Simu za TECNO na GSMArena

Simu za TECNO na GSMArena

NetworkEngineer

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2012
Posts
1,974
Reaction score
1,210
Naomba kuuliza...ukitaka kusearch specs za simu nyingi Google .
..the top search result huwa ni website inaitwa GSMArena.com...hii ni kama international database ya all mobile phones..isipokuwa TECNO. sasa je kwanini TECNO hazijawa listed katika GSMArena.com
 
Hadi unakuja kuuliza huku bado hujajichekecha tu?
GSMArena huwa hawaweki specification za simu za kuokoteza.
 
sababu kubwa ya kutokuwepo kwenye gsmarena na popular site zingine ni "Specification Inconsistency". Nadhani wengi uwa mnaona simu ya tecno inaandikwa camera 5megapixel na unakuta sio au ina ram 2gb na unakuta iko tofauti na kadhalika
 
tecno hana sifa za kuwekwa gsmarena. .kule wana list brand zinazoeleweka.
 
Hadi unakuja kuuliza huku bado hujajichekecha tu?
GSMArena huwa hawaweki specification za simu za kuokoteza.

Heheh.... Umetisha mkuu.....
Then watu wanajua ni tecno peke ake.....
Kuna hata huyu itel sijui..
Naye hawezi kukaa GSM arena..
 
sababu kubwa ya kutokuwepo kwenye gsmarena na popular site zingine ni "Specification Inconsistency". Nadhani wengi uwa mnaona simu ya tecno inaandikwa camera 5megapixel na unakuta sio au ina ram 2gb na unakuta iko tofauti na kadhalika

Sure mkuu true saying....
Kuna ndugu yangu ana tecno j7 (wenyewe wanaiita boom)
Wanavyodai ina megapixel 8
Lakini tulijaribu kulinganisha na samsung s2 camera haziendani kabisa.. Samsung wako juu..
Sasa yaweza kana hiyoo tecno c5 au hiyo c8 kwenye camera zikawa hazifikii hata camera ya s3.... Binafsi sio mpenzi wa tecno kutokana na kuwa na fake specifications kwenye advertising zao.....
 
Tecno ni kwa ajili ya Africa tu. Niliwahi tafuta simu kama ya Tecno UK lkn sikuweza hata kuiona. Kimsingi tecno ni simu ya hali ya chini sana na ni fake tu ndo maana wanathubutu kuweka specifications za uongo.
 
Sure mkuu true saying....
Kuna ndugu yangu ana tecno j7 (wenyewe wanaiita boom)
Wanavyodai ina megapixel 8
Lakini tulijaribu kulinganisha na samsung s2 camera haziendani kabisa.. Samsung wako juu..
Sasa yaweza kana hiyoo tecno c5 au hiyo c8 kwenye camera zikawa hazifikii hata camera ya s3.... Binafsi sio mpenzi wa tecno kutokana na kuwa na fake specifications kwenye advertising zao.....
Megapixel si quality ya picha, hakuna mahusiano kati ya uzuri wa picha na megapixel. Megapixel ni ukubwa wa picha,
 
sure mkuu hata mie nilidhani pixels ni quality kumbe ni dimension ya picha ni kama tv tu ukubwa wa screen sio ubora wa picha
 
Ooohh... Thanks mkuu imenifungua jambo leo... I appreciate Chief-Mkwawa

kweli kama Chief-Mkwawa alivyosema, zamani mimi nilidhani quality ya picha inapimwa na mega pixels, kumbe hizi mp ni ukubwa wa picha, camera nyingi zina megapixels ndogo ila zinatoa picha zenye quality nzuri sana, mfano Motorola moto G (first generation) ina 5MP ila inatoa picha ang'avu na zenye ubora mkubwa.. camera nyingi zenye MP ndogo huwa wanasample picha.. Ata IPhone ina Megapixels chache lakini picha zake zina mwonekano mzuri kuliko ata zile Sony zenye 20.1MP
 
Last edited by a moderator:
Sasa ili kujua kama simu camera yake ina quality tuangalie kitu gani?
 
njia trusted zaidi ni wewe kuchukua simu na kujaribu kupiga picha mbili tatu.. au nenda gsm Arena alafu cheki quality ya camera..
 
Sasa ili kujua kama simu camera yake ina quality tuangalie kitu gani?

Cha muhimu zaidi ni sensor. Simu yenye sensor kubwa na megapixel chache itakuwa na mapixel makubwa ambayo yataruhusu mwanga mwingi na kuifanya picha itokee vizuri.

Hii sensor inapimwa kwa inch, kwa simu camera zake sensor haifiki inch 1 hivyo inavyokaribia inch 1 ndio jinsi sensor ilivyo nzuri
24-megapixel-sensor-dimentions.jpg

Kitu chengine kinachofanya camera itoe vizuri ni flash, simu yenye xenon flash inapiga picha nzuri sana hasa usiku na inaweza pia kupiga picha kitu kilicho kwenye motion kama vile mtu anaepiga mbizi kwenye maji, simu yenye flash za kawaida yaani led flash inakuwa inatoa picha vibaya kuna wakati picha zinatoka vizuri zaidi kama utaweka led flash off.

Chengine kinachofanya camera iwe nzuri ni optical image stabilization (ois) ambayo husaidia camera isitingishike pale mikono inapotingishika hivyo kuruhusu mwanga mwingi pamoja na kuondoa blur kwenye picha. Simu zenye ois hutoa result nzuri za picha kwenye mwanga mdogo.

Chengine ni software optimization za kampuni, mfano apple, lg na samsung wanatumia sensor za sony kwenye simu zao lakini wote hao hapo juu wana camera nzuri kuliko sony, hii inaionesha sony ana software mbaya ya camera kuliko hao hapo juu.

Kuna mambo mengine madogo madogo pia yanaweza ongeza quality ila hayo hapo juu ni makuu
 
Back
Top Bottom