Simtaki mume wangu kabisa kimapenzi, akili yangu ipo kwa boyfriend wangu

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,408
Nina miezi 8 tu kwenye ndoa lakini nimemkinai huyu mwanaume hatari. Akiingia chumbani harufu ya mwili wake (body scent) ikinijia tu mimi naingiwa na hasira na hapo hapo moyo unajikunja kabisa.

Usiku nakosa usingizi kabisa na kuanza kujuta kwanini niliamua kuolewa na huyu kaka.

Namfanyia visa anichokoze nipate sababu ya kumuacha lakini busara, upole na hekima yake vinanipa wakati mgumu sana.

Kuna wakati naamka usiku naingia chooni na simu nampigia video call boyfriend wangu ili tu nimuone au tuzungumze (japo kwa kunong'ona). Basi tutaangaliana kwa muda hata wa dakika kumi halafu narudi kitandani.

Nampenda toka moyoni boyfriend wangu huyu. Sikutaka kuolewa naye kwasababu hela hana, nikaamua niolewe na huyu mwenye hela.

Sasa moyo wangu haumtaki kabisa. Najilazimisha lakini nimeshindwa.

Naombeni ushauri nifanyeje?
 
Sometimes love is not all about money but feelings that comes inside your heart so hapo umebugi mwenyewe na ushauri mzuri kwako its you to change your mindset. Kaa na mumeo chin then mwambie ukweli kutoka moyoni then wenda akakupa nafasi ya ww kusepa but bora ukafanya maamuzi mapema kuepuka lawama baadae.
 
Nina miezi 8 tu kwenye ndoa lkn nkmemkinai huyu mwanaume hatari. Akiingia chumbani harufu ya mwili wake (body scent) ikinijia tu mm naingiwa na hasira na hapo hapo moyo unajikunja kabisa.

Usiku nakosa usingizi kabisa na kuanza kujuta kwann niliamua kuolewa na huyu kaka.

Namfanyia visa anichokoze nipate sabb ya kumuacha lkn busara, upole na hekima yake vinanipa wakati mgumu sana.

Kuna wakati naamka usiku naingia chooni na simu nampigia video call boyfriend wangu ili tu nimuone au tuzungumze (japo kwa kunong'ona). Basi tutaangaliana kwa muda hata wa dakika kumi halafu narudi kitandani.

Nampenda toka moyoni boyfriend wangu huyu. Sikutaka kuolewa naye kwasabb hela hana, nikaamua niolewe na huyu mwenye hela.

Sasa moyo wangu haumtaki kabisa. Najilazimisha lkn inimeshindwa.

Naombeni ushauri nifanyeje???
Ngoja siku mmeo akikuacha usianze kujuta, utufungulie Uzi hapa kuomba ushauri!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom