Simuelewi shemeji yangu huyu

Someni yaliyomsibu huyu dada....
"Mimi ni dada mwenye miaka 28,nimeolewa na nina mtoto mmoja,tunakaa nyumba ya kupanga na husband+mdogo wake wa kiume mwenye miaka 23.
Kuna siku niligundua kuwa picha zangu nyingi zimepotea,pamoja na kuuliza sikupata jibu lolote,jumamosi iliyopita niliingia bafuni kuoga baada ya yule shemeji yangu kutoka kuoga (tunashea bafu/choo) kilichonishangaza nilikuta picha zangu mbili kule bafuni sikuelewa zimefikaje na ni kati ya zile zilizopotea,nilipomuuliza hakuwa na la kujibu nikamwambia nitamwambia kaka yake,akaomba sana msamaha na kurudisha zile picha akasema hana nyingine.,leo asubuhi nimeingia chumbani kwake nikakuta kabandika picha 2 pembeni ya kitanda chake.,nishaurini nimfanyaje huyu kijana?"
Angalia asije akakubaka, manake ndio vinaanzia huko huko. Ningekua miye ningemwambia kaka yake siku nyiingi.
 
Kwani inawezekana hajamwambia mumewe hadi sasa? Kwanini sasa?
Huwa sielewi sana linapokuja swala la kuchagua vitu vya kumwambia mumeo au mkeo, mi nadhani mkishaoana ni sharti muambiane kila kitu, tena mnakuwa marafiki tu. Ni shida sana dada anawaambia baadhi ya marafiki zake vitu fulani na anamficha mumewe tena kwa visingizio vidogo tu (Nitawagombanisha na mdogo wake bure! au anaweza asinielewe!) Huyo ni mkeo au mumeo, mwambie kila kitu kuepusha kutoaminika, maana kama kuna kitu kimetokea alafu hukusema na akaja kugundua mwenyewe unapoteza kabisa uaminifu japo si kosa lako na pia muelezee kila kitu ili kumfanya awe karibu zaidi na maisha yako!

well said mkuu
 
Back
Top Bottom