Simulizi; Bahari ya Hindi

Hii inaonekana itaishia kati maana toka juzi mzigo hakuna bora nipite kushoto!
Kwangu hakunaga alosto hata siku moja mkuu, najua machungu yake so usijali kabisa we soma tu.
 
BAHARI YA HINDI
SEHEMU YA 9
ILIPOISHIA…..Roda akasema,,”kaka nakusalimia…
Mwanaume huyo akageuza shingo yake,, na kumtazama Roda..
Roda akashtuka akaanza kutimua mbio…
Nibaada ya kumuona mtu huyo anafanana na Tobi kwa kila kitu..kuanzia sura mpaka mavazi!!
Roda alikimbia huku analia…
Baada ya kukimbia umbali mrefu..akahisi kuchoka akaamua kutembea…..akaanza kuhisi njaa kali,,akiangaza macho yake huku na kule hakuina mtu hata mmoja kwenye barabara hiyo…..wasiwasi na hofu ikazidi kuongezeka!!
Akajikuta ametokezea kwenye makazi ya watu..akastaajabu baada ya kuona shamlashamla za watu wakisherehekea mwaka mpya!! Roda akamfuata mtu mmoja akauliza,,”samahani dada,,nauliza eti haya ni maeneo gani?yule mwanamke akajibu..hapa ni kisiwani mpakani mwa Unguja na Pemba..
Roda akashtuka sana,,akauliza tena,,”kwani kuna sherehe gani inaendea??
Yule mwanamke akashtuka akamtazama Roda kwa macho ya mshangao..akamuuliza,,”inamaana haujui kuwa leo ni mwaka mpya? Roda akasema,”mwakampya kivipi?..mbona huu ni mwezi wa sita(6) !!
Yule mwanamke akasema leo ni tarehe 1/1/2017
Roda akashtuka!...akajisemea moyoni inamaana tangu mwaka 2007??? Ghafla kumbukumbu ikamjia akakumbuka Tobi alimwambia kuwa siku moja ya kule ujinini ni miaka kumi ya Duniani!!
Roda akaingiwa na uwoga…kwa mbali akaona machinga anatembeza vioo vya kujitazama…akamfuata machinga huyo..akachukua kioo na kujitazama uso wake…akashtuka kuona uso wake unaonekana kama mama wa makamo kiasi!!! Roda akazidi kuogopa zaidi…akarudi kwa yule mwanamke..kisha akasemaa,,”mimi nimepotea…na wenzangu wote wamekufa baharini..baada ya meli tuliyokuwa tumepanda kuzama baharini…mimi niliogelea nikabahatika kufika nchi kavu..Roda aliongeaaneno hayo..yaliyokuwa na ukweli pamoja na uwongo kiasi ndani yake!!!
Mwanamke huyo akasema,,”pole sana kwa majanga yaliyokupata..nitakusaidia kukupa sehemu ya kujihifadhi wakati unafanya mipango ya kurudi nyumbani kwenu..
Roda akafurahi sana kupata msaada…
Mwanamke huyo alikuwa anauza bidhaa ndani ya duka lake…lakini alionekana kumtazama Roda kwa macho ya msisitizo!!!
Roda hakulitambua hilo…mwanamke huyo akasema,,”itabidi ukae hapa mapaka nitakapofunga duka tuelekee nyumbani kwangu.
Roda akasema,,”sawa dada hakuna tatizo nakusikiliza wewe.
Yule mwanamke akauliza,,”umekula?
Roda akajibu,,”hapana sijala nahisi njaa kali..
Wakati huo Roda alikuwa nje ya duka hilo kasimama…
Mwanamke huyo alikuwa upande wa ndani ya duka akainama..alipoinuka akawa ameshikilia sahani yenye chakula…ilikuwa ni Chipsi kuku..
Roda alipokea chakula hicho akaanza kula…
Lakini mwanamke huyo aliendelea kumtazama Roda kwa macho ya msisitizo…kisha akatabasamu..
Roda alikishambulia chakula hicho mdani ya dakika tano tu..sahani ikawa tupu..akasema,,”asante sana dada yangu kwa msaada wa chakula.
Upande mwingine alionekana Tobi akijitokeza barabarani,,barabara hiyo ilikuwa tulivu…haikuonekana hata gari moja kupita kwenye barabara hiyo!!!akazipiga hatua kadhanaa akatoka kwenye barabara hiyo…akasimama kando kabisa.akanyoosha mkono wake..ghafla ikajitokeza ya nyumba moja iliyozungushiwa uzio akatoweka kimiujiza na kujitokeza mdani ya nyumba hiyo…
Ilipofika majira ya saa kumi na moja za jioni..yule mwanamke akafunga Duka..
Roda akajisemea moyoni,,”eneo hili hakuna biashara kabisa..yani tangu nimekaa hapa masaa yote hayo,sijaona mtu hata mmoja akija kununua hata kiberiti..mmh!!!
Yule mwanamke alipomaliza kufunga milango ya duka lake akasema,,”tuondoke twende nyumbani.
Roda akaongozana na mwanamke huyo..walitembea mwendo wa dakika saba,,hatimae wakafika nyumbani kwa mwanamke huyo..akatoa ufunguo kwenye pochi yake akafungua geti….wakaingia ndani ya uzio wakazipiga hatua kuufuata mlango wa kuingia ndani ya nyumba….akafungua mlango wakaingia ndani…akamkaribisha Roda,na kusema,”hapa ndio nyumbani kwangu…naishi na kaka yangu…nahisi atakuwa amelala wacha nimuamshe ili nimtambulishe kwako…
Roda akatabasam,,kisha akasema,,”sawa hakuna shaka..
Mwanamke huyo akazipiga hatua kuifuata korido ya kuelekea kwenye vyumba vya kulala ili amuamshe kaka yake akamtambulishe kwa Roda..
Punde si punde akaonekana mwanamke huyo akija sebuleni huku kaongozana na Tobi…
Roda alipogeuza shingo yake akashtuka kumuona Tobi..ghafla nyumba hiyo ikabadilika…..na yule mwanamke pia akabadilika akawa ni ye bibi kizee(malkia wa bahari) ambaye ni mama yake Tobi!
ITAENDELEA…..
 
Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya 10
Roda akashtuka akaingiwa na wasiwasi! Tobi akasema,,”jisikie huru mimi siwezi kikudhuru tatizo wewe ulienda kinyume na matakwa ya majini! Katika safari yako uliyokuwa unasafiri kwenye meli…ulibeba kitu ndani ya begi lako..kitu hicho kilikuwa kinahabari kuhusu majini na viumbe wa kimiujiza!
Roda akashtuka! Akajaribu kuvuta kumbukumbu,ilikuwa hivi!
Siku moja Roda alidamka asubuhi,,akajiandaa haraka haraka kwenda kazini….Siku hiyo alidamka kachelewa…… .alikuwa anahitajika aende kwenye jumba la makumbusho ya kale,,akaandike habari inayohusiana na mambo ya yanayosadikika ya kimiujiza!!
Alipofika katika jumba hilo la makumbusho aliendelea kuhoji wahusika wanaohusika na kutunza historia ya makumbusho hayo…
Akiwa ndani ya jumba hilo katika pitapita zake akaona kipande cha sanamu! Kipande chicho cha sanamu..kilikuwa kimetengenezwa kwa madini ya Rubi nyekundu. Akakiokota kipande hicho akakiweka kwenye mfuko wa suruali yake ya jinsi(kitambaa kigumu) aliyokuwa ameivaa..
Akaendelea na utafiti wa kuchambua habari zinazohusiana na majini na viumbe wa kimiujiza!
Wiki moja baadae,,akiwa kazini katika kituo cha habari ambapo alipokuwa anafanyia kazi..akaletewa barua kuwa anatakiwa aende zanzibar kukamilisha taarifa ambazo anatakiwa aziwasilishe kazini zikiwa kamili.
Pia akakumbuka kuwa siku ambayo alisafiri…aliweka nguo zote ndani ya begi lake kwa sababu safari yake ya kwenda Zanzibar..angebaki huko kwa wiki nne(4) mwezi mzima..miongoni mwa nguo alizoziweka ndani ya begi,,,ni ile suruali ya jinsi ambayo inakipande cha sanamu iliyotengenezwa kwa madini ya Rubi! Kipande hicho alisahau kukitoa ndani ya suruali hiyo….
Akashtuka akasema,,”nimefanya nini mimi? Kosa langu ni lipi? Au tatizo ni kile kidubwasha nilichokiokota kule kwenye jumba la makumbusho?
Kitendo cha Roda kuita Rubi kidubwasha! Kilimkasirisha Tobi!!!! Akabadilika na kuwa na sura ya kutisha!!! Meno yake ya mbele yakarefuka ndani ya sekunde moja….
Roda akaingiwa na hofu kubwa kupita kiasi! Hakuwahi kumuona Tobi katika muonekano huo!...
Tobi akamsogelea Roda akamwambia,,”unanikosea heshima mbele ya Malkia wa bahari..ambaye ni mama yangu mzazi!
Kutokana na hasira Tobi akajikuta anamkaba shingo Roda kwa mkono wake…
Malkia wa bahari akagundua kuwa mwanae Tobi kakasirika kwa sababu Roda kadhalilisha Rubi!!
Akamzuia Tobi asifanye jambo lolote baya kwa kusema,,”huyu ni mpenzi wako,,chaguo langu mimi pamoja na miungu wa bahari.nakusihi mwanangu isimdhuru binti huyu!
Ghafla Tobi akabadilika na kurudi katika hali yake ya kawaida….akashtuka akamwambia Roda,,”samahani,haikuwa kusudio langu wewe ndiye amani ya moyo wangu….
Roda alibaki kimya bila kujibu kitu chochote akimtazama Tobi kwa macho ya mshangao!
Tobi akasema,,”nisamehe mpenzi..Roda akabaki akimshangaa Tobi!! Kisha akamuuliza,,”kwa nini unaniita mimi mpenzi wako?
Tobi akageuka nyuma na kuzipiga hatua kadhaa,kisha akajibu,,”nakuita mpenzi kwa sababu nakupenda na wewe ndiye chaguo langu..pia ni chaguo la Malkia wa bahari!
Roda akashtuka akasema,,”mbona mimi sina hisia zozote za kimapenzi na wewe?
Tobi akasema,,”kumbuka masaa kumi na sita yaliyopita tulikuwa kitandani ukasema kuwa umekubali kuwa wangu!
Roda akaingiwa na wasiwasi akajilaumu kwa ule mpango wake aliodhani kwamba ni sahihi,,kwa kumkubalia Tobi ombi lake la yeye kuwa mpenzi wake!!!!
Tobi akacheka kicheko cha sekunde tatu kisha uso wake ukawa kama mtu ambaye hajacheka!! Akasema ,,”mimi siwezi kukudhuru bali wewe ndiye unataka kujiletea mauti.
Macho yakamtoka Roda! Baada ya kusikia kauli hiyo..akauliza kwa mshangao,,”Mauti?? Mimi nimefanya kosa gani litakalosababisha uniuwe?
Swali hilo lilimfadhaisha Tobi akajikuta amtazama Roda kwa macho ya huruma!
Malkia wa bahari akatoweka kimiujiza! Akamuacha Tobi na Roda wakiwa peke yao.
Tobi akaongea kwa sauti ya chini,,”nakukupenda sana Roda..na sihitaji kukukosa..
Tobi aliendelea kuongea maneno matamu yenye ushawishi wa asilimia mia moja(100%) Roda akajikuta anamuamini Tobi kwa asilimia zote!
Roda akasema,,”nakupenda pia!...
Tobi akafarijika na jibu la Roda lenye hamasa ya mahaba mubashara!!!! Kisha akasema,,”haupo kwenye kifungo! Mimi ndiye mkombozi wa maisha yako..Malkia wa bahari alitaka kuondoa uhai wako..kwa sababu ulibeba Rubi nyekundu ndani ya begi lako na ukapita juu ya himaya yake!!!
Lakini alishindwa kufanya hivyo kwa sababu wewe ni mtu muhimu kwangu..adhabu amboyo ulitakiwa upate wewe akaamua kuwapa abiria wenzako….kwa kunywa damu yao.
Roda akauliza,,”mama yako anakunywa damu ya binadamu?
Tobi hakutaka kuongea ukweli kuhusu hilo akajibu kwa kudanganya,,”hapana aliwapa adhabu tu ya kawaida.. /
Roda akauliza kwa msisitizo,,!!”wewe umesema alikunywa damu ya abiria wenzangu!?
Tobi akaamua kufanya miujiza ya nguvu za giza ilimradi Roda asiendelee kumuuliza maswali na asifahamu ukweli wowote kuhusu hilo!
Akatazama kando yake pakabadilika na kuonekana ni mbuga ya wanyama! Kisha akamsogelea Roda na kumkumbatia..pumde si punde wakajikuta wamo ndani ya mbuga Ya wanyama! Roda akafurahi sana..mawazo yake yote yakatoweka yakahamia kutazama wanyama aliowaona mbele yake….
Tobi akagumdua kuwa Roda amesahau kila kitu..akaamua kufanya jambo ili asije kukumbuka chochote..akamtazama machoni..ukatoka mwanga wenye rangi nyingi.ukaingia machoni mwa Roda…ukafuta kumbukumbu zote..
Roda akawa hakumbuki kitu chochote alichokiona kabla.
Tobi akamgusa Roda kichwani..pasipo Roda kujua kuwa Tobi analengo gani! Ghafla Roda akajikuta yupo nyumbani kwake akiwa chumbani.Roda hakuweza kugundua kitu chochote kilichotokea juu yake! Kwa sababu Tobi alifuta kumbukumbu ya matukio yote yaliyotokea aliyoyashuhudia Roda machoni mwake..akanyanyuka kutoka kitandani,,akajiandaa kuelekea kazini…kabla hajatoka akasikia mlango wa sebuleni unagongwa!
Akaenda kuufungua…akamuona Tobi..Roda akatabadam na kusema,,”karibu.
Tobi akajibu,,”asante nimekuja kukupitia twende kazini..
Roda akasema,,”nilikuwa namalizia kujiandaa..
Tobi akasema,,”sawa hakuna shaka wacha nikusubiri ndani ya gari…
Roda akafunga mlango na kuendelea kuweka vitu vyake sawa…..
Kule ndani ya gari alionekana Tobi,, uso wake ulikuwa umejaa tabasamu..punde si punde Roda akatoka ndani ya nyumba na kuufunga mlango wake..akazipiga hatua kulifuata gari la Tobi.
Safari ilaanza…walipofika kazini kazi zikaendelea kama kawaida,
Mmoja kati ya wafanyakazi wenzake akamfuata na kumuuliza jambo fulani…Roda akaonekana kishangaa baada ya mfanyakazi mwenzake kumuuliza mambo ambayo hayajui…
Roda akasema mbona sikumbuki! Kitu chochote kuhusu jambo uliloniuliza!
Yule mfanyakazi akaamua kuondoka kwa kuhisi kuwa Roda amemdharau!
Roda akawasha kompyuta anayoitumia kuhifadhi kumbukumbu ya kazi zake! Akastaajabu kuona ni mwaka 2017…akashtuka akahisi huenda kompyta yake imeharibu mpangilio(setting’s)
Kumbe ni miaka kumi imepita tangu apelekwe kule ujinini..
ITAENDELEA…
 
BAHARI YA HINDI
SEHEMU YA 11
ILIPOISHIA……Roda akawasha kompyuta anayoitumia kuhifadhi kumbukumbu ya kazi zake! Akastaajabu kuona ni mwaka 2017…akashtuka akahisi huenda kompyta yake imeharibu mpangilio(setting’s)
Kumbe ni miaka kumi imepita tangu apelekwe kule ujinini..
Kumbe Tobi alifanya jambo la kimiujiza..miaka hiyo yote nafsi ya Roda ambayo ni kivuli chake ilikuwa inakwenda kazini kama kawaida..lakini ilikuwa ndani ya mwili wa mtu wingine…Roda halisi alikuwepo kule ujinini kwa kipindi cha miaka yote hiyo….
Roda hakujali akaendelea kufanya kazi,bila kutambua yaliyotokea.
Siku zilizidi kusonga kusonga,,maishau yakaendelea…lakini Roda akilala nyakati za usiku.Tobi alikuwa anamtokea na kumuingilia kimwili,,pasipo Roda kujua chochote. Roda akawa anahisi ni ndoto,,lakini akajiuliza maswali mengi pasipokupata jibu,,”kwa nini kila siku naota nafanya mapenzi na mtu ambaye siioni sura yake.na nikwanini ndoto hii ijirudie kila siku?
Siku zilizidi kusonga,,na miaka ikasogea.,,,,siku moja Tobi alikwenda nyumbani kwa Roda,,ilikuwa ni siku ya mapumziko ya kazi..
Tobi akaanza kumchombeza Roda….
Roda akaishia kutabasamh tu bila kujibu kitu chochote..wakaendelea kubadilisha mawazo kwa maingezi mbalimbali..
Baada ya masaa mawili kipita Tobi akamuaga Roda na kuondoka zake.
Siku zilizidi kusonga..Tobi aliendelea kumtokea Roda nyakati za usiku na kifanyanae mapenzi pasipo Roda kufahamu…
Siku ya leo majira ya usiku wa manane..Tobi altokea Roda na kufanyanae Mapenzi…ghafla Roda akashtuka kutoka usingizini…akahisi kama kalowana sehemu zake za siri! Akanyanyuka na kuwasha taa akashtuka kukuta kweli kalowana..alipojishika kwa mkono wake akagundua kuwa ni manii..macho yakamtoka akajisemea moyoni,,”ndoto gani ya namna hii…akaanza kuingiwa wasiwasi..akaamua kusali..kisha akaingia bafuni na kujisafisha mwili.
Alipomaliza akarudi chbani akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi. ************************
Asubuhi palipokucha,Roda akadamka akajiandaa na kuelekea kazini ….alipofika akaingia ofisini..Tobi akamfuata wakasalimiana kisha akamuuliza ,,”umeamkaje?
Roda akasema niko njema..lakini kunajambo linanitatiza,
Tobi akatabasamu akajua kile ambacho Roda anataka kumwambia.
Roda akaanza kumwambia Tobi kuhusu ndoto anayoiota kila siku! Tobi akacheka kisha akasema,,”hiyo ni ndoto tu, yawezekana kunamwanaume unampenda sana…na kama hayupo basi inaonekana umeishi muda mrefu pasipo kushirikiana kimwili…mawazo yako ndio yanakufanya wewe uote ndoto kama hizo!
Wakati huo Roda alikuwa anamsikiliza Tobi kwa umakini…kisha akasema,,”labda ni kweli kwa sababu ninamida mrefu sana sijashirikiana kimwili..sikumbuki mara ya mwisho ilikuwa ni lini!
Tobi akauliza swali la kimitego,,”bafo hujafikiria kuolewa?
Roda akatabasamu kisha akajibu,,”kwa sass bado sijampata mtu ninayempenda..
Tobi akadakia! Akasema lakini kumbuka nilishakuambia kuhusu mahusiano baina yangu mimi na wewe laki hukunijibu chochote..uliishia kitabasamu tu….kwanini usinipe nafasi hiyo..nikumiliki….Tobi aliongea maneno hayo huku akimtazama Roda machoni..
Roda akauliza,,”tangu nimekufahamu sijawahi kukuona ukipiga kope! Unatatizo gani machoni mwako?
Tobi akashtuka kwa sababu alijua kuwa majini hawana uwezo wa kupiga kope kama walivyo binadamu wakawaida!! Akajibu kwa kudanganya,,”mimi ndivyo nilivyozaliwa hivi..
Roda akastaajabu lakini hakujali..
Ilipofika jioni ,,muda wa kazi ulikwisha,Roda akaondoka na kuelekea nyumbani kwake….akajilaz akabaki anatafakali,,kuhusu yale maneno ya Tobi..akajikuta anapitiwa na usingizi akasinzia!
Baada ya masaa kadhaa kupita akashtuka usingizini..alipotazama saa ilikuwa ni saa tano za usiku..akanyanyuka na kuingia jikoni..akachulua mayaianne akayakaanga …kisha akachukua juisi ndani ya friji..akaanza kula na kunywa juisi hiyo..akaingia bafuni akaoga kisha akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi….
Ilipofika saa saba za usiku,,,Tobi akajitokeza mdani ya chumba cha Roda..akamtazama kwa macho ya matamanio akavua kofia yake aliyokuwa ameivaa kichwani..akafungua mkanda,,akapanda kitandani na kuanza kumuinhilia kimwili Roda….alipomaliza tu..Roda akashtuka kutoka usingizini..Tobi akatoweka kimiujiza….akasahau kofia yake juu ya meza iliyokuwemo ndani ya chumba cha Roda..
Roda akajisemea moyoni,,”hivi ni kwanini huwa naota naingiliwa kimwili na mtu asiyeonekana sura yake? Na nikwanini mdoto hii inajirudia kila siku?
Roda akanyanyuka nabkuwasha taa…akashtuka kuona kofia ipo juu ya meza!!
Akaitambua kofia hiyo kuwa ni ya Tobi! Akajiuliza moyoni,,”kofia hii imefikaje chumbani kwangu?
Nani kaileta humu..
Roda akaingiwa na wasi wasi hofu ikazidi kuongezeka.. akatoka chumbani,, akaelekea bafuni,, akaoga kisha akarudi chumbani,, akashtuka,, macho yakamtoka alipotazama pale juu ya meza hakuiona tena ile kofia,, akajiuliza moyoni,, “hivi hii ilikuwa ni ndoto
Au niliona kwa macho yangu!!? Mbona akama niliona kofia hapa juu ya meza na nikaishika kwa mikono yangu!
Basi kama ilikuwa ni ndoto,,,nahisi naanza kuchanganyikiwa.!
Roda hakujali akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi..
Baada ya lisaa limoja kupita Roda alisinzia usingizi mzito.. Tobi akajitokeza chumbani kwa Roda,, akachukua shuka ndani ya kabati akamfunika Roda.. kisha akamvusu shavuni….
Tobi akasimama wima,, akatoweka kiujiza.
/
Asubuhi palipokucha,, Roda alidamka na kujiandaa kwenda kazini,,
Baada ya nusu saakupita Roda alimaliza kujiandaa, kisha akaondoka zake, kuelekea kazini.
Alipofika akamuona Tobi anaingia ofisini kwake,, wakasalimiana,, lakini Roda alikuwa anaitazama kofia ya Tobi aliyoivaa kichwani.
Roda akasema,, “usiku wa kuamkia leo,nimeota kofia yako,, imo chumbani kwangu juu ya meza kisha sikuiona tena,, Tobi akacheka akasema,, “inaonekana kuna habari njema kuhusu ombi langu kwako.. Roda akatabasamu akabaki kimya pasipokuongea neno lolote!
Tobi akasema wacha nikaendelee na majukumu ya kazi Tutaonge baadae.
******BAADA YA WIKI MOJA KUPITA******
Roda akaanza kujisikia tofauti.. akawa anapenda kulala pia mwili wake ulikuwa na uchovu muda wote,, akaanza kupoteza hamu ya kula!!
Siku zilivyozidi kusonga Roda akawa anatapika mara kwa mara,, akahisi huenda anamaralia, akaamua kwenda hospitali kufanyiwa vipimo vya damu!
Lakini majibu ya vipimo vya damu yakathibitisha kuwa hana tatizo lolote mwilini mwake,,
Roda akaamua kurudi nyumbani kwake,, lakini bqdo hali hiyo ilijitokeza mara kwa mara,, akawa anatamani kula vitu vyenye uchachu, kama maembe mabichi na ndimu…
Hali hiyo ilizidi kumtesa kila siku,, akaamua kurudi hospitali..
Akafanyiwa vipimo vya mkojo na haja kubwa… majibu yalipotoka yakathibitisha kuwa Roda ni mjamzito! Anamimba ya mwezi mmoja!
Roda akasema,,”wahusika wa kitengo cha maabara hawapo makini na kazi yao! Yawwzekana wamechanganya vipimo vyangu na vya mtu mwingine mimi wina ujauzito na ninamwaka mmoja sijashirikiana kimwili! Daktari akabaki mdomo wazi… Roda akazipiga hatua na kuondoka zake..
Akarudi nyumbani….
ITAENDELEA
 
BAHARI YA HINDI
SEHEMU YA 12
ILIPOISHIA….Roda akasema,,”wahusika wa kitengo cha maabara hawapo makini na kazi yao! Yawezekana wamechanganya vipimo vyangu na vya mtu mwingine mimi nina ujauzito na ninamwaka mmoja sijashirikiana kimwili! Daktari akabaki mdomo wazi… Roda akazipiga hatua na kuondoka zake..
Akarudi nyumbani….
***********************
Ilipofika majira ya saa sita za usiku.. alionekana Tobi akijitokeza kule ujinini,,, akamwambia mama yake ,,”nina habari njema,, Mchumba wangu anaujauzito! Malkia wa bahari akafurahi sana akampongeza kijana wake, kisha akasema,,, sasa fanya haraka iwezekanavyo siku atakayozaliwa mtoto huyo hakikisha haupotezi dakika wala sekunde,, kumleta huku ujinini,, vinginevyo hawezi kuwa mwenzetu kqma akivuta hewa ya duniani kwa sekunde kumi na mbili(12).
Tobi akasema sawa nimekuelewa ewe Malkia wa bahari, kisha akatoweka kimiujiza kurudi duniani..
Miezi ilizidi kusonga Roda akawa haoni mzunguko wa siku zake kila mwezi,, akaona tumbo lake linazidi kukuwa kadri miezi ilivyozidi kusonga,, Roda akaanza kuingiwa na wasiwasi akafanya iwe siri yake.. lakini tumbo la mimba halifichiki,, hatimae wafanyakazi wenzake wote wakajua kuwa Roda ni mjamzito!!
Tobi akawa na ukaribu wa hali ya juu kwa Roda..
Akawa anamuuliza maswali ambayo majibu yake anayajua,, “hivi baba wa mtoto aliye tumboni mwako yuko wapi?
Roda alikosa jibu, kwa sababu kila akijaribu kukumbuka mahusiano yake,, ni mwaka mmoja uliopita,, akilinganisha na umri wa ujauzito wake hakuna uwiano!! Kitendo hicho kilimfanya roda awe na hofu pia wasiwasi,,
Siku moja nyakati za usiku wa manane,, Roda alikuwa kalala chumbani mwake,,, ghafla Tobi akajitokeza akaanza kulipapasa tumbo la Roda,, kisha akalibusu akanyanyuka na kuzipiga hatua
Punde si punde Roda akashtuka kutoka usingizini,, akashtuka kumuona mtu anaishirizia ukutani,,, mtu huyo alioneka kavaa viatu na nguo zinazofanana na nguo na viatu vya Tobi..
Roda akanyanyuka haraka kutoka kitandani… akachukua simu yake na kumpigia Tobi…. Ukasikika mlio wa simu ikiita sebuleni kwake,, Roda akakata simu haraka kisha akapiga tena… simu ya Tobi ikaita kule sebuleni,,, Roda akaingiwa na wasiwasi.. hofu kubwa ikatanda juu yake,, akafungua mlango taratibu akatoka nje ya chumba chake,,, akazipiga hatua huku macho yake yakitazama kwa umakini mkubwa….. alipofika sebuleni,, akahisi kamuona mtu anakatisha kuufuata mlango wa kutokea nje,,, hofu ikazidi kuongezeka… akachungulia,, hakuona mtu.. akaamua kurudi chumbani kwake…. Alipogeuza shingo yake akaona tena miguu ya yule mtu inaishirizia kuingia chumbani kwake!!!!
/
Roda akaingiwa na wasiwasi,hofu ikazidi kuongezeka,, akazipiga hatua za kunyatia kuufuata mlango wa chumba chake ! akaufungua lakini hakuona mtu yeyote kuwemo ndani ya chumba chake. Roda akaingia akaketi kitandani.. akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,, akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi…
Lakini hakupata usingizi akabaki macho wazi mpaka pakakucha !!! akadamka na kujiandaa kwenda kazini……
Siku ya leo Tobi hakuja kumpitia Roda nyumbani kama ilivyo kawaida yake ! Roda akaamua kupanda daladala,,, alipoingia ndani ya daladala hilo akastaajabu kumkuta Tobi kaketi kwenye kiti ndani ya gari hilo,,,,akaamua kuketi kando yake kisha akamsalimia na kumuuliza,, “gari lako likowapi ?
Tobi akajibu,, “limepata hitirafu nimelipeleka kwa fundi…
Bqada ya nusu saa kupita wakafika mjini,, wakashuka kutoka ndani ya daladala na kuzipiga hatua kuelekea kazini ! wakiwa njiani Roda alimsimulia Tobi kuhusu matukio aliyoyaona usiku wa jana !
Tobi akasema pole sana yawezekana unamawazo,, Roda akadakia na kusema,, “pia tumbo langu silielewi kadri miezi inavyozidi kusonga linakuwa kubwa !!
Nimeenda hospitali mara kadhaa,,vipimo vi. Ethibitisha ninaujauzito !! yani hata sielewi,, mimi sijashiriana kimwili takribani mwaka mzima !
Tobi akacheka kisha akasema sio kweli kuhusu hilo ! mbona kila siku unashiriki kimwili,, pamoja na mwanaume unayemthamini na kumuheshimu !
Roda akashtuka akamtazama Tobi kwa macho ya mshangao ! kisha akauliza,, “wewe umejuaje ? kwa upande wangu mimi sijashirikiana kimwili mwaka mzima !!
Tobi akasema siku ya leo ni siku maalumu kwangu,, nataka twende tukale chakula cha usiku pamoja ! Roda akauliza,, “mbona unakwepa swali langu ?
Tobi akajibu,, “hapana nimeongea tu,, lakini ninauhakika na ulichokisikia,
Baada ya dakika kadhaa wakafika kazini..kila mmoja akaanza kufanya majukumu yake ya kazi !
Ilipofika jioni,, muda wa kazi ukawa umekwisha, Roda akazipiga hatua kutoka nje ya jengo analofanyia kazi,, akakodi bodaboda impeleke nyumbani !
Akiwa njiani likaonekana gari la kubeba wagonjwa likiwa kwenye mwendo wa kasi.. gari hilo lilikuwa limewakaribia,, Roda akapiga kelele,,” NAKUFAAA !!!
Punde si punde akaonekana Tobi akinyoosha mkono wake pikipiki ikainuka kama imebebwa ikatuwa kando ya barabara….watu wakatoka ndani ya magari yao wakatimua mbio,,,wakihisi pikipiki hiyo ni ya kichawi… Pia yule dereva bodaboda akashuka kutoka kwenye pikipiki akatimua mbio akihisi kuwa kabeba jini,, pia kitendo hicho kilimshua Roda.. akabaki mdomo wazi huku akiangaza angaza macho yake,,,kwa mbali akamuona Tobi anaishirizia kwenye ukuta wa jengo refu,, (ghorofa)
Roda akatimua mbio kumfuqta Tobi.. alipolifikia jengo hilo hakumuona Tobi.. Roda akahisi kuchanganyikiwa ! akaamua kutembea kwa miguu mpaka nyumbani kwake ! alipofika akajilaza kitandani,, akasikia mtu anagonga mlango,, akanyanyuka kwenda kufungua… alipoudungua mlango hakukuta mtu yeyote kuwepo hapo nje !
Akafunga mlango na kurudi chumbani… akajilaza kitandani… alilala usingizi mzito kupita kiasi…. Mpaka saa nne za usiku Roda alikuwa bado kalala,, Tobi akajitokeza chumbani kwa Roda, akamvua nguo zote kisha akamuingilia kimwili alipomaliza akaamua kujionyesha mbele ya Roda… akamuamsha Roda !
Roda akashtuka kutoka usingizini.. alipofumbua macho akamuona Tobi kalala kitandani kando yake… akauliza kwa mshangao !! umefikaje humu ???
Wakati anauliza swali hilo akagundua kuwa yupo uchi wa mnyama akakurupuka kutoka kitandani akaficha maungo yake kwa kutumia shuka lililokuwa kitandani.
Akahisi kalowana sehemu zake za siri akamtazama Tobi kwa macho ya uwoga wahali ya juu.. kisha akauliza,,, wewe ni nani ?
Tobi akasema,, “unamaanisha hunijui ? mimi ndiye baba wa kiumbe kilichomo tumboni mwako ! kamq unakumbuka nilikwambia kuwa siku ya leo ni siku maalumu kwangu ?
Leo nimeamua ufahamu ukweli kuhusu mimi.. mimi sio binadamu wa kawaida kama ulivyozoea kuniona,, mimi ni JINI.. lakini sina nia mbaya na wewe mimi nimekupenda.. na nimekumiliki kwa kipindi cha miaka kumi na moja sasa,
Roda akastaajabu sana akauliza kwa mshangao ! ,,”unamaanisha wewe ni jini na si binadamu ? Tobi akacheka kisha akajibu,, “ndio ni kweli kabisa uyasemayo !
Roda akataka kufungua mlango atimue mbio.. kabla hajagusa kitasa Tobi akajitokeza mbele yake ! ni kitendo cha sekunde..
Tobi akasema,, “usiniogope,, mimi ndiye baba wa mtoto aliyetumboni mwako.. sina nia ya kukudhuru.. nimekulinda kwa miaka yote hiyo pia muda na wakati umewadia !! utazaa mtoto wa kike,,,.kisha Tobi akatoweka kimiujiza !
ITAENDELEA
 
Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya Tano 13
Roda akabaki mdomo wazi,, akainamisha uso wake akalitazama tumbo lake,, akajisemea moyoni,, “Mungu wangu inamaana Tobi ni jini? Pia alikuwa akiniingilia kimwili miaka yote hiyo? Sasa nimepata jibu la swali nililokuwa najiuliza kila siku, kwa nini kila nikiamka usingizini nakuta sehemu zakungu za siri zimelowana,kumbe ni Tobi,
Nini hatma yangu? Roda alijisewmea maneno hayo huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu…,kumbe tarehe za kujifungua zilikuwa zimetimia,,, punde si punde akaanza kuhisi maumivu makali chini ya kiuno, pamoja na mgongoni!! Maumivu hayo yalikuwa makali kupita kiasi,, yakahamia tumboni Roda akajikuta anashindwa hata kusimama,
Wakati huohuo,,upande mwingine, lilionekana gari likiendeshwa kwa mwendo wa taratibu,, ndani ya gari hilo walikuwemo watu wawili,, mke na mume! Watu hao walikuwa wamepotea njia,, kwa sababu ni wageni maeneo hayo,, walikuwa wanamtafuta ndugu yao aliyekuwa anaumwa kwa kipindi kirefu,, punde si punde Tobi akajitokeza kimiujiza ndani ya gari hilo! Akabadilisha mawazo ya dereva huyo pasipo yeye mwenyewe kujionyesha,
Tobi aliamua kufanya hivyo ili dereva huyo akamsaidie Roda,, kumpeleka hospitali,,kisha akatoweka kimiujiza,,, punde si punde dereva wa gari hilo akaamua kukatisha kona na kuifuata barabara ya vumbi!!
Kwa mbali akaona nyumba,,,akaamua kuifuata nyumba hiyo,, alipofika akashuka na kugonga hodi,,
Wakati huo Roda alikuwa anatambaa utadhani mtoto mdogo,, huku akihisi maumivu makali kupita kiasi, (uchungu wa mimba) Roda akasikia mlango unagongwa, akaingiwa na matumaini ya kupata msaada wa kupelekwa hospitali.. akajaribu kulaza sauti huku akisema,, “FUNGUA MLANGO UPO WAZI, yule dereva akastushwa na sauti hiyo!
Akajisemea moyoni bila shaka mtu huyu ni mgonjwa,,
Dereva huyo hakujali,, akafungua mlango alipoingia upande wa ndani ya nyumba akashtuka kumuona Roda akiwa anatambaa huku machozi yakimtoka,,
Roda akasema naomba msaada nipeleke hospitali tafadhali nahisi uchungu wa mimba!
Dereva huyo akamnyanyua Roda na kutoka nae nje ya nyumba,, akamuingiza ndani ya gari,, mke wa dereva huyo akaingiwa na roho ya huruma akasema,,”najua unapata maumivu kupita kiasi kwa sababu hata miminpia nina watoto.. uchungubwa mimba unatesa kupita kiasi.. jikaze.. wakati anaongea maneno hayo,, dereva alikuwa tayari ameshaliondosha gari,,
Wakiwa njiani Tobi akajitokeza ndani ya gari,, Roda akamuona Tobi kaketi kando yake,, lakini dereva pamoja na mkewe hawakuweza kumuona Tobi, Roda akasema,, “haya yote umeyasababisha wewe,,, tazama ninavyoteseka! Kwa nini umenitenda hivi?
Yule dereva pamoja na mkewe wakastaajabu,, kila mmoja akabaki anajiuliza anaongea na nani?
Wakati huo Tobi alikuwa anatabasamu,, huku kashika viganja vya mikono ya Roda,
Tobi akasema,, “usiogope,, mimi ndiye mwanaume ninayekupenda na wewe ndiye mama wa mtoto wangu,, Roda akajibu,, lakini wewe ni jini,
Mke wa dereva akamwambia mume wake,, huyu anaongea peke yake,,ni mimba ndiyo imemchanganya,, huwa inatokea kwa mama mjamzito,
Safari iliendelea,, hakuna aliyetambua Roda anaongea na nani,, walihisi ni uchungu wa mimba tu inamchanganya! /
Baada ya dakika kumi kupita wakafika hospitali.. Roda akapokelewa haraka akaingizwa kenye wodi maalumu ya wazazi,,,
Roda akaandaliwa kwa ajili ya kusukuma mtoto atoke tumboni…
Alisukuma kwa muda mrefu lakini ikashindikana,,
Punde si punde Tobi akajitokeza ndani ya wodi hiyo,,Roda akashtuka kumuona Tobi.. alipojaribu kuongea na Tobi,, sauiti haikutoka Roda akawa kama bubu!
Tobi akafumba macho yake,, ishara ya kuwasiliana na mama yake,(Malkia wa bahari)
Ili apewe maelekezo jinsi ya kumchukua mtoto,,, malkia wa bahari akasema,, usichelewe ndani ya sekunde tatu.. mtoto atakapotoka tumboni… endapo utachelewa basi mtoto huyo atakuwa binadamu wa kawaida,, hatoweza tena kuwa jini! Hivyo tutakuwa tumepoteza aseti,, na mtoto huyo ni muhimu kwetu..
Tobi akafumbua macho baada ya kupata maelekezo kutoka kwa Malkia wa Bahari.
Wakati huo huo zikasikika sauti za manesi wakimuhimiza Roda asukume bila kubana miguu ili mtoto atoke akiwa hai.
Punde si punde akaingia nesi mwingine.. nesi huyo alikuwa na uwezo wa kuona majini pasipo kudhurika na chochote,, pia majini walikuwa wanamuogopa sana mtu wa aina hiyo! Nesi huyo alikuwa na pete maalumu aliyoachiwa na marehemu bibi yake,, pete hiyo ni adui mkubwa wa majini.. Tobi akashtuka kumuona nesi huyo!
Punde si punde,, ikasikika sauti ya mtu,, akimuita nesi,, aliyekuwa anaingia ndani ya wodi hiyo ya wamama wajawazito. Nesi huyo akaamua kufunga mlango na kurudi upande wa nje! Kumba daktari ndiye alimuita nesi huyo,, ampe maagizo juu ya jambo fulani.
Kule ndani ya wodi,, Tobi akaanza kuwa na wasiwasi kupita kiasi! Akajisemea moyoni,, “huyu nesi anakitu ambacho ni adui wa majini,, na kama akirudi humu basi mpango wangu utavurugika,, na sijui kama mama(Malikia wa majini )atanielewa!
Wakati huo Roda alikuwa anafanya jitihada za kusukuma mtoto huku manesi wakimuhiziza,, asukume bila kukata tamaa,, endapo ataacha kusukuma atambana mtoto hivyo mtoto huyo atakufa! Roda alijitahidi kusukuma,,
Manesi waliokuwemo ndani ya wodi hiyo,, hawakuwa na uwezo wa kumuona Tobi,, pia sasahivi Tobi hakutaka kujionyesha machoni mwa Roda,, Tobi akajisemea moyoni,, “wacha nifanye jambo fulani,, ili mpango wangu ukamilike.,,,,baada ya kuwaza hivyo akatoweka kimiujiza! Akajitokeza kwenye korido inayokwenda kwenye wodi!! Akuona yule daktari aliyempa maagizo yule nesi mwenye uwezo wa kuona majini!
Tobi akamfuata daktari huyo,, alipomuongelesha tu,, akili ya daktari hiyo ikabadilika,, akazipiga harakaharaka kutoka kwenye kordo hiyo na kuezlekea nje kabisa,,, kwa mbali akamuona yule nesi anarudi,, ni baada ya kumuagiza akalete taarifa ya maendeleo ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa wodi nyingine,, tofauti na wodi ya wamama wajawazito…. Daktari huyo akaendelea kuzipiga hatua mpaka akamkaribia nesi huyo,, kisha akamuagiza kuwa aende kwenye maabara akalete test tube.
Nesi huyo akaondoka zake kuelekea maabara.
itaendelea
 
Bahari ya Hindi
Sehemu ya 14
ILIPOISHIA
Daktari huyo akaendelea kuzipiga hatua mpaka akamkaribia nesi huyo,, kisha akamuagiza kuwa aende kwenye maabara akalete test tube.
Nesi huyo akaondoka zake kuelekea maabara.
Wakati huo huo kule kwenye wodi ya wamama wajawazito,, alionekana Roda akiendelea kufanya jitihada za kusukuma ili mtoto atoke tumboni, wale manesi waliokuwa ndani ya wodi hiyo walostaajabu sana,, kwa sababu limepita lisaa limoja Roda anasukuma lakini hakuna dalili zozote za mtoto kutoka tumboni! Nesi mmoja akatoka nje ya wodi hiyo kwenda kumuita daktari haraka,, ili wajue wanamsaidia vipi Roda! Kabla nesi huyo hajatoka ndani ya wodi hiyo,, akasikia sauti ya manesi wenzake wakisema,, “jitaidi sukuma kwanguvu, mtoto ameanza kutokeza kichwa,, endelea kusukuma,, Roda akasukuma hatimae mabega ya mtoto yakaanza kuchomoza kikabaki kiuno na miguu vikiwa upande wa ndani ya tumbo la Roda,
/
Kule nje ya wodi alionekana Tobi akimtazama yule nesi akiishilizia kuelekea maabara..
Alipohakikisha nesi huyo kafika mbali,, Tobi akaanza kupata amani,, akatabasamu kisha akatoweka kimiujiza akajitokeza ndani ya wodi ya wamama wajawazito.. akashtuka!!! Macho yakamtoka,,ni baada ya kukuta tayari Mtoto amekwishazaliwa,, hivyo amechelewa kulikamilisha jambo la kumchukua mtoto huyo ndani ya sekunde kumi ili mtoto huyo asiwe binadamu wa kawaida,awe jini!
Tobi akajisemea moyoni,,”nimechelewa! Mama (Malikia wa bahari) hawezi kunielewa!
Na sijui itakuaje? Bila kuchelewa Tobi akatoweka kimiujiza! Kuelekea kule ujinini.
Kutokana na kutumia nguvu nyingi, kusukuma mtoto lisaa limoja mfululizo, Roda aliishiwa nguvu baada ya mtoto kutoka tumboni alipoteza fahamu… manesi wakampa huduma ya kwanza,,ili kunusuru maisha yake!
***************************************
Upande mwingine,kule katikati chini ya bahari ya hindi,,(ujinini), alionekana Tobi akijitokeza mbele ya mama yake(Malkia wa bahari) akaeleza yote yaliyotokea..
Malkia wa bahari akakasirika sana,, kutokana na hasira alizokuwa nazo akabadilika na kuonekana kutisha kupita kiasi.. macho yake yalibadilika na kuwa mekundu pasipokuonekana mboni kiini cha jicho.. masikio yake yakawa marefu kama mbwa mwitu! Bahari ikachafuka,, upepo mkali ukavuma kwa kasi… upepo huo ulitengeneza mawimbi makubwa kupita kiasi…. Hata manahodha waliokuwa wakiendesha meli zilizokuwa zikipita juu ya bahari, wakaingiwa na hofu kupita kiasi!
Kule chini ya bahari, alionekana Tobi akiwa katika hali ya uwoga wa hali ya juu,, alitambua vyema kuwa mama yake kakasirika kupita kiasi!!! Na akifikia hatua hiyo ya kubadilika na kuonekana hivyo,, huwa anaingiwa na roho ya kikatiri!!mama Tobi(Malkia wa bahari) akazipiga hatua kumsogelea Tobi,, punde si punde kucha zake za mikononi, zikawa ndefu mara kumi ya kucha zake za kawaida Tobi akazipiga hatua kurudi nyuma!!!!!
Malikia wa bahari akanyanyua mkono wake iliamuadhibu Tobi,,
Kwa kiwango cha hasira alizokuwanazo Malkia wa bahari, ambaye ni mama mzazi wa Tobi,, hapo Tobi yupo kwenye hatari kubwa ya kuuwawa!
Tobi akaongea maneno ya lugha ya kijini,, maneno ya lugha hiyo yanashahbiana na maneno ya lugha ya kiarabu! Akimaanisha kuomba msamaha wa dhati kwa kutubu kosa lake mbele ya Malkia wa bahari! Punde si punde Malkia wa bahari akabadilika na kurudi kagika umbile lake la kawaida,, akaonekana vile vile alivyokuwa bibi kizee.
Akamtazama Tobi kwa macho ya mshangao! Kisha akasema,, “pole sana mwanangu wa pekee,, haikuwa dhamira yangu kukuangamiza, ni hasira tu,,, na nimejizuia kwa kiwango cha juu… lakini bado unayo nafasi,,,ingawa ni mlolongo mrefu ambao unaweza kugharimu maisha yako,, na siwezi kukubali mtoto huyo kuishi huko duniani..
Ni lazima aletwe nyumbani kwa ujinini akiwa tayari ameshakuwa jini… mtoto huyo ni aseti ya Miungu wa bahari,, akwa sababu damu yake inamchanganyiko wa nusu binadamu na nusu jini,, hivyo anauwezo mkubwa kuliko majini wa kawaida… na asipoletwa huku ujinini basi atakuwa adui mkubwa na majini kwa sababu atakuwa anawaona na atatuangamiza bila huruma,, hivyo kutakuwa na hatari ya kizazi hiki kutoweka kabisa!
Wakati huo Tobi alikuwa makini kumsikiliza mama yake(Malikia wa bahari) ili asije akarudia tena kufanya kosa kwa mara nyingine.kisha akauliza nifanye jambo gani ili niweze kuikamilisha kazi hii?
Malikia wa bahari akajibu,, “itabidi uende bahari ya saba(07)ukatafute gamba la konokono mwekundu aliyekufa,, gamba hilo ni maalumu kitalazwa kichwa cha mtoto huyo juu ya gamba hilo.. ni kinga kwa mtoto huyo,,ni muhimu sana.
Bila kuchelewa Tobi akatoweka kimiujiza, kuelekea kwenye bahari ya saba(7)
****************************************
Upande mwingine, kule hospitali alionekana Roda akizinduka, na kupata fahamu,,akashangaa kuona tumbo lake likiwa dogo,, akajiuliza,, “inamaana nimeshajifungua? Je? Mtoto yuko wapi?
Wakati Roda anasukuma mtoto,,alipotoka tumboni aliishiwa nguvu,, kwa sababu alitumia nguvu nyingi sana kusukuma mtoto,, hivyo hakujua kilichoendelea baada ya hapo kwa sababu alikuwa tayari kapoteza fahamu!
Punde si punde nesi akaingia kwenye wodi hiyo huku kambeba mtoto,, akamkabidhi Roda mwanae,, kisha akasema mnyonyeshe sasahivi,,
Roda akampokea mtot huyo huku akimtazama kwa macho ya umakininwa hali ya juu,, akajisemea moyoni,, “asije kuwa ni jini!
Alijisemea hivyo huku akiukagua mwili wa kichanga huyo.
Akagundua kuwa ni mtoto wa kawaida na sio jini! Akaanza kumnyonyesha.
Kesho yake Roda akaruhusiwa kurudi nyumbani,, wakati anatoka akakutana na yule dereva pamoja na mkewe waliompa msaada wa kumleta hapo hospitali.. Roda hakuweza kuwakumbuka kwa sababu wakati wanamleta hospitali,, ilikuwa ni nyakati za usiku,, pia Roda alikuwa amechanganywa na maumivu makali ya uchungu wa mimba,, hivyo hakuweza kuwatazama nyuso zao!
Wakamsalimia Roda kisha yule mwanamke akasema,, “hongera wana,, unatukumbuka? Roda akamtazama mwanamke huyo kwa mshangao! Kisha akauliza,, “nyinyi ni nani?
Yule mwanamke akajibu,, “sisis ndio tulikuleta hapa hospitali jana usiku,, hivyo tulikuwa tumekuja kukujulia hali.
Roda akaingiwa na kumbukumbu,, akakumbuka kuwa aliletwa hospitali lakini hawafahamu watu hao… akasema,, “nimekumbuka asanteni sana kwa msaada wenu.. mimi nimeruhusiwa kurudi nyumbani! Yule dereva akasema,, “wacha tukupeleke nyumbani, .
Roda akakubali,, wakaongozana mpaka nje kabisa ya jengo la hospitali hiyo.. wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea nyumbani kwa Roda ikaanza.
Walipofika waka, Roda akashuka kutoka ndani ya gari akaingia ndani kwake… akashtuka kukuta madhari ya ndani ya nyumba imebadilika,, kila kitu kimebadilishwa na kuwekwa vitu vipya na nyumba ilikuwa safi kupita kiasi!
Roda akastaajabu akajisemea moyoni,, “bila shaka huyu ni tobi ndio kafanya haya yote,, Eee Mungu nisaidie niomdolee hili balaa la huyu jini Tobi..Roda akazipiga hatua akaingia ndani ya chumba chake,, akastaajabu kukuta kumewekwa kitanda cha kifahari na xhumba kimependeza kwa mapambo ya kila aina pamoja na nguo za mtoto,, zikiwa juu ya kitanda,, Roda akaingiwa na hofu akidhani huenda Tobi yumo mdani ya nyumba! Akaita Tobi,, lakini Tobi hakuitika!
Roda akakisogelea kitanda akamlaza mtoto huku macho yake yakitazama huku na kule!
Baada ya nusu saa kupita akaanza kuingiwa na amani,, hakuona dalili yoyote ya Tobi kujitokeza,
itaendelea
 
Bahari ya Hindi
Sehemu ya 15
ILIPOISHIA
Roda akakisogelea kitanda akamlaza mtoto huku macho yake yakitazama huku na kule!
Baada ya nusu saa kupita akaanza kuingiwa na amani,, hakuona dalili yoyote ya Tobi kujitokeza,
Kumbe Tobi kabla hajaenda kule kwenye bahari ya saba,, alirudi duniani akaingia kwenye maduka kimiujiza na kuchukua vitu vyote hivyo ndani ya dakika moja.. kisha akaviweka ndani ya nyumba ya Roda,, akatoweka kimiujiza kuelekea kule kwenye bahari ya saba(7) Tobi alifanikiw kupata gamba la konokono mwekundu aliyekufa..
Siku zilizidi kusonga,, hatiimae mtoto akatimiza miezi miwili na nusu.
Roda alimpenda sana mwanae,, lakini akawa anaishi kwa wasiwasi kwa kuhofia huenda Tobi akamchukua mtoto wake!
Upande mwingine kule ujinini,, alionekana Malkia wa bahari, akiandaa mpango kabambe,, jinsi ya kwenda kumchukua mtoto huyo siku ya leo,, kabla jua halijazama!
Akamuongezea Tobi nguvu za kimiujiza ili aende akamlete mtoto huyo kwa wakati unaotakiwa… Malkia bahari akasema,, “nenda huko duniani mimi nipo nyuma yako,, chochote utakachokifanya mimi nitakusaidia.
Bila kupoteza muda Tobi akatoweka kimiujiza kuelekea Duniani.. pia Malkia wabahari akatoweka kimiujiza kwa ajili ya kumlinda Tobi,, ili waikamilishe kazi ya kumchukua mtoto na kumpeleka ujinini.
Nyumbani kwa kwa Roda, alionekana akimnyonyesha mwanae,, huku akimtazama usoni,, akatabasamu kisha akajisemea moyoni,, “hakika nimeza mtoto mzuri sana kafanana na Tobi,, lakini ninawasiwasi,, huenda Tobi akamchukua mtoto huyu,, yanipasa niende kwa mchungaji,, nimueleze jambo hili,, naamini atanisaidia.. huwa naona mahubiri yake kwenye kioindi cha Runinga akiwaomnea watu kwa imani na matatizo yao yanakwisha!!! Mimi sitaki kumuona Tobi,, na siwezi kuishi na jini,,lakini naamini huu ni mpango wa Mungu kutenda haya yote,, mimi sijui sababu ni nini,, ajuaye ni yeye pekee!
Real da aliongea maneno hayo kwa dhati ya moyo! Wakati huo alikuwa akimnyonyesha mtoto,, alipomtazama akagundua kuwa mtoto amesinzia akamlaza kitandani,,,
Akaingia bafuni akaoga,,kisha akarudi chumbani akajilaza kando ya mtoto wake.. ghafla wazo likamjia akajisemea moyoni,, “kwa nini nisiende sasahivi.. kanisani kwake napajua.
****************************************
Upande mwingine alionekana Tobi pamoja na mama yake(Malkia wa bahari) wakijitokeza kimiujiza kando ya bahari! Jirani na Cocobeach
Wakazipiga hatua kuifuata barabara iliyokuwa jirani na bahari… Tobi akasema,, “kuna watu wawili mume na mke,, niliwaongoza waifuate nyumba ya Roda pasipo wenyewe kujijua… wakampa msaada wa kumpeleka hospitali,,unaonaje tukiwatumia watu hao ili iwe rahisi kumchukua mtoto?
Malkia wa bahari akasema ni jambo jema,, kwa sababu huwezi kumchukua hivi hivi,, ukiwa katika umbile lako halisi,, na ukiwa katika umbile la kijini pia huwezi kumchukua! Kwa sababu damu yake ya yako zinamvutano,, ni damu moja…. Hivyo ni lazima uingie katika kiwiliwili cha binadamu wa kawaida,, hapo ndipo utaweza kumchukua pasipo tatizo lolote!
Tobi akaangaza angaza macho yake huku na kule.. kwa kutumia uwezo wake wa kijini.. akaweza kujua ni wapi wanapoishi wale wanandoa waliompa msaada Roda kumpeleka hospitali.. kisha akasema,, “nimeshapajua ni wapi wanapoishi.. wakatoweka kimiujiza kuelekea kwenye nyumba hiyo!
Wakati huo huo alionekana Roda akiwa amemaliza kujiandaa kwenda kanisani kwa mchungaji,,, akatazama saa ya ukutani ilikuwa ni saa kumi na dakika kadhaa. Akamchukua mtoto wake,, akambeba kwa kumkumbata kisha akatoka nje ya nyumba yake… akaelekea kwenye kituo cha daladala… kabla hajafika huko,, akaonekana mwanamke akimsimamisha Roda,, Roda akasimama,, mwanamke huyo ni yule nesi mwenye pete yenye uwezo wa kupambana na majini.. pia pete hiyo ni adui mkubwa wa majini!
Nesi huyo akasema najua huwezi kunikumbuka kwa sababu ulipoteza fahamu wakati unajifungua,, mimi ni nesi kwenye ile hospitali.
Roda akatabasam,kisha akasema,, “asante sana mimi naishi maeneo haya haya…….kama hautojali twende ukapafahamu pia nashukuru sana kwa msaada wenu nimejifungua salama,, bila kuchelew. A wakaongozana kurudi nyumbani kwa Roda.
Walipofika Nesi huyo akambeba mtoto,, akashtuka akamtazama kwa makini mtoto huyo,,akaona anabadilikabadilika,, anakuwa mtoto wa kutisha mwenye manyoya na masikio marefu,!!!, pia anaonekana kurudi katika umbile la mtotonwa kawaida!
Roda akauliza,, unatumia kinywaji gani?
Nesi huyo akainua uso wake na kumtazama Roda,, akasema,, “usijali kwa sasa sijisikii kunywa kitu chochote. Kwani ulikuwa unaenda wapi?
Roda akajibu,, “nilikuwa naenda kanisani kwa mchungaji… lakini hakuna shaka nitakwenda tu kwa sababu hakuna umbali kutoka hapa nyumbani kwangu..
Nesi huyo akasema,, “inaonekana unatatizo na tatizo hilo sina uhakika kama unalijua!
Roda akashtuka,, akahisi huenda huyo ni Tobi kajibadilisha kwenye umbile la kike!
Mqcho yakamtoka akauliza kwa mshangao! Wewe umejuaje?
Nesi huyo akasema,, “mumeo yuko wapi? Namaanisha baba wa mtoto huyu!
Roda akazidi kuchanganyikiwa,, akabaki mdomo wazi!
Roda akasema,, “yupo lakini katoka atarejea baadae.
Nesi huyo akasema,, “huyu mtoto wako anachembechembe za damu ya binadamu iliyochanganyikana na damu ya jini!
Roda akaingiwa na hofu kupita kiasi! Akasema,, “najua wewe ni Tobi kwanini unaninyima furaha katika maisha yangu?
Nesi huyo akashtuka! Akauliza,, “Tobi ni nani?
Roda akazidi kuchanganyikiwa.. akasema kama wewe sio Tobi ni nani? Na umejuaje haya yote?
Wati huo huo,,upande mwingine alionekana Tobi na mama yake wakijitokeza kwenye nyumba ya yulez mume na mke waliomsaidia Roda kumpeleka hospitali!
Wakawakuta wanandoa hao wamejilaza chumbani wamepumzika! Tobi akaingia kwenye kiwiliwili cha mwanaume huyo huyo,, na Malkia wa bahari akaingia kwenye kiwilwili cha yule mwanamke…
Pumde si punde wakashyuka kutoka usingizini kwa wakati mmoja,, wakawa na wazo la kwenda kumtembelea Roda ke nyumbani kwake!
Bila kuchelewa wakajiandaa na kuingia ndani ya gari,, safari ya kwenda nyumbani kwa Roda ikaanza!
Walipofika wakaingia wakashuka kutoka ndani ya gari na kugonga mlango wa Roda.
Wakati huo Roda alikuwa anamsimulia nesi kila kitu kilichompata.. Roda akashtuka kusikia mlqngo unagongwa akajisemea moyoni,, “ni nani huyo anayegonga mlango?
ITAENDELEA
 
Bahari ya Hindi
Sehemu ya 16
Kule nje Malkia wa bahari akaanza kuhisi hali ya hatari,, akasema,, “bila shaka sehemu hii kunaadui yetu!
Pia Tobi akahisi harufu hiyo ya hatari… wakatoweka kimiujiza kutoka kwenye miili ya wana ndoa hao wawili!
Punde si punde wanandoa hao wakajishangaa, kujikuta hapo!
Wakaangaza angaza macho yao wakaliona gari lao! Mwanamke huyo akamuuliza mumewe,, “tumefikaje hapa? Mbonw kila nikivuta kumbukumbu sikumbuki kitu,, zadi ya kukumbuka kuwa tulikuwa nyumbani tumelala.
Punde si punde Roda akafungua mlango,, akashtuka kuwaona watu hao.. kisha akasema,, “karibuni.
Wanandoa hao wakatazamana usoni hawakuongea neno lolote wakaondoka zao na kuingia ndani ya gari kurudi nyumbani! Huku wakiwa wametawaliwa na hofu kupita kiasi!
Malkia wa bahari pamoja na Tobi wakajitokeza kwenye ufukwe wa bahari!
Pia jua lilikuwa tayari limeanza kuzama hivyo mpango wao ukashindikana.. wakatoweka kimiujiza kurudi ujinini kule chini ya bahari!
/
Wakati huo huo kule nyumbani kwa Roda alionekana bado akiendelea kumsimulia,, yule nesi mkasa wote uliompata.. nesi huyo akamuonea huruma sana,, kisha akasema hili ni tatizo usipokuwa makini utampoteza mtoto,, kwa sababu ni lazima waje kumchukua mtoto wao!
Kisha nesi huyo akanyanyuka na kumuaga Roda,, akamrudishia mtoto wake!
Roda hakuwa na kipingamizi,, akaongozana na nesi huyo mpaka nje ya nyumba..nesi akaondoka zake Roda akaelekea kanisani kwa mchungaji… kwa bahati nzuri akamkuta mchungaji,, anatoka kwenye ofisi iliyokando ya kanisa lake.
Roda akamsalimia mchungaji,, kisha akasimulia mkasa mzima..
Bila kuchelewa mchungaji akasema,,” tuingie kanisani,, wakaongozana mpaka ndani ya kanisa,, Mchungaji akasema,, “mlaze mtoto huyo hapo juu ya meza.. nianze maombi.
Roda akafanya kama alivyoagizwa na mchungaji, akamlaza mtoto pale juu ya meza.
Mchungaji akaanza kufanya maombi……akiwa katikati ya maombi.. mtoto akaanza kulia kwa sauti kali kupita kiasi akaanza kubadilika na kuwa mtoto wa kutisha… punde si punde ukatoka mwanga mkali ndani ya mwili wa mtoto huyo… akarudi katika umbile lake la kawaida.. mchungaji akaendelea kufanya maombi kwa imani kali nila kusita.
Na baada ya dakika kadhaa kupita mchungaji akahitimisha kwa kusema,, “Amen.
Mtoto akanyamaza,, kisha mchungaji akasema,, “sasa waweza kwenda lakininusisahau kusali mara kwa mara,, usisahau kumkumbuka Mungu wako!.
Wakati huo Roda alikuwa kabaki mdomo wazi juku macho yamemtoka akimtazama mtoto wake,, yani alikuwa aamini kile alichokishuhudia… mchungaji akasema,, “ondoa shaka Mungu yu pamoja nawe,, ukimuamini na kumtumikia yeye atakulinda kwa kila jambo..kisha mchungaji akazipiga hatua akachukua biblia moja na kumkabidhi Roda huku akisema,, “mara kwa mara jifunze kusoma maandiko ya kwenye biblia…..utajifunza mabo mengi ya kumtumainia Mungu muumba.
Roda akaipokea biblia hiyo kisha akamchukua mwanae.. na kuondoka zake kurudi nyumbani!
**************************************
Upande mwingine kule ujinini, alionekana,, Malkia wa bahari pamoja na Tobi…
Malkia wabahari akasema kwa lugha ya kijini akimaanisha,, “ tumechelewa na jua limeshazama! Kule duniani usiku umeanza kuingia ambavyo huku kwetu ndio panaanza kukucha,, hivyo tutaifanya kazi hii kesho,,
Kama ilivyo kawaida viumbe wa kuzimu,, wanaishi tofauti na maisha ya binadamu!
Huku duniani,,nyakati za mchana,, lakini huko kuzimu ni usiku wa manane..
Na huko kuzimu nyakati za mchana,,,, huku duniani ni nyakati za usiku wa manane..
Kesho yake mipango ukaendelea wakajipanga kwenda duniani kumchukua mtoto wa Roda wampeleke ujinini.
Kule nyumbani kwa Roda alionekana yupo sebuleni akiwa anasali kwa imani huku kashikilia biblia.. alipomaliza akaingia jikoni kuandaa chakula wakati huo mtoto alikwa kalala usingizi juu ya sofa.
Punde si punde Tobi na Mama yake(Malkia wa bahari akasema wakajitokeza ndani ya nyumba ya Roda upande wa sebuleni,, wakastaajabu kumuona mtoto haonekani kuwa na chembechembe zozote za ujini! Malkia wa bahari akasema bila shaka hapa kunajambo limetendeka! Haiwezekani iwe hivi.. punde si punde mtoto akashtuka kutoka usingizini akaanza kulia,, Roda akatoka jikoni haraka kuelekea sebuleni.
Akashtuka kumuona Tobi pamoja na Mwanamke mzee sana ambaye ndiye
Mama Tobi(Malkia wa bahari) Roda akakumbuka maneno ya mchungaji,, kuwa afanye maombi kwa imani mara kwa mara,
Bila kuchelewa Roda akaanza kusali huku akikemea kwa imani.. Tobi na Malkia wa bahari wakaanza kuhisi wanaunguzwa na moto mkali,, walipojaribu kutoweka kimiujiza ikashindikana.. wakaanza kupiga kelele za maumivu makali!
Roda akaendelea kusali bila kusita.. punde si punde wakaanza kuwaka moto.. hatimae wakateketea kabisa na kubaki majivu… ikawa ndio mwisho wa Tobi ma Malkia wa bahari.
Roda,,akamchukua mwanae haraka akambeba.. kisha akaichukua biblia na kuikumbatia.
Akaamua kufanya mpango wa kuhama ndani ya nyumba hiyo siku hiyohiyo.. akahamia Temeke,,
Siku zilizidi kusonga,, Roda hakuona mauzauza tena.. akaishi kwa amani na furahmiaka ikazidi kusonga hatimae mtoto akatimiza umri wa miaka kumi na nane(18) binti huyo anaitwa
SIMA. /
Roda akashindwa kuvumilia kuificha siri kwa mwanae.. kwa sababu kila kukicha binti huyo alimuuliza mama yake kuwa baba yake mzazi yuko wapi… Roda akamsimulia mkasa wote… binti huyo akastaajabu sana,, lakini akajipa moyo kwa kumtumainia Mungu… huku akijisemea moyoni,, “Mungu ndiye muweza wa yote,, amenileta duniani kwa namna hii,, MUNGU ndiye baba yangu pekee.
Maisha yaliendelea,,wakaishi kwa amani na furaha.
******************MWISHO******************
 
Back
Top Bottom