Simulizi: Harakati za Jason Sizya

fungate.jpeg

115

Pole sana Jason…


Saa 10:30 jioni…

JASHO jingi lilikuwa linanitoka kwenye paji la uso wangu. Muda wote nilikuwa nimetulia kwenye sofa sebuleni katika nyumba yangu iliyokuwa eneo la Mwime Manispaa ya Kahama, huku mkono wangu wa kuume ukiwa umeshikilia chupa kubwa ya pombe kali aina ya Grant’s Blended Scotch Whisky na mbele yangu kulikuwa na meza ndogo ya kioo.

Chini ya ile meza ndogo ya kioo kulikuwa na chupa tupu kadhaa zikiwemo za Konyagi, Savanna na Heineken. Hadi muda huo nilishakunywa aina tofauti za pombe, kwanza kabisa nilikunywa Savanna mbili ambazo nilizigida kama maji. Kisha nilichukua Heineken na kunywa yote lakini bado nilihisi akili yangu ilikuwa na mawenge, nikachukua Konyagi ndogo. Nilipoimaliza nikahisi bado ‘stimu’ ilikuwa haijapanda ndipo nikachukua chupa kubwa ya Grant’s Whisky.

Macho yangu yalikuwa mekundu yanayorembua na sura yangu ilionesha uchovu mkubwa, kwa yeyote ambaye angeniona asingeshindwa kubaini kuwa nilikuwa nalia na sikuwa nimepata usingizi wa kutosha kwa takriban juma zima. Na sikuwa mtu mwenye nguvu.

Nikiwa pale sebuleni, nilikuwa nimevaa fulana nyepesi nyeupe na bukta nyekundu ya kitambaa cha kadeti. Rafiki yangu Swedi Mabushi alikuwa ameketi kwenye sofa lililokuwa jirani na lile nililokalia na alikuwa ananiangalia kwa huzuni.

Swedi alikuwa amepita nyumbani kwangu kunijulia hali baada ya kutoka kazini na nilikuwa na uhakika kuwa alifahamu kile ambacho nilikuwa napitia. Alikuwa anafahamu namna gani ambavyo nilikuwa nimeumizwa na kile kilichotokea wiki chache nyuma kufuatia ule mkasa ambao uliandikiwa hadithi ya ‘Narudi Buzwagi’, na ilikuwa vigumu sana kuukubali ukweli. Ukweli ulikuwa mchungu kuumeza.

“Jason, inakupasa sasa uache jambo hili lipite…” Swedi aliniambia kwa sauti tulivu ya kirafiki na yenye kusihi kisha aliongeza, “kuendelea kulibeba jambo hili moyoni mwako hakutaleta lolote jema zaidi ya maumivu. Sawa, Jason?”

Sikuweza kumjibu bali nilitikisa kichwa changu taratibu na kunywa funda kubwa la whisky kisha nikatazama sakafuni nikiwa mwingi wa fikira. Macho yangu yaliendelea kudondosha machozi. Hata hivyo kulikuwa na sauti fulani ndani yangu iliyoniambia kuwa nilipaswa kumsikiliza Swedi kwani kwa kutofanya hivyo ningezidi kuumia.

Niliipuuza sauti hiyo kwa kuwa suala hilo lilikuwa gumu mno kwangu. Moyo ulikuwa unaniuma sana.

Kuchanganyikiwa ni jambo linalotarajiwa kwa binadamu hasa pale mtu anapokata tamaa ya maisha au kuelemewa na msongo wa mawazo. Mimi pia nilihisi kuchanganyikiwa na akili yangu ilikuwa haifanyi kazi yake sawa sawa. Sikuwa na namna nyingine ya kufanya isipokuwa kunywa pombe nikidhani ningeweza kupunguza msongo wa mawazo. Yote niliyoyafanya yalifanyika sanjari na mawazo yaliyokuwa yakiisonga akili yangu.

Nilikuwa nimepoteza kabisa hamu ya chakula na hata ufanisi wangu katika kazi ulianza kupotea taratibu kwa sababu ya mawazo mengi yaliyonifanya niwe mtu wa kukata tamaa.

Tangu nikumbwe na masaibu mwili wangu ulianza kupungua, na kwa kweli sikujua nifanye nini! Kuna wakati nilihisi sikuwa na sababu ya kuendelea kuishi katika dunia ambayo iliamua kuniadhibu pasipo huruma, ingawa jamaa zangu hususan kaka yangu Eddy Sizya na rafiki yangu Swedi walijitahidi sana kuwa karibu nami kwa kila hali.

Mawazo yaliyonisonga yalisababisha niwe mlevi wa kupindukia kwa kuwa nilishindwa kukubaliana na kile kilichotokea, sikujua nifanye nini ili niweze kuirudisha furaha yangu iliyopotea na hali irudi kama ilivyokuwa mwanzo. Nilitamani sana kuurudisha wakati nyuma lakini jambo hilo lilikuwa haliwezekani. Waingereza husema “Life has no back space!”

Muda wote nyumbani kwangu hakukukosekana pombe kali, kuanzia K Vant, Konyagi, Whisky hadi mvinyo ghali aina ya Pinot Noir. Na kila nilipokunywa pombe niliishikilia picha ndogo ya mwanamke niliyedhani nampenda kuliko kitu chochote, picha ambayo nilikuwa natembea nayo kwenye pochi yangu.

Alikuwa mwanamke mzuri sana ambaye uzuri wake ulitosha kabisa kuudhihirisha utukufu wa Mungu kwenye sanaa ya uumbaji.

Sikuishia kutembea na picha yake tu kwenye pochi yangu bali picha nyingine kubwa za mwanamke huyo huyo nilizibandika ukutani kila mahali, kuanzia sebuleni hadi chumbani. Jikoni hadi maliwato. Karibu kila sehemu ya ukuta wa nyumba yangu kulikuwa na picha za mwanamke huyo.

Iligeuka kuwa jambo la kawaida sana kwangu kushinda ndani huku nikipitisha siku bila kuzungumza neno lolote, muda mwingi macho yangu nikiwa nimeyaelekeza kwenye moja ya picha za mwanamke huyo zilizokuwa ukutani.

Msichana huyo hakuwa mwingine zaidi ya Rehema Mpogolo, ambaye hadi muda huo hali yake kiafya ilikuwa mbaya sana, alikuwa amepooza mwili wote na kipindi chote alikuwa amelala kitandani akiupigania uhai wake, huku baba yake akiwa hataki kabisa kuniona nikiwa karibu na binti yake!

Kwangu, uamuzi wa mzee huyo ulikuwa wa kikatili sana, hakupaswa kuniachanisha na Rehema hata kama nilikuwa mkosaji. Muda mwingi mawazo juu ya mustakabali wa maisha yangu baada ya uamuzi uliochukuliwa na baba wa Rehema, yalizidi kuitesa akili yangu.

Kuna wakati Eddy na Swedi walijaribu kuziondoa zile picha za Rehema ukutani wakidhani kuwa labda kwa kufanya hivyo wangeweza kunirejesha katika hali yangu ya kawaida. Lakini kila walipojaribu kugusa moja kati ya picha hizo niligeuka kuwa mbogo kweli kweli!

Ukweli nilikuwa nimekosa mwana na maji ya moto kutokana na tabia yangu ya kumtamani kila msichana mrembo aliyepita mbele yangu. Na kila nilipopita mitaani nilijihisi kuchanganyikiwa zaidi niliposhuhudia macho ya watu yakinitazama, niliwaona kama vile walinitazama kwa namna ya kunisuta.

Tamaa yangu ya kutaka kufanya ngono na kila msichana mrembo ilikuwa imeniponza na kusababisha vifo vya wasichana watatu, kwanza kabisa ilisababisha kifo cha mwanadada Belinda Mwikongi aliyejiua kwa kunywa sumu ya panya, miaka mitatu nyuma wakati nikiishi katika Mji wa Tabora.

Na takriban miezi miwili tu ilikuwa imepita tangu vifo vya wasichana warembo, Asia na Jamila, ambao vifo vyao viliacha gumzo katika mji wote wa Kahama baada ya kutokea fumanizi lililowaacha wakazi wa Kahama mdomo wazi.

Jamila, msichana aliyeonekana kunipenda sana, alinifumania nikiwa na Asia, msichana asiye na hatia, kisha yakatokea mauaji, huku mchumba wangu Rehema akifika nyumbani kwangu muda huo huo na kushuhudia kila kitu kabla hajaanguka chini na kupoteza fahamu, na baadaye ikagundulika kuwa alikuwa amepooza mwili wake.

Ni baada ya kutokea kilichotokea ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa nampenda sana Rehema kuliko kitu chochote, ingawa mwanzoni akili yangu ilikataa kabisa kuamini kuwa duniani kulikuwa na mapenzi ya kweli. Nilidhani mapenzi ya kweli yalipatikana zaidi kwenye riwaya za mapenzi au kwenye michezo ya kuigiza tu.

Kabla ya tukio hilo la kusikitisha, nilimchukulia kiumbe aliyeitwa mwanamke kuwa alikuwepo duniani kwa ajili ya kumfurahisha na kumburudisha mwanamume tu, na hivyo katika maisha yangu kuwa na uhusiano na wasichana zaidi ya mmoja halikuwa jambo la kushangaza kabisa!

Itaendelea...
 
fungate.jpeg

116

Nilimchukua msichana niliyemtaka na nilipomaliza haja zangu niliachana naye, na ukiachana na Rehema, sikutaka kuwa na mwanamke maalumu kwa kuogopa mambo ya kuoneana wivu.

Lakini sasa maumivu makali ya moyo yalikuwa yamenivaa sambamba na mahitaji ya penzi la Rehema tu, na si penzi la msichana mwingine. Machozi yalikuwa yananitoka kila wakati nilipozikumbuka nyakati za furaha tulizokuwa pamoja na kwamba sasa Rehema alikuwa amepooza mwili wake kwa sababu ya tabia yangu chafu.

Machozi yalizidi kunitoka, tena mengi tu. Wakati mwingine machozi yalinilenga lenga au yalitoka hadharani na kushuhudiwa na watu, na wakati mwingine machozi yalinitoka hata nikiwa mbele ya watu wengine wasiostahili. Ili kujisahaulisha yote hayo ilibidi niwe nakunywa pombe kali, siku iliyotangulia nilikunywa sana, nikalewa na kujikuta nikiwa sikumbuki chochote.

Nikiwa nayatafakari yote hayo, nikaanza kuisikia sauti ya Rehema akiniita huku akilia kwa uchungu mkubwa, alikuwa analalamika kuwa nimemuumiza sana kihisia. Sauti yake ilisikika akilini mwangu na kuuchoma moyo wangu na kisha kunisababishia majuto makubwa ambayo yalidhihirika kwa sababu ya machozi yaliyokuwa yakinitoka.

Majuto hayo yaliyosababisha maumivu makali moyoni mwangu yalinifanya nijione mtu mwenye hatia na dhambi kubwa isiyosameheka.

“Naelewa, Rehema… naelewa kuwa nimekuumiza sana, naomba unisamehe mpenzi wangu na unipe nafasi nyingine niyaondoe maumivu yako,” niliongea kwa sauti ya kunong’ona huku nikiiangalia picha ya Rehema iliyokuwa mkononi kwangu katika namna ya kumaanisha kile nilichokisema.

Swedi aliniangalia kwa mshangao lakini sikumjali, nikainyanyua chupa ya Grant’s Whisky huku nikiiangalia kwa uchungu na kuigugumia pombe yote iliyokuwemo kwenye chupa kama maji na kisha nikaikita chupa tupu juu ya meza ndogo ya kioo pale sebuleni. Kisha nikajiegemeza kwenye sofa, macho yalizidi kuwa mekundu kwa kulia na ulevi juu.

“Mungu wangu!” Swedi alisema huku akinitazama kwa mshangao mkubwa. “Jason, hiyo pombe kwenye chupa umeimaliza? Mungu wangu!”

Sikumjibu kitu zaidi ya kumkodolea macho huku machozi yakizidi kunitoka.

“Dah, najua unapitia kipindi kigumu sana, lakini huna sababu ya kujikatia tamaa kiasi hicho,” Swedi aliniambia huku akiinuka na kuinyanyua ile chupa kubwa ya Grant’s Whisky huku akiiangalia kwa mshangao, kisha akairudisha juu ya meza.

Bado sikusema neno, na wakati huo mvinyo ulikuwa unashuka taratibu kwenye koo langu, nilianza kuwaza huku akili yangu ikijaribu kuwachambua wasichana wote niliowakumbuka, maana shida kubwa ilikuwa ni kuwakumbuka wasichana wote niliowahi kutoka nao kimapenzi. Hata hivyo, bado sikumwona msichana yeyote aliyeweza kufikia kiwango cha upendo wa Rehema kwangu. Hisia zangu ziliniambia kuwa nisingeweza kumpata mwanamke mwingine kama Rehema.

Mimi na Rehema tulikuwa na historia ndefu ya pamoja, tangu tulipokuwa katika umri wa utineja ingawa penzi letu lilikuwa katika mizania isiyolingana, kwani Rehema alikuwa ananipenda sana lakini sikuwa nimetulia kabisa. Ukweli Rehema alikuwa ananivumilia kwa mengi.

Mawazo hayo juu ya Rehema yalinifanya nianze kuhisi hali yangu ikianza kuwa mbaya kadiri sekunde zilivyokuwa zinayoyoma na kichwa changu kikiwa kizito mno kama niliyebebeshwa mzigo mzito kichwani nisioweza kuumudu. Macho yangu nayo yalianza taratibu kupoteza nguvu ya kuona, ukungu mwepesi ulianza kutanda kwenye macho yangu na kunifanya nianze kuona vitu vyote kama vivuli.

Nilimwona Swedi akinitazama kwa wasiwasi mkubwa kisha aliinuka na kunisogelea huku akinisemesha lakini nilikuwa namsikia kwa mbali sana na sikuweza kujua alikuwa anaongea nini! Nilijitahidi kuyakodoa macho yangu kumtazama lakini sikumwona vizuri zaidi ya kuona kitu mfano wa taswira ya mtu kwenye ukungu mzito ikiwa imenisimamia mbele yangu.

Nilitamani kuufungua mdomo wangu ili niombe msaada lakini nikajikuta nikiishilia kufumbua mdomo tu huku ile sauti ikigoma kabisa kutoka na hivyo kuishilia akilini mwangu tu, na hapo nikaanza kuhisi shughuli za mwili wangu nazo zilikuwa mbioni kusitisha utendaji wake. Nikajiuliza kitu gani kilikuwa kinanitokea lakini kabla sijapata jibu nikaanza kuhisi mwili wangu ukilegea na kuishiwa nguvu taratibu.

Nilitamani sana kufumbua macho yangu na kuona nini kilichokuwa kinanitokea lakini hilo halikuwezekana kwani macho yangu yalizidi kuwa mazito sana na hatimaye usingizi mzito sana ukaanza kuninyemelea.

* * *



Saa 2:10 usiku…

Sikujua nini kilikuwa kimenitokea, na pia sikujua ilikuwa saa ngapi zaidi ya kugundua kuwa nje kulikuwa na giza na taa zilikuwa zinawaka, nilishtukia tu nikiwa nimejilaza juu ya mapaja ya Amanda, na tulikuwa wawili tu pale sebuleni nyumbani kwangu Mwime. Pua zangu zililakiwa na harufu nzuri ya manukato yaliyokuwa yanahamasisha ngono.

Nilishtuka na kutaka kuinuka lakini kichwa changu hakikuniruhusu kufanya hivyo kwani kilikuwa kinauma sana. Amanda alikuwa ananitazama kwa macho yaliyojaa huzuni.

Kwa sekunde kadhaa shughuli za mwili wangu zilisimama huku macho yangu yakikataa kuamini kuwa mwanamke aliyekuwa ameketi pale kwenye sofa sebuleni kwangu akiwa amenilaza kwenye mapaja yake laini alikuwa Amanda.

Maswali yalianza kupita kichwani kwangu nikijiuliza alifikaje pale nyumbani kwangu na nini kilikuwa kimenitokea hadi nikawa katika hali ile, lakini sikupata jibu. Hata hivyo, tabasamu jepesi la matumaini nililoliona usoni kwa Amanda liliufanya moyo wangu utulie kidogo.

Amanda, mwanadada mrembo mwenye umbo la namba nane alikuwa katika mwonekano tofauti kabisa wa kupendeza, alikuwa amevaa gauni fupi jepesi la rangi ya maruni la kukata mikono lililohifadhi vyema umbile lake la namba nane na kuishia sentimita chache juu ya magoti yake huku likiyaacha nusu wazi mapaja yake.

Mdomo wake laini ulikuwa umekolea vizuri lipstick ya rangi ya chokleti na hivyo kuifanya sura yake ya duara yenye pua ndogo izidi kupendeza. Nyusi alikuwa amezitinda vizuri na kuzipaka wanja, na kope zake zilirembwa vyema na hivyo kuyafanya macho yake makubwa kidogo na malegevu yenye kung’ara kama nuru yaonekane vizuri na kupendeza.

Nilimtazama Amanda kwa umakini, kwa kweli alikuwa amependeza sana. Mkufu wake mwembamba wa dhahabu ulikuwa umeizunguka shingo yake nyembamba na kidani chake kikapotelea katikati ya uchochoro mdogo uliofanywa baina ya matiti yake ya wastani yenye chuchu nyeusi na imara zilizosimama kikamilifu ndani ya gauni lake jepesi.

“Pole sana Jason…” Amanda aliniambia baada ya kugundua kuwa nilikuwa nimerudiwa na fahamu zangu.

Sikumjibu, hata hivyo alinisaidia kuinuka na kuniketisha pale kwenye sofa kisha akainuka haraka na kuelekea jikoni, baada ya sekunde chache alirudi akiwa ameshika bilauri ya maji ya baridi yaliyochanganywa na ndimu na kunipa.

“Kunywa maji haya, yatakusaidia. Umekunywa pombe nyingi sana,” Amanda alisema kwa sauti nyororo ya upole.

Niliipokea ile bilauri ya maji pasipo kuhoji chochote, nikayanywa maji yote na kumrudishia ile bilauri huku nikijiangalia, nikagundua kuwa nilikuwa nimevalia bukta nyeusi na kifua changu kilikuwa wazi huku kichwani nikiwa nimelowana. Nilipatwa na mshangao mkubwa nikijiuliza kulikoni! Sikuweza kukumbuka kilichotokea kabla.

“Pole!” Amanda aliendelea kunipa pole huku akinitazama kwa huzuni.

“Kwani nini kimenitokea?” nilimuuliza Amanda huku mshangao ukijionesha wazi usoni kwangu.

“Umetapika sana, yaani sana! Ulikunywa pombe nyingi mno, Jason,” Amanda aliniambia huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Ndiyo… sasa kumbukumbu zangu zilianza kurudi taratibu, nilikuwa nimerudiwa na fahamu na hisia zangu zilinitanabaisha hivyo huku nikikumbuka vizuri, ila nilihisi maumivu makali sana ya kichwa.

Itaendelea...
 
fungate.jpeg

117

Nilikumbuka vyema na picha nzima ya kilichotokea ilikuwa ikipita kichwani kwangu kama niliyekuwa natazama filamu. Nilikumbuka jinsi nilivyokuwa nakunywa pombe kali aina ya Grant’s Whisky kama maji baada ya kunywa Konyagi, Savanna na Heineken.

Muda wote Swedi alikuwa ameketi kwenye sofa lililokuwa jirani akinitazama kwa huzuni. Na baadaye nilianza kuhisi hali yangu ikianza kuwa mbaya kadiri sekunde zilivyokuwa zikiyoyoma na kichwa changu kikiwa kizito mno. Kisha macho yangu yalipoteza nguvu ya kuona na ukungu mwepesi ulitanda kwenye macho yangu…

Hivyo tu! Ni hivyo tu ndivyo nilivyovikumbuka, hakuna kingine isipokuwa kuwa na Swedi pale sebuleni, na kugida pombe kama maji, basi! Nilipojaribu kukumbuka mambo mengine kichwa changu kiligoma kabisa kuyakumbuka!

Amanda alionekana kama aliyekuwa anataka kuniambia kitu lakini alikuwa anasita kusema.

“Swedi yupo wapi?” nilimuuliza Amanda huku nikimwangalia usoni kwa umakini.

“Ameshaondoka baada ya kuhakikisha uko salama. Ulitapika sana na nguo zote zimechafuka,” Amanda aliniambia kwa sauti ya upole huku akinitazama kwa namna ya upendo kama vile mama amtazamaye mwanawe wa pekee.

“Duh! Sasa ilikuwaje wewe ukawa hapa saa hizi wakati haukuwepo?” nilimuuliza Amanda kwa wasiwasi.

“Ni hadithi ndefu kidogo, ni vyema ukapumzika kwanza ili upate nguvu, baadaye tutazungumza,” Amanda aliniambia kwa sauti ya upole katika namna ya kunitia moyo.

“Unajisikiaje kwa sasa?” Amanda aliniuliza huku akijiweka vizuri pale kwenye sofa.

“Najisikia nafuu kidogo ingawa kichwa kinauma sana na ninahisi njaa,” niliongea kwa sauti tulivu huku nikipiga mwayo hafifu.

“Usijali, nimeshaandaa chakula ambacho naamini utakipenda,” Amanda aliniambia huku akinitazama kwa utulivu na kisha akaachia tabasamu. Taratibu akaanza kunikandakanda misuli ya mapajani na kunifanya nijisikie faraja.

Baada ya kitambo fulani cha kunikandakanda aliinuka na kuniacha pale kwenye sofa akaelekea jikoni. Mara tu alipoondoka nilijikuta nikiupisha utulivu kichwani mwangu. Nilipoitazama saa yangu ya mkononi nikagundua kuwa ilikuwa inaelekea kutimia saa 2:20 usiku. Nikajiuliza ilikuwaje Amanda akawepo nyumbani kwangu muda huo baada ya kile kilichokuwa kimetokea kati yetu?

Mimi na Amanda tulikuwa tumehitilafiana baada ya kumkuta na akiwa na mwanamume mwingine mjini Ushirombo, na wakati huo mimi pia nilikuwa na Rehama. Kilichoniudhi zaidi ilikuwa ni baada ya kugundua kuwa mwanamume huyo alikuwa mbioni kumuoa.

Baadaye nikaja kusikia tetesi kuwa Amanda na mwanamume huyo waliingia kwenye mgogoro mkubwa baada ya mwanamume huyo kugundua kuwa Amanda alikuwa bado ananipenda kuliko mwanamume yeyote aliyewahi kukutana naye. Hii ilidhihirika baada ya mkasa ulionipata wa kupigwa risasi kifuani na Jamila siku nilipokuwa nyumbani kwangu na Asia baada ya kutokea mtafaruku kati yetu.

Kipindi chote nilichokuwa nimelazwa hospitali Amanda alikuwa anakuja kuniona na alishinda pale hospitali akisaidiana na Mama na shemeji Emmy, mke wa kaka Eddy, wakinihudumia.

Kitendo cha kuonesha kuwa alikuwa ananipenda sana kilimfanya mwanamume huyo kuingiwa na wivu na kusababisha ugomvi kila siku na ilifikia hatua mwanamume huyo aliamua kuachia ngazi na hivyo Amanda akarudi kwao. Hata hivyo, bado kwangu ilikuwa vigumu sana kumrudisha Amanda moyoni mwangu.

Mara kwa mara Amanda alikuwa analia kila aliponiona nikiwa nimekata tamaa, aliahidi kufanya kila jitihada ili ahakikishe ninapona majeraha ya moyo wangu yaliyosababishwa na mkasa ulionipata hasa kitendo cha kuwa mbali na Rehema. Na kweli mwanzoni alikuwa anafika nyumbani kwangu kila asubuhi, akanifulia nguo, akasafisha nyumba yangu na kunipikia. Alikaa hapo hadi jioni akihakikisha nimekula ndipo alipoondoka kurudi nyumbani kwao Uwanja wa Taifa.

Baadaye alipunguza kuja nyumbani kwangu ingawa alichokuwa anakifanya ni kununua muda kwa kuamini kuwa kidogo kidogo ningeuona umuhimu wake na pengine ningerudisha upendo na hatimaye tungeoana.

Kaka yangu Eddy na rafiki yangu Swedi, kwa nyakati tofauti walinishauri kumuoa Amanda aliyekuwa anaonesha upendo mkubwa kwangu na kumsahau Rehema, lakini bado akili yangu ilishindwa kukubaliana na jambo hilo. Niliamini kuwa nilikuwa nimezaliwa kwa ajili ya Rehema na Rehema alizaliwa kwa ajili yangu. Basi!

“Oh Rehema! Nisamehe mpenzi wangu,” niliwaza huku machozi yakianza kunitoka hasa kila nilipokumbuka vitendo vibaya nilivyomfanyia. Machozi yakazidi kunimwagika usoni mwangu. Majuto ambayo niliyasikia moyoni mwangu kusema kweli yalianza kuniumiza sana.

“Jason, mbona unalia?” sauti ya Amanda ilinishtua sana toka kwenye mawazo yangu, nikayapangusa.

Muda huo Amanda alikuwa amesimama akinitazama kwa umakini baada ya kuweka taratibu trei kubwa iliyosheheni vyakula juu ya meza ndogo ya kioo na kisha akaisogeza mbele yangu, halafu akakaa pembeni yangu huku akinitazama usoni mwangu.

“Jason, unapaswa kuwa jasiri na kujitahidi kusahau, haya nayo yatapita tu,” Amanda aliniambia kwa sauti ya upole huku akiniangalia usoni. Nilibaki kimya nikiwa naangalia chini.

“Jason!” Amanda aliniita huku akinishika mashavu yangu, na kunigeuza uso wangu sehemu alipokaa. Tukatazamana kwa muda pasipo kuzungumza chochote.

“Nimekufahamu kwa muda mrefu sasa na hata hisia zangu nilizikabidhi kwako, sijali kama leo unanichukia au lah, ila ukweli utabaki kuwa nilikupenda, ninakupenda na nitakupenda maisha yangu yote. Kwa nini unakuwa mnyonge kiasi hiki?” Amanda alizungumza kwa sauti ya upole iliyojaa unyonge ndani yake.

“Naomba niache nile,” nilimwambia Amanda huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani kisha nilichukua sahani ili nijipakulie chakula. Sikutaka kumpa nafasi ya kunisaili kwa sababu nisingeweza kuyajibu maswali yake.

“Samahani kama nimekukwaza,” Amanda alisema kwa unyonge huku akishusha pumzi na kuninyang’anya ile sahani.

Kisha alifumba macho yake na kuanza kukiombea kile chakula na alipomaliza kuomba akachukua kijiko kikubwa na kupakua chakula kwenye sahani na kunipa huku akinikaribisha. “Karibu.”

Nilipokea ile sahani na kugundua kuwa alikuwa ameandaa wali wa nazi, mchuzi mzito wa kuku ulioungwa kwa nazi pia. Bakuli la mboga za majani pembeni, na sahani yenye matunda aina ya nanasi, embe na vipande vya tikiti maji vilivyokoza wekundu. Pia kulikuwa na jagi la maji baridi.

Nilishangaa sana maana sikujua Amanda alikiandaa chakula kile muda gani, nilitaka kumuuliza lakini nikasita. Nilianza kula kwa kasi huku nikiwa nimejawa na uchungu mwingi kwenye moyo wangu. Nilikuwa nayakumbuka mambo mengi ambayo nimeyafanya na Rehema, ahadi nyingi ambazo nilipanga na Rehema lakini nikaishia kumlipa ubaya na kumsababishia kulala kitandani akiwa nusu mfu kwa tamaa zangu za kimwili.

Hata hivyo nilijikuta nikishangaa, kwani pamoja na mawazo mengi kuniandama lakini chakula kilikuwa kinashuka vilivyo kooni kwangu kutokana na ustadi wa mapishi. Kwa kweli kilikuwa chakula kitamu sana na Amanda alikuwa msichana fundi wa kupika ingawa akili yangu iliyakubali zaidi mapishi ya Rehema.

Amanda naye alikuwa amejipakulia chakula kwenye sahani yake na kuketi kando yangu, akawa anakula kimya kimya huku akinitupia jicho la wizi. Nilimaliza kula kisha nikashushia na matunda halafu maji. Amanda akanipa kimbaka ili kuondoa masalio ya chakula kwenye meno yangu. Moyoni niliyasifia mapishi ya Amanda ingawa sikumweleza waziwazi.

Hadi muda huo swali moja lilizidi kuitesa akili kwangu, nilikuwa najiuliza ilikuwaje Amanda akawepo nyumbani kwangu muda huo! Au ni Swedi alikuwa amempigia simu? Nilitamani kumuuliza lakini nikasita. Nilichofanya ni kumshukuru kwa chakula kitamu alichonipikia. Nilihisi huenda alifanya hivyo kwa matarajio kuwa pengine angefanikiwa kuuteka tena moyo wangu ingawa haikuwa hivyo, kwani nilimwona kama dada yangu badala ya mpenzi.

Niliiangalia saa yangu nikagundua kuwa ilikuwa imeshatimu saa 3:15 usiku, nikamwambia Amanda kuwa nilihitaji kuwa peke yangu. Ingawa alionesha kusita sana lakini hakuwa na namna ya kufanya kwani sikuhitaji kuwa na mwanamke yeyote ndani ya nyumba yangu wakati huo. Kwa shingo upande Amanda aliinuka ili aondoke.

“Jason!” Amanda aliniita huku akiniangalia usoni.

“Naam!” niliitika huku nikiwa simwangalii usoni.

“Naomba tu uniambie kama kuna jambo lolote baya sana ambalo nimekufanyia!” Amanda aliniuliza huku akionekana mnyonge zaidi.

“Kwa nini?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni kwa umakini.

“Nahisi kama vile umekuwa hufurahii uwepo wangu nyumbani kwako, na kila ninachokuongelesha unanijibu kwa mkato tu ukionekana kutawaliwa na hasira! Ni kosa lipi lisilosameheka nililokufanyia?” Amanda aliniuliza huku akijitahidi kuyazuia machozi yaliyoanza kumlenga lenga.

“Wala hujanifanyia jambo lolote baya, ni kwamba mara nyingi nikiwa katika hali ya namna hii huwa sipendi kuzungumza na mtu. Ninapenda kuwa peke yangu,” nilimjibu Amanda huku nikijitahidi kuifanya sauti yangu iwe ya kawaida isiyo ya hasira.

Okay! Basi ngoja nikuache… usiku mwema,” Amanda alisema na kuanza kupiga hatua zake taratibu kuelekea mlangoni huku machozi yakianza kumtoka. Sikupenda kumwona akiondoka katika hali ile ya huzuni, ikanibidi nimuwahi.

“Amanda!” nilimwita huku nikipiga hatua kumfuata, akageuka kunitazama huku akifuta machozi. “Naomba unielewe, sijakufukuza nyumbani kwangu na siwezi kukufukuza bali nahitaji kuwa peke yangu kwa muda,” niliongea kwa sauti tulivu baada ya kumfikia na kusimama mbele yake huku nikimtazama machoni.

“Jason, mimi ni mnyonge, najua sina thamani yoyote kwako. Ni kweli nilifanya makosa wakati fulani lakini sistahili kuadhibiwa kiasi hiki. Unajua kabisa nilikukabidhi moyo wangu nikitarajia furaha ila ninachokutana nacho sasa si kile ambacho nilikitegemea,” Amanda alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.

Kusema kweli maneno yake yalipenya moja kwa moja hadi moyoni mwangu, taratibu nikamvuta hadi karibu na mwili wangu na kumkumbatia huku nikimfuta machozi kwa vidole vyangu.

“Usihuzunike, nipe muda tu natumaini mambo yatakaa sawa,” nilisema huku nikimwachia.

Tukaangaliana kwa kitambo fulani kila mmoja akiwa kimya, na baada ya kitambo kile Amanda akaachia tabasamu lililoonekana kubeba uchungu ndani yake na kisha akafungua mlango na kuondoka zake. Na mara tu nilipobaki peke yangu mawazo yangu juu ya Rehema yakaibuka upya.

Ukweli ni kwamba niligundua kuwa nilikuwa nampenda Rehema kwa dhati ya moyo wangu. Kumbukumbu juu ya Rehema zilipita akilini kwangu, nilikumbuka nyakati za raha pindi tulipokuwa pamoja, nikakumbuka pia nyakati za mgogoro. Kisha nikazipima nyakati hizo katika mizania kwa lengo la kutafuta uwiano. Raha zilizidi shida kwa uzito usio na hata chembe ya mnuso!

Kwa matokeo hayo nilijiaminisha kuwa; Rehema ndiye alikuwa mwanamke wa maisha yangu.

“Kama alikuwa mwanamke wa maisha yangu, ilikuwaje nikamsaliti na wanawake wengine?” niliwaza. Hata hivyo, jawabu lilikuwa fupi tu, kwamba sikuitambua thamani yake hadi baada ya kumpoteza katika maisha yangu.

* * *

Itaendelea...
 
fungate.jpeg

118

Jason Stop!


Saa 1:30 asubuhi…

NILIKUWA nimekaa kwenye sofa dogo sebuleni huku uso wangu nikiuelekeza juu ya dari ilihali macho yangu nikiwa nimeyafumba. Mawazo yalikuwa yamekitawala kichwa changu huku chupa kubwa ya Whisky aina ya Jack Daniel’s ikiwa mkononi kwangu.

Ndani ya chupa hiyo mlikuwa na pombe shinda, baada ya kuwa nimekwisha kunywa nyingine. Kama kawaida, mara kwa mara nilikuwa naiongelesha picha kubwa ya Rehema iliyokuwa imetundikwa ukutani. Japokuwa kuna wakati nilijaribu sana kumsahau Rehema lakini haikuwezekana kabisa.

Usiku wa kuamkia siku hiyo sikuweza kupata usingizi. Usiku ulikuwa mrefu sana! Usiku kucha nilikuwa nagaagaa kitandani kwangu nikiutafuta usingizi lakini sikuweza kuupata kutokana na mawazo juu ya Rehema.

Kila nilipoziona picha za Rehema zilizokuwa ukutani, au nguo zake ndani ya kabati langu la nguo kumbukumbu zake zilipita akilini kwangu na kunifanya nihisi akili yangu ikishindwa kufanya kazi yake sawa sawa.

Wakati nikiwa kitandani usiku niliishia kujigeuza tu; mara kushoto, mara kulia, nililala chali na kuna wakati nililala kifudifudi lakini bado usingizi haukunijia. Kumbukumbu ya tukio la Asia kupigwa risasi mbele yangu na baadaye Jamila kujiua kwa sumu, huku Rehema akiwa taaban kitandani baada ya kupatwa na kiharusi ilikuwa inajirudia kichwani kwangu kama filamu.

Niliinuka, nikakaa kitako nikiwa pale pale kitandani huku nikiukumbatia mto, “Rehema… you are such an amazing woman!” nilinong’ona.

“Wewe ni mwanamke wa ndoto yangu. Una kila kitu ninachokihitaji kwa mwanamke wa ndoto yangu,” nilijisemea na kisha taratibu nikarudi kulala.

Kisha nikaanza kuwaza kuhusiana na mustakabali mzima wa maisha yangu, kuhusu nilikotoka, niliko na nilikokuwa ninakwenda. Nilijiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa na laana. Macho yangu yalikuwa yanatoa machozi pasi na kupenda.

Mara nikakumbuka jambo na kuitwaa simu yangu, nikaanza kutafuta namba ya Rehema toka kwenye sehemu niliyohifadhi majina na kuipiga ili kama ingepokelewa ningemweleza yeyote ambaye angepokea simu hiyo kuwa bado nilikuwa namuhitaji Rehema kwenye maisha yangu.

Simu ilikuwa haipatikani kwani sauti nyororo ya mwanadada aliyeniambia kuwa ‘mtumiaji wa simu ninayempigia hapatikani…’ ilisikika vyema na kupenya kwenye ngoma za sikio langu. Sikuchoka, nikajaribu tena lakini bado simu haikupatikana.

Muda huo akili yangu ilikuwa inaenda kasi sana, nikaingia tena kwenye orodha ya majina, na moja kwa moja nikabonyeza kwenye jina la Dk. Camilla Mpogoro kwa lengo la kumpigia ili nimwombe namba ya mtu yeyote aliyekuwa karibu na Rehema niweza kuongea naye.

Bado bahati haikuwa yangu kwani simu iliita sana lakini haikupokelewa. Nilipoitazama saa kwenye simu yangu, ilionesha kuwa ilikuwa imeshatimu saa 9:15 usiku!

Oh my God!” nilisema kwa mshangao huku nikiiachia simu yangu katika hali ya kukata tamaa. Taratibu nikajilaza tena kitandani. Nilijaribu kuutafuta usingizi lakini haikuwezekana. Mawazo yalizidi kutawala akili yangu.

Kuna wakati niliilazimisha akili yangu kuachana na mawazo juu ya Rehema na kuanza kufikiria juu ya msichana mwingine ili nimuoe awe mke wangu na anilindie heshima yangu mbele ya jamii. Sikujua nifanye nini, sikuwa na cha kufanya kwani akili yangu ilikwisha vurugwa na uamuzi aliouchukua mzee Benard Mpogolo, baba wa Rehema.

Mzee huyo alikuwa amefanya uamuzi wa kikatili sana kunitenganisha na Rehema bila kujali hisia zangu, na hakutaka kaabisa niwe karibu na binti yake. Japo nilijaribu kukubaliana na matokeo lakini moyo wangu uliwaka moto, na hata kichwa changu kiliwaka moto. Basi likawa balaa juu ya balaa mwilini mwangu.

Nilianza kuwaza kuwa niachane na Rehema na kutafuta msichana mwingine, kila nilipowafikiria wasichana wengine akili yangu ilihangaika kuwachambua wasichana wote niliowahi kutoka nao, mmoja baada ya mwingine, kwa kuangalia udhaifu wa kila mmoja na uimara wake na bado sikumwona yeyote ambaye angeweza kumfikia Rehema.

Moyo wangu ulikiri kuwa ni Asia peke yake ndiye angeweza kuziba pengo la Rehema ila bahati mbaya alikuwa amekufa.

Japokuwa Amanda alijitahidi sana kunionesha mapenzi lakini sikuiona tena raha ya mapenzi, kwangu mapenzi yaligeuka shubiri yenye uchungu wa kuukarahisha moyo. Ningependaje tena ikiwa dunia iliamua kuniadhibu? Nilikuwa nimechoka kuteseka, uchungu ulionijaa moyoni uliyasukuma machozi yaliyokuja kutanda kwenye goroli za macho yangu, kabla ya kutiririka mashavuni kama maji ya Mto Rufiji.

Hakuna binadamu mwenye moyo wa chuma, wote tuna mioyo ya nyama iliyoko upande wa kushoto vifuani mwetu. Inaweza kukuwia vigumu kuamini kuwa hata mimi nilikuwa nalia, nilikuwa nalilia mapenzi! Mpaka kulipoanza kupambazuka bado nilikuwa nalia.

Wazo la kuwa nisingeweza kumwona tena Rehema lilinikaa sawia na kunisababishia maumivu makali moyoni. Maumivu hayo yalinipa wakati mgumu sana na yasingeweza kupoa kwa sindano ya ganzi. Sikuelewa ni kwa nini Mzee Benard Mpogolo aliamua kunifanyia ukatili hata kama nilikuwa nimelisaliti penzi la binti yake! Alipaswa kumwacha Rehema aamue mwenyewe.

“Haiwezekani! Mzee hawezi kunifanyia hivi!” nililalama kwa sauti ilihali nilikuwa peke yangu chumbani.

Kwangu hiyo ilikuwa adhabu kubwa sana ambayo sikuitarajia. Furaha niliyokuwa nikiipata nikiwa na Rehema ilikuwa imeyeyuka ghafla kama nta iliyowekwa kwenye moto mkali.

Maisha yalikuwa yamegeuka machungu tangu wakati huo, niliiona dunia chungu na mahali pasipostahili kukaliwa kabisa na kiumbe kama mimi na maisha yalikuwa yamekosa maana huku nikikosa hamu ya kuishi.

Niliiangalia saa nikagundua kuwa ilikwisha timia saa 12:20 alfajiri, nikajiinua taratibu kutoka pale kitandani nilipolala na kuelekea sebuleni, ndipo nikachukua chupa kubwa ya pombe kali aina ya Jack Daniel’s na kuketi kwenye sofa dogo pale sebuleni, nikaigugumia ile pombe kama maji.

Niliendelea kunywa huku nikitafakari kuhusu hatua za kuchukua ili kuepukana na kadhia hiyo, na kadiri muda ulivyoanza kusonga nilianza kuhisi joto kali sana likitambaa mwilini mwangu na damu ilikuwa inakimbia mbio kwenye mishipa ya damu. Jasho lilikuwa linanitoka usoni.

Kadiri pombe ilivyozidi kunikolea kichwani ndivyo ilivyosababisha nianze kuingiwa na mawazo mabaya, mawazo yaliyotawaliwa na chuki dhidi yangu mwenyewe. Nilijikuta naanza kujichukia.

Sasa sikuona sababu ya kuendelea kuishi, nikainuka na kuelekea chumbani, nikalifuata kabati la nguo lililokuwa ukutani mle chumbani na kulifungua, nikachukua bastola ndogo aina ya revolver na kuifungua kwenye eneo ambalo risasi hukaa ili kusubiri amri ya mpigaji, nikaziona risasi zikiwa zimesheni barabara kwenye eneo lake.

Akili yangu ilikuwa imekwisha ingiwa na chuki kubwa, nilihisi kuchoshwa kabisa na maisha ya ulimwengu huu, maisha ambayo kwangu hayakuwa na maana tena. Nilianza kulia kwa uchungu na taswira za kuzimu zilianza kuutawala ubongo wangu na kuniondolea umakini ambao ungenifanya kung’amua ubaya wa dhambi niliyokuwa mbioni kuitenda katika nukta yoyote ya saa iliyofuata.

Wakati nikiiangalia ile bastola kwa umakini, simu yangu ikaanza kuita. Sikujishughulisha nayo mpaka ilipokata, na mara ilipokata tu, niliichukua nikaizima kabisa. Kisha nikaelekea sebuleni, nikafungua mlango mkubwa wa barazani na kuuacha wazi ili isiwe taabu kwa watu ambao wangetaka kuingia ndani kwangu na kuikuta maiti yangu wakati ambao uhai wangu ungekuwa umetoka.

Itaendelea...
 
fungate.jpeg

120

“Hapana, hii whisky pekee inanitosha,” nilisema kwa sauti dhaifu kabisa huku nikimwonesha Amanda ile chupa kubwa ya Jack Daniel’s niliyoishika mkononi.

Amanda alinitazama kwa kitambo huku sura yake ikiwa haina tashwishwi yoyote, hakuonesha kushtushwa na kauli yangu, huenda alitarajia jibu kama hilo.

“Unadhani utaendelea kuishi hivi hadi lini?” Amanda aliniuliza kwa sauti tulivu ya upole huku akiwa amenitulizia macho yake usoni kwangu.

Nilimtazama pasipo tashwishwi yoyote, kisha nikajiegemeza kwenye sofa na kufumba macho. Ile picha ya kujiwekea bastola kidevuni kwangu karibu kabisa na koromeo huku kidole changu cha shahada kikiwa kwenye kitufe cha kufyatulia risasi ikanijia, ikifuatiwa na sauti kali ya Amanda iliyonishtua sana na kunifanya niminye kile kitufe cha kufyatulia risasi bila kujitambua.

Kisha nikaisikia sauti ya Eddy ikiniuliza, “…umeshawahi kujiuliza ni kitu gani kinafuata baada ya kifo?” Sauti hiyo ilipasua tena ngoma za masikio yangu kwa mara nyingine na kutuama akilini kwangu.

“Jason, utaishi maisha haya hadi lini?” Amanda aliniuliza tena huku akinitazama kwa wasiwasi.

Don't waste your time asking the same question,” (Usipoteze muda wako kuuliza swali lile lile) niliongea huku nikiwa nimekereka kidogo.

“Samahani kama nimekukwaza. Naomba unisamehe…” Amanda alisema kwa sauti ya upole yenye kusihi.

“Hujanikwaza!” nilimjibu kwa sauti tulivu kisha nikaachia tabasamu. Amanda alibaki kimya huku akinitazama kwa udadisi. Kisha kikafuatia kitambo fulani cha ukimya kila mmoja akitafakari lake.

Hali ya mle ndani iliendelea kuwa ya ukimya mno, mara nikamwona Eddy akiingia ndani akiwa amefuatana na mtu mwingine, kisha wakasimama huku wakitutazama kwa umakini kidogo.

Nilipomtazama vizuri mtu aliyefuatana naye nilijikuta nashtushwa na ugeni huo wa ghafla uliofika nyumbani kwangu. Ulikuwa ugeni ambao sikuwa nimeutarajia kabisa. Mgeni yule alisababisha ubaridi mwepesi uanze kunitambaa mwilini mwangu na kuzifanya nywele zangu kusisimka kisha woga wa aina yake ukanitambaa mwilini!

Kwa sekunde chache nilibaki nikiwa nimepigwa butwaa huku nikijiuliza ni kipi kilichomleta nyumbani kwangu muda ule wa asubuhi? Katika kuyawaza hayo shughuli mbalimbali za mwili wangu zilikuwa zimesimama kwa sekunde kadhaa huku koo langu likinikauka ghafla.

Macho yangu yalikuwa yanamtazama Dk. Camilla Mpogoro, dada wa Rehema, ambaye macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba. Hapana shaka hali hiyo ilisababishwa na kulia. Mkononi alikuwa ameshikilia kitambaa laini kwa ajili ya kujifuta machozi.

Mapigo ya moyo wangu yalianza kunienda mbio kama saa mbovu, yalikuwa yanaenda mbio isivyo kawaida na jasho jingi likaanza kunitoka na kuilowanisha singlendi yangu niliyovaa huku mwili nao ukishindwa kuzuia wasiwasi niliokuwa nao. Nilijiuliza ni nini kilimfanya Dk. Mpogoro alie? Je, Rehema alikuwa amepatwa na shida yoyote?

Ukweli hali aliyokuwa nayo Dk. Mpogoro ilinifanya nipatwe na wasiwasi mkubwa nikihisi huenda Rehema alikuwa amekufa, taarifa ambayo sikuwa tayari kuipokea. Sikujua ningeishi vipi baada ya kuambiwa kuwa Rehema naye amekufa. Kabla sijajua sababu ya ugeni ule wa ghafla na hali aliyokuwa nayo Dk. Mpogoro nilishtuliwa na sauti ya Eddy.

“Hali ya hapa ndo kama unavyoona,” Eddy alimwambia Dk. Mpogoro huku akimwonesha chupa kubwa ya Jack Daniel’s niliyoishika mkononi.

“Wala hatujui, ni kama amechanganyikiwa hivi! Amekuwa mtu wa kushinda ndani muda wote akilewa na kumlilia Rehema tu. Ulaji wake umekuwa wa shida kwa sababu ya mawazo juu ya Rehema, hata afya yake inaanza kuzorota…” Eddy alimwambia Dk. Mpogoro kwa huzuni.

Dk. Mpogoro alinitazama kwa wasiwasi mkubwa kisha macho yake yakahamia kwa Amanda na baadaye akayarusidha tena kwangu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku akipenga kamasi kwa kutumia kile kitambaa laini alichoshika mkononi. Machozi yalikuwa yanamlenga lenga machoni.

Nilibaki kimya nikimtumbulia macho pasipo kusema neno lolote kwani nilikuwa nimeshikwa na kitete na nisijue la kufanya!

“Sasa sijui utatusaidiaje, shem?” Eddy alimuuliza Dk. Mpogoro huku akionekana kukata tamaa.

“Kwa kweli hata sijui nifanyeje maana nimejaribu kumsihi Baba lakini ameshikilia msimamo wake ule ule, hali ya Rehema bado ni tete sana,” Dk. Mpogoro alisema kwa huzuni kisha akamtazama Amanda kwa umakini kabla hajayarudisha tena macho yake kwangu.

“Jason, kwa nini unafanya hivi? Nina uhakika siku uliyozaliwa wazazi wako walifurahi sana wakijua wamepata mtoto wa kiume wa kujivunia, sidhani kama mama yako atafurahi kusikia mwanawe umekuwa mtumwa wa mapenzi kiasi hiki ukishinda ndani unalia…” Dk. Mpogoro alisema na kutingisha kichwa kwa huzuni.

Nilitaka kusema jambo lakini sikujua niseme nini kwa sababu hali aliyokuwa nayo Dk. Mpogoro iliendelea kunitatiza sana, nilihisi kulikuwa na kitu kimejificha. Kwa nini alionekana mwenye huzuni na alitokwa na machozi? Nilitamani sana kujua lakini nikaendelea kubaki kimya huku nikimtumbulia macho.

* * *

Endelea kufuatilia...
 
View attachment 2218754
120

“Hapana, hii whisky pekee inanitosha,” nilisema kwa sauti dhaifu kabisa huku nikimwonesha Amanda ile chupa kubwa ya Jack Daniel’s niliyoishika mkononi.

Amanda alinitazama kwa kitambo huku sura yake ikiwa haina tashwishwi yoyote, hakuonesha kushtushwa na kauli yangu, huenda alitarajia jibu kama hilo.

“Unadhani utaendelea kuishi hivi hadi lini?” Amanda aliniuliza kwa sauti tulivu ya upole huku akiwa amenitulizia macho yake usoni kwangu.

Nilimtazama pasipo tashwishwi yoyote, kisha nikajiegemeza kwenye sofa na kufumba macho. Ile picha ya kujiwekea bastola kidevuni kwangu karibu kabisa na koromeo huku kidole changu cha shahada kikiwa kwenye kitufe cha kufyatulia risasi ikanijia, ikifuatiwa na sauti kali ya Amanda iliyonishtua sana na kunifanya niminye kile kitufe cha kufyatulia risasi bila kujitambua.

Kisha nikaisikia sauti ya Eddy ikiniuliza, “…umeshawahi kujiuliza ni kitu gani kinafuata baada ya kifo?” Sauti hiyo ilipasua tena ngoma za masikio yangu kwa mara nyingine na kutuama akilini kwangu.

“Jason, utaishi maisha haya hadi lini?” Amanda aliniuliza tena huku akinitazama kwa wasiwasi.

Don't waste your time asking the same question,” (Usipoteze muda wako kuuliza swali lile lile) niliongea huku nikiwa nimekereka kidogo.

“Samahani kama nimekukwaza. Naomba unisamehe…” Amanda alisema kwa sauti ya upole yenye kusihi.

“Hujanikwaza!” nilimjibu kwa sauti tulivu kisha nikaachia tabasamu. Amanda alibaki kimya huku akinitazama kwa udadisi. Kisha kikafuatia kitambo fulani cha ukimya kila mmoja akitafakari lake.

Hali ya mle ndani iliendelea kuwa ya ukimya mno, mara nikamwona Eddy akiingia ndani akiwa amefuatana na mtu mwingine, kisha wakasimama huku wakitutazama kwa umakini kidogo.

Nilipomtazama vizuri mtu aliyefuatana naye nilijikuta nashtushwa na ugeni huo wa ghafla uliofika nyumbani kwangu. Ulikuwa ugeni ambao sikuwa nimeutarajia kabisa. Mgeni yule alisababisha ubaridi mwepesi uanze kunitambaa mwilini mwangu na kuzifanya nywele zangu kusisimka kisha woga wa aina yake ukanitambaa mwilini!

Kwa sekunde chache nilibaki nikiwa nimepigwa butwaa huku nikijiuliza ni kipi kilichomleta nyumbani kwangu muda ule wa asubuhi? Katika kuyawaza hayo shughuli mbalimbali za mwili wangu zilikuwa zimesimama kwa sekunde kadhaa huku koo langu likinikauka ghafla.

Macho yangu yalikuwa yanamtazama Dk. Camilla Mpogoro, dada wa Rehema, ambaye macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba. Hapana shaka hali hiyo ilisababishwa na kulia. Mkononi alikuwa ameshikilia kitambaa laini kwa ajili ya kujifuta machozi.

Mapigo ya moyo wangu yalianza kunienda mbio kama saa mbovu, yalikuwa yanaenda mbio isivyo kawaida na jasho jingi likaanza kunitoka na kuilowanisha singlendi yangu niliyovaa huku mwili nao ukishindwa kuzuia wasiwasi niliokuwa nao. Nilijiuliza ni nini kilimfanya Dk. Mpogoro alie? Je, Rehema alikuwa amepatwa na shida yoyote?

Ukweli hali aliyokuwa nayo Dk. Mpogoro ilinifanya nipatwe na wasiwasi mkubwa nikihisi huenda Rehema alikuwa amekufa, taarifa ambayo sikuwa tayari kuipokea. Sikujua ningeishi vipi baada ya kuambiwa kuwa Rehema naye amekufa. Kabla sijajua sababu ya ugeni ule wa ghafla na hali aliyokuwa nayo Dk. Mpogoro nilishtuliwa na sauti ya Eddy.

“Hali ya hapa ndo kama unavyoona,” Eddy alimwambia Dk. Mpogoro huku akimwonesha chupa kubwa ya Jack Daniel’s niliyoishika mkononi.

“Wala hatujui, ni kama amechanganyikiwa hivi! Amekuwa mtu wa kushinda ndani muda wote akilewa na kumlilia Rehema tu. Ulaji wake umekuwa wa shida kwa sababu ya mawazo juu ya Rehema, hata afya yake inaanza kuzorota…” Eddy alimwambia Dk. Mpogoro kwa huzuni.

Dk. Mpogoro alinitazama kwa wasiwasi mkubwa kisha macho yake yakahamia kwa Amanda na baadaye akayarusidha tena kwangu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku akipenga kamasi kwa kutumia kile kitambaa laini alichoshika mkononi. Machozi yalikuwa yanamlenga lenga machoni.

Nilibaki kimya nikimtumbulia macho pasipo kusema neno lolote kwani nilikuwa nimeshikwa na kitete na nisijue la kufanya!

“Sasa sijui utatusaidiaje, shem?” Eddy alimuuliza Dk. Mpogoro huku akionekana kukata tamaa.

“Kwa kweli hata sijui nifanyeje maana nimejaribu kumsihi Baba lakini ameshikilia msimamo wake ule ule, hali ya Rehema bado ni tete sana,” Dk. Mpogoro alisema kwa huzuni kisha akamtazama Amanda kwa umakini kabla hajayarudisha tena macho yake kwangu.

“Jason, kwa nini unafanya hivi? Nina uhakika siku uliyozaliwa wazazi wako walifurahi sana wakijua wamepata mtoto wa kiume wa kujivunia, sidhani kama mama yako atafurahi kusikia mwanawe umekuwa mtumwa wa mapenzi kiasi hiki ukishinda ndani unalia…” Dk. Mpogoro alisema na kutingisha kichwa kwa huzuni.

Nilitaka kusema jambo lakini sikujua niseme nini kwa sababu hali aliyokuwa nayo Dk. Mpogoro iliendelea kunitatiza sana, nilihisi kulikuwa na kitu kimejificha. Kwa nini alionekana mwenye huzuni na alitokwa na machozi? Nilitamani sana kujua lakini nikaendelea kubaki kimya huku nikimtumbulia macho.

* * *

Endelea kufuatilia...
Shukrani sana
 
fungate.jpeg

121

Karibuni Mezani…


Saa 12:30 jioni…

UCHOVU ulikuwa wazi mwilini mwangu na dalili za kukosa usingizi zilionekana bayana machoni kwangu kwa kila aliyenitazama. Sura yangu haikuonesha furaha na muda wote nilikuwa nimeketi kwa utulivu kwenye meza iliyokuwa katika kona moja ya pembeni ndani ya ukumbi wa club maarufu ya Paradise.

Nilikuwa nimevaa shati la mikono mirefu aina ya Levi’s la mistari ya bluu na myeupe, na suruali nyeusi ya dengrizi. Miguuni nilivaa viatu vyeusi vya ngozi.

Juu ya meza yangu kulikuwa na mzinga wa Konyagi, huo ulikuwa wa pili na baada ya kumaliza mzinga mmoja wa Konyagi pombe ilianza kuirubuni akili yangu na taratibu nilianza kuyasahau masaibu yangu. Taratibu nilianza kujiona mchangamfu kama watu wengine mle ukumbini.

Mwanzoni nilipoingia nilijiona mnyonge na watu wengine waliokwisha changamka niliwaona kama si wapuuzi basi wenye zogo. Lakini taratibu nilianza kuwaona kama watu wa kawaida, wenye starehe na wanaojua kustarehe.

Zilikuwa zimepita siku mbili tangu lile tukio la kutaka kujiua kwa risasi, kabla Eddy na Amanda hawajaingia na kuninyang’anya bastola, na sasa niliamua kutopea kwenye ulevi. Kuanzia siku hiyo sikutaka tena kujifungia ndani, niliamua kubadilisha viwanja kila iitwapo leo, mara nipo baa hii na kesho yake baa ile, nikinywa pombe kali kama Whisky au Konyagi.

Katika muda ule wa jioni, jua lilisha anza kuzama na anga la rangi mchanganyiko wa kijivu na njano lilionekana kuanza kunywea katika ukungu. Kwa wengine siku ilikuwa imeisha lakini kwa tuliokuwa ndani ya ukumbi wa Paradise Club ndiyo kwanza kulikuwa kumekucha.

Ndani ya ukumbi huo kila mtu alikuwa kachangamka, kila mtu aliusherehekea uhai wake, njaa ilikuwa imesahaulika, kifo kilisahaulika. Kila aliyekuwemo ukumbini alikuja kustarehe na alistarehe kweli kweli. Hiyo ndiyo ilikuwa sifa kubwa ya ukumbi huo maarufu uliokuwa katika mtaa wa Kilima mjini Kahama. Ukumbi wa Paradise Club, kama lilivyokuwa jina lake, ulikuwa kama peponi na ulimfanya kila mteja ajisikie hai, akiufurahia uhai wake.

Nami nilishachangamka na kusahau kuwa muda mfupi kabla sijamaliza mzinga wa kwanza wa Konyagi nilikuwa nakabiliwa na mawazo mengi juu ya Rehema, mwanamke aliyenipenda kuliko nilivyoweza kufikiri. Ingawa sikuwa na uhakika kama alijua kilichokuwa kikinisibu au hata kukumbuka kama duniani kulikuwa na mtu aliyeitwa Jason, na kwamba nilikuwa nateketea ndani kwa ndani kwa sababu yake.

Kuna wakati mawazo juu ya Rehema yakinirudia nilijikuta nikiropoka kwa hasira bila kujali nani alikuwa ameketi karibu yangu, “Ni uchizi huu, kumfikiria mtu ambaye huna hakika kama na yeye anakufikiria, tena mbaya zaidi hajui kama unateketea taratibu kwa ajili yake… huu ni zaidi ya uchizi!” nilijisemea mwenyewe kisha nikapiga funda kubwa la Konyagi na kusisimkwa mwili, halafu nikaikita ile chupa juu ya meza.

Kadiri pombe ilivyozidi kunikolea ndivyo ilivyosababisha nianze kuwatazama wahudumu wa ndani ya ukumbi huo kwa jicho la matamanio. Kila mhudumu alionekana kuwa mrembo mbele ya macho yangu ingawa niliapa kuwa nisingetaka kuondoka na msichana yeyote kati yao. Niliishia kuwasifia tu.

Sikutaka hata kuwa karibu na Amanda wala sikumwona tena nyumbani kwangu kwa kuwa sikushinda nyumbani. Ukweli Amanda alijitahidi sana kunifanya niyafurahie maisha lakini huenda alishaanza kukata tamaa kutokana na majibu yangu kwake.

Katika kipindi hicho nilijikuta nikisahau hata kunyoa ndevu wala nywele zangu, nywele zangu zilikuwa ndefu na zisizo na matunzo, tena ambazo zilikuwa zimetimka timka kana kwamba nilikuwa sijui kama kuna chanuo duniani kwa ajili ya kuchania nywele ndefu, au wembe au hata mkasi kwa ajili ya kunyolea. Nywele hizo pamoja na ndevu na sharafa zilizokaribia kuziba mdomo zilinifanya nionekane kama kichaa!

Niliendelea kunywa pombe taratibu na baada ya muda fulani niliitupia jicho saa yangu ya mkononi na kushtuka, ilikuwa inaelekea kuwa saa mbili ya usiku. Sikutaka kuendelea kukaa pale kwani nilipanga kurudi nyumbani mapema, hivyo niliinyanyua ile chupa ya Konyagi nikapiga funda kubwa na kuinywa pombe yote iliyokuwemo ndani ya chupa na kuikita ile chupa juu ya meza.

Kisha niliitoa simu yangu mfukoni na kuangalia kama kulikuwa na simu iliyopigwa au ujumbe wowote lakini nikagundua kuwa nilikuwa nimeizima tangu asubuhi. Nikaagiza mzinga mwingine wa konyagi wa kuondoka nao kisha nikainuka na kutoka nje ya jengo la Paradise Club, nilipofika nje ya jengo nilisimama huku nikiwaangalia makahaba waliokuwa wakirandaranda pale nje.

Walikuwa wasichana wa kila sampuli; wembamba kwa wanene, wafupi kwa warefu, wenye sura mbovu na warembo! Na wengine walikuwa mabinti wadogo sana. Wote walikuwa wamevalia mavazi yaliyowaacha nusu utupu na walikuwa wanavuta sigara na kutafuna bazoka.

Niliwaona wanawaume wachache wakirandaranda eneo hilo na wawili walikuwa wamekumbatiana na makahaba wakinyonyana ndimi na kufanya matendo mengine ya kishetani. Hata hivyo hawakuonekana kushtushwa sana na uwepo wangu eneo lile na badala yake walionekana kuendelea na hamsini zao.

Muda huo nilikuwa nimechoka, akili yangu ilinituma kuondoka tu huku nikijihisi amani mpaka moyoni mwangu, ingawa nilikuwa na uhakika kuwa amani hiyo ingekuwa ya muda mfupi. Nilishusha pumzi kisha nikaanza kupiga hatua taratibu kuelekea upande wa pili wa barabara kulipokuwa na maegesho ya teksi.

Wakati natembea wasichana watatu wadogo walinisogelea na kujaribu kuniwekea ukuta njiani wakijaribu bahati zao wakidhani labda nilihitaji huduma ya ngono, lakini mwendo wangu na jicho nililowakata viliwaonya kuwa sikuwa na shida ya kununua ngono, kuona hivyo wakawahi kunipa mgongo huku wakiachia misonyo ya hasira.

Sikuwajali, nilipita kama siwaoni nikaanza kukatiza sehemu yenye mwanga hafifu kulipokuwa na maegesho ya magari ya wateja wa Paradise Club, kabla sijavuka barabara nikashtuka kumwona msichana mrefu na mweupe aliyekuwa kwenye sehemu isiyo na mwanga akiwa amejiegemeza kwenye gari moja aina ya Toyota Harrier RX la rangi nyeusi.

Alikuwa ameizungusha mikono yake kwenye shingo ya mwanamume mmoja. Msichana yule alikuwa na mashavu mfano wa chungwa, macho yake yalikuwa makubwa kidogo na legevu yenye kung’ara kama nuru na nywele zake alikuwa amezinyoa na kuzitia rangi.

Pua yake ilikuwa ndogo iliyopendezeshwa kwa kipini cha dhahabu, kifua chake kilibeba matiti imara ya wastani na kiuno chake kilikuwa chembamba kikiwa kimebeba nyonga pana kiasi na makalio makubwa kiasi. Alikuwa amevaa sketi fupi sana iliyoacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi na kuifichua hazina nzuri ya miguu yake, juu alivaa kitopu chepesi sana kilichoacha wazi sehemu kubwa ya kifua, matiti na tumbo lake. Miguuni alivaa sendozi ngumu za kamba zilizotengenezwa kwa ngozi.

Yule mwanamume alikuwa mnene na mwenye kimo cha wastani na alikuwa amevaa suruali nyeusi ya deengrizi kama yangu na juu alivaa shati la rangi nyekundu la mikono mirefu. Alikuwa amezungusha mikono yake kuzunguka kiuno cha yule msichana na walikuwa wamekutanisha midomo yao na kunyonyana ndimi.

Nilijikuta nasimama na kuwaangalia kwa umakini, sikuwa nashangazwa na kitendo chao bali nilijikuta navutiwa kumtazama yule msichana kwa umakini, kulikuwa na cha ziada kilichonifanya nimtazame na nilikuwa najaribu kukumbuka wapi nilipomwona mara ya mwisho.

Yule msichana alishtuka baada ya kuhisi kulikuwa na mtu wa tatu eneo hilo, akayazungusha macho yake kuangalia upande nilikokuwa nimesimama na kuonesha kushtuka sana, alimwachia yule mwanamume huku akitaka kujificha lakini alikuwa amechelewa, akabaki akiniangalia kwa wasiwasi mkubwa kama aliyeona mzimu.

Itaendelea...
 
fungate.jpeg

122

Japo nilikuwa nimelewa lakini sikushindwa kumtambua msichana huyo, aliitwa Tabia au Chausiku na mara ya mwisho nilimkuta stendi ya Nzega nilipokuwa safarini kuelekea kwenye usaili wa kazi katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.

Nilimkumbuka vyema kwani ukarimu wangu kwake siku nilipokutana naye mara ya kwanza mjini Tabora uliniponza, msichana huyo aliniibia simu yangu aina ya Samsung Galaxy S8 baada ya kumkaribisha ndani na kisha akatoroka.

Siku nilipomkuta mjini Nzega miezi kadhaa baadaye nilimnyang’anya simu yake mpya aina ya Tecno Camon 16 Pro kufidia simu yangu na nikajikuta nikipambana na jamaa yake, mtu hatari sana aliyeitwa Gegedu ambaye alifika kumsaidia.

Sasa nilitambua kuwa Tabia au Chausiku alikuwa kahaba mzoefu aliyechina kwa ujuvi na wala asibakishe chochote hata kile kilichompa urijali. Kwa sekunde kadhaa tulibaki tumeangaliana kama majogoo yaliyotaka kupigana huku nikihisi mapigo ya moyo wake yalikuwa yanaenda mbio isivyo kawaida.

Kitendo cha kuzubaa kilimfanya yule mwanamume aliyekuwa amemkumbatia ashtuke na kugeuka kutazama upande ule niliokuwepo, na hapo macho yetu yakakutana. Haraka nikamtambua yule mwanamume, alikuwa mfanyakazi mwenzangu, Meneja Uzalishaji wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, Mohammed Akida.

Mohammed alionesha kushtuka sana na uso wake ulipambwa na aibu ingawa alilazimisha tabasamu. Alipotaka kusema neno nikamfanyia ishara ya kutojali huku nikimtoa wasiwasi kisha nikaachia tabasamu na kuondoka zangu, nikavuka barabara na kuelekea kwenye maegesho ya teksi huku nikiwaacha wananitazama kwa mshangao. Sikutaka kujua huko nyuma nini kiliendelea.

Dereva mmoja wa teksi ambaye tulifahamiana sana aliponiona akawahi kunifungulia mlango wa mbele wa teksi yake wakati nilipokuwa mbioni kuyafikia yale maegesho ya teksi. Sikutaka kukaa mbele badala yake nilizunguka na kufungua mlango wa nyuma wa teksi ile, nikaingia ndani na kuketi.

Yule dereva wa teksi kuona vile haraka akaufunga ule mlango alionifungulia kisha haraka akazunguka na kufungua mlango wa dereva na kuingia.

“Nikupeleke home?” yule dereva aliniuliza huku akinitazama kwa umakini. Niliitikia kwa kubetua kichwa changu. Hakutaka kuuweka, akawasha gari lake na kuliondoa taratibu.

* * *



Saa 3:15 usiku…

Nilifika nyumbani kwangu eneo la Mwime na kushangaa sana baada ya kuona taa za nyumba yangu zikiwa zinawaka lakini nyumba ilikuwa kimya kabisa. Nilifikiria kidogo huku nikijiuliza kama niliziwasha wakati naondoka lakini nilikumbuka kabisa, si kwa akili ya pombe, kuwa sikuwa nimewasha taa wakati naondoka nyumbani.

Nilisimama pale nje ya geti huku nikijiuliza kama si mimi basi ni nani aliyewasha taa? Je, ni Amanda? Hapana, isingewezekana akawa Amanda kwa kuwa hakuwa na ufunguo wa nyumba yangu, angewezaje kuingia ndani na kuwasha taa? Je, alikuwa Eddy? Yeye alikuwa na funguo lakini angefuata nini wakati alijua kabisa mwenyewe sikuwepo nyumbani?

Kama si yeye, basi alikuwa nani? Niliposikilizia kwa umakini nikahisi kulikuwa na mtu au watu ndani ya nyumba yangu. Ili kujiridhisha kama hisia zangu zilikuwa sahihi nililisogelea geti dogo pembeni ya geti kubwa la mbele la nyumba yangu na kulisukuma, likasalimu amri na kufunguka!

Hali hiyo ilinidhihirishia kuwa kuna mtu alikuwa amelifungua na kisha kulirudishia tu pasipo kufunga na komeo kwa ndani, nikaingiza mkono kwenye mfuko wangu na kutoa funguo zangu za geti, nilikuwa nazo. Nikashangaa. Hata hivyo sikutaka kujiuliza mara mbili, nikaingia ndani ya uzio wa nyumba yangu kwa tahadhari.

Nilishtuka baada ya kuliona gari la kifahari aina ya Toyota Landcruiser GX V8 la rangi nyeusi likiwa limeegeshwa ndani ya uzio wa nyumba yangu, sikujua lilikuwa gari la nani. Nililitazama kwa umakini huku nikijaribu kujiuliza lilikuwa gari la nani, maana Eddy alikuwa anamiliki gari aina ya Toyota Hilux double cabin la rangi nyeupe. Sasa hilo lilikuwa gari la nani?

Au wazee walikuwa wamekuja toka Tabora? Hata hivyo katika magari waliyokuwa wanayamiliki gari hili halikuwa mojawapo kwani walikuwa na magari mawili ya Toyota Prado la rangi ya fedha na Toyota Hilux double cabin la rangi ya maruni.

Nilihisi kuchanganyikiwa huku ubaridi mwepesi ukinitambaa mwilini mwangu na kuzifanya nywele zangu kusisimka. Kwa sekunde chache nilibaki nimesimama nikiwa nimepigwa butwaa huku maswali mengi yakipita akilini kwangu kuhusu mmiliki wa gari hilo, hata hivyo sikuwa na majibu. Mara hisia juu ya Rehema zikanijia ghafla.

“Mungu wangu! Rehema amekuja! Inamaana amepona?” nilijiuliza kwa sauti huku nikishindwa kuzuia mshangao wangu. Niliilamba midomo yangu kuilainisha huku nikishusha pumzi ndefu na hapo hapo jambo moja likanijia akilini mwangu; “Inawezekana hii ni ndoto tu kama ndoto zingine…”

Lakini akili yangu ilikataa kukubaliana na ubashiri wangu hasa nilipozitazama namba za gari, lilikuwa na utambulisho wa namba binafsi wakati gari alilokuwa akitembelea Rehema kabla hajapatwa na ugonjwa lilikuwa na utambulisho wa namba za serikali.

Ili kupata majibu ya maswali yangu ilinibidi nipige hatua zangu taratibu huku nikiyumba kidogo na kwa tahadhari kukatiza katika uwa mpana na bustani ya kupendeza huku nikitupa macho yangu kuangalia huku na huko, nikaufuata mlango mkubwa wa barazani, kisha nikatulia kidogo pale barazani huku nikiyatega masikio yangu kusikiliza.

Nikiwa nimesimama hapo nikaisikia sauti ya chini ya muziki wa kwaya ikisikika kutoka kwenye redio kubwa iliyokuwepo pale sebuleni, na wakati huo huo nikaisikia sauti ya Mama akiongea na mtu, japo sikuweza kumsikia vizuri lakini nilitambua kuwa alikuwa analalamikia jambo fulani. Mwili wangu ukaingiwa na ganzi, hata hivyo nikajipa moyo na kuingia ndani.

Nilipotokea tu sebuleni nikashtuka sana na kusimama ghafla, mdomo wangu ukiwa wazi kwa mshangao na macho yangu ya kilevi yalinitoka pima kwa mduwao. Nilihisi pombe yote ikinitoka kichwani na akili yangu ilikuwa kama iliyopigwa shoti kali ya umeme hatari wenye nguvu nyingi, na hivyo kuzifanya shughuli za mwili wangu kusimama kwa ghafla kama niliyekuwa nimepigwa kumbo na ugonjwa hatari wa kiharusi.

Ilibaki kidogo niangushe chupa ya Konyagi niliyoishika mkononi, nilishindwa kunyanyua mguu wangu na kubaki nimesimama pale pale mlangoni nikiwa nimeduwaa, kilichokuwa kimenishtua sana ni kuona ugeni mzito ndani ya nyumba yangu ambao sikuwa nimeutarajia kabisa na wala sikuwa nimeelezwa kama wangekuja siku hiyo.

Kwa kuwaona tu watu hao nilijua kabisa kuwa ugeni huo haukuwa umekuja pale kwa ajili ya kunisalimia, bali kutokana na simu aliyopiga Eddy kwa Mama siku nilipotaka kujiua kwa risasi.

Pale sebuleni nilimwona Mama ambaye alikuwa ameketi kwenye sofa kubwa la watu watatu akiwa amembeba mjukuu wake Lydia wa miaka mitatu, huyu alikuwa mtoto wa kaka Eddy. Mama alikuwa na umri uliokaribia miaka sitini na alivaa gauni la kitenge na kichwani alizifunika nywele zake kwa kilemba. Pembeni yake aliketi shemeji Emmy, mke wa Eddy.

Emmy mwenye umbo kubwa lililokuwa linavutia mno alikuwa mrefu wa wastani, mweupe kiasi, alikuwa na mashavu mfano wa chungwa na nywele nyingi nyeusi fii. Alikuwa amevaa gauni zuri na pana la kitenge.

Itaendelea...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom