Simu za wanaume zina nini?

Simu za wanaume zina nini?

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,727
Katika kipindi cha leo "Mahusiano katika familia" kinachorushwa na Radio One, kulikuwa na hiyo mada. Katika maongezi na majadiliano yaliyojiri imebainika kuwa wote wawili (me/ke) ni waathirika wa Simu ya mkononi.

Swali la msingi Je, wewe ni mwathirika wa simu ya mwenzi wako? Kama ni mwathirika huwa unachukua hatua gani?
 
Wanasema Simu ya mwanaume ni kama "kitunguu maji, ukikikata lazima ulie" kwa yale utakayoyakuta kama unampenda na hauko tayari kumuacha basi usipendelee sana kushika simu yake, jiepushe na stress sizisizo na ulazima. Kila mtu abaki na simu yake tu.
Teh Teh Teh!
 
Wengine hata tukikuachia simu mwaka mzima huwezi gundua chochote maana tunawasiliana kwa kutumia coded language kama vile CIA na MOSSAD
 
Nimejitahidi kufuatilia michango yenu wote mlionitangulia juu yangu ili nipate kumuona hata muathirika mmoja, kwa bahati mbaya nimetoka kapa
 
Nimeoa au tupo kwenye mahusiano, tunalala uchi na chakula anachopika nakula bila shaka yoyote ila kwenye simu tu ndio nikae nayo mbali!? Ni bora tu niishi mwenyewe.
 
Simu ya mtu yeyote ni 💣 hatari sana hasa ikishikwa kwa uchunguzi....
 
Back
Top Bottom