Simu yenye Camera Bora tafadhali

Simu yenye Camera Bora tafadhali

Camera ni kamera na simu ni simu nunua camera ndio yenye picha nzuri achana na kamera za simu ambazo Huwa zina life time...ikiisha inaanza kukera
Ni kweli kabisa, ila biashara za mitandaoni mmh vyote ni muhimu sana. Nitazingatia ushauri wako. Asante sana.
 
Hapo kazungumzia Google pixel mkuu kiufupi ni simu nzuri kwa bajeti ya kawaida pixel nzuri kwa picha ni 4xl hiyo inacheza around laki tano

Ukiitoa hiyo katika pixel nitakushauri ununue Pro zake tu hapo ipo 6 Pro around 1.7m na 7 Pro around 2.5m

Ila kwenye video mpaka sasa iPhone 13 & 14 Pro max zipo katika peak

Pia uzuri wa iPhone haipunguzi quality ya picha au video baada ya muda fulani

Kwetu wafanya biashara ingia humu mkuu natumia iPhone 13 Pro max dukani kipindi kile ilikuwa 2.5m kwa sasa zipo 2.3/2.4m na pia chukua mpya sio hizi used au refurbished
 
Camera ni kamera na simu ni simu nunua camera ndio yenye picha nzuri achana na kamera za simu ambazo Huwa zina life time...ikiisha inaanza kukera
Ndugu itakuwa mtu wa cheap phones

Hivi unadhani camera gani Itatoa picha kali na video nzuri kwa bajeti ndogo

Nijuavyo camera nzuri ni above 1m pia kibiashara bado camera haijiendeshi yenyewe
Kuna kuzitoa picha upeleke kwenye pc/phones

Usiwe ulimwengu wa kale chochote mpaka Internet cafe
 
Nashukuru mtaalam ila sijaelewa unapozungumzia hizo pixel. Inamaana simu nyingine KAMERA zake hazipimwi kwa pixel?? Natamani nijue walao simu mbili hivi zenye pixel ambazo ni nzuri.

Ingawa hizo flagship ndio hasa nitazipa kipaumbele.
Pixel ni brand ya Simu sio specs ya Camera

Google Pixel ndio komesho kwenye Camera.
 
Google pro zote mbili zipo vizuri

Iwe 6 Pro au 7 Pro labda iwe kushuka quality baada ya muda
Hiki kipengele simu nyingi za Samsung ni shida yake kuu pia
cameras za simu zote sina muda wake wakuchoka sema zinatofautiana muda tu zingine miaka mpaka 6 au 10
 
Hapo kazungumzia Google pixel mkuu kiufupi ni simu nzuri kwa bajeti ya kawaida pixel nzuri kwa picha ni 4xl hiyo inacheza around laki tano

Ukiitoa hiyo katika pixel nitakushauri ununue Pro zake tu hapo ipo 6 Pro around 1.7m na 7 Pro around 2.5m

Ila kwenye video mpaka sasa iPhone 13 & 14 Pro max zipo katika peak

Pia uzuri wa iPhone haipunguzi quality ya picha au video baada ya muda fulani

Kwetu wafanya biashara ingia humu mkuu natumia iPhone 13 Pro max dukani kipindi kile ilikuwa 2.5m kwa sasa zipo 2.3/2.4m na pia chukua mpya sio hizi used au refurbished
Nakushukuru sana sana.. hii Elimu sikuwa nayo kabisa.
 
Kama kipengele chako ni kuchoka kila kitu kinachoka ndugu yangu
Pia inafuatana na matumizi na utunzaji wako

Maana hata camera zinachoka nunua chenye ubora kichukue muda mrefu hata kuchoka
iyo comment ni jibu ya iyo ya juu apo,. we endelea. na na window shopping ya pixel 6/7
 
1. SAMSUNG GALAXY S23 ULTRA
Hii ina kamera poa na kama haitoshi imetimia kila Kona kuliko flagship nyingine yoyote ile. Kama utaipata kwa milioni 2 na nusu kwenda juu sio mbaya. Ila rangi zake haziendani na reality according to some reviewers lakini general colour science ni nzuri pia, zoom iko poa, portrait ziko poa kila kitu kiko poa hapa. Ukishindwa hii chukua hata Samsung Galaxy S23, Galaxy S23+ au hata S22 Ultra

2. APPLE IPHONE 14 PRO MAX
Hii ni level moja na huyo Samsung S23 Ultra ila picha zake zina very high contrast kuliko kawaida, nadhani ni image processing ya iOS ndio inapelekea hii hali, ila colour accuracy iko poa sana. Kwa Bongo hili ni chaguo zuri coz inapatikana madukani kiurahisi.
Ukishindwa bei ya hii chukua hata iPhone 14 Pro, iPhone 14 Plus au hata iPhone 13 Pro Max

3. GOOGLE PIXEL 7 PRO
Hii ndio ninarecommend zaidi kuliko simu nyingine yoyote ile kwa sababu ya bei yake. Ali Express inauzwa TSh 1,800,000/=
Honestly kwa bei hii huwezi kupata simu yenye kamera bora kushinda hii
Ukishindwa bei ya hii chukua hata Google Pixel 7

4. XIAOMI 13 ULTRA
Hii inakuja na two colour modes, Leica Authentic na Leica Vibrant na kuna uwezekano picha zake ni more natural kuliko hizo nyingine zote hapo juu. Global version ni very expensive so ni heri uagize kutoka China.
Kwa ajili ya biashara tumia mode ya Leica Authentic kwa sababu picha zake zina rangi za uhalisia kuliko Leica Vibrant.
Ukinunua Xiaomi 13 Ultra unapata advantage ya kuwa na vitu kama variable aperture na Leica colour science hivyo inakuruhusu kutumia photographic style unayoipenda, it's like a camera with a phone in it
Ukishindwa bei ya hii unaweza kupata Xiaomi 13 Pro au hata Xiaomi 12S Ultra.

5. OPPO FIND X6 PRO
Hii ni simu iliyo suprise phone reviewers wengi kwenye kamera mwaka huu kwa sababu ilikuwa ni beyond expectations kwa kampuni kama Oppo kuja na simu yenye kamera bomba kama hii. Ikiwa unataka kwa ajili ya biashara basi itakufaa kwa sababu bei yake ni rafiki sana na kamera yake iko poa kuliko flagship nyingi sana. Ukishindwa hii chukua Vivo X90 Pro Plus


Nimekutajia simu tano ila Chief-Mkwawa amesema kila flagship inatoa picha nzuri. Kwa hiyo tofauti na hizi tano kuna flagship nyingine nyingi tu zinazoweza kukufaa kwa picha.
Nilichofanya mimi ni kukupa mifano tu ya hizo flagship zenye kamera nzuri
Unaweza kuangalia flagship nyingine mtandaoni, Google iko open ikiwa unataka kutafuta knowledge
 
kuna tecno kamera zao wanafunga kwa cheap material mwaka mmoja tu kwisha ukitoa cammon series
Techno simu zao inapoingia sokoni utaipenda
Niliwahi kukimbilia phantom kila baada ya muda picha/video inafifia quality


Binafsi bado kwenye simu naona iPhone yupo vizuri
Mpaka sasa hivi iPhone 7 tu ipo sokoni kitambo lakini inazishinda current phones nyingi
Simu inashindwa light optimization kila picha inakutoa kama umetoka kwenye machimbo ya makaa
 
Back
Top Bottom