Simulizi fupi kuhusu Mimi

Living kereth

Member
Feb 7, 2017
69
125
Napenda kujishughulisha hasa kupitia fani na kipawa alichonipatia mwenyezi mubgu mwingi Wa rehema kazi yangu ni Fundi ,Masonry ,plumber,home garden designer but pamoja na kuwa na uwezo huo kipato changu ni kidogo kutokana na ufinyu Wa kazi pamoja na kazi ambazo huwa nikizipata kuzifanya kwa uaminifu na ufanisi mkubwa lakini sipatagi tenda za kazi nashindwa kuelewa ni kipi kinachosababisha nisipate kazi ...najichanganyaga sana lakini wapi...wana JF naamini kuna washauri wazuri na watu wenye uzoefu na kazi kama hizi naombeni ushauri wenu Wa hali na Mali ili nipate kufahamu wapi nipokosea na kipi cha kufanya ...asanteni sana ndugu zangu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
caine

JF-Expert Member
Jul 4, 2015
345
1,000
Pole sana mkuu kuna maswali kadhaaa inakupasa kujiuliza kabla ya kuja kwetu kuomba ushauri. Nakupa assignment jiulize maswali haya then majibu yake yatakupa mwanga mzuri wa kujua wapi pa kuanzia.

1) Umesema umejaribu kujichanganya lakini bado hali ngumu umewahi kujiuliza wale ambao unajichanganya nao wanaweza kuleta effect gani kwenye kazi yako kabla ya kujichanganya nao?

2) Je uzoefu wako na utendaji wako unaridhisha kiasi kwamba ukaaminika kupewa kazi?

3) Vipi kuhusu mtaji? Kumbuka mkono mtupu haulambwi. Kujuana na watu au kujichanganya hakutoshi ww kupata tender ni lazima uingie gharama tofauti tofauti kama kujitangaza n.k.

Naomba nisikuchoshe hayo yanatosha kwa sasa ukija na majibu. Tunaweza kujua wapi kwa kuanzia kukushauri ama kukupa tender kabisa.
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,186
2,000
Tangaza shughuli zako,weka mfano wa kazi zako ktk mitandao ya kijamii kama vile fb,whatssap,jf nk.
 
Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
8,711
2,000
Tangaza shughuli zako,weka mfano wa kazi zako ktk mitandao ya kijamii kama vile fb,whatssap,jf nk.
Hakika inatakiwa ajitangaze.

Aitumie vyema JF na mafanikio atayaona.

My Take
- Tumia muda mwingi kuanzia sasa kuanda mistari michache ya tangazo lako ambayo itabebe fani zako.

- Tumia ukurasa huu: Matangazo madogo kuweka hilo tangazo lako.

- Ili kupa mwanga zaidi wa nini unatakiwa ukiandike basi pitia hapa: MWONGOZO: Zingatia haya unapoweka tangazo lako! - JamiiForums

- Hakikisha tangazo lako linakuwa na picha za kutosha kwa baadhi ya kazi ulizofanya.

- Kuwa na namba ya simu maalum kwa ajiri ya kazi na hakikisha inapatikana muda wote hewani ( muhimu) ikiwezwekana nunua simu ya pili hizi ndogo mfano nokia tochi ambazo chaji yake hukaa muda mrefu hivyo kukufanya uweze kupatikana muda wote.

- Kuwa na ahadi za kweli, kuwa muwazi, Tanguliza kazi mbele na mengine yatafuta.

- Hakika ukiitumia vyema JF utapata kazi nyingi na utaweza safiri toka sehemu moja kwenda nyingine kufanya kazi.

KILA LAKHERI NDUGU, Living kereth NINA HAKIKA UTAFANIKIWA SABABU UMEKUJA JF SEHEMU SAHIHI.
 
Living kereth

Member
Feb 7, 2017
69
125
Nimefurahi sana kuona majibu yenye kunipa matumaini ila mbali na hizi shukrani zangu za dhati napenda kumjibu ndugu mmoja alieniuliza swali

Kuhusu kujichanganya ...
Huwa najichanganya sana na watu wanaofanya kazi hizi na Mara nyingi nafanya nao kazi kwa weledi mzuri unaridhisha kwa kiasi kikubwa naamini hivyo kutokana matokeo ninayoyapata baada ya kumaliza kufanya kazi ...sijawahi kurudia kufanya kazi Mara mbili nikimaanisha kuharibu kazi ya mtu then niambie irudie huwa inatokeaga tu pale tu labda ramani ya nyumba inapotakiwa igeukie wapi mteja anapokupatia ramani na kukwambia anza kazi ...au labda mfumo Wa bomba ndani (system) yake inapokuwa inakuwa ni kubadilisha tu

Kazi nafanya kwa wakati na muda anaohitaji mteja iishe na namaliza kazi kwa wakati
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Living kereth

Member
Feb 7, 2017
69
125
Pole sana mkuu kuna maswali kadhaaa inakupasa kujiuliza kabla ya kuja kwetu kuomba ushauri. Nakupa assignment jiulize maswali haya then majibu yake yatakupa mwanga mzuri wa kujua wapi pa kuanzia.

1) Umesema umejaribu kujichanganya lakini bado hali ngumu umewahi kujiuliza wale ambao unajichanganya nao wanaweza kuleta effect gani kwenye kazi yako kabla ya kujichanganya nao?

2) Je uzoefu wako na utendaji wako unaridhisha kiasi kwamba ukaaminika kupewa kazi?

3) Vipi kuhusu mtaji? Kumbuka mkono mtupu haulambwi. Kujuana na watu au kujichanganya hakutoshi ww kupata tender ni lazima uingie gharama tofauti tofauti kama kujitangaza n.k.

Naomba nisikuchoshe hayo yanatosha kwa sasa ukija na majibu. Tunaweza kujua wapi kwa kuanzia kukushauri ama kukupa tender kabisa.
Kuhusu suala la mtaji Mkuu kwa kweli sina ila nalifikiria sana hilo jambo ..ila shida kazi ambayo ndo mtaji Wa kuanzia ili nipate kipato sipati za uhakika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Living kereth

Member
Feb 7, 2017
69
125
Hakika inatakiwa ajitangaze.

Aitumie vyema JF na mafanikio atayaona.

My Take
- Tumia muda mwingi kuanzia sasa kuanda mistari michache ya tangazo lako ambayo itabebe fani zako.

- Tumia ukurasa huu: Matangazo madogo kuweka hilo tangazo lako.

- Ili kupa mwanga zaidi wa nini unatakiwa ukiandike basi pitia hapa: MWONGOZO: Zingatia haya unapoweka tangazo lako! - JamiiForums

- Hakikisha tangazo lako linakuwa na picha za kutosha kwa baadhi ya kazi ulizofanya.

- Kuwa na namba ya simu maalum kwa ajiri ya kazi na hakikisha inapatikana muda wote hewani ( muhimu) ikiwezwekana nunua simu ya pili hizi ndogo mfano nokia tochi ambazo chaji yake hukaa muda mrefu hivyo kukufanya uweze kupatikana muda wote.

- Kuwa na ahadi za kweli, kuwa muwazi, Tanguliza kazi mbele na mengine yatafuta.

- Hakika ukiitumia vyema JF utapata kazi nyingi na utaweza safiri toka sehemu moja kwenda nyingine kufanya kazi.

KILA LAKHERI NDUGU, Living kereth NINA HAKIKA UTAFANIKIWA SABABU UMEKUJA JF SEHEMU SAHIHI.
Mkuu nashukuru sana kwa maelekezo haya maana umenifumbua macho na kunipa mwanga nilikuwa sina hii idea kwa kuwa nimeipata na hii link ninafuata maelekezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom