Simu za Google Pixel zina shida gani?

Redmi inategemea ni ipi. Wanazo zenye body ya kawaida ila si rahisi kusikia imeharibu parts au kuzimika. Hata hivyo second hand Redmi kwa bongo sio nyingi.
akipata not 11 au 12
 
Nadhani simu nyingi zipo hivyo ukiwa na simu iliyoshika roho umakini unatakiwa sana...
Simu hii ya Pixel nnayotumia haijavunjika kioo na imeangukia Sura zaidi ya mara 3 na sijawahi kuweka screen protector naitumia km ilivyo na ishatumbukia kwenye maji zaidi ya mara 3 Ila Ile Samsung iliangukia sura mara 1 tu kioo kika-bust alafu kuna siku nikakosea nikailalia ndio ikawa kwisha habari yake ikaanza kuchemka nikiichaji yaan km nimeinjika sufuria kwenye jiko la gesi kwenda kuulizia kioo nikaambiwa nikadata ikabidi niiuze tu km spear kwa wale mafundi kuanzia pale sitaki tena Samsung,
 
Hiyo Samsung iliharibu inner panel tunaita kioo namba mbili. Hasahasa ikiwa ni replaced second hand wakaweka LED ndio zina cases ikitenguka kidogo inachemka screen na kuisha chaji haraka.
 
Basi hapo ndio ulitakiwa urekebishe pale fanya editing sema sio zote maana ume-generalize kwamba zote
Sibadilishi, huo ndio uzoefu wangu. Nimesema Pixel hazidumu hiyo kauli ni data driven sijakurupuka. Simu yako kudumu haibadilishi msimamo wangu, kwenye statistics kuna outliers.

Ukileta units kadhaa za Huawei, iPhone, Mi, Pixel na Samsung utakuta Samsung na Pixel ndio ziko prone kuharibika hardware. Hii haimaanishi nyingine haziharibiki, ila tunaangalia numbers.
 
Pixel 7 kwa 700,000 miezi mitano iliyopita? Miezi mitano iliyopita pixel 7 ilikuwa inauzwa hadi 1,000,000 kule Amazon.

Alinunua simu iliyotumika au yenye changamoto. Ukitaka ufurahie hizi devices nunua mpya.

Kwa upande wako pia ulinunua Simu iliyotumika, hakuna pixel 4 mpya sokoni so nikawaida sana kupata changamoto kama hizo.

Wauzaji wengi wa Tanzania sio waaminifu, kama unaweza agiza refurbished phone Amazon na wanatoa na warrant ya miezi miwili, ni nafuu kuliko kunua kwa hawa matapeli.
 
Sawa mkuu umeshasema sio zote basi hakuna shida hapo, maana hata iPhone zinalipuka na hio Huawei hata kwa bure sichukui
 
Mimi ninayo 4xl 128,tangu 2020
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…