Simu makanisani.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu makanisani....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr. Chapa Kiuno, Sep 14, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wadau! Hili limekuwa tatizo kubwa, maana utakuta kila siku waumini wanaambiwa wasije na simu zao makanisani lakini ndy kwanza hawasikii... Simu nyengine milio ni mikubwa n mbaya zaidi utakuta ni nyimbo za kidunia...

  je! watu hawa ni wastaarabu?
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tabia hii ni mbaya sana.Watu wanaenda kanisani kama fasheni,yani sio kusali bali kama ratiba ya kukamilisha wiki na kwenda kusikiliza nyimbo.Na ndio maana utakuta wengi wanalala usingizi wakati wa mahubiri au mawazo yao hayapo kabisa hapo kanisani,hata kuangalia wenzao wamevaa nini.Cha msingi hapa makanisani kuwe na usimamizi mkali.Ni kazi kweli kuwabadilisha watu mpaka waelewe.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hii kitu inanikera sana, watu hawamuogopi Mungu wao, utakuta mtu yupo kanisani kwanza kaja na Hangover ya jana ananuka mipombe halafu anasinzia muda wote mwisho anakishtuka toka kwenye usingizi wake anachukua simu yake anaanza ku chat, Jamani hapa ndipo nnapo waona ndugu zetu WAISLAM wamestaarabika zaidi hivi uende Masjid halafu una simu inaita au unanuka pombe nadhani bakora za siku hiyo zote zitakuangukia wewe. Tafadhali waungwana ukifika kanisani ZIMA simu yako weka mfukoni mpe muda huo uliopo kanisani MUNGU wako
   
 4. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Uyasemayo ni kweli kabisa! Waislam ustaarabu 100%
   
 5. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Ni kweli mkuu! mwengine anafanya kama sehemu ya kupitia tu akishatoka hapo anaenda kufanya maovu tena.
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Yaani kuchapana bakora ndio ustaharabu, wewe vipi bwana, HUKUMU NI YA MUNGU BWANA na sio kila mtu kujichukulia hukumu yake, mara viboko, mara mawe mara kukatana mikono
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  na jana tu church mdada wa pembeni yangu hakuzima cmu, 2nackiliza mahubiri, tunackia"nataka paja mie hakinitoshi kipapatio"....alitetemeka mana kanisa lilikuwa kimyaaaa, kila mtu aligeuka kuckiliza mlio unapotokea....nadhani sio ustaarabu, unaweza kuizima tu kwa muda huo mchache wa misa.
   
 8. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Duh! huyo naye alizidi... yale yale tunayosema! Ss alitaka apewe paja kanisani?
   
 9. M

  Mary Eric New Member

  #9
  Sep 14, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Biblia inasema twende mbele ya Mungu kwa kicho na heshima,sasa simu inapiga kelele sio ustaarabu, kama unaona una ishu muhimu, basi weka hata silent, utakuta missed kol, then utawatafuta wote waliokupigia. Kwanza unapigia watu makelele wanaotaka kusikiliza ibada.
   
 10. Johas

  Johas Senior Member

  #10
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kamanda!, Hii ni kweli kabisa na leo asubuhi nime-experince the same story pale Mjengo Mrefu. Watu bwana hawamuogopi MUNGU, Mahali kama kanisani ni sehemu pakuheshimiwa kwa uchaji na MUNGU anapendezwa na kufurahishwa kama anabudiwa na kutukuzwa katika hali ya utulivu na uchaji.

  Mimi nakumbuka wakati wa mafundisho kipindi kile, Sister alitusisitiza kuto-ongea unapokuwa kanisani hasa wakati wa ibada!

  Mambo bwana siku hizi tofauti, Watu kwa ukweli wanafanya pale kama ndio kijiwe cha kukutana na kupanga Mishe Mishe zao na kupepeta umbea wao!, Ndio maana hawawezi kuzifunga Simu zao.

  Mbaya zaidi na kinachokera utakuta watu wametoka kanisani tangu misa ya kwanza basi wanapiga soga hapo na kuziba nafasi za parking kwa wale wanaoingia misa ya pili, hii hasa pale mjengo Mrefu!
  Kwakweli si wastaarabu hata kidogo.

   
 11. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Wanafanya waumini wote tuonekane na tabia moja ya kutomtii Mungu.
   
 12. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dr. Chapa Kiuno.. Kwanza jina lako hapo juu ni la madaa sana, na pia kuna watu wanaudhi sana maana kunakuwa kama fashion ya kuonyesha simu zao kwa watu wengine na pia inakuwa ni usumbufu sana kuona kuwa watu wanakwenda na simu kanisani
   
 13. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dr. Chapa Kiuno.. Kwanza jina lako hapo juu ni la madaa sana, na pia kuna watu wanaudhi sana maana kunakuwa kama fashion ya kuonyesha simu zao kwa watu wengine na pia inakuwa ni usumbufu sana kuona kuwa watu wanakwenda na simu kanisani
   
 14. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hilo jina nilipewa na mpenzi wangu wa zamani....
  Simu za kuringisha zipo unyamwezini.
   
 15. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watu wanakwenda kuchukua huko na kuna nazo hapa Bongo na kufanya yake ya unyamwezini
   
 16. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  vipi kuhusu vimini kanisani?
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Vina kuhusu? nanyie wavae basi misikitini....!
   
 18. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kuja na simu kanisani siyo issue, labda waziweke kwenye silence/ vibrate.

  Huwezi kujua inawezekana kuna mtu mahututi, au kuna deal za kanisa vile vile, muhubiri kakwama anatoa taarifa kwaya iendelee kutumbuiza wakati ana negotiate njiani.

  Au kuna madili yanayomuwezesha muumini aweze kutoa sadaka, etc.

  Kwa hiyo hoja ni kuzima/ kuweka silence/ vibrate, si kutokuja na simu.Kuna watu simu ndiyo lifeline zao.
   
 19. M

  Magezi JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nadhani maknisa mengi wenatoa onyo mara kwa mara kwa hiyo kinacho takiwa ni kwakumbusha waumini na washiriki wote kwamba wazime simu wawapo kanisani. Kusahau ni kitu kipo ila inatakiwa kukumbushana mara kwa mara.

  halafu hata sisi waumini inatakiwa tukumbushane, ukimuona mfano mtu amekaa karibu nawe na ana simu si vibaya ukimwambia ..."ndugu umezima simu?..." hii itasaidia kumkumbusha mtu, kuliko kuacha halafu baadaye ikaita na kuleta usumbufu.
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Acha hizo Masanilo, mada imewekwa barazani kila mtu ana haki ya kuchangia na kama mlitaka iwe siri mwambie alieleta mada akaitoe kanisani.

  A
   
Loading...