Hansard
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 842
- 247
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Tarehe 28/03/2016 ilisambazwa taarifa ya Uongo kwenye mitandao ya Kijamii ambayo ilikua na upotoshaji wa makusudi kwa jamii.
Taarifa hiyo imemnukuu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa George B. Simbachawene (Mb) kwamba ametoa tamko kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa “ Serikali haiko tayari kuajiri wasomi wenye vyeti vya baraza la Mitihani kuanzia vyeti viwili na kuendelea,watakaopata ajira yoyote ile moja kwa moja serikalini ni wasomi wenye cheti kimoja tu”. Lakini pia taarifa hiyo ambayo ilikua na maneno ya kudhalilisha iliendelea kusema kuwa “Wale waliosoma kwa kuunga unga, mara kutafuta credit, mara kurudia mitihani watafute ajira kwenye Mashirika Binafsi”
Taarifa hiyo imendelea kupotosha kuwa kwa Ajira za Walimu mwaka 2016 watakao ajiriwa ni wale ambao walisoma moja kwa moja tu.
Ofisi ya Rais – TAMISEMI imesikitishwa sana na uzushi huu ambao unalenga kuipotosha jamii, kudhalilisha taaluma za Wananchi na kupoteza muda wa Watanzania.
Serikali inawaonya wote wanaojihusisha na kutengeneza Uongo na Upotoshaji wa aina hii kuacha mara moja na serikali haitasita kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha jambo hili haliendelei kutokea.
Ofisi ya Rais – TAMISEMI inapenda kuwaarifu Watanzania wote kuipuuza habari hiyo kwani haina ukweli wowote.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-TAMISEMI,
29 Machi, 2016.