Simplicity MMU Award

Simplicity MMU Award

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,664
Wakuu.

Nimeona maadili ya watu yanazidi kuporomoka kwa kasi sana hasa humu MMU. Mbaya zaidi, haya maadili mabaya ambayo yanaibuka kwenye mitandao kama Jamii forums yanasambaa kwa kasi ya ajabu mpaka mitaani.

Unaweza kuta umepanda mbegu ya maadili mabovu humu halafu ikamea na kukomaa mpaka kiasi cha kwenda kuwaathiri watoto wako, ndugu, jamaa na marafiki.

Mie mwenyewe ni kama mwathirika wa hizi tabia kutokana na kuambukizwa na MMU members, ila nimeweza kujitambua na kujisimamia na sasa nimerudi kwenye mstari.

Nilikuja mtu safi kabisa humu, lakini baada ya kukutana na magarasha ya mathreads na wengine, nilijikuta tabia yangu inayumba.

Ili kujaribu kufisha hii tabia chafu iliyoonea humu sihitaji kutoa maelezo mengi, angalia comments na threads za watu, naomba uongozi wa MMU au Jamii forums uanzishe MMU Award.

Ambayo itakuwa inatolewa kila mwisho wa mwaka kwa mwanammu mwenye maadili mema. Hii itasaidia sana "kudemotivate" tabia chafu na hulka mbaya za kuzimuni zinazoendelea humu, hasa MMU.

Kama Jamii forms hawawezi kuanzisha hii award, basi wanipe nafasi ya kuongea nao ili mie nianzishe Simplicity. MMU Award. Nitaitoa kila mwisho wa mwaka, tarehe 31 Desemba na kumkabidhi mwana MMU mwenye maadili bora kabisa,

Award hiyo itakuwa sio chini ya mil 2 za Kitanzania. Mshindi atapatikana kwa njia ya kura na kuidhinishwa na bodi maalumu itakayoundwa.

Nawasilisha na kusubiri mawazo yenu.
gfsonwin, AshaDii na MwanajamiiOne wako wapi siku hizi.
 
hiyo award naomba ikuje kwangu,na naomba kuwa mwenyekiti katika kamati ya maadili...nawasilisha!!!
 
mimi nilikuwa sijui Simplicity. kama hapa mmu kama kuna watu wanatabia mbaya za kuambukizana, itabidi nami nijiangalie kama niambukizwa...
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha ha usitake tuigize na thread zikawa na one page .... kuambukizwa tabia nikutokana na upoyoyo wako kichwani na wala si kingine..... sasa award ya maadili mema kwenye jukwaa la mapenzi eeeh eh wakati watu mapenzi mnachukulia si maadili ndiyo maana yanajadiliwa kwa tafsida,... labda AWARD KWA WANAOCHANGIA WAZI WAZI BILA KUOGOPA HAPO SAWA
 
tabia hawambukizani ,labda kukamatiwa akili ndo kupo
 
Khaa!! Labda ungefafanua maadili mabaya ni yapi na mema yapi. Kwani isije kuwa umejichanganya
 
ha ha ha ha usitake tuigize na thread zikawa na one page .... kuambukizwa tabia nikutokana na upoyoyo wako kichwani na wala si kingine..... sasa award ya maadili mema kwenye jukwaa la mapenzi eeeh eh wakati watu mapenzi mnachukulia si maadili ndiyo maana yanajadiliwa kwa tafsida,... labda AWARD KWA WANAOCHANGIA WAZI WAZI BILA KUOGOPA HAPO SAWA

Nimesahauje kukutaja wewe, immoral! Kwa hiyo unapingana na top pyschologists waliofanya research na kuconclude kuwa kuna inborn na acquired behavior? Na acquired ndio zile ambazo wewe unawaambukiza watu.
 
ndio nini sasa ??

Sishangai wewe pamoja na avatar yako hiyo kumbe ni Preta, si utovu wa maadili huo maana kuna negative correlation kati ya avatar yako na wewe ulivyo.
 
Last edited by a moderator:
Khaa!! Labda ungefafanua maadili mabaya ni yapi na mema yapi. Kwani isije kuwa umejichanganya

Ni kweli ufafanuzi unahitajika kuna mambo kwa wengine ni sawa tu wakati kwa wengine sio sawa. Mfano Mzungu akitembea uchi/nusu uchi ni sawa kwao lakini sio maadili mema kwa mwafrika/mtanzania kuvaa nusu uchi/kuwa uchi hadharani. Fafanua tafadhali
 
Sishangai wewe pamoja na avatar yako hiyo kumbe ni Preta, si utovu wa maadili huo maana kuna negative correlation kati ya avatar yako na wewe ulivyo.

ndio nini sasa ?
 
Last edited by a moderator:
maadili peleka kule kene jukwaa la dini sio jukwaa lingine lolote hapa JF
 
Ni kweli ufafanuzi unahitajika kuna mambo kwa wengine ni sawa tu wakati kwa wengine sio sawa. Mfano Mzungu akitembea uchi/nusu uchi ni sawa kwao lakini sio maadili mema kwa mwafrika/mtanzania kuvaa nusu uchi/kuwa uchi hadharani. Fafanua tafadhali

Kura zitaamua mkuu, atakayepigiwa kura kuwa ndio ana maadili mazuri huyo huyo. Immorals humu mbona hawajifichi!
 
Nimesahauje kukutaja wewe, immoral! Kwa hiyo unapingana na top pyschologists waliofanya research na kuconclude kuwa kuna inborn na acquired behavior? Na acquired ndio zile ambazo wewe unawaambukiza watu.

he he he he kwa sababu ulikuwa unanisingizia
 
Back
Top Bottom