangechukua nchi lakini mambo hayako hivyo. nilimjibu kama vile najua mambo mengi lakini ukweli hata Mimi nilikuwa sijui chochote kuhusu siasa.

Haya, lakini jamaa aliyekimbilia upande wa pili ana watu, yaani ana watu , ana Kijiji kaka, Mimi naona kama meli iliyoongozwa kwa miaka mingi inaenda kugonga mwamba. dereva alizidi kutoa mtazamo wake.

Kwanza wewe ni upande gani suka maana nakuona kama , upo kwenye meli ya pili. nilimuuliza kiutani.

Hakunijibu ila alicheka tu huku akidai ile mada tuachane nayo, wakati anajiandaa kuchochea jiko, nikamwambia asimame baada ya kuwaona wale ndugu zangu,
Hawa jamaa unaowaona wanapungia malori nilikuwa nao hebu tuwachukue.

Haaaaa akina nani tena kaka, kuwa makini tunaweza kupakia watu siyo, alilalamika huku akisimama nikashuka kwenye gari.

Enhee vipi ndugu zangu usafiri bado mgumu maana nilitegemea dakika nilizopoteza nisingewakuta tena,
Kumbe bado mpo? Niliuliza kinafiki.

Kwanza walinishangaa sana, waliangaliana Kisha jamaa akanijibu,
Ndugu yangu acha hapa lengo letu tupande hata magari ya mizigo maana tumeuliza wenyeji wanadai kwasasa kupata bus ni vigumu, lakini pia hata magari ya mizigo baadhi madereva wanadai huwa hawapakii abiria, na najua ni sheria hivyo wapo sahihi, na hapa nilishawaza tulale tu.

Namna nilivyovaa Kaunda suit yangu ya blue ambayo iliwahi kuwa sare kwenye kongamano fulani kanisani kwetu , huku safari hii nikiwa Nina muonekano mwingine , najua niliwapa mtihani kidogo,
Tuondokeni basi, niliwahimiza.

Sawa ila Mimi bado nipo hapa maana nataka nielekee Kilwa Masoko, nadhani hapa utaondoka
na shemeji yako, aliongea yule jamaa kiunyonge sana, lakini hata mkewe alinyongea huku akiwa na uoga kupanda kwenye gari.

Mume wangu Mimi naona tungewaacha waende tu maana sisi shughuli zetu hatujamaliza, alisema mkewe huku Mimi nikifungua mlango ili niondoke maana niliona siyo watu wa safari.

Sorry kiongozi, naomba tu umchukue huyu ,huku akimkata jicho baya mkewe, yaani unasahau kuwa una majukumu gani kesho? Eeeeeh yaani umebahatika kupata gari ndogo bado unaleta stori, hapa si masaa machache tu mko mjini.

Jamaa alifoka kidogo Kisha mkewe akakubali kupanda gari tukaondoka , Mimi nilikuwa kwenye siti nyuma ya dereva huku yule mwanamke akiwa pembeni ya dereva, chombo ikakolezwa moto, tukiwa kimya ndani ya gari hakuna aliyemuongelesha mwenziye niligundua yule mwanamke anageuka Kila muda akiniangalia kwa kuibia.

Baada ya kuona network imeshakuwa low nikaiweka simu mfukoni Kisha nikawa naangalia mbele huku nikigundua , shemeji si haba yaani yule afande alimiliki Mali safi kabisa, nilitamani nimfahamu kiundani lakini sikumuuliza kwani ningeleta maswali kwa dereva wangu na heshima niliyojijengea ingeshuka .

Kaka hapa ndiyo njia nne, wajanja tunapaita Four ways ,japo sijazaliwa hapa tulizaliwa Kipatimo huko ndani ndani,ila wazazi wangu walikuwa wanafanya kazi hapa hivyo tukahamia hapa na maisha yote tuko hapa. Karibu sana kaka, aliongea kwa mbwembwe huku akishuka kwenye gari akiwa na mizigo kadhaa .

Acha hizo kwahiyo Kuna tofauti gani Kati ya Njia nne na hicho kiingereza chako Cha huku Kilwa, tulitaniana kisha nikakamata chuma na kuondoka, jua nalo lilikuwa limebadilika rangi kuonesha siku inaisha.

Baada ya muda fulani simu ya yule mwanamke iliita, akaipokea huku Mimi macho yakiwa mbele tu, waliongea Kisha akakata.

Hivi hapa shemu tupo wapi maana Mimi ni mara ya kwanza kuja njia hii , nishasahau. alivunja ukimya yule mwanamke.huku akiniangalia kwa kuibiaibia na aibu juu. Maana dharau walizonionesha mwanzo huenda zilianza kumsuta.

Huu ni utangulizi tu simulizi kamili ndiyo kwanza inaanza.

Itaendelea................ .....
 
Huu ni uangalizi tu simulizi kamili ndiyo kwanza inaanza.

Itaendelea................ .....
Mwamba umetisha.

Shusha vitu
Shusha vitu
Shusha vitu mwambaaaaaaaaa
 
Jamani beb moneytalk mbna hauji kukutag kote huku
 
Nimesabuskraibu huu moto naulewa sana. Na kwanza nimechelewa kuona ila sio mbaya safi tu.
 
SEHEMU YA SITA

Hapa tunakaribia Somanga, na hapa tupo lilipopita bomba la gesi lililotoka Mtwara.ndiyo maana unaziona hizi stations
nilimjibu.

Oh waoooh, kumbe tupo Somanga wakati tunakuja huku niliona Kuna samaki wengi wa maji chumvi, sorry tunaweza kusimama ili ninunue angalau wa mboga? aliniuliza huku akiniangalia kwa aibu na tabasamu lake zuri, Mashallah.

Sawa, tukifika utanunua utakacho ondoa shaka. nilitamani nimuulize maswali kadhaa lakini nikawa naona kama atanichukulia visivyo.

Tulifika Somanga tukashuka Kisha nikamuacha anaongea na akina mama ambao walikuwa na mabeseni yenye samaki, na Mimi nikaulizia Bar iliyo karibu ili nishtue akili yangu ikae sawa maana tangu jana yake usiku sikuonja
Nilichukua safari za kopo nne huku mbili nikipiga pale pale , nyingine nikaja nazo kwenye gari.

Jamani dada yangu unenunua samaki wengi kwa ndugu yangu basi niungishe na Mimi maana tangu asubuhi sijauza kitu eeh, samaki Hawa ni elfu mbili mbili lakini Mimi nitakuuzia watatu kwa elfu tano.
ni mwanamke mmoja alikuwa anambembeleza yule mwanamke anunue samaki na kwake.

Hapana dada siku nyingine nitakuungisha maana Hawa wametosha na hata hela nimeishiwa. alijibu yule mwanamke.

Shemeji hebu mwambie mkeo aache ubahili ongezeni mboga hiyo jamani.
alinigeukia Mimi yule muuza samaki huku akiropoka kwa kumuita yule mwanamke mke wangu.

Nilitoa burungutu la hela na kutoa noti ya elfu kumi, wengine wanaita msimbazi, waliovurugwa zaidi huita albino na wengine huita mwekundu.

Hebu nifungie wa hela hii yote. nilihimiza.wakati huo yule mwanamke alikuwa anaongea na simu pembeni huku akionekana akibishana na mtu.

Nakupa jumla ya samaki sita na pia nakuongeza na huyu mdogo. Ubarikiwe sana kaka yangu, Sasa vipi si nimpe wifi au. aliuliza yule muuza samaki.

Hapana hawa wananihusu mimi. Nilimjibu kisha nikachukua na kuhifadhi kwenye gari, kisha yule mwanamke akapanda kwenye gari huku akiwa bado anaongea na simu ambayo niligundua haikuwa ya heri.
Nikakanyaga chuma huku nikiangalia saa yangu maana niligundua giza limeshachanganya.

Lakini kumbuka nilikataa kitendo cha wewe kusema nitangulie, hebu acha hizo habari mume wangu, Mimi sidhani kama unapaswa kulaumu chochote halafu jua kuwa kunifikiria hivyo ni kunikosea heshima, moja kwa moja najua huniheshimu.
Jaribu kuwa na Imani mume wangu, na unajua fika mwezi huu nitahamishiwa sehemu nyingine na nitakuwa mbali na wewe eeh hapo jiulize Nini kitajiri?
Punguza wivu. yule mwanamke aliongea huku akiwa anaangalia nje kama vile hataki mazoea na Mimi.

Nikavunja ukimya,
Vipi shemu salama lakini, naona kama si kwema.

Ah nyie wanaume huwa mna matatizo sana, tena mno, eti anapiga simu mara ooh usije lala njiani, mara ooh mko wapi, mara nitampigia simu mpangaji wetu nijue kama umefika,mara kwani hupatikani,Ina maana yeye hajui kama nipo kwenye gari sometimes network inakosekana? na yote hayo ya nini, si kunidhalilisha huko jamani.kwahiyo na mpangaji ajue mimi nachungwa.,
alilalamika yule mwanamke.

Kwanza nilishangaa huku nikijizuia kucheka Kisha nikamwambia,
Mimi nadhani Mr hana nia mbaya sana na wewe,ni mkewe anajaribu kukuelezea hisia zake, na pia anakupenda sana, tena nilivyowaona tu njiani na hata mlivyokuwa mnakumbatiana Kila saa hakika niligundua mnapendana sana. Hivyo hupaswi kuchukia maana hiyo ni neema kwenu wote wawili.

Mimi hapa tangu asubuhi mke wangu hajanipigia simu, Wala hana shida ya kutaka kujua niko wapi, Sasa haya ni mapenzi gani, unadhani si tunaishi tu, yaani ndoa yetu ni kama gari la kusukuma. Niliweka kituo na kumfanya yule mwanamke acheke na nikafanikiwa kuona meno yake mazuri baada ya kuongea vile ili atulie.

We shemeji wee usinichekeshe, lakini nimependa mnavyoishi na mkeo, binafsi Mimi ndiyo nataka siyo simu Kila saa kama watoto wadogo na malimbukeni, tena mnamisiana vizuri sana. alijibu huku nikigundua kashakuwa sawa na hasira zimemtoka.

Kisha akanitupia swali ,
Kwani shemu wewe unafanya kazi gani? maana sijakusoma kabisa mwanzo tulivyokutana na sasahivi ni watu wawili tofauti. Kisha akaweka uso ule wa kusubiri majibu akiwa kama kakunja vindita vyake huku uzuri Ukiwa pale pale.

Mimi ni mkulima tu, na huko nilikotoka nilikuwa natafiti kuhusu ni kilimo gani kitanitoa, si unajua Harakati za maisha tena. nilimjibu kwa kudanganya kama walivyonidanganya wao mwanzo.

Mmmh shemuuuu ila haya bwana tuachane na hayo, Mimi naitwa mama Anifa na wewe unaitwa nani. aliuliza.

Sasa shemu tukianza kuitana kwa majina ya watoto wetuuu, inaniwia vigumu sana, ila anyway naitwa
Daniel, wengine wanakatisha kwa kuniita Dani, lakini wahuni wangu wananiita D. nilimjibu.

Akazidi kucheka, ila shemu unanifurahisha sana yaani una visa tofauti na nilivyokuona mwanzo, na ule mkofia wako, najua umekataa nisijiite mama Anifa, ok naitwa Fatma. wanaoniweza sana wanafupisha kwa kuniita Fetty. alijibu huku tukiangaliana tukacheka.

Nilifika Geti la maliasili Muhoro tukiwa tumeiacha rasmi wilaya ya Kilwa tumeingia wilaya ya Rufiji.
askari wa pale getini waliniruhusu nipite tu licha ya magari mengine hata madogo kusimama labda kwasababu ya aina ya Plate number ya gari nililokuwa nalo.

Nilimpa kopo moja la beer lakini alikataa katakata
Heee shemu samahani kumbe huwa hutumii nisamehe bwana.nilijifanya mstaarabu huku nikiigida mwenyewe na kutupa kopo nje.

Hapana huwa natumia sana tu, ila huwa nakunywa nikitulia, halafu si umeona ninavyochungwa, hivi nikifika nyumbani halafu wambea wakagundua nina harufu ya pombe huoni mambo yanaweza kuwa mengi mtu mwenyewe yule ana wivu kama nini. aliweka kituo.

Mmmh pole sana shemeji yangu,ila nimependa msimamo wako, unampenda sana mumeo,
halafu mume wako alinionesha kitambulisho anaonekana ni askari, je wewe unafanya kazi gani, au taaluma yako ni ipi. niliuliza.

Halafu yule naye, yaani upolisi sijui huwa anauchukuliaje, mambo mengine kujifedhehesha tu, na nimekuwa nikimshauri asipende kutaka Kila mtu ajue kazi yake kama hakuna ulazima, sema ndiyo hivyo hakuna namna nitafanyaje,
Ok, Mimi mwenyewe ni askari pia nafanya kazi TANAPA, tangu niajiriwe mwaka huu wa nane sasa. alijibu

Ah kumbe wote mmekutana mapot watupu hongereni sana jamani. nilimpongeza huku akicheka na kudai mbona ni kazi za kawaida sana halafu wote hawana vyeo vya juu.ni kwamba bado wanapambana kwani kazi zao hazina tofauti na vibarua

Ajira ni Ajira tu, Mimi hata niwe na mtaji wa biashara ya mabilion bado nitakuwa kwenye ajira tu, nimekuwa kama kilema yaani, Sasa wewe ukiniambia kazi yako ni ya kawaida kwangu nakataa, usije ukaacha kazi yako kwa tamaa za muda mfupi labda umepata mtaji halafu ukadharau ajira yako, usifanye hivyo hata kama unalipwa laki moja kwa mwezi, muhimu tarehe zikifika mambo yanakaa freshi. nilimshauri asijishushe.

Ila wewe hutaki niijue kazi yako, kusema wewe ni mkulima si kweli ,waweza kuwa umetoka kutafuta fursa hiyo au ni mkulima tayari, lakini naamini una kazi yako hebu niambie bwaaana. aliniuliza huku akinilegezea sauti ili niingie mkenge lakini alishachelewa. Majirani zangu wenyewe hawajui kazi yangu kwanini nimwambie mtu baki
halafu ili iweje, mambo mengine ni kama ulimbukeni tu.

Mimi bwana ni afisa kilimo na mifugo hii ndiyo taaluma yangu, na ndiyo maana natoka kufanya utafiti unaohusiana na kazi yangu.nilidanganya na akaonesha kuridhika
Japo kidogo nijichanganye baada ya yeye kuniomba namba ili siku niende kwake nikawaone ng'ombe wa maziwa anaofuga,na nimshauri mambo yahusuyo ufugaji.si nimemwambia Mimi ni afisa wa mifugo.

ila nikaona ni freshi tu nitajua wapi nitatokea baadaye, mimi taaluma yangu ni Chuma, kipindi hicho mimi niite ikiharibika Excavator yako, nije nikusetie Hydraulic pipe na vitu vingine vya mechanics
Mimi na mifugo wapi na wapi.

Naomba nipigie ili nipate namba yako kabisa shem, nilimwambia baada ya kuwa kaniomba mwenyewe namba yangu, wakati nikiangalia simu kama kweli kapiga maana niliiset simu kwenye meeting, sikuona mbele vizuri na taa za gari sikuwasha full, lahaulaaaa nipo kwenye Kona ,gari ipo speed mara kundi la ng'ombe hili hapa, linavuka barabara, jamaaani usiku huu ng'ombe wanatoka wapiiiiiiiih?
Wanasema usinywe pombe Kisha ukaendesha gari, Sasa Mimi nilikuwa naendesha huku nakunywa.
Nini kitatokea? next episode ina majibu, enjoy.

Itaendelea....................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom