Simu yangu imepigwa kwa watu usiku, pasipo piga mimi, na nilikuwa nimelala! Huu uchawi au?

Hio ishantokea, tumemaliza ongea na bebe saa 6 tukaagana. Asubuhi nashtuka nakuta missed calls zake kuwa alipiga saa 8 na saa 10 alfajiri! Nikamuuliza vipi, anadai hajagusa simu toka alipolala.
Jana me simu ya beibee imenipigiaaa akati yeye namuona kabisa Yupo instagram muda huooo wala hajanipigiaa.. Ni tigo nadhani ndo wanazinguaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana jamvi,

Rafiki yangu kanipigia SAA kumi na nusu usiku, anadai eti amepata missing call yangu. Akajua Wenda nimepata tatizo.


Kiukweli sijapiga simu usiku. Namba ya simu yangu ni tigo!

Badae tena, mdogo wangu kanipigia eti amepata missing call yangu usiku! Nimeshindwa kuelewa!

Ni mtandao, au watu wasionekana usiku a.k.a wachawi?
Na mimi kaka yangu amenipigia alfajiri akidai amekuta missed call yangu usiku.na nililala mapema na simu niliweka kwenye chaji sikuigusa hadi muda alionipigia.pia nimecheki kwenye simu nilizopiga hamna namba yake wala namba nyingine niliyopiga usiku.niliipotezea.ila nimeona post yako imenifanya na mimi nililete humu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Avatar yako inakutambulisha ulivo. Itakua ni wenzio mnaofanana walikuja kukusabahi na kuamua kuwasabahi pia rafiki zako. Unapolala jiweke chin ya ulinzi wa Mungu hayo hayatatokea tena
 
Hii nimeiona twice. Mara ya kwanza jirani yangu (hana mke) alini-beep saa saba usiku nikiwa naiona simu, akasindikiza na message kuwa nimsaidie shillingi laki na sabini na tano mkewe kapata matatizo wako hospital. Nikacheka sana sababu kama saa tano hivi usiku mchizi nilikuwa nae na akanigawia movies akilalamika kuwa simu yake haina network tokea jioni.

So baada ya kupokea SMS na Missed call nakaona nisipige wala nini kwa kuwa ni karibu Nikaenda kwake chap ni hatua chache tu kutoka kwangu. Nikamgongea mlango akafungua alikuwa sebule nae anaangalia movies, nikamuonesha simu akashangaa sana. Tukashauriana kwa kuwa ni usiku sana na hatuwezi saidika nifanye Tethering kwa simu yangu apate WiFi aweke status WhatsApp kuwa yeyote asijibu either text wala SMS kutoka namba yake kwa kuwa inatumika na asiowajua.

Baada ya ile status kama dakika tatu kapokea screen captures mbili kutoka kwa watu wake wa karibu ikionesha SMS aliowatumia Exactly kama ile yangu. Wao hawaku-react sababu wanajua mchizi hajaoa wala hana steady relationship yeyote.

Kesho yake ndio kwenda Police kisa kwenye ofisi za mtandao husika akarejeshewa network baada ya kubadilishiwa Simcard.



Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu mimi pia vodacom line ilikua haishiki network nikiwauliza vodacom wanasema wamefanya mabadiliko kwenye profile yangu... nilipigwa chenga hadi nikaamua kubadili line.
 
mkuu mimi pia vodacom line ilikua haishiki network nikiwauliza vodacom wanasema wamefanya mabadiliko kwenye profile yangu... nilipigwa chenga hadi nikaamua kubadili line.
1. Kwanini wafanye mabadiliko hayo bila kukutaarifu awali (ili uepukane na usumbufu usio lazima)?

2. Kwanini wafanye mabadiliko hayo kwa baadhi tu ya Simcards? (Atleast labda ingekuwa ni Simcards zilizosajiliwa mwaka fulani tu. Tungeelewa labda wakati wa usajili kulitokeaga makosa kwenye data entry).

3. Kwanini mabadiliko hayo ya siri yachukue muda mrefu mpaka kupelekea kupoteza mteja? (Hakuna mfanyabiashara anaependa kupoteza mteja)

4. Kama ni operations za kawaida, kwanini wateja wasiwe informed katika matangazo? (Kumbuka wana airtime kunwa sana maredioni na kwenye TV)

5. Na swali la msingi kabisa. Mabadiliko kwenye profile ya mteja ni nini? Yanahusisha nini? Na faida zake ni zipi?

Haya makampuni yawe makini, kuna mtu/watu kwa makusudi kabisa wanayahujumu kwa kusumbua wateja. Na ukitaka kushtaki utajikuta uneshtaki kampuni ila the actual culprit keshasepa zake na kawaibia wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseeeh!!! Ahsante mleta mada. Kumbe kuna utapeli wa hivi eeh umeanza, baada ya ule wa 'ile hela tuma namba hii' kuchuja? Tuchukue tu tahadhari,kama imeanza Tigo lazima itasambaa tu huku kwingine

Bado matapeli hawaja amini kuwa hawawezi
Pata mtu wana nitumiaga kila wakati hawaja ridhika kabisa!
Screenshot_20190115-165106.jpg
 
5. Na swali la msingi kabisa. Mabadiliko kwenye profile ya mteja ni nini? Yanahusisha nini? Na faida zake ni zipi?
Unaweza kudhani maskhara cheki walichonijibu ujinga mtupu hadi nikaamua kuhamia airtel
Screenshot (13).png
 
Hata mm imenitokea, nimelala na Mr akashtuka saa kumi na moja ananiamsha umenipigia saa ngapi sim ina missed call yangu bas nikawa najiuliza nimepiga saa ngapi wakati tulilala
 
Hata mm imenitokea, nimelala na Mr akashtuka saa kumi na moja ananiamsha umenipigia saa ngapi sim ina missed call yangu bas nikawa najiuliza nimepiga saa ngapi wakati tulilala
Hawa wenye mitandao waje watueleze tatizo ni nini
 
Hili si la kupuuzia wenye mtandao husika waseme nini kimetokea watavunja ndoa za watu. Mimi naamka asubuhi wife ananiuliza uliamka asubuhi ukanipigia simu? Haa nikamwambia hapana na simu yangu haina hata call dial kwenda kwake lakini yeye ana missed call kutoka kwangu. Plizzz Tigo huu sio wakati wakukaa kimya. Nimeona ni wengi limewakuta muda ni huo huo saa kumi na nusu. Tigo embu acheni hizo bwanaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom