Simu za Nokia kurudi tena sokoni muda si mrefu

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,689
39,753
kampuni ya Nokia imetangaza jana kwamba wanarudi tena kwenye soko la simu baada ya kuipa haki kampuni ya HMD kutumia jina na technology zote za Nokia.

Kampuni hii ya HMD ambayo imezinduliwa jana hio hio itakuwa na makao yake makuu Finland (kama Nokia), itakuwa inaongozwa na CEO Arto Nummela ambaye ni mfanyakazi wa Nokia toka mwaka 1994, pia Kampuni hii itakuwa na raisi anayeitwa
Florian Seiche huyu jamaa pia ni mzoefu sana alikuwa Siemens kipindi wanatengeneza simu na amefanya kazi Htc toka 2005.

unaweza cheki cv zao hapa
HMD global

na website ya HMD
HMD global

kampuni hii ya HMD watakuwa wanadesign simu, kufanya marketing na uuzaji wakati utengenezaji utafanywa na Foxconn

pia kampuni hii pamoja na Foxconn watanunua department ya simu ya Microsoft ambayo ilikuwa inahusika na Feature Phone hivyo Talent za Nokia zitarudi Nyumbani Finland.

vifaa watakavyotengeneza hawa jamaa ni smartphone na Tablets ambazo vyote vitakuwa ni vya android
Nokia-Android-concept-phone-2-490x305.jpg

Muono wangu
-Ni huzuni kwetu Fans wa Nokia sababu Nokia atakuwa hatengenezi simu (atleast kwa miaka 10 ijayo) lakini ndio mambo yameshatokea ni wakati wa kusogea mbele

-Hii kampuni ya HMD ina majina makubwa toka Nokia ya zamani lets Hope watatengeneza simu zenye quality kubwa na sio Kubrand simu za kichina

je umefurahia au hujafurahia kurudi kwa simu za nokia?

source
Nokia signs strategic brand and intellectual property licensing agreement enabling HMD global to create new generation of Nokia-branded mobile phones and tablets
 
Nikiona Brand Name ya Nokia nafurah sana. Nilisikitika jina la Nokia kupotea kiaina badala yake Lumia kusikika sana.

Kama wanarudi kutengenezea Android phones hiyo ni habari njema nitanunua Nokia. By the way kwanini Chief umehuzunika badala ya kufurahi?
 
Sidhani kama watanza mwaka huu may be awamu ya kwanza mwaka 2017 kwa sababu mkataba wa Microsoft na Nokia unaisha mwisho wa mwaka huu.
 
kwa hiyo mkuu una maanisha kwamba simu za microsoft hazitatoka tena au itasitisha huduma yake ya simu? maana najua microsoft aliinunua nokia ndo akaondoa jina la nokia na kuweka microsoft but stil ukiandalia design ni ya hardware ni kama nokia tuu sema wamebadilisha jina pia na ile symbian OS wakaitoa.
emb nipe vipengele vya mkataba kati ya nokia na microsoft mkuu nafsi yangu iwe na amani maana naipenda sana nokia. nimetimia N79,,E72, express music E71 na nyongine kibao yani nokia imo kwenye damu. pia kwenye simu za microsoft jina la nokia limo ndani ukiangalia device name, manufacture details na mengine kibao.
 
kampuni ya Nokia imetangaza jana kwamba wanarudi tena kwenye soko la simu baada ya kuipa haki kampuni ya HMD kutumia jina na technology zote za Nokia.

Kampuni hii ya HMD ambayo imezinduliwa jana hio hio itakuwa na makao yake makuu Finland (kama Nokia), itakuwa inaongozwa na CEO Arto Nummela ambaye ni mfanyakazi wa Nokia toka mwaka 1994, pia Kampuni hii itakuwa na raisi anayeitwa
Florian Seiche huyu jamaa pia ni mzoefu sana alikuwa Siemens kipindi wanatengeneza simu na amefanya kazi Htc toka 2005.

unaweza cheki cv zao hapa
HMD global

na website ya HMD
HMD global

kampuni hii ya HMD watakuwa wanadesign simu, kufanya marketing na uuzaji wakati utengenezaji utafanywa na Foxconn

pia kampuni hii pamoja na Foxconn watanunua department ya simu ya Microsoft ambayo ilikuwa inahusika na Feature Phone hivyo Talent za Nokia zitarudi Nyumbani Finland.

vifaa watakavyotengeneza hawa jamaa ni smartphone na Tablets ambazo vyote vitakuwa ni vya android
Nokia-Android-concept-phone-2-490x305.jpg

Muono wangu
-Ni huzuni kwetu Fans wa Nokia sababu Nokia atakuwa hatengenezi simu (atleast kwa miaka 10 ijayo) lakini ndio mambo yameshatokea ni wakati wa kusogea mbele

-Hii kampuni ya HMD ina majina makubwa toka Nokia ya zamani lets Hope watatengeneza simu zenye quality kubwa na sio Kubrand simu za kichina

je umefurahia au hujafurahia kurudi kwa simu za nokia?

source
Nokia signs strategic brand and intellectual property licensing agreement enabling HMD global to create new generation of Nokia-branded mobile phones and tablets

mkuu ntafrahi. sana ukinip hatima ya micrpsoft maana. najua ndo. walioinunua nokia. sasa yametokeaje hayo tena na mkataba ulikua miaka 10 au umevunjwa?? na microsoft ndo kwa. heri au b
au vipi tena?
 
Makubaliano yalikuwa kwamba, Nokia wasitumie jina la NOKIA kwenye simu hadi tarehe 31 Disemba 2015. Nokia waliuza facilities zao, pia baadhi ya teknolojia waliwaruhusu microsoft wazitumie ndani ya miaka kumi ila si zote. Ina maana kuna baadhi ya teknolojia bado ni mali ya Nokia. Watakachofanya Nokia ni kuwaruhusu HMD watumie brand pia baadhi ya teknolojia za Nokia. Pia ili zitumie jina (brand) la NOKIA bidhaa za HMD zinatakiwa zifikie viwango ambavyo Nokia wataridhika navyo kwani kwenye nafasi fulani za maamuzi za juu (nimesahau ni chombo gani ila ni chombo cha maamuzi) wamepewa Nokia.
Kwa hiyo si kwamba HMD wata-design smartphone na kuzitengeneza tu, la hasha, lazima Nokia wahakikishe zinakidhi viwango (vinavyoendana na hadhi ya brand ya Nokia) wanavyovitaka.
 
Microsoft amewauzia Foxconn biashara yake ya simu za Feature phone, Ukumbuke Microsoft alikuwa anatumia jina la Nokia kwenye feature phone tu kwenye smartphone zilikuwa zinaitwa Microsoft Lumia, hivyo kuanzia sasa hivi Microsoft hana tena uhalali wa kutumia jina Nokia. HMD na Foxconn exclusive watatumia jina Nokia bila kushare na mtu yeyote.

Kuhusu hatma ya simu za microsoft tetesi ni kwamba zitaungana na department ya Surface. kama unafatilia mambo haya nafkiri utakua unajua mafanikio ya Tablets za microsoft zinazoitwa surface pro sasa hivi zimeshakuwa billion dollar business na zinaipa joto Apple na Ipad zake. Microsoft kuanzia 2017 watatoa surface phone simu zinazorun software za computer nafkiri wanawasubiria intel wakija na processor za 10nm za canonlake ila ni tetesi tu inaweza isiwe kweli.
surface-phone-1-100577980-large.png
 
ntafurah sana hawajamaa wakirudi kwa game, coz nime miss sana bizaa zao ila sema kama zitakuwa ni android os, sijajua wao wataongeza kitu gan ili kuwazid samsung na wengine ambao kwa sasa hawakamatiki
 
Sasa umesema Nokia hata tengeneza simu kwa miaka 10, na hio HMD itakua makao makuu Finland ilipo Nokia, pia simu zitakazotoka zitakua android...hapo naona Nokia inazikwa rasmi...
Nokia wana miaka 150 katika hili game, ni kampuni ambayo hufanya maamuzi ya ajabu lakini matunda yake huonekana baadae. Miaka ya 80 wakati inaacha kutengeneza makaratasi na matairi na kujiwekeza zaidi kwenye mambo ya network (kipindi hicho hata network ya simu haijagunduliwa) watu walishangaa kama tunavyoshangaa sasa hivi lakini leo hii Imekuwa ndio kampuni kubwa zaidi ya Network za simu ikiwa na patents nyingi zaidi za 2G, 3G na 4G.

sasa hivi Nokia ameacha kutengeneza simu tu na ameamua nguvu zake kuhamishia kwenye Network na tayari ameishainunua Alcatel lucent kwa $16.6 billion moja kati ya ununuzi mkubwa kupata kutokea kwenye mambo ya tech na Sasa hivi kwa pamoja wanataka wawe juu kwenye 5G pia. Inavyoonekana kutakuwa na mabilioni ya vifaa vitakavyotumia network miaka 10 ijayo magari yataingia line za simu, kutakuwa na vifaa vidogo vidogo vijulikanavyo kama IOT (internet of things), simu, nk vyote hivi vinahitaji network na capacity ya sasa ni ndogo sana ndio maana kila kampuni inataka hii cake. Samsung, Huawei, Zte, Ericson, Nokia na wengine wengi wapo pia huku.

pia Nokia wana Department inaitwa Nokia technology ambapo hutoa bidhaa mbalimbali zinazotoka maabara za Nokia mfano mzutri ni Nokia Ozo ambayo imetoka hivi karibuni, camera kwa ajili ya Virtual Reality sema ni kwa ajili ya Film producers mtu wa kawaida si rahisi kuweza kuimudu bei yake ya dola 60,000 za kimarekani
nokia_ozo_scheda.jpg

pia Nokia Ameinunua kampuni ya Fitness na smartwatch inayoitwa withings hivyo huenda baadae na yeye akaanza kutengeneza hizi IOT kama smartwatch
 
Nikiona Brand Name ya Nokia nafurah sana. Nilisikitika jina la Nokia kupotea kiaina badala yake Lumia kusikika sana.

Kama wanarudi kutengenezea Android phones hiyo ni habari njema nitanunua Nokia. By the way kwanini Chief umehuzunika badala ya kufurahi?
Mkuu hapo HMD wakizingua ujue kuna miaka 10 bila Nokia,
 
Microsoft amewauzia Foxconn biashara yake ya simu za Feature phone, Ukumbuke Microsoft alikuwa anatumia jina la Nokia kwenye feature phone tu kwenye smartphone zilikuwa zinaitwa Microsoft Lumia, hivyo kuanzia sasa hivi Microsoft hana tena uhalali wa kutumia jina Nokia. HMD na Foxconn exclusive watatumia jina Nokia bila kushare na mtu yeyote.

Kuhusu hatma ya simu za microsoft tetesi ni kwamba zitaungana na department ya Surface. kama unafatilia mambo haya nafkiri utakua unajua mafanikio ya Tablets za microsoft zinazoitwa surface pro sasa hivi zimeshakuwa billion dollar business na zinaipa joto Apple na Ipad zake. Microsoft kuanzia 2017 watatoa surface phone simu zinazorun software za computer nafkiri wanawasubiria intel wakija na processor za 10nm za canonlake ila ni tetesi tu inaweza isiwe kweli.
surface-phone-1-100577980-large.png

pamoja mkuu kuna mahali nimesoma mda si mrefu kwamba microsoft wataendelea kutoa smartphone zao za lumia kama kawaida tuu.
 
Makubaliano yalikuwa kwamba, Nokia wasitumie jina la NOKIA kwenye simu hadi tarehe 31 Disemba 2015. Nokia waliuza facilities zao, pia baadhi ya teknolojia waliwaruhusu microsoft wazitumie ndani ya miaka kumi ila si zote. Ina maana kuna baadhi ya teknolojia bado ni mali ya Nokia. Watakachofanya Nokia ni kuwaruhusu HMD watumie brand pia baadhi ya teknolojia za Nokia. Pia ili zitumie jina (brand) la NOKIA bidhaa za HMD zinatakiwa zifikie viwango ambavyo Nokia wataridhika navyo kwani kwenye nafasi fulani za maamuzi za juu (nimesahau ni chombo gani ila ni chombo cha maamuzi) wamepewa Nokia.
Kwa hiyo si kwamba HMD wata-design smartphone na kuzitengeneza tu, la hasha, lazima Nokia wahakikishe zinakidhi viwango (vinavyoendana na hadhi ya brand ya Nokia) wanavyovitaka.

nimekupata mkuu sio mbaya. navyotumia microsoft lumia sion tofauti na nilivokua natumia nokia. ila ssymbian OS nimeimiss sana. ila microsoft naskia wataendelea kutoa lumia. smartphones zao kama kawaida.
 
Walichokosea ni kuweka Android kwenye hizo simu.

Binafsi hakuna OS inayochefua kama Android.

Nilitegemea wangekuja na OS yao kabisa.

Ningekuwa mteja wa kwanza kabisa, ila haya mambo ya Android wamenikosa.
 
mkuu hata mm ningependa iwe hivyo ila angalia microsoft wanavyotolewa jasho na windows yao watu siku hizi ku accept new thing wakati wamezoea android na os ya apple ni ngumu kweli kweli....
 
Back
Top Bottom