Simuelewi Huyu Muhindi

Simuelewi Huyu Muhindi

Wasiwasi wako tu unatosha kukudhuru sana tu..dawa ni kuhama chumba haraka, either ana mambo ya uchawi au la..!!
 
Unaweza kumwambia kuwa kuna document au kitu fulani kilikuwa chumbani kwako na hukioni.....umeulizia reception wamesema mtu pekee (ukiacha cleaners) aliyeingia chumabni kwako ni yeye. Jifanye kumuuliza kama ni kweli aliingia na hiyo document ni yeye kaichukua. Hiyo itamlazimisha kwa kiasi fulani kusema kile alichoingia kufanya au kuchukua.

Kwenye biashara, kuaminia (TRUST) ni jambo la muhimu sana. Na uamnifu unajengwa, hauji hivi hivi tu.
Asante kwa wazo jipya mkuu lakini kwa sasa nishaondoka hotelini kwa kuwa hatua za mwanzo tumemalizana. Nikiuliza sasa nitakua kama najichanganya
 
Habarini wanajukwaa,
Naombeni kujuzwa maana ya hii kitu kwani na amini kuna watu wenye ufahamu zaidi,. Katika harakati zangu za kutafuta green pasture nilikutana na wahindi watatu tukakubaliana kuanzisha kiwanda hapa nchini, basi wiki iliyopita siku ya jumatatu wahindi wakaja kutoka India kwani walikua safarini, na mimi nilikua Arusha.

Ilinipasa kusafiri kutoka Arusha kuelekea Dar es salaam na kushukia katika hoteli moja, ambapo pia na muhindi mmoja alikua akilala apo. tulikubaliana kuwa gharama zote ni juu yao nilikaa daresalaam kwa takribani siku 6 tukiwa tunaendelea na mambo mbalimbali ikiwemo kuandaa brandy name na mambo mengine ya usajili.

KISA CHENYEWE!!!
Ilikua siku ya jumamosi ambapo muhindi mmoja alinipigia simu na kuniuliza nipo wapi nikamjibu nipo maeneo ya Kimara matembezi akaniuliza Je funguo za rum kwangu niko nazo nikamjibu nimeziwacha reception basi akasema sawa, Kichwani nikajiuliza maswali mengi kwa nini aliniuliza kuhusu funguo za chumbani kwangu??? Au amehisi nmeamua kutembea nazo?? Au anataka kuniibia vyeti vyangu au passport yangu ya kusafiria?? Kwa nini aulizie kuhusu funguo?? Niliwaza sana.

Sikukawiaa sana nikarudi hotelini na kwenda kukagua chumbani kwangu sikukuta kitu chochote kimeibiwa lakini baada ya kuzidi kukagua uvunguni nikakutana na kitambaa chekundu pamoja na uzi wa kushonea pia mashuka yalikuwa kama kuna mtu aligusa kwani nilipoondoka niliacha baadhi ya document kwenye angle ya kitanda na hivo kukuta zimesogezwa mpaka katikati ya kitanda.

Niliamua kwenda kumfuata muhudumu wa mapokezi na kumuuliza ni nani ameingia chumbani kwangu alishtuka sana na kuniuliza kwani kuna kitu kimeibiwa?? sikumjibu nikamuuliza tena kwa ukali nani ameingia chumbani kwangu?? basi akanijibu kuwa boss wako alikuja akaniambia nimpe funguo aliingia dakika chache na kutoka. Nikamuuliza tena umejuaje kuwa yeye ndiye boss wangu?? Akajibu kwa kuwa ndiye anayekuja kulipia garama zako za hoteli na chakula.

Nikamwambia siku ingine kwa mteja mwingine nakuomba usirudie hiki kitendo mpaka upate ruhusa kutoka kwa muhusika Je ningekuta vitu vyangu havipo ungefanyaje?? Baada ya kumdodosa sana aliniambia kuwa yule mhindi anapenda kuchoma udi chumbani kwake na kufanya sala kwa namna fulani lakini kwa jinsi alivo nielezea nikatambua kuwa huwa atakuwa anafanya Meditation ila muhudumu alishindwa kutambua.

sikumuuliza yule muhindi kuhusiana na yeye kuingia chumba changu bila mimi kuwepo wala kupata ruhusa yangu, nilimwambia mhudumu anibadilishie chumba kingine na kuendelea na kazi yangu, ila bado najiuliza alikuja kufanya nini chumbani kwangu?? Je niendelee naye katika biashara au niachane nao???
cc mshana jr inakuhusu, mfafanulie Tape measure asije ingia mkenge, maana wanaweza kumuoa hivi hivi, hahaha utani tu
 
Dah
Hapo ni ushurikina kwa 100% mkuu.

Kuwa makini, ipo siku utanyofolewa kivuli ubaki unatembea kopo tu.

Dah inasikitisha sana Uchawi umetamalaki Tanzania kwa hawa ndugu zangu ndio usiseme.
 
Hakunaga kitu kama uchawi. Na kamwe sitaamini ukarogwa kweli ikakutokea
 
Nikichukuaga chumba huwa nawaambia wahudumu kwamba sihitaji usafi wa aina yeyote ile mpaka naondoka. Huwa nakagua chumba siku napoingia. Kila nikitoka huwa naacha viashiria ambavyo mtu akigusa tu nikirudi lazima nijue.
Kwa Tanzania ni sehemu chache wanayo hii option kwenye room zao wengi wanadhani mtu huwezi kuwazuia kuingia chumbani kwako just tu kwasababu wanatakiwa kufanya usafi.
warning do not enter.jpg
 
Back
Top Bottom