Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

Sehemu ya 72

Wakati huo geti lilikuwa limekwisha funguliwa, nikaingiza gari ndani, nikaelekea chumbani, wakati nasukuma mlango wa chumba kumbe Debora alikuwa ndani. alikuwa ametoka bafuni kuoga, amevaa kanga moja tu.

“Honey wangu huyo!!” akanilaki na kunikumbatia “What’s up Debora.” “Niko safi.” “Nasra yuko nje.” Nikamwambia. “Anataka nini?” Debora akauliza kwa ukali. “Nadhani talaka yake.”

“Leta nikampe mwenyewe.” Akafungua kabati akachukua bahasha yenye talaka, akatoka nje kumfuata mke wangu wa zamani. Nasra Mfaume.

Nikiwa ndani, wazo moja likanijia, nikagundua natakiwa nimkabidhi talaka mimi mwenyewe ili kuepusha utata wowote dhidi ya sheria ya dini juu ya talaka. “Debora…We Deboraa!”

nikamwita kwa sauti, ili anirejeshe ile talaka nikampe mwenyewe. “Abee!, unasemaje Faraji?” Debora aliyekuwa amekwishafika mlangoni aliniitikia. “Ngoja kidogo.”

Nilitoka nikamfuta mlangoni. “Natakiwa nimpe mwenyewe hiyo talaka.” Nilimwambia. Debora akaniangalia, akawa kama anajambo anataka kusema ama kuuliza, lakini hakujua ni kwa namna gani uzungumze.

“Nipe hiyo karatasi ya talaka nimpe mwenyewe,” nikamsisitiza. Akanipa katika hali ya unyonge, uso wa Debora ulikuwa ni wenye wivu. “Nataka nishuhudie tukio la kukabidhi,”akaniambia huku akinipa bahasha ile.

Tukaongozana wote hadi nje ya nyumba ambapo mke wangu Nasra nilimwacha, nilipotokeza nikiwa na Debora, Nasra akashikwa na wasiwasi, sikujali, tukamsogolea pale alipokuwa amesimama. “Nasra,” nikamwita kwa sauti tulivu huku nikimwangalia usoni. “Abee,” naye akaitika.

“Kuanzia muda huu…Wewe siyo mke wangu tena, na talaka yako hii hapa, shika.” Nilisema. Nikiukamata mkono wake na kumshikisha ile talaka. “Nadhani hiki ndicho kilikuwa kinakuzuia kuolewa, uhuru ni wako sasa bibi eeh!” Debora naye akaongeza.

Kwa sekunde za kuhesabu Nasra alibakia kimya, machozi yalijikusanya machoni mwake. Nikajiuliza: Inamaana Nasra anaumizwa kwa talaka niliyompa ama ni vipi?

Inakuwaje uso wake uoneshe kuwa na majonzi, ilihali mimi ni mwanaume nisiyependwa na moyo wake? Kwa nini alengwe na machozi? Anajutia makosa yake? Ama ananionea wivu kwa kuniona ninaye mwanamke mwingine ndani ya nyumba aliyowahi kuishi?
 
Sehemu ya 73

Mambo yote hayo yalinifanya niwe na kizungumkuti nafsini. “Faraji mpenzi wangu!” hatimaye akaniita kwa sauti ya upole, aliniangalia kwa macho yaliyo jaa huzuni. Akaendelea kusema:

“Sikuja hapa ili uyaone majonzi yangu, natambua hata nikilia machozi ya damu, nikakuomba kwa maneno yote ya Kiswahili, bado siwezi kuondoa kovu la moyo wako dhidi yangu. “Nimekuja hapa kwa jambo moja tu mpenzi. Kumwona mwanangu Mwanda,” alimaliza.

Nilitamani nimnase vibao baada ya kuzungumza kauli ile, kwa kweli nilimwona ni punguani namba moja, vipi nyakati za shubiri kwenye mahusiano yake ndipo akili yake ikumbuke kwamba alikuwa na mtoto ambaye alihitaji malezi ya baba na mama. “Hebu ishia zako.” Nilimwambia.

“Tafadhali, Faraji nahitaji kumwona Mwanda.” “Ondoka.” “Nimemmiss mwanangu.” “Nasema toka!.” “Niko chini ya miguu yako, nileteeni mtoto wangu.”

“Wewe unakichwa kigumu, husikii?” “Tafadhali nielewe Faraji, shida yangu ni mtoto tu.” “Tokaaa!”nilipayuka kwa sauti, macho yaliniiva kwa hasira.

Nasra, mke wangu wa zamani, akangua kilio, alipiga magoti, akanishika miguu, akawa analia huku akiniangalia kwa huruma, akasisitiza nimlete mtoto amsalimie.

Nilichukizwa mno na kitendo kile, picha akiwa na hawara wake kwenye maeneo mbalimbali wakiponda raha ikawa inajitengeza akilini mwangu, kitendo cha kunijia na kuomba kumwona mtoto niliona ni kama ananisanifu.

Nikamtandika vibao huku nikimsukuma. Nasra akang’ang’ania miguu yangu, akaikumbatia kwa nguvu bila kujali rabsha nililomwangushia.

Debora alikuwa kimya, hata yeye alistajabishwa na rai aliyokuwa nayo Nasra. “Kama utaniua niuwe tu, namwitaji mtoto wangu.” Nikamwongeza makofi mengine, ni kama nilimwambia nikamate zaidi miguu yangu.

Unanilazimisha?” niliunguruma “Niue tu,” alijibu.

Nikaona huyu dawa yake ni kujitoa kwenye himaya yake, kisha niingie ndani na Debora wangu na tulifunge geti.

Nikawa nang’ang’ana kujindoa, Debora naye akasogea kunisadia, akawa anaondoka vidole vya Nasra vilivyokuwa vimenata kama sumaku.

Sijui kilitokea nini bwana, Nasra akamgeukia Debora, kama nyati aliyejeruhiwa akamvaa mzimamzima, wote wakaenda chini, tendo lile hata Debora hakulitegemea.
 
Sehemu ya 74

Mpenzi wangu Debora alikuwa ameumwa meno na Nasra, nilichofanya ni kumtandika teke la tumboni mwanamke yule, aliangukia pembeni huku akigumia maumivu na kugaagaa kama mwanamke aliyeshikwa na uchungu wa kujifungua. “Amening’ata menooo!...Damu zinatoka!!!” Debora naye alilia kwa uchungu.

Maneno ya Debora yakanitia hasira hasa baada ya kuona damu inatoka kwenye titi lake la kushoto. Nikamwongeza vibao viingine Nasra.

Kutoka na na lile teke la tumboni, Nasra kulia akashindwa kuongea pia akashindwa, akabakia anakema huku akipumua kwa shida. “Unatoka huko unakuja hapa kuleta vurugu Malaya wewe, ukome vinginevyo nitakuua,” nilibwatuka.

Kufumba na kufumbua watu walifurika, sikutaka zogo, nilichofanya ni kumwingiza ndani Debora, nikamwacha Nasra akitapatapa kwenye vumbi kama samaki aliyetolewa kwenye maji.

Wakati nakomea geti, nikasikia baadhi ya watu wakilaani kitendo tulichomfanyia Nasra, kama ujuavyo mambo ya mjini, kila mtu bila kuambiwa na mtu walikwisha tambua kwamba Nasra alikuwa mke wangu na Debora alikuwa mpenzi tu.

Nikasikia baadhi ya wanawake wakilani kwa kitendo nilichokifanya. “Wanaume watu wabaya sana, huyu jamaa anashirikiana na mchepuko wake kumshambulia mkewe wa ndoa,” mwanamke mmoja alizungumza.

Sikujali lawama zao, kimoyomoyo nikajisema wangejua uchafu alionifanyia mwanamke yule, wangeona jambo lile alistahili.

Baada ya kumwingiza ndani Debora, nilimvua ile kanga aliyokuwa ameivaa lubega, nikaliona jeraha baya la meno alilong’atwa na Nasra. “Huyu kahaba ndio amekuumiza hivi!” nilinong’ona kwa hasira. Debora alikuwa akilia wakati wote.

Nilichofanya ni kumpa huduma ya kwanza, kisha nikamtaka ajiandae nimpeleke kituo cha afya, muda mfupi badaye tuliingia kwenye gari tayari kwenda zahanati ya Arafa ili akapate matibabu ya jeraha lile la meno kwenye titi lake.

Wakati natoa gari nje ya geti, nikapigwa na butwa baada ya kumwona Nasra akiwa nado yupo kando ya nyumba yangu, alikuwa amechutama akionekana mwenye maumivu makali ya tumbo. Watu wachache walikuwa wamemzunguka wakimsaili mawili matatu.
 
Sehemu ya 75

Alipoliona gari, akawa anasogea kwa kuchechemea, nikatamani hata nimgonge afilie mbali huko.

Nilimwangalia kwa chati, sikummaliza, taswira ya Nasra ilikuwa imebadilika sana, alikuwa ametapakaa vumbi, nywele zake nzuri za kichotara zilikuwa timtim, ngozi yake ilikuwa na michumbuko lukuki.

Nilibadili gia na kuliondoa gari kwa kasi, nikamwacha kwenye hamaniko kubwa, nikiwa Mkwajuni, nikampigia mlinzi wa getini na kumsihi amchunge mtu yule asije ingia ndani.

Tulipofika zahanati ya Arafa, Debora alipewa huduma, akadungwa sindano, sanjari na vidonge vya kupunguza maumivu. Tukarudi kwenye gari safari ya kurudi nyumbani ikaanza.

Nikiwa njiani nikampigia tena simu mlinzi ili nimuulize kama mwanamke yule bado yupo. “Bado yupo bosi.” “Unasema kweli!!” nilihamaki. “Hajaondoka.”

“Kwa nini?” nikauliza swali la kibwege. “Anasisitiza anataka kumwona mtoto wake.” “amekosa haya huyu changudoa, ngoja nije!” niliongea kwa hasira, nikakata simu.

Nikapanga nikifika tu namshushia mkong’ong’oto wa nguvu utakaomfanya apaone nyumbani kwangu kama jehanamu.

“Faraji.” “Nambie mke wangu mtarajiwa.” “Usimpige tena Nasra, utapata kesi.” “Hawezi kunichezea huyu Malaya.” “Nisikilize mimi,”Debora akasema, nikamsikiliza.

Ninacho mpendea Debora ni mwanamke mwenye mawazo mazuri na utashi mkubwa. Nikampa nafasi ya kunishauri. “Mwambie ukweli kwamba mtoto wenu hayupo pale nyumbani, mweleze analelewa na bibi yake huko Nguruka.

Kwa kumweleza hilo, itapeleka afanye uchunguzi kujua kama ni kweli, akijua ni kweli mtoto Mwanda yupo huko Nguruka, athari yake ni moja tu. Anaweza kwenda kumuiba. Anavyoonekana anamwitaji sana mtoto.” “Sasa nifanye nini ili yasitokee hayo? Na kwa nini anamwitaji mtoto kwa nyakati hizi?”

“Cha kufanya ni kumweleza mama awe makini na mjukuu wake, ingawa njia nzuri ni kumchukua mwanao na uishi naye wewe.” “Hilo la kumchukua ni jema zaidi, maana kwa kule Nguruka akiamua kumwiba ni rahisi kabisa kuliko nikiwa naye hapa….”

Nilishadadia. Nikamuuliza tena. “Na kwa nini anamwitaji mtoto nyakati hizi?” “Anavyo onekana huko alikokuwa yamemshinda, anaonekana ni kiumbe aliyetafakari sana maisha yake, na inavyo onesha lipo jambo kubwa lililomsi
 
Sehemu ya 76

Dakika chache zilizofuata, tuliwasili nyumbani kwangu, Kinondoni studio, kama tulivyotegemea, Nasra alikuwa ameketi kitako, amegea ukuta wa nyumba yangu.

Alipoliona gari, akasimama na kusogea, tembea yake ilionekana ni mwenye maumivu ya tumbo, nadhani ni athari za lile teke. Nilisogeza gari hadi getini, naye akasogea upande wangu.

Nilipandisha vioo, yeye hakuniona ila mimi niliomwona. Vioo vilikuwa ‘tinted’ akiwa dirishani akawa analia mikono yake akionesha ishara ya kuniomba kwa kunibembeleza.

Wakati uwazi wa geti unazidi kufunguka ndivyo Nasra alivyokazana kunisihi nimlete mtoto amwone, katika muda wa sekunde za kuhesabu, geti lakawa wazi.

Kwa kutumia kioo cha mbele, nikampa ishara mlinzi amzuia kiumbe yule asithubutu kuingia ndani wakati naliingiza gari.

Nasra akaendelea kulia machozi aliniomba nimkutanishe na mwanaye, labda kwa mtu mwingine aliyekuwa akishuhudia jambo lile angeweza kushikwa na huruma, lakini moyo wangu haukuwa na huruma hata chembe na mwanamke yule.

Nikawa nalingiza gari, huku naye akilifuata, alikaribia getini, mlinzi akamzuia. Akalia kama mtoto, masikini Nasra alitia huruma mno. Nilimteremsha mke wangu mtarajiwa Debora, nikamwingiza sebuleni.

Baadaye nika nikarudi nje kumweleza ukweli mwanamke yule kwamba mtoto alikuwa kwa bibi yake.

Nilipotokeza tu, kama kawaida Nasra alinifuata na kunipigia magoti. “Niko chini ya miguu yako, naomba nimwone mtoto japo kwa dakika moja tu.”

“Nisikilize Nasra…” nilisema, nikaendelea. “Mtoto hayupo hapa, anaishi kwa bibi yake huko Nguruka Kigoma,”nilimwambia, alibakia kimya, ni kama vile alikuwa akisubiri aambiwe jambo hilo ili atulie, alikuwa mtulivu ni kwikwi za kilio tu ndio zilimtoka.

Baada ya kumweleza hayo, nilirudi ndani. sikujua baada ya pale Nasra alielekea wapi, sikutaka kujua maisha yake wala lolote kumuhusu.

Ninachokumbuka baada ya kama siku tatu nikapoke simu kutoka kwa mama. “Mwanao amepotea,” lilikuwa ni neno la kwanza kuzungumzwa na mama baada tu ya kupokea simu yake. “Nini!!!” nilishituka. Nikamkumbua Nasra. ITAENDELEA…..
 
Dah! Kwer fupi tamu
 
Faraji ni mjinga sana...

Anajua kabisa Nasra ni mafya na keshamfanyia mengi machafu... bado anaumeleza mtoto alipo....

Cc: mahondaw
 
Tangu mwanzo jamaa namuona maamuzi yake ya kike kike
yaani boya kweli " najiuliza hata hiyo miradi yake ya biashara anaweza vipi kuiendesha" Maana anaonyesha ana low Iq "... kaniacha hoi zaidi hapo alipomueleza nasra mtoto alipo " wakati awali kabla hajamueleza tayari alishaonyesha kuwa ana wasi wasi nae'... mimi nilidhani kuwa baada ya kumwambia mtoto alipo angefanya mawasiliano ya haraka na mama yake" then kesho yake wange msafirisha kwa ndege akiwa na bibi yake"... Huyo faraji atakuwa ni popoma sio bure ..
 
Ndyo uone mkuu siyo siku unasikia jiran mtaani anapiga mkewe ukaanza kumuona mdau mtata😛
faraji boya ... hamna kitu mule ... we mtu gani siku ya kwenda kumfumania mkewe ameshindwa hata kumrecord video na kumpiga picture za mnato mkewe na mgoni wake "....

@end of the day " Mwanamke na basha wake wamemzunguka wakaenda kuwa honga waandishi" finally amebaki hana hata la kufanya "...kwakuwa hakuwa tena na evidence .. maana angekuwa nazo angeweza hata kumtafuta IT then wakazi leak mitandaoni "..

pia nimemuona zwazwa zaidi jinsi mwanamke alivyo kuwa ana simama kidete na kumwambia kuwa wameshaachana " wakati hana hati ya TALAKA. na yeye anakubali tu .. hahaa hamna mtu humo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom