Simu makanisani....

Binasfi nahisi hakuna tatizo hasa ukizingatia kama hizo simu zina miziki ya nyimbo za kidini ni moja kati ya shamra shamra za kanisa.
 
Vimini wao... hungover makanisani wao... simu na kuwasumbua wenzao wanaotaka utulivu makanisani wao... Ufisadi wao...!

Si ajabu Mungu hakawa hapatikani kanisani.
 
Kuna issues muhimu na madhambi mengi kanisani yanayotia wasiwasi wa muelekeo wa kanisa. Simu nikitu kidogo sana, misitari ya Bible ambayo ndo lazima haifuatwi, wachangiaji wengi wnavyolaani vimini makanisani, lakini hapa JF washabiki wana-ignore

Bible clearly imekataza vimini kanisani na mengineyo yanatakiwa yakomeshwe, sio Simu
 
Vimini wao... hungover makanisani wao... simu na kuwasumbua wenzao wanaotaka utulivu makanisani wao... Ufisadi wao...!

Si ajabu Mungu hakawa hapatikani kanisani.

Yaani wewe Msilamu mzimaa unaenda Kanisani kuangalia vi mini. Huna haya we,
 
na jana tu church mdada wa pembeni yangu hakuzima cmu, 2nackiliza mahubiri, tunackia"nataka paja mie hakinitoshi kipapatio"....alitetemeka mana kanisa lilikuwa kimyaaaa, kila mtu aligeuka kuckiliza mlio unapotokea....nadhani sio ustaarabu, unaweza kuizima tu kwa muda huo mchache wa misa.

Inakera lakini, imagine ume-concentrate mara unasikia mipasho, halafu simu yenyewe iwe ya kichina, noma kweli
 
wadau! Hili limekuwa tatizo kubwa, maana utakuta kila siku waumini wanaambiwa wasije na simu zao makanisani lakini ndy kwanza hawasikii... Simu nyengine milio ni mikubwa n mbaya zaidi utakuta ni nyimbo za kidunia...

Je! Watu hawa ni wastaarabu?
sio wastaarabu...
 
Biblia inasema twende mbele ya Mungu kwa kicho na heshima,sasa simu inapiga kelele sio ustaarabu, kama unaona una ishu muhimu, basi weka hata silent, utakuta missed kol, then utawatafuta wote waliokupigia. Kwanza unapigia watu makelele wanaotaka kusikiliza ibada.

IKIWA WACHUNGAJI NDIO HAWA KWELI BIBLIA ITAFUATWA????


[ame]http://www.youtube.com/watch?v=KxfThlCcfHI[/ame]

 
Mungu anapendezwa na wanaomuabudu katika roho na kweli.
Kwa hiyo kwenda na simu kanisani ina maana ukipigiwa muda wowote unapokea au unatuma msg, kwa hiyo utashidwa kuzingatia kinachoongelewa shetani anakuwa ameshachukuwa mawazo yako.
unakuwa umeenda katika ibada kusindikiza wengine au watu wakuone na wewe umeenda.
 
Wadau! Hili limekuwa tatizo kubwa, maana utakuta kila siku waumini wanaambiwa wasije na simu zao makanisani lakini ndy kwanza hawasikii... Simu nyengine milio ni mikubwa n mbaya zaidi utakuta ni nyimbo za kidunia...

je! watu hawa ni wastaarabu?

Kwa nini umkataze asije na simu! Ni kuwaaambia tu wakiingia Kanisani Waweke silent Mode or Vibration Mode kwisha mahubiri yanaendelea....Na je kuna wakati wadada waliambiwa wasiende na suruali lakini siku hizi kasi imeibuka upwa inakuaje hapo........
 
Hii ni kweli hata kwenye ibada za mazishi unasikia ngwasuma na mduara bila kusahau taarabu zinatoka kwenye milio ya simu. Bora hata wangeweka mapambio. Wakome kabisa.
 
Kuna wakati nilikuwa na rafiki yangu kutoka Nigeria akanambia kwao ukiwa na Kanisa unafanya pesa sana mimi sikumuelewa nilikuwa namini kujenga kanisa ni kwa ajili ya kuwafanya watu waje wawe na mahali kuabudu na sio kuwa kitega uchumi,kwa mana hiyo ni mawazo mazuri kama mtu ataweza kujenga kanisa kwa ajili ya kitega uchumi.
 
Waungwana dunia hii inapoelekea kunatisha sana,kanisani siku hizi imekuwa sehemu ya kijiwe watu kukutana kupanga mambo yao ya duniani,au kuonyeshana fulani kavaa nini fulani kaja na gari fulani na si kwenda kumwabudu Mungu na kufanya Toba!!!!
 
Wapendwa katika BWANA, ninavyofahamu mimi kanisani ni mahali patakatifu sana, pengine kuliko mahali pengine popote ambapo mtu unaweza kufikiria. Sijui kwa waislamu lakini naamini pia kwao msikitini ni mahali patakatifu pia, nahisi ndiyo maana hata viatu hawaruhusu kuingia navyo (mtanisamehe ndugu zangu waislam kama nitakuwa nimekosea). Ni mahali ambapo mtu unatakiwa kwenenda kwa unyenyekevu wa hali ya pekee maana unakwenda kukutana na MUNGU wako. Tujaribu kumpa Roho wa MUNGU nafasi ya kutawala mawazo yetu. Unapoacha simu yako on, maana yake mawazo yako yanakuwa yanafikiria kupigiwa simu au kupata sms na sio kupokea mibaraka ya MUNGU. Sipendi kuhukumu nisije nikahukumiwa lakini nawajibika kusema kuwa tusipokuwa makini na matumizi ya simu tutampa nafasi shetani na kupotea kabisa.
 
Back
Top Bottom