Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,177
- 34,444
hahaha wallahFaraji hana tofauti na Onesmo wote wameingia chaka kwenye ndoa zao, mwingine mwanamke malaya mwingine mke mchawi
hahaha wallahFaraji hana tofauti na Onesmo wote wameingia chaka kwenye ndoa zao, mwingine mwanamke malaya mwingine mke mchawi
Hahaa! anataka aachwe hurukwwhyo unataka akupe ww talaka
hahaaBikra ya ndimu![]()
zipo mkuu.. binaadamu kama ameweza kuunda ndege naina paa angani" hawezi shindwa jambo dogo kama hilokuna bikra ya kutengenezwa??
Doreen anaweza panda cheo ghafla...Sehemu ya 54
“Ndio.” Akajibu. Uso wake ukionekana kuwa na hamaniko kubwa. “Kwa nini sasa? Baba alikuwa na maslahi gani na binti huyu,”niliendelea kuhoji.
“Sijui hata niseme nini. Nadhani asili ya tabia za watu wa Kigoma sasa inatuhukumu.” “Unamaana gani?” “Ni kuhusu tabia ya ubishi.
Ubishi wa mume wangu sasa hii ndio matokeo yake. Liati kama Marehemu mzee Hussein angenisikiliza, haya yote yasingekuwepo.” Mama alisema.
“Kwa kweli mmeniangusha wazazi wangu,” nilisema, uchungu mkubwa ukiwa kifuni. “Dunia ya leo ni mtoto gani atawapa heshima wazee wake wamtafutie mke ama mume?
Mimi nilifanya hivyo. Badala ya kumpata mke, mmeniletea kahaba.” Kauli ile ilimumiza sana mama yangu, machozi yakambubujika, akayapangusa kwa kutumia ukingo wa kanga yake huku kwikwi za kilio zikimtoka.
“Uko sahihi Faraji. Hakuna hata moja lisilo la kweli baba, tunastahili lawama, tunastahili kuzodolewa, hata hivyo nahitaji msamaha wako mwanangu.”
“Maji yamekwisha mwagika mama, hakuna jinsi tena,” nilimwambia kumtuliza, sikupenda kumwona anavyolia kwa majuto, ukizingatia makosa yalifanywa na marehemu baba.
Siku hiyo, tulizungumza mambo mengi sana, miongoni mwa tuliyoazungumza ni kuhusu mama kumchukua mtoto wangu na kwenda naye kijijini kwa ajili ya malezi.
Siku ya pili, nilifanya taratibu za kupata tiketi ya ndege ya Fast Jet, jioni ilipotimu mama na mwanangu Mwanda, wakaondoka na ndege.
Angalau roho yangu ilitulia, sikupenda kabisa mtoto yule alelewe na mama yake, mwanamke ambaye hadi wakati ule mama anaondoka na ndege, sikusikia habari zozote kumuhusu.
Pale nyumbani, nikabakia na Doreen, msichana wangu wa kazi,naye nikafikiria nimlipe pesa zake za mshara kisha arudi kwao Iringa.
Hata hivyo, nilipofikiria ukubwa wa jumba lile, nikaona sio vizuri likiwa linabakia pweke, ingawa sikuona pia uzuri wa kuishi na mtoto yule wa kike tukiwa wawili tu ndani ya nyumba.
Sasa nifanye nini? Nimrudishe Doreen nyumbani kwao ama nimwache tuendelee kuishi wawili ndani ya nyumba, akiwa kama mwangalizi na mlinzi wa mji wangu? Nilijiuliza kimoyomoyo. Mwishowe nikaamua Doreen abaki awe mwangalizi wa mji.
Jamaa nae bwege sana... kwani hana vyeti vya ndoa, kuthibitisha kwamba huyo ni mke wake na hajamuacha...Sehemu ya 55
Niliendelea na shughuli zangu kama kawaida, ingawa kazi sikuzifanya kwa ufanisi mkubwa. Kila wakati picha ya mke wangu akifanya mapenzi na mwanaume mwingine ilijitengeneza akilini mwangu.
Na kila jambo hilo lilivyokuwa likipita kichwani mwangu, ndivyo chuki dhidi yake ilivyoongezeka. Chuki ikanifanya nimkumbuke Issa, mwandishi wa gazeti la Uwazi. Nikampigia simu.
Kujua juu ya uchapaji wa habari ya fumanizi ya mke wangu kwenye gazeti lao. “Mkuu,” Issa aliongea baada ya kupokea simu yangu. “Habari yako kaka?”
“Safi mkuu, nilikuwa nakufikiria muda huu huu” “Haya nambie.” “Jioni tunaweza kuonana?” “Jioni ya leo?”
“Ndio” “Tunaweza, kuna nini kwani? Habari itatoka kwenye gazeti?” nilimuuliza kwa kiherehere. “Njoo tukutane La_Charse pub.” Badala ya kujibu maswali, akaishia kunipa miadi.
Kiodogo kidogo nikawa na mashaka kwa kuhisi huenda mpango wangu wa kumkomesha Nasra pamoja na hawara wake umeingia dosari.
Baada ya shughuli za mchana kutwa, jioni niliendesha gari hadi La_Charse nikagiza mishikaki na pilipili, nikawa natafuna zile nyama nikimngoja Issa awasili.
Muda mfupi badaye, Issa akafika, baada ya salamu, akaagiza bia ya baridi, ilipoletwa akapiga tarumbeta, chupa ilipotua chini akaanzisha mazungumzo: “Mkuu leo mkeo alikuja ofisini kwentu.” “Alikuja kufanya nini?” nikahoji kwa wahaka.
“Alileta pingamizi kuhusu kuchapwa kwa habari inayohusu skendo ya kufaminiwa kwakwe.”
“Kwa nini?” “Anasema ameingiliwa kwenye uhuru wake wa faragha kwa kuwa wewe si mume wake na mlikwisha achana miaka mingi kwa talaka isipokuwa wewe ndio umekuwa ukimng’ang’nia” “Shubamit!!!. Kumbe huyu mwanamke fedhuli hivi?”
nilibweka hadi cheche za mate zilizochanganyikana na vinyama vikanitoka “Si kweli kaka, si kweli kabisa. Huyu mwanamke anatafuta pakujifichia, toeni hiyo habari, tena iwe kwa ukubwa ukurasa wa mbele,”
“Ishapigwa pini kaka, habari za namna hiyo huwa hazitoki ili kuto-risk kampuni, kama muhusika akiamua kwenda mahakamani” Issa alisema.
Roho iliniuma, mwili ulinitetemeka kwa hasira, Nasra alikuwa amenizidi kete, vipande vya nyama nilivyokuwa natafuna niliviona vichungu kama shubiri.
Je nini kitatoke?
Anipe talaka ya kazi gani mimi.....nachomuona anahangaika na mambo ya Nasra wakati hajamuacha rasmikwwhyo unataka akupe ww talaka