Simuelewi mpenzi wangu

Simuelewi mpenzi wangu

nusfati

Member
Joined
Aug 28, 2013
Posts
40
Reaction score
8
Nina mpenzi tupo kwenye mahusiano yapata miaka 3 , anaishi Zanzibar me Dar, amebadilika mno tangu January ndo tulionana toka hapo nikimwambia njoo Dar Mara kazi nyingi, Mara sina nauli,Mara nasubiri likizo , ukiomba Pesa anasema atatuma ila ndo mtolee hiyo ,me nimechoka sielewi nifanyeje ,ukimpigia simu anasema yupo usingizini tutaongea kesho, akikuta call anitafuti mpaka nimtafute ,jamani naomba ushauri wenu wanaJF.
 
Nina mpnz tupo kwenye mahusiano yapata miaka 3 , anaishi Znz me dar, amebadilika mno tangu January ndo tulionana toka hapo nikimwambia njoo dar Mara kazi nyingi, Mara sina nauli,Mara nasubir likizo , ukiomba Pesa anasema atatuma ila ndo mtolee hiyo ,me nimechoka sielewi nifanyeje ,ukimpigia cm anasema yupo usingizin tutaongea kesho, akikuta call anitafuti mpaka nimtafute ,jamani naomba ushauri wenu wanajf

lakini hii si tetesi
 
pole sana nusfati,ili kutatua tatizo hilo inabidi mazungumzo ya kina yafanyike mpigie simu mwenza wako muongee vizuri
 
Kakumwaga kiutu uzima huyo, wahenga walisema, "akufukuzaye, hakwambii toka". Kama ulishampa papuchi ndo imetoka hiyo, ikirudi pancha.
Cha kufanya na wewe jikaushe kimya usimtafute wala kumpigia simu na uendelee na mambo yako. Pole sana mdada ndo ukubwa huo.
 
Poleee ashasepa tena huyo keshajipatia katoto ka darajani kabiiichiiii we wazamani kwishney!! Mweeh! Jitulize zako tu ka anakupenda atakuja!!
 
Sina tabia ya kuomba omba Pesa ,naomba nikiwa nikiwa sina na nina shida ya ukweli na sio Pesa nyingi
 
Kama hana hata nauli ya kuja kukuona, mkianzisha familia ataweza kuihandle?hakutaki huo mteme tu.
 
Nina mpnz tupo kwenye mahusiano yapata miaka 3 , anaishi Znz me dar, amebadilika mno tangu January ndo tulionana toka hapo nikimwambia njoo dar Mara kazi nyingi, Mara sina nauli,Mara nasubir likizo , ukiomba Pesa anasema atatuma ila ndo mtolee hiyo ,me nimechoka sielewi nifanyeje ,ukimpigia cm anasema yupo usingizin tutaongea kesho, akikuta call anitafuti mpaka nimtafute ,jamani naomba ushauri wenu wanajf

hayo yote ni manyoya! kama unahangaika kumtafuta kuku wako wakat manyoya yanayoonekana ni rangi ileile ya kuku wako endelea! ukimpata hai tuambie
 
ushaachwa ndugu au unasubiri akutamkie!!!! basi muanze wewe kwa kujipa moyo tu kwani kiuhalisia ameanza yeye kukubwaga kivitendo
 
Back
Top Bottom