Simu yangu iliponiletea balaa

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000

Simu yangu hupata ujumbe wa aina mbalimbali ukiwemo wa utani kutoka kwa wanaume na wanawake. Utani huo unaweza kuwa wa kimapenzi, kifamilia, kikazi au mwingine mwingi. Kwa kazi yangu utani huu hunipa nguvu na hisia za ukaribu na watu, lakini kubwa zaidi hunifanya niwe mtani wa wanawake wengi wanaonifahamu kuliko kuwa kitu kingine.

Wiki kadhaa zilizopita kwa bahati mbaya au kwa kusudi, mke wangu alifungua ujumbe ulio kwenye simu yangu. Aliposoma alikutana na ujumbe wenye neno Dear. Bila shaka neno hilo likiwa limeandikwa na mwanamke, lilimfanya kuuliza maana ya neno lile. Hakujali ujumbe ulisema kitu gani, bali alijali neno Dear. Kidogo lilitutikisa. Lakini mambo yaliisha.

Lakini walisema muonja asali haonji mara moja. Nadhani aliona kusoma ujumbe unaotumwa kwenye simu yangu kunamfanya apate nguvu au kuthibitisha anachotaka kuthibitisha, Siku nyingine tena kwa kile kinachoitwa bahati mbaya, alisoma tena ujumbe kwenye simu yangu.

Ujumbe huu sasa ulikuwa na neno Darling, sio Dear tena. Pamoja na neno hilo kulikuwa na maneno yenye kuonesha kwamba, aliyeniandikia anataka tuwe wapenzi na tushiriki tendo na kwamba, angependa anipeleke mahali kwa siku mbili na nisije nikaanza kumkumbuka mke wangu.

Kwa kweli nadhani ujumbe huu na hasa neno Darling, ulimvunja nguvu mke wangu kiasi kwamba, alilia kwa muda mrefu wa usiku. Nilihuzunika kwa hilo. Lakini nilijiambia na kujiuliza, ‘alikuwa na haki gani kukagua ujumbe kwenye simu yangu?’ Ukweli ni kwamba, simu ni yangu na watu ninao wasiliana nao , nawajua mimi na najua ni kwa nini nawasiliana nao kwa namna fulani. Yeye akisoma ujumbe wa aina yoyote, atafanya majumuisho yake na sio ya hali halisi.

Kwa mfano, mwanamke huyu ambaye, mke wangu alisoma ujumbe wake alianza kuniita Darling, baada ya siku moja kimzaha kuniuliza, ningependa kuitwa nani na yeye, bosi, mheshimiwa, baba fulani, au jina langu. Nilimuuliza, ‘mbona umesahau kutaja neno Darling?’ Kwa utani, kuanzia siku hapo akawa ananiita Darling.

Ujumbe aliousoma mke wangu, ulikuwa ni utani, ambapo alikuwa anasema, akija kunitembelea atanipeleka mahali na kwa sababu mimi najifanya naaminika, nimwombe mke wangu ruhusa ya siku mbili kwamba naenda semina. Tulijibizana kwa muda mrefu kwa ujumbe katika mzaha kama tulivyokuwa tumezoea.

Bila shaka kila mmoja kati yetu alikuwa huru, kwani kila mmoja alijua kuwa anachokifanya ni mzaha. Lakini hata kama mtu mwingine angetulia, ujumbe ule ulikuwa unaonesha utani wa wazi kabisa. Lakini kwa mke wangu ingekuwa vigumu kuona mzaha ndani ya ujumbe ule. Siyo kwake tu, bali hata kwako na kwa mwingine, ingekuwa hivyo. Kwa nini?

Hapa ndipo panawaumiza wengi kwenye suala la ujumbe kwenye simu. Hadi mtu achukue simu ya mpenzi wake na kuanza kukagua ujumbe uliotumwa humo au majina ya watu walio kwenye orodha ndani ya simu hiyo, ni lazima ana wasiwasi na mwenzake. Kwa sababu ya wasi wasi huo, chochote atakachokiona ambacho kinaonesha dalili za kukosa uaminifu, hatatumia akili kukipima, bali ataendeshwa na mihemko.

Kuna mazingira mengi ambapo mtu anaweza kuamini kabisa kwamba, mwenzake anatoka nje. Hata anapowasimulia wenzake nao watampambisha moto kwa kumwambia, ‘haiwezekani, ni lazima wana uhusiano,’ wakati hakuna jambo kama hilo. Tunaona sana mambo haya kwenye sinema zinazooneshwa kwenye televisheni zetu.

Nikipi kinasema kweli, ni tabia ya mtu kama tunavyoijua au ujumbe tuliouona kwenye simu? Nafikiri kuwa unamjua vipi mume au mke wako, ndilo jambo la msingi kwanza. Kama humwamini, ni lazima utapata mazingira ya kuthibitisha wasiwasi wako. Utachakura kwenye simu yake, utapekua mkoba wake, utakagua mifuko ya nguo zake na hata ‘diary’ yake utaikagua kila wakati. Kwa sababu lengo ni kuthibitisha kwamba siyo mwaminifu, ni lazima utathibitisha.

Kushindwa kujua kwamba, simu kila mmoja ni yake na yaliyomo ndani ya simu ni yake na yeye ndiye mwenye kujua maana yake, hilo huwaumiza wengi. Niliwahi kupokea ujumbe kwenye simu ambao unasema, ‘kumbe umeshikwa na mkeo, wewe mpumbavu kweli. Kumbe umekuwa unapoteza bure muda wangu.’ Kabla sijakaa sawa, nikatumiwa ujumbe mwingine na mtu huyo huyo akisema, ‘Kama unaona vipi tuachie hapahapa kabla hatujafika mbali, tusije kuumizana bure.’

Ilibidi nimpigie simu huyo aliyetuma ujumbe huo. Nilipomwambia kwamba huenda amekosea namba , alikiri. Lakini alisema kuna mtu ameanza kufanya naye biashara na amegundua kuwa kila kitu ni hadi mke wa huyo jamaa aamue. Hivyo ameamua kumwonya, kwani kwa sababu hiyo tayari wameshapata hasara.

Je mke wa huyo jamaa angeuona ujumbe ule kwenye simu ya mumewe angeelewa hivyo? Sio rahisi, angeelewa kwamba huyo mwanamke ni hawara wa mumewe na anataka wavunje uhusiano kwa sababu hampi anachokitaka, yaani kuwa naye muda mwingi au wote.

Ubaya wa ujumbe ni kwamba huwezi kuzuia usiingie, tofauti na kupigiwa,ambapo unaweza kukata simu au unaweza kuacha mtu azungumze wakati simu umeiweka mbali. Hapo hakuna ushahidi unaoachwa, Ujumbe huacha ushahidi ambao ni dhaifu sana, hata hivyo. Kama nilivyosema awali, kuna kuvunjika kwa ndoa kwingi sana, kutokana na simu za mkononi.

Lakini bahati mbaya ni kwamba, kuna kuuana au kujiua au kuuawa ambapo chanzo ni simu za mkononi. Ni kwa nini binadamu awe kipofu kirahisi kiasi hicho?Kwa nini simu ndio imfundishe kuhusu mwenzake, badala ya mwenyewe kumjua mwenzake?
 

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Messages
10,312
Points
2,000

nyumba kubwa

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2010
10,312 2,000
Huo sawa ni utani lakini ni utani hatarishi. Ni rahisi sana kuzini na mwanamke anayekutania mambo ya mapenzi kuliko mwanamke ambaye mnaheshimiana. Kwa hiyo mkeo yuko very right. Je wewe ungependa mkeo awe na watani wa jinsi hiyo kazini. Kwa kweli kwangu mimi once mtu una mke/ mume there should be a limit to the way you relate with opposite sex. Imagine unamsikia mkeo anaongea na simu anamwamba jamaa wanayefanya wote kazi "usiku sikulala nilikuwa nakuwaza darling" Afu unamuhoji anakwambia ni utani huwa tunataniana. Utamwelewa??? Maana hapo unaongelea message kwa kuwa mkeo amepekua. What if angekusikia unaongea kwa simu??? Maana hamna tofauti kati ya sms na kuongea zote ni communication. It is safe kujiheshimu.

Na mimi kwa uzoefu wangu hao wanawake wanaopenda utani wa jinsi hiyo ni maharage ya mbeya. Hawataniwi; ukijaribu tu umenasa. Wewe unaona utani mwenzio anasali lini utamtamkia ili mfanye kweli.

Nadhani hata wewe unajua au kama hujui jua sasa kuwa wanawake cheap wanapenda sana utani wa kimapenzi na ni njia moja wapo ya kuwanasa wanaume. Hence ukiona mwanamke anakutania mambo ya mapenzi jua ANAKUTAKA period!
 

Tasia I

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2010
Messages
1,226
Points
1,195

Tasia I

JF-Expert Member
Joined Apr 21, 2010
1,226 1,195
mh! yani we jama haupo siriaz kabisa!
unataka kusema mke wako hana hai ya kusach sim yako?? unataka kusem amke wako (anekupenda)
alipokuta jumbe kama hzo angechukulia ni utani?? unataka kumfanya mke wako kua hajui risk/hatari iliyopo katika wewe kutaniana na
huyo mwanmke tena utani wa imapenzi??
kamwombe mke wako msamaha haraka sana kama kweli upo siriaz.
kwa taarifa yako ni rahuisi sana kumgonga mwanamke kwa kupitia utani kuliko ukiwa siriaz.
mfano:hapa sasa hivi nimetoka kuongea na dem flani nlisoma nae miaka miwili ilopita.
nikamweleza kiutani kua siku mingi hua namtamani ilatu nilikua nashindwa nianzeje kumwambia kwakua tuliheshimiana sana (niliku natania lakini)
cha ajab amenijib niache utani "tasia acha utania bwanaa" af et nifikirie af nimweleze tena af hapo tutaongea zaidi!!
unaona iko siu unaeza kukuta umemega hyo kitu!
 

Wabogojo

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Messages
356
Points
195

Wabogojo

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2010
356 195
mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh<br />
kwenye kusoma tu ndo balaa<br />
imenipa uvivu bhana
<br />
<br />
kaa ujue kabisa simu ya kiganja ni nyenzo no one ya kijua tabia ya mwenzi kama si mwaminifu, ikiwa m mwili mmoja (wanandoa tu) ili kudhihirisha kiapo chenu na kudumisha ndoa zenu ni bora kabisa kusiwe na mipaka ktk simu zenu. kaka utani kama huo haufai kwani ninahakika umepitiliza, hata ww uta amini ukikuta sms kama hizo kwa shem. jihemu ndg yangu ili udumishe ndoa
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Messages
3,057
Points
1,500

bitimkongwe

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2009
3,057 1,500
Ee bwana mimi mwanamme atakayeniletea message za namna hiyo 'za kiutani utani' namwambia akome mara moja.

Hakuna utani wa namna hiyo baina ya 'ke na 'me na mukiwa ofisi moja ndiyo hatari zaidi. Hebu imagine mwengine yo yote akabahatika kupata simu hiyo na kusoma msg za aina hiyo ni moja kwa moja ataona kuna uhusiano fulani.

Wacha mara moja usijitetee bure.
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,091
Points
2,000

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,091 2,000
huo utani wako umepitiliza. Hata kama simu yako ni uhuru wako haina maana mtumiane msg za namna hyo!(za darling) huyo anayekuvmia hajui umeoa? Hajui mipaka yake? Kwa nini amtumie mume wa mtu msg zisizokuwa na adabu namna hiyo? Hebu vaa viatu vya mkeo je ungekuta msg za mahaba hivyo (ingawa utadai hushiki simu ya mkeo) ungefurahi? Kama usingeng'aka na kumtuhumu mkeo kisha ukaja kuomba ushauri nini cha kufanya
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,091
Points
2,000

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,091 2,000
Ee bwana mimi mwanamme atakayeniletea message za namna hiyo 'za kiutani utani' namwambia akome mara moja.<br />
<br />
Hakuna utani wa namna hiyo baina ya 'ke na 'me na mukiwa ofisi moja ndiyo hatari zaidi. Hebu imagine mwengine yo yote akabahatika kupata simu hiyo na kusoma msg za aina hiyo ni moja kwa moja ataona kuna uhusiano fulani.
Wacha mara moja usijitetee bure.
umeona anataka ku-justify sms zake za 'darling'
 

Kbd

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2009
Messages
1,263
Points
1,170

Kbd

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2009
1,263 1,170
Yaani meseji ukutwe nayo wewe ila lawama umtupie aliyokukuta nayo.....what a joke! Ninauhakika ungekuwa wewe ndio umeiona hiyo meseji kwenye simu ya mkeo, ungekuwa umeshamdunda na saa hizi ushamfukuza hapo nyumbani. Kuwa fair kidogo na vaa viatu vyake for a minute. Mi nadhani badala ya kujusify uovu wako nenda kaombe msamaha kwa mkeo pls, umemuumiza sana.
 

Mamaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Messages
3,891
Points
2,000

Mamaya

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2011
3,891 2,000
Hebu acha utani hatarishi na jiheshimu,jua wewe ni mme wa mtu and you should have a limit in jokes.Kama unapenda utani zingatia utani usiovuka mipaka,kama ulikuwa na katabia ka utani wa namna hii kabla hujao kwa sasa acha kabisa.ulipoamua kuoa uliuza sehemu ya uhuru wako kwa mwenzio.imagine ni unamkuta mkeo na sms za namna hii utajisikiaje? Angalizo langu unakoelekea na hao unaotaniana nao tena ukizingatia ni jinsia tofauti utakuja kuishia kumgonga manake shetan naye yupo kazin kuongeza idadi ya wazinzi duniani pamoja na kusambaratisha ndoa za watu. Kwa taarifa yako ni rahisi saaaaana kumgonga mwanamke kwa utani tofauti na ukiwa serious kumtongoza,mnagongana kiutani utani hv hv na hata haustuki,utakuja kushtuka baada ya tendo. shetan naye anafurahia kashafanya kazi yake.ACHA MARA MOJA TABIA YA NAMNA HII.
 

fabinyo

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2011
Messages
2,153
Points
1,250

fabinyo

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2011
2,153 1,250
......kaka umechemka,utani wa kifala namna hiyo sio mzuri,unajua wazi mkeo hata wangu hawezi hilo wa nini ulazimishe?by the way,unaona raha gani mkeo ambaye anakuzalia watoto,kukupikia na kila kitu aumie kwa kumuintaten mtu ambaye hana faida yoyote na wewe?wewe ni mume,achana na hayo mambo ya kipuuzi,umeandika mengi ya kujitetea ila mwisho wa siku mkeo inabidi afurahie maisha na wewe zaidi kuliko wengine na anahaki na simu yako pia
 

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2010
Messages
7,320
Points
2,000

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2010
7,320 2,000
Mkuu message ni ndefu sijaimaliza ila naweza kujaribu tu kukueleza kuwa mzaha mzaha hutumbuka usaha, kwa hiyo mkeo alikuwa na haki zote za kukulilia na kuhuzunika juu ya alichokiona.
 

Forum statistics

Threads 1,352,840
Members 518,197
Posts 33,067,679
Top