Simuelewi kabisa huyu mwanamke

Mbepo yamba

JF-Expert Member
Aug 5, 2012
1,110
1,475
Ndugu zangu, niko kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa na msichana ambaye nimempenda kweli kweli. Plan yangu ni kumfanya mke wangu wakati wowote kuanzia sasa. Tumeshirikiana mambo mengi tuu.

Tatizo lipo hapa. Ni mwanamke anayenificha mengi sana. Yaani ni mtu ambaye hata picha tuu akinitumia WhatsApp huwa anaifuta hapo hapo.

Tofauti na mimi ninayemueleza karibu kila ratiba yangu, yeye ni mara chache sana kuniambia. Naweza kumuuliza kuhusu ratiba na akawa ananipa majibu ya juu juu na ya kunikatisha tamaa tuu.

Na ndio yuko hivi kwenye mambo mengi. Hayuko wazi kabisa kwangu.

Suala hili linanipa wakati mgumu sana kuendelea mbele na mchakato wa ndoa. Je, inawezekana yeye ana plan nyingine?

Msaada wenu jamani ili ama niokoe penzi hili au nigeukie ustaarabu mwingine.
 
Usiri ni tabia ya mtu... ISHU HAPO NI KWAKO, YEYE ANAKUPENDA AU MCHEPUKO? Ukishindwa piga mimba JEURI YOTE ITAKATA.

Lakini muhimu sana kwenye mahusiano wengi tunakuwa hatuendani kitabia hivyo lazima ujifunze mrengo wake nae ajifunze kwako.. usitake aishi kama unavyotaka wakati ww hupendi kuishi anavyotaka pia.. balance it...

love ni just balance katika upendo na kujaliana sio amri.. nimeachana na wanawake wengi kwa uzembe kama huu.. wengi wa hawa wanawake wanapenda mtu anayeweza angalau kuishi kwa namna fulani vile wanavyopenda..

Miaka miwili bado umeshindwa kumzoea uje ulalamike leo.. How stupid you are... Tuwapende na tuishi nao kwa akili.
 
Umejaribu kumweleza unavyokereka na kukosa Amani juu ya hayo afanyayo?
Naona ni vitu vidogo sana vinarekebishika.
Mweke chini umwambie, kama anakupenda atajirekebisha/atajaribu.
Yes. Nimemueleza mara nyingi tuu. Anakuwa kama anaelewa halafu anarudia yaleyale baada ya muda
 
Kama anarudia yale yale basi jaribu kubadilika ww ishi kama anavyoishi yeye kama haoneshi kujali na ww onesha kutojali, asipokwambia mambo yake usimwambie yako, huenda hii hali ikamfanya ajirudi
 
Niliambiwa na mtu kuwa "asiyekushirikisha matarajio yake bhasi uwezekano mkubwa ni hakuoni katika future yake, asiyekushirikisha maumivu yake bhasi haupo moyoni mwake"..

Mkuu nimesoma between lines na inaonesha umeshaelewa mchezo mzima ila unasubiri watu wakupe ujasiri tu. Jiamini
 
Niliambiwa na mtu kuwa "asiyekushirikisha matarajio yake bhasi uwezekano mkubwa ni hakuoni katika future yake, asiyekushirikisha maumivu yake bhasi haupo moyoni mwake"..

Mkuu nimesoma between lines na inaonesha umeshaelewa mchezo mzima ila unasubiri watu wakupe ujasiri tu. Jiamini
Hakika. Uko sawa kabisa
 
Kwanini mkuu una invest sehemu unayoona kabisa haitakupa faida ?
Kama unajua hupati upendo ukiendelea kumng'ang'ania utakuja pata maumivu makali sana.
Nilitazamia kuvuna upendo kwa kuwekeza upendo. Ila nayaona maji yanaleta mazoea kuvuka shingo
 
Kama anarudia yale yale basi jaribu kubadilika ww ishi kama anavyoishi yeye kama haoneshi kujali na ww onesha kutojali, asipokwambia mambo yake usimwambie yako, huenda hii hali ikamfanya ajirudi
Hii inaanza with immediate effect huku nikielekea maamuzi magumu
 
Uyo akupendi akipata mtu sahihi kwake anakuacha usimpe 100%
Lakini pia jaribu kumwambia hayo matabia yake huyapendi inaweza saidia
 
Back
Top Bottom