Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

SEHEMU YA 87

Maishani mwangu nilikuwa na tabia moja. (nitaileza) tabia ambayo kimsingi siyo nzuri na ningependa mtu mwingine ajifunze kupitia mimi.

Kila nilipokuwa nikipitia wakati mgumu, nilikuwa napenda kusikiliza na kufuata ushauri ambao ulikuwa unanifurahisha nafsi, hata kama ushauri huo siyo mzuri, kwa kuwa tu umenipendeza ungekuwa swahiba wangu mkubwa kwa kunipa ushauri huo na mwisho wa maongezi ungeondoka na zawaidi kibao kutoka kwangu.

Hivyo basi, watu wote walinishauri nirudi kwa Debora nilijikuta napenda nikae nao muda wote kisha tuzungumzie namna nitakavyorudi kwenye mikono ya Debora. Na kwa kweli watu wangu walipoijua tabia hii walinipa ushauri vile nilivyopendelea mimi.

Wachache sana waliokuwa wakiniambia ukweli wa mambo ulivyo. Ndipo katika kuishi kwa mateso makubwa kwa masiku kadhaa, mwishowe nikafuata ushauri wa marafiki. Usiku mmoja wa saa nne nikampigia simu Debora.

Wakati simu ipo sikioni mapigo ya moyo yalikuwa yakinidunda kama vile simu ile ilikuwa imetegeshwa bomu kwamba itakapo pokelewa tu ingelipuka.
Simu iliita kwa muda mrefu, bila kupokelewa. Nikapiga tana. Safari hii iliita kidogo tu ikapokewa na sauti ya mwanaume.

“Hellow” sauti ya kiume ilisikika.
Nikajikutana nashindwa kuongea, fikra lukuki zikapita kichwani mwangu juu ya mtu aliyepokelea simu ya Debora. Mtu huyu ni nani? Hawara wake? Yupo na Debora kitandani usiku huu? Nilijiuliza kimoyomoyo
“Hellooow” suati ile ilinisemesha tena kwa nguvu.
“Mwenye simu yuko wapi?” hatimaye nikaunguruma.

“We ni nani?” jamaa naye akaniuliza kwa pozi. Nilihisi tumbo likifukuta joto. Nikaamini kivyovyote vile jamaa ni bwana wa Debora. “Wewe ni nani unayeniuliza mimi hivyo?” nikaunguruma tena kwa sauti yenye mamlaka.

Simu ikakatwa. Nikabaki nimeduwaa simu ikiwa bado imenata sikioni. Roho iliniuma vibaya sana, wivu wa mapenzi ukanichemka mwilini na nafsini.

Debora yupo na mwanaume mwingine wasaa huu. Kitandani! Wanafanya mapenzi au wamelala. Fikra hizi zilipita akilini mwangu, nikajikuta napatwa na donge rohoni.

Sikukoma. nikapiga tena. Safari hii nikajisemea kimoyomoyo kama akipokea tena yule jamaa mpuuzi, matusi yote ya duniani yangekuwa halali yake.
ila huyo jamaa sijui faraji " ndio baadhi ya wanaume wa mkoani wanaochafua sifa yetu wanaume wa dar " jitu limetoka mkoani kasulu sijui ujiji bado linaushamba shamba kama vumbi la kwenye mihogo "... jamaa ni zoba sana
 
SEHEMU YA 88

Simu iliita kisha ikapokelewa. Naam! wakati huu aliyepokea alikuwa ni Debora.
“We nani?” Debora aliongea kwa ukali mara baada tu ya kupokea. Sauti yake ilionesha kama aliyetoka usingizini. Nilihisi akili ikinizunguka. Vipi leo naulizwa mie nani na Debora.

Mwanamke huyo aliyenipenda kwa hisia kali hadi kulia machozi, ambaye alifanya kila awezalo kunitoa katika machungu na simanzi ya usaliti wa mke wangu wa mwanzo, Nasra Mfaume. Akaahidi kunipenda maisha yake yote, leo ananiuliza mimi nani?

inamaana namba yangu alikwisha ifuta kwenye simu yake? Namba hiyo aliyokuwa ameishika kichwani mwake kama kiitikio cha wimbo wa taifa. Hata ungeamshwa usiku wa manane angetaja namba yangu kwa usahihi, amekwisha isahau na kuifuta kwenye simu yake?

Mambo yote hayo niyafikiria kwa harakaharaka sana simu ikiwa sikioni huku nikitakiwa kujibu swali nililoulizwa. Mimi ni nani?

“Hunijui Debora?” na mimi nikamuliza kwa upole. “Sauti yako sio ngeni.”
“Ebwana wee!” nilimaka.
“Niambie wewe nani?” akaongea kwa amri.
“Hebu amka usingizi. Unashindwaje kunijua leo.”

“Kama hutaki kusema wewe ni nani nakata simu.” Debora akang’aka.
“Faraji.” Hatimaye nikasalimu amri, nikajibu kwa mkato huku nikihisi hasira kali rohoni.
“Unasemaje?” akaniuliza kwa kiburi.
“Ushanijua ama bado hujanikumbuka?”
“Sema shida yako.”

“Ulimpa nani simu yako Debora?”
“Hiyo ndio shida uliyonayo?”
“Tuanzie hapo kwanza kisha nitakueleza sababu ya kukupigia.”
“Wewe kama nani unaniuliza swali hilo?”
“Hujui mimi ni nani kwako?” “Hebu zungumza mambo sensitive we’ mtu, maswali gani hayo unauliza?”

“Ni wiki mbili tu zimepita tangu tutarafiane, leo mwenzangu ushapata mwanaume mwingine.”
“Kwani kuna kanuni ama utaratibu wowote katika hilo?”
“Nisikilize Debora…” nilisema. Nikaendelea.

“Usiwe kama Nasra, wewe ni mwanamke wa kipekee sana, nakutegemea kwenye maisha yangu. Tafadhali.”
“Sikia wewe!!” Debora aliongea, ni kama vile alichukulia nilikuwa mpuuzi mmoja nisiye jielewa.

“Usiwe mwanaume mpumbavu…”aliniambia. Akaendelea.
“Mrudie mkeo mlee mtoto wenu. Mimi tayari nina maisha yangu mapya, ni mwanamke wa kigogo mkubwa tu hapa nchini, kama hutaki kupata matatizo kwenye biashara zako kaa mbali na mimi.
Hehee .. kapewa za uso
 
SEHEMU YA 87

Maishani mwangu nilikuwa na tabia moja. (nitaileza) tabia ambayo kimsingi siyo nzuri na ningependa mtu mwingine ajifunze kupitia mimi.

Kila nilipokuwa nikipitia wakati mgumu, nilikuwa napenda kusikiliza na kufuata ushauri ambao ulikuwa unanifurahisha nafsi, hata kama ushauri huo siyo mzuri, kwa kuwa tu umenipendeza ungekuwa swahiba wangu mkubwa kwa kunipa ushauri huo na mwisho wa maongezi ungeondoka na zawaidi kibao kutoka kwangu.

Hivyo basi, watu wote walinishauri nirudi kwa Debora nilijikuta napenda nikae nao muda wote kisha tuzungumzie namna nitakavyorudi kwenye mikono ya Debora. Na kwa kweli watu wangu walipoijua tabia hii walinipa ushauri vile nilivyopendelea mimi.

Wachache sana waliokuwa wakiniambia ukweli wa mambo ulivyo. Ndipo katika kuishi kwa mateso makubwa kwa masiku kadhaa, mwishowe nikafuata ushauri wa marafiki. Usiku mmoja wa saa nne nikampigia simu Debora.

Wakati simu ipo sikioni mapigo ya moyo yalikuwa yakinidunda kama vile simu ile ilikuwa imetegeshwa bomu kwamba itakapo pokelewa tu ingelipuka.
Simu iliita kwa muda mrefu, bila kupokelewa. Nikapiga tana. Safari hii iliita kidogo tu ikapokewa na sauti ya mwanaume.

“Hellow” sauti ya kiume ilisikika.
Nikajikutana nashindwa kuongea, fikra lukuki zikapita kichwani mwangu juu ya mtu aliyepokelea simu ya Debora. Mtu huyu ni nani? Hawara wake? Yupo na Debora kitandani usiku huu? Nilijiuliza kimoyomoyo
“Hellooow” suati ile ilinisemesha tena kwa nguvu.
“Mwenye simu yuko wapi?” hatimaye nikaunguruma.

“We ni nani?” jamaa naye akaniuliza kwa pozi. Nilihisi tumbo likifukuta joto. Nikaamini kivyovyote vile jamaa ni bwana wa Debora. “Wewe ni nani unayeniuliza mimi hivyo?” nikaunguruma tena kwa sauti yenye mamlaka.

Simu ikakatwa. Nikabaki nimeduwaa simu ikiwa bado imenata sikioni. Roho iliniuma vibaya sana, wivu wa mapenzi ukanichemka mwilini na nafsini.

Debora yupo na mwanaume mwingine wasaa huu. Kitandani! Wanafanya mapenzi au wamelala. Fikra hizi zilipita akilini mwangu, nikajikuta napatwa na donge rohoni.

Sikukoma. nikapiga tena. Safari hii nikajisemea kimoyomoyo kama akipokea tena yule jamaa mpuuzi, matusi yote ya duniani yangekuwa halali yake.
Inasikitisha sana...

Jamaa ananyota ya bundi...

Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 90

Debora hanijui tena. Amenisahau kabisa kama aliwahi kinipenda. Penzi langu anagawiwa mtu mwingine. Kadiri fikra hizo zilivyozidi kupita kwenye akili yangu ndivyo wivu wa mapenzi ulivyozidi kunifukuta kifuani. Maumivu yakawa makali hatimaye. Nikakata shauri ya kuishi.

Nikaona heri nife. Fikra za kujinyonga kwa kamba zikaanza kutekenya ubonga wangu, nikamini njia pekee ya kuondokana na maumivu ya mapenzi ni kujiua. Nikaitafuta kamba ili nijiue.

NILIPUYANGA huku na kule kuitafuta kamba, hatimaye nikaishia katika stoo, nilifanikiwa kupata aina moja ya kamba ngumu tu, nikamini ingefaa kutwaa uhai wangu bila ‘gozigozi’ Nikarudi chumbani.

Nilirudishia mlango, nikaanza kutengeneza kitanzi ambacho ningejivika shingoni. Kila nilivyokuwa nikimeza mate, nilihisi kitu fulani kichungu kinatumbukia kifuani mwangu.

Na wakati mchakato huo unatokea, ile taswira ya sura nzuri ya Debora ilizidi kuniganda kichwani mwangu, picha hiyo ikawa inapishana kwa zamu na zile fikra za usaliti aliokuwa akinifanyia ndani ya chumba chetu. Sauti moja mawazoni ikawa inaniambia: “Kama utabaki hai, usitarajie kuipata furaha maisha yako yote.”

Lakini, wakati huohuo. Sauti nyingine ikawa inaniambia: “Usijaribu kujiua, ni dhambi kubwa. Kwani mwanamke ni Debora peke yake, wapo maelfu ya wanawake wanaotamani kupendana na wewe.”

Sauti hiyo ikapingwa na ile ya mwanzo ambayo ilisema: “Jidanganye. Utaishi kwa mateso hadi siku unaingia kaburini. Bora ufe tu.” Sauti ya pili ikanisihi: “Usijiue Faraji mfikirie mwanao.”

Lakini sauti ya kwanza ikazidi kuweka hoja: “Kama ni mtoto, ndugu zako wapo, watamlea, hebu jimalize haraka uondokane na machungu haya ya dunia.” “Aaaaagh!!!!!” Nilipiga yowe kali, nilihisi akili yangu inakaribia kupata ukichaa. Zile sauti mbili mawazoni zilikuwa zikinitia wazimu vibaya sana.

Nikabaki nimeghafirika uso umeniparama, na wakati huohuo kitanzi kilikuwa kimekamlika! Nikasimama wima. “Nijiue ama nisijiue?” nikanong’ona peke yangu!
 
SEHEMU YA 91

Nikakisogelea kioo kirefu cha ‘Dressing table’ na kujitizama kama vile kwa kujiangalia vile ile taswira yangu ya pili katika kioo ingenipa majibu! Kwa muda wa dakika nzima nikajitizama tu nikajiona sio Faraji mimi yule ‘handsome boy’ wa zamani.

Faraji huyu niliyekuwa nikimwona kupitia kioo alikuwa amekonda kutokana na kutokula vizuri, mawazo pamoja na pombe, vilikuwa vimemenitafuna na kubakia mifupa.

Macho yalikuwa mekundu na yaliyotumbukia kwa ndani kama mlevi wa gongo.

Shati nililokuwa nimevaa vishikizo vilipachikwa ndivyo sivyo kiasi cha kutoa taswira ya mtu aliyedata, nywele na ndevu zilikuwa timtim kama kondakta wa daladala. “Hebu jione ulivyo, kama kikatuni cha Aloyce Jacob, na bado.

Salama yako ujiue tu.” Sauti ile ya mwanzo ilinisimanga. Mate mepesi yakanijaa kinywani, nilipoyameza nikahisi ule uchungu. Kama shubiri, kwa kweli mapenzi yalikuwa yakinitandika haswa.

Nikajikuta natokwa na machozi, nikaanza kulia kama mtoto. Katikati ya kilio hasira na wivu vilijaza kifua changu na kufura mithili ya koboko.

Niliyatupa macho katika dari, sikuona mahali pakufungia kamba ile ya kujinyongea, bahati mbaya au nzuri mule ndani kulikuwa na ‘slingbord’ “Chooni.” sauti ya kifo ikaniambia. Upesi nikaingia ndani ya choo ambacho kilikuwa ndani kwa ndani.

Naam! mule kulikuwa na bomba la maji lililopita kwa juu. Nikapanda kwa kukanyaga sink, nikafunga vizuri ile kamba, kisha nikajivika kitanzi.
 
SEHEMU YA 92

Roho ya mauti ilikuwa imenivaa, sikuona ubaya wa jambo lile, sikuipa nafasi akali yangu kufikiria mara mbili ama mara tatu na zaidi.

Kila kitu nilichofanya kilisukumwa kwa utashi wa hisia.

Kabla sijajiua sauti ya kimalaika ikanikumbusha “Sasa ukijua nani mwenye hasara? unamkomesha nani. Unajiua Debora anabaki duniani anaponda raha. Ujinga huo.”

Bahati mbaya ibirisi alikwisha nizingira pande zote za dunia, nilichofanya ni kuanza kuhesabu moja hadi tatu kabla ya kujiachia na kujinyongelea mbali: “Moja, mbili, tatuuuu!” nikajiachia!!. Kamba ikanibana shingoni kwa nguvu.

Nikaanza kutapatapa kwa kukosa hewa, kadiri sekunde zilivyojongea ndivyo nafsi yangu ilivyohitaji kuhema, niliishika ile kamba ili nijinasue. lakini wapi. Sikuwa na nafasi nzuri ya kujiondosha.

Uzito wa mwili ukazidi kuikaza zaidi ile kamba shingoni, nikauhisi mkojo ukinitoka na kulowanisha suruali yangu. Kila sekunde zilivyozidi kupotea ndivyo nilivyoona nguvu zikiniishia.

Hamu ya kuishi ikanirejea. Nikajitahidi kwa nguvu zangu zote ili nipige kelele za kuomba msaada, bahati mbaya sauti haikutoka.

Na hata kama sauti ingetoka, bado nisingeweza kupata msaada kwa wakati sahihi. Kamba ilikuwa imebana shingo yangu.

Muda ule ilikuwa ni usiku mkubwa, msichana wangu wa kazi na mwanangu Faraji walikuwa wakikoroma huko vyumbani mwao. “Nilikwambia usijiue, unaona sasa unakufa!!”ile sauti ya pili ilinilaumu fikirani nikiwa naipambania roho yangu.

Nikataka kusema neno ‘nisaidie’ nikajikutana nalitamka kimoyomoyo. “Jitahidi kuizua kamba usife, piga kelele.” Sauti ilinisihi. Wakati huu nikaitii sauti ile ya kimalaika.

Nikaing’ang’ania kamba kwa nguvu ili isizidi kunikaba shingoni, kadhalika nikijitahidi kupiga kelele. Bahati mbaya sauti haikutoka zaidi ya kuishia kukoroma kama chura au gari lililoishiwa mafuta.

Muda huohuo, giza la ajabu likazikumba mboni zangu, na wakati giza linagubika mbele ya ngu nikajiona naelea katika anga maili nyingi kutoka ardhini.

Halafu muda huohuo nikajiona naanguka kwa kasi kuelekea chini, ajabu nikawa sifiki. Katika anguko lile, nikabaini kwamba nilikuwa natumbukia kwenye shimo lenye giza zito. Kuzimu.

JARIBU KUTABIRI KITU GANI KITATOKEA.... . TUKUTANE KESHO HAPAHAPA
 
Pengine wale wanaokuwa katika harakati za kujiua huwa kama wanajuta ila huwa ni too late.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom