Simuelewi jirani yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simuelewi jirani yangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sinafungu, Apr 16, 2011.

 1. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  anaishi na mwanamke miaka kumi sasa, wamejaaliwa kuzaa watoto 2, mume ana watoto zaidi ya 5 kabla ya kuishi na mwanamke huyo. hivi karibuni kumekuwepo kutoelewana baina yake na mwenzake, mwanamke anafanya jitihada wafunge ndoa jamaa anadai hana uwezo kwa sasa, jitihada za mwanamke zimepelekea hadi ndoa kutangazwa kanisani , jamaa baada ya kuona hivyo alimfuata padri akamfokea sana, siku mbili baadaye ndo akaja kwangu kunipa short stori na akanitaka tuende naye kwa kaka wa mkewe kwa malengo ya kuulizia mahali na utaratibu mzima .( LAKINI AKITAFUTA NJIA YA KUKWAMISHA JITIHADA ZA MKEWE) mimim nikamuuliza kwani tatizo ninini akaniambia yule mwenza wake hawapendi watoto wake hivi hajamuoa, na kishawafukuza ndg kadhaa wa jamaa pale nyumbani, hivi hajamuoa je akimuoa itakuwaje na imani yake ni ya KIKATOLIKI. nikaenda kwa shemerji yake huko tukakuta jamaa wanatusubiri ilikuwa kazi , baada ya majadiliano ilitajwa mahali tsh 600000/= yeye akasema hana kiasi alichonaco ni laki na nusu, wakamueleza anaweza kulipa hata kidogokidogo amebaki na msimamo, kwa kuwa ndg hawajui lililoko ndani yake nao wakakataa kumpunguzi, tukaondoka bila maelewano na jamaa ndivyo atakavyo, huku mwanamke ametoa tishio kama hatamuoa asije juta kwani lolote laweza kutokea, sasa mimi nageuzwa chambo ngd zangu mnisaidie ushauli ni vipi niwasaidie ama kujivua zigo hilo.
   
 2. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jamaa avae sura ya kijasiri. awaite ndugu na wazazi wake na wale wa mwanamke na viongozi wa mtaa anakoishi, ikiwezekana na padri anaetaka kuwafungisha ndoa, aeleze kilakitu kwa uwazi na ukweli ikiwa ni pamoja na kutishiwa endapo asipofunga ndoa, na baada ya hapo waachane rasmi kwa kipindi cha mpito kisicho na muda maalum wakati wanatafuta namna ya kumaliza matatizo baina yao. Nashauri hiyo ndoa isifungwe kwani sio ndoa hiyo.
   
 3. g

  gracious86 JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 433
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mmmmh! Hapo kazi mkuu! Bytheway,zigo likiwa zito sana we litue tu! Lisije likakuumiza bureee
   
 4. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  huyo mwanaume:
  -Hajiamini
  -Anaishi kwa kudanganya nafsi yake
  -Hajui anataka nini katika maisha yake
  -Ataendelea kuwa viktim wa mahusiano kila siku kama hakujirekebisha.
  -Mleta mada hautakiwi kushiriki kwenye hiyo scenario, ishauri hiyo njemba halaf chapa lapa.

  USHAURI: Jamaa lazima aoneshe msimamo kwamba ndoa haitaki na atoe sababu zake, ndoa sio sinema bana kwamba unaingia kwenye ndoa kimaigizo maigizo, sasa hiyo mahari ya laki na nusu jamaa wangeikubali ina maana jamaa ndio angeliingia kwenye ndoa kwa shingo upande? what a jokes?, na kwanini asimkabili mwenza wake badili yake anawakabili mapadre na ndugu za mwenza wake? what a silly joke!
   
 5. Likasu

  Likasu JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Huyo jamaa anaonekana ni kicheche kabla hajaoa ana watoto wa5 na huyo dada kazaa nae wawili jumla 7 kwa maisha ya sasa mwanamke gani atalea watoto 7 ? Kilichopo hapa jamaa ambembeleze huyo dada akubaliane na hiyo hali na waoane. Akimuacha huyo dada mwingine atakayekuja ndo hatakubali kabisaaa ( when going get tough, tough get going ) tatizo linazidi kuwa kubwa.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,338
  Likes Received: 19,512
  Trophy Points: 280
  mahari hailipwi yote hata siku moja
  kama ni laki sita unalipa buku ishirini unachapa lapa
   
 7. E

  Epifania Senior Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli ukistaajabu ya Musa........
  Huyo mwanamke ni kiboko ya huyo mharibifu, inawezekana anampa vitisha kwakuwa anajua kilichowapata wenzie waliozaa hao watoto 5. Wewe rafiki yake una nafasi ya kumshauri, na tana anapaswa kumshukuru huyo mama kama ameamua kuwa na msimamo wa kufunga ndoa, yeye nae ajisachi, yuko vipi? na anamtendeaje mwenzie? Anaposema anafukuza ndugu, je anachukua nafasi ya kutafakari ni mambo gani yanampelekea huyo mama kufanya hivyo?
  I can't immagine kutunza watoto 5 wa mama ambao wako hai, na bado umuongezee extended family ya ndugu zake! bila kusahau watoto wa kuzaa, jamani awe na huruma kha!!!! Unless amemuweka kama mhudumu au mtumishi wa ukoo wenu. Tena asidhani kuwa anamsaidia kwa kufunga nae ndoa, binafsi naona huyo dada anajitafutia mateso.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hayo yote ya kutopenda wanawe kayajua leo?Wakati mwingine ni uzembe tu wa watu!Unamuona mtu sio alafu unakaa nae mpaka kuzaa watoto.Naweza kuelewa frastruation zinazopelekea dada kulazimisha ndoa!Mtu kamzalisha watoto 2 alafu leo hïi anamwambia sikuoi?Muda wote aliokua nae unarudi vipi?Jifunzeni kutojiachia sana kwenye mahusiano kabla ya kujua kama mtawezana kuepusha matatizo!Kama huyo dada hana kipato binafsi inawezekana hilo nalo ni tatizo!Mwanaume amwahidi kumsaidia labda then wataelewana!
   
 9. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa mujibu wa maelezo yako ina maana huyo mwanaume anaona kuwa,
  WANAWAKE/ MWANAMKE ALIYE/ALIOZAA NAO WANA TABIA MBAYA,
  HUYU NAYE ALIYEISHI NAYE MIAKA MI2 ANASEMA HAFAI KUWA MKE,
  NA KAMA NDIVYO KWELI NI KNN ANAENDELEA KUISHI NAYE NA KUMZALISHA ?,
  KWA NN HAJAMWAMBIA UKWELI HUYO MWANAMKE KUWA HAWEZI KUMWOA KUTOKANA NA A B C D??
  HAONI KAMA ANAMPOTEZEA MUDA MWANAMKE WA WATU?,
  WATOTO 7 + NDUGU WOTE HAPO NYUMBANI, JE YEYE MWANAUME ANAIHUDUMIA HIYO FAMILIA IPASAVYO?
  AU HUDUMA ZOTE ATOE MKE?? ,
  JE AMEJIPIA MWENYEWE NA KUJIONA NI MTU SAFI, WENYE MATATIZO NI MWANAMKE/WANAWAKE ANAOISHI NAO TU?
  NI KWELI KUWA YEYE HANA MATATIZO YANAYOPELEKEA HATA HAO WANAWAKE /MWANAMKE ASIWE NA UPENDO KWA HAO WATOTO NA NDUGU ZAKE???
  HAO WATOTO 5 WANAMTAZAMO CHANYA KWA HUYO MAMA YAO WA KUFIKIA??

  LILILO MUHIMU YEYE(MWANAUME) AMWAMBIE UKWELI MWANAMKE ILI KWELI IWAWEKE HURU WOTE WAWILI.
   
 10. s

  sharobaby Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  mh wanaume wengine akili zao sijui vp wanapenda sana maisha mteremko, kaishi na hyo mwanamke miaka kumi kuja kwene suala la kuoana anaanza visa mi naoana ungekaa nahuyo mdada ukamuelewesha kwa ufasaha kabisa akaelewa aachane na hilo jamaa akalee watoto wake
   
 11. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  inaonekana mapenzi ya jamaa kwa huyo dada yameisha, ikiwa hana mpango wa kuoa kabisa hata kwa mwanamke mwingine nadhani anawajibu wa kueleza stakeholder wote ukweli. Ikiwa sababu ni hao watoto inabidi akae na huyo dada wakubaliane mustakabali wote, kimsingi watoto7 ni wengi mno kulelewa na huyo dada, inahitaji uvumilivu sana na sidhani kama akija mwanamke mwingine atakubali maana namba inazidi kuongezeka...in dirty time, dirty deals needs to happen.
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Klorokwini bana, LOL!....eti ndoa sio sinema!
  Na kweli kaka,...huyu jamaa ana bargain mpaka mahari ili iweje?, ha ha ha!

  ...huyu mtu mzima mwenzetu hana ubavu kwa huyo mwanadada,
  Halafu anaonyesha hana msimamo kabisa nini anataka maishani.
   
 13. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du ndugu yangu huyo mwanamme sio mzima ana pepo la ngono, ikifika usiku anavuta ngoma tena anataka kuilipia mahari 150,000/= (je mama akimlipia zilizobaki si ataoa)
  Hana lolote atakuponza ugombane na wengi
   
Loading...