Simple principles zilizonisaidia maishani mwangu

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Binafsi naamini kuwa urahisi au ugumu wa maisha yetu kwa namna moja ama nyingine huwa tunausababisha sisi wenyewe either kwa kujua au kwa kutokujua. Baada ya kujifunza kutokana na makosa ya watu wengine kwa muda mrefu, nilifanikiwa ku develop principles zangu mwenyewe ambazo ndizo zinaongoza maisha yangu. Kwa kiasi kikubwa sana zimenisaidia hivyo kwa siku ya leo ningependa kushare na nyinyi ili kama kuna kitu cha kujifunza tuweze kujifunza na kuboresha maisha yetu. Zifuatazo ni principles zangu ambazo zimenisaidia sana maishani mwangu:-

1. Salamu yangu ni haki ya kila mtu
Binafsi siwezi kupita jirani na mtu yeyote au watu waliokaa na kutulia sehemu yoyote ambapo napita bila kuwapa salamu..Sibagui wakaka, wadada, masela, wazee au mtu wa dini wala kipato chochote. Huwa sipungukiwi kitu kumsalimia mtu yeyote ninaemkuta eneo husika. Nitakuwa sina story nawewe ila lazima nitakupa hai na kuendelea na mambo yangu. Lazima nimuheshimu kila mtu maana huenda kuna siku nitamhitaji. Nitatoa mifano miwili. Mtaa niliokuwa naishi zamani, kuna mdada mmoja mrembo sana kiasi kwamba kutoa salamu yake kukupa ni kitu impossible. Anaweza kuwapita miguuni mwenu bila hata kuwapa salau. Ndiyo, ni binti mrembo na sisi hatukuwa hadhi yake japo kwa salamu.. Siku moja sasa mida ya usiku kama saa tano hivi alikuwa anarudi home na gari, kabla ya kufika kwake gari ikamzingua na hapo ni night. Binti huyo tunaona anakuja tulipokaa..Bila aibu akaomba tukamsaidie japo kuisukuma hadi home. Wadau hawakuwa na simile, walimchana na kumsema kuhusu tabia yake ya kupita bila salamu. Dada aliomba omba msamaha pale kwa aibu na tukaamua kumsaidia tu. Ninaamini alijifunza kitu.

Mfano wa pili, nilihamia mtaa mwingine. sasa kule kuna majirani ambao sina mazoea nao (sipendagi sana mazoea na watu ambao sijawajua mda mrefu). Mazoea yetu makuu ni salamu, nikipita salamu akipita ananisalimu. Siku moja natoka home asubuhi nikawa nimedondosha funguo. Nilikuwa desperate sana hiyo siku na sikujua iko wapi. Badae nimerudi home namuona jirani ananiletea funguo kumbe aliiokota nilipoangusha..Binafsi laiti ningekuwa simpi hata salamu, asingenipa funguo na pengine hata angenikomoa kwa sababu 'naringa'. Nishapata michongo mingi sana kutokana na kuonesha hii heshima ndogo kwa watu japo wengine wanaipuuza. Salamu ina nguvu kubwa sana.

2. There is no second chance for first impression
Hii ni principle yangu ya pili. siku yoyote na muda wowote nikiwa naenda kuonana na mtu kwa mara ya kwanza, huwa najitahidi ku behave. Kama busara nitajitahidi kuact hekima na busara sana siku hiyo. Kama ni muonekano (uvaaji) nitavaa vile ambavyo hainioneshi kama bishoo au msela. Hakunaga second chance ya kumuimpress mtu. Siku atakavyokuchukulia siku ya kwanza kukuona/kuongea nawewe ndivyo atakavyokuchukulia hivyo hivyo siku zote. First impression yako ndio itamfanya mtu aamue either kukuheshimu, kukupa attention au kukupuuza siku nyingine. Hii sio tu kwa watu wazima, hata kwa watoto. Huwa sicheki cheki na mtoto siku ya kwanza. Ukimchekea atakuzoea hivyo na atakuchukulia peace kiasi kwamba hata kesho ukimkaripia atakuona unamuigizia. Mwisho wake atakushika kalio mbele ya watu.

3. Nabadilika kulingana na mazingira
Iko hivi, baadhi ya watu wameshindwa kuielewa persoality yangu hadi leo. Nikienda sehemu nikakuta watu wanaongea vitu serious, nitaadapt yale mazingira. Nikienda sehemu nikakuta wanaongea simple issues plus jokes muda wote namimi nakuwa mtu wa hivyo. Hii hufanya kila kundi linione mwenzao na hawawezi kukutenga, maana huwa sipendi kuchanganya rejesta za kijiweni na ofisini. Hii pia hunisaidia kuilinda reputation yangu kwa watu wa kundi fulani. Mfano mtu wa kundi la watu wananijua kama kijana mwenye busara hawawezi kuamini rumours zozote wakisikia fohadi ana tabia hizi aua anaongea hivi maana sijawahi onesha character hizo mbele yao hivyo hawataamini. Ukiwa na rejesta za busara kijiweni watakuona ni snitch tu na unajifanya umesoma n.k. Sometyimes unaweza poteza michogo mingi maana watakuwa hawakufikishii dili coz we sio mwenzao. Ukileta rejesta za mtaani kwa washua, watakuona mhuni tu na kijana usiyejitambua. Hii principle ndio inanifanya mimi kuwa msaka yote aliyepata yote.

4. Tabia unayonionesha ndiyo nitakayokuonesha (Heshima vs Heshima)
Binafsi, sio mtu wa jeuri au kuringa wala kujisikia maana ukiacha pumzi na afya, sina kingine cha kunifanya niringe. Ila siku zote narudisha kile unachonipa. Naomba nieleweke kwa makini hapa msichanganye. Mfano, nimefika sehemu nikakuta mmekaamnapiga story zenu, nitwasalimi wotee bila kubagua ninaowajua au nisiowajua, mara nyingi napenda kutumia salaamu ya pamoja/jumla kwa wote. Ila kunaile hali mmekaa sehemu, anakuja mtu ambae bila kujali anakujua au hakujui. Anasalimia watu wote pale kwa kuwataja majina mmoja mmoja halafu mimi akaniacha (zaidi ya mara moja), mtu wa aina hii huwa hapati salamu yangu tena labda nimkute sehemu nyeti nitamsalimia kwajili ya kufaidika na kitu fulani.

Ila kama tunaonana mtaani tu hatapata salamu yangu kamwe na nikimkuta kwenye kundi la watu nitatoa salamu kwa wote nitamuacha pia. Kuna baba mmoja wa makamo around 45's alikuwa anakuja sehemu fulani na anasalimia wale anaowajua tu. Sasa namimi kila nilipokuwa namkuta nilikuwa nampita au simsalimii kabisa. sasa kuna siku alinikuta njiani tunaelekea uelekeo sawa. Akanipa salamu akaanza kunidadisi na kunielekeza umuhimu wa kusalimia watu. Akanigusia mara kadhaa huwa simpi salamu na huwa anajisikia vibaya sana hasa mbele ya watu. Ndipo nikagundua kumbe inauma eeenh. Ila mwisho wa siku nilimweleza ukweli kuhusu hata mimi alivyowahi kunifanya nijisikie kudharaulika mbele ya watu na kweli alinielewa basi kuanzia siku hisyo ni tunasalimiana.

Mimi hata uwe na umri sawa na baba yangu, ukinikuta sehemu wewe ndo unapaswa uanze salamu mfano 'haujambo kijana?', nitajibu 'sijambo shikamo' n.k. Ila ukikaa kimya sitakupa salamu maana umenipuuza. Heshima ni kwa wote.

NB: Hii principle ya 4 najua itawafanya watu fulani fulani waseme sina nidhamu au jeuri ila ndani ya nafsi yao wanajua kuwa niko sahihi. Ukishindwa kujiheshimu wewe mwenyewe hakuna atakaekuja kukuheshimu.

Nazimalizia wakuu.
 
Maskini na watu wasiojiamini ndo hufanya hayo yote ili wapate ishi kwa huruma ya wazungukao

Huo mfano wa gari ni vile tu uyo dada alikua maskini, Mi nakumbuka siku moja hv mzee alitupita spidi mbaya na kuturushia maji sie tulikua na boda boda kufika mbele kidogo kuna sehemu inaitwa "kisima cha bibi" Iringa huko tunamkuta mzee kaingia kwene mfereji hata hakuongea sana alisema tu vijana kuna laki hapa nataka gari yangu irudi barabarani

Tukamtolea pale ndinga yake tukachukua chetu tukapita hv hv, ayo mambo ya salamu sijuhi dressing & speaking style yanawtupa favor sie maskini tu ila kwa mwenye pesa hakuna kitu ka iko

Jiamini jikubali hivo ulivo ndo ulivoumbwa, muhimu tafuta pesa kwa njia yeyote uache kutegemea huruma ya watu

Hiki ulichoandika kinawafaa watu wanaoanza maisha ila kwa mtu mwenye experience na life ataona umeandika upupu tu
 
Inaendeleaaaa....

5. Sinunui ugomvi usionihusu

Hapa nataka niwape case study moja ili iwe rahisi, kwa wale wanaomjua baba levo naamini wataelewa zaidi. Huyu jamaa toka awe jinani na Diamond amekuwa mtu wa kuwashambulia wazi wazi watu wote wenye tatizo na diamond bila kujua hata chanzo cha bifu zao. Leo hii baba levo atajiona yuko sahihi maana anafaidika ila ajue tu maisha sio leo tu, kesho dunia ikigeuka majuto yanakuwa mjukuu. Turudi kwenye mada.
Huwa naamini wagombanao ndio wapatanao hivyo kama mimi ni mshikaji wako, basi adui yako sio adui yangu. Siwezi nikaingia katika ugomvi na mtu fulani kwajili yako. Je, kesho na keshokutwa mkipatana mimi nitaificha wapi sura yangu??. Never in my life.

Miaka 5 nyuma, baba yangu mdogo alikuwa rafiki yangu mkubwa sana. Baadae baba mdogo na Baba yangu wakaingia kwenye migogoro yao binafsi, wakawa na ugomvi ambao hadi leo sijui yupi alikuwa source ya ile bifu. Lakini, pamoja na kuwa na bifu kali, bado baba mdogo aliendeleaa kuwa mshikaji wangu na wala hakuwahi kunitenga kisa tu hapatani na mshua. Sikuingilia na wala sikutaka niwe upande wowote. Kuna muda ugomvi wao uliisha na wakarejea katika hali ya kawaida. Hii ilinipa funzo kubwa sana kuwa maisha sio leo tu, kuna kesho pia so ni vyema kutoingilia mambo yasiyokuhusu.

6. Naogopa sana kuacha vinyongo kwenye mioyo ya wenzangu
Nikigundua kuwa nimemkosea mtu kwa kiwango chochote kile, huwa sioni aibu kumfata na kumuomba radhi. Huwa sina amani kuishi wakati wenzangu wana vinyongo kwa makosa ya wazi niliyowahi yafanya. Miaka ya nyuma niliwakosea sana mabinti wawili ambao niliwahi kuwa na mahusiano nao. Waliwahi kujitoa kwajili yangu lakini sikuiona thamani yao, nikawaumiza. Maisha yaliendelea nikaachana nao lakini bado nafsi ilizidi kunisuta kwa kuziumiza hisia zisizo na hatia. Ilibidi niwatafute na kuwaomba msamaha kila mmoja. Sikutaka chochote zaidi ya msamaha wao na kweli walinisamehe na ninakiri pia kuwa walinisamehe kwa dhati ya mioyop yao maana hata sasa moyo wangu una amani. Leo mimi na wao ni marafiki wazuri, tunasaidiana sana na kushauriana mema. Hatuna habari za kupasha viporo. Kila mmoja anaenjoy mahusiano yake mapya.

Yanini kujenga chuki na uhasama usio na faida? KARMA HAS NO MENU!.. Nataka nije nihukumiwe kwa mabaya yangu niliyoyafanya nyuma ila sitaki kuja kuhukumiwa kwa vinyongo walivyonavyo wenzangu.

7. Sio mwepesi kuomba msamaha kwa kitu ambacho sijawahi kufanya
Nikiwa na uhakika hiki kitu sijafanya, sistahili lawama hizi. inaweza nichukua muda mrefu sana kuomba msamaha au nisiombe kabisa. Pengine huu ni udhiafu wangu na wala sio principle hahahaha. tuiache.

8. Maskini jeuri.
Moyoni mwangu ninaamini kuwa kesho yangu ipo mikononi mwa Mungu. Na kama Mungu anataka kuipitisha riziki yangu kwa watu basi atatumia watu wengine wanaoniheshimu na kuuthamini utu wangu. Haijalishi una nafasui gani au uwezo gani, siwezi kuuza utu wangu kwako. Siwezi kujidhalilisha au kujishusha utu wangu kisa tu status yako. Huwa naenda sawa na wale tu wanaoniheshimu. Siwezi kuwa mtu wako ikiwa huniheshimu. Nishawahi kuwa na ndugu yangu mmoja mwenye conectios kibao mjini. Huku na huku tukatofautiana na mimi niliona sina kosa so sikuwahi kuappologize japo moyoni binafsi nilimsamehe maana ninaamini kuna sehemu alinikosea. Basi watu wakawa wananiambia kuwa nimalizane na yule ndugu yangu maana anaweza kunisaidia hata kimaisha. Nilikataaa, ilikuwa ngumgu sana. Nilikuwa nipo radhi bifu langu na lake liishe juu juu tu bila mimi kutamka neno samahani. Sikuwa tayari kuipoteza thamani yangu kisa tu connections zake. Watu tunapenda kutumia strengths zetu au weaknesses za wengine kuwaonea au kuwa control. Niliamini na bado naamini kuwa, kesho yangu ipo tu naitazidi kuwepo hata bila kuwategemea aina ya watu fulani maana tumaini pekee na mwamuzi ni Mungu.

9. Uaminifu
Naamini sana katika uaminifu maana ni miongoni mwa vitu ambavyo ukivipoteza sio rahisi kuvirudisha. Kama mtu akikuamini, ukipoteza ule uaminifu basi hatakuamini tena kama mwanzo badala yake atakuwa anakutilia mashaka kwa kila kitu. I always try to play fair. wanasema hard work pays basi na credibilty pays too. Najitahidi sana kuwa mwaminifu, sipendi tamaa ndogo ndogo ziniharibie mipango yangu. Kuna maeneo ukiwa mwaminifu watu watahisi we ni mshamba, hujui kutumia fursa kumbe hawajui unajiwekea hadhina kubwa sana kwajili ya kesho. Mimi pia, nikikuamini ukaniangusha huwa sikuamini tena..Never ever!

10. I spend less while Saving

Yes, akiba haiozi. 90% ya rafiki zangu wanajua mimi ni bahili and yes ni bahili kwa vitu ambayo sio productive. Kipato changu ni kidogo so siwezi kuspend too much ili ku show off kwa mtu. Matumizi yangu hayako controlled au influenced na mtu mwingine. so, najitahidi sana sana kubana matumizi kwa kupunguza zile unnecessary expenses ili tu nikidhi mahitaji yangu ya muhimu. Hii principle imenisaidia sana sana. Hata mchumba wangu anajua na naielewa hii principle. Siwezi kuspend much ili kumuimpress maana if she was meant to be mine lazima atakuwa tu. Hizi impression zinazotuzidi kimo ndizo zinafanya dada zetu wana danga na watu wengi kufanya illegal business.

11. Kugusa maisha ya watu
Sina roho nzuri sana ila najitahidi kuweka tabasamu kwenye sura za wengine kadri ninavyoweza na pengine hii ni dhamira yangu kubwa sana. Kufika hapa nilipo nimesaidiwa na watu wengi sana hivyo hata mimi huwa najitahidi kugusa maisha ya wengine. Nishafanya mambo mengi kuwasaidia watu (simaanishi pesa wala material things, namaanisha intangible supports) na leo nafurahia pale walipo na ninaziona baraka nyingi zinazotokana na maombi yao. Kila ninaposaidia, huwa sitegemei chochote in return maana hata mimi sijawalipa na sitaweza kuwalipa wote walionisaidia. Tenda wema nenda zako.

12. Family over everything
Chochote ninachotaka kufanya huwa naifikilia sana familia yangu itakuwaje baada ya matokeo. Nikitaka kuiba lazima niwaze je nikikamatwa nephews na cousins wangu watasaidiwa na nani?, nikitaka kutembea na wanafunzi au wake za watu nawaza impact ya maamuzi Yangu. Hii principle imenisaidia sana sana kusimama katika msitari mnyoofu kimaadili. Kitu kinachotucost wengi ni ile hali ya kujifikiria sana sisi kuliko wengine.

Cha mwisho, sipendi shobo...sifosi undugu, urafiki au mahusiano..Demu akinizingua zaidi ya wiki mbili simfatilii tena..Maana nitakuwa najiletea maumivu tu...Ukinithamini nitakuthamini na usiponithamini nitakufanyia same na unavyonifanyia.

Those are my principles..Zimenisaidia sana.



 
Binafsi naamini kuwa urahisi au ugumu wa maisha yetu kwa namna moja ama nyingine huwa tunausababisha sisi wenyewe either kwa kujua au kwa kutokujua. Baada ya kujifunza kutokana na makosa ya watu wengine kwa muda mrefu...​
Ni vyema kuishi kama askari, kuna mambo lakini ukiayelegezea yanakutafuna kisa ni kanuni yako,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAJIBU YA JUMLA KWA BAADHI YA COMMENTS

1. Comments chache mpaka hapa zinaonesha pesa ni suluhisho la kila kitu...Bro/sister...pesa sio kila kitu...Huo ni mfano tu wa gari. Just imagine una hela halafu hau cooperate na wenzio, siku umepata dharura ghafla ambayo inahitaji utu na sio pesa..unazani pesa zako zitakusaidia?

2. Hizi principle zimenisaidia sana..nilipata dili moja kutoka kwa stranger. ni vile tu tulizoeana kidogo akanipa deal. Unaweza ukawa unamdharau mlinzi wa kampuni fulani unaeishi nae jirani kisa tu unajua siku ukiwa na hela 'utamnunua' akusaidie. Siku moja huyo mlinzi atakuja kukutonya kuhusu nafasi ya kazi iliyopo kwenye eneo lao...Sasa wewe mpe hai mtu kwa mood, halafu utegemee pesa zako uone kama hujaja umbuka siku moja.

3. I am not a good guy and am not acting like...ila nilijifunza hizi vitu kwenye mistakes za wengine ndomana najitahidi kuzipractice ili kuepuka challlenge walizokutana nazo wao...I am not a good guy at all.

4. Wakuu..salamu na majungu ni vitu viwili tofauti...Unaweza ukampa mtu kila kitu ila akakuchafua tu..Haikwepeki hiyo. Ila hapa naongelea salaamu kama kiunganishi cha jamii na kusaidiana kwenye hali tofauti..sijaongelea kuhusu mazoea wala nini ila just salamu...anyway, tafuteni pesa mkiamini siku moja mta wanunua watu wawasaidie....Pesa sio kila kitu wakuu.

5. Yes nimeandika UPUPU ila siku ukilegeza ubongo utakuja kuelewa kipi nilimaanisha...Huna ushirikiano na watu kisa eti hujali perception za watu...trust me, kuna siku utawatafuta watu uwanunue na hutawaona...Just live a low key life.

6. Hii ni kwa wote, anaeanza, alieanza na atakaeanza maisha...Hii haiwahusu waliomaliza maisha yao...Mungu awarehemu.​
 
Inaendeleaaaa....

5. Sinunui ugomvi usionihusu

Hapa nataka niwape case study moja ili iwe rahisi, kwa wale wanaomjua baba levo naamini wataelewa zaidi. Huyu jamaa toka awe jinani na Diamond amekuwa mtu wa kuwashambulia wazi wazi watu wote wenye tatizo na diamond bila kujua hata chanzo cha bifu zao. Leo hii baba levo atajiona yuko sahihi maana anafaidika ila ajue tu maisha sio leo tu, kesho dunia ikigeuka majuto yanakuwa mjukuu. Turudi kwenye mada...
"Namba 6 inapingana na namba 7"

Nakumbuka uliishawai kuleta uzi humu unabifu na baba yako mdogo ile story aijaenda sambamba na Principles zako
 
Safi sana mkuu, hivi ndio vitu vinatakiwa vifundishwe mashuleni katika dunia ya leo.
(social skills)
 
"Namba 6 inapingana na namba 7"

Nakumbuka uliishawai kuleta uzi humu unabifu na baba yako mdogo ile story aijaenda sambamba na Principles zako
Jesse Royal...wewe ndio umechanganya..

6. Naogopa kuacha vinyongo kwa watu. Hapa nilikuwa naongelea kuhusu kam kweli mtu nimemkosea na nafsi yangu inanisuta, lazima nimtafute nimuombe radhi....Iko hivyo...Baba mdogo sikumkosea na hakuna kinyongo chochote hapo ambacho nimekisababisha kwake...sikuwahi kumkosea.

7. Sio mwepesi kuomba msamaha kama sijamkosea mtu. Yes, baba mdogo sikuwahi kumkosea ndio maana hadi leo sijawahi kumuomba msamaha kwa jambo hilo maaana sijawahi kumkosea.

Nahisi umenielewa...Ule uzi wa baba msogo ilikuwa ni kuomba ushauri kwenu nifanyeje katika ile njia panda...Huwa sipendi kuacha vinyongo kwa makosa niliyowahi kuyafanya...

so bamdogo alinisaidia ila badae akanikosea..nikaamua kukaa pembeni na sikutaka kumuomba radhi kwa kosa ambalo sijalifanya.​
 
para ya mwisho upo sahiij hata mim unilkute hujasalimia .wazee wetu ilmu wengine kidg inakua hana ufaham.sheria aliyekukuta lazima asalimu.hata awe mzee wa miaka 70 hujambo kijana.sijambo shikamoo.sasa unakut mzee kafika au mtu mzim tu.anajipweteka sio sahihi.au umepiga simu anza kusalimia wewe uliyepiga u
kisha utapata tu salam yako.ni uelewa tu ndio shida.na wewe pia salam itoe salimia hata mtoto wa miaka 3.ndio umemkuta
 
Yani kaandika upupu..Ana act u nice guy... Ukiwa na hela you don't give a **** about someone perception....unafanya yako tu....
Mkuu..siku unaenda kutambulishwa ukweni kisa tu una hela na u dont give a * about someone's perception...ulienda umevaa boxer au mlegezo?.. au unaweza ukacheza baikoko mbele ya jirani zako kisa u dont give a *?....

There is no second chance for first impression..... Achana na upupu wote nilioandika chukua hiyo single line niliyo ibold siku moja ita kusaidia...
 
Back
Top Bottom