SIMULIZI: “ANGAMIZO” (13)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email:
xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
---------------------------------------------------------
Rose alikuwa karibu mno na kipenzi chake, alimfuta machozi na kumpa maji anywe. Abdul alionekana kutia huruma kweli. Nilitamani kumwachisha kuadithia simulizi yake lakini haikuwa hivyo, bado alikuwa na mengi ya kusimulia. Wapi alimpoteza dada yake?!, kwanini alipata upofu na Baba yake mdogo yupo wapi kwa sasa!. Bado nikabaki ya shauku ya kuendelea kusikiliza na kuandika baadhi ya vitu.
“Naakika simulizi hii itavuka mipaka ya kimataifa. Haki ya Abdul kupata kila kilicho chake lazima kitimie. Nitamsaidia kupamba simulizi hii kwa kila aina ya mapambio, ifike kila kona Duniani., Nahakika!” nilijiongelea kimoyo moyo kwa kujipa nguvu na imani kuwa hipo siku Abdul atapata haki yake. Kweli nilizamilia….
ENDELEA SEHEMU YA KUMI NA TATU…..
“Rose!” Nikaita
“Ah! Abee” Rose ambaye ndiye mpenzi wa Abdul aliitika akionesha aibu.
“Kila kitu kitakuwa sawa, usijali” Nilimtia moyo.
“Haaah!, Labda! Kwani nashangaa kwanini Mume wangu amewaamini sana nyinyi. Mana katu hakuwai kumwamini mtu zaidi ya mke wake!, na sijawai kujua wala kusikia hiki asimuliacho” Rosea aliongea kwa aibu akifuta machozi. Maneno yake yakanifanya japo nitabasamu.
“Kweli wanapendana!” Nilijisemea tena kimoyomoyo.
Nikaongea na Rose mawili matatu, tukiwa tunatuliza munkari ya Adbul na kusubiri chakula.
Rose alisimulia siku aliyomuona Abdul, alisema walikutana njiani, alimwona Abdul akipata tabu kuvuka njia iliyosheheni magari. Akamsaidia hadi kuvuka na kutokea upande wa pili. Wakaachana.
Akasema akaja kumsaidia tena siku nyingine ambapo alikua anashida na chakula. Kipindi hicho alikuwa muhudumu wa muda kwa Mama ntilie. Toka siku hiyo akampenda mno Abdul na kuanza kumfatilia hadi wakaingia katika mahusiano baada ya kuzoeana. Akuendelea kuelezea tukio hilo japo nilimwona machoni kabisa kuna baadhi ya matukio anaruka au anaficha kwa kutaka kutoyasema. Kwa maana hadi kuishi na mtu kama Abdul basi kuna mengi sana mnapitia.
Tuliendelea na maongezi ya kujuana vizuri kati yetu kujenga usahihi wa taarifa, tukiwa tunasubiri chakula. Niliwaza sana chakula kinaweza kuwa kibichi kutokana na mke wangu kukosa kabisa hata chembe ya furaha. Uso wake ulijaa simulizi nzima ya Abdul.
Mke wangu alikuwa mwepesi sana katika kupoteza furaha, hasa akimuona mtu karibu yake hana furaha. Nililiona hilo, nikanyanyuka na kwenda japo kumpoteza katika mawazo yake. Baada ya muda kila kitu kikawa sawa. Na maakuli yakawa mezani.
Meza nzima ilikuwa kimya sana kila mtu akitegea kula. Kila upande ulikuwa na mawazo sana na kuwaza nani ataanzisha maongezi. Kwasababu mimi nilikuwa mwenyeji nikataka kuanzisha neno. Lakini ghafla nikawahiwa
“Hahahahaha haha!” kilisikika kicheko cha Abdul na kufanya meza nzima kuacha kula na kumshangaa. Kabla hajaulizwa kwa nini anacheka, akajibu kwa ufasaha.
“Daa!, chakula hiki na mboga kama hii ndicho kilikuwa chakula amabacho anakipenda sana mdogo wangu... Maria! Popote ulipo uje hapa kula na kaka yako.!” Akaongea akiwa na mwingi wa tabasamu na kutuacha wote tukiwa vinywa wazi.
“Mhhh! Huyo Maria atakuwa anakusikia kweli?, na je akija hapa utamuona?! Au kumjua??” Mke wangu akamtwanga swali ambalo wote pale tukaweka vijiko chini kusubiri jibu. Tulijua kabisa swali lile ni ngumu kupatikana kwa jibu fasaha. Lakini lilikuwa rahisi kwa Abdul.
“Sautiii… hapana sikumbuki!, Suraa…. Yah! Sura nakumbuka ila sitaiona sababu siwezi kuona kabisa…, hata nikimshika, siwezi kumfahamu, nilimpoteza mda sana. Wakati sina hisia juu yake. Laiti angepotea wakati nimepoteza uwezo wa kuona aaagh! Ningemjua bhana.!! na hawezi kuja hapa. Amekufa Maria!. Amekufa” Abdul akatamka neno zito ambalo lilifanya kupindua meza ya chakula na kila mmoja kubaki na huzuni ya aina yake.
Lakini kwa Abdul ilikuwa poa tu. Alitabasamu na kuweka vijiko viwili vya chakula mdomoni. Akaangaza meza nzima utazani alikuwa anatuona kila mtu wapi amekaa. Alikuwa na hisia sana Abdul. Baada ya kuzungusha kichwa meza nzima, Abdul alimwita kila mmoja akianza na upande wa kushoto alipokaa mke wake. Alipatia kila mtu na sehemu aliyokaa. Abdul alikuwa mchawi kwa kweli.
“Rose mke wangu. Ndugu mwandishi. Shemeji!... Hisia ni kitu muhimu sana katika maisha. Angali ningeishi maisha ya kutafutwa na kuangamizwa kama wanavyofanya, na hayahaya macho yangu mabovu!. Basi hakika ningekuwa mtu mmoja mkubwa sana hapa nchini. Nina uwezo mkubwa sana wa kuishi kwa hisia” Abdul alimaliza maneno hayo na kuonyesha ishara kusogeza vyombo kuwa ametosheka. Baada ya hapo akendelea.
“Ahsante Shemeji yangu!. Ahsante kwa chakula kilicho….. kilicho nikumbusha enzi hizo. Enzi amabazo tulikuwa tukigombana sana na mdogo wangu kuhusu vipimo vya chakula hicho. Kila mtu alitaka kuwa kinara kula wali mwingi.” Abdul aliongea huku akitoka mezani taratibu na kwenda sehemu ileile alipokaa mwanzo.
Mimi na mke wangu tulishangaa sana. Amewezaje!?. Tukaangaliana kwa maswali bila majibu. Hakika Abdul alikuwa kama mchawi, huwezi amani kama alikuwa ni kipofu!. ‘Hakika Hujafa, hujapatwa na mengi!’ alikaa tayari kuendelea na simulizi. Tuliokuwa mezani wote tukamaliza kwa hamu ya kujua nini kiliendelea. Moyoni nilijiandaa kupokea tena simulizi ya huzuni. Baada ya kumaliza kila kitu Abdul akaendelea pale alipoishia…
-----------------
“Nilipozimia, nilizinduka na kukuta nipo katika hali ya kiza. Niliangaza huku na huko na kumwona mdogo wangu Maria akiwa pembeni yangu huku chozi likimtoka.
“Kaka!!. Amka. Amka tuondoke hapa. Si sehemu salama..” Maria alisisitiza huku mikono yake ikiniinua mimi pale nilipo.
“Hapa wapi?” Niliuliza pasipo chukua hatua yoyote juu ya kile nilichoambiwa.
“Tupo stoo, wametuweka humu kaka, tuondokeee aagh!, mimi naogopa” akasisitiza tena.
“Mama?” Wala sikuwa mchoyo wa maswali, nikamuuliza swali lingine.
“Mamaaa!, Wameua!, Mama amekufa kaka!!! Kaka mamaa!. Nimeona kabisa wamembeba na kwenda kumtupa. niliwasikia.. kaka tukimbie jamani, naogopa!” Kilio cha Maria kikaongezeka na kuingia haswaa katika ubongo wangu. Chozi lilinitoka na mimi.
Nikakumbuka tukio la mwisho kulipata kabla sijazimia, nakumbuka niliwaona tu wanaume wakiongozana kuingia katika chumba cha Mama yangu. Waliingia kumtendea umyama Mama yangu. Baadae wakamuua!. Walimpiga risasi. Hasira zikanishika sawasawa, lakini sikuwa na chakufanya. Nikanyanyuka kwa nguvu na kuelekea mlango ulipo kwani licha kuwa na giza bado mwanga ulionyesha vyema mlango.
Kitu kilichotusaidia ni kuwa, milango yetu ilikuwa na ufunguo wa ndani. Mtu akiwa ndani ata kama akifungiwa kwa nje basi anaweza toka bila wasiwasi. Kulikuwa na kitasa kwa ndani ambacho hakikutupa shida kufungua, nikafungua taratibu kwa kuchungulia nje.
“Kwanini hukufungua mapema?” Nilihoji huku nikichungulia nje kuona kama usalama upo au la!.
“Na wewe eh!. tutoke bhana, swali gani hilo?. Eti nifungue?, nitoke si ndio? Peke yangu eh?, wakati robo saa nzima nakuamsha upo kama umekufa hapa chini!. Khaa!!, Fungua!! Bhaana aaagh!” Muda huo Maria alikuwa mkali sijawai kuona. Nilimwangalia kwa aibu kwani kweli nilikua nimezimia. Roho yake nzuri tu ndio ilifanya iniamshe na kunisubiri la si hivyo angeniacha niuliwe na mimi mle ndani.
“Twendee..” Nilimwita mdogo wangu kwa sauti ya upole mara baada ya kuchungulia nje na kuona kupo kimya.
Nilimwita tayari kwa kuondoka. Tulikuwa tayari kwa kutoroka nyumba hile. Lakini kwa jinsi alivyo nyanyuka mdogo wangu Maria. Ikanipa shaka zito moyoni. Alinyanyuka kinyonge sana kwa kujishika mapaja yake mkono mmoja, na mwingine kushika ukuta, huku nikisikia baadhi ya miguno ya maumivu ikimtoka, nikahisi jambo. Haraka nikaenda kumnyanyua na kumsaidia kutoka mahali pale. Alionyesha anamaumivu mazito mwilini kwani alishindwa tembea kwa ufasaha.
“Wamembaka!” Nilijikuta natamka neno hilo moyoni huku nikijaribu kuzuia hisia zangu zisionekane kabisa kama nimejua. Maana baada ya kumshika tu, mkono wangu uligusa damu kadhaa ambazo zilianza kukauka katika mapaja ya dada yangu Maria. Nikakaza roho na kumwongoza dada yangu kutoka eneo lile. Hata yeye Maria hakutaka kuonyesha kabisa kama kuna kitu kibaya kimempata. Alijitahidi kukaza miguu kuonesha yupo sawa lakini hapana. Ni jasiri dada yangu. Anaroho kama ya Baba yake. Akaficha maovu kifuani….
ITAENDELEA
Sent using
Jamii Forums mobile app