Simuelewi kabisa huyu mwanamke

Mtu kama hujamuingia moyoni hawezi kukujali hata kidogo. Licha ya kujali wala hawezi jistukia kwa lolote hata kama linakukera kuna ile hali mtu anachukulia poa maana haimgusi.
 
Huyo ana two competitive bonds zina fighting kuwa muwazi mtashtukia.
Unaweza fanya yafuatayo
1. Mtolee hata posa tu ili ndugu wajue
2. Weka msimamo wa maamuzi yako
3. Wekeni mipango ya pamoja kwaajili ya maandalizi ya kujenga familia. Mfano fungueni joint account mnaanza kutunza hela for future
4. Mfanye kila hatua ya maendeleo yenu ashiriki.
6. Msisitize uwazi ndo msingi wa mahusiano na ndoa.

Ukiona anagomea hayo ujue huyo hana nia na wewe kuna mtu kamshika mapembe. Ila siku atakuja kumwagwa na atakukumbuka.

Mwambie kabisa unampenda sana ila siku kuirudisha moyo nyuma asije laumu.
Ndugu zangu, niko kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa na msichana ambaye nimempenda kweli kweli. Plan yangu ni kumfanya mke wangu wakati wowote kuanzia sasa. Tumeshirikiana mambo mengi tuu.

Tatizo lipo hapa. Ni mwanamke anayenificha mengi sana. Yaani ni mtu ambaye hata picha tuu akinitumia WhatsApp huwa anaifuta hapo hapo.

Tofauti na mimi ninayemueleza karibu kila ratiba yangu, yeye ni mara chache sana kuniambia. Naweza kumuuliza kuhusu ratiba na akawa ananipa majibu ya juu juu na ya kunikatisha tamaa tuu.

Na ndo yuko hivi kwenye mambo mengi. Hayuko wazi kabisa kwangu.

Suala hili linanipa wakati mgumu sana kuendelea mbele na mchakato wa ndoa. Je, inawezekana yeye ana plan nyingine?

Msaada wenu jamani ili ama niokoe penzi hili au nigeukie ustaarabu mwingine.
 
Huyo ana two competitive bonds zina fighting kuwa muwazi mtashtukia.
Unaweza fanya yafuatayo
1. Mtolee hata posa tu ili ndugu wajue
2. Weka msimamo wa maamuzi yako
3. Wekeni mipango ya pamoja kwaajili ya maandalizi ya kujenga familia. Mfano fungueni joint account mnaanza kutunza hela for future
4. Mfanye kila hatua ya maendeleo yenu ashiriki.
6. Msisitize uwazi ndo msingi wa mahusiano na ndoa.

Ukiona anagomea hayo ujue huyo hana nia na wewe kuna mtu kamshika mapembe. Ila siku atakuja kumwagwa na atakukumbuka.

Mwambie kabisa unampenda sana ila siku kuirudisha moyo nyuma asije laumu.
Asante mkuu. Bahati nzuri kwa kweli tumefungua joint saving account. Hili la posa ngoja nijitahidi kulifanya ila kwa akili maana neno nakupenda limekuwa wimbo kwake
 
Huyo bado hajawa tayar, yuko mguu ndani mguu nje kwako.

Huenda kuna mtu wake wanaependana zaidi ila kwako n kama vile amajiegesha tu, akiona limebuma kule bas anakuja mazima kwako.

Jipe mda utayajua tu yanayosababisha, usimuache wala usimuoe kwa sasa endelea kumchunguza.
 
Nimesoma kwa makini huu uzi wako na nikasoma baadhi ya reply zako hapa,Nilicho gundua ni kuwa huyo demu hakupendi ila wew una tumia nguvu nyingi ili akupende,Wanawake ni viumbe wepesi kuwa wawazi kwenye mambo yao mengi hasa kumweleza mpenzi wake,Unapo ona ni msiri kwako ujue hana future na wewe,maybe ana mtu tayari ambaye anamweleza mambo yake au anamtafuta so jiandae kisaikolojia mkuu.
 
Huyo ni mwanamke tatizo unataka awe na tabia za kiume wakati sio jinsia yake kikubwa nikwamba anakupenda ila hataki kuwa cheap sana
 
Haitaji akili kujua huyu manzi hakupendi

Dawa ya moto ni moto

Kuwa kama yeye kuwa msiri mjibu jujuu huku ukitafuta kifaa kipya asipoelewa piga chini akielewa hapo sawa
 
Ananiuma maana nampenda sana mkuu
Tafuta mwanamke anayeweza kukidhi matarajio yako, usimlazimishe huyo huenda sio wako ama mko wengi mmpangwa foleni, kuna vitu sio vya kulazimisha,
Kosa lako, Unawezaje kukaa na msichana kwa mahusiano kwa miaka miwili ?, unajya hilo linaweza kuwa linamkwaza na yeye ?,miaka miwili unasubiri nini ? hata kama unajidai unamchunguza, usitemee unaweza kumfahamu mwanamke kiundani,
kama umedhamiria kumuoa fanya Ufunge nae ndoa inaweza kumsaidia akawa wazi kwako, kumkalisha miaka miwili anasubiri kuolewa inapelekea hata yeye asikuamini, ndio maana anashindwa kuwa open kwako, wanawake huwa hawapendi kufanyiwa maigizo/usanii, mpe heshima yake na familia yake then uone, utakuja kuleta feedback hapa Jf
 
Niliambiwa na mtu kuwa "asiyekushirikisha matarajio yake bhasi uwezekano mkubwa ni hakuoni katika future yake, asiyekushirikisha maumivu yake bhasi haupo moyoni mwake"..

Mkuu nimesoma between lines na inaonesha umeshaelewa mchezo mzima ila unasubiri watu wakupe ujasiri tu. Jiamini
Mimi natamani wanawake ndio wachangie zaidi hapa ili watuambie huwa hawataki nini na ama huwa wanataka nini, wanaume mkichangia hapa itaonekana kama tunachochora, mtoa mada amesema haelewi afanye nini, sasa bidadas ndio waweza kusema ukweli kwani naamini tatizo hilo sio lake peke yake linawasumbua wengi na wanaweza kusaidiwa hapa.
 
Nashukuru sana kwa michango yote. Kuna kitu nimekipata na kimenijenga. Nimeyaona makosa yangu na sasa nimepata nguvu.
 
Kuna watu wengine hua sio wa kujielezea elezea na sio wawazi..mfano mimi ninaweza kua naongea vitu lakini asilimia kubwa unajikuta unajielezea wewe mwenyewe lakini mimi sijielezi..nakumbuka wasichana kadhaa wameshawahi niambie "sasa mbona wewe hauniambii vitu kuhusu wewe na familia yako" maana sijui kitu chochote kile enh? Nawauliza unataka kujua nini...?
 
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Ukiona umeanza kutomuelewe mwanamke ujue ndio umeanza kumuelewa hivyo.

Wanawake huwa hawaeleweki mkuu.
 
Hakupendi huyo, unampenda wewe ila yey hakupendi (huo ndyo ukweli), utake usitake, yupo mtu anayempenda na huenda ana wanaume weng,,
Onyo: usioe mwanamke unayempenda wew kuliko yey anavyokupenda
 
Mtengeneze utakavyo ukiona haelekei pokea mapungufu yake Kama yako..

Hilo tatizo la ratiba hata Mimi ninalo..kidogo kidogo naelekea.
 
Ndio maana wenzangu wengi huwa nawashauri kuwa na msichana anaekupenda WEWE zaidi, awe tu na vigezo ambavyo wewe unaona vinakufaa, utajifunza kumpenda baadae. Ikiwa vice-versa kusema kweli dada zetu hawa wanaweza kukupasua kichwa.

Msichana akikupenda kwel kwel, wewe unakua best friend wake, uwe tu una maintain good balance ya upendo, happy and bad moments. Yani atakuambia vitu vyengine hata hukuulizia.

Huyo dada pengine anakupenda lakini ndo alivyo, au anakuzingua, au anaona wewe unamzingua. Kwakua umeshindwa kujua lipi ni lipi. Maamuzi magumu nakupa, mwambie kuwa unaona kama umuelewi elewi na japo kuwa umeshamuambia mara nyingi bado ni vile vile, halaf yeye ni mtu una malengo nae, inakunyima raha na kukupa msongo wa mawazo. Let's take a break ili tutathimini mapenzi yetu n.k.

Komaa, maana hyo stage sio rahisi. Kama kweli anakupenda, upendo wa kweli wa mwanamke ni kitu cha ajabu sana, unaweza ukapotelea sehemu hata 3yrs lakini ukirudi kwake bado atakupenda. Naongelea upendo wa kwel sio wa kununulika.

Hapo mganga ni muda tu ndo utasema ukweli. Kama kweli anakupenda atarudi tu kwako. Ila this time she'll be different, perhaps ataopen up to you kwa kuona uko serious nae kimtindo.

Za kuambiwa changanya na zako.
 
Ndugu zangu, niko kwenye mahusiano kwa muda wa miaka miwili sasa na msichana ambaye nimempenda kweli kweli. Plan yangu ni kumfanya mke wangu wakati wowote kuanzia sasa. Tumeshirikiana mambo mengi tuu.

Tatizo lipo hapa. Ni mwanamke anayenificha mengi sana. Yaani ni mtu ambaye hata picha tuu akinitumia WhatsApp huwa anaifuta hapo hapo.

Tofauti na mimi ninayemueleza karibu kila ratiba yangu, yeye ni mara chache sana kuniambia. Naweza kumuuliza kuhusu ratiba na akawa ananipa majibu ya juu juu na ya kunikatisha tamaa tuu.

Na ndio yuko hivi kwenye mambo mengi. Hayuko wazi kabisa kwangu.

Suala hili linanipa wakati mgumu sana kuendelea mbele na mchakato wa ndoa. Je, inawezekana yeye ana plan nyingine?

Msaada wenu jamani ili ama niokoe penzi hili au nigeukie ustaarabu mwingine.
Sasa unakaa na mwanamke miaka miwili bado hata mwelekeo wa kumuoa hamna unategemea nini sasa
 
Back
Top Bottom