Simu yangu inatumia muda mrefu kuchaji

Simu yangu inatumia muda mrefu kuchaji

mkuu ingia playstore download app inaitwa ampere halafu chaji simu huku hio app umeifungua itakuambia ni kiasi gani cha umeme kinaingia.

kwa smartphone ya kisasa inabidi angalau 1000ma (1A) ndio inatosheleza kucharge upesi upesi.
Chief Umechanganya Amps 1 ni kubwa sana Kwa Simu Range ya simu ni Milliampere
 
PhotoGrid_1492413251981.png
IMG_20170417_101017.jpg

Uangalie charger yako yawezekana sio inayolingana na simu yako, angalia hiyo attachment, kwa simu yako output volt inatakiwa iwe 5.0V na output current iwe 1.0A hadi 1.2A
Ila kama ni 3.7V na 800mA(0.8A) usitegemee simu yako kujaa au kuchelewa sana kujaa.
 
Chief Umechanganya Amps 1 ni kubwa sana Kwa Simu Range ya simu ni Milliampere
na zikiwa 1000 hizo milliamper si inakuwa ampere moja? simu za kisasa zote zenye fast charging na baadhi zisizo na fast charging zinavuka hizo milliampere 1000 mfano hii yangu max ni 1800 ambayo ni sawa na 1.8A

na chaja nzuri nyingi ni 2A
 
Mkuu nimedowload hiyo application, na naona hizo namba zinaongezeka kutoka 100+ hadi zimefika 450 ila bado nadhani zilikuwa zinapanda, je kama namba zinabadilika kupanda na kushuka maana yake nini? Je lazima ifike 1000?

Halafu mkuu naona Kuna maximum, minimum, nadhani na actual ambayo inabadilika badilika, je hii tafsir yake imekaaje?
kama ina vary inamaana umeme unaotoka kwenye chaja nao pia upo hivyo hivyo mara unakuja mdogo mara mkubwa, minimum inamaana ni kiasi kidogo zaidi kuingia na max ni kikubwa zaidi kuingia, kama ni ariund 400 inamaana simu yako inachukua muda sana kujaa, ikiwa 1000 kupanda ndio inajaa upesi upesi unless simu yako ni ya kizamani sana
 
Mkuu tatizo lako ni charger tu apo njoo kariakoo kesho nikuuzie fast charger za Samsung nusu SAA tu simu yako imejaa kabisa ni 10000/- za kitanzania kwa charger moja
huwa fast charging haziingiliani, huwezi tumia fast charging ya Samsung kuchajia Tecno au huawei
 
Kuna app ya namna hiyo kwa window phone, Kama ipo jina lake please

jaribu officila app ya battery au app inaitwa aida64 sema zinaonesha kwa percentage na sio actual ampere

alternative tafuta hardware solution unanunua kifaa kama hiki
wireless-chargers-usb-amp-volt-measurement-840x560.jpg

hapo unachomeka tu chaja itakuambia specs za hio chaja kwa volts na amps then utajua kama ni chaja nzuri ama la, kizuri sana kwenda nacho dukani wasikuuzie chaja feki
 
Mkuu ahasante kwa kutoonesha hiki kifaa, je kinaitwaje, na kinapatikana wapi, na kama unajua ni shilingi ngapi hivi na kama chenyewe hakuna feki?
 
Hi
huwa fast charging haziingiliani, huwezi tumia fast charging ya Samsung kuchajia Tecno au huawei
Hivi hizi fast charging hazina madhara kwenye simu? Na je ni fast huwa inachukuwa muda gani na ya kawaida inachukua muda gani pia?
 
kama ina vary inamaana umeme unaotoka kwenye chaja nao pia upo hivyo hivyo mara unakuja mdogo mara mkubwa, minimum inamaana ni kiasi kidogo zaidi kuingia na max ni kikubwa zaidi kuingia, kama ni ariund 400 inamaana simu yako inachukua muda sana kujaa, ikiwa 1000 kupanda ndio inajaa upesi upesi unless simu yako ni ya kizamani sana

OK nimekupata mkuu, ila natumia Note 4 sema charger ni ya Tecno na USB yaKe ni ile ndefuu nilinunua tu kwa machinga barabarani.
 
Mkuu ahasante kwa kutoonesha hiki kifaa, je kinaitwaje, na kinapatikana wapi, na kama unajua ni shilingi ngapi hivi na kama chenyewe hakuna feki?
kwa hapa sifahamu kama vipo ila ebay vipo bei ya kutupa

Current charger usb | eBay

kwa hapa kwetu mafundi wanakuwa navyo kama hivyo ila umbo lake linakuwa kubwa unaweza tafuta fundi wa simu akuelekeze wananunulia wapi.
 
Hi

Hivi hizi fast charging hazina madhara kwenye simu? Na je ni fast huwa inachukuwa muda gani na ya kawaida inachukua muda gani pia?

hazina madhara makubwa mkuu, sababu zinatengenezwa na manufacture wa simu wenyewe, cha muhimu tu iwe original na sio fake.

fast charging huchaji kama chaja ya kawaida nzuri sema yenyewe inatoka asilimia 0 mpaka asilimia 50 hadi 80 kwa muda mfupi.

mfano inaweza tumia saa moja na nusu kuchaji simu, kutoka asilimia 0 hadi 80 ikatumia nusu saa tu na kutoka 80 hadi 100 (asilimia 20) ikatumia saa zima.

hivyo husaidia sana pale unapokuwa na muda mdogo wa kuchaji, au unaiboost tu mara moja, ila kama ni usiku unaichaji hadi asubuhi fast charging inakuwa haina maana.
 
kwa hapa sifahamu kama vipo ila ebay vipo bei ya kutupa

Current charger usb | eBay

kwa hapa kwetu mafundi wanakuwa navyo kama hivyo ila umbo lake linakuwa kubwa unaweza tafuta fundi wa simu akuelekeze wananunulia wapi.
Ahsante mkuu nimekupata. Ila naweza pia tumia hii application ya Ampere kupima uwezo wa charger sio ninapokwenda dukan, kiasi kwamba kama ina charge chini ya 1000 haifai, au kama inbadilika badilika pia haifai?
 
ndio mkuu unaweza na hii ni bora pia sababu inapimia kwenye simu yako,

baadhi ya chaja huchagua simu hivyo kuipima na kifaa kama hicho inaweza kuwa nzuri ila ikija kwenye simu yako ikawa mbaya
 
Ahsante sana mkuu, nitatumia mbinu hii kuchagua charger
 
Back
Top Bottom