Simu za Nokia kurudi tena sokoni muda si mrefu

Simu za Nokia kurudi tena sokoni muda si mrefu

mkuu bila research leo ingekuwa
-unatembea na simu ukitaka internet unaingia kwenye kibanda unachomeka waya wa internet ili upate internet ila sababu wamespend kwenye research leo hii kuna minara ya simu na internet inapatikana ya kasi

-ingekuwa unadownload movie za full hd gb 20 lakini watu wamefanya research leo movie tunadownload chini ya gb

-ingekuwa vioo ni black and white watu wamefanya research leo vioo ni vya rangi

-fikiria camera za simu kali, microphone za sauti, speaker, display, battery nk vyote watu wamespend matrilion ya hela mpaka unaviona.

unapoponda research usifikiri vitu unavyoviona kwenye simu yako vimetokea tu watu wamehangaika hadi unaona vitu vizuri hivyo na tabia ya wanadamu hawaridhiki wanataka zaidi na zaidi hivyo siku zote kunahitajika mambo mapya.

Leo hii unafikiri Nokia akitoa simu ambayo haihitaji kuchaji inajichaji tu yenyewe toka kwenye jua, na unapotembea au kupitia minara ya simu unafikiri watu wangapi watapanga foleni kuinunua

Kwahiyo walikuwa wapi mpaka leo hii wadai wafanye research na tuendelee kuwasifia ?
Sifa nyingine tunazowapa ni zakijinga ilihali ukweli tunaujua, na ndio kuchelewa kwenyewe huko, Kampuni kama Samsung wataendelea kuwa on top in matter of android errand. kwasabu Changamoto ni nyingi walizokutana nazo.
 
kampuni ya Nokia imetangaza jana kwamba wanarudi tena kwenye soko la simu baada ya kuipa haki kampuni ya HMD kutumia jina na technology zote za Nokia.

Kampuni hii ya HMD ambayo imezinduliwa jana hio hio itakuwa na makao yake makuu Finland (kama Nokia), itakuwa inaongozwa na CEO Arto Nummela ambaye ni mfanyakazi wa Nokia toka mwaka 1994, pia Kampuni hii itakuwa na raisi anayeitwa
Florian Seiche huyu jamaa pia ni mzoefu sana alikuwa Siemens kipindi wanatengeneza simu na amefanya kazi Htc toka 2005.

unaweza cheki cv zao hapa
HMD global

na website ya HMD
HMD global

kampuni hii ya HMD watakuwa wanadesign simu, kufanya marketing na uuzaji wakati utengenezaji utafanywa na Foxconn

pia kampuni hii pamoja na Foxconn watanunua department ya simu ya Microsoft ambayo ilikuwa inahusika na Feature Phone hivyo Talent za Nokia zitarudi Nyumbani Finland.

vifaa watakavyotengeneza hawa jamaa ni smartphone na Tablets ambazo vyote vitakuwa ni vya android
Nokia-Android-concept-phone-2-490x305.jpg


Muono wangu
-Ni huzuni kwetu Fans wa Nokia sababu Nokia atakuwa hatengenezi simu (atleast kwa miaka 10 ijayo) lakini ndio mambo yameshatokea ni wakati wa kusogea mbele

-Hii kampuni ya HMD ina majina makubwa toka Nokia ya zamani lets Hope watatengeneza simu zenye quality kubwa na sio Kubrand simu za kichina

je umefurahia au hujafurahia kurudi kwa simu za nokia?

source
Nokia signs strategic brand and intellectual property licensing agreement enabling HMD global to create new generation of Nokia-branded mobile phones and tablets
Dah natumia simu yao ya mwisho kabisa kutengeneza Nokia Lumia 930 ni zinga la mashine kwa kweli nimeikubali....naombea wakirudi watengeneze na simu za windows 10 mobile sio android tu peke yake.
 
Kwahiyo walikuwa wapi mpaka leo hii wadai wafanye research na tuendelee kuwasifia ?
Sifa nyingine tunazowapa ni zakijinga ilihali ukweli tunaujua, na ndio kuchelewa kwenyewe huko, Kampuni kama Samsung wataendelea kuwa on top in matter of android errand. kwasabu Changamoto ni nyingi walizokutana nazo.
kila siku wapo usisahau Nokia ndio kampuni yenye patents nyingi zaidi za 4g, ni moja ya kampuni ambayo Technology zake zimetumika kudevelop codec mpya za video yaani x265 ambayo inakuja kuireplace x264 (kama umewahi kudownload movie/series umeshaitumia), Kampuni ya kwanza kutoa camera ya Virtual reality (VR) na tayari kampuni kubwa za filamu duniani kama Disney zimeanza kuzitumia, Ni ngumu kampuni inayofanya Research nyingi kufa kirahisi.

Na hao Samsung ni wateja wakubwa wa Technology za Nokia, Kifupi hakuna simu Duniani isiotumia Technology za Nokia

pia usichanganye mambo hapa Nokia hatengenezi simu Bali HMD na Foxconn ndio watatengeneza simu zenye jina la Nokia hivyo hakuna direct comparison ya Oem kama Samsung na Nokia
 
Kuna watu wanafikiri simu zitaendelea kuwa kama zilivyo sasa milele.
Kama wewe ni mmoja wa hao basi jua unafanya kosa kubwa sana. Teknolojia ya vifaa vya kielektroniki inabadilika kwa kasi. Kusema kwamba Nokia wamechelewa si sahihi kwa sababu hatujui wanaleta kitu gani.
Nasisitiza, kufikiri kwamba simu zitaendelea kubaki kama zilivyo sasa milele ni kosa kubwa sana.
 
Sijui kwa nn watu wanafurahia kurudi kwa NOKIA jina !! soma vizuri linarudi Jina tu. hazirudi zile classic simu zetu e63,e72 hatutapata raha na radha ya symbian v3 hata ile v2. japo Asha aliharibu ila ni jina tu wakuu.

so hata ukiwa na simu imeandikwa nokia ila ina window au android...to me thats not nokia ambayo unaijua

sitegemei kama charge ita kaa siku tatu kwa kioo kikubwa cha touch screen lazma some energ loss iongezeke
usitegemee kwamba utakuwa unaweza kuidondosha na isipate crack sababu ni jina nokia,
labdaaaaaaa baada ya miaka 10 akianza ila sijuiii

ni jina tu linarudi Ndoa ya NOKIA na Android ni sawa tu na simu yeyote ile yenye android na specification zao kubwaa bila sababu ni sawa na kubadili cover la samsung na kuweka la nokia kwenye simu yako ya android usitegemee makubwaaa
Mkuu umenikumbusha nokia e 71 daah wakati huo yaani.
 
wale mnao penda Windows phone worry out wanaendelea kutengeneza hizo OS za simu huku wakijipanga na microsoft phone nokia ilikuwa ni simu ya kukuzia jina la windows phone ingawa mambo yalienda vibaya kwenye windows 8 na windows phone 8 wamejipanga kwenye windows phone 10 na wibdows 10 PC
Stay tunein
 
Walichokosea ni kuweka Android kwenye hizo simu.

Binafsi hakuna OS inayochefua kama Android.

Nilitegemea wangekuja na OS yao kabisa.

Ningekuwa mteja wa kwanza kabisa, ila haya mambo ya Android wamenikosa.
Hata mi Android siitaki kabisa bora nijipange niende kwa IoS Tu hakuna namna sasa.
 
sijui kama nitaipenda nokia yenye Android...
labda waje na Adroid version yao sababu i know android ni open source code yeyote anaweza modify, labda watamodify na kutupia usymbian flani hivi ubelle kidogo na uwindowphone kidogo itokee kitu tofauti yaani amaizing kama na waludishe ile mi megapixel kama ya nokia n8 na nokia lumia 1020 41megapixel.. dah nokia
 
wenzako wanahangaika kumcopy microsoft na ipad pro, we kula cigar wakimaliza kucopy uataenda kuinunua na kuamini ni best technology ever
apple fan boy wana shida sana! With ipads hakuna creativity kabisa. Apple wamekua wa kukopy kila anachokifanya microsoft! Wakati microsoft alkuja na surface pen apple fan walicritisize sana! Miaka miwili baadae Apple kaja na Apple pencil! Ni mwendo wa kucopy na kupaste!
 
apple fan boy wana shida sana! With ipads hakuna creativity kabisa. Apple wamekua wa kukopy kila anachokifanya microsoft! Wakati microsoft alkuja na surface pen apple fan walicritisize sana! Miaka miwili baadae Apple kaja na Apple pencil! Ni mwendo wa kucopy na kupaste!

mkuu usipofanya research siku zote utakuwa mtu wa copy and paste sababu technology mpya haziokotwi wala hazilimwi ila zinatoka maabara.

Apple siku zote inapata hela nyingi lakini hawafanyi research wao wanacopy tu vitu vya watu. kitu pekee cha Apple ambacho wanaweza jivunia ni soc zao za A series japo nazo wameiba technology ya university moja ya huko marekani (jina nimelisahau kidogo) ila atleast kwa hizi soc wamejitahidi.

vitu vilivyobakia kila kitu wamenunua/wamecopy mahala fulani.

kuna tetesi mwaka huu kwa mara ya kwanza kwenye historia yao wataspend dola bilion 10 kwenye research nafkiri baada ya mauzo yasiyoridhisha, labda miaka ijayo tutaona technology nzuri toka kwao
 
Nilikuwa natarajia Nokia kurudi akiwa na utamu wa Symbian, lakini kusikia ni Nokia mwenye sura ya android, imenihuzunisha sana
 
Waweke na vipimo vya bangi kwa wavutaji rejea maneno ya mbunge wa Geita Msukuma kwamba kuna baadhi ya wabunge wanavuta bangi
 
apple fan boy wana shida sana! With ipads hakuna creativity kabisa. Apple wamekua wa kukopy kila anachokifanya microsoft! Wakati microsoft alkuja na surface pen apple fan walicritisize sana! Miaka miwili baadae Apple kaja na Apple pencil! Ni mwendo wa kucopy na kupaste!

We lete copy na kupaste ila brand inayouza mpka sasa unaijua na kumbuka apple ndo mwasisi wa mambo ya touch screen na mambo yote ya high tech gadget we endlea kutumia tecno
 
jamaa una mahab
We lete copy na kupaste ila brand inayouza mpka sasa unaijua na kumbuka apple ndo mwasisi wa mambo ya touch screen na mambo yote ya high tech gadget we endlea kutumia tecno

fan boy, mi naangalia productivity ya machine na sio brand. Na kwa taarifa yako natumia Lumia 950 xl with continuum. Sio kila mtu anatumia Tecno we jamaa.
 
jamaa una mahab


fan boy, mi naangalia productivity ya machine na sio brand. Na kwa taarifa yako natumia Lumia 950 xl with continuum. Sio kila mtu anatumia Tecno we jamaa.

Kama inakidhi mahitaji yako sawa ila apple forever
 
cwez tumia cm nyingne zaid ya window phone hizi lumia, nokia e6 nk nazpenda sana mtu akinipa hz cm nyingne labda nitumie nikiwa ndan ila co in puplic

swal hzi lumia ni nokia walitengeneza au vp hapo celewag
 
tuwe wakweli jamani wamgapi wapo tayari kuachana na ios na android ikitokea nokia wamekuja na mambo ya symbian? tukirejelea ilivyokuja windows ktk lumia. Wangapi walienda huko
 
Back
Top Bottom