Simulizi - Dosari (a life full of flaws)

Simulizi - Dosari (a life full of flaws)

Elton Tonny

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
416
Reaction score
3,083
DOSARI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Uhalifu, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KWANZA

★★★★★★★★★★★★★



Ni usiku wa saa tatu ndani ya hospitali moja ya mtaa, ambapo kuna watu wengi hapa na kule katika kituo hicho cha kutoa huduma za afya wanaopatiwa ama kusubiri kupatiwa huduma mbalimbali. Kuna wauguzi na madaktari wanaoshughulikia mahitaji ya wagonjwa, pamoja na ndugu ama marafiki wa wagonjwa waliopo wanaokaa kungoja taarifa za wapendwa wao.

Miongoni mwa watu hao, kuna wanawake wawili vijana, ambao wamekaa kwenye benchi moja la kusubiri nje ya mlango unaoelekea kwenye chumba cha wodi za wanawake, wakitulia hapo pamoja huku nyuso zao zikionyesha hali ya huzuni. Mmojawapo anatazama huku na huko akiangalia watu wanaopita sehemu hii au ile, na mwingine amekaa kwa utulivu huku akiweka kiganja chake kimoja mdomoni, macho yake yakikazia sehemu moja tu kwa kuonekana kuwa ndani ya tafakari nzito sana.

Mwenzake anamwangalia kwa njia yenye huruma, kisha anamsemesha kwa kumuuliza, "Ulikuwa umeshaongea na Bony?"

Lakini mwenziye hatoi jibu lolote, na badala yake anaendelea tu kutulia vile vile akiwa ameshika tama lake.

"Sikia. Unaweza ukaongea naye, unaweza ukamwambia kuhusu hali ya mama halafu umwombe hata akusaidie kukukopesha hela kidogo, utakuwa unalipia kwa kufanyia kazi kwa muda atakaokupa," akamsemesha namna hiyo tena.

Bado mwenzake hakutoa itikio lolote lile na kuonekana kuzama tu kwenye fikira nzito.

"Pau... Pau..." akaanza kumwita.

Itikio likawa lile lile tu la ukimya.

Akamtikisa begani na kusema, "We' Paulina..."

Hatimaye akamwangalia usoni, akionekana kushtuka.

"Jamani, ndiyo imeshafikia huko?" mwenzake akamuuliza hivyo.

Mwanamke huyu anayeitwa Paulina, akafumba macho yake na kutikisa kichwa kwa kusikitika, naye akainamisha uso wake na kuufunika kwa viganja vyake.

"Usifanye hivyo, inabidi tuangalie njia yenye kukusaidia ili tumtoe mama kwenye hiyo hali..." mwenzake akamwambia.

"Nimeshajaribu mengi mno Halima, lakini naona kama hayatoshi... mpaka nashindwa kujua nafanya nini zaidi..." Paulina akasema hivyo.

"Usikate tamaa. Ni lazima tu iwepo njia, Mungu ni wetu sote, lazima atatokeza tu njia," Halima akamwambia hivyo.

"Wiki imeshaisha hivyo Halima, sijafanya ama kuleta lolote hapa la maana. Mama yangu akiendelea kukaa hivyo tu... ah..."

"Ndiyo maana ni lazima tuchangamke. Nimekuuliza kama Bony ulikuwa...."

"Nimeshaongea naye, hamna lolote kwa Bony. Kazi yangu yenyewe ndiyo hiyo, unafikiri atanikopesha hela hiyo yote? Halafu nitamlipa na nini? Nimewatafuta hata ndugu zake na mama lakini hamna anayetaka kumsaidia, hili ni langu mimi mwenyewe kubeba Halima halafu sijui cha kufanya kwa sababu mikono yangu haina nguvu. Mama yangu anaenda kufa hivyo Halima, ah!" Paulina akaongea kwa hisia na kujifuta machozi.

Halima akamwambia, "Usiseme hivyo rafiki yangu. Hebu mwamini Mungu. Mungu ni wetu sote, hawezi kutuacha. Ni lazima tuombe atusaidie, halafu tufanye jitihada zaidi ili maombi yetu yajibiwe haraka. Ona... najua hela ya tiba ya mama yako ni nyingi, lakini tuko hapa kusaidiana. Nitakusaidia pia. Nimepata-pata kidogo na kutunza kwenye kazi ya cherehani, nitakuongezea tena ili wasiache kumpa mama dawa, sawa? Wakati huo angalia-angalia na sehemu zingine pia unazoweza kupata, labda milango ikafunguliwa. Rafiki yangu, usichoke. Niko pamoja nawe, sawa? Mama yako atapona, tutamsaidia atapona,"

Halima alikuwa anamtia sana moyo rafiki yake, naye Paulina akawa anajipangusa machozi huku akitikisa kichwa kukubali faraja ya mwenzake. Simu ndogo ya Halima ikaanza kuita baada ya dakika chache za utulivu, naye akapokea na kuzungumza kiufupi na mpigaji, kisha akakata na kurudisha umakini kwa rafiki yake.

"Baba Joan huyo?" Paulina akamuuliza.

"Eeeh, amenipigia anasema ndiyo ameingia nyumbani," Halima akamwambia.

"Amekuita?"

"Hajaniita kabisa, alikuwa ananiulizia tu. Si nilikuwa nimeshamtaarifu kwamba niko huku?"

Paulina akasafisha pua na kusema, "Nenda tu nyumbani Halima. Mumeo atakuwa anakusubiri, maana ni usiku. Kwanza Joan ulimwacha na nani?"

"Yupo na dada yake, sioni kama kutakuwa na shida nikikaa na wewe...."

"Hapana Halima, nakuomba uende nyumbani. Me nitakuwa sawa hapa," Paulina akasema hivyo.

"Nitajisikia vibaya kukuacha mwenyewe..."

"Hamna, usijali. Kwa sababu leo niko off, nitalala hapa hapa kumwangalia mama, kesho nitaamkia mapambano zaidi. Asante sana kuwa nami rafiki yangu," Paulina akamwambia hivyo kwa njia imara.

Halima akatabasamu kiasi, naye akamkumbatia rafiki yake na kusema, "Usikate tamaa rafiki yangu. Tuko pamoja. Na Mungu atakusaidia wewe na mama."

"Amen," Paulina akajibu kistaarabu na kumwachia.

Rafiki yake akawa ameondoka hapo na kumwacha Paulina akiwa bado ndani ya mawazo mazito kuhusu hali ya mama yake mzazi. Aliumwa sana, akiwa na tatizo la uvimbe tumboni uliosababishwa na mambo mengi ya kijadi kipindi cha nyuma, na wakati huu lilikuwa kubwa zaidi mpaka kutishia uhai wake endapo kama asingefanyiwa upasuaji upesi; na tena kwenye hospitali kubwa zaidi. Shida ndiyo ilikuwa kwenye pesa, na hata kazi ambayo Paulina alifanya haikumpa pesa ya kutosha sana. Tayari alikuwa ametumia kiasi kingi alichotunza na kingine alichosaidiwa na baadhi ya watu waliomfahamu, katika uangalizi wa awali kitiba uliomsogezea mama yake siku, na pesa hizo zilikuwa zinaisha upesi sana.

Alihitaji kutafuta njia ya haraka ambayo ingemwongoza kupata pesa ya kutosha ili kumsaidia mzazi wake pekee aliyemlea kwa shida sana mpaka kufikia hatua hiyo, kwa kuwa ni yeye tu ndiye aliyekuwa pamoja naye siku zote baada ya baba yake kupoteza maisha Paulina alipokuwa mdogo, na wao kutengana na wengi wa watu wa ukoo baadaye; ingawa si wote. Alitulia hapo kwenye benchi akiwaza sana nini afanye, na kweli kama rafiki yake mpendwa Halima alivyokuwa amemshauri, Paulina akaamua kufumba macho na kusali zaidi kwa Mungu ili aweze kumsaidia kuipata njia ambayo ingemwezesha kumwokoa mzazi wake mpendwa.


★★★


Ndani ya jiji kubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi, tunakutana na mwanaume mtu mzima ambaye ni moja ya watu wengi waliofanikiwa kimaisha. Huyu anakwenda kwa jina la Reuben Marcus (Marko), aliye na miaka 41, mwanaume mchapakazi na aliyebeba macho yenye kutazama mbele sikuzote ili kupiga hatua kubwa zaidi kwenye maendeleo ya maisha yake, na ya familia yake. Alikuwa na nafasi ya juu katika moja ya kampuni kubwa sana za kibiashara jijini, ambapo alishughulika na masuala yaliyohusiana na mapato ya jumla ya kampuni na ustawi wake akiwa mmoja wa washiriki maalumu wa bodi ya kampuni.

Reuben alitumikia kampuni hiyo kwa miaka zaidi ya kumi na mitano, na alianza kama afisa wa mauzo katika ngazi ya chini kabisa mpaka bidii yake ya kutafuta mafanikio zaidi ilipomsaidia kuvuka madaraja na kupandishwa vyeo, na hivi sasa akawa sehemu ya juu zaidi. Alikuwa mwanaume wa malengo na kuyatimiza, mstaarabu, na mwenye akili yenye kasi katika kufanya maamuzi muhimu ambayo sikuzote yalimpa faida.

Miaka tisa ya mwisho kufikia sasa, akiwa ameshaanza kupata mafanikio mengi ndani ya kampuni hiyo, alikutana na mwanamke mzuri sana aliyeitwa Lydia na kumpenda, na baada ya muda mfupi tu wa mahusiano, wakafunga ndoa na kufanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wa kike waliyemwita Larissa.

Kufikia wakati huu, binti Larissa alikuwa na miaka nane, na mama yake, Lydia, alikuwa na ujauzito wa miezi mitano, akiwa anategemea kupata mtoto wake wa pili pamoja na bwana Reuben. Lydia alikuwa mwanamke mfanyabiashara pia, akiwa na maduka mawili makubwa ya nguo na mghahawa maridadi pia ulioitwa Lydz Restaurant. Kwa pamoja walikuwa na maisha fulani ya matawi sana, uzungu yaani, na walipendana kikweli.

Katika kipindi hiki, Reuben alikuwa anapiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo, kwa sababu alitumia pesa nyingi alizochuma kuinua mradi wake wa kujenga hoteli kubwa ambayo ingepanua zaidi uchumi wake, na ufanisi wa familia yake. Tayari alikuwa na kila kitu kilichohitajika ili kuuanzisha ujenzi huo, na ungekwenda moja kwa moja mpaka hoteli hiyo aliyotaka iwe ya kifahari ikamilike vyema na kuanza kumwingizia madola zaidi. Alitaka kujenga wakati ujao mzuri sana hasa kwa ajili ya watoto wake.

Sasa ikawa ni siku moja nzuri ya mapumziko ya kikazi kwa watu wengi, yaani Jumapili, na kwa upande wake Reuben ikawa hivyo pia ingawa kuna nyakati zingine alikuwa akihitajika kwenda kazini hata kwa siku kama hizi. Aliamka kwenye asubuhi ya saa tatu, na kitandani kwake kwa pindi hii alikuwa akilala yeye pekee. Lydia mke wake alikuwa amesafiri kwenda mkoa wa jirani ambako wazazi wake ndiyo waliishi, akiwa ameenda kuwasalimu baada ya miezi mingi kupita bila kuonana nao.

Sikuzote kama Lydia angekwenda kwao kusalimia, alimchukua Larissa ili naye aende kuwasalimu babu na bibi, lakini kwa wakati huu Larissa hakwenda pamoja naye kwa kuwa bado alihudhuria shule. Ilikuwa mpaka nyakati za likizo ndiyo binti angeambatana naye. Lydia alikuwa amepitisha wiki kama moja tangu aende huko, na alikuwa akitarajiwa kuanza safari ya kurejea huku kwake hiyo kesho.

Kwa hiyo Ruben akaamka tu mida hiyo hiyo ya saa tatu sasa, maana alilala kwa uchovu kutokana na kazi nyingi za siku iliyotangulia, na alipania kulala sana sema mwili wake ulikuwa na kawaida ya kumwamsha mapema ndiyo maana hakujikuta anaamka saa sita mchana. Alikuwa ameshaanza kumkosa kweli mke wake, yaani hata kama ni siku moja tu kumkosa ndani ilikuwa inampa tabu maana alimzoea sana, kwa sababu walikuwa na ule uvutano mzuri wa kirafiki uliodumu kwa kipindi kirefu kweli. Hivyo alikuwa na hamu kubwa ya ujio wake hiyo kesho.

Lakini kwa sasa, alihitaji kushughulika zaidi na binti yake. Bila shaka Larissa bado angekuwa anakula usingizi huko chumbani kwake, na Reuben alikuwa amepanga kutumia muda mwingi wa siku hii pamoja na mwanaye kuanzia asubuhi mpaka jioni. Alitaka kuziba mapengo mengi ya wao kutoonana sana shauri ya kazi zake ambazo mara nyingine zilimbana na kufanya achelewe kurudi na kukuta binti yake ameshalala, na wakiachana asubuhi tena inakuwa ni upesi na mapema mno, hivyo alitaka kuburudika naye kwa siku nzima leo maana alihisi binti angekuwa anajihisi upweke kiasi sababu ya kukosa ushirika wa mama yake aliokuwa ameuzoea zaidi.

Kwa hiyo bwana Reuben akaingia kujisafisha bafuni kwake kwanza, kisha akaelekea chumbani kwa binti yake. Nyumba yake ilikuwa kubwa, yenye ghorofa lenye vyumba vitatu vipana na sebule nzuri hapo chini ambapo kuelekea mbele zaidi kulikuwa na jiko na vyumba vya wafanyakazi wawili wa ndani. Kulikuwa na uwanja mkubwa huko nje pia na nyumba ya mlinzi, wakiwa wanafuga mbwa mkali mwenye kulinda makazi yao, na Reuben na Lydia walikuwa na magari mawili mazuri ya kutembelea.

Kiujumla walikuwa na maisha mazuri na tulivu, wakihakikisha pia kwamba binti yao anakua vyema kabisa katika mazingira safi na malezi bora, na huyu Larissa alikuwa ni hazina. Binti wa miaka nane tu, ila alikuwa na akili nzuri sana, mchangamfu lakini mwenye mwelekeo makini kama baba yake tu. Reuben alikuwa mrefu na mweusi, huku Lydia akiwa ni mweupe na mwenye urefu wa wastani uliomfaa mwanamke, na yeye Larissa alirithi uzuri wa sura ya mama yake na zaidi rangi ya baba yake, ingawa ule weupe wa mama yake ulimng'arisha sana pia kadiri siku zilivyozidi kwenda.

Reuben akakifikia chumba cha Larissa na kukuta bado amelala, hivyo akamwamsha kwa ustaarabu na kuanza kuongea naye. Kalikuwa kamechoka kweli maana kalipenda kusoma kabla ya kulala, na hata baba yake alikuta vitabu hapo kitandani kwake kuonyesha kalisinzia kakiwa kanasoma. Wakaongea kidogo, Reuben akiuliza maendeleo ya shule ya mtoto wake na kujibiwa kuwa kila kitu shuleni kipo swadakta, naye mzee akamkumbusha binti pia kuhusu mama yake kurejea kesho.

Larissa alikuwa na shauku kweli kuhusiana na mama yake kuja maana alimkosa pia, ndiyo baba mtu akasema leo wangekwenda kuzurura, yaani wangetembelea sehemu nzuri sana jijini mpaka jioni kabisa, wanunue na vitu vingi vya kuleta nyumbani ili kesho mama yake akifika akute mambo yapo moto, na binti akafurahi kweli. Upesi akakimbilia bafu lake ili aoge, akimwambia baba yake asimtoroke. Ilimpa uradhi mwingi Reuben kuona namna ambavyo mtoto wake alikuwa na bidii sana kimasomo baada ya kupitia baadhi ya madaftari yake, na hilo likamwongezea nia ya kutaka kuhakikisha anampatia elimu bora zaidi ili aje kufika mbali sana kimaisha.

Basi, binti akawa amejiandaa vyema kabisa baada ya kuoga, akisaidiwa kuvaa nguo nzuri na msaidizi mmoja wa hapo, kisha akajiunga na baba yake sebuleni ambapo alikuwa akimsubiri. Reuben alivalia kwa njia ya kawaida tu, T-shirt na bukta, huku binti yake akivaa gauni fupi jeupe, nao wakaondoka hapo nyumbani ili kwanza ampeleke Larissa kwenye mgahawa wa mama yake huko mbele jijini; wapate kiamsha kinywa kitamu sehemu ya kibiashara ya Lydia. Mwanaume akambeba mgongoni bintiye hadi alipomweka garini, kisha akaliondoa maegeshoni taratibu na kuingia barabani kuianza safari.

Kwa mwendo wa dakika chache tu, wakawa wameufikia mgahawa huo, na kwa jinsi ambavyo ulikuwa maridadi, ungeweza kuuita hoteli nzuri ya misosi kabisa. Kulikuwa na taratibu nzuri sana hapo, wafanyakazi na wahudumu walivalia kwa njia rasmi na kutoa huduma bora kwa wateja, na watu wengi walioenda mara nyingi walifurahishwa sana na huduma hizo kuwafanya wawe wateja sugu. Yaani mgahawa haukufukuza wateja huo, na ulizidi kuwaongeza tu, hivyo uliendelea kukua sana.

Reuben na binti yake walipoingia hapo, wakasafisha mikono na kupata sehemu ya kukaa, baba na mtoto pekee, naye akaagiza chai pamoja na maandazi magumu (half cake), na mayai ya kuchemsha, huku binti yake akiagiza chai ya maziwa, sambusa za nyama, pamoja na mayai ya kuchemsha pia. Reuben alijulikana kuwa mume wa mwenye mgahawa huo, lakini mara zote alipofika hapo kupata chakula, alilipa. Yaani alikuwa anamlipa mke wake kama mteja!

Ilikuwa inaelekea kuingia saa tano, na watu wakiwa sehemu za hapa na kule kupata vyakula, Reuben aligundua kwamba binti yake alipenda sana kuchunguza na kufatilia kwa umakini mazingira yaliyomzunguka. Hii ilikuwa baada ya Larissa kumwonyesha kwa ishara ya mdomo atazame meza ya pembeni.

Reuben akaangalia hapo na kuona mwanamke na watoto wake wawili wakiwa wanapata chakula, na ambacho binti alimwonyesha baba yake ilikuwa ni jinsi ambavyo mtoto mmoja wa miaka kama mitano alikula kwa njia mbaya sana na kujipakaa vyakula usoni na kuchafua nguo, na mama yake akawa anapata shida kumwongoza vyema hadi akawa akimpiga mara kwa mara, na kimya-kimya.

Reuben akamwangalia binti yake kukuta anacheka huku amefunika mdomo, naye akacheka kidogo pia. "Usimcheke mwenzio, hata we' ulikuwa unakula hivyo zamani," akamwambia hivyo.

"We! Mimi huyo?" Larissa akamwambia hivyo.

"Nani mwingine?"

"Akhaa. Me sijawahi kula hivyo maisha yangu yote baba."

"Maisha yako yote ulijiona? Wakati upo mdogo ulikuwa unakula vibaya wewe, picha zipo kwenye album, uje uangalie uone..."

"Aaah, baba unadanganya! Mama amenifunza kutumia kijiko na uma kabla hata sijazaliwa," Larissa akasema hivyo.

Reuben akacheka kidogo na kutikisa kichwa.

"Hebu ona! Linakula vibaya," Larissa akasema hivyo.

"Hey, punguza sauti. Watakusikia," Reuben akamwambia.

Larissa akakunja midomo na kusema kwa sauti ya chini, "Yaani mimi kula meza moja na mtu hivyo, siwezi baba. Uchafu-uchafu hivyo, nahama. So uncivilized!"

"Eh! We' mtoto..." Reuben akasema hivyo.

Larissa alikuwa amesuka nywele ngumu za rasta fupi, zilizovalishwa urembo wa rangi mbalimbali, naye akazipiga kidogo nyuma ya shingo yake kimadoido, eti kama mzungu.

Chakula kikawa kimeletwa huku Reuben akiwa ameanza kufurahishwa na njonjo za binti yake, nao wakajiweka tayari kuanza kula. Baada ya Reuben kuona Larissa amekaa kuziangalia sambusa kwa umakini, akahisi labda kuna tatizo.

Akamuuliza, "Darling, vipi?"

"Bee?" Larissa akaitikia na kumtazama baba yake.

"Mbona unaangalia chakula hivyo? Kuna nini?"

"Yaani baba kuna sambusa zingine zina sura mbaya! Lakini ndiyo nazipenda," Larissa akasema hivyo.

"Sura mbaya?" Reuben akauliza.

"Eeh. Nikiziangaliaga, najua kabisa ipo sambusa ya kike, na ya kiume, na hizi tatu zilizowekwa hapa ni za kike lakini zina sura mbaya mno. Kwa hiyo zinakuwa tamu maana kama nimeshasikia ule msemo kwamba 'sura mbaya kufa hutaki, hizi za kike zikiwa na sura mbaya ni lazima ziwe zinataka kufa, na nikianza kuzitafuna zinauachia utamu wote niusikie vizuri maana zitakufa kwa raha," Larissa akaongea upesi sana kama vile hana breki.

Reuben akabaki kumtazama tu, kisha binti yake akaanza kula na kumpandishia nyusi baba yake kuonyesha anafurahia sana "kuziua" hizo sambusa. Mwanaume akacheka kidogo kwa pumzi na kunywa chai yake. Hapa alikuwa na mtoto moto kweli!

Wakati akiwa anataka kuanza kula andazi, akawa ameona watu wengine waliokuwa wakiingia mgahawani hapo, na mwanzoni hakutaka kukaza fikira kwao lakini mmoja wao akawa amevuta umakini wake. Akaendelea kuwaangalia. Walikuwa watatu, mwanaume, mwanamke, na mtoto wa kiume miaka kama minne-mitano, na ni mwanaume huyo hasa ndiye ambaye alivuta umakini wa Reuben. Alikuwa mweusi, mrefu wa wastani, na mwenye mwili mzuri wa kiume. Alinyoa kipara kichwani na kubeba ndevu hafifu kidevuni, umri wake ukionekana kuwa sambamba na rika la Reuben.

Kwa pamoja, watatu hao walionekana kuwa kama familia, na walianza kuelekea upande ambao Reuben na binti yake walikuwa wamekaa ili bila shaka kupapita na kwenda kwenye meza huru kuagiza chakula. Wakiwa wanaukaribia upande wake, Reuben akawa amethibitisha kwamba ndiyo, alimjua mwanaume huyo, na baada ya macho ya huyo mwanaume kukutana na ya Reuben, akakunja uso wake kimaswali na kuachia tabasamu la utambuzi, kitu ambacho kikafanya Reuben atabasamu kiasi pia.

Watatu hao wakaifikia meza ya Reuben, na huyo mwanaume akasema, "Eh! Mbona kama naota? Siamini yaani, ni wewe?"

Reuben akaanza kusimama huku akisema, "Labda bado ni Deja Vu. Ngoja nisimame uthibitishe."

Huyo mwanaume akacheka kidogo, naye pamoja na Reuben wakaunganisha viganja kirafiki na kukumbatiana kimabega.

Reuben akamtazama mwanamke aliyekuwa pamoja na mwanaume huyo, naye alikuwa akimwangalia machoni kwa utulivu pia. Alikuwa na ngozi ya weusi wa maji ya kunde, mwenye mwili ulionawiri na shepu nzuri. Yaani alivalia gauni la njano lililoishia magotini, lililoubana mwili wake kwa njia iliyochoresha hips nene alizokuwa nazo na kumfanya avutie. Alikuwa na macho makubwa yaliyopendezeshwa kwa wanja, midomo minene iliyong'arishwa kuiongezea sura yake urembo, akionekana kuwa wa miaka iliyokimbilia thelathini. Na mtoto huyo wa kiume alimfanana kwa kadiri kubwa kuonyesha alikuwa wa kwake.

Baada ya wanaume kuachiana, Reuben akasema, "Habari za siku bwana?"

"Ah, Mungu anasaidia. Ni Reuben, si ndiyo?" mwenzake akauliza.

"Yeah. Na we' ni Francis," Reuben akamwambia.

"Nilifikiri ungekuwa hata hujui jina langu, maana hatukuwa tight kivile enzi hizo," Francis akamwambia.

"Ah, ni wengi mbona nilikuwa nawajua kwa majina? Attendence yote ilikuwa kichwani," Reuben akasema.

"Hahahah... monta mpaka kiranja!" Francis akasema hivyo kwa shauku.

"Yeah, hahah... ndiyo mimi," Reuben akaongea kwa utulivu tu.

"Aisee, ni muda mrefu sana kaka. Mambo yamebadilika, mpaka na nywele umezipiga na mtindo, yaani dah!" Francis akasema.

"Hahah... kweli, ni muda sana. Upo huku kitambo?" Reuben akauliza.

Francis akasema, "Eeeh, ila siyo sana. Nimekuja huku, huu kama mwaka wa tano sasa hivi. Na wewe?"

"Ah, me niko huku muda. Toka tumemaliza shule, nilikuja huku kuendelea na masomo mpaka nilipoanza kazi," Reuben akamwambia.

"Ah, safi sana. Maisha yamekukubali kiranja, na kitambi kinavizia," Francis akatania.

"Kawaida tu. Hata we' naona yako yanang'aa," Reuben akasema hivyo huku akitoa ishara kumwelekea mwanamke yule pembeni.

Francis akamwangalia mwanamke huyo na kusema, "Ah, huyu ni dada yangu bwana. Anaitwa Josephina."

"Oooh, sawa sawa..." Reuben akaelewa.

"Eeh. Sister, huyu ni rafiki yangu, tumesoma wote shule ya msingi mpaka sekondari. Ndiyo tukaja ku-separate tulipomaliza... leo ndiyo tunakutana yaani," Francis akamwambia hivyo dada yake.

"Okay. Sawa," Josephina akajibu kistaarabu.

Alikuwa na sauti tulivu, na Reuben akamnyooshea kiganja kisalamu huku akisema, "Naitwa Reuben. Nimefurahi kukutana nawe Josephina."

Akakipokea kiganja chake huku akitabasamu na kusema, "Mimi pia. Niite tu Phina."

"Sawa sawa. Mwanao hajambo?" Reuben akasema hivyo na kukiachia kiganja cha mwanamke huyo.

"Yuko poa. Ana njaa kweli, imebidi tuwahi hapa kabla hajanitafuna," Josephina akajibu hivyo.

Reuben akatabasamu, naye akamwambia huyo mvulana, "Hujambo baunsa?"

Dogo akatulia tu kama vile hataki.

Francis akasema, "Inabidi awahishwe, maana! Atatafuna mtu kweli. Na huyu ni mwanao?"

Alikuwa akimaanisha binti yake Reuben, ambaye aliendelea kula huku akiwaangalia wengine kwa utulivu, naye Reuben akasema, "Ndiyo, mwanangu wa kwanza huyo ahahah..."

"Dah! Hujambo karembo?" Francis akamsalimu.

"Sijambo uncle. Shikamoo?" Larissa akajibu upesi huku akitikisa-tikisa mguu wake.

"Marahabaa, mtoto mzuri," Francis akamjibu kwa furaha.

"Aunty, shikamoo?" Larissa akamwamkia na Josephina.

"Marahaba dear. Unaitwa nani?" Josephina akajibu.

"Larissa," kakajibu.

"Wow! Jina zuri sana, Larissa. Eh, Hans... umemwona Larissa? Mwambie 'mambo?'" Josephina akasema hivyo kumwelekea mwanaye.

Huyo Hans akawa anamwangalia Larissa kwa njia fulani ya kujihami na kununa, kama mtoto aliye yeye, naye Larissa akampungia mkono kirafiki mvulana huyo huku akisema, "Hi."

Francis akasema, "Naona mwanao yuko sharp sana."

"Ahahah... tunakuza bwana," Reuben akaongea kistaarabu.

"Basi kaka, wacha sisi tuelekee mezani, chai yako isije kupoa kwa sababu yetu," Francis akamwambia hivyo.

"Hapana shida. Bado iko moto," Reuben akamwambia.

"Vipi tukiachiana mawasiliano kaka mkubwa? Tu-catch up na nini, maana ni miaka!" Francis akasema hivyo huku akitoa simu yake mfukoni.

"Yeah, yeah, itakuwa jambo zuri," Reuben akakubali na kupokea simu ya jamaa.

Akaandika namba yake hapo na kumkabidhi Francis simu, kisha wakaagana kwa ufupi na watatu hao kuwapita baba na binti yake, na Reuben akirejea mezani kuendelea kupata chai. Larissa alistareheka sana kwa kupata mlo wake kwa raha zote, na kwa upande wake Reuben, aliifurahia pia pindi hii pamoja na binti yake, lakini pia alipendezwa zaidi na hali mpya ya urafiki aliyohisi baada ya kukutana na mtu aliyefahamiana naye miaka mingi iliyopita.

Bila shaka wakiwa watu waliotoka mbali na kupotezana, wangekuwa na mambo mengi ya kufurahia pamoja endapo wangeanza kufanya ushirika tena kwa kipindi hiki, mambo ya wanaume kama hivyo lakini kwa kuenzi historia ya ujana wao, ambao kama kwa maisha ya vijana wengi, huburudisha. Angewatazama pale walipokuwa wamekaa kupata chakula, na mara kwa mara macho yake yangekutana na Josephina na wao kupeana aidha tabasamu la kirafiki, ama kuangaliana tu na kuacha.

Hii ya kuangaliana tu na kuacha ilitokana hasa na macho ya mwanamke huyo kuanza kutuma kama ujumbe fulani kumwelekea Reuben, ujumbe ambao hakujua maana yake. Yaani walipoangaliana, Josephina angekaza macho yake kwa Reuben kwa ufupi kwa namna iliyofanya mwanaume ahisi uvutano fulani baina yake na huyu mwanamke, lakini akaona aache kukazia fikira jambo hilo kwa sababu hakutaka lielekee kule ambako hapakufaa. Hakuhitaji kuiingizia akili yake majaribu.

Hivyo, mwanaume akajitahidi kuweka umakini wake kwa binti yake zaidi, akifurahia chakula na maongezi pamoja naye yenye kufurahisha, akafanya kumpigia simu na Lydia na kuongea naye pamoja na binti yao, na walipomaliza chakula kwa kushiba kabisa, Reuben akanyanyuka pamoja na Larissa tayari kuondoka. Waliona kwamba Francis na Josephina bado waliendelea kupata chakula, hivyo wakapungiana mkono kupeana kwa heri, huku Reuben akiona kwamba bado macho ya Josephina yalimtazama kwa njia yenye kutoa maana, naye akamshika tu binti yake na kuuaga mghahawa wa mke wake kwa wakati huu.


★★★


Upande wake Paulina, mambo yalikuwa yakielekea sehemu mbaya sana, tena siyo kwa njia moja tu. Zilikuwa zimepita siku mbili tokea ule usiku ambao alikuwa hospitalini na rafiki yake, Halima, walipozungumza kwa kufarijiana kuhusu jitihada walizotakiwa kuongeza ili kuweza kumsaidia mama yake Paulina atibiwe haraka. Halima alikuwa amemwahidi rafiki yake kumsaidia na kiasi kidogo cha pesa, lakini sasa jambo hilo lisingewezekana.

Usiku huo mwanamke huyo aliporudi nyumbani, alikuta mumewe akiwa amekasirishwa sana na kitendo chake cha kuacha kukaa nyumbani na watoto, akitanguliza mashoga zake badala ya kutimiza majukumu muhimu ya kifamilia, na katika hali iliyozidi kuwa mbaya sana mumewe akawa amempiga na kumkanya asijihusishe tena na matatizo ya Paulina. Ilikuwa kisa chenye kumhuzunisha sana Paulina, na sasa asingeweza hata kuonana wala kuwasiliana na rafiki yake baada ya mumewe kumnyang'anya simu. Mambo ya ndoa hayo.

Jambo hilo lilikuwa limeongezea utata kwenye suala la mama yake, ambaye hangeendelea kupata dawa za maji na uangalizi uliofaa kutokana na Paulina kuishiwa pesa, na hilo lilizidi kuwa baya hasa baada ya yeye kuachishwa kazi yake ghafla. Paulina alifanya kazi ya uhudumu kwenye moja ya baa kubwa za mitaa yao, na aliyemwajiri ndiye mwanaume aliyeitwa Bony. Huyu Bony hakuwa mtu muungwana sana, yaani karibia kila mhudumu aliyemwajiri hapo alitaka kutoka naye kimapenzi, kama siyo kuridhishana kimwili tu kwa jinsi alivyodhani kila mhudumu alitakiwa kujiendesha.

Yaani, Bony kama wanaume wengi tu aliwaona wahudumu wote wa baa kuwa malaya. Na kwa upande wa Paulina hali ilikuwa vile vile. Isipokuwa tu mwanamke huyu hakuwahi kukubali ushawishi wa huyo jamaa hata kama aliahidiwa kuongezewa pesa. Kazi aliyofanya ilikuwa na mambo mengi ambayo yangefanya watu wamwone kuwa mwanamke rahisi tu kununuliwa, lakini hakuwa wa aina hiyo. Aliifanya tu kwa sababu alihitaji kupata pesa, lakini hakutaka kujitoa kuwa chombo cha starehe kwa wanaume ili tu achume pesa.

Sasa kwa siku kadhaa zilizopita hali ya mama yake Paulina ilipozidi kuwa mbaya na kuhitaji msaada wa hali ya juu, Paulina alikuwa amejaribu kumwomba huyo Bony amkopeshe pesa ili imsaidie kuendelea kumtunza mama yake, lakini mwanaume huyo alimwambia angempa hela ikiwa tu angekubali kufanya mapenzi pamoja naye, na Paulina alipoweka pingamizi, jamaa akakataa kumsaidia kwa kusema hana pesa.

Kwa wakati huu sasa baada ya matatizo kumpata Halima ule usiku, Paulina akawa amerudi kazini na kujaribu kumwomba tena Bony msaada, lakini mwanaume huyo akamwachisha kazi. Ilimshangaza sana, hakuelewa kabisa ni kwa nini alifanyiwa hivyo hata baada ya Bony kumwambia kwamba kuna mabadiliko tu walikuwa wanafanya, na akampa kiasi kidogo cha pesa kulipia wiki za mwisho alizokuwa akifanya kazi hapo.

Lakini Paulina aliweza kung'amua sababu ilikuwa ni nini nyuma ya kitendo hicho cha Bony. Kwanza, ni yeye kukataa kujitoa kwake kimwili kwa miezi mingi, na pia, ni maneno ya chuki kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa sehemu hiyo ambao mara nyingi walimwonea wivu Paulina, hasa kwa sababu alipendwa na wateja wengi waliofika. Paulina alikuwa mwanamke kijana mwenye sura na umbo lenye kuvutia, alijitunza, na alikuwa makini na kazi. Alivutia wateja wengi ambao hawakuwahi kupata bahati ya kumbeba na kutoka naye hata mara moja, na bado walimiminika tu hapo baa.

Lakini sasa kwa wiki ambayo hali ya mama yake ilizidi kuwa mbaya, ilianza kuonekana kama vile Paulina hatumii muda mwingi kazini na kujali mambo yake tu, na wenzake wakatumia nafasi hiyo kumchongea kwa bosi wao ili aweze kuondolewa. Kila kitu kilikuwa wazi, yaani Paulina alishangaa tu yeye pekee ndiye anayeachishwa kazi na mhudumu mwingine kuwa ameshaletwa siku hiyo hiyo, ni lazima tu shabaha iliyokuwa imewekwa nyuma ya mgongo wake kwa kitambo ndiyo ilifyatuliwa hatimaye. Hakuwa na jinsi tena. Akajiondokea tu, akirudi hospitalini na kutumia pesa kidogo aliyopewa kuongeza dawa za mama yake, na sasa akawa ameachwa mikono mitupu kabisa.

Aliendelea kujitahidi kutafuta huku na kule, akauza na kitochi chake, akawaomba baadhi ya watu aliofahamiana nao wamsaidie kumuunganisha kwa kazi zingine, lakini alielewa kwamba hata kama angepata kazi, kuja kuishika pesa ambayo ingemsaidia mama yake ni jambo ambalo lingepitisha muda mrefu. Na mama yake hakuwa na muda mrefu wa kusubiri. Hapo tena bado kulikuwa na suala la kodi ya chumba chao walichopanga, yaani aliwaza labda atafute mtu wa kumuuzia makochi yao mawili madogo haraka, wakati huo akitafuta kitu cha uhakika, lakini akaishia kuvunjika moyo tu kwa kuwa alijua hivyo ni vitu ambavyo vingegoma kuleta matokeo yenye faida iliyodumu.

Akiwa ameishiwa pesa na wazo zuri la kumpa msaada aliohitaji haraka, akaamua tu kufanya jambo ambalo hakudhani angekuja kuwahi kufanya. Kulikuwa na shangazi yake mmoja aliyeishi upande tofauti wa mji aliokuwepo, na huyo alikuwa ni mdogo wake na marehemu baba yake. Kama ndugu zao wengi tu, huyo mwanamke alikuwa amejitenga nao pia, zaidi ni watoto wake wawili tu ndiyo ambao walijuana na Paulina kipindi fulani cha nyuma na kujenga urafiki wa kindugu. Walikuwa wadogo, shule za msingi, na ni kutokea kipindi hicho cha nyuma wameonana ndiyo Paulina alionana kwa mara ya mwisho na huyo shangazi yake, hata mawasiliano pamoja naye hakuwa nayo.

Alielewa kwamba shangazi yake angekuwa na kazi iliyomsaidia kuvuna pesa nyingi, kwa sababu alisikika kuwa na maisha mazuri akiwa mzazi pekee kwa watoto wake baada ya kutengana na baba yao. Hata alitembelea gari. Hivyo Paulina akaona ajaribu kwenda kwake na kuongea naye ana kwa ana, maana kwa ndugu zao wote, angalau huyo angeweza kufikika, ikiwa kama alimkumbuka bado. Kwa hiyo akakopa hela kutoka kwa mtu aliyefahamiana naye ili aitumie kwa ajili ya nauli, akiwa hata hana uhakika wa kuweza kuirudisha upesi, lakini akajipa tu matumaini.

Ikiwa ni siku ya Jumapili, Paulina alielewa kwamba shangazi yake angeweza kuwa nyumbani, na alipakumbuka kwake vizuri sana ingawa muda ulikuwa umepita. Hivyo akachukua daladala, mwendo ukiwa ni mrefu na kumlazimu apande ya ziada mpaka kufika hayo maeneo, na kutokea kituoni akatembea hadi kuifikia nyumba aliyojua shangazi yake aliishi. Alijua ndiyo penyewe, lakini palikuwa pamebadilika. Yaani, palipendeza zaidi ya vile alivyopaona zamani wakati yuko mdogo, ikionyesha kweli shangazi yake alikuwa amepiga hatua. Ilikuwa muhimu sasa kujaribu kumwomba amsaidie mama yake, na angejitoa hata kumfanyia kazi za ndani kwa muda wote ili kulipa deni.

Nyumba ilikuwa na uzio wa ukuta wa matofali ambayo hayajapigwa simenti, ukiwa na geti kubwa jeusi, naye akaenda na kugonga mara chache, kisha akasubiri. Eneo alilokuwepo lilikuwa na makazi mengi ya watu, nyumba za kawaida tu kwenye ujirani, na barabara changarawe iliyopitisha magari machache na waendesha baiskeli. Geti likaanza kusikika likifunguliwa, naye Paulina akaangalia hapo kwa utayari. Akatoka kijana wa kiume kwenye miaka ya utineja, akiwa mwembamba na mrefu, na huyo hakufahamika kwa Paulina, hata kijana mwenyewe alimwangalia huyu dada kigeni.

Paulina, akiwa amejishika viganja, akatabasamu kiasi na kusema, "Za saa hizi?"

"Nzuri tu. Karibu," huyo kijana akajibu.

"Asante. Samahani, eti... nimemkuta mama Inno?" Paulina akamuuliza.

Kijana huyo akamshusha na kumpandisha, akionekana kutafakari swali lake.

"Hapa si ni kwa mama innocent?" Paulina akamuuliza tena.

"Ndiyo. We' ni nani?" kijana akauliza.

"Mimi naitwa Paulina. Mama Inno ni shangazi yangu. Sijui nimemkuta?" Paulina akaongea kwa upole.

"Shangazi yako?" kijana akauliza tena.

Paulina akabaki kumtazama tu kwa kutatizika.

Huyo kijana alikuwa akimtazama kwa njia fulani ya kudadisi eti, akiangalia zaidi kandambili nyekundu alizovaa mgeni, kisha akamwambia, "Njoo. Ingia."

Paulina akatii na kuingia ndani hapo taratibu, huyo kijana akifunga geti, naye akaanza kuongozwa kuikaribia nyumba zaidi. Ilikuwa kubwa kiasi na pana, ikipakwa rangi nyeupe, na aliona gari dogo aina ya Toyota Corolla nyeupe likiegeshwa hapo nje. Kijana akamwambia amsubirie sehemu ya varanda ili aende kumwita mwenye mji, naye Paulina akatii. Akabaki hapo nje akiwa anatoa maombi kimoyomoyo kwamba jaribio lake lizae matunda mazuri, na ndipo mlango ukafunguliwa tena na mwanamke mtu mzima kutoka humo ndani.

Paulina alimtambua huyo kuwa shangazi yake. Alikuwa mmoja wa wale wanawake waliopenda kuonekana kuwa kama wasichana bado, maana muda mwingi alijiweka katika hali ya kupendeza. Hapa alikuwa amevalia blauzi nyeupe na suruali nyekundu yenye kubana, akiwa na umbo nene kiasi, na wigi la nywele fupi likifunika kichwa chake kipana. Alikuwa na sura nene ya nyodo. Alitoka na kusimama mbele ya Paulina huku yule kijana akiwa kwa nyuma mlangoni, na alimwangalia mgeni kwa njia makini kama vile bado hajamtambua.

Paulina akatoa ishara ya kupiga magoti na kusema, "Shikamoo shangazi?"

Huyo mwanamke akavuta fikira kwanza, kisha akajibu, "Marahaba."

Paulina akatulia na kuendelea kumwangalia usoni.

"Paulina?" mwanamke huyo akauliza.

"Ndiyo shangazi. Ni mimi," Paulina akajibu kwa unyoofu.

"Eh! Jamani! Ni siku nyingi sana, umekua! Nilikuwa hadi nimeshakusahau," shangazi akasema hivyo.

Paulina akaangalia chini tu kiwasiwasi.

"Umekuja huku mwenyewe?" shangazi akauliza.

Paulina akatikisa kichwa kukubali.

"Kulikoni? Wazima huko kwenu?" shangazi akauliza tena.

Paulina akatikisa kichwa kukanusha na kusema, "Hali siyo nzuri sana, shangazi. Nimekuja kukuomba unisaidie."

Shangazi yake akakaza macho, halafu akakunjia mikono yake kifuani na kusema, "Shida ni nini?"

Paulina akaona utata kiasi kuongelea mambo yake mazito huku kijana mdogo akiwa hapo pembeni, na shangazi yake akaelewa hilo.

"Shebby, nenda ndani. Rudi ndani!" akamwambia hivyo huyo kijana.

Baada ya kijana kuigia ndani, shangazi akafunga mlango, halafu akasimama kwa kuegamia ukuta ili amsikilize mpwa wake.

Paulina akasema, "Shangazi, kwanza naomba sama...."

"Paulina, acha kuzunguka. Ongea point iliyokuleta, maana ushaanza kunitisha. Una matatizo gani? Umefukuzwa, au?"

"Hapana, siyo hivyo..."

"Sema sasa shida ni nini. Halafu, usiniite shangazi sasa hivi, maana mpaka tunaonekana kulingana kabisa hahahah..." shangazi akaongea kimasihara eti.

Paulina akatazama tu pembeni.

"Umesikia? We' niite Roza. Kila mtu ananijua hivyo," shangazi akasema hivyo kimadoido.

"Sawa," Paulina akajibu.

"Enhe, leta maneno," Roza akasema hivyo.

"Sha... a... yaani, mama anaumwa. Sana. Amelazwa hospitali," Paulina akamfahamisha.

"Wewe! Lini jamani?" Roza akajifanya kushangaa.

"Ana kama wiki... inaelekea ya pili..."

"Anaumwa nini?"

"Ana uvimbe tumboni."

"Eh! Masikini!"

"Anatakiwa kufanyiwa upasuaji, madaktari wanasema asipoondolewa hiyo shida, atakufa..."

"Mtume!" Roza akasema hivyo.

Paulina akaanza kulengwa na machozi.

"Ah! Pole sana mwanangu. Na, pole kwa mama yako. Sasa... eh! Inakuwaje? Umeshapata hela ya kumsaidia atibiwe?" Roza akauliza.

"Hapana. Nimetumia hela niliyokuwa nayo ili madaktari wampe... hhh... wampe utunzaji hiyo wiki, halafu...."

"Kwa hiyo yote imeisha sasa hivi?"

"Ndiyo."

"Ni shi'ngapi?"

"Niliyotumia kwake, kama laki tatu na...."

"Hapana, namaanisha... hela ya kumfanyia huo upasuaji yaani. Ni shi'ngapi?" Roza akamsahihisha.

"Inafika hadi milioni mbili shangazi..." Paulina akaongea kwa huzuni, machozi yakiwa yameanza kumtoka.

Roza akapiga ulimi wake mara nyingi kwa njia ya kusikitika, naye akasema, "Hapo itakuwa kasheshe! Hiyo ni hela nyingi!"

Paulina akajifuta machozi na kusema, "Shangazi..."

"Roza. Niite Roza," akamkatisha.

"Samahani. Roza... ninaomba unisaidie. Sina... hhh... pengine pa kupata hela ya haraka, yaani sasa hivi nimeishiwa kabisa, na...."

"Paulina natamani sana kama ningeweza kukusaidia, lakini na mimi sina. Yaani sina kabisa. Na sasa hivi, sidhani hata ukienda kwa nani ukajaribu kuomba hiyo hela utapewa. Nakwambia ukweli. Ni ngumu. Mpaka uifanyie kazi kwa muda mrefu," Roza akamwambia hivyo.

Paulina akahisi huzuni zaidi, naye akakaza kilio chake na kusema, "Naomba unisaidie shangaz... Roza... nakuomba Roza unisaidie..."

"Kwani, si unafanya kazi, au?"

"Nilikuwa na kazi ndiyo, lakini... nikaachishwa..."

"Wapi?"

"Kwenye baa moja. Kipato chenyewe hakikuwa kingi, na niliyotunza ndiyo nikatumia kwa ajili ya dawa za mama... sasa hivi sina hhh..."

"Kwa nini ulifukuzwa kazini?"

"Bosi wangu alikuwa ananitaka, nikamkatalia. Ndiyo akatafuta sababu ya kuniachisha mama alipoanza kuumwa. Hhh... yaani sijui la kufanya sasa hivi..."

Roza akaangalia pembeni huku akizungusha macho yake na kutikisa kichwa.

"Roza tafadhali, nakuomba. Unaweza ukawa unajua... hhh... unajuana na watu... mfff... labda kazini kwako, au popote ambapo naweza kukopa hela ili mama afanyiwe upasuaji... halafu nifanye kazi kwa huo muda wote kufidishia...."

"He! We' Paulina! Hiyo ni akili gani wewe?" Roza akamwambia hivyo.

Paulina akawa anajifuta tu machozi.

"Unafikiri itakuwa rahisi? Mambo hayaendi hivyo. Ni bora tu kama ungekubali kutembea na huyo bosi wako ili umwombe hela, usingekuwa unahangaika hivi..." Roza akamwambia.

"Shangazi..." Paulina akamwita kwa huzuni.

"Mimi sijui nakusaidiaje sasa. Hata kama ungesema upate mtu wa kukupa hela kama hivyo, umfanyie kazi, baada ya hapo nini? Mama yako atatunzwa na nani? Maana utakuwa bize kufanya kazi kwa ajili ya hela ambayo imeshatumika, mama yako atakula nini? Na wewe utaishije? Si utakuwa unatia saini mkataba wa kifo chake na chako kwa wakati mmoja?" Roza akamwambia hivyo kwa uthabiti.

Paulina akaendelea kulia zaidi bila kutoa sauti ya juu.

"Ah... me sijui kwa kweli. Sina hela yaani, sina. Na wewe hivyo unavyolia unajua haikusaidii... kulia haikusaidii lolote Paulina. Ni vema utumie tu akili nyingine," Roza akamwambia hivyo.

Paulina akajifuta machozi na kusema, "Sijui nafanyaje, shangazi. Nimeshajaribu... hhh... najaribu... nashindwa. Nakuomba unisaidie, nitafanya kazi popote, nitaenda... mff... nitakufanyia hata wewe. Naomba unisaidie. Mama yangu ndiyo pekee niliyebaki naye, amenilea kwa maumivu, ameshinda njaa ili mimi nile, amenisaidia hata nikasoma kidogo, mff... nahitaji sana kumsaidia... hhh... ninakuomba sana shangazi..."

Mwanamke huyu mdogo aliongea kwa hisia sana, na Roza akawa anamwangalia kwa njia makini. Akamshusha na kumpandisha, akiwa ameingiwa na wazo fulani, naye akamuuliza, "Una miaka mingapi sasa hivi?"

"Ishirini na mbili," Paulina akasema hivyo upesi.

Roza akavuta fikira kwanza, kisha akamwangalia hapa na pale mwilini kama kumkagua, halafu akamshika mabegani na kumgeuza ili amtazame kwa nyuma, na hapo akawa ameridhika. Paulina hakuelewa shangazi yake anafanya nini, lakini akahisi kwamba tayari alikuwa amepata wazo la kumsaidia, hivyo akatulia tu ili angoje kuona kama matumaini yake yangezaa matunda.

Roza akamtazamisha Paulina kwake tena, na kwa sauti ya chini akamwambia, "Okay. Umenipa wazo, Paulina. Kuna kazi naijua unayoweza kufanya, ukapata hela nyingi haraka."

Paulina akaanza kucheka-kulia kwa hisia, naye akajifuta machozi zaidi na kusema, "Kweli shangazi? K-k--kama ipo... unaweza kuni...."

"Nisikilize. Siyo kwamba kama ipo, hiyo kazi ipo. Na wewe unaweza ndiyo kuifanya, kama utakuwa tayari kuifanya," Roza akamwambia hivyo.

Paulina akatulia zaidi, akibaki kumtazama mwanamke huyo kwa umakini.

"Unataka kumsaidia mama yako, si ndiyo?" Roza akamuuliza.

Paulina akatikisa kichwa kukubali.

"Sawa. Nitakusaidia uipate hii kazi. Ni rahisi sana kwa wanawake, na tena wewe... itakuwa nyepesi mno. We' siyo mtoto sasa hivi, najua unaelewa namaanisha nini," Roza akamwambia hivyo kwa sauti ya chini.

Paulina akaangalia chini kiutafakari.

"Sina njia nyingine ya kukusaidia, hii ndiyo ya haraka. Kwa hiyo, useme ikiwa kweli uko tayari, ama...."

"Niko tayari," Paulina akamkatisha kwa kusema hivyo.

Roza akashusha pumzi kwa njia ya kuridhika.

"Nitaifanya shangazi. Namaanisha... niko tayari kuifanya... Roza," Paulina akaongea kwa njia hakika.

Shangazi Roza akatabasamu kiupande, huku akimwangalia mwanamke huyo kijana kwa macho yaliyojaa... hila, naye akasema, "Vizuri. Pangusa hayo machozi sasa, nifate ndani."

Baada ya mwanamke huyo kusema hivyo, akageuka na kuufungua mlango kisha kuingia ndani kwake tena.

Kwa sekunde chache, Paulina akabaki hapo varandani akiwa ameanza kupitisha maswali mengi kichwani kwake, kwa kuwa alielewa kwamba huenda njia ambayo shangazi yake angetumia kumsaidia isingekuwa ya kipendacho-roho kwake yeye, lakini hakuona namna nyingine ya kupata msaada ikiwa tayari hapo ofa iliibuka. Angetakiwa kuichukua tu, kivyovyote ambavyo ingekuja. Akajitia ujasiri, kwa ajili ya mama yake mzazi, naye akaanza kujifuta machozi na kujisawazisha kwa njia iliyofaa kabisa kwenda kukabiliana na hali hii mpya, kisha akaingia ndani huko pia.





★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Screenshot_20250402-230106 (1).png
 
DOSARI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Uhalifu, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA PILI

★★★★★★★★★★★★★


Tunakuja upande mwingine wa jiji analoishi bwana Reuben, ikiwa ni katikati ya usiku uitwao wa manane. Pande nyingi za jiji hilo tayari hekaheka na shughuli nyingi kubwa zilikuwa zimepumzishwa kwa muda huo, na kwa huku kulikuwa na duka moja kubwa la vifaa vingi maalumu vya kielektoni kwa manunuzi ya wateja kama vile runinga maridadi, sabuba, ving'amuzi vya michezo (game), na hata vifaa kama friji, majiko ya umeme, oveni, mashine za kufua, na kadhalika. Likiwa moja kati ya sehemu nyingi ambazo zimefungwa kwa wakati huu, linapewa ulinzi na wanausalama wawili maalumu, kwa kuwa siyo kama maduka mengine kwenye eneo hilo. Ni kubwa sana, wakibeba bunduki za ulinzi, na wanalinda kwa mzunguko kuangalia usalama na sehemu zingine za karibu na hapo.

Kama ilivyo kawaida, kazi yao mara nyingi inakuwa yenye kuboa kwa sababu hakuna mtu anayethubutu kusogea eneo hilo kwa wakati huo, yaani ni utaratibu usiokwepeka kwa mtu yeyote kutoonekana katikati ya usiku akitembea karibu na hapo, isipokuwa gari moja-moja huko barabarani, na kwa wachache ambao wangepita ingekuwa kufatwa na kuombwa watoe sababu zilizonyooka kuhusu ni kwa nini wanatembea usiku sana. Basi, ikiwa ni mida ya saa nane usiku, walinzi hawa wakawa wameketi pamoja kwenye benchi fupi chini ya mti mdogo karibu na jengo hilo, na ili kupisha muda wakawa wakishushia kahawa ambayo sikuzote walitunza kwenye chupa zao ili kusaidia umakini wao mpaka kukucha.

Wakiwa wanaongelea mambo ya hapa na pale, kutokea kwenye kona ya jengo hilo kuelekea upande uliokuwa na ukuta uliokinza eneo lao na mnara mrefu wa mtandao, likarushwa kopo dogo la soda, lililopiga ardhi kwa kishindo kilichotoa sauti yenye kushtua kiasi. Mshtuko sanasana kutokana na kutojulikana kimerushwa na nani ndiyo jambo lililowatia hisi ya tahadhari walinzi hao na upesi kunyanyuka huku wakielekeza bunduki zao kuelekea upande huo. Wakiwa makini, kwa pamoja wakaanza kuelekea sehemu ambayo kikopo hicho kilitokea, na mmoja akamtangulia mwenzake ili mwingine awe nyuma kuangalia dukuduku lolote na huku walikopaacha, ingawa walienda sambamba.

Kukaribia sehemu hiyo kikopo hicho kilipokuwa, kikarushwa kingine tena kutokea upande wa pili wa ukuta ule, na ikawa wazi kwa walinzi hawa kwamba kuna mtu alikuwa akiwaletea mzaha. Wote wakafikia sehemu hiyo na kupeana ishara ya kwamba mmoja azunguke kwenda upande huo wa mnara kuona nani anawaletea zengwe, na mwingine abaki kulinda jengo lao, na baada tu ya kukubaliana, ghafla sana mlinzi aliyekuwa akitaka kwenda huko akashtukia anarukiwa na kitu kizito kilichomwangusha chini kwa nguvu!

Ile mwenzake ameshtuka pia na kutazama kilichotokea, akaona kwamba ni mtu mwingine alikuwa amemrukia mwenziye, bila shaka akitokea ukutani pale. Alionekana kuvaa nguo nyeusi karibia mwili wake wote mpaka kichwani, yaani akikiziba kwa kificha uso, na yeye mlinzi upesi akapiga hatua ili amsaidie mwenzake pale aliposhtukia anakabwa kutokea nyuma na kupigwa ngeta kali miguuni iliyomwangusha chini sambamba na aliyemkaba.

Vishindo vikazidi kuongezeka baada ya walinzi hao kuvamiwa na watu wengine zaidi, waliojiunga na wakabaji hao na kuwashushia vipondo vya nguvu kwa ngumi na mateke, nao wakanyang'anywa bunduki zao haraka huku wakikandamizwa chini. Ardhi ilikuwa ya kokoto ngumu zilizogandishwa kwa pamoja, hivyo walinzi walihisi maumivu makali na kutoa sauti zilizoonyesha hilo.

"Fasta, kafungue!"

Sauti ya mmoja wa wakabaji hao ikaamuru hivyo, na baadhi yao wakaondoka hapo kulielekea jengo la duka haraka.

"Wanyanyue."

Sauti hiyo ikaamuru tena. Walinzi kwa pamoja wakavutwa kwa nguvu na kuwekwa katika hali ya kupigishwa magoti, na sasa waliweza kuwaona wahasimu wao waliokuwa wamekuja kufanya uhalifu huo. Haikuwa kuwaona nyusoni kabisa, kwa sababu wote walizificha kwa vificha uso vyeusi vilivyofunika vichwa vyao vyote kuacha uwazi mdogo machoni na midomoni. Ikawa wazi hao hawakuwa wakabaji tu, bali walikuwa majambazi. Waliosimama hapo walikuwa wanne, na wawili wakiwa karibu na walinzi wakawaambia waweke mikono yao vichwani na watulie hivyo hivyo. Wakatii. Wengine wawili walishikilia bunduki pia ambazo hazikuwa za wale walinzi, wakiwaelekezea ili wasifanye ujanja wowote, na kweli hawakuwa na ujanja wowote tena.

Ikionekana wazi kwamba majambazi wengine walikuwa wamevunja na kuingia dukani kule, sauti ya mngurumo wa gari ikaanza kukaribia sehemu hiyo, na walinzi wakaona gari la pick-up jeusi likija kwa kasi na kisha kwenda kuegeshwa karibu na milango ya duka. Gari lingine jeusi pia kama hiace likafuata, lenyewe likisimama huko mbele zaidi kuelekea barabara, na kwenye ile pick-up akashuka mwanaume mmoja, akificha uso pia, naye akaelekea kule ndani.

Kutokea dukani, majambazi watatu wakaanza kutoka na vitu vingi na kuviweka kwenye gari, TV, ving'amuzi, sabufa, vyombo vingi vya umeme vyenye thamani ghali, yote hayo walinzi wakijionea tu, lakini hawakubeba vitu vizito kama friji kubwa. Walihakikisha wanasomba kila kitu kilichotoshea garini, na baada ya kujaza, mmoja wao akachukua dumu moja lenye mafuta ya petroli kutoka garini na kuanza kulimwagia duka hilo kutokea kule ndani kuja hadi nje.

Wakati mafuta yakiwa yanamwagwa, mmoja wa majambazi hao akaanza kuelekea karibu na sehemu ambayo walinzi walipigishwa magoti, akiwa na mwili mpana na mrefu, naye akasimama karibu nao zaidi akiwaangalia kwa umakini.

"Dakika kumi na tano, over. Twendeni," jambazi mtoa amri akasema.

"Na hawa?" mwingine akauliza.

"Waacheni. Walaze hapo tuondoke," jambazi mtoa amri akamjibu.

"What's the fun in that? (Kuna burudisho gani kwenye hilo?)"

Kauli hiyo ikatoka kwa yule jambazi aliyekuwa amewasogelea walinzi, akiwa na sauti nzito lakini tulivu, na akiongea taratibu lakini kwa njia iliyotikisa hisia upesi mno. Jambazi aliyewaongoza alikuwa tayari kuondoka hapo baada ya kuwaambia wenzake wawaache tu walinzi hao, lakini akaishia kumtazama huyo mmoja kwa umakini baada ya kumsikia anauliza hivyo. Akawaangalia walinzi na kuona namna ambavyo waliwatazama majambazi kwa maumivu, naye akarudi kumtazama tena mwenziye.

"Nimesema waachwe. Una tatizo na hilo?" jambazi aliyewaongoza akamuuliza hivyo.

Mwenzake, bila kumtazama, akauliza, "Kwa nini?"

"Hakuna lolote wameona as far as we're concerned, hiyo ndiyo sababu. Narudia tena, una tatizo na hilo?" aliyewaongoza akamuuliza.

Huyu mwenziye akamgeukia hatimaye na kutazamana naye kwa njia iliyoonyesha damu inapanda moto, kisha akavuta kificha uso chake mwenyewe na kuiacha sura yake wazi kwa makusudi. Wenzake walimshangaa!

"Unafanya nini?!" jambazi aliyewaongoza akamuuliza kwa mkazo.

Mwanaume huyu aliyevua kificha uso chake akatabasamu kiasi, naye akasema, "Wameuona uso wangu sasa... so hatuwezi kuwaacha."

Aliongea huku akitoa tabasamu lenye hila sana, naye akawaangalia walinzi tena. Mwanaume huyu alikuwa mwenye rasi nene na ndefu sana kichwani, mweusi, na sura yake yenye ukomavu ilitoa taswira moja ambayo yeyote yule aitazamaye angeipata upesi; ukatili. Alikuwa na mwili mpana na uliojengeka vyema sana kiume, mikono yake yote ikikolezwa rangi nyeusi kwa michoro ya tattoo aliyoijaza mpaka ndani ya torso. Macho yake yalikuwa na rangi ya udhahabu kwenye lenzi na hivyo kuonekana kung'aa hasa ilipokuwa giza, jambo lililotoa taswira ajabu ya mwanzo kumwelekea mwanaume huyu. Kitendo chake hapo kilionyesha kwamba nia yake ilikuwa kuwaondoa kabisa walinzi hao ingawa wenzake hawakuona uhitaji wa kufanya jambo hilo, na hilo likamtia hasira sana aliyewaongoza kwenye uhalifu wakati huu.

Aliyekuwa anamwagia jengo mafuta akafika pembeni ya wawili hawa, akiwa amelitegesha dumu la mafuta karibu na duka lile, naye akamwambia aliyewaongoza, "Tayari, tusepe. Muda umeisha."

"Ona jamaa alichofanya!" mwingine akamwambia hivyo, kumaanisha ishu ya mwenzao kuondoa kificha uso.

Aliyeendesha ile hiace nyeusi akafika hapo pia baada ya kuona kama kuna mvurugo baina ya wenzake. Sasa majambazi wote wakakutana hapo katikati, wakiwa nane.

Aliyewaongoza akamshika mkononi mwanaume huyo aliyevua kificha uso na kumwambia, "Mbona unaleta ufala mwana? Unajua hatuna muda wa kupoteza halafu una...."

Mwanaume huyo akauvuta mkono wake kwa nguvu na kumnyooshea kidole usoni kiukali, naye akasema, "Usije rudia nigusa tena!"

"Au utafanya nini?" aliyewaongoza akamuuliza kibabe na kumsogelea usoni zaidi.

Ikaonekana kwamba wanataka kupigana, na wenzao wakaingilia kati kuwaachanisha kwa kuwasukuma.

"Aisee, muda!" mmoja wao akasema.

"Hii haikuwa order ya boss... anataka tuwaue hawa kwa basi tu..." aliyewaongoza akasema hivyo.

"F(...) off! I'm dealing with this myself (Toka! Ninashughulika nalo hili mwenyewe)," mwanaume huyo mwenye rasi akasema.

"Utajua mwenyewe. Tuondokeni," aliyewaongoza akasema hivyo.

"Tunapaswa kuondoka pamoja, hiyo ndo' code," mwingine akamwambia.

"Waue basi faster, uridhike, tuondoke," mmojawapo akamwambia rasi.

Jamaa akatabasamu.

"Msi... msitufanye lolote joh... sisi hatutasema lolote, hatujaona chochote..." mmoja wa walinzi akasema hivyo kwa hofu.

Aliyekuwa akiwaongoza majambazi wenziye akatikisa kichwa kwa kuudhiwa sana na jambo hili, na huyo mwanaume mwenye rasi akachukua bunduki kutoka kwa mwenziye huku akitabasamu kwa hila. Walinzi waliogopa sana. Wakawa wanaongea na kujongea kwa kujirudi-rudi nyuma, na huyo mwanaume mwenye rasi akamtandika mmojawapo kwa uchuma wa bunduki kichwani kwake. Alimpiga vibaya sana mpaka damu zikafurumka kama bomba lililopasuka kwa pigo hilo moja tu, naye akadondokea pembeni huku akishtuka mwilini.

Huku akiwa anatabasamu, mwanaume huyu akamwangalia mlinzi wa pembeni, ambaye alipumua kwa hofu kiasi, lakini akajitia ujasiri na kunyanyuka upesi. Akamfuata mwanaume huyo na kumpamia kwa nguvu ili ajaribu pambano pamoja naye, lakini jamaa akarudi nyuma kidogo tu bila kuweweseka wala nini. Alikuwa na nguvu sana. Mlinzi akabaki kusimama huku akimwangalia kwa wasiwasi mwingi, hapo akiwa kama amezungukwa na majambazi wote, na hapo hapo mwanaume mwenye rasi akampamia kwa nguvu na kumdondosha chini. Akaanza kumpiga kwa uchuma wa bunduki kichwani mara nyingi sana na kukipasua vibaya mno, na hata ilipokuwa wazi kwamba mlinzi amepoteza maisha, bado mwanaume huyu akaendelea tu kukitoboa kichwa hicho hadi kukizagaza kwa njia isiyotamanika hata kidogo.

Majambazi wengine walimwangalia mwanaume huyo kwa ukakasi alipokuwa akifanya hivyo, mwenyewe akifurahia kweli kufanya ukatili huo, na aliporidhika, akajilamba damu zilizomrukia midomoni na kufumba macho huku anatabasamu. Wenzake wakaangaliana mmoja na mwenzake na hata kutikisiana vichwa kwa kutopendezwa na roho hiyo mbaya kupitiliza ya mwenzao aliyependa kumwaga damu, nao wakaanza kusambaa na kuyarudia magari upesi ili waondoke; akibaki yule aliyewaongoza hapo, na rasi mwenyewe. Huyu mwanaume mwenye rasi akasimama, akiwa amerukiwa na damu nyingi sana usoni, kisha akamtazama mwenzake pembeni.

Akamwambia, "Now that... that was fun (Sasa hiyo... hiyo ndiyo imeburudisha)."

Jambazi mwongozaji akasema, "We' ni psycho mmoja mbovu sana. Unahitaji msaada."

"Yeah, yeah. F(...) you too," mwanaume mwenye rasi akasema hivyo kizembe.

Mwenzake akaondoka na kuelekea garini upesi, na mwanaume huyu akaendelea kusimama hapo hapo mpaka pick-up ilipokaribia upande wake na kusimama. Akiwa ameishikilia bunduki mkononi, mwanaume huyu akaielekeza upande wa duka lile na kufyatua risasi moja kulielekea dumu la mafuta, kitu ambacho kikafanya moto uanze kuwaka kwa kasi sana kuelekea huko ndani. Akafungua mlango wa gari na kuingia haraka, ile hiace nyingine ikiwa imeshatangulia kuondoka, nao wakafata pia na kutokomea pasipojulikana huku eneo hilo likiachwa ndani ya moto mkali uliozidi kuongezeka. Kazi yao ikawa imekamilika.


★★★


Jumatatu ikakucha hatimaye. Ikiwa ndiyo jambo lililoshika kasi zaidi kujulikana, tukio hilo la duka kuungua kwa moto lilienea sehemu nyingi za jiji na nchi nzima kiujumla baada ya vyombo vya habari kusambaza taarifa. Moto huo ulifanikiwa kuzimwa baada ya magari ya zima-moto kufika eneo la tukio, na maaskari walipofanya uchunguzi wakagundua kuwa duka hilo liliunguzwa kwa makusudi na wahalifu waliofika kuiba na kuwaua walinzi wa hapo, huku wakitoa ahadi kuwatafuta na kuwakamata watu hao ili waadhibiwe. Ilionekana wazi kwamba duka hilo lilikuwa limelengwa shabaha ya moja kwa moja, kama vile kuna mtu alitaka kumkomoa mwenye nalo, hivyo maaskari walihitaji kuanza kuchunguza upande wa mmiliki kuona kama angefahamu mtu yeyote aliyetaka kumfanyia kitendo kama hicho kwa sababu za uadui.

Hayo yakiwa yanaendelea, upande wa bwana Reuben siku hii ilianza kwa ukawaida wake wa kuelekea kazini, kwenye kampuni yaani, na hata yeye pia alikuwa amepata taarifa za tukio hilo la moto. Kwake yeye lilikuwa na umuhimu wa kadiri kubwa kwa kuwa mwenye duka lile alifahamiana naye, akiwa kama rafiki wa karibu sana, hivyo alifanya kuwasiliana naye ili kumpa pole na kuchanganua namna ambavyo mambo yangekwenda kutokea hapo. Huyo mtu alikuwa mbaba mwenye umri mkubwa kumpita Reuben, aliyeitwa Stanslaus Mwita, ambaye alikuwa na maisha mazuri pia na mfanyabiashara mwenye maduka kadhaa makubwa ya vitu mbalimbali yaliyomwingizia pesa nyingi. Hilo moja ndiyo likawa limeenda.

Baada ya kuongea naye kwa kina, Reuben akajua maoni ya Stanslaus kuwa kwamba kuna watu walimlenga yeye moja kwa moja ndiyo, wakitaka kumwangusha, ndiyo sababu wakamfanyia hivyo kwenye moja ya maduka yake makubwa zaidi. Hakujua nani kihususa, lakini kwa aliokuwa amewafikiria, aliwapa majina kwa maaskari, hivyo wangemsaidia kuwatafuta watu hao na kufanikisha kuwakamata baadaye. Reuben akamuunga mkono kwa hilo na kusema ikiwa angehitaji wasaidiane kwa lolote lile, basi asisite kumwambia, nao wakaagana vizuri.

Akaendelea kuwa ofisini kwake hadi mida ya mchana, akipokea, kushughulikia, na kutuma kazi zilizohusika kwa siku hii, huku akiwa na hamu kubwa kupisha wakati ili ufike muda ambao mke wake angefika jijini hatimaye. Lydia alikuwa anarudi siku hii, na bila shaka Reuben angekwenda kumpokea stendi baadaye. Akiwa ndiyo anafikiria kutoka mara moja ili akapate chakula, akapigiwa simu na yule rafiki yake ambaye walikutana jana asubuhi mgahawani kwa mkewe, Francis. Akakumbuka kuwa, jana jioni wakati yupo nyumbani, rafiki yake huyu aliwasiliana naye, nao wakakubaliana kukutana leo hapa hapa ofisini kwake. Kumtembelea, apajue yaani.

Ah, kutokana na mambo kuwa mengi yaani jambo hili lingetoweka kabisa akilini kwa Reuben, hivyo akapokea na kuzungumza naye wapangane vizuri hata zaidi. Francis akamwambia kwamba kwa muda huo tayari alikuwa ameshafika nje ya jengo la kampuni yao Reuben, hivyo alihitaji tu mwongozo ili afike ofisini kwake waweze kuonana. Reuben hakutarajia Francis awe ameshafika eneo hilo, lakini kwake hiki kikawa kitu kizuri, angalau Francis hakusahau ahadi kama yeye alivyokuwa mbali na hilo wazo tayari. Hivyo, akamwelekeza vyema kabisa, naye Francis akapanda mpaka kwenye ghorofa iliyobeba ofisi ya bwana Reuben.

Francis akafika ofisini kwake Reuben kwa kukaribishwa na msaidizi wa hapo, mwanamke kijana mwenye mwonekano mzuri, naye akaelekea hadi mezani kwa "bosi" mwenyewe na kuunganisha naye viganja kisalamu, wote wakipeana tabasamu kwa furaha.

"Ah, mkubwa uko penyewe hapa," Francis akasema hivyo kabla ya kukaa kitini.

"Yeah, karibu sana bro," Reuben akamwambia hivyo kwa utulivu.

"Aisee, nilifikiri ningepotea huku bwana, hizi kona za haya majengo zinachanganya kweli..."

"Hahah... haujatembelea hizi pande sana?"

"Siyo sana. Yaani... mara nyingi napapita tu kama nikiwa kwenye usafiri. Kutembea si sana," Francis akasema.

"Ndiyo tuko hapa bwana, karibu sana," Reuben akamwambia.

"Nimekaribia kaka. Mambo mazuri sana haya..."

"Yeah, ila yana ugumu wake. Angalau lakini tunapata, tunasonga mbele. Vipi wewe? Familia?"

"Ah, me nipo tu kaka. Kama nilivyokwambia jana, yaani ndiyo nimeingia kwenye harakati za spare juzi kati hapo, biashara imeanza kukua kidogo, so now napangilia hilo suala la familia..."

"Hahah... ndoa iko njiani..."

"Eeh, na me nitulie kama we' mkurugenzi."

"Hongera sana."

"Asante. Vipi na wewe? Ulisema bi mkubwa yuko safarini eh?"

"Eeh, yuko njiani kurudi. Nilikuwa ndo' nataka nikapate lunch McDonald hapo nje, nimalizie ishu kadhaa hapa ndiyo nielekee huko stendi..."

"Ooh, ataingia mapema tu?"

"Saa kumi na mbili sanasana..."

"Okay. Kumbe hujapata msosi bado?"

"Toka asubuhi."

"Aah..."

"Hahahah... kazi hizo ndugu yangu. We' ushapata?"

"Yeah, saa tisa sa'hivi, tumbo lisharidhika hili. We' kama vipi, fanya twende upate msosi, halafu nitapitilizia huko huko..." Francis akasema.

"Okay. Kuna sehemu nyingine ulikuwa unaenda?" Reuben akauliza.

"Eeeh, napita kwanza maeneo... then narudi dukani kwangu. Tutapanga na we' uje upaone," Francis akamwambia.

Reuben akasimama huku akisema, "Fresh, suala ni muda kubana, ila Jumapili tutafanya jambo."

Simu yake ikaanza kuita, wakati huo Francis amesimama pia huku akisema, "Eeh, Jumapili ndo' imetulia zaidi kwenda kupiga mbili tatu na nini..."

Reuben akacheka kidogo huku akitoa simu mfukoni, kukuta namba ngeni, naye akapokea na kuchukua funguo mezani huku akianza kumwelekea Francis ili waondoke. Akaanza kuongea na mtu aliyempigia, mwanaume, akiwa mgeni kwake, naye alipomwambia yeye ni nani na dhumuni la kumpigia, Reuben akakatisha hatua zake na kubaki ameangalia chini kwa mkazo sana. Francis alikuwa ametangulia mbele kidogo na kugeuka nyuma baada ya kuona mwenzake amesimama, na kwa jinsi ambavyo sura ya Reuben ilionyesha mkazo, akahisi kwamba kulikuwa na tatizo. Reuben hakusema lolote tena kumwelekea mtu aliyempigia, naye akashusha simu kutoka sikioni huku sura yake ikianza kuonyesha wasiwasi.

Francis akamsogelea na kuuliza, "Vipi kaka?"

Reuben akamwangalia usoni rafikiye, lakini akaishia tu kushusha pumzi kali kama vile mtu aliyechoka.

"Reuben?" Francis akamwita.

Reuben akafumba macho na kusema, "Nime... gari alilopanda mke wangu...."

Francis akaingiwa na utambuzi wa maana ya maneno ya rafiki yake kabla hata hajamaliza kuongea, na Reuben akamwangalia usoni huku akianza kupumua kwa hofu kiasi.

"Imekuwaje? Yaani... nini kimetokea?" Francis akauliza.

"Sijui, anasema... limepinduka... kuna... aisee!" Reuben akaongea kwa sauti ya chini, lakini hofu yake ilionekana vyema.

"Alikuwa nani huyo?" Francis akauliza.

"Askari... sijui... daktari, I don't know. Francis, nahitaji kwenda," Reuben akaongea kwa uharakishi.

"Ninakuja nawe bro. Twende," Francis akamwambia hivyo.

Kwa pamoja wakaondoka upesi sana ofisini hapo, hali ikiwa imegeuka kuwa nzito ghafla kwa njia ambayo haikutarajiwa kabisa, na Reuben akaondoka jengoni hapo pamoja na rafikiye bila kukawia ili aende kujua mke wake alikuwa kwenye hali gani huko ambako ajali hiyo ilitokea. Yaani hakutaka kuambiwa lolote lile na yeyote ambaye angetaka kumwambia kwa njia ya simu, alihitaji kwenda kuthibitisha yeye mwenyewe ukweli wa kile alichokuwa ametaarifiwa, na aliomba kwa Mungu mke wake asiwe amepatwa na maafa ambayo yangemwacha na huzuni isiyopimika moyoni mwake.


★★


Ajali iliyotokea ilihusisha magari matatu, ambalo alisafiria mke wa mwanaume huyo likigongana na lori la mizigo baada ya gari dogo kuchanganya njia na kuingiliana na magari hayo makubwa. Watu kadhaa walikufa eneo la tukio na wengine kufia hospitali, wengi wakijeruhiwa, na Lydia alikuwa miongoni mwa wale waliopoteza maisha pale pale ajali ilipotokea. Reuben alikumbwa na jambo zito mno ambalo hakuwahi kukaa kufikiria lingempata katika kipindi hiki, ama kingine kabisa. Sehemu kuu ya furaha katika maisha yake sasa ilikuwa imetoweka baada ya safari ya kumrudisha mke wake nyumbani kugeuka kuwa sababu kuu ya majonzi kwake. Hakuamini kabisa kwamba hili lilitokea, akiwa ameuona mwili wa mkewe uliohamishwa na kupelekwa mochwari, alihisi ni kama ndoto mbaya sana ilikuwa ikimpata.

Aliuacha mwili wa mkewe na kurudi kwenye gari, Francis akiwa pamoja naye, naye Reuben alikaa humo kwa saa zima akilia kwa kuuinamia usukani kana kwamba alikuwa mtoto mdogo. Alihisi uchungu mwingi kumpoteza mke wake kwa namna mbaya sana, na rafiki yake aliendelea kujitahidi kumtia moyo na kukaa kando yake katika wakati huu mgumu mno kwenye maisha yake. Huzuni ya Reuben ilizidishwa uzito hasa kila mara alipomfikiria binti yake kule nyumbani. Angemwambia vipi yule mtoto kuhusu jambo hili, na ingekuwaje kwake yeye na mtoto wake kutokea hapa bila ya Lydia kuwa nao tena? Mwanaume aliugua sana moyoni, hakujua ingekuwaje.

Francis akamsemesha Reuben baada ya mwanaume huyo kutuliza kilio chake cha chini na kumwambia wangetakiwa kuanza kufanya maandalizi ya msiba, lakini kwa yeye Reuben sasa alipaswa tu kwenda nyumbani na kuacha mipango hiyo chini ya uangalizi wa mtu ili kuweza kumuaga mke wake kwa njia iliyostahili. Akamtia moyo zaidi kwa kumwambia anaelewa namna anavyohisi, ila huu ndiyo ungetakiwa kuwa wakati wa yeye kuonyesha nguvu kama mwanaume na baba, ahakikishe anasimama kwa uimara licha ya jambo hilo kuwa baya sana; kwa ajili ya binti yake na familia yake yote kwa ujumla.

Reuben aliyasikia vyema maneno ya rafiki yake, na hakusema chochote. Bado alihisi kudhoofika sana kihisia lakini alielewa Francis alikuwa sahihi, hivyo alichofanya ikawa ni kuweka mwongozo wa ramani ndani ya gari wa njia ya kufika nyumbani kisha akajitoa kwenye siti ya usukani na kukaa siti za nyuma ndani ya gari, akiwa amemwachia rafiki yake amwendeshe kuelekea huko. Francis aliuelewa vizuri mkazo wa rafiki yake, kwa hiyo kweli akafanya alichoombwa afanye ingawa hakuambiwa kwa maneno. Alitambua sasa angehitaji kuwa na Reuben bega kwa bega kumsaidia apambane na huzuni yake. Akawasha gari na kuanzisha safari.


★★


Mwendo wa kuwarudisha jijini zaidi ulichukua karibia masaa mawili, shauri ya mvua kubwa kunyesha na misongamano ya magari kukawiza, na hatimaye Francis akafanikiwa kuifikia nyumba yake Reuben kwenye mida ya saa mbili usiku. Ilimbidi Reuben aanze kushuka ili kumdhibiti kwanza mbwa wake mkali kwa wageni, na baada ya kwenda kumfungia akarejea upande wa mbele wa nyumba na kukutana na rafiki yake hapo. Alisimama kwa ufupi akiitazama nyumba yake, manyunyu ya mvua bado yakidondoka, na Francis akamshika begani kumtia moyo kuwa waelekee ndani ili aweze kuongea na bintiye mpendwa. Wakaanza kwenda.

Hatua chache kuelekea mlango wa kuingilia ndani na Reuben akashindwa kusonga mbele baada ya msisimko wa huzuni kumwingia hata zaidi. Francis, akiwa pembeni yake, akamshika begani tena na kumtia nguvu bila maneno, na Reuben akatulia kwa sekunde chache kutuliza hisia zake vyema zaidi ili aende kushughulika na binti yake huko ndani. Lilikuwa jukumu lake pekee kwa sasa kufikisha taarifa yenye kuchoma sana kwa mtoto wake mpendwa, na hakujua ingemwachaje binti kihisia lakini ilihitajika kumwambia Larissa kilichotokea, na baada ya hapo Reuben angepaswa kuhakikisha anamlinda zaidi binti yake.

Akaendelea kusonga na rafikiye hadi kuufikia mlango, na alipoufungua tu kuingia ndani tayari aliweza kumwona mtoto akiwa ameketi sofani huko mbele, na akionekana kuchora jambo fulani kwenye karatasi. Kwa sekunde chache Reuben tena akabaki kusimama hapo hapo mlangoni akimtazama mtoto huyo, huzuni ikianza kumvaa tena kutokana na kumwangalia Larissa lakini taswira aliyoiona ikawa ni ya Lydia, mke wake marehemu.

Kutokea mbele zaidi akaanza kuja msaidizi wa kazi, na alipomwona bosi wake akatuma salamu ya upesi na kuelekea upande wake Reuben kumpokea; ingawa hata hakubeba chochote. Larissa aliponyanyua uso pia, akamwona baba yake, naye akaacha kuchora na kunyanyuka, upesi akikimbia na kumpita msaidizi ili yeye ndiyo awe wa kwanza kumpokea baba. Reuben akabaki kumtazama bintiye hadi alipomfikia na kumkumbatia kwa shauku, na hata hapo akashindwa kurudisha kumbatio hilo na kubaki ameangalia tu mbele kama kazubaa.

"Shikamoo baba?" Larissa akamwamkia huku akimtazama kwa kuegamiza kidevu chake tumboni.

Reuben akamwangalia na kusema, "Marahaba," kwa sauti ya chini sana.

"Shikamoo," msaidizi, aliyeitwa Amina, akamwamkia Francis.

"Marahaba," Francis akamwitikia.

"Uncle shikamoo?" Larissa akasema hivyo kumwelekea Francis pia.

"Marahaba mtoto mzuri. Hujambo?" Francis akamwitikia vyema.

"Sijambo. Baba umekuja na uncle na mama? Kama vile tutafanya party leo..." Larissa akaongea kwa shauku.

Reuben akamwangalia Francis, ambaye akamtikisia kichwa mara moja kama kumpa ishara.

"Nataka niwachekeshe... yaani leo shule ahahahah... nimemuuza mwalimu..." Larissa akasema hivyo na kumwachia baba yake.

Reuben akasema, "Larissa..."

"Mama bado yuko nje?" Amina akauliza, akiashiria kutaka kuwapita wanaume.

Francis akatikisia kichwa kukanusha na kumshika mkono Amina kumzuia.

"Ngoja niwaambie kwanza nyie halafu na yeye aje acheke..." Larissa akasema hivyo.

Reuben akachuchumaa kwa kupiga goti moja na kusema, "Larissa... baby, kuna... nataka nikwambie..."

"Ngoja kwanza me ndo' nikwambiee!" Larissa akasisitiza.

Reuben akabaki kumtazama kwa hisia.

"So, mwalimu aliuliza swali, sawa? Hivi... yaani, tuseme umri wa wazazi wetu. Alikuwa anataka kuonyesha kwamba mara nyingi watoto hatujui wazazi wetu wana umri gani, which is truuue... kwa hiyo akawa anafanya ku-clarify point yake mwenyewe. Kamuuliza Thomas, Anita, Loveness, wote hawajui... halafu akaja kwangu..." Larissa akaanza kusimulia.

Reuben, akiwa anakaza hisia zake, akatikisa kichwa chake kumruhusu mtoto aendelee.

Larissa akasema, "Akauliza eti 'how old is your mother?' Nikamwangaliaaa... halafu nikamwambia 'my mother is eight years old.' Mh? Wenzangu wakaanza kunishangaa, na teacher akaniuliza eti nina matatizo ya akili? Mama yangu iweje awe na miaka nane? Nikamwambia teacher sina matatizo ya akili, ila huo ndiyo ukweli. Mama yangu ana miaka nane, kwa sababu hakuwa mama wakati sijazaliwa, alianza kuitwa mama alipomzaa baby Larissa. Kwa hiyo umri wa mama yangu ni miaka nane kwa sababu ndiyo miaka yangu mimi mtoto wake..."

Francis akatabasamu kiasi kwa kutambua jinsi binti huyo alivyokuwa mwerevu. Reuben akaendelea tu kumwangalia mtoto.

"Nikamwambia 'when you want proper answers for your questions, be specific with what you're asking.' Angeuliza Lydia ana miaka mingapi, ndiyo ningesema sijui. Lakini mama yangu ana umri mwingine. Uwongo? Hapo nani utasema ni mwenye matatizo ya akili?" Larissa akaongea kwa kujinadi.

Amina akashindwa kujizuia kucheka kidogo, naye akasema, "Ila Larissa! Ungechapwa..."

"Shubutuu!" Larissa akasema hivyo.

Reuben akatazama chini tu kwa huzuni.

"Anaanzia wapi? Ndiyo wametambua leo wasicheze na mimi. Hiki kichwa ni genius. Uwongo uncle?" Larissa akasema hivyo.

Francis akalazimisha tu tabasamu na kutikisa kichwa kukubaliana naye.

"Sa' mbona hata hamcheki?" Larissa akauliza.

Reuben akamwangalia.

"Mm, nyie old school sana. Ngoja nimwambie mama, najua ata...."

Larissa alikuwa akitaka kumpita baba yake alipoanza kusema hivyo, lakini Reuben akamshika kumzuia.

"Daddy, naenda kumpokea mama, na ye' nimsimulie. Anachelewa kuingia..." Larissa akasema.

Amina sasa alikuwa ameshaanza kuhisi kwamba kuna tatizo baada ya kumwangalia Francis na kuona hakuwa na raha kabisa kama tu bosi wake.

"Lari... ona... mama hajaweza kufika..." Reuben akamwambia hivyo.

"Hamjaja naye?" Larissa akauliza.

Reuben akashindwa kutoa jibu.

"Basi limechelewa kufika baba? Au... haji leo?" Amina akauliza.

"Aah baba! Mama si alisema anakuja leoo?" Larissa akauliza kwa kuudhika.

Reuben akachomwa na hisia kali sana iliyosababisha machozi yaanze kumjaa, naye akainamisha uso wake na kufumba macho.

Larissa kuona hivyo, akauliza, "Baba... nini?"

Reuben akabaki namna hiyo hiyo.

Larissa akamshika usoni na kuunyanyua ili baba yake amtazame, naye akasema, "Basi baba, usihuzunike. Kama haji leo basi. Labda atakuja kesho. Tutamsubiri. Eti?"

Aisee!

Reuben akatikiswa moyoni hata zaidi kutokana na jinsi binti yake alivyoongea, naye akamshika mabegani na kusema, "Larissa I'm sorry. Mama... hatawhh... hataweza kuja tena nyumbani, maana...."

Akaishia hapo, Larissa akibaki kumtazama tu kwa umakini kwa sababu ya kutoelewa.

Francis akamshika Reuben begani na kusema, "Mwambie."

Reuben akajikaza na kusema, "Larissa... unakumbuka kipindi kile bibi Rose yuko hospitali... alikuwa anaumwa sana... tukaenda kumwona, kumtembelea, halafu...."

"Halafu akafariki?" Larissa akamkatisha kwa kuuliza hivyo.

Reuben akabaki kimya.

Larissa akamwangalia Francis kwa njia yenye kuchanganywa, hata mwanaume huyu hakutarajia mtoto aende moja kwa moja kwenye pointi hiyo, na binti akarudi kumtazama baba yake na kuuliza, "Baba, unataka kuniambia nini?"

Amina naye akawa ameshaelewa na kubaki amemwangalia bosi wake kwa mshangao makini, na Reuben akasema, "Mama... alikuwa amepanda gari leo, na... kwa bahati mbaya likafika sehemu fulani lika... oh God, I don't know how to do this Francis!"

Mwanaume huyo alishindwa kabisa kwenda moja kwa moja kwenye pointi, na Francis akachuchumaa pembeni yake pia na kumshika mtoto.

Francis akamwambia, "Larissa... ni kwamba mama alikuwa kwenye basi anakuja, ila likawa limeanguka. Limeanguka... na mama akawa ameumia, kwa hiyo yaani..."

"Na yeye amekuwa kama bibi Rose?" Larissa akauliza kwa sauti ya chini, machozi yakianza kumjaa machoni.

Reuben akabaki kumtazama kwa hisia za uchungu mwingi sana. Mtoto alikuwa na uelewa mpana!

Larissa akamwangalia baba yake, machozi yakianza kumtoka na pumzi zake kushtua, naye akaanza kusema, "Baba... baba..."

Sauti yake ilionyesha maumivu sana, na jambo hili likafanya Reuben aumie pia na kushindwa kuzuia machozi yake kumwagika pia.

"Baba... hh.. ba... mama... mama aa... ma..." binti akaanza kulia na kushindwa kuzungumza vizuri.

"Larissa..." Reuben akajaribu kumshika.

Kifua cha mtoto kikaanza kushtua kwa kilio chenye uchungu mwingi huku akisema, "Baba me sitaaki.. hh.. mwambie mama arudi... hh... nilikuwa nimemcho... nimemchorea welcome sign.. ile kuule... nimwhh... nim hhh... nimwoneshee..."

Francis akasema, "Larissa..."

Reuben naye akasema, "Baby, sikia..."

"Sitaki... bab.. hh.. sitaki aende kwa bibi Rose babaa... mwambie arudii... mamaa..." Larissa akaongea kwa hisia huku akinyoosha kidole mlangoni.

Iliumiza sana. Reuben akamsogelea karibu zaidi na kumkumbatia, huku mtoto akiendelea kuita "mamaaaa" kwa sauti yenye uchungu mwingi sana. Amina alikuwa pembeni akilia kwa huzuni pia, huku Francis sasa akisimama na kumwangalia rafiki yake na bintiye kwa huruma nyingi. Larissa akaendelea kulia na kulia akiwa mikononi mwa Reuben, ambaye sasa aliachwa kuwa mzazi pekee kwenye maisha yake. Reuben aliumia sana kuliko namna ambavyo hakuwahi kudhani angewahi kuumia. Huzuni ya binti yake ilikuwa kama kioo cha ile iliyokuwa ndani yake, ingawa alijitahidi kujizuia lakini moyo wake ulichoma sana, sana, sana. Akaendelea tu kumshikilia mtoto wake kwa upendo akijaribu kumpa kitulizo ndani ya kumbatio lake, huku yeye akijihisi haba moyoni kutokana na kumpoteza mwenzi wa maisha yake.






★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Screenshot_20250402-230106 (1).png
 
DOSARI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Uhalifu, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA TATU

★★★★★★★★★★★★★



Maandalizi ya msiba kumuaga rasmi Lydia yalikamilika, zikiwa zimepita siku tano toka apatwe na ajali ile iliyosababisha atoweke duniani. Kwa kawaida ungetakiwa kuwa umekwishamalizika, lakini Reuben alitaka marehemu mkewe afanyiwe msiba wa pekee kwa kutumia siku sita za maombolezo kabla mwili haujafukiwa. Kwa hiyo mwili wa Lydia ulipewa matunzo ya hali ya juu, na wazazi wa Lydia na ndugu na marafiki zake wengi walifika jijini kwa ajili ya ibada ya kuuaga mwili wa marehemu kabla haujasafirishwa kwenda kuzikiwa kule kwao. Mama yake mzazi hakuwa katika hali nzuri kimwili, na sasa kifo cha binti yake ndiyo kilimwongezea mateso zaidi hadi kushindwa kutembea vyema, hivyo alihitaji kiti cha magurudumu kusukumwa kila alipohitajika kuwa.

Kwa upande wake Reuben, ni ndugu wachache wa ukoo, washiriki wakuu wa bodi kwenye kampuni yao, wafanyakazi wao, na marafiki waliofika kumpa pole. Hakuwa na baba, yaani baba yake mzazi alikuwa ameshakufa miaka mingi nyuma, na mama yake mzazi alikuwa amefika hapo kutokea nchi za nje, huko Uingereza, akiwa pamoja na wadogo zake Reuben wawili wanawake. Reuben alikuwa ndiyo mzaliwa wa kwanza. Kufikia hiyo siku ya tano kwa wengi wa ndugu za karibu, ule uchungu mwingi wa mwanzoni ulikuwa ukififia na wao kurudisha uimara zaidi kihisia, lakini kwa wazazi wa Lydia, Reuben, na binti yake, bado lilikuwa ni pigo zito sana. Hasa Larissa.

Misa ilifanywa kanisani kwa ibada ya pekee, watu wakivalia nguo nyeusi na kupeleka pole zao kwa wafiwa, huku mwili wa Lydia ukiwa ndani ya jeneza maridadi na kuonyesha uso wake usioweza kufumbua macho tena kamwe. Reuben alijitahidi kuwa imara, akisalimiana na watu waliompa pole, lakini binti Larissa hakuwepo kabisa hapo kwa nafsi. Alikuwepo kimwili tu, kwa kuwa watu wangejaribu kumsemesha na kumpa pole, hata wale ambao alikuwa amewazoea sana, lakini binti hakutamka neno hata moja kwa siku hizo zote toka alipofikishiwa taarifa ya kifo cha mama yake. Alikaa kwa utulivu tu, akiangalia chini, akimfuata baba yake ama mama wadogo zake walipomwongoza huku na kule, lakini kani yake ya utendaji iligeuka kuwa kama ya sanamu.

Reuben aliumia sana kumwona mwanaye hivyo. Stanslaus Mwita, rafiki yake ambaye alichomewa duka lake la bidhaa, alikuwepo pia na familia yake kumuunga mkono. Francis na dada yake, Josephina, walikuwepo pia. Francis na Stanslaus walijitahidi kuwajibika na mengi ya mambo ambayo kwa kawaida Reuben ndiye angeshughulikia, ili kumpa mkono kwa ukaribu kuhakikisha anakazia fikira zaidi hali njema ya binti yake ambaye killa mtu aliona ni namna gani alitikiswa vibaya na kifo cha mama yake.

Kwa hiyo baada ya misa kuisha, jeneza likaondolewa kanisani na kuingizwa kwenye gari tayari kwenda kuhifadhiwa kwanza kabla ya kumsafirisha marehemu hadi mahali alikozaliwa ili azikwe. Ndiyo angezikwa hiyo siku ya sita. Watu walikuwa wengi, na wakati wakiliangalia jeneza linaingizwa kwenye gari, Josephina akasogea hadi karibu na aliposimama Reuben na Larissa, akiwa pamoja na mtoto wake, yule Hans. Tokea msiba uanze, Josephina alikuwa amempa tu pole fupi Reuben akiwa na kaka yake, ila sasa alitaka kumwonyesha kwamba alikuwa karibu naye zaidi kwa kipindi hiki ingawa hawakujuana vyema. Alivalia gauni refu lenye kubana kiasi, mwonekano wake mzuri wenye kuvutia ukiwa wazi kwa wengi, hivyo kumkaribia Reuben kulifanya watazamwe zaidi.

Akiwa karibu naye hivyo, Josephina akamshika usoni Larissa kwa njia ya kuonyesha huruma na kuzilaza-laza nywele zake pia, halafu akamwangalia baba yake na kusema, "Reuben..."

Reuben akamwangalia na kusema, "Phina."

"Aa... nilitaka tu kukupa pole kwa mara nyingine tena. Mambo yamekuwa mengi, hatujaongea sana," Josephina akamwambia hivyo.

Baadhi ya watu wakawa wakiwatazama wawili hao walipoanza maongezi hayo na kuwaelekezea fikira zaidi.

Reuben akamwambia Josephina, "Asante dada. Wala usijali, nashukuru sana kwa support yenu."

Mwanaume akarudi kutazama tu jeneza, naye Josephina akasema, "Unajua... sisi kwetu huwa tunaamini kwamba kifo siyo mwisho."

Reuben akamwangalia.

"Mwenzetu anapoenda kwanza, haimaanishi katutoka kabisa. Anaendelea kuwa pamoja nasi, kutulinda... na najua mkeo ataendelea kuwa pamoja nawe na mwanao popote pale mtakapokuwa," Josephina akasema hivyo kwa kufariji.

Reuben akamwangalia na kutikisa kichwa kama kuonyesha shukrani, naye akasema, "Asante. Mna imani nzuri."

Josephina akamwonyesha tabasamu dogo.

Reuben akaangalia mbele na kusema, "Sijui sana kama hiyo ni kweli, ila... sijawahi kutarajia mke wangu aende mbali nasi ili ndiyo atuangalie. Ingekuwa ni ndani ya uwezo wangu, ningemrudisha hata sasa."

Josephina akamwangalia kwa njia ya huruma.

Reuben akashusha pumzi na kusema, "Lakini hamna namna. Najua hii huwapata wengi. Sikufikiri tu ingewahi kutupata sisi. Bado inauma sana maana... kihalisi hapo naenda kuzika watu wawili."

Josephina akamwambia, "Pole sana Reuben."

Reuben akatikisa kichwa kukubali pole hiyo.

Josephina akakishika kiganja kingine cha mwanaume huyu na kukikaza, naye akamkumbatia hapo hapo na kisha kusema, "Tutakuwa pamoja katika kila hali kuanzia sasa. Ukihitaji chochote, niko hapa kwa ajili yako... na Larissa pia."

Alisema hivyo na kumtazama binti Larissa, ambaye alikuwa ametulia tu akitazama huko mbele.

Reuben akasema, "Asante. Nashukuru sana."

Reuben akaendelea kutazama mbele, na Josephina akiwa ameendelea kumkumbatia tu, akawa akitembeza kiganja chake mgongoni kwa mwanaume huyu kwa namna ya kumbembeleza, akimwangalia kwa hisia zaidi, ndipo Francis akawa amefika hapo na kusimama karibu yao pia.

"Kaka..." Francis akamwita Reuben.

Josephina akamwachia Reuben na kiganja chake, naye akasimama kwa utulivu na mwanaye pembeni.

Reuben akamtazama Francis, na mwanaume huyu akasema, "Kuna mambo hapo kasisi anataka tu-asses... kabla hatujaondoka. Tunaweza ku..."

Reuben akatikisa kichwa kukubali akiwa ameshaelewa, naye akamwangalia Larissa na kusema, "Baby, njoo huku kwa mamdogo, nikaongee na padri mara moja..."

Akiwa anataka kumvuta binti yake, Josephina akasema, "Oh, haina shida Reuben... nitakaa na Larissa mpaka mrudi. Njoo mama..."

Mwanamke huyo akamsemesha Larissa namna hiyo na kumshika mkono, naye akamvuta pembeni pamoja na Hans huku Reuben akimtazama binti yake kwa hisia makini.

Francis akamuuliza, "Ameshaongea?"

Reuben akatikisa kichwa kukataa, kisha akampita tu Francis kuelekea upande aliokuwepo huyo kasisi.

Francis akamtazama Josephina na watoto pale waliposogea kuchanganyikana na ndugu zake wengine Reuben, akiona mwanamke huyo alipojaribu kumsemesha Larissa kwa upendo, na mwanamke huyo akamwangalia pia. Kwa sekunde chache wawili hawa walipoangaliana, Francis alimpa utizami wenye maana fulani ambayo Josephina aliweza kuielewa, na mwanamke huyo akaacha kumwangalia akionekana kutoipenda maana hiyo na kuendelea kushughulika na watoto. Francis akaachana naye pia na kuelekea alikokuwa Reuben.


★★★


Tunakuja kwake Paulina. Zikiwa zimepita siku tano sasa baada ya mwanamke huyu kijana kuwa amekwenda kwa shangazi yake kuomba msaada wa pesa za matibabu ya mama yake, Roza alimpatia wazo la kazi ambayo angeweza kufanya na upesi imwingizie pesa nyingi kumsaidia afanikishe tarajio lake la kumwokoa mzazi wake mpendwa. Kulikuwa na watu kwenye jiji la mbali, ambao Roza alifahamiana nao, waliofanya biashara za kuuza wanawake kwa wanaume wenye pesa kwa ajili ya starehe zao, na walilipa pesa nyingi.

Shangazi akamweleza mpwa wake kuwa biashara hizo zilikuwa za hali ya juu, tofauti kabisa na zile za wanawake waliojiuza kwenye madangulo ya ovyo ovyo. Hapa alikuwa akiongelea kumuunganisha kwa wanaume matajiri ndani ya sehemu za gharama, na watu waliofanikisha mambo hayo walifanya kazi hizo kwa umakini na mpangilio mzuri. Hivyo, wanawake waliochukuliwa kwa ajili ya kupelekwa huko walitakiwa kuwa wazuri haswa. Sura, umbo, vivutio vyote mwilini mwa mwanamke kwa macho ya wanaume vikiwa safi kabisa, na wajue jinsi ya kuwapa wanaume hao burudani ya aina yoyote waliyohitaji. Malipo yalikuwa manono.

Kwake Roza ilikuwa ni kazi rahisi sana, ila kwa Paulina lilikuwa ni jambo zito mno. Hakujua kama angeweza kufanya mambo ambayo shangazi yake alitarajia angeyafanya, lakini kwa sababu ya kuwa chini ya shida aliamua kukubaliana na wazo hilo. Aliahidiwa kuweza kupata hadi milioni kwa mteja mmoja tu, sasa afikirie angepata kiasi gani kwa wateja watano na zaidi! Mwanamke huyu kijana alikuwa na sura na umbo zuri kwelikweli, Roza akitumia siku hizo chache kumtengeneza vyema zaidi kwa kumpamba na kumwandaa kwa jinsi alivyotakiwa kutenda akishafika huko jijini kuanza kazi hizo. Alimwambia kwamba gharama anayotumia kumpendezesha ingetakiwa kurudi, yaani akishafanya kazi na kupata pesa angetakiwa kumlipa Roza pia, hivyo bidii ya kupata wateja wa maana ilihitajika.

Kizungumkuti kingekuja juu ya nani angekuwa karibu na mama yake kumwangalia, maana kwa sasa hakuwa na mtu wa kumwacha huko hospitalni. Roza akamwambia hilo halingekuwa na shida kabisa, kwamba yeye ndiye angesimamia taratibu zote za utunzaji wa mama yake kama ambavyo kwa siku hizi chache alikuwa ameanza kufanya, kwa hiyo akili yote ya Paulina ilipaswa kuwa kwenye kazi iliyomhitaji huko mbali ili afanikishe kutuma pesa ya vyote vilivyohitajika upesi kumtibu mama yake. Roza alitia nguvu kubwa sana kumshawishi mwanamke huyu kijana, na Paulina akawa tayari kuondoka baada ya kumwona mama yake kwa ufupi hospitalni huko. Kwa uharaka uliomhitaji kuondoka mjini kwao, hakupata hata nafasi ya kuongea wala kumuaga rafiki yake wa karibu, yule Halima, na siku ya safari ikawadia.

Paulina akapandishwa basi alfajiri ya mapema sana kutokea mjini kwao, gharama zikiwa za Roza, na shangazi yake huyo alimwambia kwamba atakapofika huko jijini kutakuwa na mtu wa kumpokea. Ni kwamba katika maandalizi ya kumpeleka huko, Roza alikuwa amempiga Paulina picha mapema na kuzituma kwa "afisa mauzo" wa hiyo biashara, ambaye alihakiki kama kweli Paulina alikuwa na vigezo vilivyotosha kumwekezea, na hilo likiwa limetiki, sasa angefika tu huko na kutambuliwa bila tatizo lolote. Kwa hiyo ingekuwa ni kushuka kwenye kituo cha basi huko jijini, na Paulina angechukuliwa na mtu ambaye Roza alimwambia kwamba anaitwa Isaya. Alimwelekeza jinsi anavyofanana na kumwambia atii kila mwongozo ambao jamaa angempa, na ajitahidi kuacha kujionyesha kama mgeni sana wa kila kitu.

Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kabisa kwa Paulina kusafiri kuelekea nje ya mkoa wao, na hakujua huko jijini pangempokeaje lakini alielewa kuzoea maisha mapya isingekuwa jambo rahisi. Hasa maisha aliyokuwa anaenda kuyaishi. Hata katikati ya safari hii, Paulina alijiona kuwa kama tamasha kwa macho ya wanaume fulani kwa jinsi alivyoangaliwa, hiyo ikitokana na namna ambavyo Roza alimpamba usoni na mwilini, kwa mavazi yenye kubana umbo lake na nywele ndefu za kusukwa zilizompendezesha kwelikweli.

Lakini alijitahidi kubaki mtulivu tu, akijali yake na kuwa makini kutozungumza mengi mno na yeyote aliyemsemesha ndani ya basi hilo. Ndiyo, alisemeshwa na abiria wenzake, wanawake waliomsifia kwa kupendeza na kutaka kujenga urafiki pia. Lakini alijitahidi kuepuka kabisa kujuana na mtu yeyote kwa undani na kuwa msikilizaji tu zaidi, mpaka wamelifikia jiji hatimaye ikiwa imekwishaingia usiku.

Paulina alivutiwa na vitu vingi vilivyoonekana kuwa maridadi sana ndani ya jiji hilo. Vitu na watu wengi walijongea kwa kasi, yaani harakati hapa au pale zilikwenda na muda, kila mtu akionekana kuwa makini na mambo yake. Yeye pia, akikumbuka vizuri lengo lake kuja huku ni ili kuchuma pesa haraka kwa matibabu ya mama yake, angehitaji kuwa makini kwelikweli, kwa hiyo akaweka ugeni pembeni na kujitia mwonekano wa mwanamke aliyeonekana kuwa. Stendi aliyoshukia ilikuwa na mambo mengi, alipokanyaga tu chini tayari akaanza kufatwa na watu, huyu akimwambia twende huku, huyu kule, lakini akajitahidi kuwaepuka na kusogea sehemu ambayo hakuandamwa sana. Alitakiwa kumwona huyo Isaya na kuondoka naye, lakini hakuweza kutambua upesi jamaa angekuwa wapi.

Ndipo, kutokea nyuma yake akawa ameshikwa begani, naye alipogeuka akakutana na mwanaume mrefu mwenye mwili mkubwa kimazoezi, akijaa ndevu nyingi mashavuni na mwenye sura iliyo makini sana. Alivalia kwa namna yenye kuvuta fikira kiasi, T-shirt nyeusi iliyomchora kifua, cheni nene shingoni, saa ya gharama mkononi, jeans nyeusi, buti za khaki, na alimshika Paulina begani kwa namna fulani ya kutaka kumtolea mkoba wake mdogo aliobeba, na mwanamke huyo akaukaza zaidi mkononi huku akimwangalia kwa kujihami.

Mwanaume huyo akamwambia, "Tulia mpenzi. Nakujua."

Paulina akabaki kumwangalia kwa umakini.

"Unanijua mimi?" mwanaume huyo akamuuliza.

Paulina akasema, "Isaya?"

"Mm," jamaa akakubali.

Paulina akalegeza mkoba wake.

"Twend'zetu," Isaya akamwambia hivyo.

Mwanaume huyo alionekana kwenda na wakati, na akiwa anataka kujenga picha fulani hivi, akamshika Paulina kwa kumwekea mkono begani kwake na kuanza kutembea naye kwa njia fulani kama namna ambavyo wapendanao hufanya. Paulina hakujihisi amani kabisa kushikwa namna hiyo, alihisi ni kama anavutwa kwa lazima yaani, lakini hakuwa na jinsi ila kukubali tu kwenda naye. Wakaelekea upande wa nje kutoka hapo kwenye stendi, na moja kwa moja wakalifuata gari lenye muundo kama hiace, jeusi, na walipolifikia, Isaya akauvuta mlango wa nyuma na kumwonyesha Paulina ishara kuwa aingie.

Mwanamke huyu akaingia taratibu ndani humo, na kukiwa kumewashwa taa, sasa akaweza kuona kwamba kulikuwa na wanawake wengine hapo. Wanawake kama sita hivi, wazuri, wakivaa kwa namna zenye kuonyesha kwamba walikuwa ndani ya ligi moja na yeye iliyomleta huku kwa ajili ya mechi zilizohitaji kuchezwa, naye akapita mpaka kwenye nafasi yenye uwazi kukaa, akaketi taratibu. Tayari Isaya alikuwa amekwishafunga mlango na kuelekea upande wa siti ya dereva, na baada ya kukaa akaonekana akiwa ameweka simu yake sikioni kuzungumza na mtu fulani.

Paulina aliwaangalia wanawake wenzake vijana kwa njia fulani ya kukagua, akiwa anajiuliza kwa upande wao ingekuwa ni nini kilichowafanya wajikute ndani ya kazi hii yenye utata, lakini mienendo yao ilionyesha ni kama hawakujali sana. Baadhi yao hata walizungumza kirafiki na kucheka kwa njia yenye kuonyesha wamestareheka kabisa, na yeye aliposemeshwa na mmojawao, hakuwa hata na ujasiri wa kutoa jibu na kubaki ametulia kama vile hayupo. Hapo sasa alikuwa katikati ya fungu moja la wanawake waliojiuza, na hakuwa na namna nyingine ya kukana kwamba yeye hakuwa mmoja wao. Alihisi huzuni sana. Isaya akamaliza kuongea na simu huku akiwa ameanza kugeuza gari, naye akawaondoa kutoka maeneo hayo.


★★★


Kwake Reuben. Mwanaume huyu sasa alikuwa mwendoni kwenye safari iliyowapeleka waombolezaji wa kifo cha mkewe huko nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi, ukiwa kama msafara kutokana na magari kadhaa kufuatana na lile lililoubeba mwili wa Lydia. Wazazi wa marehemu walikuwepo, ndugu zao, na wasindikizaji kadhaa pia, kutia ndani familia yake Reuben. Alikuwa ndani ya gari jeusi la hiace aina ya Alphard, yeye, mama yake, dada zake wawili, pamoja na Larissa, wakiendeshwa na dereva wa kuajiri. Isingewachukua muda mrefu sana kufika maeneo ya kwao na Lydia kwa sababu tayari walikuwa wameshaingia mkoani humo.

Ndani ya gari lao kulitawaliwa na hali ya ukimya hasa kutokana na dada zake kutulia tu na kufanya mambo yao kwa simu zao, huku Larissa akiwa amesinzia na kujilaza kwenye miguu ya baba yake sitini walipokaa. Reuben alitulia pia, akitelezesha kiganja chake kwenye nywele za bintiye kama kumbembeleza taratibu, na mama yake aliketi pembeni kwenye siti ambayo ilikuwa ya pekee, akimtazama mwana wake kwa kujali sana.

"Reuben..." hatimaye mama yake akamwita.

Reuben akamtazama.

"Yule rafiki yako hakuja. Ni kwa nini?" akamuuliza.

Reuben akauliza, "Yupi?"

"Yule aliyekuwa aki-handle...."

"Ooh, Francis?" Reuben akaelewa.

"Yeah," mama yake akakubali.

"Angekuja, ila... kuna mambo alitakiwa kushughulika nayo... ya kikazi," Reuben akamwambia.

"Huyo ni rafiki yako kweli? Hakusindikizi kumzika mkeo, anabaki kufanya kazi?" mdogo wake wa kwanza, aliyeitwa Sorange, akamuuliza hivyo kutokea hapo nyuma.

"Haina shida. Ni vitu vilivyopangwa, hangeweza ku-change," Reuben akasema.

"Na yule dada yake, aliyekukumbatia... nani sijui... na yeye hajaja pia," akasema hivyo Sorange.

Reuben akabaki tu kimya.

"Nilifikiri hao ndiyo mko close zaidi," Sorange akasema.

"Siyo sana. Kawaida tu," Reuben akasema hivyo.

"Wana maisha yao na mipango mingi, huwezi kuwalazimisha wawe huku. Lakini kati ya wote, nimependa walivyojitoa kukupa support. Hasa Francis. Anaonekana rafiki mzuri sana," mama yake akaongea hivyo.

Reuben akatikisa kichwa kukubali tu na kuendelea kumwangalia binti yake.

"Hautamwamsha ale?" mama yake akaongea hivyo.

Reuben akamgeukia na kumtazama kwa namna iliyoonyesha subira.

"Inaenda kuingia saa nne sasa, Reuben. Mwamshe mtoto ale," mama yake akamwambia.

Reuben akamtazama Larissa kwa ufupi, naye akasema, "Ni vyema akiamka yeye mwenyewe. Mwache tu alale."

Mama yake akawaangalia mabinti zake wawili waliokaa siti za nyuma na kaka yao, Sorange akipandisha mabega kama kumwambia mama yake hajui la kufanya, na mama huyu akamwangalia Reuben tena na kusema, "Umeshafikiria kuhusu nilichokushauri, I suppose."

Reuben akabaki kimya tu.

"Reuben, talk to me. Hii ni serious," mama yake akamwambia.

"Haiwezi kungoja mpaka tukirudi nyumbani?" Reuben akauliza.

"It can't. Niambie sasa hivi," mama yake akasema.

Reuben akaishia tu kushusha pumzi.

"Okay, najua una huzuni... sisi wote tumehuzunika, lakini ni vema uanze kufikiri kuhusu hali ya huyu mtoto haraka. Reuben... naomba ukubali kile nilichokushauri," mama yake akamwambia kwa upole.

Reuben akamwangalia kwa ufupi, kisha akasema, "Lydia ameniacha mama. Kwa nini unataka na mwanangu aniache?"

"Haiko hivyo. This isn't about you, Reuben. Hii ni kuhusu Larissa. Umeona jinsi haya yote yalivyom-affect, mpaka sasa hivi haongei, naona ni vema tufanye hivyo ili kwanza...."

Reuben akamkatisha kwa kusema, "Nitajua namna ya kumsaidia mwanangu mama. Unachotaka nifanye... kipo out of question. Siwezi."

"Reuben..." mama yake akaishia tu kutaja jina lake.

Mdogo wake wa pili, aliyeitwa Cynthia, akamshika Reuben begani kutokea nyuma na kusema, "Haitakuwa rahisi kama unavyofikiri kaka. Larissa ni mtoto wa kike. Siyo kwamba mama anasema hauwezi, ila... kwa sasa hivi, angalau kwa sasa hivi, tunaona litakuwa jambo lenye faida kwa Larissa aki... akikaa mbali na haya yote kwa muda fulani..."

Reuben akawa anatikisa kichwa kukataa.

"Kaka... suala la Larissa linahusiana na impact ya mazingira haya magumu, ninaenda kuwa psychologist, trust me... najua. Mazingira haya yanaweza ku-force hali yake iwe mbaya zaidi kuliko unavyodhani, ni suala la mazingira tu kaka. Larissa atahitaji kubadili mazingira kwanza, na atahitaji upendo wa mwanamke ili arudie hali yake ya kawaida tena. Just think about it," Cynthia akajaribu kumshawishi.

Reuben alikuwa kwenye wakati mgumu sana kihisia, na ndugu zake hawa walimfanya ahisi ni kama wanauongezea makali tu. Ilikuja kwa namna asiyotarajia mama yake alipomshauri kwamba ingefaa Larissa akiondoka nao, yaani, wanawake hao watakaporudi Ulaya, Larissa aende pamoja nao. Haikuwa kwa nia ya kumwondoa mtoto kwa baba yake, ilikuwa ni ili kumsaidia hasa Larissa kurudia hali nzuri tena, kwa sababu kama Cynthia msomi alivyomwambia, mazingira ya huku yenye kuumiza ndiyo yalifanya binti ashindwe kuwa sawa kisaikolojia, hivyo waliona kumbadilishia upesi mazingira hayo ndiyo jambo ambalo lingemfaa.

Lakini bado Reuben hakuwa tayari kuafikiana na mawazo yao. Kumwacha Lydia aende lilikuwa jambo gumu sana kwake, walitegemea vipi kwamba angewaruhusu wamchukue na binti yake ndani ya hiki hiki kipindi? Hakutaka kabisa kukubali. Kama ni kumsaidia, angemsaidia bintiye kwa namna nyingine yoyote, lakini siyo kumwondoa kutoka karibu yake. Sasa kuliko wakati mwingine wowote ndiyo alimhitaji zaidi Larissa kando yake, hivyo kwa matarajio ambayo mama yake alikuwa nayo ya yeye kumsikiliza, angekuwa radhi kumvunja tu moyo.

Akabaki kimya tu baada ya vishawishi vyao kuishia hapo, mama yake pamoja na dada zake wakiona kweli hilo lilikuwa limegonga mwamba, hivyo wakamwacha tu na kutulia zaidi ili safari hiyo iwafikishe kule mwili wa marehemu ulipohitajika kuwa.


★★★


Akiwa ndani ya gari lililompeleka mahala ambako angeenda kuanza "kazi," Paulina alikaa kwa utulivu tu huku bado hali nzima iliyomzunguka ikiwa yenye kumtatiza sana. Wanawake wenzake wangeongeleshana kuhusu vitu ambavyo hata hakuvijua, na baadhi yao walimwangalia kwa namna yenye dharau sana kutokana na yeye kujiweka kivyake zaidi. Angalau ni wawili hivi waliokuwa watulivu kama yeye, wakijali biashara zao tu, lakini waliobaki ndiyo mapepe yaliwajaa hadi Paulina akaona hao walikuwa wamebobea sana kwenye mambo haya.

Lakini kwake hilo halikuwa lenye umuhimu sana. Alikuwa akiwaza zaidi kuhusu hali ya mama yake huko alipomwacha. Hakuwa na simu, na akiwaza labda huyo Isaya angekuwa ameshawasiliana na Roza kumjulisha kuwa amefika, akafikiria angeweza kumwomba aongee naye pia ili kujua hali ya huko. Isaya huyo aliendesha tu gari kwa umakini bila kujishughulisha na wanawake hawa mpaka walipofikia eneo lililokuwa na jengo pana lenye ghorofa tatu. Ilikuwa imeshaingia mida ya saa tano sasa, na Paulina alihisi njaa.

Walipofika hapo na kuanza kushuka, mwanamke huyu akamsogelea Isaya upesi na kujaribu kumsemesha kuhusu simu, lakini mwanaume huyo akampuuza kwa kumsogeza pembeni, akiufunga tu mlango wa gari, kisha akawaambia wanawake hao wamfuate. Paulina hakuwa na namna, na yeye ndiyo akiwa mwishoni kwenye mstari huo akafuata njia pia kulielekea jengo hilo. Isaya hakuwa ameegesha gari mbele ya jengo, bali alilituliza upande wa nyuma ambao haukuwa na mijongeo mingi ya watu kama kwa kule mbele. Aliwaingiza hapo kwa njia fulani ya kificho, wakipita makopo ya takataka na kuufikia mlango mwembamba kwa nyuma, kukiwa na hali ya ugiza.

Kwenye mlango huo, Isaya akagonga mara tatu, na kwa ndani ukagongwa mara mbili, kisha yeye akaugonga mara moja tena. Hiyo ikiwa ni njia ya kujitambulisha, mlango ukafunguliwa kwa ndani, na Isaya akawapisha wanawake ili wamtangulie kuingia. Wale ambao walijiamini walipita kwa madoido yao na kunesa, na Paulina akatembea pia huku bado akiwa mwenye wasiwasi. Aliyefungua mlango alikuwa mwanaume mwingine mwenye mwili mkubwa, kisha Isaya akapita pia na kugongeana naye ngumi kirafiki, halafu akaendeleza mwendo pamoja na wanawake hao mpaka walipozifikia ngazi upande huu wa nyuma na kuanza kuzipanda.

Hapakuwa na hali nzuri kabisa, yaani palitoa harufu yenye kukera pua na kutapakaa kwa vitu vingi vichafu sakafuni, hasa chupa za bia na kondomu, na kundi hili likafika ghorofa la tatu huko na kuingia kupitia mlango mwingine. Wakiwa upande huu sasa, ikawa wazi kwa Paulina kwamba palikuwa jikoni, papana, na hakukuwa na watu wala nini isipokuwa vyombo na harufu kali za nyama iliyovunda. Wakapavuka na kuupita mlango tena wa kutokea humo, na sasa wakawa kwenye korido moja lililoonekana kuwa maridadi zaidi.

Sauti za muziki uliodunda, watu wakipiga kelele za kufurahi, zilisikika zaidi kutokea maghorofa ya huko chini. Huku palikuwa na hali fulani tulivu zaidi, na Isaya akawaongoza wanawake kupita milango ya vyumba na kumbi chache kwa upande huo hadi walipofikia mlango mpana kuelekea mwanzoni mwa mwingilio wa ghorofa hilo. Walikuwa wakiwapita wanaume na wanawake waliojistarehesha, Paulina akiona mambo mapotovu yaliyofanywa humo ambayo hakuwahi kujionea kabla, lakini akaendelea kujikaza tu. Alipaswa kuzoea, apende asipende.

Isaya akagonga hodi, lakini hakujibiwa, hivyo akafungua mlango na kuchungulia, kisha akatoka tena. Akatoa simu yake na kumpigia mtu fulani, wanawake aliowaleta wakiwa wanamwangalia kwa subira, naye akaongea kifupi na huyo mtu kumwambia kwamba mzigo ndiyo alikuwa ameuingiza, na alikuwa "ofisini" kwake huyo mtu, akimngojea aje kuuona. Ikaonekana amepewa maelekezo fulani, kisha akakata simu na kuwaambia wanawake waingie ndani ya chumba hicho pamoja naye.

Mmoja baada ya mwingine, wakaanza kuingia huku Isaya akisimama mlangoni, na alikuwa akiyapiga makofi makalio makubwa ya wanawake wachache walioingia kwa kuyatikisa haswa, wakitabasamu baada ya kufanyiwa hivyo na kumwangalia jamaa kwa uvutio. Lakini alipoingia Paulina na Isaya kutaka kumpiga kalioni, mwanamke huyu akajigeuza na kukinga mikono yake kama kumkwepa, na Isaya akamtazama kimaswali.

"Ish, we' vipi?" Isaya akamuuliza.

Paulina akajisogeza tu pembeni na kumwepuka, halafu akawahi kuingia na kwenda kusimama pamoja na wenzake.

Isaya akacheka kidogo kwa pumzi na kusema, "Usiniambie Roza ametuletea mshamba."

Kauli yake ikawafanya wanawake wengine wajichekeleshe na kumwangalia Paulina kwa kuhukumu, na mwanamke huyu akaendelea kujituliza tu kwa kutazama chini.

Isaya akafunga mlango na kusema, "Hii ndo' ofisi ya bosi. Bosi wangu, bosi wenu. Mtulie, anakuja. Huwa hapendi mambo ya kijinga, kwa hiyo nikisema mtulie, mtulie kweli. Atawapanga vizuri."

Wanawake wachache walikuwa wakimwangalia Isaya kimatamanio tayari na kuonyesha hilo waziwazi kwa matendo yao ya kimwili, lakini jamaa akawa akimwangalia Paulina zaidi.

"Wewe..." Isaya akasema.

Paulina akamwangalia.

"Umesikia nilichokwambia?" Isaya akamuuliza kwa sauti makini.

Paulina akaingiwa na wasiwasi, na akiwa anataka kutoa jibu upesi, hapo hapo mlango ukafunguliwa na kufanya wote watazame huko. Akaingia mtu aliyevuta umakini wao wote, na Isaya akatabasamu kiasi baada ya kumwona na kumnyooshea kitu kama kadi ndogo ili kumpatia.

Akakipokea, akiwa anawaangalia wanawake wengine kwa njia ya kutojali yaani, naye akamtazama Isaya na kuuliza, "Ndiyo hawa?"

"Ndiyo, madam," Isaya akajibu.

"Walitakiwa kuwa kumi, mbona wako saba?"

"Wengine watafika kesho, kulikuwa...."

"Ah, umeanza visingizio Isaya! Unajua hatuna muda wa kupoteza!" mwanamke huyu akamfokea kiasi.

Isaya akaangalia chini na kusema, "Sorry, madam. Haitatokea tena, kesho tu wanaletwa, na tutaongeza wengine."

Madam huyu, akawaangalia wanawake hao na kusogea upande wao, akiwa kama anawakagua kwa macho.

Mmoja wa wanawake hao akatoa ishara ya goti na kusema, "Shikamoo?"

Madam akasonya na kusema, "Shikamoo mwenyewe! Unaniamkia, me bibi yako?"

Mwanamke huyo akabaki kumtazama "madam" kiwasiwasi, na wengine wakaendelea kutulia. Paulina pia alimwanglia kwa hisia makini, akiona namna alivyovalia kwa njia nzuri sana lakini iliyoonyesha kwa kadiri kubwa viungo vyake vya kuvutia macho ya wanaume, na alinukia ile harufu iliyoeleweka kuwa ya kibosi kwelikweli.

"Mnajua me ni nani?" mwanamke huyo akawauliza.

Wanawake wachache wakasema, "Boss."

"Ahahahah... aaa... eti boss!" madam akasema.

Isaya akatikisa kichwa huku akitabasamu.

Mwanamke huyu akawa makini zaidi, naye akasema, "Hapa hakuna cha bosi. Mshanielewa? Niiteni madam. Nani?"

"Madam..." wakajibu, isipokuwa Paulina.

"Yeah. Atakayewalisha na kuwavisha kuanzia sasa itakuwa ni mimi, kwa hiyo eleweni hii kwenu ni sauti ya Mungu, na inawataka mfanye kila kitu inachowataka mfanye. Mshanielewa?"

Wakatikisa vichwa.

Madam akasema, "Nikiongea kwa sauti...."

"Yes madam!" wanawake wakajibu upesi.

Mwanamke huyu akaangalia chini kwa ufupi, kisha akasema, "Hmm... naona kama vile kuniita 'madam' haitatosha. Niwaongezee na ring nyingine kidogo, eti?"

Isaya akamwambia, "Yeah. Wajue ni sauti ya Mungu gani inayowasemesha."

Mwanamke huyo akatabasamu kijeuri kiasi, Paulina akiona namna ambavyo alipenda sifa, naye ndiyo akasema, "Niiteni madam Phina."

Wanawake wachache wakasema, "Madam Phina..."

Mwanamke huyu akatabasamu kwa kupenda kusikia akiitwa hivyo. Ndiyo. Ikiwa ni Josephina mwenyewe dada yake na Francis rafiki ya Reuben, mwanamke huyu ndiye aliyekuwa kwenye kiti cha utawala huu wa biashara ya wanawake, nyumba hiyo ya starehe ikiwa ni yake, na akiongoza mambo yote ambayo Paulina angejikuta akiwa chini yake. Rangi zake za kweli zilifichika kwa watu wengi ambao hawakujua aina ya maisha aliyokuwa nayo kihalisi, na kutokea hapa ndiyo ingeeleweka yeye alikuwa nani, na alitaka nini kwa kujiingiza ndani ya maisha yake Reuben.

Huyo ndiyo alikuwa Josephina!






★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Screenshot_20250402-230106 (1).png
 
DOSARI

A Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Uhalifu, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA NNE

★★★★★★★★★★★★★




Ikiwa ni kwenye mida hiyo hiyo ya saa tano usiku ndani ya kumbi moja kubwa ya starehe jijini, mwanaume fulani mtu mzima anaingia hapo akiwa anatembea taratibu na kwa kujiamini kuelekea ngazi zinazopanda hadi ghorofa ya kwanza ya jengo. Kuna umati wa watu wenye kujifurahisha, muziki mnene, pombe, wanawake wazuri wenye kuvaa kwa njia ya kujiachia kuvutia wanaume, na taa zinazobadilika rangi kwa mizunguko zinafanya kuwe na mwonekano bomba sana. Siyo sehemu wanayoingia watoto, na mwanaume huyo akiwa tu ndiyo amezifikia ngazi tayari ameshaanza kushikwa-shikwa na wanawake baadhi wanaouza miili yao, kujaribu kumvutia kwao, lakini anawapuuzia na kuendeleza hatua zake.

Anapanda ngazi hizo kwa mzunguko hadi kufikia juu, ambapo napo pana mwonekano wa aina ile ile isipokuwa tu viti na meza; hapo juu ni masofa zaidi ndiyo yamezunguka meza fupi za kioo. Kwa hakika ndiyo sehemu ambayo wanakaa wale waonwao kuwa na pesa nyingi, hata gharama za vinywaji na wanawake hapo ni ghali, hivyo hakuna mtu anayesogea kizembe. Kuna baunsa maalumu anayelinda mwingilio, na baada ya mwanaume huyu kumfikia, anaunganisha naye kiganja kwa njia ya kirafiki tu, kisha baunsa anamwachia njia asonge mbele zaidi.

Kuzungukia sehemu yote ya ghorofa hiyo walikaa wanaume wenye kuponda raha na wanawake walioenda shule, yaani wazuri, viuno na makalio vikitikiswa kwa waliosimamia wanaume zao, pombe za maana zikiwekwa hapo, na mwanaume huyu aliyefika sasa alikuwa akiwapita tu na kuelekea kwenye kona mwishoni zaidi ambapo mwanaume mwingine aliketi sofani kwa utulivu. Huyo aliyekaa alikuwa mtu mzima pia, akivalia koti gumu jeusi na kofia iliyopindia upande mmoja wa kichwa chake, akinywa kileo kikali kutoka kwenye glasi, huku chupa ya kileo hicho ikiwa mezani.

Mwanaume huyu aliyefika hapo akasimama kwanza, na huyo aliyekaa akamwangalia na kusema, "Vipi?"

"Safi boss. Nakuona," aliyesimama akamwambia hivyo huku akitabasamu kiasi.

Huyo "boss," akaangalia saa yake mkononi na kusema, "Kaa sasa. Muda ninao kidogo leo, nataka niwahi."

Akiwa anasogea kuketi, aliyeingia hapo akasema, "Ningefikiri unapanga kulala kabisa hapa, chupa nzima!"

"Ah, inaisha sa'hivi tu. Karibia pia," bosi akasema hivyo.

"Asante, kwa leo nimefunga," mwenziye akamwambia.

"Au siyo? Unaweka kichwa straight kwa ajili ya nini?"

"Ukiwa kwenye line ya kazi kama yangu mkuu, kuangalia nyuma ya mgongo wako kila mara inakuwa jambo must, kwa hiyo... lazima kujiweka makini muda wote."

"Acha mambo yako wewe! Unataka kusema hujanywa kabisa tokea jana... kama siyo leo leo? Wewe Chomoka?" bosi akauliza hivyo.

Mwanaume huyu aitwaye Chomoka, akacheka kidogo.

"Mimina bana, acha bangi," bosi wake akamwambia hivyo.

Kweli, Chomoka akavuta glasi iliyokuwa pembeni na kuanza kuimiminia kinywaji.

"Uwe care kama we' ni mchanganyaji, haina urafiki na koo hiyo," bosi akamwambia.

"Ah, bado sana. Hakuna inayonisumbua kihivyo, sijaona," Chomoka akasema na kisha kunywa kileo kavu kavu.

Bosi wake akanywa pia.

Chomoka akaangalia upande uliokuwa na wanawake wazuri, ambao waliangalia upande huu pia, naye akauliza, "Mbona hujaita mtoto hata mmoja?"

"Time. Leo siyo siku yao," bosi wake akamwambia.

Chomoka akatabasamu na kusema, "Safi sana. Ukiwa makini na muda huwa hutikiswi, hata na kalio yaani..."

"Hahah... hao wapo tu, kama unataka kuita ni wewe. Ila sasa tufanye kilichotuleta hapa kwanza, mengine baadaye" bosi akasema.

Chomoka akatikisa kichwa kukubaliana na hilo.

"Vipi kazi?" bosi akauliza.

"Fresh," Chomoka akajibu.

"Vijana?"

"Wako good. Kila mmoja ashalipwa."

"Na umeshawapanga kuhusu...."

"Ndiyo, kazi nyingine ikitokea wako tayari kukutana. Ni suala la lini na wapi, tunajua jinsi gani ya ku-handle, kwa hiyo hamna shida hapo," Chomoka akasema.

"Sawa. Kwa hiyo mambo yako poa, na yameenda vizuri so far. Ulitaka tuzungumzie nini sasa?" bosi wake akauliza.

Chomoka akaweka glasi ya kileo mezani, kisha akasema, "Morgan."

Bosi wake akatulia na kuendelea kumwangalia.

"Morgan anazingua boss. Haniheshimu, na hii siyo mara ya kwanza nakwambia hivi..."

"Najua."

"... yaani, concept yote ya mimi kuwapa amri vijana inamkera. Yeye anafikiri ukimpa order sijui unakuwa unam...."

"Amefanya nini? Usizunguke sana, shida nini?" bosi wake akamkatisha.

Chomoka akasema, "Ile ishu ya dukani ingekwenda mrama kwa upande wetu boss kwa sababu ya ujeuri wa Morgan. Kama ulivyoagiza, tulitakiwa kubeba vile vitu, tulichome duka, wale security tuachane nao. Lakini jamaa alitaka tuwaue, oh hapana... alikuwa anataka kuwaua yeye mwenyewe. Na akafanya hivyo ili ajiridhishe tu."

Bosi wake akatafakari kidogo, kisha akavuta glasi yake na kusema, "Sawa. Ndiyo kilichokukasirisha hicho, au kuna kingine?"

Chomoka akamwangalia kwa njia ya kushangaa kiasi.

Bosi wake akanywa kileo na kusema, "Unajua hiyo ni nature ya Morgan, wala hata sishangai. Hakuna shida kama alifanya hivyo ili kusiwe na... loose ends... inaweza ikasaidia..."

"Hapana, boss... tulikuwa tunaenda na muda. Kila kitu kilikuwa kimekamilika, tulitakiwa kuondoka, yeye akataka kuburudika eti... awaue, ajifurahishe, halafu mbaya zaidi... nilipomsisitizia kwamba hakuna sababu ya kuwaua, ili tu kuni-provoke mimi, akaamua kuvua mask makusudi ili atokeze sababu ya kuwaua. Halafu akawaua vibaya, yaani kama mnyama mkati... me mpaka nashindwa kuelewa ulimtoa wapi huyo mtu!" Chomoka akaongea kwa mkazo lakini kwa sauti ya chini.

Bosi wake akatabasamu kiasi na kunywa kidogo, naye akasema, "Damu bado inachemka baina yenu eti? Na yeye alivyo mbabe basi inakukera..."

"Please chukulia hili seriously..."

"Chomoka, achana na Morgan. Ndivyo alivyo. Anafanya hivyo makusudi tu... kama ulivyosema, kuku-provoke, maana nimemweka chini yako... lakini anajua hatakiwi kufanya lolote kulitia tumbua letu mchanga..." bosi wake akamwambia.

Chomoka akaangalia pembeni kwa kuudhika.

"Hakuna chochote kilichofanyika kitakachoharibu lolote. Kama ishu ni kuwaua hao security, haina umuhimu bro. Wameshakufa. Imepita. Mali tumechukua. Tupo secure. Naona kilichopo hapa ni tension mliyonayo nyie wawili tu ndo' inasumbua nerve zako, lakini Morgan yuko vizuri sana. Hata we' unajua hilo," bosi wake akamwambia.

Chomoka akatikisa kichwa kwa kukerwa.

"Kama kazi ilikuwa imeshakamilika na mkatoka fresh... fresh. Akitaka kuwaua hao wapumbavu, mwache awaue. Sikusema ni lazima muwaache hai. Na ndiyo, Morgan siyo wa nchi hii. Nimemtoa Jamaica huyo, kwa hiyo angalia usije kumpandishia bangi siku moja akakugeuza kama hao security... hahahah..." bosi wake akaongea kwa njia ya utani.

"Na wewe utakuwa sawa na hilo kwa sababu tu 'Morgan yuko vizuri?'" Chomoka akamuuliza.

"Punguza hasira Chomo, haina maana. Potezea," bosi wake akamwambia hivyo na kuvuta glasi yake ya kileo.

Chomoka akamwangalia kwa njia makini, kisha akasema, "Kulikuwa na jengo lenye ATM kuvuka barabara kutokea pale tulipokuwa."

Bosi wake akashusha glasi na kumtazama kwa umakini.

"Unajua hiyo inamaanisha nini?" Chomoka akauliza.

"Camera," bosi wake akajibu.

"Ndiyo. Wakati tunaondoka Limbe ndo' akaiona hiyo ATM, ikabidi baadaye kwenda kuzivuruga camera za pale maana zilikuwa zinaangazia mpaka ule upande tuliokuwa," Chomoka akamwambia.

"Mlizivuruga camera wakati tayari zilikuwa zimesharekodi...."

"Simaanishi muda huo huo, ila... sikukwambia, yaani... ilibidi siku iliyofuata niende pale kumlipa msimamizi wao mmoja afute footage za usiku uliotangulia. Nimetoa pesa yangu mwenyewe ili kumziba mdomo na kuziondoa hizo tape boss, la sivyo ingekuwa story nyingine hapa sasa hivi," Chomoka akamwambia.

Bosi wake akatulia kwanza kutafakari hayo.

"Umeona nilivyokuwa nakwambia? Huyu mtu wako atakuja kutu-cost boss. Usinione mjinga mimi kuja kusema haya. Nikimwambia afanye au asifanye hivi ananiona me bwege-fala sijui, ile kujipa ukubwa fulani hivi, basi hasikilizi order. Kwa nini, kwa sababu anatokea kwa wajamaica? Anataka wengine wamwogope yeye zaidi kwa kujifanya anajua sana ukatili. Yuko vizuri, lakini anajiamini kupita kiasi, na tusipoangalia... atakuja kutuangusha. Na nimeshamwona kuwa mtu ambaye akianguka, atakuangusha na wewe boss..." Chomoka akasema hayo.

Bosi wake akabaki kukunja uso tu.

"Nakwambia. Hafai," Chomoka akasisitiza.

Bosi wake akatulia kidogo, kisha akauliza, "Kwa nini hukuniambia hayo mapema?"

"Nilikuwa nangoja hali zitulie. Wewe ndo' umenipa niwasimamie hawa, siyo rahisi maana kila mmoja wao ana akili ya kivyake. Lakini wenziye huwa wanafata order tukiwa kwenye mission, yeye ndo' ana kichwa kigumu. Kama hiyo tumbua ingeingia mchanga, wewe ndiyo ungekula hasara, na mimi najua ningeumia. Nilitaka kuhakikisha hiyo haitokei ndiyo sababu nikai-handle kimya kimya," Chomoka akasema.

"Una uhakika hakutakuwa na shida kwa huo upande wa ATM?"

"Hamna, hapo hamna shida tena..."

"Tunapaswa kuangalia possibility kwamba huyo uliyemlipa anaweza kuja kufungua mdomo wake baadaye... hata akawaambia mapolisi kuhusu wewe. Hilo utali-handle vipi?" bosi wake akamuuliza.

Chomoka akatulia kidogo, kisha akasema, "Umeona?"

Bosi wake akabaki kumwangalia kwa umakini.

"Bado tunakaa kusumbua akili, tena kusumbua akili yako kwa sababu ya upuuzi alioufanya huyo jamaa. Usingekuwa hata unawaza hivyo kama asingefanya ule ujinga, hapa tatizo siyo ATM wala msimamizi... shida unajua ni kwamba kama akifikiwa, yeye ndiyo ataweza kusema sisi ni nani," Chomoka akasema hivyo.

Bosi wake akatazama pembeni kwa umakini.

"Hii imetokea kama bahati tu sa'hivi hatusakwi moja kwa moja, lakini inaweza kuja kuwa mbaya tena muda mwingine ukituleta pamoja kwa ajili ya kazi. Itabidi udili nalo hili vizuri," Chomoka akamwambia.

Bosi wake akashusha pumzi na kusema, "Unanishaurije?"

"Me siwezi kukupangia. Chochote unachoamua me nafata," Chomoka akamwambia.

Bosi wake akasema, "Namjua Morgan vizuri. Na ni wa muhimu kwetu, kwa hiyo... siwezi kufikiria kufanya jambo kama kumwondoa asiwe nasi kwenye kazi tena..."

"Ukimwondoa kwa namna hiyo kuna chance anaweza kutusaliti boss, siyo wazo zuri. Ukifanya kumwondoa... inabidi iwe kumwondoa kumwondoa," Chomoka akasema hivyo.

"Nini? Kwamba tumuue?" bosi akauliza.

Chomoka akapandisha mabega yake tu.

"Unafikiri ni jambo rahisi tu kufanya hivyo? Yule jamaa ni mta...."

"Najua," Chomoka akamkatisha.

"Kwanza kwa nini mpaka uwaze hivyo? Usisahau tuna mengi ya kufanya, ni mwenzetu, na..."

"Boss, Morgan ni tatizo. Najua unajua Morgan ni tatizo, achana na fikira za tunamhitaji sijui, sikuzote wapo watu wengine walio makini tunaoweza kuongeza. Huyu jamaa atakuja kutuharibia, I swear. Me ndo' namwona, namjua zaidi maana nipo kwenye field pamoja naye. Sisemi ni lazima mpaka.... kumuua... najua siyo rahisi, ila kama ni kumwondoa, inabidi tu tumwondoe boss. Kwa njia moja ama nyingine," Chomoka akasema.

"Kwa nini unasisitizia hilo?" bosi wake akamuuliza.

"Kwa sababu sitaki uanguke. Nakuita boss, lakini wewe ni rafiki yangu, Francis. Najua unapotoka, na najua unapotaka kwenda. Yeye hajui mengi, anajali tu anachopokea mradi anafanya kazi yake. Kitendo alichofanya juzi hapo... inapaswa iwe mwisho. Ni uamuzi wako tu iweje lakini," Chomoka akamwambia hivyo na kuvuta kinywaji chake.

Utata ndiyo ulikuwa penyewe hapo, na hizi ndizo zilizokuwa siri za mitungini! Kiongozi mkuu wa kundi lile la majambazi hakuwa mwingine ila Francis mwenyewe, rafiki yake Reuben. Aliachana na masuala ya msiba wa mke wa mwanaume yule ili abaki kushughulika na mambo yake haramu ambayo, kama Josephina tu, hakuna watu wengi waliofahamu kuyahusu. Alilimiliki kundi hilo la majambazi kutokana na kuwa na pesa nyingi kutonana na mishe nyingi haramu, na walifanya kazi alizowatuma kufanya ili wapate faida kwa hasara za wengine, aidha kwa kuiba, ama kwa kuua watu ili wapate pesa. Na sasa akawa amebaki kutafakari maneno ya "rafiki" yake huyo, Chomoka, yakiwa yamemwingizia mambo mengi ya kufikiria ili afikie uamuzi sahihi wa jinsi ya kushughulika na jambo hili alilomletea.

Chomoka akaendelea tu kutulia na kumsikilizia. Huyu ndiye yule mwanaume aliyewaongoza wale majambazi usiku ule kufanya wizi na kulichoma duka la Stanslaus Mwita, na hapa sasa baada ya tukio hilo kuwa limepita ndiyo alikuwa akizungumza na bosi wao kuhusiana na vitendo vya mwenzake mwenye jeuri ya kinyama. Yule mwanaume mwenye rasi. Morgan. Chomoka alikasirishwa sana na matendo ya mwanaume yule, na akiwa anataka kumkomesha baada ya siku ile Morgan kumwonyesha hakujali kuhusu uongozi wake, Chomoka sasa akawa amemchongea kwa bosi wao.

Na ilikuwa ni kuchongea kwa hila kabisa kwa sababu alipoona Francis hachukulii kwa uzito tabia za Morgan na hata kumtetea, Chomoka akatia uwongo huo wa jengo la ATM ili kumfanya bosi wake afikiri kuwa kweli Morgan aliwatia ndani ya hatari ya kufichuliwa; na angeweza kufanya hivyo hata wakati mwingine. Hivyo sasa Chomoka akatulia ili kuona ni hatua gani ambayo Francis angetaka ichukuliwe dhidi ya huyo Morgan wa Jamaica, akibaki na matumaini kwamba ataondolewa kabisa-kabisa kundini mwao na yeye ndiyo abaki kuwa sauti kuu kwa majambazi wenziye.

Huyo ndiyo alikuwa Francis!


★★★


Upande wa jumba la starehe lililomilikiwa na Josephina, au kama alivyopenda aitwe na waliomfanyia kazi, madam Phina. Ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Paulina na wanawake wengine kuletwa kwenye jengo hilo, walitambulishwa kwa mwanamke huyo ambaye ndiye aliyetakiwa kuwa mheshimiwa kwao. Josephina aliachana na msiba wa Reuben ili kuendelea na mambo yake haya, kama tu Francis kule, akija huku mida ya usiku wa mapema baada ya kumwacha mwanaye nyumbani, na sasa ndiyo akawa ameupokea mzigo wake huo wa wanawake walioletwa ili aanze kuutumia kujiingizia faida.

Baada ya kuweka msingi wa utambulisho wake kwa wanawake hao wapya, sasa ingekuwa ni kuwapatia maelekezo ya namna ambavyo biashara hapa zilikuwa, kisha awapitishe kwenye "madarasa" muhimu kuwawezesha kuzoea mazingira ya hapo upesi ili fursa ziwachangamkie haraka. Yaani wateja. Wanaume. Isaya alikuwa pamoja nao bado ndani ya ofisi hiyo Josephina alipomaliza utambulisho wake kwa madaha, na sasa kazi ingeanza. Akawaangalia mmoja baada ya mwingine, akiwa anawapima kwa macho yake, na yalipotua kwa Paulina, Josephina akamkazia uangalifu kwa kumshusha na kumpandisha huku akiguna mara kadhaa kama kuonyesha mshangao.

"Eh! Wewe... huyu mtoto mmemtoa wapi?" Josephina akamuuliza Isaya hivyo kwa njia ya kustaajabu.

Paulina akabaki kumwangalia kwa ugeni sana.

Isaya akamwambia, "Ndo' aliyemtuma Rozalia. Amefika leo."

Josephina akamwangalia Paulina na kusema, "Ah! Aisee, nyama nzuri hii! Baby, utanibariki sana. Ulikuwa wapi huo muda wote wa maisha yangu?"

Isaya akatabasamu.

"Huyu tunamweka level 5, unanielewa? Ni wa pochi nene tu," Josephina akamwambia Isaya.

"Hiyo ni uhakika madam. Hawaonji wengine hapo," Isaya akasema.

"Kweli. Roza amefanya kweli. Licheki kwanza. Hebu nipe 360 baby..." Josephina akamsemesha Paulina hivyo na kumsogelea.

Paulina akabaki tu kumwangalia.

Josephina akamwangalia pia na kusema, "Mtoto changamka basi!"

Bado, Paulina akatulia tu.

"Vipi, ni bubu?" Josephina akamuuliza Isaya.

"Hamna, anaongea. Ni ugeni tu madam... anakuogopa," Isaya akasema hivyo kumpamba Josephina.

Josephina akamwangalia Paulina tena.

"Zunguka madam akuone, hiyo ndiyo 360," Isaya akamwambia Paulina hivyo.

Paulina akaonekana kubabaika kiasi na kuendelea tu kumtazama Josephina usoni.

Josephina akamwangalia Paulina kwa uvutio, naye akamshika mabegani na kusema, "Oh... usiogope baby. Hapa jijini, umefika. Mali kama wewe ya uhakika, yaani unawaona hawa wote... hawajafika kwako. Kwa hiyo jiachie kabisa mpenzi, hii ndiyo himaya yako, kuua utaua yeyote unayetaka, sijui unanielewa?"

Paulina, akiwa hajaelewa, akauliza, "Kuua?"

Josephina na Isaya wakacheka kidogo, na mwanamke huyu akasema, "Ulivyo huna clue... safi sana. Nisikilizeni nyote..."

Wanawake waliokuwa hapo wakamkazia uangalifu.

"Hakuna kigeni kwa mwanamke yeyote anayefika hapa jijini hata kama ndiyo mara ya kwanza, mbele ya mwanaume wewe tayari unajua kila kitu. Mazingira mtayazoea haraka, tuna makocha wa kutosha. Kikubwa ni nyie kuwa tayari kufanya kila kitu kuingiza wateja na kuhakikisha wanarudi kwa raundi saba zaidi. Sijui mnanipata?" Josephina akaongea, ki-madam zaidi.

"Ndiyo..." wachache wakajibu.

"Ndiyo nini?" Josephina akauliza.

"Ndiyo madam," Paulina akawa wa kwanza kujibu.

Josephina akamwangalia na kusema, "Namna hiyo."

Paulina akatazama chini tena.

Josephina akasema, "Mnajua mnachopaswa kufanya, mmeshafanya sana toka zamani, ila hapa mtatakiwa kuwa ma-professional. Tuna utaratibu wa kufata, kila mmoja wenu anapaswa kuufata. Mtakula na kulala hapa lakini mnajua mjini hakuna cha bure. Wanaume wanakuja, hata wakiwa na wake zao, mnapaswa kuhakikisha hawaondoki bila kuwachomolea mtonyo. Huo mtonyo mnapaswa kuufikisha kwangu, na nyie mnalipwa kwa asilimia kuendana na kila kitu mnachopata hapa; kuanzia make-up, nguo, viatu, chakula, mpaka toilet paper mtazotumia chooni..."

Loh! Wanawake wapya wakaendelea tu kutulia, wakiona ukali wa aina yake ndani ya bosi wao huyo mpya.

"Malipo kwa bajeti. Sijui mnanielewa? Uwe na sura mbaya au nzuri, ketio kubwa ama dogo, hakikisha... agh, mnaelewa. Sidhani kuna mengi zaidi ya kueleza. Sipendi mambo ya kujivuta-vuta, mkiona mtu ni msumbufu, mnaachana naye. Akisumbua zaidi, mnamjua Isaya. Kazi, matokeo. Sijui mnanielewa?" Josephina akaongea kwa uthabiti.

Wanawake wakatikisa vichwa kukubali na kuendelea tu kumtazama kwa umakini.

"Secy yuko wapi?" Josephina akamuuliza Isaya.

Isaya akaangalia saa mkononi na kusema, "Atakuwa ashafika. Nikamwite?"

"Hamna. Wapeleke hawa kwake aanze kuwapanga. Me kichwa kinauma sa'hivi," Josephina akasema.

"Sawa," Isaya akajibu.

Akawaonyesha wanawake ishara kwa kichwa kuwa wamfuate. Walipoanza kutoka ndani ya ofisi hiyo kumpita mwanaume, Josephina akamshika Paulina mkononi kumzuia kwanza, na mwanamke huyu akamwangalia.

"We' ni keki, binti. Utakuwa na wenzio naowapendelea huko juu, achana na hayo majinga. Fanya kazi ya maana kweli, utatoka na pesa nyingi sana," Josephina akamwambia kwa njia yenye ushawishi.

Paulina alikuwa akihangaishwa sana na haya yote moyoni, lakini akajikaza na kutikisa kichwa kukubali. Josephina akamwachia, na mwanamke huyo akampita Isaya kuelekea nje.

Isaya alikuwa akiangalia umbile zuri la Paulina kwa nyuma, kisha akamtazama Josephina na kusema, "La moto!"

Josephina akazungusha macho na kuangalia pembeni, naye Isaya akatabasamu kiasi na kuanza kutoka pia. Ila kabla hajaufunga mlango, mtu mwingine akawa amefika hapo, na jamaa alipomwona akauachia mlango na kumtikisia kichwa kisalamu, lakini mwanaume huyo akampita tu na kuingia kwenye hiyo ofisi ya Josephina. Mlango ukafungwa. Josephina alikuwa tayari kukaa kwenye kiti chake, ila alipogeuka kukuta mja mpya ameingia, akaghairi kukaa na kuendelea kumwangalia kwa njia ya kawaida. Ilikuwa ni Francis. Kaka mtu. Kuu la majambazi. Alimalizana na Chomoka kule walipokuwa muda mfupi nyuma na moja kwa moja akaja mpaka hapa. Alikuja na jambo lake moyoni, na ni Josephina pekee ndiye ambaye angeweza kulipatia suluhu.

Akawa amesimama hapo mbele huku akimwamgalia Josephina kwa umakini, na mwanamke akauliza, "Nini?"

Francis akasema, "Sikukuona tena. Ulienda wapi?"

Josephina akabaki kumwangalia kama vile hamwelewi. Aliweza kuona ni kama Francis alikuwa amekunywa, na aliudhika.

"Nakuuliza," Francis akasema.

"Unaniona niko wapi sa'hivi?" Josephina akauliza pia.

"Usinijibu hivyo Phina," Francis akamwambia huku akimnyooshea kidole.

Josephina akavuta ulimi kwa kukerwa na kukaa kitini, akikiegamia na kufumba macho kabisa kuonyesha hamjali.

"Hivi saa zile ni nini kile ulichokuwa unafanya pale msibani? Mm?" Francis akamuuliza huku akianza kusogea.

"Frans, naomba usinisumbue. Kichwa kinaniuma, hayo ma-stress yako naomba usiyalete kwangu mie..."

"Ulikuwa unamwambia nini Reuben?"

"Ahah... ss.. you're pathetic..."

"Sitauliza tena, naomba jibu," Francis akaongea bila utani.

"Ama utafanya nini? Kama umekosa kazi, hata kuuliza mtoto yuko vipi haimo kichwani kwako, basi naomba usini...."

Josephina akiwa anaongea hivyo huku amefumba macho, tayari Francis akawa ameanza kumwelekea na kufika karibu naye, na ile mwanamke anafumbua macho, mwanaume akamshika mkononi na kumvuta kwa nguvu ili amsimamishe. Josephina akashtuka kiasi, na baada ya kunyanyuliwa hivyo kwa lazima, akakunja uso kwa njia yenye hasira na kumtazama Francis usoni.

"Sipendi dharau Phina!" Francis akamsemesha kiukali.

"We' vipi? Hebu niachie..." Josephina akalalamika.

"Niambie ulikuwa unafanya nini yale..." Francis akafoka.

Josephina akamsogelea karibu usoni na kusema, "We' una shida gani? Mimi huwa nakuuliza kila kitu unachoongea na watu wako, au?"

"Ndo' mpaka uanze kumshika mikono? Umsemeshee sikioni... kila mtu alikuwa anakuangalia, halafu pale ni msibani, unafikiri ilijenga picha gani?"

Josephina akamwangalia kwa njia yenye mshangao na kucheka kidogo kwa dharau.

"Unacheka nini?" Francis akamuuliza.

Josephina akasema, "Kinachokusumbua ni mimi kuongea naye msibani, au wivu tu?"

Francis akabaki kumtazama kwa hisia makini.

"Nini... ulikuwa unafikiri najitongozesha kwake? Kama watu wote wamefikiri hivyo, basi labda ni kweli. Msiba, msiba kitu gani? Cha ajabu ni nini Frans? Hata mabusu tungepiga pale pale..." Josephina akaongea kwa kejeli ya makusudi.

Francis akapandwa na hasira na kumsukumia hadi ukutani huku akimkandamiza, na Josephina akakunja uso kwa kuudhika na kujaribu kujinasua.

"We' ni mshenzi sana!" Francis akamwambia kwa sauti ya chini.

"Ndo' unajua hilo leo?" Josephina akasema huku akijaribu kujitoa kwa nguvu.

Wakaanza kuvutana, Josephina akijaribu kujitoa na Francis akiendelea kumkandamiza ilhali mwanamke mpaka kuanza kumpiga na makofi usoni, ndipo Francis akamkandamiza zaidi na kuirarua nguo yake Josephina kwa juu. Hiyo ikamwacha mwanamke akiwa amefunuka upande mmoja wa titi lake ambalo hakulisitiri kwa sidiria, na Francis akaanza tu kuvuta gauni hilo kutokea chini kwa kulazimisha na kuyafunua mapaja ya mwanamke huyo.

"Frans, hebu niachie! Ach..."

Francis akafanikiwa kuingiza mkono wake kwa ndani kupita mapaja ya Josephina, naye akaishika tight kwa humo na kuingiza kiganja chake katikati kuushika uanamke wa mwanamke huyo.

"Sitaki Frans, nimesema niache..."

Josephina akaendelea kulalamika, mwanaume sasa akiwa ameanza kuukuna uanamke wake na hata kumwingizia vidole, halafu akaanza kumsugua kwa nguvu huku akimkandamiza zaidi ukutani na kuukaribia uso wake. Josephina akalaza kichwa chake ukutani kwa upande na kuanza kutoa miguno ya kimahaba, akiwa bado anampiga-piga jamaa kwa mkono mmoja, mwingine akiukandamiza mgongoni kwake kwa kuufinya. Francis hadi akaanza kumnyonya shingoni mwanamke huyo, akiendelea kumsugua na vidole kwa jeuri sana, na Josephina akaachama na kuanza kuhangaika kwa kuhisi raha.

Kisha Francis akavitoa vidole vyake kwa mwanamke huyo, naye Josephina akampiga kofi usoni kwa nguvu, lakini mwanaume akaendelea kumkandamiza na sasa kuikaba shingo yake kwa mkono mmoja. Akatumia mwingine kuishusha tight aliyovaa Josephina, halafu akajaribu kufungua zipu ya suruali yake mwenyewe lakini ikawa inamshinda. Josephina akapitisha mikono yake kwa chini na kuanza kumfungulia suruali mwanaume, yeye mwenyewe, huku bado akiwa amekabwa, na baada ya kuuweka huru mtambo wa jamaa akaanza kuusugua kwa kiganja chake, naye Francis akalamba kiganja chake mwenyewe na kuipakaa mashine yake. Josephina akatanua mguu mmoja hapo ukutani kwa kuupandisha usawa wa paja la mwanaume, na Francis akamwingia hatimaye.

Mapigo ya utamu yakaanza baina ya wawili hawa, Francis akitumia nguvu kumpa mahaba mwanamke, na Josephina akiyapokea kwa kupenda huku anamtazama kijeuri. Hapo hapo ukutani, jamaa akaendelea kumpa na kumpa mpaka hatimaye akajiachia ndani yake, naye akailalia shingo yake huku kwa pamoja wakipumua kwa uzito. Ilikuwa ni hali yenye kusisimua kwa wote, na haikuwa ajabu hata kidogo. Francis akajiondosha taratibu kwa mwanamke huyo, naye Josephina akajirekebisha huku akivuta tight yake na kuliweka gauni lake vizuri.

"Ahh... umenichania nguo! Nitaondokaje hivi?" Josephina akasema hivyo na kupiga ulimi.

Francis akafunga zipu ya suruali baada ya kurudisha silaha mahali pake, naye akasema, "Nitamwambia Secy akuletee."

Josephina akawa anajaribu kulirudishia titi lake kwa ndani lakini likawa likitoka tu nje, naye akasonya kwa hasira na kumpita Francis kwa kumpamia, akienda upande wa pili wa meza.

Francis akamgeukia na kumwambia, "Phina... usiwe hivyo. Sometimes vitu vingine unavyofanya siyo..."

"Siyo nini? Kuongea na mtu ni vibaya? Mbona unakuwa una-panic sana?" Josephina akaongea kwa kuudhika.

Francis akajitahidi kuzuia hisia zake, naye akamfuata mpaka hapo na kujaribu kumshika, lakini Josephina akaupiga mkono wake kwa kutotaka aguswe. Akamwambia, "I'm sorry basi. Nili... nilihisi wivu tu, ndiyo... nilipatwa na wivu nilipoona umemshika namna ile, halafu ukawa unaongea naye kama yaani..."

"Kwani hujui mipango yetu sisi ni nini?" Josephina akamkatisha.

Francis akatulia.

"Faida ni nini sasa ya kumdanganya kwamba mimi na wewe ni kaka na dada kama utashindwa kuji-control kila utakaponiona niko karibu naye?" Josephina akamuuliza.

"Najua...."

"No, hujui. Unaruhusu ma-stress yako hayo huko yaje kunivurugia mimi mipango yangu..."

"Ni mipango yetu..."

"... wakati unajua siyo rahisi kufanya hizi ishu namna hii. Sasa hivi mke wake amekufa, yuko weak, naweza nika-exploit hiyo, nimvute, tupate faida. Sasa wewe ukikaa kuonyesha-onyesha wivu wako unafikiri itakuwaje?" Josephina akaongea kwa hisia kali.

Francis akashusha pumzi na kusema, "Okay, sawa. Naelewa. Usipandishe sana sauti, sipendi."

"Si ni wewe ndiyo ulikuwa unanipandishia mimi?"

"Basi, yaishe. Nimekuelewa," Francis akamwambia.

Josephina akaangalia mbele kwa kukerwa.

Francis akasema, "Ulikuwa na mipango ndiyo, sikujua tu kama ungeanza mapema, tena kama hivyo leo msibani. Kama kweli utaweza kujiingiza kwenye maisha ya Reuben, tu...."

"Ninaweza! Siyo kama nitaweza," Josephina akamkatisha.

"Sawa, Phina..."

"Tatizo we' unanidharau. Hii biashara ingesimama hivi bila me kuwepo hapa kuiendesha?"

"Ndiyo, najua, sijakataa. Ila ukumbuke bila mimi hii biashara isingekuwepo hata kidogo. Kwa hiyo nikiongea naomba unisikilize," Francis akaongea kwa uthabiti.

Josephina akatazama pembeni.

Francis akasema, "Mambo tunayofanya yanaweza kuvuta attention, tuko hapa muda tunalijua hilo. Reuben ni territory mpya Phina. Ninataka uwe mwangalifu, usije kuchukulia kwamba yuko soft sana kwa hiyo utaweza kila kitu. Hiyo ikikukaa kichwani namna hiyo utapuuzia kwamba makosa yanaweza kujitokeza kwa kujiona uko sahihi kwenye kila kitu, na hiyo ni hatari. Nimeshakufundisha. Kuna mahali na wakati wa kila jambo, na leo we' kufanya vile msibani... siyo kuongea, ila kumkumbatia namna ile... haikuwa sawa. Unapaswa uwe care. Sipendi attention..."

"Sijakuwekea attention yoyote Frans, unajifikiria kupita kiasi. Usisahau mbele ya wengine me ni dada yako. Sa' sijui unaogopa nini. Huo ni wivu wako tu wa kijinga ndo' unakusumbua... tsk..." Josephina akasema hivyo na kusogea pembeni zaidi.

Francis akainamisha uso wake kwa kuhisi kuchoka, kisha akasema, "Okay. Tuachane na hayo. Niambie unahitaji nini sasa hivi. Michongo ilitiki ile juzi, nataka niku-bless kidogo baby."

Josephina akasema, "Wala usijisumbue. Acha nifanye tu makosa, atani-bless Reuben."

"Aaa Phina..." Francis akaongea kwa kukwazika.

Josephina akaendelea kununa.

Francis akamsogelea na kumshika kiunoni, naye akasema, "Sawa. Haina shida basi. Kama unajiamini unaweza kum-handle Reuben wewe mwenyewe, basi sawa. Ukitaka usinihusishe."

Josephina akabaki kuangalia pembeni kwa kuudhika.

Francis akamshika mabegani na kumgeuza ili watazamane, naye akasema, "Ila usisahau kwamba hili game ni langu mimi na wewe. Nitaenda kule, utaenda huko... lakini sisi ni kitu kimoja bado. Sitaacha kuwa hapa kwa ajili yako baby. Kwa chochote. Nataka tu uwe makini. Always."

Josephina akaendelea kujinunisha.

Francis akamshika pajani na kusema, "Unakuwaga mtamu kweli ukikasirika."

Josephina hakutoa itikio lolote kwa kauli hiyo isipokuwa kumwangalia kwa kushusha na kupandisha.

Francis akacheka kidogo kwa pumzi na kumbana kwake kibembelezo, naye akasema, "Niambie. Juzi ulisema kuna vitu vinapungua, na nimeona wasichana wapya wameshakuja. Kuna kitu unahitaji?"

Josephina akaibana midomo yake kama hataki vile, lakini akasema, "Milioni tano."

"Mhm... sawa. Nitaituma kwenye akaunti yako kabla sijaondoka. Hiyo... pamoja na matumizi yako na Hans," Francis akamwambia.

Josephina akamwangalia na kuuliza, "Unaenda wapi?"

Francis akatoa simu mfukoni huku akisema, "Kuna ishu tunaenda kumalizia majengoni. Midomo mingi inayotakiwa kunyamazishwa."

"Si uwatume wengine waende?"

"Hamna, hii nahitaji kuwepo. Vipi, utani-miss?"

Josephina akaangalia pembeni kwa nyodo.

Francis akatabasamu kiasi na kusema, "Hans?"

"Yuko na Linah nyumbani. Atakuwa ameshalala," Josephina akasema.

"Sawa. Acha kudeka sa,' kuna kazi za kufanya. Nenda ukawe bosi," Francis akamwambia na kumwachia.

"Kichwa kinauma," mwanamke akaongea kwa kudeka.

"Nikupe dozi ya pili? Kitaacha tu," Francis akamwambia kiutani.

Josephina akasonya na kumsukuma kidogo, kisha akazunguka kukiendea kiti, naye Francis akatabasamu na kuweka simu yake sikioni baada ya kumpigia mtu.

"Hey, Secy... Safi. Uje kwa Phina sa'hivi, anataka akuagize. Wahi..."

Kisha akakata na kumwangalia mwanamke "wake" tena.

"Me naenda," Francis akamwambia.

Josephina akatikisa tu kichwa kukubali bila kumtazama, naye Francis kweli akajigeuza na kuondoka kutoka hapo.

Kama ni siri ya wawili, hii ndiyo iliyokuwa nzito zaidi baina ya wawili hawa. Francis na Josephina hawakuwa ndugu wa kimwili hata kidogo, bali wapenzi wa muda mrefu walioshirikiana kufanya kazi na mambo haramu kuvuna pesa nyingi. Na Hans alikuwa mtoto wao. Walijitahidi sana kuficha ukweli kwa wengi kuhusu maisha yao isipokuwa wachache waliowafahamu vyema, na sasa kwa kipindi hiki baada ya kukutana na Reuben ile majuzi, kwa pamoja wakawa wameunda njama ya kutaka kumwingia ili awafaidishe kimaslahi kutokana na yeye kuwa mtu mwenye pesa.

Josephina, baada ya mke wa Reuben kupoteza uhai, akawa amepata njia moja. Alikuwa akipanga kujiweka karibu na Reuben hasa kipindi hiki cha huzuni kwake kwa kumzuzua na njia zozote ili aanze kumnyonya pesa. Kwake yeye na Francis kupata pesa nyingi ndilo lililokuwa jambo muhimu zaidi, na Reuben angekuwa sehemu bora ya kujichumia matunda hayo mpaka wahakikishe wamemmaliza na kusonga mbele kwa wengine. Mambo yalikuwa hivyo.




Inaendelea Fasihinet.com



★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Screenshot_20250402-230106 (1).png
 
We jamaa hii nayo ungepeleka tu huko fasihinet.com,
sio unaleta apa kuitangaza ukiona imepata umaarufu unazingua km ulivyozingua ile ya mimi na mimi.
 
We jamaa hii nayo ungepeleka tu huko fasihinet.com,
sio unaleta apa kuitangaza ukiona imepata umaarufu unazingua km ulivyozingua ile ya mimi na mimi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom