Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
- Thread starter
- #101
SEHEMU YA 31
“Sasa hiyo pesa tunaipataje?” “Pesa ipo kwenye simu, kama inawezekana mwambie afande akupe simu kisha nikupe Paswood ukafanye muamala wa hiyo fedha.” “Sawa, nipe paswood” aliniambia. Nikamtajia nywila, kisha akaondoka tena.
Haukupita muda mrefu, yule mwenyekiti akawa amemaliza machakato wote wa kuwahonga wale polisi, niliachiwa usiku ule ule na kesi ile ikafutwa.
Walinisihi nisafanye fujo yoyote, wakanishauri ni kheri niachane na mwanamke yule kuliko kuendelea kuishi naye katika migogoro.
Niliwaitikia na kuondoka, nilikiwa sambamba na mwenyekiti yule wa mtaa, nilimshukuru sana yule kiongozi kwa msaada alionipatia ingawa haukuwa uliozingatia misingi ya kisheria. Nikampa shilingi elfu 40 kama ahsante.
Naye aliniomba kwa usiku ule siyo vizuri kurudi nyumbani, kwakuwa bado mimi na mke wangu wote tulikuwa na hasira.
Ushauri wake niliuzingatia, na niliona unamashiko, nilichofanya ni kwenda katika hoteli moja na kupumzika usiku ule wote.
Asubuhi kulipokucha, nilikwenda kuoga na kupata supu nzuri kama kifuangua kinywa, nikajitahidi kusahau matukio yaliyotokea jana usiku ili kuweka kichwa change freshi. Lakini bado nafsi yangu ilikuwa nzito sana juu ya mke wangu.
Nilitamani sana nikae peke yangu hadi pale nafsi yangu itakapookuwa safi, lakini kwakuwa nyaraka za dukani kwangu huwa zipo nyumbani na wasaa ule nilitakiwa kwenda ofisini kwangu, ilinibidi nirudi tu nyumbani.
Nilichukua tax hadi nyumbani, milango ilikuwa wazi hivyo nikapitiliza ndani, nyumba nzima ilikuwa kimya, niaendelea kuzipiga hatua, nilipokifa kwenye kijikorido cha kutokea sebuleni nikamsikia mke wangu akizungumza na simu, nikasita kuendelea kutembea baada ya kusikia maneno aliyokuwa akiyazungumza mke wangu simuni.
Nikatega sikio, jambo alilokuwa akiliongea na mtu wa upande wa pili, lilinitisha sana, mapigo yangu ya moyo yakanienda kasi hadi nikaogopa.