Simu kutoka kwa baba mkwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu kutoka kwa baba mkwe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kajuni, Jun 23, 2012.

 1. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Wana JF kwanza kabisa shalom. Ni jumamosi tulivu pande za hapa Dar na hali ya hewa ni manyunyu manyunyu! Nikiwa katika harakati za kumalizia vipolo vya kazini mara napokea simu kutoka kwa baba mkwe. Namsalimia kwa heshima na tahadhima kwani ndiye mzaa chema (mke wangu). Ama baada ya salamu baba mkwe ana anza kunishutumu kwamba sisi pamoja na binti yake hatuwaheshimu na hatuwajali kwa sababu jana tulishindwa kupeleka japo ua kwa mama mkwe kama zawadi ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa. Baba mkwe aliendelea kutiririka kwamba sisisi tumekuwa na mkono wa birika! Na hata siku moja hatujawahi kuwapa zawadi japokuwa wao wamekuwa mstari wa mbele katika hilo.
  Kikubwa ni kwamba mimi nimezaliwa na kuishi na kusomea kwenye hizi shule zetu za kayumba! Uaratibu huu wa kushelekea siku za kuzaliwa nilianza kukuana nao nikiwa chuo kikuu. Sikuwahi kushelekea katika kukua kwangu wala sikumuona baba na mama yangu wakitunulia zawadi wakati wa hii siku nyeti. Sina nia mbaya ya kutopeleka zawadi kwa mama mzaa chema lakini mazingira niliyokulia yanachangia sana mimi kutokuwa sensitive na hizi ishu!
  Sasa wandugu nifanyeje kwani Jumamosi leo nimeambulia lawama na shutuma.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  inabidi mke wako akaongee na wazazi wake, mambo ya kubebeshana nyani ukubwani kweli haifai.

  Hizi mila za kukopi na kupaste wala hazina mashiko kihivyo, je siku akilazwa ukashindwa kwenda muona si utanyang'anywa mke?

  Kukwazana bure tu kwa kweli, ila ningekuwa mie nisingemkopesha hata kidogo.
   
 3. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Pole sana,subiri siku zipite kidogo,then kamuone na ukaongee naye kwa maneno ya utararibu na heshima..nadhani hapo utakuwa umerekebisha mambo..
   
 4. L

  Lady G JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 517
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kabisa my dear, umenena vyema mdada
   
 5. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Sasa kama mkeo amekulia kwenye familia ya kubofya kwa nini asikuelekeze? Angalia mkuu usije ukanyang'anywa mke bure
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  wazazi wanapoanza kuiga mambo ya ughaibuni ni shida mnoo...ila kama ni ishu ya upande wa pili na weye unataka kushiriki ni bora ukajificha nyuma ya mkeo ili usihusike moja kwa moja...kwani utakua ni mchezo kila siku ...leo mama mkwe kesho dingi. kesho kutwa kipaimara..wiki ijayo harusi...THE LIST GOES ON
   
 7. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,366
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Zipokee tuu,lawama kaumbiwa mwanadamu!!!
   
 8. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,960
  Likes Received: 20,297
  Trophy Points: 280
  Duh! Hatupishani sana mkuu, binafsi hata siku yangu ya kuzaliwa mara nyingi nakumbushwa na mail za JF, hapa nitakumbukaje d'day za mama au baba mzaa chema . Pole mkuu:sad:
   
 9. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Sio rahisi kunyang'anywa mke. Walitoa kwa hiyo maji yalishamwagika! Hapa ni kuhifadhi tu heshima na mahusiano mazuri. Hakuna hoja ya kisheria hapo.
   
 10. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Asante sana mkuu kwa kweli nimebaki mdomo wazi na ikizingatia mie naishi Ukonga na wakwe wanaishi Mbezi mbichi na kazi ni posta sasa fikiria mziki wa foleni eti kuwaisha ua kwa mama mkwe?
   
 11. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Mkuu hata ya kwangu mie huwa nakumbushwa na hii mitandao... hata wazazi wangu wenyewe sikuzao za kuzaliwa huwa nasahau
   
 12. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Wakuu inaonekana kwamba ukipewa kitu lazima urudishe!!!
   
 13. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Mkuu hii mambo imenisubua sana sana huu uzungu naona unakuwa shida juu ya shida
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,692
  Trophy Points: 280
  Wewe na mkeo badilikeni maana kwa wakwe hili jambo linapewa uzito mkubwa.
   
 15. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kajuni sikubaliani na majibu ya Kongosho rafiki yangu wa moyoni. Kwanza kabisa nafikiri mkeo naijua vyema hali halis ya nyumbani kwao na utaratibu mzima. Kama na yeye anauona hauna mantiki kama wengi wetu hasa huu wa kusheherekea bday ni sawa pia. ila tusione kwamba ulipaswa kumjibu ama ukajipange kumrushia makombora mkweo kama alivyoonyesha Kongosho na namshukuru Mungu sana kwamba asiyo yeye manake angenitia aibu huyu.

  ushauri wangu kwako, kwanza kabisa tulia kimya upepo huu upite kabisa na hali iwe shwari kabisa. kisha siku weye na mkeo mjipange mwende kuwaona wakwezo mkiwa mmejifungasha hata kwa kajisukari tu. siku mtakayokwenda mtaongea nao kwa upole na heshima juu ya kughafilika kwenu kuhusu tarehe ya mama ya kuzaliwa. Naamini kwa wazazi wastaarabu watawasamehe na mambo yataendelea kama kawaida.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Zawadi haiombwi wala kulazimishwa, ila pia kukosa fadhila si maungwana.

  Ungepeleleza familia ikoje na wakwe wanataka nini kabla ya kuoa.

  Inaonekana wakwe zako wanaweza kuwa na lao zaidi ya hili la zawadi.Haiyumkiniki mtu mzima kulilia zawadi kama mtoto anayelilia peremende.
   
 17. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Mkuu Bak kwa jinsi tunavyoishi na wakwe zangu hatuna matatizo na tumekuwa tunashirikiana katika shida na raha. Natumekuwa pale tunapokumbuka isipokuwa nimepata picha moja kwamba kumbe ukiona mtu anakupatia zawadi jua na wewe unatakiwa urudishe kwa kile kiwango.. am wondering ndo maana watu wakati wa harusi ubwaga machozi wakijua fika zile zawadi lazima zilipwe... je ni sahii kukataaa zawadi kama unajua hutaweza kuzilipa?
   
 18. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Mkuu kiranga hapo ndo pana nishangaza kwani inaonekana kwamba kuna jambo nyuma ya pazia...
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kajuni hakuna ubaya wowote wa kubadilishana zawadi kati ya wanandoa na in laws wapande zote mbili. Kama alivyosema gfsonwin mkeo anajua hali halisi ya kwao inapokuja kwenye mambo ya kusherehekea Birthday kwa hiyo ni vizuri kuendelea kulipa uzito jambo hilo hata kama nyie wenyewe hamlifagilii. Swali kama mmejaliwa watoto je nao birthday zao zinapita kimya kimya bila hata card au kasherehe kadogo?

  Sidhani kama ukipewa zawadi ya shilingi laki moja nawe inabidi urudishe zawadi ya kiasi hicho kwani waswahili walisema mtu hujikuna pale mkono wake unafika...Hivyo wakwe zako bila shaka wanafahamu financial position yenu kama uwezo wenu ni zawadi ya shilingi 50,000 basi hawataona tatizo lakini kama kweli mna mkono wa birika pamoja na kuwa mna vipato vikubwa basi hapo pia inabidi mbadilike na kunyoosha mikono yenu ili iwe mirefu zaidi.   
 20. mito

  mito JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,613
  Likes Received: 1,992
  Trophy Points: 280
  Kajuni haya mambo ya ku-copy na ku-paste yanatusumbua wengi. Mi na wife wangu tumejitahidi kuwa tunawafanyia besdei angalau watoto wetu, cha ajabu huwa tunajikuta wote tumesahau mpaka tunakumbushwa na marafiki zetu wa nje kwa emails! watoto bado wadogo hawawezi kukumbuka ili watushtue. Kwa asili ni utamaduni ambao si wetu so unaleta shida sometimes
   
Loading...