Simu Fake za IPhone, HTC, Samsung etc zaingia Bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu Fake za IPhone, HTC, Samsung etc zaingia Bongo

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Ishina, Oct 14, 2012.

 1. Ishina

  Ishina Senior Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii ni kwa wana JF wote.


  Hivi karibuni zimeingia simu nyingi 'fake' za aina ya IPhone 4, 4S, and 5 na watu wengi saana wameumia/kulizwa/kuingizwa mkenge kwa kujua kuwa unanua IPhone ya kutoka kwa marehemu Stive Job, kumbe unauziwa kitu cha kichina, ambacho hakina hata thamani ya TSh. elf50. Watanzania hebu tuwe tunashirikisha akili zetu hata kidogo, wewe simu ‘brand new’, ikiwa ndani ya boksi, ki halali kabsa inauzwa sio pungufu ya $850, alafu mtu anakuuzia kwa laki 4 wewe hushituki hata kidogo?! Mtu anakuambia eti nimeiiba kwenye maduka ya Mlimani City na wewe unakubaliana nae?!! Ni ukweli kuiba pale mlimani city, inawezekana lakini sio kirahisi kihivyo, kama hawa wachovu wanaouzia hizo simu, ukizingatia mengi ya maduka pale Mlimani city yanatumia high tech. Security system kulinda mali zao.

  Simu hizo IPhone 4, and 4S, 5, HTC, etc zipo nyingi saaana mtaani na watu wanazinunua kama njugu. Mimi jamaa yangu mmoja kauziwa hiyo simu (I Phone 4S) na kwa mara ya kwanza nilipoiona kwa macho na kuishika tu nikagundua kuwa ni kitu fake bila hata ya kuanza kuangalia App. Zake. Mimi nimetumia hizi IPHone (3g, 4 and 4S) kwa zaidi ya mwaka na nusu, nazijua vizuri na sio rahisi mtu kuniibiia kizembe namna hiyo.


  Hawa jamaa (wachakachuaji) wamefoji kuanzia simu yenyewe hadi ma-boksi na yanaonekana kama kweli ni ya IPhone au HTC. ILa kwa mtu ambaye anatumia IPhone ni vyepesi saana kuzigundua.


  Ushauri wa Bure kwa wanataka kununua iPhone


  1. Kama utakutana na watu ambao wanauza hizo simu ni vizuri ukafuta mtu ambaye anazijua hizo simu akusaidie kukwambia kuwa ni fake au genuine (mimi nimesaidia jamaa zangu 2, mmoja alitaka kuuziwa kwa lakin4 mwingine 5), usiingie kichwa kichwa kisa umesikia ni ya deal;


  2. Pili kama una computer ambayo ni connected with internet, ichomeke hiyo simu kwenye computer kwa kutumia cable ya charge yake na kama ni genuine itakuletea program ya ITunes kwenye computer yako (au unaweza ku-downloda hiyo program kutoka Apple - iTunes - Everything you need to be entertained. ni free program; kama ni simu fake haiwezi kuwa recognized kwenye huo mtandao; na


  3. Simu nyingi za IPhone ambazo ni fake zinakuwa hazina application za ‘ITunes’ pamoja na ‘App Store’, kama hizo Application nilizozitaja hazitaonekana (au hazipo) kwenye simu yako, kuna uwezekana mkubwa kuwa simu yako ni fake. Hizo ni app muhimu sana ambazo zinaifanya simu yako iweze ku connected katika mtandao wa Apple na kuwa recognized na watu wa apple;


  Kwa kuanzia naomba nichangie hayo, hopefully wengine watachangia zaidi na kupeana mwanga zaidi kuhusiiana na hii mizigo fake ambayo imeingia hapa mjini ndugu zetu kibao tu wanalizwa, na maagenti na matapeli wengine wengi tu wa hizo ‘fake products’ wapo hapa hapa JF.
   
 2. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  nashukuru ndugu,kwa kutustua.
   
 3. Mmombo

  Mmombo Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka Poa sana kwa ushauri wako Munguakubariki
   
 4. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kuna mzee mmoja mhindi huwa ana tumia starlet au land cruiser ya blue, huwatapeli watu lwa kuwauzia simu fake. Mara nyingi huwa anapatikana maeneo ya Mlimani City ila hashuki katika gari, hudai ana ndugu mgonjwa na fedha za matibabu zimepungua hivyo anauza simu kwa bei ya hasara.
   
 5. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao wanaotapeliwa wamezowea kwani Maduka hawayajui? Kuna watu wanatoka nyumbani kuja kununua simu kariakoo, anazunguka muda mrefu sana kwa kutegemea kupata simu Kubwa nzuri kwa bei nafuu mwisho ankutana na wajanja wanaokaa mbele ya maduka yanayouzwa simu anauziwa sabuni kwa tamaa zake, Watu kama hawa sio wa kuwaonea Imani, kwanini uwe mpumbavu kiasi hicho tena unaibiwa maduka kibao yanakuzunguka, hivi karibuni niliwaona majeshi tena wamevaa magwanda hawaoni hata aibu wameshauziwa sabuni na wajanja, wanabaki wawatafuta , kumbe Hawajui Kama wao Ujanja uko msituni sio mjini.
   
 6. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  asante sana mkuu. kesho nilikuwa napeleka laki 3.5 dukani ili nichukue iphone 4s kumbe ni fake? jamaa kanionesha kabisa na box kama original vile. ina charter ya califonia usa. itabidi nichunguze kama app store na ittunes siichikui. eti anasema wananunua bei chee
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  mm mwenyewe nlikutana na kijana mmoja pale posta akaniambia ana i phone 4s niliposhika tu nkamwambia wewe mm nimetoka mbele nazijua so kama unataka elfu 50 nkupe ila siwezi kununua mzigo wa china huu nkasepa zangu.
   
 8. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tena hizi fake zina redio kabisa, iPhone original haina redio
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Watawachukuwa wa kwao!

  Hapo hatuingii ng'o!

  Tunashukuru kwa taarifa Mkuu!
   
 10. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Nijuavyo mimi, Iphone 4s used huku US ni dola 200 na hazijatumiwa kwa more than a year (most of them less than 6months with film and otterbox). Kama umempata mtu anayesafiri ukampa kumi, basi kwa laki tan unaweza ukapata milioni in like two days.

  It's possible for 4S kuwa 500,000/= au hata 400,000/=. I've sold a lot of'em no complaints.
  Kuhusu iphone 5 kuwa laki tano, thats just crazy .... Iwon't even look at them.
   
 11. b

  bdo JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante kwa taarifa, hivi hakuna njia ingine rahisi ya kutambua kama kitu ni genuine au fake, maana hapa inatakiwa nikitaka kwenda kununua hizi simu lazima niwe na computer? haya tumuombe Mungu, au weka simu yako hewani ili nikiwa na kitu mkononi niweze kuomba ushauri
   
 12. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Thanx mtoa mada
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Jamaa alitaka kuniuzia Samsung Galaxy S 2 fake, akanambia ni original. Nikatoa yangu original mfukoni nikamuuliza "ni kama hii?" Jamaa akaondoka huku anacheka.

  Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
   
 14. Ishina

  Ishina Senior Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama utaenda kununua hiyo kesho, jaribu kuwa makini sana mkuu, na kama inawezekana mshirikishe mtu ambaye anazijua vizuri, kwani ni vyepes mno kujua I Phone fake
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Wajinga Ndio Waliwao!!
   
 16. Ishina

  Ishina Senior Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mdau Kobello
  Hapo kwenye red, Nia na lengo langu ilikuwa kuwa-tahadhalisha wadau wasiibiwe ki-rahisi kwa kuuziwa simu fake, wakati wakijua wananua simu original, tena 'Brand New' zikiwa ndani ya maboksi. Vilevile sijazungumzia Used Phones na sikuwa kwenye mjadala wa simu aina gani inaweza kupataikana kwa bei ipi na wapi.

  Anyway, hata kama mdau akiipata hiyo simu kwa $200 au hata $50 iwe brand new au used naendelea kushauri 'atumie akili za mbayuwayu na achanganye za kwake'
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sure watu wanahitaji kuwa makini kama sio mzoefu unaingizwa chocho chafu
   
 18. Ishina

  Ishina Senior Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mdau bdo

  sio lazima uwe na computer wakati unaenda kununua hizo simu, kama ingekuwa hivyo mbona ingekuwa balaaa kwa sisi ambao tunatumia desktop (yaani ubebe monitor, cpu, mouse, keyboard, UPS etc, uende navyo vyote kwenye duka la muuza simu Kariokoo/Posta). Kifupi ni kwamba Kama una jamaa ambaye anazijua hizo simu jaribu kum-consult kabla hujanunua.

  Unaweza kuni PM nikakupatia namba yangu ya simu kama una hitaji msaada wa kuitambua hiyo simu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. b

  bdo JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Nimekupata, mkuu and umenena sahihi nitakucheki
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. tete'a'tete

  tete'a'tete JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 474
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nilikuwa maeneo ya kumekucha kwenye salun moja ya kike basi wakaja vijana wawili mmoja ana akaingia na simu Samsung Duos Galaxy white ina two lines but nilivyoiona tuu nilijua fake jamaa anataka ths 150,000 basi yule mwingine akiwa kwa nje akatoa Iphone 4s 400,000 completely fake kabisa huwa nimesikia wana mchezo wakiingia mahali wakiona watu mmezubaa na mna simu za ukweli kuna perfume huwa wanapulizia through kwenye hayo mabegi basi wote mnasinzia wanachukua kila kitu kwa hiyo jamani muwe makini sana na wizi huu hata pale mlimani city umekithiri sana tena kuna dada mmoja anavaa ushungi tena muogopeni...
   
Loading...