Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,546
- 2,176
Rushwa haipiganwi kwa kutishana kama alivyofanya Magu,Hii awamu rushwa imedhibitiwa kwelikweli, Hongera Rais Samia
Hii sio awamu ya kulipa pesa kama mlivyoaminishwa, Mahakama ndio waamuzi wala sio DPP,Mil 2 tu hizo wangetaifisha Mali zake zenye thaman hyo ingetosha.
Mahakaman watapoteza muda na pesa itakayozid pesa anayotuhumiwa.
Na pengine akawabwaga kwa korti pia.
Hata kama ingekuwa ni laki moja,Mil 2 tu hizo wangetaifisha Mali zake zenye thaman hyo ingetosha
Mahakaman watapoteza muda na pesa itakayozid pesa anayotuhumiwa
Na pengine akawabwaga kwa korti pia
Yeah. Tumeletewa mada ya wizi wa shilingi milioni 2 kwenye JUKWAA LA SIASA tujadili kuonyesha jinsi awamu ya 6 ilivyo serious kupambana na ufisadi!milioni 2 au milioni 200?
Chana cha msingi( CCM). Hawa watu ni nduguKATIBU WA AMCOS WILAYANI MASWA KORTINI KWA UHUJUMU UCHUMI.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) imemfikisha Katibu Wa Chama Cha Msingi cha Ushirika (Amcos)cha Mbaragane katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu,Samwel Makeja katika mahakama ya wilaya hiyo kwa makosa mawili ya Uhujumu Uchumi.
Katibu huyo alisomewa leo mashitaka yake yanayomkabili mahakamani hapo ambayo ni Ubadhirifu wa fedha na kuchepusha fedha.
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru Albertina Mwigilwa ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,Chirstian Rugumila kuwa Mshtakiwa alitenda makosa hayo Oktoba 4 mwaka 2021 katika Wilaya ya Maswa.
Mwendesha Mashtaka huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa kosa la kwanza ni kwamba mshitakiwa akiwa Katibu wa Amcos ya Mbaragane alifanya ubadhilifu Sh 2,000,000/-ambazo alipaswa kulipia ushuru wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu(SIMCU) katika musimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2021/2022.
Amesema kosa hilo ni kinyume ya kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 marejeo ya mwaka 2019.
Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa katka kosa la pili mshtakiwa alichepusha fedha hizo kwa madhumuni yake binafsi kinyume na kifungu cha 29 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2019.
Mshitakiwa mara baada ya kusomewa mashitaka hayo aliyakana na hivyo kesi kupangwa tena Juni 24,mwaka huu ambapo atasomewa hoja za awali kwani upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika.
pia soma USHIRIKA SIMIYU MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI
Bila katiba mpya tutaendelea kulaumiana sanaNasema hiviiii,"embu ifike wakati Sasa Serikali iache kuchezea pesa zetu kwa kesi ambazo mwisho wake mtu mmoja t ana simama na kusema Hana haja ya kuendelea na mashtaka,tumeshudia humu kesi nyingi zinatumia gharama kubwa at end of day unaambiwa zimefutwa, so! What for
Katiba italeta nini mzeeBila katiba mpya tutaendelea kulaumiana sana
Uhujumu uchumi!Ml 2!atatoka kesho tu huyo.KATIBU WA AMCOS WILAYANI MASWA KORTINI KWA UHUJUMU UCHUMI.