Mods. wameuondoa.........!!
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene,ameibuka na kukanusha vikali uvumi ulioenea jana kuwa amefumaniwa na mke wa mtumjini Singida usiku wa kuamkia jana na kujeruhiwa mkono kwa kisu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Karatu jana jioni,Simbachawene ambaye pia ni Mbunge Kibakwe (CCM) mkoani Dodoma, alisema habarihizo ni uongo na kudai kuwa zimeenezwa na baadhi ya wabunge wa Chademaaliokutana nao mjini Singida jana wakati akiwa njiani kwenda msibani Karatu.
Alisema kuwa katika hoteli aliyofikia, kuna mtu alifumaniwaakiwa na mke wa askari na kufafanua kuwa watu walizua jambo hilo kwa kuwa nayealilala katika hoteli hiyo.
"Ni uzushi tu walidhani kuwa mimi nimefumaniwa, ukweli nikwamba jambo hilo halijanitokea. Mimi nilifika hapa jana (juzi) nikitokeaDodoma kuelekea Karatu kuhudhuria msiba wa shemeji yangu," alisemaSimbachawene.
Aliwataja watu wanaodaiwa kueneza uvumi huo hizo kuwa niwanachama wanane wa Chadema akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho,Christina Lissu.
"Baada ya kufika Singida nilikwenda katika baa moja nakuwakuta wabunge wa Chadema na baadhi ya wanachama, nilipata kinywaji na kurudihotelini kulala," alisema Simbachawene.
Huku akivua shati kuwaonesha waandishi wa habari kwambahakukatwa mapanga mikononi kama ilivyodaiwa, alisema kuwa alipoamka asubuhindipo alianza kusikia habari kuwa amefumaniwa na mke wa mtu.
Awali taarifa kutoka Singida zilizowekwa pia kwenye mitandaoya kijamii zilidai kuwa Naibu Waziri huyo alikumbwa na mkasa huo jana alfajiri.
Tukio hilo ambalo inaelezwa kuwa lilitoka majira ya saakumi, baada ya taarifa hizo kumfikia mwenye mke, ilimlazimu mmiliki wa hotelihiyo kutoa taarifa Polisi ili kuzuia maafa zaidi
Uvumi huo ulidai kuwa baada ya taarifa hizo, iliwalazimuaskari Polisi kwenda katika hoteli hiyo ili kumuokoa Simbachawene, ambayetayari alikuwa amejeruhiwa mkono kwa sime na askari huyo mwenye mke.
Mara baada ya purukushani hizo katika eneo hilo Naibu Wazirihuyo alidaiwa kwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi mkoani Singida,ambapo ilidaiwa kuwa katika maelezo yake aliandika jina la Josephat Josephbadala ya kutumia jina lake halisi.
Hata hivyo, Mbunge Christina Lissu, alisema anashangazwa nataarifa za yeye kuhusishwa kueneza uvumi huo.
Alisema walikutana na Naibu Waziri huyo, katika hoteli hiyo,wakiwa wanatoka mkoani Tabora katika kesi na wabunge wa Chadema, ConchestaRwamlaza, Philipa Muturano na John Mrema ambaye ni Mkurugenze wa Bunge naHalmashauri ya chama hicho.
" Tulipofika Singida nilimwoa Simbachawene nimwita jina,alitufuata na kutununulia vinywaji hapo hotelini," alisema Lissu na kuongeza;
"Hata tulipofika hoteli, baada ya muda tukasikia kutoka kwammiliki wa hoteli akisema kuna watu wanataka kumharibia biashara. Tulipomuulizakulikoni? Akasema kwani hamna habari si mmewaona Polisi wakati mnaingia hapa,huku akisema kuna kigogo wa Serikali amefumaniwa na mke wa askari."
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwaalipoulizwa na Mwananchi Jumapili alisema hakuna tukio kama hilo lililotokeamjini Singida wala mahali popote katika mkoa huo.
"Huo ni uzushi tu, hakuna tukio hilo mjini Singida na walasijasikia taarifa zozote za aina hiyo kutoka maeneo mengine mkoani hapa,alisema Sinzumwa.
MY TAKE:
Kweli Pesamwanaharamu! Uongo unaweza kugeuzwa kuwa ukweli na ukweli kuwa uwongo!
Kamanda wa Polisi ndiyo katuchanganya kabisa. Simbachaweneamekiri kuwa ni kweli tukio lilitokea katika hoteli hiyo, lakini lilimhusishamtu mwingine, huku RPC anatuambia hakuna tukio kama hilo!
Au ndio ukweliumeuzwa?