Simple principles zilizonisaidia maishani mwangu

Woga Wa kimasikini ndio unakutuma hivo ,huku ukiamin kuwa

"Hawa ninaowasalimia ipo siku watanisaidia "

Matumizi mabaya ya akili


Tafuta pesa
 
MAJIBU YA JUMLA KWA BAADHI YA COMMENTS

1. Comments chache mpaka hapa zinaonesha pesa ni suluhisho la kila kitu...Bro/sister...pesa sio kila kitu...Huo ni mfano tu wa gari. Just imagine una hela halafu hau cooperate na wenzio, siku umepata dharura ghafla ambayo inahitaji utu na sio pesa..unazani pesa zako zitakusaidia?

2. Hizi principle zimenisaidia sana..nilipata dili moja kutoka kwa stranger. ni vile tu tulizoeana kidogo akanipa deal. Unaweza ukawa unamdharau mlinzi wa kampuni fulani unaeishi nae jirani kisa tu unajua siku ukiwa na hela 'utamnunua' akusaidie. Siku moja huyo mlinzi atakuja kukutonya kuhusu nafasi ya kazi iliyopo kwenye eneo lao...Sasa wewe mpe hai mtu kwa mood, halafu utegemee pesa zako uone kama hujaja umbuka siku moja.

3. I am not a good guy and am not acting like...ila nilijifunza hizi vitu kwenye mistakes za wengine ndomana najitahidi kuzipractice ili kuepuka challlenge walizokutana nazo wao...I am not a good guy at all.

4. Wakuu..salamu na majungu ni vitu viwili tofauti...Unaweza ukampa mtu kila kitu ila akakuchafua tu..Haikwepeki hiyo. Ila hapa naongelea salaamu kama kiunganishi cha jamii na kusaidiana kwenye hali tofauti..sijaongelea kuhusu mazoea wala nini ila just salamu...anyway, tafuteni pesa mkiamini siku moja mta wanunua watu wawasaidie....Pesa sio kila kitu wakuu.

5. Yes nimeandika UPUPU ila siku ukilegeza ubongo utakuja kuelewa kipi nilimaanisha...Huna ushirikiano na watu kisa eti hujali perception za watu...trust me, kuna siku utawatafuta watu uwanunue na hutawaona...Just live a low key life.

6. Hii ni kwa wote, anaeanza, alieanza na atakaeanza maisha...Hii haiwahusu waliomaliza maisha yao...Mungu awarehemu.​
Uko sahihi mkuu
Nimenukuu mahali naaamini zitanisaidia pia mahali fulani na mimi
 
Hakuna
Mkuu..siku unaenda kutambulishwa ukweni kisa tu una hela na u dont give a * about someone's perception...ulienda umevaa boxer au mlegezo?.. au unaweza ukacheza baikoko mbele ya jirani zako kisa u dont give a *?....

There is no second chance for first impression..... Achana na upupu wote nilioandika chukua hiyo single line niliyo ibold siku moja ita kusaidia...
Hakuna Cha first impression Wala Nini...unless inakua applied kwenye bussi ess issue mkuu....lakini everywhere wewe ujali tu first impression.....aaaaah mbona unajipa tabu mkuu
 
Binafsi naamini kuwa urahisi au ugumu wa maisha yetu kwa namna moja ama nyingine huwa tunausababisha sisi wenyewe either kwa kujua au kwa kutokujua. Baada ya kujifunza kutokana na makosa ya watu wengine kwa muda mrefu, nilifanikiwa ku develop principles zangu mwenyewe ambazo ndizo zinaongoza maisha yangu. Kwa kiasi kikubwa sana zimenisaidia hivyo kwa siku ya leo ningependa kushare na nyinyi ili kama kuna kitu cha kujifunza tuweze kujifunza na kuboresha maisha yetu. Zifuatazo ni principles zangu ambazo zimenisaidia sana maishani mwangu:-

1. Salamu yangu ni haki ya kila mtu
Binafsi siwezi kupita jirani na mtu yeyote au watu waliokaa na kutulia sehemu yoyote ambapo napita bila kuwapa salamu..Sibagui wakaka, wadada, masela, wazee au mtu wa dini wala kipato chochote. Huwa sipungukiwi kitu kumsalimia mtu yeyote ninaemkuta eneo husika. Nitakuwa sina story nawewe ila lazima nitakupa hai na kuendelea na mambo yangu. Lazima nimuheshimu kila mtu maana huenda kuna siku nitamhitaji. Nitatoa mifano miwili. Mtaa niliokuwa naishi zamani, kuna mdada mmoja mrembo sana kiasi kwamba kutoa salamu yake kukupa ni kitu impossible. Anaweza kuwapita miguuni mwenu bila hata kuwapa salau. Ndiyo, ni binti mrembo na sisi hatukuwa hadhi yake japo kwa salamu.. Siku moja sasa mida ya usiku kama saa tano hivi alikuwa anarudi home na gari, kabla ya kufika kwake gari ikamzingua na hapo ni night. Binti huyo tunaona anakuja tulipokaa..Bila aibu akaomba tukamsaidie japo kuisukuma hadi home. Wadau hawakuwa na simile, walimchana na kumsema kuhusu tabia yake ya kupita bila salamu. Dada aliomba omba msamaha pale kwa aibu na tukaamua kumsaidia tu. Ninaamini alijifunza kitu.

Mfano wa pili, nilihamia mtaa mwingine. sasa kule kuna majirani ambao sina mazoea nao (sipendagi sana mazoea na watu ambao sijawajua mda mrefu). Mazoea yetu makuu ni salamu, nikipita salamu akipita ananisalimu. Siku moja natoka home asubuhi nikawa nimedondosha funguo. Nilikuwa desperate sana hiyo siku na sikujua iko wapi. Badae nimerudi home namuona jirani ananiletea funguo kumbe aliiokota nilipoangusha..Binafsi laiti ningekuwa simpi hata salamu, asingenipa funguo na pengine hata angenikomoa kwa sababu 'naringa'. Nishapata michongo mingi sana kutokana na kuonesha hii heshima ndogo kwa watu japo wengine wanaipuuza. Salamu ina nguvu kubwa sana.

2. There is no second chance for first impression
Hii ni principle yangu ya pili. siku yoyote na muda wowote nikiwa naenda kuonana na mtu kwa mara ya kwanza, huwa najitahidi ku behave. Kama busara nitajitahidi kuact hekima na busara sana siku hiyo. Kama ni muonekano (uvaaji) nitavaa vile ambavyo hainioneshi kama bishoo au msela. Hakunaga second chance ya kumuimpress mtu. Siku atakavyokuchukulia siku ya kwanza kukuona/kuongea nawewe ndivyo atakavyokuchukulia hivyo hivyo siku zote. First impression yako ndio itamfanya mtu aamue either kukuheshimu, kukupa attention au kukupuuza siku nyingine. Hii sio tu kwa watu wazima, hata kwa watoto. Huwa sicheki cheki na mtoto siku ya kwanza. Ukimchekea atakuzoea hivyo na atakuchukulia peace kiasi kwamba hata kesho ukimkaripia atakuona unamuigizia. Mwisho wake atakushika kalio mbele ya watu.

3. Nabadilika kulingana na mazingira
Iko hivi, baadhi ya watu wameshindwa kuielewa persoality yangu hadi leo. Nikienda sehemu nikakuta watu wanaongea vitu serious, nitaadapt yale mazingira. Nikienda sehemu nikakuta wanaongea simple issues plus jokes muda wote namimi nakuwa mtu wa hivyo. Hii hufanya kila kundi linione mwenzao na hawawezi kukutenga, maana huwa sipendi kuchanganya rejesta za kijiweni na ofisini. Hii pia hunisaidia kuilinda reputation yangu kwa watu wa kundi fulani. Mfano mtu wa kundi la watu wananijua kama kijana mwenye busara hawawezi kuamini rumours zozote wakisikia fohadi ana tabia hizi aua anaongea hivi maana sijawahi onesha character hizo mbele yao hivyo hawataamini. Ukiwa na rejesta za busara kijiweni watakuona ni snitch tu na unajifanya umesoma n.k. Sometyimes unaweza poteza michogo mingi maana watakuwa hawakufikishii dili coz we sio mwenzao. Ukileta rejesta za mtaani kwa washua, watakuona mhuni tu na kijana usiyejitambua. Hii principle ndio inanifanya mimi kuwa msaka yote aliyepata yote.

4. Tabia unayonionesha ndiyo nitakayokuonesha (Heshima vs Heshima)
Binafsi, sio mtu wa jeuri au kuringa wala kujisikia maana ukiacha pumzi na afya, sina kingine cha kunifanya niringe. Ila siku zote narudisha kile unachonipa. Naomba nieleweke kwa makini hapa msichanganye. Mfano, nimefika sehemu nikakuta mmekaamnapiga story zenu, nitwasalimi wotee bila kubagua ninaowajua au nisiowajua, mara nyingi napenda kutumia salaamu ya pamoja/jumla kwa wote. Ila kunaile hali mmekaa sehemu, anakuja mtu ambae bila kujali anakujua au hakujui. Anasalimia watu wote pale kwa kuwataja majina mmoja mmoja halafu mimi akaniacha (zaidi ya mara moja), mtu wa aina hii huwa hapati salamu yangu tena labda nimkute sehemu nyeti nitamsalimia kwajili ya kufaidika na kitu fulani.

Ila kama tunaonana mtaani tu hatapata salamu yangu kamwe na nikimkuta kwenye kundi la watu nitatoa salamu kwa wote nitamuacha pia. Kuna baba mmoja wa makamo around 45's alikuwa anakuja sehemu fulani na anasalimia wale anaowajua tu. Sasa namimi kila nilipokuwa namkuta nilikuwa nampita au simsalimii kabisa. sasa kuna siku alinikuta njiani tunaelekea uelekeo sawa. Akanipa salamu akaanza kunidadisi na kunielekeza umuhimu wa kusalimia watu. Akanigusia mara kadhaa huwa simpi salamu na huwa anajisikia vibaya sana hasa mbele ya watu. Ndipo nikagundua kumbe inauma eeenh. Ila mwisho wa siku nilimweleza ukweli kuhusu hata mimi alivyowahi kunifanya nijisikie kudharaulika mbele ya watu na kweli alinielewa basi kuanzia siku hisyo ni tunasalimiana.

Mimi hata uwe na umri sawa na baba yangu, ukinikuta sehemu wewe ndo unapaswa uanze salamu mfano 'haujambo kijana?', nitajibu 'sijambo shikamo' n.k. Ila ukikaa kimya sitakupa salamu maana umenipuuza. Heshima ni kwa wote.

NB: Hii principle ya 4 najua itawafanya watu fulani fulani waseme sina nidhamu au jeuri ila ndani ya nafsi yao wanajua kuwa niko sahihi. Ukishindwa kujiheshimu wewe mwenyewe hakuna atakaekuja kukuheshimu.

Nazimalizia wakuu.

Binafsi Nipo kama wewe ila binadamu ni watu wa ajabu sana apo unajizungumzia wewe tu lkn hujui wanakuzungumziaje kitaa aisee ama pata tatizo ndo ujue walimwengu.....
 
Kuna aina mbalimbali za manufaa katika maisha, kwa dhati nashukuru kwa moyo wako na dhamira njema ya chakula hiki cha utashi wa maisha. Tafadhari share na mimi inbox. Usikatishwe tamaa kuhusu uchangiaji unabeba yote u learn from both -&+. Do not hesitate helping never never, this is very fundamental. "For God We Stand United" this slogan is solely mine.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom