Simu kutokupandisha signals za voice lakini signals za data zipo juu

Mboya Allie

Member
Mar 13, 2012
93
67
Habari za jioni wakuu, natumia HTC one m7 lakini tangu juzi simu yangu imekuwa kwenye mode ya limited services so siwezi kupiga simu wala kutuma meseji, lakini cha ajabu matumizi mengine ya data yanafanya kazi kawa kawaida na signals strength zipo juu..Nikibadirisha laini, signals( voice) zinarudi Kama kawaida. Naomba msaada wenu kwa hilo.
 
hio line kama ni ya 4g mitandao yetu haina vo-lte (signal za sauti za 4g) hivyo utapata data tu. kusolve hili nenda setting halafu more network halafu mobile network kwenye network mode eka auto ili ijibadili yenyewe.
 
hio line kama ni ya 4g mitandao yetu haina vo-lte (signal za sauti za 4g) hivyo utapata data tu. kusolve hili nenda setting halafu more network halafu mobile network kwenye network mode eka auto ili ijibadili yenyewe.
Asante chief, nilishafanya hivyo halafu natumia line ya kawaida tu..sasa nashindwa kuelewa tatizo lipo wapi kwani imetokea ghafla tu, natumia voda so nikiweka laini ya Tigo tatizo linakuwa palepale ila nikiweka laini nyingne ya voda signals zinatokea.
 
Kaka natumia HTC M7 kama yako.ina hilo tatizo sana ukitumia line ya Tigo. Tumia mitandao mingine kaka. Mi natumia Voda na ipo vizuri sana
 
Sometimes huwa ni issue ya Modem iliyokuwa flashed kwenye simu yako, nyingine ziko "bias" kimtindo. Personally niliwahi kukutana na hiyo case na nilivyokuja kufatilia nikakutana na hayo majibu ya modem from xda!
 
Back
Top Bottom