Simu iliyobadilisha maisha yangu

Simu iliyobadilisha maisha yangu

Theodora

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2009
Posts
806
Reaction score
584
Nawasabahi wanaMMU.


Ni Jumapili kama hii wiki moja imepita nilipokea simu ambayo imebadilisha maisha yangu na mtazamo wangu kuhusu mahusiano. Well, nilipokea simu na upande wa pili nikasikia sauti ya mwanamke, na kwa sauti ni mtu mzima.

Aliongea mengi na mwisho akaniambia kama unataka kujua zaidi kuhusu mume wako nitafute. Basi Jumatatu, akanipigia tena na nilikuwa nasita kuonana naye, basi akaanza kuniambia wewe hauko serious.

Basi kama wazungu wanavyosema - Curiosity killed the cat, but satisfaction brought it back.

Imagine kumeet na mtu haumfahamu then mawazo ya tindikali na mambo mengi yakanijia kichwani, nikaanza safari kuonana naye huku nasali novena takatifu.

Well sikuamini nilipokutana naye - ni mama mtu mzima na age diff kama 18 - 20 years. Basi nikampa heshima na kukaa, nikamuuliza mama ishu ni nini na ana mahusiano gani na mume wangu (nikidhania ni biashara) Aisee, mapigo ya moyo yalisimama sekunde kadhaa aliponiambia wanamahusiano ya kimapenzi.

Na aliponiona kama nashangaa as in seriously, akaniambia nijuwe na yeye pia ana hamu na hajakuwa na mwanamume 4 years baada ya ndoa yake ya miaka 28 kuvunjika.

Akanitolea na picha kabisa na roho inamuuma kweli kuhusu mume wangu na anajitetea hakumwambia ana mke na watoto.


To cut a long story short, wamekuwa na mahusiano miezi 3 na anavyoongea alikuwa ameambiwa mahusiano yaishe lakini she was not happy na inamuuma sana. Mwisho akaniambia mi ndoa ya 28 years imevunjika sembuse ww wa miaka michache.

Basi angesubiri na mimi nifikishe hiyo 28 na ndo amshambulie huyu kiumbe dhaifu. I am so angry, not for me only but for all those men who cheat on good women na wanawake ambao wanavunja ndoa za watu kwa ajili hawana self control au basi watafute wa rika yao.


There are some battles worth fighting but this one am throwing in my towel. Hivi mtu akikuambia ni shetani - seriously miezi 3 ni yeye tu shetani anamwandama?

Kuna mambo magumu napitia wakati huu, everything is looking down but this put the last nail on my coffin.


Swali - Why would a man take the risk of losing a diamond to pick stones?
 
Aisee pole sana ma dia be strong yani nakuona jinsi unavo jifeel aisee its so hard huyo mama si mtu mzima kabisa jamani hata haya ana si bora wangefanya tu kisiri na huyo.hubby wako ni kwamba amekosa sana hadi kujitumbukiza kwa mtu mzima be strong aisee usikate tamaa this is life tamaa ime cost na kuharibu ndoa nyingi but hiyo ni mitihani tu you will overcome
 
Hilo ni jaribu la kwanza gumu kwenye ndoa yake na bila shaka ni ndoa chache hazipitii hilo!

Pengine ni wengi huwa hawafikirii kupatwa na hili swala lakini kulikosa kwenye miaka yote ya ndoa 50%

Unatakiwa kutumia akili sana na busara kwenye hilo lasivyo ndoa yako itavunjika!
Msamehe ameona wewe ni wa muhimu ndio maana aliamua kumuacha huyo Mama!
 
Pole sana kwa yaliyokukuta lakini hakuna sababu yoyote ya kufanya maamuzi ya haraka ili kuivunja ndoa. Huyu mama anataka kuvunja ndoa yako kwa mategemeo kwamba mumeo atabaki naye yeye vinginevyo sioni sababu ya yeye kukutafuta ili akwambie mapungufu ya mume wako. Mume wako baada ya kumwambia penzi lao la miezi mitatu limefikia ukingoni akaamua amkomoe ili aharibu ndoa yenu.

Kuwa na subira na uwe na tayari kumsamehe mumeo hasa kama anaona amekukosea kwa aliyoyafanya katika hiyo miezi mitatu. Huyo mama asingeambiwa penzi la miezi mitatu limefikia ukingoni wala asingehangaika kukutafuta hata kwa sekunde moja. Pole sana.
 
Pole sana na mungu akupe wepec kwenye ndoa yako .magumu yote yatapitaa mtegeme mungu hakuna linaloshindikana kwake ndugu
 
Mmmh... Pole aisee, endelea kusali zaidi ya ulivyosali wakati unakwenda kuoanana na huyo mama. Mungu ni mwaminifu na atakupatia busara kutatua hilo jambo!
 
Pole mpenzi but kumbuka kunawanawake ving'ang'anizi akimtaka mwanamme atafanya juu chini ampate.kuwa strong don't give up jipe moyo msamehe bure mmeo mukalishe chini muulize umemkosea nini mpaka afanye ivyo then rekebishaneni muendeleze maisha yenu.hapo mwanamme ndo anatakiwa awe na msimamo.zaidi ya yote omba mungu arejeshe furaha ya ndoa yako
 
Tatizo ni hakuna mtu anayeweza kujua kwa uhakika kuhusu kama mwezake ni mwaminifu 100%.

Kwa hiyo usikute hata mumeo hajui kwa uhakika kama kweli wewe ni mwaminifu kwake.

Kutokujua kwa uhakika uaminifu wa mwenzio ndo moja ya pitfalls za mahusiano ya kimapenzi/ kindoa.

Hivyo, ukishaamua kuingia kwenye ndoa au mahusiano ya kimapenzi, kubali tu kuwa utovu wa uaminifu na uchepukaji ni sehemu yake.
 
Pole sana kwa yaliyokukuta lakini hakuna sababu yoyote ya kufanya maamuzi ya haraka ili kuivunja ndoa. Huyu mama anataka kuvunja ndoa yako kwa mategemeo kwamba mumeo atanaki naye yeye vinginevyo sioni sababu ya yeye kukutafuta ili akwambie mapungufu ya mume yako. Mume wako baada ya kumwambia penzi lao la miezi mitatu limefikia ukingoni akaamua amkomoe ili aharibu ndoa yenu.

Kuwa na subira na uwe na tayari kumsamehe mumeo hasa kama anaona amekukosea kwa aliyoyafanya katika hiyo miezi mitatu. Huyo mama asingeambiwa penzi la miezi mitatu limefikia ukingoni wala asingehangaika kukutafuta hata kwa sekunde moja. Pole sana.

Really BAK?

Yaani unataka amsamehe halafu aendelee kuishi na huyo mume mzinzi?

Wewe ukigundua mkeo anamegwa na mtu mwingine utamsamehe tu na kuendelea na maisha yeu?

Kama ni hivyo kweli watu mna moyo!
 
Last edited by a moderator:
don't give up on your man. huyu ajuza ni plani zake hizi kuzungumza na wewe ili umuachie na inavyo onyesha anajua kuwa mume wako hana nia ya kukaa nae
 
men are polygamous in nature, adui wa mwanamke ni mwanamke mwezie, hv unapomkubali mume wa mtu wht do u expect?? awe nawe daima!! aaggrrrr, anyway tuliza kichwa give it tym dont make any decision whn ur angry, hawa watu bwana ni kuwaombea tu.
 
sala zAko ndo mkombozi wako
jiulize huyo mtu mzima ovyooo
kajiamini nini mpaka kakufata kukupa live?
je km ni muong?picha zipo hata za kuunganishA!
usikurupuke anza uspy taratibu
ukweli utaujua
mi mwenzio (natoa ushuhuda )niliona mme wangu hana uhuru na simu yake ikipgwa silence tena saa 6 usiku sikuuliza nikasubir kalala nikachuku a simu nkakuta 7misd call,3dialled calls,4 ricvd calls za mtu mmoja
nikachukua namba asubuh kaondoka nkapiga mdada kapokea nkauliza unamjua fulani akasema simju nkamwambia sasa umjue usimjue huyo mtu ana mke na ana watoto na mi ndo mkewe siondoki leo walA kesho
dada akaanza kujishauashaua pale nsamehe mi kaniAmbia hana mke il sijatembea nae
nkamwambia mi sjui mtembee mruke ujumbe umeupata tena mwambie mkeo kanipigia
akaomba msamaha
AM SORY STORY NDEFU ila nataka nkwambie km ni kweli huyo mmama anatoka nae
hao ndo wanaume na ktk dunia hii UKITAKA MKAMILIFU MUUMBE MWENYEWE
 
Kwanza pole sana rafiki! Me pia km ulivyoshauriwa be strong na zaidi ya kuwa imara unahitaji utulivu wa akili kwa kiwango kikubwa sana! Lkn pia kumbuka hapa sisi tunashauri kutokana na kile ulichokileta hapa. Pengine tungekuwa na uwezo wa kupata maelezo kutoka kwa mumeo,ingesaidia zaidi kukujenga uwezo wa namna ya kurudisha ndoa yako ktk mstari. Mara nyingi ukiona mwanandoa mmoja anam-cheat mwenzake ujue km ni mke atakuwa amechangia kwa 50% halikadhalika mume. Hivyo,wakati mnatafuta suluhisho,jitafakari pia mapungufu yako ili umfanye mumeo asitamani kutoka nje.
 
Nimekupendaje weye!!! Hongera sana kwa msimamo wako madhubuti.

sala zAko ndo mkombozi wako
jiulize huyo mtu mzima ovyooo
kajiamini nini mpaka kakufata kukupa live?
je km ni muong?picha zipo hata za kuunganishA!
usikurupuke anza uspy taratibu
ukweli utaujua
mi mwenzio (natoa ushuhuda )niliona mme wangu hana uhuru na simu yake ikipgwa silence tena saa 6 usiku sikuuliza nikasubir kalala nikachuku a simu nkakuta 7misd call,3dialled calls,4 ricvd calls za mtu mmoja
nikachukua namba asubuh kaondoka nkapiga mdada kapokea nkauliza unamjua fulani akasema simju nkamwambia sasa umjue usimjue huyo mtu ana mke na ana watoto na mi ndo mkewe siondoki leo walA kesho
dada akaanza kujishauashaua pale nsamehe mi kaniAmbia hana mke il sijatembea nae
nkamwambia mi sjui mtembee mruke ujumbe umeupata tena mwambie mkeo kanipigia
akaomba msamaha

AM SORY STORY NDEFU ila nataka nkwambie km ni kweli huyo mmama anatoka nae
hao ndo wanaume na ktk dunia hii UKITAKA MKAMILIFU MUUMBE MWENYEWE
 
Really BAK?

Yaani unataka amsamehe halafu aendelee kuishi na huyo mume mzinzi?

Wewe ukigundua mkeo anamegwa na mtu mwingine utamsamehe tu na kuendelea na maisha yeu?

Kama ni hivyo kweli watu mna moyo!

Pamoja na hayo kumbuka hamna mkamilifu chini ya jua.je akimuacha ataacha wangapi.anaweza akamuacha huyo akapata Bomu zaidi.
Apo yahitaji tu uvumilivu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom