Simeoni na Lawi: Undugu ulio tukuka

Simeoni na Lawi: Undugu ulio tukuka

PutinV

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2017
Posts
1,046
Reaction score
1,649
Siku zote huwa naamini wanaume wote tuna genes fulani ambazo hazina ufumbuzi wa moja kwa moja, moja ya genes hizo ni "don't mess with my sister". Hakuna mwanaume anaye penda kuona dada yake anafanyiwa udhalilishaji hasa na mwanaume mwenzake. Kuna mifano mingi katika maisha na historia.

Wasalaam...
Katika kitabu cha Mwanzo katika Biblia, Yakobo ambaye ni mtoto wa Isaka na Rebeka anaondoka katika nchi ya baba yake huku akiwa anafanya hivyo kwa msukumo wa mambo mawili. Kwanza anamkimbia kaka yake ambaye anajaribu kumuua lakini pia kutimiza matakwa ya wazazi wake ya kutooa wanawake wa Kanaani. Basi Isaka kwa kushirikiana na mkewe Rebeka wakampa maelekezo Yakobo aende hadi kwa babu yake Bethueli aoe moja ya binti za mjomba wake aitwaye Labani.

Yakobo alianza safari yake ambayo ilikuwa na vikwazo vingi. Moja ya vikwazo hivyo ni pale ambapo Esau kaka yake alipo muamuru Eliphazi mwanaye aende na kumuua Yakobo akiwa njiani lakini kwa uwezo wa Mungu Yakobo alifanikiwa kumshawishi Eliphazi asimuue lakini aliambulia kumnyang'anywa vyote alivyo kuwa navyo. Mwisho alifika Paddan Aram ambapo alikuta wachungaji wenye makundi makubwa ya kondoo WAKISUBIRIANA ili waweze kulitoa jiwe kwenye mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo wao (yawezekana jiwe hilo lilikuwa zito sana hivyo lilihitaji nguvu kazi kubwa). Baada ya muda alifika binti wa Labani aliye itwa Raheli ambaye naye alifika kuwanywesha kondoo wa baba yake maji. Baada ya Yakobo kumuona Raheli aliviringisha jiwe lile mwenyewe na kuanza kuwanywesha kondoo wa mjomba wake maji. Bado sijatoka nje ya mada, kwa mujibu wa kitabu cha Yashari, ukoo wote wa Abraham ulikuwa na nguvu za ajabu ambazo walipewa kama baraka kutoka kwa Mungu na ndio maana haikuwa ngumu kwa Yakobo kuviringisha jiwe lile mwenyewe.

Yakobo alipokelewa vizuri na Labani mjomba wake na alimtumikia hadi pale Labani alipo muambia Yakobo achague ujira wowote naye Yakobo kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa Raheli alimchagua Raheli kama ujira wake ambapo alihitajika kumtumikia Labani kwa miaka saba. Baada ya miaka saba kuisha Labani kwa kisingizio cha kuwa mdogo haolewi kabla ya dada alimbadilishia Yakobo mke, badala ya kumuoza Raheli yeye alimuoza Lea. Ili kumpata Raheli ilimbidi Yakobo atumikue kwa miaka mingine saba lakini kwa Yakobo miaka saba ilikuwa michache kwa jinsi alivyo mpenda Raheli.

Yakobo akiwa kwa mjomba wake Labani alibarikiwa watoto kupitia mke wake Lea wa kwanza akiwa Reubeni kisha Simeoni na Lawi na watoto wengine wa kiume. Baadaye Lea alipata mtoto wa kike ambaye aliitwa Dina.

Baadaye Yakobo aliondoka kutoka kwa mjomba wake akafika katika mji wa Shekemu na kupiga kambi katika eneo alilo nunua kwa shekeli tano kutoka kutoka kwa wana wa Hamori baba yake Shekemu.

Wakati mmoja kulikuwa na sikukuu katika mji ule hivyo Dinah na mama yake pamoja na watumishi wengine wa kike walihudhuria sherehe ile pamoja na wasichana wengine wa Shekemu. Basi Shekemu mtoto wa Hamori mtawala wa mji ule alimuona Dina akampenda au tuseme akamtamani, akatuma watu wakamkamate na kumpeleka kwa Shekemu ambaye alimbaka Dina. Lea alipo rudi nyumbani na kumpa Yakobo taarifa kuwa Dina amekamatwa kwa nguvu na watumishi wa Shekemu, alituma watumishi kumi na mbili waende kwenye nyumba ya Shekemu wakamchukue Dina lakini walifukuzwa kama mbwa. Wakati haya yote yanaendelea watoto wote wa kiume wa Yakobo walikuwa wamekwenda kuchunga mifugo ya baba yao.

View attachment 1425885

Basi Shekemu akamuomba baba yake aende kuongea na Yakobo ili amchukue Dina kama mke wake kwani alimpenda sana, Hamori baba yake Shekemu aliposikia jambo lile alishangazwa na kumuuliza Shekemu kama hajaona warembo mji mzima hadi achukue mke kutoka kwa watu wageni katika nchi yao!, baada ya Shekemu kumuomba sana baba yake, Hamori alitoka na viongozi wengine wa mji na kwenda nyumbani kwa Yakobo ambaye alikataa kutoa jibu rasmi hadi pale watoto wake watakapo toka machungani.

Lakini taarifa za kubakwa kwa dada yao ziliwafikia wakiwa machungani, kwa hasira watoto wa Yakobo walirudisha mifugo nyumbani kabla ya muda wa kawaida. Walipo fika nyumbani wakawakuta Hamori na viongozi wengine wa mji ambao walirudia ombi lao huku wakitoa ahadi ya zawadi nyingi endapo kama watawaruhusu Shekemu amuoe Dina.

Labda zawadi nyingi na ofa nyingine kama vile biashara na muingilianao baina ya pande hizo mbili ulilainisha mioyo ya watoto wa Yakobo lakini hali ilikuwa tofauti kwa Simeoni na Lawi kaka zake Dina. Watoto wote wa Yakobo wakataka wapewe muda ili wafikirie jambo lile kwa kina hivyo iliwabidi Hamori na wenzake waondoke na kurudi kesho yake. Simeoni akatoa wazo akidai kuwa imewapasa watu wote wa mji ule kufa kwa upanga kwani wamemdhalilisha dada yao. Hivyo Simeoni akatoa ushauri kuwa wamuambie Hamori kuwa ni lazima watu wa mji wote wa tahiriwe, kisha wao watauvamia mji wote ambapo watu watakuwa bado wana maumivu ya kutahiriwa. Shauri hilo likaonekana kuwa ni jema!

Siku yenyewe ilipo fika, Simeoni na kaka yake Lawi waliweka ofa mezani. Ili Shekemu aruhusiwe kumuoa Dina ni lazima wanaume wote wa mji wa tahiriwe. Jambo hili lilimfurahisha Hamori pamoja na Shekemu ambao waliwashawishi watu wote wa mji ule watahiriwe. Jambo hili halikuwa rahisi kwani baadhi ya watu walipinga akiwemo Chiddekem baba yake Hamori. Chiddekem alitishia kwenda kukusanya miji yote ya Wakanaani ije kushambulia Shekemu kama hawataacha azma yao. Basi Hamori na Shekemu wakamsiihi Chiddekem asifanye hivyo bali angoje wanaume wote wa mji wapone kisha waende kuishambulia nyumba nzima ya Yakobo na kuwanyang'anya mali yao yote pamoja na Dina.

Ikumbukwe muda wote Dina alikuwa nyumbani kwa Shekemu na alipo sikia mipango yao alituma watumishi wake wapeleke taarifa kwa Yakobo. Taarifa hizi zilipo fika ziliwakera sana watu wa nyumba ya Yakobo. Simeoni na Lawi wakaapa lazima watawaua wenyeji wa mji siku inayo fuata. Siku ilipo fika wakajifunga panga zao na kuingia mjini wakiwa wawili tu, waliwaua wanaume wa mji mzima uliokuwa na wanaume zaidi ya 600 wa iache mwanaume hata mmoja. Pia Hamori na Shekemu waliuawa katika mauaji hayo kisha walienda hadi kwenye nyumba ya Shekemu wakamchukua dada yao Dina.

Watoto wa Yakobo walipo pata habari za yale waliyo fanya Simeoni na Lawi walienda kwenye mji ule na kujichukulia nyara za kutosha kama mifugo na mali nyingine. Pia walichukua wanawake ambao walikuwa mabikira, mmoja wao alikuwa Bunah ambaye alichukuliwa na simeoni kama mke.

Yakobo hakupendezwa na jambo lile kwani katika nchi ile aliishi kama mgeni hivyo alihofia kisasi cha wenyeji wa miji ya jirani. Jambo hili lilikaa katika akili ya Yakobo kwa muda mrefu hadi pale alipo wabariki watoto wake bado hakusahau hasira za wanawe simeoni na Lawi, kupitia Mungu Yakobo aliwatabiria kuwatawanya katika nchi, miongoni mwa ndugu zao.

View attachment 1425884

Yote yalitimia wakati wa kuigawa nchi ya ahadi kwa makabila ya Israeli ambapo Walawi hawakupewa ardhi yoyote na walitawanyika nchini kote. Kabila la Simeoni lilijikuta likiwa ndani ya eneo la kabila la Yuda (Yoshua 19; 1, 9).

Baadaye Dina aliolewa na Simeoni kaka yake kamzaliIa watoto watano.

Kwa mujibu wa wasomi wa agano la kale wanadai kuwa iliwapasa watu wa makabila haya kutawanywa kutawanywa kwani umoja wao huenda ungekuwa hatari zaidi. Kuna visa kwenye Biblia vinaonyesha jinsi Walawi walivyo na hasira za karibu, mfano Kuhani Finehasi mwana wa Aruni wa kabila la Lawi alivyo waua watu wawili kwa mkuki baada mbele ya watu wote baada ya watu hao kwenda kinyume na agizo la Mungu. Musa alikasirika pale alipoona Mmisri akimpiga Mwisrael naye kwa hasira akamuua Mmisri yule. Sipora mke wa Musa alimwita mumewe "Bwanaharusi wa damu", hii inaweza kutokana na na matendo mengine ya kikatili yaliyo fanywa na Musa japokuwa Biblia inasema kuwa ni kwasababu ya kutahiriwa mtoto wao. Pia Musa wakati akiwa mlimani Sinai Waisraeli walifanya uchafu wa kuabudu ndama, Musa alipo shuka na kuona jambo jile, kwa hasira alivunja vibao vya sheria kisha alimchoma ndama yule na kisha kumsaga na kukoroga vumbi lake na kuwalazimisha Waisraeli wote wanywe, hakuishia hapo aliamuru watu walio kuwa upande wa Mungu wawaue watu wote walio abudu ndama. Ikumbukwe Musa ni mtu wa kabila la Lawi.

Asanteni.
 
Musa aliambiwa na Mungu kuwa hatoona nchi ya Kaanani kwa sababu alivunja vile vibao viwili vya amri alizoandika Mungu kwa mikono yake mwenyewe. Zile amri za pili Mungu alizisoma Musa akaziandika, kwa hiyo kosa la kwanza la Musa ni kuvunja vile vibao vya amri kumi za Mungu. .

Musa alifanya makosa mengine pia mfano Mungu alimwambia sema na mwamba utoe maji yeye akaupiga mara mbili yakatoka maji mengi na wakafa wengi sana. Tatu hakusema kuwa Mungu kawaletea maji akasema kuwa yeye ndio anayotoa maji na HASIRA YA BWANA IKAWAKA JUU YA MUSA, na hakuweza kuifikia nchi ya ahadi yeye na wazee wengi kasoro wawili tu. .
 
Sijaelewa vizuri hapo kwenye kosa la kuvunja vibao mkuu...

Mimi makosa ninayo yajua ni hayo mawili ya mwisho.
 
Sijaelewa vizuri hapo kwenye kosa la kuvunja vibao mkuu...

Mimi makosa ninayo yajua ni hayo mawili ya mwisho.
Mungu aliziandika zile amri kwa kidole chake mwenyewe kwa hiyo Musa akazivunja kwa mkoni wake mwenyewe alipowakuta wana wa Israel wamejenga mwana ndama wanamwabudu kwa hasira akazivunja amri ambazo Mungu aliziandika mwenyewe. Hivyo alivyorudi kwa Mungu, hata hivyo hakupenda, hasira ya Mungu ilipoisha akamsomea Musa akaziandika ila za mwanzo ziliandikwa na Bwana Mkubwa. .
 
Mkuu Gily mimi hilo kosa silitambui kwani wakati Mungu anamwambia Musa kuwa ni kwanini hataingia katika nchi ya ahadi (Kumbukumbu la sheria 32:51-52) makosa ni hayo mawili, ukosefu wa imani na kuchukua sifa ambazo sio zake kule Meriba.
 
Sir God ana wivu kweli.
 
huyu bwana kuna mahali hakuelezea vizuri...hawa watoto waliwavamia hao watu siku ya tatu ya maumivu yao ya kutahiriwa kwao yaani hao wanaume walikua wanaugulia kutahiriwa na naamini waliingia watoto wote wa yakobo

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona kila kitu kinaeleweka hapo mkuu. Hamori alipanga kuivamia nyumba ya Yakobo baada ya kupona maumivu ya kutahiriwa. Na pia kwa mujibu wa maandiko yote ni Simeoni na Lawi tu ndio walio ingia mjini na kuua watu wote, na sio watu wote waliokuwa wametahiriwa, baadhi walipinga jambo hilo lakini wanaume wote walikufa.
 
mkuu unachanganya vitabu bro..Biblia haijasema hivyo...nipe mistari
Mbona kila kitu kinaeleweka hapo mkuu. Hamori alipanga kuivamia nyumba ya Yakobo baada ya kupona maumivu ya kutahiriwa. Na pia kwa mujibu wa maandiko yote ni Simeoni na Lawi tu ndio walio ingia mjini na kuua watu wote, na sio watu wote waliokuwa wametahiriwa, baadhi walipinga jambo hilo lakini wanaume wote walikufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Joshua na Karebu.

Back
Top Bottom