Simu Zenye Kamera Kutumika Kupimia Malaria na TB

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Unapotumia simu yenye kamera na Cellscope utaweza kujipima Malaria na TB

Friday, August 07, 2009 8:15 AM

Watu wenye simu zenye kamera hivi karibuni wataweza kujipima wenyewe kama wameambukizwa TB au Malaria kwa kutumia kifaa maalumu kidogo chenye darubini ambacho kwa kuambatanishwa kwenye simu zenye kamera itakuwa rahisi kuvipiga picha vijidudu vya TB na Malaria.

Timu ya wanasayansi katika chuo kikuu cha Berkeley University of California nchini Marekani wametengeneza kifaa ambacho kitakuwa kikiambatanishwa kwenye simu yoyote yenye kamera ili kuwawezesha watu kuvipiga picha na kuvionyesha vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa Malaria na kifua kikuu (TB).

Kifaa hicho kilichopewa jina la CellScope kina microscope ndogo lakini zenye nguvu kubwa sawa na Microscope kubwa zinazotumika kwenye maabara mahospitalini.

CellScope zimetengenezwa maalumu kwaajili ya kusaidia watu wanaoishi kwenye maeneo yenye huduma duni za afya kwa kuwawezesha watu kujipima wenyewe kama wana Malaria au TB.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na chuo kikuu hicho, kwa kutumia sampo za damu, mtumiaji wa simu yenye kamera na CellScope ataweza kuviona vijidudu vinavyoitwa Plasmodium falciparum ambavyo husababisha Malaria.

Kwa kutumia sampo za mate, mtumiaji ataweza kuwaona bacteria wanaosababisha ugonjwa wa kifua kikuu na kwa kutumia programu maalumu idadi ya bakteria hao wa kifua kikuu itakuwa rahisi kujulikana.

Dan Fletcher, Profesa wa bioengineering katika chuo kikuu hicho ambaye ndiye aliyeiongoza timu ya watafiti katika kuivumbua CellScope alisema kuwa CellScope zitawasaidia zaidi watu wanaoishi maeneo ambayo huduma za afya ni duni.

"Kwa kutumia simu zenye kamera na CellScope watu wataweza kuvigundua vijidudu vya Malaria na TB na hivyo kuwawezesha kupata tiba mapema kabla vijidudu havijasambaa mwilini" alisema David Breslauer ,mmoja wa watafiti walioshiriki katika utafiti huo.

Makampuni ya Microsoft na Nokia yamevutiwa na teknolojia hiyo mpya iliyovumbuliwa na wanatafuta njia ya kuingia ubia kwenye mradi huo.

Kwa mujibu wa ripoti za taasisi za afya duniani, theluthi ya idadi ya watu duniani wameambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu na watu milioni mbili hufariki kwa ugonjwa huo kila mwaka.

Chanzo: NIFAHAMISHE.COM
 
Back
Top Bottom