Simu kutoka kwa baba mkwe

Pole kaka, ila mkeo ndio mwenye makosa kwani yeye anajua mila za kwao zaidi yako, na anajua jinsi inavyokuwa kwenye siku za kuzaliwa kwa wazazi wake,kwanini asikuambie? Na huyo baba mkwe pia sio mstaarabu,angepaswa ampigie mwanae tena si kwa kufoka. Angemuuliza tu,mwanangu,mbona hatujawaona kwenye sherehe? Na sio kukupigia wewe tena kwa kukukaripia eti mböna hamjaja wala kuleta zawadi!! Puuuuuuh!!
 
Mke mwenyewe hakukumbuka siku ya kuzaliwa ya mzazi wake habari gani wewe? Haikustaili lawama kabisa katika hilo ukizingati maisha yetu wabongo ila kama lawama zimetolewa ilibidi zipelekwa kwa mtoto wao(mke wako) then ndo zije kwako, anyway vuta siku kadhaa then kasawazishe mambo kiutu uzima. Good luck
 
mkuu unaishi ukonga, baba mkwe anakaa mbezi beach... anyway, ukienda ROMA ishi kama warumi..
 
Mkuu Bak kwa jinsi tunavyoishi na wakwe zangu hatuna matatizo na tumekuwa tunashirikiana katika shida na raha. Natumekuwa pale tunapokumbuka isipokuwa nimepata picha moja kwamba kumbe ukiona mtu anakupatia zawadi jua na wewe unatakiwa urudishe kwa kile kiwango.. am wondering ndo maana watu wakati wa harusi ubwaga machozi wakijua fika zile zawadi lazima zilipwe... je ni sahii kukataaa zawadi kama unajua hutaweza kuzilipa?
Kajuni pole kwa hilo!
Niende nje ya maada kidogo, Hiyo ID yako inabidi tufahamiane, isije ikawa mimi ndio mkweo! Ghwalamsha?
 
La msingi wewe omba msamaha tu,
hilo la mtu mzima kudai zawadi ya b/day nalo ni neno pia,
jipange this weekend nendeni pale na mkeo na kahela kwenye
bahasha omba samahani waambie mlijisahau tu.
 
Binadamu tumeumbiwa lawama, siumeshamuomba MSAMAHA? Sikushauri ufanye chochote, msamaha unatosha sana, subiri birthday yake ya mwakani na hapo ni hadi ukumbuke ndo upeleke zawadi. Mambo ya kina camerun na akina siye wapi na wapi

La msingi wewe omba msamaha tu,
hilo la mtu mzima kudai zawadi ya b/day nalo ni neno pia,
jipange this weekend nendeni pale na mkeo na kahela kwenye
bahasha omba samahani waambie mlijisahau tu.
 
Back
Top Bottom