Serikali haitatui kero za watu hapo hapo ni mifumo. Ukiona kiongozi anafanya hivyo jua anatafita sifa binafsiMimi ni Chadema na simpendi Madelu matozo lakini kwenye hilo la kusikiliza wananchi na kutatua kero zao hapohapo tutamuunga mkono achukue nchi 2030.
Umeanza kumjua Mwigulu lini?Huyu ni muigizaji tu hana lolote, halafu yupo vizuri kwenye maigizo hana aibu kabisa akiwa anafanya maigizo.
Magufuli vyote alivyofanya ndivyo alivyokua toka akiwa waziri katika wizara mbalimbali , haigizi bali alikua vile ndio maana hata kabla hajawa raisi kwenye kampeni watu walikua wanasema kama tunaenda kuchagua dikteta kutokana na hulka na misimamo yake isiyoyumbishwa akiamua kitu huwezi kumrekebisha hata kama anakosea.
Huyu mwigulu ni muigizaji tu na haya yote anayafanya mawazo yote yapo kwenye uraisi na wala sio kusikiliza wananchi
Nimemjua toka kipindi Cha kashfa za mabomu ,kumwagia watu tindikali, kujiandika kwenye mawe kuwa ni raisi ajaye .Umeanza kumjua Mwigulu lini?
Kuna uwezekano mkubwa hii ni chuki binafsiNimemjua toka kipindi Cha kashfa za mabomu ,kumwagia watu tindikali, kujiandika kwenye mawe kuwa ni raisi ajaye .
Huyu Bila kupepesa macho ni uwezo mdogo sana na hana hoja wala utumishi wa maana wowote ule .
Tapeli asiyekua na mvuto wowote na kingine zaidi Bado ana fikra za ujima huko anaamini kuvaa mabendera ndio uzalendo.
Mwambie uzalendo unapimwa kwa matendo sio skafu na mashati yenye bendera ya Tanzania
Yaani ni kama yule mshambuliaji hatari wa simba Ibrahim Doumbia! Na yeye ni Osimhen mtupu.View attachment 3672626
Ziara ya Mhe. Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba Mkoani Simiyu imekonga mioyo ya wana-Simiyu. Katika mazungumzo na wananchi mbalimbali, wengi wameeleza kuvutiwa na namna Waziri Mkuu anavyokemea uzembe na wizi, pamoja na kusisitiza hatua za kubana matumizi ili fedha hizo zielekezwe katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande mwingine, wananchi hao wamesema utatuzi wa kero za wananchi papo kwa papo umesaidia wanyonge kupata haki zao. Kwa mtazamo wao, wameuita huo ni “Umagufuli mtu.”
Mmoja wa wananchi hao ananukuliwa akisema:
“Tumepata Magufuli mpya hapa. Haya tunayoyaona mbele ya macho yetu yanatukumbusha ule uongozi wa kusimamia haki na kukemea uzembe. Ona Maswa, wanyonge wamepata haki yao. Ona Bariadi na Itilima, tumeshuhudia kwa macho yetu.
Kuna baadhi ya watendaji ambao wamekuwa wakiwadhulumu wananchi na kuwanyima haki zao kwa makusudi. Lakini Waziri Mkuu anapofika, anawasikiliza wananchi, anachukua hatua na kutatua kero zao papo kwa papo. Huu ndio umagufuli wenyewe.
Sisi wananchi tumeona kwa macho yetu. Tumepata Magufuli mpya hapa. Huyu ni kiongozi anayesimama upande wa wanyonge na kutetea haki zao. Huyu ndiye Mtetezi wa Wanyonge.”
Tunajua haya ambayo tumeanza kuyasikia kwamba magenge yenye nguvu hayamtaki Waziri Mkuu na yanapambana kuhakikisha anaondoshwa au kumdhibiti kuelekea 2030. Tuseme tu, sisi wanyonge tutamwombea kwa Mungu.
Huyu ndiye Mtetezi wa Wanyonge.
Hamna cdm mpuuzi wa aina yako.Mimi ni Chadema na simpendi Madelu matozo lakini kwenye hilo la kusikiliza wananchi na kutatua kero zao hapohapo tutamuunga mkono achukue nchi 2030.